Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

BETHEL MISSION SCHOOL YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANANCHI

$
0
0
Mkurugenzi wa Bethel Mission School, Emmanuel Mshana, akitoa hotuba ya utangulizi, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo ya Ujasiriamali kwa ajili ya wafanyakazi wa shule hiyo pamoja wananchi kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, Leo. Semina hiyo ya siku tano itakayohusu mafunzo ya ujasiriamali yanafanyika kwenye viwanja vya Shule hiyo iliyopo Manispaa ya Ubungo ambazo zaidi ya washiriki 450 wamehudhuria.
 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manisapaa ya Ubungo, Jaffari Kunambi, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo ya wajasiriamali iliyoandaliwa na Bethel Mission School jijini Dar es Salaam.

Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe, George Yatera, akitoa mada katika semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na Bethel Mission School jijini Dar es Salaam.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe, George Yatera, akitoa mada katika semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na Bethel Mission School jijini Dar  es Salaam.

Benki ya Exim Yatangaza Washindi Kwenda Kuishangilia Starz Afcon

$
0
0
Benki ya Exim leo imewatangaza washindi wake watano watakaoungana na watanzania wengine kwenda kuishangilia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri.

Kampeni hiyo maalum inayofahamika kama “Deposit & Win – Twende Tukaliamshe Misri” ilikuwa inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano hayo.

Washindi hao wa Kampeni ya “Deposit & Win – Twende Tukaliamshe Misri” watapata fursa ya kulipiwa gharama zote za safari ya kwenda na kurudi Misri, malazi na gharama za kujikimu na ili kuweza kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano hayo.

Washindi waliotangazwa leo hii ni Bw Musa Mohamed (Mtwara) Bw Athumani Hassani (Manyara), Bw Deogratius Kessy (Arusha), Bi Msimu Ngaruka (Dar es Salaam) pamoja na Bw Justine Tembo (Arusha) ambao wamepatikana kupitia droo kubwa ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema hii leo chini ya uangalizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT)

Akizungumza baada ya kupatikana kwa washindi hao Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo alisema washindi hao watapata fursa ya kuungana na Taifa Stars katika mashindano Afcon nchini Misri huku wakiwa wamelipiwa gharama zote za safari ikiwemo gharama na Visa, tiketi ya ndege, gharama za tiketi ya kushuhudia mechi hizo pamoja na fedha za kujikimu.

Kwa mujibu wa Bw. Lyimo ili kushiriki katika kampeni hiyo, wateja wapya walipaswa kufungua Akaunti ya Akiba na kuhakikisha kila mwezi ina kiasi kisichopungua Tshs 500,000 au zaidi au kufungua Akaunti ya Current/biashara ikiwa na wastani wa kila mwezi wa Tshs 10,000,000 au hifadhi ya amana maalum (Fixed deposit) yenye thamani isiyopungua Tshs 5,000,000. 

“Kwa wateja ambao tayari wana akaunti ya benki ya Exim walichotakiwa kufanya ni kuongeza akiba kwa kiasi cha Tshs 500,000 au zaidi kwa Akaunti za Akiba au kuongeza kiasi cha Tshs 10,000,000 kwenye akaunti zao za Current/biashara au kuwa na hifadhi ya amana maalum (Fixed deposit) yenye thamani isiyopungua Tshs 5,000,000.’’ alibainisha

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu, alisema kampeni hiyo inatoa nafasi kwa washindi hao kuweza kushuhudia Taifa Stars ikitimiza ndoto zake za kushiriki katika mashindano ya AFCON baada ya zaidi ya miaka 39 kupita.

Kwa mujibu wa Bw Kafu, kampeni hiyo ni sehemu ya mkakati wa kibenki katika kutafuta kesho bora kwa wateja wake na jamii kwa ujumla ambapo pamoja na mambo mengine benki hiyo imekuwa ikiunga mkono agenda za kitaifa ikiwemo suala zima la michezo.
 Meneja Masoko na Mahusiano ya jamii wa Benki ya Exim, Bw Abdulrahman  Nkondo (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wakati akitangaza washindi Kampeni maalum ya benki hiyo inayofahamika kama “Deposit & Win – Twende Tukaliamshe Misri” watakaoungana na watanzania wengine kwenda kuishangilia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri. Wengine  ni pamoja Msimamizi Mkuu wa Matawi wateja wa rejareja wa benki hiyo Bw Mwinyimkuu Ngaliama (Kulia) pamoja na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) Bw Abdallah Hemedy
 Msimamizi Mkuu wa Matawi, Kitengo cha wateja wadogo na wakati (Cluster Head) wa benki ya Exim Tanzania  Bw Mwinyimkuu Ngaliama (Kulia) akizungumza wakati wa droo hiyo.
 Msimamizi Mkuu wa Matawi, Kitengo cha wateja wadogo na wakati (Cluster Head) wa benki ya Exim Tanzania Bi. Gertrude Mbunda (kulia) akizungumza kwenye droo hiyo.
Timu ya maofisa kutoka benki ya Exim Tanzania pamoja na msimazi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) Bw. Abdallah Hemedy wakiendesha kwa umakini droo hiyo.

JUMLA YA WASTAAFU ELFU 10, 500 BADO HAWAJAFIKA PSSSF KUHAKIKI TAARIFA ZAO

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

JUMLA ya wastaafu elfu 10,500 bado hawajafika kwenye ofisi za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ili kuhakiki taarifa zao hadi sasa, Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko huo Bi. Eunice Chiume ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akitembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2019.

Vyombo vya habari alivyotembelea leo Juni 11, 2019 kwa lengo la kujenga mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo ambao ni Mpya ni pamoja na magazeti ya serikali yanayomilikiwa na kampuni ya Tanzania Standard News Papers (TSN), Azam Media, wamiliki wa Azam TV na Uhai FM, Mwananchi Communications Limited, wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, Citizen na Mwanaspoti na Clouds Media Group, wamiliki wa Clouds TV na Clouds FM.

Alisema, zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu huwa linafanyika kila mwaka na huu ni utaratibu wa taasisi za hifadhi ya jamii na kwa upande wa PSSSF zoezi lilianza Desemba mwaka jana (2018).

”Tangu Mfuko huu uanze shughuli zake Agosti 1, 2018 PSSSF ilifungua ofisi nchi nzima Bara na Visiwani na hivyo tunatoa wito kwa wastaafu wote ambao bado hawajahakiki taarifa zao kufanya hivyo kupitia ofisi zetu zilizoenea nchi nzima na wala hawalazimiki kuja makao makuu Dodoma kupatiwa huduma hiyo. “Alifafanua Bi. Eunice Chiume.

Zoezi la kuhakiki taarifa hufanyika kila mwaka kwa upande wetu tulianza zoezi hili Desemba mwaka jana (2018) na liliendelea hadi Machi 2019 na tumeanza tena na zoezi hilo nab ado linaendelea.

“kuhakiki taarifa ni muhimu kwani kunasaidia kujiridhisha na taarifa za wastaafu wetu kwa sababu huwa kunakuwa na mabadiliko mbalimbali ikiwa ni pamoaja na kujua kama bado wapo, au taarifa zao za kibenki zimebadilika au la nah ii inasaidia kufanya malipo sahihi na kwa mtu sahihi.” Alibainisha.

