Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS AZINDUA AKAUNTI YA TABASAMU

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imefanya jitihada kubwa kuweka mazingira mazuri ya kisera na kimifumo ili kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha hapa nchini.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Akaunti ya TABASASMU, iliyozinduliwa leo na Benki ya Posta jijini Dar es Salaam.

“Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kutoa miongozo mbalimbali ili kuhakikisha watanzania takribani asilimia 50 wanafikiwa na huduma za kibenki ifikapo Mwaka 2025”alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amependezwa na wazo la kuhakikisha kuwa kupitia akaunti ya TABASAMU wanawake watauziwa bima za kijamii.

Benki ya Posta ina matawi takriban 80, ATM 54, mtandao wa Umoja Switch takriban 200 na mawakala 150 kupitia Shirika la Posta ambapo Makamu wa Rais ameitaka benki hiyo kuwafikia wanawake wengi haswa vijijini na kuhakikisha wanapata huduma na elimu ya masuala ya kifedha.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa wanawake ni nguzo kuu ya uchumi wetu, kwani wao ndiyo wazalishaji wakuu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa. Mbali ya kulea familia, huwezi kuwakosa wanawake kwenye sekta yoyote ya uzalishaji mali, na hivyo siyo upendeleo kuanzisha akaunti maalumu ya TABASAMkwa wanawake, bali ni haki yao ya msingi kama ilivyofanya benki ya TPB.

Makamu wa Rais amewataka Akaunti ya TABASAM inashirikiana na makampuni ya simu kuhakikisha kuwa wanawake hawa si tu wanapata taarifa za kibenki hata ikiwezekana kuweza kupata huduma za kibenki kama mikopo kupitia simu zao za mikononi. 


Wakati huo huo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema Tanzania ina rekodi nzuri Afrika na duniani kwa ujumla katika masuala ya huduma za kifedha 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi  Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Dkt. Edmund Mndolwa (kulia) wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Picha ya pamoja

MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ABAINI WIZI VYAMA VYA USHIRIKA

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh.Sophia Kizigo akifafanua jambo kwenye moja ya majukumu yake ya kazi.


*Ni baada ya baadhi ya viongozi kuiba Sh.milioni 33 ya tani 10 za korosho

*Aishauri Serikali kupitia upya Sheria ya Vyama vya ushirika kwani ...


Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo ametoa ombi kwa Serikali kuangalia upya Sheria ya Vyama vya Msingi,kwani amebaini zinatoa mwanya kwa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo ambao si waaminifu kuwaibia wakulima.

Kizigo ameeleza hayo baada ya kubaini wilayani Namtumbo kuna wizi ambao umefanyika kwenye moja ya vyama vya msingi na kusababisha wakulima kutoa malalamiko yao kwake na hivyo amechukua hatua kadhaa.

Baadhi ya hatua ambazo amechukua ni kufanya uchunguzi uliosaidia kuwapata viongozi wa vyama vya ushirika waliohusika na wizi huo kwa kuwaibia wakulima na kisha kuwaweka ndani.

Akizungumza na Michuzi Blog leo, Machi 28,2019,Mkuu wa Wilaya Kizigo amesema ofisi yake iliamua kufutilia na kubaini wizi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya wakulima wa zao la korosho waliokuwa wakilalamika kutolipwa fedha zao wakati yeye anajua wengi wameshalipwa.

"Baada ya kufuatilia tukabaini wapo ambao waliingiziwa fedha kwenye  akaunti zao kumbe zilishakuwa mfu, pia wengine majina yao ya akaunti zao yalikuwa yanafanana na hivyo fedha kushindwa kuingia.Hata hivyo nimeshatoa maelekezo wale ambao wanasema hawajalipwa waandike majina yao ili nifuatile kwa kuyapeleka makao makuu ili tujue nani amelipwa na nani hajalipwa.

"Sababu ya tatu ni wizi ambao wameuasisi viongozi wa vyama vya ushirika wenyewe na kisha kuibia wakulima.Ukweli viongozi wa vyama vya ushiriki mmeiba sana na njia ambazo mnatumia kuiba ni nyingi sana.Kuna wizi wa kukata kilo , mkulima anakuja na kilo 10 na ninyi mnasema kilo tisa au nane,"amesema Kizigo.

Amefafanua wamechunguza na taarifa zote za wizi ulivyokuwa unafanyika na waliohusika wote wanawajua. "Tumebaini wapo wakulima ambao hajalipwa kabisa na fedha zao zimeliwa na viongozi ambao wamewateua wao na kuwaamini lakini ndio hao hao wanawaibia wakulima.Baadhi yao baada ya kuwabana wamekiri kuiba na tuliwaweka ndani."

Ameongeza korosho inayopatikana wilayani Namtumbo ndio bora na inashika nafasi ya kwanza kwa ubora duniani na kwamba kilo moja ya korosho ilitakiwa kulipwa Sh.3500.

"Tulipoongea na viongozi wao wa chama hicho cha msingi wamekiri kuibia wakulima ambapo Sh.milioni 33 zimeliwa na viongozi hao.Tulipombana mhasibu akasema bodi yote imeshiriki ingawa wengine walikataa.Tulipoona wanasumbua nikatoa agizo wakamatwe wote na kuwekwa ndani.

"Wakakaa kama siku tano au sita hivi , nikawaambia wakitaka kuachiwa walipe fedha ambayo wanadaiwa ambapo walilipa na kubaki kama Sh.milioni tisa.Cha kushangaza wakulima ambao walikuwa wanalalamika ndio hao hao wakawa wanaomba wawawekee dhamana, waliamua kuitisha na kikao na kisha wakachangishana fedha ili kuwatoa viongozi hao wakidai ni watoto wao,"amesema Kizigo.

Kutokana na hali hiyo amesema ili kukomesha tabia hiyo umefika wakati kwa Serikali kuangalia upya Sheria ya Vyama vya ushirika kwani inatoa mwanya kwa viongozi kuwaibia wakulima kwani sheria hiyo inaeleza wazi viongozi wa vyama vya ushirika wasiingiliwe na mtu yoyote yule wanapofanya maamuzi yao na inapotokea wizi wa fedha basi aliyehusika atatakiwa kulipa fedha tu.

"Sheria iliyopo haituruhusu kuingilia vyama vya ushirika.Hivi bila kuingilia wizi ambao umefanyika hapa Namtumbo hawa wakulima wangepata fedha zao kweli.Nitoe mwito kwa Serikali kuangalia upya sheria hii ili kukomesha tabia ya wizi inayofanywa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu,"amesema Kizigo.

Article 2

0
0
Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa vinavyosimamiwa na TGNP Mtandao kutoka Mikoa ya Morogoro,Mbeya,Mara,Shinyanga na Kigoma wametembelea Shirika la Agape AIDS Control Programme na vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga. 

Lengo la ziara hiyo ya siku mbili iliyoanza Machi 27 na kumalizika Machi 28,2019 ni kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Vituo vya Taarifa na Maarifa wilayani Kishapu na Washirika wake likiwemo Shirika la Agape. 

Mwezeshaji wa ziara hiyo,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao alisema katika siku ya kwanza ya ziara,walitembelea kituo cha Taarifa na Maarifa cha kata ya Ukenyenge,kukagua vyumba vya usiri kwa wanafunzi wa kike na vyoo katika shule za msingi Kanawa na Bulimba,zahanati ya Negezi na Gender Club katika shule ya sekondari Ukenyenge. 

“Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa hiyo mitano walijifunza namna vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya ya Kishapu jinsi vinavyoshirikiana na jamii na viongozi wa serikali kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii”,alieleza Amani ambaye pia ni Meneja Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi unaotekelezwa na Agape wilayani Kishapu. 

“Washiriki wa ziara hii pia wametembelea shirika la Agape lenye makao yake Makuu katika Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga linalojihusisha na masuala ya ulinzi wa mtoto,utoaji msaada wa kisheria,kutokomeza mimba na ndoa za utotoni,ukatili wa kijinsia,malezi na makuzi bora ya mtoto”,aliongeza Amani. 

Aidha alisema wakiwa katika shirika la Agape,Washiriki wa ziara hiyo pia waliwatembelea wanafunzi wahanga wa mimba na ndoa za utotoni wanaosoma katika shule ya Agape Knowledge Open School inayomilikiwa na Agape iliyopo katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga. 

Miongoni wa madiwani hao akiwemo Pessa Pessa kutoka kata ya Bwakira Chini halmashauri ya wilaya ya Morogoro waliishukuru TGNP Mtandao kwa kuwazesha kufika mkoani Shinyanga kujionea mambo mazuri yanayofanywa na Vituo vya Taarifa na Maarifa na shirika la Agape katika kupiga vita matukio ya ukatili wa kijinsia. 

“Kwa kweli bila TGNP Mtandao tusingeweza kuyafahamu mambo mema yanayofanywa na wenzetu katika kuhakikisha watoto wanalindwa lakini pia kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia”,aliongeza Festo Mwalyego ambaye ni diwani wa kata ya Tembela halmashauri ya wilaya ya Mbeya. 

Naye Stimar Heda John (kata ya Ijombe halmashauri ya wilaya ya Mbeya),aliwaomba viongozi wa serikali kutembelea shirika la Agape kwani linafanya kazi kubwa kuwasaidia watoto wanaokumbana na vitendo vya ukatili hivyo serikali ione namna ya kuwaongezea nguvu ili kusaidia Watanzania wengi zaidi. 
Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa vinavyosimamiwa na TGNP Mtandao kutoka Mikoa ya Morogoro,Mbeya,Mara,Shinyanga (Kishapu) na Kigoma wakiwasili katika Ofisi za Shirika la Agape AIDS Control Programme katika kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga leo Machi 28,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Agape,Lucy Maganga akiwakaribisha Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Morogoro,Mbeya,Mara,Shinyanga (Kishapu) na Kigoma. 
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Agape,Lucy Maganga akikaribisha madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa.
Mwezeshaji wa ziara ya Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa ,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao akielezea historia ya Shirika la Agape.
Diwani wa Viti Maalum kata ya Ukenyenge wilaya ya Kishapu,Josephina Malima akizungumza wakati wa ziara hiyo na kueleza namna wanavyoshirikiana na vituo vya taarifa na maarifa,serikali na wadau mbalimbali likiwemo shirika la Agape na TGNP Mtandao katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Diwani wa kata ya Tembela halmashauri ya wilaya ya Mbeya,Festo Mwalyego akielezea jinsi Imani za kishirikina zinavyochangia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake katika jamii na kuitaka jamii kuepukana na imani hizo. 
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Fredina Said akielezea shughuli wanazofanya wilayani Kishapu kupiga vita ukatili wa kijinsia. 
Diwani wa Kata ya Ijombe halmashauri ya wilaya ya Mbeya,Stimar Heda John akipongeza kazi zinazofanywa na shirika la Agape katika kulinda haki za watoto.
Meneja Fedha wa Shirika la Agape Nkwimba Ng'homano Lugisi (wa pili kushoto) akieleza namna wanavyowahifadhi kwa muda mabinti waliofanyiwa vitendo vya ukatili katika chumba maalum kilichopo katika ofisi za shirika la Agape.
Nje ya chumba cha kuhifadhi mabinti waliofanyiwa vitendo vya ukatili . Kushoto ni Mwezeshaji wa ziara ya Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa ,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao akielezea jambo kwa Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa.
Hapa ni katika shule ya Agape Knowledge Open School ambapo mabinti wahanga wa mimba na ndoa za utotoni wanapewa elimu ya kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.Kulia ni Peter Amani akitambulisha Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Mbeya,Morogoro,Kigoma,Mara na Shinyanga waliotembelea shule hiyo.
Peter Amani akielezea namna mabinti wanavyosoma katika shule hiyo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo,Kalunga Zacharia akielezea changamoto zilizopo katika shule hiyo kuwa ni uhaba wa madarasa,mabweni,vitabu na madawati.
Diwani wa kata ya Bwakira Chini halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Pessa Pessa akilishukuru na kulipongeza shirika la Agape kuwapatia elimu watoto hao ambao ni wahanga wa mimba na ndoa za utotoni na kuahidi kushirikiana nao katika kuendelea kuwapatia msaada zaidi ili waweze kutimiza ndoto zao.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Songwa wilayani Kishapu Rahel Madundo akiwasisitiza watoto hao kusoma kwa bidii.
Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Mbeya,Morogoro,Kigoma,Mara na Shinyanga,viongozi wa shirika la Agape wakiwa katika picha ya pamoja.Picha zote na Kadama Malundev- Malunde1 blog

MNEC WA IRINGA SALIM ASAS ACHANGIA UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYERERE

0
0

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

 MJUMBE wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas amechangia kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyerere iliyopo katika kata ya Migoli mkoani Iringa

Akimwakilisaha MNEC Salim Asas wakati wa mahali ya kidato cha sita katika shule hiyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa nyumba za walimu na tayari ameona jitihada zinazoendelea hivyo kiasi cha shilingi milioni mbili alipewa na MNEC basi zitasaidia katika ujenzi huo.

“Nimepewa pesa hizi na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas nije niwaletee kwa niaba yake hivyo nimezifikisha salama na nyie mzitumieni katika kumalizia ujenzi wa nyumba hizo za walimu ili walimu waishi vizuri” alisema Baraza

Baraza alisema, mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas anayependa kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali ndio maana katika shule hiyo amechangia zaidi ya mara moja kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu katika shule hiyo.

“Mmesema hapa wenyewe kuwa mara kadha amekuwa akiwasaidia kuchangia maendeleo katika shule hii na leo kanituma niwaletee hizi pesa kwa ajili ya mchango wake kwenye shule hii kwa lengo la kuboresha taaluma kwa wanafunzi wa hapa” alisema Baraza

Aidha Baraza aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wasoma sana na kufaulu mitihani iliyopo mbele yao na kurudisha fadhila kwa walimu na wazazi wao waliowalea na kuwafundisha hadi hapo walipofika.

“Hakuna kitu kizuri kwa mwanafunzi kufaulu mtihani na kusonga mbele hiyo maana walimu wanawafundisha mkiwa shuleni lakini mkiwa nyumani wazazi wenu wanatumia gharama kubwa kuwa somesha huku wakitegemea kupata matokeo chanya ya mtihani wenu wa mwisho” alisema Baraza 

Baraza aliongeza kwa kuwataka wanafunzi wa kidato cha sita kusimamia kikamilifu malengo waliyojiwekea ili kuifikia ndoto ambayo wamekuwa nayo kwa miaka mingi ya kupata au kufika maisha bora ambayo kila mwanadamu anatamani kuyafikia.

Lakini Baraza aliwapongeza walimu na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kwa kupata matokeo mazuri kila mwaka na kusaidia kukuza taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo na kuwaandaa vijana ambao watakuaja kulisaidia taifa hapo baadae.

