Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1820 | 1821 | (Page 1822) | 1823 | 1824 | .... | 1897 | newer

  0 0

  WENYEVITI wa Vitongoji na Vijiji wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wametakiwa kutokwamisha shughuli za serikali kwa kutoa matamko yasiyo na tija kwenye machimbo ya madini.

  Ofisa madini mkazi wa mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima aliyasema hayo wakati akizungumza na wachimbaji wa madini ya Green kwenye machimbo ya Lemshuku Kata ya Komolo.

  Ntalima alisema wenyeviti hao wanapaswa kutambua kuwa Rais John Magufuli akishatoa maelekezo hawapaswi kuyakwamisha kwa kutoa kauli tofauti. Alisema baadhi ya wenyevi wanatoa maagizo yasiyo na tija ambayo yanakinzana na kauli ya Rais Magufuli ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini. 

  "Hili ni eneo la uchimbaji madini, Mwenyekiti wa kijiji au kitongoji hana mamlaka ya kutoa matamko ya kuwachangisha watu sh15,000 au kuwaagiza waendelee kwenye mkutano kilomita 18 kutoka hapa," alisema Ntalima. Alisema viongozi hao wanapaswa kushirikiana na ofisi ya madini endapo kuna jambo wanataka kulifanya kwenye maeneo ya madini yenye leseni kuliko kujiamulia wao wenyewe. 

  "Rais Magufuli amewapa unafuu wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwasamehe kodi sasa anapotokea mwenyekiti wa kijiji anawachangisha fedha lazima tuingilie kati," alisema Ntalima. 

  Mwenyekiti wa chama cha wachimba madini mkoa wa Manyara (Marema) Tawi la Lemshuku, Bernard Kasanu alisema wenyewe wana haki ya kuchimba na siyo kuwekewa vikwazo vya kisiasa visivyo na tija. Kasanu alisema wamekuwa wakipata vikwazo vingi kutoka kwa uongozi wa kijiji ikiwemo huduma ya maji ambayo hivi sasa imesimama. 

  Mchimbaji wa madini ya Green, Charles Shoo alisema viongozi wa wizara ya madini na kijiji wangekutana ili wapeane utaratibu wa suala hilo kwani wananchi wamebakia njia panda. Shoo alisema tatizo hilo ni la muda mrefu hivyo ni wakati muafaka wa kufanyiwa kazi ili lipatiwe ufumbuzi wa kudumu. 

  Hata hivyo, mmoja kati ya wachekechaji wa madini hayo Shedrack Ibrahim alisema viongozi wa vijiji na vitongoji wanapaswa kutoa kipaumbele kwenye huduma za kijamii kuliko kuwachangisha fedha bila utaratibu wowote. 

  Ibrahim alisema machimbo hayo hayana sehemu za kuwazikia wenzao wanapokufa hivyo wanaomba serikali iwatengee sehemu ya maziko machimboni. Mkoa wa kimadini wa Simanjiro unaongoza kwa kuwa na madini mengi katika mkoa wa Manyara, ikiwemo Tanzanite, Rubby na Green.
  Ofisa madini mkazi wa Mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima akikagua migodi ya madini ya Green kwenye machimbo ya Lemshuku Kata ya Komolo. 
  Maofisa wa Tume ya madini, wakikagua migodi ya madini ya Green kwenye machimbo ya Lemshuku Kata ya Komolo, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. 
  Ofisa madini mkazi wa Mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima akizungumza na wachimbaji madini ya Green kwenye machimbo ya Lemshuku Kata ya Komolo.

  0 0

  QNET Independent Representative, Eliah Medard Mrosso explaining to customers and visitors about QNET products and services on the second day of QNET Dar es Salaam Expo 2019.
  QNET Independent Representative Andrew Yusuf Gerald giving a testimony to crowds about his exceptional experience with QNET and its business on the second day of QNET Dar es Salaam Expo 2019. 
  QNET Independent Representative Erasmus Bahati Amani making a business presentation about QNET Products and business model to crowds on the second day of QNET Dar es Salaam Expo 2019.
  QNET Independent representatives, prospective customers, business partners and visitors at QNET Dar es Salaam Expo on the second day of the event.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha juu kitabu cha I Can, I Must, I Will kama ishara ya kuzindua toleo maalum kwa wasioona (kiatu cha nukta nundu) leo wakati wa hafla ya utoaji tuza ya I CAN pamoja na chakula cha mchana iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  7
  Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi Patterson (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni mbili za Kitanzania Bi. Rehema Said mshindi wa Tuzo ya I CAN ya Mafanikio katika Michezo iliyotolewa na  Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  9-2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsalimia Bi.Wakonta Kakunda (kulia) ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya I CAN ya Mafanikio katika Ujuzi wa Kipekee kwenye hafla ilioandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  14
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa sheria na Katiba Bw, Amon Mpanju katika hafla ya  Tuzo ya I CAN ya heshima inayoandaliwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyotolewa leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
  16-2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya I CAN ya heshima kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation Dkt. Reginald Mengi (kushoto) kwa kutambua mchango wake katika kusaidia watu wenye ulemavu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  25
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wageni waalikwa kwenye  Tuzo ya I CAN inayoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation Dkt. Reginald Mengi.
  2
  Sehemu ya Watu wenye Ulemavu waliohudhuria hafla ya utoaji tuza ya I CAN pamoja na chakula cha mchana iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  ………………………………………………………………………………….

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza watu wenye ulemavu kutumia fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi.

   Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye hafla ya utoaji tuzo ya I CAN kwa watu wenye ulemavu iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Foundation, iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

   “Serikali inapenda kuwahakikishia kuwa changamoto za walemavu zinafanyiwa kazi moja baada ya nyingine.”Alisema Makmu wa Rais. Aidha, Serikali imeendelea kuweka mifumo, taasisi mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha kuwa kuna miundombinu wezeshi ya elimu, afya na teknolojia ili watu wenye ulemavu kuajirika kwenye viwanda vyetu. “Nitoe rai kwa waajiri na wamiliki wa viwanda kote nchini kuhakikisha kuwa hawabagui wala kunyanyapaa walemavu katika kuijenga Tanzania ya Viwanda ambayo ni jumuishi kwa wote” alisisitiza Makamu wa Rais.

   Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua, inathamini na inapongeza jitihada za Dkt. Reginald Mengi pamoja na taasisi yake mpya ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation ambayo pamoja na mambo mengine inahimiza ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika ajira.

