Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1832 | 1833 | (Page 1834) | 1835 | 1836 | .... | 1904 | newer

  0 0  0 0

  Shirika la Agape AIDS Control Programme limetoa msaada wa baiskeli kwa Watoto Wafanyakazi 10 wa nyumbani katika manispaa ya Shinyanga baada ya kuwafadhili kusoma fani mbalimbali katika Chuo Cha Ufundi Stadi – VETA mkoa wa Shinyanga. 

  Baiskeli hizo 10 zilizotolewa na Shirika la Agape kupitia Mtandao wa Kusaidia Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani (Tanzania Child Domestic Workers Coalition – TCDWC) zitasaidia kuwarahisishia usafiri watoto hao kutoka nyumbani kwa waajiri wao hadi chuoni. 

  Akizungumza leo Ijumaa Aprili 5,2019 wakati wa kukabidhi baiskeli hizo mbele ya Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi,Mkurugenzi wa shirika la Agape John Myola alisema msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kumlinda Mtoto Mfanyakazi wa Ndani Dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji. 

  “Pamoja na kuwapatia baiskeli hizi zenye thamani ya shilingi 110,000/= kila moja,pia tumeshawalipia gharama zote za masomo ya Kozi mwaka mmoja katika fani za udereva,ushonaji,saluni na umeme katika chuo cha VETA kiasi cha shilingi Milioni 1.1 kila mmoja”,alieleza Myola. 

  “Agape inapenda kila mtoto hasa watoto wa kike anapata haki ya elimu,tumeona ni vyema kuwapa ujuzi wa kujiendeleza kwenye maisha yao,tunaomba waajiri wawape muda watoto hawa wasome”,aliongeza Myola. 

  Kwa upande wake,mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kukabidhi baiskeli hizo,Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi alilipongeza shirika la Agape kwa kuendelea kuwa wadau muhimu katika kuwaletea maendeleo wananchi kwani wamekuwa wakiunga kwa vitendo jitihada za serikali katika kuwasaidia wananchi. 

  “Agape mmekuwa mfano bora,mnajipambanua kwa vitendo kusaidiana na serikali kuwaletea maendeleo wananchi,naomba ‘NGO’s/mashirika mengine pia yafanye kazi za kuonekana badala ya kujinufaisha wenyewe”,alisema Chambi. Aidha aliwaasa vijana hao kutunza baiskeli hizo na kuzingatia masomo yao huku akiwataka waajiri kuwapenda wafanyakazi wao wa ndani kwani ni watu muhimu kwa ustawi wa familia hivyo wawape nafasi ya kusoma na kutowanyanyasa. 

  Naye Msimamizi wa mradi wa Kumlinda Mtoto Mfanyakazi wa Ndani Dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa shirika la Agape, Joyce John alisema lengo la mradi huo ni kuhakikisha mtoto mfanyakazi nyumbani anawezeshwa kijamii na kiuchumi ili aweze kujikwamua kimaisha. 

  “Mradi huu wa miaka mitatu (2016-2019) umejikita katika eneo la kuwapatia mafunzo ya ufundi na idadi ya watoto tuliowafikia hadi sasa ni 75,wengi wao tumewapatia elimu ya ushonaji,ujasiriamali na vitendea kazi ikiwemo cherehani”,alisema John. 

  Kwa upande wao, watoto waliopata baiskeli na kufadhiliwa kusoma katika chuo cha Veta walilishukuru shirika la Agape na kuahidi kusoma kwa bidii ili kujikwamua kielimu,kijamii na kiuchumi.
  Mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kukabidhi baiskeli hizo,Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akizungumza kabla ya kukabidhi baiskeli 10 kwa watoto wafanyakazi 10 wa nyumbani waliofadhiliwa na shirika la Agape kusoma fani mbalimbali katika chuo cha VETA - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape John Myola akielezea namna shirika hilo linavyounga mkono serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea maendeleo wananchi.Kulia ni Msimamizi wa mradi wa Kumlinda Mtoto Mfanyakazi wa Ndani Dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa shirika la Agape, Joyce John,kushoto ni Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi.
  Watoto wafanyakazi majumbani wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape John Myola.
  Baadhi ya Waajiri wa Watoto wafanyakazi majumbani waliokubali watoto wao wafadhiliwe na shirika la Agape John Myola kupata elimu ya fani mbalimbali katika chuo cha VETA.
  Msimamizi wa mradi wa Kumlinda Mtoto Mfanyakazi wa Ndani Dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa shirika la Agape, Joyce John akitoa taarifa ya mradi huo huku akitaja changamoto iliyopo kuwa ni ukosefu wa elimu ya haki na wajibu wa watoto wafanyakazi wa nyumbani kwa waajiri na jamii kwa ujumla.
  Baiskeli zilizotolewa na shirika la Agape kwa ajili ya watoto wafanyakazi wa nyumbani waliofadhiliwa na Agape kusoma katika chuo cha VETA.
  Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akikabidhi baiskeli kwa mmoja wa watoto wafanyakazi wa nyumbani.
  Zoezi la kukabidhi baiskeli likiendelea.
  Mtoto akifurahia baiskeli huku akisindikizwa na mwajiri wake.
  Mkurugenzi wa shirika la Agape,John Myola akishikana mkono na mtoto anayekwenda kusoma udereva katika chuo cha VETA.
  Mfanyakazi wa nyumbani wa kiume akisindikizwa na mwajiri wake wa kike ) anayeshikana mkono na Mkurugenzi wa Agape,John Myola)akipokea baiskeli.
  Watoto wakiwa na baiskeli zao.
  Afisa Miradi wa Shirika la Agape, Mustapha Isabuda akiwashauri wazazi na walezi kuwapenda wafanyakazi wa nyumbani na kuepuka kuwanyanyasa kwani hakuna ajuaye kesho nani anaweza kuwa nani.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), akiweka shada la Ua kwenye mnara uliopo kwenye makaburi ya wataalam 70 kutoka China waliokufa wakati wa ujenzi wa Reli ya Tazara, wakati wa maadhimisho ya utamaduni wa Wachina na kuwakumbuka wataalam hao yaliyofanyika kwenye eneo la makaburi walikozikwa wataalam hao lililopo Gongo la mboto, Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Msemaji wa Serikali Mhe. Dkt. Abbas, Kailua Kurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Caesar C. Waitara na viongozi mbalimbali wa serikali
  Prof. Palamagamba Kabudi pamoja na Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini wakitoa heshima zao kwa kuinamisha vichwa kama ishara ya kuwakumbuka wataalam hao kutoka China. 
  Prof. Palamagamba pamoja na Mhe. Wang Ke wakiweka maua katika moja ya kaburi la wataalam hao.
  Bw. Caesar Waitara akiweka Ua katika moja ya kaburi la wataalam hao.
  Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.), akihutubia katika hafla hiyo mara baada ya kumaliza zoezi la kuweka maua kwenye makaburi ya wataalam wa kichina waliokufa wakati wa ujenzi wa reli ya Tazara. Katika Hotuba hiyo waziri Kabudi aliendelea kuusifu ushirikiano wa Tanzania na China katika sekta mbalimbali ambapo Ujenzi wa reli ya Tazara ulipelekea kuanzishwa kwa viwanda mbalimbali.


  Aidha, alieleza kuwa kutoka na Ushirikiano ulipo Tanzania inatarajia kufungua ubalozi mdogo katika mji wa Guanzou pamoja na kuanzisha Safari ya Ndege za Shirika la Tanzania (ATCL) kuelekea moja kwa moja Guanzou ambapo utapelekea kuongeza watalii kutoka China kuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini Tanzania.
  Balozi Wang Ke naye akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo.
  Sehemu ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba zilizo kuwa zikiendelea kutolewa na Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Wang Ke (hawapo pichani) 
  Prof. Palamagamba John Kabudi akiweka saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya vifo vya wataalam hao.

  Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza hafla hiyo.
  Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Balozi Wang Ke wakiwa katika picha ya pamoja na wageni engine waliohudhuria tulip hilo.

