Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1799 | 1800 | (Page 1801) | 1802 | 1803 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Trekta aina ya URSUS likiendelea na kazi yakulima mashamba ya wakulima katika Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.
  Kazi ya uunganishaji matrekta katika Kiwanda cha Kuunganisha Trekta kilichopo Kibaha mkoani Pwani ikiendelea ikiwa ni juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kufufua na kukuza sekta ya Kilimo hapa nchini ambapo matrekta zaidi ya 200 yameunganishwa na kuuzwa kwa wakulima mbalimbali nchini.
  Moja ya Trekta aina ya URSUS likiwa limekamilika. 
  Matrekta yaliyounganishwa yakiwa tayari kuuzwa.

  Sehemu ya majembe ya matrekta ya URSUS yakiwa tayari yameunganishwa Kiwandani Kibaha mkoani Pwani.
  Trekta aina ya URSUS likiendelea na kazi yakulima mashamba ya wakulima katika Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.
   
  Mkulima kutoka Wilaya ya Gairo, Haji Salum akifanyia majaribio ya kuendesha trekta aina ya URSUS mara baada yakukabidhiwa trekta hilo alilonunua kutoka Kiwanda cha kuunganisha matrekta kilichopo Kibaha mkoani Pwani. (Picha na MAELEZO)

  Na: Lilian Lundo - MAELEZO

  Kiwanda cha Kuunganisha Trekta Aina ya URSUS kilichopo Mkoani Pwani kimekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima wadogo kutokana na masharti nafuu ya ukopeshaji wa trekta hizo.

  Kutokana na urahisi wa upatikanaji wa trekta hizo umepelekea kuongezeka kwa idadi ya wakulima wenye trekta ambazo zimekuwa zikiwalimia wakulima wadogo wadogo kwa gharama nafuu.

  Akizungumia Trekta hizo, Mkulima wa zao la Mahindi na Alizeti kutoka Gairo, mkoani Morogoro, Haji Salum ambaye alikutwa kiwandani hapo akichukua trekta aliyoinunua kwa mkopo, ameeleza kuwa anafuraha kubwa ya kumiliki chombo hicho ambacho atakitumia kulimia mashamba yake pamoja na wakulima wenzake.

  "Ninayofuraha kubwa kupata chombo hiki ambacho sikutarajia kukimiliki katika maisha yangu. Ninamshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kauli mbiu yake ya ujenzi wa viwanda ambayo imetuwezesha hata sisi maskini kumiliki trekta," amesema Salum.

  Mkulima huyo anayemiliki heka 120 za mashamba ya mahindi na alizeti mkoani humo amesema, kwa kulima mashamba yake peke yake anauwezo wa kurejesha fedha ambazo zimebaki kukamilisha malipo ya trekta hiyo anayoimiliki.

  Mkulima huyo amewashauri Watanzania kujitokeza kwa wingi kununua trekta hizo kwani masharti yake ni nafuu na zipo kwa ajili ya kila Mtanzania hata wale wenye kipato cha chini.

  Aidha, mmiliki mwingine wa trekta hizo kutoka Wilaya ya Malinyi, Mkoa wa Morogoro Jacob Mbifile ameishukuru Serikali kwa kupata trekta kwa gharama nafuu ambayo anaitumia kulima mashamba yake pamoja na kuwalimia wakulima wenzake kwa kuchangia kiasi kidogo kwa ajili ya marejesho ya mkopo na uendeshaji wa chombo hicho.

  "Kwa sasa tunalima kwa wakati, kutokana na uwepo wa trekta nyingi, tofauti na ilivyokuwa zamani, ambapo wakulima wengi walikuwa wakipata huduma ya kulimiwa kwa kuchelewa kutokana na uchache wa trekta uliokuwepo hivyo kusababisha kuvuna mazao machache kutokana na kuchelewa kupanda," ameeleza Mbifile.

  Kwa upande wake, Mkulima wa zao la Mpunga Wilayani humo, Ladislaus Kidunda amesema kabla ya uwepo wa trekta hizo, kulikuwa na uhaba mkubwa wa trekta hivyo kusababisha foleni kubwa ya kusubiri trekta ili kulimiwa.

  "Kipindi cha nyuma tulikuwa tukipata huduma ya kulimiwa kwa trekta kwa tabu sana kutokana na wamiliki wa trekta hizo kuwapa kipaumbele wale wenye mashamba makubwa kuanzia heka 10 na kuendelea. Tofauti na ilivyo sasa ambapo wamiliki wamekuwa wengi hata sisi wenye heka mbili au tatu tunaweza kupata huduma hiyo kwa wakati," amesema Kidunda.

  Nae Msimamizi Mkuu wa Kiwanda hicho, Godwin Mubi amesema mpaka tarehe 15 Januari mwaka huu, jumla ya trekta 261 zimenunuliwa kwa njia ya mkopo katika mikoa ya Manyara, Mwanza, Dodoma, Ruvuma, Singida na Morogoro na mikoa mingine ikiwa kwenye mchakato wa kununua trekta hizo.

  "Tunakopesha trekta hizi kwa kila Mtanzania anayehitaji, ambapo hutakiwa kutoa asilimia 25 ya gharama ya trekta na gharama inayobaki atairudisha kwa kipindi cha miaka miwili. Njia nyingine ni ile ambayo mkulima anaonesha dhamira ya kupata trekta, hivyo hulipia milioni 3 hadi 4 na kiasi kinachobaki hurejesha katika kipindi cha miaka miwili," amesema Mubi.

