Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1836 | 1837 | (Page 1838) | 1839 | 1840 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Mkoani Tanga (Tawla) Mwanaidi Kombo akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya sheria katika masuala ya ardhi na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga yaliyoandaliwa na chama hicho
   Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga Wakili Latifa Ayoub akizungumza wakati wa wa mafunzo ya sheria katika masuala ya ardhi na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga yaliyoandaliwa na chama hicho
   Mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Kisiwani wilayani Muheza Mwansiti Bashiru akizungumza wakati wa mafunzo hayo
   Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo
  Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo wakimsikiliza muwezeshaji.
   Washiriki wakipata picha ya pamoja mara baada ya kumalizika mafunzo hayo
  MFUMO dume, mila kandamizi kwa wanawake kwenye kumiliki ardhi vimetajwa kuchangia kwa asilimia kubwa upotevu wa haki zao katika jamii zinazowazunguka.

  Hayo yalisemwa na Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Mkoani Tanga (Tawla) Mwanaidi Kombo wakati wa mafunzo ya sheria katika masuala ya ardhi na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga.

  Alisema vikwazo vingine ni mila za kibaguzi kwa wanawake ambazo zimechangia kwa asilimia kubwa upotevu wa haki za wanawake hasa kwenye kumiliki ardhi na kujikuta wakishindwa kupata haki yao ya msingi.

  “Kwa kuliona hili na ndio maana sisi kama Tawla kumeamua kutoa mafunzo ya kuongezea uelewa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga kwa lengo la kuweza kutambua haki zao na namna ya kuweza kuzidai inapotokea “Alisema

  Alisema licha ya hivyo lakini pia wameamua kuanza kutoa elimu kwa kundi la wanawake ikiwemo kuanzisha klabu mbalimbali za mashuleni lengo likiwa ni kuwaoa elimu wanafunzi ili waweze kujua haki na kuweza kupunguza ubaguzi kwenye jamii.

  Awali akizumza mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Mkazi wa Bweni wilayani Pangani Mwajuma Ally alisema wanashukuru kupata elimu hiyo ambayo imewafungua kuweza kutambua haki zao na namna ya kuweza kuzidai kwa kutumia sheria.

  Mwajuma alisema awali walikuwa hawatambua wapi wanaweza kwenda kudai haki zao wakati wanapokumbana na changamoto kwenye ndoa hususani yanapokuwa yakijitokeza matatizo mbalimbali.

  Mafunzo hayo ya siku mbili yamewashirikisha washiriki kutoka wilaya za Pangani, Tanga na Muheza ambao kwa pamoja wanapewa elimu katika masuala ya ardhi na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara kuu ya TANZAM sehemu ya Mafinga-Igawa km 138.7 katika sherehe zilizofanyika Wanging’ombe Makambako mkoani Njombe.
   Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara kuu ya TANZAM sehemu ya Mafinga-Igawa km 138.7 katika sherehe zilizofanyika Wanging’ombe Makambako mkoani Njombe.
    Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Makambako mara baada ya kuwasili katika eneo la viwanja vya Polisi Makambako mkoani Njombe.
   Barabara Kuu ya TANZAM sehemu ya Mafinga-Igawa km 138.7 ambayo ukarabati wake wa Ujenzi umekamilika kama inavyoonekana.
   Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mtwango Makambako wakati akielekea kwenda kufungua mradi wa barabara.
   Ngoma ya mganda ikitoa burudani katika viwanja vya Polisi Makambako mkoani Njombe mara baada ya ufunguzi wa barabara hiyo. PICHA NA IKULU

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, wakati alipo wasili kufungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Aprili 11, 2019, katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephen Wasira, wakati alipo wasili kwenye ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Aprili 11, 2019, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Tokea kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, kwenye ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Aprili 11, 2019, katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoka kwenye jengo la Utawala la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam, kabla ya kufungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Aprili 11, 2019. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephen Wasira, kwenye ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephen Wasira, akihutubia kwenye ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo la kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakipiga makofi wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo.
  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akimkaribisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili kufungua kongamano hilo.
   
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia, kwenye ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililofanyika katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaaga wanafunzi na washiriki mbalimbali mara baada ya ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililofanyika katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0


  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Benjamin Sita akikata utepe kuzinduwa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kilichopo Kijitonyama Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Omar Nundu pamoja na Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ally Mbega (katikati).
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Benjamin Sita (kushoto) akizungumza alipokuwa akizinduwa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kilichopo Kijitonyama Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Omar Nundu pamoja na Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ally Mbega (katikati).

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Benjamin Sita akikata utepe kuzinduwa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kilichopo Kijitonyama Dar es Salaam.

  Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Ally Mbega (katikati) akizungumza kwenye afla ya uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha TTCL kilichopo Kijitonyama Dar es Salaam.  SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), leo limezinduwa Kituo cha Huduma kwa Wateja katika eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma bora kwa Wananchi za shirika hilo.

  Akizinduwa kituo hicho, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Ndugu, Benjami Sitta amelipongeza shirika hilo kwa kuendelea kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kusogeza karibu zaidi na Wananchi.

  Alisema ulimwengu wa sasa umetawaliwa na maendeleo makubwa ya Sayansi na Teknolojia ambapo dunia imekuwa kama Kijiji, hivyo kuitaka TTCL kutumia vyema faida hiyo ya Maendeleo ya kiteknolojia kwa kuhakikisha kuwa Huduma zinazotolewa zinakidhi mahitaji ya Wateja.

  "...Sina shaka na uwezo katika Eneo la Huduma kwa Wateja ila nashauri msibweteke, endeleeni kuwa mfano bora kwa wengine. Kituo hiki kiwe wazi muda wote uliopangwa, bidhaa zote za TTCL na T PESA zipatikane, Watumishi watakaotoa huduma hapa wawe na Weledi, wazingatie Lugha nzuri, ucheshi na Maadili ya kazi. Kwa kufanya hivyo, wateja wenu watageuka mabalozi wa kulitangaza Shirika letu kwa Wadau wengine.

  Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation ambaye ni Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo, Ally Mbega alisema uzinduzi wa Kituo hicho cha Huduma kwa Wateja ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu (Strategic Business Plan 2016-2019) ambao umeweka msisitizo mkubwa katika kuboresha eneo la Huduma kwa Wateja.

  Aidha aliongeza kuwa uzinduzi wa Kituo hicho unaonesha kwa vitendo jinsi gani TTCL mpya ilivyojipanga vyema kuhakikisha huduma zake zinawafikia Wateja katika mazingira mazuri, nadhifu,yanayovutia na kubeba hadhi ya Shirika."Kukamilika kwa Kituo hiki cha Huduma kwa Wateja kunaongeza idadi ya Maduka/Vituo vya Huduma kwa Wateja vipya na vilivyoboreshwa kufikia 13 ambavyo vimejengwa kwa viwango vya hali ya juu na kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya utoaji bora wa Huduma kwa Wateja," alisema Bw. Mbega.

  Pamoja na hayo alibainisha kuwa, TTCL itaendelea kuboresha Maduka na Vituo vyake Nchi nzima, sambamba na Ofisi za Mikoani na Wilayani ili ziweze kuwa mahali bora kwa Watumishi wa TTCL kutoa huduma na Wateja wote watakaofika kupata huduma za aina mbalimbali.
  Baadhi ya watoa huduma wa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) cha Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja.
  Sehemu ya wafanyakazi wa TTCL pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya viongozi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Benjamin Sita mara baada ya hafla ya uzinduzi.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari akifungua mkutano wa wadau kujadili uanzishwaji wa tozo za usalama katika Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Abeid Amani Karume (AAKIA) na Kilimanjaro(KIA) zilizopendekezwa na Menejimenti za Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA) na Kampuni ya Maendeleo Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO) uliofanyika jiji Dar es Salaam. 
  Wadau wa Usafiri wa Anga wakifuatilia wasilisho la Menejimenti za Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA) na Kampuni ya Maendeleo Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO) kwenye mkutano wa wadau kujadili uanzishwaji wa tozo za usalama Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Abeid Amani Karume (AAKIA) na Kilimanjaro (KIA) ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na kufanyika jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa Uendeshaji na Ufundi wa KADCO Mhandisi Martin Kinyamagoha akizungumza kwenye mkutano wa wadau kujadili uanzishwaji wa tozo za usalama katika Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Abeid Amani Karume(AAKIA) na Kilimanjaro(KIA) zilizopendekezwa na Menejimenti za Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA) na Kampuni ya Maendeleo Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO). 
   Mkurugenzi wa Viwanja ZAA, Zaina Ibrahim Mwalukuta akizungumza kwenye mkutano wa wadau kujadili uanzishwaji wa tozo za usalama katika Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Abeid Amani Karume(AAKIA) na Kilimanjaro(KIA) zilizopendekezwa na Menejimenti za Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA) na Kampuni ya Maendeleo Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO). 
  Meneja Usalama wa KADCO , Kisusi Justine Makomondi akiwasilisha pendekezo kwa wadau katika mkutano wa wadau kujadili uanzishwaji wa tozo za usalama katika Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Abeid Amani Karume(AAKIA) na Kilimanjaro (KIA) zilizopendekezwa na Menejimenti za Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA) na Kampuni ya Maendeleo Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO). 
  Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Huduma Viwanjani, Mhandisi Wales Cassius Chiwawa akifuatilia wasilisho la Menejimenti za Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA) na Kampuni ya Maendeleo Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO) kwenye mkutano wa wadau kujadili uanzishwaji wa tozo za usalama Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Abeid Amani Karume (AAKIA) na Kilimanjaro (KIA) ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na kufanyika jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza Johari (kulia) akizungumza na Mwandishi wa Habari wa Televisheni ya Azam, Temaluge Kasuga, kwenye mkutano wa wadau kujadili uanzishwaji wa tozo za usalama katika Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Abeid Amani Karume(AAKIA) na Kilimanjaro(KIA) zilizopendekezwa na Menejimenti za Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA) na Kampuni ya Maendeleo Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO). 
  Mkuu wa Kitengo cha Usalama Usafiri wa Anga TCAA , Burhan Majaliwa (kulia) akiongea na wadau katika mkutano wa wadau kujadili uanzishwaji wa tozo za usalama katika Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Abeid Amani Karume(AAKIA) na Kilimanjaro(KIA) zilizopendekezwa na Menejimenti za Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA) na Kampuni ya Maendeleo Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO).

  0 0

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina akiwahutubia wafugaji wa kijiji cha Kimotorok wilayani Simanjiro wakati wa uzinduzi wa program ya kitaifa ya mafunzo kwa wafugaji nchi nzima. 
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina akikata utepe kuashiria uzinduzi wa program ya kitaifa ya mafunzo kwa wafugaji nchi nzima katika kijiji cha Kimotorok wilayani Simanjiro.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina akivalishwa shuka la kimasai na mzee wa mila wa kabila la kimasai Ezekiel Lesenga kama ishara ya kumsimika katika uongozi wa sekta ya ambapo alipewa jina la Ole Mpina wakati wa uzinduzi wa program ya kitaifa ya mafunzo kwa wafugaji nchi nzima katika kijiji cha Kimotorok wilayani Simanjiro.


  Na John Mapepele

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema Wizara imeanza program maalum ya kitaifa ya kuwafundisha wafugaji na wavuvi kote nchini  kuhusu sheria za mifugo na uvuvi na sheria nyingine hatua itakayowezesha kujua haki zao na kujiepusha na migogoro baina yao na watumiaji wengine wa ardhi kwa upande wafugaji ambapo kwa upande wa uvuvi Wizara itawafundisha ufugaji bora wa samaki,utekelezaji wa sheria na kanuni za uvuvi,udhibiti wa ubora wa mazao ya uvuvi na ushirika wa wavuvi ili kuboresha maisha yao.

  Akizindua mafunzo hayo kitaifa katika Kijiji cha Kimotorok Wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina alisema mafunzo kwa wafugaji yatawezesha wafugaji kutambua namna ya kutumia fedha zitokanazo na mifugo na mazao yake kwa kuwekeza maeneo mengine kujenga makazi bora, kusomesha watoto, kukata bima ya mifugo na kujiwekea akiba benki.