Awali akisoma taarifa ya shule hiyo mkuu wa shule Laurent Manga alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya umaliziaji wa nyumba ya walimu inayojengwa kwa nguvu za wazazi,wanafunzi na serikali.

“Mgeni rasmi sis hapa tunaupungufu wa bati mia moja na ishirini,saruji mifuko mia tatu,mbao mia moja themenini na tisa pamoja na misumari kilo hamsini,hivyo ndio vinakwamisha umaliaji wa nyumba hiyo ya walimu” alisema Manga

Manga alisema, uongozi wa shule uliweka malengo yake ya kuborsha makazi ya walimu kwa kuanza kujenga nyumba tano ambazo mpaka sasa nyumba tatu zenye uwezo wa kuhifadhi walimu sita zimekamilika na nyingine moja mafundi wapo kazini na ya mwisho ikiwa hatua ya renta.

Hata hivyo Manga alimalizia kwa kutoa shukrani kwa mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas kwa mchango wake wa kimaendeleo ambao amekuwa akiufanya katika shule hiyo na mahali pengine.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akiongea na wanafunzi na wazazi wa shule ya sekondari ya Nyerere wakati wa mahafali ya kidato cha sita akimwakirisha mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi 
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akimkabidhi mkuu wa shule ya sekondari ya Nyerere fedha alipewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas kwa ajili ya kuasidia ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule hiyo
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi,wazazi mbalimbali pamoja wanafunzi wa kidato cha sita

MNEC SALIM ASAS ACHANGIA UJENZI NYUMBA ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYERERE

0
0

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akiongea na wanafunzi na wazazi wa shule ya sekondari ya Nyerere wakati wa maafari ya kidato cha sita akimwakirisha mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akimkabidhi mkuu wa shule ya sekondari ya Nyerere fedha alizopewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas kwa ajili ya kuasidia ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule hiyo
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi,wazazi mbalimbali pamoja wanafunzi wa kidato cha sita




NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas amechangia kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyerere iliyopo katika kata ya migoli mkoani Iringa

Akimwakilisaha MNEC Salim Asas wakati wa mahali ya kidato cha sita katika shule hiyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa nyumba za walimu na tayari ameona jitihada zinazoendelea hivyo kiasi cha shilingi milioni mbili alipewa na MNEC basi zitasaidia katika ujenzi huo.

“Nimepewa pesa hizi na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas nije niwaletee kwa niaba yake hivyo nimezifikisha salama na nyie mzitumieni katika kumalizia ujenzi wa nyumba hizo za walimu ili walimu waishi vizuri” alisema Baraza

Baraza alisema, mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas anayependa kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali ndio maana katika shule hiyo amechangia zaidi ya mara moja kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu katika shule hiyo.

“Mmesema hapa wenyewe kuwa mara kadha amekuwa akiwasaidia kuchangia maendeleo katika shule hii na leo kanituma niwaletee hizi pesa kwa ajili ya mchango wake kwenye shule hii kwa lengo la kuboresha taaluma kwa wanafunzi wa hapa” alisema Baraza

Aidha Baraza aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wasoma sana na kufaulu mitihani iliyopo mbele yao na kurudisha fadhila kwa walimu na wazazi wao waliowalea na kuwafundisha hadi hapo walipofika.

“Hakuna kitu kizuri kwa mwanafunzi kufaulu mtihani na kusonga mbele hiyo maana walimu wanawafundisha mkiwa shuleni lakini mkiwa nyumani wazazi wenu wanatumia gharama kubwa kuwa somesha huku wakitegemea kupata matokeo chanya ya mtihani wenu wa mwisho” alisema Baraza

Baraza aliongeza kwa kuwataka wanafunzi wa kidato cha sita kusimamia kikamilifu malengo waliyojiwekea ili kuifikia ndoto ambayo wamekuwa nayo kwa miaka mingi ya kupata au kufika maisha bora ambayo kila mwanadamu anatamani kuyafikia.

Lakini Baraza aliwapongeza walimu na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kwa kupata matokeo mazuri kila mwaka na kusaidia kukuza taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo na kuwaandaa vijana ambao watakuaja kulisaidia taifa hapo baadae.

Awali akisoma taarifa ya shule hiyo mkuu wa shule Laurent Manga alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya umaliziaji wa nyumba ya walimu inayojengwa kwa nguvu za wazazi,wanafunzi na serikali.

“Mgeni rasmi sis hapa tunaupungufu wa bati mia moja na ishirini,saruji mifuko mia tatu,mbao mia moja themenini na tisa pamoja na misumari kilo hamsini,hivyo ndio vinakwamisha umaliaji wa nyumba hiyo ya walimu” alisema Manga

Manga alisema, uongozi wa shule uliweka malengo yake ya kuborsha makazi ya walimu kwa kuanza kujenga nyumba tano ambazo mpaka sasa nyumba tatu zenye uwezo wa kuhifadhi walimu sita zimekamilika na nyingine moja mafundi wapo kazini na ya mwisho ikiwa hatua ya renta.

Hata hivyo Manga alimalizia kwa kutoa shukrani kwa mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas kwa mchango wake wa kimaendeleo ambao amekuwa akiufanya katika shule hiyo na mahali pengine.

WCF YASISITIZA UADILIFU KATIKA KUWASILISHA TAARIFA ZA WAFANYAKAZI

0
0
NA K-VIS BLOG, ARUSHA

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umewasisitizia waajiri kuwa waadilifu wanapowasilisha taarifa zinazohusu idadi ya wafanyakazi wao na viwango vya mishahara wanavyowalipa.

Rai hiyo imetolewa leo Machi 28, 2019 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo Dkt. Abdulsalaam Omary wakati wa semina ya mafunzo kwa mameneja waajiri kuhusu wajibu wa mwajiri katika kutekeleza sheria ya usalama na afya mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na kue.limisha kuhusu kazi na shughuli za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Arusha.

“Niwaombe waajiri, mnapotuletea taarifa jaribuni kutuletea taarifa sahihi kuhusu idadi ya wafanyakazi mlio nao na viwango vya mishahara mnavyowalipa, kwani baadhi yenu huleta idadi pungufu ya wafanyakazi na wengine hamuwaorodheshi.” Alisema.

Kwa bahati mbaya wale ambao hamuwaorodheshi ndio wanaopatwa na matatizo ya ajali au maradhi yatokanayo na kazi na linapokuja swala la kudai fidia taarifa zao zinakuwa hazipo nahii sio sawa.” Alisema Dkt. Omary.Alisema kuna waajiri ambao hawatoi mikataba kwa wafanyakazi kwa lengo la kukwepa wajibu.

“Kwa sheria ya WCF mfanyakazi asiye na mkataba na amehudumu katika kazi hiyo kwa siku 30 mfululizo, huyo anatambuliwa na Mfuko kama mfanyakazi anayetakiwa kusajiliwa na kulipiwa mchango wa kila mwezi.” Alifafanua.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary,(kulia), akizungumza wakati wa semina ya kuwaelimisha mameneja waajiri kuhusu umuhimu wa kuzingatia sharia juu ya usalama na afya mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya vihatarishi vya ajali mara kwa mara ili kupunguza madhara yatokanayo na ajali kazini. Semina hiyo imefanyika leo Machi 28, 2019 jijini Arusha. Kushoto ni Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Naanjela Msangi
Sehemu ya waajiri walioshiriki semina hiyo.
Sehemu ya waajiri walioshiriki semina hiyo.
Sehemu ya waajiri walioshiriki semina hiyo.
Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Naanjela Msangi, akitoa mada kuhusu umuhimu wa kufanya tathmini ya mara kwa mara mahala pa kazi.
Afisa wa WCF, Bw. Edward Kirenga, Bw. Edward Kirenga, akitoa mada mbele ya washiriki.
Mwakilishi wa ofisi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), jijini Arusha Bi. Zaria Mmanga (kulia), akizungumza mbele yawaajiri wakati wa semina ya mafunzo kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na shughuli za Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi WCF jijini Arusha Machi 28, 2019.
Mwakilishi wa ofisi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), jijini Arusha Bi. Zaria Mmanga (kulia), akitambulishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge kwa waajiri wakati wa semina ya mafunzo iliyoandaliwa na WCF kuwaelimisha kuhusu wajibu wa waajiri na wafanyakazi katika kuhakikisha masuala ya usalama na afya mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na shughuli za Mfuko wa Fidia zinafahamika vema
Picha ya pamoja ya washiriki.
Picha ya pamoja ya washiriki.