  0 0

  · Dhana potofu zilizosambaa kuhusu sekta ya mauzo ya moja kwa moja 

  Biashara ya masoko ya mtandao inakuwa kwa kasi nchini na katika kanda hii kwa ujumla ambayo ni matokeo ya ongezeko la idadi ya watu na vijana wenye umahiri. Hata hivyo bado kuna dhana zisizo sahihi kwamba hii sio biashara halali. 

  Dhana hii potofu inaendelea kuwepo licha ya kwamba biashara ya masoko ya mtandao ya kitaalamu ni sekta yenye thamani ya dola za kimarekani billioni 190 ikiwa na zaidi ya wasambazaji milioni 96 duniani kote. Kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ya QNET ni sehemu ya sekta hii ambayo imedhibitiwa na sheria, maadili na taratibu za utendaji zile zinazosimamia taasisi halali. 

  Meneja Mkuu wa kanda wa QNET Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika wakati alipotembelea jijini Dar es salaam hivi karibuni, Biram Fall alikanusha dhana potofu kwa kusema kwamba kampuni ya QNET inaendesha biashara halali katika nchini nyingi na duniani kote na wanatoa bidhaa na huduma halisi. 

  Bwana Fall alikuwa nchini wakati kampuni ilipoendesha maonesho ya Expo kuonyesha bidhaa na huduma kwa wateja, ambapo alibainisha kwamba wamekuwa wakiendesha shughuli biashara hii kwa zaidi ya miongo miwili na iwapo ingekuwa sio biashara halali haingeweza kudumu kwa muda mrefu kama hivyo. 

  “Mifumo ya Piramidi huwa haidumu kwa muda mrefu kama ilivyodumu kampuni hii ambayo imekuwa inafanya kazi tangu 1998, matapeli kama hao huwa hawawezi kustahimili” alisema bwana Fall. 

  Aliongeza zaidi kwamba kampuni hii ina nembo yenye sifa nzuri na inayojulikana duniani ambayo iko tayari kuilinda na hivyo haiwezi kujihusisha na utapeli wa aina yoyote. 

  “Watu wabaya watakuwepo siku zote hapa na pale, hii ni changamoto. Lakini kwa suala la kanuni tunawahakikishia kuwa biashara katika QNET inaendeshwa kimaadili na kwa sababu hatuko hapa kuwadanganya watu ninawahakikishia kuwa QNET itaendelea kuwa hapa kwa muda mrefu” alisema bwana Fall. 

  Tofauti kabisa na dhana hiyo kampuni ya QNET imekuja kuwawezesha watu, hasa vijana, alisema akiongeza kwamba kwa mujibu wa Tathmini ya Idadi ya Vijana Afrika iliyofanywa na Taasisi ya Maendeleo ya Afrika (African Institute for Development), kwa sasa Afrika ina zaidi ya asilimia 45% kati ya watu milioni 150 walioko Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda. 

  Wengi wa vijana hawa wana elimu, wengi wana ufahamu wa teknolojia, wanauwezo wa kuendana na mifumo mipya kwa haraka, wanahamasa ya kuweka juhudi na wana fikra za ujasiriamali – sifa ambazo ni za msingi zinazohitajika kwaajili ya mafanikio endelevu katika biashara ya mauzo ya moja kwa moja. 

  Biashara ya Masoko ya Mtandao au Mauzo ya Moja kwa moja ni dhana ya biashara ya kimataifa na inaelezewa kama ‘uuzaji wa bidhaa au huduma kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, mbali na maduka halisi ya kawaida.’ Mtindo huu wa mauzo una umri wa zaidi ya miaka 100 na ulianzishwa mwanzoni huko nchi USA. 

  Leo, kuna takribani watu milioni 117 wanaohusika katika biashara hii. Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka ya Shirikisho la Vyama vya Mauzo ya Moja kwa Moja Duniani (World Federation of Direct Selling Association) (WFDSA) ya mwaka 2018, biashara ya mauzo ya moja kwa moja ilizalisha dola bilioni $190 za marekani na takribani nusu ya mauzo yote yametokea katika masoko yanayochipukia. 

  Afrika imechangia chini ya asilimia 1% ya jumla ya mauzo ya WFDSA lakini wataalamu wanatabiri kwamba soko la Afrika Mashariki linatoa fursa ya kukua kwa wajasiriamali wenye ari na hata kwa wale wenye kazi za kudumu na wanania ya kujipatia kipato cha ziada kupitia mauzo ya moja kwa moja. 

  Katika kanda ambayo matakwa ya ajira rasmi yanazidi kuwa na ushindani na kazi za kudumu kuendelea kuwa kidogo sana, biashara ya mauzo ya moja kwa moja inatoa njia mbadala wa ajira za kawaida kwa wale wanaohitaji kipato cha ziada kuongeza kipato kwaajili kwa mahitaji ya nyumbani, au kwa wale ambao mazingira hayawaruhusu kujipatia ajira rasmi. 

  Wakati ambapo mtindo huu wa biashara inakabiliwa na changamoto, changamoto kubwa zaidi ni kuenea kwa mifumo isiyo halali ya piramidi ambayo inajiwasilisha kama kampuni halali ya biashara ya mauzo ya moja kwa moja, ambayo inawaahidi wawekezaji wanaotaka kuwekeza kuwa watapata faida kubwa iwapo watawaandikisha watu wengine. 

  Hoja ni kwamba ‘matapeli’ hawa wanajenga dhana potofu kwenye sekta ya Mauzo ya moja kwa moja, jambo ambapo linaleta vikwazo kwa kampuni halali kusajili mawakala wa mauzo na kuendesha biashara zao halisi na halali. 

  Matokeo yake, kampuni inatatua tatizo hilo kwa kuwaelimisha umma kuwa makini na ‘matapeli’ kama hao na kuwahamasisha kuthibitisha uhalali wa kampuni yoyote kulingana na inavyotekeleza na kutii kanuni, sheria na taratinbu zilizowekwa na bodi zinazosimamia na mamlaka zinazohusika. 

  Katika kuimarisha uwepo wake nchini, kampuni ilifanya maonesho ya bidhaa jijini Dar es salaam ambayo yalibarikiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Paul Makonda, ambaye aliwapa changamoto vijana wanaotafuta fursa kupitia katika kampuni hii kuwa na ujasiri wanapofanyia kazi ndoto zao ili waweze kuwa na mafanikio. 

  Makonda alisema kwamba historia ya maisha yake binafsi ni ushahidi wa kutosha kwamba kufanyakazi kwa bidii na ujasiri hatimae huleta mafanikio na kuwaasa vijana wadogo kutokutosheka na mafanikio madogo. 

  Alisema, “Historia ya maisha yangu ni ushahidi kwamba kwa kufanyakazi kwa bidii na kuwa na ujasiri kila wakati unaweza kupata mafanikio unayoyatafuta. Usiridhike kwa mafanikio au vitu vidogo vidogo kuliko ndoto zako”. 

  Maonyesho ya bidhaa ya Expo yaliyobeba jina la Kuishi Kikamilifi ‘Absolute Living’ inayoendana na falsafa ya msingi ya kampuni , maonyesho haya huwa yanafanyika kila mwaka katika nchi tofauti duniani kote kwa lengo la kuonyesha bidhaa na huduma zake zinazotolewa sokoni. 

  Pia inakuwa kama jukwaa kwa wateja na wadau wengine wanaotaka kuelewa kuhusu kampuni na mtindo wake wa biashara. Dhana hii ni taswira ya juhudi za kampuni kuhamashisha mwenendo wa kiafya, na mtindo wa maisha wenye uwiano sahihi, kwa kutilia mkazo katika afya, ustawi na Elimu. 

  “Kutoka katika kozi za elimu kwa njia ya mtandao, (online course) mpaka katika kozi za vifurushi vya sikukuu, mpaka bidhaa za kuongeza nguvu, vyakula vya nyongeza na saa, tuna aina nyingi mbalimbali zinazoweza kutuwezesha kutoa huduma kwa mahitaji mbalimbali. Katika msingi wa yote haya, ni hamu yetu ya kutoa fursa ya ‘kuishi kikamilifu”, alisema bwana Fall. 