  Aidha Mubi ameeleza, spea za trekta za Ursus zipo na zinapatikana kwa wingi nchini hivyo Watanzania watembelee kiwandani hapo kujua namna ya kumiliki trekta hizo kwani masharti na gharama yake ni nafuu.

  Kiwanda cha Kuunganisha Trekta za Ursus ni kiwanda kinachosimamiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ambapo huunganisha Trekta zinazokuja kwa vipande kutoka nchini Poland. Kiwanda hicho kilianza rasmi kufanya kazi Aprili, 2017 ambapo ni moja ya matunda ya kauli mbiu ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya ujenzi wa viwanda.


  0 0


   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza  na  Balozi  wa  Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia),  juu  ya  kubadilishana  uzoefu katika Udhibiti  wa  Mipaka. Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  PIX 2
  Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni   juu ya kubadilishana  uzoefu  katika  Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi  Ndogo  ya  wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  PIX 3
  Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan  akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  PIX 4
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi  Hamad  Masauni, akiagana na Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kubadilishana uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo  hayo  yamefanyika  leo, Ofisi  Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  ……………………………………………………………………………

  Na Mwandishi Wetu

  Serikali ya Tanzania na Nchi ya Kuwait ziko katika mpango maalumu wa kubadilishana uzoefu juu ya udhibiti wa mipaka ikiwa ni juhudi za Tanzania kuimarisha ulinzi katika mikoa yote nchini iliyopo mipakani

  Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa mazungumzo na Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan ikiwa ni mpango wa nchi hizo kubadilishana uzoefu katika kudhibiti uhalifu katika mikoa ya mipakani

  “Kama Serikali tuna vipaumbele katika kudhibiti  mipaka yetu kutokana na uhalifu unaotokea ikiwemo wahamiaji haramu,usafirishaji wa binadamu, uingiaji wa silaha,utoroshwaji wa madini na biashara yamagendo, ndio maana tumekutana leo kujadili ushirikiano wa nchi hizi mbili katika kudhibiti uhalifu huo”alisema Masauni

  Akizungumza katika kikao hicho Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan alisema Tanzania ni nchi salama na wameamua kubadilishana uzoefu katika usimamiaji na udhibiti  wa mipaka.

  “Tuna uhusiano mzuri baina ya Kuwait na Tanzania,tumekubaliana kubadilisha uzoefu ili kuweza kuimarisha sekta ya ulinzi kwa kutumia teknolojia itakayorahisisha udhibiti wa mipaka hapa nchini Tanzania” alisema Balozi Mubarak

  Katika mazungumzo hayo pia walijadili juu ya teknolojia ya udhibiti wa majanga ikiwemo moto na ajali ambapo pia ni eneo ambalo nchi hizo mbili zilishaanza kushirikiana katika shughuli za uokozi

  0 0


  Watu wanne wamepoteza maisha katika ajali iliyohusisha magari aina ya Canter lenye namba za usajili T223ATK na Hiace yenye namba za usajili T869 CHC kugongana katika Mlima Nyangoye eneo la Hamugembe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

  Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Februari 8,2019.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Revocatus Malimi,ambaye amefika eneo la ajali ambayo imetokea katikati ya barabara,amesema watu wanne wamefariki dunia katika ajali hiyo.

  "Canter ilikuwa Main Road ikitokea Rwamishenye ikiingia Mjini kati,baada ya ajali hiyo kutokea,magari hayo yalitoka nje ya barabara,bahati mbaya gari aina ya Hiace ilishika moto na watu waliokuwemo waliungua moto,tumeondoa maiti mbili za abiria na dereva mwenye hiyo Hiace pia dereva wa bodaboda aliyekuwa amefunganishwa kwenye hii ajali bahati mbaya amefariki,kwa hiyo jumla ya watu waliofariki katika ajali hii ni watu wanne,mpaka sasa maiti zipo hospitali ya Mkoa hazijatambuliwa"- RPC

  "Bado tunaendelea na shughuli ya uokoaji na uchunguzi kubaini hasa nini chanzo cha ajali hii na atakayebainika kusababisha ajali,hatua za kisheria zitachukuliwa",amesema Kamanda Malimi.  Baadhi ya Wanachi wakitoa msaada wa kuinasua miili ya watu iliokuwa imenasa kwenye magari hayo
  Watu wanne wamepoteza maisha katika ajali iliyohusisha magari aina ya Canter lenye namba za usajili T223ATK na Hiace yenye namba za usajili T869 CHC kugongana  uso kwa uso  katika Mlima Nyangoye eneo la Hamugembe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.  0 0


  NA BALTAZAR MASHAKA, SENGEREMA.

  MKURUGENZI wa kampuni ya Baraka Mining inayojihusisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu, almasi na vito, Baraka Chilu ameahidi kujenga madrasa itakayotumika kufundishia elimu ya dini hiyo, kununua pikipiki na mazuria ya msikitini hapo Kijiji cha Kasenyi wilayani Sengerema.

  Pia Chilu ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri ya BAKWATA Sengerema alitoa fedha sh. 500,000 za kulipa posho ya miezi miwili ya mwalimu wa dini ya kiislamu, kati ya fedha hizo kiasi cha sh. 150,000 zitatumika kununulia baiskeli ya kumrahisishia usafiri wa kwenda na kurudi kutoa elimu kwenye shule za msingi na sekondari za Nyamahona.

