Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1828 | 1829 | (Page 1830) | 1831 | 1832 | .... | 1903 | newer

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Askofu wa Jimbo la Ifakara, Salutaris Libena wakiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Wa pili kulia ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Fancis wa Asiz Ikwiriri, Padre Disma Kimboi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Askofu wa Jimbo la Ifakra, Salutarisi Libena baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Katikati ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa ambaye alipewa nafasi ya kusalimia wakati Waziri Mkuu alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani Rufiji, Machi 29, 2019. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na wa nne kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Wengine kutoka kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Jimbo la Ifakara, Salutaris Libena na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Francis wa Asiz Ikwiriri, Padre Dismas Kimboi
  Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani, Machi 29, 2019
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya imetoa msaada wa pikipiki yenye thamani ya Sh.milioni tatu kwa Karapina Foundation ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika harakati za udhibiti wa dawa za kulevya ikiwa pamoja na utoaji wa elimu yatonayo na matumizi ya dawa hizo. 

  Akizungumza jana Machi 29, 2019 jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi pikipiki hiyo kwa Karama Foundation , Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogars Siyanga amesema mamlaka hiyo imekuwa ikishirikiana na na mashirika yasiyo ya kiserikali na vikundi mbalimbali vya kijamii katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini. 

  Amesema mamlaka hiyo inatambua na kuthamini kazi zinazofanywa na mashirika hayo huku akifafanua Karapina Foundation ni shirika ambalo linafanya kazi za udhibiti wa dawa za kulevya kwa kutoa elimu kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya, kutembelea vituo vya kuwasaidia waathirika na dawa na kutembelea vijiwe vyao na kuwashauri waende kwenye vituo vya matibabu. 

  "Katika kufanya kazi hizo Karama Foundation kupitia Karama Masoud ambaye ndio mwenye kufanya harakati hizo amekuwa na tatizo kutoweza kuwafikia walengwa wengi na kwa wakati, hii ni kutokana na kutokuwa na usafiri .Mamlaka imeamua kumkabidhi pikipiki yenye thamani ya Sh.milioni tatu ili imsadie katika kazi hiyo. 

  "Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inawataka Karapina Foundation kuitumia pikipiki hii kwa kazi iliyokusudiwa ili kufanikisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya .Aidha Karapina Foundation wanatakiwa kuitunza ili pikipikipi idumu muda mrefu,"amesema Kamishina Jenerali Siyanga. 

  kuona  kwa lengo la kuwezesha kazi za udhibiti wa dawa za kulevya ikiwa pamoja na kutoa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya na kutembelea vit ufanisi wa shughuli muwezesha katika harakati zake za kupambana na dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kutoa elimu sema itaendelea kushirikana na taasisi mbalimbali zikiwemo za watu bi binafsi pamoja na makundi ya watu 

  Amefafanua kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikifuatilia namna ambavyo Karapina Foundation imekuwa ikiifanya kazi hiyo kwa moyo wa uzalendo na hivyo imeona ni vema ikatambua mchango wake kwa kumpa pikipiki na kwamba itaendelea kumsaidia kadri inavyowezekana hasa kwa kutambua kazi ya kupambana na dawa za kulevya ni jukumu la kila mmoja wetu. 

  Pia amesema mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, imekuwa ikishirikiana na makundi na taasisi za watu mbalimbali na hivyo wamekuwa wakisaidia makundi hayo kwa nyakati tofauti."Ni jukumu letu mamlaka kuzisaidia taasisi binafsi na makundi ya watu mbalimbali kwani tunaamini kwa umoja wetu tutafanikiwa kukomesha dawa za kulevya nchini. 

  "Leo hii tumekabidhi pikipiki hii kama kitendea kazi kwa Karama Foundation na tumekuwa tukifanya hivyo kwa taasisi nyingine pia.Kikubwa tunachoweza kueleza kwa leo, tunatambua kazi nzuri inayofanywa na Karama na hivyo katika kuthibitisha kumtambua tumeona anastahili kuwepa pikipiki.Tumekuwa tukizungumza naye Karama mara nyingi na amekuwa akija ofisini kwetu na kufanya mazungumzo .Tumeona tunakila sababu ya kumsaidia ili atekeleza kile ambachoa amekuwa akikifanya kwa shida na hara,"amesema Kamishina Jenerali Siyanga. 

  Kwa upande wake Karama Masoud ambaye ndio anayeisimamia Karama Foundation , amesema anashukuru kwa msaada wa kitendea kazi ambacho amekipata na kwamba mamlaka imethibitisha kuwa iko pamoja naye , hivyo ameahidi ataendelea kuifanya kazi hiyo kwa uzalendo mkuwa na wa hali ya juu. 

  "Harakati za kupambana na dawa za kulevya nimeianza muda mrefu , ilifika mahali nikawa nakata tamaa kwani changamoto ni nyingi ikiwemo ya kifedha na usafiri, hatimaye leo hii Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wameona ninastahili kupata pikipiki ili kurahisisha namna ya kuwafikia Watanzania wengi zaidi. 

  "Kwangu sina cha kuwalipa zaidi ya kutambua , kazi ambayo naifanya inatathiminiwa.Naomba nitumie nafasi hii kueleza wazi, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli imesimama kidete kukomesha dawa za kulevya .Kwa mazingira yaliyopo na jitihada za mamlaka nina uhakika Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana,"amesema Masoud.

  Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Siyanga  (wa kwanza kushoto) akiwa ameshika pikipiki leo jijini Dar es Salaam baada ya kumkabidhi Karama Masoud ambaye amekuwa akishiriki katika udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya na kutoa elimu kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya dawa hizo kupitia Karama Foundation.
   Kamishina  Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Siyanga (kushoto), akiwa ameshikana mkono na Karama Masoud kutoka Karama Foundation baada ya kumkabidhi pikipiki kwa ajili ya kumsaidia kwenye shughuli zake za kudhibiti dawa za kulevya na kutoa elimu kuhusu athari zitokanazo na matumizi ya dawa hizo.Kamishina Siyanga amekabidhi pikipiki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Karama Masoud kutoka Karama Foundation (kushoto) akiwa ameshikana mkono na Kamishna wa Kitengo cha Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi baada ya tukio la mamlaka hiyo kukabidhi pikipiki kwa lengo la kumuwezesha Masoud kutekeleza majukumu yake.

