Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Mheshimiwa January Makamba akihutubia waTanzania DMV

$
0
0
Naibu Waziri wa Mawasiliani, Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba alipohutubia waTanzania na jamii zao waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika Laurel Maryland Desemba 7, 2013 kwa uratibu wa blog ya VIJIMAMBO

KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA ALHAJ SALUM CHIMA AONGOZA MAHAFALI YA KWANZA YA ISTIQAAMA ENGLISH MEDIUM AND PRE-PRIMARY SCHOOL YA MJINI SUMBAWANGA

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika mahafali ya kwanza ya shule ya Awali ya Istiqaama iliyopo Majumbasita katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa  Katika hotuba yake hiyo aliwaasa waislamu kuwaendeleza watoto wao kielimu katika taasisi za kidini zilizopo ili waweze kupata elimu zote za kitaaluma na kidini waweze kuwa na ujuzi na maadili mema. Aliwataka pia Waislamu kujenga tabia ya kuchangia taasisi zao ili ziweze kusonga mbele katika malengo waliojiwekea. Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Adam Misana. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Istiqaama English Medium and Primary School ya Sumbawanga Amr Said akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza katika mahafali hayo. Katika risala iliyosomwa kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima Shule hiyo ilianza rasmi Januari mwaka huu 2013 ikiwa na wanafunzi 48 na hidi hivi sasa ina wanafunzi 6. Shule hiyo inayoendeshwa na taasisi ya kidini ya ISTIQAAMA ina mpango wa kujenga shule ya msingi katika kipindi cha mwaka 2014-2017 na shule ya Sekondari katika kipindi cha mwaka 2018-2021.  
Zoezi la utoaji wa vyeti kwa wahitimu
Wahitimu wa kike
Wahitimu wakiumeni
Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo, kushoto kwao waliketi wanawake.
Baadhi ya watoto wakiwa wanacheza katika moja ya sehemu za michezo katika shule hiyo. Pichani nyuma ni sehemu ya madarasa ya shule hiyo.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

KINANA AWASILI JIJINI DAR LEO NA TRENI YA TAZARA AKITOKEA MAKAMBAKO

$
0
0

Katibu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakipokelewa jijini Dar na Wanachama wa CCM,wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Dar-Es-Salaam,Ramadhan Madabida.
Ndugu Kinana akisalimiana na Wanachama wa CCM,mara baada ya kushuka kwenye treni ya TAZARA mapema leo asubuhi akitokea na Makambako.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana Dkt.Asha-Rose Migiro Nape Nnauye wakishuka kwenye treni mara baada ya kusimama kwa muda katika kituo cha Mlimba,mkoani Morogoro kwa ajili kuzungumza na baadhi ya Wananchi.
Ndugu Kinana na Ujumbe wake akilakiwa na baadhi ya Wanachama wa CCM,kata ya Mlimba
Kinana na Ujumbe wake wakielekea kwenye jengo la abiria kituo cha Mlimba.
Nape Nnauye akiuliza bei ya Samaki huku Dkt.Asha-Rose Migiro akitazama.
Pichani kati ni Katibu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mkuu wa Kituo cha Polisi TAZARA Mlimba,ACP Boniface Haule,wakati alipofika kituoni hapo na kupata wasaa wa kuzumgza na Wasafiri mbalimbali waliokuwa wakisari na treni hiyo kuelekea jijini Dar.Shoto ni anaesikiliza ni Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dkt Asha-Rose Migiro.
Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya abiria waliokuwa wakisubiri treni ya TAZARA katika kituo cha Mlimba.
Treni ya TAZARA ikishusha na kupakia abiria kituo cha Mlimba,Morogoro.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwapa Karanga baadhi ya akina mama walikuwa wametokea Zambia na treni hiyo kuelekea jijini Dar.
Ndugu Kinan akiagana na baadhi wanachama wa CCM,waliofika kumsabahi katika kituo cha Mlimba,wakati treni hiyo ilipokuwa imesimama kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria ,Kinana aliongozana na Wajumbe wake,katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asha-Rose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi n Uenezi,Nape Nnauye wakitokea Ziarani Mkoani Njombe,baada ya kuikamilisha ziara yao ndefu ya Mbeya na Ruvuma katika mikakati ya kukiimarisha chama chao.

MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA YAFANA SANA LEO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi na usalama leo uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.
Sehemu ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakati kabla ya kamanda wa gwaride kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kukagua gwaride hilo leo jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akiwasili jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo.
Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.
Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa haraka.

Baadhi ya Maofisa wa jeshi wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam. Picha na 9.Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam waliojitokeza kuhudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Wananchi wakifatilia
Vijana wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”.
Vijana wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana mfano wa mnyama aina ya samba kuashiria utalii katika hifadhi za wanyama za Tanzania.
Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu.
Baadhi ya Maafisha wa Jeshi wakitoa salamu.
Ujumbe ukiwasilishwa kwa njia ya picha kuhusu viongozi wapigania Uhuru wa Tanzania Bara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Rolihlahla Mandela Madiba aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa watanzania na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo madarakani.
Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.
Raia wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

MPANGO WA KUCHNGIA ELIMU MAALUM K'NDONI WAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
Meya wa  wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akionyesha simu za mkononi zitakazo tumika kuchangisha fedha kwa ajili ya   Mpango maalumu wa kuchangia wanafunzi wenye ulemavu katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam baada ya kuuzindua rasmi. Mitandao ya simu itakayotumika  ni M-Pesa namba 0768727314 na Tigo Pesa namba 0712200022.


 Wanafunzi wenye Ulemavu wa kusikia(viziwi)pamoja na walimu wao wakiimba wimbo wa Taifa kwa kutumia lugha ya alama wakati wa uzinduzi Mpango  maalumu wa kuchangia wanafunzi wenye ulemavu katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam. Mitandao ya simu itakayotumika  ni M-Pesa namba 0768727314 na Tigo Pesa namba

 Meya wa  wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akizungumza kwenye uzinduzi  Mpango maalumu wa kuchangia wanafunzi wenye ulemavu katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Elimu Manispaa ya hiyo, Hussein Ramadhani na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo aliye mwakilisha Mkurugenzi…. Mitandao ya simu itakayotumika  ni M-Pesa namba 0768727314 na Tigo Pesa namba

 Mwenyekiti wa Vitengo vya Elimu Maalum katika Manispaa ya Kinondoni,Lessly Nyambo akizungumza kwenye uzinduzi  Mpango Maalumu wa kuchangia wanafunzi wenye ulemavu katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam.

wananchi wa mpwapwa wailalamikia serikali yao kwa kujengewa makaburi feki.

$
0
0
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoa Dodoma, wameulalamikia uongozi wa serikali yao kujenga makaburi feki pasipo kuwashirikisha wahusika wa makaburi hayo.


Wakizungumza  wananchi hao wamemtupia lawama mtendaji wa kijiji YONA MGANGA, na kusema kuwa serikali imeamua kuhamisha makaburi bila kufuata utaratibu.


Akizungumza EMANUELL MKIGA mmoja wa vijana walio pata tenda ya uhamishaji wa makaburi hayo ameelezea jinsi zoezi hilo la ujenzi wa makaburi feki lilivyofanyika katika kijiji hicho kwa kusema kuwa  walilipwa shilingi elfu tisa kwa ajili ya ujenzi.


ARFEDI NDEGEULAYA Mwenyekiti wa kijiji cha mpwapwa amethibitisha kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa yeye anafanya jitihada mbalimbali ili kumaliza tatizo hilo katika kijiji chake.




