Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46367 articles
Browse latest View live

RAIS WA JAMHURI YA RWANDA PAUL KAGAME KUWASILI KESHO NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI

$
0
0
Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, atawasili nchini tarehe 7 Machi 2019 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Ziara hiyo inafanyika kufuatia mwaliko wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Ziara hii itatoa fursa kwa viongozi hao wawili kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Aidha, Viongozi hao wanatarajia kuzungumzia masuala mbalimbali ya mtangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Mhe. Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda, atawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa Tisa Alasiri tarehe 7 Machi 2019 na kupokelewa na mwenyeji wake, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Mhe. Rais Kagame anatarajia kuondoka nchini tarehe 8 Machi, 2019. 


Imetolewa na: 
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dodoma. 

6 Machi 2019

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI,MACHI 7,2019

RAIS MAGUFULI ASAMEHE KODI GARI MBILI ZA KUBEBEA WAGONJWA (AMBULANCE)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe , Dkt. John Pombe Magufuli amezisamehe kodi gari mbili za kubebea wagonjwa (Ambulance ) aina ya Mercedes Benz kwa ajili ya Hospital za Halmashauri mbili za Ortumet iliyopo Arusha Dc na Tengeru iliyopo halmashauri ya Meru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe , Dkt. John Pombe Magufuli amezisamehe kodi gari mbili za kubebea wagonjwa (Ambulance ) aina ya Mercedes Benz kwa ajili ya Hospital za Halmashauri mbili za Ortumet iliyopo Arusha Dc na Tengeru iliyopo halmashauri ya Meru.

Mhe. Magufuli amefikia hatua hiyo kufuatia ombi la Mkuu wa wilaya ya Arumeru kwa Katibu wa NEC itikadi na uenezi Ndugu Humphrey Polepole ambae pia ndie mlezi wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha alipofanya ziara katika wilaya ya Arumeru kujionea kazi mbalimbali za utekelezaji wa ilani ya chama katika wilaya ya Arumeru ambapo Dc Muro alimuomba Ndugu polepole awaombe kwa Mhe Rais Magufuli ambae pia ni Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Taifa ili waweze kupata msamaha wa kodi.

Akizungumza mara baada ya Mhe. Rais Magufuli kukubali kuzisamehe kodi ambulance hizo za kisasa ambazo zimepatikana kwa jitihada za Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akishirikiana na mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dkt Wilson Charles Mahera kutoka kwa marafiki wa asasi inayoshirikiana na wajerumani .
 
 Ndugu polepole amesema Mhe Rais katika kuhakikisha anaendelea kuboresha sekta ya afya katika wilaya ya Arumeru pamoja na kutoa zaidi ya bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vya Usa river Halmashauri ya Meru na Nduruma pamoja na mbuyuni Halmashauri ya Arusha pia ameelekeza magari hayo ya wagonjwa yapelekwe kwenye hospital hizo mbili za wilaya ambako yamesamehewa kodi na kuingizwa katika mfumo wa vifaa vya hospital hizo.

Dc Muro amemshukuru sana Mhe Rais Magufuli kwa kukubali kuwasaidia kusamehe kodi magari hayo , ambapo Kupatikana kwa magari haya mawili ya kubebea wagonjwa kumeendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya Mkuu kuu wa wilaya ya Arumeru ya kuwahudumia wananchi wa Arumeru baada ya kukabidhi gari lingine la doria kwa jeshi la polisi wilaya ya Arumeru ambalo kimekarabatiwa kwa juhudi za mkuu wa Wilaya na wadau wa maendeleo


 

MBUNGE MAVUNDE AWATAKA WANAWAKE DODOMA MJINI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amewataka wanawake wa Dodoma Mjini kuchangamkia fursa za kiuchumi na kutokubali kukatishwa tamaa kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi ili kujijengea heshima kubwa katika jamii.

Mavunde ameyasema hayo leo asubuhi katika kongamano lilioandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania(CWT) kitengo cha Wanawake katika Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha siku ya MWANAMKE DUNIANI.

“Natamani kuwaona wanawake wa Dodoma mkiwa mbele kuchangamkia fursa za kiuchumi ili kujijengea nguvu ya kiuchumi na kujiongezea kipato.Dodoma hivi sasa baada ya tamko la Makao Makuu fursa nyingi sana zimejitokeza hivyo msilaze damu kwa kubaki kuwa waangaliaji na badala yake na ninyi mshiriki moja kwa moja”Alisema Mavunde

Akisoma Risala kwa niaba ya walimu hao kitengo “KE” Mwl Joyce Kaishozi ameeleza kwamba Chama hicho kimejipanga vyema kumjengea uwezo mwalimu mwanamke ili jamii kutambua nafasi ya Mwalimu Mwanamke na ndio maana katika kongamano walimu wamepata nafasi kupata mafunzo katika maeneo ya AFYA,*UJASIRIAMALI na UONGOZI BORA.

Kongamano hilo pia lilihudhuriwa na Mjumbe Wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa Mkoa wa Dodoma Ndg Leila Burhan Ngozi na Mbunge wa Viti Maalum-Dodoma Mh Felister Bura

MPINA AONGOZA NCHI WANACHAMA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI UTIAJI SAINI UDHIBITI UVUVI HARAMU

$
0
0

Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Mhe Luhaga Mpinaa mbaye ndiye Makamo Mwenyekit i(mwenyemiwani) wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO),inayojumuishanchiwanachamawa Afrika Mashariki akiangalia taarifa aliyotia saini ya makubaliano yakuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katikaZiwa Victoria mara baada ya kumaliza kuendesha kikao hicho jijini Arusha.Kushotoni Waziri waKilimo,WanyamanaUvuviwa Uganda, VincentBamulangakiSsempijja, kushotoniKatibuMkuuwaUvuviwa Kenya Prof. Micheni Ntiba aliyemwakilisha Waziri wake anayefuata niDkt.Deo-Guide RUREMA Waziri waMazingira ,KilimonaMifugowa Burundi. Pichana John Mapepele
PichayapamojayaWatendaji,MakatibuWakuunaMawaziriwanaosimamiaSektayaUvuviwanchiWanachamawaJumuiyaya Afrika Mashariki baada ya kumaliza mkutano wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO) ambapoWaziri waMifugonaUvuviwa Tanzania MheLuhaga Mpina, ambaye ni Makamo Mwenyekiti wa Oganaizesheni(mwenye miwani kwa waliokaa msitari wa mbele) aliendesha kikao hicho kilicho malizika kwa kutilia na saini makubaliano ya kuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria.Pichana John Mapepele
Mawazirina Wawakilishi wa Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Uvuvi wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakionyesha taarifa waliyotia saini ya makubaliano yakuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria mara baada ya kumaliza kikao hicho jijini Arusha.Mwenye miwani niMheLuhagaMpina, Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania,Kushotoni Waziri wa Kilimo,Wanyama na Uvuvi wa Uganda, Vincent BamulangakiSsempijja,anayefuata ni Dkt. Shigalla Mahongo-KatibuMtendaji wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO), kulia ni Katibu Mkuu wa Uvuvi wa Kenya Prof. Micheni Ntiba aliyemwakilisha Waziri wake na anayefuata ni Dkt.Deo-Guide RUREMA Waziri wa Mazingira ,Kilimo na Mifugo wa Burundi.Pichana John Mapepele
Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania,Mhe LuhagaMpina ambaye ndiye Makamo Mwenyekiti wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO), inayojumuisha nchi wanachama wa Afrika Mashariki na Mgeniwa Rasmi wa Mkutano huo akisoma hotuba yake kwenye mkutano wa(LVFO)jijini Arusha.Pichana John Mapepele