Meneja huyo Kiongozi alitoa wito kwa wastaafu na jamii kwa ujumla kuwa PSSSF iko imara katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wastaafu na wanachama wake wote popote pale nchini. “Mafao yenu yapo wastaafu wote, nendeni mkahakik taarifai, na hata ndugu ambao ndugu zao wastaafu ni wagonjwa wafike kwenye ofisi zetu na sisi tutakwenda kufanya uhakiki huko huko aliko.” Alifafanua Bi. Enice Chiume ambaye anaendelea na ziara yake Alhamisi Juni 12, 2019.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), ambaye pia ni Meneja Masoko na Mauzo, Bw, Januarius Maganga(wapili kulia), akizungumza jambo na Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, (wakwanza kushoto), wakati alipotembelea kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 11, ikiwa ni ziara ya kujenga mahusiano lakini pia kueleza shughuli za Mfuko huo ambao umeanza kutekeelza majukumu yake Agosti 2018 baada ya serikali kuiunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, (wakwanza kushoto), akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi (wapili kushoto), wakiwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya magazeti ya serikali (TSN), chini ya Kaimu Mhariri Mtendaji, Bw. Januarius Maganga (wakwanza kulia), ikiwa ni muendelezo wa ziara ya meneja huyo kiongzi kutembeela vyombo vya habari kwa nia ya kujenga mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo mpya.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu shughuli na majukumu ya Mfuko huo.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu shughuli na majukumu ya Mfuko huo.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), ambaye pia ni Meneja Masoko na Mauzo, Bw, Januarius Maganga, akizungumza mbele ya mgeni wake Bi. Eunice Chiume wakati wa mazungumzo yao
Picha ya pamoja na uongozi wa TSN.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Bw. Tido Mhando, wakati alipotem,belea vyombo vya habari vya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Bw. Tido Mhando, (kushoto), akisalimiana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. 
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume(wapili kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, wakiwa katika mazungumzo na Afisa Mtednaji Mkuu wa Azam Media, Bw. Tido Mhando (wapili kushoto) na Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. John Mbele wakati wa ziara ya meneja huyo kwenye vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni hiyo vya Azam TV na Uhai FM.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Bw. Tido Mhando, akizungumza kwenye mkutano huo. 
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume(wapili kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji mashuhuri wa luninga ya Azam TV, Charles Hillary na Ivona Kamuntu. 
Picha ya pamoja 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Bw. Francis Nanai (kulia), akisalimiana na Meneja Kiongozi Uhusiano wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume, (wapili kushoto) huku Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Bakari Machumu akishuhudia wakati wa ziara ya meneja huyo ikiwa ni muendelezo wa kutembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019. 
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Bw. Frank Sanga (kulia), akiongozana na Bi. Eunice Chiume, wakati alipotembelea chumba cha habari cha kampuni ya Mwananchi Communications Tabata jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume, (wapili kushoto) na Bw. Abdul Njaidi (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha XXL, cha Clouds FM, kutoka kushoto, B12, Kennedy the Remedy, na DJ
Picha ya pamoja na uongozi wa Clouds Media

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 12,2019

Benki ya Azania yafungua maduka matano maalum kwa ajili ya kubadirishia fedha za kigeni

$
0
0
 Benki ya Azania (ABL) imefungua maduka matano maalum kwa ajili ya kubadirishia fedha za kigeni katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro ili kuwapa fursa wateja wa benki hiyo pamoja na wananchi wote njia rahisi ya kuweza kupata huduma hiyo muhimu katika sekta ya kifedha nchini Tanzania.

Maduka ya kubadirishia fedha yaliyofunguliwa ni pamoja na katika Jengo la IPS na Hoteli ya Seacliff jijini Dar es Salaam. Maduka mengine yamefunguliwa jijini Arusha, KIA pamoja na Moshi. Huduma za kubadirishia fedha za kigeni zitakuwa zikitolewa kwenye maduka hayo kwa saa za kawaida za kazi kama matawi mengine ya Benki ya Azania.

Uamuzi wa kufungua maduka haya mapya maalum kwa ajili ya huduma za kubadirishia fedha za kigeni tu, unatokana na mwongozo wa hivi karibuni wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama hatua ya kuhakikisha watoa huduma wote wa kubadiri fedha za kigeni wanatambuliwa na BoT.

Akizungumzia juu ya uamuzi wa Benki ya Azania kufungua maduka hayo mapya, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles J Itembe amesema benki inajivunia kupanua wigo wake hususani katika kutoa huduma za kubadirisha fedha za kigeni katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa zaidi wa huduma hiyo.

“Licha ya kutoa huduma ya kubadiri fedha za kigeni, maduka haya mapya yatakuwa na uwezo wa kutoa huduma nyingine za kibenki kama vile kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha pamoja na huduma za kifedha kwenye simu za mkononi (sim banking)”. Amesema Itembe.

Itembe pia ameongeza kuwa Benki ya Azania itaendelea kuwa na madirisha ya kubadiri fedha za kigeni kwenye matawi yake yote nchini mbayo huwa wazi kila siku kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku.

SERIKALI YATAIFISHA MALI ZA WAHALIFU ZENYE THAMANI YA TSH BILIONI 93.16

$
0
0
Na Grace Semfuko,MAELEZO

DAR ES SALAAM

Serikali imesema kuwa kati ya kipindi cha mwaka 2013 hadi Mei 2019 imetaifisha mali za wahalifu zenye thamani ya Tsh. Bilioni 93.16 zilizokamatwa kwenye sekta za Madini, Maliasili na Sekta ya fedha (Upatu) ikiwa ni sehemu ya kudhibiti uhalifu kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Uhalifu huo unaodaiwa kukithiri katika miaka ya nyuma na ambao sasa unaendelea kudhibitwa unatajwa kuliingizia Taifa hasara ya Mabilioni ya fedha, hatua iliyoifanya Serikali kuudhibiti kwa kutaifisha mali za wahusika wa uhalifu huo.

Hayo yalibainishwa leo (Jumatano Juni 12, 2019) Jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati akifungua mkutano wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Urejeshaji wa Mali Zinazohusiana na uhalifu wenye jumla ya nchi wanachama 16.

Samia alisema hivi sasa Serikali ya Tanzania inapanga mikakati ya kuondokana kabisa na uhalifu huo kutokana na sera ya kudhibiti Rushwa pamoja na kuanzisha mahakama maalum zitakazoshughulikia ufisadi Nchini Tanzania.

“Sisi Tanzania tunaimarisha Sera zetu za kupambana na Rushwa na Ufisadi, tunaenda sambamba na umoja wetu huu wa ARINSA hivyo tunazishauri nchi zingine ambazo zipo kwenye umoja huu na bado hazijatunga Sera na Sheria ziharakishe mchakato ili twende sawa” alisema Samia.

Kwa upande wake Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Augustine Mahiga alisema mkutano huo pamoja na mambo mengine utazungumzia mikakati ya pamoja ya kudhibiti uhalifu wa mipakani hasa kwenye udhibiti wa uingizwaji wa bidhaa haramu ikiwepo dawa za kulevya.

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Biswalo Maganga alisema mkakati wa kutaifisha mali za wahalifu umekuja kufuatia kuona vifungo gerezani kwa wahalifu hao havitazinufaisha nchi hizo na badala yake kuchukua mali zao ili kukomesha kabisa suala hilo.

Aidha alisema tayari wataalamu kadhaa wa upelelezi wa kufuatilia mali na kuzitaifisha wameshapata mafunzo na kwamba zoezi hilo linaendelea ili kuhakikisha linafanyika kikamilifu na kwa usiri mkubwa.

ARINSA ni umoja wa urejeshaji wa mali zinazohusiana na uhalifu wenye Nchi wanachama 16 zilizopo Barani Afrika ambao kwa pamoja wanakusudia kukabiliana na uhalifu hususan kwenye mipaka ya nchi hizo.

NI BAJETI YA KIHISTORIA ILIYOGUSA MAISHA YA KILA MTANZANIA

$
0
0
*Yajibu za kero mbalimbali za Watanzania hasa wayonge

*Yaondoa utitiri wa kodi ...Waziri Mpango atoa muelekeo

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesoma bajeti ya fedha kwa mwaka 2019/2020 kwa kutenga Sh. trilioni trilioni 33.

Dkt. Mpango wakati anasoma bajeti hiyo leo Bungeni Mjini Dodoma amefafanua kwa kina namna ambavyo Serikali imejipanga kuleta maendeleo ya Watanzania kupitia bajeti hiyo.

Akifafanua zaidi kuhusu bajeti hiyo yenye kurasa 71, Waziri Mpango amesema kuwa bajeti hiyo ni nyenzo ya kufikia matarajio ya wananchi wote.

"Hivyo, katika kuandaa bajeti hii, Serikali iliwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo, Kamati ya Bunge ya Bajeti, wafanyabiashara, taasisi za umma na binafsi pamoja na wananchi wa kawaida.

"Na wataalam wa kodi hususan wale walioshiriki vikao vya kazi vya kikosi kazi cha maboresho ya kodi kujadili na kushauri kuhusu mapendekezo ya maboresho ya kodi na tozo mbalimbali.

"Baadhi ya wadau walituletea maoni na ushauri kwa maandishi au barua pepe. Nakiri kuwa walitupatia mrejesho ambao umesaidia kuboresha será na vipaumbele  vya nchi yetu kwa mwaka 2019/20 na siku zijazo,"amesema.

