Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1842 | 1843 | (Page 1844) | 1845 | 1846 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na waandishi mbalimbali ofisini kwake juu ya kusambaa kwa habari ambayo ilitungwa na mtu mmoja  NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

  Siku chache baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameshika viungo bandia vya kiume na kuzua Taharuki katika jamii, Mkuu huyo wa Wilaya ametolea ufafanuzi.

  Akizungumza na Wandishi wa habari ofisini kwake leo Kasesela amesema kuwa taarifa zilizosambaa mtandaoni juu ya uzalishaji wa viungo bandia vya kiume, zimeleta changamoto huku akiwataka wananchi kuondokana na dhana potofu za kuchukua habari za mitandaoni na kuupotosha umma.

  “Naomba niendee kuwaomba radhi watanzania kwa ajili ya jambo ambalo lilileta taharuki kwenye mitandao ya kijamii hasa nchi ya jirani zetu hapo Kenya lilipokelewa tofauti na nilivyokuwa hapo awali” alisema Kasesela 

  Kasesela aliwataka watanzania kuacha kufuatia mambo ya ajabu na kuyapa nafasi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kupata mambo ya kujenga nchi na yenye tija.

  “Jamni ile habari ilitungwa na ni habari ya hovyo sana kwa kuwa nililishwa habari ambayo mimi sijaisema kwenye chombo chochote kile kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo habari ni ya kupuuza tu” alisema Kasesela

  Kasesela amewashauri watanzania kuhakikisha wanafatilia taarifa zenye kuleta maendeleo na zenye kujenga katika jamii inayomzunguka.“Kwa sasa habari nyingi ambazo zinazungumzwa hivi sasa ni habari ambazo ni za hovyo hovyo mno ndio maana leo wamesema kuwa wilaya ya Iringa kuna kiwanda hicho kitu ambacho sio kweli” alisema Kasesela .

  Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amelaani kitendo cha Dawson Kagine kusambaza taarifa zisizo za kweli na kuongeza kuwa mkoani Iringa kuna kiwanda cha kuzalisha vifaa vya elimu ya mapambano dhidi ya Ukimwi. 

  0 0

  SUA, Morogoro

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo Profesa. Elisante Ole Gabriel amefurahishwa na shughuli zinazofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo hususan uwepo wa Hospitali ya Rufaa ya Wanyama.

  Hospitali hiyo ni taasisi pekee nchini inayosaidia kutoa ushauri, tiba na chanjo kwa wanyama wa kufugwa na waporini ambao wamepewa rufaa kutoka katika Hospitali ndogo ndogo za wanyama, taasisi za serikali na binafsi ambazo huhifadhi na kuwatunza wanyama hao ambao hupatikana kisheria.

  Akizungumza wakati wa ziara yake ya siku moja chuoni hapo leo Aprili 23, 2019, Prof. Gabriel amesema alipata fursa ya kuzunguka nchi za Afrika Mashariki lakini hakuwahi kusikia uwepo wa Hospitali ya Rufaa ya Wanyama na hivyo kuwataka waandishi wa habari kwa kushirkiana na kitengo cha Mawasiliano na Masoko kuhakikisha Umma unafahamu kuhusu Hospitali hiyo kuwepo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.

  “Nimefurahishwa na Hospitali ya Rufaa ya Wanyama hapa SUA ambayo ni kwa Tanzania nzima, ni vyema tukauhabarisha Umma kuhusu hili na ikibidi Waziri aweze kutembelea Hoapitali hii, kiukweli nimefurahishwa sana na mambo niliyoyaona hapa SUA na nashukuru ziara yangu hii sikukosea kuifanya hapa”. Alisema Prof. Gabriel.

  Pia aliongeza kuwa SUA inaweza kuwa zaidi ya eneo la mafunzo kwani kuna utalii ndani yake ambapo aliwashauri watumishi wa Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya kuanzisha programu ya Utalii ambapo watu wakija kufanya mafunzo ya tiba ya wanyama wapate kujionea mambo ya Utalii yaliyopo katika Ndaki hiyo na hata Ndaki nyingine.

  Aidha, Prof. Gabriel alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali hiyo na kujionea shughuli zinazofanywa ambapo alipata fursa ya kuona wanyama wakipatiwa tiba ikiwemo upasuaji wakiwa katika uangalizi wa madaktari maalum wa wanyama.

  “Sikuwa najua kama paka anaweza akafanyiwa upasuaji na kukatwa mguu na bado akaendelea kuwa hai hivyo natoa wito kwa wananchi wote kutumia Hospitali hii kuleta wanyama wao ili waweze kupatiwa matibabu mbalimbali, mimi nimefanikiwa kuona paka aliyefanyiwa operesheni na kukatwa mguu pamoja na mbwa ambao wote wako katika hali nzuri”, alisema Prof. Gabriel.

  Katibu Mkuu huyo pia alipata fursa ya kuzungumza na Menejimenti ya Chuo na kuwataka kuendelea kuzalisha wahitimu bora na kuwafanya kuwa ni wahitimu waliofundishwa kwa vitendo zaidi kuliko nadharia huku akishauri kuwa Chuo kitoe uelewa kwa wanafunzi kuwa sekta ya mifugo ni sekta inayoajiri zaidi ya asilimia 50 ya wataalam wa mifugo na kutambua kuwa ni vyema wajijengee hari ya kutaka kujiari ili nao waweze kuja kuajili wengine pia.

  “Ili tumuenzi Rais wetu John Pombe Joseph Magufuli ambaye ameonyesha msukumo wa pekee ni vyema tuhakikishe wahitimu wetu wanakuwa na uelewa kwa vitendo na si nadharia tu ili kutatua changamoto za wanafunzi”, alishauri Prof. Gabriel.

  Aliongeza kuwa chuo kinatakiwa kuongeza nguvu katika kutoa mafunzo ya biashara (Business knowledge) hususan katika upande wa tiba ya wanyama na Sayansi ya wanyama ili kuwapa wataalam ujuzi wa masuala ya biashara.

  “Nina hakika tukiongeza mafunzo ya biashara kwa wataalam wetu itasaidia kupata wanafunzi wa tofauti sana ambao mara baada ya kumaliza Chuo wakienda mtaani hawatapwaya katika utendaji kutokana na taaluma waliyopewa kwani biashara ndio kila kitu”, aliongeza Prof. Gabriel.

  Prof. Gabriel amesisitiza Chuo hicho kihakikishe kinawagusa wafugaji wa chini kwa kushirikiana na Wizara kuwapeleka wanafunzi kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo katika sehemu halisia za kujifunzia.

  “Chuo kishirikiane na Wizara pamoja na Tamisemi kuandika barua ili kuomba Wilaya mbalimbali zikubali kuwapokea wanafunzi wetu na kuwapatia maradhi badala ya kuwaacha wanafunzi hao kwenda mahali ambapo hawatapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo wakijaribu kukwepa gharama za kujihudumia wawapo katika mafunzo na hivyo kuangalia wapi wana jamaa ambao wanaweza kupata hifadhi”, alisisitiza.

  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chubunda alimshukuru Katibu Mkuu kwa ujio wake na mchango wa mawazo ambapo alisema kwa kiasi Chuo kimeshaanza kushughulikia baadhi ya masuala hususani kuwa na mahali halisia pa kujifunzia na hivyo kuanzisha mashamba darasa ya mazao ya kimkakati kwa ajili ya wanafunzi na jamii kwa ujumla.

  “Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Mgufuli kwa kuwekea mkazo uwezeshaji kwenye vyuo na hasa chuo chetu kwa miaka miwili iliyopita kuna mambo makubwa ambayo huko serikali ilikuwa kama imevisusa vyuo vyake na kubaki kama yatima na kusababisha kuchakaa kwa baadhi ya miundombinu ya kufundishia mfano chuo chetu tunategemea mashamba na karakana ambazo kwa sehemu kubwa zilichakaa. Kwa sasa serikali na menejimenti ya chuo imefanya juhudi ya kupata mashamba makubwa ya chuo yaani “Modal farms na tumepanda mazao yote ya kimkakati kama vile zabibu, korosho pamoja na chai” alisema Prof.Chibunda.