SAFARI YA MWISHO YA MWANDISHI WA DW CHARLES OLE NGEREZA JIJINI ARUSHA

0
0


Na Vero Ignatus, Arusha
Kwaheri Charles Ngereza  Kiongozi wetu haya ni maneno ya Wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Arusha waliyasema wakati wa kuuaga mwili wa mpendwa wao kwa mara ya mwisho

Marehemu Charles Ngereza hadi anafariki  alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa  Arusha ambapo aliwahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali ikiwemo Radio five ya Jijini Arusha,Itv &Radio one hadi mauti inamkuta alikuwa muwakilishi wa Idhaa ya kiswahili ya DW Born Ujerumani

Ameshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2005 hadi umauti ulipomkuta, Katika uhai wake Charles Ngereza amekuwa  akifanya kazi kwa uadilifu na siku zote amekuwa mtu wa kushauri zaidi badala ya kuhoji, alisema Cloud Gwandu mwenyekiti wa APC.

Akiwa mmoja wa wanaounda kamati ya utendaji  ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha Ngereza amekuwa kiunganishi kikubwa kati ya waandishi wa habari wa ndani na nje na kwa hapa tutamkumbuka zaidi katika kutoa ushauri na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
Siku zote ngereza amekuwa akiamini katika diplomasia, hata pale mambo yanapokwama amekuwa msaada mkubwa kuhakikisha suluhisho inapatikana na katika kamati zetu pale ndani ya APC amekuwa akishirikishwa kwenye kamati  mbalimbali ikiwemo ile kamati ya  nidhamu na maadili pale mambo yanapoonekana hayaendi sawa.

Sisi kama wanahabari wa Mkoa wa Arusha tunasema tumempoteza mtu muhimu sana katika tasnia ya habari na kwa msemo wa sasa hivi tunaweza kusema tumepoteza ‘jembe’ na hakika pengo lake halitazibika japo mambo ya Mungu ni mengi tutaendelea kumuomba yeye ili aweze kupatikana mfano wa Ngereza.Alisema muweka hazina wa APC Pamela Mollel. 

Ngereza alikuwa ni zaidi ya rafiki kwa kuwa alikuwa akishiriki hata kwa mambo ya kijamii ndani ya APC tumekuwa na miradi ya kijamii ikiwemo kupanda miti katika shule za kata, Ngereza amekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi hizi ili kuona jamii na yenyewe inafaidika na uwepo wa Chama wa waandishi wa habari mkoa wa Arusha.

Wapendwa kwa ufupi nipende tu kusema yapo mambo mengi sana ambayo Ndugu yetu, kaka yetu Charles Ngereza ameyafanya lakini wacha tuishie hapa kwa ufupi sababu hata kama tukisema tuendelee kuyasema hapa hatutaweza kuyamaliza,kikubwa sisi kama wanahabari Mkoa wa Arusha, wafanyakazi wenzake tunaahidi tutaendelea kuyaenzi yale yote aliyoyaacha ili kuendeleza umoja na ushirikiano aliokuwa akiusisitiza.

Tunaamini Charles amefariki mwili lakini roho yake bado ipo mioyoni mwetu, kwa kuwa hata wakati anaugua anapambania afya yake kila siku tulimsihi na kumpatia faraja na hakika aliamini katika Mungu.

Tuliamini alipokwenda India kupata matibabu atarejea akiwa mzima na  kuendelea katika mapambano yetu ya kila siku lakini alirejea akiwa ameendelea kudhoofu,alisema Mustafa Leu Katibu wa Apc

Akiongoza ibada ya mazishi mchungaji kutoka kanisa la Anglikana ametoa angalizo kwa ndugu jamaa na marafiki kuwa makini katika kipindi hicho cha majonzi na kuwataka wasijesababisha msiba mwingine baada ya huo kwa maneno yasiyo ya hekima watakayoyatoa kwa mjane na watoto walioachwa
0688
Mara nyingi msiba unapotokea ndipo watu wengi hijitokeza haswa ndugu na kuanza kuzungumza hovyo bila hekima kaa kimya ,wacheni kuzungumza hovyo, wapendwa msimpe shetani nafasi kwenye misiba ya watu

Akitoa salamu za rambirambi mkuu wa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Lengai Ole Sabaya amesema kuwa marehemu alilikuwa mpatanishi alikuwa hapendi kuona ugomvi unatokea 

Kama wanahabari ndugu jamaa na marafiki zake niwape pole  tamaa tuliamini kila jambo linaletwa kwa mapenzi ya Mungu, tulikaa na kushauriana namna nyingine ambapo mwenzetu ataweza kupata tiba lakini wakati tukiwa kwenye mikakati hiyo Charles alizidiwa na kukimbizwa hospitali na baadae alifariki dunia.

 Inatia uchungu sana lakini hamna namna, tunasema yote ni Mapenzi ya Mungu. Nenda Charles tuko nyuma yako,
 Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoani Arusha Cloud Gwandu akitoa heshima za mwisho kwa aliyekumwa makamu mwenuekiti wa) APC)
 Muweka hazina wa Klabu ya  waandishi wa habari Mkoani Arusha Pamela Mollel akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya mwenyekiti wa (APC)
 Mratibu wa APC Arusha Seif Mangwangwi akilia kwa huzuni mara baada ya mwili wa Charles Ngereza ulipowasili waliopo pembeni yake ni Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa msibani 
 Baadhi ya Viongozi wa kanisa la Sent-James Anglican PASTOR, MICHAEL GILAISI  QAWOGA  UIJILISTI NA UMISSION.wakiongoza ibada nyumbani ya maziko ya aliyekuwa mwandishi wa Habari wa Idhaa ya Kiswahili DW 
Watoto wa marehemu Charles Ngereza, Faith na Fransis wakiwa kanisani
 Mary Mwita Mke wa marehemu Charles Ngereza akiwa kanisani ibada ikiwa inaendelea.
 Mke wa Marehemu Charles Ngereza Mary Mwita akiwa ibadani katika kanisa la Anglikana Sent. James Arusha
Mjane Mary Mwita akielekea Jeneza kuuaga mwili wa mume wake kwa mara ya mwisho
 Waandishi wa habari wakiwa msibani katika viwanja vya shule ya sekondari Baraa Jijini Arusha.
Baadhi ya waandishi wa habari Jijini Arusha wakielea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa katika kata ya baraa ambapo shughuli ya  za Ibada na taratibu zingine zinafanyika. 


MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAWATAKA WAAJIRI KUWA WAADILIFU

0
0
Na Vero Ignatus, Arusha

MFUKO wa Fidia kwaWafanyakazi (WCF), umewataka  waajiri kuwa waadilifu juu ya uwasilishaji wa  taarifa zinazohusu idadi ya wafanyakazi wao na viwango vya mishahara wanavyowalipa.

