Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1833 | 1834 | (Page 1835) | 1836 | 1837 | .... | 1897 | newer

  0 0

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali na Watanzania wote wataendelea kumuenzi shujaa wao, Marehemu Edward Moringe Sokoine.

  Amesema Marehemu Sokoine wakati wa uhai wake alijitoa kuchapa kazi kwa bidii na amelitumikia Taifa kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Aprili 6, 2019) katika mbio za marathon kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Sokoine. Mbio hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

  Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kwa makusudi kukiita Chuo Kikuu cha Kilimo jina la Sokoine ili kumuenzi shujaa huyo.Amesema Taifana Watanzania kwa ujumla wataendelea kufuata nyayo za Marehemu Sokoine katika mema mengi aliyolitendea Taifa la Tanzania na siku zote watandelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu.

  Waziri Mkuu amesema kufanyika mbio hizo za Marathon ni ushahidi kwamba Marehemu Sokoine bado anakumbukwa na kuheshimiwa na Watanzania kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika ustawi wa Taifa.

  Alisema katika uhai wake, Marehemu Sokoine alikuwa ni mfano bora wa kiongozi wa juu wa nchi aliyedhamiria kwa dhati kupambana na vitendo vya rushwa, uonevu, ubadhirifu na ufisadi.

  “Leo hii tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Sokoine sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli inayoendeleza kwa vitendo utendaji, uandilifu na mtazamo aliokuwa nao marehemu Sokoine.”

  Akizungumza kwa niaba ya familia ya Marehemu Sokoine, mtoto wa Marehemu, Namelok Sokoine alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuwaenzi kwa vitendo waasisi wa Taifa la Tanzania.Alisema anafarijika kuona kwamba yale yote aliyoyaamini na kuyasimamia Marehemu Sokoine hivi sasa yanatekelezwa kwa kasi zaidi na ufanisi wa hali ya juu na Serikali inayoongozwa Rais Dkt. Magufuli.

  Amesisitiza kwamba familia ya Marehemu Sokoine inaunga mkono kwa dhati juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na inaamini kwamba Tanzania yenye neema inakuja.Katika Marathon hiyo, washindi kwa uapnde wa wanaume waliokimbia kilomita 21 ni Joseph Panga, mshindi wa kwanza, na wa pili alikuwa ni Aliphonce Felix Simbu na mshindi wa tatu alikuwa Lazaro Damasi.

  Upande wa wanawake kilomita 21, mshindi wa kwanza alikuwa ni Faulina Abdi Matanga, mshindi wa pili alikuwa ni Magdalena Shauri na mshindi wa tatu alikuwa ni Nathalia Elisante.Waliohudhuria katika mashindano hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Wabunge na viongizi pamoja na wengine wa Serikali.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMAMOSI, APRILI 6, 2019
   
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzungumza katika Marathon ya Kumbukumbi ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha Aprili 6, 2019.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   Mtoto wa Marehemu Edward Sokoine, Namelok Sokoine akitoa salamu za familia katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha  Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine   kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Baadhi ya viongozi na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Wasanii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakti alipoozungumza katika Marathoni ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha  Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Joseph Panga zawadi ya shilingi milioni moja ambaye aliibukuka kuwa Mshindi wa kwanza wa Marathoni ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Edward Moringe Sokoine, Kilomita 21 wanaume kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. Wa tatu kulia ni mshindi wa pili Alphonce Felix Simbu na Kulia ni mshindi wa tatuLazaro Damas. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa Shirikisho la Riadha nchini, Anthony Mtaka, Mjane wa Marehemu Edwad Moringe Sokoine, Napono Sokoine na wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amezindua mradi wa ujenzi wa njia kuu ya umeme wa Kv220 Makambako-Songea na vituo vya kupoza na kusambaza umeme nje kidogo ya Halmashauri ya mji wa Songea Aprili 6, 2019.
  Katika hotuba yake Rais Magufuli ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kukamilisha mradi huo ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa mikoa ya Nkombe na Ruvuma lakini Watanzania wote kwa ujumla.
  “Mradi huu umeokoa shilingi Bilioni 9.8 ambazo zilikuwa zikitumika kununulia mafuta ya kuendesha jenereta za kufua umeme”. Alisema
  Rais alisema mradi umegharimu shilingi bilioni 216 kati ya hizo shilingi bilioni 45 zimetolewa na walipa kodi wa Tanzania na zilizosalia zimetolewa kwa ufadhili wa Serikali ya Sweden.
  Akifafanua zaidi Rais alisema, vijiji zaidi ya 122 vinavyopitiwa na mradi huu vitafaidika na umeme, vitapatiwa umemena hivyo kuondoa tishio la matumizi ya misiytu kama nishati.
  Kwa upande wake Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema Kulikuwa na kazi ya kujenga njai za kusafirisha umemehuu mkubwa wa kilovolti 220 umbali wa kilomita 250 ukitokea Makambako, Madaba hadi Songea mjini.
  Mradi utawaunganishia umeme wateja 22,700 katika vijiji unakopita na tayari vijiji 110 vimeunganishwa huku Taasisi za umma 114 na kazi ya usambazaji inaendelea.
  Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi alisema, mradi umetekelzwa kwa kioindi cha miaka miwili (2) hadi kukamilika.
  “Nia ya Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ni kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo 2023, na hatuwezi kufika kwenye uchumi wa kati bila ya kuwa na umeme wa uhakika, sisi TANESCO tunawezeshwa kwa miradi mbalimbali mikubwa ikiwemo ule wa Rufiji Hydro Power utakaoongeza Megawati 2115 zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.” Alisema.
  Alitoa rai kuwa watanzania hawana budi kufikiria uanzishaji viwanda na si lazima view vikubwa bali hata vidogo vitaleta faida ya kuwa na umeme huu wa uhakika
   Rais John Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Makambako-Songea wa msongo wa Kilovolti 220 na vituo vya kupoza na kusambaza umeme mkoani Ruvuma Aprili 6, 2019. Kushoto ni balozi wa Sweden hapa nchini, Mhe.Anders Sjoberg na kulia ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani.
   Rais John Magufuli (kushoto), Bakozi wa Sweden nchini, Mhe.Anders Sjoberg na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani. wakimsikiliza Meneja wa Mradi wa umeme wa 220kV, Makambako-Songea Mhandisi Didas Lyamuya
   Rais Magufuli akimpongeza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wakati wa hafla hiyo.
   Rais Dkt. John Magufuli akimpongeza balozi wa Sweden nchini, Mhe.Anders Sjoberg
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa hotuba yake
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa hotuba yake
   Waziri Dkt. Medard Kalemani akitoa hotuba yake.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, akitoa hotuba yake.

  0 0

  Muonekano nyanya katika moja ya vitalu nyumba vilivyotembelewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Wilaya ya Dodoma mjini.
  Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ally Msaki akiwa kwenye moja ya kitalu nyumba wakati wa ziara ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Wilaya ya Dodoma mjini na Chamwino.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU & MAELEZO)]

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea mradi wa ujenzi wa vitalu nyumba katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma Aprili 06, 2019.
  Moja ya Kitalu Nyumba cha mafano katika Wilaya ya Chamwino kama Kinavyoonekana ikiwa ni moja ya mikakati ya kuwainua vijana kupitia programu ya uwezeshaji inayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
  Sehemu ya Vijana zaidi ya 100 wa Wilaya ya Chamwino walionufaika na Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba katika kila halmashauri hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga akizungumza wakati wa ziara ya wabunge wa kamati hiyo Wilayani Chamwino Jijini Dodoma, kujionea utekelezaji wa Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba katika kila halmashauri hapa nchini.
  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Holly Green Agric Mhandisi Octavian Lasway akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu namna walivyoweza kutekeleza Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba katika halmashauri ya Wilaya ya Chamwino pamoja na kuwajengea uwezo vijana ili kufanya mpango huo unaotekelezwa na Ofisi ya Waziri mkuu.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga wakiwa ndani ya moja ya vitalu nyumba hivyo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella IKupa akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga akizungumza wakati wa ziara ya wabunge wa kamati hiyo Wilayani Chamwino Dodoma kujionea utekelezaji wa Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba.
  Mmoja wa wanufaika wa programu ya ujenzi wa vitalu nyumba na mafunzo ya kuwawezesha vijana kutumia ujuzi huo kujikwamua kiuchumi akipongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuiwawezesha vijana.
  Sehemu ya miche ya nyanya katika kitalu nyumba kama inavyoonekana katika picha ikiwa tayari kumika katika kitalu nyumba.