  “Leo tunaanza kuzindua mafunzo kwa wafugaji lengo likiwa ni kuwawezesha kuzijua sheria za mifugo na kutambua haki zao ili kujiepusha na migogoro baina yao na majirani zao wakiwemo wakulima, wahifadhi pamoja na kuelimishwa mbinu za kisasa za namna ya kuboresha maisha na ufugaji.” Alisisitiza Mpina

  Alisema kwa pande ufugaji sheria zitakazofundishwa kuwa ni pamoja na Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Namba 17 ya mwaka 2003, Sheria ya Ustawi wa Wanyama namba 19 ya mwaka 2008, Sheria ya Nyanda za Malisho na Raslimali za Chakula cha mifugo Namba 13 ya mwaka 2010 pamoja na Sheria ya Wanyama pori Namba 5 ya Mwaka 2009.

  Pia wafugaji hao watafundishwa namna ya kudhibiti magonjwa ya kimkakati 12 ambayo yanadhibitiwa kwa njia ya chanjo ikiwemo Sotoka ya mbuzi(PPR), Homa ya mapafu ya ng’ombe(CBPP), Ugonjwa wa miguu na Midomo(FMD), Homa ya mapafu ya Mbuzi(CCPP),Mdondo(ND)Homa ya Bonde laUfa(RVF).

  Magonjwa mengine ni Mapele ya Ngozi (LSD) Homa kali ya Nguruwe(ASF) Ndigana Kali (ECF) Kimeta(Anthrax), Kichaa cha Mbwa (Rabbies) na ugonjwa wa wa kutupa mimba(brucullosis) na kuokoa vifo vingi vya mifugo vinavyosababishwa na magonjwa hayo.

  Pia wafugaji watafundishwa matumizi sahihi ya dawa,chanjo na viuatilifu vya mifugo nchini,uzalishaji wa mbegu bora za malisho, utunzaji wa nyanda za malisho na machunga , ufugaji kibiashara na kuweka utaratibu wa kuvuna mifugo na kuanzisha ushirika wa wafugaji.

  Hivyo Waziri Mpina aliwahimiza wafugaji kote nchini kuchangamkia mafunzo hayo kwani ndio yatakayokuwa mkombozi baada ya kuishi kwa zaidi ya mika 50 hivyo Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kwa dhati kuwakomboa kutoka kwenye dhiki na dhuluma waliofanyiwa.

  Pia Waziri Mpina alimwagiza Katibu Mkuu wa Mifugo kuhakikisha anakarabati bwawa la Narakauo katika Kijiji cha Loibosoit kwenye Wilaya ya Simanjiro katika kipindi cha miezi miwili toka sasa ili kutatua tatizo sugu la maji kwa ajili ya kunywesha mifugo na binadamu.

  Aidha alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefled Myenzi kufanya marekebisho kwa majosho yote yaliyoharibika kabla ya Juni 30 mwaka huu.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji nchini George Bajuta aliishukuru Wizara ya Mifugo kwa uamuzi wake wa kuanzisha mafunzo hayo kwa mara ya kwanza ambayo hayajawahi kutolewa kwa wafugaji nchini na kwamba yatawasaidia kubadilisha maisha ya wafugaji ambao walikuwa wakidharaulika na kufukuzwa kila mahali walipokuwa wanakwenda kwa ajili ya shughuli za ufugaji.

  Pia alimwomba Waziri Mpina kuandaa mwongozo utakaosaidia kuondoa tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali kukamata hovyo mifugo kuitesa kwa muda kwa muda mrefu huku mingine ikipotea kwa kutaifishwa.

  Mafunzo ya sekta za Mifugo na Uvuvi yataendeshwa katika Wilaya zote 185 nchini na yatawafuata wafugaji na wavuvi kwenye maeneo yao na kwa kuanza kwa upande wa mifugo yatatolewa kwenye wilaya mbili za awali za Simanjiro na Kaliua mkoani Tabora, ambapo kwa upande wa Sekta ya Uvuvi mafunzo ya awali yatatolewa kwenye katika wilaya za Mafia, Bagamoyo,Mkuranga,Kigambni na Kinondoni.

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejeimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mary Mwanjelwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara wakifuatilia michango ya wabunge wakati wa kuchangia Bajeti ya Wizara TAMISEMI ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo Bungeni jijini Dodoma. Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akichangia hoja wakati wa mjadala wa kuchangia Bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo Bungeni jijini Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Mariam Kisiga akichangia hoja wakati wa mjadala wa kuchangia Bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo Bungeni jijini Dodoma Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akiteta jambo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza wakati wa kikao cha nane cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma. Baadhi ya wanafunzi kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) kutoka Tanga wakifuatilia shughuli za Bunge wakati wa kikao cha nane cha Mkutano wa 15 wa Bunge leo jijini Dodoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Arise Amka Afika ya jijini Arusha, Bi. Kuluthum Maabad alipomtembelea Bunge leo jijini Dodoma. Taasisi ya Arise Amka Afrika inajishughulisha na masuala ya utoaji elimu kuhusu harakati za ukombozi wa Bara la Afrika. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO)

  0 0

  Viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga (Ahmadiyya Muslim Jamaat Mkoa wa Shinyanga) wakiongozwa na vijana wa Jumuiya hiyo wamejitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto katika Zahanati ya Nhelegani iliyopo katika kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga. 

  Zoezi hilo la uchangiaji damu limefanyika leo Alhamis Aprili 11,2019 ambapo mbali na kuchangia damu vijana hao wamesafisha mazingira katika zahanati hiyo kwa kufyeka nyasi na kuzoa taka. 

  Rais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka alisema wameamua kuchangia damu ili kunusuru maisha ya mama na mtoto lakini pia kufanya usafi ili kuweka mazingira ya zanahati ya Nhelegani kuwa salama. 

  “Tumehamasishana kufanya shughuli hizi kwa mikono yetu,hali hii ya kujitolea inajulikana kwa jina la‘Waqar Amal’ ikiwa na maana ya kujitolea kusaidia kwa mikono yako mwenyewe,utoke jasho mwenyewe, hili ni zoezi endelevu tumekuwa tukijitolea katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga na maeneo mengine duniani”,alieleza Sheikh Mgeleka. 

  “Tunafanya popote na hatubagui kwa ajili ya manufaa ya viumbe vya Mwenyezi Mungu na hii ni sehemu ya mafundisho ya dini Tukufu ya Islam,malipo ya jasho letu ni mbele ya Mungu na haya ndiyo mafundisho muhimu ambayo daima tunatakiwa kukumbushana kwa ajili ya kusaidia viumbe wenzetu,pia tumefundishwa kuwa kujitolea ni heshima”,alisema Sheikh Mgeleka. 

  Naye Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko alisema zoezi la kuchangia damu ni huduma kwa viumbe ijulikanayo kwa jina la ‘Khidmatil Khalqi’ ikiwa ni utekelezaji wa kauli mbiu ya Ahmadiyya ya ‘Upendo kwa wote bila chuki kwa yeyote’. 

  “Zoezi hili limeshirikisha vijana wa Ahmadiyya mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Masheikh wa matawi mbalimbali wakionesha mfano kwa waumini tunaowaongoza, hili ni agizo la Kiongozi wetu Mtukufu Duniani Hazrat Mirza Masroor A.T.B.A Khalifatul Masihi wa tano kusaidia viumbe wenzetu”,alisema Sheikh Gesonko. 

  “Tunatoa huduma kwa yeyote aliyepata shida ili apate uhai,tumeleta huduma hii kwenye zahanati inayosimamiwa na serikali kwa sababu serikali ndiyo wanahusika na majanga na huduma mbalimbali za binadamu hasa afya,na tumekuwa tukichangia damu hata kwenye mikutano yetu mikuu mwezi Septemba kila mwaka”,alisema Sheikh Gesonko.
  Mtaalamu wa Maabara kutoka Kituo cha afya Kambarage,Devotha Omary (kushoto) akiandika jina la Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko (wa pili kushoto mwenye kanzu ya bluu) baada ya kumpima wingi wa damu wakati wa zoezi la utoaji damu katika Zahanati ya Nhelegani katika Manispa ya Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
  Rais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka(kulia) akipimwa presha wakati wa zoezi la uchangiaji damu.
  Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko akitoa damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya mama na mtoto na watu wengine wenye uhitaji wa damu.
  Mtaalamu wa Maabara kutoka Kituo cha afya Kambarage,Lucy Biseko akimhudumia Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko baada ya kumaliza kutoa damu.
  Mtaalamu wa Maabara kutoka Kituo cha afya Kambarage,Lucy Biseko akimwandaa Mwenyekiti wa Vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Abdulghani Msimba ili atoe damu.
  ais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka akitoa damu
  Mganga katika zahanati ya Nhelegani,Johanes Barnabas akiendelea na zoezi la kuwapima presha vijana wa Ahmadiyya waliojitolea kuchangia damu.
  Vijana wa Ahmadiyya wakijitolea kuchangia damu.
  Zoezi la kuchangia damu likiendelea.
  Sehemu ya damu iliyotolewa na vijana wa Ahmadiyya.
  Viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga na Wataalamu wa Maabara wakiangalia damu iliyotolewa na vijana wa Ahmadiyya.
  Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko akionesha damu iliyotolewa na vijana wa Ahmadiyya.
  Viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakitoka katika wodi ya wazazi katika zahanati ya Nhelegani kutoa zawadi ya sabuni za kufulia.
  Rais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka akitoa zawadi ya soda kwa wagonjwa katika zahanati ya Nhelegani.
  Rais/Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka,Mwenyekiti wa Vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Abdulghani Msimba na Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Gesonko wakitoa zawadi ya soda,maji na sabuni kwa wagonjwa katika zahanati ya Nhelegani.
  Vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakifyeka nyasi katika zahanati ya Nhelegani.
  Vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakiendelea kufanya usafi katika zahanati ya Nhelegani.
  Vijana wakiendelea na usafi.
  Baada ya kumaliza kufanya usafi viongozi na vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakiondoka eneo la zahanati ya Nhelegani.
  Picha ya kumbukumbu : Viongozi na vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza kufanya usafi katika zahanati ya Nhelegani.
  Picha ya pamoja baada ya kumaliza kufanya usafi katika zahanati ya Nhelegani. 
  Viongozi na vijana wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga wakisali na kufanya ibada ikiongozwa naMwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga,Sheikh Yusuph Mgeleka baada ya kumaliza kchangia damu na kufanya usafi katika zahanati ya Nhelegani. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameutaka uongozi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kuona namna bora ya kuhuwisha mitaala ya Chuo hicho ili kifikie viwango vya Elimu ya Juu.

  Mhe. Majaliwa ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo amesema mpaka sasa Chuo hicho kimekidhi viwango vya kuwa na hadhi ya Chuo Kikuu na kwamba elimu inayotolewa katika chuo hicho ndio inasisitizwa nchini.

  Ameutaka uongozi wa chuo hicho kutia mkazo katika mafunzo ya uongozi na maadili hususan yale yenye mwelekeo wa kujenga uzalendo na kuendelea kutumia fursa ya uwepo wa makongamano kukuza uelewa wa jamii ya watanzania kuhusu umuhimu wa kuenzi falsafa za mwalimu katika umoja, upendo, uzalendo, uadilifu na mshikamano wa kitaifa.

  Aidha Mhe. Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua kwa kujenga misingi ya Amani, umoja na kuleta maendeleo ya jamii nchini kwa vitendo na kuwataka watanzania kuzingatia maadili, uzalendo na utaifa katika uwajibikaji wa kila siku, kuungana kwa pamoja bila kujali itikadi za kisiasa au kabila katika kulinda na kudumisha tunu hizo.

  “Nimpongeze Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi anazochukua ili kuhakikisha anairejesha nchi yetu kwenye misingi yake ya awali ambayo ni kuwa na viongozi waadilifu, wazalendo na wenye kulinda Amani na kudumisha umoja katika jamii, watanzania wote tunapaswa kuunga mkono jitihada hizi na kuzilinda kwa nguvu zote,” alisema Mhe. Majaliwa.

  Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema ni vizuri kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa ni mtu ambaye amelipigania Taifa na kuliletea ukombozi na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufuata nyayo za Baba wa Taifa.

  Waziri Ndalichako ameeleza kufurahishwa na ushiriki wa wanafunzi katika kongamano hilo kwa kuwa linawapa fursa ya kupata uelewa mpana wa zaidi ya kile wanachofundishwa shuleni, na kwamba taifa linawategema kuwa chachu ya mabadiliko katika nchi.