Na John Mapepele- Arusha

Nchi wanachama wa Jumuiyaya Afrika Mashariki zimetiliana saini makubaliano ya kuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katika ziwa Victoria.

Makubaliano hayo ni mkakati wa nchi hizo za Kenya, Uganda na Tanzania, kulinda rasilimali hizo ziwe endelevu na zitumike kukuza uchumi wa wananchi wa mataifahayo. Makubaliano hayo yamefikiwa katika Mkutano wa Mawaziri waSekta za uvuvi zinazozungukwa naZiwa Victoria, uliofanyika Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika masharikiJijini Arusha, Tanzania.

Makamu Mwenyekiti wa Mawaziri wa Sekta za uvuvi wa Jumuiyahiyo, Mhehimi wa LuhagaMpina, alisema uamuzi huo utawezesha kuongezeka kwa samaki na mazao yake katika Ziwa Victoria. Alisema hatua hiyo itachochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa wananchi wanaozunguka ziwa hilo ikiwa ni pamoja na kuongeza kipato chao.

Alisema wananchi wa Afrika mashariki wanaozungukwa na ziwa Victoria walikuwa wanalazimika kuagiza samaki kutoka nchi ambazo hazina hata maziwa,licha ya ziwa hilo kuwa na uwezo wakulisha bara la Afrika kama litatunzwa vizuri.

Alisema samaki wachanga waliokuwa ziwani chini ya sentimita 50 walikuwa asilimia 96.3lakini kutokana na jitihada zilizofanywa za kudhibiti uvuvi haramu vifaranga vimepungua hadi kufikia asilimia 62.8 kiwango ambacho kinakubalika kwa vifaranga kuwepo majini.

Pia alisema samaki wanaoruhusiwa kati ya sentimita 50 hadi 80 waliokuwa wamebaki majini walikuwa asilimia 3.3 lakini baada ya kazi ya mwaka mmoja wameongezeka hadi kufikia asilimia 32 huku wale wenye urefu wakati ya sentimita 80 hadi 85 ambao ni samaki wa ziwalifikia asilimia 0.4 lakini kwa sasa wameongezeka na kufikia asilimia 5.2 kiwango ambacho kinakubalika.

Alizipongeza Taasisi za utafiti za Kenya, Uganda na Tanzania kwa umakini na umahiri wa kukusanya taarifa za kitafiti ilikuzisaidia nchi wanachama kupanga yale ya usimamizi warasilimali za uvuvi. “Tumefanya maamuzi makubwa ya kupanga mipango ya kufanya operesheni yapamoja ili kuwa na uwelewa wa mpango ya pamoja ya namna ya kulitunza ziwa letu na kupamba na na uvuvi haramu ya mazao ya uvuvi”alisema.

Nchi hizo zimekubaliana ziwe zimelipa madeni yote kufikia juni, mwaka huu ili kuwezeshaTaasisi ya Uvuvi ziwa victoria (LVFO) kutekeleza mipangoyake kwawakati.

AkizungumzakatikamkutanohuoKatibuMtendajiwaOganaizesheniyaUvuviwaZiwa Victoria (LVFO)Dkt. Shigalla Mahongo alisisitiza kuwa na umoja katika kuhifadhi raslimali za uvuvi katika ziwa hilo kwa kuwa idadi ya watu katika nchi wanachama wajumuiya ya Afika Mashariki kuwa ikikuwa kwa kasi na kuendelea kutegemea samaki wa ziwa hilo kwa kiasi kukubwa.

“Idadi ya watu ilikuwa milioni 23.5 mwaka 1954 wakati Sangara walipowekwa katika ziwa Victoria lakini mwaka 2018 inakadiriwa kuwa idadi ya watu iliongezeka kwa takribani mara 7 nakufikia jumla ya watu wapatao milioni 165.5 ambapo sasa inakadiriwa kufikia mwaka 2050 kuwa na zaidi ya watu milioni 323.1 hiyo inamaana kuwa itakuwa ni mara 14 ya idadi ya watu waliokuwa mwaka 1954 wakati ziwa likiwa bado nililelile” alionyaDkt. Mahongo.

BITEKO-MAISHA YA WATU YANATHAMANI KUBWA KULIKO SHUGHULI ZA MGODI

$
0
0
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko wa tatu kulia akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara wakielekea kwenye eneo la uchimbaji wa TSF kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Kigoma Malima.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akionyesha kwa kuuliza mwisho wa mpaka wa eneo la ujenzi wa TSF mpya, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya Tarime.

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekiiti wa kamati ya ulinzi na usalama na mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima wa kwanza kushoto akitoa taarifa fupi ya hali ya mkoa wake wakiwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Tarime.


…………………..


Na Issa Mtuwa – Tarime

Serikali imesema itaufunga mgodi wa North Mara ifikapo Machi 30, 2019 endapo mgodi huo utashindwa kuyadhibiti maji yenye sumu yanayo tiririka kutoka kwenye mabwawa ya kuhifadhia maji (topesumu) (Tailings Storage Facility -TSF).

ya mgodi huo kuelekea kwenye makazi ya watu.

Hayo yamesemwa leo machi 5, 2019 na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko alipotembelea mgodini hapo kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea mabwawa wa topesumu (TSF) na kuzungumza na uongozi wa mgodi na baadae na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyamongo wilaya ya Tarime kuzungumzia hatima ya malipo ya fidia za wananchi waliohamishwa kupisha shuguli za mgodi.


