Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 182 | 183 | (Page 184) | 185 | 186 | .... | 1897 | newer

  0 0

  DSC_0960

  Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Jaji Mstaafu Amir Manento akizungumza na waandishi wa habari wakati mdahalo wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ambayo hufanyika tarehe 10 mwezi Disemba kila mwaka.

  .Jaji Manento asema ni uvunjifu wa sheria kwenda na watoto harusini

  Na Damas Makangale, MOblog
  WAZAZI na Walezi wameaswa kuacha mara moja tabia ya kwenda na watoto katika sherehe na harusi mbalimbali za kwa sababu ni kosa la Jinai kwa mujibu wa sheria na Haki za Mtoto. MOblog inaripoti.

  Akizungumza kwenye mdahalo wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ambao huadhimisha kila tarehe 10 mwezi Disemba kila mwaka, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, Jaji Mstaafu Amir Manento amesema kwa mujibu wa sheria na Haki za Mtoto wazazi au walezi hawaruhusi kwenda na watoto katika sherehe za usiku.
  “wazazi na walezi na watu wa kawaida wanamazoea ya kwenda na watoto kwenye sherehe za harusi na majumba ya starehe lakini kwa mujibu wa sheria na haki za mtoto na marekebisho yake ya 2009 ni uvunjifu wa sheria na haki za mtoto,” amesema Jaji Manento.
  DSC_0885
  Meza Kuu kati kati ni msimamizi (moderator) Dkt Khoti Kamanga toka UDSM, kushoto kwake ni Bw, Godfrey Mulisa toka UN, kushoto mwisho ni Mwakilishi Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Bw, Harold Sungusia na kulia kwa msimamizi ni Francis Nzuki kutoka Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala Bora na mwisho kulia ni Bi, Felistas Mushi toka Wizara ya Sheria na Katiba. Amesema kuwa Tanzania iliridhia tamko rasmi la Haki za Binadamu ili pamoja na mambo mengine kulinda Uhuru na Haki za Binadamu pamoja na haki ya kuishi.

  “Tarehe 10 Disemba imeainishwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Kuainishwa siku ya Kimataifa ya Haki za binadamu kunakumbusha juhudi kubwa zilizofanywa kwa lengo la kuwafanya watu waheshimu Haki za Binadamu kote duniani,” alisisitiza.

  Jaji Manento amesema suala la kuheshimiwa haki za binadamu lilipewa kipaumbele cha kwanza wakati wawakilishi wa nchi mbalimbali walipokuwa wakibuni Hati ya Umoja wa Mataifa.

  Aliongeza kuwa Januari mwaka 1947 iliundwa kamati ya haki za binadamu na hati ya kamisheni hiyo ilipasishwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Disemba 1948. Jaji manento amesema kuwa kwa msingi huo siku hiyo ya tarehe 10 Disemba ilitambuliwa kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu duniani kote.
  DSC_0930
  Mwakilishi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bw. Harold Sungusia akiwasilisha mada yake kuhusu historia na chimbuko la Haki za Binadamu katika bara la Afrika tangu enzi za miaka 1200 kwenye nchi ya Mali (Mali Empire).

  Amesema kuwa imepita zaidi ya miongo sita sasa tangu kutolewa Azimio la Haki za Binadamu ambalo linakusanya thamani za pamoja kwa ajili ya kuondoa ubaguzi, kueneza uhuru na kupambana na dhuluma dhidi ya binadamu duniani.

