Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MAKAMPUNI,MASHIRIKA YAUNGANA NA LA PRINCE PUB KUTOA ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA

$
0
0
Wadau wa Maendeleo mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Kampuni ya La Prince Pub inayojihusisha na biashara ya uuzaji vinywaji na chakula Mjini Shinyanga wamesherehekea Sikukuu ya Miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kutembelea na kuwapatia misaada mbalimbali wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Miongoni mwa zawadi zilizotolewa kwa akina mama na watoto ni pamoja na sabuni,mafuta ya kujipaka juisi,poda, miswaki,dawa za meno,matunda, toilet papers,biskuti,maji na zawadi zingine.

Wadau walioungana na wafanyakazi wa La Prince Pub kutembelea na kutoa misaada kwa wagonjwa leo Aprili 26,2019 ni pamoja na Kampuni ya Lulekia,Jambo Food Products Co. Ltd,Astro Secure Co. Ltd,Uptown Holdings Co.Ltd,Msirikale Microfinance,24 Security Tanzania,Ommy Fashion, Gvenwear,Shirika la TVMC,Dellah Car Traders,Luxury Pub,Friends of Bhoke na Malunde 1 blog.


Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo,Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William alisema wameamua kuungana na wadau wa maendeleo mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii inayowazunguka.

Alisema zawadi hizo kwa wagonjwa zimetolewa kupitia Mpango maalumu ulioanzishwa na La Prince Pub unaojulikana kwa jina la ‘La Prince Charity Movement’ kwa lengo la kuisaidia jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali,makampuni na wafanyabiashara mbalimbali. 

“Tumefika hapa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutoa pole kwa wagonjwa na kuwapa misaada mbalimbali,tumejumuika sisi wafanyakazi wa La Prince na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo kutoka kwenye mashirika na makampuni ambao tumeungana kuja kurudi kurudisha fadhila kwa jamii kwa kutoa misaada kwa wagonjwa katika wodi za akina mama na watoto",alisema.

“Tukiwa sehemu ya jamii tumeona ni busara zaidi katika siku hii ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo hatufanyi sherehe za kitaifa,sisi tumeona tufanye sherehe ndogo ya kuwapa pole wanaoumwa na wenye mahitaji maalumu”,aliongeza William.

“Kilichotusukuma sisi ni moyo wa upendo,sisi tuna mpango maalumu unaitwa La Prince Movement ambapo kila mwezi tumeamua kuunganisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga kutoa misaada mbalimbali katika kada mbalimbali, leo tumeanza na hospitali na hivi karibuni tutambelea magereza”,alieleza Mkurugenzi wa La Prince Pub.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akizungumza katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakati wadau mbalimbali wa maendeleo walipotembelea wagonjwa na kuwapatia zawadi akina mama na watoto waliolazwa katika hospitali hiyo leo Aprili 26,2019 ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mmoja wa wafanyakazi wa La Prince Pub akiweka sawa zawadi mbalimbali zilizotolewa na wadau wa maendeleo mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya akina mama na watoto waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya wafanyakazi wa La Prince Pub wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali.
Wadau wa maendeleo wakiwa na zawadi zao wakijiandaa kuingia katika wodi mbalimbali katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kugawa zawadi hizo kwa wagonjwa.
Wadau wa maendeleo wakielekea katika wodi za watoto.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akizungumza katika moja ya wodi akielezea lengo la wadau kufika katika hospitali hiyo.
Wadau wa maendeleo wakiwa wodini na zawadi zao kabla ya kuanza kuzigawa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akisalimiana na mmoja wa Madaktari katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga aliyekutwa wodini.
Wadau wakitoa zawadi kwa mama aliyelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akizungumza katika moja ya wodi za akina mama.
Wafanyakazi wa Ommy Fashion wakitoa zawadi kwa mgonjwa.
Wafanyakazi wa La Prince Pub wakitoa zawadi katika wodi ya watoto.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akisalimia akina mama katika wodi ya watoto.
Utoaji zawadi ukiendelea katika wodi ya akina mama waliojifungua. katikati ni Bhoke Wambura, muanzilishi wa Friends of Bhoke.
Wadau wakiongozwa na Mkurugenzi wa shirika la TVMC,Musa Jonas Ngangala (katikati) wakikabidhi zawadi ya ndoo ya sabuni na zawadi zingine kwa mama aliyejifungua watoto mapacha wa kiume.
Wafanyakazi wa La Prince wakimsalimia na kumpa pole pamoja na zawadi mama wa mmoja mfanyakazi mwenzao aliyelazwa katika wodi ya wanawake.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AITAKA SUMA JKT KUMKABIDHI JENGO JIPYA LA UHAMIAJI JIJINI DODOMA BAADA YA MIEZI 18, WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO, LEO

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia), Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, wakisaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Ujenzi wa Jengo hilo ambalo litakua na ghorofa nane unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 18. Katibu Mkuu ameitaka Suma JKT kumkabidhi jengo hilo kwa wakati.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na wa Wizara yake, kabla ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, jijini Dodoma, leo. Suma JKT wanatarajia kujenga jengo hilo ambalo litakua na urefu wa ghorofa nane, na litakamilika baada ya miezi 18. Kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Martin Busungu. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, akizungumza kabla ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, leo. Suma JKT ndiyo Mkandarasi wa jengo hilo lenye urefu wa ghorofa nane, na linatarajiwa kukamilika baada ya miezi 18. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kushoto), akimuaga Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taida (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, mara baada ya kumaliza kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, jijini Dodoma, leo. Suma JKT wanatarajia kujenga jengo hilo ambalo litakua na urefu wa ghorofa nane, na litakamilika baada ya miezi 18

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (watatu kushoto), Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu (watatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa JKT na Wizara, mara baada ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Ujenzi wa Jengo hilo ambalo litakua na urefu wa ghorofa nane unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 18. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

………………..

Na Mwandishi Wetu, MOHA

KATIBU Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu amelitaka Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT), kujenga jengo la Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kwa ufanisi mkubwa na akabidhiwe jengo hilo baada ya miezi 18.

Akizungumza kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano wa ujenzi wa jengo hilo, kati ya Wizara yake na Suma JKT ambayo iliongozwa katika kikao hicho na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, iliyopo Mji wa Serikali, Kata ya Mtumba, jijini Dodoma, leo, alisema hana shaka na uwezo wa Mkandarasi huyo, ila anaamini ujenzi huo utakua bora na utakamilika kwa wakati.

“Baada ya maandalizi ya ujenzi huu kuchukua muda mrefu lakini hatimaye tumekamilisha, hivyo nawaomba ndugu zangu tufanye kazi vizuri kabisa, na leo ndio siku ya kusaini mkataba kwa ajili ya ujenzi huu,” alisema Meja Jenerali KIngu.