Biteko amesema serikali hairidhishwi na namna mgodi wa North Mara kwa jinsi wanavyo zingatia swala la utunzaji wa maji yenye sumu kwenye (TSF) zao. Amesema serikali inathamini sana maisha ya watu na mtu mmoja mmoja, na kwamba maisha ya mtu mmoja ni bora kuliko shuguli zote za mgodi.

“ Naomba niseme ukweli, tena kutoka moyoni, sijaridhishwa na hili jambo la utiririshaji wa maji yenye sumu kuelekea kwenye makazi ya watu. Serikali hii ya awamu ya tano ya Dkt. John Pombe Magufuli inathamini sana maisha ya watu wake kuliko kitu chochote. Thamani yamaisha ya mtanzania mmoja ni bora kuliko kinachochibwa hapa. Nitoe rai kwa mgodi ifikapo Machi 30, mwaka huu, hili jambo liwe limekwisha, kinyume cha hapo, nitafunga mgodi mpaka pale mtakapo tekeleza jambo hili” alisema Biteko.

Kwa upande wa uongozi wa mgodi umesema, utatekeleza agizo hilo na kwamba juhudi za kudhibiti topesumu kuelekea kwenye makazi ya watu limepewa kipaumbele na kwamba ndani ya muda huo litakuwa limekamilika.

Katika ziara hiyo, Waziri Biteko aliambatana na baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo akiwemo Kamishna wa Madini Mha. David Mlabwa na Afisa Madini mkoa wa Mara Mha. Nyaisara Mgaya, wengine ni kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa mara wakiongwa na mwenyekiti wake ambae pia ni mkuu wa mkoa wa Mara bwana Adam Kigoma Malima.

Ziara hiyo inafuatia vikao mbalimbali vya awali vilivyofanyika mwaka huu vikilenga masuala mbalimbali yanoyo husu mgodi huo likiwemo swala la udhibiti wa maji yenye sumu (topesumu) yanayo lalamikiwa na wananchi wanaoishi kuzunguka mgodi huo, kikao cha kwanza kilifanyika Januari 19, chini ya makatibu wakuu wa wizara saba ((Madini, Makamu wa Rais Mazingira (NEMC), Ardhi, TAMISEMI, Afya, Fedha na Maji)) ambapo serikali ilitoa miezi nane kutekeleza maagizo yaliyopewa.

BREAKING NEWZZZZ: MTANGAZAJI WA CLOUDS FM EPHRAHIM KIBONDE AFARIKI DUNIA LEO

$
0
0
Michuzi Media Group imepokea taarifa za mshituko na  masikitiko makuwa asubuhi ya leo, kufuatia kifo cha mtangazaji wa habari  wa Clouds FM,Ndugu Ephrahim Kibonde.

Taarifa zinaeleza kuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza ,Mh. John Mongella amethibitisha kufariki kwa mtangazaji huyo kutokana na kusumbuliwa na presha.

Imeelezwa kuwa Kibonde alianza kusumbuliwa na Presha tangu akiwa Bukoba kwenye msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba na baadae akahamishiwa Mwanza kwa uangalizi zaidi.

Aidha Mkuu wa vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga amethibitisha kufariki Dunia kwa Ephrahim Kibonde leo asubuhi katika hospitali ya Bugando,jijini Mwanza.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.

TUTAENDELEA KUWALETEA TAARIFA ZAIDI ,KADIRI YA ZITAKAVYOKUWA ZINATUJIA

MKE WA MAKAMU WA RAIS SMZ AONGOZA HARAMBEE MUHEZA YA KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI MAALUMU KWA AJILI YA WALEMAVU,ACHANGIA MILIONI SITA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WILAYA HIYO.

$
0
0

Mke wa Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Asha Suleiman Idd katika akiwa kwenye halfa hiyo kushoto ni Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye dhifa ya chakula cha mchana kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni maalum kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.

 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga akizungumza wakati wa halfa hiyo
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa halfa hiyo
 MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Nassib Mbaga akizungumza katika halfa hiyo
 MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Mama Asha Seif Iddi kulia akimtazama mtoto mwenye ulemavu wa viungo Maimuna Yahaya anayesoma shule ya Msingi Bagamoyo wilayani Muheza akikata keki kwa mdomo wakati wa halfa hiyo ya kuchangia watoto wenye mahitaji maalumu kwa kujenga mabweni ya wanafunzi wenye ulemavu na vifaa vya mahitaji hayo uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo
Mke wa Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Asha Suleiman Idd kulia akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa kwa kwanza kulia kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya kukagua mabanda mbalimbali vya kwenye dhifa hiyo
 Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda kushoto akimvalisha kofia mtoto mwenye ulemavu wa ngozi wakati wa dhifa hiyo
 Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda kulia akipewa mkono na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Nassib Mbaga mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake wakati wa halfa hiyo
 Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa kushoto akimkabidhi baiskeli mtoto mlemavu wilayani Muheza kwa ajili ya kumsaidia kuenda n ayo shule kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Mke wa Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Asha Suleiman Idd kushoto akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani Muheza mara baada ya kuwasili kwa ajili ya halfa ya  chakula cha mchana kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni maalum kwa ajili ya watoto wenye ulemavu kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Moyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa kushoto akisalimia na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jitegemee kwa ajili ya halfa hiyo
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto wakiteta jambo mara baada ya kuwasili kwenye halfa hiyo
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nassib Mbaga wakati wa halfa hiyo kulia ani Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu
 PRO wa Bandari ya Tanga Moni Jarufu akifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa hiyo
 Mwalikishi wa Bandari Tanga akiwa kwenye Halfa hiyo
 Sehemu ya wadau wa elimu akiwemo Nassoro Makau ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers akiwa kwenye halfa hiyo

MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Asha Suleimani Iddi ameongoza harambee maalumu ya kuchangia ujenzi wa mabweni maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wilayani Muheza huku akiitaka jamii kubadilika na kuhakikisha watoto hao wanapelekwa shule ili kupata elimu.

Alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa dhifa ya chakula cha mchana kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni maalum kwa ajili ya watoto wenye ulemavu ambapo alisema unyanyapaa, mazingira yasiyo rafiki katika shule imeelezwa kuwa ni miongoni mwa sababu za watoto wenye ulemavu kushindwa kupelekwa shule kwa ajili ya kupata haki yao ya kielimu.

