Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1815 | 1816 | (Page 1817) | 1818 | 1819 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Na Estom Sanga-DSM

  Wanawake wanaofanyakazi katika Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF wameitumia siku ya Maadhimisho ya Wanawake Duniani kuwatembelea na kuwafariji Wanawake na Watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.

  Wakiwa hospitalini hapo Wafanyakazi hao wanawake kutoka TASAF wametoa zawadi mbalimbali kwa Wagonjwa na hospitali yenyewe.

  Wakitoa salamu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii-,Bw. Ladislaus Mwamanga, Wafanyakazi hao wamebainisha kuwa Mfuko huo unaohudumia wanawake na watoto kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini-PSSN- unatambua jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za Jamii ikiwemo sekta ya Afya nchini.

  “Hii ni sehemu ndogo ya mchango wetu katika sekta ya Afya,tunaomba muipokee” imebainisha sehemu ya salamu hizo.

  Miongoni mwa zawadi zilizopelekwa katika hospitali hiyo na wanyakazi hao wa kike wa TASAF ni pamoja na viti vya wagonjwa,pumpers, na viti vya plastiki.

  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF licha ya kutumia Mpango wake wa Kunusuru Kaya Maskini kutoa ruzuku kwa Kaya Maskini zaidi ya Milioni Moja na Laki Moja kote Tanzania Bara, Unguja na Pemba, lakini pia umekuwa ukijenga miundombinu hususani majengo ya zahanati ,nyumba za Wauguzi na Waganga kwenye maeneo yenye uhitaji nchini kote.  Wafanyakazi Wanawake kutoka TASAF wakiwa katika picha ya pamoja ba baadhi ya wauguzi katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza utoaji wa zawadi kwa wagonjwa wa kike na watoto katika hospitali hiyo.

  Baadhi ya wafanyakazi Wanawake wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAFofisi ndogo ya Dar es Salaam wakibeba zawadi mbalimbali kwa Wanawake na Watoto waliolazwa kwenye hospitali ta Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.

  0 0


  Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa akizungumza na wafanyakazi wa kike wa kampuni hiyo walioungana na ‘Mama Lishe’ wa Soko la Tandale wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.
  Mwakilishi wa akina mama wanaofanya biashara ya chakula maarufu kama ‘Mama Lishe’ katika Soko la Tandale, Stamil Gereza (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa kike wa kampuni ya Coca Cola Kwanza walioungana na ‘Mama Lishe’ wa Soko la Tandale wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa (katikati) na Meneja Rasilimali watu wa Kampuni hiyo Naomi John (kulia).
  Sehemu ya wafanyakazi wanawake wa Coca Cola Kwanza waliojiunga na akina ‘Mama Lishe’ kutoka Tandale wakipanga mstari kupata chakula wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.


  Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa akitoa huduma kwa wafanyakazi wanawake wa Coca Cola Kwanza ambao waliungana na ‘Mama Lishe’ wa soko la Tandale wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.
  Mratibu na mtaalamu wa masuala ya Vicoba kwa akina mama, Anitha Ngoya akikata keki kwa niaba ya akina Mama Lishe wa Soko la Tandale ambao waliungana na wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Coca Cola Kwanza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.
  Mtaalamu wa utambuzi wa Soko kutoka Kampuni ya Coca Cola Kwanza, Jacqueline Rimoy akiwasaidia akina Mama Lishe wa soko la Tandale kupika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.

  Sehemu ya wafanyakazi wanawake wa Coca Cola Kwanza waliojiunga na akina ‘Mama Lishe’ kutoka Tandale wakipanga mstari kupata chakula wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Mwanamke Shujaa' iliyofanyika katika siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao. Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea katika uwezeshaji wa kijinsia.  Coca-Cola Kwanza imezindua kampeni ya kusherehekea mafanikio ya wanawake ya “Mwanamke Shujaa” ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake mwaka huu.

  Kampeni hiyo imelenga kubadilisha dhana ya kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu, kulingana na maudhui ya mwaka huu.

  Pia inalenga kusisitiza ahadi ya Coca-Cola Kwanza kuelekea Uwezeshaji wa Kijinsia.

  Kampeni hii imezinduliwa kutambua jitihada za wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kwenye jamii na kuwakumbusha kujiamini na kujitegemea katika kufikia malengo yao.

  Leo, wafanyakazi wa kike katika kampuni yetu wamejumuika pamoja na akina ‘Mama Lishe’

  wa Soko la Tandale katika kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani.

  Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca- Cola Kwanza, Josephine Msalilwa alisema kuwa, lengo lao ni kusherehekea na kuhamasisha wanawake kutoka sekta tofauti na pia kuwaonyesha kwamba wanathaminiwa.

  “Ni kuhusu kusherehekea mafanikio ya wanawake na kuwahamasisha kwamba pia wanaweza kufikia malengo yao na kufikia mafanikio makubwa,”amesema Msalilwa.

  Msalilwa aliongeza kuwa, kampuni yao inao wajibu katika jamii, hivyo wanaamini kuwa ni wajibu wao kuleta mabadiliko endelevu katika sekta mbalimbali ambazo wanawake wa Tanzania wanafanya kazi zao, hivyo kuanzishwa kwa kampeni hiyo ni hatua muhimu.

  “Nimekutana na wanawake wengi waliofanya mambo makubwa nchini Tanzania, ambao wameamua kuvunja vikwazo na kufikia mafanikio makubwa,”aliongeza.

  Pia akizungumza wakati wa tukio hilo, Stamil Gereza mwakilishi wa akina Mama Lishe kutoka Tandale alimuelezea mwanamke kama mtu mwenye akili na uwezo wa kujitegemea.

  Aliwahimiza wanawake kuanza kusimama kidete na kufanya mambo yote wanayoamini katika jamii licha ya changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo.

  Kwa upande wake, Anitha Ngoya Mratibu na mtaalamu wa masuala ya Vicoba kwa akina mama ambaye amekuwa akiwafundisha akina Mama Lishe juu ya ujasiriamali, usimamizi wa kifedha kwa niaba ya Coca Cola Kwanza alisema, "Mpaka sasa tumewafundisha wanawake zaidi ya 45 kwenye mtandao wetu wa akina mama wajasiriamali na bado tunajitanua zaidi ". Lengo letu ni kuwafikia wanawake zaidi ya 300 kila mwaka.

  Coca-Cola Kwanza imekuwa ikijihusisha katika mipango mbalimbali endelevu ambayo inalenga kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake nchini Tanzania.

  Ikiwemo kampeni ya ufukweni ya “Mchanga Pekee” ambayo ilizinduliwa hivi karibuni ambapo wanawake wengi wameajiriwa kwa ajili ya kufanya usafi, kukusanya chupa za plastiki katika fukwe mbalimbali nchini.

  Kupitia Kampeni ya 5by20, ambao ni mpango wa Coca-Cola wa Kimataifa kutoa usaidizi wa kiuchumi kwa wanawake milioni 5 kwa ajili ya kuendesha biashara zao katika nchi zote duniani ifikapo 2020, Coca-Cola Kwanza imesaidia kujenga vibanda vinavyotumiwa na Mama Lishe ambao wapo nje ya kiwanda hicho. Pia Coca-Cola Kwanza imewawezesha wanawake hao kwa kuwapatia mitungi ya gesi ya kilo 15.

  0 0


   Meneja Mwandamizi wa Uendeshaji wa Azania Bank, Jane Chinamo akizungumza na wanahabari  baada ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo kutoa zawadi na misaada mbalimbali kwa wanawake wenzao  wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kama sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
  Wafanyakazi wanawake wa Azania Bank watoa zawadi na misaada mbalimbali kwa wanawake wenzao wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kama sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.


   
   
   Wafanyakazi wanawake wa Azania Bank  wameungana na wanawake wenzao wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kama sehemu ya kuonyesha upendo na mshikamano katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019. Ziara ya Wanawake wa Azania Bank katika wodi za wanawake wanaopatiwa matibabu katikaa taasisi hii imelenga kuwapa moyo wagonjwa na kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya kujikimu.

  Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja Mwandamizi wa Uendeshaji wa Azania Bank, Jane Chinamo amesema, “Tuko hapa leo ili kusherekea siku hii maalum pamoja na wanawake wenzetu ambao tunawahitaji sana waweze kurejea katika afya zao ili waendeleze maisha yao pamoja na ya wapendwa wao. Kama benki, ni jukumu letu la msingi kuchangia katika kuboresha uchumi wa taifa, na hilo linaweza kufanikiwa tu pale tutakapokuwa na jamii zenye watu wenye afya bora ili waweze kusaidiana katika kulifikia lengo la kuwa na maisha yenye mafanikio”.

