Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1830 | 1831 | (Page 1832) | 1833 | 1834 | .... | 1904 | newer

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akikabidhi Vikundi mfano wa hundi ya shilingi milioni 118 ambao ni mkopo kutoka Halmashauri ya Mji Ifakara. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe. Mashaka Mbilinyi na kushoto kwake aliyevaa tai ni Mkurugenzi Mtendaji wa hiyo Francis Ndulane.
  Dkt. Kebwe akimkabidhi baiskeli Afisa Mwandikishaji wa mfuko wa Afya ulioboreshwa Shakila Limbega ili kumwezesha kufanya kazi hiyo kwa ufanisi zaidi. kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe. Mashaka Mbilinyi na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Francis Ndulane.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanavikundi ambao wamebahatika kupata mkopo wa jumla ya shilingi milioni 118. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe. Mashaka Mbilinyi na kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Francis Ndulane.

  …………………………..

  Na . Andrew Chimesela

  Halmashauri ya Mji Ifakara Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro imetoa Mkopo wa shilingi milioni 118 kwa vikundi vya akina mama, Vijana na watu wenye Ulemavu ambazo zimetokana na makusanyo ya vyanzo vya ndani kwa 2018/2019 ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani na kutoa mikopo kwa makundi hayo.

  Mkopo huo umetolewa mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Halmashauri ya mji wa Ifakara ambapo jumla ya vikundi 69 vimefaidika na Mkopo huo vikiwemo 52 vya wanawake sawa na 75%, 13 ni vya vijana sawa na 19% na Vikundi 4 ni vya watu wenye ulemavu sawa na 6% ya vikundi vyote vilivyopata mkopo huo.

  Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Ifakara Francis Ndulane amesema katika kipindi cha Julai 2018 hadi Februari 2019 Halmashauri ya Mji Ifakara imekusanya jumla ya shilingi 1.1Bil kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato yake ya ndani.

  Aidha amesema, katika kipindi hicho Halmashauri imetenga Tsh 110,000,000 ambayo inakaribia asilimia 10% ya makusanyo hayo kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye wenye ulemavu.

  Hata hiyvo amesema milioni nane zimetolewa na Wahe. Wabunge kwa ajili ya mikopo hiyo ambapo Milioni tatu zimetolewa kutoka katika mfuko wa Jimbo la Kilombero na shilingi Milioni tano zimetolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mchungaji Getrude Rwakatare na kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa kuwa 118 Milioni.

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akizungumza mara baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya fedha hizo kwa wanavikundi, amewataka waliofaidika na mikopo hiyo kuwa waaminifu na kurejesha fedha wanazokopa kulingana na mikataba wanayoweka ili wengine nao waweze kufaidi mikopo hiyo na wasiorejesha wachukuliwe hatua za kisheria.

  Sambamba na maagizo hayo Dkt. Kebwe amewataka Wakurugenzi wote wa Halmashauri kufanya uhakiki wa kina kabla ya kutoa mikopo hiyo kwa kikundi chochote kinachotaka kukopa, amesema engo ni kutaka fedha hizo za Serikali ziendelee kutoa tija kwa watu wengi kadri inavyowezekana badala ya wachache kuchukua fedha hizo na kutokomea kusikojulikana.

  Aidha, Dkt. Kebwe ametumia fursa hiyo kuwakumbusha Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro kutekeleza sharti hilo la kutenga asilimia kumi ya mapato yake na kukopesha makundi tajwa hapo juu kwa kuwa hilo sasa siyo hiari bali ni lazima kwa maelekezo ya Serikali ambapo kati ya asilimia kumi 4 ni za akina mama, 4 nyingine ni kwa ajili ya Vijana na asilimia mbili ni kwa watu wenye Ulemavu.

  “Na ole wake Mkurugenzi ambaye atajivuta atazembea katika Mkoa wa Morogoro katika utoaji wa fedha hizi za vikundi, iatakula kwake” alisisitiza Dkt. Kebwe

  Hata hivyo Dkt. Kebwe amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri wakishirikiana na Wahe. Madiwani kujaribu kubadili mtindo wa kukopesha fedha hizo. Amesema badala ya kukopesha fedha hizo vikundi vingi kwa fedha kidogo kidogo ni vema vikaunganishwa vikundi vingi pamoja na kupewa mkopo mkubwa ili waweze kuazisha hata kiwanda ambapo kitatoa ajira, kutakuwa na faida na kiwanda kitakuwa endelevu hivyo kuwa na tija zaidi.

  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Mhe. Mashaka Mbilinyi ametoa wito kwa vikundi vilivyopata mikopo kujiunga na mfuko wa Afya wa CHF ili kuwa rahisi kwao kupata tiba mara wanapopatwa maradhi huku akisisitiza kuimarisha usafi wa mazingira katika maeneo wanayoishi ili kuondoa mlipuko wa magonjwa na kusababisha watu kuwa na Afya dhaifu inayopelekea uchumi kudorola.

  Tukio la utoaji wa Mikopo liliambatana na tukio la utoaji wa vifaa vya kufanyia kazi Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (CHF) ambapo simu za viganjani tisa zenye thamani ya Tsh. 2,070,000/= zilitolewa huku baiskeli 11 zenye thamani ya shilingi 1,430,000/=pia zilitolewa kwa Maafisa Waandikishaji kuwawezesha kufika maeneo yaliyombali, kuhamasisha watu kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa.