Ameongeza kuwa kwa niaba ya Serikali wanashukuru kwa michango hiyo mizuri ambayo tumejitahidi kuizingatia na ni matarajio ya Serikali wadau hao wataendelea kufanya hivyo katika mchakato wa bajeti zitakazofuata.

Amesema kuwa bajeti ya 2019/20 inahusu kuendeleza juhudi za kujenga msingi wa uchumi wa viwanda ili kupanua fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na ustawi endelevu wa jamii  na hatimaye kuondokana na umaskini, ujinga na maradhi.

Amefafanua bajeti hiyo  imelenga kuimarisha na kujenga miundombinu ya kisasa ili kuongeza uwezo wa Taifa katika uzalishaji viwandani hasa vile vinavyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi hapa nchini na kutoa huduma bora (afya, elimu na maji) kwa wananchi.

Aidha, miundombinu hiyo itasaidia kuongeza biashara nchini, kikanda na kimataifa kwa kujenga mazingira mazuri ya kufanya biashara na uwekezaji kwa kushughulikia changamoto zilizobainishwa katika mpango wa kuboresha mazingira ya biashara (Blueprint).

Pia kuimarisha kilimo (uzalishaji wenye tija na masoko ya mazao, ufugaji, uvuvi, na misitu) kwa kuzingatia umuhimu mkubwa wa sekta hii katika uchumi wa Taifa (chakula, ajira, kipato cha mwananchi, mchango katika fedha za kigeni na muunganiko wa sekta hii na maendeleo ya viwanda).

Ameongeza kuwa inalenga kudumisha amani na usalama katika Taifa; na kujenga misingi ya Taifa kujitegemea kiuchumi

Waziri Dkt. Mpango aliyesoma hotuba hiyo kwa zaidi ya saa mbili huku kukiwa na shangwe kutoka kwa wabunge wa CCM, amesema safari ya kuijenga Tanzania mpya imeiva lakini haitakuwa rahisi.

"Hasa tukizingatia mabadiliko yanayoendelea katika uchumi wa dunia, ushindani mkali wa kibiashara, mabadiliko ya haraka ya teknolojia na demografía na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.

"Hata hivyo, bahati nzuri ni kuwa, katika historia ya nchi yetu, Watanzania ni watu jasiri katika mapambano dhidi ya changamoto zinazojitokeza na kila wakati zilipojitokeza tulizishinda  kwa kutumia ubunifu na nguvu ya umoja wa Watanzania.

"Hivi sasa tuko imara zaidi chini ya uongozi shupavu wa Dkt. John Joseph Magufuli. Uchumi wetu unaendelea kukua kwa kasi kubwa, ambapo mwaka 2018 ulikua kwa asilimia 7.0  na kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi kinazidi kupungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia 26.4 mwaka 2017/18.

"Naamini pasipo shaka yoyote kwa umoja wetu, uongozi makini, kufanya kazi kwa bidii na kwa kutumia rasilimali za nchi yetu vizuri, tutaijenga Tanzania mpya, ambayo itakuwa kitovu kikuu cha uchumi (Economic hub) katika ukanda wa Afrika Mashariki katika muda usiozidi miongo miwili ijayo,"amesema Dk.Mpango.

Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru washirika wetu wa maendeleo kwa misaada na mikopo nafuu wanayoendelea kuitoa katika kutekeleza miradi na programu mbalimbali za maendeleo nchini.

Amesema katika bajeti ya mwaka 2019/20, washirika wa Maendeleo kwa pamoja wanatarajia kuchangia jumla ya Sh.trilioni 2.78.

  Waziri Mpango amesema kwa kutambua uhusiano mzuri uliopo kati ya Serikali na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ni matarajio yao kuwa misaada ya kiufundi na fedha zilizoahidiwa na marafiki hawa zitatolewa kwa wakati na kwa kiasi kilichoahidiwa.

"Nasi kwa upande wa Serikali tunaahidi kutumia misaada hiyo kama ilivyokusudiwa.  Napenda nitumie nafasi hii kuwahimiza Mabalozi wanaoziwakilisha nchi  zao na taasisi za kimataifa hapa nchini Tanzania waongeze nguvu kukuza biashara kati ya nchi zao na nchi yetu na kuhamasisha wenye mitaji toka nchi zao kuja kuwekeza hapa Tanzania.

"Tanzania ni salama kwa uwekezaji wenye faida kwao na kwetu. Aidha, wafanye jitihada zaidi kuhamasisha watalii kuja kujionea vivutio vya utalii, ambavyo ni fahari ya Tanzania,"amesema.

Pia amesema Serikali ya Awamu ya Tano inatambua na kuthamini michango yao katika maendeleo ya Taifa letu ili mradi isiambatane na masharti yanayohatarisha uhuru wa Tanzania (national sovereignity),

Ameongeza au kwenda kinyume na mila na desturi zetu na kwamba hata pale ambapo Serikali au mihimili mingine imefanya maamuzi ambayo hawakubaliani nayo, ni vema na haki washirika wetu wa maendeleo wakatoa muda wa kuyatafakari na kujadiliana nao kwa staha badala ya kuishinikiza Serikali ibadili uamuzi wake ndipo watoe fedha, jambo ambalo halikubaliki hata kidogo.

Waziri Mpango amewasisitiza Watanzania kuendelea kushikamana katika kuijenga Tanzania mpya na kuwa wazalendo na wakae macho daima kulinda na kutetea maslahi ya Taifa letu.

"Tuongeze bidii kufanya kazi. Enzi za kutegemea wajomba hazipo tena na habari njema ni kuwa: “Tukiamua Tunaweza” na Serikali ya CCM inayoongozwa na Dkt. John Magufuli imethibitisha ukweli huo.

"Naomba kwa niaba ya Serikali kupongeza mchango mkubwa wa wafanyabiashara na wananchi wote ambao wamelipa kodi kwa mujibu wa sheria. Pia natambua mchango adhimu wa mashirika na taasisi ambazo Serikali ina hisa yaliyotoa gawio au asilimia 15 ya mapato ghafi kuingia katika Mfuko Mkuu wa Hazina,"amesema.

Amefafanua katika mwaka ujao wa fedha, Serikali inayataka mashirika yote ya umma na taasisi ambazo Serikali ina hisa kuhakikisha kuwa wanatoa gawio au mchango wa asilimia 15 ya mapato ghafi na Msajili wa Hazina asimamie kikamilifu utekelezaji wa maagizo haya ya Serikali.

Wakati huo huo amesema Oktoba mwaka huu wa 2019 nchi yetu itafanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hivyo Serikali kwa upande wake imejipanga kikamilifu katika maandalizi ikijumuisha mahitaji ya kibajeti kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi huo.

"Ninawasihi wananchi wote wenye sifa wajitokeze kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura. Aidha, katika kuchagua viongozi wa ngazi hiyo, tafuteni Watanzania wenye sifa,"amesema.

Amezitaja baadhi ya sifa hizo ni awe mchapakazi mwenye kujitoa sadaka kuwatumikia watu, hasa wananchi wa kawaida, mwepesi kuona, kusikiliza na kuguswa na shida za wananchi wake na tena awe jasiri katika kupigania haki za wanyonge na awe na uwezo na ubunifu katika kutatua kero za wananchi hao.

Pia awe mwadilifu, anayechukia na kupiga vita rushwa na ufisadi kwa matende, anayetambua fursa zilizopo katika eneo lake, kubuni mikakati ya kuwaendeleza wananchi anaowaongoza na kuwatia watu wake hamasa ya kuthubutu kutumia fursa hizo;

Sifa nyingine awe mtetezi hodari wa kulinda mazingira na mpambanaji dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, mwenye kutoabudu nyadhifa na anayetambua kuwa nafasi na vyeo tulivyopewa ni vya muda tu. Ni vya kupita!

"Thamani halisi ya kiongozi ni kufanya kazi kwa bidii na kuacha kumbukumbu nzuri kwa ustawi wa eneo analoliongoza na Taifa kwa ujumla.

