Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1811 | 1812 | (Page 1813) | 1814 | 1815 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akihutubia washiriki wa Warsha ya Mafunzo kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda kuja Tanga yaliyofanyika katika Ukumbi wa Tanga Beach Resort Machi2, 2019.
  Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shigela akihutubia wakati wa Warsha hiyo.
  Sehemu ya Wajumbe walioshiriki Warsha ya Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa warsha hiyo.
  Sehemu ya Wajumbe walioshiriki Warsha ya Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba uya mgeni rasmi wakati wa warsha hiyo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akifuatilia jambo wakati wa warsha ya mafunzo hayo
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watendaji wa Serikali wakati uzinduzi wa warsha hiyo mkoani Tanga.


  Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’i Issa akizungumza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Tanga alipokutana nao wakati wa Warsha ya Mafunzo kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Machi 2, 2019.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka Sekta ya Umma wakati wa warsha hiyo.
  (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

  ………………………………………


  NA.MWANDISHI WETU

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama leo Machi 2, 2019 amefungua warsha ya mafunzo kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda kuja Tanga, Tanzania.

  Warsha hiyo iliwakutanisha zaidi ya wadau 70 wakiwemo viongozi Waandamizi na Watendaji Wakuu wa Mkoa wa Tanga, Wafanyabiashara wa mkoa huo pamoja na wanahabari na kufanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga.

  Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo ambayo itafanyika kwa muda wa siku mbili (Machi 02 na 03, 2019),Mhagama alisema Serikali inaendelea kuhimiza wananchi kutumia fursa ya mradi huo katika kujiletea maendeleo yao nan chi kwa ujumla.

  “Mkutano huu wa leo ni matumaini kuwa, utaleta mageuzi makubwa ya mipango mikakati yetu ili kuangalia fursa za ujio wa mradi huu kwa kuzingatia ni moja kati ya mradi unaotarajiwa kuwa na manufaa mengi kwa nchi katika kuzalisha ajira, kuendeleza urithishaji wa ujuzi na teknolojia pamoja na ubia kati ya makapuni ya Tanzania na wageni,”alisema Mhagama

  Waziri aliongezea kuwa, inawapasa wananchi kutumia warsha hiyo kujadili na kuweka mikakati bora ya kuzitumia fursa zitakazotokana na mradi kwa kuzingatia malengo mahususi ikiwemo kujadili maendeleo ya mradi na fursa za ushiriki wa Watanzania katika ujio ya mradi pamoja na kuwa na majadiliano kati ya Sekta Bonafsi ya Umma ili kuchochea maendeleo endelevu ya kiuchumi

  Aliongezea kuwa, mradi huo utasaidia jamii kushiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo kwa kuzingatia kuwa, ni zaidi ya robo tatu ya Bomba hili litapita Tanzania na kuwanufaisha wananchi wake.

  “Matarajio ni makubwa kwa kuzingatia mradi huu unatarajiwa kupita katika mikoa 8 ikiwemo Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga ambapo litapita katika Wilaya 24, Kata 134 na Vijiji zaidi 180 hivyo hatuna budi kuchangamkia fursa kwa kuongeza jitihada za ongezeko la ushiriki wetu,”alisistiza Mhagama

  Naye Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shiga aliendelea kuhimiza watendaji wake kushiriki kikamilifu katika hatua zote za maandalizi kama Mkoa ili kuona namna bora za kushiriki katika fursa hiyo kubwa ya kujileea maendeleo yao.

  Naye Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa alieleza jitihada za Baraza ikiwemo kuanzishwa kwa kanzi data ya nguvu kazi ambayo inachukua takwimu za wafanyabiashara ili kiuwatambua kwa lengo la kushirikisha katika program na kuona namba bora ya kuwashirikisha katika fursa hizo.

  “Niwaombe watanzania kuendelea kujisajili katika kanzi data ya nguvu kazi ili tuweze kuwatambua, uwezo na changamoto zenu na kuwashirikisha katika miradi mbalimbali ukiwemo huu wa bomba la mafuta pamoja na kutatua changamoto hizo,” alisisitiza Beng’i

  AWALI
  Warsha ya mafunzo hayo imeratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa ufadhili wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kupitia BEST Dialogue Tanzania kwa lengo la kuwezesha viongozi na Wafanyabiashara wa Mkoa huo kufahamu maendeleo na fursa zitakazotokana na mradi huo.Bomba hilo la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki lina urefu wa KM 1,443 kati ya hizo KM 296 zipo nchini Uganda na KM 1,147 zipo Tanzania

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya Ngaya wilayani Kahama, Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  6-3
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wajasiriamali katika eneo la Bukondamoyo wakati akiwa njiani kuelekea Ushetu, Kahama mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  7
  8-2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akwahutubia wananchi wa Ushetu katika uwanja wa Mikutano Nyamilongo wilayani Kahama, Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  4-4
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Ezekiel Maige mara baada ya kuwasili kwenye kituo cha afya Ngaya wilayani Kahama, Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Mwili Wa marehemu Ruge Mutahaba tayari umekwisha wasili nyumbani kwao kijijini Kiziru Bukoba mkoani Kagera leo,ambapo watu mbalimbali wamejitokeza kumpokea,huku msafara huo ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti .
  Sanduku lenye mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba ukipokelewa uwanja wa ndege wa Bukoba 'Bukoba Airport',na kupokelewa na watu mbalimbali huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiongoza mapokezi hayo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Brigedia Jenerali Marco Gaguti  amefika uwanja wa ndege kuongoza mapokezi ya mpendwa wetu Ruge Mutahaba. Kabla Brigedia Jenerali Marco Gaguti kufika hapa Kagera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kipindi kile alikuwa ni Kanali kabla ya kupanda cheo amefanya kazi za kizalendo bega kwa bega na Ruge Mutahaba mojawapo ikiwa ni Fursa na Ile ya Umoja wa Mataifa Kigoma Programu ya pamoja.
  Wazazi wa Marehemu Ruge,Prof Mutahaba na Mkewa akiwasili uwanja wa ndege wa Bukoba.
  Mtoto wa kwanza wa Marehemu akifarijiwa baada ya kuwasili Bukoba.
  Sanduku lenye mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba likipokelewa uwanja wa ndege wa Bukoba 'Bukoba Airport',na kupokelewa na watu mbalimbali huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiongoza mapokezi hayo.


  0 0

  Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Filbert Mponzi akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenesta Mhagama (kulia) baadhi ya vifaa tiba vilivyotolewa na NMB kwenye Kituo cha Afya Mirerani. Vifaa vilivyotolewa ni vitanda vitatu maalum kwa kujifungulia, vitanda 6 vya kulalia wagonjwa na magodoro yake, mashuka 70 na vifaa vya kupima kasi ya moyo, vyote vikiwa na thamani ya Sh Milioni 10.
  Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Filbert Mponzi akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenesta Mhagama (kulia) baadhi ya vifaa tiba vyenye thamani ya Sh Milioni 10 vilivyotolewa katika Kituo cha Afya Mirerani.

  Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Filbert Mponzi akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenesta Mhagama (kulia) juu ya vifaa tiba vilivyotolewa katika Kituo cha Afya Mirerani. Vifaa vilivyotolewa ni vitanda vitatu maalum kwa kujifungulia, vitanda 6 vya kulalia wagonjwa na magodoro yake, mashuka 70 na vifaa vya kupima kasi ya moyo, vyote vikiwa na thamani ya Sh Milioni 10.  NA MWANDISHI WETU, SIMANJIRO

  BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitanda vya kujifungulia pamoja na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh Milioni 10 katika Kituo cha Afya Mirerani kilichopo mkoani Manyara. Vifaa hivyo vimekabidhiwa wakati wa ufunguzi wa Kituo cha kutolea huduma za tiba na matunzo kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU), Mirerani, kituo kilichojengwa na Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF).

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Filbert Mponzi alivitaja vifaa hivyo kuwa ni vitanda vitatu maalum kwa kujifungulia, vitanda 6 vya kulalia wagonjwa na magodoro yake, mashuka 70 na vifaa vya kupima kasi ya moyo, huku vyote vikiwa na thamani ya Sh Milioni 10.

  "Napongeza Serikali kwa juhudi za kuboresha huduma za afya, NMB tunajua ni muhimu wadau binafsi kuunga mkono juhudi za Serikali na ndiyo maana huwa tunatenga asilimia moja baada ya kodi kusaidia sekta ya elimu na afya," alisema Mponzi.

  Awali akizindua Kituo hicho, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenesta Mhagama, amewataka viongozi, wananchi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika eneo la Mji Mdogo wa Mirerani, Mkoani Manyara, ambalo lina asilimia 16 ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

  Amesema jitihada za wadau zinahitajika ili kupunguza maambukizi mapya katika eneo hilo kwani Mamlaka ya mji mdogo ina maambukizi makubwa ikilinganishwa na maambukizi ya Mkoa mzima wa Manyara ambayo ni asilimia 2.3, huku akikemea vitendo vya unyanyapaa kwa walio na maambukizi.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, amesema bado kuna tatizo kubwa nchini la watu wengi kutokujitokeza kupima Ukimwi na ndiyo maana wamelazimika kusogeza huduma ya Kituo hicho katika eneo la Mirerani hususani kwa ajili ya wachimbaji.

  Amesema kuwa licha ya Kituo hicho kulenga wananchi wote,kitasaidia wachimbaji wengi kuhamasika kupima ili wajue afya zao na kuiomba Serikali na wadau kwa ujumla kufanya survey katika migodi yote nchini ili kujua hali ya maambukizi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenesta Mhagama (kulia) akiangalia sehemu ya vifaa vya afya vilivyotolewa na Benki ya NMB.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara Aziza Mangosongo akisaidiwa kupandishwa katika gari la wagonjwa baada ya kupata Rufaa toka hospital ya sokoine kwenda muhimbili..
   Mkuu wa mkoa wa lindi akiwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda(kulia ) wakimsindikiza mkuu wa wilaya ya Newala Aziza Mangosongo aliepata ajali jana usiku katika kijiji cha mandawa wilayani kilwa mkoani lindi na kukimbizwa katika hospital ya sokoine akiwa na majreuhi wengine watatu
   kuu wa wilaya ya Newala Aziza mangosongo akiwa tayari katika gari la wagonjwa kuanza safari ya matibabu Zaidi katika hospital ya Muhimbili
   Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi,akimsalimia mkuu wa wilaya ya newala Aziza Mangosongo kabla ya kupewa rufaa mchana leo

   Mkuu wa mkoa wa lindi,Godfrey zambi akibadilishana mawazo na mkuu wa mkoa wa mtwara,Gelasius Byakanwa mara baada ya kumtakia hali mkuu wa wilaya ya Newala Aliepata ajali jana na kulazwa katika hospital ya sokoine Mjini Lindi
   Mkuu wa mkoa wa lindi,Godfrey zambi akiwa na mkuu wa mkoa wa mtwara Gelasius Byakanwa ,pamoja wakuu wa wilaya waliofika kumtakia heri Mkuu wa wilaya newala katika hospital ya sokoine

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akifanyiwa uchunguzi wa sikio na Daktari bingwa wa masikio Dkt. Godlove Mfuko
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza maelekezo ya namna bora ya kutunza sikio kutoka kwa Daktari Bingwa wa Masikio Dkt. Godlove Mfuko kutoka Hospitali ya Taifa muhimbili - Mloganzila.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(kulia) akisalimiana na watoto waliofika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya usikivu.  Na WAMJW - Dar Es Salaam 

  Spika za masikioni maarufu kwa jina la “Headphones” zimetajwa kuwa chanzo kinachopeleka tatizo la usikivu hafifu kwa watu. 

  Hayo yamesemwa leo na Waziri mwenye dhamana ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na wananchi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Jijini Dar Es Salaam katika kuadhimisha siku ya usikivu duniani. 

  Waziri Ummy amesema kuwa matumizi ya simu za kisasa yameongeza kasi ya watu kutumia spika za masikioni jambo ambalo linahatarisha kuwa na watu wengi wenye matatizo ya usikivu. 

  “Unakuta kijana kuanzia asubuhi mpaka jioni ameweka spika za masikioni anasikiliza muziki hawajui wanajiweka katika hatari ya kupata tatizo la usikivu” amesema Waziri Ummy na kuendelea kusema kuwa kundi la vijana liko hatariki kupata matatizo ya usikivu. 

  Waziri Ummy ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kupunguza matumizi ya spika za masikioni ili kuweza kujikinga na matatizo ya usikivu. 

  “Nitoe rai kwa vijana wapunguze matumizi ya spika za masikioni kwa muda mrefu, tusipo kuwa makini tunaweza kujikuta tuna taifa lenye watu wengi wenye matatizo ya kutosikia vizuri” amesema Waziri Ummy. 

  Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa tatizo la usikivu hutokea pia kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa kuzaliwa na tatizo hilo au kulipata ukubwani kutokana na sababu nyinginezo ambazo zinaambata kwa kukaa kwa muda mrefu kwenye sehemu zenye kelele nyingi pamoja matatizo yanayoambata na afya ya sikio. 

  Waziri Ummy amesema kuwa ni jambo jema kuona sasa matibabu ya matatizo ya usikivu hafifu yanapatikana hapa hapa nchini huku akiwataka wananchi kukata bima za afya ili kuweza kupata matibabu kwa uhakika. 

  “Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha tatizo hili linazuiliwa kabla ya kutokea lakini pia kuhakikisha matibabu yanapatikana yakiwemo kutumia mashine ya mawimbi ya sauti, upasuaji wa kuziba tundu la ngoma ya sikio pamoja na kupandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia” amesema Waziri Ummy. 

  Hata hivyo alisema takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2018 Hospitali ya Muhimbili imefanikwa kuwapatia wagonjwa 116 vifaa vya mawimbi ya sauti, wagonwja 43 walifanyiwa upasuaji wa kuziba tundu la ngoma ya sikio. 

  Waziri Ummy amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa na kuhakikisha matibabu yanapatikana hapa hapa nchini. 