  0 0

  I4ID kwa kushirikiana na Taasisi binafsi ambao ni wabia wake walishiriki kwenye Maonyesho ya ubunifu yaliyofanyika kuanzia tarehe 25 mpaka 29 Mwezi March 2019 COSTECH BUILDING,Sayansi kijitonyama,Dar es salaam.
  Wabia wa I4ID wakizungumzia katika maonesho hayo walishukuru serikali kuondoa tozo ya ushuru (VAT) katika soko la bidhaa za taulo za kike,wabiahaowalioshiriki katika maoneshohayo ni kama ANUFLO (Hedhicup),ELEA,GLORYPADS pamoja na BINTI FOUNDATION.
  Kwa upandewa mabaloziwa hedhisalama/hedhi salama inatuhusu Wasanii JB na Wastara alishiriki kikamilifu katika kuelimisha umma katika maonesho hayo.  0 0


  Wataalamu 25 wa Ulinzi na Usalama wa vyanzo vya mionzi kutoka katika nchi sita za Afrika wanaoshiriki katika mafunzo ya wiki mbili ya jinsi ya kuendesha mafunzo ya ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionz katika nchi zao wakiwa katika picha ya pamoja katika Makao Makuu ya Ofisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Jijini Arusha. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kwa ushirikiano na Jumuia ya Umoja wa Ulaya (EU).

  Wataalamu wa Ulinzi na Usalama wa vyanzo vya mionzi kutoka katika nchi sita za Afrika wanashiriki katika mafunzo ya wiki mbili ya utoaji mafunzo ya ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi yanaoendeshwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa ushirikiano na Jumuia ya Umoja wa Ulaya (EU) 

  Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano cha Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo amesema kuwa mafunzo hayo yanafanyika katika ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania jijini Arusha na jumla ya washiriki 25 wanashiriki mafunzo hayo kwa kwa lengo la kupata ujuzi wa namna ya kufundisha wataalamu mbali mbali wanaohusika na ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi katika nchi zao. 

  Ngamilo amesema kuwa baada ya wakufunzi hao wa ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi kumaliza mafunzo yao watakuwa na uwezo wa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wenzao wa idara mbalimbali za kitaifa katika nchi zao katika kuhakikisha kuwa vyanzo vya mionzi vinatumika katika njia zilizo salama na halali. 

  “Wakufunzi hawa waliopo kwenye mafunzo wakitoka hapa watakuwa na uwezo wa kuandaa na kufanya mafunzo ya ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi kwa wadau mbalimbali katika nchi zao, pia watatumika kama wataalamu katika kushughulikia matukio yoyote ya maafa ya vyanzo vya mionzi iwapo yatatokea katika nchi za bara la Afrika”alisema Ngamilo. 

  Hata hivyo amesema kuwa vyanzo vya mionzi visipodhibitiwa vinaweza kutumika katika vitendo vya kigaidi na kuleta madhara makubwa kwa jamii na kuathiri shughuli za kimaendeleo na kiuchumi 

  Na pia amesema kuwa wakufunzi hao wanajengewa uwezo wa kutoa mafunzo ya kubaini usafirishaji haramu wa vyanzo vya mionzi hasa kwa wataalamu wa mamlaka za ulinzi na usalama ikiwemo Polisi, Walinzi waliopo mipakani na wasimamizi wa Tekinolojia ya Nyuklia, maafisa forodha na wataalamu wa kupambana na majanga ya nyuklia. 

  Amezitaja metaja nchi wanazotoka washiriki wa mafunzo hayo ni pamoja na Burundi, Uganda, Congo(DRC), Zambia,Ghana na wenyeji Tanzania.   0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasha Mwenge kuashiria kuzinduliwa kwa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Mlowo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwenge kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa kwa mwaka 2019 Ndugu Mzee Mkongea Ali kutoka Mjini Magharibi kuashiria kuanza kwa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutumia mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019 kumkumbuka Baba wa Taifa kwa kupinga vitendo vya dhulma, ufisadi, rushwa, maradhi, chuki, dharau na kuwataka kuenzi umoja na mshikamano wetu kuchapakazi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge Kitaifa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mlowo mkoani Songwe na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

  Kaulimbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 ni “Maji ni haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke  kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”

  “Nimependezwa na kaulimbiu hii ambayo inauwiano wa moja kwa moja na jukumu langu la kila siku la kusimamia na kutunza mazingira ya nchini. Sote tunafahamu kuwa bila utunzaji thabiti wa mazingira basi vyanzo vya maji hupotea”alisema Makamu wa Rais

  Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama nchini inaendelea kuimarika ambapo huduma ya maji vijijini  imeongezeka kutoka wastani  wa asilimia 58.7 kwa mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 64.8 mwezi februari 2019 na miji mikuu ya mikoa kutoka asilimia 78 mwezi machi 2018 mpaka asilimia februari 2019.

  “Niwahakikishie wananchi tutatekeleza kwa vitendo ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi inayotutaka kuboresha huduma ya maji vijijini kufikia asilimia 85 na mijini kwa asilimia 95 ifikapo 2020”alisisitiza Makamu wa Rais 

  Aidha, Makamu wa Rais kupitia hadhara ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019 ametoa wito kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, ufugaji, ujenzi, ukataji na uchomaji miti kwenye vyanzo vya maji.

  Makamu wa Rais pia amewakumbusha wananchi juu ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwezi oktoba 2019 kuhakikisha wanachagua Viongozi wachapakazi na wenye dhamira ya maendeleo kwa jamii.

  Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 zitaongozwa na Ndugu Mzee Mkongea Ali kutoka Mjini Magharibi

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Mbunge wa Mtwara Vijijini Hawa Ghasia pamoja na Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mtwara wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi la mradi wa Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara hafla iliyofanyika leo tarehe 2 Aprili 2019 mkoani humo. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakwanza kutoka kulia pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Ujenzi, Wabunge pamoja na viongozi wa mkoa, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara.


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa upanuzi wa uwanja huo.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Mtwara mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la mradi wa Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara hafla iliyofanyika leo tarehe 2 Aprili 2019 mkoani humo. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa kushoto pamoja na  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe kulia wakati Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Mtwara na Dar es Salaam ilipoku wa ikitumbuiza uwanjani hapo. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Woinde Shizza Globu ya jamii.

  Zoezi la uandikishwaji wa mbio za kumuenzi hayati Edward Sokoine linafanyika usiku na mchana ili kutoa nafasi kwa wale waokuwa kazini wakati wa mchana ili wapate nafasi ya kujiandikisha kushiriki mbio hizo.

