Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1819 | 1820 | (Page 1821) | 1822 | 1823 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii wakipewa maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Hashimu Paschal kuhusiana na matumizi ya silaha za moto aina ya AK-47 i wanapofanya doria wakiwa Hifadhini wakati wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge walipotembelea chuo hicho mjini Moshi. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shabani Shekilindi (wa pili kulia) akiwa na Wajumbe wa Kamati hiyo wakipewa maelezo huku wakiangalia baadhi ya taswira za wanyamapori mbalimbali wanaotumika kwa ajili ya kuwafundishia wananfunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro wakati kamati hiyo ilipofanya ziara Chuoni hapo.

  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii wakipewa maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Judith Mwela kuhusiana na handaki lililotengenezwa na kabila la Wachaga mnamo karne ya 18 kwa ajili ya kujihami dhidi ya maadui kabla ya Wajumbe hao kuingia ndani ya Handaki hilo kwa ajili ya kujionea , Handaki hilo lipo katika Chuo hicho

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shabani Shekilindi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na watumishi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shabani Shekilindi akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwasalimia na baadhi ya Watumishi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara Chuoni hapo.

  Baadhi ya magari maalum yAnayotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka wakati wanapofanya mafunzo kwa vitendo katika Hifadhi nchini. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII) 

  …………………………………………………………………………………………
  Wizara ya Maliasili na Utalii imesema imeanza kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto zinazokikabili Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka ili kiendeleze hadhi yake ya kuwa Chuo cha Kimataifa. 

  Hatua hiyo inakuja kufuatia kupungua kwa idadi ya wanafunzi wa kigeni wanaojiunga na Chuo hicho kila mwaka. 

  Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii iliyotembelea Chuo hicho mkoani Kilimanjaro, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema shabaha ya Wizara ni kukiona chuo hicho kikiendelea kuwa na hadhi ya Kimataifa. 

  Amewaeleza Wajumbe hao kuwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Wizara kuendelea kufanya mazungumzo na vyombo vya udhibiti na Usimamizi wa Elimu hapa nchini ( TCU na NACTE) ili viangalie namna ya kuondoa masharti magumu yanayosababisha baadhi ya masomo yanayotolewa na nchi nyingine yasitambuliwe chuoni hapo. 

  Mhe.Kanyasu ameiambia kamati hiyo kuwa sababu nyingine ya idadi ya Wanafunzi wa kigeni kupungua ni baadhi nchi kama Malawi na Kenya kuanzisha vyuo vyao tofauti na ilivyokuwa mwanzo. 

  Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Shabani Shekilindi amesema Chuo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za uhaba wa wahadhiri pamoja na uchakavu wa miundombinu. 

  Amesema kupitia Kamati anayoiongoza atahakikisha kuwa changamoto zote zinapatiwa majibu ili chuo hicho kiendelee kutoa huduma bora. Amekishauri chuo hicho kiendelee kuzitangaza kozi zake ndani na nje ya nchi. Naye Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Boniphace Getere amekishauri chuo hicho kiingie mkataba na watu binafsi kwa ajili kujenga mabweni yatayokayosaidia kutatua changamoto ya wanafunzi 228 kati ya 600 wanaolazimika kupanga nyumba nje ya Chuo hicho.
  Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori , Mweka kilianzishwa mwaka 1963 kikiwa na wanafunzi 25 kutoka Kenya, Uganda Malawi , Cameroun na Tanzania.

  0 0

   Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.
   Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.
   Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.
   Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.
   Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.
   Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Bw, Paul Rwegwasha akitoa taarifa fupi ya Mamlaka kuhusu mpango wa  usimamizi na uendeshaji jengo la III la abiria kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo mapema leo.
   Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu  ambaye ni Mbunge wa Kasulu mjini Mhe, Daniel Nsanzugwako (mwenye kofia) akiuliza swali mara baada ya kusomwa taarifa ya mradi wa Jengo la III la abiria wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo mapema leo.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa (Mb) akijibu hoja maswali mbalimbali ya kisera kwa wajumbe wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la III la abiria  mapema leo.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Atashasta Nditiye alipokuwa akijibu maswali kwa wajumbe wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la III la abiria  mapema leo aliekaa kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Mpanda Vijijini Moshi Selemani Kakoso. 
  Mhandisi Burton Komba kutoka Wakala wa Barabara akitoa maelezo ya Ujenzi wa Jengo la III la abiria kwa Wajumbe wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipofanya ziara katika Jengo hilo mapema leo.  MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imebainisha kwamba itakua tayari kwa ajili ya utoaji wa huduma za uendeshaji katika Jengo la tatu la abiria pale mradi wa Ujenzi utakapokuwa umekamilika.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha alipokua akitoa taarifa fupi ya TAA kwa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu ilipofanya ziara katika eneo la Ujenzi huo.

  Bw. Rwegasha amesema hatua mbalimbali za Maandalizi tayari zimeshachukuliwa kwa kushirikiana na wadau wa huduma hizo, ikiwa ni pamoja na utoaji wa mafunzo yanayohitajika kwa watendaji wa ngazi mbalimbali.

  “Mamlaka inaendelea kufanya taratibu za maandalizi ya utoaji huduma za uendeshaji katika Jengo la tatu la abiria, katika mpango huo tayari mafunzo kwa watendaji mbalimbali yameanza na hivi sasa watendaji 40 wapo Korea ya kusini katika mafunzo” amesema Bw. Rwegasha.

  Aidha Bw. Rwegasha amebainisha kwamba katika utekelezaji mpango wa uhamishaji shughuli, Mamlaka imejipanga kuhakikisha hakuna madhara yeyote ya kiuendeshaji yanajitokeza.

  “Mamlaka itahakikisha kwamba inazuia athari zote zinazoweza kutokana na zoezi la uhamishaji wa shughuli za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa Ndege na abiria, uharibifu wa mitambo,madhara ya kiusalama na kadhalika.

  Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Idara ya Viwanja vya Ndege katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Emmanuel Raphael amebainisha kwamba hadi kufika mwezi February 2019 utekelezaji wa kazi zote ulifikia asilimia 95.

  “Ujenzi wa kazi zote za Ujenzi umefikia 95%, ambapo mchanganuo unaonesha kwamba ujenzi wa jengo umefikia 96%, maegesho ya magari 92%, maegesho ya ndege 98% na kwa ujumla kazi zinaenda vizuri na zinatarajiwa kukamilika Mei 31, 2019”, alisema Mhandisi Raphael.

  Naye, Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amebainisha kwamba mpaka sasa Wananchi wa Kipawa waliopisha upanuzi wa Kiwanja wameshalipwa fidia na kwamba mpaka sasa hamna mgogoro wa fidia.

  Akitoa majumuisho baada ya ziara ya kamati katika eneo la ujenzi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Mhe. Seleman Kakoso amesema kwa ujumla Kamati imeridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kwamba wameridhishwa na namna pesa ya serikali ilivyotumika.

  “Kwa ujumla Kamati imeridhishwa na hatua ya Ujenzi iliyofikiwa, matumizi ya pesa ya Serikali yanaonekana ni mazuri, lakini natoa wito kwa TAA kuongeza kasi ya maandalizi ili kwenda sawa na kasi ya ujezi huu, lakini pia mjipange kuongeza wafanyakazi ili kuhakikisha kwamba watendaji wa huduma za uendeshaji wanajitosheleza”, amesema Mhe. Kakoso.  0 0

  Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii.

  Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Mashariki imesema kuwa njia ya bora ya kufanya watumiaji wa mawasiliano kufuata sheria na taratibu za mawasiliano hayo ni kuwapa elimu.

  Hayo aliyasema Mkuu wa Kanda ya Mashariki Mhandisi Lawi Odiero wakati wa maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mlaji Duniani ambapo Kanda hiyo ilitoa elimu katika shule ya Sekondari Minaki iliyopo Kisarawe mkoani Pwani amesema wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita ndio wanaingia katika utumiaji wa mawasiliano hivyo lazima wapewe elimu ya kutosha katika kutumia mawasiliano hayo.

  Odiero amesema wanafunzi wakipata njia bora ya utumiaji wa mawasiliano wanakuwa chachu katika kuelimisha watu wengine kutokana na uelewa wao kuwa mkubwa.Amesema katika maadhimisho ya siku ya haki ya walaji duniani inatoa fursa katika TCRA kuwa na muendelezo ws kutoa elimu ya mawasiliano kwa wadau ili wajue sharia mbalimbali za mawasiliano hayo ili yasitumike visivyo na kuondoa maana ya mawasiliano.