  Kampuni pia inatoa fursa za biashara kwa gharama nafuu kwa watu wanaotaka kuifanya, bila kujali kiwango chao cha elimu. 

  “Tanzania ni moja kati ya masoko yetu ya kitaalamu katika QNET na kwa kuwezesha kufanyika kwa onyesho la Expo jijini Dar es salaam ni njia ya kurudisha kwa viongozi wetu hapa na kuwa karibu zaidi nao.“ aliongeza. 

  Kama taasisi kampuni inaamini kwamba hakuna kinachompa nguvu zaidi mtu kama uhuru wa kifedha ambao unatokana na kufanyakazi katika sekta ya mauzo ya moja kwa moja na inaweza kuwa kazi ya kujitosheleza kwa wale watakaoamua kuifanya fursa hii muda wote au katika muda wa ziada. 

  Tofauti na biashara zingine za kawaida ambazo zinahitaji mtaji mkubwa wa kuanzisha, rasilimali na hata uzoefu, Biashara ya Mauzo ya Moja kwa moja inatoa biashara hii kwa gharama nafuu kwa kila mmoja anayeta kuanza kuifanya bila kujali kiwango chao cha elimu au uzoefu. 

  Manufaa makubwa ya biashara ya moja kwa moja katika masoko yanayochipukia kama Afrika Mashariki ni kwamba mtindo huu wa biashara una athari kubwa zaidi kuliko katika masoko yaliyoendelea kwa sababu ya athari za kifedha inayoweza kuleta kwenye maisha ya watu, kutoa fursa za ujasiriamali kwa wote, bila kujali sifa au uzoefu, hatimae kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza kiwango cha umaskini katika jamii.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda (katikati) na Meneja wa QNET, kanda kusini ya Afrika Biram Fall (kushoto) wakikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya bidhaa za QNET 2019 yaliyofanyika hivi karibuni . Kulia ni Mshauri wa Biashara wa QNET Tanzania, Edward Mkony.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wawakilishi, wafanyakazi na waalikwa wa QNET kuhusu maadili ya kazi kwenye uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za QNET jijini Dar Es Salaam hivi karibuni.
   

  0 0

  Na Estom Sanga-DSM 

  Menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umekutana na Wadau wa Maendeleo kutoka mashirika ya kimataifa yanayochangia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko huo. 

  Katika kikao kazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo za Mfuko huo jijini Dar es salaam,Wadau hao wa Maendeleo na Menejimenti ya TASAF wamepongeza hatua ya serikali ya kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja nchini kote . 

  Wamesema utekelezaji wa Mpango huo umekuwa wa manufaa na mafanikio makubwa na hivyo kuvutia mataifa mengine kuja nchini kujifunza namna Serikali kupitia TASAF ilivyotekeleza mpango huo na kuzaa matunda katika kipindi kifupi tangu kuanza kutekelezwa. 

  Aidha kikao kazi hicho kimeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini inakamilika kwa ufanisi na kufanya maandalizi thabiti ya awamu ya pili inayotarajiwa kuanza katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha. 

  Akizungumza katika kikao kazi hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mkazo mkubwa katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika awamu ya pili itakuwa ni kuwashirikisha walengwa wa Mpango kushiriki katika kazi kwenye miradi itakayoibuliwa kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira ili kuinua kipato chao. 

  Kwa upande wake, Mkuu wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia hapa nchini Bwana Mohamed Muderis amesema kwa ujumla Benki ya Dunia na Washirika wengine wa Maendeleo wameridhishwa na namna Serikali ya Tanzania kupitia TASAF ilivyoonyesha dhamira ya dhati katika kutekeleza Mpango wa kunusuru Kaya maskini kwa lengo la kuboresha hali za maisha ya wananchi ambao wamekuwa wakiishi katika hali ya umaskini . 

  Menejimenti ya TASAF na wadau wa maendeleo hukutana mara moja kila mwezi kufanya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwa lengo la kuhakikisha kuwa utekelezaji huo unakuwa wa manufaa kwa Walengwa .

  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bw. Ladislaus Mwamanga (mbele) akiongoza kikao kazi cha menejimenti na Wadau wa Maendeleo jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia nchini Bw. Mohamed Muders (aliyesimama akizungumza kwenye kikao kazi kati ya menejimenti ya TASAF na Wadau wa Maendeleo) kushoto kwake ni mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga . 

  Baadhi ya Wadau wa maendeleo na menejimenti ta TASAF (picha ya juu na chini ) wakiwa katika kikao kazi kilichojadili utekelezaji wa shughuli za TASAF.
  0 0

  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Morogoro (TAKUKURU),imefanya uchunguzi wa mfumo ukusanyaji wa mapato kwa njia ya Point of sale (POS) na kubaini baadhi ya Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo kutokuwa Waaminifu.

  Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Morogoro, Janeth Machulya,amesema kufuatia kufanyika kwa uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya point of sale (pos) wamebaini baadhi ya Halmashauri mkoani Morogoro kuwa na watumishi wasio waadilifu,ambapo katika kipindi cha robo mwaka 2019 januari hadi machi jumla ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 2.5 zimefuatiliwa na shilingi milioni 370.2 zikirejeshwa kutoka halmashauri nne za mkoani Morogoro.
   
  Amesema Halmashauri zilizorejesha fedha hizo ni pamoja na Kilombero imerejesha milioni 355,950,600/= ikifuatiwa na Kilosa milioni 5,952,00/= huku Mvomero wakirejesha milioni 8,731,850/= na Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ikirejesha milioni 5,000,000/=, jumla kwa Halmashauri zote nne zikiwa zimerejesha milioni 370,277,650 na kufanya kiasi cha bilioni 2.5 zilizofuatiliwa kupungua na kubaki bilioni 2.1 ambapo Takukuru Morogoro imeahidi kuzifuatilia na watakaoshindwa kurejesha fedha hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

  Kufuatia zoezi hilo takukuru morogoro imeanza kuchukua hatua kwa kuanzisha uchunguzi ambapo mpaka sasa jumla ya majalada 10 yamefunguliwa.

  “Ningependa kuwakumbusha watumishi wa serikali waliopewa dhamana ya kukusanya mapato na mawakala wote wa Halmashauri za wilaya katika mkoa wa morogoro kuhakikisha kuwa wanawawasilisha benki kwa wakati fedha zote za makusanyo zilizobaki mikononi mwao na maafisa masuhuli kuacha kupanga matumizi ya fedha kabla utaratibu wa kuidhinishwa fedha hizo haujafanywa na mamlaka zinazohusika ” alisema Janeth Machulya.
  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Morogoro, Janeth Machulya akizungumza na Waandishi wa habari leo kuhusu
  uchunguzi wa mfumo ukusanyaji wa mapato kwa njia ya Point of sale (POS) na kubaini baadhi ya Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo kutokuwa Waaminifu.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako kuzindua chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Godfrey Zambi, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya kuzindua chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya kuzindua chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma.
  Sehemu ya Wananchi wa Namtumbo waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma. PICHA NA IKULU


  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, handisi Evarist Ndikilo na Kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa wakikagua ujenzi huo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, handisi Evarist Ndikilo akijadiliana jambo na kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa.  Mafundi wakiendelea na ujenzi wa nyumba hizo. 

  …………………………………………………………………………………………..
   
   
  NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

  ASKARI wa jeshi la polisi mkoani Pwani, wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa makazi ya kuishi, hali inayosababisha kushindwa kuwahi wakati wakihitajika haraka katika dharula za majukumu yao ya kikazi.
  Kutokana na hali hiyo, kwasasa jeshi hilo linajenga nyumba 20 za makazi ya askari polisi hao,zitakazogharimu milioni 500 ili kukabiliana na hali hiyo. 