Meja Jenerali Kingu alisema Wizara yake itafuatilia kwa karibu ujenzi huo, ambapo Mkandarasi ni Suma JKT na Mshauri Elekezi ni Chuo Kikuu cha Ardhi, hivyo jengo hilo anatarajia kuwa bora zaidi kutokana na uwepo wa wadau hao.

Kwa upande wake, Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Busungu, alisema aliishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuwa na imani na Suma JKT na kuipa kazi ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya uhamiaji jijini Dodoma.

“Tunaishukuru Wizara yako kwa kutupa kazi hii ya ujenzi wa jengo hili ambalo ni la ghorofa nane, tunaahidi kulikamilisha baada ya miezi 18, na tutapiga kadiri inawezekana, tupo tayari kwa kazi yenye uweledi wa kuzingatia muda na ubora ambao utawauza zaidi Suma JKT,” alisema Meja Jenerali Busungu.

Mkataba huo ulisainiwa na viongozi hao huku ukishuhudiwa na wanasheria wa taasisi hizo ambao ni Mkurugenzi wa Sheria, Marlin Komba wa Wizara hiyo na Kapteni Joyce Mwaikofu kutoka JKT.

UBALOZI URUSI WAADHIMISHA MUUNGANO KW KUTANGAZA BIDHAA ZA TANZANIA

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Maj. Jen. Mstaafu Simon Mumwi akitoa neno la ukaribisho kwa wageni mbalimbali walioalikwa kushiriki kilele cha kuadhimisha Siku ya Taifa ya Tanzania (Maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano) yaliyofanyika jijini Moscow tarehe 26 Aprili 2019. Maadhimisho hayo yalipambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo Maonesho ya bidhaa na vivutio vya utalii vya Tanzania; kukabidhi vyeti kwa wadau mbalimbali ili kutambua mchango wao katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania, hususan katika sekta ya utalii, uwekezaji, sanaa, lugha na utamaduni pamoja na kutoa fursa ya kubadilishana mawazo baina ya Mabalozi na taasisi za Urusi zinazojihusisha na masuala ya uwekezaji. Mwingine katika picha ni Naibu Mkurugenzi wa Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Bw. George Cherpisk. 
Naibu Mkurugenzi wa Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Bw. George Cherpisk akisoma hotuba katika maadhimisho hayo. 
Wageni waalikwa wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi wa nchi mbalimbali zenye uwakilishi Urusi wakisikiliza hotuba. 
Mhe. Balozi Mumwi na Waheshimiwa Mabalozi wa mbalimbali wa nchi za Afrika zenye uwakilishi nchini Urusi wakikata keki ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanzania. 
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Maj. Jen. Mstaafu Simon Mumwi akikabidhi cheti kwa mmoja wa wadau wanaochangia maendeleo na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania. 
Mdau akipokea cheti chake ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya Tanzania. 
Picha ya pamoja ya baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi, wageni, maafisa wa ubalozi na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Urusi walioshiriki katika maadhimisho hayo.

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 7 KWA WAKUU WA MIKOA INAYOZALISHA DHAHABU KUFUNGUA MASOKO YA MADINI

$
0
0
Na Ripota Wetu-MAELEZO

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku saba kwa Wakuu wa Mikoa inayozalisha dhahabu nchini kushirikiana na Wizara ya Madini katika kufungua masoko ya madini ikiwemo dhahabu ili kuifanya sekta ya madini kuweza kuleta tija ya kiuchumi kwa Watanzania wote hususani wachimbaji wadogo.

Akizungumza Mkoani Mbeya leo Jumamosi (April 27, 2019) wakati wa katika hafla ya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi la barabara ya Mbeya-Lwanjilo-Chunya-Makongosi yenye urefu wa Kilometa 111, Rais Magufuli alisema Serikali anayoiongoza kamwe haitokubali kuona wachimbaji wadogo wakiendelea kuteseka nchini.

Aliongeza kuwa tangu mwaka 2017, Serikali imepitisha Sheria Bungeni inayotoa maelekezo kuhusu usimamizi wa sekta ya madini nchini na hivyo anashangwa na baadhi ya Viongozi wake hususani Wakuu wa Mikoa inazozalisha dhahabu kusuasua katika kusimamia maelekezo ya maelekezo yake aliyoyatoa katika siku za nyuma.

Alisema kuwa Serikali pia imefuta kodi mbalimbali za madini na kuendelea kuwahamasisha wachimbaji wadogo kupeleka dhahabu zao katika masoko hayo, lakini hadi sasa baadhi ya Wakuu wa Mikoa wameshindwa kujenga masoko hayo, pamoja na faida mbalimbali zinazopatikana katika masoko hayo ikiwemo kuepusha dhuluma kwa wachimbaji, kupata dhahabu yenye ushindani pamoja na kuzuia upotevu wa kodi ya Serikali.

Aliongeza kuwa katika mkutano wake alioufanya hivi karibuni na Viongozi wa Wizara ya Madini na Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara inayozalisha Dhababu, alitoa maelekezo ya kufungua masoko ya madini katika maeneo yao, ingawa ni Mkoa wa Geita pekee uliyotekeleza maelekezo hayo wakati ujenzi huo hauhitaji nyumba au eneo kubwa.

“Kama Mkoa wa Geita, umeweza kuwa na Kituo cha soko la kuuzia madini, nashangazwa kwanini Wakuu wengine wa Mikoa wanashindwa kutekeleza maelekezo hayo, hivyo hili ni agizo kwa Wakuu wa Mikoa ya Katavi, Singida na Arusha kuhakikisha kuwa watatekeleza maagizo haya” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema Serikali anayoiongoza haiwezi kuwa na Viongozi na Watendaji wasiotaka kutekeleza maagizo, hivyo ametoa kipindi cha muda huo kuhakikisha kuwa vituo hivyo vinafunguliwa na hivyo kuwahakikishia masoko ya uhakika wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakidhulumiwa dhahabu zao na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.

Aidha Rais Magufuli aliutaka Uongozi wa Mkoa wa Mbeya hususani Wilaya ya Chunya kuhakikisha kuwa soko hilo la dhahabu linafunguliwa haraka iwezekanavyo kwa kuzingatia kuwa rasilimali zote muhimu za kufanikisha maagizo hayo zipo ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vitatumika kwa ajili ya ulinzi wa madini ya dhahabu wakati wa mauzo hayo yakifanyika.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, alisema kuwa suala la kujiletea maendeleo kwa Watanzania linacheleweshwa na baadhi ya Viongozi Watendaji Serikali kwani wananchi hususani wachimbaji wadogo wa madini wamekuwa na juhudi kubwa za kujiletea maendeleo yao lakini wamekuwa wakikatishwa tamaa pamoja na juhudi kubwa wanazozionyesha katika kuchimba dhahabu.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Dotto Biteko alisema tangu kutungwa kwa Sheria ya Madini mwaka 2017, Serikali imeweza kuokoa kiasi kikubwa cha madini kutoroshwa nje ya nchi, ambapo katika Wilaya ya Chunya ambayo ni Wilaya ya pili kwa uzalishaji wa dhahabu Serikali imeweza kutoa jumla ya kilo 30 zilizokuwa zikitoroshwa nje ya nchi kutokana na kukosekana kwa mtambo wa kuchenjulia madini.