  Amesema katika kuelekea uchumi wa viwanda mawasiliano ni njia ya kufungua fursa ya watumiaji wa mawasiliano hayo kutengeneza ajira kutokana na teknolojia iliyopo katika mitandao ya simu.Aidha amesema kuwa sheria iliyopo kwa kampuni za simu ni kuhakikisha wanatoa huduma bora ya mawasiliano na wale ambao wanakiuka sheria kushika mkondo wake.

  Amesema watumiaji wa mawasiliano wanatakiwa kutuma ujumbe wenye maadili na wanaofanya kutuma ujumbe wa uchochezi,matusi kufunguliwa mashitaka mahakamani lengo ni kufanya mawasiliano kuwa salama.

  "Dunia hii imekuwa kijiji kutokana na mawasiliano hivyo kila kitu kinachofanyika kiendane na maadili yetu nchini pamoja na watu wengine wajifunze kwani sio kila kitu kiwekwe katika mawasiliano na njia rahisi kila mtu anayepata ujumbe usiofaata maadili hayo ni kufuta"amesema Odiero.

  Nae Mwalimu wa Shule ya Sekondari Minaki Sweatbert Kijumba amesema wanafunzi wakipewa elimu ndio nguzo ya kufanya nchi kuwa na mawasiliano salama kwani wenyewe ndio wanaingia kwa kasi katika utumiaji wa mawasiliano.

  Amesema Teknolojia ya mawasiliano inabadilika hivyo TCRA iendelee kutoa elimu katika makundi mbalimbali ili watumiaji wajue sheria za mitandao kwa kuwafikia moja kwa moja.Kwa upande wa Afisa Masoko wa TCRA Joyce Paul amesema kuwa wanafunzi wakipata uelewa wa matumizi ya simu ndio mabalozi wa kuelimisha jamii katika ngazi za familia.

   Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wakati Kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ikiwa ni maadhimisho ya Siku Haki ya Walaji ambayo hufanyika kila Machi 15 ya kila Mwaka.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wakiwasikiliza TCRA Kanda ya Mashariki wakati wa maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani ambayo hufanyika Machi 15 ya Kila Mwaka.
   Afisa Masoko wa Mamlaka ya Mawasiliano Joyce Paul akitoa maelezo kuhusiana utendaji wa mamlaka katika udhibiti wa mawasiliano wakati Kanda ya Mashariki TCRA ilipokwenda kutoa elimu katkka shule ya Sekondari Minaki iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
   Mhandisi Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TCRA Robson Shaban akitoa maelezo namna wanavyofatilia mawasiliano wakati akitoa elimu katika Shule ya Sekondari Minaki ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani.
   Mwalimu wa Shule ya Sekindari Minaki Sweatbert Kijumba akitoa maelezo juu ya ujio wa TCRA Kanda ya Mashariki katika shule hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani.

  0 0

  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakipokea taarifa za maendeleo ya miradi ya gesi asilia jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni. 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba (mwenye overall ya bluu) akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya PIC kazi ya kusambaza gesi asilia kwa wateja kwa matumizi ya majumbani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni. 
  Mhandisi Dora Ernest (alieshika mic ya TBC) akitoa maelezo ya huduma ya kusambaza gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC). 


  Kamati ya Bunge inayosimamia uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) imefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya miradi ya gesi asilia jijini Dar es Salaam.

  Kamati hiyo inayoongozwa na Mhe. Dkt. Raphael Chengeni ilitembelea kituo cha kupokea gesi asilia Kinyerezi na kujionea kazi za kitaalam zinazofanywa na wazawa katika kupokea gesi na kuisambaza kwa wateja mbalimbali wakiwemo wazalishaji umeme. 

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba akitoa wasilisho juu ya mikakati ya TPDC katika kujiendesha kibiashara alisema “katika mwaka huu wa fedha tunategemea kuanza kutoa gawio Serikalini”. Mhandisi Musomba aliieleza Kamati ya PIC kwamba kwa sasa Shirika liko katika mageuzi makubwa ya kiutendaji nia ikiwa ni kuongeza ufanisi na hatimaye kutengeneza faida itakayoruhusu kutoa gawio kubwa Serikalini. 

  Katika kipindi cha miaka mitatu TPDC imekuwa ikijeindesha kwa hasara kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia. 

  Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Mh. Dkt. Raphael Chengeni alisema “Sisi kama Kamati tumefurahishwa sana na mageuzi makubwa ambayo yanaendelea kufanyika TPDC kwani hili lilikuwa moja ya Shirika ambalo linaonekana kuwa mzigo kwa Serikali kwa kushindwa kutoa gawio kwa Serikali”. 

  Dk. Chengeni aliongeza kwamba kwa taarifa waliyopokea TPDC sasa wanaamini mambo yatakuwa mazuri katika Shirika hili ambalo linategemewa sana katika kufikia Tanzania ya viwanda kwa kuzingatia upekee wa bidhaa wanayozalisha, gesi asilia. Wajumbe wengine wa PIC pia walionekana kuridhishwa na utekelezaji wa miradi na mageuzi ambayo TPDC imeshaanza kuyafanya.

  Katika ziara hiyo Wabunge walipata nafasi ya kutembelea eneo la Ubungo na kujionea wa mtambo wa kupunguza mgandamizo wa gesi kwa ajili ya kusambaza kwa wateja wa majumbani na viwandani. Pia walitembelea maeneo ya Mlimani City na kujionea zoezi la kuunganisha gesi kwa wateja wa majumbani na baadae kiwanda cha Coca-Cola maeneo ya Mikocheni ambao nao wanatarajiwa kuanza kutumia gesi baada ya kazi ya kuunganisha kukamilika. 

  Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma inaangalia mambo matatu makubwa, kwanza gawio linalokwenda Serikalini, kupokea mtaji unaozidi na suala la mapato ghafi ambayo ni 15%, alieleza Mwenyekiti wa Kamati, Dk. Raphael Chegeni.


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na dada yake, Fatma Majaliwa kijijini kwake Nandagala Machi 15.2019, kushoto ni mtoto wa dada yake Hidaya Rashid.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na vijana waendesha bodaboda kijijini Nandagala wilayani Ruangwa Machi 15.2019.
  aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi bakora mwanakijijini wa Nandagala Mzee Khamis Kandege Machi 15.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kisima cha maji safi, katikakijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa Machi 15.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwashukuru Halima Athumani (kulia) na Zuena Bakari (katikati) kwa zawadi yamahindi, katika kijiji cha Nandagala Wilayani Ruangwa Machi 15.2019
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia watoto, katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa Machi 15.2019
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na vijana kijijini kwake Nandagala wilayani Ruangwa Machi 15.2019

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Bi. Fatu Omar kijijini kwake Nandagala Machi 15.2019, aliye soma nae darasa moja shule ya msingi
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo na mmoja wa Watoto waliopo kijijini kwake Nandagala

  0 0

   WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto), akisoma moja ya bango liloandikwa na wananachi kabla ya kuanza mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Tarafa ya Kimamba, Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, alipofika katika tarafa hiyo kwa lengo ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo inaleta uvunjifu wa amani katika eneo hilo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Adamu Mgoyi. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi.
  WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, akizungumza na mamia ya wananchi wa Tarafa ya Kimamba, Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, alipofika katika tarafa hiyo kwa lengo ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo inaleta uvunjifu wa amani katika eneo hilo. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi.
   WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza mwakilishi wa wananchi katika Tarafa ya Kimamba, Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro, akisoma hukumu zilizotolewa na mahakama kuu na ya rufaa ambayo inaonyesha Mfuaji Lipasio Mbokoso (hayupo pichani) wa Tarafa hiyo alishinda kesi hiyo dhidi ya wananchi wachache waliofungua kesi ya ardhi wakidai ni mali yao. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mkazi wa Tarafa ya Kimamba, Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro, Iris Diamond, akitoa kero yake kuhusiana na mgogoro wa ardhi kati yake na wananchi wa Tarafa hiyo. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Na Felix Mwagara, Kilosa

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ametumia saa tano kuwatuliza wananchi wa Tarafa ya Kimamba Wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, ambao walikuwa na hasira kali wakilalamika kunyang’anywa ardhi na wafugaji pamoja na Polisi kuwanyanyasa wananchi hao kwa kuwaweka ndani.

  Waziri Lugola ambaye aliwasili saa sita mchana akitokea mjini Morogoro kwa ajili ya kutekeleza ahadi yake kwa wananchi hao baada ya kuwaahidi wiki iliyopita alipofanya ziara katika Tarafa hiyo ambayo ina wakazi zaidi ya elfu hamsini, ili aweze kutatua kero zao za ardhi wakiwa na nyaraka zao za uthibitisho.

  Kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi hao, Waziri huyo alifanya kikao cha ndani na viongozi wa Wilaya hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya, kwa lengo viongozi hao kumpa sura halisi ya mgogoro huo ambao unaelekea katika uvunjifu wa amani.

