Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46317 articles
Browse latest View live

Jumia Mobile Week: Gulio la mauzo ya simu mtandaoni kwa punguzo la bei mpaka 60%!!!

$
0
0


Simu ya Tshs. 820,000 kuuzwa kwa Tshs. 8,000 tu!!!!!

Wateja kupelekewa bidhaa bure wakifanya manunuzi yatayaozidi Tshs. 50,000!!!
Dar es Salaam: April 9, 2019. Ulikuwa unajiuliza ni wapi na lini unaweza kununua simu mpya, za kisasa na kwa bei nafuu ambayo haukuitegemea?




Katika jitihada za kuhakikisha kuwa inarahisisha upatikanaji na matumizi ya simu za kisasa kwenye maisha ya kila siku ya Watanzania, Jumia imezindua gulio kubwa la mauzo ya simu za mkononi mtandaoni likijulikana kama ‘Mobile Week.’ Hili ni tukio kubwa la mauzo ya bidhaa zinazohusiana na simu ambapo limeanza leo Aprili 8 na kufikia kikomo mnamo Aprili 14. Lengo kuu la kampeni hii ni kuwapatia wateja muda wa kutosha na fursa ya kununua aina tofauti za simu za kisasa wazipendazo kwa bei nafuu, punguzo kubwa la bei, kujipatia vocha za kurahisisha manunuzi pamoja na zawadi kemekem ndani ya kipindi chote cha kampeni.


Akizungumzia sababu zilizopelekea kuwa na kampeni kubwa ya ‘Mobile Week’ kila mwaka, Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Bw. Albany James ameelezea kuwa, “Simu ni miongoni mwa bidhaa ambazo zinanunuliwa zaidi kwenye mtandao wetu wa Jumia. Lakini pia hata kwa takwimu zinazotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kwamba watumiaji wa simu za mkononi wanaendelea kuongezeka kila mwaka. 
Mwaka 2018 idadi ya watumiaji wa simu walikuwa takribani milioni 43.6 ukilinganisha na milioni 40 mwaka 2017. Hivyo basi sisi kama wadau katika urahisishaji wa mauzo ya bidhaa mbalimbali tumeona ni vema kuwa na kampeni kubwa ya mauzo ya ‘simu pekee’ kila mwaka ambayo itawawezesha Watanzania kufanya manunuzi kwa urahisi na bei nafuu ukilinganisha na sehemu yoyote ile.”


“Mobile Week’ kwetu sisi ni kampeni muhimu zaidi kutokana na manufaa makubwa iliyonayo si tu kwa wateja wetu bali na Watanzania kwa ujumla. Na ndiyo sababu iliyopelekea kila mwaka kujitahidi kuwa wabunifu na kuiboresha kwa kuja na simu za aina tofuati zaidi kutoka kwa washirika wetu, ofa kabambe, punguzo kubwa la bei, vocha za kurahisisha manunuzi pamoja na zawadi kemkem kupitia ‘Treasure Hunt’ siku ya Jumatano ya Aprili 10 kuanzia saa nane mchana. Ambapo simu aina ya Infinix inayouzwa Tshs. 820,000 itauzwa Tshs. 8,000 tu kwa mteja atakayebahatika kuisaka na kuipata kwenye mtandao wetu. Pia kutakuwa na vocha za manunuzi za kila siku ambapo mteja atakuwa anarahisishiwa manunuzi yake pindi atakapozitumia,” aliongezea Bw. James

“Ningependa kutoa wito kwa Watanzania wote kuitumia fursa hii ya ‘Mobile Week’ kununua simu ambazo walikuwa wanatamani kuwa nazo kwani aina ni nyingi na punguzo la bei ni kubwa tofauti na siku za kawaida. Kampeni ya mwaka huu imekuja kitofauti kwasababu kwa manunuzi yoyote ambayo yatazidi Tshs. 50,000 yatakayofanyika kwenye mtandao wa Jumia, mteja atapelekewa bure kabisa bila ya gharama yoyote ya usafirishaji mpaka pale alipo!” Ikipita fursa hii ni mpaka mwakani tena ambapo sidhani kama kuna mtu anaweza kuvumilia kuishi kpindi chote hiko bila ya simu au kuwa tayari kuingia gharama kubwa kufanya manunuzi mara baada ya kampeni hii kupita,” alihitimisha Meneja Masoko wa Jumia Tanzania.


Miongoni mwa sababu zinazopelekea kuendelea kuenea kwa upatikanaji na matumizi ya simu za mkononi na: kuendelea kuongezeka kwa makampuni ya mawasiliano ya simu, kuongezeka kwa makampuni yanayouza simu hivyo kupelekea upatikanaji kuwa rahisi na kwa bei nafuu, pamoja na uwepo wadau wanaorahisisha upatikanaji wa haraka wa bidhaa kama vile Jumia, soko kubwa la uuzaji na manunuzi ya bidhaa mtandaoni.

Tembelea tovuti ya Jumia sasa, https://www.jumia.co.tz/, kujionea bidhaa tofuati zinazopatikana katika kipindi hiki cha kampeni ya ‘Mobile Week’ kabla haijafikia ukomo. Jumia imejizatiti kuhakikisha manunuzi ya uhakika na usalama, urahisi kwa kukutanisha wanunuzi na wauzaji tofauti kutoka sehemu tofauti kwa wakati mmoja, bidhaa ni halisi na za kisasa, bei ni nafuu ukilinganisha na sehemu zingine, na kikubwa zaidi ni kwamba malipo ya bidhaa ni mpaka pale mteja atakapofikiwa na kujiridhisha nazo, na amepewa uwezo wa kuzirudisha na kuomba kubadilishiwa bila ya gharama yoyote ile!

Serikali Yanunua Mtambo wa Madini

$
0
0
Na Immaculate Makilika- MAELEZO 

Serikali imenunua mtambo mkubwa wa madini ambao utasaidia kufanya utafiti wa madini, sambamba na kuwasaidia wachimbaji wadogo katika shughuli za madini nchini 

Akizungumza Bungeni leo jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kwa lengo kuunga mkono wachimbaji wadogo nchini kote wakiwemo wachimbaji wa kijiji cha Busiri wilaya ya Biharamulo. 

Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa ili kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini, Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imenunua mtambo mkubwa wa kumsaidia kufanya utafiti wa kina kwa kuchoronga miamba kwa bei nafuu ili kubaini mashapo zaidi na kuongeza uzalishaji. 

Naibu Waziri, Nyongo aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa wachimbaji wadogo ili wanufaike zaidi na kazi ya uchimbaji. 

Wizara kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini inakamilisha uandaaji wa kitabu cha madini yapatikanayo Tanzania toleo la nne ambacho kitaonesha uwepo wa madini katika mikoa, wilaya na vijiji, ambapo kitasaidia wachimbaji wadogo kutambua madini yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na matumizi ya madini hayo. 

Aidha, Wizara kupitia Mradi wa Usimamizi endelevu wa Raslimali Madini (SMMRP), inakamilisha kujenga vituo vya umahiri katika wilaya ya Bukoba, Bariadi, Songea, Handeni, Musoma, Mpanda na Chunya ili kuwezesha wachimbaji wadogo kujifunza kwa vitendo.

MAKABIDHIANO YA TUZO BIKOSPORTS

$
0
0
 Msemaji wa Bikosports, Geoffrey Lea, kushoto akimpongeza Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, kulia baada ya kumkabidhi zawadi yake ya kuwa Kocha Bora wa mwezi Machi, ambapo tuzo hizo ambazo wadhamini Wakuu ni Kampuni ya kubashiri michezo mbalimbali ya Biko Sports.
 Msemaji wa Bikosports Geoffrey Lea kushoto akimpongeza mshambuliaji mahiri wa Simba SC, John Bocco, baada ya kuibuka mchezaji bora wa mwezi Machi, ambapo tuzo hizo zinadhaminiwa na Kampuni ya kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali ya Bikosports.
 Kocha Mkuu wa Simba SC, Mbelgiji Patrick Aussems kulia akiwa na mshambuliaji wake John Bocco, ambaye yeye amepewa zawadi yake ya kuwa Kocha bora wa mwezi Machi, huku Bocco akitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi.

WAKULIMA KASULU WALIA BEI ZA PEMBEJEO

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kasulu

BAADHI ya wakulima wa Wilayani Kasulu wameiomba serikali kupunguza bei za pembejeo za kilimo hususani mbolea za kupandia na kukuzia ili waweze kulima kilimo chenye tija.

Wakulima hao wameiomba serikali kupunguza bei ya mbolea ya kupandia kutoka shilingi elf sabini bei ya sasa kwa mfuko wa kilo hamsini hadi elf arobaini pia kwa upande wa mbolea ya kukuzia ambayo kwa sasa bei yake ni shilingi elf arobaini kwa mfuko wa kilo hamsini wameomba ipungue hadi elf ishirini.