Alisema kuwa bado jamii haijapa mwamko mkubwa wa kutoa fursa ya kuwapatia elimu watoto wenye ulemavu hali inayosababisha wengi wao kubaki majumbani tu

Alisema kuwa licha ya serikali kufanya jitihada kubwa za kuboresha mazingira ya kielimu katika maeneo mbalimbali lakini bado kundi hilo limekuwa likikabaliwa na changamoto ikiwemo uhaba wa vifaa visaidizivya kuwawezesha kusoma.

Aidha alisema mkakati huo wa  ujenzi wa mabweni wilayani humo utaweza kutoa fursa kwa watoto wengi wenye ulemavu kupata haki yao ya kusoma bila ya kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ambavyo vilikuwepo hapo mwanzoni

Hata hivyo aliwataka wazazi na walimu kuhakikisha wanawalinda watoto hao dhidi ya vitendo vyote viovu ikiwemo ubakaji pamoja na uzalilishaji wa kijinsia .

Mama Asha alisema kuwa mara tuu baada ya mabweni hayo kukamilika wazazi wanajukumu la kuhakikisha wanawatoawatoto hao na kuwapeleka shule kwa ajili ya kupata elimu badala ya kuwaficha. 
Katika hafla hiyo Mke huyo wa Makamu wa Pili wa Rais SMZ Asha alimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kiasi cha sh.milio sita (6000,000)

SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA AFUNGUA MKUTANO WA WANAWAKE, KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Spika Mstaafu Mh. Mama Anne Makinda akizungumza na wanawake katika mkutano wa majadiliano kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayofanyika Machi 8 Kila mwaka, Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha Wanawake Wanasheria TAWLA na Shirika la OXFARM unafayika kwenye hoteli ya Protea Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 
 
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la OXFARM Bw. Odokorach Francis akizungumza katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Protea Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake Wanasheria TAWLA Bi. Tike Mwambipile akikmaribisha mgeni rasmi ili kuzungumza na wanachama na waalikwa wa mkutano huo na kufungua mkutano huo.
 
Mary Matui Mwebdeshaji wa mkutakuhusu matukio mbalimbali yatakayofanyika kwenye mkutano huo.no huo akizungumza jambo 
Kulia ni Mkuu wa Mipango Chama cha Wanasheria Wanawake Mary Richard kulia na Mkamiti Mgawe Ofisa Ubia wa Miradi Oxfarm wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waalikwa wakiwa katika mkutano huo
 
Katikati ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akiwa katika mkutano huo kulia ni Mbunge wa jimbo la Hanang Dk. Mary Nagu na kushoto ni Mkutugenzi Mtendaji wa TAWLA Bi Tike Mwambipile.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akiimba wimbo maalum wa kuwahamasisha wanawake pamoja na Mbunge wa jimbo la Hanang Dk. Mary Nagu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akisalimiana na mmoja wa wanachama wa TAWLA wakati alipowasili katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawasheria Wanawake Bi. Tike Mwambipile akimuongoza Spika Mstaafu wa Bunge Mama Anne Makinda wakati akiingia kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA akiwaongoza wanawake kuimba wimbo maalum wa kuwahamasisha wanawake katika mkutano huo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akizungumza na Mbunge wa Hanang Dk. Mary Nagu kushoto ni Mama Kijo Bisimba mwanaharakati.
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akizungumzana baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA wa kwanza kulia ni Mbunge wa viti maalum Chadema Bi. Suzan Lyimo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mstaafu Mama Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mara baada ya kufungua rasmi.

Taxify kuanza kufahamika kwa jina la ‘Bolt’

$
0
0
KAMPUNI inayotoa huduma za usafirishaji Barani Afrika na Ulaya Taxify imebadilisha nembo na jina lake kuwa ‘Bolt’. 

Mabadiliko hayo ya alama ya utambulisho wa kampuni yamelenga kuenda sawia na malengo ya kampuni katika huduma za usafirishaji ambapo mpaka sasa tayari imepanua huduma za safari zake kwenye magari na pikipiki. 

Akizungumza na na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu mabadiliko hayo Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi mwenza wa Bolt, Markus Villig, alisema jina hilo jipya la Bolt litaanza kufahamika hatua kwa hatua katika masoko ya kimataifa katika wiki zijazo. 

Alisema Taxify ilizinduliwa miaka mitano iliyopita kwa malengo ya kutoa huduma za usafiri mijini kwa njia rahisi na bei nafuu. 

“Kampuni hiyo ya kiteknolojia kutoka Estonia imefanikiwa kukua na kuvuka mipaka tangu kuanzishwa kwake ambapo sasa imewafikia wateja milioni 25 katika nchi zaidi ya 30 duniani, na kuifanya kuwa kampuni inayoongoza barani Ulaya na Afrika. 

“Ilikuwa pia kampuni ya kwanza ya kurahisisha huduma za usafiri na kwa sasa inafanya kazi katika kupanua huduma ya usafiri wa pikpiki kwenye miji kadhaa ya Ulaya,” alisema. 

Aidha, Meneja Mkazi nchini Tanzania kutoka Bolt, Remmy Aseka alisema bidhaa ya kwanza ya kampuni hiyo ya usafirishaji ilikuwa ni kutoa suluhisho la kurahisisha upatikanaji wa huduma za teksi kwa wateja wake. 

"Tumefanikiwa kuongeza uboreshaji katika malengo yetu, tumeanza pia kukuza jina la kampuni yetu katika maeneo mbalimbali. Lengo letu ni kutatua matatizo ya usafiri kwa kiwango kikubwa zaidi, tunataka jina la kampuni liendane na mambo yajayo ya kampuni na sio yaliyopita. Jina jipya la 'Bolt' linamaanisha kufanya jitihada bila kutumia nguvu, hasa uzoefu wa kuzunguka katika mji kwa gari, pikipiki au usafiri wa umma. 

“Pia inaendana na matarajio yetu kuwa baadaye huduma za usafirishaji zitakuwa kwa njia ya umeme. Pia watumiaji wa Bolt hawatahitaji kufanya mabadiliko yoyote kwenye program zao kwa kuwa Bolt itajibadilisha moja kwa moja kwenye program hizo,” alisema.

WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRI JIJINI DODOMA WASHAURIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA KUTOA HUDUMA YA USAFIRI KWA WANANCHI WATAKAOHUDUMIWA NA TAASISI ZINAZOJENGWA KWENYE MJI WA SERIKALI

$
0
0

Muonekano wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linalojengwa katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma
IMG_5308
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwasili katika Mji wa Serikali kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Utumishi katika mji huo Ihumwa, jijini Dodoma. 
IMG_5325
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akitoa maelekezo kwa Mhandisi, Lucas Lipambila (kushoto) wakati wa ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
IMG_5486
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza jambo baada ya kukamilika kwa ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb).
IMG_5563
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
IMG_5591
Afisa Tawala Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Donald Bombo akisisitiza jambo kwa Mhandisi Lucas Lipambila (wa pili kutoka kulia) baada ya kumalizika kwa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Utumishi katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma

Wanawake wa soko la Feri pamoja na maeneo jirani waishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0

Na Mwandishi Maalum

Wanawake wa soko la Feri pamoja na maeneo jirani wameishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kufanya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na kutoa elimu ya magonjwa hayo.

Upimaji huo umefanywa leo na wafanyakazi wanawake wa Taasisi hiyo ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kitaifa yatafanyika kesho.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wanawake hao walisema muda mwingi wamekuwa wakiutumia katika biashara na kutunza familia zao na hivyo kukosa nafasi ya kwenda kupima afya zao.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi Ashura Omari ambaye ni mfanyabiashara wa chakula katika soko hilo alisema wamefarijika sana kuona wataalamu wa magonjwa ya moyo wamewafuata katika soko la Feri la kuwapa huduma ya upimaji pamoja na kutoa elimu.

“Tunashukuru sana kwa kupimwa afya zetu, nimepimwa urefu, uzito, wingi wa sukari na msukumo wa damu mwilini (BP). Tunaiomba Taasisi hii na Serikali kwa ujumla waweze kutoa huduma kama hii katika maeneo mengi zaidi”, alisema Ashura.Naye Mariam Mohamed ambaye ni mkazi wa Kinondoni alisema amefika katika soko hilo la feri kupata huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake.

Mariam alisema amepata elimu ya jinsi ya kuandaa chakula bora kwa familia, kutotumia chumvi nyingi na mafuta mengi katika chakula, pia anapoandaa chakula ni ahakikishe familia ile chakula chenye mboga za majani na matunda.

“Pia nimeambiwa unywaji wa pombe uliokithiri pamoja na kutokufanya mazoezi ni vitu ambavyo vinapelekea kupata magonjwa ya moyo nitajitahidi mimi na familia yangu kufuata haya yote niliyofundishwa leo”, alisema Mariam.

Akitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa wanawake waliohudhuria upimaji huo Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hildegard Karau alisema mtindo wa maisha unapelekea watu wengi kupata magonjwa ya moyo ikiwemo shinikizo la damu na kuwataka wanawake hao pamoja na familia zao kufanya mazoezi.

“Wanawake ni watu wa muhimu sana katika familia kama mtazingatia mafunzo mliyopewa leo na kuandaa vyakula bora katika familia zenu itawasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda familia familia zao”, alisema Hildegard.

Wakati huo huo wanaume wa soko la Feri waliiomba Taasisi hiyo wakati mwingine watakapoandaa upimaji kama huo wasiwasahau wanaume kwani nao muda mwingi wanahangaika kutafuta fedha za kutunza familia na kukosa muda wa kwenda kupima afya zao.

Mzee Husein Mbaraka alisema, “Katika soko hili kuna watu wengi wanaofanya kazi mbalimbali wakiwemo wavuvi ambao muda mwingi wanashinda Baharini , tunaiomba Taasisi hii siku nyingine waje kutupima na sisi magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na kutupa elimu.

Vodacom watoa msaada kwa watoto wenye uhitaji maalumu

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bw. Filberto Sanga akipokea msaada uliotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kutoka kwa Meneja Mawasiliano na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Christina Murimi (kushoto) na Meneja Mahusiano, Alex Bitekeye (kulia), kwa ajili ya kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu wanaoshi katika kituo cha Mwanangu Special kilichopo Vikindu mkoani Pwani. 



Meneja Mawasiliano na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Christina Murimi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha Mwanangu Special, Walter Miya vifaa vya watoto wenye mahitaji maalumu kutoka taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation. Akishuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bw. Filberto Sanga (katikati). Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC kupitia mpango wao wa Pamoja na Vodacom wametoa msaada wenye thamani ya TZS 9.5m kwa watoto hao kwa lengo la kuwawezesha katika maisha yao ya kila siku ili kufikia ndoto na malengo yao. 



Katika kusherehekea wiki ya wanawake duniani wafanyakazi wa kampuni hiyo kupitia mpango wao wa Pamoja na Vodacom wametoa vifaa vyenye thamani ya TZS 9.5m kwa watoto hao ili kuwezesha maisha yao ya kila siku na kufikia ndoto na malengo yao. Wengine ni Mkurugenzi wa kituo hicho, Walter Miya (kati) na Jennifer Shumbusho (wa pili kulia) mmoja wa wazazi wa watoto hao.

Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani, wafanyazi wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc, kupitia mpango wake wa Pamoja na Vodacom ulio chini ya taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation leo wamechangia vifaa mbali mbali vyenye thamani ya shilingi milioni 9.6 kwa kituo cha watoto wenye uhitaji maalum kiitwacho Mwanangu Special kilichopo Mkuranga, mkoani Pwani. Kituo hicho kina jumla ya watoto 40, kati yao 20 ni wale wenye mahitaji maalum kama vile mgongo wazi, vichwa vikubwa na down syndrome.

Wafanyakazi hao wametoa vifaa kama vile; viti maalum, magongo ya kutembelea, magongo ya kusimamia, mashine za uzito, viatu vya ‘Special Orthopedics’, vitanda vya watoto walemavu, mashine za kufulia nk. ambavyo ni mahitaji muhimu kwa watoto hao. Mbali na misaada hiyo, wafanyakazi wa Vodacom pia walijitolea muda wao kucheza na kufurahi pamoja na watoto hao kwa ajili ya kuwapatia faraja.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bw. Filberto Sanga aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa mpango huo akisema “Serikali yetu imedhamiria kuboresha maisha ya kila mtanzania ili kutimiza dira ya maendeleo ya taifa na jitihada kama hizi kutoka kampuni binafsi zinasaidia serikali kutimiza malengo yake”. Bw. Sanga pia aliishukuru kampuni ya Vodacom huku akifafanua namna ambavyo msaada huo utasaidia kuhudumia watoto wenye ulemavu nchini na kuhimiza taasisi zingine kufuata nyayo za Vodacom. 

