Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1812 | 1813 | (Page 1814) | 1815 | 1816 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakikimbia mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon 2019 Kilomita 21, zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanajro.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakikimbia mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon 2019 Kilomita 21, zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanajro.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakifurahia Medali walizokabidhiwa baada ya kushiriki na kumaliza mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanajro.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakifurahia Medali walizokabidhiwa baada ya kushiriki na kumaliza mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon Kilomita 21 zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanajro.
  Sehemu ya wanariadha walioshiriki mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanajro wakiwa katika picha ya kumbukumbu.

  0 0

  Mchezaji wa timu ya DTB FC, Godfrey Wambura, akikabiliana na washambuliaji toka timu ya Buyuni FC katika mechi ya mwisho ya hatua ya Sita Bora ya ligi ya Kanda ya Dar es Salaam iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala B. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
  Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya benki ya (DTB FC) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanikiwa kufuzu katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayosimamiwa na Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF).  Timu ya mpira wa miguu ya benki ya (DTB FC) imefanikiwa kufuzu katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayosimamiwa na Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF).

  DTB FC imepata nafasi hiyo baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Mbuyuni FC katika mchezo wa mwisho uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala B katika manispaa ya Kinondoni.

  Timu hiyo imemaliza katika nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi tisa (9) baada ya kucheza mechi tano.Ubora wa Timu ya DTB umedhihirika baada ya kushinda michezo miwili (2), kutoka suluhu katika michezo mitatu (3) na kutokupoteza mchezo hata mmoja.

  Timu nyingine zilizopata nafasi ya kuiwakilisha mkoa wa Dar es Salaam ni Pan African na Buyuni FC.Mbali ya timu hizo tatu, timu nyingine zilizoshiriki katika hatua ya Sita bora ni Kigamboni FC, Ungindoni FC na Panama.

  Meneja wa timu ya DTB FC, Michael Lugalela amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya ligi ya mabingwa wa mikoa na kuwataka wasibweteke.

  “Natoa shukrani kwa uongozi wa benki ya DTB kwa kuihudimia timu kuanzia kushiriki katika mashindano mbali mbali na mpaka kushiriki katika ligi ya mkoa na kufuzu kuwania nafasi ya kushiriki ligi daraja la pili ya TFF, tunajivunia na tumedhihirisha kuwa tunaweza,” alisema Michael.

  Alisema kuwa bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanafanya vyema katika mashindano hayo ambayo ushirikisha timu bingwa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

  0 0

  Anaandika Dixon Busagaga.Hai.

  WAZIRI wa fedha na Mipango Dkt Philip Mpango akiwa ameongozana na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angela Kairuki wamefika katika wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro kushughulikia kile alichokiita unyanyasaji kwa wawekezaji.

  Mawaziri hao wanakutana na Makundi mbalimbali kwa nyakati tofauti kusikiliza malalamiko yao waliyowasilisha kwa Mh Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

  Miongoni mwa Makundi na taasisi zinazoshiriki kikao hicho kinachofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai n pamoja na kundi la wawekezaji, Viongozi wa vyama vya ushirika,Mamlaka ya Mapato (TRA) ,Uhamiaji,TIC na Viongozi was serikali ngazi ya mkoa na wilaya ya Hai na Siha.
  Waziri was Fedha na Mpango ,Dkt Philip Mpango (katika) akizungumza wakati wa kikao na wawekezaji wenye malalamiko pamoja na Viongozi wa serikali na baadhi ya taasisi zake.kushoto ni Waziri was nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angela Kairuki na kulia no Mkuu wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira.
  Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango kuhusu unyanyasaji kwa wawekezaji.


  0 0

  LONDON, UINGEREZA

  WIKI tatu tu baada ya Kundi la Himaya ya Kibenki la United Bank of Africa (UBA Group) kuzindua shughuli zake nchini Mali, limefanya hivyo pia katika jiji la London, Uingereza.

  Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa hafla maalumu Alhamisi iliyopita wakati jiji hili la kibiashara lilipokuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa kibiashara na sekta ya umma.

  Katika hafla maalumu ya mkutano huo, UBA UK ilitambulishwa rasmi kwa viongozi wa kibiashara kutoka Ulaya na Afrika ikiwa na dhamira na utayari wa kuchochea biashara baina ya mabara hayo.

  Kwa uzinduzi huo, UBA Group inazidi kujipanua katika sekta ya kibenki ikiwa kama taasisi ya kwanza na pekee ya kifedha kusini mwa jangwa la Sahara Afrika inayoendesha shughuli nchini Uingereza na Marekani.

  Hilo linaifanya kuzidi kuitambulisha hadhi yake kama benki ya kidunia kutoka Afrika inayowezesha biashara na mtiririko wa mitaji baina ya Afrika na Dunia.

  Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti wa UBA Group, Tony Elumelu alisema benki imefurahishwa na mamlaka za Uingereza kuiruhusu kuimarisha na kupanua operesheni zake na hivyo kutimiza dhamira yake ya kupanua biashara na uwekezaji baina ya Afrika na Ulaya.

  Elumelu pia alieleza furaha yake kuona UBA kama benki kutoka Afrika inavyoweza kuchomoza na kusaidia wawekezaji katika miji muhimu ya kifedha duniani.

  Akizungumza katika tukio hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa UBA Group, Kennedy Uzoka, alisema; “Wakati huo huo tunahudumia mahitaji ya kibiashara na mitaji kwa wateja wetu wa Afrika, ambao wanatafuta masoko Ulaya.

  “Kwa kuzindua UBA UK Limited, tunafurahi kupanua huduma hizo kwa wateja wa sasa, wakati huo huo tukikaribisha wapya waweze kikamilifu kutimiza ndoto zao za kifedha kupitia mtandao wetu wa kibenki.”.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Uingereza, Patrick Gutmann, Mkurugenzi Mtendaji, UBA Plc, Kennedy Uzoka, Rais Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote, Mwenyekiti wa UBA Group, Tony Elumelu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wakati wa uzinduzi wa UBA London nchini Uingereza.

  0 0

  Andrew Chimesela - Morogoro
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Mkoa na Wilaya ya Kilosa kuwakamata wale wote wanaotuhumiwa kuwavamia wananchi wanaolima  katika mashamba yaliyofutiwa umiliki wake na Mhe. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Dkt. Kebwe ametoa kauli hiyo Machi, 3 Mwaka huu alipofanya ziara Wilayani Kilosa iliyolenga kujiridhisha utekelezaji wa mashamba yaliyofutwa mwaka 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na kuagiza mashamba hayo kupangiwa matumizi mengine ikiwa ni pamoja na kuyagawa kwa wananchi wa maeneo jirani na mashamba hayo.
  Akiwa Wilayani Kilosa, Dkt. Kebwe aliongea na wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe ambavyo viko jirani na shamba hayo matano kati ya 11 yaliyofutiwa umiliki Wilayani humo huku wananchi waliopewa kuyatumia kwa muda wakilalamika kupewa vitisho na baadhi ya watu kutojihusisha kulima mashamba hayo kwa madai kuwa ni mali yao.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro baada ya kupokea malalamiko hayo anaagiza Jeshi la polisi kuwakamata wale wote wanaowatishia wakulima hao. “Na hili naelekeza  Vyombo vya Ulinzi na Usalama, muanze kupekua kuanzia sasa, kama kuna kikundi cha watu kuna watu au hata mtu binafsi kafanya hivyo chukua hatua, kwa sababu sheria zipo” alisema  Dkt. Kebwe. 
  Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliwahakikishia wananchi wa vijiji hivyo kuwa kila mtu ambaye hana eneo la kulima atapatiwa kupitia mashamba hayo yaliyofutwa na Mhe. Rais ili kila mwananchi aweze kuzalisha na kujikimu kimaisha huku akionya kutoingiza itikadi ya aina yoyote kwenye mashamba hayo yaliyofutwa na Mhe. Rais.

