Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI NYONGO AFUNGA MITAMBO YOTE YA KUCHENJULIA MADINI KAHAMA

0
0




Kutoka kulia, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha wakiangalia steel wire iliyokuwa na mabaki ya kaboni yaliyonasa, kwenye ziara yake ya kushtukiza katika kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group tarehe 31 Machi, 2019.
Kutoka kushoto Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha wakishuhudia kaboni ikichomwa ili kupata dhahabu katika kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group tarehe 31 Machi, 2019.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na vyombo vya habari juu ya maamuzi ya Serikali kuhusiana na udanganyifu uliofanywa na kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group



Na Greyson Mwase, Kahama

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amefunga mitambo yote ya kuchenjulia madini ya dhahabu Wilayani Kahama baada ya kubaini udanganyifu mkubwa kwenye uchenjuaji wa madini.

Naibu Waziri Nyongo amechukua hatua hiyo kwenye ziara yake aliyoifanya mapema leo tarehe 31 Machi, 2019 Wilayani Kahama yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Kamishna Msaidizi, Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Saidi Ali, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama, Andrea Fabian, wataalam kutoka Tume ya Madini, wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na waandishi wa habari.

Akiwa katika ziara hiyo, alifanya ziara ya kushtukiza katika kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group inayomilikiwa na Theogenes Zacharia pamoja na mwenzake aliyejulikana kwa jina la Antidius na kubaini kampuni hiyo imekuwa ikiwaibia wateja wake kupitia mfumo wa uchenjuaji wa madini ya dhahabu.

Akiwa ameambatana na msafara wake mara baada ya kuwasili katika kampuni hiyo alioneshwa na wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini waliopewa kazi maalum ya kuchunguza mfumo wa uchenjuaji wa dhahabu wa kampuni hiyo, sehemu ya mabomba ya mfumo iliyoharibiwa kwa makusudi kwa lengo la kunasa kiasi cha dhahabu kabla ya kufikishwa katika chombo maalum cha kupokelea kwa ajili ya mteja.

Alisema kuwa, kiasi cha kaboni iliyokuwa na dhahabu iliyokamatwa ilipelekwa kwa ajili ya kuchenjuliwa ili kubaini kiasi cha adhabu kilichokuwa kimeibiwa na kusisitiza kuwa baada ya kuchenjuliwa kiasi cha gramu 102 kiligundulika kutaka kuibwa.

Katika hatua nyingine mbali na kufunga mitambo ya kuchenjua madini ya dhahabu katika Wilaya ya Kahama, Naibu Waziri Nyongo alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya ya Kahama kuhakikisha watuhumiwa wote wa kampuni ya Ng’ana Group wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Aidha, Naibu Waziri Nyongo alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Madini wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama na uchunguzi kuanza mara moja.

Katika hatua nyingine, Nyongo alisema kuwa maafisa madini wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama wataanza kufungua mtambo mmoja mmoja wa kuchenjua madini ya dhahabu mara baada ya kujiridhisha na uendeshaji wake.

Awali akielezea siri ya wizi unaofanywa na kampuni ya Ng’ana Group, mmoja wa wateja kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Joseph Magunila & Partners, aliyepeleka kaboni kwa ajili ya kuchenjuliwa ili kupata madini ya dhahabu, Wema Shibitali alisema kuwa, wakati zoezi la uchanjuaji likiendelea alishangaa kupata kiasi kidogo cha dhahabu tofauti na kaboni iliyokuwa imewekwa.

Alisimulia kuwa aliomba maafisa kutoka vyombo vya dola kufungua mfumo ili kubaini kama kuna madini yamebaki na kuongeza kuwa mara baada ya mfumo kufunguliwa walibaini kiasi kikubwa cha kaboni kilichokuwa kimebaki kwenye mfumo.

Aidha Shabitali aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuwatetea wachimbaji wadogo kwa kuwa wamekuwa wakiibiwa na wachenjuaji wa madini ya dhahabu kwa muda mrefu.

Wakati huo huo akizungumza katika msafara huo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha mbali na kumpogeza Naibu Waziri Nyongo kwa kutembelea Wilaya yake na kushughulikia changamoto mbalimbali kwenye Sekta ya Madini, alisema kuwa ziara hiyo imewapa mwanga zaidi wa mbinu zinazotumiwa na wachenjuaji wa madini na kusisitiza kuwa ataendelea kusimamia kwa karibu zaidi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Aliwataka wachimbaji na wachenjuaji wa madini nchini kuunga juhudi zinazofanywa na Rais wa Awamu ya Tano pamoja na Serikali yake, Dkt. John Pombe Magufuli katika kulinda rasilimali za madini kwa kuwa waaminifu kwenye ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.

WAKULIMA WA TUMBAKU WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWALETEA FAO LA MATIBABU

0
0

Mmoja wa wakulima wa tumbaku katika kijiji cha kasokola akichambua zao hilo
Baadhi ya wakulima wa kasokola wakisiliza elimu ya Bima ya Afya kutoka kwa wataalamu wa mfuko huo
Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Juma Michael akitoa elimu juu ya mpango wa ushirika afya kwa wakulima wa chama cha ushirika kasokola
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Katavi Luhigiza Sesemkwa akizungumza na wakulima katika kijiji cha Kasokola

……………………………..


Na Ripota Wetu… Katavi


Wakulima wa zao la tumbaku katika kijiji cha Kasokola katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameishukuru serikali kwa kuwaanzishia mpango wa Ushirika Afya; unaosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya; utakaowawezesha kupata matibabu kwa urahisi bila malipo kwa kipindi cha mwaka mzima; na hivyo kuwezesha familia zao kupata matibabu na kuondokana na adha ya kutegemea dawa za kienyeji pindi wanapougua kutokana na kukosa fedha za matibabu

wakulima hao wametoa shukurani hizo katika mkutano mkuu wa sita wa chama cha msingi cha ushirika cha kasokola ambapo walisema mpango huo utaondoa adha ya kushindwa kutibiwa kwa kukosa fedha hasa katika msimu ambao sio wa mavuno

Bwana Hussein Mobi ni mmoja wa wakulima wa tumbaku katika kijiji hicho, alisema mwaka uliopita alitakiwa kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa tumbo na alitumia gharama kubwa lakini ujio wa mpango huo utakuwa mkombozi kwa wakulima walio wengi

Aidha wakulima hao walikitaka chama hicho kuandaa utaratibu wa kuwakata fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kuchangia mfuko wa bima ya afya

Akizungumzia mpango huo uliozinduliwa rasmi na waziri mkuu mheshimiwa Kassim Majaliwa Julai mwaka jana; Mrajis Msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Katavi bwana Luhigiza Sesemkwa amesema serikali imeona iko haja ya kuwajumuisha wakulima katika fao la matibabu

Naye afisa masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya bwana Juma Michael alitaja baadhi ya faida za mfuko huo kuwa ni pamoja na kuwa na hakika ya kupata matibabu wakati wowote kwa zaidi ya vituo 7000 vya afya hapa nchini na hospitali mbalimbali

Aliongeza kuwa kwa sasa shirika linafanya zoezi la kutoa hamasa kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchi nzima ili wapate kuelewa umuhimu wa mfuko huo na kujiunga nao

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Katavi Bwana Said Juma alisema wakulima wa mazao matano ya kimkakati ikiwemo pamba, kahawa, korosho, chai na tumbaku wanahusishwa na mpango huo kuipitia vyama vya ushirika

Ametoa wito kwa wakulima kujiunga na mfuko ili kuondoa mashaka ya kupata matibabu pale wanapougua wakati familia hazina fedha hasa ukizingatia kuwa wakulima wanapata fedha kwa msimu wa mauzo ya mazao yao

WASAIDIZI WA KISHERIA WAPEWA MAFUNZO YA SHERIA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA KWENYE MASOKO

0
0
Jumla ya Wasaidizi wa Kisheria 36 katika Masoko ya Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa mafunzo ya sheria na Shirika la Agape AIDS Control Programme ili wakasaidie kutoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara kwa lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wasichana na wanawake wafanyabiashara sokoni. 

Mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa siku tatu katika Ukumbi wa Katemi Hoteli Mjini Shinyanga yamefungwa leo Jumapili Machi 31,2019 na Mkurugenzi wa shirika la Agape,John Myola. 

Myola amesema katika mafunzo hayo,Wasaidizi wa Kisheria wamepewa elimu kuhusu sheria mbalimbali na kutambua haki za binadamu,haki za kiuchumi,jinsi ya kufanya biashara,ukatili wa kijinsia na mahali sahihi pa kutoa taarifa za vitendo vya kikatili. 

Amesema mafunzo hayo ni Mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” kwa lengo la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabishara katika masoko unaofadhiliwa na shirika la UN WOMEN kupitia Shirika la kitaifa la Equality for Growth (EfG). 

“Naomba mafunzo haya mliyopata yatakuwa msaada kwenu binafsi lakini pia nendeni mkawasaidie wananchi,katoeni huduma bila upendeleo na bila kuonea mtu ili kuhakikisha kila mfanyabiashara anapata haki sokoni”,alisema Myola. 

“Nawashauri pia kutunza siri za watu,msiwe waoga kutatua migogoro inayotokea sokoni,naamini mtakuwa mstari wa mbele kupiga vita dhuluma mbalimbali ikiwemo rushwa ya ngono na kuwapigania akina mama na wasichana ambao wana maumivu ya kutendewa vitendo vya kikatili”,aliongeza Myola. 

Aliyataja masoko ambako mradi huo unatekelezwa katika manispaa ya Shinyanga kuwa ni soko Kuu Mjini Shinyanga,Kambarage,Nguzo Nane,Ibinzamata,Ngokolo Mitumbani na Majengo Mapya.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape,John Myola akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Sheria ya siku tatu kwa Wasaidizi wa Kisheria ili wakataokwenda kutoa elimu kwa wafanyabiashara kwenye masoko yaliyopo katika Manispaa ya Shinyanga ili kukabiliana na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape,John Myola akiwasisitiza Wasaidizi wa kisheria kutumia mafunzo waliyopata kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko.
Wasaidizi wa Kisheria kwenye masoko wakimsikiliza Myola.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape,John Myola akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Awali Afisa Masoko Manispaa ya Shinyanga,Alex Hinda akitoa mada kuhusu namna bora ya kufanya biashara na kuwataka wafanyabiashara kujitahidi kutunza taarifa zao za fedha.
Afisa Masoko Manispaa ya Shinyanga,Alex Hinda akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa ukumbini.
Wasaidizi wa kisheria wakiwa ukumbini.
Wasaidizi wa Kisheria wakifanya Mtihani wa kipimo cha uelewa wa mafunzo waliyopatiwa kwa kipindi cha siku tatu kuhusu masuala mbalimbali ya sheria ili kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
Wasaidizi wa Kisheria wakifanya mtihani.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo kufungwa.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo kufungwa.icha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

KILIMANJARO SAR WATIMIZA MWAKA MMOJA,WATANGAZA KUTOA HUDUMA BURE YA UOKOAJI KWA WAONGOZA WATALII MLIMA KILIMANJARO

0
0
Kikosi cha uokoaji kwa kutumia Helkopita kikiwa katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kutoa msaada kwa wageni .
Ndege aina ya Helkopta inayotumiwa na Shirika la Kilimanjaro SAR katika kufanya shughuli za uokoaji katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shrika la Kilimanjaro SAR,Ivan Brown akitoa taarifa za shirika hilo kwa  wanahabari (hawapo pichani) kuhusu shughuli mbalimbali za uokoaji ilizofanya katika kipindi cha mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu katika shirika la Kilimanjaro SAR,Amour Abdalah akizungumza na wanahabari (hawapo pichani kuhusu mwaka mmoja wa operesheni ya shirika hilo.

Na Dixon Busagaga wa globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA la Kilimanjaro SAR linayojishughulisha na utoaji wa huduma ya utafutaji na uokoaji wa watalii wanaopata matatizo ya kiafya katika maeneo yenye muinuko ikiwemo  Mlima Kilimanjaro limetangaza kutoa bure huduma zake kwa  waongoza watalii  pamoja na wapagazi .

Hatua hiyo imefikiwa baada ya  baadhi ya watu wanaojishughulisha na shughuli za kusaidia wageni katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kupata matatizo ya kiafya na kushindwa kupata huduma huku kundi kubwa la watu hao kukosa  Bima za Afya ,wengine wakikosa kabisa kipato cha uhakika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Kilimajaro SAR,Ivan Brown alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya shughuli zilizofanywa na kampuni hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanza operesheni za uokoaji kwa kutumia njia ya Helkopta.

“Sisi ni wa kwanza na pekee katika Dunia hii tunaotoa huduma ya uokoaji Bure kwa wote wanaofanya shughuli za mlima ,tunafahamu Wapagazi,Waongoza watalii hawana bima, hawana njia zozote za kujipatia kipato ambazo zingesaidia katika uokoaji”alisema Brown .

“Watakaopata matatizo ya kiafya au ajali wawapo  mlimani wanaweza kuwasiliana nasi ,tutaaenda juu na kumuokoa bila ya gharama zozote kwa sababu mipango yetu ni kuokoa maisha ,ndio sababu tunasema kwa waongoza watalii au wapagazi , uhai ndio kipaumbele cha kwanza”aliongeza Brown .

Alisema shirika hilo likiwa linaadhimisha mwaka mmoja wa utoaji huduma katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro tayari imetoa matibabu kwa zaidi ya watu 250 huku akieleza kuweka rekodi ya kwanza Afrika kwa kumuokoa mgonjwa aliyekuwa katika hali mbaya ,umbali wa Mita 5000.

 “ Tayari tumetoa huduma kwa zaidi ya wagonjwa 250 na miongoni mwao aliingia kwenye historia Afrika ya kuwa mtu wa kwanza kuokolewa kwa na Helkopta katika eneo lenye urefu wa Mita 4800 ,katika kambi ya Cosovo Mlima Kilimanjaro June 22 mwaka jana”alisema Borown .

“Tumeokoa waongoza watalii na wapgazi 50 bila malipo ,bado tunashukuru kwa ushirikiano na msaada  kutoka kwa taasisi mbalimbali kwa kuruhusu mazingira kwa shirika letu kuweza kufanya shughulizaek za uokoaji maisha kwa urahisi.

Mbali na shughuli ya utafutaji na uokoaji ,Kampuni ya Kiliamanjaro SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph kwa kuanzisha Kliniki ya kisasa  “Kilimanjaro SAR High Altitude Medicine Clinic” kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu kwa magonjwa yatokanayo na muinuko .

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa shirika hilo ,Amour Abdalah alisema kliniki hiyo ya kwanza Afrika imeanzishwa baada ya kubaini kwamba mgonjwa anapookolewa kutoka mlimani anahitaji pia kupata huduma stahiki za matibabu .

“Magonjwa ya mlimani yanahitaji ,matibabu maalumu ,na ndio sababu tukaanza na operesheni ya kutoa huduma kwa kutumia Helkopta ikiwa ni huduma ya kwanza kwa afrika na baadae mgonjwa huyu hufikishwa katika kliniki yetu na kupatiwa matibabu”alisema Abdalah.

Alisema wazo la kuanzishwa huduma hizo lilianza mwaka 2013  baada ya kuona kwamba utoaji wa huduma sahihi ya uokoaji na vifaa vya kitabibu vilihitajika na si pekee kwa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro bali pia kwa Sekta ya Utalii Tanzania.