Hayo wameyasema jana kwenye mafunzo ya siku moja juu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa Wilaya hiyo na mawakala wanaouza pembejeo ambapo mafunzo hayo yalitolewa kwa udhamini wa kampuni ya GSM sambamba na  uzinduzi wa mbolea yao ya GS Agro.

Said Shaaban ni mmoja wa wakulima waliohudhuria mafunzo hayo alisema kuwa kwasasa bei za pembejeo nyingi zipo juu ambapo wakulima wenye kipato cha chini wanashindwa kumudu gharama hizo za bei na kushindwa kulima kilimo cha kisasa chenye tija.

"Unajua sisi tumezowea kulima kwa mazowea tumekuwa tukitumia mbolea kwenye mazao ya chakula tunayolima ambayo ni mahindi na maharage ambapo hatuwezi kupata mavuno mengi sababu ya kutolima kisasa,Serikali naomba ituangalie sisi wakulima wa chini kwa kupunguza bei za pembejeo za kilimo"alisema

Naye Mwezeshaji wa wakulima Fatuma Bahi kutoka kijiji cha Msambala alisema kuwa changamoto wanayokutana ni upungufu wa maofisa ugani katika vijiji hali inayopelekea kata zaidi hata ya tatu kuhudumiwa na ofisa ugani mmoja.

"Tuletewe maofisa ugani vijijini ili waweze kutupa elimu ya kulima kilimo cha kisasa na chenye tija ili tuweze kufikia malengo yetu na ya Taifa,maana sasa wengi unakuta wanalima kilimo cha mazowea bila ya kuwa na elimu yoyote"alisema

Mhandisi kilimo na umwagiliaji wa Mkoa wa Kigoma Yohana Zephania wakulima wengi hawatumii pembejeo badala yake wanalima kilimo cha mazowea na kujikuta wakipata mavuno machache,lakini wakitumia pembejeo watapata uzalishaji mkubwa.

Mkuu wa kitengo cha mauzo kutoka kampuni ya tanzu ya GS Agro Remi Nindi alisema mbali na kampuni yao kuuza mbolea wamekuwa wakiwatembelea wakulima wao mara kwa mara na kujua changamoto zao.

"Huu ni msimu wa pili tunaenda mbolea yetu ya GS Agro imekuwa ikifanya vizuri kwa shuhuda mbalimbali za wakulima,msimu ujao tutabadilisho muonekano wa rangi ya mfuko tunaoweka mbolea pia tukuwa na mbolea kuanzia kilo tano ili wakulima wote waweze kumudu kuinunua na kulima kilimo chenye tija"alisema.
 Mkuu wa Kitengo cha mauzo kutoka kampuni tanzu.ya GS Agro Remi Nindi akiongea na wakulima na mawakala wa pembejeo Wilayani Kasulu baada ya uzinduzi wa mbolea yao ya GS Agro.

 Mbolea za kupandia na kukuzia GS Agro.kutoka kampuni ya GSM zikiwa kwenye mfuko wa kilo 50 zilizozinduliwa Wilayani Kasulu .
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo

WAZIRI MKUU: MIFUKO YA PLASTIKI MWISHO JUNI MOSI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Juni mosi mwaka huu, itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote na matumizi yake yatakoma ifikapo Mei 31, 2019.


“Hivi karibuni nimemwagiza Waziri anayesimamia masuala ya mazingira ikiwemo kuzungumza na wadau mbalimbali, ikiwemo wenye viwanda vya kutengeneza mifuko ya plastiki kwa ajili ya kuhakikisha jambo hili linatekelezwa kwa haraka.”

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Aprili 9, 2019) Bungeni jijini Dodoma, kwenye mkutano wa 15 wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2019/2020.

“Kuanzia sasa tunatoa fursa ya viwanda kubadilisha teknolojia, wauzaji kuondoa mzigo uliopo, Ofisi ya Waziri wa Nchi, Makamu wa Rais itajiandaa kutumia kanuni chini ya Sheria ya Mazingira ili kulifanya katazo hili kuwa na nguvu ya kisheria. Tunachukua hatua hii ili kulinda afya ya jamii, wanyama, mazingira na miundombinu dhidi ya athari kubwa zinazotokana na taka za plastiki,” amesema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua kwamba kuna baadhi ya bidhaa lazima zifungwe kwenye vifungashio vya plastiki na kwamba vifungashio kwa bidhaa hizo havitapigwa marufuku.“Kwa msingi huo, katika hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, yatatolewa maelezo ya kina kuhusu katazo la vifungashio vya aina hii, hasa katika maeneo ya uzalishaji viwanda, sekta ya afya, na kilimo,” amesema.

Amesema ana imani kuwa utaratibu huo pamoja na kutunza mazingira, utatoa fursa ya kutengeneza ajira nyingi husasan za watu wa chini kupitia utengenezaji wa mifuko mbadala ya plastiki pamoja na kutumia kikamilifu fursa ya viwanda vya karatasi vilivyopo nchini ikiwemo cha Mgololo.

Amesema matumizi ya plastiki nchini yameendelea kuleta madhara makubwa ikiwemo vifo vya mifugo kwa kula plastiki, kuziba kwa mifereji, uchafuzi wa mazingira na kushindikana kwa kuozesha taka kwenye vituo vya kukusanya taka. 

Bunge lilikubali kupitisha sh. 148,886,523,581/- kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake kwa mwaka 2019/2020. Kati ya hizo, sh. 86,290,355,000/- ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 62,596,168,581/- ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Vilevile, Bunge liliidhinisha sh. 124,182,537,600 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo kati ya hizo 116,573,026,000/- ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 7,609,511,600/- ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

WAKAZI WA KISARAWE, PWANI KUPATA MAJISAFI NA SALAMA IFIKAPO MWEZI NANE

$
0
0
Uchimbaji wa mitaro wa ajili ya kulaza mabomba ukiendelea.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelekezo wakati akikagua ulazaji wa mabomba ya maji kutoka kwenye tenki la Kibamba na kuelekea tenki la Kisarawe kwa ajili ya kuwapatia maji kwa wakazi wa Pwani. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja  (wa tatu toka kulia) akipata maelezo toka kwa Msimamizi wa mradi wa Usambazaji wa Maji Mhandishi Kakwezi wakati akikagua ulazaji wa mabomba ya maji kutoka kwenye tenki la Kibamba na kuelekea tenki la Kisarawe kwa ajili ya kuwapatia maji kwa wakazi wa Pwani. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo toka kwa Msimamizi wa mradi wa Usambazaji wa Maji Mhandishi Kakwezi wakati akikagua ujenzi wa tenki la Kibamba litakalokuwa likipeleka majisafi na salama kwenye tenki la Kisarawe kwa ajili ya kuwapatia maji kwa wakazi wa Pwani. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelekezo mara baada ya kufika kwenye umaliziaji wa ujenzi tenki la Kisarawe litalokuwa likiwasambazia wakazi wa Pwani.
Mabomba.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelekezo mara baada ya kufika kwenye zoezi la uchimbaji wa mitaro ya kulaza mabomba.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akishiriki katika uchimbaji wa mitaro eneo la Kisarawe- Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akiongea na wanahabari na wananchi waliofika kuangalia zoezi la utandikaji wa mitaro kwa ajili ya kulaza mabomba itakayokuwa ikiwasambazia wakazi wa Pwani.

BEI YA NYAMA TANDIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Bei za Nyama katika bucha  mbalimbali katika soko  la Tandika  wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,kama zinavyo onekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Bei za Nyama katika bucha  mbalimbali katika soko  la Tandika  wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,kamazinavyo onekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

Benki ya Exim Yazindua Kampeni ya Afcon Kwa Wateja Wake

$
0
0
Benki ya Exim leo imezindua kampeni maalum inayofahamika kama 'Afconika na Exim' ambayo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri.

Akizungumza wakati wa unzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Samaam leo, Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo alisema kampeni hiyo ya miezi miwili itakamilika mwanzoni mwa mwezi Juni na ipo wazi kwa wateja wapya na wale ambao tayari wana akaunti za benki hiyo.

“Kampeni hii inakuja ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki ya Exim katika kusimamia ustawi wa wateja unaofahamika kama 'Exim kazini leo, kwa ajili ya kesho' (Exim at Work Today, for tomorrow) unaoendana na dira na muelekeo wa benki hiyo. Ni kampeni inayothibitisha nia ya benki ya Exim katika kutafuta kesho iliyo bora kwa wateja na jamii inayoizunguka.’’ Alisema.

Alisema washindi wa kampeni hiyo watapata fursa ya pekee ya kufurahia mchezo wanaoupenda huku pia wakipata fursa ya kuungana na Taifa Stars katika mashindano hayo huku wakiwa wamelipiwa gharama zote za safari ikiwemo gharaza na Visa, tiketi ya ndege, gharamza za tiketi ya kushuhudia mechi hizo pamoja na fedha za kujikimu.