  Katika hatua nyingine Dkt. Kebwe amewataka wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe, kufuata utaratibu uliotolewa na Serikali wa kuyatumia mashamba hayo kwa muda wakisubiri mpango rasmi unaoendelea kuandaliwa na Serikali huku akiwaonya wanaotaka kuanzisha mipango mingine ya matumizi ya Ardhi hiyo  kinyume na mipango ya Serikali kusitisha mara moja mipango hiyo.
  “Vyombo vyangu vinaniambia wale walikwenda wakavamia maeneo hayo walitaka waanzishe  mpango mwingine mpya, yaani juhudi zote hizi ambazo Serikali imefanya kwake yeye  si kitu. sasa hao mtusaidie tuwafahamu ni akina nani na tuwachukulie hatua, sio kuwafahamu tu” aliongeza Dkt. Kebwe.
  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amewataka wananchi wa vijiji vya Mvumi na Gongwe kukomesha tabia ya ubishi na ugomvi baina yao, badala yake watekeleze maagizo ya Serikali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na kuwatahadhalisha kuwa atakayekwenda kinyume na maagizo hayo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za sheria.
  Awali Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Kati, Hezekiely Kitilya aliewaeleza wananchi wa vijiji vya Mvumi na Gongwe kuwa Ardhi ya mashamba hayo matano kwa sasa bado ni ya Mhe. Rais na iko chini Kamishna wa Ardhi na wananchi wamepewa kuitumia kwa muda, hivyo ni vema wananchi wakawa watulivu na kuacha ugomvi baina yao.
  Sambamba na hilo Bw. Kitilya aliwakumbusha wananchi maelekezo yaliyotolewa na ya Mhe. Rais mara baada ya kuyafuta, ambapo alisema kipaumbele cha kwanza kinawalenga  wananchi wanaozunguka mashamba hayo, cha pili ni kutenga Ardhi hiyo kwa ajili ya Uwekezaji wenye tija wa ndani na nje ya nchi na kuwa na hazina ya Ardhi kwa ajili matumizi mengine ya baadae.
  Kwa mujibu wa Afisa Ardhi Wilaya ya Kilosa Bw. Ibrahim Ndembo, alisema Mashamba hayo matano Na. 32 hadi 36 yenye jumla ya Ekari 2,685, baada ya Mhe. Rais kuyafuta, Wilaya ilipeleka maombi Serikalini ili kupewa idhini ya kutumia mashamba hayo kwa muda ombi ambalo lilikubaliwa.
  Baada ya kukubaliwana Wilaya iliunda Kamati za ugawaji maeneo ya mashamba hayo na kuyagawa katika sehemu mbili, Ekari 1000 kwa ajili ya wananchi wa Kijiji cha Mvumi na Ekari 1000 nyingine kwa ajili ya kijiji cha Gongwe. Hii inatokana na asili ya vijiji hivyo ambavyo awali kilikuwa ni kijiji kimoja na mwaka 2014 kiligawanyika na kuwa vijiji viwili, Mvumi na Gongwe.
  Kwa upande wao Wananchi wa vijiji hivyo akiwemo Bi. Lakero Mkandawile wa kijiji cha Gongwe na Bi. Sara Seleman wa Kijiji cha Mvumi pamoja na Adhi Valaluke wa Kijiji cha Gongwe walimweleza  Mkuu wa Mkoa kero zao kuhusu mashamba hayo ikiwa ni pamoja na kupewa maeneo ya kulima kwenye mashamba ambayo tayari yana watu, kunyang’anywa mashamba waliokwisha pewa na kutishiwa kukatwa na mapanga tuhuma ambazo zilimhusisha pia Mwenyekiti wa Kijiji cha Mvumi Bw. Abdul Tumbo.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiongea na wananchi wa Vijiji vya Mvumi na Gongwe Wilayani Kilosa Mkoani humo kuhusu matumizi ya mashamba matano yaliyofutiwa Umiliki na Dkt. John Pombe Magufuli.
  Umati wa Wananchi kutoka Vijiji vya Mvumi na Gongwe waliofika kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuhusu matumizi ya Ardhi ya mashamba matano yaliyofutiwa Umiliki na Dkt. John Pombe Magufuli .
  Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adamu Mgoyi (anayeongea na kipaza sauti) akiwaonya wananchi kufuata maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa kuhusu utaratibu wa kuyatumia mashamba yaliyofutiwa umiliki wake.

  0 0


  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage akifungua mkutano kati ya tume hiyo na viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 unaofanyika kwenye ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchuguzi (NEC), Athuman Kihamia akitoa utangulizi wa majadiliano katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchuguzi (NEC), Athuman Kihamia kutoka kulia wakiwa pamoja na viongozi wengine wa tume ya uchaguzi katika kutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa JNCC jijini Dar es Salaam.
  Picha zikionyesha wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya siasa wakiwa katika mkutano huo leo.
   
  Tume ya Uchaguzi NEC na Viongozi wa vyama vya siasa wamekutana leo Machi 5,2019 jijini Dar es Salaam ambapo kwa sehemu kubwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 huku wakitumia mkutano huo kujadili namna ya kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, pia mchakato wa uchaguzi mkuu ili kuhakikisha unakuwa huru na haki. 
   
  Akizungumza mbele ya viongozi wa vyama vya siasa , Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Semistocles Kaijage amesema wadau na watanzania wanafahamu kuwa nchi yetu ipo katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 . 

  “Katika maandalizi hayo ,Tume chini ya Ibara ya 74(6) ya Katiba ya nchi yetu ya mwaka 1977 imepewa mamlaka ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya msingi ikiwa ni pamoja na jukumu la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge pamoja na uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara,” amesema. 

  Ameongeza kuwa NEC imeanza maandalizi ya mchakato wa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni mkakati wa kujiandaa na Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka 2020. 

  Amefafanua kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ,sura ya 324 na ya kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa sura ya 292 ,Tume inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mara mbili katika Uchaguzi Mkuu mmoja na uchaguzi mwingine unaofuata. 

  “Napenda kuwataarifu ,Tume inaendelea na maandalizi ya kuboresha Daftari ambapo mpaka sasa tayari imekamilisha baadhi ya michakato kama vile uhakiki wa vituo vya kujiandikisha ,maandalizi ya vifaa vya uboreshaji daftari na mkakati wa elimu ya mpiga kura,” amesema Jaji Kaijage. 

  Ameongeza mchakato wa uhakiki wa vituo lililenga kuona kama kuna haja ya kuongeza vituo katika baadhi ya maeneo, vituo vilivyopo kama bado vinakidhi matakwa ya kisheria na kufanya marekebisho mengine kama kubadilisha majina ya vituo au kurekebisha majina ya vituo yaliyokosekana. 

  Jaji Kaijage amesema matokeo ya uhakiki huo kwa Tanzania Bara yanaonesha kuwa vituo vya kuandikisha wapiga kura vimeongezeka kutoka vituo 36,549 vilivyotumika kuandikisha wapiga kura mwaka 2015 hadi vituo 37,407.Vituo 6,208 vimebadilishwa majina na vituo 817 vimehamishwa kutoka Kijiji/ Kata mmoja kwenda kata nyingine. 

  “Matokeo ya uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura kwa Tanzania Zanzibar yanaonesha kuwa vituo vimeongezeka kutoka 380 hadi vituo 407 na kwamba wadau watapewa orodha ya vituo vya kuandikisha wapiga kura kabla kuanza kwa mchakato wa daftari la kudumu la wapiga kura,” amesema.
  Kuhusu vifaa kwa ajili ya uboreshaji wa daftari hilo ,Jaji Kaijage amesema mchakato wa kupata vifaa vya kukarabati mashine za BVR umekamilika na kinachosubiriwa ni kufanyia majaribio ya uandikishaji katika kata mbili za Kihonda iliyopo Manispaa ya Morogoro na Kata ya Kibuta iliyopo wilayani Kisarawe. 

  Amefafanua ni kawaida kabla ya kuanza kwa mchakato wa uandikishaji ,hufanyika majaribio ili kuona namna na jinsi vifaa vya uandikishaji vinavyofanya kazi katika mazingira tofauti ,lengo likiwa ni kupata na kuwa na namna bora ya kufanikisha mchakato huo. 

  Ameongeza maandalizi mengine ambayo tayari yamefanyika ni uchapishaji wa miongozo mbalimbali kwa wadau ikiwemo ya kutoa elimu kwa mpiga kura na maelekezo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ,kwa watendaji na wadau wa uchaguzi vikiwemo vyama vya siasa. 

  Pamoja na mambo mengine Jaji Kaijage amesema Tume imejiwekea utaratibu wa kuwashirikisha wadau katika hatua mbalimbali za uchaguzi ,kwa lengo la kuhakikisha inajenga na kutekeleza misingi ya kidemokrasia katika kusimamia ,kuratibu na kuendesha chaguzi zilizo huru ,wazi ,za haki na kuaminika.
  “Madhumuni ya kukutana kwetu leo ni kuwafahamisha kuwa Tume imekamilisha jukumu lake la kuhuisha na kuboresha kanuni ambazo ziliandaliwa chini ya sharia hizo mbili mwaka 2008. 

  ” Tume imeona ni vema ikawapitisha katika kanuni hizo kwa kuangalia Yale maeneo ambayo yamefanyiwa marekebisho ama kwa kuondoa au kuongeza vifungu lakini kwa kueleza sababu za marakebisho hayo,”amesema Jaji Kaijage.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack ametambulisha rasmi mradi wa 'Badilisha Tabia Tokomeza Malaria' unaotekelezwa na asasi ya T- MARC Tanzania kwa ajili ya kazi za uhamasishaji jamii kupambana na ugonjwa wa malaria katika halmashauri za wilaya za Ushetu,Msalala na Kishapu mkoani Shinyanga.

  Mradi huo umetambulishwa leo Jumanne Machi 5,2019 katika ukumbi wa Submarine Hoteli Mjini Kahama wakati wa mkutano wa utambulisho wa mradi huo uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa kutokomeza Malaria.

  Lengo la mradi huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili ni uhamasishaji wa kuzuia ugonjwa wa malaria ambapo walengwa ni akina mama wajawazito,wanaonyonyesha,walezi wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na watoa huduma kwenye kliniki za akina mama na watoto.Akitambulisha mradi huo,Telack alisema ripoti ya Viashiria vya maambukizi ya Malaria ngazi ya jamii ya mwaka 2017/2018 inaonesha kuwa maambukizi ya ugonjwa wa malaria yamefikia asilimia 6 kutoka asilimia 17 kwa mwaka 2015/2016.

  “Pamoja na kupungua kwa maambukizi kulikochangiwa na juhudi za serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa mikakati ya udhibiti wa malaria iliyopo inatakelezwa kwa ufanisi,hivyo bado juhudi zinatakiwa kufanyika ili kupunguza kiwango hiki kufikia asilimia 1 na hatimaye kutokomeza kabisa Malaria katika mkoa wetu”,alieleza.