  Alilisitiza kwamba hapana shaka kuwa kutetea haki za binadamu kwa ajili ya kutimiza lengo hilo ni kazi yenye thamani kubwa. Hata hivyo aliongeza kadhia hiyo inayumbishwa na nchi za Magharibi ambazo zinatumia haki za binadamu na ripoti zinazotolewa na taasisi za haki za binadamu kama nyenzo na fimbo ya kisiasa kwa baadhi ya nchi zinazoendelea.
  Kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ni “mafanikio na changamoto katika kuhamasisha na kulinda Haki za Binadamu Tanzania” .
  DSC_1003
  Juu na chini ni Baadhi ya vijana wa shule za sekondari mbalimbali na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  DSC_0972
  Mjumbe kutoka Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala bora Bw, Francis Nzuki (wa pili kulia) akizungumzia uzoefu wake katika kuhamasisha Haki za binadamu katika Magereza nchini Tanzania hasa kwa Wafungwa.
  DSC_0989
  Mwakilishi kutoka Wizara ya Sheria na Katiba, Bi.Felistas Mushi akiwasilisha mada kuhusu kwanini kuna mpango mkakati wa serikali katika kutekeleza Haki za Binadamu nchini Tanzania.
  DSC_1052
  Mtaalamu wa mambo ya Utawala bora , Grainne Kilcullen kutoka UNDP akiwahamasisha vijana waliohudhuria mdahalo huo kuwa mstari wa mbele katika kusimamia Haki za Binadamu na kuwaelimisha jamii inayowazunguka kuzitambua Haki zao za msingi.
  DSC_1061
  Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, Jaji Mstaafu Amir Manento (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za sheria waTume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala bora, Bw. Nabor Assey ( wa pili lulia), Mtaalamu wa mambo ya Utawala bora , Grainne Kilcullen kutoka UNDP na Afisa Habari wa Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumziwa kwenye mdahalo huo.
  DSC_1025
  Pichani Juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakitoa maoni na kuchangia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mdahalo huo.
  DSC_1029
  DSC_1043
  Wanafunzi mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa Investigation Officer wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Getrude Alex (kushoto) juu ya machapisho mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini.
  DSC_1067
  Afisa Habari wa Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama akitoa neno la shukrani kwa wote walioshiriki mdahalo huo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Petired Bishop Elinasa Sendoro wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
  Sehemu ya wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Petired Bishop Elinasa Sendoro kulia na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Costa Ricky Mahalu katikati, wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata keki ya mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013, kulia Mkuu wa Chuo hicho Petired Bishop Elinasa Sendoro, kushoto Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Costa Ricky Mahalu.Picha na OMR

  0 0

  Na Miza Othman Maelezo-Zanzibar  .

  Serikali Jamii na Taasisi zisizokuwa za kiserikali zimeombwa kushughulikia suala la udhalilishaji wa kijinsia kwa vitendo ili kuhakikisha kwamba suala la ukatili wa kijinsia linaondaka kabisa  Visiawani hapa.

  Hayo yameelezwa leo huko Ea- crotanal na Mkurugenzi wa Maendeleo Wanawake na Watoto Rahma Ai Khamiss ikiwa ni  maadhimisho ya siku ya 16 za wanaharakati wakupiga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

  Amesema kwamba Wizara imetayarisha mpango wa utekelezaji wa kisekta zidi ya udhalilishaji wa kijinsia ambao unalengo la kuweka mtandao wa sekta na kuunganisha jitihata za kupiga vita vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

  Aidh Mkurugenzi Rahma Ali amesema kwani hivi sasa kumeshapitshwa sheria ya motto zidi ya uzalilishaji iliyopitishwa mwenzi wa Machi 2011 uliozingatia upatikanaji wa haki, fursa na ulinzi wa motto wakiwemo wakikie kupitia taasisi husika na jamii kwa ujumla.

  Wizara kwa kushirikiana na taasisi husika imefanyia mapitio sheria ya mahakama ya kadhi ya mwaka 1985 ili kubaini mapungufu yake katika kutoa haki kwa waathirika  wa vitendo vya udhalilishaji wakijinsia, alisema  Mkurugenzi Rahma Ali.

  Nae Msaidizi Afisa Watoto Mohammed Jabir Makame amesema endapo mtoto amefanyiwa ukatili wa kijinsia hupata athari ya ulemavu wa viungovya kawaida na uzazi,kushindwa kusoma vizuri,kuongezeka kwa mimba zisizo tarajiwa  na kuongezeka kwa virusi vinavyosababisha ukimwi. 

  Hata hivyo amesema ni vyema wazazi  kuwa na wawasiwasi  wa mara kwa mara na kuchukuwa jitihada za makusudi kwa kufuatilia nyenendo za watoto wao wakati wanapo kwaenda Skuli, Chuoni na hata wanapokwenda kucheza na wenzao.