Kauli hiyo imetolewa  na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo Dkt. Abdulsalaam Omary wakati wa semina ya mafunzo kwa mameneja waajiri kuhusu wajibu wa mwajiri katika kutekeleza sheria ya usalama na afya mahala pa kazi .

Amewataka waajiri kupeleka idadi sahihi ya wafanyakazi sambamba na  kuelimisha kuhusu kazi na shughuli za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Arusha.

“Niwaombe waajiri, mnapotuletea taarifa jaribuni kutuletea taarifa sahihi kuhusu idadi ya wafanyakazi mlio nao na viwango vya mishahara mnavyowalipa, kwani baadhi yenu huleta idadi pungufu ya wafanyakazi na wengine hamuwaorodheshi.” Alisema.

Kwa bahati mbaya wale ambao hamuwaorodheshi ndio wanaopatwa na matatizo ya ajali au maradhi yatokanayo na kazi na linapokuja swala la kudai fidia taarifa zao zinakuwa hazipo nahii sio sawa.” Alisema Dkt. Omary.

Alisema kuna waajiri ambao hawatoi mikataba kwa wafanyakazi kwa lengo la kukwepa wajibu.“Kwa sheria ya WCF mfanyakazi asiye na mkataba na amehudumu katika kazi hiyo kwa siku 30 mfululizo, huyo anatambuliwa na Mfuko kama mfanyakazi anayetakiwa kusajiliwa na kulipiwa mchango wa kila mwezi.” Alifafanua.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary,(kulia), akizungumza wakati wa semina ya kuwaelimisha mameneja waajiri kuhusu umuhimu wa kuzingatia sharia juu ya usalama na afya mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya vihatarishi vya ajali mara kwa mara ili kupunguza madhara yatokanayo na ajali kazini. Semina hiyo imefanyika leo Machi 28, 2019 jijini Arusha. Kushoto ni Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Naanjela Msangi
  Sehemu ya waajiri walioshiriki semina hiyo.
  Sehemu ya waajiri walioshiriki semina hiyo.
 Sehemu ya waajiri walioshiriki semina hiyo.
 Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Naanjela Msangi, akitoa mada kuhusu umuhimu wa kufanya tathmini ya mara kwa mara mahala pa kazi.
 Afisa wa WCF, Bw. Edward Kirenga, Bw. Edward Kirenga, akitoa mada mbele ya washiriki.
 
 Mwakilishi wa ofisi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), jijini Arusha Bi. Zaria Mmanga (kulia), akizungumza mbele yawaajiri wakati wa semina ya mafunzo kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na shughuli za Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi WCF jijini Arusha Machi 28, 2019.
 Mwakilishi wa ofisi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), jijini Arusha Bi. Zaria Mmanga (kulia), akitambulishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge kwa waajiri wakati wa semina ya mafunzo iliyoandaliwa na WCF kuwaelimisha kuhusu wajibu wa waajiri na wafanyakazi katika kuhakikisha masuala ya usalama na afya mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na shughuli za Mfuko wa Fidia zinafahamika vema
 Picha ya pamoja ya washiriki.
Picha ya pamoja ya washiriki.

MAGAZETI YA LEO IJUMAAA MACHI 29,2019

0
0



















ASASI ZA KIRAIA ZASHINDA KESI YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016 DHIDI YA JAMUHURI

0
0
Na. Vero Ignatus,Arusha
Shauri Namba 2 la mwaka 2017 kati ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kituo cha Sheria na Haki na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania jana limeamuliwa na mahakama ya Afrika Mashariki ambapo waleta maombi wameishinda Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imesema baadhi ya vipengele katika Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 inakiuka uhuru wa kujieleza pia vinapingana na Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao Tanzania imeuridhia.

Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imetoa hukumu jana dhidi ya sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Novemba 2, 2016 na kusainiwa na Rais. 

Kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2017 ilifunguliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wakilalamikia ukandamizaji wa uhuru wa habari.

Hivyo upande wa waleta maombi waliomba mahakama itamke kuwa; 1. Vifungu vya 7 (3) (a) (b) (c) (f) (g) (h) (i) na (j),  13, 14, 18, 19, 20, 21, 35, 36, 37, 38, 39, 40, 50, 54, 52, 53, 58, na 59 vya Sheria ya Huduma za Habari, 2016 vifutwe kwa kuwa vinaminya uhuru wa habari

Vipengele vilivyolalamikiwa vipo 18, walalamikaji wakiiomba mahakama hiyo itamke kwamba vipengele hivyo vinakiuka mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuilazimisha serikali kuvifuta kabisa.

Hukumu hiyo imesomwa jana Alhamisi Machi 28, mbele ya Jopo la majaji watatu Jaji Charles Nyachae, Monica Mugenyi na Jaji Justice Ngie.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Nyachae amesema vifungu vilivyo kwenye sheria hiyo ni vibovu na vinavyokiuka mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo ameitaka Serikali ya Tanzania kurekebisha vifungu vya Sheria ya Uhuru wa Habari kutokana na kukiuka Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Sheria hii inapaswa kufanyiwa marekebisho ili iendane na mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya," amesema Jaji Nyachae.

Wadai halo walikua wakitetewa na mawakili, Fulgence Massawe, Jebra Kambole, Mpale Mpoki , Donald Deya na Jenerali Ulimwengu.

Mahakama ya EACJ imekubaliana na walalamikaji kuwa vifungu katika sheria ya Huduma ya Habari vya (3)(a), 13, 1920, 21,34 pamoja na vifungu vingine vinakiuka utawala bora, demokrasia na utawala unaozingatia sheria na inapingana na mkataba ulioanzisha EAC.

Mara baada ya hukumu hiyo, Wakili kiongozi wa walalamikaji, Fulgence Massawe amesema ushindi huo ni wa kihistoria na unathibitisha hoja za wadau mbalimbali walizokua wakisema sheria hiyo siyo nzuri kwa maslahi mapana ya nchi.

BENKI YA NMB YADHAMINI JUKWAA LA BIASHARA MKOANI LINDI,YAAHIDI KUWAPA HUDUMA BORA WAKAZI WAKE

0
0
BENKI ya NMB imewahakikishia wajasiriamali, wafanyabiashara na wakulima mkoani Lindi kuwa itaendelea kuwahudumia kupitia huduma zake za kutunza fedha lakini pia kwa utoaji wa mikopo.

Hayo yalibainishwa na Meneja wa Kanda ya Kusini wa benki hiyo – Janeth Shango, wakati akizungumza kwenye jukwaa la fursa za biashara na uwekezaji lilofanyika mkoani humo. Kama wadau wa sekta ya biashara nchini, Benki ya NMB imedhamini wa jukwaa la Biashara linalofanyika mkoani Lindi.

Jukwaa hilo lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, liliwakutanisha washiriki takribani 350 wakiwemo wawekezaji, wakulima, wajasiriamali, wafanyabiashara, taasisi mbalimbali na viongozi mbalimbali wa serikali.

Benki hiyo imefanya vizuri katika sekta ya kilimo na kwa kutoa mikopo kulingana na mnyororo mzima wa zao husika kupitia matawi yake 7, pamoja na kutoa huduma zingine za kifedha kupitia mawakala zaidi ya 105 na mashine za kutolea fedha za ATM mkoani humo.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kilimo wa benki hiyo Carol Nyangaro alisema katika benki hiyo ambayo serikali ina hisa ya asilimia 30 kupitia bodi ya mikopo iliidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya mikopo ya wakulima na tayari shilingi bilioni 450 zimetumika.