  Mkuu huyo wa mkoa alisema kupitia Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015-2020) wa Kudhibiti Malaria ulioandaliwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, kumekuwepo mafanikio mkoani Shinyanga ikiwemo kuongezeka kwa uwepo wa vyandarua vyenye dawa kwa jamii. 

  Aidha alisema kutokana na kuwepo kwa mwitikio mdogo wa wanajamii kushiriki katika mikakati ya kupambana na malaria ni imani yake kwamba kupitia mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria utatumika kuhamasisha jamii kushiriki kwenye mikakati ya kudhibiti malaria kwa vitendo. 

  Telack aliwataka viongozi na wataalamu wa ngazi ya mkoa,wilaya na halmashauri kushirikiana na T- MARC kutekeleza mradi huo vizuri ili kutokomeza Malaria huku akiitaka T-MARC kujipanga kutekeleza mradi huo kwenye mkoa mzima. “Malaria inazuilika na inatibika,tiba ya mapema baada tu ya dalili za homa kuanza ni muhimu kuzuia vifo hususani kwa watoto na akina mama wajawazito”,aliongeza Telack. 

  Awali Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC, Hamid Al- Alawy alisema kupitia mradi watahamasisha wanawake wajawazito,wanaonyonyesha na watoto kutumia vyandarua vyenye dawa kuzuia ugonjwa wa malaria lakini pia jamii kupima afya badala ya kuanza kutumia dawa kwani siyo kila homa ni malaria. 

  Naye Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Teresia Shirima aliwataka wananchi kuondokana na dhana potofu kuwa vyandarua vinapunguza nguvu za kiume huku akiwahamasisha kutumia vyandarua kwa matumizi yaliyokusudiwa. Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria' unatekelezwa na asasi ya T- MARC Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais -TAMISEMI na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ili kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti Malaria. 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria unaotekelezwa na asasi ya T- MARC kwa ajili ya kuhamasisha jamii kupambana na ugonjwa wa malaria katika halmashauri za wilaya za Ushetu,Msalala na Kishapu mkoani Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog. 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack, akiwasihi viongozi na wataalamu kushirikiana na asasi ya T- Marc kutekeleza mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria.Wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akifuatiwa na Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Teresia Shirima. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC, Hamid Al- Alawy akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha. 
  Kushoto ni Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- Marc, Hamid Al- Alawy akifuatiwa na Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka T- MARC, Levina Thobias na Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Teresia Shirima (kulia). 
  Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Teresia Shirima akielezea kuhusu Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015-2020) wa kudhibiti Malaria ulioandaliwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto. 
  Wadau wakiwa ukumbini. 
  Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- Marc, Hamid Al- Alawy akielezea kuhusu mradi huo na shughuli mbalimbali zinazofanywa na T-MARC katika kuwahudumia wananchi. 
  Wadau wa kupambana na ugonjwa wa malaria wakiandika dondoo muhimu. 
  Wadau wa kuzuia ugonjwa wa malaria wakiwa ukumbini. 
  Wadau wakiwa ukumbini. 
  Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka T- MARC, Levina Thobias akiwasilisha mada kuhusu tafiti mbalimbali zilizofanywa na T-Marc ambapo walibaini kuwa bado jamii ina imani potofu kuwa utumiaji wa vyandarua unapunguza nguvu za kiume lakini pia kuleta kunguni. 
  Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akiwataka wadau wanaotekeleza miradi mbalimbali wilayani Kahama kuhakikisha wanatumia lugha ya Kiswahili badala ya Kiingereza akibainisha kuwa baadhi ya wadau wamekuwa wakisambaza vipeperushi vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza wakati wananchi wanaelewa vizuri zaidi Kiswahili. 
  Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC, Hamid Al- Alawy akiagana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack. 
  Picha ya pamoja. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Machi 5, 2019) amewaongoza wakazi wa jijini la Dar es Salaam katika mazishi ya Imamu wa Msikiti wa Mtoro Sheikh Zubeir Yahya Mussa yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu.

  Sheikh Zubeir ambaye ni miongoni mwa masheikh maarufu jijini Dar es salaam alifahamika sana kutokana na kuwa Imamu wa msikiti huo, ambao ni miongoni mwa misikiti mikubwa na maarufu zaidi hapa nchini, alifariki dunia jana usiku.

  Pamoja na Uimamu wake, Sheikh Zubeir aliwavutia watu wengi sana kutokana na darasa zake alizokuwa akiziendesha kwa ufundi mkubwa katika msikiti huo wa Mtoro na maeneo mengine.

  Sheikh Zubeir alikuwa miongoni mwa masheikh waliojiweka karibu sana na jamii na kuwa na uhusiano mzuri na masheikh wenzake kutoka taasisi mbalimbali.

  Sheikh Zubeir alipata elimu yake ya juu katika chuo kikuu cha Madina, (Ummul- Quraa) akiwa pamoja na Sheikh Juma Omar Poli, Sheikh Muharram Juma Doga, Sheikh Abdallah Ahmad Bawazir na wengineo.

   Baadhi ya viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba.

  Wengine ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, Mbunge wa Kibaha Vijijini, Abuu Jumaa, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, MACHI 5, 2019.

  0 0

   Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) mkoani Shinyanga (UVCCM) kwa kushirikiana na Marafiki wa Taasisi ya Dkt. Tulia Ackson 'Friends of Tulia' wameendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake lengo likiwa ni kutoa fursa kwao ili waweze kujikwamua kiuchumi.

  Mafunzo hayo yanayotolewa pia na wakufunzi kutoka taasisi ya Mjasiriamali Kwanza Enterprises yamezinduliwa leo Machi 5,2019 kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ushetu wilayani Kahama. 

   Awali akizungumza,Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Barack Shemahonge, alisema katika kuelekea Tanzania ya viwanda ili kufikia uchumi wa kati ni lazima wananchi wajitume kufanya kazi, jambo ambalo limemgusa na kuamua kuendesha mafunzo hayo ili kukuza uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla. 

  Alisema moja ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuondoa umaskini kwa wananchi, hivyo kupitia mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo yanatolewa bure, ana imani kuwa maisha ya watu hao ambao wamejitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo yatabadilika na kukuza vipato kwenye kaya zao. “Naomba pia mjiunge kwenye vikundi ili muweze kupata mikopo kwenye halmashauri asilimia 10, ili mpate mitaji na kupanua wigo wa biashara zenu na kuinuka kiuchumi ikiwa fedha ni za makusanyo ya mapato ya ndani na mikopo yake haina riba,”amesema Shemahonge.

   Akizindua mafunzo hayo ya ujasiriamali, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa wabunifu kwenye biashara zao pamoja na kuzingatia ubora wa bidhaa jambo ambalo litawafanya kupata wateja wengi na kukua kiuchumi. Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu (CCM) mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga, aliwataka wajasiriamali hao kutokata tamaa pale wanapokumbana na changamoto katika biashara zao, bali wawe majasiri na kuendelea kupambana, kitendo ambacho kitawakomaza na hatimaye kuja kuwa wafanyabiashara wakubwa. 

  Nao baadhi ya wajasiriamali hao akiwemo Custa Mwambuli ambao wanafanya shughuli ya kutengeneza mkaa kwa kutumia karatasi, walipongeza utolewaji wa mafunzo hayo na kubainisha kuwa yatawapatia mbinu mbalimbali namna ya kupanua wigo wa biashara zao na kutambulika kimataifa na hatimaye kukua kiuchumi. 