Mpango wa Pamoja na Vodacom umekuwa ukitumiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ili kurejesha fadhila kwa jamii. Mpango huu umewafanya wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa mawakala wa mabadiliko kwa kusaidia kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Jacquiline Materu alisema “Wafanyakazi wa Vodacom, tunashauku ya kuisaidia jamii yetu na huu umekuwa ni utaratibu wetu kwa miaka zaidi ya 12 kupitia Vodacom Tanzania Foundation. Katika kusherehekea wiki hii ya wanawake duniani, tumeona ni vyema kusherehekea na wadogo zetu, kuwapatia mahitaji muhimu na pia kuwawezesha kuwa na nyenzo muhimu za kuwasaidia kufikia ndoto zao kwani ulemavu sio kikwazo cha mafanikio”. 

Mzazi XXX ambaye pia ni mfanyakazi wa kituo hicho alieleza furaha yake kupokea vifaa vitakavyosaidia watoto anaowalea “ahsanteni kwa ukarimu wenu na kwa kutukumbuka. Zawadi hizi zitawasaidia watoto hawa katika maisha yao ya kila siku”. Walezi wengine pia walionyesha kufurahishwa na kushukuru kwa zawadi zitakazo wasaidia katika malezi ya watoto hao kwani wengi wao wametoka familia duni.

WAZIRI NDALICHAKO ASEMA SAYANSI NA TEKNOLOJIA NI MUHIMU KATIKA UKUAJI WA UCHUMI

$
0
0
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ilboru Maximillian Masesa akitoa maelezo kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako juu ya kifaa cha kubaini wanafunzi ambao wanatumia simu shuleni alichobuni.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiangalia ubunifu wa injini ya Ndege uliofanywa na Emmanuel Chibula kutoka Musoma, Mkoani Mara wakati wa kilele cha mashindano ya kitaifa ya sayansi, teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Wanafunzi mbalimbali wa shule za msingi na baadhi ya wananchi wakifuatilia mashindano ya kitaifa ya Sayansi,Teknlojia na Ubunifu yaliyofanyika katika viwanja vya mwalimu Nyerere jijini Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na washiriki mbalimbali hawapo pichani wakati wa kufunga mashindano ya kitaifa ya kitaifa ya sayansi, teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji nchini NIT wabuni gari lisilotumia injini, na badala yake linatumia umeme kuendesha mifumo yake. Pichani Waziri akiwa kwenye gari hilo akipewa maelezo ya namna gari hilo linavyofanya kazi.

…………………………

Serikali imewataka wabunifu nchini kujikita katika kuangalia shughuli za ambazo zinafanyika katika mazingira yao na wabuni jinsi ya kuzirahisisha kwa kutumia Sayansi na kiteknolojia ili kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako katika kilele cha Mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu mjini Dodoma. Waziri Ndalichako pia aliongeza kuwa eneo la Sayansi na Teknolojia ni muhimu kwa taifa na likitumika vyema litasaidia kuongeza uzalishaji na Kurahisisha utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

“Kwa muda mrefu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa ikisimamia zaidi Elimu kuliko masuala ya Sayansi na ubunifu hivyo ni vyema wabunifu waendelee kujitokeza zaidi na wajikitike katika ikubuni mbinu za kurahisisha mifumo ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo Kilimo, ufugaji na njia bora za upatikanaji wa maji”, alisema Waziri Ndalichako.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Profesa James Mdoe amesema lengo la Mashindano hayo yaliyohusisha wabunifu kutoka ngazi mbali za Elimu ni kuibua ubunifu, umahiri, kuchochea ugunduzi kwa lengo la kukuza matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika maendeleo.

Mashindano hayo yalifunguliwa rasmi na Naibu Waziri Mhe. William Ole Nasha Machi 5, 2019 na leo yamefikia kilele ambapo washindi mbalimbali walipata zawadi za fedha na kutunukiwa vyeti.

Kauli mbiu ya mashindano hayo kwa mwaka huu ni ” kukuza ujuzi na ubunifu kwa uchumi wa viwanda”.

MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0

Mimi ninajua, Wewe unafahamu na Tanzania inaelewa juu ya Safari Huru aliyoifunga dada yetu @mwasitij kuelekea Mafanikio kupitia Talanta ya muziki aliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu.

Katika Safari yake amekutana na Changamoto zilizomtoa machozi na kumkwamisha, ila kutokana na Juhudi, Maarifa na Ubunifu alipambana nazo na hatimae alijongea mbele na kutimiza Ndoto zake hatimae kuwa Shujaa.

Kesho ataungana na Wazungumzaji Mahili akiwa ni Mgeni wa Heshima katika tukio la #BintiShujaa ambalo litafanyika katika Ukumbi wa Anatoglo uliopo Mnazi Mmoja.

Kwa taarifa zaidi tembelea kurasa yetu Instagram @safarihuru au tupigie kwa namba 0715171587.

@tanisah_mansour @kijanapositive
#SafariHuru #Womensday #KijanaPositive #BintiPositive #ActivatedBillionaire

WAZIRI NDALICHAKO KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA KIMATAIFA WA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI

$
0
0
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojiaa Profesa Joyce Ndalichako anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kimataifa wa waratibu wa kitaifa wa miradi inayotekelezwa na Shirika la nguvu za Atomiki duniani kwa nchi 46 kanda ya Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 15 mezi Machi jijini Arusha wenye lengo la kujadiliana na masuala mbali. 

Mkutano huo utashirikisha washiriki 60 kutoka nchini 46 duniani kutoka baara la AFRIKA ambao ni wanachama wa Shirika la nguvu za Atomiki duniani ambao wataweza kujadiliana masuala mbali mbali . 

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ,Profesa Lazaro Busagala amaesema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na kwamba wana imani mkutano huo utaweza kusaidia nchi washiriki kuweza kusonga mbele katika namna ya uboreshaji wa sekta mbali mbali kutokana na miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani(IAEA). 

Amesema katika mkutano huo ,washiriki watapata nafasi ya kujadiliana kwa mapana juu ya namna ya. 

Pia Profesa Busagala ameongeza kuwa mkutano huo pia utahudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki kanda ya AFrika Bwana Shaukat Abdrazak ambaye baada ya mkutano huo ataweza kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali na uongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Wizara nne ambazo zimekuwa zikihusika katika miradi mbali mbali ya kitaifa inayotekelezwa na Shirika la Nguvu za Atomiki duninia(IAEA) . 

Amesemsa kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,Mkurugenzi Shaukat atakutana na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi . Kwa upande wa Tanzania Bara Shaukat atafanya mazungumzo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Waziri wa Maji . 