Mara baada ya kujiridhisha na taratibu zote za kisheria, tumeweza kufungua mitambo 38 ya kuchenjulia dhahabu hapa Chunya, ambayo tulisimamisha shughuli hizi huko nyuma kutokana na utoroshaji mkubwa uliokuwa ukifanyika” alisema Biteko.
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA MBEYA-LWANJILO-CHUNYA KM 72 NA KUWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA CHUNYA-MAKONGOLOSI KM 39 CHUNYA MKOANI MBEYA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, pamoja na viongozi mbalimbali Wabunge, Mawaziri, Viongozi wa Mkoa wa Mbeya, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya Chunya hadi Makongolosi km 39 itakayojengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Chunya mkoani Mbeya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chhalamila mara baada ya kufungua barabara ya kutoka Mbeya-Lwanjilo-Chunya yenye jumla ya kilometa 72.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa barabara itakayojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Chunya hadi Makongolosi km 39.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, pamoja na viongozi mbalimbali Wabunge, Mawaziri, Viongozi wa Mkoa wa Mbeya, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya  Mbeya-Lwanjilo-Chunya yenye jumla ya kilometa 72 iliyokamika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Chunya mkoani Mbeya.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa Sabasaba Wilayani Chunya kwa ajili ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa Hadhara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono kuwasalimia wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Sabasaba Chunya kabla ya kuwahutubia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mhandisi Profesa Ninatubu Lema kutoka Wizara ya Ujenzi wakati alipowasili katika uwanja wa Sabasaba Chunya mkoani Mbeya. PICHA NA IKULU

Mongella amwakilisha vyema Pinda harambee wilayani Sengerema

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella jumamosi Aprili 27, 2019 amemwakilisha Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa, Mizengo Peter Kayanza Pinda kwenye harambee katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana wilayani Sengerema.

Harambee hiyo imelenga kukusanya fedha kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki vya kwaya ya “New Life” ya kanisa hilo linaloongozwa na Mchungaji Leonard Giligwa pamoja na gari kwa ajili ya Parishi ya Bomani wilayani humo ambapo zaidi ya shilingi milioni 20 zimepatikana ikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana Sengerema, Leonard Giligwa (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) picha maalum ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa, Mizengo Peter Kayanza Pinda kwenye harambee hiyo ambapo Pinda alikuwa mgeni rasmi na akawakilishwa na Mongella.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella, Mchungaji wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana Sengerema Leonard Giligwa, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi pamoja na Mkuu wa Wilaya Ukerewe Colonel Magembe wakiwa kwenye harambee hiyo.
Mlezi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Lweru, Askofu Godfrey Mbelwa akiwa kwenye harambee hiyo.
Baadhi ya washirika na wananchi waliohudhuria harambee hiyo.
Tazama Vidio hapa chini

WAZIRI MKUU AWAAGA WATALII 1,000 KUTOKA ISRAEL

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimvalisha kikoi Mkurugenzi wa Kampuni ya Another World Shlomo Carmel, iliyoleta Watalii 1000 kutoka nchini Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA Aprili 27, 2019. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Kigwangala.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiagana na watalii kutoka nchini Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA Aprili 27, 2019. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Another World Shlomo Carmel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

…………………..

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watalii kutoka Israel wakawe mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania pindi wakirudi huko kwao. 

Ametoa wito huo leo mchana (Jumamosi, Aprili 27, 2019) kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) wakati akiwaaga watalii 274 walioondoka nchini leo mchana kurejea kwao.

Watalii hao ni miongoni mwa watalii 1,000 waliowasili nchini tangu Aprili 20, mwaka huu na kutembelea maeneo kadhaa ya vivutio kwenye ukanda wa Kaskazini. Kundi la kwanza liliondoka jana usiku, la pili leo mchana, la tatu litaondoka leo saa 10 jioni na la mwisho litaondoka leo saa 2 usiku.

Waziri Mkuu amewaomba watalii hao wapange muda wao na watafute fursa nyingine ya kuja Tanzania kutembelea mbuga nyingine za ukanda wa Kusini pamoja fukwe nzuri za Zanzibar. “Tumefarijika sana na ujio wenu na tunaamini mtaenda kutangaza mazuri mliyoyaona kwa wengine. Tunazo mbuga nyingine za Rubondo, Katavi, Ngorongoro, Ruaha, Selous, fukwe nzuri za Zanzibar na mlima Kilimanjaro,” amesema.

Pia amewashukuru mawakala wa utalii nchini pamoja na Mkurugenzi wa kampuni wakala wa utalii ya Another World kutoka Israel Bw. Carmel Shlomo kwa kuamua kuitangaza Tanzania kama kivutio namba moja cha utalii barani Afrika.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla aliwashukuru watalii hao kwa kuamua kuitembelea Tanzania licha ya kuwa wangeweza kwenda maeneo mengine yaliyo jirani na Israel.

“Natambua uchovu mlionao sababu ya urefu wa safari kutoka Israel hadi hapa, lakini nawashukuru kwa uamuzi wenu wa kuja Tanzania katika kipindi hiki ambacho tunafanya maboresho kwenye sekta ya utalii ili tuweze kutoa huduma bora zaidi,” alisema.

Alisema Tanzania ina vivutio vingi vya utalii na hii inawezekana kwa sababu iliamua kutenga zaidi ya robo ya ardhi yake kwa ajili ya mbuga na hifadhi za taifa za wanyama.

Pia alizishukuru kampuni za utalii za Tanzania na Israeli kwa kushirikiana kuleta watalii wengi kiasi hicho. Alizitaja kampuni hizo kuwa ni Excellent Guides, Mauly Tours and Safaris, Matembezi, Leopard Tours and Safaris, African Queen Adventures na TAWISA zote za kutoka Tanzania. Kamuni za kutoka Israeli ni Another World, My Trip, Camel na Safari Company.

Kwa upande wao, baadhi ya watalii kutoka Israel wamesema wamevutiwa na waliyaona hapa nchini na wameahidi kurudi tena ili watembelee vivutio vingine zaidi. Bibi Naomi Peer Moscovich na mabinti zake Dana na Lihi wamesema wamevutiwa na wingi wa wanyama waliowaona lakini pia wameguswa na ukarimu wa watu waliokutana nao.

“Tunaondoka na neno moja kubwa nalo ni kwamba hatutaisahau Tanzania (we say Unforgettable Tanzania) na tutarudi tena hivi karibuni,” alisema Dana Peer Moscovich ambaye ni dada yake Lihi.