Abdalaha alisema kwa sasa kampuni ya Kilimanjaro SAR imepanua wigo wa utoaji wa huduma za utafutaji na uokoaji katika maeneo mengine zikiwemo hifadhi za taifa za Serengeti,Arusha,Manyara,Ruaha na Mikumi.

 “Mlima Kilimanjaro umekuwa na wageni wengi wakifanya shughuli za utalii ,na wengi wao baada ya kuapanda mlima Kilimanjaro wanaendelea na safari nyingine kutizama vivutio vya utalii,jambo kubwa tunalofanya katika sekta ya utalii ,tumewahakikishia usalama wageni wanaokuja Tanzania kupanda Mlima Kilimanjaro “alisema Amour.

Katika kipindi cha mwaka mmoja Shirika la uokoaji ya Kilimanjaro SAR tayari imejinyakulia tuzo tano za uongozi moja ikiwa ni ya Tanzania ambazo ni “C.E.O of the Year 2018 Afrika “ ,“ H.R of the Year 2018 Afrika” ,“Dream Company to work for “ , “Employer Brand Afrika “  ,” Shirika Bora la kati Tanzania “ tuzo iliyotolewa na ATE .

RMO SIMANJIRO ATOA UTARATIBU MPYA KUINGIA NDANI YA UKUTA WA MAGUFULI

0
0


Ofisa madini mkazi wa kimkoa wa kimadini wa Simanjiro Daudi Ntalima akizungumza juu ya utaratibu wa kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani (maarufu kama ukuta wa Magufuli).


Wanawake wanaojihusisha na shughuli mbalimbali wakiwa kwenye mstari wa kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Wanawake wachekechaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakifanya kazi yao ya kuchekecha mabaki ya udongo unatolewa migodini.
………………………..
Ofisa madini mkazi wa kimkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima amepiga marufuku uuzwaji wa bia, viatu na wamachinga, pombe haramu ya gongo na vibanda vya uuzwaji baruti, ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani. 

Ntalima aliyasema hayo wakati akizungumzia utaratibu mpya wa kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi hiyo. Alisema utaratibu huo mpya utaanza kutumika April mosi mwaka huu na hakutakuwa na ruhusa ya watu kuingia na kukaa bila kazi maalum ndani ya ukuta huo. 

Alisema migodi yote ndani ya ukuta inatakiwa kuzungushiwa uzio wa bati ndani ya miezi miwili na migodi au leseni ambazo hazifanyiwi kazi zitafutwa.
“Vibanda au makazi yoyote nje ya uzio wa mgodi husika hayaruhusiwi tena na hairuhusiwi kukata mti wowote ndani ya ukuta bila kibali,” alisema Ntalima.
Alisema hairuhusiwi mtu yeyote kuonekana maeneo ya machimbo tofauti na maeneo ya masoko bila kibali na vibanda au makazi yoyote nje ya uzio wa mgodi hayaruhusiwi. 

Alisema maeneo mapya ya masoko yaliyotengwa kwa kupewa namba maalum ya kufanya biashara wanapaswa kuwa na kitambulisho cha mjasiriamali.
“Watu wote wanaofanya biashara mbalimbali ndani ya ukuta tofauti na uchimbaji madini wanapaswa kufuata utaratibu huu mpya uliotolewa,” alisema Ntalima. 

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Mirerani, walipongeza hatua hiyo kwani siyo vyema kwa kila mtu anapaswa kuingia ndani ya ukuta hadi migodini. Hassan Juma alisema hivi sasa kuna watu wengi kwenye maeneo ya migodini huku huduma za vyoo ikiwa ni tatizo hivyo kuhofia magonjwa ya milipuko pindi mvua zikinyesha. 

Kaanael Minja alisema biashara nyingine ambazo hazina umuhimu wa kuwepo ndani ya ukuta zinapaswa kukomeshwa hasa wamachinga na wanawake wanaojiuza kwa wanaApolo. “Watu ni wengi migodini vumbi la ulanga linatimka na kuhofia ugonjwa wa Silikosis pia baada ya watu kuruhusiwa kuna wanawake wanaojiuza migodini,” alisema Minja.

WAZIRI WA MADINI UGANDA, ATEMBELEA TANZANIA

0
0
Kutoka kushoto, Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella wakimsubiri Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris pamoja na ujumbe wake kabla ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza tarehe 01 Aprili, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto mbele) akiwaongoza Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo, Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris pamoja na ujumbe wake kwenye ukumbi wa mikutano.
Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris (wa pili kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella
Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo, akielezea mafanikio ya nchi ya Tanzania kwenye usimamizi wa sekta ya madini kwa ujumbe wa Uganda.
Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris akifafanua jambo kwenye mkutano huo.

Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo pamoja na Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris (waliosimama katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka nchini Uganda na Tanzania.



Greyson Mwase na Remija Salvatory, Mwanza 


Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris pamoja na ujumbe wake wameanza ziara nchini Tanzania leo tarehe 01 Aprili, 2019 yenye lengo la kujifunza namna sekta ya madini nchini Tanzania inavyoendeshwa. Waziri Lokeris ameongozana na maafisa waandamizi kutoka Serikali ya Uganda pamoja na wawakilishi wa wachimbaji wadogo. Waziri wa Madini Nchini Uganda pamoja na ujumbe wake walipokelewa na Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. 

Akizungumzia lengo la ziara hiyo kupitia mahojiano maalum aliyoyafanya na vyombo vya habari, mara baada ya kupokelewa na Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo, Waziri Lokeris alisema kuwa lengo la ziara yake ni kujifunza sheria na kanuni za madini nchini Tanzania zinavyosimamiwa vyema pamoja na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji wa madini nchini Tanzania kwa vitendo kupitia wawekezaji waliowekeza nchini pamoja na wachimbaji wa wadogo wa madini. 

“Tulifanya utafiti na kubaini Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa wa madini na uzoefu mkubwa kwenye uchimbaji wa madini na tumeona wachimbaji wadogo wakisaidiwa sana na Serikali ya Tanzania,” Alisema Lokeris. 

Aliongeza kuwa, kati ya maeneo wanayotarajia kujifunza ni pamoja na ushirikishwaji wa wazawa kwenye shughuli za uchimbaji wa madini (local content) utoaji wa huduma kwa jamii inayozunguka shughuli za uchimbaji wa madini (corporate social responsibility), usimamizi wa sheria ya madini pamoja na kanuni zake. 

Aliongeza kuwa ushirikiano wa Tanzania na Uganda umekuwa ni wa muda mrefu na kusisitiza kuwa Serikali ya Uganda ipo tayari kujifunza na kubadilishana uzoefu kwenye usimamizi wa sekta ya madini. 

Aliendelea kusema kuwa, Serikali ya Tanzania inapenda kuona wananchi wake hususan waishio vijijini wananufaika na sekta ya madini kupitia uboreshwaji wa huduma za jamii kama vile elimu huduma za afya, na ili kuhakikisha wananchi wake wananufaika, Serikali imeamua kutuma wataalam wake Tanzania kujifunza kutokana na hatua kubwa iliyopigwa na nchi ya Tanzania kwenye usimamizi wa sekta ya madini. 

Akielezea changamoto kwenye usimamizi wa sekta ya madini kwa nchi ya Uganda, Waziri Lokeris alieleza kuwa ni pamoja na kutokuwa na teknolojia ya kutosha kwenye uongezaji thamani wa madini pamoja na utoroshwaji wa madini unaofanywa na wachimbaji wadogo. 

Wakati huohuo Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo alisema kuwa nchi ya Tanzania ipo tayari kutoa uzoefu wake kwenye usimamizi wa sekta ya madini kwa nchi ya Uganda kupitia wataalam wake. 

Alisema katika ziara ya ujumbe huo, mbali na nchi ya Tanzania kutoa uzoefu wake kwenye usimamizi wa sekta ya madini nchini, wanatarajia kuupeleka ujumbe huo kwenye soko la madini mkoani Geita lililozinduliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kasim Majaliwa pamoja na baadhi ya mitambo ya kuchenjulia dhahabu. 