  Kongamano hilo Dlilijumuishavitengo mbali mbali wakiwemo Askari, Dactarina Maafisa kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja,Kusini Unguja na Mkoa wa Mjini. Ujumbe wa mwaka huu ni Amani ya Duniani huanzia Nyumbani tupigane na vitendo vya utumiaji wa nguvu zidi ya wanawake na watoto.

  IMETOLEWA NAIDARAYA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.  

  0 0

  Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja Emmy Njau(kushoto) na kiongozi wa kitengo hicho Geoffrey Wilfred(kulia)wakiwafariji baadhi ya watoto wenye ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,walipofika hospitalini hapo kutoa msaada wa vyakula na viti vya kutembelea vyote vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000).

  =========  ========  =========
   Imeelezwa kuwa tatizo la watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi limekuwa kubwa zaidi tofauti na jamii inavyolichukulia tatizo hilo. Huku ikibainika zaidi kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa kwa mwaka na ugonjwa huo ni zaidi ya elfu huku 250 tu ndio wanafika katika taasisi ya tiba ya mifupa, mishipa ya fahamu na upasuaji wa Ubongo (MOI).

  Hayo yamebainishwa na Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Patrick Mvungi wakati akipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia kampeni ya pamoja na Vodacom inayoendeshwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

  “Tatizo la Ugonjwa wa kichwa kikubwa na uti wa mgongo ni kubwa sana katika nchi yetu na linaongezeka siku hadi siku, na tunapenda kuweka wazi kuwa tatizo hili linasababishwa na wakina mama, kuanzia wanapopata ujauzito hadi kufikia kipindi cha miezi mitatu hapa ndipo tatizo linapotokea, alisema, “Katika kipindi hiki mama asipokuwa anakula chakula chenye lishe (Lishe Bora) na kwenda Kliniki kwa wakati inapelekea kupata upungufu wa madini ya Folic acid.” 

  Alisema Mvungi na kuongeza “Tunahitaji jamii ituelewe na ndipo tunapo hitaji msaada wa wadau wengine kama Vodacom kutuwezesha kuweza kutoa elimu kwa jamii, kwa mfano hali ilivyo sasa, watoto wanaozaliwa na ugonjwa huu kwa mwaka inafikia zaidi ya elfu nne (4000) kwa mwaka, lakini watoto tunaowapokea hapa kwa mwaka wanafikia 250 tu. Ni jambo la kusikitisha sana. Alisema Mvungi na kuongeza.

  “Idadi ya watoto wanaozaliwa ukilinganisha na tunaowapokea hapa kwetu ni tofauti kabisa, wengi wanakuwa wanaamini tatizo hili linatokana na mambo ya kishirikina na inapelekea watoto wa aina hii kuuwawa wengine wanafichwa na wazazi wao, tunapashwa kuondokana na hali hii ili tuweze kukabiliana na tatizo hili.” Alihitimisha Mvungi.

  Akizungumzia juu ya misaada hiyo yenye thamani ya shilingi Milioni nane Afisa Mkuu  wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Vodacom Tanzania Harriet Lwakatare amesema kuwa kampuni yake itaendelea kuunga mkono sehemu muhimu zinazogusa maisha ya jamii kwani wao ndio wanaowaunga mkono kila siku.

  “Tunatambua mahitaji muhimu waliyonayo jamii ya Watanzania, hasa watoto hawa wenye ugonjwa huu wa Vichwa vikubwa na mgongo wazi, Tumeguswa sana na maisha ya watoto hawa na tumejisikia faraja kuwasaidia na kuwafariji, tumefarijika kuwa sehemu ya maisha yao,” alisema Lwakatare.

  Kwa upande wake moja ya Wazazi wa watoto hao amesema kuwa amefarijika kupokea misaada hiyo, na kuomba jamii iweze kumsaidia aweze kupata ada ya kuendelea kumsomesha mtoto wake.

  “Pamoja na tatizo hili alilonalo mtoto wangu ameweza kujitahidi kusoma hadi kufikia darasa la tatu lakini nimeshindwa kumuendeleza kwa sababu ya kukosa ada ya kuendelea kumsomesha naomba kwa mtu yoyote atakae kuwa na  uwezo wa kunisaidia anisidie japo kumsomesha tu.” Alisema Mzee Joseph Kaza, baba wa motto Selemsni Joseph (13) mwenye ugonjwa huo.

