Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

AGAPE YAENDESHA KIKAO CHA USHAWISHI NA UTETEZI WA MASUALA YA AFYA NA UJINSIA

$
0
0
Shirika la Agape AIDS Control Program limeendesha kikao cha ushawishi na utetezi wa masuala ya afya ya uzazi na ujinsia katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.

Kikao hicho kimefanyika leo Jumatano Aprili 17,2019 katika shule ya msingi Shingida na kukutanisha pamoja viongozi wa ngazi ya kata,walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari,viongozi wa dini na kimila,wawakilishi wa wanafunzi na wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya idara ya elimu na maendeleo ya jamii.

Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana unaotekelezwa na Shirika la Agape kwa ufadhili wa shirika la Sida na nchini Sweden, Lucy Maganga alisema mbali na kutokomeza mila na desturi kandamizi pia washiriki wa kikao hicho watakuwa chachu ya mapambano dhidi ya mimba za utotoni hasa kwa watoto wa shule.

“Kupitia kikao hiki cha ushawishi na utetezi washiriki hawa wa kikao watakuwa mstari wa mbele kuishauri halmashauri ya wilaya kuongeza bajeti ya masuala ya afya ya uzazi ikiwemo miundombinu rafiki shuleni hasa vyoo,maji na vyumba vya kujisitiri kwa watoto wa kike”,alisema Maganga.

Kwa upande wake,Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Idara ya elimu sekondari halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Lucas Mambile alisema tayari halmashauri imeshatenga bajeti kwa mwaka 2019/2020 kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kike shuleni.

Aidha alisema halmashauri inaendelea kushirikiana na jamii kujenga na kujenga vyumba vya watoto wa kike kujistiri. Kwa upande wao,wajumbe wa kikao hicho waliahidi kuendelea kutoa elimu katika jamii ili iondokane na mila na desturi zinazochangia ukatili dhidi ya watoto lakini pia kulea watoto katika maadili mema.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Aisha Omary akizungumza katika kikao hicho na kueleza kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kuwa walinzi wa watoto wao na kuwalea katika maadili mema.


Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape ACP Lucy Maganga akizungumza wakati wa kikao cha ushawishi na utetezi wa masuala ya afya ya uzazi na ujinsia katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo katika shule ya msingi Shingida- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape ACP Lucy Maganga akizungumza ambapo wajumbe wa kikao hicho watakuwa mabalozi wa kuishauri halmashauri ya wilaya kuongeza bajeti ya masuala ya afya ya uzazi ikiwemo miundombinu rafiki shuleni hasa vyoo,maji na vyumba vya kujisitiri kwa watoto wa kike.
Wajumbe wa kikao hicho wakimsikiliza Lucy Maganga.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Idara ya elimu sekondari halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Lucas Mambile akielezea mikakati iliyopo katika halmashauri katika kusaidia masuala ya afya ya uzazi na ujinsia kwa wanafunzi ambapo alisema wametenga bajeti kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kike shuleni.
Kaimu Ofisa Elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mary Maka akiwaomba viongozi wa kata na walimu kuwa na mawasiliano na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa inapobainika watoto wa kike wamepewa ujauzito ili watuhumiwa wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Wajumbe wa kikao wakimsikiliza Lucy Maganga.
Kiongozi wa kimila,Lucas Kiyenze akizungumza katika kikao hicho.
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape ACP Lucy Maganga akiangalia kazi ya kundi la walimu wakuu shule za msingi katika kata ya Usanda wakijadili mikakati mbalimbali ya kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni.
Viongozi wa jamii wakiwemo watendaji wa vijiji na maafisa maendeleo ya jamii wakijadili mikakati ya kumaliza mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi.
Wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga idara ya elimu na maendeleo ya jamii wakijadili mikakati wanayoendelea nayo kuongeza bajeti ya masuala ya afya ya uzazi na ujinsia ikiwemo miundombinu rafiki shuleni hasa vyoo,maji na vyumba vya kujisitiri kwa watoto wa kike .

Afisa Idara ya Miradi kutoka shirika la Agape Prosper Ndaiga akifuatilia majadiliano ya wawakilishi wa wanafunzi shule za sekondari Shingita na Samuye kuhusu mikakati yao ya kutokomeza mimba kwa watoto wa shule.

Afisa Mtendaji kijiji cha Singita akiwasilisha kazi ya kundi la viongozi wa jamii kuhusu mikakati ya kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.Alizitaja baadhi ya mila hizo kuwa ni 'watoto kuogeshwa dawa ' samba' ili wapendwe, watoto kusindikiza bibi harusi.
Mkuu wa shule ya sekondari Samuye,Jackson Mganga akiwasilisha kazi ya kundi la wakuu wa shule namna walivyoweka mikakati kutokomeza mimba kwa watoto wa shule.
Sheikh Soud Ally wa msikiti wa Usanda akielezea mikakati ya kulea kwenye maadili ya dini watoto ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Mchungaji Lameck Makungu kutoka kanisa la AICT Busanda akielezea namna kanisa linavyotoa elimu kwa watoto ili kuepuka mimba na ndoa za utotoni.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

MAREKANI WAAAPISHA WAFANYAKAZI 59 WA KUJITOLEA KUSAIDIA AFYA NA KILIMO

$
0
0


Na Hussein Stambuli, Morogoro…

Ubalozi wa marekani umewaapisha wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa marekani watakao hudumu nchini ndani ya wilaya 35 kwa muda wa miaka 2 katika sekta ya kilimo na afya lengo kuongeza uzoefu na maarifa mapya katika sekta hizo…

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuwaapisha wafanyakazi hao kutoka shirika la wafanyakazi wa kujitolea wa kimarekani peace corps kaimu balozi wa marekani dk inmi patterson amesema kuwa wafanyakazi hao wataongeza uzoefu na maarifa katika sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo huku katika upande wa afya wakiwa na lengo la kujenga uelewa juu ya ugonjwa wa hiv na utapiamlo.

“Kupitia program hii mtaweza kuleta mabadiliko kwa watanzania mtakaofanya nao kazi na hata kwenu nyinyi wenyewe” amesema dr inmi patterson

Naibu waziri ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) mwita mwikabe amesisiti viongozi wa wilaya walizopangiwa wafanyakazi hao wameombwa kudumisha ushirikiano na wafanyakazi hao ili kuhakikisha maarifa waliyonayo wanayapokea pamoja na kulitangaza taifa katika nyanja mbalimbali na kutaka kuenziwa kwa ushirikiano huo wa kupokea wafanyakazi wa kujitolea ulioasisiwa na rais wa taifa hilo john f kennedy mwaka 1961.

“ningeomba kuweza kuwasisitiza wakuu wa wilaya na viongozi wote watakao husika moja kwa moaja kuwapokea wageni hawa ni muhimu kuwapa ushirikiano kwani kubadilishana maarifa kutasaidia wananchi wetu kujifunza mambo mapya ambayo yatasaidia kukua katika sekta ya kilimo na afya na umoja huu ni muhimu ukaenziwa” amesema mwikabe, Naibu waziri ofisi ya rais (tamisemi)

Wafanyakazi kutoka marekani waliopata mafunzo ya lugha na tamaduni kwa muda wa wiki 10 wameonesha kuvutiwa na aina ya maisha ya watanzania na wakiahidi kutoa ushirikiano zaidi kwani wanaamini watanzania wengi wanapenda kujifunza na wao watajitahidi kurithisha maarifa waliyonayo hasa kwenye sekta ya kilimo na afya bora.