  Lugola aliwasili eneo la mkutano mara baada ya kumaliza kikao cha ndani, ambapo alipokelewa na mabango ya wananchi ambayo yalikuwa yameandikwa ujumbe mbalimbali ikiwemo ‘Polisi wa Dumila wanatumika kuwanyanyasa wananchi na polisi wa Chanzulu wanakamata watu na kuwaweka ndani wananchi wanaotafuta haki ya ardhi’, wafugaji wanapora ardhi zetu, polisi wanapewa rushwa na wafugaji kutuweka ndani’. 

  Akizungumza na mamia ya wananchi hao, Lugola alisema amekuja kusikiliza kero za wananchi hao baada ya kutoa ahadi yake wiki iliyopita, hivyo anatumaini wananchi hao wanavielelezo kama alivyowaagiza waje nazo katika mkutano huo.

  Lugola alisema Jeshi la Polisi alihusiki na masuala ya ardhi isipokuwa limekua likichukua hatua pale migogoro hiyo inapopelekea kwenye uhalifu ama uvunjifu wa amani.

  Lugola alishangiliwa na wananchi hao alipowaita waje mbele ya meza kuu ili waweze kutoa kero zao, ndipo idadi kubwa ya wananchi hao waliitikia wito huku baadhi yao wakiwa na nyaraka mbalimbali kama walivyoelekezwa na Waziri huyo waje nazo katika mkutano huo.

  Licha ya wananchi hao kutoa kero mbalimbali lakini tatizo kubwa walikuwa wanamtuhumu mfugaji maarufu ambaye ni Mmasai katika Wilaya hiyo, Lipasio Mbokoso, anayedaiwa kunyang’anya ardhi zaidi ekari 270 ambazo wanadai sio zake lakini anatumia nguvu ya fedha kuichukua ardhi ya wananchi hao.

  Waziri Lugola alimwita Mbokoso katika mkutano huo ili aweze kujitetea kwa nyaraka zake, ndipo ikajulikana kuwa Mmasai huyo ardhi hiyo ni mali yake halali baada ya kushinda kesi iliyofunguliwa na wananchi hao mahakamani. 

  “Nyaraka zinaonyesha Mbokoso ni mmiliki halali wa ardhi hii, na pia wananchi ambao nimewataja walifungua kesi, na Mbokoso akashinda kesi hiyo mahakama kuu, baadaye mkakata rufaa mkaenda mahakama ya rufaa, pia akashinda, ndugu wananchi naomba mueleze na hakuna haja ya malumbano, huyu ni mmiliki halali wa mali hiyo, musidanganywe na mtu yeyote, fuateni sheria pamoja na kuiheshimu hukumu ya mahakama,” alisema Lugola.

  Aliongeza kuwa, kuna baadhi ya wanasheria feki katika eneo hilo wanawarubuni wananchi kwa kuwapotosha na kuwasababisha munaingia katika migogoro ya ardhi na amani inatoweka katika eneo hilo kwasababu tu ya watu wachache ambao wanawapotosha. 

  “Wanasheria feki ndio wanaochangia migogoro ya ardhi katika sehemu mbalimbali ya Wilaya ya Kilosa, nawataka wananchi kutowatumia badala yake mufuate sheria kama inavyoelekeza,” alisema Lugola.

  Kutokana na matatizo ya ardhi kuendelea kutokea katika eneo hilo, Waziri Lugola amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Wilbroad Mutafungwa kuchunguza nyaraka zote za migogoro ya ardhi inayowasilishwa na wananchi ili kujua kama ni halali au zimeghushiwa.

  Sambamba na hilo, Lugola amemtaka Kamanda huyo kuwachukulia hatua kali za kinidhamu askari wote wasiokuwa waadilifu katika eneo hilo na Mkoa kwa jumla, watakaohusika kuwanyanyasa wananchi hasa katika masuala ya ardhi. 

  Kauli ya Waziri huyo ilileta furaha kwa sehemu kubwa ya wananchi hao licha ya kuwa baadhi yao wakilalamika kuwa, Polisi wameshindwa kutatua kero zao na kuwadharau wakulikuma na kuwathamini wafugaji, hata hivyo Waziri huyo aliahidi kufuatilia mara kwa mara amani ya eneo hilo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tayari amewasili kwenye Kongamano la Kumpongeza Dkt. Ali Mohammed Shein Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika uwanja wa Hoteli ya Verde, leo tarehe 16 Machi, 2019.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa, Gaudencia Kabaka ,wakati akiwasili kwenye Kongamano la Kumpongeza Dkt. Ali Mohammed Shein Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika uwanja wa Hoteli ya Verde, leo tarehe 16 Machi, 2019.


  0 0

  Na Estom Sanga- Mtwara 

  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wameridhishwa na mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ambao umeleta hamasa kubwa kwa Walengwa wake kupambana na umaskini. 

  Wajumbe wa Kamati hiyo ambao wametembelea kijiji cha Namela katika wilaya ya Mtwara ambako wamepata fursa ya kuonana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kushuhudia namna Walengwa hao wanavyotumia fursa za Mpango huo kujiletea maendeleo. 

  Wakiwa kijijini hapo Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wamepata ushuhuda kutoka kwa baadhi ya Walengwa wa TASAF ambao wametumia fursa ya kuwepo kwenye Mpango huo kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji wa mbuzi na Kuku wa Kienyeji kuhamasisha watoto wao kuhudhuria masomo huku wengine wakiboresha makazi yao na kununua vifaa vya umeme jua ( solar systems. 

  ‘’…….nimetumia fursa ya kuorodheshwa na TASAF kwa kununua mbuzi ambapo hadi sasa nina zaidi ya mbuzi kumi” ninaishukuru sana serikali kwa kuniwezesha kujikomboa amesisitiza mmoja wa walengwa mbele ya Wajumbe wa Kamati hiyo ya bunge. 

  Taarifa ya mkoa wa Mtwara imeonyesha kumekuwapo na manufaa ya kujivunia ambayo yamepatikana kutokana na utekelezaji wa shughuli za TASAF mkoani humo hususani katika sekta za Afya, Elimu,Miundombinu,uundaji wa vikundi vya kuweka na kuwekeza akiba na kujiongezea kipato kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi. 

  Walengwa hao wa TASAF mkoani Mtwara pia wamehamasishwa kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana vipatavyo 3,070 vyenye jumla ya wanachama 43,872 ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka uliopita vikundi hivyo vimefanikiwa kujiwekea akiba ya zaidi ya shilingi milioni 537 na kukopeshana kiasi cha shilingi milioni 409 kwa ajili ya kuwekeza kwenye shughuli za kiuchumi hususani kilimo na ufugaji. 

  Akizungumza kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati hiyo Mwenyekiti wake Mheshimiwa Steven Rweikiza amepongeza mafanikio yaliyopatikana katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuwapunguzia Wananchi na adha ya umaskini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF. 

  Hata hivyo kilio kikubwa ambacho kimekuwa kikipazwa sauti na Wajumbe wa Kamati ,Viongozi na Wanachi kwenye maeneo mengi nchini ni sehemu ya Wananchi ambao bado wanaishi kwenye hali ya umaskini ambao bado hajapata fursa ya kujumuishwa kwenye huduma za Mpango wa Kunusuru Kasya Maskini. 

  Kwa nyakati tofauti Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Kapteini Mstaafu George Mkuchika amekuwa akisisitiza azma ya serikali ya kuhakikisha kuwa katika utekelezaji wa sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru kaya maskini vijiji /shehia na wananchi ambao watakidhi vigezo vya kuorodheshwa kwenye Mpango wanapata fursa hiyo . 

   Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya bunge ya kudumu ya bunge ua utawala na serikali za mitaa wakifurahia maelezo baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Namela mkoani Mtwara.
   Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe.Venance Mwamoto (aliyevaa shati jeupe) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga aliyenyoosha mkono wakiwa na mmoja wa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Namela wilaya ya Mtwara mbele ya nyumba aliyoijengwa kwa kutumia fursa za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.   
  Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu ya Utawala na serikali za mitaa Mhe. Steven Rweikiza (mwenye Kaunda suti) akiwasikiliza  Walengwa wa TASAF wakielezea mafanikio waliyoyapata baada ya kujumuishwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Namela mkoani Mtwara.


  0 0

   
  Mtendaji Mkuu wa kampuni ya VodaCom Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Macfydene Minja (kushoto) akionesha bango lenye orodha ya viwango vya kutoa pesa vinavyotozwa wakati wa kutoa fedha kwenye Mpesa kwa wanafunzi wa Sekondari kutoka mikoa saba ya kanda hiyo ambao wamechaguliwa katika mradi wa Interantional Girls in ICT kwa ajili ya kushindani katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Wasichana ya TEHAMA, walipofika katika makao makuu ya Vodacom kanda hiyo zilizopo Uhindini Jijini Mbeya ili kujifunza.