Hafla ya kuwaaga watalii hao ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini, Jaji Thomas Mihayo, Katibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Adolf Mkenda na Wakuu wa Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. Mama Anna Mghwira na Bw. Mrisho Gambo.

SPIKA NDUGAI AFUNGUA WARSHA YA UFUATILIAJI NA TATHMINI ZA SERA NA PROGRAMU ZA MAENDELEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wabunge na Wajumbe Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania na wawezeshaji kutoka nchi za Uganda na Srilanka(hawapo kwenye picha) wakati akifungua warsha ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na Programu za Maendeleo kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania (TanEA), Dkt. Francis Mwijande, Katibu wa Wabunge Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania , Dkt. Semesi Sware (wa pili kushoto) na Mjumbe kutoka Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania (TanEA), Ndg. Isaac Kiwango
V25A3557A
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wabunge na Wajumbe Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania (TanEA) pamoja na wawezeshaji kutoka nchi za Uganda na Srilanka wakati akifungua warsha ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na Programu za Maendeleo kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
V25A3513A
Katibu wa Wabunge wa Afrika upande wa Tanzania Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania (wa pili kushoto), Dkt. Semesi Sware akizungumza na Wabunge Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania(hawapo kwenye picha) na wawezeshaji kutoka nchi za Uganda na Srilanka wakati akifungua warsha ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na Programu za Maendeleo kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Mwenyekiti Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania (TanEA), Dkt. Francis Mwijande (wa pili kulia) na Mjumbe kutoka Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania (TanEA), Ndg. Isaac Kiwango
V25A3592A
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia warsha iliyotolewa na Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania (TanEA) kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
V25A3704A
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania na wawezeshaji kutoka Uganda na Srilanka baada ya kufungua warsha ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na Programu za Maendeleo tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
V25A3672A
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge, Wajumbe Chama cha Tathmini na Ufuatiliaji Tanzania na Wawezeshaji kutoka nchi za Uganda na Srilanka baada ya kufungua warsha ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na Programu za Maendeleo tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WASHIRIKI IBADA YA KUSIMIKWA KWA ASKOFU GERVAS NYAISONGA KUWA ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU KATOLIKI MKOANI MBEYA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimpongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga mara baada ya kusimikwa kuwa Mkuu wa Jimbo hilo.
8
9..
 Mke wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli  Mama Janeth Magufuli akimpongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga mara baada ya kusimikwa kuwa Mkuu wa Jimbo hilo.
1
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akiongoza Ibada ya kumsikima Askofu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya katika Ibada iliyofanyika katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
23
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akiwa amekaa kwenye kiti wakati Ibada ya kusimikwa kwake ikiendelea katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
5
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akisalimiana na Mapadre wa Kanisa Katoliki mara baada ya kusimikwa Rasmi kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya.
6
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akiwa ameketi kwenye Kiti cha Uaskofu pamoja na Maaskofu wengine wa Kanisa Katoliki nchini.

9.11
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akipongezwa na Maaskofu mbalimbali wa Kanisa Katoliki mara baada ya kusimikwa Rasmi. PICHA NA IKULU
12
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akiwa amekaa kwenye kiti wakati Ibada ya kusimikwa kwake ikiendelea katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
034A1097
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikusanya Sadaka kwa waumini mbalimbali waliokusanyika katika uwanja wa Sokoine katika ibada ya Kumsimika Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga
034A1098034A1101034A1135034A1143034A1190034A1215034A1218

Naibu Waziri Shonza awataka Watanzania Kuandaa Mashindano ya Kusaka Vipaji vya Muziki kuanzia ngazi ya Wilaya Mpaka Mkoa

$
0
0


Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watatu kulia) akiwasili katika viwanja vya   Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU) jana na kupokewa na vijana wanaoshiriki mashindano  ya Kabati Star Search ambapo mashindano hayo yanafanyika hapo, watatu kushoto ni  Ritha Kabati Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa ambaye ndiye mwandaaji wa mashindano hayo.
PIX 4 B
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (wapili kushoto)akisalimiana na mchekeshaji maarufu Baraka Mwakipesile anayeigiza kama Rais Magufuli ambapo kwa sasa anajulikana  kama Baraka Magufuli mara baada ya uzinduzi wa mashindano ya Kabati Star Search yaliyofanyika jana Mkoani Iringa, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mufundi Bw.Netho Ndilito.
PIX 4PIX 5
Mmoja ya washiriki wa mashindano ya  Kabati Star Search Yahya Hamadi  kutoka Kata ya Mwangata  Mkoani  Iringa  akionyesha uwezo wake kwa kuimba  wimbo wa Msanii Young Killer katika mashindano hayo yaliyofanyika jana ambapo yalizinduliwa na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (hayupo pichani).
PIX 6
Mmoja ya washiriki wa mashindano ya  Kabati Star Search Sophia Kalinga kutoka Kata ya Gangilonga  Mkoani  Iringa  akionyesha uwezo wake kwa kuimba  wimbo wa You Raise Me Up  kutoka kwa msanii Josh Groban katika mashindano hayo yaliyofanyika jana Mkoani hapo.
PIX 7
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watatu kushoto ) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Shindano la Kabati Star Search mara baada ya uzinduzi wa shindano hilo lililofanyika jana  Mkoani  Iringa, wapili kushoto ni muandaaji wa shindano hilo Ritha Kabati Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa .
PIX 8
Msanii wa Mkoa wa Iringa Ezra Msiliova maarufu kama Eze Nice akiimba  kwa hisia wimbo  wa kuisifia Tanzania mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza wakati wa uzinduzi wa Shindano la Kabati Star Search lilofanyika jana Mkoani Iringa.
………………………………………………………………………………

Na Anitha Jonas- Iringa

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ameto wito  kwa  wadau mbalimbali nchini kujitokeza kuandaa Mashindano ya kusaka vipaji vya Muziki kwa vijana kwa kuanzia ngazi za Mikoa na Wilaya.
Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo jana Mkoani Iringa alipokuwa akizindua Tamasha la Ritha Kabati Star Search lililolenga kusaka  vipaji vya vijana wanaojua kuimba muziki na tamasha hilo limekusanya vijana zaidi ya 150 kutoka maeneo mbalimbali ya wa Mkoa wa Iringa.

“Ninapenda kumpongeza Mhe.Ritha Kabati  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kwa kuandaa Tamasha lenye tija kwa taifa kama hili, pia ninaomba wadau mbalimbali wenye uwezo kuandaa matamasha kama haya kwa kuanzia ngazi za mbalimbali ndani ya mikoa na wilaya zetu kwa ndiko waliko vijana wenye vipaji,  tuwasaidie kufikia ndoto zao kwa manufaa ya taifa,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika uzinduzi huo wa Kabati Star Search Naibu Waziri huyo alimtaka Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Iringa kuandika barua kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ya kuomba wataalamu kuja kutoa mafunzo kwa wasanii chipukizi wa muziki wa mkoa huo kwa lengo la kuwa ongezea maarifa wasanii hao.

