Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WANAWAKE TPA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MSAADA MUHIMBILI

$
0
0
 Mmoja wa wafanyakazi wa TPA, Zahara Malika akikabidhi moja kati ya katoni za Biscuit na misaada mbalimbali walizozitoa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi kwa wazazi wenye watoto wenye Kichwa kikubwa na mgongo wazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kilele chake ni leo. Wengine pichani ni baadhi ya wanawake kutoka TPA waliowatembelea watoto hao hospitalini hapo leo na anayepokea kwa niaba ya wagonjwa wengine ni Nesi wa hospital hiyo, Bi Rehema Ally. 
 Mmoja wa wafanyakazi wa TPA, Hilda Mwakatobe akikabidhi moja kati ya katoni za juisi na misaada mbalimbali walizozitoa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi kwa wazazi wenye watoto wenye Kichwa kikubwa na mgongo wazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kilele chake ni leo. Wengine pichani ni baadhi ya wanawake kutoka TPA waliowatembelea watoto hao hospitalini hapo leo na anayepokea kwa niaba ya wagonjwa wengine ni Bi. Cheusi Selemani.
Baadhi ya wanawake ambao ni wafanyakazi wa TPA wakiwasili katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi kwa wazazi wenye watoto wenye Kichwa kikubwa na mgongo wazi ili kuwatembelea na kuwapa misaada ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kilele chake ni leo.
 Mkurugenzi wa Fedha wa TPA, Bi. Nuru Mhando akimbeba mmoja wa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi waliolazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi ambacho wamelazwa watoto hao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kilele chake ni leo.
Baadhi ya wanawake ambao ni wafanyakazi wa TPA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali na pesa taslimu kwa wazazi wenye watoto wenye Kichwa kikubwa na mgongo waliolazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi.

Sakata la Chuo cha Diplomasia lahamia Takukuru

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe (kulia) akikabidhi ripoti za ukaguzi za Chuo cha Diplomasia, kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (PCCB), Bw. Diwani Athumani kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tuhuma za ubadhilifu wa fedha uliofanywa na baadhi ya viongozi wa chuo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar Es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia, Balozi Ombeni Sefue akishuhudia makabidhiano ya ripoti za ukaguzi ambazo zimeainisha ubadhilifu wa fedha katika Chuo cha Diplomasia. 
Balozi Sefue (kushoto), Dkt. Mnyepe na Bw. Diwani wakibadilishana mawazo kuhusu utendaji kazi wa Chuo cha Diplomasia. 
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Diwani Athumani akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia, Balozi Ombeni Sefue.

Airtel Divas washerehekea siku yao kwakushukuru wanaume wote

$
0
0
Airtel DIVAS Ikiwa ni siku ya wanawake inayoadhimishwa ulimwenguni kote wanawake wote wanaofanya kazi katika vitengo mbalimbali ndani ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel (Airtel Divas) leo wamesherehekea kwa style ya kipekee ambapo wamewashukuru wanaume wote wanaofanya nao kazi kila siku kwa kuwapatia zawadi.

Akiongoza wanawake wenzie wote (Airtel Divas) katika maadhimisho hayo Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Bi Stella Kibacha alisema “leo ni siku yetu Wanawake, ambapo inaadhimishwa dunia nzima kila tarehe 3 Machi. Lakini style yetu sisi Divas wa Airtel tumeamua kuwashuru kwa zawadi mwanaume wote hapa Airtel, ni ukweli kuwa tunashinda nao kila siku wanatuonyesha ushirikiano wa kutosha, hawana ubaguzi tunafanya kazi kwa usawa na kusikilizana, kwa kweli tunawashukuru sana”

Bi Kibacha alieleza kuwa “Mwaka huu kauli mbiu ya siku ya wanawake ni ‘#BalanceforBetter’ ikipambanua mambo mengi kati yao ni kujipanga na kupangilia kila jambo ili kuwa na mafanikio” “Airte Divas Tumejipanga kisawasawa kuhakikisha kila jambo kazini au nyumbani yanakaa sawa kwa manufaa yetu na taifa kwa ujumla” alimaliza kwa kusema Bi Kibacha

Airtel Divas wakiwa kwenye picha ya pamoja leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyobeba kauli mbiu ‘Balance for better’ Siku ya wanawake huadhimishwa kila mwaka tarehe 08 Machi kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii 



Airtel Divas Mkurugenzi wa Airtel Rasilimali watu Bi stella Kibacha akimshukuru mmoja kati ya wafanyakazi wa airtel wakiume bw Dunia Yusufu leo walipoadhimisha siku ya wanawake Duniani yenye kauli mbiu ‘Balance for better’. Siku ya wanawake huadhimishwa kila mwaka tarehe 08 machi ikiwa na lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii.
Airtel Divas Meneja uhusiano Airtel Bi, Dangio Kaniki akitoa zawadi kwa Edward Mtingwa kwa lengo la kuwashukuru wanaume wote wanaofanya kazi nao. ‘Airtel Divas’ leo wameadhimisha siku ya wanawake Duniani yenye kauli mbiu ‘Balance for better’ kwa kutoa shukrani kw wanaume wote. Siku ya wanawake huadhimishwa kila mwaka tarehe 08 Machi ikiwa na lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii
Airtel Divas Mkurugenzi wa Airtel Huduma kwa wateja Bi, Adriana Lyamba akitoa zawadi kwa Ezekieli Mwakangata ikiwa ni ishara ya kushukuru wanaume wote wanaofanya kazi na wafanyakazi wa Airtel ‘Airtel Divas’ leo walipoadhimisha siku ya wanawake Duniani yenye kauli mbiu ‘Balance for better’ kwa kutoa shukrani kwa wanaume wote. Siku ya wanawake huadhimishwa kila mwaka tarehe 08 Machi ikiwa na lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii

WAHAMIAJI HARAMU 12 WAKAMATWA NA WATU WENGINE 14 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI PWANI KWA MAKOSA YA UHALIFU MBALIMBALI

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

WAHAMIAJI haramu 12 raia kutoka Ethiopia ,wamekamatwa mkoani Pwani, eneo la Mwidu porini, Chalinze kwa kosa la kutokuwa na kibali kinyume na sheria.

Aidha watu 14 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo wizi wa pikipiki na kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi.

Akielezea juu ya matukio hayo, kamanda wa polisi mkoa wa Pwani,ACP Wankyo Nyigesa, alisema usiku wa kuamkia march 8 ,askari polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu uwepo wa wahamiaji hao waliojificha kichakani eneo la Mwidu barabara ya Dar es salaam -Morogoro.

Alieleza baada ya polisi kufika eneo hilo waliwakamata wakiwa safarini kutoka Ethiopia kuelekea Afrika ya Kusini. :”Baada ya mahojiano ilionekana watu hao walifichwa hapo na mtu ama watu ambao bado hawajafahamika kwa lengo la kuwatafutia usafiri wa kuelekea nchini Afrika Kusini kutafuta ajira. “

Hata hivyo Wankyo alibainisha, afya ya wahamiaji haramu hao walikuwa wamedhoofika. Wakati huo huo jeshi hilo linawashikilia watu nane kwa kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo wizi wa pikipiki.Pia watu sita wamekamatwa kwa kupatikana na dawa za kulevya ikiwemo bangi kete 172.