  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Lembrisi Kipuyo aliyasema hayo Leo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mwisho ya mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika April 6 jijini Arusha.

  Akizungumzia swala la uandikishwaji usiku na mchana alisema awali walikuwa wanaandikishwa mchana lakini kutokana na maombi ya watu wengi kuchelewa makazini ndio maana wameamua kuandikisha adi usiku wa SAA mbili.

  Alisema uandikishwaji umeanza tangu wiki iliopita katika vituo viwili ambavyo ni uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini hapa pamoja na ofisi za utamaduni na michezo wilayani Monduli huku akibainisha kuwa muitikio wawashiriki wa mbio hizo ni mkubwa.

  Kwa upande wake Katibu wa chama cha riadha mkoani Arusha Alfred Shahanga alisema kuwa njia zimeshapimwa na kuthibitishwa na njia za mbio hizo zitakuwa katikati ya jiji la Arusha na kwaupande wa swala la usalama ni la uhakika.

  "Mbio zote zitaanzia mnara wa saa na zitamalizikia katika uwanja wa sheik Amri Abeid na mgeni rasmi wa mbio hizo atakuwa Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa Kasimu " alisema Shahanga

  Alitaja zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa kilometa 21 kuwa mshindi wa kwanza atapatiwa kiasi cha shilingi milioni moja ,mshindi wa pili shilingi laki saba na mshindi wa tatu atapatiwa laki tano.

  Shahanga aliwataka wakazi wa Mkoa wa Arusha na Mkoa Jirani kujitokeza kushiriki mbio hizo ili kuenzi kwa pamoja kuanzimisha miaka 38 ya kifo cha aliekuwa Waziri mkuu wa zamani hayati Edward Moringe Sokoine.


  Picha Mwenyekiti wa Sokoine Marathon Lebris kipuyo akiongea na waandishi wa habari

  0 0

  SUALA la ukuzaji wa kada ya ujasiriamali mdogo na wa kati (SME) siyo tu limesisitizwa na Ilani ya Chama Tawala, bali pia ni utekelezaji wa majukumu ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kama lilivyoanishwa na Mpango Mkakati wa Kituo 2016-2021.

  Hivyo katika kutekeleza majukumu hayo Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe, aliyekuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo la uchumi na uwekezaji lililoandaliwa na UVCCM amefafanua mambo mbalimbali kuhusu uwekezaji nchini.

  Kongamano hilo limefanyika mkoani Mtwara ambapo kwa sehemu kubwa lilijikita kujadili uwekezaji unavyotatua changamoto za ajira kwa vijana.

  Hotuba ya Mwambe kwenye kongamano hilo imewatia hamasa vijana ambapo amewataka kujiamini na kuthubutu katika kuibua na kutekeleza miradi ya uchumi kwenye sekta za kipaumbele ambazo ni kilimo, viwanda, madini, mifugo na uvuvi.

  Pia amewaaleza washiriki kutafiti na kutambua fursa zinazowazunguka mahali walipo na kuibua miradi ya uwekezaji inayoweza kutekelezwa kwa lengo la kutengeneza ajira na kuzalisha bidhaa au huduma zinazolenga kuinufaisha jamii na Taifa kwa ujumla.

  Amefafanua kuwq kwa muktadha huo vijana amesema kuwamtazamo wao wa kwanza wa kupata ajira iwe ni ile inayotokana na uwekezaji wao wenyewe/ kujiajiri. Hivyo kujiamini na kuthubutu ni hatua kwa vijana katika kutengeneza ajira badala ya kutegemea dhana iliyozoeleka ya kutafuta ama kusubiri kuajiriwa.

  "Elimu ya uwekezaji na uchumi iliyotolewa kupitia kongamno hili, inatafsiriwa kuwa ni mbegu bora ya maendeleo iliyopandwa kwa takribani washiriki 600 wengi wao wakiwa vijana ambao ni wawekezaji watarajiwa kwa jamii ya Watanzania na Taifa kiujumla.

  "Kinachotakiwa ni vijana kuanza utekelezaji wa kuyaishi yote waliyoelekezwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha vikundi vya watu watano sambamba na kusajili kampuni. Baada ya kusajili kampuni wafuate hatua inayofuata ya kubuni/kuibua miradi mbalimbali ya uchumi kwa utekelezaji," amesema.

  Pia Mwambe alisema ‘utekelezaji wa uanzishaji wa vikundi ni hatua muhimu kwa vijana kutokana na ukweli kwamba itawasaidia kunufaika na vyanzo vya fedha za uwezeshaji kutoka Serikalini na sekta binafsi inayotolewa kupitia kwenye vikundi kwa ajili ya mitaji ya kutekeleza shughuli/miradi ya kiuchumi na uwekezaji .

  Ametumia kongamano hilo kuwatambulisha washiriki Ofisi za Kanda ambapo kuna Kanda ya Kusini zinapatikana Mtwara Jengo la Mkuu wa Mkoa, Ofisi za TIC Kanda ya Mashariki zinapatikana Dar es Salama Jengo la TIC Makao Makuu na Ofisi za TIC Kanda ya Kati zinapatikana Dodoma Jengo la Manispaa.

  Pia kuna ofisi za TIC Kanda ya Magharibi zinapatikana Kigoma Jengo la Mkuu wa Mkoa, ofisi za TIC Kanda ya Kaskazini zinapatikana Moshi Jengo la Mkuu wa Mkoa, Ofisi za TIC Kanda ya Ziwa zinapatikana Mwanza Barabara ya Kenyatta na ofisi za TIC Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini zinapatikana Mbeya Jengo la Benki ya NBC.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali alitumia kongamano hilo kutoa ufafanuzi zaidi ya kwamba vijana waamke kutumia fursa za uwekezaji zilizopo ili kuibua miradi ya uchumi na uwekezaji katika maeneo yanayowazunguka.