Naye muandaaji wa Tamasha hilo Mhe.Ritha Kabati alieleza kuwa amekuwa akiwaona  vijana wa mkoa huo na kuwa wanavipaji  ila wamekuwa wakikosa jukwaa la kuonyesha vipaji vyao na ndiyo maana aliamua kuanzisha mashindano hayo ambayo yatawainua vijana wa mkoa wa Iringa nao kuanza kusikika Kitaifa na Kimataifa kama wasanii wengine maarufu hapa nchini.

“Katika kuhakikisha mashindano haya yanaleta mafanikio nilizungumza na mmoja wa walezi  wasanii wa Muziki  nchini  Bw. Said Fella Maarufu kama Mkubwa Fella kuhusu kuwasaidia washindi wa mashindano haya na tukakubaliana kuwa mshindi wa kwanza mpaka watatu  atawachukua na kwenda kuwafunza vizuri kisha watarekodi  nyimbo zao na pia wataimba na wasanii maarufu hapa nchini na atahakikisha na hizo nyimbo zao zinapigwa katika vituo vya redio na televisheni mbalimbali nchini,”alisema Kabati.

Pamoja na hayo Kabati alieleza kuwa vijana wa Iringa wamesema wanataka nao Mkoa wao uonyesha  kuwa unavipaji vyenye uwezo mkubwa wakufikia ngazi za Kimataifa kwani  kupitia mashindano ya mpira wa miguu ya Kabati Challenge Cup vijana watatu tayari wamechukuliwa na timu za mpira za Afrika Kusini kwa lengo la kwenda kuchezea timu za vijana na watakuwa wanasomeshwa huko pia .

Halikadhalika na mmoja wa washiriki wa mashindano hayo  Yahya Hamadi alimshukuru mbunge huyo wa viti maalum kwa kuandaa mashindano hayo na ameahidi kuwa atajitahidi kufanya vizuri kwani  anaamini  kupitia jukwaa hilo nae anaweza kuja kuwa msanii maarufu katika Taifa.

Hata hivyo Naibu Waziri Shonza aliwasihi majaji wa mashindano hayo kutenda haki katika maamuzi wanayoyafanya kwani  wao ndiyo wenye dhamana ya  kutoa msanii atakayetangaza mkoa na taifa kwa ujumla katika ngazi za Kimataifa,ambapo mmoja  wa majaji hao Bw.Roger Magoha kwa niaba ya wenzake aliahidi kusimamia hilo.

WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA

$
0
0

 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Watalii kutoka Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA, kutoka kushoto ni Naomi Moscovich, akiwa na binti zake, Dana Moscovich(kulia) na Lihi Moscovich (katikati). Aprili 27, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
PMO_8646
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mlango (geti) la kielektroniki kwa ajili ya ukaguzi wa abiria, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA Aprili 27, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
…………………………………………………………………….

*Ni yenye kuonyesha wanyama, milima, fukwe, mambo ya utamaduni
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa bodi ya KADCO uhakikishe unaweka mabango ya kielektroniki yenye kuonesha vivutio vya utalii kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

 “KADCO na Wizara ya Maliasili na Utalii, shirikianeni kuweka utaratibu wa kutangaza vivutio vyetu vya utalii hasa wanyama kwenye viwanja vyote vya ndege. Tunazo mbuga, milima, fukwe za bahari na ngoma za makabila mbalimbali, wekeni mabango yanayobadilisha picha.” 

 “Screens zenye wanyama wanaobadilikabadilika zinaleta mvuto lakini pia ni fursa ya kutangaza vivutio vyetu. Nimezunguka humu ndani, kuta zote ni nyeupe tu, tumieni fursa hiyo kutangaza tamaduni zetu na vivutio tulivyonavyo,” Waziri Mkuu alimweleza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO), Mhandisi Christopher Mukoma. 

Alitoa agizo hilo jana mchana (Jumamosi, Aprili 27, 2019) wakati akikagua miundombinu ya uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kuwaaga watalii 274 kutoka Israeli wanaowawakilisha wenzao 1,000 walioondoka nchini jana kurejea kwao.

Akiwa uwanjani hapo, Waziri Mkuu alikagua eneo la mapokezi, sehemu ya abiria wanaoondoka na wanaowasili, sehemu ya uhamiaji, mashine za kukagua mizigo ya wanaoondoka na wanaowasili, sehemu za kutolea huduma na maduka.
Pia alimwagiza Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji kwenye kiwanja hicho cha ndege, Bw. Filbert Ndege awasiliane na makao makuu yake ili waangalie uwezekano wa kuongeza madirisha ya kutolea huduma za uhamiaji (counters) ili huduma hiyo itolewe kwa kasi zaidi. 

 “Angalieni cha kufanya, ikibidi eneo hili lipanuliwe na counters nyingine ziongezwe ili kufasttrack utoaji wa huduma hasa msimu ambao watalii wengi huingia nchini.”

 Pia aliwataka KADCO waboreshe eneo la maegesho ya magari kwa kufanya upanuzi na kujenga maturubai ya vivuli (shades) ili kuyakinga na jua kali magari ya wateja

USAJILI WA LAINI ZA SIMU KWA KUTUMIA ALAMA ZA VIDOLE, WANANCHI WOTE KUFIKIWA.

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv, Morogoro

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Kanda ya Mashariki imesema kuwa wananchi wote wenye laini za simu za simu watafikiwa na huduma ya usajili wa laini za simu kwa vitambulisho vya Uraia na alama za vidole na watoa huduma wa kampuni za simu nchini.

Hayo yamesemwa kutokana na kuibuka kwa sintofahamu ya namna wananchi watakavyofikiwa na watoa huduma kwa ajili ya kusajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na kitambulisho cha uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Mamlaka hiyo imewatoa hofu wananchi wote na kuwahakikishia kwamba watafikiwa na watoa huduma za mawasiliano.

Akizungumza katika Mnada wa Dakawa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema wananchi wote watapata usajili wa laini zao kwa kutumia alama za vidole kwa kuwa na vitambulisho vya taifa.

Mhandisi Odiero amesema kazi yao ni kutoa elimu kwa wananchi wote hivyo watawafikia kwa njia yoyote kuhakikisha wananchi hawapati changamoto wakati wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Amesema usajili ni jitihada za Serikali katika kuhakikisha usalama wa watumiaji wa huduma za Mawsiliano kutokana na changamoto kwa baadhi ya watumiaji kutumia mawasiliano kinyume na utaratibu uliowekwa lakini kwa sasa ni kitambulisho kimoja tu ambapo mtu akifanya uharifu ni rahisi kumfikia na hatua zitachukuliwa.