“Tumefurahishwa na uwepo wetu hapa katika nchi hii tunahakika ushirikiano uliopo utatuwezesha kubadilishana uzoefu wa kiufundi na tamaduni tunauhakika tumeishi vyema na kutambua changamoto ambazo zinatukabili tumejipanga katika uvumilivu na tunaamini mwishoni wote tutafurahi kuyaona mafanikio” amesema sidney cech, muwakilishi wafanyakazi

Peace corps ni taasisi ya seriakli ya marekani iliyoanzishwa mwaka 1961 chini ya rais john f kennedy ambayo mpaka hivi sasa wafanyakazi wapatao 7000 wanahudumu katika nchi 70 duniani kwa zaidi ya miaka 50 huku lengo likiwa ni kuendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na tamaduni.
 Kaimu Balozi wa Marekani Dkt Inmi Patterson akiwaapisha wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa Marekani watakao hudumu nchini ndani ya wilaya 35 kwa muda wa miaka 2 katika sekta ya kilimo na afya.
Kaimu Balozi wa Marekani Dkt Inmi Patterson akizungumza jambo na wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa Marekani.
 Wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa Marekani watakao hudumu nchini ndani ya wilaya 35 kwa muda wa miaka 2.

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO.

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simoni Sirro amefanya ziara katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo kwa lengo la kutaka kujua hali ya kiusalama katika maeneo hayo, zaidi ikiwa kuwasikiliza wananchi wan maoni gani juu ya ushirikiano wao na Jeshi la Polisi katika utendaji kazi wa kila siku.

Aidha amewashukuru wananchi na wafanyabiashara wa Kariakoo kwa ushirikiano wao huku akiwataka waendelee kuwafichua wahalifu wa mifukoni na wale wanaotumia udanganyifu wa kuwaibia watu kwa kuwauzia sabuni na kusema mwisho wao hauta kuwa mzuri maana uhalifu hauna nafasi nchini.

IGP Sirro amewataka wananchi wote kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi hasa pale wanapokuwa na shaka na jambo fulani ili hatua z mapema ziweze kuchukuliwa kwa lengo la kuulinda usalama na amani iliyopo nchini, lakini pia amewahakikishia wananchi kuwa katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha kuwa linasimamia usalama wa raia na mali zao ili waweze kusherekea wakiwa salama.

BENKI YA UBA YAJIVUNIA USHIRIKI WAKE KATIKA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO NCHINI TANZANIA

$
0
0
*Yaahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa njia ya kidigitali, wagusia changamoto ya mikopo
 
Na Agnes Francis ,Globu ya jamii

BENKI ya UBA imesema inajivunia uwepo wake wa miaka 10 nchini kwani imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kuchangia maendeleo ya nchi ya Tanzania huku ikieleza wazi moja ya changamoto kubwa iliyopo katika taasisi za kibenki ni urejeshwaji wa mikopo iliyokopwa na wateja.

Kuhusu mikakati yao katika kujiimarisha kutoa huduma kwa Watanzania katika sekta hiyo ya kibenki, imesema imeweka nguvu zaidi kutoa kutoa huduma kwa njia ya mtandao(Kidigiali) hasa kwa kuzingatia kuna idadi kubwa ya watumiaji wa simu, hivyo imetoa siri benki hiyo iko mbioni wateja watatumia WhatsApp kwa ajili ya kufanya miamala mbalimbali ya kifedha kwa maana ya kutuma au kupokea tena kwa usalama zaidi.

Wakizungumza leo Aprili 18,2019 jijini Dar es Salaam na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, viongozi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Usman Isiaka wamesema wanajivunia kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha uchumi unaimarika na kubwa ambalo linawapa faraja ni namna ambavyo benki yao imekuwa mstari wa mbele kusaidia miradi ya maendeleo na hivi karibuni wameungana na Benki ya CRDB kutoa fedha ili kusaidia ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji.

Mkurugenzi Mkuu wa United Bank For Afrika(UBA) nchini Tanzania Usman Isiaka amesema benki yao imetimiza miaka 10 tangu ifungue tawi lake nchini Tanzania na imefikisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake ambapo ina matawi katika nchi mbalimbali Afrika na nje ya Afrika na lengo kuu la uwepo wake ni kusaidia katika kukuza uchumi na maendeleo ya nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.

"Tumekuwa tukishiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo na hii imetupa nafasi ya benki yetu kuwa mstari wa mbele kutoa fedha kwa ajili ya kuwa sehemu ya kufanikisha miradi ya maendeleo.Uwepo wetu wa miaka 10 nchini Tanzania tumekuwa tukichangia ukuaji wa uchumi kwa kutoa mikopo kwa wananchi wa kada mbalimbali,"amesema na kuongeza wataendelea kutoa kila aina ya ushirikiano kwa Serikali ili iweze kutimiza malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Hata hivyo, amesema benki hiyo imeweka mkakati wa kuendelea kuwa karibu na wananchi ikiwa pamoja na kujitangaza ili ifahamike zaidi na kuongeza kwa kipindi cha miaka miwili sasa wamefanikiwa kujitambulisha na huduma za kibenki ambazo wanazitoa huku akisisitiza wameamua kujikita katika kutoa huduma kidigitali zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Corporate Mussa Kitambi ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa pamoja na mafanikio ambayo benki hiyo imeyapata kwa kutoa huduma bora kwa wateja wao, changamoto kubwa inayowakabili ni urejeshwaji wa mikopo kutoka kwa wateja wao na kwamba kwa mazingira ya sasa hata walioweka hati ya nyumba kama dhamana ya mkopo nako hakuko sawa kwani bei ya nyumba imeshuka.

"Changamoto ambayo tunakabiliana nayo ni katika eneo hili la mikopo, wapo ambao wamekopa lakini katika kurejesha kuna shida, wapo ambao waliweka hati ya nyumba lakini nako soko la bei ya nyumba limeporomoka, hivyo inakuwa ngumu fedha iliyokopwa kurejea yote.

"Pia changamoto nyingine iliyokuwa inatukabili ni katika eneo la kubadilisha fedha ambako benki zilikuwa katika wakati mgumu kwani hakukua na uhakika wa bei ya kubadilisha fedha lakini baada ya BoT kuamua kuweka mfumo mzuri sasa mambo yanakwenda vizuri.Hiyo changamoto iliyotokana na kubadilisha fedha za kigeni haiko tena,"amesema.

"Tunafahamu kuwa Serikali iliamua fedha zake zote ziwekwe Benki Kuu, hivyo baada ya kuondolewa kwa fedha hizo ilileta changamoto kwetu, hivyo baada ya kuziondoa ndio maana mtaona hivi sasa benki zote zimekimbilia kwa wananchi kwa kuwa karibu nao na kuwahudumia,"amesema Kitambi.

Ameongeza changamoto nyingine ambayo wamekuwa nayo ni kwamba walikuwa wanafanya kazi kwa sehemu kubwa na Serikali na hasa ya kuweka fedha katika benki binafsi la kwetu ni eneo hili la urejeshwaji wa mikopo kutoka kwa wateja wetu ambao tuliwakopesha.Wapo walioweka hati za nyumba lakini ukweli hivi sasa soko la nyuma liko chini.Hivyo hata unapotaka kuuza nyumba kurejesha mkopo bado haitishi.Changamoto nyingine ilikuwa ni kupanda kwa Dola lakini tunaishukuru Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa kuwema mfumo rasmi wa kubadilisha fedha za kigeni.