  0 0

   Bi. Amina Jumanne Mkazi wa kipera ambaye ni kibarua katika ujenzi unaoendelea eneo la Maekani akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) wakati alipotembelea shughuli ya Ujenzi inayoendelea. 
   Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akiwa na mwenyeji wake Makamu Mkuu wa Chuo sili Chuo Pro. Lughano Kusiluka; baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe; alipofanya ziara hivi karibuni.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akiweka saini kwenye kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango akiwasili eneo la Maekani ambako ujenzi wa mabweni ya wanafunzi unaendelea. Kushoto ni Prof. Ernest Kihanga Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, akifuatiwa na Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB), mwenye kofia ni injinia na msimimizi ya mradi Injinia Focus Alex Odecho, na wa mwisho kulia ni Prof. Lughano Kusiluka Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akielekeza jambo kwenye moja wapo ya majengo ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea eneo la Maekani. Kulia ni msimamizi wa mradi Injinia Focus Alex  Odecho.
   Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) afurahia zawadi yenye kumbukumbu ya Chuo Kikuu Mzumbe alichosoma na kufanya kazi kabla ya kuingia kwenye siasa.
  Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (katikakati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe alipotembelea hivi karibuni.  Naibu Waziri Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) ametembelea Chuo Kikuu Mzumbe na kukagua ujenzi wa Mabweni ya Wanafunzi unaoendelea katika eneo la Maekani, Makao Makuu ya Chuo hicho, Morogoro.

  Mhe. Naibu Waziri, amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Uongozi wa Chuo kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua kero ya malazi kwa wanafunzi na kusisitiza umuhimu wa kuanza mara moja awamu ya pili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na mihadhara katika eneo hilo ili kuwarahisishia wanafunzi kutotembea umbali mrefu wakati wa masomo.

  “Serikali inategemea mchango mkubwa wa Vyuo Vikuu katika kutimiza malengo; hasa kwenye hili la ukuaji wa uchumi. Pamoja na kwamba tunajivunia uchumi wetu kukua lakini tusibweteke, badala yake tufanye tafiti na kuandaa vema vijana ambao watakuwa watumishi bora wa Umma wanaoendana na dhana ya sasa ya nidhamu ya kazi. Hivyo, nimefarijika sana kuona maendeleo na hatua kubwa ambayo mmepiga kitaaluma na katika miradi ya maendeleo mnayosimamia” alisema Mhe. Naibu Waziri.

  Akikamkaribisha Naibu Waziri huyo, ambaye pia alipata fursa ya kuzungumza na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe; Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka amemweleza Mheshimiwa Naibu Waziri kuwa, kwa sasa Chuo Kikuu Mzumbe kinatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu katika Kampasi Kuu ya Morogoro, Kampasi ya Mbeya na Kampasi ya Dar-es-salaam na kwamba, lengo ni kuendelea kutumia ruzuku inayotolewa na Serikali na vyanzo vya mapato ya ndani kuendeleza ujenzi na kuboresha miundombinu ya Chuo ili kujenga mazingira bora ya utoaji wa Elimu ya Juu.

  “Napenda kuipongeza sana Serikali yetu kwa kutambua mchango mkubwa wa Vyuo Vikuu nchini, na kwa upande wa Taaluma, Chuo chetu kitaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuendeleza Uchumi wa Viwanda; kwa kuendelea kufanya tafiti, kubuni miradi ya maendeleo na kutoa nguvu kazi itakayowezesha Tanzania kufikia malengo yake” alisema Prof. Kusiluka.

  Ameahidi Chuo Kikuu Mzumbe kuendelea kuimarisha uhusiano na kufanya kazi kwa karibu zaidi na Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Umma kwa kubadilishana ujuzi na uzoefu, pamoja na kutumia wanataaluma kuboresha utendaji Serikalini, kulinda nidhamu na kuinua kiwango cha elimu inayoendelea kutolewa na Chuo hicho.

  Mradi wa Ujenzi wa Mabweni katika Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu Mzumbe ambao unafadhiliwa na Serikali,unatekelezwa na SUMA JKT na unategemewa kukamilika ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu. Mradi unategemea kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.5 hadi utakapokamilika. Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha wanachuo wengi zaidi katika Kampasi Kuu kukaa kwenye hosteli za Chuo.

  0 0

  Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo (Kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 30, 2019 Jijini Dodoma kuhusu kuliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kusimamia Uchaguzi ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ufanyike ndani ya siku 30 kuanzia leo.Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bw.Alex Nkenyenge.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Alex Nkenyenge (Kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 30, 2019 Jijini Dodoma kuhusu kutekeleza maagizo ya Serikali kwa Baraza hilo kusimamia Uchaguzi ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ndani ya siku 30 kuanzia leo.Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo.

  ……………………

  Na Shamimu nyaki –WHUSM

  Serikali imeliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kushirikiana na Shirikisho la mpira wa Miguu (TFF) kuhakikisha uchaguzi ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) unafanyika ndani ya siku 30 kuanzia leo.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo katika mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa migogoro iliyokuwepo huko nyuma imeshafika tamati hivyo uchaguzi ndani ya Klabu hiyo ni lazima ufanyike.

  “Nailekeza BMT iwaelekeze TFF kuhakikisha taratibu zote za uchaguzi zinafuatwa na uchaguzi ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans unafayika ndani ya siku 30 kuanzia sasa”.amesema Bw.Singo

  Aidha Bw.Singo amewahisi Viongozi, wanachama na wapenzi wa Klabu ya Dar es Salaam Young Africans kutoanzisha migogoro wala vikwazo vingine bali kutumia siku 30 hizo kufanya uchaguzi ili kupata viongozi watakaoisimamia na kuiongoza Klabu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mpira wa miguu ndani na nje ya nchi.

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw.Alex Nkenyenge amesema amepokea maagizo na atayafanyia kazi mara moja ili kipindi kilichowekwa na Serikali cha siku 30 Klabu ya Yanga iwe tayari ina uongozi.