  Katika kuwatakia kupona haraka, Chinamo amesema wanawake wana mchango mkubwa katika jamii na kwamba wamekuwa mstali wa mbele katika juhudi za kuliletea taifa maendeleo. Kauli mbiu katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa mwaka huu ni ‘Usawa kwa Maendeleo’ #BalanceForBetter

  Katika ziara hiyo, wanawake wa Azania Bank wametoa zawadi na misaada mbalimbali kwa wagonjwa pamoja na vifaa tiba kwa wauguzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road.

  Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka ili kutambua na kupongeza mchango wa wanawake katika nyanja za kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Siku hiyo pia hutumika kama mojawapo ya njia za kuikumbusha dunia juu ya umuhimu wa usawa wa kijinsia.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  CHUO cha VETA Chang’ombe kimetoa msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni Moja katika Kambi ya Wazee Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  Msaada huo umetokana na mchango wa Wanawake wa chuo hicho katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila Machi 8 ya kila mwaka.

  Akizungumza na Wazee wa Kambi ya Nunge Kaimu Msajili wa Chuo cha VETA Chang’ombe Clara Kibodya amesema kuwa wanawake wamekuwa na mwitikio katika kambi ya Nunge na hivyo kuamua kutoa mchango wao kwa jamii inayoishi hapo.

  Amesema kuwa Kambi hiyo inahitaji msaada, na kutaka wadau na mtu mmoja moja kuona kuna umuhimu wa kutoa msaada kwani serikali pekee yake haiwezi kutosheleza.

  “Tumefika na kujionea hali ya wazee na kuamini wanauhitaji wa msaada na tumevutiwa kama wanawake ndio wasimamizi wa familia hatuwezi tukawaacha wazee hao kwani ni baba zetu na babu zetu katika mila na tamaduni za Afrika”.amesema Kibodya.

  Nae Katibu Mukhtasi wa Chuo hicho Bena Maimu amesema katika kuadhimisha siku wanawake duniani Kambi ya Nunge imewagusa na kutaka kuwa na utaratibu wa kuwatembelea mara kwa mara na kujua changamoto zao ili wazee wasione jamii imewatupa.

  Kwa upende wa Afisa Kilimo na Msimamizi wa Kambi ya Nunge Frank Munuo amesema kuwa msaada huo ni mkubwa sana kwani kuna watu wana uwezo lakini hawajawahi kusaidia kambi hiyo.

  Amesema kambi imepokea mssada kwa mikono miwili na kuwataka VETA kuwa mabalozi wa kuwambia watu wengine katika kuwasaidia.

  Akitoa shukrani mmoja wa wazee wa Kambi ya Nunge Salum Ubwabwa amesema kuwa wanawake VETA wamekuwa mstari wa mbele katika kuwajali hivyo waendelee kuwa na moyo huo huo kuwakumbuka kwani wanauhitaji wa msaada.
   Kaimu Msajili wa Chuo ch VETA Chang'ombe Clara Kibodya akizungumza na Wazee wa Kambi ya Nunge wakati  Wanawake Chuo hicho walivyokwenda kutoa msaada Kambi hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
   Kaimu Msajili wa Chuo cha VETA Chang'ombe Clara Kibodya akitoa msaada  kwa Wazee wa Kambi ya Nunge katika maadhimisho ya Siku Wanawake Duniani.
   Wanawake wa Chuo cha VETA Chang'ombe wakiwa katika picha ya pamoja na Wazee wa Kambi ya Nunge wakati walipotembelea na kutoa msaada katika maadhimisho ya Siku Wanawake Duniani.
   Afisa Kilimo na Msimamizi wa Kambi ya Wazee ya Nunge Frank Munuo akizungumza kuhusiana na historia ya Kambi hiyo wakati Wanawake wa Chuo cha VETA Chang'ombe  walivyokwenda kutoa msaada kambini hapo wakati wa kilele  cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Macho 8.
   Bidhaa mbalimbali walizozitoa Wanawake wa Chuo cha VETA Chang'ombe katika Kambi ya Wazee Nunge.
  Baadhi ya a Wazee na Wanawake wa Chuo cha VETA Chang'ombe wakiwa na Wazee wa Kambi ya Nunge  wakati walipotembelea ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

  0 0

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi akimkabidhi zawadi ya kitabu Mwandishi Mkuu wa Sheria Bibi Sarah Kinyamfula Barahomoka katika hafla ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi Saba wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao wamestaafu na wanastaafu Utumishi wa Umma. Bibi Sarah Barahomoka ambaye anastaafu rasmi mwezi Julai Mwaka huu ni Mwanamke wa Kwanza kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria ( Chief Parliamentary Draftsman) amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 33.
  Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao wanastaafu utumishi wa Umma.Halfa ya kuwapongeza na kuwaaga ilifanyika mwisho mwa wiki. miongoni mwa zawadi walizopewa ni pamoja na Kitabu 'Retiring Gloriuosly'. Kutoka kushoto na miaka yao ya utumishi kwenye mabano ni Bw. Hussein Shabani Kaweto (37), Bibi Esther James Manyesha (35), Bibi Sarah Kinyamfula Barahomoka (33), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Evaristo Longopa, Bibi Mary Mahingu Maganga(30), Bibi Benadetha Cosmas Karadisy (36) na Bw. Cosmasi Bayi Machupa (16).


  Na Mwandishi Maalum, Dodoma 

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi amesema, Ofisi yake itaandaa utaratibu wa kuwatumia watumishi wake waliostaafu katika maeneo mbalimbali yakimamo ya kufundisha na ushauri. 

  Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki,( Ijumaa) wakati wa hafla ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi saba ambao wamestaafu na wanastaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria. Hafla hiyo na ambayo pia ilihudhuriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Evaristo Longopa ilifanyika katika ukumbi wa Veta Jijini Dodoma 

  Miongoni mwa watumishi hao wanaostaafu ni pamoja na Mwandishi Mkuu wa Sheria Bibi Sarah Kinyamfula Barahomoka , Mwanamke wa Kwanza kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria tangu Tanzania ipate uhuru na amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 33. Miaka hiyo yote amefanya kazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

  “Watumishi wenzangu mnaostaafu. Mnastaafu bado mkiwa na akili timamu na afya njema, mnastaafu utumishi wa Umma kwa Heshima kubwa hongereni sana. Uzoefu mnaoondoka nao hamkuupata kwa mwaka mmoja au mwili, ni uzoefu ambao umejijengea katika kipindi chote cha utumishi wetu” akasema Mwanasheria Mkuu . 

  Na kuongeza “ Ofisi yangu tutaandaa utaratibu wa kuangaliana namna ya kuutumia uzoefu wenu huu, iwe kwa kutoa ushauri au kwa kuja kufundisha. Na kwa hiyo msishangae mkiona hata katika ustaafu wenu tunawaomba mje mtusaidie katika kutuongezea nguvu katika maeneo fulanifulani mkiwa kama washauri au wakufunzi.Na ninaomba sana tutakapowaomba na kuwahitaji mtukubalie” akasisitiza na kushangiliwa na watumishi. 

  Profesa Kilangi amewataka wastaafu hao kwenda na kuutumia uzoefu wao waliojijengea katika utumishi wa umma kwa maendeleo na manufaa yao wenyewe na familia zao lakini pia kwa manufaa na maslani pamana ya Serikali na Nchi kwa Ujumla. 

  Kuhusu watumishi wate wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Kilangi amewashukuru na kuwapongeza kwa namna ambavyo wameupokea na kuanza kuutekeleza Muundo Mpya wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufuatia mabadiliko yaliyofanya na Mhe Rais John Magufuli mwaka  jana. 

  “Niwashukuruni sana kwa namna mnavyotekeleza majukumu yenu, wengi wetu tumeyapokea vema mabadiliko ya Muundo wa Ofisi aliyoyafanya Mhe Rais mwaka jana na mmeelewa lengo na nia yake ambayo ni kuboresha huduma zinazotolewa na Ofis ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na nipende kusema mbele yenu kwamba sasa ukizungumza na wadau wetu wengi huko nje wanafurahi sana, wanaridhika sana na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali” akasema . 

  Pamoja na pongezi hizo, amewataka watumishi wote wa Ofisi yake ni vema wakafahamu ulimwengu wa sasa unahitani watu au watumishi wasomi na wenye uwezo wa juu wa kuelewa mambo na kutatua matatizo na katika muktadha huo ametoa wito wa watumishi wote kila mmoja kwa mujibu wa kada yake kujiendeleza ili Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikawe kioo na kielelezo bora katika Taifa letu. 