  Awali Mwenyekiti wa Bodi ya uendeshaji wa Chuo cha Kumbu Kumbu ya Mwalimu Nyerere Steven Wassira alimweleza Waziri Mkuu kuwa wanaomba katika kumenzi Baba wa Taifa Chuo hicho kipandishwe hadhi na kuwa Chuo Kikuu na kwamba mazingira yake yaboreshwe yawe na hadhi ya Hayati Baba wa Taifa.

  Kwa upande wake mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Shadrack Mwakalila amesema, uongozi wa chuo hicho unaendelea na maboresho ya kutoa taaluma yenye kujenga uzalendo kwa vijana wa kitanzania.

  Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa limechagizwa na mada isemayo Mchango wa Mwalimu Nyerere katika kujenga Amani, umoja na Kuleta Maendeleo ya Jamii nchini.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wananchi waliohudhuria Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililofanyika katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni
  Mwenyekiti wa Bodi ya uendeshaji wa Chuo cha Kumbu Kumbu ya Mwalimu Nyerere Steven Wassiraakizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu.
  Mwenyekiti wa Kongamano hilo Jaji Joseph Warioba akizungumza wakati wa kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere.
  Waziri wa Elimu , Profesa Joyce Ndalichako akizungumza kukubali kuwa atafanyia kazi Ombi la chuo cha Mwalimu Nyerere kuwa Chuo Kikuu
  mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Shadrack Mwakalila, akizungumza juu ya maboresho yaliyofanyika chuoni hapo
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri mara alipowasili katika ukumbi wa Mkutano
  Sehemu ya Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali zinazojadiliwa

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


  SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marukufu kuuzwa kwa nyaya za kupitia mawasiliano (Data Cable) zilizokuwa zikiuzwa kwenye baadhi ya maduka ya vifaa vya kielektroki baada ya kubainika hazikidhi viwango.

  Hatua hiyo ilifikiwa na maofisa wa shirika hilo kwenye baadhi ya maduka jijini Dar es Salaam baada ya sampuli za nyaya hizo kupimwa kwenye maabara na kudhibitika hazikidhi viwango.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mkaguzi wa TBS, Saimon Emmanuel, amesema tayari wenye maduka yaliyokuwa yakiuza nyaya hizo wamepewa muda wa siku 14 kujieleza ni kwa nini wasichukuliwe hatua.

  Amesema baada ya kujiridhisha kuwa nyaya hizo hazikidhi viwango, hatua ya kwanza iliyochukuliwa ni kuzuia nyaya hizo kuendelea kuuzwa na ametoa mwito kwa Watanzania kutozinunua na kigezo kimoja wapo wanachoweza kutumia kuzitambua ni kuuzwa bei ndogo.

  Pia amesema baada ya kupimwa kwenye maabara za shirika pamoja na kasoro nyingine, nyaya hizo zilibainika kuwa na kiwango kidogo cha madini ya shaba (copper) na kwamba hata nguvu kinzani kwenye nyaya hizo zilifeli kwenye maabara .

  "Hivyo tumezizuia kwenye maduka tukisubiri hatua nyingine," amesema na kutoa mwito kwa wafanyabiashara wanapotaka kununua bidhaa kutoka nje ya nchi kuhakikisha zinakaguliwa ubora wake nje ya nchi kabla hazijaingia nchini mpangao ambao kitaalamu unaojulikana kama kama Pre-Shipment/Export Verification of Conformity to Standards (PVoC).

  Pia ameongeza kuws wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi bila kukabuliwa kupitia PVoC, pindi bidhaa zao zinapofika nchini wanatozwa faini ya asilimia 15 kulingana na thamani ya mzigo, kulipia gharama za upimaji kwenye maabara na kwamba zinapofeli kufikia viwango muagizaji anaamuriwa kuzirudisha alikozitoa kwa gharama zake au kuteketezwa hapa nchini pia kwa gharama zake.

  Emmanuel amesema hiyo ni kwa mujibu wa Sheria Na:2 ya Viwango ya mwaka 2009. Ametoa mwito kwa wafanyabiashara kuhakikisha wazingatia sheria na taratibu ili kuepuka hasara.

  Shirika hilo kwa sasa linaendesha awamu ya pili ya msako wa kushtukiza wa bidhaa zilizopo sokoni ili kubaini bidhaa ambazo hazina ubora na kuziondoa kwenye soko.

  0 0  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais wa Shirikisho la la Michezo la Jumuiya ya Madola Bi. Dame Louis Martin alipowasili katika ukumbi wa mkutano Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo,11-4-202019
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Rais wa Shirikisho la Michezo la Jumuiya ya Madola Bi. Dame Louis Martin, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo, 11-4-2019. akiwa na Ujumbe wake.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiuliza Rais wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola Bi. Dame Louis Martin, alipofiki Ikulu Zanzibar , kuonana na kufanya mazungumzo leo 11-4-2019.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Rais wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola Bi. Dame Louis Martin, kushoto akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo.11-4-2019
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola Bi. Dame Louis Martin, wakitowa ukumbi wa mkutano baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar 11-4-2019
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake baada ya kumaliza mazungumzo yao Bi. Dame Louis Martin yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)

  0 0


  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga (katikati mbele), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya(wa sita kushoto mbele) wakiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali na wanafunzi wa kidato cha Sita mwaka 2019 Mkoani Simiyu, wakati wa makabidhiano ya chakula (mchele na maharage), kilichotolewa na Ndg. Emmanuel Gungu Silanga na Wajumbe wenzake wa NEC na baadhi ya viongozi CCM mkoa kwa wanafunzi hao walio katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa .
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, alipotembelea shuleni hapo wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga na viongozi wengine walipokabidhi msaada chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kabla ya kukabidhi msaada wa chakula kwa ajili ya wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
  Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita walio katika Kambi ya Kitaaluma katika Shule ya Sekondari Maswa, wakifurahia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) na Mkoa wa Simiyu, waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa chakula na kuzungumza na wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka Mkoa wa Geita, Ndg. Idd Kassim Idd akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, alipotembelea shuleni hapo wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga alipokabidhi msaada wa kilo 100 za mchele na kilo 400 za maharage kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya akimpongeza mmoja wa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kutoa maneno ya shukrani kwa baadhi ya viongozi mbalimbali wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC na Mkoa wa Simiyu waliofika shuleni Aprili 11, 2019 hapo na kutoa msaada wa chakula.
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya(katikati) akizungumza jambo na baadhi ya viongozi na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, allipotembelea shuleni hapo Aprili 11, 2019.
  Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu, Mariam Manyangu akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, wakati alipotembelea shuleni hapo wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga alipokabidhi msaada wa kilo 1000 za mchele na kilo 400 za maharage kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.

  ………………………….

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mikoa ya Arusha na Geita wamewapongeza viongozi Mkoani Simiyu kwa ubunifu waliofanya kuanzisha kambi za kitaaluma kwa ajili ya kuongeza ufaulu na kutoa wito kwa viongozi wengine kuiga ubunifu huu ili waweze kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao.

  Hayo yamesemwa na Ndg. Anna Agatha Msuya Mjumbe wa NEC (Arusha) na Ndg. Idd Kassim Idd Mjumbe wa NEC(Geita) mara baada ya kutembelea wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, mara baada ya viongozi hao kuungana na Mjumbe wa NEC kutoka Mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga kukabidhi msaada wa chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.

  Akizungumza mara baada ya msaada wa chakula kukabidhiwa Ndg. Anna Agatha Msuya amesema laiti kambi hizi zingekuwa zinafanyika katika maeneo mengi matokeo ya Mitihani hususani ya Taifa yangekuwa mazuri zaidi ya sasa kwani zimeonekana kuusaidia mkoa wa Simiyu kupanda kielimu.

  “Nimevutiwa na ubunifu wa Simiyu kuwa na kambi za kitaaluma, tungekuwa na matokeo mazuri kama tungekuwa na viongozi wa Serikali wabunifu kama hapa Simiyu, naomba tulichokiona Simiyu kifanyike na mikoa mingine; mwaka juzi walikuwa wa 26 Kitaifa, mwaka jana wakawa wa 10 na naamini kwa kambi hii hatutaikosa Simiyu katika mikoa mitano bora” alisema Anna Agata Msuya.

  Naye Ndg. Idd Kassim Idd Mjumbe wa NEC(Geita) pamoja na kupongeza juhudi za mkoa wa Simiyu katika elimu, ameahidi kuwa amejifunza kupitia kambi hiyo ya kitaaluma na kulichukua wazo hilo kwa jili ya kushauri viongozi wa mkoa wa Geita kuona namna ya kulifanyia kazi ili kuwa na ufaulu mzuri.

  Aidha, Mwl. Ezekiel Mollel mwekezaji katika Sekta ya Elimu amesema suala la kambi za kitaaluma ni la kipekee kwa mkoa wa Simiyu, hivyo akatoa wito kwa mikoa mingine kuiga huku akiwaomba wadau mbalimbali wa elimu kuendelea kuchangia mahitaji mbalimbali ya wanafunzi walio katika kambi ili waweze kujifunza kwa amani wakiwa na mahitaji ya msingi.

  Kwa upande wake Mjumbe wa NEC kutoka Mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga amesema ametimiza ahadi yake ya kutoa kilo 1000 za mchele na kilo 400 za maharage kwa wanafunzi wa kidato cha Sita na kueleza matarajiao ya wana Simiyu kwa wanafunzi hao kuwa, ni kuwaona wanasoma kwa bidii na hatimaye waifanye Simiyu kuwa ya kwanza Kitaifa mwaka 2019.

  Wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzao wa kidato cha Sita mwaka 2019 walioko kambini Hidaya Simba(Maswa Girls) na Masanja Ng’hwenu (Meatu) wamewashukuru viongozi hao kwa msaada wa chakula walioutoa na kuahidi kuwa shukrani yao kubwa kwa walimu, viongozi, wazazi na wadau wa elimu wanaowasaidia ni kufanya vizuri na kuifanya Simiyu iwe nambari moja.

  Pamoja na kilo 1000 za mchele na kilo 400 za maharage zilizotolewa na Mjumbe wa NEC (Simiyu), Ndg. Emmanuel Gungu Silanga, Ndg. Idd Kassim Idd Mjumbe wa NEC(Geita) ametoa kilo 200 za mchele, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu ametoa kilo 100, Mdau wa Elimu Ezekiel Mollel kilo 50 na Ndg. Anna Agatha Msuya Mjumbe wa NEC (Arusha) ameahidi kutoa zawadi kwa wanafunzi watakaopata daraja la kwanza(divion one)

  0 0

  Wananchi wanaonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) wametakiwa kutunza na kuiendeleza miradi waliobuni na kutekelezwa na serikali ili iendelee kuwahudumia na kuwanufaisha mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha miradi hiyo.

  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Shaaban Seif Mohamed alieleza hayo wakati alipokuwa katika ziara maalum iliojumuisha Wilaya ya Magharibi “A”na Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa lengo la kukagua miradi hiyo ya TASAF awamu ya tatu na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi hao ili kuzipatia ufumbuzi.

  Katibu Mkuu Shaabani alisema, serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuwaanzishia wananchi wake miradi mbali mbali lakini hujitokeza changamoto ya kuilinda na kuendeleza miradi hiyo pale serikali inapoiwacha mikononi mwa wananchi pindi miradi inapofikia ukingoni.

  Akikagua kituo cha Afya kilichopo Kianga na Nyumba ya Madaktari iliopo Matamwe Kijini ambavyo vyote vimesaidiwa kupitia Mradi wa TASAF Katibu Mkuu amesema wananchi wanapaswa kuiendeleza miradi hiyo kwa niaba ya serikali na wasisite kuwachukulia hatua endapo watawaona watu wasiokuwa waaminifu wakiharibu miradi yao.

  “Baadhi ya watu hawathamini jitihada za serikali ambazo zinalenga kuwaletea maendeleo wananchi wake, hivyo hufanya hujuma za makusudi nawaombeni msisite kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi” Alieleza Katibu Shaaban.