MeTL yazindua show ya mwaka kwa watoto na vijana

$
0
0
IMG_9729
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kusaidia jamii kupitia (Corporate Social Responsibility) kama njia mojawapo ya kupiga vita umaskini katika nchi za bara la Afrika. Kushoto kwake ni Meneja Mkuu Ledger Plaza Bahari Beach, Wissem Souifi, Kulia ni Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi na Kushoto ni Irfaan Jaffer kutoka MeTL.

.Lengo la maonyesho ni kusaka vipaji miongoni mwa vijana
.Kuanzia siku ya Krimasi hadi Boxing day zawadi mbalimbali na Tsh m kushindaniwa
Na Damas Makangale, MOblog-

KAMPUNI YA MOHAMMED ENTERPRISES (MeTL) Tanzania kwa kushirikiana Ledger Plaza Bahari Beach wamezindua maonyesho ya elimu ya mwaka kwa watoto nchini yenye kushindaniwa zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla kujinyakulia fedha taslimu Tsh5m.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwenye hoteli ya Ledger Plaze Bahari Beach Hotel, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Bi Fatema Jaffer, amesema kampuni ya Metl ina jail maslahi ya wateja wake na watanzania kwa kupitia dhana ya Kusaidia Jamii na Kujenga mahusiano (Corporate Social Responsibility) kwa kusaidia kuinua vipaji vya watoto.
“Kwenye maonyesho haya ya wazi ya kutazama vipaji mbalimbali vya watoto hasa kwenye elimu tumeamua kudhamini maonyesho haya ili kusaidia jamii kuweza kukuza vipaji vyao vya manufaa yao binafsi na jamii kwa ujumla,” amesema.

Bi. Jaffer amesema kuwa katika taifa la Tanzania kuna vipaji vingi hasa kwa vijana na watoto lakini wanakosa msukumo na jamii kuwatia moyo ili vipaji vile viweze kufanya kazi kwenye jamii na taifa kwa ujumla.

Amesema maonyesho hayo yataanza rasmi kuanzia tarehe 25th, 26 na 27 kwenye viwanja vya Ledger Plaze Bahari Beach yenye dhumuni ya kugundua, kutambua kuendeleza, kutia moyo na kupapanua vipaji vya watoto vilivyojivicha kwenye jamii ya watanzania.
IMG_9735
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho hayo ya watoto na vijana katika kuonyesha vipaji vyao mbalimbali.

Bi. Jaffer amesema maonyesho hayo yanaitwa (MO KIDS GOT TALENT) kwa sababu mdhamini mkuu ni Metl na watakuwa tayari kufanya kazi bega kwa began a watoto, vijana na wazazi wao katika kutambua, kuendeleza na kukuza vipaji vya watoto kupitia maonyesho haya.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Wissem Souifi, amesema maonyesho hayo ni jukwaa pekee kwa vijana na watoto wa Tanzania kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika elimu na Nyanja nyingine za kuburudisha.

“Maonyesho haya yatawajenga vijana kuwa na ujasiri na kuzalisha watu wenye mafanikio mbalimbali katika maisha na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele,” amesema
Amesema kuwa katika maonyesho hayo wazazi wanaombwa kuwaruhusu watoto wao waende kwenye tamasha hilo kubwa na la kipekee kuandaliwa na makapuni makubwa hapa nchini.
IMG_9722
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi, akihamasisha wazazi nchini kuruhusu watoto wao wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 25, 26 na 27 mwezi Desemba ambapo watoto 100 wa kwanza kujisajili wataingia bure.
DSC_0034
Kisura na Balozi wa MO Beauty Soap Jokate Mwegelo akielezea umuhimu wa tamasha hilo kubwa la Elimu kwa Vijana na manufaa ya kusaka vipaji kwenye umri mdogo ambapo pia amewataka wazazi kuwapa ushirikiano wa kukuza vipaji vya watoto wao.
DSC_0004
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
DSC_0064
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer kwenye picha ya pamoja na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi pamoja na Kisura na Balozi wa MO Beauty Soap Jokate Mwegelo.
DSC_0076
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali, Irfaan Jaffer kutoka MeTL Group pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Fros Africa, Bw. Peter Sekasiko.
DSC_0080
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi akimtembeza Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer maeneo mbalimbali ya hoteli hiyo.