  Awali akitoa taarifa yake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw. Makwaiya Makani amesema kuwa wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali katika eneo la usikivu ikiwemo kutoa huduma ya upandikizaji vifaa vya usikivu kwa Watoto wenye matatizo ya hayo. 

  “Tangu mwezi Juni mwaka 2017 tayari watoto 21 wamepandikizwa vifaa vya usikivu kitaalam kwa jina la 'cochlear implants” amesema Bw. Makani 

  Bw. Makani amesema kuwa wameendesha kliniki ya siku mbili katika Hospitali ya Mloganzila kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya matatizo ya usikuvu ambapo watu 264 wamejitokeza kati yao watu 172 walihitaji uchunguzi zaidi wa usikivu, watu 64 wamekutwa na matatizo ya usikivu na tayari wamepatiwa rufaa kwa ajili ya matibabu zaidi na watu 31 wamekutwa na nta za masikioni,pia watu 26 wamekutwa na maambukizi kwenye masikio ambao wamepatiwa rufaa ya matibabu zaidi. 

  Tatizo la usikivu linazidi kuongezeka siku hadi siku. Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 5 ya watu duniani wana tatizo la usikivu. Tatizo hili litaongezeka maradufu ifikapo mwaka. Kila mmoja wetu achukue hatua kujikinga na tatizo hili ikiwemo kuepuka sehemu zenye kelele na pia kusikiliza mziki kwa sauti kubwa na kwa muda mrefu na kwa kutumia spika za masikioni. 

  0 0

  Na Frankius Cleophace Tarime.

  Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA North Mara Uliopo Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara unatarajia kuanza kulipa malipo yafidia ya ardhi kiasi ch Shilingi Billioni 3.8 ambapo zaidi ya Wananchi 200 kutoka vijiji Vilivyofanyiwa tathimini Mwaka 2011-2012 pamoja na awamu za 35, 41,na 42 katika vijiji vya Nyabichune, Mjini kati, Nyangoto, na Nyakunguru watalipwa fedha hizo.

  Akiongea na Waandishi wa habari Richard Ojendo ambaye ni Menejani wa idara ya Jamii Endelevu Mgodi wa Dhahabu wa North Mara alisema kuwa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unakusudiua kuanza zoezi la malipo ya fidia ya ardhi kwa wananchi waliopo kwenye vijiji Vinne katika eneo la Nyamongo.

  Ojendo aliongeza kuwa vijiji hivyo vilifanyiwa tathimini katika awamu ya 20 ya mwaka 2011-2012 pamoja na awamu za 35,41,na 42 vitalipwa kuanzia kesho.

  Pia aliongeza kuwa wananchi wa kijiji cha Nyabichune waliofanyiwa tathimini eneo la Makerero awamu ya 47 kwa waende kuechukua malipo yao ya fidia ifikapo 04 Machi Mwaka huu.

  “Zoezi hili ni kwa wananchi halisi wa maeneo na awamua ambazo zimetajwa ambao taarifa zao zilichukuliwa na mgodi kwa ajili ya malipo ya fidia na orodha kamili wananchi watakaolipwa tayari tumekabidhi viuongozi wa vijiji na vitongoji huska” alisema Ojendo.

  Aidha Richard aliongeza kuwa malipo kwa awamu nyingine yataendelea kulipwa na wahuska watajulishwa pale muda utakapofika na kuomba wananchi kuendelea kutoa ushirkiano mkubwa dhidi yao na Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA North Mara.

  Picha ya Richard Ojendo ambaye ni Menejani wa idara ya Jamii Endelevu Mgodi wa Dhahabu wa North Mara akiongea na Waandishi wa habari juu ya zoezi zima la malipo ya fidia kwa vijiji zaidi ya 200.
  Richard Ojendo ambaye ni Menejani wa idara ya Jamii Endelevu Mgodi wa Dhahabu wa North Mara

  0 0


   Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Marehemu Ruge Mutahaba ukiwa tayari umewekwa katika uwanja wa Gymkana,Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya kuagwa,Ibada  na baadae kurejeshwa tena Kiziru kwa ajili ya Mazishi.Katika sughuli hiyo viongozi mbalimbali wa Serikali,ndugu jamaa na marafiki wamefika uwanjani hapo kumpa heshima ya mwisho mpendwa wao.V
    Sanduku lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Marehemu Ruge Mutahaba ukiwa tayari umewasili katika uwanja wa Gymkana,Bukoba mkoani Kagera tayari kwa kupewa heshima ya mwisho.

   
  0 0

  *Ni zile ambazo zimepelekwa na Kiluwa,Mkurugenzi Mtendaji TIC atoa neno
  *Kiluwa asema ni jukumu la kila Mtanzania kufanikisha uwekezaji nchini

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  SERIKALI ya Mkoa wa Pwani,kupitia Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo amesema hawako tayari kuzikosa kampuni 13 ambazo zimepelekwa mkoani kwake kutokana na jitihada za Mkurugenzi wa Makampuni ya Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa.

  Mhandisi Ndikilo amebainisha hayo ofisini kwake baada ya majadiliano kati ya wawekezaji kutoka China, viongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na idara nyingine serikalini zinazohusika na uwekezaji.

  Ambapo Mhandisi Ndikilo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia juhudi ambazo zinafanywa na Kiluwa za kuleta wawekezaji kuwekeza mkoani humo zikiwemo Kampuni hizo 13 ambazo zimekuja kuwekeza na wamepata baraka za mkoa wake.

  Amefafanua baada ya kikao cha majadiliano Mhandisi Ndikilo amesema kazi iliyobaki ni kuangalia namna wawekezaji hao watakavyomalizana na mamlaka nyingine za nchi ili kufuata taratibu zinazotakiwa.

  "Hawa watu wamejipanga kuwekeza katika viwanda mbalimbali 13, mtaji wanao wapo tayari kuanza hata kesho. Naagiza kila idara ifanye kazi yake ili hawa wawekezaji tusiwakose," amesema Mhandisi Ndikilo.

  Katika maelezo yake kutokana na kutumia muda wa zaidi ya saa sita kujadiliana kuhusu mustakabali wa wawekezaji hao wakiwa na kamati ya ulinzi na usalama na maofisa mbalimbali wakiwemo wa TIC na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Ndikilo alisema:

  “Fursa na sifa tulizonazo kama mkoa kunavutia wawekezaji wengi, ila kama tunavyofahamu uwekezaji haufanyiki angani bali kwa kutumia ardhi, kulikuwa na mvutano kuhusu ardhi ndio mana tumetumia muda mwingi kujadiliana.

  “Vilevile tumejadili mambo mengi kuhusu aina ya uwekezaji mkubwa unaotaka kufanyika, sote tumeridhia namna walivyojipanga wamekuja na mitaji mikononi na aina ya bidhaa na huduma watakazozalisha, wanataaka kuhamisha teknolojia kutoka China kuja Tanzania. Ndiyo maana nimetoa wiki mbili majibu yapatikane hawa wawekezaji waanze kazi.”