Wankyo alielezea kwamba, baada ya mahojiano na upelelezi kukamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria

.

Wanawake Wizara ya Habari waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kutoa misaada Kituo cha Afya Chamwino.

$
0
0


 Mwenyekiti wa Wanawake Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Prisca Shewale akikabidhi vitu mbalimbali kwa  niaba ya wanawake wa Wizara hiyo kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Chamwino Dkt.Zipora Mfugale  kwa ajili ya wanawake, watoto na wenye uhitaji maalum waliolazwa kituoni hapo ikiwa ni kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
PIC 2
Afisa Utumishi Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Jacquiline Kalua akimpa vifaa mbalimbali Bibi Marietha Maiko alielazwa Kituo Cha Afya Chamwino wakati wanawake wa Wizara hiyo walipotembelea kituo hicho katika kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
PIC 3
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Lorietha Laurence akitoa vifaa mbalimbali kwa Bibi Regina Balabaido alielazwa Kituo Cha Afya Chamwino wakati wanawake wa Wizara hiyo walipotembelea kituo hicho katika kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
PIC 4
Afisa Habari wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi.Lilian Lundo akitoa vifaa mbalimbali kwa Bibi Molen Mwaiko alielazwa Kituo Cha Afya Chamwino wakati wanawake wa Wizara hiyo walipotembelea kituo hicho katika kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
PIC 5
Baadhi ya Wanawake Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Kituo Cha Afya Chamwino mara baada ya kutembelea Kituo hicho na kutoa misaada mbalimbali kwa wagojnwa waliolazwa kituoni hapo ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI JAMII KUKAMATA BODABODA, ASKARI POLISI KUKAMATA VYOMBO VYA MOTO BILA KUVAA SARE ZA JESHI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimfafanulia jambo Katibu wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Morogoro, Juma Bega, alipokuwa akilalamika kuhusu Polisi Jamii kuwanyanyasa waendesha bodaboda, katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mafisa B, Mwembesongo, mjini humo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimfafanulia jambo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Regina Chonjo (katikati), mara baada ya kumaliza Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, SACP-Wilbroad Mutafungwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akifurahi jambo wakati Mkuu wa Nidhamu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Marko Nehemia, alipokuwa anajibu maswali yake kwa ufasaha katika Kikao cha Askari na Watumishi raia wa Wizara yake, kilichofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Umwema, mjini Morogoro, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Na Felix Mwagara, MOHA-Morogoro. 


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku Polisi jamii kukamata bodaboda zinazofanya makosa ya usalama barabarani nchini. 


Pia Waziri huyo amepiga marufuku polisi wa usalama barabarani kukamata vyombo vya moto wakiwa hawajavaa sare za Jeshi. 

Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mafisa, Kata ya Mwembesongo, mjini Morgoro, jana, Lugola alisema Polisi Jamii hawana ujuzi wa kijeshi wa ukamataji wa bodaboda hivyo kuendelea kuifanya kazi hiyo ni kuwanyanyasa wananchi. 

“Nimepata malalamiko mengi ninapofanya ziara zangu hapa nchini, wengi wanawalalamikia Polisi Jamii kuwaonea, kuwaomba rushwa na kuwakamata pasipofuata utaratibu unaotakiwa kijeshi, hapa Morogoro pia, katika mkutano huu wa hadhara mnayasema yale yale, sasa natangaza kuanzia leo, marufuku Polisi Jamii kukamata bodaboda,” alisema Lugola. 

Waziri Lugola pia alipiga marufuku baadhi ya Polisi wa Usalama barabarani ambao wenye tabia ya kutovaa sare za Jeshi na kuingia barabarani au mitaani na kuyakamata magari na bodaboda. 

Lugola alisema lazima polisi wafate sheria za usalama barabarani hasa wanapokamata magari yanayofanya makosa, uvaaji wa sare za Jeshi ni muhimu na unapaswa kufutwa. 

Waziri Lugola aliongeza kuwa, bodaboda au vyombo vingine vya moto, zinazovunja sheria za usalama barabarani zinapaswa kukamatwa bila kuwaonea huruma, ila ni kosa Polisi kuwanyanyasa vijana hao ambao wanapata ridhiki kupitia biashara hiyo. 

“Mnapaswa kukamata hizi bodaboda zinapofanya makosa, tabia ya kukurupuka huku mkitafuta fedha zisizo halali, huko ni kuwaonea waendesha bodaboda,” alisema Lugola. 

Lugola alifafanua kuwa, bodaboda zinazotakiwa kuwepo kituo cha polisi ni zile zilizopo katika makundi matatu ambayo ni Bodaboda zilizohusika kwenye uhalifu, zilizotelekezwa au zilizookotwa na zilizohusika katika ajali. 

“Bodaboida hizo ndizo zinapaswa kuwepo vituoni, lakini kuziweka bodaboda ambazo hazipo katika makundi hayo, napiga marufuku na hii nataka Polisi nchi nzima munielewe,” alisema Lugola. Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda mjini Morogoro na Tanzania kwa ujumla wafate sheria za usalama barabarani zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa. 

Lugola ameanza ziara yake ya siku tatu mkoani humo akitembelea Wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilosa na Gairo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake. 

Lugola mwaka jana alitoa maagizo kwa makamanda wa mikoa nchini ambayo ni dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe. 

Waziri Lugola amemaliza ziara Wilaya ya Morogoro na leo ataanza ziara yake katika Wilaya ya Movemero, na Machi 10, 2019 atamalizia Wilaya ya Gairo ambapo katika Wilaya hizo pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni.

TSC yashiriki Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani

$
0
0

 Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wakiwa katika hali ya furaha wakati wa Maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Machi 8, 2019 jijini Dodoma.
2
Wafanyakazi wa TSC wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani jijini Dodoma.
3
Watumishi kutoka Taasisi mbalimbali wakiwemo wa Tume ya Utumishi wa Walimu wakiwa katika Maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika  jijini Dodoma.
4
Wafanyakazi wa TSC wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
5
Wafanyakazi wa TSC wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.

KIKAO CHA 40 CHA BODI YA TAIFA YA PAROLE CHAFANYIKA LEO UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0



Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto) akiongoza Kikao cha 40 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole. Kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo Machi 8, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
PIX 2
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole akitoa taarifa fupi ya Sekretarieti kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(hayupo pichani)afungue rasmi kikao hicho.
PIX 3
Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakifuatilia majadiliano ya wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole leo Machi 8, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
PIX 4
Ujumbe kutoka Zanzibar wakishiriki mazungumzo maalum yenye lengo la kubadilishana uzoefu na Bodi ya Taifa ya Parole Tanzania katika ziara yao ya kikazi leo Machi 8, 2019. Wa kwanza kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Said Hassan(katikati) ni Waziri wa TAMISEMI na Vikosi Maalum vya Zanzibar, Mhe. Haji Omari na Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Polisi kutoka Zanzibar, Hasina Ramadhani.
PIX 5
Sekretarieti wakifuatilia kwa makini majadiliano katika kikao hicho.
PIX 6
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(wa nne toka kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, leo Machi 8, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam baada ya ufunguzi wa Kikao cha Bodi ya Taifa ya Parole(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Tigo kuwawezesha wasichana kujiendeleza kiteknolojia