  0 0

  Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

  Zikiwa zimebaki siku mbili Tanzania iadhimishe miaka 52 ya Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadick ametoa wito kwa watanzania kusherehekea maadhimisho hayo kwa  kuenzi , kulinda na kudumisha mafanikio makubwa yaliyopatikana  tangu Uhuru.

  Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Meck Sadiki amesema kuwa Tanzania katika kipindi cha miaka 52 ya Uhuru imepata mafanikio makubwa ya kiuchumi, ulinzi, usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa na kuongeza kuwa mafanikio hayo yanatokana na umoja na mshikamano ulioonyesha tangu kuasisiwa kwa taifa la Tanzania.

  “Kipindi chote cha miaka 52 ya Uhuru  tumepata mafanikio makubwa sana na  ya kujivunia kiuchumi, ulinzi na usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa, tuna kila sababu ya kuendeleza mafanikio haya”

  Amesema maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru kwa mwaka 2013 kitaifa yatafanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete chini ya kauli mbiu isemayo “Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu, Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ya Taifa Letu”

  Ameongeza kuwa maadhimisho ya mwaka  huu yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi na kupambwa na burudani za vikundi vya ngoma za asili kutoka bara na visiwani,Gwaride maalum la vikosi vya ulinzi na Usalama, kwaya mbalimbali, bendi za muziki, maonyesho ya ndege za kijeshi na halaiki maalum. 

  Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi  na kuwahi mapema wakati wa maadhimisho hayo   na kubainisha kuwa kutokana na maadalizi mazuri yaliyofanyika milango ya uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:30 Asubuhi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraimu Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hali ya kuendelea kudhibitiwa kwa mfumuko wa bei nchini.
  ==========  ========  ==========
  MFUMUKO WA BEI NCHINI WAENDELEA KUDHIBITIWA.
  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema Tanzania inapiga hatua nzuri katika maendeleo ya uchumi kutokana na hali ya mfumuko wa bei nchini  kuendelea  kudhibitiwa  hali inayoleta unafuu wa maisha kwa mlaji.

   Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraimu Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwezi Novemba 2013 umepungua hadi kufikia asilimia 6.2 kutoka 6.3 za mwezi Oktoba 2013 kutokana na kupungua kwa bei za bidhaa na huduma.

  Amesema kuwa hali hiyo imesababishwa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula  kwa mwezi Novemba ikilinganishwa na mwezi Oktoba na kuongeza kuwa kumekua na ongezeko dogo la mfumuko wa bei wa bidhaa za nyumbani na migahawani hadi kufikia asilimia 7.6 kutoka 7.3 za mwezi Oktoba.

  Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula Kwesigabo ameeleza kuwa kasi ya ongezeko la bei imepungua hadi asilimia 5.7 kwa Mwezi Novemba 2013 kutoka asilimia 6.1 za mwezi Oktoba.

  Aidha amefafanua kuwa taarifa za matokeo ya  mfumuko wa bei unaopimwa  kwa kipimo cha mwezi unaonyesha kubaki kuwa asilimia 0.6 kama ilivyokuwa mwezi Oktoba huku fahirisi za bei zikiongezeka hadi kufikia 142.23 mwezi Novemba kutoka 141.39 za mwezi Oktoba

  Amezitaja baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kwa kuongezeka kwa fahirisi za bei kuwa ni pamoja na mahindi kwa asilimia 2.4, vitafunwa ailimia 4.0, unga wa Muhogo kwa silimia 2.5, nyama kwa asilimia 1.1, kuku kwa asilimia 3.7, samaki waliokaushwa kwa mafuta kwa asilimia 5.2, nazi asilimia 5.7.

  Bidhaa nyingine ni pamoja na dagaa kwa asilimia 2.5, mbogamboga kwa asilimia 3.0, nyanya asilimia 6.0, Maharage 4.5, karoti kwa asilimia 5.8 na viazi mviringo asilimia 4.6.