   Vilevile Makamu wa Rais aliwaambia wananchi waliohudhuria hafla hiyo kuwa Serikali imeweka mkazo maalum katika masuala ya elimu jumuishi ambapo watu wenye ulemavu watasoma vizuri kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.
   Kwa Upande mwingine Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amesema Tuzo za I CAN zimekuwa chachu sana kwa watu wenye ulemavu ambapo alimpongeza na kumshukuru Dkt. Reginald Mengi kwa moyo wake wa kipekee wa kutambua na kuwasaidia walemavu.

   Aidha, amesema Serikali ina mpango endelevu  wa kutoa elimu ya masuala ya ulemavu ikiwa pamoja na kuendelea kufanya jitihada za kuongeza wakalimani wa lugha za alama. Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe amesema sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 inatambua fursa na haki sawa katika kupata elimu hivyo Serikali inaendelea kuboresha miundombinu wezeshi kwa wote wenye mahitaji maalumu.

  0 0


  WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umewahimiza Watanzania kutunza misitu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho huku ikifafanua ni vema changamoto zilizopo zikatatuliwa kwa majadiliano na hatimaye misitu ibaki salama.

  Hayo yamesemwa na Meneja wa Rasilimali za Misitu Dkt. Masota Abel kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo baada ya kumalizika kwa kikao cha mazungumzo na majadilano kati ya maofisa wa TFS na ujumbe wa watu 15 kutoka nchini Ethiopia ambao wamekuja nchini Tanzania kujifunza namna nzuri ya utunzaji misitu.

  Raia hao wa Ethiopia wametoka katika taasisi mbalimbali zinazohusika na utunzaji misitu na tafiti katika nchi yao na wakiwa nchini wamepata fursa ya kwenda katika maeneo mbalimbali katika mikoa ya Tanga, Morogoro,Iringa na Dar es Salaam.

  Dkt.Masota amesema ni vema Watanzania wakahakikisha wanatunza misitu iliyopo nchini Tanzania na kufafanua wageni hao kutoka Ethiopia wamefurahishwa na namna TFS inavyotunza misitu, hivyo ametoa ombi kwa Watanzania kuwa sehemu ya kila mmoja kwa nafasi yake kuitunza kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho kwa maslahi mapana ya Taifa.

  "Ujumbe wangu kwa Watanzania watunze misitu.Tuitunze kwa kufuata taratibu zinazostahili na hata kama kunachangamoto nyingine tutumie nafasi za majadiliano kutafuta ufumbuzi na hatimaye ibaki salama. Tuache kuvamia misitu na kuikata, tuache kufanya shughuli za kilimo maeneo ya hifadhi na misitu kwa ujumla.

  "Tunapaswa kufahamu misitu tuliyonayo nchini ni keki ya Taifa na hivyo lazima tuitunze na ilete tija kwa ajili ya kizazi kilichopo sasa na kizazi kinachokuja. Kwetu TFS tutaendelea kuweka mikakati ya kuhakiksha misitu inabaki salama lakini wakati huo huo wananchi nao wanalojukumu kama hilo,"amesema Dk.Abel.

  Alipoulizwa changamoto kubwa ambayo TFS wanakabiliana nayo, amejibu ongezeko la watu ni moja ya changamoto kwani wengi wanakosa nishati mbadala ya miti ambayo itakidhi mahitaji kama nchi na kukosekana kwa nishati mbadala imesababisha misitu kuvamiwa na kuharibiwa.

  Pia ongezeko la watu limesababisha kuwe na mahitaji makubwa ya ardhi na hivyo wengi kuvamia maeneo ya misitu yaliyohifadhiwa. Mabadiliko ya tabianchi nayo yanachoche watu kuvamia misitu kwa lengo la kutafuta ardhi yenye rutuba kwa shughuli za kilimo.

  Alipoulizwa kwanini Waethiopia hao wameichagua Tanzania , Dk.Abel amesema kuwa nchi yetu inasifika kwa utunzaji wa mazingira na hivyo wameona ni sehemu sahihi ya kuja kujifunza kuhusu uhifadhi wa misitu .

  "Wageni wetu wamekiri na kukubali kazi nzuri ambayo inafanywa na Serikali yetu kupitia TFS katika kutunza misitu, wameeleza namna kile ambacho wamejifunza watakavyokwenda kwao kuweka mikakati itakayowawezesha kuitunza misitu yao.Ethiopa misitu yao imeendelea kuharibiwa .Tunaweza kusema hawana misitu tena.Kwao eneo kubwa limebaki kuwa jangwa, ndio maana wanasema hata asali yao wanafuga katika mabanda .Hivyo hata asali yetu inabaki kuwa bora na ya asili kuliko ya kwao,"amesema.

  Kuhusu ujumbe wa TFS kwa wageni hao waliotoka Ethiopia, Dkt.Abel amesema wanashauri waje kuwekeza nchini Tanzania kwani kuna maeneo mengi ya kuwekeza yakiwemo katika sekta ya misitu na viwanda.

  Kwa upande wa wageni hao wamesema Serikali ya Tanzania kupitia TFS wamefanya kazi kubwa na nzuri katika kuhakikisha misitu inatunzwa vizuri na kubwa zaidi ni namna ambavyo kuna utaratibu mzuri wa usimamizi.

  Akizungumza wakati akitoa shukrani kwa TFS na Serikali ya Tanzania kwa niaba ya wenzake Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti cha Central Ethiopia EV+ & Forest Wondnossen Tsadik amesema kikubwa ambacho wamejifunza ni namna ambavyo sekta ya misitu inavyoangaliwa kwa ukaribu zaidi.

  "Tumeona hapa misitu inasimamiwa na TFS ambayo iko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, hii inafanya kuwepo na ukaribu wa kufuatilia hatua kwa hatua kuhusu uhifahi.Kwetu sisi mambo ya misitu yamechangwa na mambo ya kilimo.Tunaipongeza Tanzania kwa namna ambavyo inasimamia misitu yake,"amesema.

  Pia amesema wakiwa katika maeneo mbalimbali ambayo wamekwenda wamepata nafasi ya kukutana na watalaam wa masuala ya misitu pamoja na watafiti wa kada mbalimbali ambapo wamebadilisha uzoefu na wanaamini kila mmoja atakuwa amejifunza kutoka kwa mwingine.