  Akizungumza wakati alipokwenda kutembelea ujenzi wa nyumba hizo zinapojengwa Kibaha Mjini, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alitaka ujenzi huo ,ukamilike ifikapo June 30 mwaka huu, kama amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama ,dkt. John Magufuli alivyoelekeza. 

  Alisema ,askari wanapaswa kulinda mali ya mwananchi na kulinda usalama wa raia hivyo wanatakiwa waishi kwenye mazingira yaliyo bora. “Kanda maalum ya kipolisi Rufiji imepatiwa milioni 500, pamoja na jeshi la polisi Pwani milioni 500, jumla milioni 100, ambazo zimetolewa na serikali kuhakikisha kila mkoa askari wanajengewa makazi ya kuishi “ “Hivyo ni wajibu wa jamii, wenye viwanda kushirikiana na serikali na jeshi la polisi kujenga mazingira bora ya askari hawa waweze kutulinda kwa moyo na upend “alifafanua Ndikilo. 

  Awali akitoa taarifa fupi kwa mkuu wa mkoa huyo juu ya ujenzi unavyoendelea, kamanda wa polisi Pwani, Wankyo Nyigesa alibainisha, kutokana na ufinyu wa bajeti wamepewa milioni 500 na kwa wastani kila nyumba itagharimu milioni 25 mpaka kukamilika kwake. 

  Aliwashukuru wadau waliojitokeza kusaidia akiwemo Said Salim Bakhresa, jeshi la wananchi wa Tanzania kupitia kikosi cha usafirishaji (KJ 95) ambao waliwapatia lowbed kwa ajili ya kubeba buldoza kutoka bakhresa sugar company huko Bagamoyo. 

  Wengine ni Chila mkurugenzi wa Creative Intertraders ltd ambae ametoa mifuko 100 ya saruji na Twyford Ceramics (KEDA )ya Chalinze na wengine ambapo amewashukuru na kuomba wadau wengine waendelee kuwashika mkono. 

  Mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa ambayo , Amiri Jeshi wa Majeshi dk. Magufuli akiwa anazindua nyumba za askari polisi mkoani Arusha ,april 7 mwaka 2018, alitoa maelekezo kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) kwamba atapatiwa fedha kwa ajili ya makazi ya askari ,ambapo mkoa huo umeanza utekelezaji baada ya kupokea fungu hilo.

  0 0

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MWANAMUZIKI wa kizazi kipya mwenye uwezo mkubwa wa kuteka hisia za mashabiki Amini Mwinyimkuu anatarajia kuipua kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Nimenasa akimshiriki mwanadada aliyekwe ubora wake Esterina Peter Sanga a.k.a Linah.

  Akipiga stori na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam Amin amesema wimbo huo utauachia wiki ijayo na kwamba ameufanyia Studio ya C9 chini ya mtayarishaji Kichwa Touch Killer.

  Kama kawaida yake akiwa anazungumza kwa upole wa hali ya juu ukiambatana na umakini wa kujieleza amesema ni wakati muafaka wa kutoa wimbo huo akiwa amemshirikisha Linah kwani ni mwanamuziki wa kike anayemkubali.

  Ujue iko hivi Amini na Linah huko nyuma walikuw na uhusiano ule wa kibaba na mama lakini safari hii wameamua kukutana kwa ajili ya kufanya kazi moja tu ya kutoa wimbo kwa ajili ya mashabiki wao.

  Alipoulizwa kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi kama wameruadia au laa, Amini akizungumza kwa kujiamini kama jina lake kuwa hakuna uhusiano huo zaidi ya ule wa kufanya kazi kama wasanii.

  "Hatuna uhusiano ila nimeamua tu safari hii katika wimbo wangu mpya nishirikiane na dada Linah."Swali likawa tena kwanini Amini anamuita dada Linah ,eti akajibu hivi "Wanawake ndio mama zetu, na akiwa mdogo kwangu atakuwa dada,ndio maana nasema ni dada Linah."

  Kwanini ameamua kumshirikisha Linah katika kibao hicho cha Nimenasa, amejibu anavutiwa na uwezo na kipaji cha mwanadada huyo na kwamba Linah hata akiamshwa kutoka usingizi ubora wa sauti na uwezo wa kuimba uko palepale.
  "Linah anao uwezo mkubwa sana wa kuimba na ndio maana nimeamua kumshirikisha,pia na hata pale unapokuwa umetunga mashairi ya wimbo ukimpa anaweza kukariri kwa muda mfupi," amesema Amini.

  Alipoulizwa kama Caple yao yaani Amini na Linah inaendana ,amejibu ukweli ni kwamba mashabiki wanaofuatilia muziki wao wamekuwa wakisema wanafurahia Caple yao na wanatamani wafanye kazi pamoja.Mbona raha.Acha tusubiri tuone kama kweli wanaweza kuishia kwenye kuimba tu au watarudi kuleee kwenye mahusiano ya michezo ya kibaba na kimama.

  Kwa kukumbusha tu msanii Amini umaarufu katika muziki umetokana na nyimbo zake mbalimbali zikiwemo Ni wewe,Mtima wangu, Robo Saa, Unikimbie, Nyota,Yameteka dunia na Novemba or Desemba.

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Alim Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuufungua Msikiti wa Masjid Maryan Mtende Wilaya ya Kusini Unguja kushoto Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar Ndh Said Salim Bakhressa, hafla hiuyo imefanyika katika Kijiji hicho leo
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekitin wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Waumini wa Dini ya Kiislam wa Kijiji cha Mtende Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa hafla hiyo ya Ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende, uzinduzi huo umefanyika leo 5-4-2019
  MWANAMCHI wa Kijiji cha Mtende Wilaya ya Kusini Unguja Sheikh Khamis Ramadhan Mbarak. akisoma risara ya Wananchi wa Kijiji cha Mtende wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Msikiti wao Mpya uliojengwa kwa Ufadhili wa Bw. Said Salim Bakhressa.
  BAADHI ya Wananchi wa Mtende Wilaya ya Kusini Unguja wakifuatilia hutuba ya ufunguzi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende Mkoa wa Kusini Unguja leo 5-4-2019
  MIFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kumalizika hafla ya Ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende Wilaya ya Kusinu Unguja, kushoto Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Mfanya Biashara Maarafu Tanzania Bw. Said Salim Bakhressa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Khamis Maalim Juma na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan, wakiitikia dua wakati wa hafla hiyo
  MKURUGENZI wa Mashtaka Zanzibar Mhe. Ibrahim Mzee mwenye miwani akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Mtende Wilaya ya Kusini Unguja wakiitikia dua wakati wa hafla ya ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende leo
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Utumishi wa Umma Zanzibar na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduzi Mhe. Haroun Ali Suleiman akitowa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende Wilaya ya Kusini Unguja leo, baada ya uzinduzi wake leo.(Picha Ikulu).

  0 0


  Baadhi ya wanafunzi wa kikewa kidato cha Sita mwaka 2019 mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama (katikati), mara baada ya kupokea msaada wa taulo za kike zilizotolewa kwa ajili yao na mamlaka hiyo, katika kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kushoto)akiwa na baadhi ya wanafunzi wa kike wa kidato cha sita mkoani humo, wakipokea sehemu ya msaada wa taulo za kike zilizotolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na kuwasilishwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama (wa tatu kulia), katika kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya wanafunzi sehemu ya maboksi ya taulo za kike ambazo zimetolewa msaada kwa wanafunzi kike walio kwenye kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.
  Mwanafunzi Winfrida Nasoro kutoka Shule ya Sekondari Dutwa, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake mara baada ya kupokea msaada wa taulo za kike uliotolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kwa wanafunzi wa kike 538 walio katika kambi ya Kitaaluma ya Kidato cha Sita inayoendelea wilayani Maswa.
  Sehemu ya katoni za taulo za kike zilizotolewa msaada Aprili 05, 2019 na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kwa wanafunzi wa kike 538 walio katika kambi ya Kitaaluma ya Kidato cha Sita mwaka 2019 Mkoani Simiyu inayoendelea wilayani Maswa.
  Baadhi ya wanafunzi wa kikewa kidato cha Sita mwaka 2019 mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama (katikati), mara baada ya kupokea msaada wa taulo za kike zilizotolewa kwa ajili yao na mamlaka hiyo, katika kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.