  Akizungumzia eneo la uwekezaji la Kiluwa Free Processing Zone, Mhandisi Ndikilo amesema hatakubali kuona wazo hilo la mtanzania mzalendo linapotelea hewani wala kuona wawekezaji wanakwenda nchi jirani kwa kukimbia mizengwe nchini.

  “Mkoa wetu una ardhi kubwa ya uwekezaji, Kibaha ina maeneo mengi nay a kutosha hata kule Mlandizi tuna ekari zaidi ya 5,000 hazijaguswa. Hivyo, nataka waelewe Mkoa wetu ni wa amani ndio mana tumeiita na kamati ya ulinzi na usalama ishiriki mkutano huu.

  “Serikali inataka kuipeleka nchi katika uchumi wa kati kwa kutegemea viwanda, sasa tukiona watu wenye nia ya kuanzisha viwanda wanasumbuliwa hatuwezi kukaa kimya. Taratibu zote wamefuata lakini ikionekana mkoa wangu ndio kikwazo sitakubali,” amesema Mhandisi Ndikilo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geofrey Mwambi alisema kazi ya kuleta wawekezaji ni ya serikali. Hivyo, wanavyoona watu wanaisaidia serikali hawawezi kuwavunja moyo.

  "Hawa ni wa mwanzo tu wapo wengi, kati ya hao 13 tayar wawekezaji sita wameshakuja na vifaa vyao wanasubiri kupewa ruhusa waanze kazi. Kuna viwanda vya Battery, bidhaa za ngozi na mabehewa," anasema Mwambi.

  Mwakilishi wa kundi la wawekezaji hao ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sinoma East Africa Co. Limited, Lu Xiaoqiang alisema wameichagua Tanzania kwa kuwa wanaamini kuna fursa nyingi za uwekezaji na kwa muda wa miaka 10 waliyofanya kazi nchini wamevutiwa na namna watanzania walivyo wakarimu.

  “Tupo tayari kushirikiana na watanzania na kuwafundisha ujuzi wa mambo mbalimbali, tunataka kuanzisha viwanda vya bidhaa za plastiki, chuma, battery na vifaa vingine vya kielektroniki. Tunahamisha utaalamu kutoka China kuja Tanzania,” alisema Xiaoqiang.

  Naye Kiluwa amesema TIC inawaelekeza nini cha kufanya hivyo hawawezi kuwaangusha na wataendelea kufanya kazi nao kadiri ya uwezo wao.“TIC kazi yao imeshakamilika, huwa wanatupatia elimu ili kufuata taratibu zinazostahiki kusajili wawekezaji, naishukuru serikali ya Mkoa wa Pwani kwa msaada mkubwa iliyotoa kwetu na kukubali kutusikiliza hadi kuelewa lengo letu katika uwekezaji.

  “Kuna zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 100 zinataka kuwekezwa hapa, hiyo ni fursa ya ajira na Mamlaka ya Mapato Tanzania itaongeza mapato. "Hawaii wawekezaji wamejipanga hawana muda wa kupoteza, kati ya viwanda 13 wawekezaji sita tayari wameshaleta hadi vifaa wanasubiri kupewa ruhusa tuwaanze kazi,” alisema Kiluwa.

  Amesema ni jukumu la Watanzania kila mmoja kwa nafasi take kuhakikisha maono ya Rais Dk.John Magufuli ya kuhamasisha ujenzi wa viwanda unafanikiwa kwa vitendo,hivyo mkakati wake ni kuendelea kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini.

  "Nina ardhi ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji,hivyo wawekezaji ninapowamasisha kuja nchini kuwekeza pia nawaeleza na uwepo wa ardhi na wakija nchini wanakwenda TIC ambako ndiko watapewa utaratibu kwani niliamua hati ya ardhi niliyonayo kwa ajili ya uwekezaji iwe wazi kwa TIC pia," ameongeza.

  Amesisitiza katika kufanikisha uwekezaji kwake anaona ni jambo jema kwani kikubwa anachoamini mbali ya watanzania kupata ajira,teknolojia ambayo inaletwa na wawekezaji itabaki nchini kwa maslahi ya Watanzania.",Ninachokifanya ni kama nang'oa teknolojia nje naileta nyumbani."

  Mkuu wa MKoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mwishoni mwa wiki ,mara baada ya kumaliza kikao cha pamoja wakati wa majadiliano kati ya wawekezaji kutoka China, viongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na idara nyingine serikalini zinazohusika na uwekezaji.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geofrey Mwambe akisalimiana na mmoja wa wekezaji mara baada ya kumaliza kikao chao cha pamoja na Mkuu wa Mkoa
  Mhandisi Evarist Ndikilo.
   Mwakilishi wa kundi la wawekezaji hao ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sinoma East Africa Co. Limited, Lu Xiaoqiang akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu kwanini wameichagua Tanzania kuwekeza,ambapo alieleza kuwa wanaamini kuna fursa nyingi za uwekezaji na kwa muda wa miaka 10 waliyofanya kazi nchini wamevutiwa na namna watanzania walivyo wakarimu.
   Mkurugenzi wa Makampuni ya Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari mwisho mwa wiki Kibaha mkoani Pwani,mara baada ya kumaliza kikao chao cha pamoja.

  Baadhi ya wadau wa maendeleo ya uwekezaji wa Viwanda mkoa wa pwani,kwamati ya Ulinzi na usalama  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
  Mhandisi Evarist Ndikilo,wakati wa majadiliano kati ya wawekezaji kutoka China, viongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na idara nyingine serikalini zinazohusika na uwekezaji.
  Picha ya pamoja

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Dkt. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Yahya Simba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha Mawaziri wawili, Balozi mmoja na kushuhudia uapishwaji wa Maofisa watano wa Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna Benedict Michael Wakulyamba mara baada ya hafla ya uapisho kukamilika Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Makamishna watano kutoka jeshi la Polisi, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi, pamoja na Balozi Yahya Simba mara baada ya hafla ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Dini mara baada ya hafla ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na Maofisa Mbalimbali wa Jeshi kutoka Jeshi la Polisi mara baada ya hafla ya Uapisho wa viongozi mbalimbali  Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma   na  Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na Makamishna watano kutoka Jeshi la Polisi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimvalisha cheo kipya cha Kamishna Liberatus Sabas ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimuapisha Kamishna Liberatus Sabas ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akimvalisha cheo kipya cha Kamishna Leonard Paul Lwabuzala ambaye ameteuliwa kuwa kamishna wa kamisheni ya polisi Fedha na Lojistiki, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU 


  0 0

  Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Meneja Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo na kushoto ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Ali Said.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akizungumza wakati akimkaribisha Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Hassan Mwang'ombe (kulia), kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mkakati wa shirika katika kuimarisha maduka yake ya kubadilishia fedha za kigeni nchini. Katikati ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Said. 
  Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakiwa kwenye mkutano huo.
  Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakimsikiliza Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, wakati akizungumza na waandishi leo jijini.
  Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakijadiliana jambo wakati wa mkutano huo.  
  Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (katikati), akuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mkakati huo wa shirika.
  Baadhi ya wateja wakipata huduma kwenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ya Shirika la Posta leo, Ofisi ya Posta Kuu jijini Dar es Salaam. 
  Wateja wakiwa katika Kituo cha huduma mbalimbali za shirika wakisubiri kupatiwa huduma, Ofisi ya Posta Kuu jijini Dar es Salaam leo.
  Moja ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ya Shirika la Posta, jijini Dar es Salaam. 