$
0
0

Wasichana wanaojengewa uwezo kwenye sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na taasisi ya Apps and Girls wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafadhili wao ikiwamo Kampuni ya Tigo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Simon Karikari, akipata maelezo kutoka kwa wasichana wanaojengewa uwezo kwenye sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano muda mfupi baada ya uzinduzi wa mradi wa ‘TECH IS FEMALE’ ambao Tigo imeufadhili katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Simon Karikari, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam ambapo kampuni ya Tigo ilitoa msaada kwa ajili ya kuwajengea uwezo wasichana na wanawake kwenye sekta ya Habari na Mawasiliano. Wa kwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Imni Patterson, na anayefuatia ni mwanzilisi wa taasisi ya Apps and Girls, Caroline Ekyariisma.
Halima Okash kutoka Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii cha Tigo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ufadhili wa kampuni ya Tigo kwa mradi wa ‘TECH IS FEMALE’ unaolenga kuwajengea wanawake na wasichana uwezo kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Wa kwanza kulia ni mwanzilishi wa taasisi ya Apps and Girls, Caroline Ekyariisma, akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Simon Karikari






Kampuni ya mawasiliano ya Tigo, imeelezea dhamira yake ya kusaidia kuwajengea uwezo wasichana na wanawake kwa ujumla kwenye eneo la teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kupitia taasisi ya hapa nchini inayojulikana kama Apps and Girls.

Akizungumza mbele ya wasichana wenye ndoto za kuwa wajasiriamali kwenye sekta ya TEHAMA wakati wa uzinduzi wa mradi wa ‘TECH IS FEMALE’, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Simon Karikari alisema, Tigo inatambua mchango wa wasichana na wanawake kwenye maendeleo na kuelezea utayari wa kampuni hiyo kuunga mkono jitihada za kuwawezesha kutoa mchango wao.

“Uwezeshaji unaofanywa na Tigo kwa wasichana na wanawake, unalenga kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kigunduzi kwenye TEHAMA kwa makundi ya wasichana waliofanyiwa mchujo na ambao watapewa mafunzo maalum kabla ya kuwekwa chini ya uangalizi maalum wakati wakifanya miradi waliobuni wenyewe ya kibunifu,” alisema Karikari.

Karikari aliongeza kuwa, mradi huo wa ‘TECH IS FEMALE’ unalenga kutoa fursa sawa kwa wasichana wote wenye umri kati ya miaka 14 na 24 (wanafunzi na sio wanafunzi) nchini Tanzania ili kuwawezesha kiuchumi na kidijitali, waweze kuwa vinara katika ulimwengu huu wa kidijitali unaokwenda kwa kasi kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia ya kila siku.

Kwa upande wake, Muasisi wa Apps and Girls, Caroline Ekyariisma, alisema kwamba kampeni hiyo itakuwa ni ya mwaka mzima. “Lengo letu ni kutoa mafunzo ya kutengeneza programu kwa wasichana katika shule 61 za sekondari zilizo chini ya mpango wa Tigo E-schools nchi nzima. Mpango huu pia utahusisha makundi ya wasichana ambao hawapo mashuleni, hivyo wasichana ambao sio wanafunzi pia watapata fursa sawa ya kushiriki na kunufaika,” alisema.

“Tunapenda pia kutoa shukrani zetu kwa Mpango wa Uvumbuzi kutoka Afrika ya Kusini (SAIS 2) pamoja na Mfuko wa Uvumbuzi kwa ushirikiano na uwekezaji wao katika kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupata ujuzi kwenye TEHAMA,” alishukuru Ekyarisiima.

Mchakato wa kuwapata wasichana watakaoshiriki katika mradi huu utafanyika nchi nzima na utakuwa na mchujo mkali ambapo wasichana 30 bora ndiyo watakao fuzu. Wasichana hawa ambao watakuwa mchanganyiko wa wanafunzi na sio wanafunzi, wataingizwa katika mpango maalumu ya mafunzo na uangalizi. Wengine watafanya mafunzo kwa vitendo katika idara ya TEHAMA ya Tigo kwa ajili ya kujiendeleza na kujifunza zaidi, huku wengine wakishughulika na miradi mengine. Wakati huo huo tutakuwa tunawajengea uwezo na kuwasaidia kupata kazi na kuwapatia mazingira bora ya wao kujiajiri,” alifafanua Ekyarisiima.

“Tigo inaendelea kutengeneza kizazi cha kidjitali. Ushirikiano wetu na Apps and Girls ni kuwekeza katika vijana wanawake ambao wanaonesha dalili nzuri za kuwa wajasiriamali, wavumbuzi, viongozi na mifano mizuri katika sekta ya teknolojia nchini Tanzania na Kusini mwa Jangwa la Sahara. Tunaamini kwamba katika siku za usoni ‘TECH IS FEMALE’ na tunaahidi kujitolea kupunguza tofauti za kijinsia kwenye sekta ya kidijitali nchini Tanzania,” alisisitiza Karikari.

Kwa miaka kadhaa sasa Tigo imekuwa ikishirikiana na kampuni ya Apps and Girls ili kuweza kupunguza tofauti ya kijinsia katika sekta ya kidijitali hususani katika eneo la Dar es Salaam. Ushirikiano huu kwa Apps and Girls umefanikiwa kuwafikia wasichana zaidi ya 3000 mashuleni na kwenye maeneo mengine ya jamii nje ya shule, na kuwezesha kuzaliwa kwa wajasiriamali, wavumbuzi, vioo kwa jamii na viongozi katika sekta ya teknolojia ambao wanaleta mabadiliko chanya katika nchi ya Tanzania.

RC MAKONDA AJITOLEA KUWASOMESHA HADI KIDATO SITA WATOTO 100 WA KIKE WALIOFAULU MASOMO YA SAYANSI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa ahadi ya kuwasomesha kuanzia kidato cha tano hadi cha sita bure wasichana 100 waliofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi katika matokeo ya mtihani wa kidato nne ili kuongeza idadi ya wanawake wataalamu na wabobezi wa nyanja mbalimbali.

RC Makonda amesema amegundua kuwa wapo mabinti wengi waliofaulu vizuri masomo yao lakini kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza kielimu wameishia kupoteza ndoto zao hivyo ameona ni vyema akawaendeleza.

Aidha RC Makonda ameeleza kuwa wasichana hao watagharamiwa kila kitu kuanzia ada,mabegi,vitabu na sare za shule ili wabaki na kazi moja pekee ya kusoma na kufaulu.

Hayo yote yamejiri leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na Maelfu ya wanawake.

SHIRIKA LA DHWYT YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI MTWARA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mlango wa matumaini kwa wanawake  na Vijana Tanzania DHWYT Clemence Mwombeki akitoa mafunzo kwa Wanafunzi waliohudhulia Mafunzo Juu ya Usawa wa Kijinsia ,Ukatili na Rushwa ya Ngono maeneo ya kazi na Shuleni.
 Baadhi ya wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wakisikiza Mafunzo kuhusiana na Afya ya Uzazi pamoja na Ujasiliamali katika kuadhimisha siku ya wanawake Dunia Mkoani Mtwara.
 Mratibu wa Huduma za Afya ya uzazi Baba,Mama na Mtoto Mkoa wa Mtwara Bi.Rosalia Arope akitoa mafunzo juu ya Afya ya Uzazi kwa wanafunzi wa Vyuo katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Mkoa wa Mtwara.
Blandina Emanuel Nguli  Mwanafunzi wa Kozi ya sekretari chuo cha Utumishi Mkoani Mtwara akiuliza swali juu ya Afya ya Uzazi katika mafunzo yaliyofanyika siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Shirika la Mlango wa Mtumaini Tanzania.