  Aidha, katika kuimarisha utoaji wa elimu bora Chuo kimeboresha maeneo ya mifugo kama vile ngombe, samaki na maabara kwa lengo la wanafunzi kujifunzia kwa vitendo.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na waandishi mbalimbali ofisini kwake juu ya kusambaa kwa habari ambayo ilitungwa na mtu mmoja


  NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
   
  Siku chache baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameshika viungo bandia vya kiume na kuzua Taharuki katika jamii, Mkuu huyo wa Wilaya ametolea ufafanuzi.

  Akizungumza na Wandishi wa habari ofisini kwake leo Kasesela amesema kuwa taarifa zilizosambaa mtandaoni juu ya uzalishaji wa viungo bandia vya kiume, zimeleta changamoto huku akiwataka wananchi  kuondokana na dhana potofu za kuchukua habari za mitandaoni na kuupotosha umma.

  “Naomba niendee kuwaomba radhi watanzania kwa ajili ya jambo ambalo lilileta taharuki kwenye mitandao ya kijamii hasa nchi ya jirani zetu hapo Kenya lilipokelewa tofauti na nilivyokuwa hapo awali” alisema Kasesela 

  Kasesela aliwataka watanzania kuacha kufuatia mambo ya ajabu na kuyapa nafasi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kupata mambo ya kujenga nchi na yenye tija.

  “Jamni ile habari ilitungwa na ni habari ya hovyo sana kwa kuwa nililishwa habari ambayo mimi sijaisema kwenye chombo chochote kile kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo habari ni ya kupuuza tu” alisema Kasesela

  Kasesela amewashauri watanzania kuhakikisha wanafatilia taarifa zenye kuleta maendeleo na zenye kujenga katika jamii inayomzunguka.

  “Kwa sasa habari nyingi ambazo zinazungumzwa hivi sasa ni habari ambazo ni za hovyo hovyo mno ndio maana leo wamesema kuwa wilaya ya Iringa kuna kiwanda hicho kitu ambacho sio kweli” alisema Kasesela

  Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amelaani kitendo cha Dawson Kagine   kusambaza taarifa zisizo za kweli na kuongeza kuwa mkoani Iringa kuna kiwanda cha kuzalisha vifaa vya elimu ya mapambano dhidi ya Ukimwi.


  0 0

  Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao wa  Hospitali ya Meditrina ya nchini India wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa  siku tatu ya kuzibua mishipa ya damu  ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa (Chronic Total Occlusion) na hivyo kushindwa kupitisha damu vizuri.

  Kambi hiyo ni maalum kwa ajili ya  kuwasaidia wagonjwa wenye matatizo hayo ambao bila ya kupata mtaalamu mwenye ujuzi wa hali ya juu wa kuzibua mishipa hiyo wangefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.

  Matibabu hayo yanafanyika kwa kutumia mtambo wa Cathlab ambapo mgonjwa anatobolewa tundu dogo katika paja ambalo linapitishwa vifaa maalum vya kuzibua mishipa ya damu ya moyo (Stent).

  Katika kambi hiyo wataalamu wa afya wa JKCI watapata elimu ya jinsi ya kuzibua mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa.

  Jumla ya wagonjwa 15 ambao mishipa yao ya damu mmoja hadi mitatu imeziba wanatarajiwa kutibiwa  katika kambi hiyo iliyoanza leo tarehe 23 hadi 25/4/2019. Hadi sasa wagonjwa watano wameshatibiwa na hali zao zinaendelea vizuri.

  Imetolewa na:
   
  Anna Nkinda
  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

  0 0

  Na Ahmed Mahmoud Arusha

  Jumuiya ya Afrika (AU) ipo katika mkakati wa kukamilisha uwepo wa soko huru la bidhaa ambapo Kwa sasa ipo kwenye mchakato wa baadhi ya bidhaa kufunguliwa Kwa zaidi ya asilimia 90 ambapo Tanzania inatarajiwa kunufaika katika soko hilo.

  Akizungumza katika kongamano lililowakutanisha wataalamu wa biashara kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika mwakilishi wa wizara ya viwanda na biashara Thomas Mcharo alisema kuwa nchi hizo wanachama wataweza kuchagua bidhaa ambazo zitaweza kufunguliwa baada ya mkataba kuanza kufanyakazi ambapo Tanzania ipo njiani kuridhia mkataba huo.

  Alisema kuwa uwepo wa Tanzania katika kongamano hilo ni kuona na kuufahamu zaidi mtangamano huo hivyo wakati wowote kuweza kuingia ikiwa ni faida ya nchi kwani Sera ya viwanda inaendana na masoko ya bidhaa tutakazozalisha hapa nchini

  "Unajua Sera ya serikali ya awamu ya Tano ni uchumi wa Kati wa viwanda na kongamano hili tunajadili mkataba wa kubadilishana biadha katika nchi za Afrika utaona faida Kwa nchi katika kukuza biashara za bidhaa zetu"

  Kwa upande wake mwakilishi wa mwenyekiti wa meza ya majadiliano ya biashara kutoka umoja wa nchi za Afrika Alexander Rubanga alisema kuwa kuondoa tozo hizo zotasaidia kukuwa Kwa biashara katika mataifa ya Afrika.

  Aliziomba nchi ambazo hazijaridhia mkataba huo kuona umuhimu wa kuwepo makubaliano kuhusu soko la pamoja la bidhaa litakalosaidi bara la Afrika kukua kiuchumi.

  Awali mtaalamu wa majadiliano kutoka time ya umoja wa Afrika Dkt.Halima Noor Abdi alisema kuwa mpaka sasa ni nchi 52 zimekwisha weka sahihi ambapo nchi zingine bado zinaendelea na majadiliano kuhusiana na umoja huo.

  Amesema kuwa faida kubwa ya kujiunga na mkataba huo wa mtangamano utaidia nchi moja kuweza kuzalisha bidhaa ambazo zitaweza kuuzwa kwenye nchi nyingine barani humo.

  0 0

   Mtaalamu wa Uchumi kutoka Stanbic Bank, Jibran Quereishi akizungumza katika jukwaa la kujenga ujuzi kwa wateja lilioandaliwa na benki hiyo, kwa ajili ya kuwaonyesha wateja wake fursa mbali mbali zilizopo katika kilimo cha biashara pamoja na utalii, hivi karibuni mkoani Arusha. Benki ya Stanbic iliandaa jukwaa hilo ili kutekeleza ahadi ya kuwasaidia wateja wake kufikia mafanikio yao ya kifedha kwa kupitia fursa mbali mbali zilizopo katika sekta husika.


  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umetangaza rasmi kuanza kupitia maombi ya vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na masomo ya elimu ya juu mwaka huu ambapo matarajio yao ni kuhakiki vyeti vya wanafunzi 100,000.

  Kwa mujibu wa RITA ni kwamba ili mwanafunzi mwenye sifa ya kupata mkopo kwa ajili ya masomo ya vyuo vikuu anapaswa cheti chake cha kuzaliwa kufanyiwa uhakiki ili kujiridhisha na taarifa zake na baada ya kuhakikiwa majibu yanayorudishwa kwa mwanafunzi na kutumwa Taasisi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Kendelea na mchakato wa kutoa mkopo.

  Hivyo katika kufanikisha wanafunzi wanapata mikopo kwa wakati RITA imeamua kuanza mchakato wa kuhakikiwa vyeti vya kuzaliwa mapema wakiamini itasaidia wanafunzi hao kuwa na uhakika wa taarifa zilizomo kwenye vyeti vyao.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam , Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu/ Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA) Emmy Kalomba Hudson amesema uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi unaanza leo na kuendelea huku akifafanua kuwa moja ya kielelezo au kiambatanisho ambacho kinatakiwa na taasisi ya mikopo ni uthibitisho wa mwanafunzi anayeomba mikopo.

  "Hivyo tumeona ni busara kuanza mchakato mapema ili wanafunzi waweze kupata mikopo. Tunajua kuna taasisi nyingi zinahusika lakini kwa upande wetu tumeona tuanze mapema. Kwanini tunahakiki? Tunajua watu ambao tunawasajili wanavyeti lakini lengo ni kuhakikisha wanafunzi wote wanaostahili kupata mikopo basi wapate," amesema Hudson.