Mhandisi Odiero amesema awali TCRA iliruhusu vitambulisho vingi hata barua za Serikali za Mtaa katika kusajili hali iliyofanya baadhi ya watumiaji kukiuka taratibu ikiwemo kudanganya na kutoa taarifa za uongo wakati wa usajili na hivyo na kutoa mwanya hata kwa wahali kutumia vitambulisho hivyo kujisajili na kufanya utapeli wa kujipatia kipato kisichokuwa halali.

Naye Eng. Robson Shaban (Mhandisi mwandamizi wa Mamlaka hiyo) ameasihi wananchi ambao tayari wana vitambulisho vya Uraia kusajili mapema (Ifikapo tarehe 01/05/2019 ambayo ndio mwanzo wa Usajili) laini zao na sio kusubiri mwisho na kuonekana usajili una changamoto wakati muda ulikuwepo na wakashindwa kufanya hivyo.

Katika Mnada huo watu wengi waliuza maswali na kujibiwa na maofisa kutika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Mashariki. Mamlaka inaendelea kuwaelimisha watumiaji juu ya umuhimu wa zoezi hilo.
 Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Robson Shaban akiwapa maelezo ya kitabu cha muongozo wa mawasiliano katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.
Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Robson Shaban akitoa elimu ya usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.


 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mfumo mpya wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akimpa maelekezo mwananchi wakati wa otoaji wa elimu ya namna ya usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.

Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Annastella Mchomvu akitoa maelezo kwa mwananchi katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.

Benki ya NMB Yazidi kujitanua, yazindua Rasmi Tawi lake Mbogwe

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Geita – Mhandisi Gabriel Luhumbi Robert (Kushoto) akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la NMB Mbogwe mkoani Geita. Tawi la NMB Mbogwe linafanya Benki ya NMB kuwa na matawi 229 na ATM Zaidi ya 800 nchi nzima. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Tawi la NMB Mbogwe – Daudi Mkanza na Mkuu wa Kitengo cha Biashara – Donatus Richard.


Mkuu wa Mkoa wa Geita – Mhandisi Gabriel Luhumbi Robert akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la NMB Mbogwe lililopo wilayani Mbogwe Mkoani Geita mwishoni mwa juma. Wakishuhudia tukio hilo ni Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse (kushoto), Meneja wa Tawi la NMB Mbogwe – Daudi Mkanza na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara – Donatus Richard, Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe - Martha Mkupasi na Meneja Uhusiano Biashara ya Serikali NMB – Suma Mwainunu.


Mkuu wa Mkoa wa Geita – Mhandisi Gabriel Luhumbi Robert (mwenye Kofia) akimpongeza Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi – Sospeter Magesse mara baada ya kuzindua rasmi tawi la NMB Mbogwe la wilayani Mbogwe mkoani Geita. Tawi la NMB Mbogwe linafanya Benki ya NMB kuwa na matawi 229 na ATM Zaidi ya 800 nchi nzima. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara – Donatus Richard.
Mkuu wa Mkoa wa Geita – Mhandisi Gabriel Luhumbi Robert akitoa hotuba kwenye muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Tawi la NMB Mbogwe, wilayani Mbogwe mwishoni mwa juma. Tawi la NMB Mbogwe linafanya Benki ya NMB kuwa na matawi 229 na ATM Zaidi ya 800 nchi nzima.


Benki ya NMB imezindua tawi jipya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kwa lengo la kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi katika kanda ya Magharibi. Hilo ni tawi la 25 kwa mkoani Geita na la 229 nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua tawi hilo, mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Geita Eng. Gabriel Luhumba amesema ufunguzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka kwa kuwa ofisi za serikali zinampango wa uchumi wakimkakati ambao utafanya Geita kuwa chachu ya maendeleo nchini.

Akiongea na wananchi wa wilaya ya Mbogwe Eng. Gabriel Luhumba pia ametoa rai kwa wananchi kubadilika na kuacha mazoea ya kuweka pesa majumbani na kuwataka kuwa na tabia ya kuweka benki na kwenye taasisi za fedha.

Eng.Luhumba alisema wananchi wa mkoa wa Geita wenye neema nyingi ya madini aina ya dhahabu wamekuwa na tabia ya kutunza fedha zao nyumbani hali ambayo imekuwa ni hatari kwa usalama wa maisha yao na kuwataka kuacha tabia hiyo.

Alisema mazoea na tabia ya kuweka fedha kwenye vitanda , kuchimbia chini au kwenye mazizi ya mifungo ilishapitwa na wakati kwa kipindi hiki na kuwataka vipato vyao vya pesa wanapopata kwenda kuziweka benki na kwenye taasisi za zinazotunza fedha.

“Ndugu zangu wananchi uhai katika maisha yetu ni bora sana, katika familia zetu , tabia ya kuendelea kukaa na fedha majumbani kwetu ni hatari sana kwa sababu unaweza kuvamiwa na watu waharifu wakawashambulia na kupoteza maisha kwa hiyo rai yangu mnapopata pesa iwe hata kidogo lazima tupeleka kuziweka benki,, Alisema Eng.Luhumba.

Eng. Luhumba katika hotuba yake alitoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Mbogwe kutumia fursa zinazotolewa na benki hiyo kujiletea mafanikio kiuchimi katika maisha yao na kuwataka kuwa wakopaji wazuri wa mikopo na kulejesha kwa wakati.

Mbali na kuipongeza menejimenti ya benki hiyo, aliipa changamoto ya kuhakikisha inaweza kuandaa Kongamano la biashara katika mkoa wa Geita ilikuwapa msasa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu kuchangamkia fursa zilipo mkoani humo ilikuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yenye tija ndani na nje ya kanda ya Magharibi na Afrika Mashariki.

Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Martha Mkupasi alisema anaishukuru benki ya NMB kwa kuwasogezea huduma za kibenki kutokana na kuwa wananchi walikuwa na kilio cha siku nyingi kwa serikali kuitaka benki kwa sababu walikuwa wasafiri zaidi ya kilimita 50 kufaata huduma hizo wilaya jirani za Bukombe na Kahama mkoa wa Shinyanga.

Mkupasi alisema kufunguliwa kwa tawi hilo la benki hiyo kumewaondolea aza waliyokuwa wanaipata kusafiri na fedha umabari mrefu hali iliyokuwa inahatarisha maisha yao kwa kuhofia kuvamiwa na majambazi , kwa kusogezewa huduma hiyo na kuwahimiza kutumia fursa hiyo kuichumi na kujiletea maendeleo.