Akielezea mikakati ya Serikali ya Tanzania kwenye usimamizi wa sekta ya madini, Naibu Waziri Nyongo alieleza kuwa ni pamoja na uboreshaji wa sheria ya madini pamoja na kanuni zake ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa wachimbaji wadogo wa madini. 
Alieleza mikakati mingine kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini katika kila mkoa ili kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini.

DKT ANNA MGHWIRA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MVUA ILIYOAMBATANA NA UPEPO KILIMANJARO.

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakitembelea maeneo yaliyoathirika na mvua iliyonyesha juzi ikiambatana na upepo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira akizungumza na mmoja wa maafisa wa Magereza waliokuwa katika uismamizi wa wafungwa wakati wa kukata miti mikubwa iliyofunga barabara baada ya kuanguka. 
 Moja ya miti mikubwa iliyoanguka katika ya barabara ukiwa umekatwa. 
 Kukatika kwa miti hiyo kulikuwa ni fursa kwa watu wengine waliojitokeza kuokota kuni. 
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akitizama mafundi wa shirika la umeme Tanesco wakati wakijaribu kurejesha miundo mbinu ya umeme iliyoharibika kufuatia mvua iliyoambatana na upepo. 
 Mafundi wa TANESCO wakijaribu kurejesha nyaya zilizokatika . 
 Sehemu ya nyaya zilizokatika kufuatia mvua hiyo. 
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakitembelea Kiwanda cha kuzalisha vifaranga vya kuku ambacho kuta zake zilianguka pamoja na mti mkubwa kukatika. 
 Mti ulikuwa jirani kabisa na jengo lililokuwa na mashine za kuangulia vifaranga na kuharibu mashine mbili pamoja na kuahribu mayai zaidi ya 15,000. 
 Mafundi wakijaribu kuondoa sehemu ya mti ulioangukia jengo hilo. 
 Sehemu ya mashine hizo. 
 Mayai yakiwa kwenye mashine tayari kwa ajili ya kuanguliwa. 
 Vifaranga vya kuku vikiwa katika mashine baada ya kuanguliwa. 
 Kuku wakubwa wakiwa katika kiwanda hicho kwa ajili ya mayai. 
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira akitizama moja ya nyumba ya mwalimu katika shule ya sekondari ya Old Moshi ambaye paa la nyumba hiyo liliezuliwa kutokana na upepo. 
 Nyumba nyingine katika shule ya sekondari ya Old Moshi ikiwa imeezuliwa na upepo. 
 Moja ya miti iliyoanguka katika shule ya sekondari ya Old Moshi ,mti huu uliangukia bweni la wananfunzi bahati nzuri haukuweza kusababisha madhara. 
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Annag Mghwira akitoa pole kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Old Moshi alipowatembelea kuwajulia hali baada ya mvua iliyoaambatana na upepo kuharibu baadhi ya miundo mbinu zikwemo nyumba za walimu. 
 Baadhi ya wanafunzi katika shule ya sekondari ya Old Moshi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira (hayupo pichani).
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

NMB YATOA MSAADA WA MABATI,VITANDA NA MADAWATI CHUO CHA VETA KALAMBO MKOANI RUKWA

0
0
Naibu Waziri Tamisemi Mh Josephat Kandege akizungumza jambo mara baada ya kukabidhiwa Msaada wa Mabati 802 ,Vitanda 8 vya Hospital pamoja na Madawati 50 vyenye Jumla ya Thamani ya shilingi Mil 35 Kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ,Straton Chilongola Mwenye Suti nyeusi (kulia) hafla ambayo imefanyika katika Soko la Wakulima Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.March 30,2019.
Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Straton Chilongola(Kulia) akimkabidhi Naibu Waziri wa Tamisemi Mh Josephat Kandege msaada wa Vitanda 8 vilivyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya Chuo cha Veta Kalambo Mkoani Rukwa,Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangambo na Juliet Benyura Mkuu wa Wilaya ya Kalambo ,hafla ambayo imefanyika katika Soko la wakulima Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo March 30,2019.
Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Straton Chilongola(Kulia) akimkabidhi Madawati 50 Naibu Waziri wa Tamisemi Mh Josephat Kandege (MB) kwa ajili ya Chuo cha Veta Kalambo Mkoani Rukwa,Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangambo , Vitu vingine vilivyotolewa na Benki hiyo ya NMB kwa ajili ya Chuo hicho ni pamoja na Vitanda 8 vya hospital,Mabati 802 ,hafla ambayo imefanyika katika Soko la wakulima Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo March 



RAIS DKT. MAGUFULI ATOA POLE KWA MBUNGE WA IRINGA MJINI MCHUNGAJI PETER MSIGWA ALIYEFIWA NA DADA YAKE JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuwasili Kimara kwa ajili ya kutoa heshma za Mwisho kwa mwili wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika jeneza la marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Msibani pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakwanza kulia, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa wakwanza kushoto aliyekaa pamoja na ndugu zake kufatia kifo cha Dada yake marehemu Tryphosa Simon Sanga kilichotokea juzi jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili Kimara msibani huku akizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa ambaye alifiwa na Dada yake marehemu Tryphosa Simon Sanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wakati akitoka kutoa heshma za mwisho kwenye msiba wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka eneo la msibani Kimara mara baada ya kutoa heshma za mwisho kufatia kifo cha wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA DC MURO.

0
0

Kamati ya Bunge, Mifugo, Kilimo na Maji imempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro kutokana na mkakati wake wa kukwamua miradi ya maji iliyokwama kwa muda mrefu katika wilaya hiyo.

Hayo yamejiri kwenye ziara ya kamati hiyo wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya kamati ya Bunge Mifugo, Kilimo na Maji kufanya ziara yakukagua miundo mbinu ya miradi mikubwa ya maji ya vijiji 10 inayoendelea kujengwa yenye lengo la kuondoa changamoto ya uhaba wa maji safi na salama .

Akizungumza mara baada ya kukagua Miradi hiyo ya Maji Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Eng. Emmanuel Kalobelo amesema amefurahishwa na kitendo cha Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Muro ya kuwasaidia wakandarasi kupata vifaa vya ujenzi yakiwemo mabomba makubwa ya maji kwa dhamana ya ofisi yake kwa wenye viwanda uku taratibu za malipo zikiendelea hatua inayosaidia miradi hiyo kukamilika kwa wakati

"Nashukuru kwa maelezo ya Mhe. Mkuu wa Wilaya ambaye tangu asubuhi ameonyesha jinsi gani anavyofuatilia miradi yote ndani ya wilaya yake, na anafahamu takwimu zote za miradi na stegi zilizofikiwa hivyo Mimi kama mtu wa sekta ya maji nimefarijika kweli na uongozi wa Wilaya ya Arumeru." Alisema Naibu Emmanuel Kalobelo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge Ndugu Mahamoud Mgimwa amesema DC Muro anaitaji pongezi na kuungwa mkono kutokana na juhudi zake anazoonyesha zakuwaletea wananchi wake maendeleo kwa kufuatilia miradi kila hatua , pamoja na kuhakikisha wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya miradi wananufaika kwanza *, hatua ambayo amesema inadhihirisha kuwa *Dc Muro hakai ofisini na badala yake anatumia muda mwingi katika kutembelea miradi

"Mhe Muro hapa anafanya kazi nzuri kuna kazi nyingine ambazo so za kwake lakini anajitolea,naomba tumpongeze sana, unawezajiuliza anafanya kwa ajili ya nani? Lakini ameamua kufanya kwa ajili ya kuwasaidia nyinyi ndugu zake, kwa zile juhudi anazozifanya mkuu wa wilaya na waombeni sana mumuunge mkono." Alisema Mahamoud.