  Wanufaika wa programu ya kukuza ujuzi eneo la kilimo cha kisasa kupitia teknolojia ya kitalu nyumba “green house” wameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwawezesha katika masuala ya kilimo hicho na kujikwamua 
  kiuchumi.

  Pongezi hizo wamezitoa hii leo Aprili 06, 2019 wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ilipotembelea kukagua utekelezaji wa Programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma.

  Katika kupongeza jitihada hizo wanufaika wa programu ya kilimo hicho walibainisha mafanikio ikiwemo, kupata ujuzi wa kilimo cha mazao mbalimbali, kujikwamua kiuchumi ikiwa ni sehemu ya kujipatia vipato halali pamoja na kusaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana wanaowezeshwa elimu hiyo.

  Mtaalam kutoka kampuni ya Holly green Bw. Octovian Lasway alieleza kuwa, zaidi ya vijana 100 wamenufaika na elimu ya kilimo cha kitalu nyumba katika Wilaya hiyo na kusaidia kuondokana na changamoto za ukosefu wa ajira nchini.

  “Programu hii imekuja wakati sahihi na imesaidia kundi kubwa la vijana kwa kuzingatia mafanikio yatokanayo na kilimo hiki cha kisasa kinacholeta tija kwa kuwa na mazao bora na kuongeza kipato kwa wananchi,”alisisitiza Octovian.

  Akitoa maelezo kwa wanufaika hao, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde alieleza jitihada za Serikali katika kufikia kundi kubwa la vijana katika kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa masuala ya ukuzaji ujuzi ili kuendelea kuongeza tija na kujikwamua kiuchumi kwa kuzingatia falsafa ya uchumi wa viwanda.

  “Mradi umekusudiwa kutekelezwa kwenye Halmashauri zote 185 Tanzania Bara ambapo awamu ya kwanza itafikiwa mikoa 12 na Halmashauri 83 kwa lengo la kuwezesha vijana kuwa na ujuzi pamoja na stadi za maisha ili kufikia malengo tuliyojiwekea kama Serikali,”alieleza Mavunde

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira wa ofisi hiyo Bw.Ally Msaki alieleza kuwa, mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati ya Serikali katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana na kuboresha kipato kwa watanzania.

  “Mpango huu unalenga kufikia vijana 18800 nchi nzima ambapo kila Halmashauri itafikia vijana 100 na hadi sasa tumefikia halmashauri za mkoa 10, ikiwemo;Dodoma, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kagera,”alieleza Msaki

  Naye Makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Nagma Giga alifurahishwa na utendaji na bidii ya vijana hao na kuwaasa kuendelea kutumia ujuzi huo kwa vijana wengine nchini.

  Naye Naibu Waziri wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa aliwataka vijana kutodharau kilimo kwa kuzingatia mchango wake katika kujikwamua kimaisha.

  “Maisha hayapo kwenye karamu peke yake bali jembe linauwezo wa kuwatoa na kuwakwamua kiuchumi endapo kutakuwa na umakini na kujitoa kwa bidii,”alisisitiza Ikupa.

  Kwa upande wake mwanagenzi Bw.Festo Ezikiel aliendelea kuipongeza serikali kuendelea kuwaamii na kuwajengea uwezo wa kilio cha kisasa cha kutumia kitalu nyumba.

  “Tunaipongeza Serikali kutuamii na kutupa ujuzi kuhusu kilimo hiki nasi tunaahidi kushirikisha vijana wengine waliopo katika maeneo yetu ili kujikwamua kiuchumi,”alisema Ezekiel

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe.Selemani Mzee akifungua kikao kazi cha kupokea rasimu ya sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka jana mjini Masasi
   Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Edwin Mgendera akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu rasimu ya sera mpya ya madaraka kwa umma jana mjini Masasi.
   Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha kupokea maoni ya rasimu ya taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ambao ni Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Weenyeviti wa Halmashauri, wabunge, na viongozi wa asasi za kiraia kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma wakishiriki kikao hicho mjini Masasi jana.


  Na Mathew Kwembe, Masasi 

  Serikali imesema Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ya mwaka 2019 ambayo hivi sasa ipo katika hatua ya rasimu itakapokamilika itakuwa na nguvu ya kisheria na kisera tofauti na ile ya mwaka 1998 ambayo ilikuwa ni sera ambayo haikuwa na nguvu ya kisheria. 

  Hayo yameelezwa jana mjini Masasi, mkoani Mtwara na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Kisheria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Edwin Mgendera mara baada ya kufunguliwa kwa kikao kazi cha kupokea maoni ya wadau juu ya rasimu ya sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka ya mwaka 2019 kwa wananchi wa mikoa ya kusini ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. 

  Bwana Mgendera amesema mafanikio na changamoto zilizotokana na utekelezaji wa Sera ya Ugatuaji ya mwaka 1998 imeiwezesha serikali kuja na Sera ya jumla ya ugatuaji kitaifa ambayo itakuwa na nguvu za kisheria na namna bora ya kutekeleza na kutoa huduma kwa ufanisi kwa wananchi toka juu serikalini hadi ngazi za chini za Kitongoji na Mtaa kule kwenye Halmashauri. 

  Amesema mwelekeo wa serikali kwa sasa ni huo wa kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ambayo itawekewa nguvu za kisheria na kisera ili kurahisisha suala la utoaji huduma kwa wananchi moja kwa moja kutoka serikali kuu hadi ngazi za kitongoji na mtaa. 

  Mkurugenzi huyo wa huduma za Sheria amefafanua kuwa Msingi wa Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka, 1977 Ibara ya 145 na 146 ambazo zimetoa uhalali wa kuanzishwa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na kubainisha madhumuni ya kuanzishwa kwa Mamlaka hizo yakiwemo kuzipa Mamlaka za Serikali za Mitaa madaraka ya kujiamulia mambo yao ya Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi katika maeneo yao kwa uhuru. 

  “Aidha Sheria Na. 7 ya Halmashauri za Wilaya ya mwaka 1982 (sura 287) na Sheria Na. 8 ya Halmashauri za Miji ya mwaka 1982 (sura 288) zinazipa mamlaka hizo majukumu ya kutoa huduma kwa jamii katika maeneo husika,” amefafanua bwana Mgendera. 

  Pia Mkurugenzi huyo ameitaja sheria ya Tawala za Mikoa ya Mwaka 1997 ambayo inazipa Tawala za Mikoa jukumu la kuratibu maendeleo katika Mikoa yao ikiwemo kuzisimamia na kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa huduma bora kwa usawa kwa jamii. 

  Ni kutokana na msingi huo wa sheria bwana Mgendera amesema kuwa masuala ya Ugatuaji wa Madaraka yanafanyika na yataeendelea kufanyika katika hatua mbili muhimu ambazo ni kugatua Madaraka kutoka Serikali Kuu kwenda Ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji) na pili kugatua Madaraka kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenda ngazi za Msingi yaani Kata, Vijiji, Mitaa na Vitongoji. 