  Katika ziara hiyo ametembelea mradi wa Kilimo katika bonde la kizimbani bonde ambalo Mpango wa kunusuru kaya maskini umeliendeleza kwa kuligawa kwa kujenga matuta maalum na kuweka miundombinu ya kupitishia maji kwa vile serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dk. Ali Mohamed Shein itaendeleza jitihada hizo.

  Akitolea ufafanuzi suala la baadhi ya watu kutoa upinzani kwa kuwabeza na kuwapuza katika shughuli zao za kilimo alisema serikali italipatia ufumbuzi suala hilo kwa kuendelea kuwaelimisha watu hao ili waachane na vitendo visivyofaa ili lengo la serikali la kuwaletea maendeleo wananchi wake liweze kufikiwa.

  Wakulima walionufaika na mradi wa kupunguza Kaya Maskini walimueleza Katibu Mkuu kupitia ziara yake hiyo kuwa, wameishukuru serikali ya mapinduzi kutokana na miradi walioanzishwa imewaletea matunda kwa kupata kipato kinachowasaidia katika kutatua matatizo yanayowakabili.

  Pamoja na mambo mengine wananchi hao kupitia katibu mkuu huyo wameiomba serikali kuwapatia vifaa vitakavyowasaidia kuendeleza shughuli zao za kilimo ili waweze kuzalisha za kupata kipato cha ziada.

  Akiwa katika kijiji cha Kijini Katibu mkuu Shaaban alipokea changamoto inayolalamikiwa na wananchi hao juu ya kukosekana kwa daktari wa kudumu katika spitali yao licha ya kuchukuwa jitihada ya kujenga nyumba maalum ya kulala daktari pamoja na kuweka miundombinu yote ikiwemo umeme, maji safi na salama.

  Wamesema kukosekana kwa daktari wa kulala kijijini hapo kumepelekea wananchi wanapatwa na maradhi nyakati za usiku kupata usumbufu na kupelekea kutafuta huduma masafa marefu.

  Nae Mkurugenzi Uratibu wa shughuli za serikali SMT, SMZ Khalid Bakar Amrani amewaeleza wananchi hao kuwa hivi sasa serikali ipo katika mchakato wa kuwapelekea awamu nyengine ya TASAF. hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupitia kwa masheha katika shehia zao na kutoa taarifa sahihi zitakazoisaidia serikali kupanga mipango yake.

  Ziara hiyo ya Katibu mkuu imejumuisha shehia za Kianga, Kizimbani, Donge mbiji, na matemwe kijini ambapo amepata fursa ya kutembelea miradi ya ujenzi wa Vituo vya Afya na Kilimo iliyobuniwa na wanakaya husika.

  Kassim Salum Abdi
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  Mashamba ya kilimo cha mpunga cha Kizimbani yanayoendelezwa na Wakulima kupitia Kaya Maskini chini ya Mradi wa Tasaf Awamu ya Tatu.
  Wanakaya Maskini wa Kijiji cha Donge Mbiji wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Shaaban Seif hayupo pichani alip[ofanya ziara ya kuangalia changamoto zinazowakabili.
  Sheha wa Shehia ya Donge Mbiji Abdulla Machano Haji akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Shaaban Seif alipofika kuangalia changamoto zinazowakabili.


  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mophamed akizungumza na Wananchi wa Matemwe Kijini kwenye Kituo cha Afya cha kijiji hicho alipokuwa katika zaiara ya kutembelea Miradi ya Tasaf iliyobuniwa kwa Kaya Maskini.Wa kwanza kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Uratibu wa shughuli za serikali SMT, SMZ Khalid Bakar Amrani.
  Muonekano wa Kituo cha Afya cha Shehia ya Kianga kilichojengwa kupitia Mradi wa Tasaf Awamu ya Tatu kikiwa katika hatua ya mwisho lakini tayari kimeanza kutoa huduma.
  Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0

   
  1. Usuli:

  Ijumaa ya leo, tarehe 12 April 2019, Taifa letu linatimiza miaka 35 toka kipenzi cha watanzania, marehemu EDWARD MORINGE SOKOINE, afariki kwa ajali ya gari tarehe 12 April 1984 eneo la Dakawa, wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.

  2. Kuzaliwa kwa SOKOINE:

  Jumatatu ya tarehe 1 Agosti 1938, katika kitongoji cha Kilasho, kijiji cha Emairete, Monduli Juu, Arusha, huku mvua kubwa ikirindima, alizaliwa mtoto wa kiume aliyekuja kuitwa EDWARD MORINGE SOKOINE. Baba yake aliitwa SOKOINE OLE SEVERE na mama yake aliitwa NAPELEL SINYATI NOOMAYAKI.

  3. Elimu:

  SOKOINE alisoma Shule ya Msingi Monduli kuanzia mwaka 1949 hadi 1953 na kisha akajiunga na "Monduli Middle School" toka mwaka 1953 hadi 1956. Baada ya hapo alijiunga na Shule ya Sekondari ya Umbwe alikosoma mwaka 1956 hadi 1958.

  4. SOKOINE Ajiunga na TANU:

  Tarehe 1 Januari 1961,SOKOINE alijiunga na chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ikiwa ni miezi michache kabla ya Tanganyika haijapata uhuru.

  5. SOKOINE Agombea Ubunge:

  Tarehe 25 Octoba 1965, SOKOINE, akiwa kijana mdogo tu wa miaka 27 lakini mwenye akili na ubunifu mkubwa, aligombea na kushinda ubunge jimbo la Monduli.

  6. Mh. SOKOINE Aukwaa Uwaziri Mdogo:

  Mwaka 1967, Mh.SOKOINE aliteuliwa na Rais NYERERE kuwa Naibu Waziri, Wizara ya Mawasiliano, Usafirishaji na Kazi.

  7. Mh. SOKOINE Aukwaa Uwaziri Kamili:

  Mwaka 1970, Rais NYERERE, baada ya kuvutiwa na uchapakazi wake, alimteua Mh. SOKOINE kuwa Waziri wa Nchi na mwaka 1972 akamteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

  8. Mh. SOKOINE Awa Mjumbe wa CC ya CCM:

  Baada ya CCM kuzaliwa kutokana na TANU na ASP kuungana tarehe 5 Februari 1977, Mh. SOKOINE akawa mjumbe  wa Kamati Kuu ya CCM.

  9. Mh. SOKOINE Ateuliwa kuwa Waziri Mkuu:

  Tarehe 13 Februari 1977, kutokana na utendaji kazi wake mujarab, Rais NYERERE alimteua Mh. SOKOINE kuwa Waziri Mkuu.

  Hata hivyo, tarehe 7 Novemba 1980, Mh. SOKOINE alijiuzuru na kwenda masomoni Yugoslavia na nafasi yake ikachukuliwa na Mh. CLEOPA DAVID MSUYA.

  Baada ya kurejea, Rais NYERERE alimteua tena Mh. SOKOINE kuwa Waziri Mkuu tarehe 24 Februari 1983. Aidha, mwaka huo wa 1983, Mh. SOKOINE alianza kusomea shahada ya "Political Science" Udsm na alikuwa amebakiza sura moja tu umauti ulimpomfika.

  10. Mh. SOKOINE "Aliota" kifo chake:

  Mh. SOKOINE alihudhuria kikao cha bunge jijini Idodomia mwezi April 1984. Hata hivyo, matendo ya Mh. SOKOINE kabla ya kifo chake yanaashiria huenda alihisi maisha yake duniani yalikuwa yakifikia tamati.

  Jumatatu ya tarehe 9 April 1984, Mh. SOKOINE alikwenda kusali kanisa la Mtakatifu PAUL, Idodomia. Usiku wa Jumanne, tarehe 10 April 1984, Mh. SOKIONE aliandaa karamu ya chakula cha jioni kwa Mawaziri na Wakuu wa Mikoa ambapo alionekana kuongea na kila Waziri na kila Mkuu wa Mkoa. Jumatano, tarehe 11 April 1984, aliandaa chakula cha jioni "The Last Supper" kwa Wabunge wote wa mkoani kwake Arusha ambapo aliwasihi wafanye jitihada kuwaondoa wananchi wao kwenye lindi kubwa la ufukara.

  11. Mh. SOKOINE Atema Cheche na Kuliaga Bunge:

  Mh. SOKOINE, siku ya Jumatano ya tarehe 11 April 1984, akilivunja Bunge, alitiririka:

  "Ndugu Spika, ningependa kumalizia kwa kukubaliana na wabunge wote waliosema na ambao hawakusema lakini wana mawazo haya kwamba jambo hili la kutumia fedha bila idhini ya bunge lazima tutafute kila njia ya kulikomesha..... Mungu akipenda tutakutana tena kwenye kikao kijacho cha  bunge. Mimi nasafiri kwa njia ya barabara ili nijionee hali ya mazao ya wakulima...".

  12. Mh. SOKOINE Apata Ajali, Afariki:

  Mapema Alhamis, tarehe 12 April 1984, Mh.  SOKOINE aliondoka na msafara wake Idodomia akiwa ndani ya Mercedes Benz ambapo msafara huo uliongozwa na gari la polisi. Magari yote yaliyokuwa yakikutana na msafara huo yalikuwa yakipaki pembeni kuupisha.

  Baada ya msafara huo kufika eneo la Dakawa, ghafla kilisikika kishindo kikubwa. Gari la Mh. SOKOINE liligongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Landcruiser lililokuwa likiendeshwa na DUMISAN DUBE (23), mpigania uhuru wa chama cha ANC aliyekuwa akiishi Mazimbo, Morogoro. DUBE, licha ya kusimamishwa na polisi, hakusimama kwavile alikuwa kwenye mwendo wa kasi. DUBE, katika Landcruiser hiyo, alikuwa na abiria wawili, Bw. BOYCE MOYE na PERCY GEORGE.

  Mh. SOKOINE, ambaye alikuwa amekaa kiti cha nyuma huku hajafunga mkanda, alirushwa na kugonga kioo cha mbele ambapo aliumia sana kifuani na shingoni na kufariki kabla ya kufikishwa hospitali ya serikali mkoani Morogoro ambako madaktari walithibitisha kifo chake.Bw. YUSTO CHUMA, aliyekuwa bodigadi wake aliyekuwa amekaa kiti cha mbele kushoto, aliumizwa vibaya na Bw. ALLY ABDALLAH,ambaye alikuwa ndiye dreva wake, alivunjika mguu.

  13. Rais NYERERE Alitangazia Taifa Kifo cha SOKOINE:

  Alasiri ya siku hiyo ya alhamis, Radio Tanzania, ikiwa inaendelea na vipindi vyake, ghafla vikasitishwa na wimbo wa Taifa ukapigwa.

  Rais NYERERE, baada tu ya wimbo wa Taifa, kwa uchungu mkubwa lakini kwa ujasiri wa hali ya juu, akalitangazia Taifa msiba huo wa kihistoria nchini kama ifuatavyo:

  "Ndugu wananchi, leo hii, ndugu yetu, kijana wetu, EDWARD MORINGE SOKOINE, Waziri Mkuu wa Tanzania, alipokuwa akirudi Dar Es Salaam toka Dodoma, gari lake lilipata ajali na amefariki dunia. Ndugu Watanzania, naomba muamini EDWARD amefariki kwa ajali na si kitu kingine".

  Mara tu baada ya tangazo hilo, vilio na simanzi vilivyotamalaki nchi nzima "havikuwa vya nchi hii". Aidha, watanzania waliokuwa nje ya nchi nao walibubujikwa na machozi kwa kuondokewa na kipenzi chao. Watanzania kila mahali walikuwa wenye simanzi kubwa. Watu walionekana "dhahir shahir" wamevurugwa!

  Kikao cha UWT kilichokuwa kikifanyika Ofisi ya CCM Lumumba kilisambaratika ghafla bila kuahirishwa mara tu Mwenyekiti wake, mama SOPHIA KAWAWA, alipowatangazia wajumbe habari hizo zilizoleta jakamoyo na jitimai kubwa!.

  Serikali ikatangaza wiki 2 za maombolezo huku bendera ya Taifa ikipeperushwa nusu mlingoti nchi nzima.