  …………………………

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) imetoa msaada wa katoni 111 za taulo za kike zenye thamani ya shilingi milioni tano, kwa wanafunzi wa kike 538 walio katika kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019, inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya wasichana Maswa Mkoani hapa.

  Akikabidhi msaada huo Aprili 05, 2019 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama, amesema Mamlaka hiyo imetoa msaada huo kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuinua elimu mkoani Simiyu, ili kuwasaidia watoto wa kike wasome kwa uhuru na utulivu kambini hapo hususani wakati wa hedhi.

  Amesema TFDA kama wadau wa mkoa wataendelea kushirikiana na Serikali mkoani Simiyu katika sekta ya elimu na masuala mengine ya Maendeleo, huku akiwasisitiza wanafunzi walio kambini kusoma kwa bidii na kutumia vizuri muda walionao ili waweze kufikia malengo yao.

  Akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Mamlaka hiyo kwa msaada uliotolewa kwa wanafunzi wa kike, huku akiwasisitiza wanafunzi wote walio katika kambi ya kitaaluma kusoma kwa bidii.

  Aidha, Mtaka amewashukuru wadau mbalimbali ambao wameendelea kutoa michango kwa ajili ya kufaninisha kambi ya kitaaluma inayoendelea mkoani humo, huku akiahidi kuwa wadau wote waliochangia watatambuliwa na kupewa vyeti.

  Katika hatua nyingine Mtaka ametoa ufafanuzi kwa wadau na wananchi kuhusu utaratibu wa kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, kwamba kambi hizi hufanyika katika ngazi za shule na baadaye huundwa kambi moja ya mkoa kuwakutanisha wanafunzi kwa ajili ya kambi ya mkoa.

  “Kambi za Kitaaluma kwenye mkoa zilianza muda mrefu lakini kama mkoa tumeweka utaratibu wa kuwa na kambi moja ya kimkoa inayounganisha shule zote za kidato cha sita; kambi za kidato cha nne nazo zinaendelea kwa hiyo tutakapofika mwezi wa saba tutaanza kuunganisha shule, kama tulivyofanya mwaka jana tuliunganisha shule 24 pale Simiyu Sekondari” alisema.

  Nao wanafunzi wa kike wa Kidato cha Sita walio katika Kambi hiyo ya Kitaaluma wameishukuru Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa msaada huo ambao wamesema utawasaidia sana kusoma kwa uhuru na kujiamini zaidi wakati wa hedhi.

  “Tulikuwa tunakumbana na changamoto ya kutokuwa na amani na kushindwa kujiamini wakati wa hedhi kwa hiyo hata kusoma tulikuwa tunasoma lakini tunakuwa na wasiwasi, kupitia msaada huu ‘tutakuwa comfortable ‘ (tutakuwa na amani) kabisa tunaishukuru sana TFDA”Mwanaidi Halfan.

  “Huu msaada tuliopata utanisaidia kufikia ndoto zangu maana wasichana wengi wanapokosa taulo hizi za kike wanashindwa kusoma, wanakuwa na hofu wengine hata darasani hawaendi, lakini kwa kuwa wote tumepata msaada huu najua muda tutakao kuwa hapa tutakuwa huru kujisomea hatutaogopa tena maana zinatuhakikishia usalama tunapokuwa hedhi” alisema Hidaya Simba

  Jumla ya wanafunzi 1166 wa kidato cha Sita mwaka 2019 kutoka shule 12 mkoani Simiyu wako katika kambi ya kitaaluma kwa siku 28 katika shule ya sekondari Maswa, kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa unaotarajia kufanyika mwezi Mei, 2019.

  0 0
 • 04/05/19--12:43: TAARIFA MUHIMU KUTOKA NIDA


 • 0 0


  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO) Joseph Bukombe akizungumza na madereva wa magari ya abairia, binafsi na madereva bodaboda katika uzinduzi wa kampeni ya kunywa kistaarabu iliyozinduliwa leo jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.
  Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha akizungumzia kampeni ya kunywa kistaarabu maarufu kama ‘Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto’
  Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha akizungumza na madereva bodaboda katika stendi kuu ya mabasi Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO) Joseph Bukombe akimvisha kizibao cha kisibqo chakung'aa mmoja wa madereva bodaboda katika stendi kuu ya mabasi jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.

  Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Bakari Msangi akimvisha mmoja wa dereva bodaboda kizibao cha kung'aa (reflector) katika kampeni iliyozinduliwa Jijini Arusha ya kunywa kistaarabu na kampuni ya Serengeti.Picha na Vero Ignatus.
  Mwenyekiti wa bodaboda akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya kunywa kistaarabu stendi kuu ya mabasi Jijini Arusha.


  Na. Vero Ignatus, Arusha


  Madereva wa vyombo vya moto Mkoani Arusha watakiwa kutotumia vilevi wakati wawapo barabarani

  Arusha, Aprili 5, 2019, Kampeni ya unywaji wa kistarabu inayoendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imezinduliwa rasmi Mkoani Arusha ambapo madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kuzingatia sheria za barabarani na kutotumia vilevi wakati wa kazi.

  Kampeni hiyo maarufu kama ‘Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto’ imeenda sambamba na ugawaji wa makoti ya usalama (Reflectors) kwa madereva bodaboda mkoani humo ikiwa ni mkakati wa kuhimiza matumizi ya vifaa hivyo kwa usalama wa watumiaji wa barabara.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika leo katika Makao Makuu ya Traffic jijini hapa, Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha amesema kampeni hiyo imelenga kutoa elimu kwa wateja wake nchini ili kupunguza matukio yanayoepukika kama ajali zitokanazo na unywaji wa pombe kupindukia.

  “Pombe isipotumika kiistarabu inaweza kuleta madhara katika jamii na mojawapo ya madhara ni pale mtu anapokunywa pombe na akaendesha chombo cha moto ikasababisha ajali jambo ambalo ni hatari kwa madereva na pia ni hasara kwa Taifa,” alisema

  Kampeni hiyo inashirikisha wadau mbalimbali ikiwamo Jeshi la Polisi-Kikosi cha usalama barabarani, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), madereva bodaboda pamoja na jamii kwa ujumla ikilenga katika kupunguza ajali zitokanazo na ulevi wa kupindukia nchini.

  Kwa upande wake,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO) Joseph Bukombe alisema kampeni hiyo itasaidia katika kupunguza ajali zinazosababishwa na ulevi huku akiwataka madereva kuzingatia kuacha kutumia vilevi ili kujihakikishia usalama wawapo barabarani.

  Madereva bodaboda atakayekamatwa anaendesha hana leseni pikipiki itazuiliwa atalipia shilingi 25,000 ataingia darasani kusoma akimaliza kusoma atapewa cheti chake halafu anaanza kushughulikia leseni yake. Alisema RTO.

  “Unywaji wa pombe kiistarabu ni suala la muhimu sana kwa madereva kwasababu madereva wakiwa kwenye hali ya ulevi ni moja ya chanzo cha ajali za barabarani hivyo tunaipa kipaumbele kampeni hii hapa mkoani Arusha na tutaendelea kutilia mkazo suala hili,” alisema

  Bukombe amewakumbusha madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa Stika za usalama barabarani zimeshatoka hivyo wapeleke pikipiki zao kukaguliwa kwa shilinhi 1000,magari ya watu binafsi 3000,magari ya biashara 5000

  Aliipongeza SBL kwa kuona umuhimu wa kuwalinda watumiaji wa barabara kwa kutoa elimu hiyo kwa madereva na umma kwa ujumla. “Pamoja na kuwa wao (Serengeti) ni watengenezaji wa pombe lakini wameona wajibu wao wa kumlinda na kuleta usalama wa madereva na watumiaji wengine wa barabara,” alisema

  Kwa upande wake mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani (RSA) Bakari Msangi amewataka madereva waendesha bodaboda na magari ya Abiria kuwa makini wawapo barabarani na wafuate sheria kama inavyotakiwa

  Tunachowasii na kusisitiza ni kutii sheria mnapokuwa kwenye vyombo vya moto, wacheni ulevi mkiwa kazini, kunywa wakati umeshamaliza kazi, tuhqkikishe tunaondoa ajali zote zinazo epukika

  0 0

  Mratibu wa afya ya mama na mtoto mkoa wa Morogoro Santiel Kinyongoakizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Morogoro


  Na. Vero Ignatus.