"Jumla kutakuwa na washindi watano ambapo washindi wawili watapatikana katika mwezi wa awali wa kampeni na washindi wa wengine watatu watapatikana katika mwezi wa mwisho wa kampeni hii.’’ Alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Lyimo ili kushiriki katika kameni hiyo, wateja wapya wanapaswa kufungua Akaunti ya Akiba na kuhakikisha kila mwezi ina kiasi kisichopungua Tshs 500,000 au zaidi au kufungua Akaunti ya Current/biashara ikiwa na wastani wa kila mwezi wa Tshs 10,000,000 au hifadhi ya amana maalum (Fixed deposit) yenye thamani isiyopungua Tshs 5,000,000. "Alisema.

Kwa wateja ambao tayari wana akaunti ya benki hoyp, Bw Lyimo alisema wanachotakiwa kufanya ni kuongeza akiba kwa kiasi cha Tshs 500,000 au zaidi kwa Akaunti za Akiba au kuongeza kiasi cha Tshs 10,000,000 kwenye akaunti zao za Current/biashara au kuwa na hifadhi ya amana maalum (Fixed deposit) yenye thamani isiyopungua Tshs 5,000,000.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu, alisema kampeni hiyo ni fursa adimu ambapo itatoa nafasi kwa washindi hao kuweza kushuhudia Taifa Stars ikitimiza ndoto zake za kushiriki katika mashindano ya AFCON baada ya zaidi ya miaka 30 kupita.

Kwa mujibu wa Bw Kafu, kampeni hiyo ni sehemu ya mkakati wa kibenki katika kutafuta kesho bora kwa wateja wake na jamii kwa ujumla ambapo pamoja na mambo mengine benki hiyo imekuwa ikiunga mkono agenda za kitaifa ikiwemo suala zima la michezo.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum inayofahamika kama 'Afconika na Exim' ambayo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo (katikati)
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum inayofahamika kama 'Afconika na Exim' ambayo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo Bw Arafat Haji (Kulia) na Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo (kushoto)
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim makao makuu jijini Dares Salaam wakionesha ishara ya ushangiliaji wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum inayofahamika kama 'Afconika na Exim' ambayo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kulipiwa gharama zote za safari na malazi ili waweze kushuhudia mechi za timu ya taifa, Taifa Stars katika mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019 nchini Misri. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.

WAHITIMU WA MAFUNZO YA UONGOZI HAKIKISHENI MNAZINGATIA UZALENDO,UADILIFU-DK.MWANJELWA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dk.Mary Mwanjelwa amewataka wahitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi kuhakikisha katika maeneo yao ya utumishi wanafanya kazi kwa uadilifu mkubwa na uzalendo kwa nchi yetu.

Ameshauri wahitimu hao waliomaliza mafunzo hayo katika Taasisi ya Uongozi wanakuwa mfano wa kuigwa katika maeneo yao ya utumishi kwa kuhakikisha mafunzo ya Uongozi ambayo wameyapata yanakuwa dira ya wao kutekeleza majukumu yao ya uongozi katika misingi ya kutenda haki huku akiwataka kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo ya pili ya Taasisi ya Uongozi jijini Dar es Salaam, Dk.Mwanjelwa amesema wahitimu wa mahafali hayo ya pili ya Stashahada ya Uzamili katika Uongozi wanakilsababu ya kuonesha wameiva katika uongozi na kutekeleza majukumu yao katika kiwango cha kimataifa.

"Wahitumu mliopata mafunzo ya Uongozi kutoka hapa Taasisi ya Uongozi tambueni mnalo jukumu la kwenda kufanya kazi zenu kwa kutanguliza uadilifu na uzalendo mkubwa kwa Taifa letu.Kufanya kazi kwa umahiri peke yake haitoshi, hivyo hakikisheni mnafanya kazi kwa misingi ya maadili na uzalendo.

" Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu Dk.John Magufuli pamoja na mambo mengine inahimiza watumishi wa kada zote kuwa waadilifu katika maeneo yao ya utumishi.Hivyo kupitia mafunzo hayo tunaamini wahitimu ambao wengi wenu tayari ni viongozi huko mnakofanya kazi nendeni mkawe mfano wa kuigwa,"amesema Dk.Mwanjelwa.

Ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Taasisi ya Uongozi kwa namna ambavyo imeamua kujiongeza kwa kuona haja ya kutafuta fedha ili kuhakikisha viongozi wanapata mafunzo hayo ambayo yanatija kubwa kwa Taifa katika kuandaa viongozi.

"Tunafahamu wapo viongozi ambao wanatokana na karama ya Mungu katika kuongoza lakini hiyo peke yake haitoshi kwani kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa amepikwa na kupata mafunzo ya uongozi kutoka kwa walimu wabobezi tulionao katika Taasisi ya Uongozi na wale wabobezi wa nje ya Tanzania.Hivyo mliohitimu leo hii niseme tu mmeiva na Taifa linawategemea ,"amesema Dk.Mwanjelwa.

Pia amewakumbusha watumishi wa umma na sekta binafsi wakiwamo wahitimu wa mafunzo ya Uongozi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kukomesha rushwa kwani rushwa ni adui wa haki.

"Mafunzo ambayo mmeyapata mkayetende kwa kiwango cha kimataifa.Mmefundishwa maadili,vipaji,utawala bora,athar za rushwa na kuajiri. Hatutarajii kuona wahitimu wa mafunzo haya mnapokea rushwa na viongozi au kufumbia macho vitendo vya rushwa,"amesema.

Awali hotuba iliyotolewa na Taasisi ya Uongozi kwa mgeni rasmi ilisema mafunzo hayo ya Stashahada ya Uzamili katika Uongozi yanayotolewa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiama na Chuo Kikuu cha Aalto Finland yalizinduliwa Mei 19,2017 na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Anjellah Kairuki.

Mahafali ya kwanza yalifanyika Machi 21,2018 ambapo wengi wa washiriki walikua maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi la Tanzania. "Leo tunaazimisha mahafali ya pili, ambapo wahitimu wote pia ni maafisa waandamizi na viongozi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma. Mafunzo haya ya Stashahada ya Uzamili katika Uongozi yanachukua mwaka mmoja kukamilika, na yanatolewa kwa mfumo wa moduli.

" Mafunzo yana jumla ya moduli kumi, kila moja ikichukua mwezi mmoja kukamilika. Aidha, kila moduli inachukua siku mbili au tatu za darasani; na muda mwingine masomo hufanyika kwa njia ya mtandao. Kwa moduli zote, washiriki hulazimika kuhudhuria darasani bila kukosa, na kufanya mazoezi na mitihani yote. Kila mwanafunzi analazimika kufaulu mitihani na mazoezi yote ili atambulike kama mhitimu wa Programu hii na kupatiwa cheti,"imesema sehemu ya hotuba liyotolewa kwa mgeni rasmi.

Imeelezwa lengo la mafunzo hayo ya Stashahada ya Uzamili katika Uongozi ni kuwaimarisha washiriki katika maeneo makubwa matatu ya kiuongozi na kiutendaji.Maeneo hayo ni kuimarisha uwezo wao katika kufanya maamuzi ya kimkakati. Pia maamuzi ya kimaono, yanayozingatia mahitaji na manufaa mapana ya sasa na ya baadaye kwa jamii.

Eneo jingine ni kuimarisha uwezo wao katika kuongoza watu na kusimamia rasilimali nyingine, ili kutekeleza kwa kikamilifu na kwa mafanikio maamuzi ya kimkakati, waliyoyafanya katika kipengele cha kwanza pamoja na kuimarisha uwezo wao katika kujijengea sifa binafsi za uongozi.

" Ni imani yetu maofisa Waandamizi na Viongozi hawa 34 ambao wametunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi watatumia sifa hizi walizozipata katika utekelezaji wa majukumu yao. Hata hivyo Programu hii bado ni changa. Kwa hivyo, pamoja na mafanikio tunayojivunia leo bado kuna changamoto.

"Kubwa ni ile ya gharama za kuandaa na kutoa mafunzo haya; gharama hizi ziko juu. Hili ni jambo la kawaida kwa Programu zote nzuri kama hii, ambayo pia inatambulika kimataifa. Wakati wa mahafali ya mwaka jana tulizungumza umuhimu wa kushirikiana na wadau mbalimbali kuchangia mafunzo haya. Hili tumejaribu kulitekeleza kuanzia awamu hii ya tatu,"imesema .
 Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora aliyekuwa mgeni rasmi katika.mahafali ya pili ya Taasisi ya Uongozi ( ) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi na viongozi wa taasisi hiyo
 Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dk.Mary Mwanjelwa akikabidhi cheti kwa mhitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi John Mongella ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza .Mahafali hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam
 Mgeni rasmi katka mahali ya Taasisi ya Uongozi Dk.Mery Mwanjelwa ambaye ni Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akilishwa keki kama inashara ya wahitimu kutambua uwepo wake na ujumbe ambao ameutoa kwenye mahafali hayo
 Baadhi ya wahitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dk.Mary Mwanjelwa(hayupo pichani)
 Baadhi ya wageni waliohudhuria mahafali ya pili katika Taasisi ya Uongozi kushuhudia wahitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dk.Mary Mwanjelwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Uongozi na wafadhili wa mafunzo ya Stashahada ya Uzamili katika Uongozi

WIZARA YAHAMASISHA WATANZANIA KUNUNUA BIDHAA ZA NGOZI ZINAZOZALISHWA NA VIWANDA VYA NDANI

$
0
0
*Yakutana na wadau kujadili namna ya kuimarisha soko, ubora wa ngozi

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imewahamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kupenda kununua bidhaa za ndani na hasa bidhaa zinazotokana na mazao ya ngozi huku ikiweka wazi mikakati yake katika kuhakikisha ngozi za Tanzania zinaendelea kuwa bora.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mbele ya wadau wa ngozi nchini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel amesema ipo haja ya Watanzania kuhakikisha wananunua bidhaa zitokanazo na mazao ya ngozi ambazo zinatengenezwa na viwanda vya ndani ya nchi badala ya kununua bidhaa za ngozi zinazotoka nchi nyingine.