  CHINI ni Taarifa iliyotolewa na Postamasta Mkuu kwa waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo

  TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGULIWA KWA MADUKA NA VITUO VYA KUBADILISHIA FEDHA ZA KIGENI VYA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

  Tarehe 28 february 2019 Benki kuu ya Tanzania ilitangaza kwamba maduka ya kubadilishia fedha yatabaki kwenye mabenki, taasisi za kifedha pamoja na maduka ya fedha za kigeni za Shirika la Posta Tanzania tu.

  Tunapenda kuutarifu umma wa watanzania kuwa Shirika la Posta limejizatiti katika kutoa huduma hiyo kwa umma wa watanzania na tunapenda kuwajulisha kuwa mpaka sasa tunavyo vituo kumi (10) vinavyotoa huduma ya kubadilisha fedha ambapo ni Kariakoo, Posta Mpya, Kijitonyama, Oysterbay, City drive (Sokoine ) , Libya Posta, Uwanja wa ndege, vituo hivi vyote vipo jijni Dar es Salaam na mpaka ifikapo tarehe 15 Marchi 2019 tutakuwa na vituo ishirini(20) vya kubadilishia fedha za kigeni.

  Pia tuna mikoa miwili ambayo tayari huduma hii imeanza nayo ni ofisi kuu ya Posta Zanzibar na Arusha, Pia tunatarajia mwishoni mwa mwezi Marchi mikoa 17 yenye ofisi za posta zitaanza kutoa huduma hiyo. Tungependa kuutaarifu Umma ,watembelee katika vituo vyetu vya posta kupata huduma hii ya ubadilishaji fedha za kigeni.


  Shirika la Posta Tanzania linapenda kuujulisha Umma kupokea taarifa hii muhimu kwao na kwa maendelea ya Taifa.

   imetolewa na ;
  POSTAMASTA MKUU NA MTENDAJI MKUU
  SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

  0 0

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Sheria Ndg Goerg Joseph Kazi, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
   MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, wakihudhuria hafla ya kuapishwa Mawaziri na Makatibu Wakuu walioteuliwa hivi karibuni,hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar leo,(Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi, anayeshuhulikia Masuala ua Uvuvi na Mifugo Dr.Omar Ali Amir.(Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dkt. Ali Mohamed Shein,akisaini Hati ya Kiapo ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar anayeshughulikia Masuala ya Mifugo na Uvuvi Dr.Omar Ali Amir.(Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Ndg Seif Shaban Mwinyi, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba, Maji na Nishati. Ndg. Salhina Ameir Mwita, hafla hiyi imefanyika leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Bi.Mansura Misi Kassim, hafla hiyo imefanyika Ikulu leo Zanzibar.(Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Serikali  Said Hassan Said na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh, Omar Saleh Kabi,waliosimama nyumba ni Mawaziri aliowaapisha leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)   
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Serikali  Said Hassan Said na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh, Omar Saleh Kabi,waliosimama nyumba ni Makatibu Wakuu na Manaibu aliowaapisha leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)     
   MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, wakihudhuria hafla ya kuapishwa Mawaziri na Makatibu Wakuu walioteuliwa hivi karibuni,hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar leo,(Picha na Ikulu)

  0 0
 • 03/04/19--08:21: DC PANGANI AWAFUNDA VIJANA
 • MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Zainabu Abdallah akizungumza wakati akifungua warsha ya vijana juu ya kutambua malengo 17 ya maendeleo endelevu ya Dunia yaliyoendeshwa na serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) yakishirikisha vijana 100 wa kike na kiume kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Alvaro Rodrigues kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange 
  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Alvaro Rodrigues akizungumza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia ni Mwenzeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Didi Nafisa ambaye pia ni Afisa Habari wa Shirika hilo 
  Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange akizungumza 
  Mwenzeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Didi Nafisa ambaye pia ni Afisa Habari wa Shirika hilo akizungumza 
  Sehemu ya Vijana kutoka maeneo mbalimbali wilayani Pangani wakifuatilia warsha hiyo kwa umakini   MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Zainabu Abdallah amesema umaskini hauwezi kuondoka ikiwa vijana bado watakuwa mawazo ya potofu kuhusiana na umaskini huku wakitakiwa kuuchukia. 

  Zainabu aliyasema hayo mjini Pangani wakati akifungua warsha ya vijana juu ya kutambua malengo 17 ya maendeleo endelevu ya Dunia yaliyoendeshwa na serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) yakishirikisha vijana 100 wa kike na kiume. Alisema lazima vijana watambua upo umuhimu wa kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao badala ya kukaa na kuacha kufikiria kukaa vijiweni na kujiingia kwenye makundi yasiyokuwa na tija kwa maendeleo. 

  “Matatizo ya vijana wanayafahamu vijana hivyo serikali ipo tayari kuwaunga mkono kwa juhudi zozote mnatakazo anzisha …lakini pia mwaka huu kuna chaguzi za serikali za mita hivyo tunataka viongozi vijana tutakaoweza kuzungumza nao lugha moja na kusimamia maendeleo endelevu ya dunia”Alisema. 

  Aidha alisema kupitia mafunzo hayo yatasaidia kuongeza wigo mpana wa fursa kwa vijana wilayani humo ambao watakwenda kuibadilisha wilaya hiyo na kuwataka wazazi kuhakikisha wanawapatia elimu bora watoto waop badala ya kujiingiza kwenye shughuli za uvuvi. Mkuu huyo wa wilaya aliwataka vijana wa Pangani kuchangmkia fursa hiyo ili iweze kuwasaidia ikiwemo kujitambua kwamba wana nafasi gani kwa Taifa na wilaya kwa kujiletea maendeleo kwani wao ndio chachu ya mafanikio kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kiuchumi, kisiasa na kujamii. 

  Awali akizungumza wakati wa warsha hiyo Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Alvaro Rodrigues alisema uwepo wao ni kwa ajili ya kutekeleza malengo endelevu ambayo ndio malengo ya dunia 2016 hadi 2030 kwa kuwapatia elimu vijana ili wawezi kujitambua na kuona namna ya kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao. 

  Alisema pia kwenye mafunzo hayo wanajikita kuwasaidia wanawake kutokana na kwamba asilimia 50 ya watu duniani ni wanawake hivyo wakiachwa nyuma dunia inaweza kudhoofisha maendeleo. 
  “Nusu ya idadi ya watu dunia ni wanawake hivyo ikiwa wataachwa nyuma kwenye Nyanja zote za kimaendeleo maanake tutakuwa tumerudisha nyuma ukuaji wa uchumi kwa wananchi”Alisema .

  Hata hivyo alisema ifikapo 2030 wawe na ulimwengu bora kwa kuzingatia malengo ya milenia katika kuhakikisha vijana wanazingatia malengo ya maendeleo endelevu ambayo ni watu, sayari, ustawi, amani na ushirikiano. 