  Ameongeza kuwa mwenendo wa bei za bidhaa za vyakula hasa mchele  kwa mwezi Novemba 2013 umeonyesha kupungua kwa asilimia 26.0 ikilinganishwa na mwezi Novemba mwaka 2012, bidhaa nyingine zilizopungua ni mahindi kwa asilimia 9.4, unga wa mahindi 5.7, viazi mviringo 7.6 na karanga kwa asilimia 9.7.  

  Kuhusu mchango wa bidhaa zisizo za chakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi Novemba 2013  ni pamoja na mitandao kwa asilimia 4.7, radio asilimia 4.3 na vifaa vya kielectroniki kama luninga kwa asilimia 2.7.

  Hata hivyo kufuatia hali hiyo  ya mfumuko wa bei Bw. Kwesigabo ameeleza kuwa  uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii kwa mwezi Novemba umeonyesha kuwa imara kwa kufikia shilingi 70 na senti 31.

  “Napenda niwahakikishie kuwa fahirisi za bei za Taifa zimeonyesha kuwa na mwelekeo imara kwa kipindi chote, kwa hiyo uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umeonyesha kuwa na mwelekeo imara kwa kufikia shilingi 70 na senti 31 ” amesema.

  Kuhusu ulinganifu  mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umefikia asilimia 7.36 kwa mwezi Novemba kutoka asilimia 7.36 za mwezi Oktoba,  huku nchini wa Uganda Ukifikia asilimia 6.8 kwa mwezi Novemba  kutoka asilimia 8.1  za mwezi Oktoba.
   

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua kitambaa kuzindua mradi wa maji safi na salama katika shehia ya Chumbuni mjini Zanzibar zilizofanyika leo Disemba 7-2013, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua mradi wa maji safi na salama katika shehia ya Chumbuni mjini Zanzibar zilizofanyika leo Disemba 7-2013, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.(Picha na OMR). 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Bomba kuashiria kuzindua mradi wa maji safi na salama katika shehia ya Chumbuni mjini Zanzibar zilizofanyika leo Disemba 7-2013, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.

  0 0

  Pichani kati ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifafanua jambo mbele ya wananfunzi hao (hawapo pichani) baada ya kueleza kero zao. wengine kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa NJombe na Mbunge wa Njombe Kaskazini,Mh.Deo Sanga kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Naoe Nnauye na katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge Mteule, Dk. Asha-Rose Migiro.

  Ndugu Kinana na Ujumbe wake leo amekutana na Wanafunzi mbalimbali wa vyuo vya elimu ya juu mkoani humo na kusikiliza changamoto na kero zao mbalimbali na namna ya kuzifanyia kazi ikiwemo na kuzitatua.Kinana amefanya ziara maalum ya kikazi katika mkoa huo wa Njombe,baada ya kumaliza ziara yake ndefu ya mkoa wa Ruvuma na Mbeya,akiwa ameambatana na Wajumbe wa kamati kuu ya CCM,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asha-Rose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

  Kama vile haitoshi leo jioni kabla ya kurejea jijini Dar kwa njia ya Treni ya TAZAR kutokea Makambako, Ndugu Kinana alishiriki uzinduzi wa albamu ya kikundi cha Sanaa za Vichekesho cha mjini Njombe.

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wanafunzi hao jioni ya leo katika chuo cha Maendeleo ya Jamii,kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakumba,mkoani Njombe.
  Mkuu wa Wilaya ya Njombe,Mh,Sarah Dumba akitoa sehemu ya ufafanuzi kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo katika chuo cha Uuguzi Kibena,Mkoani Njombe wakati wa kujibu maswali ya wanafunzi wa chuo hicho kama waonekanavyo pichani.
  Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo cha Iringa akielezea changamoto mbalimbali zinazowakabiri mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake aliokuwa ameambatana nao.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akionesha Albamu ya Amani Tanzania iliyorekodiwa na kikundi cha vichekesho Sanaa Group,mkoani humo leo katika uzinduzi uliofanyika mkoani Njombe mbele ya mashabiki wa  kikundi hicho,hawapo pichani.