  Dkt. Mkuu wa mkoa wa Morogoro, daktari Kebwe Steven Kebwe amewataka akina mama wajawazito mkoani humo kuzingatia chanjo zote muhimu wakati wa ujauzito ili wajifungue salama.

  Daktari Kebwe pia amewataka akina mama hao kuhakikisha watoto wanaowazaa wanapata chanjo zote muhimu katika vituo vya Afya.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya " Jiongeze Tuwavushe Salama " ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni hiyo ya kitaifa Kwa ngazi ya mkoa, Daktari Kebwe amesema chanjo zinawalinda mama na mtoto atakayemzaa na maradhi mbalimbali yakiwemo pepopunda.

  Kuzinduliwa kwa kampeni hiyo katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara ukiwemo wa Morogoro ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la serikali kuu kwa wakuu wote wa mikoa nchini kuzindua na kutekeleza ajenda ya kuhakikisha vifo vya wajawazito na watoto wachanga vinapungua.

  Daktari Kebwe amesema serikali imewekeza vya kutosha katika sekta ya afya kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana.Amewataka wanawake wajawazito wa mkoa wake kuhudhuria kliniki wakiwa na wenza wao na kuhakikisha chanjo wanazipata Kwa sababu zinatolewa bure.

  Amesema mama mjamzito anayehudhuria kliniki atajua mapema changamoto za uzazi atakazopitia ili kuepuka uzazi pingamizi, ambao ni moja ya vyanzo vya kifo kwa akina mama, ikiwemo kutokwa damu nyingi wakati na baada ya kujifungua.

  Amewataka watendaji wa mkoa, wakiwemo wakuu wa wilaya wote, wakurugenzi, waganga wakuu, wananchi na wanaohusika katika kutoa huduma kuhakikisha vifo vinapungua.Pia ametia sahihi ya makubaliano ya uwajibikaji wa "kasi" Kwa wakuu wa wilaya zote kuhakikisha maazimio ya kimkoa ya kupunguza vifo yanafikiwa.

  " Tunatengeneza utaratibu wa kuwapima ( score card) kuona nani ametimiza wajibu wake ambao kila baada ya miezi 6 utafanyika ," amesema daktari Kebwe.Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama ilizinduliwa na makamu wa Rais, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mwezi November mwaka juzi mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wakuu wote wa mikoa, utekelezaji wake ukiwa chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

  Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto wa mkoa wa Morogoro , Santiel Kinyongo amesema mkoa unafanya jitihada kupunguza vifo vya mama na mtoto, ingawa bado kuna changamoto ndogo ndogo.Amesema kwa mfano kuna upungufu Wa wakunga katika vituo vya vingi vya mkoa wa Morogoro, isipokuwa Wilaya ya Ifakara na Manispaa ya Morogoro hali inaridhisha.

  Pia ameongelea umuhimu wa mama mjamzito kuhakikisha anahudhuria kliniki si chini ya mara 4 wakati wa ujauzito wake ili apate chanjo za kumlinda yeye.Ameshauri pia mama mjamzito kumpeleka Mtoto atakayemzaa kliniki ili aweze kupewa chanjo zote muhimu.

  Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama inatekelezwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo UNICEF
  Picha mbalimbali za matukio ya uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama iliyofanyika mkoani Morogoro.

  0 0

  Shirika la Agape AIDS Control Programme limetoa elimu ya afya uzazi na ujinsia kwa vijana kwa njia ya michezo katika kijiji cha Manyada kata ya Usanda Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI,mimba na ndoa za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia. 

  Elimu hiyo imetolewa Ijumaa Aprili 5,2019 katika Uwanja wa Kitongoji cha Mwagala ambapo michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,kukimbiza kuku na mbio za baiskeli kwa wanaume na wanawake imefanyika ikihusisha vijana walio nje ya shule. 

  Washindi katika michezo hiyo kutoka vitongoji vya Buchamike,Mwagala,Uswahilini,Sagabahi na Munge wameondoka na zawadi ikiwemo kuku na mbuzi huku wakipata ujumbe wa aina mbalimbali kuhusu namna ya kulinda afya zao lakini pia kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake katika jamii. 

  Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga alisema elimu hiyo inatolewa kwenye maeneo ya pembezoni ‘Hard to reach communities’ katika kata ya Usanda ili jamii ichukue tahadhari kuhusu maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni. 

  “Michezo hii imeshirikisha vijana ambao wapo nje ya shule,tunaamini elimu hii itawasaidia vijana ikizingatiwa kuwa vijana ndiyo wapo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya VVU na vijana hawa ndiyo wamekuwa wakiwatia mimba watoto na kuwakatisha masomo shuleni”,alieleza Maganga. 

  Akitoa elimu ya afya,Muuguzi kutoka Kituo cha Afya Usanda,Jesca Mabula aliwahamasisha vijana kufanyiwa tohara kwani inakinga kwa asilimia 60 dhidi ya maambukizi ya VVU na kutumia kondomu huku akiwashauri kupima afya zao ili kubaini kama wana maambukizi ya VVU au la. 

  Pia aliwataka wanaume kuachana na tabia ya kuchepuka pindi wake zao wanapojifungua kwani kitendo hicho kinachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa. 

  “Wanaume tunzeni wake zenu,acheni kuchepuka na kuuza vyakula kwa ajili ya kuwahonga na hata kuoa wanawake wengine,pia muwaruhusu wake zenu kupanga uzazi wa mpango na muwe na tabia ya kutembelea vituo vya afya kwa ajili ya ushauri kuhusu masuala ya afya”,alieleza. 

  Muuguzi huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi juu ya umuhimu wa kukaa karibu na watoto wao wa kike na kuwaeleza kuhusu mabadiliko ya mwili na kuhakikisha wanawapeleka shule badala ya kuwaozesha wangali wapo katika umri chini ya miaka 18. 