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Kisekta kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Juma Idd ambaye pia ndiye Mratibu wa kikao kazi cha kupokea maoni ya wadau juu ya rasimu ya sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka ya mwaka 2019 ameeleza kuwa hivi sasa timu yake ipo katika mikoa hiyo ya kusini baada ya zoezi hilo kukamilika katika mikoa ya nyanda za juu kusini ya Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa. 

  Ameongeza kuwa baada ya kukamilika katika mikoa hiyo, timu ya kupokea maoni itaelekea katika kanda ya mashariki ambapo Mikoa ya Morogoro, Dar es salaam, Pwani na Dodoma itashirikishwa, na baadaye zoezi hilo kuhamia mikoa ya kaskazini, magharibi na kanda ya ziwa. 

  “Lengo letu ni kuhakikisha kuwa wadau wetu muhimu wanapata fursa ya kutoa maoni yao juu ya nini wangependa kiwemo katika sera yetu hii mpya ya Ugatuaji wa Madaraka,” amesema bwana Idd. 

  Awali akifungua kikao kazi cha kupokea maoni Mkuu wa Wilaya ya Masasi bwana Selemani Mzee ameeleza umuhimu kikao hicho ambapo amesema kuwa toka mwaka 1998 Serikali kupitia Rasimu ya maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) imekuwa ikitekeleza dhana ya ugatuaji wa Madaraka ili kufikisha na kuharakisha utoaji wa huduma za Kijami,Kiutawala na Kiuchumi kwa wananchi kwa haraka na kwa usawa. 

  Amesema kuwa kupitia dhana ya ugatuaji wa madaraka, wananchi wanapata fursa ya kutosha ya kushiriki na kushirikishwa katika shughuli na masuala yote yanayohusu maendeleo yao na ustawi wa maisha yao. 

  Miongoni mwa wanaoshiriki kikao hicho ni pamoja na waheshimiwa Wabunge wanaotoka Mikoa ya kusini ambapo Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mheshimiwa Hassan Elias Masala amesema kuwa kikao hicho ni muhimu kwao kama wawakilishi wa wananchi kwani utekelezaji wa ahadi nyingi za serikali kupitia chama kilichopo madarakani hivi sasa unategemea sana utekelezaji wa sera hii ya ugatuaji wa madaraka. 

  Naye Bi Miriam Mwaibula mshiriki kutoka asasi isiyo ya kiserikali ya TWAWEZA amesema kuwa maoni yao ni muhimu kwani yatawezesha serikali kupata sera madhubuti na ambayo itakubalika na jamii yote na hivyo kurahisisha utekelezaji wake. 

  Kikao hicho cha siku mbili kimewahusisha Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi kutoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Viongozi wa dini na Washiriki kutoka Asasi za Kiraia kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma.

  0 0


  Rais mpya wa chama cha wanasheria nchini TLS Dkt. Rugemeleza Nshala
  Rais TLS aliyemaliza muda wake Fatma Karume akitoa neno la shukrani leo Jjini Arusha
  Dkt. Rugemeleza Nshala kabla ya matokeo ya uchaguzi wa kuwa Rais wa TLS
  Dkt.Rugememelela Nshala mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha urais wa TLS leo Jijini Arusha katika ukumbi wa AICC.
  NA:Vero Ignatus , Arusha

  Wanachama wa chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamewataka viongozi wapya watakao kiongoza chama hicho kutoa fursa sawa kwa mawakili walemavu ili kuweza kuhudumia vyema jamii Katika masuala ya kisheria na kuondokana na fikra potofu dhidi ya Watu walemavu.

  Wakizungumza Mara baada ya kupiga kura baadhi ya mawakili ambao ni wanachama wa chama hicho wamesema ni vyema kwa viongozi kushirikiana na mawakili walemavu ili kutoa hamasa Katika jamii.

  Elibariki Maeda ni Mwenyekiti wa chama chama mawakili wa kujitegemea Kanda ya Arusha amesema Ulemavu sio Sababu ya kushindwa kutekeleza majukumu yao Huku Rais wa chama hicho anaemaliza muda wake Fatma Karume akatoa neno kwa viongozi wajao.

  Kwa upande wake Rais aliemaliza muda wake Fatma Karume amesema kuchaguliwa kwa Dkt Rugemeleza Nshala kuongoza chama hicho anaamini chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) iko Katika mikono salama.

  Katika hatua nyengine bi Fatma Karume ametumia fursa hiyo kuwashukuru wanachama waliompa dhamana ya kuongoza kwa kipindi alicho kuwa madarakani hivyo ni wakati muafaka kwa wanasheria kumpa ushirikiano chanya Rais Mpya wa TLS.

  Matokeo ya uchaguzi huo yametoka kutangazwa jioni ambao Katika Nafasi ya wagombea urais ilikuwa ikigombewa na Godfrey wasong, Gaspar Nicodemas,Godwin Simba,Rugemeleza Nshala na John seka ambapo Dkt Rugemeleza Nshala ameobuka kidedea.


  MATOKEO YA RAIS 2019/2020 (TLS)

  Jumala ya Kura zilizo poigwa na wanachama wa TLS Ni 1217.

  1-Dkt Rugemeleza Nshala kura 647.
  2-Godwin Simba kura 354
  3-Godfrey Wasonga kura 123
  4-58 Gaspar Nicodemas kura 58
  5-John Seka kura 29

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika ibada ya dominika ya 5 ya Kwaresma katika Parokia ya Mt. Mathias Mulumba Jimbo Kuu Katoliki la Songea mkoani Ruvuma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika ibada ya dominika ya 5 ya Kwaresma katika Parokia ya Mt. Mathias Mulumba Jimbo Kuu Katoliki la Songea mkoani Ruvuma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Mathias Mulumba Jimbo Kuu Katoliki la Songea mkoani Ruvuma mara baada ya kuwachangia shilingi milioni tano  kwa ajili ya ukarabati wa Kanisa hilo. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na Masista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Mathias Mulumba Jimbo Kuu Katoliki la Songea mkoani Ruvuma mara baada ya Ibada ya dominika ya 5 ya Kwaresma. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono waumini wa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Mathias Mulumba Kalemba Jimbo Kuu Katoliki la Songea mkoani Ruvuma mara baada ya ibada.PICHA NA IKULU  0 0

  Dar es Salaam. Jumla ya klabu 10 zimethibitisha kushindana katika mashindano ya klabu bingwa ya mchezo wa kuogelea yaliyopangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Upanga jijini Dar es Salaam.

  Mashindano hayo yamepangwa kufanyika Aprili 13 na 14 na yamedhaminiwa na kampuni za Asas, Samsung, DTB Bank, Snow Cream, Knight Support na kituo cha utangazaji cha Clouds FM.

  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Hadija Shebe amezitaja klabu hiyo kuwa ni Bluefins, Champion Rise, Mis Piranhas, klabu ya kuogelea ya Mwanza (MSC), FK Blue na Wahoo ya Zanzibar.

  Hadija amezitaja klabu nyingine kuwa ni ISM-Moshi, ISM-Arusha,FK Blue Marlins, Talis-IST na mabingwa watetezi, Dar es Salaam Swim Club (DSC).

  Alisema kuwa mashindano hayo yamepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi siku ya Jumamosi na waogeleaji watashindana katika staili tano ambazo ni Freestyle, Breaststroke, Butterfly, Backstroke na Individual Medley.

  Kwa mujibu wa Hadija, waogeleaji hao pia watashindana katika relay katika mashindano ambayo yamepitishwa na Shirikisho la Mchezo wa kuogelea Duniani (Fina) kuwa ya kutafuta alama za kufuzu mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika nchini Korea mwezi Julai.