"Kabla ya BoT kutoa maelekezo katika eneo hili la kubadilisha fedha za kigeni benki yetu na huenda hata benki nyingine zilikuwa katika wakati mgumu lakini sasa kuna unafuu maana kuna mfumo mzuri katika kubadili fedha za kigeni.Kwa sasa mambo yanakwenda vizuri,"amesema Kitambi. 

Aidha Mkuu wa Kitengo cha kuhudumia Serikali na mashirika ya Umma Dominick Thimoth amefafanua wamekuwa wakisaidia kwa kutoa mikopo kwa Serikali kwenye miradi pamoja na kuchangia bajeti ya Serikali.Wakati huo huo Mkuu wa Kitengo cha Wateja UBA Asupya Nalingigwa ametumia nafasi hiyo ya kuzungumza na wahariri kuelekeza namna ambavyo wamejipanga kutoa huduma kimtandao kwa kutumia simu za mkononi na hivi karibuni watazindua huduma ya Whtsap kwa ajili ya wateja kufanya miala.
 
 Pia amesema katika kurahisisha namna ya kujiunga na benki yao, wanayo huduma ya mwananchi kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi kwa kusaidia huduma ya Leo ambayo ni ya kisasa.
 Mkurugenzi wa UBA Usman Isiaka akizungumza na waandishi wa habari akifafanua huduma zinazotolewa na banki ya UBA kwa serikali na hata sekta binafsi leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu Kitengo cha wateja  UBA Asupya Nalingigwa akielezea namna ya kufungua akaunti ya benki hiyo kwa kutumia mfumo wa kisasa kupitia simu kwa lengo la kutaka kuwafikia watanzania wengi leo Jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wa Benki ya UBA wawakisikiliza maswali ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam
Viongozi wa UBA katika picha ya pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali leo Jijini Dar es Salaam.

MAELFU WAJITOKEZA KAMBI YA MATIBABU YA MACHO JIJINI TANGA,WAZIRI UMMY AELEZA TATIZO LILIVYO KUBWA NCHINI

$
0
0






Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kambi ya macho kwenye shule ya Sekondari Maawal Jijini Tanga chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanzania wakishirikiana na Mbunge huyo chini ya Ufadhili wa better Charity ya nchini Uingereza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Mwenyekiti wa Bilal Muslim Africa Mohsin Abdallah (Shein) 
Mwenyekiti wa Bilal Muslim Africa Mohsin Abdallah (Shein) akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto ni Mkuu wa Maawal Sheikh Mohamed Hariri
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo 
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Clemence Marcel akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mratibu w Bilal Muslim Mission of Tanzania Sharriff akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na Mratibu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Sharrif mara baada ya kufanya uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na mmoja wa wanafunzi ambaye alijitokeza kwenye kambi hiyo ya matibabu ya macho mara baada ya kuizindua 
Sehemu ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri Ummy wakati akizindua matibabu hayo
Wananchi kutoka maeneo 
Sehemu ya wananchi wakisubiriwa kupata huduma ya matibabu wakati wa kambi hiyo
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye kambi hiyo ya macho


MAELFU ya Wakazi wa mji wa Tanga wamejitokeza kwenye kambi ya Matibabu ya Macho inayoendelea kwenye shule ya shule ya Sekondari Maawal mjini hapa chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission tanzania wakishirikiana na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto chini ya Ufadhili wa better Charity ya nchini Uingereza

Akizungumza wakati akizindua kambi hiyo ya matibabu ya Macho Waziri Ummy alisema kuwa tatizo la ugonjwa wa macho nchini limekuwa kubwa ambapo kila watanzania mia moja wanne wanakabiliwa na matatizo ya macho. Alisema takwimu hizo zimefafanua kuwa katika idadi hiyo kila mtanzania mmoja anakabiliwa na tatizo la upofu wa mamcho na watanzania watatu wanakabiliwa na matatizo ya upungufu wa uoni wa kati na hali ya juu tatizo ambalo limekuwa kubwa sana. 

Aidha alisema kwa mujibu wa takwimu wizara ya afya katika kila watanzania 100 mmoja ana tatizo la upofu huku kwa ikieleza kwa watanzania 100 kati yao watatu wana matatizo ya upungufu wa kuona wa kati na hali ya juu tatizo hilo ni kubwa kwa sababu kati ya watu 100 wa nne wana matatizo ya macho. 

Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy alitoa wito kwa watanzania kujiwekea utaratibu wa kuhudhuria kwenye vituo vya Afya ili waweze kupata matibabu pindi wanapoona kuwepo dalili za ugonjwa wa macho. “Ukiona una tatizo la macho nenda kwenye vituo vya afya upate matibabu haraka lakini niwaambie pia wana tanga na watanzania hakikisheni mnachunguza afya ya macho na afya ya kinywa mara moja kila mwaka “Alisema .

Waziri huyo aliwataka watanzania kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa hasa vyenye vitamin ikiwemo kuhakikisha wanakula mbogamboga huku akiwataka kuacha dawa kwenye macho bila kuandikiwa na daktari kwa sababu inaweza kupelekea kuharibu macho yao .Awali akizungumza katika halfa hiyo Mwenyekiti wa Bilal Muslim Afrika Mohsin Abdallah (Shein) alimshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kuhakikisha huduma za afya nchini zinaimarika kwenye maeneo mbalimbali na kuondosha changamoto zilizopokuwepo awali.

“Namshukuru Rais Magufuli miaka yote tumefanya kazi tunatumia hospitali za serikali huduma zilikuwepo lakini hazikuwa kama ilivyo sasa lakini leo serikali ya awamu ya tano hospitali zimekuwa na vifaa muhimu kwenye hospitali”Alisema 

Aidha alisema wao kama bilal Muslim wamekuwa wakienda kwenye maeneo ambayo yana matukio makubwa lakini kutokana na ombi la Waziri Ummy tumeona kuja hapa kumuunga mkono pia tunashukuru mwamko umekuwa mkubwa sana,

HAKUNA SIKUKUU KWENYE KAZI ZA UMEME – WAZIRI KALEMANI

$
0
0

HAKUNA SIKUKUU KWENYE KAZI ZA UMEME – WAZIRI KALEMANI

Na Veronica Simba – Kongwa

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewaagiza amewaagiza wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kuendelea na kazi katika maeneo yao kwa siku zote zikiwemo sikukuu.

Alitoa maagizo hayo Aprili 18, 2019 Kongwa, Dodoma alipokuwa akikagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini; ambapo pia aliwasha umeme katika vijiji vya Ngonga na Mjini Mashariki B.

“Wakandarasi, najua kuna sikukuu lakini hakuna sikukuu kwenye kazi za umeme. Jipangeni na magenge yenu. Mameneja na vibarua muendelee na kazi. Hakuna Pasaka kwenye umeme. Umeme ni usalama na umeme ni uhai,” alisema.

Aidha, Waziri pia alimwagiza Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Kongwa, kuwaunganishia umeme wananchi wa kijiji cha Ngonga ambao nyumba zao zimerukwa.