NA JOSEPH MPANGALA,MTWARA
Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani shirika lisolokuwa la kiserikali la Mlango wa matumaini kwa wanawake na Vijana Tanzania DHWYT limetoa elimu kwa Wanafunzi wa Vyuo kuhusiasna na elimu ya afya ya uzazi pamoja na Ujasiliamali Mkoani Mtwara.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na jinsia zote huku wanafunzi wengi wakitaka kujua juu ya afya ya uzazi baba,mama na Mtoto hasa katika taratibu za upatikanaji wa mimba na umuhimu wa Baba kuhudhulia kliniki pamoja na Athari zake iwapo hata hudhulia.

Akizugumza katika mafunzo hayo Mratibu wa huduma za afya ya uzazi Baba,Mama na mototo Mkoani Mtwara Bi.Rosalia Arope amesema wanawake wengi wamekuwa wakiwatumia madereva wa Boda boda kama waume zao na kwenda nao Kliniki kwa kuwalipa kiasi kidogo cha pesa kutokana na taratibu zilizowekwa kliniki za kuja na baba wa Mtoto.

“Kuna wanawakewanapokuja Kliniki unabaini kuwa sio mwenza wake halisi anamchukua tu dereva wa bodaboda ili aweze kukidhi kwa sababu kuna baadhi ya wilaya wamejiwekea sheria ndogo kila mwanamke lazima aje na mume wake kwahiyo anaamua kumchukua Dereva Boda boda ili kuepukana na Kero hiyo”amesema Bi.Rosalia.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Mlango wa Matumaini Tanzania amewataka Vijana kushiriki katika maswala mbalimbali ya kijamii kama moja ya njia ya kufatilia maendeleo katika jamii inayowazunguka kuanzia ngazi ya mtaa kata mpaka wilaya.

WAZIRI UMMY ANG’AKA MIKOPO KIDUCHU KWA WANAWAKE

$
0
0

 Baadhi ya wanawake na wakazi wa mkoa wa Mwanza wakiwa katika maandamano katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019 ambayo yalifanyika katika Viwanja vya Bujora Kisesa.
????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Msanii Nurdin Bilal “Shetta” mara baada ya kuzindua kampeni ya SAWA ya Kupambana na Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto inayomshirikisha Msanii Nurdin Bilal “Shetta” wakati wa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo Mhe Ummy aliungana na wanawake na wananchi wa mkoa wa Mwanza kuienzi siku hiyo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiangalia bidhaa zinazozaliswa na wanawake  mbalimbali katika moja ya banda lililokuwepo katika viwanja vya Kisesa Bujora  wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.
????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja Wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriques na  Balozi wa Anders wa Sweden wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.
????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza  na wanawake na wananchi wa mkoa wa Mwanza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake yaliyofanyika mkoani humo katika viwanja vya Bujora Kisesa.
????????????????????????????????????
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Dkt. Philis Nyimbi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana akitoa  salamu za mkoa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake yaliyofanyika mkoani humo katika viwanja vya Bujora Kisesa.
 Mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez akielezea ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unapatikana nchini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.
????????????????????????????????????
Mwakikishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women Bi. Hodan Addou akisisitiza ushirikishwaji wa mwanamke katika masuala ya kimaendeleo ili kufikia usawa wa kijinsia wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.ummy Mwalimu akiserebuka mziki pamoja na wanawake wa mkoa wa Mwanza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Mwanza wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


……………….


Na Mwandishi Wetu Mwanza 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amepiga marufuku mikopo ya laki tano kwa wanawake nchini bali wawezeshwe kupata mikopo yenye tija ili kuwa na uwezo wa kujikwamua kiuchumi.

Ameyasema hayo leo mkoani Mwanza alipokuwa akizungumza na Wanawake na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Waziri Ummy Mwalimu amesema lengo la kuadhimisha Siku ya Wanawake katika nagzi ya mikoa kwa miaka mitano ni kutoa nafasi ya kujitathimini katika utekelezaji wa masuala mbalimbali kuhusu hali ya ka Maendeleo ya mwanamke.

Amesema kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019 inasema “Badili Fikra Kufikia Ustawi wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu” Kauli mbiu hii isaidie kubadili fikra katika kuhakikisha tunafikia uchumi wa viwanda kwa kutoa umuhimu kwa mwanamke, mwanaume na taifa zima ili kuona ni kwa jinsi gani ataweza kushiriki katika kulifanikisha hilo.

Amemuagiza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi kuhakikisha Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wanatoa taarifa za kila robo mwaka za utoaji wa mikopo inayotolewa kwa vikundi mbalimbali katika kila mkoa husika. 

“Nimesikitishwa na utoaji mikopo kwa wanawake maana nimetembelea kikundi cha Wanawake kwenye mabanda chenye watu 30 lakini wamepatiwa mkopo wa milioni moja ambao hauna tija kulingana na idadi ya wanachama hao” alisema.

Amesema kuwa ushiriki wa wanaume ni muhimu katika kufikia suala la kijinsia na maendeleo endelevu katika Taifa letu kwani wanaume ni sehemu kubwa katika kuwezesha mwanamke kiuchumi.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano iliandaa na kutekeleza Mpango Mkazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto zikiwemo mimba na ndoa za utotoni ambazo ni kikwazo kwa Maendeleo ya wanawake na Mtoto wa kike nchini.


Serikali imeendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoka Bilioni 8 mwaka 2015 hadi Bilioni 16 kwa mwaka 2017/18 kiasi ambacho ni mara mbili zaidi hivyo kuongeza nguvu katika kumuwezesha mwanamke kiuchumi.

Amewataka wanawake kundokana na unyonge uliopo na kusimama na kujitoa na kupambana hasa katika kugombea nafasi za maamuzi katika uongozi na pia kupendana na kuinuana katika kupeana taarifa na fursa mbalimbali za kimaendeleo.

Aidha ameitaka jamii katika maeneo ya kazi kuondokana na rushwa za ngono jambo ambalo ni tatizo katika upatikanaji wa haki za wanawake na waajiri wa Sekta za Binafsi ni muhimu kuzingatia usalama na haki za wanawake wafanyakazi.

Akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Philis Nyimbi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana amesema mkoa unatekeleza mikakati mbalimbali katika kumuwezesha Mwanamke na Mtoto wa kike kwa kumuweka mbali na Vitendo vya Ukatili dhidi yao ili kuwawezesha kupata fursa zitakazowezesha kufikia usawa wa kijinsia.

Ameongeza kuwa Mkoa unaendelea na Kampeni za kutoa elimu kwa wananchi katika suala zina la kupinga Ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza vitendo hivyo.

“Katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa kuanzisha Kamati za ulinzi wa Mwanamke na Mtoto kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Kata, Mitaa na Vijiji na kuimarisha utendaji wake ili zisaidie kupambana na Vitendo vya Ukatili katika sehemu zao” alisema.