"Tunatoa rai kwa wananchi wote tujenge tabia ya kupenda bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi yetu na hasa bidhaa za ngozi kama viatu, mkanda, mikoba na aina nyingine ya bidhaa.Binafsi viatu vyangu ambavyo nimevaa vimetokana na ngozi ya mifugo ya kwetu na kiwanda ambacho kimetengeneza nacho ni cha hapa hapa Tanzania.

"Ni viatu vizuri sana na kwa bei nafuu.Hivyo hakuna sababu ya kununua bidhaa za ngozi ambazo zinatoka nje wakati kwetu uwezo wa kutengeneza tena katika kiwango bora upo,"amesema Profesa Gabriel.

Kuhusu ubora wa ngozi, Profesa Ole Gabriel amesema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati mbaimbali ya kuhakikisha ngozi ambayo inatokana na mifugo iliyopo nchini Tanzania inaendelea kuwa bora ambapo amefafanua umefika wakati wa kuhakikisha ng'ombe wanaandaliwa tangu wanapozaliwa ngozi yao inalindwa ili iwe bora zaidi na hiyo si tu itafanya kuwepo na ngozi bora bali kuongeza thamani ya ngozi na bidhaa zake.

"Tumekutana na wadau wa ngozi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu, tumejadili mafanikio na changamoto na kwa pamoja tumekubaliana kuendelea kushirikiana kuhakikisha bidhaa zetu za ngozi zinapata nafasi ya kununuliwa na Watanzania.Wote tuwe na utamaduni wa kupenda vya kwetu kwani kuna baadhi ya watu wana ugonjwa wa kuona vinavyotoka nje ndio bora kuliko vya kwetu wakati si kweli.Bidhaa zinazozalishwa nchi ni bora , hivyo nitoe rai tununue vya kwetu,"amesisitiza.

Akizungumzia kuhusu soko la bidhaa zitokanazo na ngozi, amesema Wizara yao inawahakikisha wadau wa ngozi kuwa Serikali imejipanga katika kuhakikisha kunakuwa na soko la uhakika ambapo ameahidi kuendelea kufanya mazungumzo na Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na wadau wengine kwani dhamira ya Serikali ni kujenga viwanda na hivyo kuna kila sababu ya uwepo wa viwanda vya ngozi. "Tutahakikisha tunakuwa na soko la uhakika katika bidhaa za ngozi hasa katika kipindi hiki cha ujenzi wa viwanda ambapo tunataka kuwepo na viwanda vya bidha za ngozi."

Wakati huo huo, Profesa Ole Gabriel amesema wamepokea ombi la wadau wa ngozi la kutaka iwepo bodi ya ngozi ambayo itasimamia sekta ya ngozi nchini na kwamba ombi hilo wamelipokea na Wizara italifanyika kazi kwani lina tija na nia njema.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Chama cha Wadau wa Ngozi chini Joram Wakari amesema kwa sasa wanakwenda vizuri kutokana na jitihada ambazo zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuhakikisha sekta ya ngozi inapewa kipaumbele nchini na tayari kuna mafanikio.
"Tukiri kuna mafanikio makubwa katika eneo hili la sekta ya ngozi.Hivyo iwapo changamoto chache zilizopo zikiondolewa tutafanya vizuri zaidi ya tunavyofanya sasa.Nitoe ombi kwa Wizara ni vema ikaanzisha Bodi au Mamlaka ya kusimamia sekta ya ngozi kwani kukosekana kwa chombo maalumu kwa ajili ya ngozi kuna mambo yanashindwa kutatuliwa kwa wakati,"amesema Wakari.

Wakati huo huo Meneja wa Operesheni wa Woiso Original Products Co Teya Herman amesema ombi lao kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kusaidia kuzuia uingizwaji wa bidhaa za ngozi kutoka nje ambazo ziko chini ya ubora na zinapoingia nchini zinauzwa kwa bei ya chini na hivyo kusababisha wao kukosa soko.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) akizungumza na wadau wa ngozi nchini kuhusu namna ya kuimarisha sekta ya ngozi nchini na bidhaa zake
Mkurugenzi Mtendaji wa Woiso Original Products Co Kenneth Woiso(kulia) na Meneja Opereshenj wa Woiso Original Products Co Teya Herman wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) baada ya wadau wa ngozi kukutana kujadili sekta ya ngozi nchini.
 Baadhi ya wadau wa sekta ya ngozi nchini walioshiriki kikao cha wadau wa ngozi kilichoitishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel

HALOTEL YAKABIDHI MSAADA KWA NAIBU WAZIRI WA MIPANGO NA FEDHA DKT. ASHATU KIJAJI KONDOA.

$
0
0


Kampuni ya simu za mikononi ya Halotel imetoa msaada wa madawati 55 kwa ajili ya shule za Sekondari za wilaya ya Kondoa ikiwa ni malengo yake ya kuunga mkono juhudi za wilaya hiyo na Serikali katika kuboresha elimu.

Akipokea msaada huo wilayani humo juzi, Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji mbali na kuipongeza Halotel kwa msaada huo alisema madawati hayo ni msaada mkubwa kwa wilaya hiyo iliyojipambanua katika mkakati wa kipekee wa kukuza elimu.

Alisema Halmshauri hiyo na wanakondoa wote kwa ujumla wanatambua juhudi mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ya simu katika kuboresha maisha ya wananchi hayo ikiwemo ya kuwaunganisha na nchi nzima kupitia njia ya mawasiliano ya simu za mkononi.

Dkt Kijaji alisema kupokelewa kwa madawati hayo kwa kiasi kikubwa kutasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati uliomo katika wilaya hiyo na hivyo kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kutokana na uhitaji uliopo kwa sasa.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza Halotel kwa msaada huu ikiwa kama mdau mkubwa wa maendeleo ya elimu ndani ya wilaya hii na Tanzania kwa ujumla, nitoe wito kwa taasisi na kampuni zingine kuiga mfano huu kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika Taifa letu” alisema Dk Kijaji.

Aidha aliiomba Kampuni hiyo kuisaidia wilaya hiyo kuboresha elimu kwa kuwajengea maabara itakayokuwa imeunganishwa na mfumo wa mtandao wa intaneti kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo masomo mbalimbali hususani ya sayansi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Nguyen van Son, alisema kampuni hiyo kama mdau mkubwa maendeleo inayo mikakati mbalimbali katika kuboresha ya sekta ya elimu na afya nchini ikiwa ni mipango yake ya kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali zilizopo nchini.

Alisema kwa kutambua changamoto za kielimu zilizopo katika wilaya hiyo, Halotel iliona ina kila sababu ya kutoa msaada wa c madawati hayo kwa lengo la kumuunga mkono juhuzi za wilaya hiyo za kuboresha elimu zinazofanywa na Naibu Waziri wa Wizara ya fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo hilo la Kondoa Dk Ashatu Kijaji.

Alisema Halotel imekuwa ikiunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuboresha maisha ya wananchi wake kwa kushiriki katika mambo mbalimbali hususani katika sekta za afya na elimu, na hivyo kupunguza changamoto hizo zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini.

Akitolea mfano katika sekta ya afya, Van Son alisema katika siku za hivi karibuni Halotel imenzisha mpango maalumu utakaowawezesha watu wenye matatizo ya kiafya kukutana na kupata ushauri wa tiba na matibabu kwa kuwaunganisha na madaktari bingwa chini ya mpango maalumu ulioanzishwa na kampuni hiyo.

Alisema Halotel inatambua changamoto zilizopo katika eneo hilo hivyo wao kama wadau wakubwa wa maendeleo wanaona wana kila sababu kushirikiana na Serikali katika kuzitatua na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo nchini inayofanywa chini ya uongozi wa awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli.