  Meneja Mawasiliano na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Christina Murimi, akigawa vifaa kwa wanafunzi waliotembelea ofisi za Vodacom kujifunza juu ya utendaji kazi wa kidijitali wa kampuni hiyo. Katika kusherehekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Vodacom iliwakaribisha wanafunzi hao wa kike kutoka shule mbalimbali na kuwapatia mafunzo ya ufanyaji kazi wa kidijitali katika idara na vitengo vya kampuni hiyo.
  Mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania PLC, Grace Chambua akizungumza juu ya umuhimu wa elimu kwa wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali za kanda ya kati walipotembelea ofisi za kampuni ya Vodacom jijini Dodoma. Katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, Vodacom iliwakaribisha wanafunzi hao na kuwapatia mafunzo juu ya ufanyaji kazi wa idara na vitengo mbalimbali katika sekta ya mawasiliano.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na baadhi ya wazee waliokuwa wakaazi wa nyumba za Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kuona maendeleo ya ujenzi wa nyumba za ghorofa alizoziwekea jiwe  la msingi Aprili 15, 2017 ambapo mpaka sasa ujenzi wake umesimama kwa sababu ambazo hazikuweza kujulikana mara moja.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari Magereza huko Ukonga jijini Dar es salaam alikofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwangalia Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza  Julius Ntembala akipima nguzo wakati akikagua  maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari Magereza huko Ukonga jijini Dar es salaam alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za ghorofa za Magomeni Kota jijini Dar es salaam alizoziwekea jiwe  la msingi Aprili 15, 2017 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za ghorofa za Magomeni Kota jijini Dar es salaam alizoziwekea mnamo  Aprili 15, 2017 ambapo mpaka sasa ujenzi wake umesimama alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari Magereza huko Ukonga jijini Dar es salaam alikofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wana familia ya moja ya nyumba za askari Magereza huko Ukonga jijini Dar es salaam alikotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari hao alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019
  PICHA NA IKULU


  0 0

     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa ambaye pia ni mjumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni iliyowasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa ambaye pia ni mjumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa wapili kutoka kushoto, Balozi wa Uganda hapa nchini Richard Kabonero pamoja na Balozi Zuhura Bundala mara baada ya mazungumzo na mjumbe huyo maalum Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa ambaye pia ni mjumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. wakwanza kushoto Balozi wa Uganda hapa nchini Richard Kabonero.  PICHA NA IKULU


  0 0  Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda (katikati) na Meneja wa QNET, kanda kusini ya Afrika Biram Fall (kushoto) wakikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya bidhaa za QNET 2019 jijini humo. Kulia ni Mshauri wa Biashara wa QNET Tanzania, Edward Mkony.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wawakilishi, wafanyakazi na waalikwa wa QNET kuhusu maadili ya kazi kwenye uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za QNET jijini Dar Es Salaam jana.

  ………………………………………………………………………….

  *Maelfu wa hudhuria maonyesho ya QNET Dar es salaam

  *Watanzania kunufaika na bidhaa mbalimbali pamoja na fursa za biashara

  Kampuni yenye asili ya Asia ya mauzo ya moja kwa moja QNET imeendesha maonyesho ya bidhaa na huduma zake jijini Dar es salaam siku ya tarehe 16 na 17 Machi 2019. 

  Maonyesho yenye jina la Absolute Living, (Kuishi kikamilifu) sambamba na falsafa ya bidhaa za kampuni ya mauzo ya moja kwa moja, huwa yanafanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali duniani kote ikiwa na lengo la kuonyesha bidhaa zake na huduma kwenye masoko mapya. Onyesho hilo pia ilikuwa kama jukwaa kwa wateja na wadau wengine wanaotaka kufahamu kuhusu QNET na mtindo wake wa biashara. 

  Nadharia ya Absolute Living (Kuishi kikamilifu) inaakisi juhudi za QNET za kukuza mwendendo wa kujali afya, mtindo wa maisha wenye uwiano sahihi, ikiwa inatilia mkazo katika Afya, ustawi na elimu. 

  Mgeni rasmi katika hfla hiyo, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda alisema ‘Maisha yangu ni mfano wa kufanya kazi kwa bidi na kujiamini katika kitu chochote unachokifanya. Hii ndiyo njia pekee yakuleta mabadiliko na maendeleo kwa mtu, familia na jamii”. 

  Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari Meneja Mkuu wa QNET kwa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, Biram Fall alisema kwamba, “Tunatoa aina mbalimbali za bidhaa za kiwango cha juu na huduma kwa wateja wetu kuwasaidia waweze kuishi maisha yenye uwiano sahihi, na pia kutatua tatizo la msingi kama vile elimu, ufahamu, na maendeleo binafsi kupitia program za mafunzo yetu, ambayo yanawasaidia katika safari yao ya kujiajiri mwenyewe. 
   
  Kutoka katika kozi za elimu kwa njia ya mtandao kama vile SELI/qLearn, mpaka katika vifurushi vya sikukuu kama vile Tripsavr, mpaka bidhaa za kuongeza nguvu kama vile Bio Disc3, virutubisho kama EDGE, na saa za mkononi kama Bernhard H. Mayer, QNET ina aina mbalimbali za kukidhi mahitaji mbalimbali ya watu. Katika kitovu cha yote haya, ni hamu yetu ya kutoa fursa ya Kuishi Kikamilifu “Absolute Living”

  Zaidi ya watu elfu mbili walipata fursa ya kuona bidhaa za mfano katika onyesho hilo na kufundishwa namna ya matumizi ya bidhaa na faida zake kwa wateja na watumizji wa mwisho. Kwa kuongezea, wataalamu wa bidhaa na biashara walikuwepo kwaajili ya kujibu swali lolote kutoka kwa wageni ili kuelewa vizuri ulimwengu wa QNET.

  Maonyesho ya Dar es salaam yanafuata mfululizo wa maonyesho kama hayo yaliyofanikiwa nchini Togo, Guinea, Ivory Coast, Senegali, Burkina Faso na Cameroon mwaka jana.

  Msafara wa maonyesho utasisimama katika mji wa Kumasi, Ghana, baada ya Dar es salaam kuanzia tarehe 23 mpaka 24 Machi mwaka 2019.

  0 0

  Mtoa hudua katika wiki ya Maji Duniani toka Mamlaka ya majiSafi na MajiTaka (DAWASA) Tumaini Samwel akitoa elimu kwa mmoja ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam aliyejitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimishpo ya wiki ya Maji Dunia iliyoanza leo Machi 16- 22, 2019 ambapo wananchi wanajitokeza kutoa matatizo yao pamoja na kupewa elimu juu ya matumizi sahihi ya maji na utunzaji wa vyanzo vya maji.
  Watoa huduma katika wiki ya maji Clementina Mbogellah (Kushoto) na Neema Mbalamwezi wakitoa elimu kwa mmoja ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam aliyejitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja katika kuadhimisha wiki ya Maji Dunia iliyoanza Machi 16- 22, 2019.
  Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa DAWASA, Evelasting Lyaro akitoa elimu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji Duniani inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
  Burudani za amsha amsha wiki ya maji Duniani zikiendelea katika mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam.
   Afisa Mwasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi akitoa elimu na vipeperushi wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji Duniani inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
  Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka imeandaa utaratibu wa kusikiliza kero za maji kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Maji Dunia iliyoanza jijini Dar es Salaam. DAWASA wameandaa dawati maalumu pamoja na wataalam ambao watatatua kero za wateja wa Maji kuanzia Machi 16- 22, 2019. Lengo ni kuwezesha wananchi kupata majibu ya kina ya changamoto mbali mbali zinazohusu huduma za majisafi na majitaka. Kauli mbiu: 'Hakuna atakayeachwa: Kuongeza kazi ya upatinaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira kwa wote katika dunia inayobadilika kitabia nchi,"

  0 0


   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka akimkabidhi zawadi ya Saa yenye picha yake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan (Kulia) katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.Picha Zote na Elisa Shunda

  MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AWAONGOZA WANAWAKE WA UWT TANZANIA KATIKA KONGAMANO LA KUMPONGEZA RAIS DK.SHEIN KWA KUTIMIZA MIAKA MITATU YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM YA MWAKA 2015/2018 MJINI UNGUJA.

   Pwani Kucheleeeeeeeeeee

    Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka akiongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan (Kulia) katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

    Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

   Viongozi Wakiongozwa na Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan (katikati) wakiimba wimbo wa taifa katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.