Pia ataweza kufanya ziara katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Seliani,Taasisi ya Chakula na Lishe na Taasisi ya Saratani Ocean Road. Profesa Busagala amesema kuwa mazungumo hayo yataweza kusaidia nchi kwenye uboreshaji wa miradi mbali mbali inayofanyika hapa nchini hasa katika sekta ya Afya,Kilimo,maji. 

Ameeeleza kuwa Tanzania ni moja ya nchi iiliyoweza kufadika kwa kiasi kikubwa kwa miradi katika ya udhibiti na kuhamasisha matumizi salama ya tekenolojia ya nyuklia inayotekelezwa na Shirika la Nguvu za Atomiki duniani .

MAGAZETI YA LEO IJUMAA,MACHI 8,2019

RC Wangabo aagiza kusakwa na kukamatwa kwa “Lambalamba”

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa Kapelo) akiongoza ukaguzi wa ujenzi wa madarasa manane yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi na michango ya wadau katika shule ya Msingi Msia, kata ya Milepa Wilayani Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akipewa maelezo juu ya marekebisho yanayoendelea katika ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Msia na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mh. Kalolo Ntila (kaunda suti nyeusi) wakati wa kuyakagua madarasa hayo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akikabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa niaba ya umoja wa waalimu wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Kipeta kwaajili ya wanafunzi ambao vitabu vyao vilirowa na mvua kutokana na mabweni kuezuliwa.

………………………………………………………..

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameliagiza jeshi la polisi Mkoani Humo kuhakikisha wanamsaka na kumkamata mganga wa jadi anayesadikiwa kuwaibua na kuwaadhiri wachawi katika bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga.

Agizo hilo limekuja baada ya kufanya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali katika bonde hilo pamoja na kujionea maendeleo na changamoto za shule ya sekondari Kipeta iliyoezuliwa paa pamoja na shule ya msingi Msia iliyobomoka madarasa manne kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyosababisha madhara hayo mwezi Disemba mwaka 2018.

Ameonya kuwa hataki yaliyotokea mkoa wa Njombe yajirejee katika Mkoa wa Rukwa ikiwa bado watu hawajasahau machungu waliyoyapata kutokana na matukio hayo, na kuongeza kuwa mganga huyo wa kienyeji analindwa na kiongozi wa chama cha kisiasa na hivyo kumtaka mkuu wa kituo cha Kijiji cha Kilyamatundu kuhakikisha anamkamta kiongozi huyo hata kama ni wa Chama cha Mapinduzi.

“OCS na vyombo vyako vile fanya upepelezi wa kina na ukamate yeyote yule ambae ametoka nje ya mkoa huu, nje ya Kilyamatundu anayefanya shughuli hizi, kamata weka ndani fanya mahojiano ya kina, na wengine nimeambiwa hap ani viongozi wa vyama vya kisiasa, usijali huyu ni chama tawala, huyu ni nani, kama ukijua kwa uhakika kamata mhoji mpaka kieleweke, sisi hatutaki kuletewa Lambalamba hapa,” Alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Mh. Wangabo aliwapongeza waalimu, Uongozi wa vijiji husika pamoja na wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha katika kuhakikisha majengo yaliyobomoka na kuezuliwa katika shule hizo yanarudi katika hali yake ya kawaida na hatimae wanafunzi kuendela na masomo.

Pamoja na michango ya wadau mbalimbali iliyohamasishwa na Mh. Wangabo ambayo imesaidia kurudishisa mapaa ya majengo ya utawala, mabweni mawili, nyumba sita za waalimu na vyoo vya wasichana na wavulana kwa shule ya sekondari Kipeta na kujenga madarasa manane kwa shule shule ya Msingi Msia, Wizara ya Elimu pamoja kwa ushirikiano na Wizara ya TAMISEMI imetoa shilingi Milinoni 75.2 kwaajili ya kuongezea ujenzi wa madarasa na vyoo kwa shule hizo.

Naye Diwani wa kata ya Milepa Mh. Apolinari Macheta alipongeza juhudi za Mkuu wa Mkoa kwa kuhakikisha shule hizo zinakuwa bora zaidi ya zilivyokuwa na kumuahidi kuwa Shilingi Milioni 48.6 walizopatiwa kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili na vyoo matundu sita kwa shule ya msingi Msia atahakikisha kwa ushirikiano wa wananchi watapata darasa jingine kwa fedha hizo.

MWENYEKITI WA UWT TAIFA BI.GAUDENSIA AFANYA ZIARA WILAYA YA MKOANI PEMBA

$
0
0


MWENYEKITI wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka, Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Thuwayba Kisasi, Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Bi.Tunu Juma Kondo wakipewa maelezo na Mhandisi Abubakar Khamis Mati juu ya maendeleo ya ujenzi wa shule ya Kisasa ya Sekondari ya Wara iliyojengwa na SMZ kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
MWENYEKITI wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akishiriki shughuli za ujenzi wa Tawi la CCM Kangani ambalo ni Tawi la asili la harakati za ASP linalojengwa upya ili liendane na hadhi ya CCM.
MWENYEKITI wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akishiriki shughuli za ujenzi wa Tawi la CCM Kangani ambalo ni Tawi la asili la harakati za ASP linalojengwa upya ili liendane na hadhi ya CCM.

……………………………………………………………………..

NA IS-HAKA OMAR,PEMBA.

WANAWAKE wa Chama Cha Mapinduzi kisiwani Pemba wametakiwa kufanya Mapinduzi ya kisiasa kwa kuhakikisha CCM inavunja na kusambaratisha ngome ya CUF na hatimaye kushinda majimbo yote ya Uchaguzi ya mwaka 2020.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka katika mwendelezo wa ziara yake huko Shule ya Sekondari ya Mohamed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, alisema ni wakati wa wanawake kuonyesha uwezo wao na kutekeleza kwa vitendo falsafa ya ‘Wanawake ni jeshi la ukombozi la CCM’.

Alisema hakuna chama cha siasa, wala taasisi yoyote itakayoweza kuzuia ushindi wa CCM mwaka 2020 kisiwani Pemba endapo wanawake wataamua kuungana kwa pamoja ili kufanikisha ushindi wa CCM.

Katika maelezo yake Ndugu Gaudensia alisema Jeshi la UWT la Chama Cha Mapinduzi litakuwa mstari wa mbele kupambana vita ya kisiasa kwa mbinu zote ili kuandika historia mpya katika uwanja wa siasa za ushindani Tanzania kwa kuhakikisha CCM inashinda kwa kiwango kikubwa Zanzibar na Tanzania bara.