Naye Afisa elimu wa Wilaya ya Kondoa Hildegard Segunda alisema wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa madawati 906 uliotokana na ongezeko la wanafunzi katika shule za Sekondari zilizopo katika wilaya hiyo.Alisema hatua hiyo imetokana na muitiko wa wanafunzi kuingia shuleni kwa wingi na hususani baada ya kuondolewa gharama za malipo chini ya mpango bure wa elimu uliotolewa na Rais Magufuli.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akikabidhiwa madawati 55 na Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Nguyen Van Son, kwa ajili ya shule za Sekondari za wilaya ya Kondoa ikiwa ni moja ya malengo yake ya kuunga  mkono juhudi za wilaya hiyo na Serikali  katika kuboresha elimu katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Nguyen Van Son,wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla fupi ya kukabidhi madawati kwa ajili ya shule za Sekondari za wilaya ya Kondoa ikiwa ni moja ya malengo yake ya kuunga  mkono juhudi za wilaya hiyo .Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kondoa na baadhi wa maofisa na watendaji katika wilaya hiyo.

SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

$
0
0
Na Lulu Mussa,Dodoma 

Serikali imejipanga kuhakisha kuwa mifuko mbadala wa plastiki inapatikana kwa wingi ili kukidhi mahitaji. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika hii leo Jijini Dodoma na kusisitiza kuwa katazo la Mifuko ya Plastiki lililotolewa jana na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa linakuwa na nguvu kisheria kwa kuandika kanuni za katazo ya mifuko ya plastiki zitakazotangazwa katika gazeti la Serikali chini ya Sheria ya Mazingira na kutoa adhabu kwa kila mtu atakaekiuka utaratibu uliowekwa. 

“Kabla ya Serikali kutangaza hatua ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki, ulifanyika utafiti na maandalizi ya mifuko mbadala. Uwezo wa kuzalisha upo na mifuko ya karatasi inayotumika Kenya na Rwanda inatumia malighafi inayozalishwa Mgololo-Iringa,Tanzania.” Makamba alisistiza 

Waziri Makamba ameainisha kuwa kuna vifungashio ambavyo havitapigwa marufuku ambavyo ni pamoja na vifungashio vya dawa za hospitalini, vifungashio katika sekta ya kilimo na ujenzi pia vile vya kuhifadhi maziwa na kutolea mfano wa vifungashio vya maziwa ya ASAS na Tanga Fresh, hata hivyo utaratibu maalumu utawekwa kwa wamiliki wa kukusanya vifungashio hivyo mara baada ya matumizi yake. 

Akizungumzia juu ya ushirikishwaji, Waziri Makamba amesema kuwa zoezi hili limekuwa ni shirikishi na hatua iliyotangazwa na Waziri Mkuu sio ya kushtukiza kwa kuwa Ofisi yake iliratibu mikutano katika maeneo kadhaa nchini kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu zuio la mifuko ya plastiki. 

Katika kukamilisha utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Waziri Makamba amesema Ofisi yake imeunda kikosi kazi cha kusimamia katazo hilo kikihusisha wajumbe kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Shirika la Viwango Tanzania, Mamlaka ya Chakula na Dawa, Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Wengine ni Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Katika hatua nyingine Waziri Makamba amesema kuwa mapema wiki ijayo ataitisha mkutano wa wawekezaji wa mifuko mbadala kote nchini na kujadili kwa kina namna bora ya kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala rafiki wa mazingira. 

Serikali imetangaza kuanzia Juni Mosi 2019 kuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote na matumizi yake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na waandishi wa Habari kufafanua tamko la Serikali la kupiga marufuku uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini. Mkutano huo umefanyika hii leo katika jengo la PSSSF jijjini Dodoma.

TAASISI YA PINK HIJAB INITIATIVES YAANDAA MBIO NA MATEMBEZI YA KILOMETA KUMI JIJIN DAR

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Tasisi ya Pink Hijab Initiatives imeandaa mbio na Matembezi ya Kilometa kumi kuanzia Viwanja vya Green Ground Osterbay na kuishia katika Viwanja hivyo kwa kupitia barabara ya  Kenyata, Chole Road,Karume Road , Haile Salasi Road kupitia Coco Beach na kurudi katika Viwanjani hapo.

akizungumza na Globu ya Jamii Mratibu wa Mbio hizo kutoka Pink Hijab Initiative, Alhaj Jamal Mwarab Khalfan amesema kuwa lengo la mbio hizo ni kusaidia watoto waliopo katika Mazingira hatarishi katika Mkoa wa Tanga Wilaya ya Pangani.

"Sisi kama Tasisi ya Kislamu tumeona vyema kuitumia Ramdhani hii kama sehemu ya kurudisha tunachokipata kwa jamii kwa kuandaa mbio hizi na matembezi hili tuweze kuwasaidia watoto wetu waliopo katika Wilaya ya Pangani hivyo tunawaomba wote wenye mapenzi mema na watoto wetu kuja kujumuika na sisi April 21 Mwaka huu"amesema Alhaj Jamal.

Amesema mtu anayependa kushiriki mbio hizi anaweza kuchangia kiasi cha shilingi 20,000/-pia naweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0713433407 au 0655445105 hili aweze kushiriki na kuchangia zaidi.

--

MKUTANO WA TANO MABADILIKO YA TABIANCHI WAFANYIKA DODOMA

$
0
0
Waziri Nchi,Ofisi yaMakamu wa  Rais, Anayeshughulikia  Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika leo jijini Dodoma katika ukumbi wa hotel ya Morena

Na.Vero Ignatus ,Dodoma 

Mkutano mkuu wa Mabadiliko ya Tabianchi umefanyika leo Jijini Dodoma ukiwashirikisha wadau zaidi ya 100 wameshiriki katika mkutano huo ukiwa na lengo la kujadili mabadiliko ya Tabia nchi na kujikwamua katika taizo hilo kama Taifa

Akifungua mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Eric Mugurusi amesema lengo kuu la mkutano huo ni kujadili Sera ambazo zitatilia maanani mabadiliko ya Tabia nchi na namna ambavyo wananchi watashirikishwa ili kupunguza athari za mabadiliko hayo.  

 Amesema kuwa mkutano huo ni maalum kwaajili ya kuona nam,na ambavyo sera zinavyoweza kuwaondoa kwenye tatizo hiolo na ushirikiswahwaji wa wananchi katika hayo yote.

Waziri Nchi,Ofisi yaMakamu wa  Rais, Anayeshughulikia  Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi amesema katika kuhakikisha tunaondoa tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kuwajumuishe watu wote,  kujifunze katika nchi zilizofanikiwa na kuzitumie mbinu hizo, Kuaanda Sera nzuri,Kuwahimiza watunga Sera kuamuru uchukuliwaji wa hatua

Mhe.Makamba amesema kuwa kwenye baadhi ya nchi Mabadiliko ya tabia ya nchi yametangazwa kama usalama wa nchi ambapio nasi kama nchi ipo haja ya kuonesha kuwa changamoto zinaweza kuwa kubwa kwani Utalii wetu ni Fukwe ambazo zinalika na thamani yake inaondoka sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi,hivyo utalii unapotea.

"Mama  yangu alikuwa Nesi miaka ya 1980 anasema kipindi hiko hakukuwa kabisa na kesi za wagonjwa wa malaria, lakini angali miaka ya sasa,Wagonjwa wa malaria wamekuwa wengi na ndo ugonjwa mkubwa hii ni sababu ya ongezeko la Mbu kwa kasi kubwa na kutokutunza mazingira yetu”Alisema Makamba

  Amesema kati ya miaka 5-10 mabadiliko ya tabia nchi yalionekana kama nadharia au yanawahusu wanasayansi ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivbyo tatizo linavyozidi kuwa kubwa, hata kwenye kilimo sababu ya mabadiliko ya Majira kumesababisha kuchelewa kwa mvua hivyo Kilimo kinafanyika kwa shida  pia yanapelekea umasikini.

Mimi nilisomeshwa sana kwa kilimo cha Chai na Kahawa ambacho ndio kikubwa Tanga, lakini sasa hivi kilimo cha mazao haya kinapotea,hali hii ni ishara ya kuongezeka kwa umasikini''Alisema Makamba

Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam Jovita Mlay amesema kuwa Mabadiliko ya Tabianchi yanaongeza umasikini kwa wanawaume na wanawake lakini wahanga wakubwa zaidi ni wakina mama na watoto kwani inagusa maeneo ambayo wanawake wanajipoatia kipato napo no kwenye kilimo.


Amesema kuwa wakati wa kushughulikia majanga kama hayo ni muhimu kuhakikisha kuwa inawekwa mipango na usimamizi wa kisera unaoweza kupunguza na kumaliza madhara ya yatokanayo na mabadiliko ya Tabianchi kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali

Amesema Oxfam inaendelea kufanya kazi  ili kuhakikisha kuwa maswala yanayoingizwa katika mipango mikakati na kuendelea kusapoti juhudi zinazofanywa na wadau katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi.

Kwa upande wake mbunge wa Babati vijijini Mhe,Jitu Soni amesema kuwa jamii nyingi zinaishi katika mazingira magumu kutokana na mabadiliko ya Tabianchi amesema kuwa mabadiliko hayo siyo jambo la mazingira peke yake bali linahusisha maswaka ya uchumi,miundombinu,mifumo ya uzalishaji,rasilimali,na nishati.