  Wakati huo huo Ofisa kutoka Idara ya Ununuzi wa mbegu ICRAF nchini Ethiopia Kedra Mohammed amesema pamoja na mambo mengine amejifunza ukarimu wa Watanzania na kuhusu ziara yao imekuwa ya mafanikio makubwa kwani kuna mengi wamejifunza.
   Meneja wa Rasilimali za Misitu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Dk.Masota Abel akifafanua jambo kwa Waethiopia ambao wamekuja nchini kujifunza utunzaji wa misitu na kubadilisha uzoefu,Aliyekaa ni Meneja wa Kituo cha Uzalishaji mbegu za miti-TFS cha Morogoro Dk.Hamza Katety
   Mkurugenzi wa Kituo cha Utafititi cha Central Ethiopia EV+& Forest Wondnossen Tsadik akizungumza wakati wa kikao cha majadiliano kati yao na TFS baada ya kumalizika kwa ziara waliyoifanya katika mikoa  ya Tanga,Morogoro,Iringa na Dar es Salaam
   Baadhi ya wageni waliotoka nchini Ethiopia kuja nchini Tanzania kujifunza kuhusu utunzaji misitu wakimsikiliza Meneja wa Rasilimali za Misitu kutoka TFS Dk.Masota Abel (hayupo pichani)
   Raia kutoka nchini Ethiopia wakifuatilia mazungumzo
   Sehemu wa ugeni wa watu 15 kutoka taasisi mbalimbali za uhifadhi misitu na tafiti wakifuatilia majadiliano katika Ofisi za TFS zilizopo jijini Dar es Salaam

  0 0

  0 0

  Na. Vero Ignatus, Arusha.

  Mamlaka ya Mapato nchini TRA imewataka wafanyabiashara wakubwa mkoani Arusha, kutumia teknolojia za kisasa kwa mtandao kwaajili ya kulipa kodi zao ili kuongeza uwazi na kutunza kumbukumbu zao. 

  Wito huo umetolewa na Kaimu Kamishna wa Idara ya walipakodi wakubwa wa TRA, Yeremiah Mbaghi katika warsha ya walipa kodi wakubwa juu ya mifumo ya kulipa kodi na sheria na kanuni mbali mbali za kodi ambazo zimepitishwa na serikali.

  Amesema kuwa Matumizi ya mtandao katika malipo ya kodi, yanarahisisha ulipaji wa kodi na yanapunguza gharama kwa wafanyabiashara hao kwenda ofisi ya TRA."TRA imefanya maboresho makubwa katika mfumo wake wa kulipa kodi kupitia mtandao na tumeongeza ufanisi katika utunzaji wa kumbukumbu za kodi ya zuio kwani sasa malipo yote ya kodi zuio hungia moja kwa moja kwenye akaunti ya mlipakodi husika"alisema

  Amewataka walipa kodi hao kuzingatia sheria ya fedha ya mwaka 2018 na maboresho ya kanuni, ikiwepo kuwasilisa taarifa za miamala baina yake na washirika kwa kamishna mkuu pale anapowasilisha ritani ya mapato kwa mwaka.

  Akifungua warsha hiyo, Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Mrisho, Gambo, amesema serikali mkoani Arusha, itaendelea ushirikiana na TRA na walipa kodi ili kuhakikisha mapato ya serikali yanaimarika.

  Amesema upatikanaji wa mapato yataiwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendelo ambapo serikali ya awamu ya tano imejikita katika kutekeleza miradi endelevu katika kutatua kero za wananchi,kubadili mfumo wa uchumi na kuwa wa kati kwa kukuza sekta ya viwanda.

  "kodi ambazo zinalipwa pia zinasaidia sana katika miradi ya huduma za kijamii, maji, barabara, umeme pembejeo na kupatikana huduma bora za afya"alisema.Hata hivyo, amesema kuwa serikali itaendelea kujenga mazingira bora ya biashara nchini, ili kuhakikisha wafanyabiashara wananufaika, serikali inapata kodi na wananchi wanapata mahitaji yao.

  Mfanyabiashara Peter Minja alipongeza TRA kuanza kuwatembelea na kutoa elimu juu ya sheria mpya zilizopitishwa na serikali lakini pia juu ya mifumo sahihi ya malipo ya kodi, ikiwepo kodi za mabango.

  0 0

  UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, umezindua kampeni ya ‘Dar es Salaam ya Kijani’ ikiwa na lengo la kurudisha mitaa na majimbo yaliyokwenda upinzani.

  Kampeni hiyo inalenga kuweka mikakati kwa kuanzia ngazi za jumuiya zote za mkoa huo, kuanza kujipanga kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

  Akizugumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema kuwa kampeni hiyo itachochea ustawi zaidi wa CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuzidi kukita mizizi katika ngazi zote kuanzia mkoa hadi majimbo, wilaya hadi kata, na matawi hadi mitaa.

  “Leo tunazindua kampeni yetu ya “Dar es Salaam ya Kijani kuelekea serikali za mitaa 2019”, kampeni kabambe kwa ajili ya kuirejeshea CCM mitaa iliyopotea katika uchaguzi uliopita ambayo kwayo itatusaidia kupata ushindi mkubwa kimkoa katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 wa udiwani, ubunge na urais.

  “Sote tu-mashuhuda kwamba katika uchaguzi uliopita wa 2014 wa Serikali za Mitaa na ule Mkuu wa 2015 tulipoteza baadhi ya mitaa, kata na majimbo yaliyokuwa yakishikiliwa na CCM.

  “Na sababu za kupoteza huko zinajulikana, sina haja ya kuzirejea sasa. Hivyo sisi vijana wa CCM tunatambua kuwa ndiyo damu na roho ya chama chetu, na kwamba tunao wajibu wa asili wa kusafisha njia katika kutimiza malengo ya uwepo wa vyama vya siasa kikatiba ya kushika dola,” amesema Kilakala

  Mwenyekiti huyo wa UVCCM, amesema kuwa CCM inahitaji ushindi mkubwa kwa kuweka mikakati ya awali kwa kuwahusisha wanachama wa chama hicho wa ngazi zote.

  “Kampeni yetu hii itashuka katika wilaya, kata na matawi yote katika Mkoa wetu ili kuwa na ufahamu wa pamoja na kuhakikisha kila Kijana wa UVCCM anawajibika ipasavyo kuhakikisha falsafa ya Dar es Salaam ya kijani yaani Dar es Salaam ya CCM inaenea kwa wanachama na wananchi ili ikifika wakati wa uchaguzi tuvune wapiga kura wa kutosha.

  “Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitatoa pongezi zangu za dhati kwa niaba ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Rais Dk. John Magufuli kwa kutuongoza vyema kupitia Serikali yetu ya CCM katika jukumu la kutatua changamoto za watanzania na kuwaletea maendeleo.