   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka akijadiliana jambo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan (Kulia) katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

   Mwenyekiti wa Uwt Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi (wa pili kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu Uwt Taifa,Mwalimu Queen Mlozi (wa tatu kutoka kushoto) katika kongamano hilo.

    Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

   Viongozi Mbalimbali wa Serikali Mawaziri,Manaibu Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Wakurugenzi toka Sekta Mbalimbali wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

    Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

    Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

    Mwenyekiti wa Uwt Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi (katikati) na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Uwt Wilaya ya Kibaha Mjini,Mwalimu Joyce Francis (kushoto) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Dk.Gaudentia Kabaka (aliyekaa chini)  katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

    Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

   Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

  Mwenyekiti wa Uwt Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka (kulia) akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana. Kulia ni Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan.

   Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akijadiliana Jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Abdallah Juma Mabodi (katikati) na Katibu Mkuu wa Uwt Taifa,Mwalimu Queen Mlozi (Kulia) wakati wa Kongamano hilo likiendelea.

   Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume, Mama Fatuma Karume akitafakari jambo wakati wa Kongamano hilo likiendelea kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar jana.

    Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Taifa,Dk.Gauedentia Kabaka.

   Katibu Mkuu wa UWT Taifa,Mwalimu Queen Mlozi akizungumza katika Kongamano hilo.

  Naibu Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Subira Mgalu,akisalimiana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ushirikiano uliopo kati ya Shirika la Umeme la Tanesco na Shirika la Umeme la Zanzibar katika kuhakikisha umeme unapatikana na Kuelezea wizaara hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika sekta ya Nishati nchini katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka.

   Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiagana na Mwenyekiti wa Uwt Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka (kulia) baada ya Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.  NA:ELISA SHUNDA,UNGUJA,ZANZIBAR.
  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
  amesema Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar Dk.Ali
  Mohamed Shein ameitendea haki ilani ya uchaguzi wa Chama Cha
  Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2015/2018 katika kipindi cha miaka mitatu
  aliyoongoza Zanzibar.

  Pia, amesema utendaji huo umejidhihirisha katika jitihada zake za
  kuendeleza na kuimarisha kwa ufanisi mkubwa azma ya machi 3 mwaka 1965
  ya Rais wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hayati Abeid
  Aman Karume ya kutoa huduma za matibabu bure kwa wananchi.

  Kauli hiyo ameitoa jana katika kongamano la wanawake la kumpongeza
  Rais Dk.Ali Mohamed Shein kwa kutimiza miaka mitatu ya utekelezaji wa
  ilani ya uchaguzi ya CCM iliofanyika mjini Unguja liloandaliwa na
  Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) ya Chama cha CCM.

  Makamu huyo wa Rais alisema katika uongozi wa Rais Dk.Shein
  ametekeleza zaidi katika azma hiyo kwa kuhakikisha anaongeza bajeti ya
  dawa kwa kila mwaka ambapo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ametenga
  sh.bilioni 12.7 huku akiongeza watumishi wa afya pamoja na upatikanaji
  wa vifaa tiba vya kisasa.

  "Huduma hizi zimeendelea kuboreshwa zaidi hususan kwa wazee nampongeza
  kwa hatua ya kuwapatia vitambulishi 2,314 wazee kwa lengo la kuwapatia
  pensheni ili kuhakikisha wanapata huduma za matibabu bure,"alisema
  Makamau huyo wa Rais

  Katika maelezo yake Samia alisema wanzanzibar ni mashahidia wa namna
  utekelezaji wa ilani ambao Dk.Shein ameufanya kwa kiwango cha juu
  ambapo shule za maandalizi zimeongezeka kwa mara 272 baada ya kipindi
  cha mapinduzi.

  Alisema kwa upande wa shule za msingi zimeongezeka mara 7 huku kwa
  sekondari zikiongezeka kwa mara 67 na kwamba katika kipindi cha miaka
  mitatu mbali na kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo
  madarasa,maabara na matundu ya vyoo.

  "Pia Rais Dk.Shein amewaondolea wazazi na walezi mzigo wa kuchangia
  elimu ya msingi mwaka 2016 na ya sekondari mwaka 2018 na hatua hii
  itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza mahudhurio na kuondoa ujinga na
  kuongeza idadi ya watu walioelimika,"alisema

  Makamu huyo wa Rais alisema katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya
  CCM Dk.Shein ameendelea kuwajali watu wa iana zote bila ya ubaguzi
  ambapo wazee ambao wamefikisha miaka 70 na kuendelea wanapewa fedha za
  kujikimu ya sh.20,000 kwa kila mwezi.

  "Kwa upande wa sekta ya uvuvi ambayo bado hatujaitumia ipasavyo kwa
  dhati jitihada za kutengeneza meli mbili ambazo zitakuwa na uwezo wa
  kuhifadhi tani 86 za samaki kwa kipindi cha wiki mbili wakiwa baharini
  pamoja na mapitio ya sheria ya vyama vya ushirika na uandaaji wa mfumo
  wa kietroniki wa kukusanya,kuchambua na kutoa takwimu za vyama vya
  ushirika vitaleta matokeo chanya,"alisema Makamu huyo wa Rais

  Samia aliongeza kuwa anampongeza Rais Dk.Shein kuendelea na jitihada
  zake za kutoa ruzuku kwa wakulima hususan kwa zao la mpunga na kwamba
  zimeongeza uzalishaji na kuongeza kipato kwa wananchi na mapato kwa
  serikali ya SMZ.

  "Pia nampongeza kwa kuendeleea kuhakikisha kuwa zao letu la karafuu
  linasimamiwa vizuri na wananchi wanafaidika na kilimo hichi na wazo la
  kuanzisha Taasisi ya utafiti wa mifugo na kwamba wazo hili limekuja
  kwa wakati kipindi ambacho tayari kiwanda kikubwa cha kuzalisha maziwa
  kimeshafunguliwa Zanzibar,"alisema

  Makamu huyo wa Rais aliongeza kuwa Dk.Shein ameendelea kutendea haki
  katika utekelezaji wa ilani kwa upande wa ujenzi wa viwanja vya ndege
  ambapo ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa Abeid Karume mjini Unguja
  unaendelea kutekelezwa na uwanja wa ndege wa Pemba unatarajia kuanza
  ujenzi wake hivi karibuni.

  Hata hivyo, Samia aliwataka wanawake visiwani humu kuchukua jukumu la
  kuzisemea na kuzitangaza kwa sauti kazi kubwa nzuri zinazofanywa na
  viongozi wa serikali mbili ili wananchi wazijue na wasipotoshwe.

  Kwa upande wa Mwenyekiti Taifa wa Jumuiya ya Umoja wa
  Wanawake(UWT),Gaudencia Kabaka alisema katika kipindi cha hivi
  karibuni jumuiya hiyo imefanya ziara kwa upande wa Unguja na Pemba kwa
  ajili ya kuelezea namna CCM ilivyotekeleza ilani yake.

  Alisema kwa asilimia kubwa CCM imetekeleza ilani yake visiwani humu
  ambapo hali hiyo inatokana na ushirikiano mkubwa na wa karibu uliopo
  kati ya serikali ya SMZ na CCM.

  "Nimejifunza mambo mengi hasa nilipofika kwenye ziara zangu ikiwemo
  ushirikiano mkubwa ulioko kati ya Serikali ya SMZ na chama na kwamba
  kila tulipoenda tulikutana na watendaji wa serikali ambao ndio
  watekelezaji wa ilani huku wakitueleza mambo yalivyotekelezwa,"alisema

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UWT,Queen Mlozi alisema jumuiya hiyo
  itaendelea kushirikiana na viongozi wa CCM ambao kwa kiasi kikubwa
  wameendelea kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi wa CCM.

  Alisema kupitia viongozi hao wameendelea kuwapatia wanawake nafasi
  mbalimbali za uongozi ikiwemo nafasi za Uwakilishi,Ubunge na katika
  ngazi za serikali za SMZ na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
  Tanzania.