  Shirika la Agape la mkoani Shinyanga linatekeleza mradi wa afya ya uzazi na ujinsia katika kata ya Usanda kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la Sida nchini Sweden kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii ili kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni,maambukizi ya VVU na ukatili wa kijinsia. 
  Mgeni rasmi, Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu akizungumza wakati Shirika la Agape likitoa elimu ya afya uzazi na ujinsia kwa vijana kwa njia ya michezo katika kijiji cha Manyada kata ya Usanda Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga akiwahamasisha wananchi kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali kukabiliana na maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa,kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia. 
  Muuguzi kutoka Kituo cha Afya Usanda,Jesca Mabula akitoa elimu ya afya ya uzazi na kuwashauri vijana kujitokeza kufanyia tohara na kuwahamamisha kutumia kondomu na kuachana na michepuko watunze wake zao.
  Muuguzi kutoka Kituo cha Afya Usanda,Jesca Mabula akiwataka akina mama kuacha tabia ya kupeleka watoto wao wa kike kwa waganga wa jadi kutafuta dawa ya kupendwa 'samba' ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni pamoja na maambukizi ya VVU.
  Afisa Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akiwasisitiza vijana wafanyiwe tohara na kuacha kutamani watoto wa shule kuhusu akiwashauri wanaume wanaopenda watoto wa shule wawashonee sketi za shule wake zao ili tamaa ya kutamani watoto wa shule.
  Washiriki wa mbio za baiskeli wakichuana vikali katika round 20 kuzunguka uwanja ambapo mshindi wa kwanza alipata zawadi ya mbuzi mmoja.
  Ni burudani tu!! Vijana wa kike hawakuwa nyuma katika mbio za baiskeli wakichuana vikali...Hapa wanaoneshana nani mkali katika round 5 kuzunguka uwanja.
  Mchezo wa kukimbiza kuku ukiendelea ambapo aliyefanikiwa kukamata kuku,ndiyo ilikuwa zawadi yake...kama atakwenda kumfanya kitoweo ama kumfuga basi kazi kwake!!
  Kikosi cha timu ya mpira wa miguu Mwagala kikiwa tayari kabisa kukabiliana na timu ya Buchamike katika uwanja wa Mwagala.
  Kikosi cha timu ya mpira wa miguu Buchamike kikiwa tayari kabisa kuwavaa Mwagala.
  Mchezo kati ya Mwagala na Buchamike ukiendelea.
  Mchezo unaendelea....Hata hivyo Buchamike waliibuka washindi kwa kuwachapa Mwagala bao 1 - 0.
  Mashabiki wa timu ya Mwagala wakiwa uwanjani.
  Mashabiki wa timu ya Buchamike wakishangilia baada ya timu yao kuwachapa Mwagala bao 1 - 0
  Mgeni rasmi, Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu (kushoto) akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa mshindi wa kwanza shindano la mbio za baiskeli upande wa wanaume Jeremiah Dotto.
  Mgeni rasmi, Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa mshindi wa kwanza shindano la mbio za baiskeli upande wa wanawake Juke Jackson (aliyebeba mtoto).
  Washindi wa pili shindano la mbio za baiskeli (Emmanuel Malale upande wa wanaume na Mariam Segese upande wa wanawake) wakiwa wamebeba zawadi ya kuku baada ya kukabidhiwa.
  Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu (kushoto) akikabidhi zawadi ya mbuzi wawili kwa washindi wa kwanza shindano la mpira wa miguu (Buchamike).
  Golikipa wa timu ya Buchamike Ntalike Juma(kushoto) na Kapteni wa timu hiyo Jimogela Mwita wakibeba zawadi ya mbuzi wawili.
  Golikipa wa timu ya Buchamike Ntalike Juma(kushoto) na Kapteni wa timu hiyo Jimogela Mwita wakiondoka na zawadi ya mbuzi wawili.
  Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

  Na: Theresia Mallya - Afisa Habari Tunduru DC
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametoa maagizo kwa waziri wa Tamisemi Mhe.Selemani Jafo kutoa shilingi milioni 200 za kukamilisha ujenzi na upanuzi wa  kituo cha afya Juma Homera kilichopo Nakayaya wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.

  Maagizo hayo ameyatoa wakati akitoa hotuba kwa wananchi wa wilaya hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko la Mchele –Nakayaya akiwa katika ziara ya kikazi siku ya pili mkoani Ruvuma.

  Rais Magufuli alifikia uamuzi huo baada ya kuguswa na michango ya wananchi waliotoa katika kuchangia ujenzi wa kituo cha afya Juma Homera ya shilingi Milioni 189 ili kujenga kituo hicho kitakachosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya
  Tunduru.

  “Waziri wa Tamisemi nakuagiza ulete shilingi milioni 200 kwa ajili ya kufanya upanuzi wa kituo cha afya Juma Homera ili kitoe huduma za upasuaji,mionzi,kuongeza wodi za kutosha ili kurahisha huduma za afya kwa wananchi wa Tunduru”

  aidha katika hatua nyingine Rais Magufuli Alimuagiza waziri wa Tamisemi Selemani Jafo kutoa shilingi milioni 500 za ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Namiungo ambayo haina zahanati wala kituo cha Afya katika vijiji saba vya kata hiyo.

  Magufuli alilazimika kusimamisha msafara na kuwasikiliza wananchi waliokuwa wamefunga barabara ambapo alisema kuna kila sababu ya kata hiyo kuwa na kituo bora na cha kisasa ili kupunguza vifo vya kinamama na wajawazito na watoto vinavyosababishwa na kusafiri umbali mrefu
  kufuata huduma za afya.

  Hata hivyo alimaliza kwa kuwataka wananchi kufanya kazi na kushikamana katika kuijenga Tunduru na kuepuka chuki za kisiasa kwani  maendeleo hayana chama, niwatake wanatunduru muungane kwa pamoja katika kuleta maendeleo chanya.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo ameitembelea  Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania almaarufu Twiga Stars katika kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe mapema leo alipoitembelea  Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania almaarufu Twiga Stars katika kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia leo alipoitembelea  Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania almaarufu Twiga Stars katika kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
    
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wachezaji wa  Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania almaarufu Twiga Stars alipoitembelea timu hiyo leo katika kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg wakiminya kitufe kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa mradi wa Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme KV 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na vituo vya kupooza umeme KV 220/33  katika sherehe zilizofanyika Songea mkoani Ruvuma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg mara baada ya uzinduzi wa mradi wa Ujenzi wa njia kuu wa umeme KV 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na vituo vya kupooza umeme KV 220/33  katika sherehe zilizofanyika Songea mkoani Ruvuma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg wakiangalia mradi huo wa umeme utakavyosambaza umeme katika maeneo mbalimbali kutoka kutoka Makambako hadi Songea
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg, Waziri wa Nishati Medard Kalemani wakielekea eneo la uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa usafirishaji wa umeme.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg wakipungia mikono wananchi waliohudhuria katika sherehe hizo za uzinduzi wa mradi wa umeme.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa mradi wa Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme KV 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na vituo vya kupooza umeme KV 220/33  katika sherehe zilizofanyika Songea mkoani Ruvuma.
   Moja ya kituo cha kupooza umeme cha Songea.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua kituo Kikuu cha Mabasi cha Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo Kikuu cha Mabasi cha Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
   Sehemu ya wananchi wa Songea mkoani Ruvuma wakiwa ndani ya Uwanja wa mpira wa Majimaji kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. PICHA NA IKULU  =====  ========   ========  =======

  Rais Magufuli aendelea na ziara Ruvuma azindua mradi wa umeme na aweka jiwe la msingi la stendi na barabara


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Aprili, 2019 amezindua mradi wa njia ya umeme ya msongo wa KV 220 kutoka Makambako hadi Songea na ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha mabasi na barabara za lami katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

  Sherehe za uzinduzi wa mradi wa njia ya umeme zimefanyika katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Unangwa Mjini Songea na zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Anders Sjöberg, Mawaziri, Wabunge na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Godfrey Zambi.

  Mradi huo umehusisha ujenzi wa njia ya umeme yenye urefu wa kilometa 245, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Makambako, ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Madaba na Songea na usambazaji wa umeme wa msongo wa kilovoti 33 zenye urefu wa kilometa 900 zilizounganishwa kwa wateja 22,700 katika Wilaya za Njombe, Ludewa, Mji wa Makambako, Songea Vijijini, Songea Mjini, Namtumbo na Mbinga.

  Ujenzi wa mradi huo umegharimu shilingi Bilioni 216 na Milioni 941, fedha ambazo zimetolewa kwa mkopo nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Sweden na Serikali ya Tanzania, na baada ya kukamilika kwake Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limezima mitambo ya kuzalisha umeme kwa mafuta katika vituo 5 na hivyo kuokoa shilingi Bilioni 9.8 kwa mwaka.

  Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutilia mkazo wa kuhakikisha mradi huo unaanza kutekelezwa mara alipoingia madarakani na kwamba hivi sasa Mkoa wa Ruvuma wenye mahitaji ya megawati 12 za umeme unapata megawati 48 zitakazowezesha uanzishaji wa viwanda na vijiji vyote kupatiwa umeme ifikapo mwaka 2012.

  Mhe. Kalemani amebainisha kuwa tangu Mhe. Rais Magufuli aingie madarakani idadi ya vijiji vilivyopatiwa umeme kupitia Wakala wa Umeme Vijiji (REA) imeongezeka kutoka 2,018 hadi kufikia 6,464 (sawa na ongezeko la asilimia 214).

  Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Andrers Sjöberg ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa uhusiano na ushirikiano mzuri na Sweden ambao umesaidia kutekelezwa kwa miradi mingi ya maji tangu miaka ya 90 na baadaye kufuatiwa na miradi ya kupeleka umeme vijijini ambako wananchi wengi wamenufaika hususani wanawake.

  Kwa upande wake, Mhe. Rais Magufuli ameishukuru nchi ya Sweden kupitia SIDA kwa ufadhili wake katika mradi huo na ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo pamoja na mradi mkubwa ambao Tanzania inaujenga hivi sasa wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji utasaidia kuinua uchumi kupitia viwanda na pia utasaidia kuokoa mazingira kwa kuwa wananchi watatumia umeme badala ya kuni na mkaa ambao unapatikana kwa kukata miti.

  “Takwimu zinaonesha ekari 400,000 za miti huvunwa kila mwaka kwa lengo kupata kuni na mkaa wa kupikia, hii yote inasababishwa na umeme kidogo na wa gharama kubwa tulionao, tunapotekeleza miradi hii tutaokoa uharibifu huu wa mazingira, kwa hiyo nakuomba Mhe. Balozi ukawaeleze Mabalozi wenzako kuwa Tanzania tunapotekeleza miradi hii tunataka kuimarisha uchumi wetu na pia kuokoa misitu yetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

  Ametoa wito kwa Sweden na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Tanzania katika uzalishaji wa nishati ya umeme kupitia vyanzo mbalimbali vikiwemo gesi, makaa ya mawe, urani, upepo na joto ardhi, na pia amewataka Watanzania waongeze juhudi katika utunzaji wa mazingira.

  Kabla ya kuzungumza na wananchi wa Manispaa ya Songea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Majimaji, Mhe. Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi katika eneo la Shule ya Tanga, na ujenzi wa barabara za Manispaa hiyo ambapo ameagiza miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakikana.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amesema ujenzi wa mradi huo ulioanza tarehe 25 Machi, 2018 unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Septemba, 2019 kwa gharama ya shilingi Bilioni 6.2 na utahusisha ujenzi wa kilometa 2 za barabara, eneo la kuegesha mabasi 92 na ujenzi maegesho ya magari mengine na huduma mbalimbali. Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri 18 zinazotekeleza mradi kama huo hapa nchini.

  Majira ya jioni, Mhe. Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Manispaa ya Songea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Majimaji ambapo amewahakikishia kuwa Serikali anayoiongoza inatekeleza miradi hii mikubwa ili kuimarisha ustawi wa wananchi na kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zikiwemo ujenzi wa viwanda.

  “Juzi nimefungua barabara ya Mtambaswala – Mangaka – Nakapanya – Tunduru yenye urefu wa kilometa 202, jana nimefungua barabara ya Tunduru – Namtumbo yenye urefu wa kilometa 193, leo nimezindua mradi mkubwa wa umeme ambao umewaletea umeme mwingi kupita mahitaji yenu na sasa tunaanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Lumecha – Londo – Ifakara, hizi zote ni juhudi za kuimarisha fursa za uchumi, nataka mnufaike” amesema Mhe. Rais Magufuli.

  Mawaziri wengine waliongozana na Mhe. Rais Magufuli wamewahakikishia wananchi wa Ruvuma kuwa Serikali imeanza kuchukua hatua za kuhakikisha wanapata pembejeo za kilimo za kutosha na kwa gharama nafuu, kuimarisha miundombinu ya barabara na ukarabati wa uwanja wa ndege.

  Akiwa uwanjani Majimaji, Mhe. Rais Magufuli amezungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songea ambapo ametoa shilingi Milioni 5 kwa ajili ya shule hiyo na ameiagiza TAMISEMI kuhakikisha inatatua tatizo la mabweni na vyoo.
  Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli kesho anaendelea na ziara yake hapa Mkoani Ruvuma ambapo ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Mbinga – Mbambabay na kuzungumza na wananchi.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Songea
  06 Aprili, 2019

  0 0

  Na Woinde Shizza Globu ya jamii

  Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema kuwa serikali itaendelea kutambua
  mchango wa hayati Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine kwani alikuwa mfano
  katika kupambana na vitendo vya rushwa pamoja na kukemea ufisadi.

  Majaliwa aliyasema hayo katika Uwanja wa Shekhe Amri Abeid wakati wa
  mbio za madhimisho za kumbukumbu ya kifo cha hayati Waziri Mkuu Edward
  Moringe Sokoine.

  Alisema serikali itaendelea kumuenzi hayati Sokoine kwa kuchapa kazi kuwa
  bidii kwani mbio hizo ni sehemu ya uimarishaji wa afya ikiwemo kudumisha
  amani na upendo.Alipongeza mafanikio makubwa ya kimichezo nchini pamoja na kuipongeza timu ya vijana wenye umri wa miaka 17 na kusisitiza kuwa hii ni historia kwa nchi ya Tanzania.

  "Hii ni historia na Tanzania inawezekana kwani ushindi Tanzania unawezakana
  na ni zamu yetu "Pia alipongeza Bondia Hassan Mwakinyo kwa kazi nzuri anayofanya ikiwemo kuitikia heri timu ya Simba.Naye Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza alisema serikali itaendelea kushirikiana na Chama cha Riadha Tanzania katika kuhakikisha vipaji vingi vinaibuliwa ikiwemo Tanzania kung'aa zaidi katika michezo mbalimbali.

  Awali mtoto wa hayati Sokoine, Namelock Sokoine alishukuru serikali kwa
  kuleta maendeleo ikiwemo katika sekta ya afya, miundombinu na nk na
  kusisitiza kuwa hayati baba yake, Edward Moringe Sokoine alipokuwa hai
  aliweza kutoa asilimia 50 ya mshahara wake kwaajili ya watu maskini.

  Hivyo washiriki wa mbio hizo wamelipia fedha zao na wamechangia maskini
  ambao hawana uwezo.Awali Rais wa Chama Cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka alisema michezo hiyo ni hamasa na ni kumbukumbu ya kifo cha hayati Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine

  Alisema mwaka huu timu ya riadha itakwenda kushiriki mashindano ya riadha
  Nchini Qatar na nchini Tokyo Japani na kusisitiza wadhamini mbalimbali
  kujitokeza kwaajili ya kudhamini mchezo huo wa riadha na aliwashukuru
  wadhamini wa Dstv pamoja na Mamlaka ya Hifadhi(NCAA) kwakuwezesha kudhamini mashindano hayo.

  "Tunapata hamasa tunapoona vipaji vipya vinaibuliwa kwani michezo ni ajira
  hivyo ninaomba wadhamini wengi zaidi kujitokeza " Pia alitoa rai kwa watu wanaoanzisha mashindano hayo ya riadha kila Mkoa na Wilaya wahakikishe wanafuata taratibu na sheria za ikiwemo kusajili mbio hizo, zawadi pamoja na kupewa masharti ya mbio za riadha.

  Washindi wa mbio hizo walipewa medali fedha katika mashindano hayo ya
  kilomita 21 ni Felix Simbu aliyeshika nafasi ya pili, mshindi wa kwanza ambapo amepokia kitita cha shilingi milioni moja Joseph Panga na Faraja Lazaro kwa upande wa wanaume akiondoka na shilingi laki nane.

  Huku upande wa wanawake kilomita 21 wakiwa ni Failuna Matanga, mshindi wa
  pili Magdalena Shani na mshindi wa tatu Natalia Sule huku watoto wanawake kilomita tano Glory Patrick, Sharon Boniface na wanaume ni Said Barae, Omary Ramadhani na Msabaha Idd.
  Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa akiwapa zawadi washindi wa kwanza wa kilometa 21katika mashindano ya mbio za moringe marathon

older | 1 | .... | 1832 | 1833 | (Page 1834) | 1835 | 1836 | .... | 1904 | newer