  Bw.Nkenyenge ameongeza kuwa atahakikisha Kamati ya Uchaguzi ya TFF inapanga utaratibu unaotakiwa kufuatwa kulingana na Katiba ya Shirikisho hilo ili Uchaguzi huo ufanyike hatimaye migogoro iliyodumu kwa muda mrefu ndani ya Klabu hiyo ifikie mwisho na Klabu iendelee kufanya vizuri katika mpira wa miguu.

  Klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ni miongoni mwa Klabu kubwa za mpira wa miguu hapa nchini ambayo kwa muda mrefu haijatekekeleza uchaguzi kwa mujibu wa Katiba yao

  0 0


  SPIKA 2
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya madini wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, mafunzo hayo yamefanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
  SPIKA 5
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa mgeni ramsi katika semina ya wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya madini wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ,kulia kwake ni Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko  na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati  na Madini Mhe, Dunstan Kitandula. Semina hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma

  0 0


  V25A7464
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Ndg. Florence Mattli alipomtembelea leo Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
  V25A7482
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) katika picha ya pamoja na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Ndg. Florence Mattli baada ya mazungumzo yaliyofanyika  leo Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. 
  V25A7426
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Ndg. Florence Mattli alipomtembelea leo katika Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hashim Mgandilwa (kushoto), akisalimiana na Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Kusini, Bw. Eliamini Mkenga (katikati), mara baada ya kuwasili kijijini Namungo kwa ajili ya kufungua mafunzo ya matumizi salama ya kemikali kwa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa mgodi wa Namungo. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. Davidi Elias na kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Gemini, Bw. Alfred Michael, ambaye ni mmoja ya viongozi wa kampuni za wachimbaji wanaoshiriki mafunzo hayo.
  Mkuu wa Wilaya ya Namungo, Mhe. Hashim Mgandilwa (kushoto), akiongea na wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa Namungo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wachimbaji hao yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kusini na kufanyika katika kijiji cha Namungo kilichopo wilayani Ruangwa katika Mkoa wa Lindi leo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. David Elias (kushoto), akiongea kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hashim Mgandilwa (wa pili kushoto), kufungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa Namungo. Wengine kutoka kulia ni Katibu wa Mkuu wa Wilaya na Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Kusini, Bw. Eliamini Mkenga.
  Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hashim Mgandilwa (aliyekaa katikati), akiwa pamoja na wawezeshaji wa mafunzo kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Kijiji cha Namungo, Bw. Abraham Pasati (wa pili kulia, waliokaa), na washiriki wa mafunzo kutoka mgodi wa Namungo.

  ……………………….

  Na Sylvester Omary – GCLA

  Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa amewataka wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa mgodi wa Namungo kuzingatia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali wanapokuwa wanatekeleza shughuli za uchimbaji kwa lengo la kulinda afya zao na mazingira.

  Mgandilwa ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya Matumizi Salama ya Kemikali kwa wachimbaji hao yanayotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kusini na kufanyika kwenye kijiji cha Namungo wilayani Ruangwa.

  “Nawaomba wachimbaji wa mgodi huu mtumie fursa hii ya mafunzo kujifunza Sheria zinazohusu usimamizi na udhibiti wa kemikali ili muweze kuzingatia matumizi salama ya kemikali katika shughuli zenu kwa lengo la kulinda afya zenu na mazingira yanayowazunguka kwani natambua uchimbaji wa dhahabu unahusisha matumizi ya kemikali na hakuna kemikali isiyo na madhara duniani, hivyo mafunzo haya yawasaidie kujua namna bora ya kujilinda na madhara bila kuathiri shughuli zenu za uchimbaji”, alisema Mgandilwa.

  Alifafanua kuwa sekta ya madini ni sekta muhimu sana katika uchumi na ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano inajitahidi kuwawekea mazingira mazuri wachimbaji ili kuhakikisha wanafaidikia na kazi hizo pia wanalinda afya zao kwa kuwa athari za kemikali nyingine zinaweza kuonekana baada ya miaka mingi.

  Aidha, Mkuu wa Wilaya huyo aliwataka wachimbaji hao kujisajili Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kutambulika kama wadau wanaotumia kemikali katika shughuli za uchimbaji wa madini hayo.

  “Pia, niwaombe wachimbaji wa mgodi huu kutumia mafunzo haya kujifunza namna na taratibu sahihi za kujisajili, hivyo mnapaswa kuuliza maswali pale mnapoona mnahitaji ufafanuzi wa kutosha kutoka kwa wawezeshaji wa mafunzo kwa lengo la kuboresha shughuli zenu na kuwa mabalozi wazuri kwa wengine ambao hawajaweza kupata elimu hii kwa sasa,” Aliongeza.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. David Elias alisema kuwa Mamlaka hiyo imeamua kuwafikia wadau wake na kuwapa elimu ya matumizi salama ya kemikali kwa lengo la kuongeza uelewa wa masuala ya kemikali ili kuepusha madhara makubwa ya kiafya na kimazingira yanayoweza kusababishwa na matumizi yasiyo salama ya kemikali. Vile vile alisisitiza kuwa wachimbaji hao ni sehemu ya wadau wengi ambao Mamlaka imejipanga kuwafikia na kuwapatia elimu hiyo.

  Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji ya Gemini, Alfred Michael ameishukuru Mamlaka hiyo kwa kuamua kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuimarisha shughuli zao za uchimbaji hasa kwenye matumizi ya kemikali.

  “Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuona umuhimu wa kuja kutoa mafunzo haya kwetu kwa sababu yatatusaidia katika kujilinda dhidi ya madhara ya kemikali kwenye kazi zetu za uchimbaji, tunaamini mafunzo haya yatakuwa chachu ya kufuata Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali kwa lengo la kuboresha uchimbaji na kulinda afya na mazingira kwa ujumla”, alisema Michael.

  Mafunzo hayo yamehusisha jumla ya wachimbaji wadogo wadogo 50 kutoka Kampuni za uchimbaji za Gemini na Majini zinazojihusisha na uchimbaji wa dhahabu kwenye mgodi wa Namungo uliopo wilayani Ruangwa katika Mkoa wa Lindi.