  “Natoa wito mjiendeleze kwa kulingana na kada zanu mwenye certificate basi apate diploma, mwenye diploma apate degree ya kwanza na mwenye degree ya kwanza apate ya pili na na mwenye ya pili alenge kupata udaktari na hatimaye uprofesa hakuta kuwa na shinda kama ofisi hii itajaa madokta” akasisitiza kwa mkazo. 

  Pia amewataka watumishi wote kujiandaa kifikra kwa mapokeo ya matumizi ya tehama katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku pamoja na kutumia vema muda wa kazi na kutumia vema raslimali na vitendea kazi vilivyovopo ili kutekeleza vema na kwa tija kauli mbiu ya ‘hapa Kazi tu’ 

  Aidha amesema anaridhiswa na kufurahishwa na idadi kubwa ya watumishi wanawake ambao wameshika nafasi na Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Vitengo utaratibu ambao amesema ameukuta hataka kabla yake. 

  Akitoa salamu za Shukrani kwa niaba ya wastaafu wenzie Mwandishi Mkuu wa Sheria Bibi Saraha Barahamoka amemshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuwaandalia hafla ya kuwapongeza na kuwaaga ikiwa ni pamoja na kuwapatia vyeti vya utumishi. 

  Akasema yeye binafsi na wenzake wamefurahishwa sana na namna Ofisi ilivyotambua na kuthamini mchango wa utumishi wao katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Serikali na Nchi kwa Ujumla. 

  Aidha akasema, katika kipindi chote cha utumishi wao katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamepata ushirikiano mzuri kutoka kwa viongozi wa juu na watumishi wenzao na kwamba wanaomba ushirikiano na moyo huo wa kusaidiana unaendelezwa baina ya viongozi wa wajuu na watumishi wote. 

  Watumishi wengine waliostaafu ni Bibi Ester James Manyesha ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Uandishi wa Sheria na amekuwa katika utumishi wa umma kwa miaka 35, Bibi Grace Mlondezi Mfinaga, Mwandishi wa Sheria Mkuu Daraja la kwanza na amekuwa katika utumishi wa umma kwa Miaka 36 na Bw. Hussein Shabani Kaweto Msaidizi Kumbukumbu Daraja la kwanza  ambaye amedumu katika utumishi wa Umma kwa Miaka 37. 

  Wengine ni Bibi. Benadetha Cosman Karadisy ambaye ni Msaidizi wa Mtendaji Mkuu Daraja la Pili na amedumu katika utumishi wa Umma kwa miaka 36, Bw. Cosmasi Bayi Machupa ambaye ni Dereva daraja la Kwanza yeye amedumu katika utumishi wa Umma wa miaka 16 na Bibi Mary Mahigu Maganga ambaye ni Msaidizi wa Ofisi Mkuu yeye amedumu katika utumishi wa Umma kwa miaka 30 

  Imetolewa na Kitengo 
  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali 
  Dodoma

  0 0


  MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka akipokelewa na Viongozi mbali mbali wa CCM na Jumuiya zake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Unguja akitokea Pemba.

  Viongozi mbali mbali wa UWT Taifa wakiwa katika Chumba cha Wageni Mashuhuri(V.I.P),mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Unguja wakitokea Pemba.

  WANACHAMA wa CCM na Jumuiya zake wakicheza kwa furaha katika mapokezi ya viongozi mbali mbali wa UWT Taifa kisiwani Unguja.
  ……………………………………………………………………….
  NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

  MWENYEKITI WA Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka leo amewasili Unguja kwa lengo la kuendelea na ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 katika Wilaya mbali mbali za Unguja.

  Ndugu Gaudensia mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, aliwapongeza Wanachama wa CCM na Jumuiya zake kwa mapokezi na maandalizi mazuri ya Kongamano la kupongeza Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka mitatu ya Dk.Shein pamoja na ziara yake kisiwani Pemba.

  Alisema kupitia ziara hiyo amejiridhisha kuwa Chama Cha Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar kina mtaji na azna kubwa ya wanachama hai wenye uwezo,uzalendo na uthubuti wa kusimamia maslahi ya taasisi hiyo bila kuyumba na kwa mafanikio makubwa.

  Alieleza kuwa CCM inaisimamia Serikali zote mbili ya Zanzibar na Tanzania bara ziendelee kuwatumikia wananchi wa makundi yote bila ya ubaguzi kwa kuwasogezea huduma muhimu za kijamii, kiuchumi,kisiasa na kimaendeleo.

  Naye Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo, alipongeza Mwenyekiti huyo na Ujumbe aliofuatana nao kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kukagua miradi mbali mbali ya CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kisiwani Pemba.

  Alieleza kuwa ziara hiyo imeleta mafanikio makubwa ya kisiasa kwani wanachama wengi hasa wanawake, wamehasasika na kutambua kuwa viongozi wa ngazi za Taifa wanawathamini na kuwajali.

  Pamoja na hayo Naibu Katibu Mkuu huyo Ndugu Tunu, alisema Wanawake mbali mbali hasa Wajasiriamali wamejenga matumaini makubwa kwa kuungwa mkono juu ya kazi wanazozifanya za kuwaingizia kipato chao cha kila siku.

  Awali Naibu huyo Tunu, alifafanua ratiba ya ziara ya Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia, kuwa Machi 11, mwaka 2019 kuanzia saa 2:00 asubuhi atawasili katika Ofisi ya UWT Mkoa wa Magharibi na kuzungumza na Viongozi mbali mbali katika Wilaya ya Dimani kichama,ambapo saa 9:00 ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Mfenesini kichama kwa kutembelea miradi mbali mbali na kuzungumza na Wana CCM.

  Machi 12,mwaka huu Mwenyekiti wa UWT Taifa ataendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja kwa kukagua Utekelezaji wa Ilani katika Wilaya mbili za Mkoa huo.

  Aidha ziara ya Mwenyekiti huyo itaendelea Machi 13, mwaka huu katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM sambamba na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Wilaya mbili za Mkoa huo.

  Sambamba na hayo ziara hiyo itahitimishwa katika Mkoa wa Mjini Machi 14,mwaka huu ambapo Mwenyekiti huyo atatembelea miradi mbali mbali katika Wilaya mbili za Mkoa huo pamoja na kushiriki shughuli mbali mbali za Ujenzi wa Taifa.

  Mwenyekiti huyo ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwaiba Kisasi, Katibu Mkuu wa UWT Mwl.Queen Mlozi pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Bara Ndugu Jesca Mbogo na kupokelewa na Viongozi mbali mbali wa Chama na Jumuiya zote Tatu za UWT,uvccm pamoja na Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kilosa, Mkoani Morogoro, jana, ambapo amewaagiza Makamanda wa Polisi nchini kuwachunguza na kuwakamata wapinzani wanaomtukana Rais pamoja na Serikali kwa ujumla kupitia vikao vyao vya ndani vya siasa, nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kilosa, Amer Mbaraka, wakati alipokuwa anawasili katika Mkutano wa hadhara, mjini humo, Mkoani Morogoro, jana, kwa ajili ya kuzungumza na wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya Wizara yake. Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Adam Mgoyi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

   
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimfafanulia jambo Mkazi wa Mji wa Kimamba, Wilayani Kilosa, Aris Diamond, wakati alipokuja kutoa kero yake, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini humo, jana. Lugola aliwataka Polisi Mkoani Morogoro kufuata sheria na utaratibu uliopangwa na Jeshi la Polisi bila kuwanyanyasa wananchi wakati taarifa za malalamiko ya ardhi yanaporipotiwa vituoni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mkazi wa Mji wa Kilosa, Mkoani Morogoro, Juma Haruni akitoa malalamiko yake ya ardhi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Waziri huyo, na kufanyika katika uwanja wa Kilosa Town, Mkoani Morogoro, jana. Lugola aliwataka Polisi Mkoani Morogoro kufuata sheria na utaratibu uliopangwa na Jeshi la Polisi bila kuwanyanyasa wananchi wakati taarifa za malalamiko ya ardhi yanaporipotiwa vituoni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ( wa pili kulia) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wanawake wa Mkoa Mwanza katika moja ya banda lililokuwepo katika viwanja vya Kisesa Bujora wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani humo kulia ni Mwalikishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women Bi. Hodan Addou na wa tatu kulia ni Balozi wa Sweden Bw. Anders.

  ……………………………………………………………………………..

  Na Mwandishi Wetu Mwanza

  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametaka kupewa taarifa za waajiri wote hasa Sekta Binafsi waliowafukuza wanawake kazi au kuwashusha vyeo kwa sababu wamepata ujauzito wakiwa kazini.

  Ameyasema hayo mkoani Mwanza alipokuwa akizungumza na Wanawake na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

  Aidha ameitaka Jamii katika maeneo ya kazi kuondokana na rushwa za ngono jambo ambalo ni tatizo katika upatikanaji wa haki za wanawake na waajiri wa Sekta za Binafsi kuzingatia utu na haki za wanawake wafanyakazi.