"Awe kama mchezaji mzuri wa kiungo katika timu ya ushindi, anayetambua kwamba mkono mmoja hauwezi kupiga makofi ya shangwe, awe mwenye kutambua kazi za kiongozi zina maana sana kwa kuwa zinamwezesha kubadilisha maisha ya maelfu ya Watanzania, hasa wanyonge, kuwa bora zaidi;

"Pia awe na uwezo wa kuwaeleza wananchi kinaganaga kuhusu Serikali yao inawapeleka wapi na wajibu wa kila mmoja ili waendelee kuiunga mkono; na awe anatoka ndani ya chama cha siasa kinachotetea maslahi na haki za wanyonge na chama hicho ni CCM,"amesema.

Dk.Mpango amekiri kuwa, sifa hizi alizozitaja  ameziazima kutoka kwa Dkt. John Magufuli, bila ridhaa yake na kutumia nafasi hiyo kuomba viongozi wote wa dini pamoja na waumini wote kila mmoja kwa imani yake, tuendelee kumwombea Rais.

 "Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia afya njema, hekima, busara na kumwongoza kwa kila jambo alifanyalo kuliletea Taifa letu maendeleo,"amesema Dk.Mpango.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akiwasili katika viwanja vya  Bunge kwa ajili ya kusoma Bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2019/2020 Jijini Dodoma, Juni 13.2019. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akisoma Bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2019/2020, Bungeni jijini Dodoma Juni 13, 2019.

TFDA YAWEKA MIFUMO MAALUM YA UDHIBITI SALAMA WA CHAKULA KINACHOZALISHWA AMA KUINGIZWA NDANI YA NCHI

$
0
0
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA imeweka mifumo maalum ya udhibiti wa usalama wa chakula kinachozalishwa ndani ya nchi na kile kinachoingizwa kutoka nj e ili kuhakikisha afya bora kwa walaji.

Mifumo hii ni kufanya tathmini ya vyakula vilivyofungashwa,kusajili maeneo na kutoa vibali vya biashara za vyakula, kufanya ukaguzi wa vyakula katika soko pamoja na ukaguzi wa maeneo ya kusindikia, kuhifadhia na kuuzia vyakula.

Akizungumza wakati akifungua Semina ya siku mbili kwa waandishi wa Habari iliyofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa chakula TFDA Moses Mbambe alisema mifumo hii pia husaidiwa na  uchunguzi wa sampuli za vyakula katika maabara.

“Ndugu zangu Waandishi wa Habari, naomba muufahamishe Umma kuwa mifumo hii inahakikisha kila Mtanzania anatumia chakula salama, na tunaanzia mipakani na kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini” alisema Mbambe.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu Usalama wa TFDA Bw. Adam Fimbo alisema umuhimu wa usalama wa chakula Nchini Tanzania unapewa kipaumbele kwa kushirikiana na Baraza Kuu la umoja wa mataifa ambapo kupitia kikao chake cha Desemba 28 2018 ilipitisha siku ya usalama wa Chakula Duniani kuwa   Juni 7 ya kila mwaka ambapo kwa mara ya kwanza Duniani kote siku hiyo ilianza mwaka huu wa 2019.

“Tanzania tunaungana na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha tunakuwa na kiwango cha hali ya juu cha usalama wa chakula,tunawaomba wananchi wazingatie uzalishaji bora wa vyakula na hii   itaongeza ufanisi na kuimarisha afya za wananchi wetu” alisema Fimbo

Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani WHO takribani Watu Milioni 600 Duniani sawa na Mtu mmoja kati ya watu 10 huugua kila mwaka kutokana na kula chakula kisicho salama na kati yao watu 420,000 hufariki  na huku watoto wakiwa  125,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano ambapo kwa Bara la Afrika zaidi ya watu milioni 91 wanakadiriwa kuugua huku watu 137,000 hufariki dunia kila mwaka.


Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw. Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akifungua kikao kazi leo katika ukumbi wa Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.
Kaimu Mkurungezi wa Usalama wa Chakula wa (TFDA),Moses Mbambe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusajili vyakula ili kuhakikisha vinakidhi  viwango vilivyoweka kabla ya kuruhusiwa kwenye soko la Tanzania.
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) , Bi. Gaudensia Simwanza akizungumza na waandishi wa habari kuhusu usalama wa chakula na kuwawezesha kutoa taarifa sahihi kwa jamii wakati wakiandika habari zihusuzo chakula,kwenye kikao leo katika ukumbi wa Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv Pwani)

Waandishi wa habari  wakiendelea na kikao katika ukumbi wa Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijirii kwenye kikao hicho leo katika ukumbi wa Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.

RAIS WA KONGO (DRC) MHE. FELIX TSHISEKEDI AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA MWENYEJI WAKE DKT. MAGUFULI JUNI 13, 2019

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.

Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi akikabidhiwa Ua la ishara ya Upendo na kumkaribisha Nchini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Jijini Dar es salaam ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.  


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa. 
Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi akikagua paredi maalumu aliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi wakati wakitazama kikundi cha ngoma wakati wa sherehe za kumkaribisha Rais wa Kongo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi wakati wakiwapungia mikono wananchin waliojitokeza katika sherehe za kumkaribisha Rais wa Kongo katika Uwanja
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akizungmza na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antonio Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es salaam kabla ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu kwa Mwaliko wa Rais Dkt.Magufuli. 



WAZIRI MAKAMBA KAUTANA NA WAJUMBE WA KIKOSI KAZI CHAKATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI JIJINI DODOMA

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akifafanua jambo alipokutana na Wajumbe wa Kikosi kazi cha katazo la mifuko ya plastiki jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akiongea wakati alipokutana na Wajumbe wa kikosi kazi cha katazo la mifuko ya plastiki jijini Dodoma, ikiwa ni kutathmini zoezi zima la marufuku ya plastiki lilivyokua. Pembeni yake ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Mussa Sima.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWACHAGUA HIVI KARIBUNI

$
0
0


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mkuu wa Wilaya Mpya wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Ndg. Abeid Juma Ali, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar. Ndg Juma Hassan Juma Reli, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Ndg. Juma Hassan Juma Reli, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, akihudhuria hafla hiyo na Viongozi wa Serikali na Dini.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Ndg. Juma Hassan Juma Reli, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, akihudhuria hafla hiyo na Viongozi wa Serikali na Dini.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Viongozi aliowaapisha ikulu leo kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwaapisha Viongozi aliowachagua hivi karibuni.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg. Juma Hassan Juma Reli, baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapisha leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

JESHI LA POLISI LAWAMANI IRINGA

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza na wamiliki wa bar na mameneja mara baada ya kuwasikiliza malalamiko yao ya kufanyiwa vurugu na polisi nyakati za usiku
Meneja wa bar ya Shine Pub ya mkoani Iringa, Richard Sanga akitoa kero yake mbele ya wanahabari
Mmoja wa wamiliki wa bar akizungumza mbele ya mkuu wa wilaya walipofika ofisini kwake kuzungumza juu ya malalamiko ya jeshi la polisi

*************************



NA DENIS MLOWE, IRINGA



WAMILIKI wa bar na klabu za usiku mkoani Iringa wamepinga na kulalamikia kitendo cha jeshi la polisi mkoani Iringa kuwafanyia vitendo vya kupiga wateja na wahudumu kwa kile kinachosemekana muda wa kufunga bar kuzidishwa.

Wakizungumza mara baada ya kuandamana hadi kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela, wafanyabiashara hao Zaidi ya 30 wanaomiliki bar mkoani hapa walisema kuwa kitendo kinachofanywa na baadhi ya askari wa jeshi hilo wanaofanya doria nyakati za usiku wamekuwa wakiwapiga wateja na wahudumu pindi wakikuta muda wa kufunga bado ni kitendo kinachohatarisha Amani.

Mmoja wa wamiliki wa Bar mkoani hapa aliyezungumzia hali hiyo, Happy Matanji alisema kuwa tarehe 8 mwezi huu walipita polisi katika bar anayomiliki wakaamuru bar ifungwe lakini walitumia nguvu kubwa na kuanza kuwapiga wateja na wahudumu na kila mtu aliyeonekana katika eneo hilo licha ya kuwa na kibali kinachoruhusu kutoa huduma muda wa zaida.

Alisema kuwa manispaa walimpatia kibari ambacho nikaruhusu kufunga bar hiyo hadi saa nane badala ya muda wa saa sita lakini askari waliokuwa doria hawakutaka kabisa kusikiliza wala kukubaliana na kibari ambacho kinaruhusu kufungwa kwa huduma za bar kutokana na kibari hicho.