  “Tunatarajia kuona ushindania mkali kwa waogeleaji wetu ili kutafuta nafasi ya kufuzu mashindano ya dunia. Waogeleaji wengi wapo katika maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mashindano hayo, bado tunahitaji wadhamini wa mashindano haya,” alisema Hadija.

  Kwa mujibu wa Hadija, kutakuwa na jumla ya vipengele vya mashindano 108 na kila klabu imetakiwa kuwakilishwa na waogeleaji wawili katika kila kipengele cha mashindano ambavyo pia vimepangwa kutokana na umri. “Zaidi ya waogeleaji 200 watashiriki katika mashindano haya makubwa ya Tanzania. Tunaomba wadau wajitokeze kusaidia na kuwapa hamasa waogeleaji wetu ambao kwa sasa wamepata mafanikio makubwa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,” alisema.
   waogealeaji waki-dive katika mashindano ya kuogelea
   waogeleaji wakichuana
    Natalia Ladha akipiga mbizi

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC  afungua mkutano wa mafunzo ya usalama katika uendeshaji wa shughuli za reli Kwa wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa bandari jijini Dar es Salaam.

   Lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha wafanyakazi wa reli kuimalisha ulinzi Na usalama wa binadamu Na miundombinu ya reli Kwa kutoa elimu ya usalama katika shughuli za uendeshaji wa reli Kwa madereva, wakaguzi wa reli, wahandisi mawasiliano, wahandisi mitambo, walinzi Na wabadilisha njia za reli.

  Aidha, Mkurugenzi Mkuu Ndugu Kadogosa amesisitiza usalama wa reli unagusa maisha ya watu na kila mmoja ndani ya shirika Anawajibu wa kusimamia sheria Na kanuni zilizowekwa katika uendeshaji wa treni ili kuokoa maisha ya watanzania Na kutunza miundombinu ya reli,Aliendelea kusisitiza Mkurugenzi.

  " tunaendelea Na ukarabati wa reli ya zamani kutoka Dar es Salaam Mpaka Isaka, tunategemea ndani ya mwaka mmoja ujao tutakuwa Na reli nzuri sana maana yake tusipokuwa Na umakini wa usalama tunaweza kusababisha ajari zikaongezeka Na Uharibifu kuwa mkubwa,"

  Kwa upande wake kaimu mkuu wa kitengo cha usalama wa reli TRC Mhandisi Adolphina Ndyetabula amefafanua kuwepo Kwa elimu ya usalama ambayo hutolewa wa Shirika na wakazi wanaoishi maeneo ya reli ili kuzingatia swala Zima la usalama wao na miundombinu ya reli.
  Mkurugenzi Mkuu shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa TRC kipindi cha ufunguzi wa mafunzo ya usalama katika uendeshaji wa shuguli za Reli katika ukumbi wa bandari hivi karibuni Aprili.

  0 0


  Mkurugenzi wa bank ya CRDB tawi la Iringa Kissa Samweli akizungumza na wateja wa CRDB jana wakati wa warsha ya siku moja ya wanahisa juu ya kuchangamkia kutafuta fursa za kufanya kuunga mkono jitihada za serikali juu ya sera ya Tanzania ya viwanda
  Mkurugenzi wa bank ya CRDB tawi la Iringa Kissa Samweli (kushoto) akimsikiliza mteja wa CRDB mfanyabiashara George Kaundama ambae ni mmoja kati ya wateja wakongwe ambao wanamiliki hisa katika bank hiyo jana wakati wa warsha ya siku moja ya wanahisa juu ya kuchangamkia kutafuta fursa za kufanya kuunga mkono jitihada za serikali juu ya sera ya Tanzania ya viwanda


  washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mafunzo hayo

  …………………………

  NA Francis Godwin, Iringa

  Benk ya CRDB imetoa rai makundi mbali mbali kama ya wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa kuchangamkia fursa ya mikopo ili kujikita kutafuta fursa ya kuendeleza ama kuboresha viwanda vidogo vidogo na viwanda vikubwa kama utekelezaji wa sera ya taifa ya Tanzania ya viwanda .

  Akitoa rai hiyo wakati wa semina ya siku moja kwa umma iliyotolewa kwa wanahisa wa CRDB tawi la Irina jana mkurugenzi wa CRDB tawi la Irina Kissa Samwel alisema kuwa bank hiyo imekuwa mbele kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya viwanda kwa kutoa mikopo kwa makundi mbali mbali kwa ajili ya kuyawezesha kuboresha shughuli zao.

  Mkurugenzi huyo alisema kuwa aina ya mikopo ambayo wamekuwa wakiitoa ni ile ya chini kabisa ya vikundi kuanzia kiasi cha shilingi 300,000 na kuendelea pia mikopo ya wafanyabiashara wa kati na wakubwa pamoja na mikopo binafsi .

  Alisema mikopo ya uendeshaji wa biashara ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya uendeshaji biashara ya kila siku kama kununua malighafi katika uzalishaji viwandani ,kununua vipuli vinavyohitajika katika matengenezo ya mara kwa mara ya mitambo ikiwa ni pamoja na kununua vitu vinavyohitajika katika usindikaji kiwandani .

  Aidha mikopo hiyo hutolewa kwa ajili ya mahitaji ya gharama za uendeshaji ya kila siku kama kulipa mishahara ,gharama za maji ,umeme ,usambazaji wa bidhaa na gharama za riba ya mikopo ,mahesabu na ukaguzi na kodi na kuwa mkopo huo hutegemea mahitaji ya biashara kwa kuzingatia mtiririko wa mahesabu .

  Alisema kuwa aina ya wateja ni watu binafsi ,biashara za ubia,makampuni ,biashara muunganiko ,mashirika ya umma ,vikundi na vyama vya ushirika

  Makundi mengine ni azaki ,taasisi zisizo za serikali ,serikali kuu ,wakala wa serikali na wizara kuwa lazima wakopaji wawe wanaishi aum wamesajiliwa nchini Tanzania na si vinginevyo.

  Aidha alisema wakopaji wasiokubalika ni watoto chini ya miaka 18 ,wale waliotangazwa kufilisika ,wasio na akili timamu ,kampuni zilizofilisika au ziko katika mchakato wa kutangazwa kufilisika hao pia hawatahusika na mikopo hiyo .

  Kwani alisema lengo la CRDB kuona wenye sifa ya kunufaika na mikopo hiyo wananufaika na kuendelea kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda kwa kuwapa mikopo wote wenye sifa stahiki katika kutekeleza sera hiyo na wao kujikwamua kiuchumi.

  “Mitaji iko mingi sana CRDB sera nzuri ya serikali ipo hamna sababu ya kusumbuka pia wateja wakubwa tunawakaribisha kuna mikopo mikubwa kwao kwani hakuna sababu ya kundi lolote kulalamikia mitaji kwetu mitaji iko wazi hivyo tunawakaribisha wote ili kuunga mkono juhudi za serikali na sisi wenyewe kuwa na maisha bora “ alisema mkurugenzi huyo

  Mwanahisa Georege Kaundama ambae ni mmoja kati ya wafanyabiashara mkoani Iringa alipongeza CRDB kwa kuandaa semina hiyo kwa wanahisa wake na kuwa elimu iliyotolewa imewahamasisha wengi kuona sababu ya kuboresha biashara zao zaidi kwa kupitia bank hiyo .

  Alisema kuwa kwa upande wake hajutii kuwa mmoja kati ya wanahisa kwani bank hiyo hataka kama uchumi umeyumba kiasi gani wamekuwa wakitoa gawio kwa wanahisa wake na hivyo silaha pekee ni kuendelea kuwepo badala ya kukimbilia bank mpya zinazoanzishwa kwani tofauti ya CRDB na hizo mpya ni ukongwe wake na mwanga ambao wanauona mbele si mwanga hafifu ni mwanga unaong’aa.