  "Kwa mfano Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi ni mwanamke na Naibu
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ni mwanamke nataka niseme na
  hiyo inatokana na kujitambua na kujiamini kwetu hivyo tupo bega kwa
  bega kuhakikisha CCM inaendelea kuongoza kwa upande wa Zanzibar na
  Tanzania,"alisema


  Akizungumza kwa niaba ya Uwt Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi,alimpongeza Rais Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM katika miaka 3 tokea 2015 hadi 2018 kupitia mawaziri wake waliowasilisha maelezo ya utendaji kutoka kwenye wizara zao na amemshukuru katibu mkuu wa Uwt Taifa,Queen Mlozi kwa mwaliko na amewakumbusha viongozi wenzake ngazi ya mkoa na wilaya kuandaa makongamano katika ngazi zao kuisemea serikali yao kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.  0 0


   Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alie mbele akikagua na kutoa maelekezo kwa Meja Atupele Mwamfupe Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini kulia kwa Meja ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu  wa Wizara ya Madini Issa Nchasi kabla ya kuwasili kwa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini
  IMG_20190316_143451_8
  Meneja wa Kanda ya Ujenzi SUMA JKT, Meja Atupele Mwamfup akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa kituo na kutafsiri michoro mbalimbali ya jengo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa Nchasi, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Makamu Mwenyekiti Mhe. Mriam Mzuzuri na wajumbe wengine.
  IMG_20190316_143702_4
  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akitoa maelezo ya ujenzi wa kituo cha umahiri songea kwa Makamu Mwenyekiti wa kamati Mhe. Mariam Mzuzuri kushoto kwake. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa Nchasi na Meja Atupele Mwamfupe Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini.
  IMG_20190316_145341_9
  Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mariam Mzuzuri akimueleza jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wa kulia kwake mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha umairi.
  …………………….
  Na Issa Mtuwa Songea.

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri amesema kamati yake inaipongeza na itaendelea kuiunga mkono Wizara ya Madini kwa kazi nzuri wanayoifanya.

  Akiongea na waandishi wa habari mbele ya kamati yake Machi 13, 2019 mjini songea baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha umahiri (Centre of excellence) kwa mkoa wa ruvuma, Mzuzuri amesema kamati yake inaridhishwa na kazi za Wizara ya Madini na wataendelea kuiunga mkono (support) hasa swala la wachimbaji wadogo.

  “Tunawapongeza sana Wizara ya Madini, mnafanya kazi nzuri na sisi kama kamati niseme tutaendelea kuwaunga mkono (support) hasa hili la wachimbaji wadogo” alisema Mzuzuri.

  Naibu Wziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo ameiambia kamati kuwa wizara yake imejipanga katika kukamilisha ujenzi wa vituo vyote vya umairi kikiwemo cha Songea kwa kuzingatia ubora. Amesema ujenzi wa vituo vyote unakwenda vizuri, hata hivyo kituo cha songea kilichelewa ujenzi wake tofauti na vituo vingine kwa sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa kokoto tatizo ambalo lilisha tatuliwa na kwa sasa ujenzi unaendelea kwa kasi.

  “Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekusudia kukamilisha ujenzi wa kituo hiki na vingine kwa wakati na kama nilivyo tangulia kusema zile changamoto zimesha tatuliwa na tuaendelea vizuri. Naishukuru kamati yako kwa kutuunga mkono na ushauri wote uliotolewa tutauzingatia.” Alisema Nyongo.

  Nae Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma Prof. Riziki Shemdoe akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo amewambia wajumbe wa kamati kuwa ni kweli kuna kipindi mkoa wa Ruvuma ulikumbwa na changamoto za upatikanaji wa kokoto na miradi mingi ya serikali ilisimama kutokana na kuwa na kampuni moja tu ya uzalishaji wa kokoto mkoa nzima, mara baada ya mitambo yake kuharibika na uzalishaji kusimama upatikanaji wa kokoto ulikuwa ni tatiizo.

  Kituo cha Umahiri Songea ni miongoni mwa vituo mbalimbali vinavyo jengwa hapa nchini katika maeneo mbalimbali kama vile, kituo cha Bukoba, Simiyu, Tanga, Chuya kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo kujifunza na kupata uelewa wa masuala mbalimbali madini.

  0 0


  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipowasili katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali.Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akifafanua hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa kikao katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali. Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima akifafanua hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa kikao katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya Ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali. Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Shamsi Vuai Nahodha akiuliza swali wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Chuo cha Polisi Kidatu, lengo ikiwa ni kukagua na kutoa ushauri kwa miradi inayotekelezwa na serikali. Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Richard Marika, akifafanua hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa kikao katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali.Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Serikali imetenga jumla ya Shilingi Trilioni 1 .27 kwa ajili ya ukarabati wa Vyuo vitano vya Polisi nchini katika bajeti ya mwaka 2018/2019 gharama hiyo ikijumuisha ukarabati wa majengo ya ofisi, mabweni, makazi ya wakufunzi na maeneo mengine yaliyoanza kuchakaa.

  Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyotembelea Chuo cha Polisi Kidatu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhnadisi Hamad Masauni alisema hali ya miundombinu ya majengo kwa vyuo vyote ni chakavu,nia ya Serikali na Jeshi la Polisi ni kukarabati majengo hayo ili yaweze kukidhi mahitaji.

  “Tuna vyuo vitano vya polisi nchini;Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Dar es Salaam,Shule ya Polisi Moshi, Chuo cha Polisi Zanzibar, Chuo cha Maafisa Kidatu na Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza hivi vyote vinahitaji ukarabati na tumetenga jumla ya Shilingi Trilioni 1.2 kwa ajili ya ukarabati huo na tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli ameshatoa milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo kimojawapo kati ya hivyo nilivyovitaja” alisema Masauni

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho wajumbe wa kamati hiyo ya bunge waliitaka serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kusimamia mafunzo yanayotolewa vyuoni humo ikiwemo suala la wapelelezi kubambikia kesi wananchi ikiwa ni kinyume na wanchofundishwa vyuoni huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mussa Azzan Zungu akiitaka serikali kuwachukulia hatua askari polisi wachache wanaolichafua jeshi na kuivunjia heshima nchi kwa matendo yao ambayo yako kinyume na maadili.

  “suala la kubambikiwa kesi lipo , natoa wito kwa serikali kuwachukulia hatua askari dhidi ya tuhuma hizo ambao ni wachache wanakiuka taratibu na ueledi katika shughuli zao za kuhudumia wananchi” alisema Zungu.

  0 0

  Mkurugenzi wa Halmashaur ya Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi(katikati) akiwa na Afisa wa Bonde la Pangani , Segule Segule (Kushoto) kwa pamoja wakishiriki zoezi la kufanya usafi katika soko la Mbuyuni ikiwa ni uzinduzi rasmi ya wiki ya Maji .
  Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi,Bonde la Maji la Pangani,Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakishiriki katika zoezi hilo lililofanyika katika masoko ya Manyema na Mbuyuni.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Michae Mwandezi akifagia katika neo la soko la Mbuyuni.
  Afisa wa Maji ,Bonde la Pangani,Segule Segule akifanya usafi katika soko la Mbuyuni .
  Afisa wa Maji ,Bonde la Pangani ambao ndio waratibu wa Wiki ya Maji kwa mkoa wa Kilimanjaro ,Segule Segule akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi la usafi katika masoko ya Mbuyuni na Manyema.
  Baadhi ya  watumishi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi,Bonde la Maji la Pangani,Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) walioshirki katika zoezi la usafi kwenye masoko hayo.
  Biashara zikiendelea katika soko la Mbuyuni mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Michael Mwandezi pamoja na Afisa wa Maji ,Bonde la Pangani Segule Segule wamewaongoza watumishi kutoka Halmashauri,Bonde la Pangani na Mamlaka ya Maji mjini Moshi (MUWSA) kufanya usafi katika masoko ya Mbuyuni na Manyema.

  Zoezi hilo lililoanza majira ya saa 12:00 za asubuhi na kudumu kwa saa sita limefanyika ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi Wiki ya Maji Duniani ambayo hufanyika kila mwaka na kuadhimishwa  katika maneo mbalimbali nchini.

  Tofauti na miaka iliyopita ,mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro kupitia Ofisi za Bonde la Maji la Pangani ambao ndi waratibu kwa mwaka huu wameanza katika eneo la Mazingira ambalo pia ni sehemu ya kazi zinazotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira  na Ofisi za Bonde
  kwa kushirikiana na ofisi za Halmashauri.

  Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi katika masoko ya Mbuyuni na Manyema ,Ofisa wa Bonde la Maji,Pangani Segule Segule alisema wamechaguliwa kama taasisi itayoongoza maadhimisho ya wiki ya Maji na kwa kuanza limefanyika zoezi la usafi na baadae matukio mengine yatafuata.

  kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi alisema manispaa ya Moshi imekua yenye bahati kutokana na uwepo wa vyanzo vya maji vinavyotosheleza mahitaji ya mji wa Moshi.

  "Mwishoni mwa mwaka jana manispaa ya Moshi ilipata ushindi sio kwa Tanzania pekee bali kwa nchi za Afrika MAshariki kuwa ni manispaa inayotoa maji ya kutosha safi na salama,sisi tunabaraka hiyo lazima tumshukuru Mungu"alisema Mwandezi.