“Sitaki kuona nyumba haina umeme. Nyumba hizi zote mzipelekee umeme. Mmeziruka mkidhani ni za hovyo-hovyo, hakuna nyumba ya hovyo. Nawapa hizi UMETA (Vifaa vya Umeme Tayari), kesho muwaunganishie umeme,” alisisitiza Waziri.

Akihamasisha kuhusu matumizi ya UMETA, Waziri Kalemani aliwataka viongozi mbalimbali wa Halmashauri za Vijiji na Wilaya kuhakikisha wanatumia kifaa hicho katika Taasisi za Umma ambazo majengo yake hayana vyumba vingi ili kupunguza gharama za kutandaza nyaya za umeme.

Aidha, aliwahamasisha wananchi wenye nyumba zenye vyumba vichache (visivyozidi vinne) kutumia vifaa hivyo ili kuepukana na gharama za kutandaza nyaya za umeme.

Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kulipia gharama za kuunganishiwa umeme kwenye makazi yao ambazo ni shilingi 27,000 kwa wananchi wa vijijini.

“Siyo lazima ulipe yote kwa mkupuo. Unaweza kulipia kidogo kidogo hadi ukafikisha 27,000 na TANESCO watakuunganishia umeme.”

Katika ziara hiyo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, ambaye ndiye Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, alitoa salamu za shukrani kwa serikali kwa kuwapelekea wananchi wake umeme kwa ajili ya maendeleo yao.

“Nasimama kwa niaba yenu (wananchi), kutoa shukrani nyingi kwa serikali, kwa será hii nzuri ya kutuletea umeme. Umeme ni maendeleo, umeme ni maisha, umeme ni uhai. Kinachotakiwa sasa ni tuutumie umeme huu.”

Aidha, Mheshimiwa Ndugai alimpongeza Dkt. Kalemani kwa kuwa Waziri wa kwanza tangu Tanzania ipate Uhuru, kufika katika Kijiji cha Mjini Mashariki B, kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, kwa kuhakikisha wananchi wanapelekewa huduma za maendeleo.

Waziri aliambatana na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, TANESCO na REA.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Kijiji cha Mjini Mashariki B, kilichopo wilayani Kongwa, alipokuwa katika ziara ya kazi, Aprili 18, 2019. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme kwenye nyumba ya mkazi wa Kijiji cha Mjini Mashariki B, Lilia Boma (katikati), alipokuwa katika ziara ya kazi wilayani Kongwa, Aprili 18, 2019. Kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akiwagawia bure vifaa cha Umeme Tayari (UMETA), wakazi wa Kijiji cha Mjini Mashariki B, wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma ili waweze kuunganishiwa umeme pasipo kuingia gharama za kutandaza nyaya. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi, ambapo aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho, Aprili 18, 2019.
Sehemu ya umati wa wananchi wa Kijiji cha Ngonga, wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) na kushangilia alipowaahidi kuwa serikali itasambaza umeme katika vitongoji vyote vya kijiji hicho. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi, ambapo aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho, Aprili 18, 2019.

UMEFIKA WAKATI SASA WASOMI KUANDIKA NA KIUBUA MASHUJAA WA FANI MBALIMBALI-BALOZI SEID ALI IDDI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Wasomi au Watu wa kawaida wenye uwezo na Taaluma ya kuandika kuibua na kuiweka hadharani hazina ya Mashujaa wa fani mbali mbali ili Vizazi vya sasa na vile vijavyo viweze kufaidika na michango yao.
Alisema Visiwa vya Zanzibar vimebahatika kukaliwa na mashujaa wa fani tofauti ikiwemo, Uchumi, Siasa na Utamaduni, lakini kwa bahati mbaya Wasomi wengi wamekuwa wavivu kutafiti maisha yao na hatimae kuyawasilisha kwa Jamii kwa nia ya Vitabu.
Balozi Seif Ali Iddi aliseMa hayo wakati akizindua Tamthilia ya Mtumwa hadi Siti Binti Saad iliyotungwa na Mwandishi Mahiri na mpenzi mkubwa wa Lugha ya Kiswahili Nchini Profesa Emmanuel Mbogo hapo katika Ukumbi wa Sheikh Idiss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Alisema kunakili hadhithi na kuzichapisha kwenye Vitabu ni njia murua na muwafaka  ya kuwaenzi mashujaa hao na itapendeza zaidi iwapo simulizi zao zitachapishwa kwa kutumia Lugha Mama na sanifu iliyozoeleka ya Kiswahili ili zipate wasomaji wengi zaidi.
Balozi Seif alieleza anaamini kuwa Historia ya Zanzibar haiwezi kukamilika bila ya kuelezea maisha ya Msanii maarufu wa Taarabu Afrika Mashariki Bibi Siti Binti Saad ambapo kwa bahati nzuzi Profesa Emmanuel Mbogo ameifanya kazi hiyo ya kuinawirisha Historia ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza kwamba Uandishi wa Historia za Mashujaa wa Fani mbali mbali Visiwani Zanzibar na Mwambao wa Afrika Mashariki ni muhimu kwa Jamii kwa vile Hadithi zao husaidia kuchangamsha na kushajiisha kuiga mwenendo wa maisha yao.
“ Kwa hakika Hadhithi za Maisha ya Mashujaa zikisomwa na kuzingatiwa hutuangazia mwanga  wa kuona uwezekano wa kubadilisha maisha yetu pengine siku moja na sisi tukaweza kugeuka tukawa kama wao au zaidi”. Alisema Balozi Seif.
Alimpongeza na kumshukuru Profesa Emmanuel Mbogo kwa mchango wake wa kupanda mbegu ya mashujaa wa baadae kupitia Tamthilia  yake  inayohusu Maisha ya Siti Binti Saad inayoweza kuzalisha katika Jamii hii akina Siti Binti Saad wengine  katika siku zijazo.
Balozi Seif alitoa wito kwa Vijana wa sasa kuisomaTamthilia hiyo ya Mtumwa hadi Siti Binti Saad na kuizingatia kwa vile inatoa funzo la umuhimu wa kung’ang’ania ndoto mpaka itowe matunda anayoyakusudia Mtu.
Alisema Vijana wengi kwa sasa wamejenga hulka ya kutojiamini na kuacha ndoto zao za Kimaisha na badala yake hutafuta njia za mkato ambazo mara nyingi haziwezi kuwaletea hatma njema ya maisha yao.
Balozi Seif aliwanasihi Vijana kuiga  mfano bora wa Marehemu  shujaa Bibi Siti Binti Saad kutokana na ujasiri wake aliyoujenga wakati alipoamua kuzisimamia ndoto zake zilizompa shime ya kujifunza kusoma na kuimba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akichambua baadhi ya maneno yaliyomo ndani ya Tamthilia hiyo ya kurasa 88 kwenye onyesho la kwanza katika kichwa cha Habari kisemacho Uchumba, akijikita zaidi kwenye lugha ya Mahaba alisema kwa sasa imetoweka katika jamii Nchini.
Alisema kutoweka kwa maneno matamu kunachangia kwa kiasi kikubwa Vijana wengi walio kwenye Ndoa kutumia njia ya mkato ya kutoa Talaka kwa Wake zao kutokana na kushindwa kuwashawishi kudumu kwenye ndoa kwa kutumia lugha ya Mahaba.
Balozi Seif  alifahamisha kwamba kukosekana kwa maneno matamu Mitaani hata katika Familia kipindi hichi cha kizazi cha sasa inawezekana ikawa ndio chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano katika Jamii.
“ Tafadhali egesha sikio lako kifuani kwangu ili upate kusikia jinsi moyo  wangu unavyodunda, ukikutaja, ukikuita na kusema  - Mtumwa,  nakupenda”. Balozi Seif akikariri baadhi ya maneno matamu kutoka kwa Bwana Khamis akitafuta penzi la Mkewe Bi. Siti.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Taasisi ya Siti Binti Saad Zanzibar kwa juhudi iliyochukuwa ya kufanikisha tukio hilo muhimu la uzinduzi wa Tamthilia ya Shujaa huyo wa Sanaa Afrika Mashariki ambayo itaendelea kubakia  sehemu ya Urithi wa Taifa hili.
Akitoa maelezo ya siku ya Urithi wa Utamaduni Duniani Mshika Fedha wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad Bibi Aziza Saleh alisema Taasisi hiyo kupitia Azimio linaloshajiisha Nchi zilizomo katika Uhifadhi wa Urithi wa Kimataifa limeandaa mambo yanayorithisha Vijana kurithi Tamaduni za Taifa.
Bibi Aziza alisema zipo hatua ambazo tayari zimeshachukuliwa kutekeleza Malengo hayo ikiwemo Makongamano ya Watu na Jumuiya tofauti, kutoa mafunzo ya uchoraji wa aina mbali mbali hata kuendeleza Lugha adhimu ya Kiswahili ambayo kwa sasa inashika nafasi ya Kumi Duniani.
Alieleza kwamba Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad bado inazingatia kutosahau thamani ya Utamaduni wa asilia unaopaswa kuonyeshwa kwa Vijana wa kisasa hasa upishi na vyakula vya Ladu za mtama, vileja, visheti pamoja na kashata za nazi na njugu  ili wathamini cha asili.
Akimkaribisha kuzindua Tamthilia ya Mtumwa hadi Siti Binti Saad Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,  Bibi Nasra Hilal alisema yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana tokea kuasisiwa kwa Taasisi hiyo Miaka Mitano iliyopita.
Bibi Nasra alisema ushirikiano wa karibu uliopatikana baina ya Wana Taasisi hiyo na Wadau wa Utamaduni wa Mswahili umewezesha kupiga hatua kubwa Malengo ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo ikiwemo matayarisho ya ujenzi wa Jengo la Utamaduni la Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Tamthilia ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikabidhi Hati za Uanachama wa Heshima kwa washirika wa Taasisi hiyo.
Uzinduzi huo wa Tamthilia ya Mtumwa hadi Siti Binti Saad umefanyika ukiambatana ndani ya Wiki ya Uhifadhi wa Urithi wa Utamaduni Duniani { World Culture Heritage Day } inayoadhimishwa na Umoja wa Mataifa { UN } kila ifikapo Tarehe 18 Aprili ya Kila Mwaka.
Mji Mkongwe wa Zanzibar { Maarufu Stone Town } umebahatika kuwemo miongoni mwa Miji iliyoidhinishwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Elimu, Sayansi na Utamaduni {Unesco} kuwa ndani ya Urithi wa Kimataifa.
 Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua Kitabu cha Tamthilia ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad kilichoandikwa na Profesa Em,manuel Mbogo.
 Waswahili wakijimwaga kwenye burdani ya muziki wa asili uliokuwa ukitumbuizwa na Kikundi cha Taarab cha Akheri Zamani hapo katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Tamthilia ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad kilichoandikwa na Profesa Em,manuel Mbogo.
 Balozi Seif Kulia akikabidhi Hati ya Uwanachama wa  Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimwa Ayoub Mohamed Mahmoud.
  Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Mwanaharakati ya Bibi Siti Binti Saad Bwana Mbarawa akimkabidhi Balozi Seif picha mahiri ya kuchora ya Bibi siti na Kikundi chake wakati wa enzi zake ya uimbaji.
 Balozi Seif Kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad mara baada ya uzinduzi wa Kitabu cha Tamthilia ya Mwanaharakati huyo.
Balozi Seif Kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha Taarab cha Akheri zamani kilichokuwa kikitoa burdani kwenye hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Tamthilia ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL 21,2019