Nae Mwenyekiti wa Bunge ya Bajeti na mbunge wa Kibakwe Mhe.George Simbachawene amesema kuwa mgawanyo wa shughuli za kibinadamu imekuwa sababu kubwa ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya Tabianchi,amesema bado elimu inahitajika zaidi katika jamii zetu haswa vijijini ili kujinasua katika tatizo hilo.

Aidha watu wengi wanaharibu mazingira kwasababu ya kutafuta maji na nishati,uwekezaji wa kutafuta maji unatumia gharama kubwa sana,amesema nchi inahitaji kutengeneza mfumo wa kitaalam katika uharibifu wa mazingira kwani hali ni mbaya sana 

Mshiriki kutoka Asasi za kiraia mkoa wa Kagera bi Zainabu Shakiru amewaomba Serikali pamoja na wadau kuwa mchakato wa utekelezaji wa sera ya mabadiliko ya tabianchi wananchi nao washirikishwe ipasavyo ili waweze na wao kuitambua sera hiyo
Akifungua mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Eric Mugurusi amesema lengo kuu la mkutanowa tano wa mabadiliko ya tabianchi Jijini Dodoma leo
Meneja Mradi Jovitha Mlay kutoka Shirika la Oxfam akizungumza katika mkutano wa tano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika leo Jijinj Dodoma katika hotel ya Morena
Washiriki wa mkutano wa tano wa mabadiliko ya Tabianchi Jijini Dodoma leo
Ndugu Jensen Shuma kutoka shirika la TaTEDO akichangia mada katika mkutano wa tano wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma
Dkt.Lucy Ssendi Mshauri wa Maswala ya Mabadiliko ya Tabianchi ,Mradi wa Decentralized Climate Finance -TAMISEMI akichangia mada katika mkutano wa Tano wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma
Makamu Balozi wa EU Nchini Tanzania Charles Stuart akizungumza na washiriki wa mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Jijini Dodoma leo.
Jovita Mlay Meneja wa Mradi kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Oxfam Tanzania akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika leo Jijini Dodoma katika hoteli ya Morena
Washiriki kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini Tanzania waliohudhuria katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma katika Hotel ya Morena.
Mkurugenzi mtendaji wa Jumuiko la maliasili Tanzania( TNRF)Zakaria Faustin akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma.

Waziri Kabudi akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi, akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo baina yake na Balozi wa Ufaransa nchini Mheshimiwa Frédéric Clavier. Katika mazungumzo hayo Tanzania na Ufaransa wamekubaliana kushirikiana katika kilimo cha zabibu, uzalishaji na uuzaji wa mvinyo katika nchi mbalimbali duniani na usafiri wa anga.

Mazungumzo yakiendelea.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Palamagamba John Kabudi akiagana na Balozi wa Ufaransa nchini Mheshimiwa Frédéric Clavier baada ya mazungumzo baina yao. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi, akimkaribisha Balozi wa Ufaransa nchini, Mheshimiwa Frédéric Clavier alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 10 Aprili 2019. 

AGIZO LA WAZIRI HALIJADILIWI,NI KUTEKELEZA-PROF.KIKULA

$
0
0
Wachimbaji wadogo wakiwa chini ya mgodi katika shimo lenye urefu wa zaidi ya mita hamsini wakiwa wanaendelea na shuguli za uchimbaji katika eneo la Ipanko.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula wa pili kushoto akiwa katika eneo la wachimbaji wadogo Ipanko wilayani Ulanga akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Madini Mkazi Morogoro Mhandisi Emmanuel Shija alipotembelea kujionea namna shuguli za uchimbaji zinavyofanyika. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari kwenye eneo la mgodi wa wachimbaji wadogo Ipanko.


Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akionyesha jambo kwenye ramani ya mwekezaji wa Madini ya Graphite; TanzGraphite (T) Ltd. Wa tatu kushoto ni Meneja Uhusiano wa Jamii Bernad Mihayo, wa pili kushoto ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki.
Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Macheyeki kushoto akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula mara baada ya kuzunguka na kukagua eneo la wachimbaji lililopo Iponka eneo ambalo awali lilifungiwa kufanya shuguli za uchimbaji. 
 …………………..

Na Issa Mtuwa- Ulanga Morogoro

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amewataka Watumishi wa tume hiyo ofisi ya Morogoro na Ulanga kutambua kwamba agizo la Waziri linalowataka kufuta leseni zisizofuata utaratibu wa kisheria sio la kujadili bali ni kutekeleza.

Prof. Kikula ameyasema hayo Aprili 10, 2019 wilayani Ulanga wakati akizungumza na watumishi wa tume hiyo wakati wa ziara yake.

Taarifa iliyosomwa kwake na Afisa Migodi Mkazi ofisi ya Mahenge Ulanga, Tandu Jilabi inaonyesha kuwa wilaya ya Ulanga ina leseni za wachimbaji wadogo 221 kati ya hizo ni leseni 9 tu ndio zinazofanya kazi huku leseni za uchimbaji wa kati zikiwa 5 na leseni za utafiti wa madini 13.

Kufuatia hali hiyo, Afisa Migodi Mkazi ofisi ya Mahenge ameiomba tume ya madini kufuta leseni zisizofanya kazi ili wapewe wenye uhitaji ili waweze kuziendeleza. Kufuatia ombi hilo, Mwenyekiti wa tume amesema jukumu la kuzifuta leseni hizo ni la kwake pamoja na Afisa Madini Mkazi Morogoro na halina mjadala kwakuwa muongozo wa utekeleza wa suala hilo ulishatolewa na waziri wa Madini.

“Suala la leseni zisizofanya kazi sio la kujadili, hili ni agizo la Waziri na kazi yetu ni kutekeleza na wenye kuzifuta ni ninyi, fuateni taratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria katika kuzifuta na sio kuzifuta lazima wote waliozishikilia leseni hizo kwa muda wote walipe fidia na wasipo fanya hivyo taratibu za kisheria zifuatwe kwani katika kipindi hicho chote serikali imekosa mapato yake. Kuanzia leo pitieni leseni zote na ifikapo Juni 30 mwaka huu leseni zote zisizo hai ziwe zimefutwa”, amesema Prof. Kikula.

Wakati huo huo, mwenyekiti wa tume amekutana na kuzungumza mwakilishi wa mwekezaji wa kampuni ya TanzGraphite (T) Ltd ambae ni Meneja Uhusiano wa Jamii na kuzungumzia kuhusu mgogoro uliopo baina ya mwekezaji huyo na baadhi ya wananchi wanaotakiwa kufanyiwa tathimini ili kupisha shuguli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo.

Prof. Kikula ameonyesha kusikitishwa na mgogoro huo ambao amesema ni wa muda mrefu sasa na unachelewesha maendeleo ya watu na kuikosesha serikali mapato.

Ameongeza kimsingi wananchi wanapaswa kuelewa kuwa “right surface” (haki ya kumiliki vitu vilivyo juu ya ardhi) inampa mwananchi haki ya kulipwa fidia ya mali zilizo juu ya ardhi anayo miliki lakini watambue kuwa kuna “resource right” (haki ya kumiliki raslimali zilizo chini ya ardhi) ikiwemo madini ambayo mmiliki wake ni serikali, ndio maana inapohitaji raslimali hizo humuondoa na kumfidia mliliki wa mali za juu ya ardhi, hivyo wananchi wanapo ng’ang’ania wanatakiwa walitambue hilo.

Pia, amesema kuwa, kwa mpango ulioanishwa na mwekezaji huyo unaonyesha manufaa kwa wananchi kupitia miradi ya maendeleo (CSR) ambapo amebainisha kuwa mwekezaji ameahidi kuwalipa fidia, kuwajengea nyumba za kisasa wale wote walio ndani ya eneo.

Mambo mengine ni pamoja na kuwapatia chakula kwa muda wa miaka miwili wakiwa kwenye makazi mapya watakayo jengewa na kila kaya kusomesha mtoto mmoja kwenye vyuo vya veta na wakihitimu wataajiriwa na mgodi ili waweze kupata kipato cha kusaidia na kuendeleza kaya zao.

Pamoja na hayo, mwekezaji huyo amemweleza mwenyekiti wa tume kuwa tayari wameshakubaliana kujengaa kituo cha afya, matundu ya vyoo kwa baadhi ya shule, kujenga shule na ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali. Hata hivyo hakusita kuonyesha kusikitishwa kwake na watu wachache wanaogoma kuondoka kupisha shuguli za uchimbaji huku kila kitu ikiwemo mtaji wa shuguli hizo ukiwa tayari.