  Alisema kama ishara ya kuadhimisha wiki ya maji Duniani wameanza kwa kufanya usafi katika masoko na kwamba hali hii ndiyo imekuwa ikiuweka mji wa Moshi kwenye ramani ya miji misafi Afrika.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wapili kulia) akitoa maelekezo kwa uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kuweka alama za mipaka madhubuti badala ya Mawe katika mipaka ya maeneo ya Chuo hicho, alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana kwa lengo la kutambua mipaka ya Chuo hicho pamoja na kuzungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo hicho,wakwanza kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya BW.Richard Mganga.

  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wapili kushoto) akifanya ziara ya kukagua mazingira ya hostel za wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana,watatu kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga na watatu kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Orest Mushi.  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wapili kulia) akiwa anatoka kukagua mazingira ya choo katika moja ya hosteli za Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana, anayeongoza kutoka ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga.


  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wakwanza kulia) akikagua mipaka ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo Jijini Mwanza alipofanya ziara ya kikazi Chuoni hapo jana, katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo jijini Mwanza (hawapo pichani) jana alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho,wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga,na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Orest Mushi.
  Mhasibu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw.Mustapha Majura akimwomba Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (hayupo pichani) kupatiwa nafasi ya kusoma kozi fupi kwa mwaka ujao wa fedha za masuala ya uhasibu kufuatia mifumo utendaji wa kazi za uhasibu sasa kubadilika na kuwa za kieletroniki wakati wa kikao cha Wafanyakazi wa chuo hicho na Katibu Mkuu huyo jana alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.

  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (aliyeketi wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo Jijini Mwanza mara baada ya kumaliza kikao na Wafanyakazi hao jana alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo hicho kilichopo jijini Mwanza,aliyeketi( wa tatu kushoto ) ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw.Richard Mganga na (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw.Orest Mushi kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana.

  ……………………………

  Anitha Jonas – WHUSM ,Mwanza

  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ameutaka uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kupanda miti ya mbao kwa maeneo ya wazi ya chuo hicho badala ya kuacha ardhi hiyo bila matumizi rasmi.

  Katibu Mkuu Mlawi ametoa agizo hilo jana alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Mkoani Mwanza kwa lengo la kuzungumza na uongozi na wafanyakazi wa chuo hicho mambo mbalimbali ikiwemo kuweka mikakati ya kuboresha chuo hicho pamoja na kujua mipaka ya chuo hicho.

  “Chuo hichi kina eneo kubwa sana ekari 161 ni nyingi na eneo hili lote haliwezi kuendelezwa sasa hivi hivyo ni vyema mkapanda miti ya mbao itakayo wasaidia kuongeza kipato cha chuo na kupata rasilimali fedha itakayo wasaidia kufanya maendeleo katika chuo hichi wasalianeni na Wakala wa Misitu Tanzania watawashauri aina ya miti inayofaa kwa ardhi hii,”alisema Bibi.Mlawi.

  Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo ameusistiza uongozi wa Chuo hicho kufanya vikao na wafanyakazi wake pamoja na wanafunzi wa chuo hicho mara kwa mara ilikuweza kusikiliza kero zao na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali,pia amewasihi watumishi hao kuzingatia maadili ya utumishi wa umma pamoja na kuwa na nidhamu kazini.

  Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Richard Mganga hicho alieleza kuwa Chuo hicho kimekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madai mbalimbali ya watumishi ,uhitaji wa kuchimba kisima cha maji ilikuweza kuwa na maji ya kutosha kufuatia ongezeko la wanafunzi wa Chuo hicho.

  “Udahili wa Wanafunzi kwa Mwaka huu umeongezeka na kufikia 261 na hivyo kulingana na miundo mbinu tuliyokuwa nayo awali kuwa na uwezo mdogo tumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ya kutosha,hivyo tunaomba tusaidiwe kupata fedha za kuchimba kisima cha maji mapema ili kuondokana na kero hii,”alisema Mganga.

  Hata hivyo Mkuu huyo wa Chuo alitoa wito kwa watu kujitokeza kujakusoma Kozi mbalimbali za Michezo kwani Chuo hicho kinafundisha Diploma ya Uongozi na Utawala katika Michezo,Diploma ya Elimu ya Michezo pamoja na Diploma ya Ufundishaji Michezo

  Pamoja na hayo nae Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Orest Mushi aliwatoa hofu watumishi wa Chuo hicho waliyokuwa na madeni ya malipo ya stahili mbalimbali kuwa hivi karibuni malipo hayo ya madeni yatafanyika kwa hazina wanatoa fedha hizo.

  Vilevile nae Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Steven Dalasia aliusistiza uongozi huo kuandaa mpango wa manunuzi kwa bajeti ya 2019/2020 ili kupunguza hoja wakati wa ukaguzi wa mahesabu.

  Halikadahali nae Mkufunzi wa Chuo hicho Bw.Omari Mataka aliupongeza uongozi wa wizara kwa kufanya ziara chuo hapo pamoja na kuwasililiza kero zao na kutoa majibu ya hoja zao mbalimbali

  0 0   Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (wapili kulia) akiwa ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu, mjini Morogoro, wakati alipokuwa anafanya ukaguzi na kupima kilevi kwa madereva wa mabasi kituoni hapo pamoja na wa malori katika barabara ya Morogoro-Dodoma. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa.
  B
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kulia) akiangalia zoezi la upimaji wa kilevi kwa dereva wa basi la Kimbinyiko, Omary Sauli (katikati). Dereva huyo hakuwa na kilevi chochote na aliruhusiwa aendelee na safari yake
  C
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akiwauliza maswali abiria wa basi la Kimbinyiko kuhusiana na mwendokasi wa dereva wa basi hilo, na pia kuwapa elimu kuhusiana na kujua haki zao wanapokuwa safarini. Abiria hao walimweleza Waziri huyo dereva huyo yupo makini na pia walimshukuru kwa kufanya ukaguzi kwa mabasi mbalimbali nchini.
  D
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akitoka ndani ya basi la Kimbinyiko kufanya ukaguzi na kuzungumza na abiria wa basi hilo, mjini Morogoro, leo. Abiria hao walimweleza Waziri huyo dereva huyo wa basi hilo yupo makini na pia walimshukuru kwa kufanya ukaguzi kwa mabasi mbalimbali nchini.
  E
  1. Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na madereva wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu, Mjini Morogoro, leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kituo hapo kwa ajili ya kukagua na kupima kilevi kwa madereva wa mabasi kituoni hapo. Pia Lugola aliwapima madereva wa malori barabara kuu ya Morogoro Dodoma. Wapili kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  …………………………..
  Na Felix Mwagara, MOHA, Morogoro.
  WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amefanya operesheni kubwa ya kukagua na kupima ulevi wa pombe kwa madeveva wa mabasi na malori mjini Morogoro, leo.
  Lugola pia alizungumza na abiria wa mabasi hayo, pamoja na viongozi wa madereva waliopo stendi kuu ya mabasi Msamvu, mjini humo, ambapo walimwelezea kero mbalimbali zinazowakabili.
  Ukaguzi wa mabasi na malori hayo ulifanyika barabara kuu itokayo Dodoma kuja Morogoro-Dar es Salaam ambapo Waziri huyo akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa huo (RPC), Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa huo (RTO), alisimamisha vyombo hivyo vya moto vilivyokuwa vinaingia Mizani iliyopo eneo la Kihonda, nje kidogo ya Mji wa Morogoro.
  Akizungumza na madereva, kondakta, wapiga debe na abiria mara baada ya kufanya ukaguzi huo, Lugola alisema ni wajibu wake kufanya hivyo katika hatua ya kupunguza kwa kasi ajali mbalimbali zinatokana kwa uzembe wa madereva nchini.
  “Mimi ni Waziri wa vitendo, nikiagiza nataka nitekelezwe, na pia nikiahidi lazima nilifuatilie, niliwaambia nitakua nakuja kufanya ukaguzi muda wowote ambao hamuujui, na ninafanya hivi kwa lengo moja tu, kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinafuatwa ikiwa ni hatua ya kumaliza kupunguza au kumaliza kabisa ajali za barabarani hapa nchini,” alisema Lugola.
  Aliongeza kuwa, kwasasa ajali zimepungua nchini, hasa Mkoa wa Morogoro, kwasababu ya askari wa usalama barabarani kufanya kazi zao kiweledi, na pia madereva kufuata sheria za usalama barabarani.
  Lugola aliwataka madereva nchini, kuacha uendeshaji wa mashindano, kuwa na leseni na pia kuhakikisha wanapokuwa barabarani wanakua makini kwasababu ya kuwabeba abiria au mizigo mbalimbali wanayoisafirisha sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi.
  “Madereva wa mabasi na malori ambao nimefanikiwa kuwapima kilevi leo, ambao wasiopungua sita, sijawakuta na kilevi, wapo makini na hii inaleta nguvu na imani kuwa madereva wanaelewa na kuzingatia sheria za usalama barabarani, na pia ndani ya mabasi niliyokuwa nayakagua nimezungumza na abiria wakaniambia madereva wanaendesha vizuri na pia niliwakuta wamevaa mikanda, naamini safari yetu ya kuondoa ajali za barabarani tunazidi kufanikiwa,” alisema Lugola.
  Wakizungumza kwa wakati tofauti katika stendi kuu ya mabasi, madereva walilipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kwa usimamizi mzuri ambao umewaunganisha na kuwafanya waifurahie kazi wanayoifanya.
  Dereva Juma Rashidi wa basi linalosafiri kutoka Ifakara kuja Morogoro, alisema wanajisikia furaha kubwa kwa uongozi mpya wa Jeshi la Polisi ulioletwa Mkoani Morogoro hivi karibuni.  
  “Naomba niseme ukweli, RPC na RTO hakika wanatuongoza vizuri, hakuna kero za ajabu kama zamani, tupo huru kufanya kazi zetu, hii inaonyesha viongozi hawa wanataka tufanye kazi ili tuweze kupata riziki zetu kwa njia halali bila usumbufu wa kusumbuana kama ulivyokuwa siku za nyuma,” alisema Rashidi.
  Lugola alifanya ziara katika kituo hicho, na baadaye kutoka nje ya kituo hicho kuyakagua mabasi na malori, mara baada ya kumaliza ziara yake aliyoifanya Wilayani Kilosa ya kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa Tarafa ya Kimamba wilayani humo, juzi.