NMB ni benki inayotambua kuwa kilimo ndio uti wa mgongo nchini kwani asilimia 75 ya watanzania wanajishughulisha na kilimo na hivyo itaendelea kuwekeza zaidi katika kilimo.
Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kilimo wa benki ya NMB, Carol Nyangaro akitoa mada baada ya ufunguzi wa Jukwaa la tisa la fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Lindi mbele ya Meza kuu pamoja na wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk harrison Mwakyembe akizikiliza maelezo ya Meneja NMB kanda ya Kusini Janeth Shango alipotembelea banda la benki hiyo kabla ya ufunguzi wa Jukwaa la tisa la fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Lindi.

Serikali imewekeza nguvu katika sekta yw mawasiliano-Naibu Waziri Nditiye

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Serikali imesema katika sekta ya mawasiliano na kufanya nchi zingine kuiga katika mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA).

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wa Mkutano Mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Kusini Mwa Afrika (CRASA) amesema katika mawasiliano Tanzania imepiga hatua kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na Nchi zilizo kusini Mwa Afrika.

Nditiye amesema kuwa nchi nyingi zinajifunza katika udhibiti wa mawasiliano pamoja na kuangalia gharama za utoaji huduma kwa TCRA katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za mawasiliano.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika mawasiliano kutokana na Teknolojia za mawasiliano hayo kubadilika kila siku.
Aidha amesema mkutano huo watachagua viongozi ambapo na kutoa tathimini ya mawasiliano ambapo Tanzania tuko nafasi nzuri kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini(TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema changamoto ya mawasiliano ni watumiaji wenyewe katika vifaa vya mawasiliano.Amesema mtu ananunua simu lakini matumizi yake hajui ambapo anaweza kuminya kitufe chochote bila kujua na mwisho wa siku anatuma vitu vilivyokuwa nje ya maadili ya watanzania.

Mhandisi Kilaba amesema kuwa katika matumizi ya Data Tanzania tuko chini ukilinganisha na nchi nyingine na hiyo ni kutokana na uwekezaji wa miundombinu ya kuwaunganisha watoa huduma.Amesema hata upigaji wa simu kwenda mitandao moja ni ndogo na kufanya kila mtanzania kumudu mawasiliano ya kumiliki simu.
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Kusini Mwa Afrika (CRASA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Kusini Mwa Afrika (CRASA) pamoja na wageni waalikwa uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jimmy Yonas akitoa maelezo katika mkutano mkuu wa CRASA uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye alizungumza na wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Kusini Mwa Afrika (CRASA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba akitoa maelezo kuhusiana na mkutano mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Kusini Mwa Afrika (CRASA) uliofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa Tanzania ndio wenyeji wa mkutano huo.

HESLB:Sio wote wanahitaji mkopo wa elimu ya juu

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema utoaji wa mikopo unazingatia vigezo kwa wenye uhitaji wa mkopo huo kwa ajili ya kusoma elimu ya Juu na wengine sio wahitaji wa mkopo kutokana na hali za familia zao.
 
Hayo yamesemwa na Afisa wa Bodi hiyo Christina Chacha wakati Bodi hiyo ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Shule ya Sekondari Jitegemee, amesema kuwa mikopo haitolewi kwa wanafunzi kwa sababu ameomba kinachoangaliwa ni uhitaji msingi ambapo mwanafunzi huyo asipopata mkopo hawezi kuendelea na elimu ya juu.

Amesema kuwa kuna baadhi ya wazazi wanabudu gharama za kusomesha watoto hivyo wengine ambao kwa sababu mbalimbali hawezi kumudu ikiwemo umasikini na wakati mwingine ulemavu hivyo serikali inachukua jukumu ya kumkopesha mwanafunzi anayotoka familia hiyo.

Chacha amesema kuwa kuna wanafunzi wengine ni walemavu na familia zao ni masikini kwa vigezo hivyo anakuwa sehemu ya mhitaji mkopo kutoka bodi.
Aidha Chacha amesema kuwa mkopo wa bodi kwa wanafunzi wa elimu ya juu wote ila sifa yake ni kuwa Mtanzania bila kujali shule ya serikali au binafsi na kuzingatia ufaulu wowote.

Amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sanaa wanahisi kama wanabaguliwa wakati bodi inawaangalia wote kwa jicho moja kwa kwani wote wakihitimu shahada zao wanaijenga nchi."Tunatoa elimu hii ya uombaji mikopo ili muweze kujaza fomu zetu kwa usahihi na kurahisha bodi kutumia muda mdogo katika kupanga mikopo na shughuli zingine zikaendelea"amesema Chacha.

Mwanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Jitegemee Abdul Shafii amesema kuwa ujio wa bodi umetoa hofu katika uombaji mikopo kutokana na kupata taarifa zisizo sahihi.

Amesema elimu walioipata kutoka bodi ni muda mwafaka hivyo atatumia maelekezo hayo wakati wa kuomba mkopo.
 Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Christina Chacha akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa elimu ya uombaji wa mkopo wa elimu ya juu kwa wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Jitegemee.
 Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Shule ya Sekondari Jitegemee wakisilikiza bodi ya Mkopo ya Wanafunzi wa Elimu Juu (HESLB)
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Jitegemee Abdul Shafii akitoa maelezo namna walivyopokea elimu ya uombaji mkopo katika Bodi ya Mkopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)

BENKI YA NMB KANDA YA NYANDA ZA JUU YACHANGIA MILIONI 19 MAANDALIZI UZINDUZI WA MWENGE MKOA SONGWE

0
0

MKUCHIKA AMTEMBELEA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI NA MAMA MARIA NYERERE IKIWA NI SEHEMU YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiagana na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akimsikiliza Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), wa pili kushoto ni Mama Siti Mwinyi na wa kwanza kushoto ni Afisa anayesimamia Dawati la Viongozi Wastaafu wa Kitaifa, Bi. Nyasinde Mukono.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiteta jambo na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza na watoto wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipomtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wa kwanza kulia ni Andrew Nyerere na wa kwanza kushoto ni Magige Nyerere. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akimsikiliza Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
 Afisa anayesimamia Dawati la Viongozi Wastaafu wa Kitaifa, Bi. Nyasinde Mukono, akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Mkuchika ya kuwatembelea Viongozi Wastaafu wa Kitaifa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Shabiki wa Simba atetema na Sh84.8 milioni za M-BET

0
0
 Shabiki wa timu ya Simba, Chelsea, Juventus na Real Madrid , Semistocles Mkiza (41) ameshinda kiasi cha Sh 84,814,160 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali katika droo ya Perfect 12 inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet.

Mkiza ambaye ni mkazi wa Muleba Mkoa wa Kagera liibuka kidedea katika droo iliyofanyika Machi 24 na anakuwa mshindi nne kushinda mamilioni ya fedha ya M-Bet tokea kuanza kwa mwaka huu.

Msemaji wa kampuni ya M-Bet, David Malley alisema kampuni yao imedhihirisha kuwa ni nyumba ya mabingwa kutokana na kutoa mamilioninya fedha kwa Watanzania kadhaa na kuweza kubadili maisha yao.

Malley alisema kuwa kwa kuwa kampuni yao inafuata sheria za michezo ya kubahatisha nchini, Mkiza amekatwa Sh16, 962,632 kama kodi ya ushindi na kupelekwa serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Mkiz anaungana na washindi wengine wanne ambapo tokea Januari mwaka huu wameshinda mamilioni ya fedha na kuweza kubadili maisha yao. Tunaomba watanzania wenye umri kuanzia miaka 18, kujiunga na bidhaa zetu mbalimbali za kubahatisha ili kuweza kushinda,” alisema Malley.