Kamati hiyo pia ilipata fursa ya kutembelea Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji * mifugo kwa njia ya chupa NAIC Kilichopo Wilayani Arumeru. ambapo walijionea kazi zinazofanywa za kutengeneza mbegu za Ng’ombe wa kisasa wa maziwa na nyama .

KIKUNDI CHA GONGA GONGA WAFANYA UKARABATI NA USAFI ZAHANATI YA MJI MWEMA

0
0
Vijana wa Kikundi cha Gonga Gonga cha Mji Mwema, Kigamboni wakifanya usafi cha choo cha wagonjwa cha Zahanati ya Mji Mwema. Mwishoni mwa wiki (Picha na Andrew Chale
Vijana wa Kikundi cha Gonga Gonga cha Mji Mwema, Kigamboni wakikarabati mlango wa chumba cha leba cha Zahanati ya Mji Mwema. Mwishoni mwa wiki
Vijana wa Kikundi cha Gonga Gonga wakifanya usafi wa eneo la mtaro wa maji machafu kwenye Zahanati ya Mji Mwema, Kigamboni mwishoni mwa wiki.
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Mji Mwema, Dk. Beno Constatino, akitoa mkono wa pongezi kwa Vijana wa kikundi cha Gonga Gonga, muda mfupi baada ya kumaliza shughuli za ukarabati na usafi wa mazingira wa Zahanati hiyo, mwishoni mwa wiki.

…………………………..


NA Andrew Chale


KIKUNDI cha Gonga Gonga kinachojishughulisha na shughuli za useremal, wamejitolea kufanya ukarabati na usafi katika Zahanati ya Mji Mwema, iliyopo wilayani Kigamboni, Dar es Salaam.

Kikundi hicho kiliweza kutengeneza milango iliyokuwa inasumbua ikiwemo ya vyoo, vyumba vya madaktari na maeneo mengine huku pia wakirekebisha vifaa vya umeme ikiwemo feni za majengo hayo.

Mbali na kufanya ufundi mdogomdogo pamoja na kuweka vifaa vipya, vijana hao walifanya usafi wa mazingira ikiwemo kufyeka majani na kuzibua mtaro wa maji machafu uliokuwa maeneo ya zahanati hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Katibu wa Gonga Gonga, Ali Rajab Ali, alishukuru kwa nafasi waliyopewa na uongozi wa zahanati hiyo na kusema walichofanya ni kuonesha kuunga mkono juhudi mbalimbali katika jamii.

“Tunashukuru kwa kupewa nafasi ya kufanya tukio hili, kwani lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunawatoa kwenye msongo wa kufikiria kifaa fulani hakifanyi kazi ama mlango haifungi.

Kwa umoja wetu pia tumefanya usafi wa mazingira maeneo yote yanayozunguka zahanati” alisema Ali.Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Mji Mwema, Dk. Beno Constatino, alikipongeza kikundi hicho kwa namna walivyojitolea kufanya shughuli za kijamii kwenye zahanati hiyo huku akiwaomba kuwa na utaratibu huo mara kwa mara.

Dk. Beno alisema awali walikuwa wanapata changamoto kwenye hasa milango ukiwemo mlango wa leba.Dkt. Beno alibainisha kuwa, awali walikuwa wanapata changamoto kwenye mlango huo wa leba na hata walikuwa wakiamua kusafirisha mgonjwa kuhamishiwa kituo cha Vijibweni.

Nae Mwenyekiti wa Gonga Gonga, Seleman Omari amesema wameamua kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali hivyo kujitolea kwao huko ni kuungana na Rais katika kauli yake ya Hapa kazi.“Tunaungana na Serikali kuhakikisha kazi zinafanyika kwa ufanisi mkubwa kwa madaktari na wauguzi ama wagonjwa wanaofika hapa kuwa mazingira salama.

Kwa ujuzi wetu wa ufundi tumejitolea kufanya shughuli hii bure kabisa kwani inawasaidia ndugu zetu na pia hata sie wenyewe” alisema Omari.

Aidha, Omari aliongeza kikundi hicho cha Gonga Gonga kimesajiliwa kisheria na kipo toka mwaka 2005 wakiwa vijana sita na baadae kuhamasishana na sasa kufikia 22 ambapo wanashughulika na ufundi mkubwa wa useremala, Sanaa za vitu vya uselemala, Umeme, Kilimo na mambo mengine.

WAZIRI MHAGAMA AWAASA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Machifu wa Tamaduni za Asili na wakazi wa Ichenjeziya alipotembelea eneo kujionea chazo cha maji asilia kilichopo Ichenjeziya, Mkoani Songwe. (Kushoto) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume, (Kulia) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume akieleza jambo kwa Machifu wa Tamaduni za Asili na wakazi wa Ichenjeziya alipotembelea eneo kujionea chazo cha maji asilia Aprili 1, 2019 Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza jambo kutoka kwa mmoja wa Machifu wa Tamaduni za Asili kuhusu chanzo cha maji cha Ichenjeziya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipanda mche wa mti karibu na chanzo cha maji asilia kilichopo Ichenjeziya, Aprili 1, 2019 Mkoani Songwe.
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume akipanda mche wa mti karibu na chanzo cha maji asilia kilichopo Ichenjeziya, Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akicheza pamoja na wanakwaya wa JKT Mlale alipofanya ziara ya kukagua maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 katika uwanja wa Kimondo, Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde wakati wakiangalia kikundi cha Ngoma Asili (hakipo pichani) walipotembelea uwanja wa Kimondo kukagua maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019, Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akiangalia Vijana wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 (hawapo pichani) alipotembelea uwanja wa Kimondo kukagua maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Songwe. (Kushoto) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akieleza jambo kwa Viongozi mbalimbali walihudhuria uwanjani hapo kujionea maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru.
ana wa Halaiki wakitengeneza umbo la Mlima Kilimanjaro kuashiria kupandisha Bendera ya Taifa katika mlima Kilimanjaro wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipotembea kukagua maandalizi hayo.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENE ULEMAVU)




Na; OWM (KVAU), SONGWE

Wananchi waaswa kutunza rasimali mbalimbali katika mazingira yao na kuyapenda ili kuepuka kuathiri na kuharibu mazigira yaliyopo.

Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 1, 2019 Mkoani Songwe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Ichenjeziya alipotembelea eneo hilo lenye chanzo cha maji ya asili na kupanda mche wa mti ikiwa ni siku ya Kitaifa ya upandaji miti.

Waziri Mhagama alieleza kuwa Nchi yetu imeamua kutumia uchumi wa viwanda ili kutekeleza azma ya Serikali kuelekea uchumi wa pato la kati, hivyo hata upandaji miti na maliasili ya misitu inaendana na uchumi wa viwanda,” alieleza Mhagama.

Aliongeza kuwa kuelekea kwenye Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019, ni vyema wananchi wakashiriki kauli mbiu ya upandaji miti ambayo inaendana na kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru isemayo “Maji ni Haki ya kila Mtu, Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”.

“Wanaichenjeziya mnatakiwa kuweka historia kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu kwa kupanda miti kwenye vyanzo vya Maji ili kupata maji safi na salama,” alisema Mhagama

Aidha, Waziri Mhagama alitoa wito kwa kila mwananchi kuhakikisha anakuwa msimamzi wa mazingira na anatunza vyanzo vya maji kwa kufuata sheria na taratibu ili kuhakikisha kila mtu anafikiwa na maji safi na salama kama haki ya msingi. 

Hata hivyo Mhe. Mhagama alitumia pia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wa Songwe na Mikoa ya jirani kushiriki kwa wingi katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazozinduliwa Aprili 2, 2019 katika Uwanja wa Kimondo uliopo Kata ya Forest, Wilayani Mbozi. 

“Hii ni nafasi ya kipekee kwa wananchi na ni siku ya kuhamasishana kwa vijana kwa kujitathimini na kutambua mchango wa Baba wa Taifa na Mhasisi wa Mapinduzi ya Zanzibari katika kujenga Taifa,” alisema mhagama 

Naye Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume alisema kuwa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ni siku muhimu sana kwa wananchi kutambua historia ya Tanzania Bara na Zanzibar iliyopelekea Taifa katika mwanga.