  Mgeni rasmi huyo wa maonyesho ya umahiri wa kuhifadhi Kuran na hadithi za Mtume Muhammad S.A.W.lililofanywa na wanafunzi wa madrasa ya Msikiti wa Kasenyi, alilionyeshwa kuguswa na changamoto ya wanafunzi hao kukosa sehemu sahihi ya kujifunzia elimu ya dini kutokan na risala iliyosomwa na katibu wa madrasa hiyo.

  "Fanyeni tathmini ya gharama za ujenzi wa madrasa na nitakuwa tayari kuijenga.Kwa kuanzia natoa sh.500,000 za usafiri na posho ya mwalimu na baadaye nitamletea pikipiki mpya,nitanunua sare za wanafunzi wote 30 pamoja na mazuria ya msikitini,"alisema.

  Awali akisoma risala Katibu wa Madrasa ya Msikiti wa Kasenyi,Hamidu Basinda alisema wana changamoto ya ukosefu wa jengo la madrasa kujifunzia, posho na usafiri wa mwalimu, sare za wanafunzi na maji kwa matumizi mbalimbali.

  "Tunayo changamoto ya madrasa ya watoto kupata elimu ya dini na mazingira, tunatumia msikiti kutoa elimu hiyo, hakuna usafiri wa uhakika wa mwalimu kwenda kutoa elimu ya dini kwenye shule za umma.Changamoto ambazo zinakwamisha uislamu kustawi Kasenyi,"alisema Basinda.

  Alisema licha ya uchumi wao mdogo wamefanikiwa kuboresha Msikiti wa Kasenyi kwa kuweka madirisha ya mbao na umeme kwa fedha walizouza mazao (vyakula anuwai) na kuimarisha nguzo za uislamu. 

  Aidha, baada ya mfanyabiashara huyo kuahidi kujenga madrasa, Sheikh wa Msikiti wa Kasenyi Swadiki Mchwampaka ili kuunga mkono ufadhili huo aliwashauri waumini wa msikiti kuchangia nguvu zao.

  "Shule ni biashara baina ya waja na Mwenyezi Mungu, tunahitaji kushikamana vizuri katika kuendeleza elimu ya dini (kiroho) na watoto ni haki yao kupata elimu ya mazingira na kiroho pia!Lakini pia ibada ndio msingi wa dini,inaleta heri na kukataa maovu,"alisema Sheikhe Mchwampaka na kuongeza;

  "Usafiri umepatikana na tumeambiwa tutasaidiwa kujenga madrasa.Sasa na sisi tuchangie nguvu zetu ili kuunga mkono juhudi za mfadhili,."
  Jengo la Msikiti wa zamani wa Kasenyi linalotumika kama madrasa ya kufundishia elimu ya dini ya Kiislamu likiwa nimechakaa na kupata nyufa na hivyo kuhatarisha Maisha ya wanafunzi.
    Mkurugenzi wa kampuni ya Baraka Mining, Baraka Chilu (kulia) akimkabidhi fedha sh.500,000 Sheikhe wa Msikiti wa Kasenyi Sheikhe Swadiki Mchwampaka kwa ajili ya posho ya mwalimu wa madrasa na kununulia baiskeli.Chilu ameahidi kujenga madrasa ya msikiti huo. 
    Sheikhe wa Msikiti wa Kasenyi Swadiki Mchwampaka (kulia) akimuonyesha Mkurugenzi wa Baraka Mining, Baraka Chilu (kushoto) jengo la msikiti wa zamani ambalo limechakaa lakini limekuwa likitumika kama madrasa. Picha na Baltazar Mashaka

  0 0

  Serikali imesema haitakua tayari kuona Amani na Utulivu wa Nchi inachezewa huku ikisisitiza uwepo wa Umoja kati ya wananchi bila kujali tofauti ya imani, kabila au itikadi yoyote.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifungua Semina ya siku mbili iliyofanyika jijini Dar es Salaam ikiwahusisha Viongozi wa Taasisi za Kiislamu lengo ikiwa ni kuwakumbusha kuhubiri amani katika sehemu zao

  Amesema muelekeo na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kukuza maendeleo katika sehemu mbalimbali nchini lengo ikiwa kuinua maisha ya wananchi nan chi kwa ujumla

  “Serikali hii imejidhatiti kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa kasi na maendeleo hayawezi kuja ikiwa amani na utulivu haupo, sisi kama serikali tutahakikisha tunalinda amani iliyopo ili wananchi wapate kufanya shughuli za kiuchumi bila wasiwasi wowote” alisema Masauni

  Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum aliihakikishia serikali kutokuwepo kwa mifarakano kati ya taasisi mbalimbali kama ilivyokuwepo awali huku akisisitiza kuendelea kwa umoja huo ili jamii ipate kuendelea

  “Sisi kama Bakwata tunaihakikishia serikali uwepo wa umoja na ushirikiano baina ya baraza na taasisi zingine na tofauti zetu hazipelekei kukoseana au kuvunjiana heshima kwahiyo tunaomba serikali iamini uwepo wa maelewano mazuri tu kwa maendeleo ya nchi hii” alisema Sheikh Mussa

  Semina hiyo ya Siku mbili imejumuisha viongozi wa Taasisi mia moja huku mada ya Nafasi ya Taasisi za Kiislam katika Kuleta Umoja na Kuishi kwa Amani itajadiliwa.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, ambapo aliwahakikishia uwepo wa Amani na Utulivu nchini.Ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam
  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, ambapo aliihahakikishia serikali kuwepo kwa maelwano kati ya taasisi mbalimbali za dini lengo ikiwa ni kurahisisha maendeleo nchini.Ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) akisalimiana na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum baada ya kuwasili katika Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, ambapo aliwahakikishia uwepo wa Amani na Utulivu nchini.Ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  Na Grace Semfuko-MAELEZO 

  Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imetoa jumla ya shilingi Bilioni 28 kwa Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuendeleza miradi miwili ikiwepo ujenzi wa soko la Tandale na uboreshaji kwa kuendeleza ufukwe wa Osterbay, maarufu Coco Beach, lengo likiwa ni kulipa thamani eneo hilo na kuongeza watalii wa ndani nan je. 