  Kwa upande wake Mwenzeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Didi Nafisa aliwataka vijana walioshiriki kwenye warsha hiyo kuzingatia mafunzo hayo ili yaweze kuwa na tija ikiwemo kubadilisha maisha yao. 

  Nafisa ambaye pia ni Afisa Habari wa Shirika hilo alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwakwamua vijana na tatizo la ukosefu wa ajira ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa nchi nyingi dunia. 
  “Tatizo la ukosefu wa kazi dunia linaongezeka kutoka watu milioni 170 kwa mwaka 2007 hadi kufikia milioni 202 mwaka 2012 hapo utaona sasa watu milioni 75 kati ya hao ni vijana wa kike na kiume”Alisema.

  0 0

   
   


  0 0

  Wawakilishi wa vikundi vya Wanawake, vijana na walemavu wakipokea hundi ya mfano yenye thamani ya shilingi milioni 53 kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo (kaunda nyeusi) katika hafla fupi ya kukabidhi mikopo hiyo kwa vijana.
  Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akikabidhi mkopo kwa mmoja wa wanakikundi cha Mshikamano kutoka kijiji cha Chala katika hafla fupi ya utoaji mikopo katika Halmshauri ya Wilaya ya Nkasi ambapo vikundi 15 vilipatiwa mikopo ya jumla ya Shilingi milioni 53.
  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akitoa nasaha zake kwa wanavikundi wajasiliamali waliopewa mikopo (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kutoa mikopo hiyo. 
  Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa nasaha zake kwa wanavikundi wajasiliamali waliopewa mikopo (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kutoa mikopo hiyo.


  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wajasiliamali wa Wilaya ya Nkasi kuhakikisha fedha ya mkopo waliyopewa na halmashauri hawazitumii katika matumizi binafsi bali wazielekeze katika biashara ili ziweze kuwapatia faida na kuwainua kiuchumi na hatimae kupata fedha za kujikimu kimaisha.

  “Kwenye vikundi vyenu mna malengo mahususi na ili haya malengo mahususi yaweze kutimia kwenye biashara hakuna kingine zaidi ya kuwa bahili lazima muwe mabahili, lazima muwe watu ambao hamkubali kutoa fedha hovyo hovyo, uskibali kutoa fedha ambayo haina mpango, leo unaambiwa kuna msiba pale wewe unachukua fedha ya mkopo unapeleka, huu sio ubahili, weka fedha yako vizuri, kama kuna shida tafuta hela nyingine,na ukichukua fedha inayotokana na hapo labda ni faida,” Alisema.

  Ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 53 ikiwa ni asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani ya halmashauri kwa vikundi 15 vya halmashauri ya wilaya ya Nkasi ikiwa ni utekelezaji wa kisheria chini ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lililoanzishwa Mwaka 2005 chini ya sheria na 16 ya mwaka 2004 yenye adhima ya kuwainua wananchi kiuchumi ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Katika kulisisitiza hilo Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini Mh. Ally Kessy alisema kuwa pesa hizo ni kodi za wananchi ambazo halmashauri inapita kuzikusanya nahatimae asilimia 10 ya mapato hayo kuyagawa kama mikopo kwa wajasiliamali wanawake, vijana na walemavu na kusisitiza kuwa fedha hiyo irudishwa kadiri inavyotakiwa.

  “Fedha hii ni mkopo na sio sadaka, isiwe kukopa harusi na kulipa matanga, kulipa ni wajibu, hizi pesa sio sadaka ni kodi ya wananchi na kodi ya wanachi haiendi bure, mnakopeshwa mkafanye maendeleo sio muanze kununua magauni au kwenda harusini hakuna ni kufanyia mtradi, kama unaona kikundi chako hakina uwezo na kulipa msichukue ili wapewe wengine,” Alisisitiza.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emanuel Sekwao wakati akiseoma taarifa alisema kuwa Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Jumla ya vikundi 15 viliomba mikopo ya Tshs. 68,292,000.00. lakini baada ya Kamati ya Mikopo kukaa na kupitia maombi ya mikopo jumla ya kiasi cha Tshs 53,000,000 kiliidhishwa.

  “Vikundi vitakavyokopeshwa ni 15 ambapo Vikundi vya Vijana vitatu Jumla ya fedha Tshs 12,687,000 Kikundi cha Walemavu kimoja, Jumla ya fedha Tshs 2,000,000 na Vikundi vya Wanawake kumi na moja, jumla ya fedha Tshs 38,313,000. Vikundi hivyo vimetoka katika kata za Mashete, Kipundu, Majengo, Sintali, Namanyere, Chala, Kipande, Kabwe, Kate, Kirando na Kala.”

  Nae mkuu wa wilaya hiyo Mh. Said Mtanda alimuhakikishia mkuu wa mkoa kuwa watajitahidi kuhakikisha wanakusanya mapato ya halmashauri kwa asilimia 100 na kutoa mikopo hiyo kwa vijana na kuwapa fursa ya kujiajiri lakini pia kuongeza viwanda vidogovidogo kutokana na shughuli mbalimbali za uzalishaji wanazojihusisha nazo wajasiliamali hao.

  Katika kutoa shukrani mmoja wa vijana wa kikundi cha Panda Miti Rukwa (PAMIRU) Uswege Mwasomola alisema kuwa lengo lao ni kuwa na shamba la miti la kikundi ili kusaidia kutunza mazingira na kuongeza kuwa kutokana na mkopo huo walioupata wataweza kutatua changamoto walizokuwa nazo kwa asilimia 100.

  “Mkuu wa Mkoa pamoja na viongozi wote nadhani mwaka ujao hatutakuja kukimbizana kufuatilia mikopo zaidi tutakwenda kifua mbele kwa kuhakikisha tunairudisha kwa muda muafaka ili tutoe fursa kwa vijana wengine,” alisema.

  Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi katika mwaka wa fedha 2018/2019 inatarajia kukusanya jumla ya Tshs 2,304,000,000/= kupitia vyanzo vyake vya ndani. Katika kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi Februari 2019 jumla ya Tshs 1, 511,915,838.67 ilikusanywa ambapo sawa na asilimia 65.62 ya bajeti ya mwaka wa fecha 2018/2019.

  0 0


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisema jambo na wadau wa biashara ya kemikali (hawapo pichani) kwenye mkutano na wafanya biashara za kemikali nchini.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Prof Esther Hellen Jason akisema jambo na wadau wanaojihusiha na biashara ya kemikali (hawapo pichani) katika mkutano na wadau wanaojihusisha na biashara ya kemikali.

  Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akisema jambo kwa wadau wa biashara ya kemikali nchini (hawapo pichani) katika mkutano na wadau wanaojihusisha na biashara ya kemikali nchini.

  Mdau wa bishara ya kemikalina Katibu Mkuu wa Mawakala wa Forodha Tanzania Mhandisi Anthony Swai akiwa amebeba sampuli ya kemikali mapema leo kwenye kikao cha wadau wanaojihusisha na bishara ya kemikali nchini.