  Miongoni mwa mafunzo yanayotolewa kwenye semina hiyo ya ujasiriamali ni utengenezaji keki za harusi, mikate, sambusa,burger, ubuyu wa rangi, ufugaji wa kuku, nyuki, samaki, kilimo cha uyoga, sabuni za miche, dawa za usafi, mishumaa, karanga za mayai chaki za mashuleni, mafuta ya mgando, ushonaji wa mawigi, pamoja na mapambo ya sherehe. Mafunzo hayo yatadumu kwa siku tatu kuanzia leo Machi 5,2019.  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akizungumza kwenye uzinduzi wa semina ya mafunzo ya ujasiriamali ambayo yatadumu kwa muda wa siku tatu kwa vijana na wanawake kupewa ujuzi na mbinu namna ya kuendesha biashara na kukua kiuchumi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog  Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Elias Kwandikwa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ushetu wilayani Kahama akizindua mafunzo ya ujasiriamali mkoani Shinyanga na kuwataka washiriki wawe wabunifu kwenye biashara zao pamoja na kuzingatia ubora wa bidhaa ili wapate wateja wengi na kukua kiuchumi.  Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachambwa akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali na kuwataka wayatumie vizuri katika kubadilisha hali ya maisha yao kiuchumi.  Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya Shinyanga Mjini wakiwa kwenye uzinduzi wa mafunzo yao ya kutengeneza bidhaa mbalimbali pamoja na kupewa mbinu za kibiashara ili wapate kukua kiuchumi.  Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya Shinyanga mjini wakiendelea kusikiliza nasaha za viongozi mbalimbali juu yao kabla ya kuanza kufundishwa namna ya kutengeneza bidhaa na mbinu za kibiashara.  Wajasiriamali wakiendelea kusikiliza nasaha za viongozi kabla ya kuanza kufundishwa namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.  Awali Mwenyekiti wa Taasisi ya Marafiki wa Dkt. Tulia Ackson mkoani Shinyanga Shabani Wisandara akitambulisha marafiki wa taasisi hiyo ambayo imejipanga katika kuhakikisha wanashirikiana na serikali kuhudumia wananchi.  Usikilizaji wa nasaha ukiendelea kabla ya kuanza ufundishwaji wa kutengeneza bidhaa mbalimbali.   Msemaji wa Taasisi ya Dkt Tulia Ackson nchini Tanzania Matiko Nyaiho akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wameshirikiana na UVCCM mkoa wa Shinyanga, kuleta mafunzo hayo ya ujasiriamali bure kwa vijana na wanawake ili kuwafundisha namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali na hatimaye kujikwamua kiuchumi.  Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akimpatia cheti cha pongezi Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) kwa kuleta mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake mkoani humo, ili kuwakwamua kiuchumi.  Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akimpatia cheti cha pongezi Mwenyekiti wa taasisi ya Marafiki wa Dkt. Tulia Ackson kwa kushirikiana na UVCCM Mkoa wa Shinyanga kuleta mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake ili kuwa kwamua kiuchumi na katika kuelekea Serikali ya viwanda na kufikia uchumi wa kati.  Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa naye akionyesha cheti cha Pongezi katika kushirikia kuzindua mafunzo ya ujasiriamali na kutoa mbinu za namna ya kufanikiwa kibiashara.  Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akikagua baadhi ya bidhaa za wajasiriamali ambao walifika kwenye mafunzo hayo kuongeza mbinu namna ya kupanua wigo wa biashara zao na kukua kiuchumi.  Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa, akiwasisitiza wajasiriamali kuyatumia vizuri mafunzo hayo kujikwamua kiuchumi.  Custa Mwambuli ni mjasiriamali ambaye anafanya shughuli ya kutengeneza mkaa kwa kutumia karatasi, akipongeza utolewaji wa mafunzo hayo kuwa yatawapatia mbinu mbalimbali namna ya kupanua wigo wa biashara zao na kutambulika kimataifa na hatimaye kukua kiuchumi.  Awali Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa (kulia) akijiandaa na hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali, katikati ni mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, na kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Dotto Joshua.  Mbunge wa Viti Maalumu Lucy Mayenga (kushoto) akiwa na msemaji wa Taasisi ya Friends of Dkt Tulia Ackson, Matiko Nyaiho mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa mafunzo ya ujasiriamali.  Awali Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Elias Kwandikwa akiwasili ukumbini kwenda kuzindua mafunzo ya ujasiriamali kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, akiwa na mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge.  Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM. Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

  0 0

   Benki ya Exim Tanzania imezidi kujitanua na kujiimalisha zaidi  hapa nchini baada ya kuonesha nia na utayari wa kuinunua  rasmi kuwa  benki ya UBL Tanzania Limited (UBTL) kwa asilimia 100. Hii ikiwa ni baada ya kusainishana barua ya kuonesha nia (Letter of Intent)
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  leo jijini Dar es Salaam na  Naibu Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu, inasema  ununuzi huo  unaohusisha mali na madeni unazidi kuifanya benki hiyo ambayo kwasasa ni miongoni mwa benki tano kwa ukubwa hapa nchini kuzidi kujitanua zaidi ndani na nje ya nchi.
  “Kwetu ni furaha kubwa kuona kwamba familia yetu inazidi kuongezeka  kwa kuwa tayari tunaungana na wanafamilia kutoka benki ya UBTL . Zaidi ya yote tunaamini pia kuwa wafanyakazi  wa benki ya UBTL wataongeza nguvu ambayo kwa pamoja tutaweza kutoa huduma bora zaidi za kibenki kwa wateja wa UBTL,’’ alisema bw Matundu.
  Alisema kuwa benki ya Exim inatarajia kukaribisha wateja wa benki ya UBTL katika mtandao mpana wa matawi ya benki ya Exim huku akiongeza kuwa hatua ya ununuzi huo ni upanuzi wa asili na uimarishaji wa uwepo wa benki hiyo katika soko la ndani ya nchi.
  Benki ya Exim ilianzishwa mwaka 1997 na ndio benki ya kwanza hapa nchini kuvuka mipaka na kujiimarisha nje ya nchi ambapo kwasasa imefanikiwa kuwa na matawi yake katika nchi za Uganda, Comoro and Djibouti.
  Tangu kuanzishwa kwake benki hiyo imekuwa ikijipambanua kwa ubora wa huduma ikilenga kujenga thamani ya uwekezaji kwa wadau wake  na kufikia ukuaji wake kwa kutoa huduma kwa upekee na iliyoboreshwa.
  Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa UBTL Bw Gasper Njuu alisema benki hiyo pamoja na wanahisa wake wamekuwa na mtazamo chanya juu ya fursa za ukuaji nchini Tanzania na kwasasa hilo linakwenda kufanikiwa kupitia benki ya Exim.
  “Wakati tukiwa kwenye mkakati wa mabadiliko ya kibiashara kupitia uwekezaji zaidi kwenye huduma za kidigitali ndipo tulipokea ombi kutoka benki ya Exim wakiomba kununua benki ya UBTL na baada ya kufikiria kwa kina  pande zote wakiwemo wanahisa wetu walikubaliana na ombi hilo hasa kwa kuzingatia ubora, weledi na sifa za benki ya Exim kwa hapa nchini ambao kimsingi unaleta tija kubwa kwa wadau na wateja wetu,’’ alibainisha  bw Njuu
  Benki ya UBTL ilianzishwa mwaka 2013, kama benki tanzu inayomilikiwa na  Benki ya United Bank Limited (UBL) ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini Pakistan na imetoa huduma za benki za rejareja na za jumla kwa wateja mbalimbali.
  Alisema hatua ya ununuzi inahusisha taratibu kadhaa za kisheria zikihusisha  nchi za Tanzania na Pakistan na zinatarajiwa kukamilika katikati ya  mwaka 2019.

  Kufuatia hatua hiyo  pande zote yaani Benki ya Exim na UBTL wameahidi kushirikiana vyema na Benki Kuu ya Tanzania  ndani ya wiki zijazo kuhakikisha kwamba mabadiliko hayo yanafanyika kwa urahisi na kwa kuzingatia taratibu zote za kisheria.
  Naibu Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu

  0 0

  Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori nchini(TAWA),imejipanga kuendelea kuboresha sekta ya uwindaji wa kitalii na imesitisha kibali cha uwindaji wa kitalii cha kampuni ya Green Miles Safaris Ltd, kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya umiliki wa vitalu vya uwindaji.

  Naibu Kamishna wa Utalii na Biashara wa TAWA, Imani Nkuwi alisema kampuni hiyo, imeshindwa kulipa ada za kutotumia zaidi ya asilimia 40 ya mgao wa kuwinda katika vitalu.

  "kampuni hii tumeinyia huduma za kuwinda katika vitalu vyake vyote wakati suala lao likifanyiwa kazi"alisema.Kampuni hiyo, inamiliki vitalu wilayani Longido na katika pori la akiba la Selous na katika siku za karibuni, imekuwa na migogoro na vijiji ilipowekeza wilayani Longido.

  Hata hivyo, Nkuwi alisema bado wamiliki wengi wa vitalu wanazingatia sheria na taratibu zilizowekwa na serikali, ikiwepo kutunza vitalu vyao, kuzuia matukio ya ujangili na kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka.

  Katika hatua nyingine, Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe ametoa agizo , kukamatwa mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Green Miles Salim Abdalah Awadhi, kutokana na kushindwa kulipa deni hilo la vijiji na halmashauri ya Longido mkoa wa Arusha.

  Mwaisumbe alisema vijiji 23 vya wilaya hiyo, vinaidai kampuni hiyo, kiasi cha sh 329 milioni kutokana na makubaliano walioingia tangu mwaka 2017/18 na jitihada za malipo zimekwama kwa njia ya mazungumzo.

  Mkurugenzi wa halmashauri ya Longido, Wakili Jumaa Mhina, alisema ofisini yake imekuwa ikiitaka kampuni hiyo kuwa na mahusiano na vijiji na kulipa fedha za vijiji na halmashauri bila ya mafanikio.

  Hata hivyo,Mkurugenzi wa Green Miles Safari Ltd, Salim Abdalah Awadhi ambaye yupo nje ya nchi , amekuwa akikanusha tuhuma mbali mbali dhidi ya kampuni yake,ikiwepo kudaiwa na vijiji fedha .

  0 0

  Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akifungua Kongamano la wafanyakazi Wanawake jiijini Dodoma liliofanyika kwa lengo la kuwakutanisha wafanyakazi hao kujadiliana na kupata namna bora za kuweza kumuwezesha kiuchumi mwanamke.
  Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Silvia Siriwa akieleza chimbuko la Siku ya Wanawake Duniani katika Kongamano la wafanyakazi Wanawake jiijini Dodoma liliofanyika kwa lengo la kuwakutanisha wafanyakazi hao kujadiliana na kupata namna bora za kuweza kumuwezesha kiuchumi mwanamke.
  Mkurugenzi Msaidizi Wanawake kutoka Idara ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza akielezea umuhimu wa Siku ya Wanawake Duniani katika kiuchumi mwanamke katika kongamano la wafanyakazi wanawake Dodoma. 
  Baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa Mkoa wa Dodoma wakifuatlia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika Kongamano la wafanyakazi Wanawake jiijini Dodoma liliofanyika kwa lengo la kuwakutanisha wafanyakazi hao kujadiliana na kupata namna bora za kuweza kumuwezesha kiuchumi mwanamke
  Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wanawake waliohudhuria Kongamano la wafanyakazi Wanawake jiijini Dodoma liliofantika kwa lengo la kuwakutanisha wafanyakazi hao kujadiliana na kupata namna bora za kuweza kumuwezesha kiuchumi mwanamke.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
   
   
  Tanzania inaungana na Nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku Wanawake Duniani kwa lengo la kutafakari mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto lakini pia kuwakomboa kifikra, kiutamaduni, kisiasa, kijamii na kiuchumi.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongomano la wanawake wafanyakazi kuhadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike alisema wanawake na wasichana wafanyakazi ni kundi kubwa na muhimu katika jamii linalohitaji kulindwa.