WILAYA YA KILOSA YAEPUKANA NA UPOTEVU WA ZAO LA MPUNGA KUTOKA ASILIMIA 45 HADI 30

$
0
0
Wilaya za kilosa na mvomero mkoani morogoro zimefanikiwa kupunguza changamoto kubwa ya upotevu wa mazao ya mpunga mashambani kutoka asilimia 45 zilizokuwepo kufikia asilimia 30 jambo ambalo litawanufaisha wakulima wanaojihusisha na kilimo cha zao hilo.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa mradi wa kuwezesha makundi ya wanawake na vijana wanaojihusisha na kilimo cha mpunga kupunguza upotevu wa mpunga kabla na baada ya mavuno (ripoma) ulio chini ya shirika la elvetas tanzania, daniel kalimbiya ambaye amebainisha wameweza kudhibiti tatizo hilo kwa kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora, wanalima na kuvuna kisasa na kuhifadhi mazao yao kwenye maghala bora waliyojenga.

“wakulima walikuwa na changamoto kubwa hasa kwenye uzalishaji na kutunza mazao, hivi sasa upotevu wa mazao umepungua kutoka asilimia 45 hadi asilimia 30 huku pia tumefanikisha kuwafahamisha namna bora ya kutunza mazao kwa ubora Zaidi, amesema kalimbiya

Mkuu wa wilaya ya kilosa adam mgoyi akawasisitiza maafisa kilimo na mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo kusimamia vyema miradi yenye tija kwa wananchi kama ilivyo kwa mradin huo ili kuwa na muendelezo hata baada ya kumalizika ili ulete tija na mabadiliko kwa wakulima wa wilaya hiyo.

“ningependa kuwashauri wataalam kutoka halmashauri tuwe na mwenendo mzuri wa kushiriki katika kutunza na kufahamisha miradi yenye tija kama hii na tunatakiwa kuongeza umakini katika usimamizi hasa usimamizi mara baada ya kumalizika kwa mradi” amesema Mgoyi

meneja wa ripoma greyson regemalila akasema licha ya kudhibiti upotevu, kwa kushirikiana na mamlaka ya chakula na dawa tfda na shirika la viwango vya ubora nchini tbs wame7ongeza thamani ya mazao ya wakulima na kutoa msimbo milia yaani barcode kwa baadhi yao ili kuongeza thamani ya mazao kuuzwa ndani na nje ya nchi.



MAAZETI YA LEO JUMATATU APRIL 22,2019

MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA YANAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA -WAZIRI WA AFYA

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jisnia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema mapambano dhidi ya Malaria yanaonesha mafanikio makubwa kutokana na kushuka kwa Maambukizi hayo kutoka aslimia 14.5 mwaka 2015 hadi kufikia aslimia 7 mwaka huu.

Waziri Ummy amesema licha ya kushuka kwa maambukizi hayo lakini bado kuna mikoa kadhaa ambayo bado maambikizi ya ugonjwa wa Malaria yapo juu na hivyo kutoa wito kwa wadau kuongeza jitihada katika kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.