  Ameongeza kuwa cheti cha kuzaliwa mwenye mamlaka yenye kuthibitisha uhalali wake ni RITA,na kwa kutambua jukumu hilo wameona ni bora wakaanza mapema na kwamba gharama za kuhakikiwa Sh.3000 huku akitoa rai kwa wanafunzi au wazazi kufungua akaunti email ili kurahisisha kujaza maombi na kutuma RITA yakahakikiwe

  "Wale ambao tutahakiki vyeti vyao na kuthibitisha taarifa zao tutawajibu na kisha taarifa zao kupeleka bodi ya mikopo kwa maana wanastahili kupata mkopo na wale ambao taarifa zao hazitakuwa RITA nao watajulishwa ili waangalie namna ya kufanya.

  "Pia uhakiki huu mbali ya kuhakiki cheti cha mwanafunzi,tunafahamu wakati mwingine mwanafunzi anaweza kuwa amepoteza mzazi mmoja wapi au wote, na hivyo mwenye kuthibitisha cheti cha kifo ni sisi RITA," amesema na kuongeza ni vema wananchi wakajenga utamaduni wa kuwa na vyeti vya kuzaliwa mapema ili kuepuka unaoweza kujitokeza mbele ya safari.


  Amefafanua zaidi kuwa kuna haja ya kuanza mapema ili kufanya zoezi kuwa rahisi na kupata muda unaofaa na kwamba wanaanza leo na kama mtoto yupo shule wanajua  wazazi wanatunza vyeti, na kama hawana basi ndio muda mzuri wa kufuatilia na kwamba maombi 100,000 ndio ambayo yatahakikiwa kwa mwaka huu.

   Amesema kuwa " Ada ya uhakiki wa maombi ni Sh.3000 tu,mwaka jana tulisikia wanafunzi wametapeliwa kwenye vibanda vya Intaneti, wapo waliotozwa hadi Sh.30,000 na hiyo imekuwa kero.

  Wazazi wafungue akaunti wenyewe za email ili kupunguza gharama. Wapo wengine ambao walilipa fedha na maombi yao hayakwenda. Wanafunzi waache kuzembea wajitume kwa kujaza maombi wenyewe. Zoezi hilo ni endelevu na vizuri wakaanza mapema kabla ya muda wa kuomba mikopo haujafika,"amesema Hudson

  Hata hivyo amesema maombi yatumwe kwa njia ya mtandao kwani hiyo itasaidia kupitia.maombi mengi na ndani ya siku tatu wahusika watakuwa wamejibiwa huku akitoa rai kwa makatibu tawala walioko wilayani ambao wanatambuliwa na RITA kuhakikisha wanafunzi wanajaza maombi kwa njia ya mtandao kwani mwaka jana wapo ambao walijaza maombi bila kutumia mtandao na hivyo kusababisha maombi kuchelewa RITA.

  Akizungumzia changamoto ambazo zilijitokeza mwaka jana wakati wa uhakiki wa vyeti kwa wanafunzi, Hudson amesema kulikuwa na changamoto katika upigaji picha wa vyeti ambapo zilikuwa hazionekani kwa uharaka, wengine walikosea nywila(paswadi) hivyo hata majibu yalipotumwa wengine walichelewa kupata kwasababu ya kusahau nywila.

  Pia changamoto nyingine kuna wanafunzi wengine walikuwa wazembe maana walikuwa wanajipiga selfie na kisha kutuma Rita,jambo ambalo haliko kwenye utaratibu."Changamoto nyingine wapo ambao walikuwa wamezaliwa nje ya nchi lakini nao wanakuja RITA.Hao tulikuwa tunawapa maelekezo ya namna ya kufanya.

  "Kulikuwa na changamoto pia ya mtandao kuzidiwa kutokana na idadi kubwa ya waombaji.Ndio maana tumeanza mapema kuondoa changamoto hiyo.Na baada ya kuona changamoto tumeamua kuboresha mtandao wetu kwa mfano iwapo mwanafunzi atasahau nywila basi Luna sehemu ataiona," amesema Hudson.

  Alipoulizwa kuhusu vyeti vyeki,amejibu ni kweli vipo kwa watu wachache ambao wamevipata kutoka kwa wahuni ambao wamekuwa wakitengeneza vyeti feki,view vya kuzaliwa au vya kielimu na vyeti vingine,na wanapobaini wanachukua hatua za kuwafikisha wahusika katika vyombo vingine vya kisheria."Ndio vipo huwa tunaona kwenye televisheni wakionesha watu wamekamatwa na mitambo ya kutengeneza vyeti.Hata hivyo vyeti vyeti vinausalama wa kutosha ."

  Ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa iwapo watabaini kuna mtu au watu wanatengeneza vyeti.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Haki za Kisheria Lina Msanga amesema kinachohakikiwa na RITA ni cheti cha kuzaliwa au cheti cha kifo na sio matangazo,hivyo kinachotakiwa kutumwa RITA ili kihakikiwe ni cheti.
   Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu /Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Kalomba Hudson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam wakati akitangaza kuanza uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wanaojiandaa kujiunga na masomo ya elimu ya juu ambao wanasifa za kupata mkopo
  Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Haki za Kisheria kutoka RITA Lina Msanga akifafanua jambo kuhusu uhakiki wa vyeti kwa wanafunzi wanaosubiri kupata uhakiki wa mkopo baada ya RITA kuthibitisha taarifa zao

   

  0 0

   Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Jopo la Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili lililokuwa likimfanyia Uchunguzi Mwanadada Mariamu Rajabu kwenye kidonda chake cha Mgongoni limekubaliana kwa pamoja kumuhamishia mgonjwa huyo katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ibrahim Mkoma amesema kuwa mara baada ya jopo la madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kufanya uchunguzi kwa kina na wameamua kumpa rufani mgonjwa huyo kwenda Ocean Road ili aweze kupata matibabu zaidi.

  hata hivyo waandishi wa habari walipohoji nini matokeo ya uchunguzi  na kwanini wanamuhamishia katika Hospitali ya Saratani ,Dk Mkoma alikataa kutoa taarifa ya matokeo ya uchunguzi wake na kusema kuwa matokeo hayo ya ugonjwa huo ni siri ya Daktari na Mgonjwa kama kanuni za kitabibu zinavyohitaji.

  hata hivyo globu ya jamii ilipomuuliza Mariamu Rajabu juu ya ugonjwa wake alisema kuwa awezi kuzungumzia ugonjwa huo kwa sasa na ayupo tayari kuzungumzia ugonjwa wake.

  Muhimbili (MNH) ilianza  kumfanyia uchunguzi Mariam Rajab kubaini chanzo cha kidonda alicho nacho mgongoni. Taarifa za ugonjwa wa Mariam zilisambaa siku chache zilizopita kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha binti huyo akiomba msaada wa matibabu kufuatia kidonda hicho kilichodumu kwa muda mrefu.

  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha alizungumza na waandishi wa habari  Alhamisi Aprili 18,2019 amesema hospitali hiyo imechukua jukumu la kumtibia Mariam baada ya kupata maelekezo kutoka wizara ya afya na serikali itabeba gharama zote.

   alisema waliona ile video nakufanya juhudi za kumtafuta na hatimaye ametoka Singida na kukaa naye wodini, kwa  matibabu  yanaendelea na tayari madaktari wamechukua vipimo kwa ajili ya uchunguzi zaidi,

   Mariam alieleza kuwa kidonda hicho amekuwa nacho kwa muda mrefu na amekuwa akikitibia mara kwa mara ila Agosti 2018 kimefuka upya na kumsababishia maumivu makali. 24/04/2019

    Mkuu wa idara ya upasuaji MNH, Ibrahim Mkoma amesema matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa ndiyo yatakayotoa mwongozo ni aina gani ya matibabu ambayo Mariam anatakiwa kupatiw

   Mwanadada Mariamu Rajabu  akiwa amelala kwenye kitanda akisaidiwa  na muhudumu wa afya wa hospitali ya Tiafa Muhimbili.
  Jopo la Madaktari walikuwa wakimuhudumia Mwanadada Mariamu Rajabu  akiwa amelala kwenye kitanda  hospitali ya Taifa Muhimbili.
  --

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

  SERIKALI ya Tanzania imekabidhi hundi ya fedha yenye thamani ya Sh. Bilioni 688.615 kwa mkandarasi wa Kampuni ya Arab Contractors kutoka nchini Misri anayejenga mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP). 