  “Tumejionea dhahiri shahiri namna yale yaliyochelewa yakiwahishwa, yaliyoshindikana yakiwezekana, magumu yakiwa mepesi, yaliyokwama yakikwamuliwa,”amesema Kilakala

  Kwa upande wake mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa UVCCM, Mwal. Raymond Mwangwala, amesema ameridhishwa na kasi kubwa inayofanywa na vijana wa Dar es Salaam ya kuhakikisha chama kinapata heshima katika chaguzi zote.

  “Leo ninachokiona hapa, hii ndiyo UVCCM ninayoijua na sina shaka na uongozi wa mkoa kwani unafanyakazi kubwa na nzuri, ninachoweza kusema kwenu ninawaomba sana vijana tukilinde chama na kuhakikisha tunapata ushindi katika chaguzi zote. “Na ikiwezekana si waachieni (upinzani) asimilia mbili tu ya mitaa na pindi ikibidi hata hakikisheni tunachukua asilimia yote 100. Vijana tushikamane na tulinde heshima ya chama chetu,” amesema Mwal. Mwangwala

  0 0

  Spika wa Bunge Job Ndugai na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele wakichukua mkasi tayari kwa uzinduzi.
  Spika wa Bunge Job Ndugai na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele wakiwa tayari wamekata utepe kuzindua ofisi za ATCL jijini Dodoma.
  Spika wa Bunge Job Ndugai (kushoto) akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele wakichukua mkasi tayari kwa uzinduzi.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele akisalimiana na mmoja wa wahudumu wa ofisi hiyo ya ATCL jijini Dodoma. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai.
  Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa ofisi za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) jijini Dodoma leo. Baada ya maboresho makubwa ndani ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege mpya za kisasa na kuongeza wigo wa safari zake, ATCL imeamua kufungua ofisi zake jijini humo badala ya kuendelea kutumia mawakala pekee.
  SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewataka wabunge, Maofisa wa Serikali, wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia huduma za ATCL popote zilipo ndani na nje ya nchi ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kufufua na kulijengea uwezo shirika hilo.

  Akifungua ofisi ya ATCL mkoani hapa, Ndugai alisema Watanzania wote kwa ujumla wao wakiwemo wanatakiwa kutumia huduma za ndege hizo ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kuinua usafiri wa shirika hilo ambalo asilimia 100 ni mali ya Tanzania.

  Alisema kwa kutumia usafiri ATCL wa ndani na nje ya nchi na katika nchi mbalimbali inakofika, ni uzalendo ambao hata mashirika ya ndege ya nje yanafanya hivyo, isipokuwa inapokuwa kuna sababu maalumu zinazochangia kutotumia usafiri huo.

  Ndugai alitoa rai kwa mawakala 300 wa shirika hilo waliosambaa ndani na nje ya nchi, kuzitangaza huduma nzuri na bora za ATCL popote zinapotolewa na kuzionesha kwamba ni za ubora wa hali ya juu na za daraja la juu. 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele akizungumza katika hafla hiyo na kuwataka watendaji wa shirika hilo kuendelea kupanua na kuboresha huduma za usafiri wa ndani na nje ili kushinda katika soko la usafiri wa anga katika maeneo hayo.

  Aliwatoa hofu Watanzania na akawataka waendelee kutumia huduma za ATCL kutokana na mkakati wa kutunza rekodi za usalama wa anga kwani huduma za shirika hizo ni za kiwango cha juu.
  Baadhi ya watumishi wa ATCL na wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo wa ofisi za ATCL jijini Dodoma.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Richard M. Mayongela akizungumzia huduma za ATCL katika viwanja mbalimbali nchini. 
  Mmiliki wa Kiwanda Mvinyo cha Alko Vintage cha jijini Dodoma, Archard Kato akionesha bidhaa za kiwanda chake ambazo zinapatikana katika Ndege za ATCL jambo ambalo linachangia ukuaji wa soko la zabibu jijini Dodoma.

  0 0  0 0

  Benki ya Exim mwishoni mwa wiki iliandaa chakula maalum kwa ajili ya wateja wake jijini Tanga ili kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika jiji hilo.
  Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, Naibu Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu alisema kupitia hafla hiyo  walilenga pia  kutoa fursa miongoni mwa wateja hao ili waweze kufahamiana na kufungua wigo wa kufanya biashara pamoja.
  “Pamoja na kushukuru kwa namna ambayo wateja wetu wamekuwa nasi hadi kufikia mafanikio ya kuikuaji na ubora wa huduma zetu, hafla hii inatoa fursa kwa wateja wetu pia kufahamiana wao kwa wao na hivyo kufungua milango ya fursa baina yao,’’ alisema Matundu.
  Alisema ukuaji wa benki hiyo unaoshuhudiwa kwasasa ni matokeo ya ushirikiano baina yake na wateja wake ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha imani kubwa kwa benki hiyo hali ambayo imekuwa ikiiwezesha benki hiyo kubuni huduma bora na rafiki za kibenki ili kulinda na kurejesha imani hiyo kwa wateja wa benki hiyo.
  Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997 benki hiyo imezidi kujitanua ndani na nje ya nchi ambapo hivi karibuni ilionesha nia na utayari wa kuinunua  rasmi benki ya UBL Tanzania Limited (UBTL) kwa asilimia 100 baada ya kusainishana barua ya kuonesha nia (Letter of Intent).
  “Kwa muda wote wa uwepo wake ndani na nje ya nchi benki ya Exim imekuwa ikijipambanua kwa ubora wa huduma ikilenga kujenga thamani ya uwekezaji kwa wadau wake  na kufikia ukuaji wake kwa kutoa huduma kwa upekee na iliyoboreshwa. Haya yote yamekuwa yakifanikiwa kwa urahisi sababu utekelezaji wake umekuwa ni jumuishi kwa kuwa unahusisha wadau wote kwa majadiliano na wateja wetu kama hivi,’’ alisema.
   Pamoja na mambo mengine hafla hiyo ilipambwa na shuhuda mbalimbali kuhusu ubora wa huduma za benki hiyo kutoka kwa wateja mbalimbali wa benki hiyo.
  Meneja Uendeshaji wa Benki ya Exim Bi Doreen Mcharo (katikati)  akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo  wakati wa tafrija ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki yaExim  kwa ajili ya wateja wake wa jiji la Tanga  iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.

  Naibu Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani)  wakati wa tafrija ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki yaExim  kwa ajili ya wateja wake wa jiji la Tanga  iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
  Mmoja wa wateja wa benki ya Exim Tanzania jijini Tanga Bi Anna Saimo akizungumza kwenye hafla hiyo.
  Mmoja wa wateja wa benki ya Exim Tanzania jijini Tanga Bw Sifaeli Mafunga  akizungumza kwenye hafla hiyo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa banki  ya Exim tawi la Tanga pamoja na Naibu Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu, kwenye picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.