  Bw. Golwike alitoa Rai kwa wanawake hao kuwa Haki inakwenda pamoja na Uwajibikaji lakini pia Usawa unakwenda pamoja na kukidhi vigezo, ambavyo ni sifa za kielimu, kitaaluma na uzoefu wa kazi.

  Ameongeza kuwa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 8, kwa mwaka huu hapa Tanzania yanafanyika ngazi ya Mkoa, ambapo kila Mkoa umeadhimisha sikukuu hii kulingana na mazingira yake na rasilimali zilizopo kwa kuzingatia Kaulimbiu ya mwaka husika ambayo ni “Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu”.

  Aidha Bw. Golwike aliyataja Madhumuni ya Maadhimisho haya kuwa ni kutoa fursa kwa Serikali, Wananchi, Wadau, Wanawake na Jamii yote kubadili fikra na mtizamo ili kuleta Usawa wa Jinsia na kuonesha nia ya kuhamasisha jamii, juu ya umuhimu wa kutambua uwezo wa wanawake katika kuchangia na kuleta Maendeleo Endelevu lakini pia Kuwezesha ushiriki na kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake kufikia maendeleo jumuishi.

  Wakati huo huo Msimamizi wa Maadhimisho hayo kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Silivia Siriwa alitaja mafanikio yaliyopatikana kutokana na juhudi za Wizara kuwa ni pamoja kutoa elimu kwa jamii kuhusu utatuzi wa changamoto zinazowakabili wanawake ikiwemo Madhara ya Mila na Desturi potofu ambazo zinaelekeza aina ya kazi na nafasi za uongozi za kushikwa na wanawake ambazo ni za kutoa huduma zaidi.

  Aliyataja mengineyo ni kuhamasisha jamii kuhusu kuondoa madhara ya ndoa na mimba za utotoni, ambazo zinafifisha ndoto na matarajio ya mtoto wa kike, hamasa na ushiriki wa wafanyakazi katika majukwaa ya uwezeshaji wanawake ambayo yanatumika kwa ajili ya kuelimishana, kubadilishana uzoefu na kujiunga katika mtandao wa mashirikiano.

  Bi. Siriwa pia alizitaja baadhi ya changamoto zinazojitokeza kwa wanawake mahali pa kazi ni pamoja na kukosa taarifa za mabadiliko ya Sheria na Kanuni za utumishi, Matumizi ya lugha ya kiingereza katika matumizi ya vifungu vya kisheria inawanyima baadhi ya wafanyakazi, haki ya kuzifahamu sheria.

  Aidha Wingi wa shughuli na majukumu ya kifamilia, kikazi na kijamii ni hali inayopunguza ufanisi wao, kipato kidogo cha kumudu mahitaji ya familia na ongezeko la wahitaji kutoka katika makundi maalum ya jamii ambayo wanawake wafanyakazi wanayabeba.

  Chimbuko la Siku ya Wanawake lilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kufuatia maandamano ya wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani kupinga mazingira duni ya kazi.

  Waandamaji hao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira ikiwemo wanawake kulipwa mshahara mdogo kwa kazi sawa na wanaume

  0 0

  mafunzo ya udhibiti wa uingizaji wa vyanzo vya mionzi yakitolewa na Umoja wa Ulaya ambayo yanafanyika kwa siku tano kwenye ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania jijini Arusha.
  Washiriki kutoka nchi za Kenya,Rwanda,Malawi,Zambia na wenyeji Tanzania wakimsikiliza kwa makini mkufunzi Bwana Olydcaegers Greet kwenye mafunzo ya udhibiti wa uingizaji wa vyanzo vya mionzi kwenye mipaka ya nchi isivyo fuata utaratibu.Mafunzo hayo yametolewa na Umoja wa Ulaya ambayo yanafanyika kwa siku tano kwenye ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania jijini Arusha.


  Umoja wa Ulaya EU umetoa mafunzo ya udhibiti wa uingizaji wa vyanzo vya mionzi kwa nchi tano za AFRIKA kwa lengo la kusaidia udhibiti wa uingizaji wa vyanzo vya mionzi bila kufuata utaratibu pamoja na utoroshwaji wa vyanzo vya mionzi vilivyoibiwa kwa matumizi yasiyo salaama na hatarishi. 

  Washiriki wa mafunzo haya ni kutoka taasisi mbali mbali zikiwemo Mamlaka za Mapato, Forodha na vyombo vya ulinzi na usalama kutoka katika nchi za Malawi, Rwanda, Kenya, Zambia na wenyeji Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki. 

  Huu ni mwendelezo wa mafunzo kwa nchi za Afrika katika kusaidia kupambana na tabia ya uingizwaji wa vyanzo vya mionzi ambavyo kwa namna moja ama nyingine hupelekea kuleta madhara kwa binadamu. 

  Mafunzo hayo yanahusisha mafunzo kwa vitendo ikiwemo utambuzi kwa kutumia vifaa maalumu vilivyopo katika mipaka yote katika nchi hizo ambapo husaidia kugundua uhalifu wa namna hiyo. 

  Mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Tanzania Mhandisi Exavier Zakaria amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia sana hasa kwa wao waliopo katika mipaka amesema wamekuwa wakikutana na masuala mengi ikiwemo baadhi ya wafanyabiashara ambao huenda kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa za usafrishaji wa vyanzo vya mionzi. 

  ‘’Ukweli mafunzo yamekuja kwa wakati sahihi na yatasaidia sana katika kuongeza ujuzi kwenye utambuzi wa vyanzo vya mionzi ambavyo ni hatarishi kwa binadamu’’ alisema Mhandisi Zakaria 

  Naye mshiriki mwingine wa mafunzo hayo kutoka Tanzania , Bwana Patrick Simpokolwe amesema kuwa kutokana na mbinu za uhalifu za uingizaji wa mionzi isiyo salama katika mipaka mbali mbali katika nchi za Afrika anaamini mafunzo haya yatamsaidia katika kugundua mbinu mbali mbali za uhalifu na kuweza kudhibiti. 

  ‘’Tumekuwa tukikumbana na udanganyifu mkubwa kwenye mipaka kutokana na mbinu mpya zinazotumiwa na wasafirishaji wa bidhaa mbali mbali zikiwemo zenye vyanzo vya mionzi kutoka na kuingia ndani ya nchi hivyo mafunzo haya yatawezesha kuwabaini wahalifu wa namna hiyo’’ alisema Simpokolwe. 

  Mshiriki mwingine kutokea nchini Kenya Bi Evalyne Rotich amesema kuwa kutokana na uwezekanao wa kutokea uhalifu kila wakati na kwamba mafunzo hayo yatawezesha sana kutambua watu ambao sio wema wenye lengo la kupitisha vitu vyenye vyanzo vya mionzi mipakani ambavyo vinaweza kudhuru wananchi katika nchi husika . 

  ‘’Umakin utaongezeka kwetu kwani mbinu tulizopatiwa zitatuwezesha kutambua vitu vyote ambavyo vitapitishwa bila kufuata utaratibu husika’’ alisema Rotich. 

  Kwa upande wake mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo kutoka umoja wa Ulaya (EU) , Bi Katrijin Vandersteen amesema kuwa katika nchi za Afrika kumekuwa na tatizo la uingizaji wa vyanzo vya mionzi visivyo salama hivyo kwakutolewa mafunzo hayo kutolewa yataweza kusaidia katika uimarishaji wa utambuzi na udhibiti katika maeneo ya mipaka kwenye nchi mbali mbali. 

  ‘’Tunaamini kuwa washiriki hawa watapata uelewa zaidi juu ya utambuzi wa vyanzo vya mionzi visivyo salama kwa lengo la kusaidia kutoleta madhara kwa binadamu kwenye nchi husika na dunia kwa ujumla mara baada ya kukamilika kwa mafunzo haya ’’ alisema Vandersteen. 

  Mfunzo haya yanafanyika katika Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, jijini Arusha kuanzia tarehe 4 hadi 8 Machi 2019.

  0 0

   Mfanyakazi Mwandamizi ndani ya Ndege (Senior Cabin Crew) Mohamed Ngananya akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kuhusu madai ya Wafanyakazi katika Kampuni ya FastJet PLC, 
  Afisa Mwendeshaji Mkuu, Upande wa Airport, Alex Mjoge akizungumzia suala hilo la madai yao kama Wafanyakazi wa FastJet PLC. Kulia ni Mfanyakazi Mwandamizi ndani ya Ndege (Senior Cabin Crew) Mohamed Ngananya.
   Sehemu ya Wafabyakazi wa Kampuni ya Fastjet (Fastjet Plc)


  *Waiomba Serikali chini ya Rais Dk. Magufuli kuingilia kati kuhakikisha haki inatendeka, 

  * Wamshauri Masha akae kimya kwani naye ni mfanyakazi kama wao na anadai mshahara


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Fastjet(Fastjet Plc) nchini Tanzania wameiomba Serikali kuzishikilia ndege mbili za kampuni hiyo ili walipwe madeni yao ambayo wanadai kwa sasa yanayofikia Sh.Bilioni 2.75.