  Fedha hizo ni malipo ya awali kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo huku ikielezwa kuwa ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kutoa fedha nyingi kiasi hicho tena kwa mkupuo kwa ajili ya kulipa malipo ya awali kwa ajili ya mradi huo. 

  Wakati Serikali inakabidhi fedha hizo kwa mkandarasi, wa ujenzi huo baadhi ya maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), Mkurugezi Mtendaji wa TANESCO, Mwakilishi wa Benki Kuu(BoT) pamoja na viongozi wa Wizara ya Nishati walikuwepo kushuhudia tukio hilo. 

  Akizungumza baada ya kukabidhi hundi hiyo leo Aprili 24, 2019 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Doto James amesema Wizara hiyo kwa niaba ya Serikali imekabidhi fedha hizo kwa mkandarasi wa kampuni ya Arab Contractors na fedha nyingine zilizobaki zitaendelea kulipwa hatua kwa hatua kulingana na maendeleo ya ujenzi. 

  " Hazina kwa niaba ya Serikali tumekabidhi fedha Sh.bilioni 688.615 kwa mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji ni mradi wa kihistoria kwani ni utekelezaji wa wazo la muasisi wa Taifa hili Mwalim Julius Nyerere aliyelitoa mwaka 1971 na Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kutekeleza kwa kuanza ujenzi. 

  "Mradi huu utakapokamilika utakuwa na megawati 2,115 ambazo zitazalishwa na kwa sasa nchi yetu kwa ujumla wake inazo mewagati 1, 602 kutoka vyanzo vyote vilivyopo nchini lakini kwa mradi huu peke yake tutakuwa tumeongeza megawati zaidi ya 2000,"amesema Katibu Mkuu James. 

  Amefafanua mradi huo utakamilika baada ya miezi 36 na fedha za mradi zinatolewa na Serikali kwa asilimia 100 Kwa umuhimu wa mradi huu ndio maana Serikali imetoa fedha nyingi kwa mkupuo. "Hakuna mradi mwingine wowote ambao fedha za awali zimetolewa nyingi kiasi hicho tena kwa mara moja.Miradi mingi fedha zake hazikuwahi kuzidi Sh.bilioni 50,"amesema James. 

  Amesisitiza mradi huo utakapokamilika utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu hasa kwa kuzingatia muelekeo wa Serikali ni kuwa na Tanzania ya viwanda ambapo nishati ya umeme wa uhakika inahitajika zaidi ili kuvutia wawekezaji huku akieleza faida nyingine ya mradi huo ni kwamba utakapokamilika hata bei ya umeme itapungua. 

  Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa wakati wa ujenzi wa mradi huo ajira zitaongezeka kati ya 4500 hadi ajira 6000 wakati wote wa ujenzi, hivyo ni fursa kwa wananchi wa Tanzania. Pia eneo la mradi kutakuwa na uhakika wa maji kwa ajili ya umwagiliaji kutokana na maji ya maporomoko hayo. 

  "Pia shughuli za utalii katika pori la Selous na faida nyingi ujenzi wa mradi huo ni kwamba hakutakuwa na mafuriko kwani maji yatajengewa kuta imara na hivyo kzuia mafuriko. Faida nyingine mradi utakapokamilika na umeme kusambaa sehemu kubwa ya nchi utasaidia utnzaji wa mazingira,"amesema James. 

  Hata hivyo amefafanua kiasi cha fedha ambacho kimetolewa hadi sasa kwa ajili ya mradi huo wa umeme wa maporomoko ya Mto Rufiji ni Sh.trilioni moja kati ya Sh.trilioni sita ambazo zinahitajika kuukamilisha mradi huo. Pia amesema Serikali kupitia hazina imejipanga kufanikisha mradi huo wa kimkakati na wamejiandaa kikamilifu katika kuutekekeza. 

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dk.Hamis Mwinyimvua ameongeza kuwa Aprili 15, mwaka huu Benki ya CRDB na UBA walitoa dhamana ya fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi huo wa Rufiji. "Kutolewa kwa dhamana hizo kuliwezesha kuanza kwa baadhi ya hatua kwa mkandarasi Kwa mujibu wa mkataba asilimia 70 ni fedha zitakuwa za kigeni na asilimia 30 ni fedha za ndani. 

  Fedha za kigeni tayari imelipwa kwa asilimia 70 na ndani zitaendelea kulipwa. 
  "Mkandarasi kama ambavyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango alivyosema , tunakuhakikishia fedha zipo na hivyo asiwe na wasiwasi.Malipo ya awali kwa ajili ya mradi huu ni muhimu na tayari yamelipwa, hivyo ni matarajio yetu sasa vifaa vyote vinavyotakiwa kwa ajili ya kuanza ujenzi vitakwenda eneo la mradi,"amesema Dk.Mwinyumvua. 

  Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dk. Alexandra Kyazuri amesema Tanesco wamefurahi sana na kwamba umeme uliopo ni megawati 1600 na sasa kupitia mradi huo zitapatikana megawati 2000 

  "Tunaishukuru Serikali chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuamua kuanza kwa mradi huo.Kwa siku ya leo hii TANESCO hatutaki kuwa na maneno mengi zaidi ya kuwa na furaha sana,"amesema Dk.Kyaruzi .
   
  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua akionyesha Hundi yenye thamani ya Tsh.Bilioni 688 fedha zilizolipwa kama malipo ya awali  kwa Mkandarasi(Arab Contructors) kwa  utekelezaji wa Mradi wa kufua umeme mto rufiji, kulia ni Mwenyekti wa Bodi  TANESCO , Alexander Kyaruzi  na Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt.Tito Mwinuka.
   

  0 0

  Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Arusha Mjini Saipulani Abdallah Ramsey 

  Na. Vero Ignatus


  Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Arusha Mjini Saipulani Abdallah Ramsey amekanusha vikali taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa CCM imemfukuza kazi mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Ngarenaro.

  Akizungumza na Vyombo vya habari jijini Arusha Ramsey amesema kuwa kilichofanywa na katibu wa itikadi na uenezi wa ccm kata ya levolosi ni kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.

  Aidha alisema kuwa ipo mitandao ya kijamii iliyotoa taarifa hiyo na kusema ccm imemfukuza kazi daktari huku  swala hilo likizua mjadala kwa jamii nzima.

  "Alichokifanya mwenezi ni kusimamia utekelezaji na ndio kazi yetu sisi kama chama tawala alifika katika kituo cha afya Ngarenaro na kukuta hakuna huduma na kumtafuta daktari ambaye hakuwapo pia katika eneo hilo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma na malalamiko hapo mengi tu na sio kiki za kisiasa muelewe hivyo" alisema Ramsey

  Hata hivyo mwenyekiti huyo alisema kuwa ccm haimfukuzi mtu kazi Bali kusimamia mienendo mizima ya uwajibikaji na watanzania wanapata huduma.

  Alisema kuwa wanashangaa namna ambavyo mjadala huo unakuwa makubwa wakati kazi yao ni kuhoji wataalamu.