  0 0

  *Asema yeye na wenzake wameutua mzigo wa CUF na wala hawana habari tena

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  HATIMAYE Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF) Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na viongozi wenzake wametangaza rasmi kuondoka Chama hicho na kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo leo Machi 18,2019.

  Ametangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema baada ya kutafakari kwa kina wameona wanayo nafasi ya kuendelea na mapambano ya kisiasa na hivyo wamejiunga ACT-Wazalendo kuendeleza mapambano hayo.

  Uamuzi wa Maalim Seif na wenzake umekuja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo asubuhi kutoa uamuzi wa kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF.

  "Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa uamuzi wa kesi 23 ya mwaka 2016 ambayo tuliifungua kupinga uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kuingia maamuzi ya Chama ya kutomtambua Lipumba.

  "Kwa mujibu wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni kwamba Msajili kumtambua Profesa Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF.Tunajua sababu za kutolewa kwa uamuzi huo ni kuihujumu CUF pamoja na demokrasia nchini.Mahakama ilichelewa kutoa uamuzi kwasababu ya kutoa nafasi kwa Lipumba kusajili Bodi ya Wadhamini,"amesema.

  Akifafanua zaidi Maalim Seif anasema wanahamia ACT wakiamini umma wa Watanzania haujawahi kushindwa mahali popote na kusisitiza wana-CUF wote na wananchi kuwaunga mkono na sasa ni wakati wa shusha Tanga pandisha Tanga.

  Ametumia nafasi hiyo kueleza kuna watu walijitolea nyumba zao kwa ajili ya Ofisi za CUF na ombi lake kwao waendelee na moyo huo huo kwa kuzifanya nyumba hizo kuwa ofisi za ACT-Wazalendo na safari inaendelea.

  Pia amesema kitendo cha wao kuhama katika Chama ambacho wamepambana kukijenga inakwenda kuandika historia mpya kuelekea Tanzania mpya ambayo itasimamia haki kwa Watanzania wote na kwamba huko wanakokwenda wanakwenda wakiwa wanachama wa kawaida.

  Ameongeza mzigo wa CUF kwa sasa wameutua na hawana habari tena na Chama hicho , kwani wao wameshamalizana nao na ni mwendo wa kusonga mbele na Watanzania wafahamu kabla ya kujiunga na Chama hicho wamefanya upembezi wa kutosha kwa kupitia Katiba ya chama kimoja baada ya kingine na wamejiridhisha ACT ndio sehemu sahihi ya wao kwenda.
   
  "Eneo ambalo tunaamini mapambano yetu yataendelea ni ACT- Wazalendo, tunakwenda huko kupigania wananchi na si kutafuta vyeo.Hatuendi na masharti ya aina yoyote yale.Tunajua wanachama wa CUF wakiwamo wabunge wanatuunga mkono sana lakini tunaacha wachukue maamuzi wenyewe na sio sisi,"amesema Maalim Seif.

  0 0


  Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara


  Kumekuwa na dhana ya kila mkulima wa korosho kulalamika kuwa hajalipwa fedha za korosho zake jambo hili limeibua sintofahamu katika jamii.


  Katika hali hiyo serikali sasa imeamua kuja na mkakati kabambe wa kubandika majina ya wakulima wote waliolipwa fedha zao ili kuondokana na kadhia ya lawama za wakulima wasioitakia mema serikali.


  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa agizo hilo leo tarehe 18 Machi 2019 wakati akizungumza mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge, Mifugo na Maji kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.


  Agizo hilo limetolewa kwa wataalamu wanaoongoza timu ya Oparesheni Korosho kubandika majina ya wakulima wote waliolipwa ili kuondoa sintofahamu katika jamii.


  “ Mimi nashangaa sana kila mkulima akiulizwa anasema hajalipwa jambo hili sio sawa nadhani wanafanya hivi kukwepa madeni wanayodaiana huko vijiji, sasa naitaka timu ya wataalamu wa Oparesheni korosho kuhakikisha majina yote ya wakulima waliolipwa yanabandiikwa kwenye ofisi za vijiji ” Alikaririwa Mhe Hasunga


  Alisema kuwa wanapaswa kubandika orodha ya majina ya watu waliolipwa na kiasi cha korosho walicholipwa.“Mpaka sasa Tani 222,684 zimekwisha kusanywa huku hadi kufikia tarehe 14 Machi 2019 tayari jumla ya Shilingi Bilioni 596.9 zilikuwa zimekwishalipwa kwa wakulima kati ya Shilingi Bilioni 723 

  lakini nashangaa wakulima wanasema hawajalipwa hili sio sawa” Alisema Mhe Hasunga

  Sambamba na hayo Waziri Hasunga alisema kuwa Serikali imejipanga hadi kufikia tarehe 31 Machi 2019 wakulima wote watakuwa wamelipwa fedha zao kwani uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa.


  Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli inapaswa kuungwa mkono kwa maamuzi magumu kwenye korosho kwa kuamua kuwalipa wakulima shilingi 3300 kwa kila kilo moja ya korosho.


  Kadhalika, ameshangazwa na Mkoa wa Mtwara ambao unazalisha kwa karibu nusu ya korosho zote nchini lakini imebaini idadi ndogo ya wafanyabiashara wanaofanya biashara ya Korosho kinyume na sheria maarufu kama kangomba ukilinganisha na mkoa wa Lindi ambao una idadi kubwa ya Kangomba.


  “ Nashangaa sana Mkoa wa Mtwara una Kangomba 10 lakini ndio wazalishaji wakubwa wa korosho huku Mkoa wa Lindi ambao unafuatia kwa uzalishaji wa korosho ukiwa na idadi kubwa ya Kangomba ambao wapo zaidi ya 400” Alisema


  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Dkt Christine Ishengoma amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kwa kuanzisha zoezi la usajili wa wakulima nchini.


  “ Nakupongeza sana Waziri Hasunga kwa hili lakini hakikisha unalisimamia kwa weledi jambo hili ili liwe na matokeo chanya na wakulima waweze kutambulika kote nchini kwani kufanya hivyo serikali itakuwa na uwezo wa kuwahudumia kwa ufasaha” Alisema


  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiongozwa na Mhe Dkt Christine Ishengoma wameanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara wakikagua miradi ya maendeleo katika sekta husika za Kilimo, Mifugo na Maji.
  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)

  0 0  *Ni baada ya kufurahishwa na mafunzo yanayotolewa na Puma Energy Tanzania kwa wanafunzi wa shule za msingi 

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

  KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy, imezindua mafunzo na uchoraji la usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi, mafunzo ambayo yatawapa uelewa wa usalama huku Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamadi Masauni akitoa ombi kwa Puma kutoa elimu hiyo kwa shule zote nchini. 