Akitoa Salamu kwa Wanawake Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula amesema kuwa katika Siku hii mwanamke anatakiwa kujitambua na ni wakati wa wanawake kusimama na kufanya Maendeleo na mwanamke asiyesimama imara mambo mengi huharibika na wanayofursa za kuunga mkono juhudi za mapambano ya kumuwezesha mwanamke.

“Tushikamane mikono wenyewe kwa wenyewe tujikombe sisi kama wanawake ili kuondokana na ukandamizaji na kusisimama na kuwa na sauti moja ili kujiletea Maendeleo yenye fikra chanya” alisema


Naye Mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez amesema kuwa Umoja wa Mataifa unataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia na kuondoa vikwazo vyote vinavyosababisha kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia kama vile mimba na ndoa za utotoni ambazo zimekuwa zikiwanyima fursa watoto wa kike kutimiza ndoto zao.

Ameongeza kuwa mapambano ya usawa wa kijinsia yatafanikiwa pale yatakaposhirikisha wanaume na wavulana katika kuhakikisha wasichana na Wanawake wanapata fursa sawa katika kutikiza ndoto zao.

Kwa upande wake Mwakikishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women Bi. Hodan Addou amesema kuwa Shirika hilo linashirikiana na Serikali na Mashirika ya kitaifa kuhakikisha elimu inatolewa na usawa wa kijinsia unakuwa suala la kipaumbele katika Jamii zetu.

Akizungumzia kuhusu Kampeni ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto msanii Nurdin Bilal maarufu kama Shetta amesema lengo la Kampeni hiyo ni kubadili fikra wanaume ambao ni watendaji wakubwa vitendo vya Ukatili Dhidi ya wanawake na Watoto.

Ameongeza kuwa Ukatili wa kijinsia hauathiri wanawake pekee bali hata wale ambao wanaowazunguka hasa Watoto hivyo amewaasa wanaume kuachana na vitendo vya kikatili kwa wanawake.

“Mimi nina amini ukimthamini Mwanamke unaleta maendeleo katika Taifa kwani mwanamke ni nguzo ya Maendeleo kwa Taifa” alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wanawake Mkoa wa Mwanza Bi. Grace Bunyinyiga amesema kuwa bado mwanamke ana vikwazo vingi katika kuleta chachu ya Maendeleo na kuna haja ya kuwakomboa wanawake wenyewe kifijra wawe mabadiliko katika Jamii husika.

“Wanawake wa Mkoa wa Mwanza wawe kipaumbele katika kuhakikisha uwepo wa usawa wa kijinsia katika Jamii zao na ushiriki wa wanaume na kuondokana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ili kuondokana na vitendo vya kikatili” alisema

Katika Maadhimisho hayo Waziri Ummy Mwalimu alizindua Kampeni ya Kupambana na kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ijulikanayo kama SAWA inayoratibiwa na Msanii SHETTA.

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI SHEREHE ZA MWAKA MPYA 2019 NA MABALOZI WANAOWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika Sherehe za Mwaka mpya 2019 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika Sherehe za Mwaka mpya 2019 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Kiongozi wa mabalozi haonekani pichani wakati wa Sherehe za Mwaka mpya 2019 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kabla ya chakula cha jioni alichowaandalia Mabalozi hao katika Sherehe za Mwaka mpya 2019 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

FARU 12 KUINGIZWA NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wizara ya maliasili na utalii Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund inatarajia kuingiza faru 10 nchini kwa ajili kuongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini.

Kuagizwa kwa Faru hao kutaongeza idadi yao kutoka 2 walioagizwa na taasisi hiyo hapo awali hadi kufikia 12.

Akizungumza katika kikao kilichowahusisha wadau hao wa uhifadhi kilichofanyika katika chuo cha Uhifadhi wa Wanyamapori cha Pasiansi jijiji mwanza, Prof. Mkenda amewashukuru wadau hao kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini.

Amesema Serikali itaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina yake na wadau wote wapenda maendeleo kwa lengo la kulinda na kukuza shughuli za uhifadhi wa wanyamapori nchini.

Prof. Mkenda amesema kuwa kuletwa kwa faru hao kutaongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini na kuongeza kuwa taasisi ya Grumeti imesaidia kuwaleta watu maarufu kutoka katika mataifa mbalimbali kuja kutembelea hifadhi za Taifa na hivyo kuchangia kutangaza utalii na kuongeza pato la Taifa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa idara ya wanyamapori Tanzania Canisius Karamaga akizungumzia kuhusu ujio wa Faru hao amesema kuwa jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo zinalenga kuwaongeza Faru hao hapa nchini.

Ameongeza kuwa Faru hao wataingizwa nchini kwa lengo la kuboresha kizazi cha wanyama hao waliokuwa hatarini kutoweka ikiwa ni moja ya juhudi za kuwafanya waongezeke kwa kuzaliana na wale waliopo nchini.

Amesema kikao hicho kati ya wizara na wadau hao ni muhimu sana kwa kuwa kimejadili na kuangalia kwa utalaam Zaidi namna Faru hao watakavyoingizwa nchini, kutunzwa na kulindwa kwa kuwa wanyama hao ni adimu na muhimu kwa utalii.

Amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele kulinda rasilimali za nchi ili ziwe na faida kwa vizazi vijavyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda akisalimiana na watumishi wa Wizara hiyo kutoka katika taasisi za Uhifadhi wa Wanyamapori na wadau kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund inayotarajia kuingiza faru 10 kwa ajili kuongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini.
Wadau wa Uhifadhi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund wakifuatilia kikao cha pamoja kilichowahusisha viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na watumishi wa Wizara hiyo kutoka katika taasisi za Uhifadhi wa Wanyamapori, kikao hicho kimefanyika katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori, Pasiansi jijini Mwanza.
Baaadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka katika taasisi za Uhifadhi wa Wanyamapori wakiwa katika kikao cha pamoja na Wadau wa Uhifadhi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund kilichofanyika katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori, Pasiansi jijini Mwanza.PICHA/ Maliasili na Utalii-Mwanza.
 

WAFANYAKAZI WA DAWASA WASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Wanawake ambao ni Wafanyakazi wa Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) leo wameungana na akinamama wa jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Wafanyakazi hao waliingia na bango lenye ujumbe wa kumshukuru rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweza kumtua mama ndoo kichwani huku wakiwa wamebeba ndoo ya maji ikiwa ni ishara.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo katika ujumbe wake aliishukuru Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka kwa kuweza kufika asilimia 60 ya utoaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani. 
Pia katika salamu zake Mhe Makonda amewataka akinamama wote kuacha kuwa mstari wa nyuma katika kufanyakazi bali wajitokeze katika kupigania haki zao kwa usawa bila kujali jinsia yao. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia hotuba ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
Wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia hotuba.
 Akinamama wa jiji la Dar es Salaam walifurika katika ukumbi wa Mlimani City kuhudhuria katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
 Mwimbaji Stara Thomas akitoa burudani
 Akinamama kutoka nchini Kenya ambao waliungana na wenzao katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani.
 Msanii Mrisho Mpoto akitoa ujumbe kwa akinamama wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

KUELEKEA MIAKA 25 AZIMIO LA BEIJING,WADAU WAKUTANA KUTATHIMINI MUSTAKABALI WA JUHUDI ZA UKOMBOZI WA MWANAMKE NCHINI

$
0
0
Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyolenga kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing hapo mwakani.