MJASILIAMALI SOKO LA MACHINGA COMPLEX AJINYAKULIA KITITA CHA SHILINGI MILIONI TANO KUTOKA BIKO

0
0
 Mshindi wa sh milioni tano Omary Abdallah Kapungu, akifurahia fedha zake alizokabidhiwa kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko, katika droo kubwa iliyofanyika Jumapili, maarufu kama Jumadili Jenga. Kapungu ni mjasiriamali katika soko la Machinga Complex, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL 2,2019

0
0



























WIKI YA MAADHIMISHO JUMUIYA YA WAZAZI-CCM KITAIFA YAZINDULIWA MKOANI RUKWA

0
0
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wazazi Tanzani Erasto Sima akishiriki kupanga matofali ya ujenzi wa hosputali ya Nkasi, katika mji mdogo wa Namanyere mkoani Rukwa, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya Jumuiya hiyo Kitaifa, leo. KWA PICHA NYINGI ZAIDI>>BOFYA HAPA

Na Bashir Nkoromo, Nkasi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi ya Umoja wa Wazazi Tanzani, Erasto Sima leo amezindua kwa kishindo Maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya hiyo Kitaifa katika mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Uzinduzi huo ameufanya kwa mkutano maalum uliohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Jumuiya zote CCM ukitanguliwa na shuguli ya kukagua Zahanati ya Nyamanyere na ujenzi wa Hosoitali ya Wilaya ya Nkasi.

Manaibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Tija Magoma (Bara) na Othman Ali Maulid (Zanzibar) ni miongoni mwa viongozi walioshiki kwa karibu shughuli mbalimbali za uzinduzi wa maadhimisho hayo pamoja na viogozi wa Jumuiya zote za CCM tangu ngazi ya mkoa huo wa Rukwa.

Baada ya kuwasili Namanyere na ujumbe wake akitokea Mjini Sumbawanga, Nsima alizungumza na umati wa Wana CCM na viongozi mbalimbali katika viwanja vya Zahanati ya Namanyere ambako alikuta Kada wa CCM Mkuu wa Wilaya hiyo Saidi Mtanda akiongoza wana CCM hao na Wananchi kufanya kufanya usafi wa mazingira kwenye Zahanati hiyo.

Akizungumza. Nsima aliwataka wananchi kujenga tabia ya wanachi kwenda Kliniki wawapo wahawazito na kupeleka watoto  kwenye kliniki ya zahanati hiyo na pia kwenda kupata matibabu wanapougua kwa kuwa serikali imeijenga na kuiboresha kwa kuwa inajali afya za wananchi.

Aliwataka pia kujitolea damu mara kwa mara ili kusawiri lengo la serikali kuweka benki ya damu kwenye zahanati hiyo, akisema ni lazima wajivunie kwa kufanya hivyo kwa sababu ni zahanati chache nchini ambazo zina huduma ya benki ya damu kama ilivyo ya Namanyere.

Sima aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha ya wananchi zinazofanywa na Serikali CCM ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli ambapo Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania alieleza miradi ya kimaendeleo na huduma zilizokwisha tekelezwa na zinazoendelea kutekelezwa chini ya uongozi wa Rais Dk. Magufuli.

Baadaye Nsima aliikagua zahanati hiyo na kushudia ilivyoboreshwa hasa upande wa majengo ikiwemo chumba cha kisasa cha kuhifadhia maiti ambapo alihitimisha ukaguzi huo kwa yeye na msafara wake kupanda miti ya aina mbalimbali.

Nsima alimaliza ziara kwa kukagua ujenzi wa hopsitali kubwa ya Wilaya ya Namanyere ambayo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wakazi wa wilaya hiyo na wa maeleneo ya wilaya jirani ambako alishiriki kupanga matofali yanayofyatulia hapo kwa ajili ya ujenzi huo.

Akizungumza na viongozi kwenye mkutano wa ndani wa kuzindua maadhimisho hayo, Nsima aliwataka wananchi kuwafichua watendaji au viongozi watakaokuwa wanazembea kushiriki kikamilifu utekelezaji wa ilani ya CCM.

Nsima ataendelea kuwepo Nkasi akishirikiana na wananchi kufanya shughuli mbalimbali za kijamii hadi Aprili 6, 2019, kabla ya jerejea mjini Sumbawanga ambako Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa atafunga kilele cha maadhimisho hayo kesho yake. TAZAMA PICHA KEMKEM ZA UDINDUZI WA MAAHIMISHO HAYO>>BOFYA HAPA


BEI ZA MATUNDA SOKO LA MWENGE,KINONDONI JIJINI DAR

0
0

Bei za matunda mbalimbali katika Soko la Mwenge wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,kama zinavyoonekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

Wafanyabiashara wa matunda katika soko la Mwenge jijini Dar es Salaam wakiendelea na kazi kama wanavyooneka pichani.


WAHANDISI WANAWAKE WASISITIZA WASICHANA KUCHANGAMKIA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI

0
0
Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, Bi. Upendo Sanze, akielekeza jambo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya KwaMtoro wilayani Chemba mkoani Dodoma, kuhusu umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari KwaMtoro wilayani Chemba mkoani Dodoma, Bi. Neema Muna (mwenye miwani), akieleza changamoto zinazoikabili shule hiyo kwa Wahandisi wanawake kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, walipofika shuleni hapo kuhamasisha umuhimu wa usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wasichana. 

Mwanafunzi Siminza Mambo, kutoka Shule ya Sekondari ya KwaMtoro wilayani Chemba mkoani Dodoma, akitoa maoni kwa Wahandisi wanawake kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) walipofika shuleni hapo kuhamasisha usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wasichana.
Maabara ya Shule ya Sekondari ya KwaMtoro wilayani Chemba mkoani Dodoma licha ya kukamilika lakini bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa.
Wahandisi wanawake kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari ya Dalai, wilayani Kondoa mkoani Dodoma mara baada ya kutoa elimu ya umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wanafunzi hao.
Picha na WUUM

…………………….

Na Siti Said

Wahandisi wa kike wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kupitia Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, wamewataka wanafunzi wa kike mkoani Dodoma, kuchangamkia fursa za usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati ili kuongeza wataalam katika fani ya Uhandisi.

Akizungumza kwa niaba ya wahandisi hao katika shule ya Sekondari ya KwaMtoro, Wilayani Chemba mkoani Dodoma, Mhandisi Rahma Mwinyi , amesema kuwa sekta hiyo bado ina uhaba wa wataalamu wa kike hivyo inahitaji wanafunzi kusoma masomo hayo ili kuongeza idadi ya wataalamu hao na kuweza kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

“ Hakikisheni mnasoma masomo ya Sayansi na Hisabati kwa bidii, ufaulu wa masomo haya utategemea ufanyaji wa maswali na mazoezi ya kujipima mara kwa mara ambayo yatawajengea uelewa na kupelekea kufaulu vizuri, Serikali bado inahitaji wataalam wa fani hii na pia fursa za ajira kupitia fani hii zipo nyingi, kazi kwenu kujipanga ili mfikie malengo yenu”, amesema Mhandisi Mwinyi.

Aidha, Mhandisi Mwinyi amewataka wanafunzi hao kuachana na dhana potofu ya kuwa masomo hayo ni magumu na badala yake kutafuta njia mbadala ikiwemo ya kupanga ratiba ya masomo yao vizuri na kuzingatia yale wanayofundishwa na walimu darasani.

Kwa upande wake, Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya KwaMtoro, Bi. Neema Muna, kwa niaba ya walimu wenzake ameishauri Serikali kuhakikisha wanapeleka vifaa vya maabara kwa shule ambazo hazina vifaa hususan vijijini kwani ufaulu wa masomo hayo hutegemea sana kufanya mazoezi kwa vitendo.