  Itakumbukwa kuwa ipo video clip ambayo inasambaa mitandaoni kumuonesha katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho akiwasiliana na mganga mfawidhi wa kituo hicho akimtaka kufika kituoni hapo,na mganga huyo kudai kuwa hawezi kufika yupo mbali shambani ambapo tukio hilo pia limesababisha mkurugenzi wa jiji la Arusha Daktari Maulid Madeni kumvua nafasi hiyo na kubaki kuwa daktari wa kawaida.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka ndani ya ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa na Mizinga 21 ya Rais mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Malawi kwa heshima yake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Malawi waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Prof. Arthur Peter Mutharika wakiwasalimia baadhi ya wananchi waliojitokeza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika, Mama Janeth Magufuli pamoja na Prof. Gertrude Mutharika kabla ya kuweka mashada ya maua katika kaburi la Rais wa Tatu wa Malawi, Prof. Bingu Mutharika,katika eneo la Bunge la Malawi Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa wameshika mashada ya maua tayari kuyaweka katika kaburi la Rais wa Tatu wa Malawi, Prof. Bingu Mutharika,katika eneo la Bunge la Malawi. April 24, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiweka mashada ya maua katika kaburi la Rais wa Tatu wa Malawi, Prof. Bingu Mutharika,katika eneo la Bunge la Malawi. April 24, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali mara baada ya kuweka mashada ya maua katika kaburi la Rais wa Tatu wa Malawi, Prof. Bingu Mutharika,katika eneo la Bunge la Malawi. April 24, 2019.

  Kaburi la Rais wa Tatu wa Malawi Hayati Prof. Bingu Mutharika.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Bunge Malawi (nyuma yake ni mkewe Mama Janeth Magufuli akishuhudia) April 24, 2019.

  0 0

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Makampuni ya Simu nchini, itawezesha zoezi la uandikishaji wa watumiaji wa simu nchini kwa kutumia Namba za Utambulisho wa Taifa au Kitambulisho cha Taifa.  Zoezi la Uandikishaji wa laini za simu linatarajia kufanyika kuanzia tarehe 01-Mei-2019. Mazoezi ya majaribio ya zoezi hili yamefanyika katika baadhi ya Mikoa na Taasisi na kuonyesha mafanikio.

  NIDA tayari imesajili asilimia 88 ya watu wote wanaostahili kusajiliwa kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa nchi nzima. Zoezi la Utambuzi na usajili ni endelevu, hivyo asilimia 12 ya lengo la usajili lililobaki linaendelea kutekelezwa katika wilaya zote nchini kwa kusajili watu ambao hawakusajiliwa kwenye zoezi la usajili wa umma (Mass Registration) na ambao wamekisha umri wa miaka 18, ambacho ni kigezo cha kisheria kinachoruhusu mwananchi kusajiliwa kwa ajili ya Utambulisho wa Taifa.  Vile vile usajili wa umma unafanywa tena katika mikoa ambayo watu wengi hawakusajiliwa katika usajili wa awali. Mikoa hiyo ni pamoja na Dar es salaam, Tanga, Pwani na Kigoma.

  NIDA tayari imetengeneza Namba za Utambulisho wa Taifa Milioni 12, sawa na asilimia na 59 ya usajili uliofanyika. Zoezi la uhakiki, kuchakata na kutengeneza Namba za Utambulisho wa Taifa linaendelea kutekelezwa kwa kasi usiku na mchana. Aidha tunatoa rai kwa wale wote ambao wamejulishwa kuwa vitambulisho vyao vipo tayari wafike Ofisi za NIDA au Ofisi za Serikali za Mitaa walipo jiandikishia kuvichukua. Vitambulisho vya Taifa vinaendelea kuzalishwa na kusambazwa kwa wananchi. Namba za Utambulisho wa Taifa zitatumika katika usajili wa Namba za simu na matumizi mengine. Hivyo wale ambao tayari wana Namba za Utambulisho wa Taifa wazitumie kujisajili wakati vitambulisho vinazalishwa.

  Wananchi mnaweza kupata Namba ya Utambulisho wa Taifa na huduma zingine zitolewazo na NIDA kwa njia zifuatazo:-
  a.Kupiga namba * 152 *00#; chagua Ajira na Utambuzi; Chagua NIDA
  b.Kupakua nakala ya Kitambulisho cha Taifa kwa kutembelea tovuti: https://services.nida.go.tz/nidportal/NID_Copy.aspx au tovuti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.
  c.Kupiga simu huduma wateja; 0673 333444, 0743 202020, 0743 201020, 
  d.0759 102010, 0765 201020. 
  e.Kufika ofisi za NIDA ya Wilaya ilyopo karibu.

  Ni Muhimu kwa Wananchi wote wenye sifa za kusajiliwa kwa ajili ya Utambulisho wa Taifa kufanya hivyo sasa pasipo kusubiri mpaka wanapokuwa na hitaji la haraka kwani uhakiki wa taarifa zako lazima ufanyike kabla ya utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Taifa na baadae kitambulisho cha Taifa.

  “Utambulisho wa Taifa kwa Maendeleo na Ustawi wa Nchi Yetu”


  Imetolewa na

  MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA
  23 APRILI, 2019.

  0 0


  Waziri wa Afya ashiriki kwenye ungawaji wa vyandarua ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,amesema kuwa Serikali imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7.

  Hayo ameyasema leo wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya ya Dodoma.

  Aidha,amesema kuwa halmashauri kutenga fedha za ndani kwa ajili ya kununua viuwadudu ikiwa ni katika kupambana na maambukizi ya Malaria katika maeneo yao.

  Waziri Ummy amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 2 ya utawala wa Rais John Magufuli, Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya Malaria kwa asilimia 50 kutoka wastani wa asilimia 14 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 7.

  Hata hivyo amesema kuwa serikali imekuwa na mikakati mingi ya kupambana na maambukizi wa ugonjwawa malaria ambayo yamekuwa ikiuwa Watanzania wengi kuwa mbali na kugawa vyandarua pia wanapulizia dawa katika mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi.

  ”Serikali imenunua takribani lita 60,000 ya viuawadudu kwa ajili ya kuua mazalia ya mbu na kuzigawa katika mikoa yenye maambukizi makubwa ya malaria kama vile Mkoa wa Kagera, Geita, Kigoma, Lindi na Mtwara lakini pia niwaombe wananchi kutunza mazingira ili kujiepusha na mbu waenezao malaria,” amesisitiza Mwalimu

  Aidha, Mwalimu alisema mkakati wa serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 angalau wajawazito 80 kati ya 100 waweze kuhudhuria kiliniki angalau mara nne hivyo kutoa fursa ya kufanyiwa vipimo mbalimbali ikiwamo malaria.

  Kwa upande wake mratibu wa ugonjwa wa malaria mkoa wa Dodoma, Fransis Bujiku amesema kuwa Mkoa huo umefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka asilimia 1 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 0.6 kwa sasa.
  Bujiku amesema kuwa kwa pamoja wamefanikiwa kwa kutuna mazingira ikiwa ni pamoja na kunyunyiza dawa ya kuua mbu kipindi cha masika na kufukia madimbwi yote yanayotuamisha maji pamoja na kuwahamasisha wananchi kulala kwenye vyandarua.

  Siku ya malaria duniani inafanyika kesho ambapo kitaifa itafanyikia mkoani Lindi ikiwa na kauli mbiu isemayo Ziro malaria inaanza na mimi .

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akigawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya ya Makole jijini Dodoma.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akionesha nchandarua kwa akina mama wajawazito (hawapo pichani) wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwapongeza baadhi ya wanaume ambao waliwaleta watoto klinik wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisalimia na baadhi ya viongozi wa wilaya ya mkoa wa Dodoma alipowasili kwa ajili ya kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali hiyo iliyopo Makole jijini Dodoma.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.
  Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa na ambaye ni mratibu wa Malaria mkoa wa Dodoma, Francis Bujiku,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma
  Sehemu ya akina mama wajawazito wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.