Mhe. Waziri ameitaja mikoa ambayo maambukizi ya ugonjwa Malaria yapo juu kuwa ni pamoja na Mara, Geita, Kagera, Mtwara, Lindi na Ruvuma ambapo amewataka wananchi kuongeza jitihada katika kupunguza kiwango cha Ugonjwa huo.

"Licha ya jitihada zinazofanywa kumaliza ugonjwa huu lakini bado jitihada zinahitajika zaidi katika kufikia lengo la ZERO MALARIA ifikapo 2030". Amesisitiza Mhe. Ummy.

Kuhusiana na maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya Malaria Duniani, Mhe. Ummy amewataka wananchi wote kushiriki katika kufikia lengo la Zero Malaria kwa kutomeza mazalia ya Mbu, kutumia vyandarua vilivyowekwa Dawa, kwenda hospitalini pindi wanapohisi wana viashiria vya Malaria na kumaliza dozi kama watakavyo elekezwa na watalaamu wa Afya.

"Wito wangu kwa watanzania wote ni kuhakikisha wanafuata maelekezo ya watoa huduma za afya pindi wauguapo Malaria na pia kuweka mazingira yao safi ili kukabiliana na mbu waenezao Ugonjwa wa Malaria" Alisema Mhe. Waziri.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Malaria kwa Mwaka huu ni ZIRO MALARIA INAANZA NA MIMI huku maadhimisho ya Siku ya Malaria hapa nchini yanatarajiwa kufanyika April 25, Mkoani Lindi.

RPC SHANNA ATAJA MAJINA YA MAJERUHI WA AJALI/DC MURO ATEMBELEA MAJERUHI

$
0
0

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shanna alipotembelea eneo la oldonyosambu ajali ilipotokea jana na kusababisha vifo vya watu wawili.
Kamanda wa wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna akitolea ufafanuzi ajali iliyotokea jana eneo la Oldonyosambo barabara ya Arusha Namanga.,Kulia kwakwe ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani hapa Joseph Bukombe
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akipokea maelezo kitoka kwa Dkt. Wa Halmashauri ya Arusha Petro Mboya katika hospital ya Seliani
Mkuu wa wilaya ya Arumeru jerry Muro akimjulia hali mmoja wa majeruhi aliyelazwa katika hospitali ya Seliani Ngaramtoni.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Arusha Dkt Petro Mboya akifafanua jambo kwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro.


Na. Vero Ignatus, Arusha

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limetoa onyo kali kwa madereva ambao wanendesha magari bila kufuata sheria usalama barabarani na kusababisha ajali katika kupoteza maisha ya watu sababu ya uzembe.

Onyo hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha kutokana na ajali iliyotokea jana eneo la Oldonyosambu na kusababisha vifo vya watu 2 na wengine 5 kujeruhiwa vibaya, amesema kwa dereva atakayekutwa na kosa la uzembe sheria itafuata mkondo wake.

Vilevile RPC Shanna ametoa onyo mitandao ya jamii ambayo inatoa taarifa ambazo siyo sahihi hazijathibitishwa, amesema mitandao mingi hapo jana ilieneza uvumi kwamba watu waliofariki ni 8 wakati siyo kweli na ikaleta taharuki katika jamii.

Amewataja majina kuwa ni bwana Robby Alan (kenya) Rajab Essa (mmakoe) (31)mkazi wa Arusha, Robby Mkurya (kenya) Anold Twahir (mshirazi) mkazi wa Arusha Shadrack Anold (13)ni mwanafunzi mkazi wa Arusha, Stellah Mathon Mngai(kenya ) (21)Bosco Mshanga mkazi wa Arusha wote hawa walikuwa abiria ndani ya magari hayo na wawili kati yao hali zao ni mbaya.

RPC amesema mbali na tukio hilo lililoleta majonzi, mkoa wa Arusha upo swari hakuna matukio mengine katika msimu huu wa sikukuu wala uhalifu kwani jeshi la polisi lilijipanga vilivyo na wananchi walionyesha ushirikiano mkubwa.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ajali ya Oldonyosambu inayodaiwa kuwa katika ajali hiyo watu nane Walifariki dunia kitu ambacho siyo kweli katika ajali hiyo watu wawili ndio Walifariki dunia.

Muro Ameyasema hayo mara baada ya kuwatembelea Majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Selian Lutheran Ngaramtoni ambapo ilitokea katika eneo la Oldonyosambu na kuwataka wananchi kuacha kukurupuka na kuandika ovyo katika mitandao ya kijamii vinavyozua taaruki pindi tatizo linapotokea badala yake wasubiri taarifa kutoka mamlaka husika.

Amewataka wananchi wa Arumeru na mkoa wa Arusha iwapo watataka kufanya matukio yoyote ambayo yatakuwa na kusanyiko lolote linalolenga shughuli pembezoni mwa barabara lazima tukio hilo liripotiwe kwa serikali ili serikali iwaandalie vitu vya Usalama na watu waache kufanya vitu kwa mazoea kwani serikali haiendeshwi kwa mazoea.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya Arumeru Petro Mboya amekiri kupokea miili miwili ya watu waliofariki hapo jana,majeruhi ambao wanaendelea kutibiwa ambapo wawili wameumia vichwani, mmoja uti wa mgongo na wengine wapo ICU ambapo mmoja wamemuhamisha kwaajili ya kufanyiwa vipimo zaidi.

VODACOM YATOA MAFUNZO YA TEKNOLOJIA ZA KIFEDHA KWA WANAFUNZI IFM

$
0
0
Meneja wa Biashara na Mkakati wa Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Caleb Majo (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa wa teknolojia za kifedha jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Semina hiyo imefanyika chini ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Green Hope ili kuhakikisha wanafunzi hao wanapata ufahamu wa teknolojia hizo na mchango wake katika kuchochea ushirikishwaji wa kifadha.
Meneja wa Biashara na Mkakati wa Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Caleb Majo (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa wa teknolojia za kifedha jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Meneja mauzo wa eneo la katikati ya jiji wa Vodacom Tanzania Plc, George Nyanda (kulia) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa wa teknolojia za kifedha jana jijini Dar es Salaam. Semina hiyo imetolewa chini ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Green Hope ili kuhakikisha vijana wanapata ufahamu wa teknolojia hizo na mchango wake katika kuchochea ushirikishwaji wa kifedha.
Meneja mauzo wa eneo la katikati ya jiji wa Vodacom Tanzania Plc, George Nyanda (kulia) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa wa teknolojia za kifedha jana jijini Dar es Salaam.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL 23,2019

Wateja wa Tigo Kilolo wapata huduma ya kasi zaidi ya 3G

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kililo Mkoani Iringa Philemon Namwenga  (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara mpya wenye uwezo wa 3G katika kijiji cha Idete, Wilaya Kilolo, mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani na wa kwanza kulia ni diwani wa viti maalum kata ya Idete Elina Kivegele na anayemfuatia ni Meneja Mauzo wa Tigo Iringa, Samwel Chanai.
 Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kililo Mkoani Iringa Philemon Namwenga (wa pili kulia) muda mfupi baada ya uzinduzi wa mnara mpya wenye uwezo wa 3G katika kijiji cha Idete wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mauzo wa Tigo Iringa, Samwel Chanai  diwani wa viti maalum kata ya Idete Elina Kivegelea
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Philemon Namwenga pamoja na Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani, wakisalimiana na wananchi wa kijiji cha Idete Wilayani Kilolo mkoani Iringa muda mfupi baada ya uzinduzi wa manra mpya wenye uwezo wa 3G kijijini hapo.
Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani (wa pili kushoto) akimuonyesha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Philemon Namwenga baadhi ya smart phone za gharama nafuu zinazouzwa na kampuni ya Tigo muda mfupi baada ya uzinduzi wa mara mpya wenye uwezo wa 3G katika kijiji cha Idete wailayani Kilolo. Wa kwanza kulia ni Meneja Mauzo wa Tigo Iringa, Samwel Chanai.