  Wamesema kuna madai mengi ya fedha ambayo wafanyakazi wa Fastjet Plc walioko nchini Tanzania wanadai huku wakitoa ombi kwa Serikali ya Awamu ya Tano kuwasaidia ili wapate haki zao ikiwemo malimbikizo ya mshahara wanayodai.

  Pamoja na kutoa kilio chao ,wafanyakazi hao wamesikitishwa na madai ambayo yametolewa na mfanyakazi mwenzao Laurance Masha ya kudai wafanyakazi wamelipwa mshahara wakati sio kweli kwani hata yeye naye anadai mshahara.

  Wakizungumza leo Machi 6,2019 katika ofisi za Fastjet zilizopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ,wamesema katika kuhakikisha wanapata haki zinazostahili wamechukua hatua mbalimbali ikiwemo ya kwenda kwenye mamlaka husika ambazo wanaamini zitawasaidia kupata haki zao.

  Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wengine wa Fastjet zaidi ya 125, Mfanyakazi Mwandamizi ndani ya Ndege (Senior Cabin Crew) Mohamed Ngananya amesema kuwa kikubwa ambacho wanaiomba Serikali ni kuzishikilia Ndege mbili za Fastjet ambayo moja ipo nchini Tanzania na nyingine ipo Nairobi nchini Tanzania.

   "Tunapenda kutoa dukuduku letu kwa Serikali yetu ya Tanzania kuingilia kati na kutusaidia kupata madai na maslahi yetu kama wafanyakazi wa Tanzania toka kampuni Mama(Fastjet Plc) ambayo ndio mmiliki wetu mpaka leo hii tunazungumza na vyombo vya habari," amesema.

  Ametaja baadhi ya madai yao ni malipo ya kisheria ya kuvunjwa kwa mkataba wa mfanyakazi ,malipo ya kisheria ya kiinua mgongo ya iliyokuwa Fly540 Tanzania Ltd, michango yao ya mifuko ya hifadhi (NSSF na PSSSF ya tangu Agosti 2018.Pia madai ya mshahara ya January 2019 ambayo baadhi yao wamelipwa nusu mshahara na kuahidiwa kulipwa kiasi kilichobakia baada ya wiki mbili lakini hawajalipwa mpaka leo.

  Madai mengine ya wafanyakazi hao ni mshahara yao ya Februari 2019 ambayo haijalipwa kabisa."Tunaomba Serikali yetu kuzuia ndege mbili aina ya Embrear 190 zenye usajili wa Tanzania 5H- FJH na 5H-FJI na zisifutiwe huo usajili au kuruhusiwa kuondoka nchini kabla ya kulipwa madai yetu haya,"amesema Ngananya.

  Ameongeza kuwa.menejinenti ya Kampuni yao hapa nchini Tanzania ulishawishi kutoa muongozo kwa Fastjet Plc kuwa kampuni hiyo ifungwe kwa taratibu zilizo rasmi na kisheria ili kuwezesha kila mfanyakazi na watoa huduma wote walipwe stahiki zao lakini hilo halikuzingatiwa na matokeo yake kusikia ghafla kuwa kampuni ya Fastjet Tanzania imeuzwa,hivyo wamtoa mwito kwa taasisi za Serikali kufuatilia kwa makini ununuzi huo.

  " Zaidi Menejimenti ilitoa ushauri kwa mamlaka husika  TCAA ambayo inaratibu safari za anga na mashirika ya ndege hapa Tanzania kuwa wasitambue au kukubali mbadilishano huo wa umiliki wa kampuni hii hapa nchini kwasababu menejimenti haikuwa na taarifa za kina na za kutosha kuhusu uwezo wa kifedha kuendesha shughuli za usafirishaji abiria na kwa muda gani,"amesema.

  Ngananya ameongeza kwanautaarifu umma wa Wa Tanzania kuwa kinachoendelea Fastjet Tanzania si kwasababu za kisasi kama wengi wanavyosema au kufikiria bali ni matatizo ya kiutendaji ya mwajiri wao mkuu ambaye ni Fastjet Plc kwa kutaka kukimbia madeni ambayo wanakataa kuyalipa madai yetu

  "Tunaomba ujumbe kwa wafanyakazi wenzetu waliopo Zimbabwe na Msumbiji ,wachukue tahadhari ili mambo kama haya yasiwakute," amesema.

  Alipoulizwa kuhusu Laurance Masha ambaye amekaririwa na baadhi ya vyombo kuwa wafanyakazi wa Fastjet wamelipwa mshahara,amejibu madai hayo hayana ukweli na kwamba hata yeye Masha naye mshahara wa Januari mwaka huu na mshahara wa February bado hajalipwa.

  Alipoulizwa Masha ndio mmoja wa wanahisa,Ngananya amejibu kuwa wanachojua wao Masha ni mfanyakazi mwenzao kama walivyo wengine na wala hausiki na chochote ikiwemo ya kulipwa mishahara.

  "Ni mfanyakazi kama tulivyo wengine tu,naye anadai kama sisi na hapa kwetu tunaye kiongozi wetu ambaye tunashirikiana kwa kila hatua ambayo tunaifanya ili kupata haki zetu,"amesema.

  Kwa upande wake mfanyakazi mwingine ambaye ni Mkufunzi Ignace Tarimo  amesema chini ya utawala wa Rais Dk.John Magufuli wanaamini haki yao itapatikana ingawa amesisitiza umuhimu wa Serikali kuzuia ndege hizo kwani ndizo zitawafanya wao wapate haki yao.

  Wakati huo huo wafanyakazi wa Fastjet wamemshauri Masha ni bora akawa kimya badala ya kutoa kauli ambazo hazina ukweli na matokeo yake umma unapotoshwa kwa kupewa taarifa ambazo hazina ukweli.

  Hats hivyo Masha mwishoni kwa wiki akizungunza na kituo cha Azam TV ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mambo ya kampuni hiyo ambapo aligusia suala la mishahara kuwa mishahara wa January umelipwa na mkakati wa kampuni hiyo ni kuingiza ndege sita.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wawekezaji na Wanachama wa Ushirika wa kilimo cha zao la Kahawa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro (Murososangi). 
  Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) wakisikiliza kwa makini maelezo ya wanaushirika wa kilimo cha Kahawa wilayani Hai- Murososangi, kuhusu kiini cha mgogoro na Mwekezaji wa Kampuni ya Tudeley Estates Limited kutoka Uingereza kuwa ni kuletwa kwa Mwekezaji mwingine kutoka Ujerumani Bw. Marcus Shiber, bila ridhaa yao. 
  Wanaushirika wa kilimo cha Kahawa wilayani Hai- Murososangi, wakiwa katika Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki (hawapo pichani) walipofika wilayani hapo kutatua mgogoro ya uwekezaji katika zao la kahawa. 
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira, akizungumza na wadau wa kilimo cha Kahawa wilayani Hai wakati wa mkutano kati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki (hawapo pichani) na wadau wa kilimo cha kahawa wilayani Hai. 
  Mwekezaji wa Kilimo cha Kahawa kutoka Ujerumani Bw. Robert Clowes (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kahawa ya Mbosho Bw. James Powell wakiwa katika mkutano wa kutatua mgogoro ya uwekezaji katika zao la kahawa chini ya uenyekiti wa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na kuwashirikisha Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki (Mb) (hawapo pichani) na wadau wa kilimo cha kahawa Wilayani Hai. 
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira (kulia) akipeana mkono na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipofika wilayani Hai, kutatua mgogoro ya wawekezaji katika Sekta ya kilimo cha kahawa katika Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro. 
  Wadau wakiwa katika mkutano wa kutatua migogoro kati ya wawekezaji na Chama cha Ushirika wa wakulima wa Kahawa Wilayani Hai, Mkoani Kilimanjaro (Picha na Josephine Majura, Wizara ya Fedha na Mipango) 

  …………………………….. 

  Na Josephine Majura na Peter Haule, WFM, Kilimanjaro

  Serikali imeitaka Kampuni ya Tudeley Estates Limited kutoka Uingereza iliyoingia mkataba na vyama vya Ushirika Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro vinavyojishughulisha na uwekezaji wa Kilimo cha Kahawa (Murososangi), kurudi nchini ili kufanikisha utatuzi wa mgogoro uliosababishwa na kuibuka kwa mwekezaji mpya ambae mkataba wake haujulikani. 

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angela Kairuki walipofanya mkutano na Wawekezaji, Vyama vya Ushirika na Wadau wengine kuhusu mgogoro na Mwekezaji huyo Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro. 

  Dkt. Mpango alisema kuwa, Vyama vya Ushirika vya Murososangi, viliingia mkataba na Kampuni ya Tudeley Estates Limited ya nchini Uingereza ambapo washirika hao wenye mashamba eneo la Kibo na Kikafu wilayani Hai, yenye ukubwa wa hekari 2054 walimpa Mwekezaji huyo ili kuendeleza zao la kahawa kuanzia mwaka 1998. 