  Utiaji saini kwa ajili ya mkataba wa ujenzi huo ulifanywa February 4 mwaka huu, kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dotto James na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagulumjuli, ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 14 zitaendeleza Ufukwe wa Osterbay, eneo la Coco Beach na zingine Bilioni 14 zitajenga Soko la Tandale. 

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mazingira ya “Mchanga Pekee” iliyo na lengo la kubadilisha mazingira ya fukwe za bahari ya Hindi, jijini Dar Es salaam, iliyofanyika leo asubuhi kwenye ufukwe wa Coco, zoezi lililoambatana na usafi wa mazingira kwenye eneo hilo. 

  “Wilaya yangu ya Kinondoni tumekuja na mpango maalum wa kuimarisha mazingira ya Bahari, tunazo Bilioni 28 kwa ajili ya miradi miwili ya kuimarisha mazingira; zikiwemo fukwe za Osterbay zinazojumuisha eneo hili la Coco pamoja na kuimarisha mazingira ya soko la Tandale” Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Chogolo Wanavikoba wa Buguruni na taasisi mbalimbali zilizofika kushiriki. 

  Akisikilizwa na karibu mamia ya watu, wengi wao wakiwa akina mama wa vikoba, Bw. Chongolo alisema zoezi lililopo sasa ni hatua ya kutangaza mzabuni kwa ajili ya ujenzi huo ambapo katika kipindi cha miaka miwili ijayo shughuli hiyo itaanza. 

  Mbali na fedha hizo za miradi miwili, Serikali mwaka jana ilitoa zaidi ya shilingi Bilioni 9 kwa ajili ya ukarabati wa soko la Magomeni, Jijini Dar Es Salaam zoezi ambalo linaendeleo mpaka sasa, aidha Chongolo alitoa wito kwa jamii kuhusu kuendeleza na kuzitunza fukwe za bahari ili kutengeneza mazingira mazuri ya wananchi kupumzika pia kubarizi 

  Naye Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania – TTB, Geofrey Tengeneza alisema fukwe za Bahari ni maeneo muhimu kwani watalii wengi wa ndani na nje ya nchi hutembelea maeneo hayo na hivyo yanahitaji kutunzwa katika hali ya usafi. 

  “Fukwe hizi ni muhimu sana kwa utalii katika nchi yetu, hivyo tunahitaji kuzitunza na tusichafue mazingira ya fukwe zetu” alisema Tengeneza na kusisitiza kuwa ufukwe wa Coco ni maarufu kwa watu wote na serikali inatambua hilo na kwamba utaendelea kutumiwa na watu wote kwa ajili ya kupumzika na burudani. 

  Kampeni ya “Mchanga pekee” imeanzishwa na Kampuni ya Cocacola kwanza na inalenga kuboresha mazingira ya fukwe za Bahari na kuwa safi na Cocacola inashirikisha Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na mashirika na taasisi mbalimbali nchini. 

  Kampeni hiyo imekuja kufuatia ripoti ya Shirika la “International Council of Beverages Associations (ICBA)” iliyotolewa mwishoni mwa mwaka 2018 ikionesha uchafuzi mkubwa wa fukwe za bahari duniani kufikia wastani wa vipande vya plastiki kilomita elfu 13 na kubainika kuwepo kwa tani milioni 150 za plastiki kwenye fukwe hizo mpaka leo. 

  Mkurugenzi Mkuu wa Cocacola, Bazil Gadzios leo alisisitiza kuwa kampeni hiyo inalenga kufanya usafi kwenye fukwe wa Coco Beach, kukusanya chupa za plasitiki elfu kumi kila mwezi, kutoa elimu kwa jamii kuhusu kuhifadhi mazingira ya fukwe za bahari, kupunguza chupa hizo pamoja na kuhifadhi ekolojia ya viumbe vya Baharini na nchi kavu. 


  0 0  Tabitha Luhuja wa Benki ya NMB (wa pili kulia), akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya nane ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata. Kutoka kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Sinza Mori, Mnkande Zawadi, Sophia Mwamwita, Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemedy na Bi. Saumu Rajabu kutoka Selcom.


  Meneja Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala akizungumza wakati wa Promosheni ya washindi wa droo ya nane ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBatan iliyofanyika katika Tawi la Benki hiyo la Sinza Mori jijini Dar es Salaa. Kushoto ni Meneja wa Tawi la Benki hiyo la Sinza Mori, Mnkande Zawadi.


  Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo, Yusuph Achayo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu promosheni hiyo.  WATEJA sita wa Benki ya NMB wamejishindia simu janja 'Samsung S9+' baada ya kuchezeshwa droo ya nane ya shindano la Benki hiyo ya kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata'. Washindi hao wapya wanakamilisha idadi ya washindi 12 hadi sasa waliojishindia simu kama hizo katika shindano hilo.

  Washindi walioshinda na kujinyakulia simu hizo wametajwa kuwa ni Taha Karimjee kutoka maeneo ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam, Gladys Gilbert, Salim Abdallah, Raphael Schuurmans wa Masaki jijini Dar es Salaam, Imara Noah wa Meatu na Burton Anyisile wa Kahama mkoani Shinyanga.