  0 0

  WazirI Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika kipande cha dhahabu mali Mchimbaji Mdogo Bw. Christopher Thadeo (kushoto) chenye uzito wa gramu 141.01 kikiwa na thamani ya sh. 13,537, 439/= wakati alipofungua Soko la Dhahabu mjini Geita, Machi 17, 2019. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (kulia) wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kufungua Soko la Dhahabu mjini Geita, Machi 17, 2017. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaji Said Kalidushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko baada ya kufungua Soko la Dhahabu mjini Geita, Machi 17, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita, Alhaji Said Kalidushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).  WAZIRI MKUU AWATAHADHARISHA WADAU WA MADINI

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa tahadhari kwa wadau wote wa madini kuwa atakayekamatwa anatorosha madini, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo utaifishaji wa madini atakayokuwa akiyatorosha. 

  Pia amewataka viongozi na watendaji wote wa Serikali wasimamie kwa weledi, uaminifu na uadilifu, sheria, kanuni na miongozo kuhusu sekta ya madini kwa lengo la kudhibiti utoroshwaji wa madini hususan dhahabu kwenda nje ya nchi.

  Waziri Mkuu ametoa tahadhari hiyo leo (Jumapili, Machi 17, 2019) wakati akifungua soko la madini la Mkoa wa Geita. Ufunguzi wa soko hilo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilotoa tarehe 22.01.2019 la kuitaka mikoa yote ianzishe masoko ya madini.

  Waziri Mkuu ameitakaWizara ya Madini, Tume ya Madini, Serikali ya Mkoa, Idara na Taasisi nyingine za Serikali zinazohusika na maendeleo ya sekta ya madini waheshimu mipaka ya majukumu yao ili waweze kulisimamia vizuri soko hilo na kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

  “Wizara ya Madini ishirikiane na vyama na mashirikisho ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuandaa mpango kazi mahsusi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya soko hili ili lisigeuke kuwa kikwazo kipya kwa wachimbaji na wafanyabishara wa madini”

  Waziri Mkuu ameviagizaVyombo vya Ulinzi na Usalama vihakishe soko hilo linapata ulinzi wa kutosha muda wote ili watendaji, mali zitakazokuwemo, vitendea kazi na miundombinu yote iwe salama muda wote. “Mkuu wa mkoa na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, nawaagiza hakikisheni Suala hili mnaliandalia utaratibu haraka iwezekanavyo”.

  Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuielekeza mikoa mingine yenye kiwango kikubwa cha uzalishaji wa madini hususan ya metali na vito iharakishe uanzishwaji wa masoko ya madini sanjari na miundombinu yote muhimu ili masoko hayo yaanze kufanya kazi kabla ya kwisha kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019.

  Amesema anaamini kwamba, usimamizi mzuri wa soko hilo na masoko mengine ya madini yanayoendelea kuanzishwa nchini utaimarisha makusanyo ya kodi za Serikali na kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la Taifa. Vilevile, amesema wafanyabiashara wa madini, hususan kutoka nje ya nchi wataongezeka kwa sababu tutakuwa tumewaepusha na matapeli na vikwazo vingine vya kibiashara. “Uimara wa soko hili pia, utaboresha uhusiano kati ya wadau wa biashara ya madini na Serikali”.

  Waziri Mkuu amesema Serikali imefuta baadhi ya tozo na kodi ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa madini hususan wachimbaji wadogo. Miongoni mwa tozo zilizofutwa ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Zuio ya asilimia tano ya mwisho (final withholding tax) inayotozwa kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote.

  Amesema baada ya kufutwa kwa kodi na tozo hizo Serikali inatarajia kuwa utoroshwaji wa madini utapungua, pia kutasaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa kupitia uanzishwaji wa masoko ya madini; kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato kwa nchi. 

  “Nitoe wito kwa wachimbaji wote wadogo kwamba endeleeni kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yenu kwa kufuata taratibu, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali”. AmesemaSerikali inachukua hatua zote hizo si kwa lengo jingine bali kuziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi, na hivyo, kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika maeneo mengi ya nchi yetu. 

  Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vema katika kuhakikisha vikwazo vyote vilivyomo katika mnyororo wa biashara ya madini vinaondolewa kwa lengo la kukuza sekta hiyo na kuwanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla. Amesema Serikali imeamua kutoa mwelekeo mpya katika usimamizi na maendeleo ya sekta ya madini. “Utekelezaji wa dhamira hii unakwenda sambamba na kuweka mazingira mazuri na miundombinu itakayowezesha kuimarika kwa sekta ya madini nchini”. 

  Kadhalika, Waziri Mkuu amesema wachimbaji wadogo wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa masoko ya uhakika ya madini ambao umekuwa sababu ya utoroshwaji madini, hivyo kuanzishwa kwa soko hili kunawahakikishia wachimbaji wadogo masoko na kukua kwa kipato kutokana na shughuli za madini.

  Waziri Mkuu amesema kwa muda mrefu sasa, kumekuwepo na malalamiko ya kudhulumiwa au kupunjwa kutoka kwa baadhi ya wachimbaji wadogo, vitendo hivyo vimekuwa vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu. “Ndugu wachimbaji wadogo, soko hili linakwenda kuwa mwarobaini wa tatizo hilo kwani litasheheni vifaa vya kupimia uzito na ubora wa madini kabla hayajauzwa. Naielekeza Tume ya Madini, isimamie ipasavyo vifaa na taratibu za vipimo kwenye soko hili na kuhakikisha hakuna manung’uniko juu ya utendaji kazi wa vifaa hivyo”. 

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa soko hilo pia litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati hawana. “Nawasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko hili kikamilifu ili kuepuka udanganyifu na matapeli”.

  Pia ameiagiza Tume ya Madini kuratibu bei za madini ndani ya soko hilo na ihakikishe mchimbaji anapata stahiki zake, Serikali inapata mapato yake na mfanyabiashara naye ananufaika. “Tunaimani kabisa tatizo la kudhulumiana na kupunjana linaenda kwisha kabisa. Na kwa kweli ikitokea mtu amepunjwa, atakuwa amejitakia mwenyewe”.

  “Ndani ya soko hili kutakuwa na huduma zote muhimu kwa mfanyabiashara ikiwemo huduma za Tume ya Madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mabenki na nyinginezo, hivyo kuokoa muda na gharama nyingine katika kuendesha biashara hii ya madini. 

  Amesema soko hilo litasaidia sana katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na takwimu za biashara ya madini. Hivyo, niwasihi wachimbaji wa madini kulitumia soko hili na kuacha vitendo vya utoroshaji wa madini. Serikali kwa upande wake, haitomvumilia mtu yeyote yule atakaye jihusisha na utoroshaji wa madini. 

  Ufunguzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Wabunge wa mkoa wa Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robertt Gabriel, wakuu wa mikoa jirani na maafisa wa Serikali.

older | 1 | .... | 1819 | 1820 | (Page 1821) | 1822 | 1823 | .... | 1898 | newer