  Uzinduzi huo umefanyika leo Machi 18 , 2019 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Yussuf Masauni, ambapo Mkurugenzi wa Puma, Dominic Dhanah, amefafanua mafunzo hayo yanakwenda sambamba pia kwa wanafunzi waliowahi kufundishwa. 

  Amesema madhumuni ya kuwahusisha wanafunzi wa shule za msingi ni kutokana na imani yao kwamba, watoto hao wanakabiliwa na hatari za ajali za barabarani na kuhitaji mafunzo ya usalama barabarani ili kuepukana na ajali. 

  “Usalama barabarani ni kipaumbele namba moja katika Kampuni ya Mafuta Puma na tumeamua kuwafundisha watoto wadogo kwani tunfahamu hatari za barabarani wanazokabiliana nazo. Kampuni ya Puma inafanya biashara ya mafuta katika nchi 49 duniani na kwa Afrika tupo katika nchi 19. Mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi yalianza mwaka 2013 hapa Tanzania na mpaka sasa shule 75 zimenufaika na mafunzo haya wakati wanafunzi 80,000 wamepata mafunzo haya,"amesema 

  Ameongeza kuwa "Tumefanya utafiti na kugundua kuwa shule tulizoendesha mafunzo haya , ajali kwa wanafunzi zimepungua na hivyo basi kwa mwaka 2019 mafunzo haya yataendeshwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar,” alisema Dhanah 

  Kwa upande wake Naibu Waziri Masauni, amesema Serikali inafarijika na kazi inayofanywa na Kampuni ya Puma kwa kurudisha faida inayopatikana kwa jamii ikiwamo kutoa mafunzo muhimu ya usalama barabarani. 

  Amesema elimu ni suala la kipaumbele kwa jamii na mkakati wa wao Wizara ya Mambo ya Ndani na Serikali kwa ujumla ni kupunguza ajali za barabarani na Puma inafanyakazi hii kwa karibu na Machi 30, mwaka huu tutakuwa na kongamano la wiki ya usalama barabarani pia tujadili hili kwa kina. 

  "Serikali tunatambua kazi nzuri ambayo inafanywa na Puma Energy Tanzania katika kutoa elimu hii inayohusu usalama barabarani.Ni jukumu letu na wananchi kwa ujumla kuunga mkono jitihada hizi.,” alisema Masauni 

  Akifafanua zaidi Mhandisi Masauni amesema kitendo cha Puma kuwa na programu hiyo kinaonesha namna ambavyo wanakataa ajali za barabarani kwa vitendo na kwamba wanafunzi ambao wanapata elimu hiyo anauhakika watakuwa mabalozi wazuri wa kuelezea kwa usahihi mtembea kwa miguu anatakiwa kufanya nini akiwa barabarani. 

  "Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Usalama Barabarani wana program nyingi za kusaidia kutoa mafunzo kwa shule zote zilipo kwenye mazingira hatarishi na zisizo kwenye mazingira hayo pia. Programu hizo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto mbalimbali za kifedha. Ninaomba kutumia fursa hii kuomba uongozi wa Puma kukisaidia Kikosi cha Usalama Barabarani kuzifikia shule zote nchini kwa kupitia askati walioko kwenye maeneo yote nchini,"amesema Pia amemuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani kuanza mchakato wa kuandaa andiko la kutoa mafunzo kwa shule zote nchini na kuliwasilisha kwenu (Puma) ili muone namna yambavyo mnaweza kusaidia kuokoa kizazi chetu cha kesho,” amesema Masauni.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akimpa zawadi mmoja wa Wanafunzi wa shule ya msingi Bunge jijini Dar,mara baada kujibu vizuri swali lililohusu mambo ya usalama barabarani,kabla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania iishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.
  Mmoja wa Watoa Mafunzo ya Usalama barabarani kwa Wanafunzi wa shule ya msingi chini ya Ufadhili wa kampuni ya Puma Energy Tanzania,Neema Swai kutoka taasisi ya AMEND akionesha moja ya mchoro ulioshinda kwenye shindano la Wachoraji kuhusu Usalama barabarani mwaka 2018,mbele ya mbele ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi ( wa pili kulia ) Mhandisi Hamad Masauni,wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania 
  Ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ukiendelea leo jijini Dar

  Mwanafunzi Shule ya Msingi Bunge jijini Dar, Omari akifafanua kuhusu namna ya matumizi sahihi kwa watembea kwa miguu mbele ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchi ( wa tatu kulia ) Mhandisi Hamad Masauni,wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania,Dominic Dhannah akizungumza leo jijini Dar wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni hiyo,ambapo mgeni rasmi ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi ( wa kwanza kulia ) Mhandisi Hamad Masauni 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy  Tanzania kishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania akiwa na baadhi ya Wanafunzi ambao ni pia ni Mabalozi wa shule ya msingi Bunge jijini Dar,ambao wamehudhuria ufunguzi wa mafunzo ya usalama barabarani yanayotolewa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania kishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni akiwaaaga baadhi ya wanafunzi ambao ni pia ni Mabalozi wa Usalama barabarani wa shule ya msingi Bunge jijini Dar,mara baada ya kufungua rasmi mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania kishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya mteule wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya mteule wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  0 0  0 0

  Na. Vero Ignatus, Arusha

  Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa jangwa la Sahara( MISA) imeendesha mjadala wa siku moja wawaandishi wa habari, na wadau mbalimbali vya habari Jijini Arusha katika chuo cha Uandishi wa habari cha Fanikiwa ikiwa na lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye vyombo vya habari.

  Gasirigwa Sengiyumva ni Mkurugenzi wa MISA nchini amesema kuwa lengo kuu la mjadala huo ni kuboresha namna ambayo vyombo vya habari vinafanya kazi, kukuza uhuru wa habari, kupata habari, uhuru wa vyombo vya habari

  Amesema kuwa upo umuhimu wa waandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi, kuendana na sheria ya habari ya mwaka 2016 na kumtaka kila mwandishi kutimiza wajibu wake kwa kutafuta ukweli wa habari na uripoti ukweli sahihi, na kuepuka kuandika habari zinazodanganya jamii

  Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya MISA nchini Tanzania Mussa Juma amesema kuwa ni vyema waandishi wa habari kuepuka uchochezi unaokinzana na maslahi ya Taifa kwani kulingana na sheria ya habari ya mwaka 2016 kosa la mwandishi ni faini ya shilingi milioni 3,na kifungo hadi miaka 3

  Pia amesisitiza waandishi kujiongeza Kielimu kwani serikali ilitoa kipindi cha miaka mitano kuanzia januari 01,2017 ndipo ilipitiswa kuwa kila mwandishi wa habari kuwaanzia kiwango cha diploma ya uandishi wa habari kutoka vyuo vinavyotambulika.