  Akizungumzia kuhusu promosheni hiyo Meneja wa Benki hiyo Tawi la Sinza Mori, Mnkande Zawadi alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi za simu hizo.

  Alisema katika droo ya mwisho washindi watatu watapata ofa ya kwenda kula 'Bata' Dubai huku wakiambataba na mtu mmoja wa kila mshindi ambapo jumla yao watakuwa sita na gharama zote za safari hiyo zitalipwa na benki hiyo kwa siku nne watakazo kuwepo nchini humo.

  "Tunawaomba wateja wetu ambayo akaunti zao hazifanyi kazi wazifungue katika muda huu uliobaki wa promosheni hii ili waweze kushiriki na kushinda zawadi hizo pamoja na safari hiyo" alisema Zawadi.Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo, Yusuph Achayo , aliwaomba wateja wa Benki ya NMB kuendelea kutumia huduma hiyo ili kujiweka katika nafasi kubwa ya kuibuka mshindi na kwenda kula bata Dubai.

  Katika droo ya kwanza wateja 100 wa Benki hiyo walifanikiwa kujishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila mmoja huku wengine sita wakijishindia simu hizo za 'Samsung S9+' zenye thamani ya shilingi milioni 300.

  0 0

  Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

  Tamasha kubwa la Pasaka linalosubiriwa kwa hamu linatarajiwa kuanza kuwasha moto kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, April 21, 2019.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema tamasha hilo litakuwa la kihistoria kutokana na kuzunguka mikoa isiyopungua 10, amesema Mikoa hiyo itaongezwa kwa ajili yakutoa fursa kwa wengine kushuhudia burudani hiyo.

  Msama amesema Mikoa ambayo imethibitishwa mpaka sasa kwa Wananchi kukaa mkao wa burudani ni Simiyu, Mwanza na Iringa ambayo imepitishwa na Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo.

  ‘’Wakazi wa Dar es Salaam na Mikoani mjiandae na Tamasha hili la Kihistoria, kuna Msanii mkubwa anatarajiwa kuhudhuria tamasha hili, si lakukosa’’, amesema Msama

  Pia Msama amesema kuwa lengo kubwa kufanya Tamasha hilo ni kuombea Amani Taifa pamoja na Viongozi wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amefanya kazi kubwa na nzuri katika kipindi cha uongozi wake ndani ya miaka mitatu.

  Kaulimbiu ya Tamasha hilo ni: Umoja na Upendo, hudumisha amani katika nchi.


  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari maandalizi ya tamasha la Pasaka linalosubiriwa kwa hamu,ambalo linatarajiwa kuanza kuwasha moto kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, April 21, 2019. Msama amesema kuwa tamasha hilo litakuwa la kihistoria kutokana na kuzunguka mikoa isiyopungua 10, amesema Mikoa hiyo itaongezwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa wengine kushuhudia burudani hiyo.

  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Msama Promotions, Alex Msama alipokuwa akizungumza nao leo jijini Dar kuhusu muendelezo wa maandalizi ya tamasha la pasaka.

  0 0
 • 02/09/19--05:09: TANZIA

 • Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit C.V Kakoko anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake mzazi, Mzee Conatus Vitalis Kakoko (81) kilichotokea juzi katika Hospitali ya Agakhan alipokuwa amelazwa kwa takribani wiki moja akisumbuliwa na maradhi ya Ini na Figo.

  Hadi umauti unamkuta, Mzee Conatus Vitalis Kakoko ameacha watoto wanne (4) na wajukuu kumi na tano (15).

  Misa ya kumuaga marehemu Mzee Conatus Vitalis Kakoko itafanyika katika kanisa la MT. Petrol lililopo Oysterbay siku ya Jumatatu, tarehe 11/2/2019 saa tatu asubuhi.

  Mara baada ya misa hiyo, mwili wa marehemu Mzee Conatus Vitalis Kakoko utasafirishwa siku ya Jumatato tarehe 13/02/2019 kweda kijijini kwake, Munjebwe, Rulenge mkoani Kagera kwa mazishi.
  Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa. Jina lake litukuzwe.

  0 0

  Na Said Mwishehe, Glob ya Jamii 

  MUIGIZAJI maarufu nchini Steven  Mengere almaarufu Steve Nyerere amemuomba radhi msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpozy.

  Kwakukumbusha Steve Nyerere alitoa kauli ya kwamba Ommy Dimpoz hawezi tena kutoa nyimbo yeyote kutokana na maradhi yanayomsumbua.

  Hata hivyo msanii Ommy Dimpoz ameipua wimbo wake kabisa unaokwenda kwa jina la Ni wewe.Steve Nyerere baada ya Kutoka kwa wimbo huo amekuwa akishambuliwa na makundi ya watu mbalimbali mitandaoni .

  Kupitia ukurasa wake wa Istagramu Steven Nyerere leo februari 9,2019 ameandika hivi ." kwanza nichukuwe fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu ,lakini pili nichukuwe fursa hii kumuomba radhi ndugu yangu Dimpoz kwa namna alivyopokea kauli yangu niliyoitoa dhidi yake na zaidi niwaombe radhi watanzania wote na wapenzi wa Sanaa .Binadamu unapoona hapa umekosea busara inatutaka kukiri kukosea nami nikiri kukosea kutokana na ile kauli yangu kwa Dimpoz.