Katika mgogoro huo, kaya 347 zinatakiwa kuondoka kupisha mwekezaji huyo na kati ya hizo kaya 62 ndio zinazo goma kuondoka ili mwekezaji aanze kazi ya uchimbaji. Mwenyekiti amesikitishwa na hali hiyo na na kuuomba uongozi wa mkoa na wilaya kuzungumza na kaya hizo sambamba na Baba Askofu aliyeko ndani ya eneo hilo ili mradi huo uanze kwani ni wa muda mrefu na serikali inakosa mapato.

Amesema kwa sasa anaziachia juhudi za serikali ya mkoa na wilaya katika kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.

Mapema mwenyekiti alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya ambapo amemshukuru kwa ushirikiano anao utoa kwa viongozi na wafanyakazi wa tume ya madini wilaya ya Ulanga.

Amesisitiza suala la uadilifu kwa wafanyakazi wa tume na amesema hilo litakuwa jambo la kwanza kulisema kila aendapo sambamba na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali. Aidha, amesema kipimo kikubwa cha kila mkuu wa kituo cha tume ya madini kitakuwa ni ukusanyaji wa maduhuli ambapo katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 tume ilipangiwa kukusanya Bilioni 310 na mwaka wa fedha ujao tume imepangiwa kukusanya Bilioni 467.

Upande wake, Kamishna wa tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki amewakumbusha na kuwasisitiza watumishi wa tume na wachimbaji wa madini kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji na ulipaji wa tozo na stahiki zote za serikali kwa wakati.

Amesema kwa kufanya hivyo raslimali za madini zitakuwa na tija kwa taifa kama anavyo sisitiza Rais John Pombe Magufuli kuwa anataka raslimali za madini ziwanufaishe watanzania wote na namna za kuwanufaisha ni kulipa stahiki za serikali zinazo tokana na madini ili zikatumike kujenga uchumi wa taifa.

Prof. Kikula na Dkt. Macheyeki wanaendelea na ziara yao mkoani Morogoro kukagua shuguli za Tume katika Wilaya mbalimbali ambapo leo walitembelea eneo la wachimbaaji wadogo ipanko wilayani ulanga.

AKWILAPO ATAKA SUA KUSAIDIA ONGEZEKO LA UZALISHAJI KILIMO

$
0
0
katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dokta Leonard Akwilapo amesema hali ya uzalishaji wa chakula nchini inaelezwa kuwa ndogo,ambapo takwimu za uzalishaji za mwaka 2015 zinaonesha kuwa ni asilimia tatu nukta tatu kwa mujibu wa mpango wa Taifa ya maendeleo ya awamu ya pili 2016/ 2017, 2020/ 2021 ambapo mpango wa serikali unatajwa kupandisha kiwango hicho kufikia asilimia nne nukta sifuri ifikapo kabla ya mwaka 2025…

Katika kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa,Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo anatumia kumbukizi ya miaka kumi na sita ya kifo cha hayati Edward Moringe Sokoine kukiagiza chuo kikuu cha Sokoine (SUA ) kuhakikisha kinatumia wataalamu wake katika kufanikisha dhana hiyo.

“kwa pamoja tunakazi kubwa ya kufanya ili kufikia lengo hili kilimo chetu kinapaswa kukuzwa na kuwa cha kisasa Zaidi” alisema dkt akwilapo. Pia katibu mkuu amehaidi kutoa million 750 kutoka mradi wa kukuza ujuzi na stadi za kazi kwa ajili ya kuboresha kalakala ya idara uhandisi kilimo katika chuo hicho cha kilimo SUA..

Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Raphael Chibunda amesema chuo kimeaandaa mdahalo kwa kuwakutanisha wanasanyansi na watu ambao wamefanya kazi pamoja na Sokoine ili kupata kwa kiina yale aliyofanya Marehemu huyo ambapo mada kuu ni Uzalishaji wa kilimo na Viwanda na Maendeleo ya Tanzania mabo ya kujifunza kutoka kwa sokoine na na siku zijazo..

“Tumewaalika wazee waliofanya kazi na hayati sokoine enzi za uhai wake na wametukubalia ambao watatupatia uzoefu wa namna ya utendaji wake enzi za uhai wake jambo litakalokuwa na tija kwetu” alisema Prof chibunda.. mwakilishi wa familia ya aliyekuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya kwanza hayati Edward Moringe Sokoine Bw. Ole Edward amesema kama familia wameanda wakfu ili kuendelea kuyaenzi yale aliyofanya marehemu Sokoine…

Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki aprili 12 mwaka 1984 katika eneo la Wami sokoine wilayani Mvomero akitokae Bungeni katika majukumu ya kikazi na wiki ya kumbukikizi hiyo imeanza aprili 9 mwaka huu na inatarajiwa kufikia kilele aprili 12 mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Raisi mama samia Suluhu Hassani.
 Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dokta Leonard Akwilapo kulia akiwa na makamu mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha  Kilimo SUA Profesa  Raphael Chibunda wakitazama moja ya njia rafiki ya kkilimo ch
 Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dokta Leonard Akwilapo, wa pili kutoka kushoto akiambatana na katibu tawala mkoa wa morogoro cliford tandari katika ukaguzi wa miradi mbalimbali ya kilimo chuo cha Sokoine.

WAZIRI WA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI WA SMZ DK. UBWA MAMBOYA AIPONGEZA TTCL

$
0
0

Mhandisi wa Mitambo ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Aman Kichere (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (katikati) namna mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inavyofanya kazi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba akishuhudia.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (kushoto) akizungumza mara baada ya ziara yake kutembelea Miundombinu na Mitambo ya Mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba akiwa na mgeni wake.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw. Waziri Kindamba (mwenye kipaza sauti) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (kushoto) alipotembelea miundombinu na Mitambo ya Mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation.

Waziri, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (kulia mbele) alipotembelea miundombinu na mitambo ya mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation. Wengine ni maofisa kutoka TTCL Corporation, na Wizara ya Mawasiliano Zanzibar.







Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (mbele) akitembelea miundombinu na mitambo ya mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation. Wengine ni maofisa kutoka TTCL Corporation, na Wizara ya Mawasiliano Zanzibar.



WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mamboya, amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Shirika lsa Mawasiliano Tanzania( TTCL Corporation) katika kutoa huduma bora za Mawasiliano na usimamizi wa Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano Nchini.

Mhe Waziri Dkt. Sira Ubwa Mamboya,ametoa pongezi hizo Jijini Dar Es Salaam mara baada ya ziara yake katika Shirika la Mawasiliano Tanzania, kutembelea Miundombinu na Mitambo ya Mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation.

Katika salamu zake, Mhe Waziri amepongeza utendaji wa TTCL mpya ambayo inafanya juhudi kubwa za kuliimarisha Shirika na huduma zake na kuonesha kufurahishwa na utaratibu wa Shirika hilo kutoa ajira kwa kuzingatia pande zote za Muungano hali inayoimarisha udugu na uhusiano mwema.

Akizungumza katika salamu za kumkaribisha Mhe. Waziri, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw Waziri Kindamba amewashukuru viongozi Wakuu wa SMZ kwa uongozi wao thabiti unaodumisha Muungano na kustawisha ushirikiano unaoiwezesha TTCL Corporation kutimiza vyema majukumu yake katika Ofisi zake zote Tanzania Visiwani ambapo inaihudumia Serikali, Taasisi za Umma na Sekta binafsi.

“Tunapopata ugeni kama huu, tunafarijika sana kwani kupitia tukio hili, uhusiano mwema wa kindugu baina ya pande mbili za Muungano unaimarishwa, Aidha, tunabadilishana ujuzi na uzoefu pamoja na kujenga mtazamo wa pamoja wa namna bora zaidi ya kuwahudumia Wananchi wetu” amesema Kindamba.

Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation lilizaliwa tarehe 01 Februari 2018, kwa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2017. Kuundwa upya kwa Shirika hili la TTCL Corporation ni matokeo ya kukamilika kwa mchakato wa kutunga sheria uliopitia katika hatua zake zote ikiwemo kuridhiwa na Bunge na hatimaye kupata idhini ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 28 Novemba, 2017.

Huduma za mkongo wa Taifa wa Mawasiliano zinazosimamiwa na kuendeshwa na TTCL zimeiwezesha Tanzania kuwa Nchi ya kupigiwa mfano katika Ukanda wa kiuchumi wa Nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara kutokana na kuwa na mfumo mzuri zaidi kukusanya kodi kwa kutumia mfumo maalumu wa kielektroniki wa Serikali ujulikanao kama GePG.

KAMPUNI YA CLOUDS MEDIA GROUP YAMKOSHA WAZIRI DK.MWAKYEMBE

$
0
0


*Ni baada ya Kampuni hiyo kupata leseni ya kuonesha mashindano makubwa ya kukuza vipaji

*Amwambia Joseph Kusaga ubunifu, uthubutu wao ni fahari kubwa kwa nchi ya Tanzania

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Clouds Media Group wameandika tena historia! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya kampuni hiyo kupewa leseni kamili ya kuendesha mashindano makubwa ya vipaji kwa Ukanda wa Africa Mashariki (East Africa’s Got Talent).