  Wakichangia mjadala huo, Mwenyekiti wa Arusha Press Klabu, Claud Gwandu kushirikiana na wadau kudai mabadiliko ya sheria ya huduma za habari amesema kuwa sheria hiyo ina mapungufu kadhaa, ikiwepo kutotambua kada za chini katika vyombo vya habari, ambazo hazihitaji kuwa na elimu ya diploma na pia kufanya makosa ya habari kuwa makosa ya jinai.

  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha uandishi wa habari cha Fanikiwa Bwana Andrea Ngobole amesema kuwa siyo kweli kwamba hawatoi elimu ya kutoshawaandishi watarajiwa katika vyuo vyao bali wanatoa sawasawa na mtaala toka Nacte ila wanapokwenda nje ya chuo wanakutana na shinikizo la muda na kiuchumi wa habari tofauti ambazo kile jamii inahitaji kusikia.

  Amekubaliana hoja wadau wa mkutano huo wa kuwachukua wataalamu wa habari wenye uzoefu wa muda mrefu ili waweze kutoa mafunzo yenye uhalisia katika tasnia ya habari ili waweze kutoa taarifa zenye uhalisia wa maisha ya watu wengi.

  Kwa upande wake Inspekta wa polisi Rashid Nchimbi ambae amemuwakilisha RPC Jonathan Shana amesema jeshi polisi wanaushirikiano na waandishi hivyo yapo madawati mengi ambayo wanaweza kupata habari za kipolisi kila leo wakihitaji wasikariri sehemu moja.

  Pia amewashauri vyuo vya uandishi wa habari kutafuta waalimu wenye uzoefu na kazi hiyo kwaajili ya kutoa mafunzo kwani asilimia kubwa wanakauwa na uzoefu mkubwa na kazi wanayoifanya.Nae Mkurugenzi Civic and Legal Aid Organization (CiLAO)amesema kuwa wanajiandaa kufanya mkutano na wadau wa Habari, haki za binadamu, tume ya uchaguzi nchini na Tamisemi ili kuona namna Waandishi wa Habari watashiriki kwenye uchaguzi kama waangalizi wa uchaguzi.

  ''Tayari tumefanya utafiti kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya ambako Vyombo vya Habari vina haki ya kushiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia upigaji, uhesabuji wakiwa ndani kama ambavyo waangalizi wa uchaguzi walivyo na haki hiyo"alisema Odero Odero

  Gasirigwa Sengiyumva ni Mkurugenzi wa MISA nchini akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa habari
  Baadhi ya washiriki wa mjadala wa changamoto za vyombo vya habari na namna vinavyofanya kazi
  Baadhi ya washiriki wa mjadala wa changamoto za vyombo vya habari na namna vinavyofanya kazi
  Mjumbe wa bodi ya MISA nchini Tanzania Mussa Juma akifafanua juu ua sheria mpya ya habari ya mwaka 2016
  Mkuu wa Chuo cha uandishi wa habari cha Fanikiwa Bwana Andrea Ngobole akuchangia mjadala kuhusiana na elimu kwa wanaandishi

  0 0


  Na Teresia Mhagama,

  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, chini ya uenyekiti wa Mariamu Ditopile Mzuzuri, imefanya ziara ya kikazi mkoani Iringa iliyokuwa na lengo na kukagua kazi ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini ili kijiridhisha endapo fedha zinazoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

  Kamati hiyo ilikagua utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika Kijiji cha Ngano, wilayani Iringa na katika Kitongoji cha Ikuvala kilichopo wilayani Kilolo ambapo waliambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga na watendaji kutoka TANESCO.

  Pamoja na kukagua utekelezaji wa mradi huo, Kamati hiyo ilipata fursa ya kuwasha rasmi umeme katika Kisima cha Maji, Shule ya Msingi na Zahanati katika Kijiji cha Ngano wilayani Iringa pamoja na kuwasha umeme katika Kitongoji cha Ikuvala, wilayani Kilolo.

  “ Tunaipongea Wizara kwa kuzingatia agizo la Kamati ya Bunge la kuhakikisha kuwa umeme unafika katika Taasisi za Umma na Kijamii, kwani wakati tunakagua mradi huu mwaka jana, tuliongelea suala la wigo wa wakandarasi na tuliwashauri kwamba umeme ufike katika Taasisi za kijamii ikiwemo zahanati na Shule,” alisema Mzuzuri.

  Mzuzuri alisema kuwa, haitaleta maana kama Wakandarasi wa umeme wa vijijini watasambaza umeme katika makazi ya watu pekee kisa tu wako katika wigo waliopangiwa na kuacha Taasisi muhimu za kijamii hivyo aliipongeza Wizara ya Nishati kwa kuitikia agizo hilo la Kamati na kulifanyia kazi.

  Aidha, Kamati hiyo ya Bunge imeipongeza Wizara ya Nishati, kwa kufanyia kazi ushauri wa kupunguza bei za umeme ambapo sasa bei ya kuunganisha umeme vijijini ni 27,000 tu, iwe kwa miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) au TANESCO.

  “ Sisi kama Kamati tunapata faraja, pale tunapotoa ushauri na nyie mnaufanyia kazi, tunawatia moyo muendelee kufanya kazi kwa bidii ili mradi yale tunayoyapanga kwa pamoja yaweze kufanikiwa zaidi na zaidi,” alisema Mzuzuri.

  Akitoa taarifa ya usambazaji umeme vijijini mkoani Iringa, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alisema kuwa vijiji 179 mkoani humo vimepangwa kupelekewa umeme kupitia miradi mbalimbali ikiwemo wa REA III na mradi wa Backbone ambapo gharama zake ni takriban shilingi bilioni 30.

  Naibu Waiziri alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa bei ya kuunganisha umeme vijijini ni shilingi 27,000 tu bila kujali kama mradi unatekelezwa na TANESCO au Wakala wa Nishati Vijijini kwani Serikali imedhamiria kurahisisha zoezi la kuwapelekea wananchi umeme.