  Alisema kuwa baada ya mwekezaji huyo, Bw. Conrad Legg, kuonesha nia ya kutoendelea na uwekezaji huo aliondoka nchini, wakaja wawekezaji wengine kutoka Ujerumani ambao waliingia mkataba na Kampuni ya Tudeley Estates Limited, kwa kununua hisa bila kuvishirikisha Vyama vya Ushirika vilivyoingia mkataba wa awali jambo lililosababisha sintofahamu kwa wana ushirika hao. 

  “Aliyeingia mkataba na Murososange, arudi nchini ili kutatua mgogoro huo ili kuona Wananchi wanawezaje kuingia mkataba mwingine na mwekezaji mpya ambao utalinda maslahi ya wananchi wenye mashamba hayo na pia mwekezaji”, alisema Dkt. Mpango. 

  Alisema Wanaushirika hao wanataka Mwekezaji wa kwanza arudi nchini ili wavunje mkataba wa awali kwa kuwa mkataba huo haujaisha muda wake hivyo hawawezi kuingia mkataba na mwekezaji mpya wakati ule wa awali bado unaendelea. 

  Aidha, alisema kuwa mwekezaji mpya kutoka Ujerumanim Bw. Marcus Shiber, alianza kuleta fedha katika eneo la uwekezaji na kulipa baadhi ya kodi za mtangulizi wake, madeni, mishahara na kuboresha miundombinu ya mashamba hayo bila kupata muafaka na Vyama vya Ushirika jambo ambalo liliendelea kuleta mgogoro. 

  Dkt. Mpango alisema kuwa, wamepata maelezo kutoka pande zote na baadhi ya maelezo hayo yanahitaji ushauri wa kisheria hivyo tumeiomba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuyafanyia kazi mambo hayo ili kuweza kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, namna bora ya kumaliza mgogoro huo bila kuingizia Serikali hasara. 

  Aliwatahadharisha watendaji wakuu wa serikali kutotumia ubabe na vitisho kwa wawekezaji ili kutoharibu taswira ya taifa katika masuala ya uwekezaji unaopigiwa chapuo hivi sasa na Serikali ya Awamu ya Tano, ili kuvutia mitaji, mapato ya serikali, ajira kwa vijana na kuvutia teknolojia za kisasa kwa maendeleo ya Taifa. 

  Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Angela Kairuki, alisema kuwa kutokana na mgogoro huo wa kiuwekezaji akaunti za Mwekezaji mpya kutoka Ujerumani ikiwemo ya Kampuni ya Kuza Afrika inayojishughulisha na kilimo cha parachichi Mkoani Mbeya ilifungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kuhusiana na masualaya kodi, jambo lililosababisha baadhi ya shughuli za Mwekezaji huyo kukwama. 

  Alisema kuwa kikosi chao kupitia Waziri wa Fedha na Mipango aliyetumwa na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kutatua mgogoro huo, wameangalia iwapo taratibu za kufungwa akaunti hizo zilifuatwa na kutafuta njia bora ya kutatua tatizo hilo na pia kuona ni Mwekezaji yupi anafaa kuingia mkataba na Vyama vya Ushirika vya Murososangi, nia ikiwa ni kuona Vyama hivyo vinanufaika na Uwekezaji unakua nchini. 

  Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mgwira, aliishukuru Serikali kwa hatua yake ya kutuma Mawaziri ili kutatua mgogoro huo wa muda mrefu ambao utatuzi wake utasaidia Wananchi kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla. 

  Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini-TIC, Bw. Geofrey Mwambe, alisema kuwa katika mkutano kati ya Mawaziri, Wawekezaji na Vyama vya Ushirika wamebaini kuwa utaratibu walioukuta Wawekezaji kutoka Ujerumani haukuwa sawa na ule ambao waliwekeana na Mwekezaji wa kwanza kutoka Uingereza, hivyo kuleta ugumu kiutendaji kwa Mwekezaji wa pili. 

  Alisema kuwa, Serikali inahitaji uwekezaji katika Sekta ya Kilimo ili kupata malighafi ya viwanda nchini, kuongeza mnyororo wa thamani na kukuza pato la Taifa, hivyo inafanya jitihadi za kuvutia wawekezaji watakaoleta mitaji na teknolojia ya kisasa ili Taifa liweze kukabiliana na ushindani wa bidhaa katika soko la Kimataifa. 

  Mwakilishi wa mwekezaji mpya kutoka Ujerumani Bw. Robert Clowes, alimshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuwatuma Mawaziri wake kuja kutatatua mgogoro huo, alisema Tanzania kuna fursa nyingi za uwekezaji hivyo yupo tayari kuendelea kuwekeza zaidi nchini kwa lengo la kupata manufaa kwa pande zote ikiwa ni pamoja na Kampuni yake na vyama vya ushirika wa kilimo cha Kahawa Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madawati 62 yaliyotolewa na Benki ya NMB kama msaada kwa ajili ya Shule kutoka halmashauri za Mkoa wa Katavi. 

  Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Straton Chilongola akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga (walioshikana mkono) sehemu ya msaada wa mabati 1,248 kwa ajili ya Shule 5 za Sekondari na shule 3 za Msingi zote kutoka halmashauri za Mkoa wa Katavi.
  Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madawati 62 yaliyotolewa na Benki ya NMB kama msaada kwa ajili ya Shule kutoka halmashauri za Mkoa wa Katavi.

  Wanafunzi wakiwa na sehemu ya madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB kama msaada.


  BENKI ya NMB imetoa msaada wa mabati 1,248 na madawati 62 kwa ajili ya Shule 5 za Sekondari na shule 3 za Msingi zote kutoka halmashauri za Mkoa wa Katavi ikiwa ni kusaidia kutatua changamoto anuai kwenye sekta ya elimu.

  Msaada huo uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 40 umekabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Straton Chilongola huku akisisitiza benki hiyo itaendelea kusaidia jamii katika sekta ya afya, elimu pamoja na majanga ikiwa ni kuchochea maendeleo kwa jamii.

  Akipokea msaada huo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga aliishukuru Benki ya NMB kwa kuchangia maendeleo ikiwemo kuthamini sekta ya elimu kwa msaada huo wenye tija.

  Awali akitoa taarifa, Afisa Elimu Taalum Sekondari Manispaa ya Mpanda, Raphael Mkupi amebinisha kuwa wanafunzi katika shule ya Sekondari Rungwa hulazimika kukaa wawiliwawili kwa kiti kimoja kutokana na kuwepo kwa upungufu wa viti zaidi ya 300.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa vifaa vya umeme kutoka kwa Mhandisi Anectus Nduguru wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati alipotembelea Ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa betri kutoka kwa Mhandisi Anectus Nduguru wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati alipotembelea Ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu upimaji wa betri kutoka kwa Mhandisi Anectus Nduguru wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati alipotembelea Ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salaam, Machi 6, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Cunbert Kapilima wa Shirika la Viwango Tanzania -TBS (kushoto) kuhusu upimaji wa ubora maguani unaofanywa na TBS wakati alipotembelea ofisi za TBS, Ubungo jijini Dar es salam, Machi 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa Kilimo, Uwekezaji, Viwandana Biashara, Mifugo na Uvuvi na Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakutane na wafanye mapitio ya taasisi zao na kuangalia maeneo yanayogongana kiutendaji ili kila mmoja abaki na jukumu lake.

  Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Machi 6, 2019) alipotembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hizo na amewaagiza mawaziri wakutane na wampelekee taarifa ya mapendekezo yao ifikapo Machi 30, 2019.

  Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa malalamiko na manung’uniko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamedai kuwepo kwa muingiliano wa majukumu ya kiutendaji ya taasisi hizo, hivyo kuwasababisha washindwe kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

  Waziri Mkuu amesema taasisi hizo zinashughuli ambazo zinaingiliana na kusababisha malalamiko kwa wateja wao, ambapo ametolea mfano suala la kudhibiti ubora wa bidhaa ambalo linafanywa na TFDA na TBS kwa mujibu wa sheria. Amewataka wapitie sheria zao na wajue ukomo majukumu yao.

  “Kutaneni pitieni maelekezo ya Serikali yanayoelekeza namna ya kuzifanya taasisi hizi na zingine zinazofanya shughuli zinazofanana zilizo katika wizara zenu bila kusanau Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (blue print). Ifikapo tarehe 30 mwezi huu niwe nimepata mapendekezo yenu,” amesisitiza.

  Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watendaji wa taasisi hizo wabadilike na waache urasimu kwasababu hauna tija katika utekelezaji wa majukumu yao na badala yake unaweza kuwayumbisha kwenye ufanyaji wao wa kazi. “Kila mmoja atekeleze majukumu yake kwa uzingatia maadili ya taaluma yake.”

  Pia, Waziri Mkuu amewataka waangalie namna ya kuwahisha majibu ya vipimo vya bidhaa wanazoletewa na wateja, kama watakuwa wamekamilisha kabla ya siku za kisheria wawajulishe wateja wao na kuhusu sampuli ambazo zitakuwa hazijaharibika wakati wa vipimo wawarudishie.

  Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuzitaka taasisi hizo ziangalie namna ya kusogeza huduma kwa wananchi kwa kuwa na watumishi katika ngazi za wilaya na kwa TFDA ameitaka ianzishe maabara nyingine mbili kwenye kanda ya Nyanda za Juu Kusini na ya Kaskazini ili kusogeza huduma kwa wananchi.