  “ Imekuwa ni tabia ya kila mwanadamu anapoona kitu kipya kimekuja ama kuna usemi usemao kipya kinyemi ni lazima aende akaguse kuona ila tofauti ya CRDB toka tulipo gusa wakati huo hadi leo wao wapo imara hawayumbi wanazidi kusonga mbele “ alisema Kaundama.

  Meneja Msimamizi usalama wa bank hiyo Theophel Akoro alisema kuwa sera ya viwanda iko bayana na kuwa watanzania waliowengi bado hawajajua kuwa ushiriki wao katika shughuli mbali mbali za uzalishaji iko kwenye sera ya Taifa ya kuendelea Tanzania ya viwanda .

  Hata hivyo alisema kwa kuwa wengi wameshindwa kutambua vipaumbele katika sekta hiyo ambavyo wangeweza kuchukua hatua ya kuvifanyia kazi vipaumbwele hivyo ili kunufaika na sera ya Taifa ya viwanda .

  Aidha alipongeza serikali ya mkoa wa Iringa kwa kutambua fursa ya uwekezaji katika uboreshaji wa miundo mbinu ya uwanja wa ndege wa Nduli pamoja na utalii kwani maeneo hayo ni sehemu kubwa zaidi yaukuzaji wa sekta ya viwanda nchini na kuwataka wananchi kila mmoja kwa uwezo wake kutafuta fursa anayoweza kunufaika nayo kuelekea Tanzania ya viwanda kama ni mkulima kusindika na kulima kisasa kama maana kilimo biashara ili kuwa mmoja wao katika endelezaji viwanda nchini.

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akivalishwa medali mara baada ya kumaliza mbio KM 21 za Tanga City Marathon zilizomalizikia Uwanja wa Mkwakwani. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akifurahia baada ya kuvalishwa medali mara alipomaliza mbio za Tanga City Marathon 2019 iliyofanyika na kumalizikia Uwanja wa Mkwakwani.  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akimaliza Mbio za KM 21 katika Uwanja wa Mkwakwani-Tanga. 
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akihojiwa na mwanahabari mara baada ya kumaliza mbio KM 21 za Tanga City Marathon zilizomalizikia Uwanja wa Mkwakwani. 
  Wakimbiaji wakionyesha umahili wao.


  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Tanga. 

  KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe amesema mkoa huo utaendelea kutumia mashindano ya riadha ya Tanga City Marathon kuweza kutangaza fursa za uwekezaji na utalii zilizopo mkoani Tanga. 

  Gondwe ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Handeni ameyasema hayo leo wakati akifunga mashindano ya Tanga City Marathon yaliyofanyika jijini Tanga ambapo msimu huu yameshirikisha washiriki 1,300 kutoka mikoa mbalimbali na nje ya nchi. 

  Amesema watafanya hivyo kutokana na kwamba mkoa huo kuwa na maeneo makubwa ya uwekezaji yaliyopo mkoani Tanga ili kuweza kuwa vutia kuwekeza kutokana na fursa kubwa zilizopo. “Ndugu zangu tutaendelea kuitumia Tanga City marathon kuweza kutangaza mkoa wa Tanga... Lakini pia kutangaza utalii hata uwekezaji mkoa wa Tanga kwani tuna fursa nyingi sana ambazo mnaweza kuzichangamkia kwenye kufanya uwekezaji “ Amesema. 

  Hata hivyo aliwapongeza washiriki ambao wamefanya vizuri kwenye mashindano hayo na kuwataka kuendelea kujiweka imara kwa kushiriki kwenye mazoezi mara kwa mara ili kuweza kujiandaa na yale yajayo. “Mashindano hayo ya Tanga City Marathon yameufanya mkoa wetu uweze kuendelea kutangazika lakini niwaambie waandaaji wafungue mapema dirisha la usajili msimu ujao “Alisema.

  Amesema kwani iwapo watafungua mapema dirisha la usajili wanaweza kupata wadhamini ambao wataweza kuongeza chachu kwenye mashindano hayo msimu ujao. “Pia niwaambie kwamba Mkuu wetu wa Mkoa Martine Shigella anatambua anatambua sana mchango wenu mlijitokeza kushiriki mashindano hayo na sio kwenye michezo pekee anathamini Tanga City Marathon lakini kubwa amenielezea amefurahi kusikia vijana wa shule zetu wameshiriki nao Tanga City Marathon”Amesema.

   Hata hivyo pia aliwaagiza wakuu wa shule za Sekondari, Msingi na Vyuo vikuu kuhakikisha wanajiandaa kikamilifu ili kuweza kujipanga kwa ajili ya mashindano yajayo ili nao waweze kupeleka washiriki ambao watashindano kwenye mbio za kilomita tano.

  0 0


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea hotuba kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Benzi wakati walipofanya ziara ya kukagua jengo la mama na mtoto (Maternity Block). Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na nyuma viongozi wengine wa Wizara na Hospitali.
  Jengo jipya la Mama na Mtoto (Maternity Block) lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kushoto)akiongea jambo wakati alipofanya ziara ya kukagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General). Kulia ni katibu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na mama aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la Mama na Mtoto katika Hospitali hiyo.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula wakiangalia kitu katika wodi ya akinamama waliojifungua wakati walipofanya ziara ya ukaguzi wa jengo jipya la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.


  ……………………..
  Na WAMJW-Dodoma

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameahidi kutoa Tsh. Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

  Waziri Ummy ametoa ahadi hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la mama na mtoto (Maternity Block) katika Hospitali hiyo ili kujionea hali ya utoaji huduma kwa akina mama wajawazito na watoto.

  “Ninaahidi kutoa Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la OPD ya kisasa yenye uwezo wa kupokea wagonjwa wengi zaidi tofauti na OPD iliyopo sasa”. Amesema Waziri Ummy.

  Waziri Ummy ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kurekebisha na kufanya maboresho katika baadhi ya maeneo yaliyoonekana kuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuyapa majina majengo yote ya Hospitali hiyo ili kuepusha usumbufu kwa wagonjwa pindi wanapotaka kupata huduma katika majengo tofauti.

  Aidha, Waziri Ummy ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kujenga ghorofa ambayo itakua maalum kwa ajili ya matibabu ya watoto pekee yenye uwezo wa kulaza watoto wengi sambamba na chumba cha uangalizi maalum kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda (Intensive Neonatal Care Unit) na wale wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amesema Wizara itaendelea kushirikiana na uongozi wa Hospitali hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali zilizoonekana katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja kuongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kukidhi mahitaji.
  a
  “Naomba niwaahidi tutaongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kuziba mapungufu yanayoonekana, lengo likiwa ni kuboresha huduma katika Hospitali hii inayotegemewa na watu wengi wa Dodoma na kutoka maeneo ya jirani”. Amesema Dkt. Chaula.

  Hata hivyo Dkt. Chaula amewataka watumishi wa Hospitali hiyo kushirikiana ili waweze kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wanaokwenda hospitalini hapo.

  Katika ziara hiyo iliyoenda sambamba na siku ya Afya Duniani imejumuisha viongozi mbalimbali wa Wizara akiwemo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Edward Mbaga wameondoka na azimio la kufanya maboresho katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa jengo maalum la kupokea wageni mbalimbali wanaokuja Dodoma.