  0 0

  WAKATI Mamlaka ya Hali ya Hewa(TMA)ikitangaza uwepo wa mvua nchini,wakazi wa Mbagala Kiuzuiani Mtaa wa Juhudi wameiomba Halmashauri ya Temeke na Mkoa wa Dar es Salaam kuwawekea mifereji au mitaro ya kupitisha maji ili kunusuru makazi yao na watu wa maeneo hayo.

  Wamesema katika eneo la Juhudi changamoto kubwa ni maji kujaa katika makazi ya watu ambayo msingi wake mkubwa ni kukosekana kwa mifereji ya kupitisha maji ya mvua,hivyo yanalazimika kupata katika barabara  na matokeo yake yanakwenda kutuama katika makazi ya watu.

  Wakizungumza leo wakazi wa mtaa huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Juhudi Athuman Namna, wamesema ombi lao kubwa ni eneo hilo kuwekwa mifereji kwani wanaamini ndio ufumbuzi wa kero ya maji kutuama ambayo ni ya muda mrefu huku wakieleza matumaini yao kwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imejikita kuwasiliza wanyonge na kutatua kero zao.

  Wakati mvua za masika zikianza kushika kasi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo  mkoa wa Dar es Salaam wakazi wa mtaa wa Juhudi kata ya Kiburugwa wameeleza hofu yao kufuatia mvua hizo.

  Wamesema kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji makazi yao  yamekuwa njia ya maji taka na inapofika msimu wa mvua maisha yao wanakuwa hatarini pamoja na uwepo wa magonjwa ya mlipuko yakiwamo ya kipindupindu.

  Mkazi wa eneo hilo Hawa Kombo amesema mvua zinaponyesha wakazi wa mtaa huo wanakuwa hatarini kutokana na maji mengi kuelekezwa kwenye nyumba zao.

  Amesisitiza wapo roho juu, kwani wakiona dalili ya mvua au manyunyu  wanakosa raha huku akifafanua mvua ikinyesha maji yote ya juu yanakuja kwenye nyumba zao na barabarani nako maji yanajaa na kusababisha njia kutopitika kabisa

  “Sasa wapo ambao wanatumia mwanya huo kufungulia vyoo vyao basi hapo ndio hatari inapozidi kuwa kubwa magonjwa kama kipindupindu yanakuwa sehemu ya maisha yetu mvua zikianza,”

  Wakati huo huo mkazi mwingine wa eneo hilo Rashid Mgaza amesema kuwa hali ya kufurika maji wakati mwingine inasababisha watoto kushindwa kwenda shuleni kwani kuna wakati maji yanakuwa mengi kiasi cha kufika usawa wa madirisha ya nyumba.

  “Mvua zikinyesha wakazi wa Juhudi hatuna amani kwanza hata mtoto akienda shule unakuwa roho juu hayo maji yanayotiririka hata mtu mzima ni hatari kupita sasa ndio apite mtoto.Ombi letu kwa Serikali itusikie huku nako tunaoishi ni watu na kwa kuwa serikali yetu ni ya wanyonge basi itusikie na kutupatia ufumbuzi wa changamoto hii,” amesema Mgaza

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Juhudi Athuman Namna amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza kuwa imesababishwa na maji yanayotoka maeneo ya juu kukosa mwelekeo na matokeo yake yanashuka chini kwenye makazi ya watu.

  Ameongeza kwa nafasi yake na kwa kushirikiana na wananchi wamechukua hatua mbalimbali za kuwasilina na viongozi wa Manispaa ya Temeke lakini bado hawajapata ufumbuzi wa tatizo hilo.

  “Tukisikia mvua amani inatoweka huku kwetu na kama hii iliyotangazwa watu wanalazimika kuacha nyumba zao lakini ikitengenezwa mifereji hili tatizo litakuwa historia,”

  “Niwaombe viongozi wangu wasikae ofisini waje kuona hali ilivyo maana kwa kuambiwa unaweza usielewe ila ukweli ni kwamba tuna wakati mgumu sana kuelekea hiki kipindi cha mvua,”amesema Namna

  Wakazi wengine wamesema hawana tatizo na Serikali kwani wanaimani na ndio maana haja ya kutoa kilio cha hasa kipindi hiki ambacho mvua hazijashika kasi kwani kuna hatari zaidi kama hakutafanyika jitihada za kuwekwa mitaro hivi sasa."

  Michuzi Blog ambayo ilifika eneo hilo,imeshuhudia baadhi ya wakazi wakiwa wameacha nyumba zao na kwenda kutafuta maeneo ya kujisitiri wakiohofia mvua ambazo zimeanza kunyesha zinaweza kusababisha madhara .
   Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Juhudi uliko Mbagala Kizuiani Athuman Namna akionesha uharibifu wa makazi ya watu ambao umetokana na maji kutuama eneo hilo kutokana na kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji ya mvua katika mtaa huo.
   Moja ya nyumba ambayo iko hatarini kudondoka kutokana na mvua kuharibu miundombinu ya barabara ambayo inaelezwa ni kutokana na kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji ya mvua na hivyo kusambaa barabarani
   Watoto wakiwa katika barabara ya Mtaa wa Juhudi katika eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo barabara hiyo ambayo inatagemewa imeharibiwa na maji ya mvua kwani haina mitaro ya kupitisha maji
   Gari ikiwa imesimama baada ya dereva kukwama katika eneo hilo la Mtaa wa Juhudi lililopo Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.Barabara hiyo pamoja na maeneo hayo yameharibiwa na mvua na kusababisha kero kwa wananchi walio wengi