RAIS KIKWETE NA VIONGOZI WAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA NELSON MANDELA LEO UWANJA WA FNB JOHANNESBURG

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura Bush wakiwa jukwaa la viongozi na watu mashuhuri baada ya  Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela leo Desemba 10, 2013 katika uwanja wa FNB jijini Johannesburg. PICHA NA IKULU
Add caption
 =========   ======== ============ 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Desemba 10, 2013, ameungana na viongozi wa mataifa mbali mbali duniani na maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela.


Maelfu kwa maelfu ya wananchi wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa nguvu kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee Mandela ambaye alikuwa ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa rangi za makaburu wa Afrika Mashariki.


Mheshimiwa Mandela ambaye alifariki duniani Ijumaa iliyopita, Desemba 5, 2013, alikuwa Kamanda wa Jeshi la Ukombozi la Chama cha African National Congress la Umkhoto we Sizwe akafungwa jela kwa uhaini kwa miaka 27 na utawala wa Makaburu.


Baada ya kutoka jela mwaka Februari 1990, Mzee Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini ya mwaka 1994. Lakini Mheshimiwa Mandela alitumikia kipindi kimoja tu cha miaka mitano na kukataa kutumikia kipindi cha pili.


Kiasi cha viongozi 91 kutoka sehemu duniani wamehudhuria Kumbukumbu hiyo iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa hisia – wengine wakiwa na majonzi na wengine wakicheza na kuimba kwa muda wote wa shughuli hiyo iliyochukua kiasi cha jumla ya saa tano.


Mbali na Rais Kikwete ambaye amefuatana na Mama Salma Kikwete, marais wengine mashuhuri duniani waliohudhuria Kumbukumbu hiyo ni Mheshimiwa Barack Obama wa Marekani, Mheshimiwa Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon.


Kumbukumbu hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa zamani wa Marekani wakiwemo marais watatu wa zamani wa Marekani – Mheshimiwa Jimmy Carter, Mheshimiwa Bill Clinton na Mheshimiwa George W Bush na mawaziri wakuu wawili wa zamani wa Uingereza, Mheshimiwa Tony Blair na Mheshimiwa Gordon Brown.


Rais Kikwete kesho, Jumatano, Desemba 11, 2013, ataungana na viongozi wenzake katia katika kutoa heshima za mwisho na kuuaga rasmi mwili wa Marehemu Mandela ambao utawekwa kwenye Majengo ya Urais wa Afrika Kusini ya Union Buildings mjini Pretoria.


(Kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Pretoria, Afrika Kusini)



MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA UBOU SABAA AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwa Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Ubou Sabaa (aliyeketi upande wa kulia).
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akitoa maelezo  juu ya maendeleo ya sekta ya nishati kwa Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Ubou Sabaa (aliyeketi upande wa kulia). Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya sekta ya nishati katika maeneo ya ulipaji kodi, mapato,  ujenzi wa bomba la gesi ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa shirika la Tanesco
Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Ubou Sabaa akizungumza katika kikao hicho. Makamu huyo aliambatana na ujumbe wake ambapo alifurahishwa na  kasi ya ukuaji  wa sekta ya nishati na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha pale itakapohitajika

watch live Madiba's memorial service!

Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...Majukumu ya Mama katika Familia

$
0
0
Muendeshaji wa kipindi cha FAMILIA Dada Georgina Lema akiongea nano katika Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion kwenye maada ya Majukumu ya Mama katika Familia.
Mubelwa Bandio pia akichangia maada katika kipindi cha Familia kinachoendeshwa na Dada Georgina Lema.