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka Shada la Maua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika kwa kisomo cha Hitma iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
  MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la Mareheme Mzee Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika dua ya kumuombea iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar leo
  MWAKILISHI wa Familia ya Marehemun Mzee Abeid Amani Karume, Balozi Ali Karume baada ya kumalizika hafla ya kisomo cha Hitma na Dua kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibaer leo.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, kuhudhuria hafla ya Hitma ya Dua ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhuria Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
  RAIS Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhguria Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
  RAIS Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Abeid Karume akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja akihudhuria hafla ya Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Leo
  KATIBU Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ali akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud Mohammed alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhuria hafla ya Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Viongozi na Wananchi katika Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,. Balozi Seif Ali Iddi na Rasi Mstaaf wa Tanzania Mzee Aliu Hassan Mwinyi na kulia Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali,Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ameni Karume na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dr. Abdallah Juma Sadala
  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika Hitma na Dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, kushoto Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma na kulia Mama Shadya Karume na Mama Fatma Karume, wakiitiikia dua wakati wa hafla hiyo ya Hitma ya Mzee Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika leo Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
  WANANCHI kutoka sehemu mbalimbali ya Mji wa Zanzibar wakihudhuria Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika leo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar
  WANAINCHI wakishiriki katika Kisoma cha Hitma ba Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika leo Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ya kuhitimisha Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ,ikisomwa na Sheikh Jaffar Abdallah Abdald, katika hafla hiyo iliofanyika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Salif Omar Kabi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seiff Ali Iddi na Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi na kulia Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali nac Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dkt Amani Abeid Karume

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aakizungumza na wananchi wa Kata ya Ilolangulu Wilayani Mbogwe, Mkoani Geita (hawapo pichani) baada ya kusikiliza malalamiko yao kuhusu polisi kuchukua rushwa. Lugola alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilayani humo (OC CID), pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa na wananchi hao.
  Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Ilolangulu Wilayani Mbogwe wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani) alipokuwa anazungumza nao baada ya kusikiliza malalamiko yao kuhusu polisi kuchukua rushwa. Lugola alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilayani humo (OC CID), pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa na wananchi hao.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoani Geita, baada ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Ilolangulu wilayani humo, akiskiliza malalamiko yao kuhusu polisi kuchukua rushwa. Lugola alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilayani humo (OC CID), pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa na wananchi hao.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani na Nchi


  Na Mwandishi Wetu, Geita.

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mbogwe (OC CID) Mkoani Geita, pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa kuomba na kupokea rushwa.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata za Ilolangulu na Busabaga wilayani humo, Lugola alisema Polisi hao ambao waliomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni nne kutoka kwa wananchi wa Kata hizo

  ambao walikuwa wanataka kuwaombea dhamana ndugu zao, ndipo polisi hao wakaomba fedha kiasi hicho ili watolewe mahabusu ya Polisi katika Kituo cha Polisi Mbogwe.Maafisa hao wa Polisi ambao wanadaiwa kupokea rushwa kutoka kwa wananchi hao ni OC CID wa Wilaya hiyo, Luitiko Kibanda na Mkaguzi wa Polisi aitwaye kwa jina la Kessy ambao wananchi hao pamoja na Mbunge wao
  walisema waliwakabidhi fedha kiasi hicho.

  ”Wananchi walipitisha mchango kila kaya ili kuwanusuru wenzao na viongozi wao haikutosha wakamuomba Mbunge wao akawachangia shilingi laki tano pia wakachukua na hela yao iliyokuwa ni ya kujengea zahanati wakawapelekea polisi, bila hata aibu polisi hawa wakachukua fedha hizo, bila kujali hali za kiuchumi walizonazo wananchi hao”alisema Lugola.

  Lugola alisema licha ya Kata hizo kukithiri vitendo vya wizi na ubakaji na Polisi kufanya wajibu wao kuwakamata watuhumiwa mbalimbali, lakini ni kosa kuwaonea wananchi kwa kuwaomba rushwa kupitia kisingizio cha utoaji wa dhamana huku sheria ikieleza kwa makosa yanayodhaminika dhamana itolewe kwa mujibu wa sheria na siyo kuwanyanyasa wananchi.

  Aidha, Waziri Lugola alitoa onyo kwa Polisi nchini ambao wanawafanya wananchi mtaji kwa kuwabambikiza kesi kisha kuwaomba pesa, kuacha tabia hiyo mara moja na endapo wakibainika hatawavumilia, hatawaonea huruma
  hivyo sheria itafuata mkondo wake.

  Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Ikobe, Wilayani humo, Costantine Kwezi, alimuomba Waziri kuwasaidia kukamilisha kituo cha polisi katika Kata yake na pia kuongeza idadi ya askari kituoni hapo, kwasababu kituo hicho kina askari mmoja ambaye anazidiwa na majukumu.

  Baadhi ya kina mama katika mkutano huo, nao walimuomba Waziri huyo kuwasaidia waume zao waliokamatwa kwa kosa la kusingiziwa kuwa ni majambazi kuachiwa huru, kutokana na kukosa hela ya kuhudumia familia na wao wameachwa bila kazi na watoto wadogo.

  0 0


  Na Ahmed Mahmoud,Arusha.

  Mamia ya Wanyarandwa wamekusanyika na kuandamana katika viunga vya jiji la Arusha ikiwa ni ishara ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 tangu kutokea kwa mapigano na mauaji ya Kikabila Nchini na kusababisha mauaji ya maelfu ya Wanyarandwa.

  Maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Arusha yanalenga kuhamasisha umoja na amani miongoni mwa wanyarandwa kuungana kama taifa bila kujali tofauti za kikabila .

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanyarandwa wanaoishi katika Mataifa mbalimbali duniani Murenzi Daniel amesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwakumbusha kudumisha amani na umoja kama nguzo muhimu ambayo kwasasa hawako tayari kuipoteza na wanawataka Wanyarandwa duniani kote kuungana

  Tedy Shungushu ni Mnyarandwa anayeishi jijini Arusha amesema kuwa kumbukumbu hiyo ni ya muhimu kama taifa kujitafakari na kuona namna ambavyo wanawakumbuka watu waliowapoteza katika mauaji hayo na kuwaenzi kila mwaka.

  Kwa upande wao Watanzania walioshiriki katika maadhimisho hayo Maurin Njobi na Omega Urio wamesema kuwa yanawakumbusha kama Watanzania kudumisha amani na upendo na mshikamano kama taifa ili kuondoa uwezekano wa matukio kama hayo kutokea nchini

  Zaidi ya watu Laki nane wanatajwa kupoteza maisha kwenye mauaji hayo ya Rwanda nchi ambayo kwa sasa inaongozwa na Rais wake Paul Kagame.

   


  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mwenye Tai nyekundu akiwa na viongozi wa Mataifa mbalimbali Aprili 7/2019 wakitoa heshima katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akibadilishana Mawazo na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo walipo kutana leo Aprili 7/2019 katika Mji wa Kigali wakati waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais Dkt Magufuli katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994 nchni Rwanda.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Mkapa walipo kutana leo Aprili 7/2019 katika Mji wa Kigali wakati waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais Dkt John Magufuli katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994 nchini Rwanda.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mwenyeji wake Waziri wa mambo ya Nje wa Rwanda Balozi Richard Sezibera aliyempokea  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kigali alipo wasili leo Aprili 7/2019 alipo fika kumuwakilisha  Rais Dr John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994 Kkulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda Balozi Ernest Mangu.

  PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Mbinga mjini mpaka Mbamba Bay km 67, sherehe zilizofanyika Mbinga mkoani Ruvuma. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Alex Mubiru akishuhudia
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akikata utepe pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Alex Mubiru wa pili kutoka kushoto , Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Godfrey Zambi watatu kutoka kulia, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga wapili kutoka kulia, Mwalikishi wa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Chrisianus Ako wa kwanza kulia.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Alex Mubiru wa kwanza kulia aliyekaa wakiwa katika picha ya pamoja na wakandarasi wa ujenzi wa barabara ya Mbinga mjini mpaka Mbamba Bay km 67, wafanyakazi, wasimamizi pamoja na viongozi wengine.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa kwa wafuraha na wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Mbinga mjini kabla ya kuwahutubia.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi(Albinism ) wanaosoma Shule ya St. William iliyopo Mbinga mkoani Ruvuma. Rais Dkt. Magufuli amewachangia watoto hao kiasi cha Shilingi milioni tatu.
   