Alisema kuwa meneja wa bar hiyo alichukua jukumu la kwenda kituo cha polisi kupata msaada Zaidi lakini alipofika kituoni walimweka ndani kwa kumwambia kwamba hadi kituoni amewafata licha ya kuwa kibali cha kufanya biashara hadi muda huo.

“Unaamua kuepusha shari na kufata sharia ya kuomba kibali lakini cha kushangaza mamlaka ya jeshi la polisi wanakuwa hawakitambui na mwisho wa siku wateja na wahudumu wanaambulia kipigo hapo unakuwa unaingia hasara kubwa ya kulipia kibali na hela kupotea na haitoshi wanapelekwa mahabusu sasa hapo inakuwaje” alisema

Alisema kuwa alichukua jukumu la kumpigia kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa na kumwabarisha kuhusu hali hali na kusema kuwa analifanyia kazi na kumjulisha laki alipotafutwa siku ya pili hakuweza kupokea simu na juzi alipopigiwa rpc alisema kuwa yuko katika kikao atapigiwa lakini hakuna hatua yoyote ile.

Matanji aliongeza kuwa anashangaa kwa kiasi kikubwa ni mafunzo ya aina gani wanayopatiwa jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa katika kuwakabili wateja ambao hawana shida yoyote hali ambayo inawashangaza wengi kwani hapo awali hali hii haikuwepo.

Richard Sanga meneja wa bar ya Shine Pub alisema kuwa vitendo ambavyo wanafanya jeshi la polisi limefanyika katika bar hiyo na kusema kwamba leseni za biashara hazionyeshi ni muda gani wa biashara hiyo inafungwa saa ngapi tofauti na leseni za zamani zilizokuwa zinaonyesha muda wa kufungua na kufunga hivyo unaambiwa tu unatakiwa kufunga muda Fulani.

Alisema kuwa polisi anapofanya kazi yake inabidi afate uongozi wa eneo husika na kufanya mazungumzo kwamba muda wa kufunga umewadia ikiwezekana kumshauri na kumpa onyo ila wao wakifika hakuna onyo wala ushauri wowote kikubwa ni nguvu mwanzo mwisho na kutoa amri za watu kukaa chini licha yaw engine kuwa wamekaa hapo ndipo hasara inaanza kwani wengi wa wateja wanakuwa wanadaiwa bili lakini nguvu inayotumika ni kubwa.

Alisema kuwa askari wanatembea na viboko, nyaya za umeme za kumpigia mtu bila kufikiria kwamba raia ni askari jamii na wanafanya kazi kwa Amani iweje wao watumie nguvu badala ya kujenga ushirikiano ambao utasaidia kuwabaini wahalifu na kuuweka mji kuwa sawa lakini askari wa doria wakija wao na mabavu kwa kila mtu ndani ya bar na kisha wanakamatwa na kupelekwa mahabusu.

Alisema kuwa faini inayotolewa mahakamani ni kubwa Zaidi kuliko ilivyowekwa kisheria ambapo unakuta mtu unalipa Zaidi ya laki sita kwa kuwalipia faini wahudumu sita wa bar waliofikishwa mahakamani hapo na mbaya Zaidi wanakuwa hawana makosa kwa kuwa wanakuwa wanakamatwa katika eneo la kazi lakini wanafunguliwa makosa uzembe na uzururaji.

Sanga aliongeza kuwa biashara wanayofanya wanakumbuna na changamoto nyingi sana ambazo nyingine wanashindwa kukabiliana nazo zikiwemo utitiri wa kodi lakini licha ya hivyo muda wa kufanya biashara mchache na hapo unakutana na changamoto nyingine ya doria na wateja kuondoka na bili.

Akiwajibu wamiliki wa bar waliofika ofisini kwake, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alisema kuwa mzunguko wa fedha kwa asilimia kubwa unaletwa na wamiliki wa sehemu za vinywaji na kukiri kuwa jeshi la polisi limefanya kosa na kuwaomba msamaha kwa wamiliki wa bar na klabu kwa niaba ya jeshi la polisi.

Kasesela ambaye na Mwenyekiti wa Usalama wa Wilaya ya Iringa alisema kuwa awali hakukuwa na tabia kama hiyo hivyo ataongea na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa na kubaini nini hasa chanzo ambacho kinasababisha haya yote ambayo yanatokea sasa kwa wahudumu na wateja wa bar.

Alisema kuwa kwa upande wa jeshi la polisi na serikali walitalifanyia kazi na kuwahakikishia kuwa hakuna askari atakayepona endapo atabainika kuwanyanyasa Watanzania wenzake bila sababu na kutangaza kwa wamilki wa bar na pub zote wilaya ya Iringa mwisho wa kufunga ni saa sita na ikifika saa tano wamiliki wa bar wanatakiwa kupunguza sauti ya muziki na ikifika muda was aa saba askari wasiwabugudhi wateja.

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUWAPONGEZA WABUNIFU WA UMEME WA MAJI KUTOKA MKOANI NJOMBE. IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijiandaa kuwakabidhi kifuta jasho cha shilingi milioni 5 wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute(Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita kuwapongeza na kuongea nao pamoja na Mkurugenzi Mkuu na Waandaji wa Kipindi cha Hadubini TBC, Makatibu wakuu wa Wizara ya Nishat, Elimu Sayansi na teknolojia, Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu na wataalamu kutoka TANESCO,Kamishna wa Umeme na Mkurugenzi Mkuu na Wataalamu wa COSTECH Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwakabidhi kifuta jasho cha shilingi milioni 5 wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita kuwapongeza na kuongea nao pamoja na Mkurugenzi Mkuu na Waandaji wa Kipindi cha Hadubini TBC, Makatibu wakuu wa Wizara ya Nishat, Elimu Sayansi na teknolojia, Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu na wataalamu kutoka TANESCO,Kamishna wa Umeme na Mkurugenzi Mkuu na Wataalamu wa COSTECH Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasindikiza baada ya kuwakabidhi kifuta jasho cha shilingi milioni 5 kuwakabidhi wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita kuwapongeza na kuongea nao pamoja na Mkurugenzi Mkuu na Waandaji wa Kipindi cha Hadubini TBC, Makatibu wakuu wa Wizara ya Nishat, Elimu Sayansi na teknolojia, Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu na wataalamu kutoka TANESCO, Kamishna wa Umeme na Mkurugenzi Mkuu na Wataalamu wa COSTECH Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute
(Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo pamoja na Mkurugenzi Mkuu
na Waandaji wa Kipindi cha Hadubini TBC, Makatibu wakuu wa
Wizara ya Nishat, Elimu Sayansi na teknolojia, Viwanda na
Biashara, Mkurugenzi Mkuu na wataalamu kutoka TANESCO,
Kamishna wa Umeme na Mkurugenzi Mkuu na Wataalamu wa
COSTECH Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwapongeza wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13,2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwapongeza wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahi na wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
Mbunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) aliyepongezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapongeza na mwenzake Bw. Jailosi Ngairo aliowaita Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
Mbunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. Jailosi Ngairo aliyepongezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapongeza na mwenzake Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) aliowaita Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
Mtangazaji wa Shirika la utangazajinTanzania TBC Tatu Abdalah kutoka Njombe akifuatilia kwa umakini tukio la kuwaponeza wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na mwenzake Bw. Jailosi Ngairo waliopongezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.


PICHA NA IKULU

Wachimbaji Wasisitizwa Matumizi Salama ya Kemikali

$
0
0
Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Mbeya, Leonard Manyesha (aliyesimama), akiongea wakati wa Mkutano wa viongozi wa wachimbaji wa madini ya dhahabu Wilaya ya Chunya na viongozi kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mkemia Mkuu wa Serikali (hawapo pichani).
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akiongea na viongozi hao wa wachimbaji wa madini ya dhahabu Wilaya ya Chunya (hawapo Pichani) katika Mkutano huo uliofanyika wilayani Chunya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason (wa pili kulia) akiongea na viongozi wa wachimbaji wa dhahabu katika migodi ya Chunya (hawapo pichani). Mwenyekiti wa Bodi na Mkemia Mkuu wa Serikali (wa tatu kulia), walikutana na wadau hao kwa lengo la kuwasikiliza maoni waliyonayo juu ya huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Profesa Esther Hellen Jason (aliyekaa katikati), Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kushoto), wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Dhahabu Mkoa wa Mbeya, Leonard Manyesha (wa pili kulia), Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Gaspar Mushi (kulia) na viongozi wengine wa wachimbaji  na wamiliki migodi ya dhahabu iliyopo katika Wilaya ya Chunya.