  "Vijana kuweni na tabia ya kujishughulisha kutekeleza miradi ya kiuchumi ikilenga maeneo ya uzalishaji, usambazaji na ulaji. Kwa msisitizo Mhe.Machali alisema ‘Vijana wakati huu ni wa kupambana na kuthubutu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

  "Ni wajibu wa vijana kuchukua hatua kwa vitendo katika kuanzisha miradi ambayo itachangia kwenye maeneo matatu makuu ya uchumi ambayo ni uzalishaji, usambazaji na ulaji, "amesema.

  0 0

   Meneja wa Vodacom Tanzania (PLC), mkoani Mtwara, Charles Minungu (kushoto) akiwa na meneja wa vodashop Mtwara, Frank Daud wakimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/-mmoja wa washiriki wa kampeni ya Vodacom M-Pesa Tuzo Points, Eladius Lutha mkazi wa Naliendele katika hafla iliyofanyika Mtwara. Kupitia kampeni hii wateja 140 wa Vodacom walizawadiwa shilingi 25,000/-kila mmoja na baada ya kampeni kumalizika wateja 10 wa Vodacom nchi nzima watazawadiwa shilingi 500,000/-kila mmoja

  0 0

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akiwasha Mwenge wa Uhuru kuashiria uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2019, Mkoani Songwe.
  ????????????????????????????????????
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akihutubia wananchi wa Songwe walioshiriki kwa wingi katika uwanja wa Kimondo – Forest, Wilayani Mbozi kushuhudia uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2019.
  ????????????????????????????????????
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa Songwe waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Songwe walioshiriki kwenye hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2019.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Balozi Ali Karume akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Uwanja wa Kimondo, Wilayani Mbozi Aprili 2, 2019.
  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela akieleza jambo kuhusu Mkoa wa Songwe.
  ????????????????????????????????????
  Sehemu ya Vijana wenye dhamana ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 (waliosimama mstari wa mbele).
  ????????????????????????????????????
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akiwa pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakifuatilia matukio ya vijana halaiki. (Kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Balozi Ali Karume.
  ????????????????????????????????????
  Vijana wa Halaiki wakionesha picha ya Mwl. Julius K. Nyerere wakati wakiimba nyimbo ya kumsifu kwenye hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
  ????????????????????????????????????
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bw. Mzee Mkongea Ali. (Kulia) ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.
  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bw. Mzee Mkongea Ali baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge zilizofanyika Aprili 2, 2019 Mkoani Songwe katika Uwanja wa Kimondo.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Viongozi mbalimbali walipokuwa wakicheza na kufurahi wakati wanakwaya ya JKT Mlale walipokuwa wakiimba nyimbo na kutoa burudani kwa wananchi wa Songwe waliohudhuria uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya wananchi wa songwe wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu (hayupo pichani). Makamu wa Rais alikuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2019. 
  PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
  (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
  …………………………


  Na OWM (KVAU) – SONGWE

  Serikali imedhamiria kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi waishio mijini kufikia asilimia 95 na vijijini asilimia 85 ifikapo 2020.

  Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Aprili 2, 2019 zilizofanyika uwanja wa Kimondo – Forest Mlowo, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe.

  Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019 isemayo “Maji ni Haki ya kila Mtu, Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”

  Makamu wa Rais amesema kuwa dhamira ya Serikali inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ni kuboresha huduma za jamii ikiwemo sekta ya elimu, afya, barabara, umeme vijijini, usafiri wa anga, uvuvi, kilimo, viwanda na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wote.

  “Sera yetu ya Maji ya mwaka 2002 inasisitiza upatikanaji wa maji safi na salama ambayo ni muhimu kwa maisha ya kila mtu, shughuli za kiuchumi na ustawi wa mazingira,” alisema Makamu wa Rais.

  Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa maji safi, alieleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji nchini ikiwemo mabwawa ya kimkakati na kuboresha miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji safi.

  Aidha, Makamu wa Rais alitoa wito kwa Wananchi kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji kwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kando ya vyanzo hivyo.

  Kupitia hadhara ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Makamu wa Rais, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao ni muhimu katika kuleta maendeleo ya watu na huduma za kijamii.

  Awali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ndio msingi mkubwa wa amani, Mshikamano, Uzalendo na Umoja tulionao katika Taifa.

  “Tunu hii imekuwa ni kichocheo cha maendeleo kwa wananchi na wamekuwa wakihamasika kushiriki katika kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo ya kijamii na kiuchumi iliyopo katika maeneo yao,” alisema Mhagama.

  Waziri Mhagama aliongeza kwa kuwashukuru wadau mbalimbali waliosaidia kufanikisha tukio hilo muhimu la Kitaifa.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela alishukuru Serikali kwa kuchagua Mkoa wa Songwe kuwa wenyeji wa Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2019.

  0 0   Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris na Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo (katikati) wakiangalia namna kifusi cha mchanga kinavyotolewa kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Blue Creef  uliopo Wilayani Geita Mkoani Geita unaomilikiwa na Christopher Kadeo tarehe 02 Aprili, 2019
  PICHA NA 2 A
  Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris (wa pili kulia) akifafanua jambo kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Blue Reef  uliopo Wilayani Geita Mkoani Geita unaomilikiwa na Christopher Kadeo mara baada ya yeye pamoja na ujumbe wake kufanya ziara kwenye mgodi huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo.
  PICHA NA 3 A
  Mkurugenzi wa kampuni ya Tan-Discover Mineral Consultancy Co. Ltd, Peter Kaheshi (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris (kulia) mara baada ya yeye pamoja na ujumbe wake kufanya ziara katika kituo cha mfano cha Rwamgaza kwa ajili ya kutoa mafunzo ya namna bora ya uchimbaji na uchenjuaji wa madini kilichopo katika eneo la Rwamgaza Wilayani Geita Mkoani Geita.
  PICHA NA A
  Mtaalam kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Busolwa uliopo Wilayani Geita Mkoani Geita, Felix Adolf Ishebabi  (katikati) akielezea shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinavyofanywa na mgodi huo kwa Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris, Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo pamoja na wajumbe kutoka Uganda na Tanzania kwenye ziara hiyo.
  PICHA NA 5A
  Afisa Migodi Mkazi wa Mkoa wa Geita, Ernest Maganga (kulia) akielezea namna biashara ya madini inavyofanyika kwenye Soko la Madini la Geita kwa Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris (kushoto) na Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo (katikati) pamoja na wajumbe kutoka Uganda na Tanzania kwenye ziara hiyo
  ……………..