  Wadau wanaojihusisha na biashara ya kemikali wakiwa kwenye mkutano uliotishwa na Ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kujadili namna bora ya kuboresha biashara ya kemikali nchini.  Serikali itaendelea kusimamia na kudhibiti matumizi ya kemikali ili kuhakikisha hazileti madhara kwa afya za wananchi.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo alipokuwa kwenye mkutano na wadau wa kemikali kujadili namna ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara ya kemikali nchini.

  “Kemikali zisipodhibitiwa vizuri zinaweza kuleta madhara katika afya, mazingira pamoja na kuhatarisha usalama wa nchini, ipo haja ya kuweka mazingira mazuri ya kusimamia na kudhibiti uingizaji na matumizi ya kemikali nchini ili zisilete madhara” amesema Waziri Ummy.

  Hata hivyo takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2014 zinaonyesha vifo milioni 12.6 vilitokana na mazingira duni ya kuishi, mojawapo ya kichocheo ni athari za kemikali ambazo zimekuwa zikisababisha magonjwa na vifo.

  Waziri Ummy amesema kuwa kemikali zimekuwa na athari kubwa kwa binadamu kwa kusababisha magonjwa zaidi ya 100 huku akiyataja magonjwa ya moyo, saratani, ngozi, athari katika mifumo ya fahamu, upumaji pamoja na chakula kuathiri zaidi wananchi wengi.

  “Tukubali kuwa kemikali zina madhara kwa wananchi lakini sasa tuwe na mazingira mazuri ya kuzidhibiti” amesema Waziri Ummy na kuendelea kusema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira mazuri kwa wafanya biashara ya kemikali nchini.

  Kwa upande mwingine Waziri Ummy amezitaka Taasisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) kuangalia upya tozo wanazotoza kwa wafanyabiashara za kemikali nchini pamoja na kupunguza urasimu usiokuwa na ulazima ili kuwawekea mazingira rafiki wafanya biashara za kemikali.

  “Msiwe ni kikwazo kwa uwekezaji na biashara, kikwazo cha kushamiri na kukua kwa uwekezaji nchini, nataka muwe mawakala wa kukuza biashara na uchumi nchini” amesema Waziri Ummy.Awali akisoma taarifa yake Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema Sheria ya Kemikali ya mwaka 2003 imekuwa na mchango mkubwa katika udhibiti wa matumizi ya kemikali nchini.

  “Kabla ya kutungwa kwa sheria hii, kemikali zilikuwa zikiingizwa nchini kiholela na kutumika bila ya kuwa na ufatiliaji au udhibiti wowote” alisema Dkt. Mafumiko.Dkt. Mafumiko amesema Sheria ya kemikali imewawezesha kudhibiti usafirishaji, utumiaji pamoja uteketezaji wa taka zinazotokana na kemikali.

  “Ofisi ya Mkemia inasimamia kwa ukaribu matumizi ya kemikali zote zinazoingizwa nchini kuanzia zinapoingia, mahali zinapokwenda pamoja na matumizi yaliyokusudiwa” alisema Dkt. Mafumiko.Naye Katibu Mkuu wa Mawakala wa Forodha Tanzania Mhandisi Anthony Swai amesema tozo zimekuwa nyingi kiasi cha kuwaumiza wafanyabiashara wa kemikali huku urasimu pia ukisababisha wafanyabiashara kutumia muda mwingi kufuatilia vibali vya uingiza wa kemikali nchini.

  Aidha Mhandisi Swai ameiomba Serikali kuainisha mipaka ya taasisi za umma pamoja na tozo wanatostahili kulipa kwani kumekuwa na mwingiliano wa majumuku baina ya taasisi za Serikali ambazo amezijata kuwa ni GCLA, TDFA na TBS (Shirika la Viwango Tanzania

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda (aliyeshika tofali) akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo wakati wa ziara fupi ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya hiyo ulioanza mapema mwaka huu na kutakiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka 2019.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (rainboot za kijani) akiangalia uimara wa matofali yaliyojengewa msingi katika moja ya majengo saba ya hospitali ya wilauya ya Sumbawanga inayojengwa katika bonde la ziwa Rukwa, kata ya Mtowisa. (mwenye shati ya kitenge) Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule.


  ………………………….

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakuu wa Wilaya za Mkoani Rukwa kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa pamoja katika kutembeleana na kuelezana changamoto na mafanikio katika maeneo ya mradi wa ujenzi wa hospitali za wilaya ili kujenga hospitali hizo katika hadhi sawa na hatimae kupeana ujuzi wa utekelezaji wa mradi huo.

  Amepongeza ushirikiano unaoonyeshwa na uongozi wa wilaya ya Nkasi unaoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo mh. Said Mtanda pamoja na wabunge, madiwani na mkurugenzi na kusifu mafunzo waliyoyapata na kuyarekebisha wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa vituo vitatu vya afya katika wilaya hiyo na kuonyesha dalili za kutojirudia kwa makosa waliyoyafanya wakati wakitekeleza ujenzi wa vituo hivyo.

  “Wakuu wa Wilaya waweke program ya kutembeleana kwa pamoja ili kujifunza, wanakuja kwa mfano (wilaya ya) Nkasi, wanakwenda wilaya ya Sumbawanga, Wanakwenda wilaya ya Kalambo halafu watakaa chini wafanye tafakari ili waone ni namna gani wanweza wakasimamia vizuri hizo hospitali zetu za wilaya kwasababu tunapaswa tuwe na kitu bora, hospitali zote tatu ziwe bora ndani ya mkoa wetu,” Alisisitiza.

  Alisema kuwa halitakuwa jambo jema kwa wilaya moja kuwa na ufanisi sana ilihali wilaya nyingine inakuwa na changamoto na hivyo vyema wakaungana kama timu na kutembelea miradi hiyo ya ujenzi wa hospitali za wilaya ili kila mmoja aweze kujifunza kutoka kwa mwenzie.

  Ameyasema hayo baada ya ziara yake ya kutembelea ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga ili kujionea changamoto mbalimbali zinazoukabili mradi huo ambao unatakiwa kuisha mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu.

  0 0   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mataka (wa pili kushoto) akimpongeza mshindi wa kwanza katika mbio za kilomita 21 maarufu kamaTigo Kili Half Marathon Emmanuel Giniki baada ya kuibuka mshindi. Wa kwanza kulia aliyeshikilia mfano wa hundi kwa ajili ya kumkabidhi mshindi huyo ni ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Kamuni ya Tigo Simon Karikari.