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua Albamu ya Amani Tanzania iliyorekodiwa na kikundi cha vichekesho Sanaa Group cha mkoani humo leo katika uzinduzi uliofanyika mkoani Njombe mbele ya mashabiki wa  kikundi hicho,hawapo pichani.Anaeshuhudia pichani (koti jeusi) ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Njombe na Mbunge wa Njombe Kaskazini,Mh.Deo Sanga.
  Pichani shoto ni Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asha-Rose Migiro wakijadiliana jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe,Mh.Deo Sanga pamoja na Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Kinana wakati wa uzinduzi wa albamu ya Amani Tanzania,ambapo wote walishiriki hafla hiyo.
  Baadhi ya Wanachama wapya wa CCM,kutoka vyuo vya juu mjini Njombe wakila kiapo huku wakiwa wamezinyanyua kadi zao juu mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo jioni.
  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akishiriki kupiga ngoma katika uzinduzi huo wa albamu ya Amani Tanzania.

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a joint press conference at the end of the Elysee Summit for Peace and Security held in Paris and ended this afternoon. The Summit discussed among other things, Peace and Security in Africa, The Economic partnership and Development and Climate Change. Others in the pictures from left The UN Secretary General Ban Ki Moon, The host French President Francois Hollande and right is Senegal’s President Macky Sall(photos by Freddy Maro).


  0 0

   Mshindi wa Kwanza wa Mbio ndefu za KM 42 katika Mashindano ya Uhuru Marathon,Jamin Ikai (kutoka nchini Kenya) akiwasili kwenye viwanja vya Leaders Club wakati akimaliza mbio hizo,zilizofanyika leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania.
   Mshindi wa Kwanza wa Mbio ndefu za KM 42 katika Mashindano ya Uhuru Marathon,Jamin Ikai akishangilia ushindi wake huo leo.
  Mshindi wa Tatu wa Mbio fupo za KM 21,Elia Daud akishangilia wakati akimaliza mbio hizo.
   Washindi wa Mbio ndefu za KM 42 katika Mashindano ya Uhuru Marathon wakiwa wamesimama mbele ya mgeni rasmi,mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.Mshindi wa Kwanza ni Jamin Ikai (kutoka Kenya),Steven Selevestor (kutoka Jeshi la Magereza Tanzania) pamoja na Aley Sanka (Tanzania).
   Washindi wa Mbio ndefu za KM 42 (wanawake) wakiwa wakiwa wamesimama mbele ya mgeni rasmi,mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.Mshindi wa wa Kwanza ni Thabita Kibet (kutoka Kenya),Naum Jerkosgei (Kenya) pamoja na Banoela Brigton.
   Washindi wa Mbio fupi za KM 21 (wanaume) wakiwa wakiwa wamesimama mbele ya mgeni rasmi,mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.Mshindi wa Kwanza ni Aliya Tirot (Kenya),Wilson Titoe (Kenya) pamoja na Elia Daud.
   Washindi wa Mbio fupi za KM 21 (wanawake) wakiwa wakiwa wamesimama mbele ya mgeni rasmi,mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
   Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Mbio za Uhuru Marathon,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mratibu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon,Innocent Melleck wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara.
   Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Mbio za Uhuru Marathon,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho mbio hizo zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania. 
   Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,wakati wa maadhimisho mbio hizo zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania. 
   Mkuu wa Wilaya Temeke,Mh. Sophia Mjema akizungumza wakati wa maadhimisho ya mbio hizo zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania. 
   Mratibu wa Mbio za Uhuru Marathon,Innocent Melleck akizungumza wakati wa maadhimisho ya mbio hizo zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania. 