Mwenyekiti wa TGNP Mama Assen Muro akitoa rai kwa wadau wote kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazosimama kama vikwazo ili wanawake waweze kupiga hatua katika kufikia maendeleo endelevu. Mwenyekiti wa TGNP Mama Assen Muro akimueleza jambo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa alipowasili kwenye warsha hiyo.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza na washiriki wa warsha hiyo ambapo aliwahimiza kutorudi nyuma katika jitihada za kutetea haki na nafasi ya mwanamke katika jamii.

Na Mwandishi Wetu,

Ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kilele ni tarehe 8 ya mwezi Machi kila mwaka,wadau mbali mbali wamekutana jijini Dodoma kujadili na kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing hapo mwakani.


Warsha hiyo siku moja ambao iliyowakutanisha washiriki zaidi ya 100 kutoka kote nchini  wakiwemo wadau mbalimbali likiwajumuisha wanawake wakiwakilisha  makundi mbalimbali,wabunge,madiwani,wanasheria,waandishi wa habari pamoja na wanafunzi wa vyuo na sekondari,iliandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na TAWLA, Landesa, Msichana Initiative, Haki Ardhi, Haki Elimu, Care International na TAMWA.

Mkutano huo wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 ulilenga kuwashirikisha na kuwawezesha wanawake katika maendeleo ili kuimarisha mapambano dhidi ya umaskini na hiyo yote ni kwa wanawake kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.

Katika kuhakikisha kila mshiriki anachangia mawazo,ilitumika njia ya kuwagawa katika makundi na kujadili maana,uelewa,umuhimu,mitizamo pamoja na changamoto la azimio la Beijing katika jamii na nchi kiujumla ambapo miongoni mwa hoja zilizoibuliwa katika kuboresha jitihada za kuleta usawa wa kijinsia  ni pamoja na elimu juu ya azimio bado inahitajika sambamba na ushirikishwaji wa jamii yote kwa ujumla sambamba na kueleza faida ya usawa wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia ili kutengeneza kizazi chenye kuelewa manufaa yake.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanasimamiwa na kauli mbiu inayosema Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu”.

Wawakilishi wa wanawake wa jamii ya wafugaji wilayani Mvomero wakiongozwa na mwenyekiti wa umoja huo Bi. Mariam Simango (wakwanza kushoto) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika warsha hiyo.

 Akifafanua lengo la warsha hiyo, Mary Ndaro kutoka Care International aliwaambia washiriki kwamba warsha hii ni fursa kwa wanawake kurejea azimio la Beijing imefanikiwa kwa kiasi gani na kujua ni zipi jitihada za kuongeza ili kuendelea kuikwamua hali ya mwanawake katika jamii . Kundi liliojumuisha wanafunzi katika ngazi zote pamoja na vijana likiwa makini kujadili mitazamo na uelewa juu ya azimio la Beijing ambapo kufikia 2020 litatimiza miaka 25 ya maazimio. Akichangia wakati wa majadiliano ya katika makundi,mbunge wa Mtera Mhe.Livingstone Lusinde alisisitiza kuwa azimio la Beijing halina azma ya kuwafukuza wanaume kutoka nafasi zao katika jamii, bali ni juu ya kuinua wanawake kwa hali ya juu ili waweze kupata haki zao kama wanaume na kufanya kazi pamoja kwa maendeleo ya nchi. Anna Marwa kutoka Pelum Tanzania akichangia jambo wakati wa majadiliano ya makundi yaliyolenga kupima umuhimu,mitazamo na uelewa juu ya azimio la Beijing miongoni mwa washiriki wa warsha hiyo.   Zawadi Kondo mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha majibu kwa niaba ya kundi lililojumuisha wanafunzi katika ngazi zote pamoja na vijana.

Washiriki wakifuatilia kwa karibu mawasilisho.

Mdau wa masuala ya wanawake ambaye pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Rachel Chibwete akiwasilisha majibu kwa niaba ya kundi lililojumuisha wabunge,madiwani pamoja na waandishi wa habari. Wanafunzi kutoka shule ya sekondari Manchali iliyopo Chamwino jijini Dodoma wakicheza kuashiria furaha yao kutokana na fursa ya kushiriki katika warsha hiyo. 

Washiriki wakishikana mikono kama ishara ya umoja na mshikamano ambayo kwa pamoja waliafiki kuwa ni nguzo muhimu katika kufanikiwa kuitetea nafasi ya mwanamke katika jamii.


 Sehemu ya washiriki wakipata picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa 
Waandaaji nao hawakuwa nyuma kupata kumbukumbu na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa 

    TFDA KANDA YA KATI YAANZA KUTOA ELIMU KUHUSU MADHARA YA VIPODOZI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI

    $
    0
    0
      Na Jumbe Ismailly SINGIDA

    MAMLAKA ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Kati Dodoma imeanza kutoa mafunzo ya namna ya kudhibiti natumizi ya vyakula,dawa,vipodozi pamoja na vitendanishi kwa lengo la kutoa elimu kwa shule 30 za sekondari zenye jumla ya wanafunzi 12,000.

    Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Kati,Abeli Daule aliyasema hayo alipokuwa akitoa elimu juu ya bidhaa ambazo Mamlaka ya Chakula naa Dawa inadhibiti zikiwemo bidhaa za chakula,dawa,vifaa tiba na vitenganishi katika shule nane za sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Singida.

    Aidha Daule ambaye pia ni Afisa elimu kwa umma wa TFDA aliweka bayana lengo la kutoe elimu katika shule za sekondari kuwa ni sehemu za kazi ya Mamlaka hiyo kutoa elimu na kwamba sekondari ni wanafunzi wengi ambao tayari wanajitambua, kukiwepo watumiaji.

    “Lakini pia sekondari wanafunzi ambao wengi tayari wanajitambua kwa maana kwamba wengine ni watumiaji lakini na wengine majumbani kwao wanatumwa,lakini pia ni muda ambao wakipewa elimu wanaweza kujua kufanya uchaguzi sahihi lakini pia watapeleka elimu hiyo nyumbani.”alisisitiza Mkaguzoi huyo.

    Kwa mujibu wa Daule endapo wanafunzi hao wa sekondari watapatiwa elimu itasaidia pia kwa namna moja au nyingine kuwadhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu wenye utamaduni wa kuikwepa serikali wanapobaini Mamlaka hiyo inafanyakazi, huamua kufunga biashara zao kutoweka kabisa.

    “Kwa hiyo utaratibu huo ni wa taasisi kwa maana kwamba Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati katika utekelezaji wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019 basi tumeona tupite katika hizi shule ili tuweze kuwapitia.”alibainisha Daule.

    Naye Kaimu Afisa elimu sekondari wilaya ya Singida,Wolta Jenaeli aliweka bayana manufaa ya mpango huo utasaidia kwa akiasi kikubwa sana kwenye shule 30 zilizopo katika Halmashauri hiyo kupunguza madhara yatokanayo na vipodozi hususani kwa wanafunzi wa kike ni makubwa sana.