Awali katika hotuba yake mkuu wa kitengo cha biashara wa benki ya NMB , Donatus Richard alisema sasa tawi hilo ni la 229 kwa nchi zima na huo ni wajibu wao katika kuwasogezea huduma hizo wananchi, wafanyabiashara wa dogo, wa kati na wakubwa ili kuwawezesha watu kupata mitaji kwa ajili ya biashara na shughuli mbalimbali nalengo la kuwanyanyua kiuchumi na kuwaomba wachangamikie fursa zionazotolewa na benki ili kujiletea maendeleo.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRIL 29,2019

ZIARA YA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI JIJINI MBEYA


UCSAF YAZINDUA CLUB ZA ICT SHULE ZA SEKONDARI DODOMA,MSALATO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mawasilono na Uchukuzi, Atashasta Nditiye (kulia) akifurahia jambo baada ya kutazama kazi iliyofanywa na mwanafunzi wa Dodoma Sekondari wakati akizindua Club ya ICT na Maabara ya Kompyuta sjuleni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 10 ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF). UCSAF wamekabidhi kompyuta 10 katika maabara hiyo. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (katikati) akikata utepe kuzindua maabara ya Compyuta na ICT Club katika Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) yanayofanyika Mkoani Dodoma kitaifa. Wengine pichani toka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule, Naibu Katibu Mkuu, Mawasiliano, Dk Jim Yonazi , Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Peter Ulanga, Mwenyekiti wa Bodi ya CSAF, Joseph Kilongola, Mwalimu Mkuu Dodoma Sekondari, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Maria Sasabo pamoja na watumishi wa UCSAF na walimu .UCSAF imetoa wamekabidhi Computa 10 kwa shule hiyo. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kulia) akiangalia mwanafunzi wa shule ya Sekondari Msalato wakitumia maabara ya Computa baada ya kuzindia maabara hiyo jijini Dodoma jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya UCSAF ambao ndio wamekabidhi Computa 10 kwa shule hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Mawasilino na Uchukuzi, Dk. Jim Yonazi akiangaklia kazi iliyofanywa na mwanafunzi wa Sekondari ya Msalato. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Peter Ulanga wakiangalia wanafunzi wa shule ya Sekondari Msalato wakitumia maabara ya Computa baada ya kuzindia maabara hiyo jijini Dodoma jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya UCSAF ambao ndio wamekabidhi Computa 10 kwa shule hiyo
 Naibu Waziri wa Mawasilono na Uchukuzi, Atashasta Nditiye akizungumza na na wanafunzi wa Sekondari ya Msalato. 
Naibu Waziri wa Mawasilono na Uchukuzi, Atashasta Nditiye akiangalia kazi za wanafunzi katika maabara hiyo. 
Wanafunzi wakiwa maabara ya Compyuta 
Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Peter Ulanga akizungumza
Naibu Waziri wa Mawasilono na Uchukuzi, Atashasta Nditiye akizungumza na kusisitiza umuhimi wa matumizi sahihi ya TEHAMA katika kufikia uchumi wa kati. 
Wanafunzi wa kidato cha sita wanaosoma masomo ya Sayansi Dodoma Sekondari wakifuatilia hotuba za viongozi 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kushoto) akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Peter Ulanga (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya CSAF, Joseph Kilongola, wakati wa hafla hiyo Dodoma Sekondari.
Picha ya pamoja

ELIMU YA AFYA YA UZAZI BADO NI CHANGAMOTO KWA WASICHANA NA VIJANA

$
0
0
Pamella Chogo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya "Chanya Change"akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
Anna Mahenge Mtaalamu wa Masuala ya Afya ya uzazi anasema familia nyingi zimekuwa zikishindwa kukaa na mabinti zao na kuwaeleza ukweli kuhusu afya uzazi 

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Kutokana na asilimia kubwa ya wasichana na vijana kutokuwa na uelewa juu ya Afya ya uzazi jamii kuanzia ngazi ya familia zimetakiwa kuwajengea uwezo ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha kuhusiana na afya ya uzazi katika maisha ya kila siku,

Taasisi ya Kimataifa ya "Chanya Change"imeendelea kutoa elimu ya kujitambua na kuchukua tahadhari kutokana na vihatarishi katika mazingira wanayo ishi wasichana zaidi ya 100 katika shule mbalimbali katika jiji la Arusha wakiwa na lengo la kuwasaidia kujitambua ,kutoa hamasa katika masomo ya sayansi pamoja na mafunzo ya Tehama kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo 

Akizungumza na Michuzi Blog Pamela Chogo ambae ni muandaaji wa warsha hiyo iliyo andaliwa na taasisi ya Kimataifa ya "+Chanya Change" kwa ajili ya wasichana amesema Msichana ana nafasi kubwa katika kuchochea shughuli za kimaendeleo ya taifa hususani katika Masuala ya Sayansi na teknolojia (TEHAMA) 

Amesema jamii inatakiwa kuondokana na mtazamo hasi kuhusu watoto wa kike kwamba hawawezi kufanikisha mambo,badala yake watambue wanawake wengi wamekuwa wakutumia changamoto hiyo Kuwa fursa katika jamii wanazo ishi hatimae wameleta chachu ya Maendeleo kuelekea Tanzania ya Viwanda.

"Ni wakati muafaka kwa jamii kuondokana na mtazamo Hasi kuhusu mtoto wa kike Kuwa hawezi kufanikisha Mambo muhimu katika jamii,mwanamke ndio msingi wa maendeleo"alisema Pamela.

Amesema bado kumekuwa na wimbi kubwa kwa baadhi ya wasichana kuto jitambua kutokana na kukosa elimu ya Afya ya uzazi kwa Vijana ngazi ya familia hivyo wazazi wanajukumu kubwa la kuelimisha Watoto wao wa kike wakaribiapo Rika la balehe ili kuepukana na ongozeko la ndoa,mimba za utotoni.

"Wazazi wengi bado wanatamaduni za kizamani ambazo zimekuwa chanzo Cha wasichana wengi kujiingiza Kwenye makundi Hasi yanayo pelekea kupata magonjwa na Matumizi ya madawa ya kulevya kwa kukosa elimu ya jinsi"

Anna Mahenge ni mtaalamu wa Masuala ya Afya ya uzazi anasema familia nyingi zimekuwa zikishindwa kukaa na mabinti zao na kuwaeleza ukweli kuhusu afya uzazi jambo ambalo limekuwa likichangia ongezelo la vihatarishi na maambukiIi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba za utotoni.

"Kuficha ficha mambo kwa wazazi juu ya wasichana kuhusu maumbile na maungo ya uzazi bado ni Changamoto kwa jamii, hivyo jamii ibadilike"alisema muuguzi huyo.

Nao baadhi ya wasichana waliowashiriki katika warsha hiyo wamesema Asasi za Kiraia zinazo hudumia jamii waige mfano wa kinacho fanywa na taasisi ya Chanya Change ili kufika katika maeneo husika na kutoa elimu ili kukiandaa kizazi chanya kwa siku zijazo.

Dar ya kijani ya UVCCM yavuna wanachama 500

$
0
0
Na Ripota Wetu,Michuzi TV

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rodrick Mpogolo, amewapokea wanachama wapya wa chama hicho kupitia kampeni ya Dar ya kijani inayoratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam.