  “Mwanamke kupata mimba ni haki yake ya asili kutokana na uumbaji wa Mungu na hivyo ni marufuku kuwafukuza kazi Wanawake wafanyakazi hasa Sekta Binafsi kisa kuwa na ujauzito” alisema.

  Ameongeza kuwa suala la usawa wa kijinsia ni muhimu kwa wanaume kushiriki kwani wao ni pia ni wahusika wakuu wa kuwepo kwa vitendo vya Ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

  Waziri Ummy amesema yeye kama Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Wanawake atahakikisha wanapata fursa sawa katika masuala muhimu kwa manufaa ya haki na ustawi wao.

  Ameagiza kutekelezwa kwa haki ya Mwanamke kunyonyesha mara baada ya kumaliza likizo zao za uzazi kwani ni suala la muhimu sana kwa Mtoto kupata maziwa ya mama katika ukuaji wa Mtoto katika umri wa miezi ya awali.

  Aidha Waziri Ummy amekemea vitendo vya rushwa ya nono na kuipongeza Taasisi ya kuoambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU
  kwa kukiona suala hilo ni moja kti ya vitendo vya kikatili afanyiwavyo mwanamke na kumyima haki yake.

  Akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Philis Nyimbi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana amesema mkoa unatekeleza mikakati mbalimbali katika kumuwezesha Mwanamke na Mtoto wa kike kwa kumuweka mbali na Vitendo vya Ukatili dhidi yao ili kuwawezesha kupata fursa zitakazowezesha kufikia usawa wa kijinsia.

  Naye Mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez amesema kuwa Umoja wa Mataifa unataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia na kuondoa vikwazo vyote vinavyosababisha kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia kama vile mimba na ndoa za utotoni ambazo zimekuwa zikiwanyima fursa watoto wa kike kutimiza ndoto zao.

  Ameongeza kuwa mapambano wa usawa wa kijinsia yatafanikiwa pale yatakaposhirikisha wanaume na wavulana katika kuhakikisha wasichana na Wanawake wanapata fursa sawa katika kutimiza ndoto zao.

  Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women Bi. Hodan Addou amesema kuwa Shirika hilo linashirikiana na Serikali na Mashirika ya kitaifa kuhakikisha elimu inatolewa na usawa wa kijinsia inakuwa suala la kipaumbele katika Jamii zetu.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (kushoto) akipata maelezo ya kitaalamu juu ya hali ya mazingira katika eneo la mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Rufiji Hydro Power Project kutoka kwa Dkt. Samuel Gwamaka Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Naibu Waziri amefanya ziara ya kikazi kutembelea eneo hilo mwishoni mwa wiki.
   
  Na Lulu Mussa,Morogoro

  Serikali imesema itahakikisha kuwa vyanzo vya maji vinavyopeleka maji Mto Rufiji havivamiwi kwa shughuli za kilimo na kibinadamu ili Mradi Mkubwa wa kufua umeme katika bonde la Mto Rufiji uweze kutekelezeka.

  Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima mara baada ya kukamilisha ziara yake katika Mikoa sita hapa nchini kwa lengo la kukagua maeneo yenye changamoto za kimazingira pamoja na kutafuta ufumbuzi kwenye ikolojia ya vyanzo vya maji vinavyo changia maji katika bonde la Rufiji.

  Akiwa katika eneo la mradi litakapojengwa bwawa la kufua umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji Naibu Waziri Sima amesema amefanya ziara ya kukagua vyanzo vya maji vya Bonde la Rufiji ambavyo vinahusisha matawi matatu ya mito ambayo ni Mto Ruaha Mkuu, Kilombero, Luegu, na kutoa wito kwa wananchi kutoharibu vyanzo hivyo ili kuwa na maji ya kutosha kutekeleza mradi huo mkubwa.

  “Ziara yangu imeanzia Lindi, Ruvuma, Njombe, Mbeya, Iringa na Kilombero kote huko nimelenga kujione vyanzo hivi vikuu. Mito hii ya Ruaha Mkuu, Kilombero na Luegu inapoungana ndio inatengeneza Mto Rufiji ambako ndiko kuna maporomoko ya “Stiglers Gorge”. Na nimeridhishwa na hatua za watendaji katika ngazi zote za Serikali kwa kuwa mstari wa mbele kukahikisha kuwa vyanzo vya maji vinalindwa na kuhifadhiwa.” Sima alisisitiza.

  Katika ziara yake Naibu Waziri Sima ameweza kutoa miongozo muhimu yenye kukuza, kulinda na kusimamia mazingira kwa namna endelevu husunan Ikolojia ya Vyanzo vya maji katika Mikoa aliyopita. Naibu Waziri Sima amesema Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa kufua umeme wa Maji wa Rufiji Hydro Power Project ambapo zaidi ya MW 2100 za umeme zitazalishwa, hivyo kulingana na ukubwa wa mradi huu ni wazi uhifadhi wa Mazingira katika vyanzo hivyo ni muhimu ukatiliwa mkazo.

  “Uhifadhi wa Mazingira katika Bonde la Rufiji ni wafaida kwa pande zote hasa ustawi wa wananchi. Wananchi ndio walinzi na wahifadhi wa kwanza katika kutunza Mazingira, aidha Sheria ya Mazingira, 2004 kifungu cha 6 kimetamka wajibu wa kila mwananchi kutunza Mazingira kwamba; Mtu yeyote anayeishi Tanzania atakuwa mdau na atawajibika kutunza na kuendeleza Mazingira na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu shughuli au jambo lolote ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kuathiri mazingira. Hivyo kupitia sheria hii si jukumu la Serikali pekee kusimamia uhifadhi wa Mazingira, wananchi nao wana wajibu wa moja kwa moja wa kutunza Mazingira”. Sima alisisitiza.

  Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini Dkt. Samuel Gwamaka alieambatana na Naibu Waziri Sima katika ziara hiyo amesema kuwa Baraza limedhamiria kufungua Ofisi katika eneo hilo la mradi ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya kila siku za Baraza.

  Bonde la Rufiji lina ukubwa wa KM2 177,420 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya Tanzania na linapita katika mikoa 11 ya Tanzania na Wilaya 32 za Tanzania, Bonde hili ni Mashuhuri kwa Kilimo, ufungaji, uvuvi na uzalishaji wa umeme katika vituo vya Mtera na Kihansi.

  0 0


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akifunga Mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Mwanza.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Canisius Kalamaga (kulia) mara baada ya Naibu Waziri huyo kufunga Baraza la 26 la Wafanyakazi wa Wizara lililofanyika jijini Mwanza kwa muda wa siku mbili. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Dkt. James Wakibala.
  Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda akizngumza kabla ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kufunga Mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Mwanza
  Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara akizungumza na watumishi kabla ya Mhe. Constantine Kanyasu kufunga Mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Mwanza.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Adolf Mkenda akiwa ameshikana mikono na baadhi ya watumishi wakiimb wimbo wa mshikamano wakati wa Baraza la 26 la Wafanyakazi jijini Mwanza.
  Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa wameshikana mikono wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa Baraza la 26 la Wafanyakazi jijini Mwanza.

  ……………………………….

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amewataka wananchi kuwachukulia askari wa Wanyamapori na Misitu kama rafiki wa umma na watendaji waliotumwa na Serikali kulinda rasilimali hizo kwa niaba yao.

  Akifunga kikao cha 26 cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Mwanza, Mhe. Kanyasu amesema Askari hao waliopewa dhamana ya kulinda maeneo ya hifadhi nchini wanafanya kazi nzuri ya kuifanya Tanzania iendelee kuwa na maeneo mazuri yaliyohifadhiwa.

  Amesema Askari hao wameajiriwa kwa mujibu wa sheria hivyo hutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi zao na pale wanapokiuka sheria mamlaka zinazohusika huwachukulia hatua.

  “Sisi kama Wizara tunaamini kwamba askari wetu na wahifadhi wetu wanafanya kazi nzuri, pale ambapo wamekuwa wakilaumiwa kwa kuwapiga na kuwanyanyasa watu kwa namna yoyote ile tumetuma Tume maalum kuchunguza na kuchukua hatua” Amesema

  Mhe, Kanyasu amesema uchunguzi unapofanyika na ikathibitika kuwa tukio lililofanyika halikuongozwa na matumizi ya sheria na kuwepo kwa haki wizara imekua ikichukua hatua.

  Ameeeleza kuwa askari wanaolinda Hifadhi nchini wanategemewa na bila wao hakuna uhifadhi unaoweza kuendelea nchini akibainisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipinga juhudi za uhifadhi kwa kuwatetea watu wanaovunja sheria.