  0 0

   Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kabla ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 146 wa kundi la 65 la mwaka 2018 katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania 146 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Wakivalishana vyeo mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika tukio lililofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakila kiapo cha Utii mbele ya Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutunukiwa Kamisheni Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoka katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
    Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakati wakielekea kwenda kupiga picha za kumbukumbu Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Maafisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kutunukiwa Kamisheni Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha Mchoro wa Majengo inayotarajiwa kujengwa katika eneo la Bungi Kwa Bihole sehemu ya historia,Wilaya ya Kati Unguja, wakati wa mkutano wake na Viongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar,Uongozi wa Kamisheni ya Utalii na Makamishna ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo,30-3-2019.
  MWANASHERIA Mkuu Mhe. Said Hassan Said na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Ndg. Khamis Mussa wakiwa na Makamishna wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, wakifuatilia mkutano huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
  MAKAMISHNA wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa mkutano huo uliofanyika leo 30-3-2019,Ikulu Zanzibar kuzungumzia masuala ya Utalii Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibare na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Uongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar,Uongozi wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
  KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Ndg. Khamis Mussa akizungumza wakati wa mkutano huo, kulia Mwanasheria Mkuu Mhe. Said Hassan Said na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Zanzibar Ndg Salum Maulid, wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Ikulu leo
  KATIBU Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt. Abdallah Mohammed Juma, akizungumza wakati wa mkutano huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika Ikulu Zanzibar, kulia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Dkt, Amina Ameir Issa na Katibu Mkuu Bi. Khadija Bakari wakifuatilia mkutano huo
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, akichangia Mada wakati wa mkutano huo uliofanyika Ikulu Zanzibar kulia Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bi. Sabaah Saleh na kulia Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Mwenasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu na Makamishna wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  0 0

  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

  Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kutoka Vituo vya Afya mkoani Mwanza, yanayolenga kuwajengea uwezo katika kutoa msaada na huduma za kisaikolojia kwa watoto na vijana wanaoishi na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).


  Mafunzo hayo ya siku tano yalianza jumatatu Machi 25, 2019 hadi Ijumaa Machi 30, 2019 katika ukumbi wa “Isamilo Lodge” Jijini Mwanza ambapo yamewashirikisha wataalam wa afya zaidi ya 60 kutoka Halmashauri mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo Nyamagana, Ilemela, Misungwi, Magu, Ukerewe na Buchosa.


  Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona amesema mafunzo hayo yatawasaidia watoa huduma za afya katika vituo vya tiba na matunzo kutambua namna bora ya kuwahudumia wateja wao hususani watoto na vijana.


  Amesema mafunzo hayo yatawasaidia pia kuwatambua watoto na vijana wenye changamoto kisaiklojia na namna ya kuwasaidia huku wakizingatia upatikanaji wa huduma bora na rafiki kwa wateja kupitia mbinu mbalimbali ikiwemo michezo.


  “Tunatarajia pia wataenda kuanzisha vikundi vya akina mama wanaoishi na maambukizi ya VVU ambao wako kwenye kitengo cha kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili nao waweze kujifunza kupitia uzoefu wao huku vikundi vilivyopo vikiimarishwa zaidi”. Amesema Yona.

  Baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walikuwa wakikumbana na changamoto ya kutambua mazingira halisi yanayowakabili watoto na vijana kupitia klabu zao.


  Shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia taasisi ya Centres for Disease Control (CDC), linashirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutekeleza afua mbalimbali za kupambana na maambukizi ya VVU pamoja na kuwahudumia watu wanaoishi na maambukizi hayo.

  Mmoja wa Wawezeshaji, Margaret Safe kutoka Kibaha mkoani Pwani akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
  Mwezeshaji, Margaret Safe akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
  Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akizungumza kwenye mafunzo hayo.
  Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
  Washiriki wakimsikiliza Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona.
  Mwezeshaji, Dkt. Nikodemas Kikoti akiendelea kutoa mada kwenye mafunzo hayo.
  Washiriki wakimsikiliza Mwezeshaji, Dkt. Nikodemas Kikoti kutoka mkoani Iringa.
  Wataalam wa afya walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia mada kwa umakini.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
  Timu ya wakufunzi wa mafunzo hayo.
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo.
  Washiriki wa mafunzo pia walipewa mtihani na hapa wakiwa kwenye chumba cha mtihani ili kupima uelewa wa kile walichofundishwa.
  Washiriki wakijibu mtihani kuhusu walichofundishwa.
  Baada ya mafunzo ya nadharia darasani yaliyofanyika Isamilo Lodge, washiriki walielekea Lesa Garden kukutana na baadhi ya watoto na vijana kutoka klabu za elimu na makuzi kwa ajili ya kucheza na kufurahi pamoja ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
  Washiriki wa mafunzo hayo wakiwasili Lesa Garden iliyopo Luchelele Jijini Mwanza.
  Mafunzo kwa vitendo kupitia michezo.
  Inaelezwa vijana hujifunza na kuelewa vyema kupitia michezo na hapa michezo imepamba moto.
  Michezo mbalimbali ikiendela.
  Mafunzo kwa vitendo kupitia michezo.
  Washiriki wa mafunzo wakifurahi pamoja na vijana.
  Michezo ikiendelea Lesa Garden.
  Watoa huduma za afya wamehimizwa kutumia michezo kufikisha elimu kwa watoto na vijana.
  Inaelezwa michezo husaidia watoto na vijana kuelewa vyema yale wanayofundishwa hivyo watoa huduma za afya wamehimizwa kutumia michezo pia kuwaelimisha vijana na watoto.
  Washiriki wakifurahia pamoja na vijana.
  Pia kulikuwa na burudani ya muziki ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo ambapo husaidia watoto na vijana kuwa huru kwa watoa huduma za afya.
  Burudani ya muziki.
  Washiriki wa mafunzo wakifurahia muziki pamoja na watoto/ vijana.
  Michezo na burudani ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
  Tazama BMG Online TV hapa chini

  0 0

  Katibu Tawala Wilaya ya Rombo (DAS)Bw. Abubakar Asenga akimuongoza  Dkt. Jimmy Yonazi  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, alipotembelea Minara inayojengwa Rombo na maeneo yenye uhaba wa mawasiliano  ili kuongeza usikivu wa Radio na upatikanaji wa Mawasiliano ya Simu .

  Ziara hii inalengo la kumaliza Changamoto ya maingiliano ya Simu na Radio toka nchi Jirani ya Kenya.