  0 0

  Katibu mkuu wizara ya kilimo mhandisi mathew mtigumwe amekitaka kikosi kazi kinachojihusisha na uandaaji wa mpango mkakati wa kuendeleza uzalishaji wa zao la mpunga nchini kuhakikisha kinaanda rasimu itakayowezesha uzalishaji wa zao hilo kukuwa mara mbili zaidi kutoka tani milioni 2.2 hadi kufikia tani 4.5 ifikapo 2030.
  Akizungumza na wataalam hao na wadau kutoka taasisi binafsi katika katibu mkuu mtigumwe amesema kufuatia wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuanzisha mpango mkakati wa kuendeleza zao la mpunga yaani national rice development strategy (nrsd) 1 mwaka 2008 kuwa na matokeo chanya ya kuongeza uzalishaji wa mpunga kutoka tani laki  899,000 hadi kufikia tani milioni 2.2 mwaka 2018 ambapo ili kukuza zaidi uzalishaji imeanzishwa nrds 2 itakayokwenda mpaka mwaka 2030 huku lengo likiwa ni kufikia tani za mpunga milioni 4.5…
  "Mpango huu utatekelezwa kwa muda was miaka 12 kuanzia mwaka 2018 had I mwaka 2030 na tayari maandalizi Yake yalianza mwaka 2018 kwa kuanzia kuainishwa takwimu zinazohitajika" amesema mtigumwe.
  Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho  joseph lubiloh, amesema kuwa matarajio waliyonayo mara baada ya kukamilika kwa mpango wa awamu ya pili na hadi sasa kikosi hicho kimefanikisha kukusanya takwimu kamili za kufanikisha mpango huo huku wadau wengine wakifafanua mipango iliyopo katika kufanikisha mpango huo kuwa ni kushirikiana na serikali kukamilisha juhudi hizo.
   Katibu mkuu wizara ya kilimo mhandisi mathew mtigumwe akizungumza jambo na wanakikosi kazi pamoja na wadau mbalimbali.
   kikosi kazi kinachojihusisha na uandaaji wa mpango mkakati wa kuendeleza uzalishaji wa zao la mpunga nchini pamoja na Katibu mkuu wizara ya kilimo mhandisi mathew mtigumwe aliyekaa katikati
   wadau mbalimbali na kikosi kazi kinachojihusisha na uandaaji wa mpango mkakati wa kuendeleza uzalishaji wa zao la mpunga nchini

  0 0

  Na Woinde Shizza Michuzi TV, Arusha

  Tatizo la ajira kwa Vijana ni changamoto kubwa nchini na ulimwengu mzima kwa ujumla, hivyo Vijana wametakiwa kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali zenye heshima na staha.

  Hayo yamebainishwa katika mahafali sita ya kidato cha sita ya shule ya
  Sekondari St. Mary’s Duluti hayo yamebainishwa na Father Fr.Peter Makao alipokuwa mgeni rasmi wa mahafali ya sita katika shule hiyo ambapo alisema katika ulimwengu wa sasa ajira ni chache sana ukilinganisha na idadi ya watu wanaoingia katika soko la ajira.

  Alibainisha kuwa ushindani katika soko la ajira ni kubwa sana hivyo ni vyema Vijana wengi waliopo majumbani na mitaani kuliko kukaa bila kazi yeyote ile wakajihusisha na shughuli za ujasilia mali zenye heshima na staha, pia wawe wabunifu

  Aliongeza kuwa Vijana walio wengi wa leo wanapenda kuwa huru(freedom) katika kufanya mambo ,Uhuru si jambo baya lakini uhuru usiokuwa na mipaka na uwajibikaji huo sio uhuru,Lazima mtu awajibike kwa matendo yake mwenyewe Hivyo basi uhuru wa kweli lazima uendane na uajibikaji

  Akiongea katika mahafali hayo mkuu Wa shule hiyo brother Essau Mlengule aliwaambia kuwa hatua waliofikia ni kwa sababu ya bidii kubwa, nidhamu na kujituma katika masomo mbali na hivyo pia kumtegemea Mwenyezi Mungu, akazibariki nguvu na bidii zao katika kuyatekeleza majukumu yao mema.

  Aliwataka wakaendelee kujituma, kuwa na bidii na nidhamu pindi tu warudipo nyumbani pia wasiache hata siku moja kumtegemea Mungu katika kilajambo walifanyalo

  Alisema kuwa kuhitimu kwao kwa masomo ni ishara ya kuwa wamekomaa kiakili, kiroho na kimwili na wapotayari kuelekea hatua mpya ya maisha kitaaluma, na maisha ya kujitegemea kiujumla.

  "Ninyi kama wasomi wa kidato cha sita, mnajukumu kubwa la kuwa wachangiaji wakubwa katika maendeleo ya maisha yenu binafsi, maendeleo ya familia, jumuniya zenu na hatimaye maendeleo ya Taifa zima la Tanzania kwa fikra yakinifu, kwa matendo na kwa njia halali zinazokubalika na jamii ya watu walioelimika." Alisema Mlengule

  Alisema kwamba mafanikio/maendeleo ya kweli hayaji kwa njia za mkato, kutokufuata taratibu za jumuiya husika, Kujichukulia maamzi bila ruhusa ya mamlaka husika, bali kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa malengo, kujiamini, kuwa weledi (kuwa wabobezi) katika kazi zenu, elimu ya fedha pamoja na kuwa na nidhamu ya fedha.

  Alisema Elimu yenu ya kidato cha sita iwasaidie kuwa na ujasiri wa kuishi kwa mifano maisha ya uadilifu katika familia na jumuiya pia Elimu mliopata iwasaidie kuepukana na uvivu, ulevi, uzushi, kiburi, wizi, matumizi ya madawa ya kulevya, uasherati na matendo mengine maovu yasiyokubaalika katika jamii yetu ya Tanzania kwani jamii inatarajia kuona ndani yenu maisha ya fadhila, utulivu, usikivu, uwajibikaji, ushiriki wenu katika kazi za kiuchumi na kijamii

  Alitaja baadhi ya changamoto zinazokabili shule hiyo ni pamoja na upungufu Wa mabweni ,ukosefu Wa jengo la utawala pamoja na viwanja vya michezo.

  0 0

  Maadhimisho ya siku ya Vitabu Duniani yaliadhimishwa kwa aina yake na Chuo kikuu Mzumbe Aprili 23; 2019 ambapo mbali na maonyesho ya machapisho yaliyoandikwa na Wanazuoni; Chuo hicho kilikabidhi msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwa shule za Msingi na Sekondari zilizopo kwenye Kata hiyo.

  Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvombero Bw. Florian Kyombo ambaye pamoja na mambo mengine alipongeza jitihada zinazofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe katika kuchangia na kuboresha sekta ya elimu nchini hususani matumizi ya teknolojia hasa kipindi hiki cha Awamu ya Tano ya Uongozi ambapo elimu ni agenda inayopewa kipaumbele na hivyo kutolewa bila malipo kwa ngazi ya elimu ya Awali, Msingi na Sekondari.

  “Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa msaada wa vitabu, shelfu na elimu mnayoendelea kuitoa kwa shule zetu kuhusu matumizi sahihi ya vitabu hivyo, sambamba na matumizi ya teknolojia ya utunzaji. Kwangu hili ni deni kuhakikisha tunatenga bajeti kuwezesha shule zingine za Msingi na Sekondari kwenye Kata 30 zilizopo kwenye Wilaya ya Mvomero zinaiga mfumo huu kwa kuifanya Kata ya Mzumbe kuwa ni ya kujifunzia.” alisisitiza.

  Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka amesema Chuo hicho kina wajibu wa kuhakikisha jamii inayokizunguka inanufaika na uwepo wake kwa kusaidia katika masuala ya maendeleo ikiwemo kuinua kiwango cha elimu kwa kujenga hamasa ya usomaji wa vitabu, kuwakuwa hiyo ndiyo mbinu pekee inayoweza kuwapatia Wanafunzi maarifa ya kutosha na kuweza kufikia ngazi zote za elimu hadi Chuo Kikuu.

  Amesema “ Mpango wa kuzifikia na kutatua changamoto za Shule za Msingi na Sekondari kwa jamii inayotuzunguka ni endelevu na ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa nne (IV) wa Chuo Kikuu Mzumbe ambapo kwa awamu hii, tumetoa Vitabu vya kiada na ziada kwa shule za Msingi Tangeni, 
  Mnyanza,Vikenge, Masanze, Changarawe na Mzumbe na shule tatu za Sekondari ambazo ni Mongola,Askofu Adrian Mkoba na Mzumbe; na tayari tumetoa msada wa Komputa na kutoa mafunzo ya matumizi ya programu mbalimbali ili kuziwezesha shule zetu kuendeshwa kisasa kwa kutoa mafunzo yanayoendana na wakati tulionao”.

  Aidha; ameahidi Chuo Kikuu Mzumbe kuendelea kuwa chachu katika kuhamasisha usomaji na utunzaji vitabu wenye lengo la kurithishana elimu na ujuzi kwa manufaa mapana ya Taifa.