  “Watu hawafahamu tu, tukiwaondoa askari wetu wote katika maeneo ya hifadhi na tukawaondoa Maafisa ukaguzi wa mazao ya Misitu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) barabarani, katika kipindi cha miezi 6 nchi hii itageuka kuwa jangwa” Amesisitiza Mhe. Kanyasu.

  Amesema yapo madhara makubwa yanayoweza kutokea kama hakutakuwa na uhifadhi imara ikiwemo maeneo mengi ya nchi kugeuka kuwa jangwa kutokana na uharibifu wa misitu, ukosefu wa mvua, ukosefu wa maji, chakula na ukosefu wa hewa safi.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa kumekuwa na tuhuma za vitendo vya ukatili dhidi ya raia vinavyofanywa na baadhi ya askari wa Hifadhi nchini na kutoa wito kwa wananchi wote wenye ushahidi na taarifa juu ya vitendo hivyo kuziwasilisha ili hatua stahiki zichukuliwe.

  Amesisitiza kuwa Serikali hairuhusu askari kufanya vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya raia badala yake imekua ikiwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali zinazowazunguka.

  Amewatahadharisha na kuwataka wananchi wawe makini dhidi ya kampeni zenye nia ovu zinazoendeshwa na baadhi ya watu zenye lengo la kuwavunja moyo askari wanaojitolea maisha yao kulinda rasilimali za taifa akieleza kuwa wapo askari waliopata madhara makubwa na kupoteza maisha kwa kushambuliwa na majangili kwa kuchomwa mishale yenye sumu na kukatwa vidole wakati wakitimiza wajibu wao.

  Prof. Mkenda amesema kuwa wizara itaendelea kulinda hadhi ya vijana hao waliojitolea maisha yao kulinda rasilimali za Taifa akibainisha kuwa Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria watakaokiuka kanuni na taratibu za kazi kazi ili iwe fundisho kwa wengine.

  Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo amesema kuwa watumishi 23 wa wanyamapori na misitu wamepoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa katika matukio tofauti yaliyotokea wakati wakipambana na majangili.

  Amesema matukio hayo yametokea mwaka 2018/2019 na hifadhi inayoongoza kwa matukio hayo ni Sengereti, Prof. Mkenda amesema kuwa watumishi hao waliofariki na wengine kujeruhiwa walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi hivyo Wizara inaangalia namna ya kuwaenzi kutokana na mchango wao.

  0 0

    Katika Kumuenzi Marehemu Ruge Mutahaba kwa Vitendo na maisha alokuwa akiyaishi, yakiwemo kusaidia vijana na kuinua vipaji vya Vijana katika sekta mbalimbali, Diwani wa Kata Ijuganyondo iliyopo Manispaa ya Bukoba Al-Masoud Kamala ametangaza kuanzisha Rasmi ligi ya Mpira wa Miguu itayojulikana kama "Ruge Cup"

  Diwani Kamala ameyasema hayo katika fainali ya kombe la Wazee lililoandaliwa na Wazee wa Kata ya Kibeta chini ya Mwenyekiti wao Bwana Sadru Nyangasha, ambapo katika Fainali hizo zilizochezwa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kibeta na kuhudhuriwa na wakazi wa kata hiyo na kata jirani, Timu ya Omkituri Fc imeibuka kidedea kwa Ushindi wa Goli 2 kwa 1 dhidi ya Anyama Fc.

  Mh. Kamala amesema ili kumuenzi Ruge kupitia Tasnia ya Michezo hususani mpira wa Miguu anaratibu ligi ya Mpira wa Miguu itayoanza hivi Karibuni itakayoitwa Ruge Cup. Katika mashindano hayo ya Kombe la wazee yaliyoshirikisha jumla ya timu sita, Zawadi kutoka kwa Waandaaji Mshindi wa Kwanza kajipatia Kikombe chenye Thamani ya Shilingi Laki Moja, Mbuzi (mnyama) mwenye thamani ya Shilingi laki moja, mshindi wa pili elfu 30, mshindi wa tatu elfu 20, ukiacha zawadi alizotoa Diwani Kamala Pesa taslimu pamoja na mipira miwili.
   Nahodha wa Timu ya Omkituri Gerevazi Nyomo akiwa amebeba Kombe la Wazee Mara baada ya kumalizika mchezo wa fainali uliowakutanisha na Anyama Fc, na Kuibuka kwa ushindi wa bao 2 kwa 1.
  Pichani Diwani Kamala akisaidiana na Mzee Sadru Nyangasha muaandaji wa mashindano ya Kombe la Wazee, kukabidhi zawadi ya Mbuzi kwa Timu ya Omkituri Fc.
   Mbuzi aina ya Beberu mwenye thamani ya Shilingi laki moja aliyetolewa kama zawadi kwa Mshindi wa kwanza katika mashindano ya Kombe la Wazee.
  Kombe lenye thamani ya Shilingi laki moja likiwa Mezani kabla ya Kupewa Mshindi wa Mashindano ya Kombe la Wazee timu ya Omkituri Fc.  0 0


  VINARA wa huduma za kibenki nchini, Benki ya NMB, wamezindua huduma ya kidijitali ya kuwawezesha Mawakala wa NMB kupata mkopo wa salio la kuhudumia wateja ‘Floti Fasta,’ kupitia NMB Mobile na NMB KLiK pindi wanapoishiwa salio.

  Floti Fasta ni huduma ya uwezeshaji, inayolenga kuwapa nguvu ya ziada mawakala wa NMB waliotapakaa kila kona, kupata salio la dharura wanalohitaji kuhudumu nyakati za usiku ama wikiendi, wanapokosa huduma za kuongeza salio katika matawi ya benki hiyo.

  Huduma hiyo ya kwanza na ya aina yake nchini, imezinduliwa mwishoni mwa wiki, ikilenga kukuza mitaji ya mawakala, lakini pia kuwasaidia kukuza biashara zao, huku wakitengeneza ajira kwa Watanzania wengi kupitia biashara zao za NMB Wakala.

  Kiwango cha chini cha kupata salio kupitia ‘Floti Fasta’ni Sh. 50,000 na kiwango cha juu ni Sh. Milioni 5, huduma ambayo haina riba, bali mwombaji atatozwa asilimia 3 itakayojumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambako tozo litafanyika kabla ya mkopo kutolewa.

  Akizungumza wakati wa kuzindua Floti Fasta, Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Akaunti, Michael Mungure, aliscma kuwa huduma hiyo, itawawezesha zaidi ya mawakala 6,800 kukuza biashara zao na kuwapa uwezo wa kuhudumia wateja wao muda wote.

  “Kupilia huduma hii ya Floti Fasta, tatizo la kuishiwa salio kwa mawakala wetu limepatiwa ufumbuzi, Mteja anatakiwa kutumia NMB Mobile au NMB KliK kuweza kupopa hususani kwa nyakati ambazo hakuna huduma za kibenki kama usiku ama wikiendi,” alisema Mungure.

  Mungure aliongeza kuwa: “Dhamira yetu kila siku imekuwa ni kubuni bidhaa na huduma bora kwa kuangalia changamoto mbalimbali za kifedha nchini na kuzipatia suluhu.

  “Imekuwa wazi kuwa kuna changamoto kubwa kwa mawakala ya kuishiwa floti na hivyo kusababisha wateja kutopata huduma stahiki za kutoa na kuweka fedha hususani baada ya matawi ya NMB kufungwa.

  “Tulipoliona hili tukaona ni fursa kubwa kutoa suruhisho la kifedha ambalo ni rafiki kwa mawakala kupitia NMB Mobile na NMB KLiK,” alisisitiza Mungure.

  Mawakala wa NMB wana mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za kifedha na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa, ambapo Mungure amebainisha kuwa NMB ikiwa kama benki kubwa hapa nchini, inaona umuhimu wa kuwasaidia mawakala wake ilikukidhi mahitaji ya soko.

  “Kwa sasa, wateja wanaopata huduma za kifedha kupitia NMB Wakala wana uhakika wa kupata huduma pasipo hofu ya kukosa floti, kwani kupitia huduma hii, Mawakala wa NMB wanakuwa ndio wa uhakika zaidi katika utoaji huduma za kifedha muda wowote na sehemu yoyote,” alisema.

  Mungure alisema kuwa, pamoja na kwamba huduma hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia mawakala wa NMB, faida yake inakwenda mbali zaidi na kumfikia hata asiye mteja wa NMB, ambaye ataweza kulipa Kodi za Serikali na bili kama za Dawasco, LUKU, muda wa maongezi na kulipa ving’amuzi.

  Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, Donatus Richard akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma mpya ya kiditali Floti Fasta. Kulia ni Mkuu wa malipo na akaunti, Michael Mungure.

   Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, Donatus Richard akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma mpya ya kiditali Floti Fasta. Katikati ni  Mkuu wa malipo na akaunti, Michael Mungure na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha wakala, Ericky Willy.

  0 0  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kuelekea Kampala, Uganda kushiriki kwenye Mkutano wa mwaka 2019 wa ‘Africa Now Summit’unaotarajiwa kufanyika tarehe12 na 13 Machi.Mhe. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

  Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano huu. Mkutano utakuwa na mada mbalimbali ikiwemo ya Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika, mada hii itatolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
  Viongozi wengine watakaotoa mada ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA) Mhe. Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. William Ruto; na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Ahmed Abiy. Mada zote hizi zitajikita kwenye kuonesha chachu ya Uongozi katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika. 
  Mkutano utamalizika tarehe 13 Machi 2019 utaanza na hotuba kutoka kwa Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi na baadae kufungwa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.
  Makamu wa Rais ataambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. 

  Imetolewa na: 
  Ofisi ya Makamu wa Rais 
  Dar es salaam 
  11/03/2019

  0 0

  The United Bank for Africa Tanzania (UBA) has celebrated the International Women’s Day by donating 100 bed sheets to Temeke Referral Hospital in Dar es Salaam being one of the banks Corporate Social Responsibility (CSR) initiative in supporting the surrounding community.

  The Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki, Temeke Member of Parliament Abdallah Mtolea and the Hospitals Senior Consultant Dr Amaan Malima received the donation of the bed sheets on behalf of the hospital.

  Speaking after receiving the donations, the Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki said the International Women’s Day is a special day for women to celebrate the social, economic, cultural and political achievements of women. For that matter, I am very happy to learn that the United Bank for Africa Tanzania women staff have contributed their own funds that they have used to purchase the donations of bed sheets we are receiving today. You could have used the money on your celebrations but they decided to and celebrate with the less privileged and sick in this hospital. That is something that must be emulated by others and to me you have set a very good example and I must congratulate you for that, Minister Kariuki said.

  The minister added that women are important pillars for our family and nation. You must always work hard and set goals in order to be successful. In addition, it is good to understand that women have the same talents and ability to work just like your counterpart men but is good to stay focused and set your time properly in order to continue being successful on your careers, said Kariuki. Adding, “I call upon UBA Tanzania and other stakeholders to continue supporting us our communities and especially in health sector so that we grow as one nation.

  The Temeke Referral Hospital Hospitals Senior Consultant Dr Amaan Malima appreciated the banks donation saying that the hospital has been experiencing shortage of bed sheets for quite long time. ‘Your donation has come at very right time our hospital has been going a difficult time due to bed sheets. We receive large number of patients and so the number cannot match on the bed sheets we have. We cherish you danations and wish you good luck on your activities and we welcome you again for any other donations in future, Dr Malima said.

  On his part, UBA Bank Tanzania Chief Operating Officer Flavia Kiyanga said that giving back to the community has been one of the banks’ long time initiatives. The surrounding society means a lot to us, by extending our hands to less privileged is our concern and this time we have decided to support Temeke Referral Hospital putting in mind that some of the patients admitted at this hospital have no close relatives to support them and therefore donating and visiting them will make them feel just like the others.

  Kiyanga said that the donation of the bed sheets has been as result of UBA Tanzania women who have decided to contribute their own funds to come and celebrate the women’s International Day by donating bed sheets to this hospital. We are happy that we have managed to fulfill one of our longest commitments and most important we thank the Temeke Referral Hospital for good treatment they have offered to us, said Kiyanga.
  UBA Bank Tanzania Chief Operating Officer Flavia Kiyanga (right) hands bed sheets to Temeke Member of Parliament Abdallah Mtolea (left) in Dar es Salaam over the weekend. UBA Bank Tanzania donated 100 bed sheets to Temeke Referral Hospital as way of celebrating this year’s Women Day. Looking on are The Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki (2nd right) and the Hospitals Senior Consultant Dr. Amaan Malima (2nd left).

  UBA Bank Tanzania Chief Operating Officer Flavia Kiyanga (right) hands bed sheets to The Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki (2nd right). UBA Bank Tanzania donated 100 bed sheets to Temeke Referral Hospital as way of celebrating this year’s Women Day Left is Temeke Member of Parliament Abdallah Mtolea and the Hospitals Senior Consultant Dr. Amaan Malima (2nd left).

  The Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki (2nd right) and Temeke Member of Parliament Abdallah Mtolea (left) keenly examine bed sheets donated by UBA Bank Tanzania to Temeke Referral Hospital. UBA Bank Tanzania donated 100 bed sheets to Temeke Referral Hospital as way of celebrating this year’s Women Day. Right is the Hospitals Senior Consultant Dr. Amaan Malima.
  The Minister of State in the Prime Minister’s Office responsible for Investment Angela Kariuki (2nd right) and Temeke Member of Parliament Abdallah Mtolea (left) display bed sheets donated by UBA Bank Tanzania to Temeke Referral Hospital. UBA Bank Tanzania donated 100 bed sheets to Temeke Referral Hospital as way of celebrating this year’s Women Day. Right is the Hospitals Senior Consultant Dr. Amaan Malima.

  0 0

   Ofisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Jennifer Kotta akitambulisha meza kuu wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akitoa neno la ukaribisho wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo.
   Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili kushoto) akibariki kuanza kwa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Balozi wa Ubalozi wa Korea Kusini nchini, Jiin An, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (kushoto).
   Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO nchini, Faith Shayo akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia Dk. Noel Mbonde akiwasilisha mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
   Naibu Balozi wa Ubalozi wa Korea Kusini nchini, Jiin An akishiriki kwenye majadiliano na makubaliano kuhusu mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla akiwasilisha maoni kwenye majadiliano na makubaliano kuhusu mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo na kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos.
   Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (katikati) akiendesha majadiliano na makubaliano kuhusu mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla na kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos
   Ofisa Mwandamizi Elimu, kitengo cha Elimu ya Ufundi Stadi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Fides Lubuva akiwapitisha wajumbe kwenye bajeti wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Unesco (UNESCO-NATCOM), Francis Msungu akishiriki kwenye majadiliano na makubaliano kuhusu mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya wajumbe wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
   Mmoja wa wajumbe akichangia maoni wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.

  Na Mwandishi wetu
  KAMATI ya kitaifa ya mradi mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) imekutana jijini Dar es salaam kupitia pamoja na mambo mengine ratiba ya utekelezaji wa mradi huo.
  Mradi huo ambao unajulikana kama The Better Education for Africa's Rise, (BEAR) unaendeshwa pia katika nchi za Madagascar, Ethiopia, Uganda na Kenya na ni sehemu ya mradi wa kimataifa wa elimu maarufu kama Education 2030 Agenda , moja ya malengo ya maendeleo endelevu ya kimataifa, lengo namba nne, na unafadhiliwa na Korea kusini kwa dola za Marekani milioni 10.
  Akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO nchini, Faith Shayo alisema kwamba mradi huo unaotarajiwa kukamilika 2021 umelenga kuboresha utaalamu na kuwezesha vijana kuajiriwa au kujiajiri wenyewe kwa kuangalia fursa zilizopo kwa kadri ya mahitaji ya nchi.
  Mradi huo ambao sasa unaingia katika awamu ya pili,na hivyo kujulikana kama BEAR ll ulianza mwaka 2017 na unatarajiwa kutekelezwa hadi 2021, kazi kubwa ikiwa ni kuwezesha vijana kupata ajira zenye staha na pia kujenga uwezo wa kujiajiri kwa vijana kwa kuboresha mifumo na ufundishaji wa elimu ya ufundi stadi.
  Alisema nchini Ethiopia, mradi huu umejikita zaidi katika sekta ya uchakataji mazao ya kilimo; Kenya ipo uhifadhi wa mazingira, utengenezaji wa nafasi za kazi za kutunza mazingira; Madagascar ipo kwenye viwanda vya nguo; Uganda imejikita katika menejimenti ya mazao baada ya kuvunwa na uchakataji wa bidhaa za chakula zinazotokana na kilimo wakati nchini Tanzania imejikita katika biashara za mazao ya kilimo na ubunifu.
  “Tunatarajia baada ya kukamilika kwa mradi huu kutakuwepo na maendeleo makubwa katika mifumo ya elimu na ufundishaji wa elimu ya ufundi stadi nchini Tanzania,” alisema Shayo wakati akiwasilisha mpango kazi unaotakiwa kufuatwa katika kikao hicho cha kitaifa mwishoni mwa wiki.
  Alisema kwamba BEAR II inatekelezwa kwa kuzingatia fundisho lililopatikana kwenye awamu ya kwanza iliyoanza 2011-2016 ambayo ilisaidia kunoa mifumo ya ufundi stadi na ufundishaji wake katika nchi 5 za Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Afrika (SADC)  za Botswana, DR Congo, Malawi, Namibia, na Zambia.
  BEAR II ambayo inajengwa  kwa kuzingatia vipaumbele vya kila taifa, inaingilia maeneo matatu ili kufanya mafunzo ya ufundi kuwa na maana zaidi kwa kuzingatia mahitaji ya kiuchumi na soko; kuboresha zaidi programu zinazoambatana na elimu hiyo na pia kuboresha uelewa na matamanio ya elimu ya ufundi miongoni mwa vijana.
  Mradi wa BEAR kwa kila nchi unafanywa kwa ushirikiano kati ya wadau mbalimbali wa elimu, wizara ya elimu na serikali za nchi husika.
  Imeelezwa kuwa kazi kubwa ya UNESCO katika mradi huo ni ya menejimenti, ufuatiliaji na ufanyaji wa tathmini na serikali ya Korea yenyewe itatengeneza mfumo wa ufuatiliaji na kufadhili utekelezaji wake.