“Wanawake tuna nguvu, uwezo, ujasiri, mikakati,nyenzo na mbinu za medali za kisiasa hivyo hatuna sababu ya kuyaachia majimbo ya Pemba yaendelee kubaki kwa wapinzani bali yatarudi mikononi mwa CCM.”,alisema Bi.Gaudensia.

Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia, alipongeza hatua za kimaendeleo zilizofikiwa katika Sekta ya Elimu Pemba hasa katika suala zima la miundombinu ya Majengo ya Kisasa ya kiwango cha Ghorofa.

Aidha aliyataja mageuzi makubwa katika miundombinu ya Barabara za kisasa mijini na Vijiji kuwa ni ya kiwango bora cha kuridhisha hatua ambayo wananchi wa kisiwa cha Pemba wanastahiki kuithamini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo mema yaliyotekelezwa.

Pamoja na hayo aliwasisitiza hakina Mama Visiwani Pemba bila kujali tofauti zao za kisiasa kushiriki katika kongamano la Kitaifa litakalofanyika Machi 9 mwaka 2019, katika Kiwanja cha Tibirinzi Wilaya ya Chake Chake Pemba.

Alieleza kuwa Kongamano hilo lililoandaliwa na UWT ni la kupongeza utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 pamoja na masuala mbali mbali ya kimaendeleo yaliyoasisiwa na Serikali za CCM kwa awamu tofauti za Uongozi.

Pamoja na hayo aliwapongeza Wabunge na Wawakilishi wa Viti Maalum Pemba kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Naye Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mwl.Queen Mlozi alikemea vitendo vya udhalilishaji wa Kijinsia kwa Watoto wa Kike vinavyochangia kukwamisha maendeleo ya wanawake katika kunufaika na fursa za elimu.

Mwl.Queen aliwasihi Wazazi,Walezi pamoja viongozi wa dini na kisiasa kusimamia ajenda za kulinda na kutetea haki za wanawake hasa vijana na watoto ili wanufaike na fursa mbali mbali ndani ya jamii.

Akizungumzia changamoto za dawa za kulevya kwa vijana, Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania bara Ndugu Jesca Mbogo alisema baadhi ya vijana kisiwani Pemba wameingia katika changamoto za kutumia dawa za kulevya hali ambayo ni hatari katika ustawi wa maendeleo ya nchi.

Mapema Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kusini Pemba, ndugu Bimkubwa Khamis Mohamed alisema hali ya kisiasa ndani ya mkoa huo imeendelea kuimarika na wanawake wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kujiunga na CCM.

Alisema Pemba ya Sasa sio Pemba ya zamani kwani wananchi wengi wameanza kutambua ukweli baada ya kuona kwa vitendo mambo mema yanayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayotokana na Chama Cha Mapinduzi.

Daraja la Momba Kufungua fursa za kiuchumi kwa Wanarukwa.

$
0
0


Daraja la Momba linalounganisha Mkoa wa Rukwa na Katavi lenye urefu wa mita 84 na kugharimu shilingi bilioni 17.7
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa kapelo) pamoja na wataalamu alioambatana nao wakitembea juu ya daraja hilo ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa daraja hilo lipo tayari kwa matumizi ya kuvuka kutoka mkoa wa Rukwa na kuelekea mkoa wa Songwe.
Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wakitembea juu ya daraja hilo kuonyesha mwanzno wa matumizi ya daraja hilo muda mfupi baada ya kusikiliza nasaha za Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo.
Picha ya pamoja ya wataalamu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani Rukwa pamojana Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (wa nne toka kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa kapelo)

……………………………………………………………………….

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewasisitiza wakati wa Kijiji cha Kilyamatundu, Kata ya Kipeta, Wilayani Sumbawanga kuhakikisha wanaitumia vyema fursa inayoletwa kwa kukamilika kwa ujenzi wa daraja la momba ili kuinuka kiuchumi.

Amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo ni kufunguka kwa neema ambayo muda mrefu wanacnhi wamekuwa wakiisubiri na kuongeza kuwa kazi ya serikali ni kuhakikisha inaweka miundombinu sahihi ili kuwarahisishia wananchi wake kupata huduma wanazostahili na sio kuwawekea fedha wananchi mifukoni.

“Kwahiyo daraja hili la mto momba, nina hakika litakuza uchumi wa mikoa yetu, ndani ya mkoa wetu wa Rukwa na mikoa ya jirani, kuna Katavi watakuja kutumia lakini kuna jirani zetu wa Songwe na hata Mbeya, iliyopo ni kuongeza juhudi katika kuzalisha na hasa kilimo cha mpunga ambacho ndicho kinakubali huku, tulime zaidi halafu tuchakate, tuweke viwanda, awali nilishasema na nitarudia tena kutoa wito kwa wadau mbalimbali waje kuweka viwanda huku,” Alisisitiza.

Aidha, alisikitishwa na baadhi ya wafanyabiashra wanaotoka nje ya Mkoa wa Rukwa kuchukua mazao ya mkoa huo na kuyapeleka kwao na kisha kuweka kwenye vifungashio na kudai kuwa mazao hayo yanatoka katika mikoa yao.

Wakati akisoma taarifa ya mradi huo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani Rukwa Mhandisi Ndelalutse Karoza alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo ni muhimu sana kwa mikoa ya Rukwa na Songwe pamoja na Tanzania kwa ujumla na kubainisha kuwa ukamilifu wa daraja hilo utawainua wananchi kiuchumi na kijamii ikiwemo kupunguza gharama za usafirishaji wa mazao.

“Maendeleo ya kazi hadi kufikia Februari 2019 ni asilimia 95 kwenye daraja na asilimia 97 kwenye barabara za maunganisho, kazi muhimu zimekwisha kamilika na daraja linaweza kutumika, kazi ambazo hazijakamilika ni pamoja na alama za barabarani na kazi ya kuweka taa,” Alimalizia.

Ujenzi wa daraja la mto Momba linalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe kwa upande wa bonde la ziwa Rukwa umefadhiliwa kwa asilimia 100 na serikali ya Tanzania na litagharimu shilingi bilioni 17.7 hadi kukamilika kwake tarehe 24.5.2019 ambapo mpaka sasa limekamilika kwa asilimia 95 na mkandarasi wa ujenzi huo ni Genjio Engineering Group Cooperation kutoka China.
Viewing all 46367 articles
Browse latest View live




Latest Images