    “Kwa hiyo ina maana tunapunguza zinazotokea kwenye mashule yetu kwa sababu umri wa watoto wetu walionao kutumia kila kitu bila kujua madhara yake ni yapi.”alisema kaimu afisa elimu wilaya ambaye pia ni afisa elimu sekondari wa wilaya hiyo.

    Alizitaja baadhi ya shule za sekondari zilizopatiwa elimu hiyo kutoka TFDA kuwa ni pamoja na Ntonge,Amana,Mrama,Kijota, Kijota Hull,Mtinko,Singitu na Mikiwu.

    Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi walionufaika mpango huo kutoka shule ya sekondari Kijota,Hajra Juma alisema mpango huo utawasaidia baadhi ya wanafunzi walioanza kutumia vipodozi hivyo endapo wataendelea kutumia vipodozi hivyo.
     Mmoja wa Maafisa wa TFDA Kanda ya Kati akielezea madhara ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kutumika kutokana na muda wake wa matumizi kwisha alipokuwa akitoa elimu ya madhara hayo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Ntonge,wilaya ya Singida Vijijini.  
     Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Kati,Abeli Dauli akitoa elimu katika shule ya sekondari Singitu,Halmashauri ya wilaya ya Singida juu ya madhara ya matumizi ya vipodozi vilivyokwisha muda wake. 
    Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kijota wakiwa katika viwanja vya shule hiyo wakiwasikiliza  maafisa wa TFDA kutoka Kanda ya Kati walipokuwa wakitoa elimu juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya vipodozi vyenye viambato vyenye sumu.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

    THTU:Mkakati unahitajika katika kupunguza idadi ya watoto wenye kichwa kikubwa na Mgongo wazi.

    $
    0
    0

    Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

    Chama cha wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) kimesema katika kupunguza vifo vya Watoto chini ya miaka mitano nchini, lazima jitihada za kimkakati zichukuliwe katika kupunguza ongezeko la kuzaliwa Kwa watoto wenye ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi.

    Akizungumza na wazazi wa Watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi waliopo katika kituo cha Uzima Mission Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake THTU Taifa Salma Fundi amesema katika kusherekea siku ya wanawake wameona kuna umuhimu wa kujua hali ya Watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi na kueleza jamii juu ya tatizo hilo na kutaka wadau kuongeza nguvu katika utaoaji wa elimu kwa wanawake pindi wanawake wanapokuwa wajawazito lakini pia utoaji huduma Kwa watoto wenye hali hiyo kwani wanamahitaji mengi. 

    Fundi amesema kuwa matatizo ya ugonjwa huu kwa Watoto wakati mwingine hutokana na kukosa elimu juu ya matumizi ya vidonge vya Folic acid, hivyo kama elimu ikitolewa kwa msisitizo tatizo hili linaweza kupungua  kuliko ilivyosasa.

    Taasisi mbalimbali na Jamii kwa ujumla, lazima tubadilike na kuweka mkakati juu ya Watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi ili kufikia malengo yakupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano, kupunguza gharama za matibabu kwa serikali pamoja na umaskini kwani mama mwenye mtoto wa ugonjwa huo huwa hawezi kuzalisha na kubaki tegemezi kipindi chote cha kuuguza.

    Katika kuadhimisha siku hiyoTHTU kwa kushirikiana na wadau wengine ( NMB Bank Tawi la Morogoro Road na kampuni ya HQ wamepeleka msaada wa kadi za bima ya Afya kwa Watoto 12, vipima Joto kumi na katoni Moja ya pampers ikiwa ni kuchangia huduma za Afya kwa watoto hao. 

    Nae Mratibu wa Chama cha Wazazi wenye Kichwa kikubwa na Mgongo Wazi Hidaya Alawi amesema chama kinawatoto zaidi 1200 ambao hao wamefikishwa katika sehemu za huduma za Afya. Alawi anasema japo kundi kubwa la watoto wenye tatizo hili bado hawajafikishwa kwenye huduma.

    Nae Mkurugenzi wa Youth With A Mission Tanzania Jeremiah Kiwinda amesema kuwa baada ya kuona wazazi wanaotoka mikoani na kuja Hospitali ya Muhimbili kwa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wakaona kuna umuhimu wa kuwapatia malazi na chakula ili kuwaokolea gharama kwa huduma hizo katika Kituo cha Uzima Mission ni Bure.

    Amesema kuwa wakiwa katika kituo hicho wanapatiwa mazoezi kwani bila kufanya hivyo kutokana na gharama mbalimbali akiruhusiwa wazazi wengi ni vigumu kurudi.
     Kaimu Katibu wa Kamati ya Wanawake THTU  Roselyne Massam akimkabidhi bima ya afya mmoja ya wazazi wenye watoto wenye Kichwa na Mgongo Wazi katika kituo cha Uzima Mission wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
     Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake THTU Taifa Salma Fundi akipeana na Mkona na mmoja wazazi wenye kichwa kikubwa na Mgongo Wazi ikiwa shukrani ya msaada katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
     Picha ya pamoja ya wadau waliojitokeza kutoa msaada wakiwa na viongozi wa Kituo cha Uzima Mission na wazazi wenye watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi waliokaa chini katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

     Mratibu wa Chama cha wazazi wa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi Hidaya Alawi akizungumza kuhusiana na malezi ya watoto hao na mahitaji wanayotakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
    Wazazi wenye watoto wa kichwa kikubwa na mgongo wa wazi wakipokea msaada wa pampers  ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

    AGA KHAN FANYENI MAPITIO YA GHARAMA ZENU-MAJALIWA

    $
    0
    0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Binti Mfalme Zahra Aga Khan (wapili kushoto) wakifungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi, 9, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamaii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zaynab Chaula, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa, (Agence Francaise de Developpment)

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Binti Mfalme Zahra Aga Khan baada ya kufungua awamu ya pili ya hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019.
    Baadhi ya waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpokea mtoto Claribel Mwakatumbula (1)  kutoka kwa mama ya Delfina Audax wakati alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali hiyo, Machi 9, 2019. Mtoto Claribel amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amembeba mtoto, Claribel Mwakatumbula (1) wakati alipotembelea wodi ya watoto kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mtoto Claribel amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mtoto Ilham Ally wakati alipotembelea wodi ya watoto kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mtoto Ilham amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.
    Wazari Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Jackline Vicent aliyejifungua mtoto Lois Ladislaus katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mheshimiwa Majaliwa alitembelea wodi ya wazazi kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa haospitali hiyo
     ……………………………

    SERIKALI imeutaka Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), ufanye mapitio ya gharama za afya katika hospitali ya Aga Khan ili wananchi wa kawaida waweze kumudu na kunufaika na huduma za tiba wanazozitoa.

    Imeelezwa kuwa pamoja na jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya, pia inatambua mchango unaotolewa na taasisi zisizo za Kiserikali ikiwemo Hospitali ya Aga Khan katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kisasa.
    Hayo yamesemwa leo (Jumamosi, Machi 9, 2019) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

    Amesema upanuzi wa hospitali hiyo ni miongoni mwa jitihada za kuwafikishia Watanzania huduma za afya katika maeneo yao na kwa ngazi zote na kwa gharama nafuu, hivyo amewataka watoa huduma wote nchini waangalie upya gharama zinazotozwa katika huduma mbalimbali hususan za matibabu.