Ameongeza kuwa ipo haja ya Serikali kuajiri na kupeleka walimu wa kutosha katika shule zilizopo vijijini kulingana na idadi ya wanafunzi na pia huduma za maji na umeme ziboreshwe ili kukidhi mahitaji ya ufanyaji wa mazoezi kwa vitendo kupitia katika maabara zao.

Naye, Mwanafunzi Siminza Mambo wa shule hiyo, ameiomba Serikali kuongeza walimu wa kike wa sayansi shuleni hapo kwani kwa sasa shule hiyo ina mwalimu mmoja tu wa jinsia hiyo hali inayowakatisha tamaa wanafunzi wa kike kujiunga na masomo hayo.

Pia, Mwanafunzi Lucy Isack, kutoka shule hiyo ameiomba Serikali kuongeza walimu wa sayansi na hisabati, vitabu na kuboreshea miundombinu ya maabara ikiwemo vifaa vya kupimia kemikali.

Ziara ya wahandisi hao katika shule mbalimbali za Sekondari za mkoa wa Dodoma inalenga kuhamasisha usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wasichana ambapo leo wametembelea shule ya KwaMtoro, Dalai na Mondo.

TFS YAHAMASISHA WATANZANIA KUJENGA TABIA YA KUPANDA MITI KWA WINGI NCHINI

0
0
 Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo akiwa ameshika mche wa mti kabla ya kuupanda katika eneo la Kilongawima lililopo Kunduchi jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kilele cha upandaji miti kitaifa. 
 Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) akipanda mti katika eneo la Kilongawima jijini Dar es Salaam jana  Aprili 1,2019 ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya upandaji miti kitaifa nchini.

 Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) akizungumza jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya upandaji miti kitaifa nchini ambapo ametumia nafasi hiyo kuhamasisha watanzania kupanda miti kwa wingi.
 Mkurugenzi wa Miradi wa Great Hope Foundation Noella Mahuvi  akipanda mti katika eneo la Kilongawimba lililoko Kunduchi jijini Dar es Salaam.

 Mmoja ya wakazi wa wa Kilongawimba akishiriki upandaji miti katika eneo hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya upandaji miti kitaifa ambayo yamefanyika leo Aprili Mosi mwaka huu.

 Baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) wakishiriki upandaji miti katika eneo la Kilongawima jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa waandishi wa habari kutoka Michuzi Blog na Michuzi TV Said Mwishehe akipanda mti katika eneo la Kilongawima ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa nchini.






Said Mwishehe,Globu ya jamii 

WAKATI leo ikiwa ni Siku ya Maadhimisho ya kilele cha Upandaji Miti nchini kitaifa,Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umesema kuna kila sababu kwa Watanzania kuendelea kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ili kukabiliana na kasi ya uharibifu wa mazingira inayoendelea kufanywa na baadhi ya watu. 

TFS katika kuhakikisha miti inaendelea kupandwa leo wameadhimisha siku hiyo kwa kupanda miti katika mikoa mbalimbali ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wamepanda miti zaidi ya 1000. 

Akizungumza wakati wa upandaji miti katika eneo la Kilongawima lililoko Kunduchi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema ni jukumu la kila Mtanzania kupanda miti iwe ya mbao, matunda au kivuli kwani kwa kufanya hivyo kutasaia uwepo wa misitu ambayo faida zake ni nyingi ikiwemo ya kuzalisha hewa safi kwa ajili ya binadamu. 

Amesisitiza kuwa ni kilele cha maadhimisho ya upandaji miti, hivyo TFS imeendelea na utaratibu wake wa kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba kwa mwaka huu wameamua kuweka utaratibu kila mkoa kupanda miti na wanaendelea kuhamasisha jamii ya watanzania kuwa na utamaduni wa kupanda miti kila siku na isiwe mara moja tu kwa mwaka. 

"Kupanda miti iwe ni jambo la kila siku bila kujali unapanda miti kiasi gani.Nitoe mfano hapa hapa Dar es Salaam kuna watu hawalali kwasababu ya joto ambalo msingi wake unatokana na kukosekana kwa miti kwenye maeneo hayo wakati kuna maeneo mengine ya Dar hakuna joto kwasababu tu wananchi wa maeneo hayo wamepanda miti kwa wingi na kufanya hali ya hewa kuwa tulivu na hakuna joto.Hivyo tunaendelea kuhamasisha watu kupanda miti kadri wanavyoweza. 

"Pia tunahimiza upandaji miti kwasababu itasaidia kuondoa athari 

mbalimbali zikiwemo za hewa ya ukaa.TFS pamoja na kuhimiza Watanzania kupanda miti tumebaliana kila mkoa upande miti.Tunafahamu kasi ya uharibifu misitu ni kubwa mno kulikoa kupanda, hivyo tunaendelea kupanda miti alau kuddhibiti uharibifu wa misitu na ukataji miti hovyo.Kwetu tunaamini upandaji huu wa miti malengo yake ni mawili moja kurudisha misitu ya asili na pili kukabiliana na uharibifu wa ukataji miti kwa kupanda miti,"amesema. 

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa waandishi wa habari nao kujenga utamaduni wa kupanda miti mbali ya kuhamasisha upandaji miti nchini kwani kwa kufanya hivyo nao watakuwa sahemu ya watanzania ambao wamepanda miti kwa maslahi ya nchi yetu na uhai wa misitu nchini. 

Kuhusu miti ambayo imepandwa Kilongawima amesema katika eneo hilo TFS imepanda miti 1000 ikiwemo ya mikoko ambayo moja ya kazi yake kubwa ni kulinda mmomonyo wa ardhi, inazuia mafuriko katika maeneo ya ukanda wa Pwani, pamoja kubadilisha hewa ukaa. 

Kwa upande wake Meneja wa Misiti wa TFS Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Dotto Tumbikwa amesema baada ya kupanda miti hiyo ni jukumu lao kuhakisha inalindwa, hivyo ametoa rai kwa wananchi kuhakiksha wanakuwa walinzi wa miti hiyo. 

"Miti ambayo imepandwa leo ni wajibu wetu TFS kuilinda , tutaendelea kushirikiana na wananchi wa maeneo haya kuwahakikisha tunasaidiana nao kuilinda.Tunafahamu faida za uwepo wa miti katika maeno yetu,"amesma na kuongeza kuwa wanaendelea kutoa mwito kwa Watanzania kote nchini kujenga tabia ya kupanda miti. 

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Miradi wa Great Hope Foundation Noella Mahuvi amesema wanatambua umuhimu wa misitu, hivyo wameona ni vema akaungana na TFS katika kupanda miti eneo hilo huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa umedika wakati kwa wanafunzi katika shule mbalimbali nchini kupanda miti. 

"Ni wajibu wetu kuendeleza uwepo wa misitu nchini, na hii itatokana kwa sisi wenyewe kuamua kuilinda misitu iliyopo, kuzuia uharibifu wa misitu na kubwa zaidi kuendelea kupanda miti .Hivyo nitoe rai kwa wanafunzi nchini kushiriki kikamilifu katika kupanda miti,"amesema Mahuvi. 

WANANCHI WA KAGEZI,MLANGE WILAYANI KIBONDO WALALAMA MRADI WA MAJI WA SH.BILIONI MOJA KUTOKAMILIKA KWA WAKATI

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma

WANANCHI wa vijiji vya Kagezi na Mlange wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita mbili kufuata maji katika Chanzo cha maji kutokana na mradi wa maji ulioghalimu zaidi ya Sh.bilioni moja kutokamilika tangu mwaka 2014 hadi sasa.

Wakizungumza jana kijijini hapo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani kwa baadhi ya miradi ya Serikali uliofanywa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Serikali ya Wilaya hiyo, baadhi ya Wananchi hao waliokuwa wakigombania maji katika chanzo cha mto Kagezi, walisema wanapata shida ya kuchota maji na hasa ukizingatia kilima kilichopo katika chanzo hicho kinawachosha.