Kwa upande wake, Mkiza alisema kuwa amefurahi sana kushinda kiasi hicho cha fedha ambacho atakitumia kwa masuala ya maendeleo.

Alisema kuwa hajaamini alipoambiwa kuwa ameshinda kiasi hicho cha fedha na kusubiri kwa hamu sana siku ya kakabidhiano. Alisema kuwa kushinda zaidi ya Sh milioni 84 kwa kutimia sh1,000 tu ni bahati ya hali ya juu.

“Mimi ni mjasiliamari, sikuwahi kupata kiasi hiki cha fedha pamoja na kubeti mara kadhaa, nitatumia kuhimarisha biashara zangu, kujenga nyuma na vile vile kusomesha watoto wangu,” alisema Mkiza.


Msemaji wa kampuni ya M-Bet, David Malley (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh 84,814,160 mshindi wa droo ya Perfect 12, Semistocles Mkiza (41) kutoka Muleba, mkoa wa Kagera. Mkiza amebashiri kwa usahihi matokeo ya mechi 12 tofauti katika ligi mbalimbali duniani. Picha na Mpiga Picha Wetu

BARAZA LA FAMASI NCHINI YAJIZATITI KUENDELEA KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI

0
0
* Yawashauri wananchi kuhusu matumizi sahihi ya dawa

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

BARAZA la Famasi nchini lililopo chini ya Wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto limejipanga katika kuendelea kutekeleza majukumu yao hasa kwa kuendelea kuboresha mifumo hasa ya ukaguzi, usajili pamoja na kujenga uwezo kwa wataalamu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika kikao kazi kilichowakutanisha, Msajili kutoka Baraza la Famasi nchini Elizabeth Shekalage amesema kuwa dira ya baraza hilo ni kuzidi kuwa taasisi bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kukidhi mahitaji ya jamii.

Amesema kuwa baraza hilo lina majukumu mbalimbali ikiwemo kusajili, kutambua na kutunza kumbukumbu za wanataaluma wa fani ya famasi ambao hadi sasa wataalamu wa kada hiyo waliosajiliwa imefikia 1863.

Pia amesema kuwa baraza hilo lina jukumu la kuhamasisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya dawa na kuwataka wananchi kutotumia dawa bila ushauri wa daktari kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.

Imeelezwa kuwa  baraza hilo hufuatilia malalamiko yote  yanayohusiana na usimamizi wa taaluma ya famasi yanayotolewa na wananchi na kusema kuwa wananchi wapo huru kupiga simu bure 0800110015 na malalamiko yao kutoka katika famasi na maduka ya dawa muhimu na yatafanyiwa kazi punde.

Akieleza mafanikio yaliyopatikana hadi sasa Shekalage amesema kuwa baraza limefikia malengo mengi ikiwa ni pamoja na kuwa moja ya taasisi ya mfano katika kutekeleza mpango wa kuboresha upatikanaji wa dawa (mpango wa maduka ya dawa muhimu) ambapo baadhi ya nchi zimekuja kupata ujuzi na kutekeleza mpango huo ambapo nchi za Uganda, Liberia, Zambia, Nigeria, Ghana, Burundi na Bangladesh zimejifunza namna ya utekelezaji wa mpango huo.

Pia Baraza hilo limefanikiwa katika masuala ya kusajili wafamasia, na hadi sasa baraza hilo limesajili fundi dawa sanifu 1863 na fundi dawa wasaidizi 625 huku wakijivunia uanzishwaji wa kozi ya mmoja ya utoaji wa dawa ambayi inethibitishwa na Baraza la Elimu ya Ufundi la Taifa (NACTE.)

Shekalage amesema kuwa mipango yao ya baadae kuzidi kuendelea kuboresha mifumo na wamejipanga zaidi katika masuala ya ukaguzi, usajili pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya mafunzo na maendeleo ya taaluma Grace Mallange amesema kuwa idara hiyo ambayo ina majukumu ya kusimamia mafunzo ya Famasi vyuoni ambapo inasimamia vyema katika hilo ili kuhakikisha kuwa vyuo hivyo vinazalisha wataalamu wenye tija na hiyo ni kwa kuandaa mitaala inayoongoza vyuo vyote, kuandaa na kusimamia miongozo ya kufundishia  ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu wanaofundisha vyuo hivyo.

Mallange amesema kuwa kuwa idara hiyo pia husimamia mafunzo ya vitendo kwa wafamasia (Intership) kwa kuhakikisha wanafanya mafunzo hayo katika sehemu zinazotambuliwa  na baraza pamoja na kusimamiwa na wafamasia wanaotambuliwa na baadaye kupimwa na mitihani kabla ya kuanza kazi zao za kitaaluma.

Pia Mkuu wa Idara ya usajili na utambuzi wa viwango vya kufuzu Suma Jairo amesema kuwa wanaendelea kutumia mfumo wa kieletroniki katika usajili ili kuthibiti kughushi leseni na vibali kwa maduka ya dawa muhimu na dawa moto.

Jairo amesema kuwa mahitaji wa wafamasia bado hayatoshelezi kulingana na idadi ya wananchi waliopo huku ushauri ukitolewa kwa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili kuweza kuweza wataalamu katika sekta hiyo.

Baraza la famasi nchini ambalo limeendelea kuratibu, kuboresha mifumo ya ukaguzi ili jamii ipate huduma bora hadi sasa imesajili wafamasia 1863, fundi dawa sanifu 2302, fundi dawa wasaidizi 652, na majengo ya kuuzia na kutunzia dawa 1683.

Msajili kutoka Baraza la Famasi nchini,Bi. Elizabeth Shekalage 

MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO

0
0
Na Woinde Shizza Globu ya jamii

Mahakama kuu kanda ya Arusha imeamuru familia ya watu zaidi ya saba wenye asili ya kiasia walioondolewa kimabavu kwenye nyumba yao na kukosa mahala pa kuishi, kurejea katika Nyumba hiyo bila masharti yoyote iliyopo eneo la Sabena katikati ya Jiji la Arusha.

Uamuzi huo umetolewa na jaji wa mahakama hiyo,Thadeo Mwenempazi baada ya kupitia maombi yaliyowasilishwa na upande wa familia hiyo kupitia Wakili wao ,Bariki Maeda na kuamuru familia hiyo kurejea katika nyumba yao wakati kesi ya msingi ikiendeleà kusikilizwa.

Jaji Mwenempazi alidai kuwa familia hiyo inapaswa kurejea katika nyumba hiyo na kuendelea na makazi wakati wakisubili maamuzi ya kesi ya msingi iliyopo mahakamani hapo.

Jaji katika maamuzi yake alidai kuwa mahakama hiyo imezingatia hoja zilizowakilishwa na upande wa mlalamikaji,ambaye ni familia hiyo kupitia Wakili Maeda na hivyo kuamuru kurejea katika Nyumba yao .

Familia hiyo iliondolewa kimabavu February 21 mwaka huu na kundi la watu zaidi ya 20 wakidai wanatekeleza amri ya mahakama na kusababisha usumbufu na uharibifu mkubwa wa Mali huku familia hiyo ikikosa mahala pa kuishi na kujikuta ikilala chini kwa wasamalia wema.

Akizungumza na vyombo vya habari mama wa familia hiyo,Chandni Hussein ameishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki na kumrejesha tena katika nyumba yake kwani taratibu zilizotumika kumtoa ndani yeye na watoto wake hazikufuatwa.