  0 0


  0 0

   
  SEHEMU ya Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakishiki maandamano katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Maandamano yalianzia Chuoni hapo na kuhitimishwa eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
   SEHEMU ya Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakishiki maandamano katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Maandamano yalianzia Chuoni hapo na kumalizikia eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  BAADHI ya Wanawake wa Tawi la Chama cha wafanyakazi wa Elimu ya juu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakiwa wakipita mbele ya jukwaa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyohitimishwa katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri na viongozi mbalimbali. 
  SEHEMU ya Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifuatilia matukio mbalimbali katika ukumbi wa Mlimani City  wakati wa maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam.
   BAADHI ya Wanawake wa Tawi la Chama cha wafanyakazi wa Elimu ya juu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakiwa wamebeba dawa na mahitaji muhimu ya kibinadamu walipowasili katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutoa msaada kwa watoto wenye saratani jijini Dar es Salaam Machi 9 2019. 
  MWENYEKITI wa Kamati ya Wanawake wa Tawi la Chama cha wafanyakazi wa Elimu ya juu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Dkt. Kerbina Moyo (wa pili kushoto) na Mhazini Grace Nakoba (kushoto) wakimkabidhi Peter Massawe, Mwakilishi wa wagonjwa wanaotibiwa kwenye wodi ya watoto wenye saratani katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), sehemu ya msaada wa dawa na mahitaji muhimu ya kibinadamu jijini Dar es Salaam Machi 9 2019. Pamoja nao (wa pili kulia) ni Kaimu Msimamizi mkuu wa Wodi hiyo, Ephraim Kiswaga.

  0 0


  Mauzo ya moja kwa moja yanazidi kuongezeka Afrika Mashariki wakati vijana wenye ujuzi wa teknolojia wakitafuta fursa mpya za ujasiriamali. 

  · QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inaimarisha soko la kanda kwa kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na kukuza ari mpya ya ujasiriamali. 

  Mauzo ya moja kwa moja (maafuru kama network marketing) yanakuwa kwa kasi katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara ya Afrika na hasa Afrika Mashariki, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limesababishwa na ongezeko la idadi ya watu katika kanda hii pamoja na vijana mahiri ambao kwa mujibu wa taarifa ya Uchambuzi wa Ongezeko la Vijana ya Taasisi ya Maendeleo ya Afrika - sasa Afrika Mashariki ina zaidi ya 45% ya vijana kati ya watu milioni 150 walioko Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda. Wengi wa vijana hawa wana elimu, kwa ujumla wana ufahamu wa teknolojia, wepesi kufuata mienendo mipya, wana hamasa ya kuweka juhudi na fikra za ujasiriamali - jambo ambalo ndio sifa ya awali ya mafanikio endelevu katika biashara ya uuzaji wa moja kwa moja. 

  Kwa wanaoanza, mauzo ya moja kwa moja ni wazo la biashara ya kimataifa na linaelezewa kama 'uuzaji wa bidhaa za matumizi au huduma, kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mtu mwingine, mbali na maeneo ya maduka ya kawaida'. Mtindo huu wa mauzo una zaidi ya miaka 100 na mwanzoni kabisa ulianzia huko USA. Leo, sasa karibu takribani watu milioni 117 wanajihusisha nayo. Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2018 ya Shirikisho la Chama cha Wauzaji wa moja kwa moja Ulimwenguni.(World Federation of Direct Selling Association (WFDSA), mauzo ya moja kwa moja yalizalisha $190 bilioni na karibu nusu ya mauzo yote yametoka katika masoko yanayochipukia: 


  Inatosheleza kusema, Afrika ina chukua chini ya 1% ya jumla ya mauzo ya WFDSA lakini wataalamu wanakadiria kwamba soko la Afrika Mashariki linatoa fursa ya kukua kwa wajasiriamali wanaochipukia na hata kwa wale walioajiriwa na wana kiu ya kujipatia kipato cha nyongeza kupitia mauzo ya moja kwa moja. 

  Katika kanda ambayo mahitaji ya ajira rasmi yanazidi kuwa na ushindani mkubwa na uhaba wa ajira rasmi, mauzo ya moja kwa moja yanatoa njia mbadala za ajira tofauti na ilivyozoeleka kwa wale wanaohitaji kipato cha ziada au mazingira haya ruhusu ajira. 

  Akiongea hivi karibuni wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET kwa kanda ya kusini mwa Jangwa la Sahara alisema "QNET imesaidia kuwawezesha maelfu ya watuAfrika, hasa vijana, katika muongo uliopita. Tunaona ongezeko la kukubalika kwa Mauzo ya Moja kwa Moja, na idadi ya watu zaidi ya milioni 200 katika Afrika Mashariki, Mtindo huu ni mtindo unaobadilisha maisha kwa wengi" 

  QNET inatoa aina mbalimbali za bidhaa za afya, ustawi na mitindo ya maisha kupitia mifumo yake ya biashara ya mitandao (e-commerce) kwa mamilioni ya wateja katika zaidi ya nchi 100, ikiwa inasaidia watu kuishi maisha bora, na kutoa njia mbadala ya kujipatia kipato kwa yeyote anayehitaji kutumia fursa hii. Kampuni pia ina ofisi na mawakala washirika katika nchi 25 duniani kote, na zaidi ya stoo 50, shughuli za uendeshaji na maduka na wauzaji katika nchi kadhaa duniani. Sasa kwa uwepo wake imara katika Afrika Mashariki, QNET imejidhatiti katika kuendeleza mtindo wa mauzo wa moja kwa moja katika kanda hii. 

  Kwa kuongezea QNET pia inarudisha faida yake kwa jamii. Baadhi ya wanufaikaji wa Majukumu ya Kampuni kwa jamii ni pamoja na kituo cha kulelea yatima cha Maunga, na Kituo cha kulele yatima cha Newlife Orphans Home ambavyo vimepokea msaada wa chakula na michango kwa miaka ya hivi karibuni. 

  Kwa mujibu wa Biram Fall Meneja Mkuu wa QNET katika Kanda ya Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara; "QNET ina nia ya kurudisha kwa jamii, Hii ndio sababu kwa nini tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika miradi ya uwajibikaji endelevu ya kampuni kwa jamii katika maeneo mbalimbali ya Afrika kupitia katika mkono wetu wa uwajibikaji kwa jamii” alisema Fall. 

  QNET Ghana, kwa kupitia RYTHM Foundation, imetoa vifaa maalumu 50 vya kusomea vitabu vya kielektroniki (Kindle e-readers) ambavyo vina vitabu 100 vinavyoendana na tamaduni zao kila kimoja. kwaajili ya wanafunzi wa Nima, eneo lenye watu wa kipato cha chini zaidi ndani ya jiji wa Accra, Ghana. Ilikuwa ni mradi uliofanyika kwa ushirikiano na Worldreader, NGO ya utoaji wa elimu duniani na Achievers Ghana, taasisi ya elimu kwa jamii. 

  QNET pia inafanya vizuri katika udhamini wa michezo duniani. Baadhi ya ushirikiano mkubwa wa hivi karibuni unajumuisha kuwa Wauzaji wa Moja kwa Moja wa Klabu ya Mpira wa miguu ya Manchester City na Klabu ya mpira wa miguu kwa wanawake ya Manchester city na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwaajili ya ligi ya mabingwa ya Total CAF, Kombe la shirikisho la Total CAF na Total CAF Super Cup kwa mwaka 2018 na 2019. Hapo awali washirika wakubwa walikuwa ni pamoja na Formula One, badminton na zaidi, kutokana na imani thabiti ya kampuni kwamba msukumo, shauku na kufanya kazi katika timu iliyopo katika michezo inaendana na ule wa QNET.   Manufaa 

  Imani thabiti ya QNET kwamba hakuna kinachowezesha zaidi kwa mtu binafsi kama uhuru wa kifedha ambao unatolewa na jitihada katika sekta ya mauzo ya moja kwa moja, na inaamini kwamba watu wa Afrika Mashariki, pamoja na shauku yao na fikra za ujasiriamali, watafurahia kiwango bora cha bidhaa zinazotolewa na QNET na fursa za kibiashara kwaajili ya maendeleo binafsi. 