  " Lakini ifahamike kwamba kauli ile haikuwa kwamba namtakia mabaya Dimpoz hapana ila kwa tulivyokuwa tunapata taarifa kwakweli zilikuwa zinatukatisha tamaa," amesema Steve Nyerere.

  Ameongeza kuwa mengi yameongelewa lakini ifahamike kwamba hakuwa na nia mbaya wala hakuwa na ugomvi na Dimpoz bali kama Binadamu hutokea kuteleza kwenye kuzungumza na hivyo asichukuliwe kwaniambaya .

  "Lakini tunafahamu kwamba Mwenyezi Mungu hufanya miujiza yake kutokana na sababu furani hivyo miujiza ya kumuinua ndugu yetu na kurudi kwenye kazi zake imetokana na imani aliyonayo Dimpoz kwa muumba wake.

  " Najua mie niliteleza kwa kusema kwamba Dimpoz hatoimba tena lakini sikuwa na nia hiyo ,kwangu natamani Dimpoz asiimbe tena Hapana kutokana na vichekesho mbalimbali vinavyotolewa juu yangu lakini vinanifurahisha kwani vinazidi kuupaisha wimbo mpya wa Ni wewe. 

  "Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba watanzania na wapenzi wa
  Muziki kuzidi kumsapoti ndugu yetu pamoja na Kumuombea dua kwa Mwenyezi Mungu ili azidi kuimarika kiafya."amesema Steven Nyerere.
  Ikumbukwe kuwa Ommy Dimpoz kwa muda mrefu amekuwa kimya katika muziki kutokana na kusumbuliwa na tatizo la koo ambapo alilazimika kwenda nje ya nchi kwa matibabu .

  Hata hivyo kwasasa afya yake imeimarika na tayari ametoa wimbo mpya wa Ni wewe ambao umeaza kukubalika na kupendwa na wapenzi wa muziki.

  0 0

    I don’t doubt many politicians have done things worthy of regret, but it is becoming difficult to keep up with the sorry spectacle. I would like to share with you this story, please take some few minutes to read it.

  “A group of people were travelling in a boat. One of them took a drill and began to drill a hole beneath himself. His colleagues said to him: “Why are you doing this?” The man replied: “Why are you concerned about it? Am I not drilling under my own place?” They said to him: “But you will flood the boat for all of us!” 

  Imagine being a passenger on this boat, and one person, without concern for you or others, endangers  your safety and security. The person drilling a hole on the boat may have valid reasons for doing so. Perhaps they want to drop a fishing line because they are hungry. Maybe they want to use the water to cool their feet or wash. Maybe the boat is on a lake and they want water to drink. But no matter how rational the reason, drilling a hole in a boat to fulfill the desires of just one individual jeopardizes everyone’s safety. 

  This story warns us of the destructive power of letting our selfish desires overtake all other considerations. It’s not about whatever floats your boat.”


  It is true that patriotism has lost feeling for most of politicians, the hierarchy of importance has been Self, family, friends and finally Country. Self interests has driven politicians to the extent of setting their peaceful Countries to war, for example in 1992 Angola ,more than 300,000 people died, in 1994 more than 800,000 died in Rwanda. I believe under President Magufuli’s administration this will not happen, he promised to protect Tanzanian and he is walking the talk.

  Tindu Lissu may have valid reasons for what he is currently doing , touring abroad and tarnishing our Country’s image, he might be revenging against the so called “unknown people” thinking that the government is behind them for the tragedy incident which happened to him in Dodoma. He may also have hidden intentions such as trying to win a Presidential nomination from his political party and therefore gaining popularity through western media. However no matter how rational the reason may seem to him, spoiling your Country’s reputation globally has absolutely no excuse, and therefore he needs to apologize to Tanzanians for what he has done to our beloved Tanzania.


  For a mature politician who was born and raised up in Tanzania, studied in Tanzania where education by the time was free, and he was paid by the Government at University level, cannot be pushed this far by circumstantial evidence of the tragic incident that happened to him. The wise thing is to cooperate with the police and other security organs to allow intensive investigation of the incident and send the suspects to the court of law.

  Moreover, you seem to be in a fit state to come back home and continue with your responsibility of representing your constituency, bearing in mind in several occasions people have believed in you and voted for you to represent them in Parliament, it is not that you are very special among other people in your constituency, but the person your people used to see inside you before becoming greedy and start drilling the boat Tanzania to fulfill your desires. The cost of doing what you’re doing in western media will be reflected in vote ballot in 2020! be careful for the citizens of Tanzania love President Magufuli because he is working for them.

  Another important advice, please learn to appreciate, too much demanding is not going to help you, there are so many good things the people and Government of Tanzania has done to you, the Government has paid for your medical expenses with taxpayers money when you were in Nairobi, more than Tsh 246.7 million has been paid in Belgium.

  Now letting you destroy the plate in which more than 50 million Tanzanians are served including yourself by spreading malicious lies against Tanzanians and the Government is unacceptable. Who doesn’t know what the current Administration has done, in three years time? We have corruption in the Country going down and public embezzlement diminishing faster than ever.


  President Magufuli has revived the public airline which had only one plane with six brand new airplanes which has facilitated local and international trade, major projects with significant impact to ordinary people’s income are underway like Stigler’s Gauge, SGR project, Port expansions and road networks to name a few.

  My fellow Tanzanian Mr.Lissu, as you may be aware in fighting corruption and bringing about real economic transformation for a developing country like Tanzania there are serious challenges, this shift will never bring smile to those who are greedy and those who want to see us as a receiving Country other than a donor Country.