  Na Greyson Mwase, Geita

  Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris ames ema kuwa amefurahishwa na usimamizi wa sekta ya madini nchini Tanzania na kusisitiza kuwa Uganda bado itaendelea kutuma wataalam wake pamoja na wachimbaji wadogo wa madini nchini Tanzania kwa ajili ya kujifunza namna bora ya uchimbaji na uchenjuaji wa madini.

  Lokeris aliyasema hayo jana tarehe 02 Aprili, 2019 mara baada ya kutembelea migodi ya wachimbaji wadogo na wa kati ya madini iliyopo Wilayani Geita Mkoani Geita, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne nchini Tanzania yenye lengo la kujifunza namna Tanzania ilivyofanikiwa katika Sekta ya Madini kupitia Wizara ya Madini hususan katika kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini.

  Akiwa ameongozana na ujumbe wa maafisa waandamizi kutoka Serikali ya Uganda pamoja na wawakilishi wa wachimbaji wadogo aliwasili mkoani Geita na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita pamoja na Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo.

  Ziara hiyo pia ilihusisha wataalam kutoka Wizara ya Madini. Tume ya Madini, vyombo vya ulinzi na usalama vya mkoa pamoja na waandishi wa habari.

  Akielezea hali iliyopelekea nchi ya Uganda kuichagua nchi ya Tanzania kama sehemu ya kujifunza kuhusu Sekta ya Madini, Lokeris alisema kuwa, baada ya kutanya utafiti katika nchi za Aftika Mashariki, walibaini kuwa nchi ya Tanzania ni nchi iliyopiga hatua kubwa kwenye usimamizi wa sheria na kanuni za madini hali iliyopelekea wananchi wengi kunufaika nayo hususan wachimbaji wadogo wa madini.

  Aliendelea kusema kuwa, Sekta ya Madini Nchini Uganda ndio inaanza kukua, hivyo wameona ni vyema kuja Tanzania kwa ajili ya kujifunza na kwenda kuimarisha Sekta ya Madini ili baada ya miaka kadhaa angalau iwe inakaribiana na nchi ya Tanzania.

  Akielezea mikakati ya matumizi ya uzoefu mkubwa ujumbe huo ilioupata kutoka kwa nchi ya Tanzania, Waziri Lokeris alisema hatua ya kwanza itakayofanywa na Serikali ya Uganda kupitia Wizara yake ya Madini ni kuhamasisha wachimbaji wadogo wa madini kuunda vikundi na kuwapatia leseni.

  Aliongeza kuwa, mara baada ya kuwapatia leseni hatua itakayofuata itakuwa ni kuwaleta Tanzania kwa ajili ya mafunzo ambapo watajifunza kupitia wachimbaji wadogo wa madini wa Tanzania waliofanikiwa kwenye shugfhuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini.

  Aliendelea kueleza kuwa, nia ya Serikali ya Uganda kupitia Wizara yake ya Madini ni kuhakikisha sekta hiyo inakua kwa kasi na kuanza kuzalisha dhahabu na kuuza nyingine nje ya nchi na kujipatia mapato makubwa.

  “Tumefurahishwa na usimamizi mzuri kwenye sekta ya madini hususan kwenye eneo la uwezeshaji wa wachimbaji wadogo, tumeona namna wanavyochenjua madini huku wakizingatia sheria na kanuni za mazingira,”alisisitiza Waziri Lokeris.

  Naye Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo akielezea mafanikio ya sekta ya madini nchini alieleza kuwa, mafaniko yaliyopatikana ni pamoja na uboreshaji wa sheria mpya ya madini pamoja na kanuni zake inayotambua madini kama mali ya watanzania na kusisitiza kuwa wachimbaji wadogo wamekuwa wanufaika kwa kiasi kikubwa.

  Aliongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeondoa tozo mbalimbali zisizo za lazima hali iliyopelekea wachimbaji wadogo kuzalisha madini kwa gharama nafuu na kulipa kodi na tozo mbalimbali serikalini.

  Alieleza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko nchini kama njia mojawapo ya kudhibiti utoroshwaji wa madini kwa kuhakikisha wachimbaji wa madini wanakuwa na soko la uhakika la kuuzia madini yao kwa bei yenye faida.

  Naye mmiliki wa mgodi wa dhahabu wa Blue Reef uliopo katika eneo la Rwamgaza Wilayani Geita mkoani Geita ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Geita (GEREMA), Christopher Kadeo akizungumza na ujumbe huo uliofanya ziara kwenye mgodi wake akielezea mchango wa mgodi wake katika jamii iliyopo jirani alisema mgodi wake tangu ulipoanzishwa mwaka 1991 mpaka sasa umefanikiwa kuajiri watumishi 160 na vibarua takribani 200.

  Alieleza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na uboreshaji wa huduma za jamii kama vile afya, elimu, ulinzi kupitia ujenzi wa vituo vya polisi na kusisitiza kuwa mgodi umekuwa ukishirikiana kwa karibu zaidi na Tasisi nyingine za Serikali kama vile Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Chuo Cha Ufundi Dar es Salaam (DIT), Wizara ya Madini, Tume ya Madini na mashirika mengine ya kimataifa.

  Aidha, aliongeza kuwa mgodi wake umewahi kupewa tuzo ya utunzaji bora wa mazingira na Rais wa Awamu ya Tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

  Akielezea mikakati ya mgodi wake kwenye shughuli za uchimbaji wa madini alisema mgodi wake unatarajia kufanya utafiti zaidi ili kugundua madini zaidi na kuunganisha leseni zake tano unazomiliki na kutoka kwenye uchimbaji wa kati hadi mkubwa.