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi pamoja na Wanafunzi wa Shule mbalimbali za eneo la Kigonsera (hawaonekani pichani) Mbinga mkoani Ruvuma.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Liganga wakati akiwa njiani kuelekea Mbinga mkoani Ruvuma. PICHA NA IKULU


  0 0

  Na Ripota Wetu, Musoma

  SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeamua kuendesha ukaguzi wa kushutukiza katika masoko yaliyopo  wilayani Musoma Mjini, mkoani Mara ikiwa ni mwenedelezo wa mkakati wa shirika hilo kuondoa bidhaa ambazo hazina ubora kwenye soko nchini.

  Ukaguzi huo umeendeshwa na maofisa wa TBS ambapo ukaguzi huo umekwenda sambamba na kuondoa kwenye soko nguo za ndani za mitumba kutokana na matumizi yake kupigwa marufuku nchini kwa kuwa zina madhara kiafya kwa watumiaji.

  Mbali na hatua hiyo, pia sampuli mbalimbali za bidhaa zimechukuliwa katika masoko hayo kwa lengo la kwenda kuzipimwa kwenye maabara za shirika hilo ili kujiridhisha kama zinakidhi  viwango, huku vilainishi vya magari visivyokuwa na ubora vikiondolewa kwenye soko, kwenye baadhi ya maeneo ya kanda ya ziwa ambako operesheni hiyo imefanyika.

  Akizungumza wakati wa operesheni hiyo Mkaguzi wa TBS, Baraka Bajije, amesema kuwa katika ukaguzi huo unaendelea Kanda ya Ziwa kabla ya Musoma Mjini umefanyika pia masoko maeneo ya Mwanza Mjini, Sengerema, Magu, Bunda na sasa Musoma  Mjini ambapo wamefanikiwa kukamata shehena ya nguo za ndani za mitumba pamoja na taulo zinazokadiriwa kuwa na thamani ya Sh. milioni 10.

  Amesema kuwa Sheria ya Viwango Namba 2 ya mwaka 2009 inazuia matumizi ya nguo za ndani za mitumba pamoja na taulo, lakini bado watu wasiowaaminifu wamekuwa wakiziingiza  kwenye soko la Tanzania kupitia njia za panya.

  Pia Bajije amesema bidhaa hizo haziruhusiwi kabisa kuwepo sokoni kutokana na madhara yake kwa watumiaji ikiwemo kusababisha magonjwa sugu ya fangasi, kansa ya ngozi na magonjwa mengine.

  Ametoa mwito kwa Watanzania kuacha kabisa kutumia nguo hizo kutokana na madhara yake kuwa makubwa.Wakizungumza wakati wa operesheni hiyo baadhi ya wananchi wameunga mkono hatua zinazochukuliwa na TBS kuondoa sokoni nguo hizo. "Nguo hizi za ndani za mtumba watu

  tulikuwa tunazipenda kwa sababu uimara na unafuu wa bei, lakini baada ya  kuelimishwa madhara yake na TBS, lazima na sisi Watanzania tubadilike," amesema Joyce Magesa.

  "Leo hii watu wanapenda kuzinunua kwa kuvutiwa na bei ya Sh. 1,000 kwa sidiria, lakini ukipata kansa ya matiti gharama za kujitibia hazilingani kiasi hicho cha fedha.Nikiri wanawake walio wengi ndio watumiaji wa kubwa ikilinganishwa na  wanaume,lakini elimu tunayoendelea kuipata kutoka TBS itatusaidia kuachana na uvaaji wa nguo za ndani ambazo ni za mtumba,"amesema.

  Imefafanuliwa nguo za ndani zilizopigwa marufuku ni pamoja na soksi, taiti, sidiria, taulo na nyingine. Wakati huo huo  TBS inaendesha operesheni ya ukaguzi wa bidhaa sokoni ili kubaini bidhaa zisizo na viwango zilizopo humo. Kwa sasa maofisa wa shirika hilo wapo mikoa ya kanda ya ziwa wakiendesha uendesha msako huo wa bidhaa hafifu sokoni.
   Sehemu ya shehena ya nguo za mitumba zikiwa zimekamatwa kwenye masoko mbalimbali ya Musoma Mjini baada ya maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) kufanya msako wa kushtukiza
   Taulo ambazo zimeshutumika maarufu taulo za mtumba zikiwa zimeshikiliwa na maofisa wa TBS baada ya kuzikamata katika masoko ya wilayani Musoma Mjini baada ya kufanya msako mkali

   
   Nguo za mitumba zikipakiwa kwenye gari baada ya kukamatwa na maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS)waliopo mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo wanaendelea na msako wa kushtukiza katika masoko kwa lengo la kuondoa bidjaa zisizokuwa na ubora pamoja na nguo za mitumba

  0 0

  0 0

  WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umeweka mkakati kuhakikisha inatoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani na Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam kwani wanaamini iwapo wanafunzi hao watakuwa na uelewa mzuri kuhusu misitu iliyopo watakuwa mabalozi wazuri na walinzi wa misitu nchini.

   Akizungumza na wanafunzi wa shule hizo kwa nyakati tofauti, Meneja Masoko wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Mariam Kobero amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kuhakikisha misitu yetu nchini inalindwa na kudhibiti uharibifu wa mazingira na katika jitihada hizo hizo TFS nayo imekuwa na mikakati ya kufanikisha misitu nchini inatunzwa na kulindwa wakati wote.

  Kobero amesema kwa kutambua umuhimu na faida za misitu TFS imeona ni vema ikakutana na wanafunzi wa shule hizo kwa lengo la kutoa elimu ambayo itajikita zaidi kuelezea faida za misitu na umuhimu wa kuilinda kwani ili misitu iwe salama ni jukumu la kila Mtanzania kuwa mlinzi ikiwa pamoja na kutokuwa tayari kuona msitu unaharibiwa halafu anakaa kimya.

  "Wakala wa Huduma za Misitu hatujalala, tunatambua pamoja na mambo mengine ni wajibu wetu kukutana na makundi ya watu mbalimbali ili kutoa elimu inayohusu umuhimu wa misitu kuilinda na kutokata miti hovyo.Hivyo leo hii tumeamua kuzungumza na wanafunzi wetu hao ambao tunaamini watakuwa mabalozi wetu waa wazuri kwa wananchi wengine.

  "Pia wanafunzi hawa tunawaleza si tu kuhusu misitu tuliyonayo bali tunawaeleza na uwepo wa fursa ya kufanya utalii wa ndani kwa watanzania kwani katika misitu yetu kuna vivutio mbalimbali. Kwa hapa Pugu tu , katika kilele cha Mlima Pugu ukienda unauona mji wote wa Dar es Salaam.Watalii wengi kutoka nje wanakuja , hivyo tunawaambia wanafunzi wafahamu na wao watawafahamisha wengine," amesema Kobero.

   Alipoulizwa iwapo ipo haja ya kuwa na mitaala inayozungumzia kwa kina kuhusu misitu na mazao yatokanayo na misitu pamoja na utalii, Kobero amesema anatambua uwepo wa masomo yanayozungumzia kuhusu faida za misitu na utalii lakini kwake anaona ni vema ukaweka msisitizo zaidi kwa kuweka masomo yaliyojikita katika maeneo hayo ili kuwajengea wanafunzi uelewa mpana zaidi.