   Wadau mbali mbali wakati kwenye maadhimisho ya mbio hizo zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania. 
   Mmoja wa washiriki wa mbioa hizo akitoa salamu ya Kijeshi kwa Makamu wa Rais.
   Washiriki Mbali mbali wa Mbio za Uhuru Marathon wakimaliza mbio hizo. 
   Wadau.
   Ankal Hashim Lundenga pia alishiriki mbio hizo.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo na familia zao wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia wa NBC kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa NBC wakichuana katika mchezo wa soka ili kumpata mshindi katika hafla hiyo leo.
  Hapa wakionyesha umahiri wa kucheza mpira wa kikapu katika sherehe hizo jijini humo leo.
  Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara wakifurahia kuogelea ndani ya bwawa la kuogelea katika hoteli hjiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Kulikuwa na aina mbalimbali za vyakula kukidhi haja ya kila mmoja aliyehudhuria sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa NBC jijini Dar es Salaam leo.
  Manahodha’ wa timu za michezo za benki hiyo wakionyesha umahiri wao kusakata rumba katika hafla iliyowakutanisha wafanyakazi na familia zao jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa wingi hivi sasa wilayani Makete, zimeshaanza kuleta madhara baada ya magari kuanza kuteleza kutokana na aina ya kifusi kilichomwagwa katika eneo la Mang'oto wilayani Makete barabara ya Makete - Njombe, kuteleza kupita kiasi

  Pichani hapo juu ni basi ma Mwafrika linalofanya safari zake kati ya Iringa-Makete likiwa limekwama kwa muda Kutokana na mvua zinazonyesha wilayani Makete, na hapa ni katika kata ya Mang'oto wilayani hapo, mita chache tu kabla ya kufika kwenye lami

  Hii inatokana na kifusi kilichowekwa kwenye barabara hiyo kuonekana na utelezi wa hali ya juu pindi mvua inaponyesha hata kwa sekunde chache
   
  Na Edwin Moshi

  0 0

   Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi cheti kwa Meneja Rasilimali Watu Uhusiano wa Kibiashara (HR Business Partner) wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Emmanuel Christopher (kulia), baada ya kampuni hiyo kupata tuzo ya utoaji mafunzo na maendeleo kwa wafanyakazi yakiwemo ya elimu ya jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bw. Almas Maige, Waziri wa Kazi na Ajira, Bi Gaudentia Kabaka na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Bw. Guy Ryder. Hafla hiyo ya kukabidhi tuzo kwa waajiri bora ilifanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Waziri wa Kazi na Ajira, Bi Gaudentia  akiipongeza TBL kupitia kwa Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo,Emmanuel Christopher
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Bw. Guy Ryder. akiipongeza TBL kupitia kwa Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo,Emmanuel Christopher

  0 0

  BONDIA Fransic Miyeyusho wa Tanzania amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wake na  David Chalanga kutoka Kenya utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani Klabu mchezo uhu wa kufunga mwaka na kufungua mwaka utakuwa wa raundi nane

  Utakuwa chachu kwa mabondia hawo wanaotamba Afrika Mashariki kugombea mikanda mikubwa ya ubingwa na kujiongezea rekodi ya ushindi mpambano huo unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki  wa mchezo wa masumbwi kila kona ya tanzania sasa imekuwa gumzo

  akizungumzia mpambano huo miyeyusho amesema yeye yupo fiti wakati wowote hule kwani ata sasaivi kama mpinzani wake yuko tayali yeye yupo kwa ajili ya kupigana katika mpambano huo kutakuwa na mapambano ya utangulizi

  bondia Iddy Mnyeke ataoneshana ubabe na Cosmasi Cheka,Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akizichapa na Mohamed Kashinde

  Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
  Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
  pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo vitakaokuwa vikitolewa na Super D kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha ngumi

  0 0

  Juma Nature akiwapagawisha mashabiki wake Dar Live.
  Mzee Yusuf akizikonga nyoyo za mashabiki.
  Tunda Man nae akikamua.
  Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Omar Kopa akiwapagawisha mashabiki.
  Snura Mushi ‘Mamaa wa Majanga’ na kundi lake wakitoa burudani.
  KR Muller wa kundi la Wanaume Halisi akifanya mambo jukwaani.
  Bambo akionyesha umahiri wake wa kukata mauno.
  Mwanamuziki JB 'Mkuu wa Majaji' akiwapagawisha mashabiki.
  Wanenguaji wa Snura wakionyesha machejo stejini.
  Khadija Kopa akiserebuka.
  Tunda Man akipeana ‘hi’ na mashabiki wake waliofurika Dar Live.
  Juma Nature (kushoto), KR (katikati) na Tunda Man wakipozi katika picha ya pamoja.
  Tunda Man (kushoto) akipozi na Snura.
  WASANII Juma Nature, Tunda Man, Snura, Mzee Yusuf, Malkia wa Mipasho Khadija Kopa, Bambo, JB 'Mkuu wa Majaji', usiku wa kuamkia leo ndani ya Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, Dar waliwasha moto katika shoo ya Sayona Twist.
  (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)