  Naibu katibu Mkuu Dkt Yonaz aliambatana na viongozi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote ili nao waweze kuongeza nguvu zaidi katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ilioahidi kuendelea kuboresha Mawasiliano kwa Wananchi.   Katibu Tawala Wilaya ya Rombo (DAS), Abubakar Asenga akimueleza jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano,Dkt Jimmy  Yonaz alipotembelea Minara inayojengwa Rombo na maeneo yenye uhaba wa mawasiliano  ili kuongeza usikivu wa Radio na upatikanaji wa Mawasiliano ya Simu .  0 0

  Mkakati wa kuhakikisha maendeleo yanawafikia watu wa Hali ya Chini ndiyo msingi utaowafanya Wananchi waendelee kuipenda na kuichagua Ccm. Maneno hayo ameyasema leo Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete alipokuwa anaweza jiwe la Msingi la Zahanati ya Kitongoji Cha Chahua huko mjini Chalinze mapema hivi leo.

  Akiweka jiwe la Msingi ,Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alieleza furaha yake juu ya mafanikio ambao Halmashauri yake imepata kwa upande wa Afya,Elimu,Maendeleo ya Jamii na kusisitiza kuwa haya yanatokana na msimamo ambao Chama Cha Mapinduzi kinasimamia inapofika katika utekelezaji wa ilani yake ambayo inawalenga kuwapelekea Mabadiliko ya Kweli wananchi wa hali za chini kabisa.Mheshimiwa Mbunge Ridhiwani hakusita kueleza jinsi Raisi Magufuli anavyoendelea kupambana kuwasaidia Watanzania hasa katika kuwapatia huduma bora hasa kwa Upande wa Afya.

  "Katika Halmashauri ya Chalinze tumejenga zaidi ya Zahanati 86 katika vitongoji na Vijiji ,Vituo vya Afya zaidi ya 13 na Sasa tunakamilisha Hospitali ya Wilaya ambayo fedha Kiasi cha Shilingi Milioni 500 zinatarajiwa kuletwa kumalizia Ujenzi pamoja na kununua vifaa tiba. Tunachopaswa wana Chalinze wenzangu ni kuendelea kuunga mkono juhudi hizo ambazo Raisi Magufuli anafanya akishirikiana nami Mbunge wenu,Diwani wetu na Mwenyekiti wetu wa Kitongoji." Mbunge Ridhiwani Kikwete alisisitiza.

  “Katika Kata yetu ya Bwilingu, mambo mengi ya kimaendeleo tunayatekeleza ikiwa ni pamoja na kumalizia ahadi za Mheshimiwa Raisi alizozitoa kipindi cha kampeni. Katika Upande wa Elimu ,tunapambana kupunguza wingi wa Wanafunzi pale Shule ya sekondari ya Chalinze kwa kumalizia shule ya sekondari ya pera na mkakati mwengine wa kuanzisha ujenzi wa Shule ya sekondari ya Chahua." Mheshimiwa Mbunge pia aligusia juu ya Ujenzi wa Maabara ya Kisasa katika kituo cha Afya Chalinze ili kusaidia vipimo vya ziada vya Kiafya.

  Akizungumza kabla ya Mbunge kuweka jiwe la Msingi Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Sadallah Maisha alimshukuru Mbunge kwa Msaada anaowasaidia Watu wa Chahua hasa katika maendeleo ya Jamanii. " Mheshimiwa Mbunge tunakushukuru kwa Kutupatia Nondo 80 na fedha taslimu Shilingi Milioni Mbili,LAki Mbili na Nusu. Pamoja nawe Halmashauri na Nguvu zetu Wananchi."

  Mbunge wa Chalinze anaendelea na Ziara ya kuangalia Shughuli za Maendeleo na Utekelezaji wa Ilani katika Vijiji,Kata na Vitomgoji mbalimbali Vya Halmashauri hiyo. Katika Hali nyengine Mvua kubwa iliyonyesha kuanzia Alhamisi imeharibu Miundo mbinu katika Mji wa Chalinze na pera na Vitongoji mbalimbali.
   

   

  0 0

  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) akikagua mashine ya kupima dhahabu katika kampuni ya Busami iliyopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa huo ya kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini tarehe 30 Machi, 2019.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akijadiliana jambo na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Said Ali (katikati) katika kampuni ya Busami iliyopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
  Kutoka kulia Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Said Ali wakisikiliza kero za wamiliki wa mitambo ya kuchenjulia dhahabu (hawapo pichani) kupitia mkutano maalum uliofanyika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

  ………………………..

  Na Greyson Mwase, Kahama

  Ofisi ya Afisa Madini Mkazi, Mkoa wa Kimadini wa Kahama inatarajia kuanzisha soko la madini mapema ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Madini katika kudhibiti utoroshwaji wa madini.

  Hatua hiyo imekuja kufuatia ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliyoifanya mapema leo tarehe 30 Machi, 2019 katika Wilaya ya Kahama lengo likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

  Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Nyongo aliambatana na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Said Ali wataalam kutoka Tume ya Madini pamoja na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

  Mara baada ya kufanya ziara katika baadhi ya mitambo ya kuchenjua dhahabu, Nyongo alifanya kikao na wamiliki wa mitambo hiyo na kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kuzitatua.

  Mara baada ya kusikiliza kero husika ikiwa ni pamoja na ya kutokuwepo kwa soko la madini katika Wilaya ya Kahama, Naibu Waziri Nyongo alimwelekeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama, Adrea Fabian kuhakikisha sehemu ya ofisi yake inatumika kama soko la madini ya dhahabu ambapo wauzaji na wanunuzi watakuwa wanafanya biashara huku serikali ikipata mapato yake, kauli ambayo ilipokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa madini ya dhahabu.

  Aliendelea kusema kuwa kutokuwepo kwa soko la madini katika Wilaya ya Kahama, kunachochea utoroshwaji wa madini ya dhahabu kwakuwa inakuwa vigumu kwa wauzaji wa madini hayo kusafiri umbali mrefu hadi Geita kwa ajili ya kwenda kuuza madini hayo.

  “Hapa tunataka kuhakikisha biashara ya madini inafanyika hapa hapa ili kuwarahisishia wafanyabiashara wa madini ya dhahabu huku Serikali ikipata mapato yake,” alisisitiza Naibu Waziri Nyongo.

  Katika hatua nyingine, Nyongo aliutaka uongozi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama kushirikisha mamlaka nyingine za Serikali kama vile Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mabenki na soko kuanza mara moja.

  Aidha, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wamiliki wa mitambo ya kuchenjua dhahabu kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika kulinda rasilimali za madini kwa kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Madini.