  14. Rais NYERERE Aangua Kilio Baada ya Kuuona Mwili wa SOKOINE:

  Mwili wa SOKOINE uliwasili Ikulu kutoka Morogoro saa 11 jioni ukiwa umefunikwa bendera ya Taifa. Rais NYERERE, akiongozana na mama MARIA, alijongea kwenye mwili huo na akafunua bendera ya Taifa. Mwalimu akaweka mikono yake miwili kwenye paji la uso wa SOKOINE na yeye na mama MARIA, aliyekuwa na kitambaa cheupe, wakalia kwa uchungu sana hadi kuondolewa na walinzi wao. Kwa wengi, ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona Mwalimu akilia hadharani. Kwa hakika, ilikuwa ni siku ya uchungu mkubwa kwa taifa letu kwa jinsi kifo kilivyotokea na hasa kwavile SOKOINE alikuwa akipigiwa chapuo na wengi kuja kuwa Rais wa Tanzania baada ya Mwalimu.

  15. JOSEPH NYERERE Azua Kimuhemuhe na Taharuki Ikulu:

  JOSEPH NYERERE, mdogo wa Mwalimu, ambaye alijulikana kwa ufyatu wake na kutomun'gunya maneno, ghafla bin vuu, aliingia eneo ulipowekwa mwili huo na kuonekana amefura hasira huku akilia kwa sauti ma kwa uchungu. Ghafla akatamka:
  "Mwalimu, huna ulinzi. Waziri Mkuu anakufa barabarani?" . Walinzi wa Ikulu, si tu walimtoa "mkuku" bali pia walihakikisha ameondolewa eneo la Ikulu haraka.!

  Mwili wa SOKOINE ukapelekwa hospitali ya Muhimbili kwaajili ya kuhifadhiwa.

  16. Jeneza la SOKOINE Latengenezwa Fastafasta Usiku wa Manani:

  Shuguli ya kutengeneza jeneza hilo alipewa Bw. GEORGE CHRISTOS (86). Huyu alizaliwa na baba Mgiriki na mama Msukuma aliyeitwa MARIA, aliyekuwa mmoja wa mabinti wa Chifu KIDAHA. Bw. CHRISTOS alikuwa ndiye Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu Tanzania.

  Saa 12 jioni siku hiyo, yeye na mkewe, Bi. ELIZABETH WALKER, walitinga Muhimbili ili kuangalia mwili na kuchukua vipimo.

  Wakati huo, bohari zote mikoani ilikuwa ni lazma ziwe na majeneza 5 ili ikitokea msiba wa kiongozi kusiwe na tatizo.

  SOKOINE alikuwa mtu wa miraba minne "aliyekwenda hewani" hivyo majeneza yote kwenye bohari zote hayakumfaa.

  Bw. CHRISTOS, mkewe na Bw. PAUL MKANGA, aliyekuwa Katibu Mkuu Ujenzi, baada ya kupata vipimo, walienda kwenye kiwanda cha HEM SINGH-Chang'ombe ambako walimkuta mwenyewe akiwa katika harakati za kufunga. Kazi ya kulitengeneza jeneza ikaanza mara moja na kumalizika usiku wa manani. Kisha, Bi. WALKER akalipamba jeneza hilo na likapelekwa Muhimbili.

  17. SOKOINE Aagwa na Wakazi wa Dsm:

  Ijumaa, tarehe 13 April 1984, wakazi wa jiji la Dsm na mikoa ya jirani walifurika kuuaga mwili wa SOKOINE. Kwa hakika, umati huo ulikuwa haujawahi kutokea nchini na rekodi hiyo ilikuja kuvunjwa na msiba wa Baba wa Taifa, Octoba 1999.

  18. Daladala Zote Zawapeleka Watu Bure "Airport"

  Jumamosi ya tarehe 14 April 1984, mwili wa SOKOINE ulipelekwa "airport" kwaajili ya kusafirishwa kuelekea Arusha. Daladala zote jijini ziliacha "kula vichwa" na badala yake zikawasafirisha wananchi bure kwenda "airport" kama mchango wao kwa kipenzi chao. Ikumbukwe kuwa mwaka 1983, baada ya kuona UDA "inambwelambwela", Mh. SOKOINE ndipo alipoanzisha utaratibu wa "DALADALA", jina lililotokana na neno "Dollar" ambapo "Exchange rate" wakati huo ilikuwa shilingi Tano ambayo ndiyo ilikuwa nauli ya Daladala.

  19. SOKOINE Azikwa kwa Heshma Zote:

  Kaburi la aina yake la marehemu SOKOINE lilijengwa kwa ustadi mkubwa na Jenerali JOHN BUTLER WARDEN "Black Mamba", Mtanzania Chotara, akisaidiwa na askari wa TPDF.

  Kutokana na ubunifu huo wa aina yake, Jenerali WARDEN akapewa heshima ya kujenga kaburi la aliyekuwa Rais wa Msumbiji, SAMORA MOSES MACHEL, ambaye alifariki baada ya ndege yake aina ya Tupulov Tu 134, kuanguka tarehe 19 Octoba 1986.

  Mazishi ya SOKOINE yalipewa  heshima zote za kitaifa na yalihudhuriwa na maelfu ya wananchi wakiongozwa na Baba wa Taifa na viongozi toka nje ya nchi.

  Miongoni mwa waliohudhuria toka nje ni Mh. OLIVER TAMBO, aliyekuwa Rais wa ANC na Mh. ALFRED NZO aliyekuwa Katibu Mkuu wa ANC ambao walieleza kusikitishwa kwao na ajali hiyo iliyosababishwa na raia mwenzao wa Afrika Kusini.

  20. SOKOINE Aacha Wake 2 na  Watoto 11:

  SOKOINE alikuwa na wake wawili ambao ni mama NAPONO SOKOINE na mama NAKITETO SOKOINE na watoto 11 wakiwemo Mh. Balozi JOSEPH na Mh. Mbunge NAMELOK.

  21. DUMISAN DUBE  Afikishwa kwa Pilato, "Apigwa Mvua 3"

  Tarehe 17 Mei 1984, DUMISAN DUBE, aliyesababisha kifo cha SOKOINE, alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro kwa mara ya kwanza. Kesi hiyo iliahirishwa hadi tarehe 29 Mei 1984.

  ANC Tawi la Mazimbo lilimchukua wakili nguli, MOHAMED ISMAIL, kumtetea DUBE. Hata hivyo, ANC HQ Lusaka ilipanga kumtafuta wakili mwingine guru ili kumtetea mpigania uhuru huyo.

  Tarehe 12 Juni 1984, upande wa Mashtaka ukiwa "Kamili-Gado" ukiongozwa na  JOHNSON MWANYIKA (SSA) aliyekuwa na mashahidi 21 akiwemo mkulima aliyeshuhudia ajali hiyo,  DUBE aliposomewa tu mashtaka 7 akakiri na Pilato wa wakati huo, Mh. SIMON KAJI (PRM) "akamtwanga mvua 3".

  22. SOKOINE Alikuwa Kipenzi Kikubwa cha NYERERE:

  Baba wa Taifa alimpenda sana SOKOINE kutokana na uadilifu wake, uchapakazi wake usio wa kawaida, uchamungu wake na ubunifu wake kuntu.

  23. Mambo Yaliyofanya SOKOINE Kuwa Kiongozi wa Kipekee na Kupendwa Sana na Watanzania:

  23.1 SOKOINE alichukia sana wazembe. "Ole wake Kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta. Viongozi wazembe na wabadhilifu wahesabu siku zao". 26 Machi 1983.

  23.2 SOKOINE alitaka wazazi wawajibike kwa watoto  wao- "Vijana wengi leo wana mali kuliko wazee wao waliofanyakazi kwa miaka 40 lakini wazee hao wanataka serikali ndio iwaulize vijana mali wameipata wapi! Hivi kwanini mzazi usimuulize mwanao -"Hii mali umepata wapi"?.

  23.3 SOKOINE alihimiza majeshi yawe kwa faida ya wote -  "Katika nchi inayojali haki na usawa, Majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya wengi. Kamwe hayaruhusiwi kuwa chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao"
  1 Februari 1977.

  23. 4 SOKOINE alipenda Uzalendo na alikuwa Mzalendo wa kweli kwa nchi yake. "Viongozi wanaoteuliwa lazma wawe Wazalendo. Naskia huko mikoani baadhi ya viongozi wanagombania magari na nyumba. Mambo hayo si muhimu. Viongozi wanatakiwa kugombania juu ya maendeleo ya wanavijiji. Huu ni ugomvi mtakatifu."
  11 Desemba 1982.

  23.5 SOKOINE alichukia upuuzi. Mwezi Machi 1983, SOKOINE alifanya ziara Singida. Mmoja wa viongozi mkoani humo akamfuata Bw. ACCADOGA CHILEDI aliyekuwa "Press Secretary" wa SOKOINE na kumwambia - "Mzee tumeishamtayarishia Blanketi Chapa ya Binadamu"(akimaanisha Kimada). Bw. CHILEDI akamuuliza Kiongozi huyo- "SOKOINE unamjua au unamsikia? Hilo Blanketi ondoka nalo na toweka hapa haraka, nikimwambia ujue unapoteza kazi yako sasa hivi".

  23.6 SOKOINE alikuwa mchapakazi hodari. Daima alifanya kazi hadi usiku na mara nyingine hadi usiku wa manani. Aliwachagua vijana 2 hodari; PHILEMON LUHANJO na MARTENS LUMBANGA waliokuwa chini ya Katibu Mkuu, HORACE KOLIMBA. Hawa watatu walibatizwa jina la "WAFUASI WA SOKOINE" kwani walizunguka nae kote alikoenda na kufuatilia maagizo yote "Bampa tu Bampa".

  23. 7 SOKOINE hakupenda utajiri. Maisha yake yalielezewa kwa ufasaha na Mwalimu msibani : "EDWARD hakuwa na mali yoyote ukiachilia mbali ng'ombe wake wa urithi. Alikuwa na suti tatu na viatu pea mbili".

  23.8 SOKOINE alikuwa ni mbunifu sana. Alianzisha "PRESIDENTIAL TRUST FUND" Ikulu ambapo alikuwa akiweka sehemu ya mshahara wake ili kuwasaidia akina mama kuweza kukopa!.

  23. 9 SOKOINE alikuwa Mchamungu sana. Alikuwa Mkristu mkatoliki na mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisca.

  24. NUKUU MUJARAB ZA MH. JPM NA PM KUHUSU SOKOINE:

  24.1 "Tarehe 12 April 1984, aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. SOKOINE alipofariki ilikuwa siku ya huzuni kubwa. Mimi nilikuwa JKT Mpwapwa "Operesheni ya Nguvukazi". SOKOINE hatasahaulika Tanzania kwani alipiga vita rushwa, wizi na unyonyaji. Alikuwa Mzakendo wa kweli. Ni wito wangu Watanzania tumuige na tumuishi.."
  Mh. JPM, 12 April 2018.

  24. 2 "SOKOINE alikuwa Kiongozi bora aliyechukia rushwa na ulanguzi. Hakuwa na ubinafsi, kinyongo wala tamaa ya mali. Namuomba Mungu niwe kama SOKOINE"
  Mh. K.MAJALIWA, 12 April 2018.

  25. Tafakuri Jadidi:

  Je, wewe kama Kiongozi (wa ngazi yoyote ile iwe Kata, darasani au serikalini) unamuenzi na kumuishi marehemu SOKOINE kama alivyotuasa Mh. Rais MAGUFULI?
  Jitafakari.

  NB: NYIE WOTE MNAOFOWADI ATIKALI ZANGU BAADA YA KUONDOA CHATA LA "ALLEZ LIVERPOOL FC👇 DAWA YENU IPO JIKONI!!.


  ALLEZ ALLEZ ALLEZ LIVERPOOL FC!!!🔥🔥🔥KUMBUKIZI YA 35 YA KIFO CHA EDWARD MORINGE SOKOINE


  1. Usuli:

  Ijumaa ya leo, tarehe 12 April 2019, Taifa letu linatimiza miaka 35 toka kipenzi cha watanzania, marehemu EDWARD MORINGE SOKOINE, afariki kwa ajali ya gari tarehe 12 April 1984 eneo la Dakawa, wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.