  0 0


  Mtaalam wa Fiziotherapia, Beppie Hylkema kutoka Chuo Kikuu cha Fiziotherapia nchini Uholanzi akitoa mafunzo kwa wataalam mbalimbali ambao wametoka hospitali mbalimbali nchini kuhusu tiba kwa kina mama na wanaume wenye matatizo kwenye mfumo wa mkojo, mfumo wa uzazi na maumivu katika nyonga. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

  Wataalam kutoka hospitali mbalimbali nchini nchini wakiwa kwenye mafunzo hay leo.
  Mtaalam wa Fiziotherapia, Liesbeth Westerih kutoka Chuo Kikuu cha Fiziotherapia nchini Uholanzi akijibu moja maswali kutoka kwa washiriki kuhusu matatizo yanayowapata kinamama katika mfumo wa uzazi wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua.
  Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo leo.Mmoja wa washiriki akiuliza swali kuhusu matatizo yanayowapata kinamama kwenye mfumo wa uzazi.

  Baadhi ya vifaa ambavyo vinatumika kutoa tiba kwa kinamama wenye matatizo kwenye mfumo wa uzazi.


  ……………………………………………………………………………………

  Wataalam wa Fiziotherapia kutoka hospitali mbalimbali nchini leo wameanza mafunzo kuhusu tiba afya eneo la nyonga, mfumo wa mkojo na mfumo mzima wa uzazi kwa kina mama.

  Mafunzo hayo ambayo ni ya siku tatu yanaendeshwa na Chama cha kitaaluma cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA) kwa kushirikiana na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Fiziotherapia nchini uholanzi.

  Katibu wa chama hicho, Bw. Abdallah Makalla amesema mafunzo hayo yamelenga kuinua kiwango cha utoaji huduma kwa wataalam wa fiziotherapia katika eneo hilo ili waweze kutoa huduma ya ubobezi wa juu kwa kinamama na wanaume wenye matatizo kwenye mfumo wa uzazi, mfumo wa mkojo na eneo la nyonga.

  Mtaalam wa Fiziotherapia, Liesbeth Westerih amesema wataalam hao wanapaswa kutumia vifaa maalum kwa ajili kutibu kina mama na wanaume wenye matatizo kwenye mfumo wa uzazi, mfumo wa mkojo, mfumo wa haja kubwa, viungo vinavyozungukwa na nyonga na wenye maumivu ya nyonga.

  Pia, wataalam hao wamepatiwa mafunzo ya kutumia vifaa maalum kwa kinamama wenye matatizo kwenye mfumo wa uzazi na wale wanaopata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

  Washiriki katika semina hiyo wamefundishwa jinsi ya kutibu kina mama wenye matatizo kwenye eneo la nyonga na mfumo wa uzazi kwa kutumia njia mbalimbali kitaalamu kama vile kufanya uchunguzi na kutoa ushauri kwa wagonjwa kabla ya kupatiwa tiba.

  “Wewe ni mtaalam, hakikisha unaelwa historia ya mgonjwa, fanya uchunguzi ili kujua unamtibu mgonjwa wa aina gani, jua sababu za ugonjwa wake na pia hakikisha unamshauri kiasi kwamba mgonjwa anakuelewa vizuri,” amesema Mtaalam wa Fiziotherapia, Beppie Hylkema kutoka Chuo Kikuu cha Fiziotherapia nchini Uholanzi.

  Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwajengea uwezo wataalam hao ambao watatoa tiba kwa kinamama nchini ili kukabiliana na ongezeko la matatizo kwa kinamama wajawazito na wale waliojifungua.

  Washiriki wanatoka katika hospitali mbalimbali nchini ikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), CCBRT, Physiocare Arusha, London Health Centre, Police Barracks, Dar group Hospital, The Aga Khan Hospital -Dar es Salaam, GEMSA Polyclinic, Waja Hospital Geita na International Rescue Committee CBR ya mkoani Kigoma.

  0 0


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisema jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Masuala ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya mapema jana
  Mama Salma Kikwete, Mjumbe wa Kamati ya Bunge inajishughulishana Masuala ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya akisoma nyaraka wakati wa ziara ya kamati walipotembelea Shule ya Sekondari Makoka.
  Mjumbe wa Kamati ya Bunge inajishughulisha na Masuala ya UKIMWI na Madawa ya Kulevya Mama Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Suzana Paul mwanafunzi katika Shule ya Sekondari Makoka.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Masuala ya UKIMWI na Madwa ya Kulevya, Mhe. Oscar Mukasa akisema jambo kwa wajumbe wa kamati hiyo (hawapo pichani) katika ziara ya wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea Mkoa wa Dar Es Salaam kujionea hali ya utoaji wa huduma za afya kwenye matibabu ya Virusi vya Ukimwi.
  Wajumbe wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Masuala ya UKIMWI na Madawa wakimsikiliza mtoa huduma za afya katika Kituo cha kutolea dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi (CTC) katika Hospitali ya Sinza.
  Wajumbe wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Masualaya UKIMWI na Madawa (waliosimama) wakimsikiliza mtoahudumazaafyakatikaKituo cha kutoleadawazakufubazaVirusivytaUkimwi (CTC) katikaHospitaliyaSinza  ……………………..

  Na WAMJW – Dar Es Salaam.

  Serikali imetakiwa kutenga bajeti ya kutosheleza ili kuuwezesha Mfuko wa Taifa wa Ukimwi kujitegemea na kuepukana na utegemezi wa fedha za wafadhili katika mapambano ya Virusi vya Ukimwi.

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia masuala ya UKIMWI na Madawa ya kulevya Oscar Mukasa wakati wa kamati hiyo ilipofanya ziara katika Kitengo cha kutolea dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI (CTC) katika Hospitali ya Wilaya ya Ubungo kujionea hali ya utoaji huduma.

  Mhe. Oscar Mukasa (MB) amesema suala la upatikanaji wa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ni jambo la kitaifa na kamati yake ina mkakati wa kuhakikisha inaongeza nguvu kwenye Mfuko wa Taifa wa Ukimwi (ATF) na nchi kuweza kujitegemea kuhusu masuala ya UKIMWI.

  “Tuna haja ya kujipanga wenyewe kuhakikisha kwamba tunajitegemea, ule utegemezi wa fedha za wadau za mapambano ya Ukimwi unaweza kupungua”. amesema Mhe. Mukasa. Mhe. Mukasa amesema Serikali imekuwa ikitegemea fedha za wafadhili kutoka nje ya nchi na sasa ni vizuri tukajipanga wenyewe na kuacha utegemezi wa wafadhili hao kutoa fedha muda wote.

  Hata hivyo Mhe. Mukasa amesema kamati yake itaendelea kusimamia Serikali hasa Wizara ya fedha na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wanapata chanzo mahsusi cha kodi kwa ajili ya ATF.

  Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo na pia Waziri mwenye dhamana ya Afya, Maendeleo ye Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amefurahishwa kuona Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeanza kutekeleza agizo alilolitoa la kutoa ushauri, kupima pamoja na matibabu ya kufubaza virusi vya ukimwi.

  Aidha, Waziri Ummy ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kutekeleza agizo la Serikali kwa kutoa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi kwa muda kwa kipindi cha miezi mitatu kwa wagonjwa ambao wameshachunguzwa na kubainika virusi kufubaa.

  “Mpango wetu Serikali kwa wagonjwa ambao watakao kidhi vigezo basi watazipate dawa hizo kwa miezi sita”. Alisema Waziri Ummy na kuendelea kuwa wanalenga kuwaondolea usumbufu wa kuja mara kwa mara

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (mbele) akiwaongoza viongozi wa Wilaya ya Uyui na wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo leo. Picha na Tiganya Vincent.


  Na Tiganya Vincent


  UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(UYUI) umeagizwa kuongeza kasi katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ili ifikapo Juni mwishoni mwaka huu majengo yote waliyopangiwa yamewe yamekamilika.

  Agizo hilo limetolewa leo wilayani Uyui na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo.

  Alisema fedha zipo hakuna sababu ya kazi ya ujenzi kwenda pole pole kwa kuwa wananchi wanasubiri huduma hiyo kwa hamu.Jafo alisema katika Halmashauri nyingine ambapo walipewa fedha pamoja tayari majengo yao yako usawa wa madirisha lakini ya Uyui bado yako katika ngazi za msingi.

  Alisema sio vizuri kutumia fundi mmoja kujenga majengo yote ni vema wakatumia mafundi wengi ili kuharakisha kazi ya ujenzi wa Hospitali hiyo.

  Aidha Waziri huyo alisema ni jambo la kusikitishwa kuona Halmashauri hiyo imetumia kiasi cha milioni 8 kusafisha eneo badala ya kuwahamisha wananchi kushiriki katika usafishaji wa ili fedha hizo zisaidie ujenzi.

  Alisema fedha walizozitumia katika usafishaji wa eneo zingeweza kusaidia katika uendeleza wa ujenzi wa majengo hayo kama wananchi wangeshiriki katika usafishaji wa eneo badala ya kukodi Greda na kulipa kiasi hicho cha fedha.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya alimwakikishia Waziri kuwa watajitahidi kukamilisha majengo hayo katika kipindi kilichopangwa na kwa kuzingatia maelekezo ya TAMISEMI ili fedha zitakazobaki zisaidie kujenga kichoma taka.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui Said Ntahondi huku akishuhudiwa na viongozi mbalimbali wakati wa ziara yake kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo leo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya ( wa pili kutoka kulia) kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo leo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akitoa maagizo kwa viongozi wa Wilaya ya Uyui na wa Hamashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo leo.

older | 1 | .... | 1812 | 1813 | (Page 1814) | 1815 | 1816 | .... | 1897 | newer