  0 0

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja wakifurahi jambo na Mhamasishaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa Stars, Ndg. Peter Mollel alimaarufu kama Pierre Liquid ( wa tatu kushoto) walipokutana leo katika Hoteli ya Nashera Jijini Dodoma, kabla ya kumualika Bungeni kwa ajili ya kusikiliza Vikao vya Bunge vilivyoanza jana Jijini Dodoma. Wa tatu kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kushoto), Mbunge wa Vijana kutoka Mkoa wa Dodoma, Mhe. Miriam Ditopile (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Ndg. Billy Chidabwa
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akifurahi jambo na Mhamasishaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa Stars, Ndg. Peter Mollel (wa pili kulia) alimaarufu kama Pierre Liquid walipokutana leo katika Hoteli ya Nashera Jijini Dodoma, kabla ya kumualika Bungeni kwa ajili ya kusikiliza Vikao vya Bunge vilivyoanza jana Jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mhamasishaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa Stars, Ndg. Peter Mollel alimaarufu kama Pierre Liquid walipokutana leo katika Hoteli ya Nashera Jijini Dodoma, kabla ya kumualika Bungeni kwa ajili ya kusikiliza Vikao vya Bunge vilivyoanza jana Jijini Dodoma. Katikati ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai
  Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akisalimiana na Mhamasishaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa Stars, Ndg. Peter Mollel alimaarufu kama Pierre Liquid (Kushoto) walipokutana leo katika Hoteli ya Nashera Jijini Dodoma, kabla ya kumualika Bungeni kwa ajili ya kusikiliza Vikao vya Bunge vilivyoanza Jana Jijini Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

  0 0


  0 0

  Na Ripota Wetu-Lagos, Nigeria

  MKURUGENZI Mtendaji mpya wa Taasisi ya Tony Elumelu ya nchini Nigeria, Ifeyinwa Ugochukwu, ameanza majukumu yake mapya kuanzia Aprili 1, mwaka hu.

  Ifeyinwa anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa tatu na wa kwanza kwa Afrika kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tony Elumelu, ambapo kabla ya kuchukua nafasi hiyo aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Ushirikiano na Tahmini wa taasisi hiyo.

  Desemba mwaka jana Taasisi ya Tony Elumelu ambayo inafanyakazi ya kuwawezesha wajasiriamali wa Kiafrika, ilitangaza uteuzi mpya wa Ifeyinwa kama Mkurugenzi Mtendaji nafasi ambayo ilikuwa ikishikiwa na mtangulizi wake Parminder Vir, ambaye kwa sasa anakwenda kuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Ushauri wa Tony Elumelu.

  Katika jukumu yake Ifeyinwa alisema atazingatia kuongeza umuhimu wa Programu ya Uwekezaji wa Tony Elumelu ya dola milioni 100 kwa kipindi cha miaka 10 na kuimarisha mahusiano kati ya Afrika na mfumo wa kimataifa wa ujasiriamali, kuwawezesha wajasiriamali wa Afrika na matokeo ya kujenga ajira na mali juu ya bara. 

  Pia atachukua jukumu la kuweka nafasi ya TEF Connect- ambalo ni jukwaa la mitandao ya digital kwa wajasiriamali wa Afrika kama kitovu cha kuunda uhusiano wa biashara, kubadilishana uzoefu na kusambaza ujuzi kwa Bara la Afrika.

  Katika kipindi cha miaka miwili Ifeyinwa Ugochukwu, alikuwa katika kutoa uzoefu wake hasa kupitia nafasi yakwe yake ya zamani ya Mkurugenzi wa Ushirikiano na Tathmini kabla ya kupata nafasi mpya ya kuongoza taasisi hiyo.

  Taariga kwa umma iliyotolewa na Taasisi ya Tony Elumelu, ilieleza kwamba kwa nafasi yake mpya pia ni kiongozi anayethibitishwa na maono ya biashara kwa akili na uwezo wa kuwaleta watu pamoja. 

  Ilielezwa kuwa uwezo wake wa namna ya kuisuka taasisi inavyostahili, kulingana na mazingira. Lakini pia ataangazia maendeleo na mazingira ya taasisi kwa kuona namna gani inaweza kupiga hatua zaidi.

  Akizungumza kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini, Tony Elumelu, Mwanzilishi wa Tony Elumelu Foundation alisema “Tuna hakika kwamba Ifeyinwa ndiye mtu makini wa kuimarisha Taasisi katika awamu yake ya uongozi. Uteuzi wake kama Mkurugenzi Mtendaji utaimarisha taasisi yetu ya kuongeza kiwango cha kujitolea na kufungua fursa katika mazingira ya ujasiriamali kote katika Bara la Afrika.

  “Nimekuwa nikisema kuwa hakuna mtu wa ulitengeza Bara la Afrika, na maonyesho zaidi na utekelezaji wa azimio hili ni wajibu wetu wote,” alisema Mwasisi wa taasisi hiyo Tony Elumelu

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Viongozi wengine wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkoa wa Mtwara, Wabunge na viongozi wengine akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itaayotumika katika ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi km 210 sehemu ya Mtwara-Mnivata km 50 katika hafla iliyofanyika sehemu ya Naliendelea mkoani Mtwara.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Viongozi wengine wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkoa wa Mtwara, Wabunge na viongozi wengine akivuta utepe kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi km 210 sehemu ya Mtwara-Mnivata km 50 katika hafla iliyofanyika sehemu ya Naliendelea mkoani Mtwara.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Naliendele mkoani Mtwara kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi km 210 sehemu ya Mtwara-Mnivata km 50.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachi wa Naliendele mkoani Mtwara wakati akielekea kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi km 210 sehemu ya Mtwara-Mnivata km 50.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Mtwara mjini Murji mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi huo wa barabara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nanguruwe mkoani Mtwara wakati akielekaea Newala.
   Wananchi wa Nanguruwe Mtwara vijijini wakishangilia mara baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwatatulia sehemu itakapojengwa hospitali katikka eneo hilo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nanyamba mkoani Mtwara wakati akielekea Newala. PICHA NA IKULU