  0 0

   Wasanii wa Kikundi cha ngoma wakitumbuiza wakati wa Tamasha la mimi ni Afrika,Afrika ni mimi
   Kikundi cha ngoma kikiendelea kutumbuiza   Mshehereshaji wa Tamasha la mimi ni Afika,Afrika ni mimi Adam mchomvu akionge na wakazi wa arusha waliojitokeza kwa wingi kwenye viwnja vya general tyre.

   Adam mchomvu akifurahi na wakazi wa arusha
   Wakazi wa Arusha wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kupinga rushwa.
   Msaniii chaba akiwaburudisha wakazi wa Arusha jana
   Msanii chaba na back voclist wake wakiendelea kutawala stji jana kwenye viwanja vya general tyre
   Nasty Nastyyyy msaniiii chaba akiimbaaaa jukwaaani
   Msanii Joh makini akiwa kwa steji akiwaburudisha wakazi wa Arusha jana kwenye Tamasha la kupinga Rushwa mimi ni afrika na afrika ni mimi.
   Kundi la weusiiiiii wakikamata steji vilivyo jana kwenye viwanja vya general tyre


   Sema beiiii ya mkaaa,bei ya mkaaaa kundi la weusi wakiwaimbisha wakazi wa arusha jana kwenye Tamasha la kupinga Rushwa la mimi ni afrika na afrika ni mimi   Dogo janja akiwa kwa steji akiwarusha mashabiki
   Kundi la jambo Squadwakirukaaa kingarerooooo na mashabiki wao
   Machaliii machaliiiii wa araaaaa hivyo ndio ilikuwa ikisikika wakati jambo squad wakifanya yao jukwaaani.
   Msanii stamina akiwa kwa steji akiwarusha mashabiki

  Lile tamasha la kupinga matumizi ya Rushwa na utoaji limefana sana jana Jijini Arusha kwenye viwanja vya general tyre.Kauli mbiu ya tamasha hilo ilikuwa "RUSHWA SIO" na kubebwa na ujumbe mzito wa mimi ni afrika na afrika ni mimi.

  Dhumuni kubwa la tamasha hilo ilikuwa ni kutoa elimu kwa wanainchi juu ya madhara ya utoaji na upokeaji rushwa,kiingilio ilikuwa ni bure kabisaaa.Sambamba na elimu iliyotolewa viwanjani hapo pia wakazi wa Jiji la arusha walipata nafasi ya kupata burudani ya kufa mtu kutoka kwa wasanii kama izo b,stamina,weusi,chindo man,roma,fid q,linah,naziz na vanessa mdeee.  PICHA NA HABARI KWA HISANI YA DJ SEK BLOG

  0 0  0 0  0 0


  0 0

  Bwana Makamba akipata taarifa mbalimbali za chama kutoka kwa viongozi wa CCM DMV
  Na Swahili TV
  Mjumbe wa Halimashauri kuu ya CCM Taifa Bwana Januari Makamba alikutana na viongozi wa CCM DMV kwaajili ya kupata taarifa za uhai wa chama, kujua ugumu,mahitaji na mafanikio ya  kukiimalisha chama hicho.

  Katika kikao hicho cha faragha mjumbe huyo ambaye pia ni Naibu waziri wa sayansi & teknolojia na mbunge Bumbuli alipata taarifa kutoka kwa viongozi wa CCM DMV wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bwana George Sebo.Hadi sasa tawi la DMV limeshafungua mashina zaidi ya 4 ambayo yote yana wenyeviti na makatibu wake.
  Akisikiliza maelezo kutoka kwa katibu Mwenezi Bi salma Manyoka

  PICHA ZAIDI BOFYA SWAHILITV.BLOGSPOT.COM

older | 1 | .... | 182 | 183 | (Page 184) | 185 | 186 | .... | 1897 | newer