Kampuni ya mawasiliano ya simu, Tigo, leo imezindua mnara wa 3G katika kata ya Kidete, mkoani Iringa kama moja ya jitihada zake za kufikisha huduma bora za kupiga na kupokea simu, intaneti na kutuma na kupokea pesa kwa wateja wake.
Akizungumza katika uzinduzi huo katika kata ya Idete, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo, Aloyce Kwezi, aliwakaribisha na kuwashukuru Tigo kwa kuongeza ufanisi wa mnara huo kutoka teknolojia ya 2G hadi 3G.

Serikali ya Tanzania imefanya suala la viwanda kuwa agenda yake kuu. Na sisi kama serikali tunatambua umuhimu wa mawasiliano katika kufanikisha hii dira. Tunapenda kuwashukuru sana kwa kuifikiria Kilolo na wananchi wake, maana sekta hii ya mawasiliano ni chachu kubwa sana katika ukuaji na ubunifu wa viwanda mbalimbali,” alisema Kwezi. 

Kwa upande wake, Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini, Abbas Abdurahamani, alisema kwamba kipaumbele ya Tigo ni kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma za kisasa za kiteknolojia za simu kama ya 3G.
Uzinduzi wa leo unaofanyika Kilolo ni mwanzo wa kampeni ya nchi nzima ambapo kutakuwa na uzinduzi wa minara 52 kutoka Tigo zitakazo zinduliwa kutoka kanda ya Ziwa, Kaskazini, Pwani na Kusini. 

Uzinduzi wa minara uaenda sambamba na ofa maalum. Wateja ambao watahudumiwa na minara ambayo imeongezewa uwezo kutoka 2G hadi 3G. Wateja watazawadiwa kiasi cha MB 100 za data kila mara watakaponunua kifurushi chochote cha intaneti. Huku wateja katika maeneo ya minara ya 4G itakayozinduliwa, watazawadiwa GB 4 za data bure pale wanapobadilisha laini zao za simu kuingia 4G. 

“Kuongeza ubora wa mnara huu kutoka 2G kwenda 3G ina maana kwamba wateja wetu wa Kilolo sasa wataweza kupata huduma rahisi na kasi zaidi. Kwa mfano, 3G itaweza kuwapatia huduma ya intaneti iliyo bora ambayo itafungua jamii zilizopo vijijini kuweza kupata huduma za kielektroniki katika nyanja za kibiashara, afya, elimu na serikali ambazo walishindwa kupata huko nyuma. Jambo hili litabadilisha namna watu watakavyojifunza na kufanya biashara,” alisema Abdurahamani. 

Abdurahamani pia alisisitiza kuhusu kazi ambayo Tigo inafanya kuwezesha sera ya TEHAMA ya Taifa na kuunga jitihada ya serikali katika viwanda kwa kupanua na kuboresha wigo wa mtandao ili kuwezesha nchi kufaidika katika nyanja mbali mbali za kijamii kama uchumi na elimu kupitia mfumo wa kidijitali. 

Minara mengine ambayo imeboreshwa na zitazinduliwa hivi karibuni katika Kanda ya Kusini ukiondoa Kilolo zinapatikana katika maeneo ya Sumbawanga, Katavi, Mufindi, Njombe, Songwe, Mbeya and Songea.

MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAWAHUKUMU RAIA SABA WA SOMALIA KIFUNGO CHA MAISHA GEREZANI

$
0
0
 

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu raia saba wa Somalia kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya uharamia wa kuvamia meli na kuipiga risasi.

Washtakiwa hao walihukumiwa mwishoni mwa wiki mbele ya Jaji Yose Mlyambina baada mahakama kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi 14 wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mlyambina amesema, ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa na wote wametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kufungwa jela maisha.

Washtakiwa waliotiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo hicho ni Mohammed Nuru, Bashir Rooble, Muhsin Haji, Abdulwaidi Abdallahamani, Farahani Abdul, Ally Ally na Omary Mohammed.

Wote walikuwa wanakabiliwa na kosa la uharamia kinyume cha kifungu cha 66(1)(a)((I) na (2) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Katika kesi hiyo upande wa Jamuhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga, akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Cecilia Shelly na Wakili wa Serikali, George Barasa huku washtakiwa wakijitetea wenyewe.

Katika hati ya mashtaka imedaiwa, Oktoba 3 mwaka 2011 majira ya saa moja na nusu usiku maeneo ya Bahari ya Hindi, maharamia hao walifanya uvamizi kwenye meli ya Sams All good kwa kuipiga risasi hadi wanajeshi wa majini walipoanza kuipiga boti ndogo aina ya Skiff.

Wanajeshi hao walifanikiwa kuwakamata na kuwafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Pwani na February 29, mwaka huu ikasikilizwa na kutolewa maamuzi.

Wakati wa keai hiyo, washtakiwa waliwakilishwa mahakamani hapo na mawakili, Aloyce Komba, Domicus Mkwera, Rupia Abraham, Omary Msemo, Dennis Tumaini, Benedict Pius na Velasquez Severine.

RC Wangabo apongeza mshikamano na kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Jaochim Wangabo akitembelea maendeleo ya ujenzi wa jengo la Utawala katika hospitali ya Wilaya ya Nkasi wakati jengo hilo likiwa katika hatua ya msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Jaochim Wangabo akimpatia fredha ya “kunywa maji” mmoja wa wakinamama kwa niaba ya wakinamama wenzie wanaoshiriki ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Nkasi kama vibarua.

Baadhi ya vibarua wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi wakiendelea na pirika zao wakati Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ( hayupo pichani) alipokwenda kutembelea maendeleo ya ujenzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akisaidia kuweka mchanga kwenye viroba kwa mmoja wa kinamama walioshiriki ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi wakati alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Hoachim Wangabo (wa tatu toka kushoto) akipokea maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Nkasi kutoka kwa mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Said Mtanda (wa kwanza kushoto) wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Hoachim Wangabo (wa kwanza kulia) akipokea maelezo ya ufyatuaji wa matofali kwaajili ya ujenzi wa majengo saba ya hospitali ya wilaya ya Nkasi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Said Mtanda na kueleza kuwa matofali yanayohitajika ni 78,000 na hadi tarehe 18.4.2019 tayari wamefyatua matofali 58,000.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akijaribu uimara wa matofali hayo ambayo aliambiwa kuwa mfuko mmoja wa saruji unatoa matofali 20 kwaajili ya kujenga kuta za majengo saba ya hospitali ya wilaya ya Nkasi.

…………………………………………………………………………….

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amepongeza mshikamano uliopo katika uongozi wa wilaya ya Nkasi unaongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mh. Said Mtanda baada ya kuona namna uongozi huo ulivyojipanga katika kuhakikisha maelekezo na maagizo ya serikali yanatekelezwa kwa wakati hasa maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi.