  Siku ya Vitabu Duniani huadhimishwa kila mwaka Aprili 23; kwa lengo la kuhamasisha usomaji wa vitabu na kuwaenzi watunzi wa Vitabu duniani kote.
  Mwanafunzi wa Kidato cha sita Mark Malekela wa shule ya Sekondari Mzumbe, akionyesha moja ya kitabu alichotunga kwenye maadhimisho ya siku ya Vitabu Duniani yaliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro. Maadhimisho hayo yalilenga kuhamasisha usomaji na utunzi wa vitabu Duniani.
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero Bw. Florian Kyombo (mwenye kaunda suti - kushoto), kwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Pro. Lughano Kusiluka wakikabidhi msaada wa Vitabu kwa shule ya Sekondari ya Mzumbe na Adrian Mkoba zote za Kata ya Mzumbe wakati wa maadhimisho ya siku ya Vitabu Duniani yaliyofanyika Kampasi Kuu Morogoro.
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero Bw. Florian Kyombo (mwenye kaunda suti - kushoto), kwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Pro. Lughano Kusiluka wakikabidhi msaada wa Vitabu kwa shule ya Sekondari ya Mzumbe na Adrian Mkoba zote za Kata ya Mzumbe wakati wa maadhimisho ya siku ya Vitabu Duniani yaliyofanyika Kampasi Kuu Morogoro.
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero Bw. Florian Kyombo (mwenye kaunda suti - kulia), akikabidhi msaada wa vitabu kwa shule ya msingi Mnyanza. Kulia kwake ni Prof. Lughano Kusiluka Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe (mwenye sare ya kitenge) na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Myanza Bw. Robert Ngelima na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
  Wakiwa katika picha ya pamoja ni Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero Bw. Florian Kyombo (mwenye kaunda suti - katikati), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Pro. Lughano Kusiluka (mwenye sare ya kitenge – kulia), Mhe. Rachel Kingu Diwani wa Kata ya Mzumbe (Kushoto), Dkt. Albogast Musabila Mkurugenzi wa Makitaba na huduma za Kiufundi Chuo Kikuu Mzumbe ( mwenye sare ya Kitenge wa kwanza kulia) na Dkt. Hawa Petro Tundui ( wa kwanza kushoto) akimwakilisha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma. Kwa nyuma ni baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika pamoja na Mawaziri na Watendaji wa Serikali kabla ya Kusaini Mikataba ya Makubaliano ya Masuala mbalimbali yanayohusu Nchi zote mbili  katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 24, 2019.
  2
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika pamoja na Mawaziri na Watendaji wa Serikali kabla ya Kusaini Mikataba ya Makubaliano ya Masuala mbalimbali yanayohusu Nchi zote mbili  katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 24, 2019.
  3.34
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika pamoja na Mawaziri na Watendaji wa Serikali kabla ya Kusaini Mikataba ya Makubaliano ya Masuala mbalimbali yanayohusu Nchi zote mbili  katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 24, 2019.
  56789
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof.  Arthur Peter Mutharika kwa Zawadi aliyompatia mara baada ya Mazungumzo ya Kiserikali katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Nchini Malawi.Aprili 24, 2019.
  10
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Picha ya Twiga na Mlima Kilimanjaro Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya Mazungumzo ya Kiserikali katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Nchini Malawi.Aprili 24, 2019.
  11
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Kinyago Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya Mazungumzo ya Kiserikali katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Nchini Malawi.Aprili 24, 2019.
  12
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya kumkabidhi zawadi ya kinyago katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Nchini Malawi.Aprili 24, 2019.
  13
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Prof. John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi Dkt.Lois Fabiano pamoja na Mawaziri na Viongozi wengine wa Sreikali ya Tanzania na Malawi katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 24, 2019.Picha na Ikulu

  0 0

  Na Lydia Churi na Dennis Buyekwa-Mahakama

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema kuwa uelewa wa sheria, ujuzi na tabia ni mambo matatu muhimu wanayotakiwa kuwa nayo Majaji wa Mahakama ya Rufani ili yaweze kuwasaidia katika kutoa maamuzi kwenye mashauri.

  Akifungua Mkutano wa mwaka wa Majaji wa Mahakama ya Rufani wa kutathmini utendaji kazi wa Mahakama hiyo wa mwaka 2018 na kuweka mikakati ya kazi kwa mwaka 2019, Jaji Mkuu alisema Majaji kuwa na uelewa wa sheria na ujuzi haitoshi pasipo kujenga tabia ya kufanya kazi kwa kasi na kwa weledi.

  “Uvivu, uchonganishi, kulalamika pamoja na ubishi usio na mwelekeo ni tabia za kibinadamu zinazoweza kuathiri utendaji kazi kwa kuchelewesha upatikanaji wa haki”, alisema Jaji Mkuu. Alisema Majaji wanao umuhimu wa kipekee katika jamii hivyo hawana budi kutoa haki kwa kufuata sheria ili wananchi waweze kuwa na imani na mfumo wa utoaji haki pamoja na utawala wa sheria.

  “Kupitia mkutano huu mtapata fursa ya kubadilishana uzoefu wa namna ya kumaliza mashauri kwa kasi kwani utoaji haki uko katika utamaduni ambao haujaandikwa popote hivyo naamini mtaibua tamaduni zitakazorahisha utoaji wa haki”. Akizungumzia ongezeko la idadi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Mkuu alisema kuongezeka kwa Majaji hao kutasaidia Mahakama kupunguza changamoto ya mlundikano wa mashauri ya muda mrefu yaliyopo Mahakamani. Hivi sasa kuna Majaji 21 wa Mahakama ya Rufani ambapo awali kulikuwa na Majaji 15.

  Kuhusu changamoto, Jaji Mkuu alisema Mahakama inakabiliwa na upungufu wa bajeti kwa ajili ya vikao vya kusikiliza mashauri. Alisema endapo kungekuwa na bajeti ya kutosha vikao vingi Zaidi vya mashauri vingefanyika na kumaliza mlundikano wa mashauri ya muda mrefu.

  Alisema sheria imerekebishwa na kuwapa mamlaka Mahakimu na Manaibu Wasajili kusikiliza mashauri ya Mahakama Kuu hususan yale yanayohusu migogoro ya Ardhi ambapo hatua hii itasaidia kupunguza mashauri mahakamani. Aliongeza kuwa ili Mahakama iweze kuwatumia inahitaji kuongezewa bajeti Zaidi ya iliyopo sasa.

  Mkutano wa Mwaka huu wa Majaji wa Mahakama ya Rufani pia umewashirikisha Manaibu Wasajili, wasaidizi wa kisheria wa Majaji, Makarani na watunza kumbukumbu ili waweze kusaidiana na Majaji kupanga mikakati ya kumaliza mashauri kwa wakati.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

  0 0


  MAHAKAMA ya Mwanzo ya Maji ya Chai wilayani Arumeru,mkoani Arusha imemteua Kabidhi Wasii Mkuu,kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Anderson Mtui na kumpa muda wa miezi minne kutambua,kukusanya na kugawanya mali za marehemu kwa warithi stahiki.

  Baada ya mgao huo atatakiwa  kupeleka taarifa ya mgawanyo na hesabu mahakamani hapo.Aidha Mahakama hiyo imemvua usimamizi wa mirathi,Aunieli Mtui baada ya kuandika jina marehemu(baba yake mzazi),Anderson Mtui,kama moja ya mashahidi wake waliofika mahakamani hapo wakati wa kufungua mirathi.

  Katika shauri hilo la mirathi namba 39 la mwaka 2008,waombaji Royson Mtui na Rehema Mtui,ambao pia ni watoto wa marehemu waliiomba  Mahakama hiyo imtengue Aunieli  kuwa Msimamizi wa mirathi ya marehemu Anderson Mtui kwa madai kuwa msimamizi huyo siyo muaminifu kufanya kazi hiyo.