  Those who believe that this positive transformation Tanzania is going through is a threat to their interests will never stop fighting to undermine the efforts of our beloved President Dr John Magufuli. It is true that corruption in most of African countries have benefited a few people, record shows how much politicians like you have benefited from minerals contracts,and other contracts when working in different parliamentary committees as well as the foreign countries.

  I would therefore advice my fellow Tanzanian Mr Lissu, that it seems he is one of the very few people in Tanzania who have a notion that, Tanzania is still under colonialism and not a free country. It is high time you realize that Tanzania is a free Country and can choose between what is democracy and what is violence, what is free speech and what is hate speech, as well as crime. We are governed by a Constitution and the rule of Law.

  Most of our people and good friends of Tanzanian appreciates what Dr Magufuli is doing, the benefits of trade can be enjoyed in a peaceful and democratic state, and democracy can be exercised in a peaceful environment. One cannot exercise true democracy where there is no peace.We are sailing in this boat together , therefore we will never allow you to drill a hole and flood our Boat Mr.Tundu Lissu.


  Eng Abdalah Kileo


  0 0   Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akishangilia ushindi wa timu ya mpira wa pete baada ya timu hiyo kuifunga timu ya pete ya Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila magoli 17-1 katika mchezo wa Bonanza uliofanyika katika  Viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu) jijini Dar es Salaam.  Wengine katika picha ni  wakurugenzi na watumishi wa hospitali hizo wakishangilia pamoja.
  ????????????????????????????????????
  Kepteni wa timu ya mpira wa miguu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila akishangilia baada ya kuifunga timu ya Muhimbili ,Upanga bao moja kwa sifuri. Muhimbili Mloganzila 1-0 Muhimbili Upanga. Wengine katika picha hii ni Wakurugenzi wa Muhimbili Upanga na Muhimbili Mloganzila.
  ????????????????????????????????????
  Mashabiki wa timu ya mpira wa miguu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakishangilia pamoja baada ya timu yao kuifunga timu ya Muhimbili Upanga bao 1-0.
  ????????????????????????????????????
  Mashabiki wa mpira wa miguu wakifuatilia mechi kati ya timu ya Muhimbili Upanga na Muhimbili-Mloganzila. 
  005
  Mechi ikiendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu) leo.
  ????????????????????????????????????
  Wachezaji wa mpira wa pete wa Muhimbili Upanga wakiifungia timu yao bao la sita katika mchezo uliofanyika Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu).  Muhimbili Upanga 17- 1 Muhimbili-Mloganzila.
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mpira wa pete uliofanyika leo kwenye viwanya vya  Jakaya Kikwete Youth Park (Kidongo Chekundu).
  008
  Baadhi ya watumishi wa Muhimbili wakifanya mazoezi ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wa mpira wa pete na mpira wa miguu.
  ????????????????????????????????????
  ????????????????????????????????????
  Wachezaji wa Muhimbili Upanga na Muhimbili-Mloganzila wakiwa katika picha ya pamoja.
  …………………………………………………………………………
  Bonanza la michezo lililoandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) limefana na kuleta ushindani mkubwa kwa timu shiriki za mpira wa pete na miguu za hospitali hiyo na hivyo timu hizo kugawana makombe.
  Bonanza hilo limehusisha timu za Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Upanga pamoja na Hospitali Taifa Muhimbili-Mloganzila ambapo katika mchezo wa mpira wa Pete Muhimbili-Upanga imeichapa Muhimbili-Mloganzila magoli 17 kwa 1.
  Katika mchezo huo timu ya Mloganzila ilionekana kuelemewa kwani walipokua wakifika langoni mwa timu pinzani walishindwa kufunga na hivyo kuwapa uhakika wa kushinda mabao mengi.
  Kwa upande wa mpira wa miguu katika kipindi cha kwanza dakika ya 14 timu ya  Muhimbili Mloganzila imeichabanga bao 1 kwa 0 timu ya Muhimbili Upanga bao lililofungwa na mshambuliaji machachari  Edger  Mtitu. Katika kipindi hicho  cha kwanza timu ya Muhimbili Mloganzila ilitawala mpira na kusababisha Muhimbili Upanga kushindwa kufurukuta uwanjani.
  Baada ya kumalizika kwa mchuano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence Museru alizungumzia umuhimu wa kuendeleza michezo mahala pa kazi ili kudumisha amani, umoja na upendo na pia watumishi kuwa na afya bora hatua ambayo italeta tija katika maeneo ya kazi.
  “Nitaendelea kuunga mkono suala la michezo na kusapoti kadiri inavyowezekana maana michezo ni afya, hivyo nawasihi watumishi wa Hospitali ya Muhimbili Upanga na Mloganzila kuendeleza michezo na mjitokeze kwa wingi kushiriki katika michezo mbalimbali,”amesema Prof. Museru.
  Kwa upande wao washiriki wa Bonanza hilo wameushukuru uongozi wa hospitali kwa kufanikisha shughuli hiyo ambayo imewaweka karibu watumishi wote wa MNH Upanga na Mloganzila.
  Bonanza la michezo la Hospitali ya Taifa Muhimbili, Upanga na Mloganzila limefanyika katika viwanja vya michezo vya Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam.