    “Mtakubaliana nami kuwa gharama zikiwa kubwa hazitawanufaisha wananchi hususan wa kipato cha chini na wananchi hawataona unafuu wa kutibiwa nchini na nje ya nchi, hivyo fanyeni mapitio ya gharama hizo.”

    Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua gharama kubwa za uwekezaji na uendeshaji wa shughuli za afya nchini hususan kwa sekta binafsi. “Lengo la Serikali kutoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya taasisi zisizo za kiserikali kama Aga Khan ni kuwezesha huduma zinazotolewa kuwa nafuu.”

    Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeanzisha na kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na mwitikio wa ni mkubwa na lengo lake ni kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya matibabu tena kwa uhakika.

    “Nitoe wito kwa taasisi zote zisizo za Serikali kuunga mkono jitihada hizi za Serikali na kuhakikisha wananchi wote wananufaika na huduma zenu kupitia mfumo huu bila kubaguliwa.”

    Pia ameutaka uongozi wa Hospitali ya Aga Khan na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakamilishe majadiliano yao katika matumizi ya NHIF kwenye hospitali hiyo ya rufaa. “Dr. Konga Mkurugenzi Mkuu wa NHIF upo hapa kamilisheni mjadala.”

    Amesema nia ya Serikali ni kuona wananchi wanakwenda hapo kwenye jengo hilo zuri na wanapata huduma kupitia bima ya afya. “Ni matumaini yangu kwamba jambo hili litafanyiwa kazi kwa kuzingatia maslahi mapana ya pande zote mbili.”

    Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuhakikisha uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji, kuimarisha amani na utulivu, ambapo ametoa rai kwa sekta binafsi ziendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo nchini kwa kuzingatia sheria za nchi, utamaduni na mila za Watanzania.Awali, Waziri Mkuu alitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma katika jengo hilo ikiwemo maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya watoto, wodi ya wazazi. Ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu sh. bilioni 192, kati yake sh. bilioni 134 ni mkopo wa muda mrefu wenye masharti nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).

    Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameupongeza Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan kwa upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwani unakwenda kuboresha huduma za afya nchini.

    Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kutolea huduma za afya ambapo kwa sasa imeanzisha ushirikiano na sekta ya umma na binafsi kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.

    NayeBalozi wa Ufaransa nchini, Balozi Frederic Claiver amesema awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali hiyo utasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya Tanzania.

    Pia Balozi huyo amesema Ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha inatimiza mkakati wake wa kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025.

    LOWASSA ALIVYOPOKELEWA MONDULI KWA KISHINDO

    $
    0
    0

    Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa akizungumza leo mara baada ya kupokelewa rasmi Ccm Monduli, kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Loata Sanare, kulia kwake ni Katibu wa Itikadi nauenezi CCM Taifa Humphrey Polepole. Picha na habari na Vero Ignatus
    Katibu wa Itikadi na uenezi Taifa Humphrey Polepole, Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa na Mwenyekiti wa CCM mkoa Alota Sanare wakiwa wameshikana mkono kama ishara ya Umoja
    Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa akisalimiana na wanachama wa Ccm waliofurika katika ofisi ya CCM wilaya ya Monduli leo
    Lowasa akiwapungia wanachama wenzake wa CCM leo
    Wanachama wa CCM wakiwa katika uwanja wa Ofisi ya CCM wilaya ya Monduli leo.

    Katibu wa Itikadi na uenezi Huphrey Polepole akizungumza katika uwanja wa ofisi za CCM wilaya ya Monduli mkoani Arusha leo.
    Baadhi ya wanachama wa CCM waliofurika katika ofisi,za CCM wilaya ya Monduli leo
    Mbunge wa CCM wilaya ya Monduli Julius Kalanga akishuhudia tukio la kurudi rasmi CCM na kukabidhiwa kadi ya uanachama katika ofisi ya CCM wilaya ya Monduli


    Na. Vero Ignatus, Monduli

    Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Edward Lowasa amepokelewa Leo rasmi kurudi katika chama cha mapinduzi na mwenyekiti wa katibu wa itikadi nauenezi wa chama hicho Humphrey Polepole

    Akizungumza mara baada ya kukaribishwa rasmi Lowassa amewashukuru watanzania milioni 6 waliompigia kura mwaka 2015 na kuwaomba kura hizo waje kumpa rais Magufuli

    Amesema kuwa ameamua kurudi Ccm kwa kuvutiwa na kazi anazozifanya Dkt. Magufuli hivyo amewasihi wana monduli kumuunga mkono kwa kazi anazozifanya kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania

    '' Nimerudi nyumbani, sina maneno mengi ila nasema nimerudi nyumbani, Chadema nawashikuru sana neno langu kuu nasema nawashukuru, msinilishe maneno mdomoni"alisema Lowassa

    Lowassa amesema kuwa wananchi wa Tanzania wanathamini sana Amani nakuwataka watanzania wasisikilize maneno ya kibaguzi bali wailinde Amani iliyopo kwani jambo la msingi

    '' Mwalimu nyerere aliwahi kuhutubia halmashauri kuu ya ccm Taifa na kutueleza kuwa kuna viongozi wa aina mbili ambapo ni bookkikeeper na visionary leader '' alisema Lowassa, Amesema kuwa visionary leader ni kiongozi anayetazama miaka 50 ijayo atafanya vitu gani '' Nimekuwa nikisikia maneno ya kibaguzi kwamba mtu akienda kwa Lowassa anapelekwa jina kwa mkuu wa wilaya achaneni na hayo maneno hayana ukweli tuoendane, mwuislamu ampende mkristo ili amani iendelee''. Alisema

    Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Loata Sanare amesema kuwa wote waliokwenda upande wa pili wa upinzani wakitaka kurudi lazima wafuate utaratibu kama Lowassa kwani Lowasa licha ya kupokelewa na mwenyekiti wa ccm Taifa aliandika barua kwenye tawi.

    '' Wote ambao mnataka kurudi ombeni kwa kufuata utaratibu, Wengi wenu mmevaaa nguo za ccm lakini siyo wanachama bali ni washabiki wa ccm"

    Amesema kuwa wanamkaribisha nyumbani mhe. Lowasa ila wangemshangaa kama aangeendelea kubaki kwenye kundi la ajabu ajabu, Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na uenezi CCM Huphrey Polepole amesema kitendo alichokifanya kuwa Mhe. Lowassa ni cha ukomavu wa kisiasa ametangaza tutangulize mbele maslahi ya Taifa na kuilinda Amani ya nchi

    POLEPOLE amesema kuwa Lowassa amefuata taratibu zote za chama cha mapinduzi hivyo wamejadili na kuona anafaa kurudi CCM bila kuleta madahara katika chama hicho,Sambamba na hayo wanachama wengi waliokuwa chadema wamerudisha kadi zao na kujiunga na CCM ambap0 Ikumbukwe kuwa Lowasa alijiunga Chadema 2015 na kuchaguliwa kuwa mgombea wa Urais wa chama hicho na machi mosi 2019 alirudi rasmi CCM
    Viewing all 46389 articles
    Browse latest View live




    Latest Images