  Mkurugenzi Mtendaji Tigo Simon Karikari (wa kwanza kulia)akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa RT Anthony Mtaka waki mkabadhili mfano wa hundi ya Sh milioni 1, 025,000 Falluna Abdi aliyeshika nafasi ya pili kwa wanawake kwenye mbio za Kilometa 21 maarufu kama Tigo Kili Half Maratahon zilizofanyika mjini Moshi.
  PIC 02-min
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Tigo wakiwa na nyuso za furaha huku wakionyesha medali zao baada ya  ‘kufuta vilimia’ na kufanikiwa kumaliza mbio za kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon zilizofanyika mjini Moshi ambazo ziliwashirikisha wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 duniani
  PIC 03-min
  Mshindi wa mbio za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon Emmanuel Giniki akihojiwa baada ya kufanikiwa kuibuka mshindi  wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika mjini Moshi na kuwashirikisha wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 duniani

  MTANZANIA Emmanuel Giniki ameibuka mshindi wa mbio za kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon zilizofanyika mjini MoshI.
  Giniki amevunja mwiko kwa mbio hizo ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikitawaliwa na raia wa kigeni na husasani Wakenya ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiibuka washindi.
  Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili, Giniki alisema anayofuraha kushinda mbio hizo na kuiletea heshima nchi yake jambo ambalo amekuwa akilitamani.
  “Pamoja na kwamba mbio hizi zimekuwa zikifanyika hapa nyumbani, tumekuwa tukishindwa kuzitendea haki kwa kuwa wageni ndiyo wamekuwa wakizitawala. Ninayofuraha leo nimeweza kulitoa taifa langu kimasomaso,” alisema.
  Akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari alisema kampuni yake inayofuraha kuchangia maendelea ya michezo nchini na hususani riadha ambayo pia huboresha afya
  Karikari alisema Tigo imekuwa mdhamini wa mbio za Kili half Marathon kwa kipindi ch miaka minne mfululizo na kuongeza kuwa itaendelea kudhamini pamoja na kuboresha mbio hizo kila mwaka.
  Waziri wa Habari, utamaduni vijana na Michezo Dk Harrison Mwakyemba aliishukuru Tigo kwa kudhamini mbio hizo na kuwataka wakazi wa Moshi kutumia fursa zitokanazo na mbio hizo kujijenga kiuchumi.
  “Mbio hizi zimeleta wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 hapa mjini Moshi. Idadi hii kubwa ya watu itokanayo na mbio hizi ni fursa nzuri ya kibiashara na ni vyema wakazi wa Moshi wakaichangamkia,” alisema Waziri Mwakyembe.
  Mbio za Kilimanjaro Marathon hufanyika mjini Moshi kila mwaka. Idadi ya washiriki wa mbio hizo imekuwa ikiongezeka kwa mujibu wa waandaaji kutoka wakimbiaji 750 wakati za kikianza hadi kufikia washiriki 11,000 kwa sasa.

  0 0


  Anaandika Abdullatif Yunus – Kagera.

  Mwili wa marehemu Rugemalila Gerazi Mutahaba umepumzishwa jana katika Nyumba yake ya Milele , Nyumbani kwao Kable Bukoba Mkoani Kagera, huku mazishi hayo yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Waziri, Wabunge, na Viongozi wa Siasa, Wakuu wa Mikoa wasanii na watu mashuhuri.

  Wakiongea mara baada ya shughuli hiyo ya mazishi baadhi ya Viongozi hao wamezidi kumzungumzia Marehemu Ruge kama lulu ya Taifa kwa yale yote aloyafundisha na kuelekeza njia kuwa yafaa kuigwa na kuenziwa kwa namna moja ama nyingine.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa kilimo na Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mh. Innocent Bashungwa akiongea na Michuzi Tv amemuelezea Ruge kuwa, Alikuwa kijana tofauti mwenye maono ya mbali, na ameweza kuyaishi na kutuonyesha kwamba na sisi kama vijana wakati wa ujana tutumie ujana wetu kuhakikisha tunaacha alama hapa Duniani. Pia ameongeza kuwa, kama vijana wa Kitanzania tumeachiwa changamoto kwamba hata kama muda wa kuishi ni mfupi, tukitumia vizuri muda wetu tutaweza kulisaidia Taifa letu la Tanzania.

  Nae Naibu Waziri wa Maji Jumaa Awesso amesema Marehemu RUGE kwake ni kama Daktari wa fikra kwani ameweza kubadiri fikra hasi kuwa fikra chanya, na ameweza kuwasaidia Vijana, na akitusisitiza tusiwe vijana Kaa badala yake tusaidiane, kuhakikisha taaluma na Vipaji tulivyonavyo tuinuane katika mambo mbalimbali na kuweza kulisaidia Taifa letu, hivyo katika kumuenzi tunatakiwa kuwa na upendo, ushirikiano na ubunifu kwamba changamoto zipo lakini tunaweza kuzigeuza kuwa fursa, hivyo na sisi kama Vijana tutahakikisha hatuwi Vijana Kaa ili tuweze kusaidiana na kulisaidia Taifa letu.

  Katika Upande Mwingine Mh. Deodatus Kinawiro Mkuu wa Wilaya ya Bukoba alipozikwa Ruge amesema Marehemu Ruge amekuwa mhamasishaji mkubwa katika kutumia fursa zilizopo nchini kwa ajili ya kujipatia kipato, kujenga Uchumi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla, kupitia fikra alizokuwa nazo na ndoto kubwa za kuinua vijana wenzake, hivyo mchango ake katika Taifa hili utazidi kuwa mkubwa kupitia kuyaenzi matendo yake.

  Nae Mh. Murshidi Ngeze Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba anasema Ruge amekuwa mpambanaji ambae ametuachia somo kubwa kwetu, na alama yake haiwezi kufutika ambapo ni kazi yetu kuzingatia yale yote aliyotufundisha na kuyaenzi, hivyo kama Halmashauri wananafikiria kuiomba familia Watengeze Foundation ambayo itayaishi yale yote alokuwa akiyafanya, huku akiongeza kuwa kazi kubwa sasa imebaki kwa Pacha wake Marehemu Ruge, Bwana Joseph Kusaga kuhakikisha anandelea kijenga familia ya Clouds kuwa pamoja na wasione kama Ruge amewatoka kimoyo bali kisura hivyo ni Jukuma la Clouds kama Taasisi kuendelea kuimarika na kusonga mbele.
   Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akiwa ameketi pembeni yake ni Mh. Ridhiwani Kikwete (MB), Mh. Angella Kairuki _ Waziri wa Uwekezaji Mh. Dotto Biteko Waziri wa Madini na Na Mh. Innocent Bashungwa Naibu Waziri wa Kilimo, wakifuatilia Shughuli ya Kuaaga Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba katika Viwanja vya Gymkhana Bukoba.
   Mh. Innocent Bashungwa Naibu Waziri wa Kilimo akiweka maua katika kaburi la Marehemu Ruge kama Ishara ya Kuzika.
    Mh. Deodatus Kinawiro Mkuu wa Wilaya Bukoba akiweka maua katika kaburi la Marehemu Ruge kama Ishara ya Kuzika.
    Mwenyekiti Halmashauri ya  Wilaya Bukoba,Murshidi Ngeze akiweka maua katika kaburi la Marehemu Ruge kama Ishara ya Kuzika.
  Wakuu wa Mikoa ya Kagera na Dar es salaam Mh. Gaguti na Mh. Makonda wakiweka shada  la maua katika kaburi la Marehemu Ruge kwa Niaba ya Wananchi wa Mikoa yao.


older | 1 | .... | 1811 | 1812 | (Page 1813) | 1814 | 1815 | .... | 1897 | newer