  2. Kuzaliwa kwa SOKOINE:

  Jumatatu ya tarehe 1 Agosti 1938, katika kitongoji cha Kilasho, kijiji cha Emairete, Monduli Juu, Arusha, huku mvua kubwa ikirindima, alizaliwa mtoto wa kiume aliyekuja kuitwa EDWARD MORINGE SOKOINE. Baba yake aliitwa SOKOINE OLE SEVERE na mama yake aliitwa NAPELEL SINYATI NOOMAYAKI.

  3. Elimu:

  SOKOINE alisoma Shule ya Msingi Monduli kuanzia mwaka 1949 hadi 1953 na kisha akajiunga na "Monduli Middle School" toka mwaka 1953 hadi 1956. Baada ya hapo alijiunga na Shule ya Sekondari ya Umbwe alikosoma mwaka 1956 hadi 1958.

  4. SOKOINE Ajiunga na TANU:

  Tarehe 1 Januari 1961,SOKOINE alijiunga na chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ikiwa ni miezi michache kabla ya Tanganyika haijapata uhuru.

  5. SOKOINE Agombea Ubunge:

  Tarehe 25 Octoba 1965, SOKOINE, akiwa kijana mdogo tu wa miaka 27 lakini mwenye akili na ubunifu mkubwa, aligombea na kushinda ubunge jimbo la Monduli.

  6. Mh. SOKOINE Aukwaa Uwaziri Mdogo:

  Mwaka 1967, Mh.SOKOINE aliteuliwa na Rais NYERERE kuwa Naibu Waziri, Wizara ya Mawasiliano, Usafirishaji na Kazi.

  7. Mh. SOKOINE Aukwaa Uwaziri Kamili:

  Mwaka 1970, Rais NYERERE, baada ya kuvutiwa na uchapakazi wake, alimteua Mh. SOKOINE kuwa Waziri wa Nchi na mwaka 1972 akamteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

  8. Mh. SOKOINE Awa Mjumbe wa CC ya CCM:

  Baada ya CCM kuzaliwa kutokana na TANU na ASP kuungana tarehe 5 Februari 1977, Mh. SOKOINE akawa mjumbe  wa Kamati Kuu ya CCM.

  9. Mh. SOKOINE Ateuliwa kuwa Waziri Mkuu:

  Tarehe 13 Februari 1977, kutokana na utendaji kazi wake mujarab, Rais NYERERE alimteua Mh. SOKOINE kuwa Waziri Mkuu.

  Hata hivyo, tarehe 7 Novemba 1980, Mh. SOKOINE alijiuzuru na kwenda masomoni Yugoslavia na nafasi yake ikachukuliwa na Mh. CLEOPA DAVID MSUYA.

  Baada ya kurejea, Rais NYERERE alimteua tena Mh. SOKOINE kuwa Waziri Mkuu tarehe 24 Februari 1983. Aidha, mwaka huo wa 1983, Mh. SOKOINE alianza kusomea shahada ya "Political Science" Udsm na alikuwa amebakiza sura moja tu umauti ulimpomfika.

  10. Mh. SOKOINE "Aliota" kifo chake:

  Mh. SOKOINE alihudhuria kikao cha bunge jijini Idodomia mwezi April 1984. Hata hivyo, matendo ya Mh. SOKOINE kabla ya kifo chake yanaashiria huenda alihisi maisha yake duniani yalikuwa yakifikia tamati.

  Jumatatu ya tarehe 9 April 1984, Mh. SOKOINE alikwenda kusali kanisa la Mtakatifu PAUL, Idodomia. Usiku wa Jumanne, tarehe 10 April 1984, Mh. SOKIONE aliandaa karamu ya chakula cha jioni kwa Mawaziri na Wakuu wa Mikoa ambapo alionekana kuongea na kila Waziri na kila Mkuu wa Mkoa. Jumatano, tarehe 11 April 1984, aliandaa chakula cha jioni "The Last Supper" kwa Wabunge wote wa mkoani kwake Arusha ambapo aliwasihi wafanye jitihada kuwaondoa wananchi wao kwenye lindi kubwa la ufukara.

  11. Mh. SOKOINE Atema Cheche na Kuliaga Bunge:

  Mh. SOKOINE, siku ya Jumatano ya tarehe 11 April 1984, akilivunja Bunge, alitiririka:

  "Ndugu Spika, ningependa kumalizia kwa kukubaliana na wabunge wote waliosema na ambao hawakusema lakini wana mawazo haya kwamba jambo hili la kutumia fedha bila idhini ya bunge lazima tutafute kila njia ya kulikomesha..... Mungu akipenda tutakutana tena kwenye kikao kijacho cha  bunge. Mimi nasafiri kwa njia ya barabara ili nijionee hali ya mazao ya wakulima...".

  12. Mh. SOKOINE Apata Ajali, Afariki:

  Mapema Alhamis, tarehe 12 April 1984, Mh.  SOKOINE aliondoka na msafara wake Idodomia akiwa ndani ya Mercedes Benz ambapo msafara huo uliongozwa na gari la polisi. Magari yote yaliyokuwa yakikutana na msafara huo yalikuwa yakipaki pembeni kuupisha.

  Baada ya msafara huo kufika eneo la Dakawa, ghafla kilisikika kishindo kikubwa. Gari la Mh. SOKOINE liligongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Landcruiser lililokuwa likiendeshwa na DUMISAN DUBE (23), mpigania uhuru wa chama cha ANC aliyekuwa akiishi Mazimbo, Morogoro. DUBE, licha ya kusimamishwa na polisi, hakusimama kwavile alikuwa kwenye mwendo wa kasi. DUBE, katika Landcruiser hiyo, alikuwa na abiria wawili, Bw. BOYCE MOYE na PERCY GEORGE.

  Mh. SOKOINE, ambaye alikuwa amekaa kiti cha nyuma huku hajafunga mkanda, alirushwa na kugonga kioo cha mbele ambapo aliumia sana kifuani na shingoni na kufariki kabla ya kufikishwa hospitali ya serikali mkoani Morogoro ambako madaktari walithibitisha kifo chake.Bw. YUSTO CHUMA, aliyekuwa bodigadi wake aliyekuwa amekaa kiti cha mbele kushoto, aliumizwa vibaya na Bw. ALLY ABDALLAH,ambaye alikuwa ndiye dreva wake, alivunjika mguu.

  13. Rais NYERERE Alitangazia Taifa Kifo cha SOKOINE:

  Alasiri ya siku hiyo ya alhamis, Radio Tanzania, ikiwa inaendelea na vipindi vyake, ghafla vikasitishwa na wimbo wa Taifa ukapigwa.

  Rais NYERERE, baada tu ya wimbo wa Taifa, kwa uchungu mkubwa lakini kwa ujasiri wa hali ya juu, akalitangazia Taifa msiba huo wa kihistoria nchini kama ifuatavyo:

  "Ndugu wananchi, leo hii, ndugu yetu, kijana wetu, EDWARD MORINGE SOKOINE, Waziri Mkuu wa Tanzania, alipokuwa akirudi Dar Es Salaam toka Dodoma, gari lake lilipata ajali na amefariki dunia. Ndugu Watanzania, naomba muamini EDWARD amefariki kwa ajali na si kitu kingine".

  Mara tu baada ya tangazo hilo, vilio na simanzi vilivyotamalaki nchi nzima "havikuwa vya nchi hii". Aidha, watanzania waliokuwa nje ya nchi nao walibubujikwa na machozi kwa kuondokewa na kipenzi chao. Watanzania kila mahali walikuwa wenye simanzi kubwa. Watu walionekana "dhahir shahir" wamevurugwa!

  Kikao cha UWT kilichokuwa kikifanyika Ofisi ya CCM Lumumba kilisambaratika ghafla bila kuahirishwa mara tu Mwenyekiti wake, mama SOPHIA KAWAWA, alipowatangazia wajumbe habari hizo zilizoleta jakamoyo na jitimai kubwa!.

  Serikali ikatangaza wiki 2 za maombolezo huku bendera ya Taifa ikipeperushwa nusu mlingoti nchi nzima.

  14. Rais NYERERE Aangua Kilio Baada ya Kuuona Mwili wa SOKOINE:

  Mwili wa SOKOINE uliwasili Ikulu kutoka Morogoro saa 11 jioni ukiwa umefunikwa bendera ya Taifa. Rais NYERERE, akiongozana na mama MARIA, alijongea kwenye mwili huo na akafunua bendera ya Taifa. Mwalimu akaweka mikono yake miwili kwenye paji la uso wa SOKOINE na yeye na mama MARIA, aliyekuwa na kitambaa cheupe, wakalia kwa uchungu sana hadi kuondolewa na walinzi wao. Kwa wengi, ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona Mwalimu akilia hadharani. Kwa hakika, ilikuwa ni siku ya uchungu mkubwa kwa taifa letu kwa jinsi kifo kilivyotokea na hasa kwavile SOKOINE alikuwa akipigiwa chapuo na wengi kuja kuwa Rais wa Tanzania baada ya Mwalimu.

  15. JOSEPH NYERERE Azua Kimuhemuhe na Taharuki Ikulu:

  JOSEPH NYERERE, mdogo wa Mwalimu, ambaye alijulikana kwa ufyatu wake na kutomun'gunya maneno, ghafla bin vuu, aliingia eneo ulipowekwa mwili huo na kuonekana amefura hasira huku akilia kwa sauti ma kwa uchungu. Ghafla akatamka:
  "Mwalimu, huna ulinzi. Waziri Mkuu anakufa barabarani?" . Walinzi wa Ikulu, si tu walimtoa "mkuku" bali pia walihakikisha ameondolewa eneo la Ikulu haraka.!

  Mwili wa SOKOINE ukapelekwa hospitali ya Muhimbili kwaajili ya kuhifadhiwa.

  16. Jeneza la SOKOINE Latengenezwa Fastafasta Usiku wa Manani:

  Shuguli ya kutengeneza jeneza hilo alipewa Bw. GEORGE CHRISTOS (86). Huyu alizaliwa na baba Mgiriki na mama Msukuma aliyeitwa MARIA, aliyekuwa mmoja wa mabinti wa Chifu KIDAHA. Bw. CHRISTOS alikuwa ndiye Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu Tanzania.

  Saa 12 jioni siku hiyo, yeye na mkewe, Bi. ELIZABETH WALKER, walitinga Muhimbili ili kuangalia mwili na kuchukua vipimo.

  Wakati huo, bohari zote mikoani ilikuwa ni lazma ziwe na majeneza 5 ili ikitokea msiba wa kiongozi kusiwe na tatizo.

  SOKOINE alikuwa mtu wa miraba minne "aliyekwenda hewani" hivyo majeneza yote kwenye bohari zote hayakumfaa.

  Bw. CHRISTOS, mkewe na Bw. PAUL MKANGA, aliyekuwa Katibu Mkuu Ujenzi, baada ya kupata vipimo, walienda kwenye kiwanda cha HEM SINGH-Chang'ombe ambako walimkuta mwenyewe akiwa katika harakati za kufunga. Kazi ya kulitengeneza jeneza ikaanza mara moja na kumalizika usiku wa manani. Kisha, Bi. WALKER akalipamba jeneza hilo na likapelekwa Muhimbili.

  17. SOKOINE Aagwa na Wakazi wa Dsm:

  Ijumaa, tarehe 13 April 1984, wakazi wa jiji la Dsm na mikoa ya jirani walifurika kuuaga mwili wa SOKOINE. Kwa hakika, umati huo ulikuwa haujawahi kutokea nchini na rekodi hiyo ilikuja kuvunjwa na msiba wa Baba wa Taifa, Octoba 1999.

  18. Daladala Zote Zawapeleka Watu Bure "Airport"

  Jumamosi ya tarehe 14 April 1984, mwili wa SOKOINE ulipelekwa "airport" kwaajili ya kusafirishwa kuelekea Arusha. Daladala zote jijini ziliacha "kula vichwa" na badala yake zikawasafirisha wananchi bure kwenda "airport" kama mchango wao kwa kipenzi chao. Ikumbukwe kuwa mwaka 1983, baada ya kuona UDA "inambwelambwela", Mh. SOKOINE ndipo alipoanzisha utaratibu wa "DALADALA", jina lililotokana na neno "Dollar" ambapo "Exchange rate" wakati huo ilikuwa shilingi Tano ambayo ndiyo ilikuwa nauli ya Daladala.