*****************************
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Esther Hellen Jason amewataka wachimbaji wa madini ya dhahabu wa Chunya kuzingatia matumizi salama ya kemikali wanazozitumia katika shughuli zao za uchimbaji kwa lengo la kulinda afya na mazingira.

Prof. Esther Hellen Jason ameyasema hayo wilayani Chunya wakati akiongea na viongozi wa wachimbaji na wamiliki wa migodi ya madini ya dhahabu.
“Ndugu zangu tuzingatie matumizi salama ya kemikali kwa lengo la kulinda mazingira, afya zetu na vizazi vyetu, tunatambua sekta ya madini ni moja ya sekta muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi kwa sababu dhahabu inaingiza mapato ndani ya Serikali lakini huwezi kuipata dhahabu bila kutumia baadhi ya kemikali.” Alisema Prof. Jason.

Ameongeza kuwa, kukutana na wadau na kujadiliana namna bora ya kuimarisha mahusiano ya kikazi ni njia sahihi ya kutatua changamoto na kuboresha utendaji kazi wa pande zote katika shughuli hizi za uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu.
Hivyo changamoto zenu mlizowasilisha leo tunazichukua kwa uzito mkubwa na tutayafanyia kazi ili kuboresha zaidi utendaji wetu na shughuli zenu.

“Kwa zile zilizo ndani ya uwezo wa Bodi ya Wakurugenzi tutazifanyia kazi kwa lengo la kurahisisha utendaji wenu na zinayohitaji maamuzi ya juu zaidi tutayawasilisha ili kupatiwa ufumbuzi maana zikitatuliwa changamoto hizi tunaamini hazitakuwa kwa faida ya Chunya tu bali kwa wachimbaji wa Tanzania nzima wanaotumia kemikali.” Alimalizia

Kwa upande wake, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, alisema mkutano huo ni mwanzo wa ushirikiano wa Mamlaka na wachimbaji hao wenye lengo la kutatua changamoto na kuzifanya kuwa fursa za kuboresha utendaji na kuwezesha wadau hao wa Chunya na maeneo mengine ya migodi nchini.
 Akiongea kwa niaba ya wachimbaji, Mwenyekiti wa Wachimbaji wa dhahabu Mkoa wa Mbeya, Leonard Manyesha, alisema anashukuru kwa mkutano huo na anaamini mazuri yaliyojadiliwa yataleta tija yakifanyiwa kazi.
“Nimefurahishwa na mkutano huu na naamini tuliyojadili yakifanyiwa kazi yataleta tija kwenye kazi zetu za uchimbaji wa dhahabu. Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wamekuwa karibu sana kwetu hasa kwenye mafunzo ya matumizi salama ya kemikali na kutatua changamoto zetu pale tunapoziwasilisha.” Alisema Manyesha.

NMB YAZIPIGA TAFU S/M LIWITI, KITUO CHA AFYA GAIRO

$
0
0




Mkuu wa wilaya ya Urambo,Angelina Kwingwa akipokea madawati na vifaa vya afya kwa naiba ya shule ya msingi ya Vumila kutoka kwa Meneja wa NMB kanda ya Magharibi,Sospeter Magesse. Benki ya NMB izipiga tafu shule na vituo vya afya kwa wiki hii ikiunga mkono jitihada za Serikali kuboresha Sekta za Elimu na Afya.
……………………….

KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali kuboresha Sekta za Elimu na Afya, Benki ya NMB imekabidhi mabati 180 kwa Shule ya Msingi Liwiti, iliyoko Tabata, Dar es Salaam, huku ikitoa msaada wa vifaa katika Kituo cha Afya Gairo, mkoani Morogoro vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 20. 

Hafla za makabidhiano hayo zimefanyika kwa nyakati tofauti jana, ambako Shule ya Msingi Liwiti imekabidhiwa mabati ya kuezekea madarasa matatu, yakiwa na tahamni ya Sh. Mil. 5, wakati Kituo cha Afya Gairo kikipokea mashuka 62, vitanda vya kulala wagonjwa vitano na magodoro yake. Pia benki hiyo wilayani Urambo imekabidhi Kituo cha afya cha Uyoga vifaa vyenye thamani ya millioni tano pamoja na madawati kwa ajili shule ya msingi ya Vumila. 

Wakati msaada wa mabati kwa Shule ya Liwiti ukipokelewa na Mkuru
genzi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri, katika hafla iliyofanyika Liwiti shuleni, msaada mashuka, vitanda na magodoro vyenye thamani ya Sh. Mil. 5 kwa Kituo cha Afya Gairo, vilipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Seriel Mchemba.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mabati Liwiti Shuleni, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, alisema misaada wanayotoa katika Sekta za Elimu, Afya na Majanga, inaongeza chachu ya benki hiyo kujiweka karibu na jamii, na kubaki kuwa kinara miongoni mwa taasisi zinazosapoti Serikali. 


Badru aliongeza ya kwanza, misaada yao inatokana na utaratibu wa benki hiyo kupitia Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kutoa asilimia moja ya faida yao ya mwaka baada ya kodi na kwamba mwaka huu wametenga kiasi cha Sh. Bilioni 1, ambako hadi sasa wametoa misaada inaayofikia Sh. Mil. 500. 

Kwa upande wake, Shauri aliishukuru NMB kwa namna inavyosaidia utatuzi wa changamoto za elimu na afya wilayani Ilala, huku akisema misaada ya hiyo katika mashule wilayani humo, imesaidia kukuza kiwango cha ufaulu, ambako mwaka uliopita ilikuwa ya nne kati ya wilaya 185, ikifaulisha wanafunzzi 21,000. 

Alibainisha ya kwamba, kupita misaada ya wadau muhimu kama NMB na ruzuku ya Mpango wa Elimu Bure wa Serikali ya Awamu ya Tano – unaowaingizia kiasi cha Sh. Mil. 70 kwa mwezzi (sawa na zaidi ya Sh. Mil. 800 kwa mwaka), matumaini yao ni kupandisha zaidi kiwango cha ufaulu wa sasa wilayani humo. 

Shauri aliongeza ya kwamba, ukiondoa misaada ya wadau kama NMB na ruzuku ya Elimu Bure, eneo lingine wanalotegemea kupata pesa za kutatuzi changamoto za elimu na kukuza ufaulu, ni pamoja na asilimia 30 ya mapato ya ndani ya wilaya hiyo, iliyokamilisha ujenzi wa shule mpya 10 (tano za Msingi na tano za Sekondari). 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mchemba, alisema kuwa kwa sasa wananachi wa wilaya hiyo wamepunguza kasi ya kupiga simu kwake na kutoa malalamiko juu ya huduma mbovu zilizokuwa zinatolewa na wahudumu wa Kituo cha Afya Gairo, tuhuma walizokuwa wakipata kwa miaka mitatu sasa kutoka kwa jamii. 

Akizungumza wakati wa kupokea msaada kutoka NMB, Mchemba alisema ku
wa, kwa sasa baada ya kukaa na watumishi hao hali imeadilika na inaweza kupita mwezi mmoja bila kupigiwa simu na wananchi kutoa malalamiko juu ya huduma zisizo bora na bila shaka mambo yamebadiliko kituoni hapo. 

Aidha, Meneja Mahusiano na Biashara za Serikali, Kanda ya Mashariki wa Benki ya NMB, Anneth Kwayu, alisema kuwa Kituo cha Afya Gairo kimekuwa kikipokea vifaa mbalimbali kutoka NMB kwa miaka mitatu mfulilizo, katika jitihada za benki hiyo kusaidia kupunguza changamoto za afya. 

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Urambo, Angelina Kwingwa, akizungumza mapema jana kabla ya kupokea vitanda saba na mashuka ishirini na tano vyote vikiwa na jumla ya shilingi milioni tano kutoka benki ya NMB,ameipongeza benki hiyo kwa kupunguza adha za wagonjwa hasa wajawazito na watoto waliokuwa wakilala wawili hadi wanne kitanda kimoja.