  Aidha, alilisisitiza kuhusu matumizi ya vifaa vya UMETA kwa wananchi vijijini na kuwataka wakandarasi kuhakikisha kuwa wanawapatia wananchi vifaa hivyo kwani baada ya kukamilika kwa mradi, Serikali itakagua endapo wakandarasi hao wametekeleza agizo hilo la Serikali.

  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme katika Kitongoji wa Ikuvala wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (katikati), akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati walipofika katika Kijiji cha Ngano wilayani Iringa kukagua mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu. Wa Pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mariamu Ditopile Mzuzuri na Wa Tatu kulia ni Kaimu Kamisha wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mariamu Ditopile Mzuzuri akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa umeme katika Kitongoji wa Ikuvala wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh amesema kuwa jamii iache kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu kwani watu wenye ulemavu wanaweza kufanya vitu vikubwa na kusaidia nchi katika maendeleo mbalimbali.

  Nuru aliyasema hayo wakati wa hafla ya Tuzo ya I Can ya Mafanikio katika Ujuzi wa Kipekee hafla ilioandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Nuru amesema Tuzo mbili alizozipata zimetokana na kuwa na mchango katika jamii licha ya kuwa na ulemavu wa kuona lakini ameweza kutumia kipaji chake na kuiletea maendeleo nchi pamoja na wananchi.

  Amesema kuwa yeye angefungiwa ndani asingeweza kupata elimu na kufanya maisha yake ya ulemavu kufunga kipaji pamoja na ndoto zake ambapo leo anaongoza watu wa makundi mbalimbali na wanamuamini katika uongozi.

  ‘’Namshukuru Rais Dkt. John Pombe Mgufuli kwa kuteua viongozi mbalimbali wenye ulemavu katika serikali yake ni kutokana na kutambua mchango wa wenye ulemavu kushiriki katika ngazi za maamuzi na sasa kufanya walemavu kijiamini kwa kupita kifua mbele”.amesema Nuru.

  Nuru amesema watu wenye ulemavu wana kipaji kikubwa huvyo jamii iache kuwafungia ndani kwa kuona hawawezi kufanya chochote katika jamii yao wanayoishi.

  Aidha amesema kuwa watu wenye uleamvu kwa vijana wanaosoma wasife moyo kwa ulemavu wao wasome kwa bidii kwani elimu ndio mkombozi kwa mtu mwenye ulemavu.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipongeza Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya I CAN ya Mafanikio katika Ujuzi wa Kipekee kwenye hafla ilioandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
  Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akipokea hundi ya sh.milioni mbili kutoka kwa mwakilishi wa Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika hafla ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akizungumza na Michuzi Blog wakati hafla ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka.MMG)
  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na watu wenye ulemavu mara baada ya ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akiwa katika picha ya pamoja na Familia yake katika ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka.MMG)

  0 0

   Meneja wa Vodacom mkoa wa Lindi, Omary Kilumanga akikabidhi baadhi ya taulo za kike kwa mkuwa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga kwa ajili ya kugawa kwa wanawake wa wilaya hiyo hivi karibuni kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Sherehe hizi ziliandaliwa na taasisi ya T-Marc Tanzania chini ya mradi wa Hakuna wasichoweza unaotoa elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana kwa kudhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation.
  Meneja wa Vodacom mkoa wa Lindi, Omary Kilumanga akikabidhi taulo za kike kwa wanawake wa Lindi hivi karibuni kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani chini ya mradi unaotekelezwa na taasisi ya T-Marc Tanzania wa Hakuna wasichoweza unaotoa elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana kwa udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation. 


  0 0


  LAGOS, NIGERIA

  TAASISI ya Hisani la Tony Elumelu Foundation (TEF), ambayo inaongoza kwa uwezeshaji wajasiriamali wa Afrika, linatarajia kutangaza majina ya waombaji waliopitishwa kushiriki programu ya ujasiriamali Machi 22, mwaka huu.

  Tukio hilo, ambalo litaashiria awamu ya tano ya programu ya uwezeshaji ya shirika hilo, itafanyika kwenye Hoteli ya Transcorp Hilton Hotel, mjini Abuja Nigeria.

  Kila mwaka TEF hukaribisha maombi ya uwezeshaji kwa wajasiriamali wa Afrika, wenye biashara zenye umri usiozidi miaka mitatu.

  Kupitia programu yake yenye thamani ya dola milioni 100, taasisi hiyo huwezesha wajasiriamali 1,000 kila mwaka, ambao hupokea dola 5,000 kama mtaji wa kuchochea biashara zao.

  Aidha hukutana na wataalamu, programu ya mafunzo ya wiki 12 na fursa za kutangaza biashara zao kwa ulimwengu wa kibiashara.

  Waombaji wote hupata fursa ya kuunganishwa na mtandao wa kidijitali wa TEFConnect, ambao ni kitovu cha dijitali ya ujasiriamali barani Afrika, ukitoa fursa ya kuunganishwa na mitandao, mafunzo na vyanzo zaidi vya mitaji na fursa za kibiashara.

  Katika miaka mitano tangu taasisi hiyo izindue programu ya ujasiriamali, imewezesha moja kwa moja wajasiliamali 4,000 wa Afrika na wengine 470 wakisaidiwa na wabia wa TEF.

  Akizungumzia programu hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu mpya wa TEF, Ifeyinwa Ugochukwu, ambaye anachukua nafasi ya Parminder Vir, atakayebakia katika bodi ya ushauri kuanzia Aprili Mosi, mwaka huu, alisema kuna umuhimu wa kuongeza idadi ya wanufaika wa kila mwaka kutoka 1,000 ya sasa.

  “Kila mwaka tunashuhudia ongezeko la waombaji hivyo idadi ya wanufaika itapaswa kuongezeka. Mbia wetu, Accenture Development Partnerships, kwa sasa anatathimini na kupitisha waombaji.

  “Zaidi ya wajasiliamali 215,000 wa Afrika kutoka mataifa 54 waliwasilisha maombi likiwa ongezeko kutoka waombaji 151,000 wa mwaka jana na kutoka 62,000 mwaka 2018 hadi 90,000 mwaka 2019 kwa pande wa wanawake. “Kupanda kwa takwimu hizi kunaonesha dhamira tya mjasiriamali wa Afrika kuendeleza bara letu na tunatakiwa kugeuza dhamira hii kuwa fursa ya biashara itakayochochea maendeleo ya bara letu,” alisema Ugochukwu.
   
   Baadhi ya wajasiriamali kutoka nchi za Afrika waliohudhuria mafunzo mwaka jana
   
   

older | 1 | .... | 1820 | 1821 | (Page 1822) | 1823 | 1824 | .... | 1897 | newer