  Wakizungumza katika nyakati tofauti wamiliki wa mitambo ya kuchenjulia dhahabu walioshiriki katika kikao hicho mbali na kumpongeza Naibu Waziri Nyongo wamesema kuwa uwepo wa soko hilo utawarahisishia sana biashara ya madini kutokana na kuepukana na matapeli huku serikali ikipata mapato yake stahiki.

  Walisema kabla ya uamuzi huo wamekuwa wakisafirisha madini hadi Geita kwa ajili ya kuuza hali inayopelekea baadhi yao kuuza kwa watu wasio waaminifu.

  0 0

  Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) Balozi Ali Abeid Aman Karume amewataka Watanzania kutembelea sehemu za Vivutio vya Utalii na kuondokana na dhana kwamba utalii unafanywa na wageni tu.

  Balozi Karume ameyasema hayo leo Wilayani Mbozi,Mkoa wa Songwe wakati alipotembelea eneo la urithi na uhifadhi ambapo kulidondoka KIMONDO chenye uzito wa tani 12 kinachokifanya KIMONDO hicho kinachopatikana Mkoa wa Songwe kuwa ni cha nane(8) duniani na cha pili Afrika kwa Uzito.

  “Nimefurahishwa sana na Historia ya kimondo hichi,ni vyema Watanzania wengi zaidi wakatenga muda kuja kujifunza hapa.Ni jambo la kujivunia kidunia kuwa sehemu ya nchi zanye Vimondo vizito zaidi duniani”Alisema Balozi Karume.

  Wakati huo huo Balozi Karume aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jenarali Mwangela,*Naibu Waziri Mavunde* na Naibu waziri wa Vijana SMZ Mh Lulu Mshamu kukagua maandalizi ya mwisho ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge Kitaifa zinazotarajiwa kuzinduliwa tarehe 2.4.2019 Mkoani Songwe.
  0 0

  Taswira ya Tanzania kimataifa imeendelea kupaa baada ya Taasisi ya Global Peace Index (GPI) kuitangaza Tanzania kushika nafasi ya 51 miongoni mwa nchi zenye amani zaidi duniani katika kipindi cha mwaka 2018. 

  Tanzania imeshika nafasi hiyo ikiwa ni ya juu zaidi kufikiwa tangu mwaka 2010 na kuzishinda nchi kubwa duniani kama Marekani, China, Uingereza na Ajentina ambapo kwa Afrika ipo katika nafasi 10 bora na kuwa kinara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
  Tangu Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli iingine madarakani, Tanzania imekuwa ikipanda nafasi kila mwaka ambapo mwaka 2017 ilishika nafasi ya 54, mwaka 2016 nafasi ya 58 na mwaka 2015 nafasi ya 64. 

  Kwa mujibu wa GPI, sababu zilizoipaisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye amani zaidi duniani ni pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kupambana na rushwa, mgawanyo sahihi wa rasilimali, upatikanaji huru wa taarifa, mazingira wezeshi ya biashara, uhusiano mzuri na nchi za jirani, kiwango cha rasilimali watu, kuheshimu haki za watu wengine na ufanyaji kazi mzuri wa Serikali. 

  “Nchi 71 zilikuwa na amani zaidi mwaka 2018 kuliko mwaka 2017”, inaeleza sehemu ya taarifa ya Global Peace Index na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi hizo 71 baada ya kushika nafasi ya 51 kulinganisha na nafasi ya 54 iliyoshika mwaka 2017. 

  Akitoa maoni yake juu ya kupaa kimataifa katika suala la amani, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbasi, kupitia akaunti yake yaTweeter, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuienzi amani ya Tanzania. 

  Aidha, Msemaji Mkuu wa Serikali amewapongeza wananchi na wadau wote waliotimiza wajibu wao katika kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani duniani. 

  Taarifa hii ya 12 kutolewa na Global Peace Index ambayo huzipima nchi 163 kulingana na hali ya amani katika nchi hizo. Taasisi hii inaongoza na kuheshimika katika masuala ya kwa kupima hali ya amani katika nchi mbalimbali duniani.

  0 0

  Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga akizungumza katika mkutano mkuu wa TFA uliofanyika jijini Arusha

  Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tanganyika Peter Sirikwa akizungumza katika mkutano mkuu wa TFA

  Viongozi wa TFA wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga  Na Vero Ignatus,Arusha.

  Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga amefungua mkutano mkuu wa wanahisa wa Chama cha Wakulima la Tanganyika (TFA) kilichowakutanisha wadau wa kilimo na wanahisa kwa pamoja ili kujadili maendeleo ya kilimo

  Hasunga ameipongeza TFA kwa juhudi wanazozifanya katika kukuza sekta ya kilimo nchini ambayo ni kiinua mgongo na imeajiri watu wengi zaidi ya asilimia 80% ya Watanzania.

  Akizungumza katika mkutano huo ambao uliambatana na utoaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wakulima hao .Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na TFA katika kutatua changamoto za wakulima ili kuboresha sekta ya kilimo.

  Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima TFA Peter Sirikwa amesema kuwa TFA iko mstari wa mbele katika kuhamasisha maendeleo ya kilimo nchini na kuwanganisha wadau wa kilimo kwa pamoja .

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

  VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilayani Kibondo mkoani Kigoma wametakiwa kuacha kupokea rushwa kwa baadhi ya viongozi wanaotaka kwenda kugombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.

  Rai hiyo ilitolewa juzi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa Chama hicho kwa ngazi ya tawi, kata na jumuiya hasa namna gani ya kuongoza ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Louis Bura  aliwataka kuwaacha wananchi kuchagua kiongozi aliebora na si kumpendekeza kiongozi ambae amepita na kuwagawia rushwa katika kata zao.

  Alisema Katika kuelekea uchaguzi mwaka huu na mwaka 2020 ni lazima viongozi wa chama wanakuwa makini na viongozi wanaotaka Kugombea kwa kuwa watapita mitaani kuwashawishi kwa kuwa wao ndio wapiga kura wa kwanza , na kuwataka viongozi hao kuacha kuchochea kiongozi furani apitishwe kwakuwa katoa hela kiongozi mtoa rushwa hafai katika uchaguzi huu kwa kuwa anakuwa ana lengo lq kuja kujitengenezea masilah yake binafsi.