WASTAAFU 10,000 WA PSSSF WALIOKUWA WANADAI MALIMBIKIZO YA PENSHENI YA MKUPUO NA ILE YA KILA MWEZI WALIPWA BILIONI 880

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) umefanya malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 880 kwa wastaafu elfu 10,000 ambao walikuwa wanadai malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ya kila mwezi, Meneja Kiongozi wa Mfuko huo Bi. Eunice Chiume amesema.

Amesema malipo hayo yamefanyika katika kipindi cha mpito kilichotolewa na serikali kuanzia Agosti 2018 hadi Februari 2019 hii ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu Mfuko huo uanze kutekeleza majukumu yake Agosti 1, 2018 baada ya serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii, ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.

“Ili kuhakikisha PSSSF inatoa huduma bora na za haraka, imefungua ofisi mikoa yote Tanzania bara na Visiwani na tunatoa wito sasa, kwa wale wastaafu takriban elfu 10,500 ambao bado taarifa zao hazijahakikiwa wafike kwenye ofisi zilizo karibu nao ili kukamilisha zoezi hilo muhimu linalofanyika kila mwaka.” Alisema Meneja huyo kiongozi wakati akizungumza na waendesha bloggers na waendesha mitandao ya kijamii kwenye ofisi za PSSSF, barabara ya Ohio jijini Dar es Salaam Juni 13, 2019.

Alisema uhakiki wa wastaafu sio kitu kipya ingawa mwaka huu zoezi hilo lilionekana kama ni geni.

“Lengo la uhakiki ni kuupa Mfuko fursa ya kufanya malipo kwa wakati, usahihi na kwa mtu anayepaswa kulipwa kwani taarifa zinaweza kubadilika ikiwa ni pamoja na zile za kibenki huenda muhusika akahama kutoka benki moja kwenda nyingine, mabadiliko ya wategemezi lakini haka kifo pia.” Alifafanua Bi. Chiume.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (katikati), akisikilzia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mmoja wa bloggers katika kikao baina ya meneja huyo na wamiliki na waendeshaji wa blogu hapa nchini. Kikao hicho kilicholenga kujenga mahusiano na kuutambulisha Mfuko huo Mpya kwa wamiliki hao wa mitandao ya kijamii kilifanyika ofisi za PSSSF jengo la Jubilee Tower jijini Dar es Salaam Juni 13, 2019.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akizungumza.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, akizungumza.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN), Bw. Joachim Mushi(kulia), akitoa maoni yake wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi. 
Bi. Eunice Chiume (kushoto), akimsikilzia Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN), Bw. Joachim Mushi (watatu kushoto), wakati wa kikao hicho.
Bi. Eunice Chiume, akisalimiana na Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network, (TBN) Bw. Joachim Mushi, wakati wa kikao hicho.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (watatu kushoto) na Afisa Uhusiano Mewandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi (wakwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Bloggers mara baada ya kikao hicho.

Mawakala wa Tigo wajinyakulia mamilioni

$
0
0

Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi kwa mawakala wa Tigo Pesa waliofanya vizuri katika promosheni inayojulikana ‘Wakala Cash In Promotion’. Kushoto ni Suleiman Hussein na kulia ni Vicky Ibrahim wote wakiwa ni washindi wakubwa kutoka kanda ya Pwani.
Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 3.5 Suleiman Hussein ambaye ni mmoja kati ya washindi wakubwa wawili wa promosheni ya ‘Wakala Cash In Promotion’ kutoka kanda ya Pwani.
Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2.5 Vicky Ibrahim ambaye ni mmoja kati ya washindi wakubwa wawili wa promosheni ya ‘Wakala Cash In Promotion’ kutoka kanda ya Pwani.
Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Katikati) akiwa na washindi wa ‘Wakala Cash In Promotion’ kutoka kanda ya Pwani Vicky Ibrahim (kulia) na Suleiman Hussein (kushoto) muda mfupi baada ya kuwakabidhi zawadi zao za fedha baada ya kuibuka washindi.


==========  =========  ======== = =======

Zaidi ya mawakala 200 wa huduma ya Tigo Pesa, wamejishindia zawadi za fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 160 kwenye promosheni ya mwezi mmoja inayojulikana kama ‘Wakala Cash In Promotion’.

Promosheni hiyo ya nchi nzima iliyozinduliwa mwezi Mei mwaka huu, ililenga kuwahimiza Mawakala wa Tigo Pesa nchini kufanya miamala kwa wingi ili kuweza kujishindia zawadi za fedha taslimu.

Akiwakabidhi zawadi washindi wa promosheni hiyo, kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha alisema, kampuni ya Tigo inathamini juhudi kubwa zinazofanywa na mawakala na kuongeza kuwa promosheni hiyo ililenga kuwazadia mawakala kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.

“Kampeni hii siyo tu inaonyesha dhamira yetu ya kuwekeza kwenye biashara lakini pia adhma yetu ya kugawana tunachokipata kutokana na biashara tunayofanya pamoja na wadau wetu. Promosheni hii ni fursa nyingine ya kuwazawadia mawakala wetu fedha taslimu na bonasi ambazo tunawaamini zitawapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kuendelea kufikisha huduma jumuifu za kifedha kwa wananchi wengi zaidi,” alisema

Kwa mujibu wa Pesha, pamoja na washindi wengine, washindi wawili wakubwa kutoka kila kanda walipatikana ambao ni Suleiman Hussein na Vicky Ibrahim kutoka Kanda ya Pwani, Peter Myovela na Stivin Katoto kutoka kanda ya Kusini, Anton Masawe na Athuman Mbwana kutoka kanda ya Kaskazini pamona na Harry Lwila na Joseph Kabeba kutoka Kanda ya Ziwa.

“Pamoja na washindi 2000 ambao wamejinyakulia zawadi mbali mbali za fedha taslimu kutokana na juhudi zao, tumepata washindi wengine wawili wakubwa kutoka katika kila kanda ambao kwa jumla wao ni 8 ambao wameweza kujishindia shilingi milioni 12 zaidi kutokana na jitihada zao. Tunawapongeza sana Mawakala wote ambao wamefanya vizuri na kujishindia zawadi na kwa wale ambao wahakuweza kushinda waongeze bidii ili waweze kuwa washindi katika promosheni zijazo,” alisema.

Akipokea zawadi ya shilingi milioni 3.5, Suleiman Hussein ambaye ni Wakala kutoka Kanda ya Pwani alisema “Napenda kuishukuru sana kampuni ya Tigo. Promosheni hii inaonyesha ni kwa kiasi gani sisi mawakala ni kiungo muhimu kwenye huduma nzima ya Tigo Pesa. Kuibuka mshindi kwenye promosheni hii ni rahisi sana kwa kuwa unahitajika kufanya kazi kwa bidii tu. Nawashauri Mawakala wenzangu wafanye kazi kwa bidi kwani Tigo Pesa inalipa,”

Vicky Ibrahim, Wakala aliyejishindia shilingi milioni 2.5 alisema amefurahi kuwa mshindi wa zawadi hiyo na kuwataka wanawake kuwa mawakala wa Tigo Pesa na wale ambao tayari ni mawakala kuwekeza zaidi na kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa Tigo Pesa.

“Tigo Pesa imetuwezesha sisi wanawake kujiajiri na kuboresha maisha yetu. Nawashauri wanawake wenzangu kujiajiri au kujiongezea vipato vyao kupitia Tigo Pesa. Kwa kuwa Mawakala pia wanaweza kujishindia zawadi kupitia promoshei hii kama ambavyo mimi nilivyojishi,” alisema

Rais Tshisekedi amaliza Ziara ya Kitaifa ya siku 2 hapa nchini Tanzania

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antoine Tshisekedi amemaliza Ziara ya Kitaifa ya siku 2 aliyoifanya hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 

Mhe. Tshisekedi ameagwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuelekea nchini Burundi. 

Mapema leo asubuhi Mhe. Rais Tshisekedi ametembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge Railway) katika eneo la Vingunguti Jijini Dar es Salaam na baadaye akatembelea Bandari ya Dar es Salaam ambayo hutumika kupitisha mizigo ya DRC. 

Akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais Tshisekedi amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli na baadaye viongozi hao wamezungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari. 

Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Tshisekedi kwa kufanya Ziara ya Kitaifa hapa nchini na kwa dhamira yake ya kukuza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya DRC na Tanzania hususani katika uchumi. 