Ameongeza kuwa Nyumba hiyo iliyopo katikati ya jiji la Arusha yeye maduka ya kupanga huku familia hiyo ikiishi and a no ipo kwenye mgogoro na shemeji yake aitwaye Mortaza Hussein ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa jijini Dar es salaam

Akizungumza huku akibubujikwa machozi mahakamani hapo mama huyo amemshukuru rais John Magufuli kwa kuendeleà kuwa mtetezi wa wanyonge ambao wamekuwa wakionewa na watu wenye kipato kikubwa cha fedha.

Kesi hiyo ya Ardhi namba 6/2019 , wakili ,Maeda ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mawakili Tanganyika Mkoa wa Arusha, aliiomba Mahakama hiyo iwarejeshe kwenye Nyumba yao hadi kesi ya msingi itakapomalizika kwa kuwa taratibu zilizotumika kuwaondoa zilikuwa na mapungufu ya kisheria .
 Pichani mama wa familia hiyo Chandni Hussein akilia kwa furaha  mara baada ya mahakama kutoa maamuzi.
 

DKT. MPANGO AAGIZA KUTOTUMIA FUNGU LA LISHE KWA MATUMIZI MENGINE

0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipeana mkono na Binti Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Duniani, Sarah Zeid (kushoto), baada ya kumalizika mkutano kuhusu Lishe uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Binti Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya lishe Duniani, Sarah Zeid (kushoto), wakifurahia jambo katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Shirika la Chakula Duniani- WFP, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)

…………………………..


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Binti wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, ambaye ni Mwanaharakati wa masuala ya lishe, wanawake na watoto Duniani, jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao, Dkt. Mpango, alimweleza Princess Sarah Zeid kwamba Tanzania bado inakabiliwa na changamoto ya masuala ya lishe, utapiamlo na udumavu wa watoto licha ya nchi kuwa na chakula cha kutosha.

Dkt. Mpango alisema kuwa iwapo eneo la lishe halitasimamiwa kikamilifu Taifa litazalisha watoto wenye udumavu wa ubongo na kusababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiri na utendaji hafifu wakiwa katika shughuli mbalimbali.

Alisema ipo mikoa ambayo inazalisha mazao mengi kama Mbeya na Njombe lakini ina kiwango kikubwa cha watoto wenye utapiamlo, na kutoa wito kwa kila mtanzania kuhakikisha anaangalia ni chakula gani kinahitajika kwa ajili ya lishe ya watoto na wakinamama wajawazito ili kupunguza udumavu na vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.

Aidha amempongeza Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, kwa kampeni yake anayoifanya duniani kote kupambana na vifo vya wakinamama wajawazito na watoto kwa kuwa mchango wa wanawake ni mkubwa katika jamii ikiwemo uzalishaji mali.

Alisema idadi ya wanawake nchini Tanzania ni asilimia 51 ya idadi ya watu wote wanaokadiriwa kufikia milioni 55 ambapo mchango wako katika sekta mbalimbali za uchumi umekuwa mkubwa hivyo jitihada za kuwalinda zinahitajika.

Alimweleza Binti Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid kwamba kwa kutambua umuhimu wa lishe serikali imelivalia njuga suala la lishe kwa kutenga bajeti kila mwaka katika kila wizara na kwamba fedha hizo zimewekewa wigo zisitumike kwa matumizi mengine.

“Nimeziagiza Wizara, Mikoa na Halmashauri zote nchini kutumia fungu lililotengwa kwa ajili ya lishe kwa matumizi yaliyopangwa ili kuhakikisha watanzania wanaimarika kiafya na kushiriki kikamilifu katika Shughuli za Maendeleo” Alisema Dkt. Mpango.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa Mkutano kati yake na Mwana wa Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Dunia, Sarah Zeid na

Kwa upande wake Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, ambaye aliambatana na Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) nchini Tanzania, Bw. Michael Dunford, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake katika kupambana na utapiamlo unaosababishwa na ukosefu wa lishe.

Amewataka watanzania kuhakikisha suala la Lishe linapewa kipaumbele na kila mmoja kwa manufaa ya Taifa na Dunia kwa ujumla na kwamba atahamasisha jumuiya ya kimataifa kuchangia jitihada za Serikali za kupambana na tatizo la lishe, na vifo vya wanawake wajawazito na watoto.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa-WFP nchini Tanzania Bw. Michael Dunford, amesema kuwa shirika lake linatambua mchango mkubwa wa Serikali katika kupambana na masuala ya lishe duni na shirika lake litaendelea kushirikiana na nayo ili kufikia malengo yanayotarajiwa.

WAZIRI WA MAJI PROF.MBARAWA AKAGUA MIRADI YENYE CHANGAMOTO MKOANI SONGWE

0
0

Moja ya miundombinu ya maji inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ambapo Waziri Mbarawa alifika kukagua ujenzi huo.

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akiwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Generali Mstaafu Nicodemus Mwangela katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe David Kafulila.


Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Generali Mstaafu Nicodemus Mwangela.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akipata maelezo ya ujenzi wa tanki (halipo pichani) kutoka kwa Mhandisi wa Maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya Mhandisi Ndele Mengo. Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Momba Halmashauri ya Tunduma Bw. Juma Said Irando.

…………………………

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) leo ameanza ziara ya kukagua miradi ya maji mkoani Songwe hususan miradi yenye changamoto ambayo imechukua muda mrefu kukamilika.

Waziri aliyasema hayo alipofika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela mara tu baada ya kuwasili ofisini kwa Mkuu wa mkoa huyo.

“Nimekuja kukagua miradi ambayo ina changamoto kubwa ambayo haijakamilika kwa muda mrefu na wananchi wanaisubiri kwa muda mrefu” alisema Profesa Makame Mbarawa.

Serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeahidi kwamba ifikapo mwaka 2020 kwenye miji mikuu ya mikoa wananchi wawe wamepata maji asilimia 95 na miji ya wilaya asilimia 90 na vijijini asilimia 85.

Hata hivyo, Waziri alisisitiza kwamba tunapopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji inabidi lazima tusimamie kwa uadilifu, ukaribu zaidi na kuhakikisha kwamba wakandarasi wanaolipwa pesa kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maji wanaanza kazi mara moja baada ya kulipwa, kwa sababu wakandarasi wengine wamekuwa na tabia ya kuchukua pesa za miradi ya maji na kupeleka kwenye miradi mingine.

Naye, Mhandisi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya, Mhandisi Ndele Mengo akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Itumba Isongole amesema Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi Singilimo Enterprises Ltd. ya jijini Dar es Salaam ambapo gharama ya mradi ni Tsh. 804,162,330/= na hadi sasa ameshalipwa Tsh. 313,238,780/= ambazo zikihusisha uchimbaji wa mitaro kwenye bomba kuu chanzo cha umbali wa mita 4332 na ulazaji wa bomba za plastic wenye kipenyo cha nchi 8 umbali wa mita 3924 pamoja na tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita laki. Mradi huu amesema unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya. Matazamio ya kukamilika kwa mradi huu ni 30/5/2019.

Aidha, Waziri Profesa Mbarawa ameagiza mradi wa Itumba Isongole uwe umekamilika ifikapo tarehe 30/5/2019 na mradi wa maji wa mji wa Tunduma uwe umekamilika ifikapo 13/4/2019 ili wananchi wapate majisafi na salama kwa sababu karibu wakandarasi wote wameshalipwa pesa zao walizokuwa wanaidai Serikali.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images