  19. SOKOINE Azikwa kwa Heshma Zote:

  Kaburi la aina yake la marehemu SOKOINE lilijengwa kwa ustadi mkubwa na Jenerali JOHN BUTLER WARDEN "Black Mamba", Mtanzania Chotara, akisaidiwa na askari wa TPDF.

  Kutokana na ubunifu huo wa aina yake, Jenerali WARDEN akapewa heshima ya kujenga kaburi la aliyekuwa Rais wa Msumbiji, SAMORA MOSES MACHEL, ambaye alifariki baada ya ndege yake aina ya Tupulov Tu 134, kuanguka tarehe 19 Octoba 1986.

  Mazishi ya SOKOINE yalipewa  heshima zote za kitaifa na yalihudhuriwa na maelfu ya wananchi wakiongozwa na Baba wa Taifa na viongozi toka nje ya nchi.

  Miongoni mwa waliohudhuria toka nje ni Mh. OLIVER TAMBO, aliyekuwa Rais wa ANC na Mh. ALFRED NZO aliyekuwa Katibu Mkuu wa ANC ambao walieleza kusikitishwa kwao na ajali hiyo iliyosababishwa na raia mwenzao wa Afrika Kusini.

  20. SOKOINE Aacha Wake 2 na  Watoto 11:

  SOKOINE alikuwa na wake wawili ambao ni mama NAPONO SOKOINE na mama NAKITETO SOKOINE na watoto 11 wakiwemo Mh. Balozi JOSEPH na Mh. Mbunge NAMELOK.

  21. DUMISAN DUBE  Afikishwa kwa Pilato, "Apigwa Mvua 3"

  Tarehe 17 Mei 1984, DUMISAN DUBE, aliyesababisha kifo cha SOKOINE, alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro kwa mara ya kwanza. Kesi hiyo iliahirishwa hadi tarehe 29 Mei 1984.

  ANC Tawi la Mazimbo lilimchukua wakili nguli, MOHAMED ISMAIL, kumtetea DUBE. Hata hivyo, ANC HQ Lusaka ilipanga kumtafuta wakili mwingine guru ili kumtetea mpigania uhuru huyo.

  Tarehe 12 Juni 1984, upande wa Mashtaka ukiwa "Kamili-Gado" ukiongozwa na  JOHNSON MWANYIKA (SSA) aliyekuwa na mashahidi 21 akiwemo mkulima aliyeshuhudia ajali hiyo,  DUBE aliposomewa tu mashtaka 7 akakiri na Pilato wa wakati huo, Mh. SIMON KAJI (PRM) "akamtwanga mvua 3".

  22. SOKOINE Alikuwa Kipenzi Kikubwa cha NYERERE:

  Baba wa Taifa alimpenda sana SOKOINE kutokana na uadilifu wake, uchapakazi wake usio wa kawaida, uchamungu wake na ubunifu wake kuntu.

  23. Mambo Yaliyofanya SOKOINE Kuwa Kiongozi wa Kipekee na Kupendwa Sana na Watanzania:

  23.1 SOKOINE alichukia sana wazembe. "Ole wake Kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta. Viongozi wazembe na wabadhilifu wahesabu siku zao". 26 Machi 1983.

  23.2 SOKOINE alitaka wazazi wawajibike kwa watoto  wao- "Vijana wengi leo wana mali kuliko wazee wao waliofanyakazi kwa miaka 40 lakini wazee hao wanataka serikali ndio iwaulize vijana mali wameipata wapi! Hivi kwanini mzazi usimuulize mwanao -"Hii mali umepata wapi"?.

  23.3 SOKOINE alihimiza majeshi yawe kwa faida ya wote -  "Katika nchi inayojali haki na usawa, Majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya wengi. Kamwe hayaruhusiwi kuwa chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao"
  1 Februari 1977.

  23. 4 SOKOINE alipenda Uzalendo na alikuwa Mzalendo wa kweli kwa nchi yake. "Viongozi wanaoteuliwa lazma wawe Wazalendo. Naskia huko mikoani baadhi ya viongozi wanagombania magari na nyumba. Mambo hayo si muhimu. Viongozi wanatakiwa kugombania juu ya maendeleo ya wanavijiji. Huu ni ugomvi mtakatifu."
  11 Desemba 1982.

  23.5 SOKOINE alichukia upuuzi. Mwezi Machi 1983, SOKOINE alifanya ziara Singida. Mmoja wa viongozi mkoani humo akamfuata Bw. ACCADOGA CHILEDI aliyekuwa "Press Secretary" wa SOKOINE na kumwambia - "Mzee tumeishamtayarishia Blanketi Chapa ya Binadamu"(akimaanisha Kimada). Bw. CHILEDI akamuuliza Kiongozi huyo- "SOKOINE unamjua au unamsikia? Hilo Blanketi ondoka nalo na toweka hapa haraka, nikimwambia ujue unapoteza kazi yako sasa hivi".

  23.6 SOKOINE alikuwa mchapakazi hodari. Daima alifanya kazi hadi usiku na mara nyingine hadi usiku wa manani. Aliwachagua vijana 2 hodari; PHILEMON LUHANJO na MARTENS LUMBANGA waliokuwa chini ya Katibu Mkuu, HORACE KOLIMBA. Hawa watatu walibatizwa jina la "WAFUASI WA SOKOINE" kwani walizunguka nae kote alikoenda na kufuatilia maagizo yote "Bampa tu Bampa".

  23. 7 SOKOINE hakupenda utajiri. Maisha yake yalielezewa kwa ufasaha na Mwalimu msibani : "EDWARD hakuwa na mali yoyote ukiachilia mbali ng'ombe wake wa urithi. Alikuwa na suti tatu na viatu pea mbili".

  23.8 SOKOINE alikuwa ni mbunifu sana. Alianzisha "PRESIDENTIAL TRUST FUND" Ikulu ambapo alikuwa akiweka sehemu ya mshahara wake ili kuwasaidia akina mama kuweza kukopa!.

  23. 9 SOKOINE alikuwa Mchamungu sana. Alikuwa Mkristu mkatoliki na mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisca.

  24. NUKUU MUJARAB ZA MH. JPM NA PM KUHUSU SOKOINE:

  24.1 "Tarehe 12 April 1984, aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. SOKOINE alipofariki ilikuwa siku ya huzuni kubwa. Mimi nilikuwa JKT Mpwapwa "Operesheni ya Nguvukazi". SOKOINE hatasahaulika Tanzania kwani alipiga vita rushwa, wizi na unyonyaji. Alikuwa Mzakendo wa kweli. Ni wito wangu Watanzania tumuige na tumuishi.."
  Mh. JPM, 12 April 2018.

  24. 2 "SOKOINE alikuwa Kiongozi bora aliyechukia rushwa na ulanguzi. Hakuwa na ubinafsi, kinyongo wala tamaa ya mali. Namuomba Mungu niwe kama SOKOINE"
  Mh. K.MAJALIWA, 12 April 2018.

  25. Tafakuri Jadidi:

  Je, wewe kama Kiongozi (wa ngazi yoyote ile iwe Kata, darasani au serikalini) unamuenzi na kumuishi marehemu SOKOINE kama alivyotuasa Mh. Rais MAGUFULI?
  Jitafakari.


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju akiwa na Mkurugenz wa Mashtaka (DPP) Bw. Biswalo mganga na wanasheria wengine nje ya Gereza Kuu Lilungu la Mtwara baada ya kulitembelea na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya gereza hilo mjini Mtwara. 


  Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe. Ngwembe akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju (mwenye miwani), Mkurugenzi wa Mashtaka DPP Bw. Biswalo Mganga (wa kwanza kushoto), Naibu DPP Dkt. Edson Makallo (wa kwanza kulia) walipomtembelea Ofisini kwake mjini Mtwara wakati timu ya wanasheria wakiongozwa na Bw. Mpanju walipokuwa mjini Mtwara kutembelea gereza kuu la Lilungu.

  Naibu DPP Dkt. Edson Makallo (wa kwanza kushoto) akizungumza kitu na Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Newala wakati timu ya wanasheria ilipokuwa wilayani humo kutembelea gereza la wilaya hiyo na kuzungumza na wafungwa na mahabusu na kutatua kero za kisheria wanazokabiliana nazo.
  Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Newala (katikati) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju (kushoto) na Naibu DPP Dkt. Edson Makallo (kulia) walipomtembelea Ofisini kwake mjini Newala wakati timu ya wanasheria wakiongozwa na Bw. Mpanju walipotembelea gereza la wilaya hiyo.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju na timu ya wanasheria wakiwa nje ya Gereza la Wilaya ya Newala baada ya kulitembelea na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya gereza hilo mjini Newala.
  Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Newala Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Juma Mgunda aliyeshika karatasi akijiandaa kusoma taarifa ya gereza kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju wa kwanza kulia alipofika katika gereza la Wilaya ya Masasi kulitembelea na kuzungumza na wafungwa na Mahabusu
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju na timu ya wanasheria wakiwa nje ya Gereza la Wilaya ya Masasi baada ya kulitembelea na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya gereza hilo mjini Masasi.

  ………………..

  Timu ya Wanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Mahakama, Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza mkoa wa Mtwara wamefanya ukaguzi katika Magereza mkoani Mtwara kusikiliza na kujionea changamoto za kisheria zinazowakabili wafungwa na mahabusu walioko ndani ya magereza mkoani humo.

  Timu hiyo inayoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Amon Mpanju na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt. Edson Makallo imetembelea gereza Kuu la Lilungu lililoko Mtwara mjini, gereza la wilaya ya Newala na gereza la wilaya ya Masasi.

  Timu hiyo imefanya ukaguzi wa maeneo yanayotumiwa na wafungwa na mahabusu ndani ya magereza hayo na kuzungumza nao ili kujua changamoto za kisheria na kijamii zinazowakabili na kuchukua hatua stahiki.

  Katika ziara hiyo Timu ya wataalamu hao imechukua majina ya mahabusu ambao kesi zao ni ndogo ndogo na waliokiri kufanya makosa husika na kujutia, wenye watu wa kuwawekea dhamana, walio tayari kulipa fedha za vitu walivyoiba, au kurudisha vitu walivyoiba, kupigana, kutukanana na wako tauari kuombana msamaha, kujeruhiana na walioafikiana kumaliza kesi zao nje ya mahakama ili ziweze kufutwa na hivyo kuachiwa huru baada ya DPP kujiridhisha nayo.

  Timu pia kwa kushirikiana na Mahakimu wa Mkoa na Wilaya husika wamekubaliana kufanya mapitio ya adhabu za wafungwa wa chini ya miaka mitatu ili wabadilishiwe adhabu kwa kufanya kazi za jamii au vifungo vya nje ambapo wakimaliza watakuwa raia huru.

  Akizungumza ndani ya magereza hayo Naibu Katibu Mkuu Bw. Mpanju amesema ukaguzi huo ndani ya magereza hayo ni jukumu la kisheria la Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi zinazohusika na utoaji haki nchini.

  “Sisi kama Wizara na taasisi zote zilizo katika mfumo wa utoaji haki nchini ni jukumu letu kisheria kuangalia jinsi mambo yanavyoendeshwa humu ndani na wadau wetu, kutembelea huku kunatuwezesha kuona kama mwanachi anapata haki yake kwa mujibu wa Sheria, na ikiwa kuna tatizo ni wajibu wetu kumuondolea kero za kisheria akiwa humu ndani,ndio maana tunafanya ukaguzi huu na kuzungumza nanyi ili tuwasikie na kuondoa kero au malalamiko mtakayotuambia,” alisema Bw.Mpanju.

  Akizungumza baada ya kubaini mahabusu na wafungwa watakaonufaika na ziara ya wataalamu hao Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Dkt.Edson Makallo amewataka wananchi hao ambao watafutiwa Mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili na wafungwa watakaopata adhabu mbadala kuwa raia wema na kubadili mienendo yao ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa Taifa.