Mhe. Rais Magufuli amesema kiwango cha biashara kinachofanywa kati ya Tanzania na DRC ni kidogo ikilinganishwa na ukubwa wa uhusiano na fursa zilizopo kati ya nchi hizo, ambapo katika mwaka uliopita biashara kati ya Tanzania na DRC ilikuwa na thamani ya shilingi Bilioni 305.375, wafanyabiashara wa DRC walikuwa wamewekeza nchini Tanzania miradi 8 yenye thamani ya shilingi Bilioni 13.144 na kukiwa na Watanzania wachache ambao wameweka nchini DRC. 

Amefafanua kuwa japo kuwa sekta ya usafirishaji inaridhisha kidogo kwa DRC kuongeza mizigo inayopita Bandari ya Dar es Salaam kutoka tani Milioni 1.176 ya mwaka 2017 hadi kufikia tani Milioni 1.78 ya mwaka 2018, kuna haja ya kuchukua hatua madhubuti zaidi za kukuza biashara na uwekezaji ikiwemo kuondoa vikwazo, kutumia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo madini, uvuvi, kilimo, ujenzi wa viwanda na kulitumia ipasavyo soko la nchi hizo lenye jumla ya watu Milioni 140. 

Kwa upande wa Tanzania, Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kujenga reli ya kati (SGR), kupanua Bandari ya Dar es Salaam, kuanzisha huduma za pamoja za bandari kwa saa 24 (siku zote 7 za wiki) na kuimarisha miundombinu ya barabara katika njia 8 za kuingia na kutoka DRC, Tanzania imeongeza muda wa kusubiri bandarini kutoka siku 24 hadi 30 kwa mizigo ya DRC, imeondoa katazo la ufunguaji makontena na kufuta tozo ya kusindikiza mizigo hadi mpakani mwa Tanzania na DRC. 

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema Tanzania itaikarabati meli ya MV. Liemba inayotoa huduma kati ya Tanzania (Kigoma) na DRC, itajenga meli mpya mbili ambapo moja itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na mizigo tani 400 na ya pili itakuwa meli ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 2,000 na ameafiki mapendekezo ya Mhe. Rais Tshisekedi ya reli ya kati ya Tanzania kujengwa kutoka Isaka – Rusumo – Kigali hadi Mashariki ya Kongo ili kufikisha mizigo moja kwa moja nchini DRC. 

Mhe. Rais Magufuli amewataka Mawaziri na Wataalamu wa Tanzania na wenzao wa DRC (watakaoteuliwa) ndani ya mwaka huu, kuitisha kikao cha Kamati ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission – JPC) ambacho hakijawahi kufanyika tangu mwaka 2002 ili kujadili na kurejesha maeneo muhimu ya ushirikiano ikiwemo ushirikiano katika usafiri wa anga kati ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na Shirika la Ndege la Congo (Congo Airways). 

Mhe. Rais Magufuli amemtakia heri Mhe. Rais Tshisekedi katika uongozi wake na amemshauri kusimama kidete kutatua matatizo ya wananchi wa DRC huku akisisitiza kuwa kwa utajiri wa DRC, uchumi wa nchi hiyo haupaswi kukua kwa kiwango kidogo cha asilimia 4. 

Kwa upande wake, Mhe. Rais Tshisekedi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumwalika kufanya Ziara ya Kitaifa hapa nchini na amebainisha kuwa lengo la ziara yake ni kuimarisha na kukuza zaidi udugu, urafiki na uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na DRC. 

Mhe. Tshisekedi amesema katika mazungumzo yake na Mhe. Rais Magufuli wamekubaliana kuwa bila amani jitihada za maendeleo katika eneo lote la maziwa makuu hazitafanikiwa, hivyo wana kila sababu ya kuhakikisha kunakuwa na amani ya kudumu pamoja na kutumia vizuri fursa mbalimbali za kukuza uchumi ukiwemo ukanda wa ziwa Tanganyika wenye urefu wa kilometa 554. 

Amesema ana matumaini kuwa JPC itakayofanyika itatatua changamoto zote za kukuza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na DRC na ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Mhe. Rais Magufuli. 

Pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa ahadi yake ya kuunga mkono ombi la DRC kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Rais Tshisekedi ameahidi kuhudhuria Mkutano wa 39 Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu hapa Tanzania na amebainisha kuwa anaamini kuwa SADC ni jumuiya yenye fursa na manufaa makubwa ya kiuchumi. 


Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU 
Dar es Salaam 
14 Juni, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo
Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo anayeagana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa afrika Mashariki Mhe. Faraji Kasidi Mnyepe baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda wakati wakisumbiri ili kumuaga mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo anayeagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Profesa palagamaba Kabudi baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo anayeagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiagana kwa furaha na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia 54 ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili leo Juni
14, 2019 
PICHA NA IKULU

Fedha za Biko kumalizia ujenzi wa nyumba ya mshindi Dodoma

$
0
0
Mwandishi Wetu, Dodoma
 
Mshindi wa Biko jijini Dodoma, Hamad Ibrahim Ramadhan, amesema kwamba ameamua fedha zake za ushindi sh milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko kumalizia ujenzi wa nyumba yake ili kuepuka adha alizokuwa anakutana nazo.

Mshindi huyo alisema kwamba kabla ya fedha hizo, aliamua kuhamia kwenye nyumba yake yenye chumba kimoja akiishi na familia yake, jambo lililotatuliwa na ujio wa fedha za Biko nchini Tanzania.

Naye mke wa mahindi huyo, Mwashabani Bakari Mwingi, aliishukuru Biko kwa kupunguza makali ya maisha yao kwa sababu nyumba yao itakamilika na wataanza kuishi maisha bora.

Mama huyo alisema kuwa maisha ni magumu, hivyo mumewe kushinda Biko ni jambo la kumshukuru Mungu, maana hakuna aliyetarajia kwamba kuna siku watapata suluhu ya changamoto zao za kimaisha katika familia yao.

Biko mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa kufanya miamala kuanzia sh 500 na sh 1000 na kuendelea, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba ni 2456, huku washindi wa papo kwa hapo wakiibuka na kuanzia sh 5000 hadi sh milioni moja.

Mbali na zawadi za papo kwa hapo, Biko inatoa ushindi mnono katika droo zake kubwa za Jumatano na Jumapili, ambapo washindi wake huibuka na mamilioni pamoja na bodaboda Ikiwa na lengo kubwa la kugawa utajiri kwa Watanzania wote.

JESHI LA MAGAREZA LAISHUKURU NMB KWA USHIRIKIANO KIMICHEZO

$
0
0
JESHI la Magereza limekabidhi cheti maalum cha kuishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa fulana ambao iliutoa kwa wanamichezo walioshiriki tamasha la michezo kati ya Magereza Bara na Vyuo vya Mafunzo Zanzibar.

Cheti hicho maalum kimekabidhiwa leo na Ofisa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Matilda Mlawa kwa Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite ikiwa ni kutambua mchango wa benki hiyo mara kwa mara.

Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la Magereza kabla ya kukabidhi cheti hicho, afisa huyo alisema wataendelea kujenga ushirikiano mzuri na benki hiyo kwa kuwa inawathamini hata maeneo mengine ya kijamii.

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite alilishukuru Jeshi la Magereza kwa kutambua mchango na mahusiano mazuri kati ya pande hizo na kusema NMB itaendeleza ushirikiano huo. Aliongeza kwa sasa Benki hiyo imekuja na bidhaa bora zaidi ambazo wateja wao hasa taasisi zinazofanya biashara nao itafurahiya bidhaa hizo.
 Maofisa washiriki katika tukio hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo fupi. 
 Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Ofisa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Matilda Mlawa (wa pili kulia) kwa kutambua mchango wa benki hiyo ambao imekuwa ikiutoa kwa wanamichezo wa Magereza. Wa kwanza kulia ni Ofisa Michezo Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Mrakibu waMagereza, Joseph Siwale pamoja na maofisa wa NMB wakishuhudia tukio hilo.

 Ofisa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Matilda Mlawa (wa pili kushoto) akimkabidhi cheti maalum cha shukrani Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite kwa kutambua mchango wa benki hiyo ambao imekuwa ikiutoa kwa wanamichezo wa Magereza. Wa kwanza kushoto ni Ofisa Michezo Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Mrakibu waMagereza, Joseph Siwale pamoja na maofisa wa NMB (kulia) wakishuhudia tukio hilo.

Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images