Baybe Mgaza akichangia kwenye  Kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Productuion...Majukumu ya Mama katika Familia.
Mgeni wetu rasmi kwenye kipindi cha FAMILIA  walikua ni Mayor Mlima.

Karibu katika kipindi hiki cha FAMILIA kutoka Jamii Production.

Katika kipindi hiki, tunaendeleza mjadala juu ya WAJIBU WA MZAZI KATIKA FAMILIA na kwa wiki hii, tumejadili WAJIBU WA MAMA KATIKA FAMILIA.

Mbali na washiriki waliokuwa studio, pia tuliweza kusoma maoni toka kwa wasikilizaji wetu wanaoacha katika kurasa zetu za FACEBOOK
Karibu uungane nasi


CHRISTIAN BELLA AOMBA KUSHIRIKI TAMSHA LA GURUMO JUMAMOSI HII TCC CLUB

$
0
0
MWIMBAJI anayesadikika kuwa na sauti tamu zaidi kwa sasa, Christian Bella kutoka Malaika Music Band, amesema atashiriki tamasha la Gurumo litakalofanyika Jumamosi hii kwenye viwanja wa TCC Club Chang’ombe.

Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo amesema Christian Bella, ameomba awekwe kwenye ratiba ya waburudishaji ambapo atapanda kuimba japo wimbo mmoja kama ishara ya kuonyesha kuukubali mchango wa gwiji Muhidin Maalim Gurumo.


Kama ilivyoelezwa hapo awali, tamasha la Gurumo, limeandaliwa mahsusi kwaajili ya kumuaga kwenye muziki wa jukwaani baada ya kutangaza rasmi kustaafu.



Mbizo ameongeza kuwa Christian Bella amesema miongoni mwa kazi anazozikubali sana hapa nyumbani, ni kazi za Msondo Ngoma chini ya Gurumo.

BANK OF AFRICA – TANZANIA HOSTS FAMILY DAY

$
0
0
 BANK OF AFRICA – TANZANIA hosted this year’s family day celebrations on Sunday at Landmark Hotel in Mbezi beach. The fun - filled event saw the bank engage their staff and their families in various sporting and mind games that sought to bring out creativity and innovation which forms part of the group’s core values.

Speaking during the event, the banks Managing Director - Mr. Ammish Owusu - Amoah stressed on the importance of family in the organization and that the bank will always strive to ensure that their staff concerns both in and out of the office are adequately addressed thereby reducing chances of staff suffering from depression or stress.  In addition, he reiterated that the event was meant to enhance a sense of togetherness within the bank in line with the banks slogan “As close as a group as strong as a partner” hereby clarifying that the same not only applies to the relationship with the banks to its customers but also to their relationship with staff and their families.


He further mentioned that the event saw the bank group the staff and their families into 4 teams that will compete with each other and see 8 winners being awarded from those groups depending on the different games they will have engaged in. Moreover, the Managing Director took this time to remind the community to be mindful of others in society as we approach the December festivities and that the bank looks forward to serving them as we close the year 2013 and look forward to 2014. He also thanked the banks customers for choosing BANK OF AFRICA – TANZANIA and they are looking forward to serving them even better in the year 2014.



BANK OF AFRICA TANZANIA LTD has a network of 19 branches in Tanzania currently. 10 branches are located in Dar es Salaam, and the other 9 branches are in the region of Arusha, Mwanza, Kilimanjaro (Moshi), Morogoro (Morogoro city centre and Mtibwa), Mbeya, Tunduma Kahama and Mtwara. 

USIKU WA WAKONGWE WA MUZIKI WA DANSI

WAPO KAZINI WAKITAFAKARI KWA KINA

$
0
0
ULINZI NA USINGIZI NI HATARI !! Hawa ni walinzi wa kutumainiwa  boss akilini unajua wako vijana wa kazi wanalinda biashara yako kumbe wamelala! Taswira hii imechuliwa pale IPS Building mitaa ya posta! 
Na. Mdau Aron.