  0 0

  TANZANIA PRIVATE SECTOR FOUNDATION 


  TAMKO LA KUMUUNGA MKONO MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA MSIMAMO WAKE THABITI NA MAELEKEZO KWA WIZARA YA FEDHA NA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA JUU YA UMUHIMU WA KUPANUA WIGO WA WALIPA KODI 

  Kwa niaba ya Wadau wa Sekta Binafsi, Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Menejimenti, tunachukua fursa hii kwa mara nyingine tena kumpongeza Mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumshukuru kwa Hotuba yake na Maagizo yake aliyoyatoa wakati akizungumza na Wizara ya Fedha na Mipango, Watendaji wa TRA na Taasisi zingine za Umma tarehe 1 Aprili 2019. Tumefarijika sana na juhudi zake binafsi za kuona umuhimu wa kuhakikisha kuwa Nchi yetu ina Mazingira Bora na ya Kuvutia Uwekezaji na Ufanyaji Biashara. 

  Mheshimiwa Rais, amezitaja na kukemea Changamoto za Kodi kuwa ni kubwa na nyingi; utitiri wa taasisi za usimamizi na gharama zao ambazo zimekuwa zinatukwaza sana Sekta Binafsi kwa muda mrefu. Mzigo wa kodi ni mkubwa kwa wachache ambao wameandikishwa kwa sekta binafsi na hivyo maagizo yake kwamba zirekebishwe haraka yametupa faraja na hamasa ya kuongeza mchango wetu katika Uchumi wa Nchi Yetu tukielekea katika Uchumi wa kati na wa Viwanda. 

  Sekta Binafsi tupo tayari kukaa na Serikali kupendekeza na kufikia muafaka wa njia mbalimbali za kupanua wigo wa walipa kodi, ili kwa pamoja, tufanyie kazi maagizo haya wa Mheshimiwa Rais. Sekta binafsi tutakutana ili kujadili na hatimaye kuwasilisha mapendekezo yetu kwa Mheshimiwa Rais kupitia Waziri wa Fedha na Mipango yatakayosaidia kuongeza wigo na kupunguza mzigo wa kodi kwa wadau. 


  Katika kuratibu zoezi hili, TPSF na Sekta Binafsi katika ngazi zote kuanzia mawilayani na mikoani hadi Taifa tutashirikiana na Serikali na Taasisi za Sekta ya Umma ili kwa pamoja tujadiliane na kukubaliana hatua za haraka za kuchukuliwa kurekebisha mapungufu na changamoto alizoziainisha na kuzitolea maagizo Mheshimiwa Rais. Tuna uhakika kuwa tukitekeleza azma yake tutapanua wigo wa kulipa kodi na mapato ya Serikali na Uchumi wetu utaimarika na kuongezeka kwa kasi kubwa. 

  Aidha, Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kumteua Naibu Katibu Mkuu (Sera) katika Wizara ya Fedha na Mipango. Sekta Binafsi tyumepokea uteuzi huu kwa mikono miwili na kuuona kama ni mwanzo mzuri wa kujengea uwezo wa Wizara katika kufanyia kazi masuala ya Sera, badala ya kutegemea TRA kama mshauri pekee. Tuna imani kwamba mtizamo wa Wizara ya Fedha na Mipango ni wa kukuza uchumi kupitia Sera ya Kodi lakini Mamlaka ya Mapato mtizamo wake ni wa kukusanya kodi hivyo basi kuna mgongano wa maslahi. Wizara pia itakuwa na uhuru wa kufanyia kazi masuala mtambuka. 

  TPSF tunaungana na Mheshimiwa Rais kuhimiza na kuhamasisha Watanzania wote tulipe kodi kwa manufaa ya maendeleo yetu wenyewe. TPSF inamhakikishia Mheshimwa Rais kwamba tupo tayari kushirikiana na Serikali kupanua wigo wa walipa kodi pamoja na kushiriki kikamilifu katika Kamati za ushauri kuhusu masuala ya kodi, kama alivyoelekeza. Tuna uhakika kuwa kodi zikipunguzwa na taratibu za ulipaji zikiboreshwa na kufanywa rafiki zaidi, WaTanzania tutakuwa tayari kulipa kodi halali bila kushurutishwa au kutishwa. 

  Tunaahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali na Sekta nzima ya Umma kwa kuwa na majadiliano ya kudumu yenye nia ya kuboresha mazingira ya kuwekeza, kushindana ndani na nje ya nchi na kuhakikisha kuwa WaTanzania, wadau wa Sekta Binafsi, wananufaika kutokana na jitihada hizi na kukuza uchumi wao na Taifa Zima kwa Ujumla. 

  Imetolewa na Salum Shamte 
  Mwenyekiti - Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) 
  April 3, 2019

  0 0  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Seneti ya Burundi, Mhe. Reverien Ndikuriyo kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dodoma, Aprili 3, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Seneti ya Burundi, Mhe. Reverien Ndikuriyo, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na. Paschal Dotto-MAELEZO

   Rais Dkt John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa Nanyamba, Tandahimba, na Newala Mkoani Mtwara kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya uhakika ili kuunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi na wananchi wa Mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ili kuweza kujiletea maendeleo yao.

  Akizungumza katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, Rais Magufuli amesema Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba-Nanyamba yenye urefu wa kilometa 50 itakayogharimu kiasi cha Tsh.bilioni 86 na kumwagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe kutangaza zabuni ya ujenzi wa kilometa zingine na kufikia kilometa 100 na hivyo kuunganisha kwa urahisi nyanda za kiuchumi katika mikoa ya kusini.

  “Barabara hii itakuwa ni kiunganishi cha uchumi mikoa ya kusini, hatuwezi kushindwa kujenga kilometa 100, lengo letu kuu ni kuiunganisha Bandari yetu ya Mtwara na mizigo inayotoa Malawi,” alisema Rais Magufuli.