  Kuhusu iwapo elimu hiyo ambayo imetolewa kwa wanafunzi wa Sekondari ya Pugu na Minaki, Kobero amesema mkakati wa TFS ni kuhakikisha kanda zote kunakuwa na utaratibu huo na kwamba waaamini watawafikia wanafunzi wengi zaidi pamoja na makundi ya watu mbalimbali kwani lengo ni kuunganisha nguvu katika ulinzi wa misitu iliyopo nchini.

  Kwa upande wa wanafunzi wa shule hizo wamesema wanaipongeza TFS kwa uamuzi wake wa kuona haja ya kutoa elimu inayohusu utunzaji misitu kwao, kwani kuna mambo wamejifunza na wanaamini yatawasaidia kushiriki kikamilifu kwenye utunzaji misitu nchini.

  Wamesema ni kweli wanafahamu faida za misitu lakini elimu ambayo wameipata kutoka TFS wamebaini kuna mambo mengi ambayo hawakuwa wanayajua lakini sasa wamepata mwanga huku wakitumia nafasi hiyo kuomba mafunzo hayo yawe endelevu na sio kwao tu bali na kwa wengine kwani wote wanajenga Tanzania moja na kwamba misitu ni uhai.
   Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wilayani Kisarawe mkoani Pwani na Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kuwapeleka kwenda kushuhudia vivutio vilivyomo kwenye Msitu wa asili wa Pugu
   Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakionesha furaha yao baada ya kufanya utalii wa ndani kwa kwenda Msitu wa Asili wa Pugu .
   Baadhi ya wanafunzi wakishangilia baada ya kufika juu ya kilele cha Mlima wa Pugu ambapo walitembea kwa saa moja na nusu hadi kufika keleleni
   Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam wakiwa ndani ya msitu wa asili wa Pugu ambapo lengo la ziara hiyo ni kujifunza kuhusu uhifadhi wa mazingira lakini msitu huo ndiko unakopatikana mti wa Mpugupugu ambao ndio chimbo la jina la Sekondari ya Pugu
   Moja ya mti mrefu uliopo ndani ya msitu wa asili wa Pugu

  0 0


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  IMEELEZWA kuwa binadamu kukang'atwa na mdudu nyuki kuna faida nyingi sana katika mwili wa binadamu ikiwemo ya kusaidia kuondoa sumu mwilini, hivyo kwa wale ambao watang'atwa hawana sababu ya kumuua nyuki.

  Hayo yameelezwa na Ofisa Ugugaji Nyuki kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Rueben Nyambita wakati anazungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wilayani Kisarawe pamoja na Shule ya Sekondari Pugu ya jijini Dar es Salaam ambapo TFS imeamua kuzungumza na wanafunzi hao kwa lengo la kuwapa elimu inayohusu utunzaji wa misitu , faida za uwepo wa misitu na ufugaji nyuki katika misitu mbalimbali chini.

  Hivyo TFS imeamua kuja na mkakati wa kuhakikisha inazungumza na wanafunzi mbalimbali kuanzia shule za msingi, sekondari na vyuo ambapo wanaamini wakiipata vema elimu kuhusu utunzaji misitu na rasilimali za misitu watakuwa mabalozi wazuri kwa wengine.Hivyo maofisa wa kada mbalimbali wa TFS walienda katika shule hizo kuzungumzia misitu na faida zake pamoja na utalii unaopatikana ndani ya hifadhi za misitu ikiwemo ya asili na hasa ambayo iko chini ya TFS.

  Wakati wanazungumza na wanafunzi hao kwa nyakati tofauti, Nyambita pamoja na kuzungumzia faida nyingi zinazopatikana kutoka kwa mdudu nyuki akatumia nafasi hiyo kueleza iwapo binadamu atang'atwa na nyuki, basi sumu iliyokuwa mwili itaondoka."Kukang'atwa na nyuki kuna faida, hivyo ukiona amekung'ata mahali ujue anakwenda kuondoa sumu na tunatarajia kuwa uvimbe wake hauwezi kuwa mkubwa."

  Nyambita ameongeza hata kama binadamu ataumwa na nyuki watatu, wanne, watano au hata 10 bado watasaidia kundoa sumu na iwapo mhusika atavimba sana kuliko kawaida maana yake mwili wake utakuwa na sumu nyingi , hivyo inapokutana na sumu ya nyuki inasababisha aleji.

  Hata hivyo amefafanua nyuki anayo sumu lakini haina madhara sana kwa binadamu zaidi ya tiba lakini iwapo binadamu ataumwa na nyuki wengi sana kwa wakati mmoja basi ni rahisi kupata madhara kwani sumu ya nyuki itakuwa nyingi mwilini."Wanafunzi na wananchi kwa ujumla msigope kuumwa na nyuki kwani ni sehemu ya tiba."

  Kuhusu asali inavyotengenezwa, Nyambita amewaambia wanafunzi hao kuwa, asali ya nyuki inatengenezwa kutokana na mimea mbalimbali ambayo nyuki hupendelea kwenda kufyonza maji na hasa kwa maua ambayo yanatoa maji yenye ladha ya sukari.

  "Asali ya nyuki inatengenezwa na sukari ambayo inaitwa glukosi inayopatikana kwenye mimea mbalimbali.Nyuki anapotua kwenye mmea anavyonza maji na kisha anachuja sukari inayopatikana kwenye ule mmea ambayo ni kati ya asilimia 25 hadi 40 maji ya mimea hiyo inakuwa na sukari.Pia nyuki mwenyewe anavyo vimeng'enya vya kutengeneza asali kwa asilimia 75 hadi asilimia 80,"amesema Nyambita.

  Alipoulizwa na wanafunzi hao kwanini asali inaganda, amewajibu inatokana na glukosi ambayo ipo kwenye asali na ndio maana inasababisha kuganda na kuganda haina maana imeharibika.Kuhusu rangi tofauti ya asali , amesema hiyo inatokana na mimea ambayo nyuki ameifikia na kwa kuwa mimea ina rangi tofauti ni jambo la kawaida asali nayo kuwa na rangi tofauti tofauti.

  Wanafunzi hao wameelezwa kuwa nyuki anapotengeneza asali, kwa kawaida anatengeneza kwa ajili ya chakula chake kwa kutambua kuna nyakati za ukame na njaa na hivyo anajiandaa kwa kuwa na chakula cha akiba lakini binadamu kwa uroho wao wameamua kula chakula cha nyuki ambayo ndio hiyo asali inayopendwa na watu wa rika mbalimbali.

  Pia amesema kuna maziwa ya nyuki na hayo ni maalumu kwa ajili ya kulishwa malkia wa nyuki kutokana na jukumu ambalo analifanya kwa nyuki wengine, huku ikielezwa maziwa ya nyuki yana protini nyingi na kwa mwenye kuitumia anakuwa na akili nyingi sana na kama ni mwanafunzi atakuwa anafanya vizuri kwenye masomo kwa kushika nafasi za juu.

  "Wanafunzi na Watanzania wenzangu kwa ujumla niwaambie tu kuna faida nyingi sana za uwepo wa nyuki , hivyo ni vema tukahakikisha tunazalisha kwa wingi mazo ya nyuki ambayo yanaweza kutuingizia kipato kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.Kuna aina mbili za kufuga nyuki ikiwemo ile ya asili na ya kisasa lakini hii ya kisasa ambayo ni kutumia mzinga nyuki wanatoa asali nyingi zaidi,"amesema Nyambita.

  Pamoja na hayo yote TFS kupitia maofisa wake ambao walikuwa sehemu ya kwenda kuzungumza na wanafunzi hao wametumia nafasi hiyo kueleza kwa kina kuhusu umuhimu wa kufidhi misitu ya asili na kuhamasisha watanzania kuwa na utamaduni wa kufanya utalii wa ndani wa kutembelea hifadhi hizo.


older | 1 | .... | 1833 | 1834 | (Page 1835) | 1836 | 1837 | .... | 1897 | newer