Vionjo, vyakula vya asili kupatikana ndani ya Tamasha la Handeni Kwetu Jumamosi

$
0
0
BAADHI ya vyakula vya asili ya Handeni, vinatarajiwa kuwapo katika Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu 2013 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika Viwanja vya Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
 
Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa tayari wametoa nafasi kwa wanaoweza kazi hiyo kwa umakini na usafi wa aina yake ili kuliweka tamasha hilo kwenye mguso wa aina yake.
 
Alisema taratibu zote zimeshafanyika ikiwamo kutembelea vikundi vitakavyotoa burudani, ambapo Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alitumia muda mwingi kuwahamasisha wadau kuhudhuria kwa wingi katika tamasha hilo, kupitia sherehe za Uhuru zilizofanyika wilayani humo Desemba 9 mwaka huu.
 
“Kila kitu kimekamilika, tukiamini kuwa wadau wote watakaohudhuria kwenye tamasha hilo watapata fursa ya kula vyaku7la vya asili, maana pia ni sehemu ya utamaduni wa Handeni.
 
“Sisi tunaamini hili ni tamasha la aina yake ambalo litashangaza watu wengi kutokana na kuandaliwa kwa kiwango cha juu, huku likianzia kwa maandamano katika Ofisi za Halmashauri ya mji Handeni kuanzia saa 2 asubuhi na kuelekea Uwanja wa Azimio,” alisema.
 
Kwa mujibu wa Mbwana, watu hawataruhusiwa kuingia uwanjani na vyakula wala vinywaji ili kudhibiti suala la afya za watu kwa kupitia tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na Watanzania wote, hususan wapenzi wa utamaduni hapa nchini.

Wadhamini katika tamasha hilo ni gazeti la Mwananchi, Clouds Media Group, Phed Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters, Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD), Michuzi Media Group, duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Partnership, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.

Samson Mwigamba (CHADEMA),aomba mwongozo kwa msajili wa Vyama kuhusu mgogoro uliopo ndani ya Chama chake

Zitto Kabwe akata rufaa ya kupinga kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya chama chake

MDAU DADA DORA ANATAFUTA MWENZA WA KUISHI NAYE.

$
0
0
Salamu ndugu yangu Michuzi, pole sana na shughuli za kila kukicha. Jina langu naitwa dada Dora, natafuta mwenza wa kuishi naye hivyo nimeona nitumie blog yako labda ninaweza fanikiwa kupata mtu sahihi.

Mtu ninayemtafuta, awe na umri kuanzia miaka 32 mpaka 44 sio mbaya, pia awe hajaoa wala hana familia kwa maana ya mke na watoto. Ni vizuri kuishi na mtu mnayeendana, hivyo ningependa awe mkristo, dhehebu lolote haijalishi mradi awe mcha Mungu na atambue uwepo wa Mungu.

Pia awe na elimu kuanzia degree. Mimi kwa sasa nipo nje ya Tanzania, naomba atakaye niandikia asiandike tu sababu ameona tangazo bali awe na nia ya dhati ya kuanzisha familia hivi karibuni. mwenye malengo ya maisha, mpole na asiwe mbabe. Ajue nini maana ya kuwa mme. Awe pia mwepesi wa mawasiliano, yeyote anayeona yupo busy sana na hataweza mawasiliano ya mara kwa mara tafadhali naomba asiniandikie.
Kwa aliye tayari napatikana kwenye barua pepe:

Hotuba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF George Yambesi kwa waTanzania Washington DMV

$
0
0
Hotuba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Manejimenti ya Utumishi wa Umma , George Yembesi alipozungumza na waTanzania waishio Washington DC waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika Laurel Maryland Desemba 7, 2013 kwa uratibu wa blog ya VIJIMAMBO
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images