  Mauzo ya Moja kwa Moja yanaweza kuwa ni kazi ya kutosheleza kwa wale ambao wanachagua kuchukua fursa hii kama kazi yao kuu au hata kuchukua kama kazi ya ziada kwa sababu inatoa faida za kifedha kutegemeana na muda na juhudi unazoweka katika kukuza biashara yako. Kwa kuongezea, tofauti na biashara zingine za kawaida ambazo zinahitaji mtaji mkubwa, rasilimali na hata uzoefu, biashara ya mauzo ya moja kwa moja inatoa fursa hii ya biashara yenye gharama nafuu kwa kila mmoja anayehitaji kuianzisha, bila kujali kiwango chao cha elimu au uzoefu. Zaidi ya hayo, mafunzo na maelekezo ambayo wafanyabiashara wanaoanza wanapitia (Wawakilishi wa Kujitegemea au IRs kama ilivyo katika QNET) inawapatia ujuzi wa pekee ambao unapelekea kuwa na ujasiri, kujitambua na hatimae ukuaji binafsi ambao unatambua utaalamu wa mtu kama mjasiriamali aliyekamilika. 

  Huenda, manufaa makubwa zaidi ya mauzo ya moja kwa moja katika masoko yanayoibukia kama Afrika Mashariki ni kwamba mtindo huu unakuwa na athari zaidi hapa kuliko katika masoko yaliyoendelea kwa sababu ya athari za kifedha inayoweza kuleta katika maisha ya watu - kutoa fursa za ujasiriamali kwa wote, bila kujali ujuzi au uzoefu, hivyo hatimae kuchangia katika kupunguza umasikini katika jamii. 

  Katika mizizi ya QNET kuna falsafa ya RYTHM – Raise Yourself To Help Mankind - ambayo inaongoza jitihada zake zote, na kuendesha kampuni sio tu kubadilisha maisha ya watu duniani kote, lakini pia kushirikiana nao katika kupanua athari hizi. 

  Kama alivyosema bwana Trevor Kuna, Mkurugenzi Mtendaji wa QNET "Tunaamini kwamba mafanikio ya kifedha peke yake hayatoshelezi" Ili tuweze kuleta athari, tunahitaji kuendeleza watu kuwa binadamu bora ili waweze kutumia mafanikio yao kuchangia katika jamii zao" 


  Changamoto 

  Kama ilivyo katika biashara nyingine yoyote Sekta ya Mauzo ya Moja kwa moja pia inakabiliana na changamoto. Changamoto ambayo ni kubwa zaidi miongoni mwa hizi ni kuenea kwa mifumo ya pyramid schemes inayoenda kinyume cha sheria ambayo inaonekana kama makampuni halisi ya biashara ya moja kwa moja, ikiwa inaahidi wawekezaji kuwa watajipatia faida nyingi kupita kiasi iwapo wataunganisha watu wengine. Ukweli ni kwamba hawa 'matapeli' wanatengeneza taswira potofu ya Sekta ya Mauzo ya Moja kwa Moja, jambo ambalo linatengeneza kikwazo kwa makampuni halisi kama QNET kusajili washauri wa kibiashara kuendesha biashara zao halisi na halali. Wakati inapokabiliana na hali kama hizo, QNET inasema inatatua tatizo kwa kuelimisha umma kuwa makini na 'matapeli' kama hao na kuwahimiza kuthibitisha uhalali wa kampuni yeyote kufuatana na kutii kwake kwa kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa na bodi zinazosimamia na mamlaka zinazohusika. 

  Mpaka kufikia hapa, maelezo kutoka QNET yanasema: "Kampuni yoyote inayokuahidi njia rahisi ya kuwa tajiri inapaswa kuangaliwa kwa tahadhari. QNET kwa mfano, ina maelezo ya kutosha ya mapato yanayopatikana kwenye tovuti yake na vifaa vya mauzo. Kampuni za Masoko ya mtandao zinatoa bidhaa zenye ubora au huduma tofauti na mifumo ya pyramid schemes ambayo haina bidhaa halali au huduma. Kampuni bora ya Masoko ya mtandao huwa inatenga kiwango kikubwa cha rasilimali kwaajili ya utafiti na uendelezaji, kutengeneza bidhaa zenye ubora ambazo zina matumizi halisi kwa watu wakati mifumo ya pyramids scheme huwa haifanyi hivyo" 

  Inaongeza: "Kampuni za masoko ya mtandano yana sera na taratibu sahihi, pamoja na kanuni za maadili za masoko. Kamuni yoyote halisi ya masoko ya mtandao ina lengo la kufikia ukuaji endelevu kwa kukuza utamanuni wa masoko ya kimaadili. QNET inaweka msisitizo mkubwa katika kanuni za maadili za utendaji kwa wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs) na kuwapatia miongozo ya kina kuhusu masoko ya kitaalamu pamoja na sera na taratibu". 

  Kusisitiza uhalali wa mauzo ya moja kwa moja, utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Ngazi Mbalimbali za Masoko ya India (India Multi-Level Marketing Institute) ilichunguza uendeshaji wa aina mbalimbali kama vile Avon, Mary Kay, QNET na Tupperware na kubaini kwamba 'sio mifumo ya scheme) ya aina ya piramidi au aina nyingine yoyote. 

  Changamoto nyingine inayoikabili sekta ya mauzo ya moja kwa moja ni ujuzi ambao haujaendelezwa hasa kwa wale ambao wamechukua fursa hii hivi karibuni. QNET inasema kwamba inatatua changamoto kwa kuweka msisitizo mkubwa sana katika mafunzo na elimu kwa IRs. Mafunzo hayo sio tu kamba yanaendeleza ujuzi wao wa kitaalamu lakini pia unalenga katika ukuaji na maendeleo binafsi. 

  Ni wazi kwamba, kufikisha bidhaa katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mbali ni kikwazo kingine lakini QNET imeweza kutatua hili kwa kuajiri IRs ambao wanatengeneza mtandao ndani ya jamii zao kwaajili ya kurahisisha upatikanaji na pia kuwasaidia kuagiza mzigo mkubwa kwa punguzo kwa lengo la kutoa mzigo, hivyo kuhakikisha usambazaji endelevu wa bidhaa. 

  Kuingia kwa QNET katika soko la kanda inaweza pia kukabikiana na ushindani kutoka kwa kampuni ambazo tayari zilishaanzishwa za bidhaa za reja reja na nembo za kimataifa lakini mtindo wake wa pekee wa usambazaji utaiweka QNET tofauti na kutengeneza njia ya mafanikio.

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Aziz P. Mlima mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe nchini Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe. Philemon Mateke mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe tayari kwa kushiriki mkutano wa Africa Now Summit 2019 utakaofanyika mjini Kampala tarehe 12 na 13 mwezi Machi, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya ndege ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300 wakati akielekea nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa Africa Now Summit 2019 unaoanza kesho tarehe 12 mjini Kampala Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Uganda na kupokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Philemon Mateke pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Aziz P. Mlima katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebe.

  Makamu wa Rais pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaru wamesafiri na ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Tanzania aina ya Airbus A220-300 (Dodoma) kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Entebe kupitia Kilimanjaro.

  Kesho Makamu wa Rais atashiriki mkutano wa mwaka 2019 wa “Africa Now Summit 2019” ambao utafunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambapo viongozi mbalimbali wa Afrika wanakutana ili kupata majibu ya changamoto za Afrika katika masuala ya kiuchumi.

  Katika mkutano huo wa Viongozi wa Afrika, Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo katika mada mbalimbali zitakazojadiliwa Makamu wa Rais atazungumzia suala la Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika. 

  Viongozi wengine watakaotoa mada ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA) Mhe. Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. William Ruto; na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Ahmed Abiy na Rais Paul Kagame wa Rwanda. Mada zote hizi zitajikita kwenye kuonesha chachu ya Uongozi katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika. 

  Mkutano utamalizika tarehe 13 Machi 2019 utaanza na hotuba kutoka kwa Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi na baadae kufungwa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

  Makamu wa Rais ataambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.

older | 1 | .... | 1815 | 1816 | (Page 1817) | 1818 | 1819 | .... | 1896 | newer