Kampeni hiyo ya Dar ya Kijani ina lengo la kurudisha mitaa, kata na majimbo yote katika himaya ya chama, inawataka vijana na wanachama wote kuimarisha ushirikiano na kupata ushindi wa pamoja wenye heshima kwa chama hicho tawala.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Wilaya ya Kinondoni, Mpogolo, amewataka vijana kuwa makini na waadilifu kwani wao ndio wataokaojenga hehima ya chama na Taifa kwa ujumla.

“Vijana ndio tunao wategemea katika uchaguzi ujao tunahitaji vijana makini na waadilifu ambao watakitumikia chama chetu cha Mapinduzi na Serikali yetu. jiepushieni mbali na tabia ambazo zitawaondelea maadili yenu. Ili mkawe viongozi makini kwani taifa letu linaitaji viongozi makini na wachapakazi .

Amesema yeye hatoita Dar ya Kijani ila anaitambua Tanzania ya Kijani kutokana na kaz kubwa inayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

“Mimi sitaita Dar es Salaam ya Kijani bali nitaita Tanzania ya Kijani kwa sababu Rais wetu mpendwa Dk. John Magufuli anafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo nchini, tunaona ujenzi wa barabara za juu pale Ubungo na tunashuhudia maendeleo makubwa yanayofanywa katika sekta ya elimu vituo vya afya, kuwasaidia wamachinga kwa kuwapa vitambulisho vya ujasiriamali, bodaboda.

“Pia ameleta usawa kwa Watanzania wote kuwa sawa. Kwahiyo kwa namna hii lazima chama chetu kiendelee kushika hatamu kwa sababu tunawatumikia wananchi ipasavyo kwa namna hii nina uhakika Tanzania inaenda kuwa ya kijani,” amesema Mpogolo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ya Dar es Salaam ya Kijani ni kuwaandaa vijana na chaguzi zijazo ikiwamo wa Serikali za Mitaa mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 ili chama hicho kipate ushindi wa kishindo.

“Lengo la Dar es salaam ya Kijani ni kuwaanda vijana wa Mkoa wa Dar es salaam katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini kuwataka vijana kuhakikisha wanajitokeza katika kugombea nafasi lakini pia kuhakikksha CCM kinapata ushindi wa kishindo kwa mkoa wote,” amesema Kilakala

Amesema tangu kampeni hiyo ilipozinduliwa Machi 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuvuna zaidi ya wanachama 500 ambao wamejiunga na chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizunguka kwenye uzinduzi wa Dar ya Kijani ambayo sasa imetua Wilayani Kinondoni
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, akizungumza katika uzinduzi huo 
 Vijana wa CCM wakiwe kwenye uzinduzi huo Wilayani Kinondoni 

WAKALA YA SERIKALI MTANDAO WAJA NA MFUMO WA KUONGEZA UFANISI SERIKALINI

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao umetengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa usikivu Taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao umetengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Sehemu ya wafanyakazi wa Wakala wa Serikali Mtandao wakifuatilia taarifa ambayo ilikuwa inatolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
Picha na Alex Sonna-Fullshangwe blog




Na.Alex Sonna,Dodoma


WAKALA wa Serikali Mtandao umetengeneza Mfumo Shirikishi wa Kusimamia Shughuli na Rasilimali za Taasisi (ERMS) utakaowezesha kusimamia, kufuatilia, kukagua na tathmini ya utekelezaji wa shughuli zote za umma kwa ufanisi.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari,wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa matumizi ya tehama katika kuboresha utendajikazi serikalini.

Dk.Bakari amesema kuwa wameamua kutumia utaalamu wetu wa kidigitali kutengeneza mfumo wa ERMS ambao ni dirisha moja linalounganisha shughuli zote za ndani ya taasisi kuongeza ufanisi katika utendajikazi na utoaji huduma bora kwa umma.Aidha amesema kuwa kuwa mfumo huo utakuwa na moduli 18 zinazounganisha shughuli mbalimbali za utendajikazi zinazotegemeana kuwezesha kubadilisha taarifa miongoni mwa idara na kusimamia rasilimali watu, fedha na vitendea kazi.

Dk.Bakari amesisitiza kuwa mfumo huo unawezesha ushughulikiaji wa miamala kutoka idara moja hadi nyingine zikiwemo ankara za bidhaa na huduma, mapato na matumizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa shughuli kulingana na mipango na bajeti.Pia utawezesha usimamizi wa majukumu ya watumishi, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi, utekelezaji wa shughuli za manunuzi na utayarishaji wa taarifa mbalimbali za utendaji''amesema Dk.Bakari

Hata hivyo amesema kuwa mfumo huu utawawezesha maofisa masuuli na watumiaji wengine wa mfumo kupata taarifa mbalimbali kulingana na mahitaji yao.

Dk. Bakari amesema kuwa mfumo huo wa ERMS unaweza kuunganishwa na kubadilishana taarifa na mifumo mingine mikuu ya serikali ikiwemo Mfumo Mkuu wa Uhasibu, Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Rasilimaliwatu (HCMIS), Mfumo wa Malipo ya Serikali Kieletroniki (GePG), Mfumo wa Barua pepe Serikalini (GMS) na Mfumo wa Ofisi Mtandao.

Pia amesisitiza kuwa moduli za mfumo huo zinaweza kuongezwa au kupunguzwa bila kuathiri utendaji kazi wa moduli nyingine au mfumo kwa ujumla.

Amezitaja baadhi ya mifumo mingine ambayo wakala umeitengeneza katika utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao ambao ni tovuti kuu ya serikali, tovuti kuu ya ajira, mfumo wa barua pepe serikalini ambao unatumiwa na taasisi za umma 402 zikiwemo ofisi za ubalozi nje ya nchi kwa ajili ya kubadilishana taarifa serikalini.

Aidha Dk. Bakari amezitaka taasisi za umma kuendelea kutumia tehama katika kuboresha utendaji kazi serikani na utoaji huduma kwa umma kwa kuzingatia miongozo na viwango vya serikani mtandao

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIWIRA PAMOJA NA KUFUNGUA KIWANDA CHA MAPARACHICHI KILICHOPO RUNGWE MKOANI MBEYA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya wakati akiwa njiani kuelekea Wilayani Rungwe.
 Wananchi wa Kiwira wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo hilo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kiwira Wilayani Rungwe wakati aliposimama kuwasalimia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Mkoa wa Mbeya, Mawaziri, Wabunge akikata utepe kufungua kiwanda cha Maparachichi cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maparachichi yanayohifadhiwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi katika kiwanda cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya. 
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mashine maalumu ya kuangalia ubora wa maparachichi katika kiwanda cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi katika eneo la kiwanda cha cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya. PICHA NA IKULU
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images