  Akitoa hukumu hiyo juzi,Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Rweyemamu Kashero,alisema Mahakama hiyo imeamua kumteua Kabidhi Wasii Mkuu huyo baada ya Aunieli kuonesha taswira mbaya ya kushindwa kusimamia na kugawa kwa usawa mali za marehemu.

  Alisema baada kwa kuzingatia wingi na thamani ya mali za marehemu,Mahakama hiyo inamteua Kabidhi Wasii Mkuu huyo kuwa msimamizi na kugawanya mali hizo ili mirathi hiyo ili iweze kufungwa.

  Aidha baada ya Mahakama hiyo kumtengua msimamizi wa awali ya mirathi hiyo, ilimwagiza msimamizi huyo(Aunieli),kurudisha nyaraka zote alizopewa na Mahakama hiyo kuhusiana na mirathi hiyo ndani ya siku 14 kuanzia sasa.

  "Kwa kuzingatia kwamba marehemu alikuwa amezaa watoto wake na wamama wanne tofauti na msuguano uliopo katika familia hii ambao unathibitishwa na shauri hili,ni vigumu kumpata msimamizi wa miirathi asiyekuwa na upande katika  familia hii,si tu kwamba haki itendeke bali ionekane kuwa imetendeka namteua Kabidhi Wasii Mkuu kuwa msimamizi wa mirathi hii,"alisema.

  Alisema Mahakama imefikia uamuzi hul baada ya kusikiliza hoja za mashahidi  wa pande zote ambapo mahakama iliona msimamizi wa mirathi hakuwa sahihi kwani alitumia majina ya marehemu kama shahidi wakati wa kufungua mirathi.

  "Kwa namna yoyote ile marehemu asingeweza kufufuka na kuja kutoa ushahidi katika mirathi yake mwenyewe,"alisema Hakimu huyo

  Hakimu Kashero alitaja sababu za kumtengua msimamizi huyo ni pamoja na kwenda tofauti na mashahidi wake kuhusiana na baadhi ya mali za marehemu pamoja na msimamizi huyo  kufanya  kinyume na masharti ya usimamizi wake kwa makusudi ikiwemo kushindwa kuwa msimamizi na kumkasimisha mama yake ambaye ni mke mkubwa kuwa msimamizi wa mali hizo.

  Hakimu huyo akirejea ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo,alisema mahakama imebaini msimamizi wa awali alichanganya mali ambazo hazikuwa za marehemu,ambapo mali hizo marehemu alizigawa kabla ya kifo chake.

  Hakimu Kashore alisema suala la msimamizi kujiamulia mali zote ni za mama yake kwa kigezo kuwa ni mke wa marehemu hivyo mali hizo walizitafuta wote siyo sawa kwa sababu suala lililopo mbele ya mahakama hiyo ni la mirathi halipaswi kuchanganywa na suala la ndoa.

  "Kwa kuzingatia kwamba marehemu alikuwa amezaa watoto 14 na wamama wanne tofauti,kwa kusingatia msuguano uliopo katika familia hii ambao unathibitishwa na shauri hili,ni vigumu kumpata msimamizi wa mirathi asiyekuwa na upande katika familia hii,"alisema na kuongeza

  "Kwa kuzingatia wingi na thamani ya mali za marehemu mahakama hii inamteua Kabidhi Wasii Mkuu kuwa msimamizi wa mirathi kuanzia leo na kumpa muda wa miezi minne kutambua,kukusanya na kugawanya mali za marehemu kwa mujibu wa sheria kwa warithi stahiki na kuleta taarifa ya mgawanyona hesabu ili mirathi hii ifungwe,"

  Awali waombaji hao waliiomba Mahakama imtengue kuwa msimamizi wa mirathi kwa madai kuwa hakutenda haki,hajawahi kuwaonyesha mali zao huku akigawa mali kwa kuwapendelea watoto wa familia ya mke mkubwa ambaye ana wa watoto saba na kuwabagua watoto wengine saba waliozaliwa na mama watatu tofauti.

  0 0


   Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa (Mbele) akizungumza na wananchi wakati wa uzindunzuzi wa kampeni ya Data Datani iliyofanyika viwanja vya Mbagala Zackiem hapo jana. Data Datani ni huduma inayowezesha wateja wa Vodacom kupata Mb hadi mara mbili zaidi ya kiwango walichonunua kila wanunuapo bando la intaneti. 
   Wasanii wakitumbuiza katika uzinduzi wa kampeni ya Data Datani iliyofanyika viwanja vya Mbagala Zackiem hapo jana. Data Datani ni huduma inayowezesha wateja wa Vodacom kupata Mb hadi mara mbili zaidi ya kiwango walichonunua kila wanunuapo bando la intaneti. 


   Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa  (wapili kulia) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifurahia uzinduzi wa kampeni ya Data Datani, iliyofanyika viwanja vya Mbagala Zackiem hapo jana. Data Datani ni huduma inayowezesha wateja wa Vodacom kupata Mb hadi mara mbili zaidi ya kiwango walichonunua kila wanunuapo bando la intaneti.    Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc, leo imezindua kampeni kabambe ya data iitwayo “Data Datani’ ambayo inawezesha wateja wake kupata bonus Mb hadi mara mbili zaidi kila wanunuapo bando la intaneti. Kampeni hiyo imezinduliwa katika viwanja vya Mbagala Zackhem jijini Dar es Salaam.

  Kampeni ya Data datani inalenga kuwawezesha watumiaji wa intanet kufaidi zaidi matumizi ya vifurushi vyao na pia kuwajuza mbinu mbali mbali za kutunza data isiishe kwa haraka, jambo ambalo limekuwa likiwatatiza wateja wake kwa muda mrefu.

  Ili kupata ofa hii, wateja wa Vodacom Tanzania Plc wanatakiwa kupiga *149*01# kisha chagua intaneti, halafu chagua intaneti bando kisha nunua kifurushi, hii itakuwezesha kupata hadi mara mbili ya bando uliyonunua awali kwa bei ile ile.

  Katika Uzinduzi wa kampeni hiyo kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa alitilia mkazo umuhimu wa data katika maisha ya kila siku. “Tukiwa ni Kampuni inayoongoza nchini kwa kutoa intaneti yenye kasi zaidi nchini, ni muhimu kuzingatia pande zote mbili za sarafu, yaani huduma na wateja wetu. Ndio maana tumeleta kampeni hii ili kuwawezesha wateja wetu kupata zaidi ya kile walicholipia kila wanaponunua bando la data,” alisema Linda huku akiongeza kwamba wanafahamu umuhimu wa data hasa katika zama hizi za kidijitali, habari zote na biashara ziko mitandaoni, hivyo wasingependa ukosefu wa data uwe kikwazo kwa wateja wao katika kufanikisha shughuli zao za kila siku.

  Mwaka 2017 Kampuni ya Vodacom Tanzania ilizindua mtandao wa 4G katika mkoa wa Dar es Salaam ili kuwawezesha wateja wake kupata intaneti yenye kasi zaidi, na mpaka sasa mtandao huu wa 4G umesambaa kufikia mikoa 24.

  Mfanyabiashara na mkaazi wa Mbagala Justin Joseph aliyehudhuria uzinduzi huu nae alisema, “Sasa ni wakati wa kudata datani, internet sio tu teknolojia bali pia ni kiuwezeshaji. Inatuwezesha kupata habari haraka, inatuwezesha kufanya biashara za mtandaoni, inawezesha serikali kupata kipato na kuwezesha shughuli za kijamii, yani kudata, ni zaidi ya data tu”.

  Kampeni hii inalenga kuwezesha wateja kutumia data zaidi na kikamilifu kwa shughuli zao zote za mtandaoni bila kuwa na wasiwasi wa data kuisha.

  Ili mteja aweze kufurahia huduma hii anapaswa kununua kifurushi kupitia mfumo wowote iwe ni M-Pesa, vocha, My Voda App, na ataweza kuperuzi habari, kuangalia video, kusikiliza muziki au kununua bidhaa mtandaoni. Changamkia fursa hii kwa kubofya *149*01, pata kifurushi chako cha intaneti uendelee kudata datani.

older | 1 | .... | 1842 | 1843 | (Page 1844) | 1845 | 1846 | .... | 1904 | newer