  "Tunafahamu wapo baadhi ya watu wanaotaka kugombea wanapita wanawashawishi muwachague niseme tu kwa yeyote tutakae mkamata hatutasita kumuadhibu na ikiwezekana tutashirikiana na viongozi wa chama kumfuta kabisa katika watu wanaogombea hatutaki viongozi wanaotoa rushwa kiongozi apite kwa kujiamini mwenyewe na kuaminiwa na Wananchi", alisema Bura.

  Akiwakaribisha watoa mada walioandaliwa Katibu Wa CCM Wilaya ya Kibondo Stanley Mkandawile aliwataka viongozi wa matawi na kata kuwa wakweli kutoa tathimini za kweli ni mgombea gani anakubalika na  Wananchi ilikuhakikisha  wanakipatia ushindi wa kutosha chama.

  Alisema viongozi wanaotoa fedha kuwashawishi wapiga kura kuwachagua hawafai na viongozi ambao hawakubaliki kwa Wananchi hawafai lazima viongozi wa chama wa kata na matawi, kupita kwa Wananchi kujua ni kata gani Chama kina mgombea ambae anakubalika na kata gani ambako kunachangamoto kiongozi aliepo hakubaliki.

  Aidha Mkandawile alisema lengo la chama ni kuhakikisha kata 19 na vijiji vyote vya kata hizo wanapata ushindi pamoja ilikufanikisha hilo ni lazima  viongozi kupata idadi ya Wanachama waliopo katika kata zao na kutatua kero zote ambazo zinaweza kusababusha Chama kukosa ushindi.

  Katibu Kata ya Misezero Benjamini  Mlinjie  alisema Semina ya kuwajengea uwezo imeweza kuwafungua  fikira za uongozi na mpaka sasa wamejipanga kushirikiana na TAKUKURU  kuwafichua wale wote wasiojiamini na wanataka kutoa rushwa iliwapitishwe.

  Alisema wapo baadhi wanatabia hizo na kwa sasa Watahakikisha viongozi wote wanaopita wanauwezo wa kuongoza na Wanapita kutokana na Wananchi wanavyo wakubali na sio kwasababu ya kutoa rushwa.

  Alisem wako tayari kumuunga Mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa kuhakikisha chama kinapata viongozi waadilifu na wanaokubalika na Wananchi kwa kuwa chama kinahazina ya kutosha.
  Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Louis Bura akizungumza na Viongozi wa CCM Wa Wilaya ya Kibondo
   Katibu Wa CCM Wilaya ya Kibondo Stanley Mkandawile akiwakaribisha watoa mada walioandaliwa huku akiwataka viongozi wa matawi na kata kuwa wakweli kutoa tathimini za kweli ni mgombea gani anakubalika na  Wananchi ili kuhakikisha  wanakipatia ushindi wa kutosha chama chao.
   Baadhi ya Viongozi wa CCM Wilaya ya Kibondo Wakiwa katika Semina ya kujengewa uwezo wa uongozi

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe. Gabriel Daqqaro akizungumza kwenye mahafali ya 35 katika chuo Kikuu Huria Jijini Arusha
  Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe. Gabriel Daqqaro akizungumza kwenye mahafali ya 35 katika chuo Kikuu Huria Jijini Arusha, kushoto kwake ni makamu mkuu wa chuo hicho kwa tawi la Arusha Marcel Masalu
  Naadhibya wahitimu wa Chuo Kikuu huria Kituo cha Arusha kama wakiwa kwenye magafali
  Bi Joyce Bendera akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Gabriel Daqqaro mara baada ya kuhitimu masomo yake kagika chuo kikuu huria kituo cha Arusha. 
   Ndugu Godfrey Mmassy Kipokea cheti mara baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu yake ya Master of monitoring and Evaluation (M&E) katika chuo kikuu huria kituo cha Arusha. 
  Mgeni rasmi katika mahafali hayo ya 35 ya Chuo kikuu huria Kituo cha Arusha, mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe. Gabriel Daqqaro, viongozi wa juu wa chuo kikuu huria, na viongozi wa serikali ya wanafunzi, pamoja na mwenyekiti wa chama ctawala mkoa wa Arusha Aloota Sanare. 

  Na. Vero Ignatus, Arusha. 

  Katika kufanikisha ujenzi wa Tanzania ya viwanda wasomi wametakiwa kutumia elimu yao kuweza vizuri kwa kuweza kujiajiri na kutoa fursa kwa watu wengine kuliko kutegemea kuajiliwa hali inayosababisha kuendelea kuzorota kwa uchumi wa nchi 

  Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro kwenye mahafali ya Chuo Kikuu Huria Tanzania tawi la arusha ambapo amewasisitiza wahitimu hao kuweza kuenda kulitumikia taifa lao kwa weredi utakao lisogeza taifa katika uchumi wa kati

  Pamoja na hayo makamu mkuu wa chuo hicho kwa tawi la Arusha Marcel Masalu amesema wanafunzi waliohitimu masomo yao mwaka 2017/18 ni 145 kwa Arusha peke yake. 

   Masalu amesema Chuo hicho ndicho pekee cha Elimu ya juu Tanzania kinachotoa kozi kwa njia ya Cheti, Estashahada, Stashahada, Shahada za uzamili (Masters) na Uzamili PHD kwa njia ya masafa. 

  Aidha mewataka wahitimu hao kuweza kukitangaza chuo hicho huko wanapokwenda kwa kufanya kazi zao kwa ufasaha 

  Kwa upande wawanafunzi hao waliohitimu wameeleza changamoto wanazozipata ikiwa nipamoja na upungufu wa madarasa pamoja na majengo ya walimu hali inayosababisha mrundikano wawanafunzi wengi.

  Nae Ndugu Godfrey Mmassy aliyehitimu  elimu yake ya Master of monitoring and Evaluation (M&E) amesema mtu yeyote akiamua kusoma akiwa kazini inawezekana kabisa ni maamuzi ya mtu binafsi. 

  0 0
older | 1 | .... | 1828 | 1829 | (Page 1830) | 1831 | 1832 | .... | 1903 | newer