Agnes Kunjira ni mmoja kati ya wananchi hao alisema wanalazimika kuamka asubuhi kuwahi kuchota maji ndipo waende mashambani, kutokana na kero hiyo wanashindwa kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa wakati kwa kuwa maji ni uhai na wanahitaji maji.

Aidha aliiomba Serikali kufuatilia kwanini mradi huo hautoi maji kwa kuwa kero waliyonayo inawatesa sana na endepo mradi huo ukikamilika na wakaanza kuchota maji vijijini itawasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya shughuli zao za maendeleo.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji cha kagezi mwenyekiti wa Kijiji Zabroni Ntimba, alisema tangu mradi huo uanze kujengwa ni muda mrefu na mpaka sasa ulitakiwa uwe umekamilika lakini mwaka 2018 wananchi walipata maji kwa muda wa miezi mitatu tu na baada ya hapo maji hayakutoka tena.

Alisema wananchi wanalalamika kwani katika mradi huo walichangia asilimia 20 ya mradi hali hiyo inayosababisha kushindwa kuchangia hata shughuli zingine za maendeleo, kwa kuwa wamechangia mradi wa maji lakini hawaoni mradi ukifanya kazi.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mradi huo Mhandisi wa maji Wilaya ya Kibondo Michael Nguruwe alisema mkandarasi wa mradi huo aliingia mkataba ,wa Sh. 244,629,764, mradi ulitakiwa kuwa umekamilika 2014 lakini kutokana na changamoto ya fedha kulipa kwa wakati kwa mkandarasi mradi uliongezewa muda hadi 2018 lakini mpaka sasa haujakabidhiwa kwa wananchi.

Alisema tatizo kubwa lililopelekea mpaka sasa mradi huo kutokamilika kwa wakati, ni changamoto ya mfumo wa umeme, ambao mkandarasi alishindwa kuukamilisha na kama halmashauri wamezuia kiasi cha shilingi milioni 50 kwaajili ya umaliziaji wa mradi huo.

Alisema mpaka sasa wanaendelea kutafuta mkandarasi wa mfumo wa umeme katika mradi huo kwaajili ya kuweka kifaa kitakacho saidia kuongoza mfumo wa umeme katika mradi huo na mradi ukabidhiwe kwa Wananchi kwaajili ya kutumika.

Kutokana na changamoto zilizopo katika mradi huo na kero wanayoipata wananchi, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Hamisi Tahilo alisema Chama kinaagiza mradi huo kukamilika kwa kipindi cha mwezi mmoja na baada ya mwezi mmoja watafika katika mradi huo kuangalia kama kweli Wananchi wameanza kupata maji.

Alisema Serikali imetoa zaidi ya bilioni moja kwaajili ya mradi wa Wananchi lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika, Serikali iliahidi kuhakikisha wanamtua mama ndoo kichwani ni lazima watendaji kuhakikisha Wanasimamia miradi ya serikali inafanyiwa kazi.

" Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM na fedha zinatopewa kwaajili ya kukamilisha miradi Wananchi wataiamini Serikali bqada ya kuona miradi hii inakamilika niombe ndani ya mwezi huo mmoja mradi huu uwe umekamilika", alisema Tahilo.

Aiwaomba wananchi kuwa na subira na kuendelea kujenga imani na CCM kwa kuwa imejipanga kuhakikisha wananchi wote wa vijijini na mijini wanapata huduma sawa sawa na wanaondokana na changamoto zote.
 Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kagezi wakichota maji katika chanzo cha mto Kagezi baada ya kero kubwa ya  maji kijijini humo
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kibondo wakiwasaidia Wannanchi kubeba maji. 
 Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kagezi wakichota maji katika chanzo cha mto Kagezi baada ya kero kubwa ya  maji kijijini humo

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kagezi wakichota maji katika chanzo cha mto Kagezi baada ya kero kubwa ya  maji kijijini humo
 Kifaa kinachodaiwa kusababisha maji yasitoke katika mradi wa Maji kagezi.

USHIRIKA UCHUKUE MIKOPO KWA AJILI YA WAKULIMA –MHE.MGUMBA

0
0

Naibu waziri Kilimo Mhe. Omari T. Mgumba (Mb) akiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa arusha alipokutana na wataalamu wa kilimo ,ushirika na umwagiliaji kabla ya kuanza ziara ya kuzungukia maeneo mbalmbali mkoani hapo.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoani Arusha bwana Loata Erasto Sanare akieleza jambao baada ya kutembelewa na Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari T. Mgumba katika ofisi ya chama hicho hivi karibuni.


………………………….

Bashiri Salum,Wizara ya Kilimo Arusha

Vyama vya Ushirika vimeshauriwa kukopa fedha kwenye Mabenki kwa ajili ya wanachama wao kwa kuwa waliowengi hawakopesheki hivyo kufanya shughuli za kilimo kuwa ngumu.

Akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha Maafisa Ushirika, umwagiliaji na afisa kilimo Mkoani Arusha Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari Mgumba amesema miundombinu mingi ya umwagiliaji inahitaji marekebisho makubwa ili kuweza kutumiwa na wakulima.

Aidha miundombinu hiyo imekosa ukarabati kutokana na wakulima kutokuwa na mitaji ya kutosha na kutoaminiwa na taasisi za fedha kusaidia ukarabati huo.

Ameshauri tume ya Ushirika kuvisimia vyama vya ushirika ili viweze kukopa fedha Benki Kwa ajili ya wanachama lengo likiwa ni kufanya ukarabati Wa miundombinu ya umwagiliaji ambapo kila mwanachama atawajibika kuchangia huduma hiyo.

Hatuwezi kufanya Kilimo cha kibiashara Kwa kutegemea mvua ambazo Nazo zimekuwa haziyabiriki nawashauri tume ya Ushirika na tume umwagiliaji kusimamia vyama hivyo kwenye skimu mbalimbali za umwagiliaji kukopa fedha ambazo zitatumika kurekebisha miundombinu ya umwagiliaji badala ya kutegemea serikali .alisema Mhe. Naibu Waziri

Naibu Waziri aliwataka maafisa ugani kuwafikia wakulima na kuelimisha namna ya kutumia na kutoa elimu juu ya matumizi bora ya viuatilifu vya mimea ili kupambana na visumbufu vya mazao ambavyo vimekuwa vikimsababishia mkulima hasara kubwa.

Naye afisa Umwagiliaji wa kanda mhandisi Juma Mdete amesema katika ukanda huo eneo ambalo linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta elfu 40 kati ya hilo linalotumika ni hekta elifu 24 tu

Amesisitiza kwamba pamoja na matumizi kidogo ya eneo la umwagiliaji lakini maeneo yanayomwagiliwa yanasaidia upatikanaji wa chakula wakati wa ukame.

Akichangia wakati wa mjadala huo Afisa Kilimo Mkoa wa Arusha Bwana Daniel Loiruck amethibitisha kwamba ukiondoa Magonjwa ya mlipuko na uvamizi wa visumbufu vya mimea maafisa kilimo wamekuwa wakijitahidi kuwafikia wakulima ili kutatua changamoto zinazowakabili.

Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoani Arusha bwana Loata Erasto Sanare akamueleza Mhe. Naibu waziri kwamba hali ya ukame mkoani humo ni kubwa hivyo kuishauri serikali kuanza kufikiri njia mbadala ya kupambana na hali hiyo.

‘Msimu wa kilimo upo katikati lakini mpaka sasa hakuna mvua na tumezunguka sehemu mbalimbali hapa arusha mahindi yamekauka hata mvua ikinyesha haiwezi kuleta mabadiliko tunaishauri serikali kufikiri mbinu za kukabiliana na hali hiyo’. Alisisitiza bwana Loata Sanare
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images