Amesema kuwa mshikamano huo ni tunu kwa wanarukwa katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo na hasa linapokuja suala la utekelezaji wa upatikanaji wa huduma ambazo zinawagusa moja kwa moja wananchi waliokuwa wakisubiri huduma hizo kwa muda mrefu.

“Nimeona kwamba mmejipanga kwa kuleta vifaa, na kama hakuna vifaa ujenzi utasuasua, kuna mawe naona yanakwenda kwasababu yanahitajika kwa kasi kubwa, basi hilo eneo liwekewe nguvu kubwa sana, ndio eneo lenye hitaji kubwa kwa sasa na kama hakuna mawe tutashindwa kusogea hatua ya kuweka matofali hadi kufikia hatu ile ya linta,” alisema

Aliongeza kuwa hivi sasa mvua hakuna, hivyo ni wakati muafaka wa kuhakikisha vifaa vyote vinavyohitajika kwaajili ya ujenzi vinakuwa katika eneo hilo la ujenzi ili kila hatua ya ujenzi isikumbane na kikwazo cha kukosa vifaa na kutoa sababu ya mvua kuharibu barabara na hivyo vifaa kushindwa kufika.

Halikadhalika ametoa pongezi kwa namna vibarua wa ujenzi huo wanavyolipwa kwa wakati na kufanya kazi wakiwa wameridhika na malipo wanayopewa jambo linaloashiria kuwa ujenzi huo unakwenda bila ya dosari zozote na kuagiza kuwa hadi kufikia tarehe 10 Mei, 2019 majengo yote saba ya hospitali hiyo yawe yamefikia usawa wa linta ili kwenda na kasi ya utoaji huduma kwa jamii.

Mh. Wangabo ameyasema hayo alipokwenda kuona maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya inayojengwa katika makao makuu ya wilaya ya Nkasi mjini Namanyere ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa juu ya kuwataka Wakuu wa Mikoa kusimamia kwa karibu ujenzi wa hospitali hizo na hatimae kumalizika kwa wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda alisema kuwa ili kuhakikisha vibarua na wagonga kokoto wanalipwa na mafundi walioingia nao mkataba, wameweka utaratibu wa mafundi hao kuwalipa mbele yake, zoezi linalofanyika katika ukumbi wa ofisi yake ya wilaya na wakati huo huo wakitumia fursa hiyo kuwapatia wagonga kokoto hao vitambulisho vya ujasiliamali.

Imeelezwa kuwa ili majengo saba ya hospitali hiyo yakamilike yanahitajika matofali 78,000 huku hadi tarehe 18 Aprili,2019 matofali 58,000 tayari yameshafyatuliwa ili kuendelea na ujenzi huo.

SERIKALI YAKUSANYA KODI YA SH.MILIONI 5554 ZA TAULO ZA KIKE

$
0
0

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)


Serikali imesema kuwa imekusanya Sh. Milioni 3,010.5 kwa mwaka fedha 2016/17 na Sh. Milioni 2,545.6 kwa mwaka wa fedha 2017/18 za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika taulo za kike(sanitary pads) zilizozotengenezwa nchini na zilizoingizwa kutoka nje ya nchi.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Upendo Peneza (Chadema) aliyetaka kujua Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokusanywa na Serikali katika mwaka wa fedha wa 2016/17 na 20017/18.

Dkt. Kijaji alisema kiasi hicho cha kodi kilikusanywa kabla ya kuondolewa kwa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)Juni, 2018.

Katika maswali ya nyongeza, yaliyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Dkt. Immaculate Swale kwa niaba ya Mhe. Peneza, alisema pamoja na Serikali kuondoa baadhi ya kodi katika uzalishaji wa taulo za kike lakini bado bei ya bidhaa hiyo ipo juu, na kutaka kujua mkakati wa Serikali kushusha bei ya bidhaa hiyo ili kuhakikisha inawafikia walengwa.

“Kama Serikali imeshindwa kusimamia kushuka kwa bei, haioni kwamba iendeleze zile kodi za awali lakini kodi hii ikusanywe na iwe refinance ili kuweza kununulia hizi taulo za kike na izigawe bure mashuleni”, aliongeza Dkt. Swale.

Akijibu maswali hiyo, Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali haijashindwa kusimamia bei ya bidhaa hizo na kwa sasa inaendelea kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi ili kuona namna bora ya kuwafikia walengwa.

Alisema Serikali inaendelea kufanya tafiti mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuona namna ya kuwasaidia watoto wa kike ila kuna changamoto kodi inakusanywa ikiwekwa kwa ajili ya kununua na kugawa taulo za kike mashuleni.

“Yapo makundi mengine ambayo kodi zinazotozwa kwenye bidhaa zinazotumika na makundi hayo, tutatengeneza ombwe la kila kundi kuja kuomba kodi inayotozwa kwenye makundi hayo waweze kupewa wao”, alisema Dkt. Kijaji.

Aidha, Dkt. Kijaji alishauri kuwa kinachotakiwa kufanywa ni kubuni njia nyingine ili kuona watoto wa kike wanaweza kupata bidhaa hii bila kuhusisha kodi, au tozo zozote zinazotozwa katika bidhaa hii kwasababu imebainika kuwa inapoondolewa kodi wanaonufaika ni wazalishaji kwa kuwa taifa lipo katika soko huria.

Imetolewa na;

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC

RUKSA WANANCHI JIJI LA MBEYA KUWASILISHA KERO ZAO MBELE YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI-MWENYEKITI WA CCM MBEYA

$
0
0
Na EmanuelMadafa,Mbeya

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbeya mjini Humphrey Nsomba, amesema ni ruksa wanachi wa jiji la Mbeya kuwasilisha kero zao mbele ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli ambaye anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye sikuku za mei mosi zitakazo kitaifa Jijini Mbeya .

 Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujuo wa rais Magufuli jiji la Mbeya, Nsomba amesema kuwa  chama cha mapinduzi Mbeya mjini kimejipanga kikamilifu kumpokea kiongozi huyo mkubwa, kwani ujio wake utakuwa chachu ya maendeleo.

“Tumefurahi sana sisi kama Chama Wilaya ya Mbeya Mjini kuhusu ujio wa Mh Rais Katika Sherehe za Mei Mosi ambazo kitaifa zitafanyika  Jijini Mbeya,kwa Upendo huu ambao ametupa sisi wanambeya   tutajitokeza kwa wingi kwani tunahamu  kubwa ya kumuona na kusikia mambo mazuri kutoka kwake.”Mwenyekiti wa CCM  Wilaya ya Mbeya Mjini ,Afrey Msomba..

Amesema kitendo cha Rais Magufuli kukubali kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za Mei mosi ni heshima kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi na Mkoa wa Mbeya kwa Ujumla.

Amesema Rais Magufuli ametoa kiasi cha Shilingi Bil12 kwa ajili ya ujenzi wa barabara sita za Jiji la Mbeya pamoja kutoa Fedha za ujenzi wa Kituo cha Iyunga na Nzovwe hivyo wanakila sababu ya Kumshukuru.

Kufuatia hatua hiyo Mwenyekiti huyo wa Ccm Wilaya ya Mbeya mjini amewataka wakazi wa Jiji la Mbeya bila kujali itikadi ya vyama vyao kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za Meimosi ambazo zitafanyika katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini hapa .
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images