  Aidha Rais Magufuli alisema kuwa katika kuwainua wakulima wa Mkoa wa Mtwara, ambapo Serikali imetekeleza ununuzi wa korosho kutoka kwa wananchi wenye korosho zaidi ya kilo 1500, na Tsh Bilioni 50 tayari zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa wakulima hao, na kwa upande wa wakulima wa korosho wenye kilo chini ya 1500 wamelipwa kiasi cha Tsh Bilioni 578.

  Rais Magufuli amewahiza wafanyabiashara walanguzi wa zao la korosho ‘Kagomba’ kuacha kuwadhulumu wakulima wadogo kwa kuwapa bei ambayo hailidhishi huku wakijua wametumia gharama kubwa katika kuendeleza zao hilo, na kusema serikali ya Awamu ya tano haitarudi nyuma kuwatetea wakulima hao.

  “Utakuta mtu amelima korosho zake, amenunua madawa, ametumia gharama kuzivuna unakuja kumpa bei ya 1500, kwa Serikali ya Awamu ya Tano hili halikubaliki”, alisema Rais Magufuli.

  Akiongelea miradi mingine inayotekelezwa serikali ya Awamu ya Tano kuwa ni pamoja na upanuzi wa bandari ya Mtwara, , upanuzi wa uwanja wa Ndege na ukarabari wa mradi wa maji wa makonde ambao utagharimu kiasi cha Tsh.bilioni 160 zikiwa ni fedha za mikopo kutoka Serikali ya India unaowezesha ujenzi wa miradi ya maji katika miji 28 nchini.

  0 0

  Na Farida Ramadhani na Josephine Majura, WFM, Dodoma

  Serikali imeleeza kuwa imeshawalipa Wazabuni 2048 kiasi cha Shilingi 199 tangu kutolewa kwa tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 3 Januari, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam la kutaka Wazabuni wote wanaoidai Serikali walipwe.

  Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM), Mhe. Ritta Kabati, aliyetaka kujua baada ya tamko la Mhe. Rais kuhusu Wazabuni wote wanaoidai Serikali walipwe ni Wazabuni wangapi wameshalipwa.

  Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alieleza kuwa kati ya Wazabuni 2048 waliolipwa na Serikali, Wazabuni 1,277 walihudumia Sekretarieti za Mikoa na 771 walihudumia Wizara, Taasisi na Wakala za Serikali. Dkt. Kijaji alifafanua kuwa Shilingi 3,729,605,175 zimetumika kulipa Wazabuni waliotoa huduma kwa Sektretarieti za Mikoa na Shilingi 195,334,409,791.64 zimetumika kulipa Wazabuni wa Wizara, Taasisi na Wakala za Serikali.

  “Ikumbukwe kuwa madeni yote haya yalilipwa baada ya uhakiki kufanyika”, alisisitiza Dkt. Kijaji. Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kulipa madai mbalibmali ya wazabuni kulingana na upatikanaji wa fedha, sambamba na uhakika wa madai husika. Dkt. Kijaji amesema kuwa ili kukamilisha zoezi la uhakiki kwa wakati, wazabuni wote wanatakiwa kutoa ushirkiano, hususan kuwasilisha taarifa na vielelezo sahihi vya madai yao pindi wanapotakiwa kufanya hivyo.

  Katika swali la nyongeza Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Kabati alitaka kujua vigezo vilivyotumika kuwalipa wazabuni hao.

  Akijibu swali hilo la nyongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa vipo vigezo vingi ambavyo Serikali imevitumia kulipa madeni hayo moja ikiwa umri wa deni, madeni ambayo yamekaa kwa muda mrefu na ambayo tayari yamehakikiwa ndiyo yanapewa kipaumbele katika malipo.

  Aliongeza kuwa kigezo cha pili ni riba Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kwa madeni ambayo riba yake inakuwa kulingana na muda, ili Serikali isiendelee kuumia wala mwananchi asiendelee kuumia.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji

  0 0


  KUHARIBU MIUNDOMBINU YA UMEME.

  Mnamo tarehe 01.04.2019 saa 23:00 usiku huko Kitongoji cha Mwaisongoli, Kijiji cha Mpunguti, Kata ya Ikama, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliwakamata watu wawili waliofahamika kwa majina ya 1. ELIA CHARLES [24] na 2. AMIR OMAR [27] wote vibarua wa Kampuni ya Umeme wa REA – STEG International Service na wakazi wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe kwa kuharibu miundombinu ya umeme.

  Watuhumiwa walikamatwa wakiwa wanakata nyaya za umeme za kampuni ya REA – STEG International Service kwa kutumia plaizi kwa lengo la kwenda kuuza ili wajipatie fedha. Thamani halisi ya uharibifu huo bado kufahamika. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

  MAUAJI – MBEYA MJINI.

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawasaka watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la AIDAN PAUL CHONGOLA [27] Mkazi wa Hayanga, Dereva Bodaboda.

  Ni kwamba mnamo tarehe 03.04.2019 saa 02:00 usiku huko maeneo ya Ilomba, Jijini Mbeya, marehemu akiwa katika kituo chake cha kazi akiwa na Pikipiki yake yenye namba za usajili MC 557 BBT aina ya Kinglion rangi nyeusi alikodishwa na watu wawili wanaume wasiofahamika ili awapeleke Ituha lakini walipofika maeneo ya Ituha Relini watu hao walimchoma kitu chenye ncha kali upande wa kulia tumboni na kusababisha kifo chake na kasha kuondoka na Pikipiki hiyo.

  Mwili wa marehemu ulikutwa kando kando ya reli ya Tazara, Mtaa wa Tonya April, 03, 2019 saa 07:00 asubuhi ukiwa na jeraha tumboni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu. Aidha msako mkali wa kuwatafuta waliohusika katika tukio hili kwa hatua zaidi za kisheria.

older | 1 | .... | 1830 | 1831 | (Page 1832) | 1833 | 1834 | .... | 1904 | newer