Mashindano hayo yatakuwa yanaonekana katika mabara mbalimbali na takribani nchi zaidi ya 58 duniani zitakuwa zikifuatilia hatua kwa hatua namna ya vipaji vinavyoibuliwa kupitia mashindano hayo.

Akizungumza Aprili 10 , 2019 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe amesema anawapongeza Clouds Media Group kwa kufanikiwa kupata leseni ya kuonesha mashindano hayo makubwa kwani wameletea heshima nchi yetu ya Tanzania.

Dk.Mwakyembe amesema " Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Joseph Kusaga na Clouds Media kwa ujumla mnafanya kazi kubwa sana katika nchi yetu na mmeendelea kuwa mstari wa mbele katika ubunifu na kuthubutu .Kwa kitendo hiki cha kupata leseni ya kuonesha mashindano haya makubwa ya kukuza vipaji , tukiri mmetutoa tena kimaso maso na sina maneno ya kusema.Leo hii naweza kutamba na kesho nikiwa bungeni nitatamba sana.

"Hongereni sana Clouds Media Group na kama ambavyo Joseph Kusaga ameeleza mashindano haya yataangaliwa na mamilioni ya watu duniani, kwetu sisi kama nchi hii ni fursa kwetu ya kujitangaza, kama mnavyofahamu tuna vivutio vingi vya utalii lakini bado havijatangazwa vya kutosha lakini kupitia mashindano haya kwetu ni sehemu ya kujitangaza na tutaitumia vema,"amesema Dk.Mwakyembe.

Amefafanua kuwa kama kipindi kitaangaliwa na mamilioni ya watu duniani maana yake ni fursa kwa nchi kutumia show hiyo kujitangaza kadri inavyoweza na tayari Wizara yake imejipanga kutumia fursa hiyo.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga wakati anazungumzia kupata leseni ya kuonesha mashindano hayo makubwa ya kukuza vipaji amesema kwa zaidi ya miaka 30 kampuni yao imejikita katika kutengeza fursa za kuhakikisha watanzania wenye vipaji wanapata nafasi ya kuonekana kufanikiwa kimaisha.

"Habari kubwa ya kiburudani ni kuzinduliwa rasmi kwa mashindano makubwa ya vipaji kwa ukanda wa Africa Mashariki (East Africa’s Got Talent). Mashindano haya yanaendeshwa kwenye mabara mbalimbali takribani nchi 58. Kwa mara ya kwanza katika historia Clouds Media Group tumepewa kamili (Franchised) ya kuendesha EAGT.

"Kwetu hili ni jambo kubwa na tunaamini tunakwenda kufungua fursa ya vijana wengi wenye vipaji mbalimbali, na kwa zaidi ya miaka 30 ya uwepo wetu tumekuwa tukiangalia namna ya kufungua fursa na maelfu ya vijana wa Tanzania wamefanikiwa,hivyo kama una kipaji chochote jiandae kwani tunakufungulia Dunia kuwa unachotaka,"amesema Kusaga.

Amefafanua zaidi pamoja na mambo mengine Clouds Media Group malengo yake ni kufungua milango kwa vijana wengi kwa kutengeneza Platfom ya kufungua fursa."Katika kuona hilo tuliona tunajaribu kila linalowezekana kufungua milango mingi zaidi na kubwa zaidi ni kupata International Brands na kisha kuzirudisha Tanzania ili kuinua vipaji vya vijana wetu."
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza mbele ya Wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa shindano hilo,Dkt Mwakyembe alisema "Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Joseph Kusaga na Clouds Media kwa ujumla mnafanya kazi kubwa sana katika nchi yetu na mmeendelea kuwa mstari wa mbele katika ubunifu na kuthubutu .Kwa kitendo hiki cha kupata leseni ya kuonesha mashindano haya makubwa ya kukuza vipaji , tukiri mmetutoa tena kimaso maso na sina maneno ya kusema.Leo hii naweza kutamba na kesho nikiwa bungeni nitatamba sana.

"Hongereni sana Clouds Media Group na kama ambavyo Joseph Kusaga ameeleza mashindano haya yataangaliwa na mamilioni ya watu duniani, kwetu sisi kama nchi hii ni fursa kwetu ya kujitangaza, kama mnavyofahamu tuna vivutio vingi vya utalii lakini bado havijatangazwa vya kutosha lakini kupitia mashindano haya kwetu ni sehemu ya kujitangaza na tutaitumia vema,"amesema Dk.Mwakyembe. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akifafanua jambo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe kuzindua rasmi shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akipiga makofi mara baada ya kumkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe kuzindua rasmi shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akipeana mkono na
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe mara baada ya kumkaribisha kuzungumza na Wageni waalikwa kabla ya uzinduzi wa shindano hilo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi wa Clouds Media Bw. Joseph Kusaga wakiwa na waratibu wengine wa tamasha hilo kutoka kushoto ni Mmoja wa waratibu Godfrey Mkama, Mchekeshaji kutoka Uganda Anne Kansiime na Lee Ndayisaba Mtayarishaji wa maudhui ya tamasha la , East Africa’s Got Talent.


Mkurugenzi Mkuu wa Cluds Medai Group Joseph Kusaga akiwa ameambatana na Mgeni rasmi Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe walipokuwa wakiwasili ukumbini kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar

Baadhi ya Wadau wakijadiliana jambo kabla ya uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar

Baadhi ya Wadau wakijadiliana jambo kabla ya uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa tayari kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Baadhi ya Wageni waalikwa wakijadiliana jambo kabla ya kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Mmoja wa Wadau akisubiri kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa tayari kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe kuzindua rasmi shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar.

Baadhi ya Watangazaji Mahiri wa Clouds FM wakisubiri kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar



Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Fancy Nkuhi wa pili kutoka kushoto ni miongoni mwa wageni waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Muongozaji wa shughuli nzima (MC),ambaye pia ni mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,Masoud Kipanya akitoa muongozo wa namna ya shughili nzima ya uzinduzi eleza taratibu mbalimbali na ufafanuzi



Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Uganda Anne Kansiime akifafanua jambo


Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa tayari kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar.

Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa tayari kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar.

HII NI KUBWA ZAIDI, WATEJA HALOTEL KUONGEA BURE

$
0
0

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Huduma mpya ya TOMATO PLUS katika ofisi za makao makuu ya Kampuni ya simu ya Halotel, ambapo mteja wa Halotel atapata uhuru wa kupiga simu na kuongea dakika 5 za kwanza kwenda mitandao yote bila kikomo. Kujiunga na huduma hii piga *148*66# Kisha chagua namba 8.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Huduma mpya ya TOMATO PLUS katika ofisi za makao makuu ya Kampuni ya simu ya Halotel, ambapo mteja wa Halotel atapata uhuru wa kupiga simu na kuongea dakika 5 za kwanza kwenda mitandao yote bila kikomo. Kujiunga na huduma hii piga *148*66# Kisha chagua namba 8. Pamoja naye ni Afisa Uhusiano wa Kampuni hiyo Stella Pius.

…………………………………………………………………………..

Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Halotel, imeendelea kuongeza thamani na ubunifu katika mawasiliano kwa kuzindua huduma mpya iliyoboreshwa ili kuwawezesha wateja wake nchi nzima kufurahia mawasiliano wakiwa mtandao wa Halotel pekee.

Huduma hiyo mpya iendayo kwa jina la TOMATO PLUS itamuwezesha mteja wa Halotel kuongea kwa dakika 5 za mwanzo bure mitandao yote kwa kila simu atakayopiga pale atakapojiunga na huduma ya Tomato Plus.

Akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa kitengo cha Mawasiiano wa Halotel Mhina Semwenda,amesema huduma hii ni ya wateja wote wa Halotel na Mteja akijiunga na huduma ya Tomato Plus, anaweza kuongea kwa dakika tano za mwanzo bure mitandao yote kwa kila simu atakayopiga.

“Huduma hii imeboreshwa zaidi kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wetu katika mawasiliano ili kuwawezesha kuwasiliana bila kikomo kwa kupiga simu mitandao yote na kuongea kwa dakika 5 za mwanzo bure kwa kila simu watakayopiga” alisema Semwenda.

“Mteja wa Halotel anaweza kujiunga na kufurahia huduma hii kwa kupitia menu yetu ya kwaida ya *148*66# na kasha atachagua namba namba 8 ambapo ataweza kujiunga kwa siku, wiki au mwezi na kufuraha huduma ya Tomao Plus wakati wowote na mahali popote.” Alisema na kuongeza Semwenda.

Huduma ya TOMATO PLUS imelenga katika kuongeza ufanisi, nafasi na uwezo wa mawasiliano kwa wateja wa Halotel na kwa watanzania wote, wakiwemo wafanya biashara, wafanyakazi wa sekta binafsi na serikali na wateja wengine walioko sekta zingine mijini na vijijini ambako maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kuwasiliana na kupata taarifa mbali mbali kwa uhakika.
Viewing all 46317 articles
Browse latest View live




Latest Images