  0 0

   1

  2
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mafinga mara baada ya kuwasili wakati akitokea Makambako mkoani Njombe. 
  4
  6
   . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kijana Baraka Mwakipesile (Anko Magu) wa Mafinga ambaye anaigiza sauti ya Rais Dkt. Magufuli mara baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza.
  3
  7
  8
  9
   Umati wa Wananchi wa Mafinga  wakimsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akizungumza nao.
  11
  Baraka Mwakipesile (Anko Magu) Kijana anayeigiza sauti ya Rais Dkt. Magufuli akipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia. Picha na IKULU

  0 0

   Jumla ya klabu 10 zimethibitisha kushindana katika mashindano ya klabu bingwa ya mchezo wa kuogelea yaliyopangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia kesho Jumamosi.
  Klabu ambazo zitashiriki katika mashindano hayo ni i Bluefins, Champion Rise, Mis Piranhas, klabu ya kuogelea ya Mwanza (MSC), FK Blue na Wahoo ya Zanzibar.Nyingine kuwa ni ISM-Moshi, ISM-Arusha,FK Blue Marlins, Talis-IST na mabingwa watetezi, Dar es Salaam Swim Club (DSC).
  Mashindano hayo ambayo yatamalizika kesho Jumapili, yamedhaminiwa na IST, Azam, Pepsi, Asas, Samsung, DTB Bank, Kaka’s, Food Lovers na Snow Cream.
  Wadhamini wengine ni Kastipharn Ltd, Ruru Logistics, Knight Support, Oppotune Travel ltd, Pyramid Consumers, Print Galore, ITV Media, Clouds FM, Subway, NMB Bank and Umoja Grand Belt na  Road Restaurant.
  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Hadija Shebe alisema kuwa waogeleaji wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi wamewasili kwa ajili ya kushiriki katika mashindano hayo.
  Waogeleaji  hao ni Sonia Tumiotto, Maia Tumiotto , Collins Saliboko, Dennis Mhini, Chichi Zengeni, Natalia Sanford, Smriti Gorkarn  na Delvin Barick ambao wote wanasoma shule ya from St Felix , Uingereza.Wengine ni  Christian Shirima anayetokea nchi ya Ukraine,  Isam Sepetu (Afrika Kusini), Hilal Hemed Hilal na Kangeta wanaotokea klabu ya Hamilton Aquatic ya Dubai.
  Alisema kuwa mashindano hayo yamepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi siku ya Jumamosi na waogeleaji watashindana katika staili tano ambazo ni Freestyle, Breaststroke, Butterfly, Backstroke na Individual Medley.
  Kwa mujibu wa Hadija, waogeleaji hao pia watashindana katika relay katika mashindano ambayo yamepitishwa na Shirikisho la Mchezo wa kuogelea Duniani (Fina) kuwa ya kutafuta alama za kufuzu mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika nchini Korea mwezi  Julai.
  “Tunatarajia kuona ushindania mkali  kwa waogeleaji wetu ili kutafuta nafasi ya kufuzu mashindano ya dunia. Waogeleaji wengi wapo katika maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mashindano hayo, bado tunahitaji wadhamini wa mashindano haya,” alisema Hadija.
  Kwa mujibu wa Hadija, kutakuwa na jumla ya vipengele  vya mashindano 108 na kila klabu imetakiwa kuwakilishwa na waogeleaji wawili katika kila kipengele cha mashindano ambavyo pia vimepangwa kutokana na umri.
   

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari(katikati) akiwapongeza kwa kuwanyanua mikono juu washindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’. Kulia ni Mojelwa Mlinga kutoka Dar es Salaam na kushoto Said Khatibu kutoka Zanzibar

  Washindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa ikijulikana kama ‘Cash In Promotion’.Said Khatibu (kushoto) kutoka Zanzibar na Mojelwa Mlinga kutoka Dar es Salaam na (kulia) wakifurahia mfano wa hundi walizabidhiwa baada ya kuibuka washindi katika promosheni hiyo.  

   Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni mbili, Mshindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’, Said Khatibu kutoka Zanzibar, jijini Dar es Salaam jana.
  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni mbili, Mshindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’, Mojelwa Mlinga kutoka Dar es Salaam kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya Tigo, jijini Dar es Salaam jana  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari(katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kukabiudhi zawadi kwa washindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’,Kulia ni Mojelwa Mlinga, mshindi kutoka Dar es Salaam na kushoto Said Khatibu kutoka Zanzibar.
  Kampuni ya Tigo Tanzania, leo imetoa zawadi za mamilioni ya shilingi kwa mawakala wake wa huduma ya Tigo Pesa kupitia promosheni iliyomalizika hivi karibuni ya ‘Wakala Cash In Promotion’.

  Promosheni hiyo ya nchi nzima ilianza Machi 1 na kumalizika Machi 31 ikilenga kuwahamasisha mawakala wa Tigo Pesa kufanya miamala zaidi na wateja ili kujishindia zawadi za fedha taslimu.

  Akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa baadhi ya washindi jijijni Dar es Salaam jana,mkuu wa kitengo cha bidhaa wa Tigo Pesa James Sumari alisema jumla ya Mawakala 97,000 walishiriki katika promosheni hiyo ya mwezi mmoja.

  “Promosheni hii ya aina yake, ni ya saba kwa Mawakala wetu. Tangu tulipoanza hadi kufikia hivi sasa, tumewazawadia mawakala 12,000 zaidi ya fedha taslimu shilingi bilioni 1. Washindi hawa wametoka kila kanda hapa nchini na tumeendelea kuona mwitikio mkubwa wa Mawakala kupitia promosheni hii na ni mpango wetu kuendelea kuwarushia tunachokipata kupitia wao wakati tukiendela na safari ya kufikisha huduma jumuifu za kifedha nchi nzima,” alisema Sumari

  Kwa mujibu wa Sumari, Promosheni ya mwaka huu, ilishuhudia washindi wakubwa 8 kutoka sehemu mbali mbali za nchi ambao waliweza kujishindia fedha zaidi kutokana kuwa washindi wa jumla kwenye promosheni.

  “Tumechagua Mawakala wawili waliofanya vizuri kuliko wengine katika kanda zote nne na kuwazawadia kutokana na jitihada zao za kufanya miamala mingi zaidi na wateja. Leo pia tunawashindi ambao watapata zawadi zaidi za fedha taslimu.

  Washindi wakubwa ambao leo wanakabidhiwa zawadi zao wanatokea kanda ya Pwani ambao ni pamoja na Said Khatib kutoka Zanzibar ambaye atakabidhiwa shilingi milioni 2 na Mojelwa Mlinga Mojelwa kutoka Dar es Salaam ambaye amejinyakulia Shilingi milioni 1.

  Tunayo furaha kuhitimisha promosheni yetu kwa kishindo.Tunaamini fedha tulizowazawadia Mawakala wetu zitawasaidia kukuza biashara zao pamoja na kukidhi mahitaji yao mengine. Napenda kumalizia kwa kumpongeza bwana Khatib na Mojewa pamoja na maelfu ya washindi wengine. Mchango wao unatusaidia kuweza kufikisha huduma jumuifu za kifedha hapa Tanzania kupitia Tigo Pesa,” alifafanua Sumari.

  Sumari aliongeza kuwa, makabidhiano ya zawadi kwa washindi wa jumla katika kanda za Kaskazini, Kusini na Kanda ya Ziwa yatafanyika baadaye mwezi huu.


  0 0

  MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), umeendesha semina fupi kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuhusu shughuli za Mfuko ikiwa ni miezi nane tangu kuanzishwa kwake.

  PSSSF imeundwa kwa Sheria ya Utumishi wa Umma namba 2 iliyopitishwa na Bunge Januari 31, 2018 ambayo inaunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, LAPF, PPF na PSPF.

  Katika semina hiyo iliyofanyika Aprili 12, 2019, wajumbe walielimishwa kuhusu majukumu ya Mfuko, Wanachama wa Mfuko na Mafao yatolewayo na Mfuko.
  Afisa Mkuu wa Matekelezo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Mordgard Maten, (kulia), akitoa elimu kuhusu shughuli za Mfuko huo kwa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Aprili 12, 2019. Wakwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Japhet Maselle.
  Afisa Mkuu wa Matekelezo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Mordgard Maten (kulia), akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu shughuli za Mfuko kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Aprili 12, 2019.
  Afisa Mtekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw.Msafiri S. Mugaka (kulia), akiwa na Afisa Mkuu wa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. Mordgard Maten kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Aprili 12, 2019.
  Baadhi ya wajumbe wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF.
  Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle (kulia), akiwa na baadhi ya viongozi wa baraza hilo wakisikilzia mada zilizokuwa zikitolewa na maafisa wa PSSSF.
  Baadhi ya wajumbe wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF.
  Afisa Uhsiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, akizunumza wakati wa semina hiyo.
  Baadhi ya wajumbe wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF.
  Maafisa wa PSSSF kutoka kushoto, Bw.Msafiri S. Mugaka, Bw. Abdul Njaidi na Bw.Donald Peter.
  Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle (kulia), akizungumza wakati wa semina hiyo.
  Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle (watatu kulia), na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA, na maafisa waandiamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu shughuli za Mfuko kwa wajumbe wa Baraza hilo.

  0 0

  Na Hussein Stambuli-Morogoro.

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Bashiru Ally amesema ili Taifa lifikie malengo ya maendeleo na amani idumu inapaswa viongozi waliopewa nyadhfa mbalimbali katika jamii kutenda haki na usawa na kuachana na wizi wa mali za umma, unyonyaji kwa wanyonge, rushwa pamoja na ufisadi. 

  Dk.Bashiru ameyasema hayo leo Aprili 12, 2019, wakati akizungumza na wakulima kwenye mdahalo ulioandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) ikiwa ni maadhimisho ya kutafakari maisha ya Waziri Mkuu wa zamani nchini Hayati Edward Moringe Sokoine kwa kuangalia mtazamo wake kuhusu maendeleo vijijini na mchango wa wakulima wadogo katika ujenzi wa uchumi wa kitaifa ambapo akataka kiongozi huyo kuenziwa kivitendo. 

  "Usawa ni kila binadaam anastahili heshima ya kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wake sio usawa wa rangi wala kimo au umaarufu au uduni wao lakini woote ni binaadam ambao utu wao unastahili kuheshimiwa, na mtu anaeamini katika usawa wa binaadam lazma pia akubali katika jamii ile ile watokee watu ambao wanakula na kusaza na kutupa wakati wengine wanakufa na njaa,"amesema Dk.Bashiru. 

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kavazi la Mwalimu Julias Nyerere, Profesa Issa Shivji amesema wananchi hawawezi kujikomboa bila mapambano, hivyo ni muhimu kuwa na umoja na kukemea uovu wowote unaofanywa kwa kwenda kinyume na sharia na taratibu za nchi. "Lazima tuwe na chombo chetu kama wakulima chombo cha kutuelimisha, kutulinda hasa wananchi wa vijijini jambo litakalowasaidia kufahamu haki zao,"amesema Shivji. 

  Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA Steve Ruvuga amesema lengo kuu la mdahalo huo ni kujadili na kufikisha maoni kwenye ngazi mbalimbali ili uzalishaji uwe na tija zaidi kwa wakulima nchini."Naamini tunayoyazungumzia hapa yanahusu masuala mapana ya kilimo yanayohusu masuala mapana ya kilimo pamoja nauzalishaji wa kilimo chenyewe hasa kwa wakulima wadogo kwahiyo tunaamini tafakari ya leo itatufanya tufaham namna bora ya uzalishaji na kukuza uzalishaji."
  Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (ccm) taifa dr bashiru ally akizungumza na wakulima wadogo katika maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani wa tanzania  hayati edward moringe sokoine
   2. wakulima waliojitokeza katika  mdahalo ulioandaliwa na  mtandao wa vikundi vya wakulima tanzania mviwata ikiwa ni maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani wa tanzania  hayati edward moringe so
   Mwenyekiti wa kavazi la mwalimu julias kambarage nyerere prof issa shivji akizungumza na wakulima wadogo katika maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani wa tanzania  hayati edward moringe so
   5.katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (ccm) taifa dr bashiru ally katikati, kulia Mwenyekiti wa kavazi la mwalimu julias kambarage nyerere prof issa shivji na kuliadk.ng’wanza kamata, mhadhiri kutoka chuo kikuu ch
   Mkurugenzi mtendaji wa mviwata steven ruvuga akifafanua jambo katika mdahalo ulioandaliwa na  mtandao wa vikundi vya wakulima tanzania mviwata ikiwa ni maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani .

older | 1 | .... | 1836 | 1837 | (Page 1838) | 1839 | 1840 | .... | 1898 | newer