  0 0

   Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas,ameongoza kikosi maalum katika kupambana na uhalifu nchini kilichoungana na vikosi  vya jeshi la Polisi mkoa wa Njombe katika kufanya Operesheni katika mapori ya  Nundu na Tanwat mkoani Njombe kuwasaka watuhumiwa wa Mauaji ya watoto. Picha na jeshi la Polisi     
   Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa Njombe Kamishina Msaidizi Mwandamizi SACP Afande  Renata Mzinga  wameongoza kikosi maalum cha  kupambana na uhalifu nchini kilichoungana na vikosi  vya Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe katika kufanya Operesheni katika mapori ya  Nundu na Tanwat mkoani Njombe.(Picha na jeshi la Polisi) 

  Jeshi la Polisi Makao Makuu Kitengo Maalum cha Kupambana na uhalifu kikiongozwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, kimeshirikina na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kuendesha Operesheni Maalum ya kukabiliana na matukio ya mauaji ya watoto wadogo ambayo yamejitokeza mkoani humo, mpaka sasa watuhumiwa 30 wamekamatwa waliojihusisha na matukio hayo, 

  Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, amesema watuhumiwa hao ifikapo Jumatatu watakuwa wamefikishwa Mahakamani kukabiliana na tuhuma za mauaji ya watoto, Aidha Naibu Kamishna Sabas, amewataka watanzania kutoa Taarifa za wahalifu popote walipo na amewahakikishia watanzania kuwa matukio hayo yamekoma sasa 

  Aidha Naibu kamishna Sabas amesema Jeshi La Polisi halitamuonea mtu yoyote haya awe Mfanyabishara, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Dini, au Waganga wa Kienyeji watakaojihusisha na matukio ya mauaji kwa njia yoyote ile sheria itachukua mkondo wake huku akiapa kupambana na wahalifu wa mauaji yoyote yale kindakindaki


  0 0


   Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah akitoa maelekezo kwa mkuu wa Polisi wilaya ya Hai,Lwelwe Mpina mara baada ya kufanikiwa kukamata watu tisa wakiwa na Dawa za Kulevya aina ya Mirungi ikiwa ndani ya Mabegi yanayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi Daftari.
  Askari Polisi wakitoa vifurushi vya Dawa za Kulevya aina ya Mirungi iliyokuwa imehifadhiwa katika mabegi yanayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi Daftari.
  Sehemu ya Dawa za kulevya aina ay Mirungi iliyokamatwa ikiwa imehifadhiwa kwenye mabegi madogo ikisafirishwa kuelekea mkoani Arusha.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi Hamisi Issah akiangalia vifurushi vidogo vya Dawa za kulevya aina ya Mirungi iliyokamatwa Latina eneo la KIA Juction.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Hamisi Issah akionesha sehemu ya Dawa za kulevya aina ya Mirungi iliyokamatwa katika wilaya ya Hai ikisafirishwa kuelekea Arusha .
  Baadhi ya watuhumiwa wa usafirishaji wa Dawa za kulevya  wakiwa kaaika gari la Polisi tayari kuelekea Mahakamani kusomewa mashtaka yanayowakabili.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya kaskazini . 
   
  WAFANYABIASHARA na Wasafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wamekuja na mbinu nyingine mpya ya kujigeuza wanafunzi na kisha kuficha Mirungi katika mabegi madogo yanayotumiwa na wanafunzi kuhifadhi Daftari kwa lengo la kukwepa mkono wa askari Polisi.
   
  Mbinu nyingine ambazo jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro imezigundua hivi karibuni ni pamoja na kutumia magari ya Kifahari yakiwemo Toyota Land Cruser ,Toyota Alphasad,Toyota Vanguard huku mbinu nyingine zikiwa ni kufanyia mabadiliko gari aina ya Toyota Noah ili kurahisisha ubebaji wa Mirungi kwa kificho.
   
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah alisema wasafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wameendelea kubuni mbinu kila kukicha baada ya zile za awali kushtukiwa na Polisi huku akitoa onyo kwa wamiliki wa Magari ya abiria kujiingiza katika mtego wa kusafirisha dawa hizo.
   
  “Hapa kuna mizigo ambayo imekamatwa na askari wetu wakiwa barabarani ,hii ni mbinu mpya  ya usafirishaji  ,haya mabegi unayoyaoona yote ni mabegi yanayoonesha mbebaji amebeba Madaftari  anaenda shuleni ,lakini haya sio madaftari ni Mirungi ,ni mizigo iliyokamatwa kwenye mabasi tofauti tofauti”alisema Kamanda Issah. 
   
  Alisema katika tukio hilo watuhumiwa tisa  wakiwemo wanawake wawili wamekamatwa wakiwa na jumla ya kilogramu 64 baada ya sakari Polisi kupekuwa magari matatu ya Abiria yaliyokuwa yakitokea  yakiendelea na safari kutokea Moshi yakielekea Arusha.
   
  “Naona mbinu zinaendelea kubadilika ndani ya wiki mbili ,mbinu tatu tofauti,kwanza ya kujaza kwenye magari,pili ya kutoboa magari kabisa,tatu kama mwanafunzi  nyingine kama mtu anaenda hospitali amejifunga maplasta sasa hizi mbinu zitafika mpaka lini na sisi tunashukuru askari wangu wanafanya kazi vizuri”alisema Kamanda huyo wa  Polisi Kilimanjaro.
   
  Kamanda Issah amewataja wanaoshikiliwa hadi sasa kuwa ni pamoja na  Ibrahim Masuli, Godfrey Richard, Chrispin  Baltazar, Fanuel Hamad,na Jackline Mushi huku wengine wakiwa ni Lucy Petro ,Nuru Haruna,Silvesta Fabian naMinyari Miandei.
   
  Alisema kwa sasa askari polisi wameamua kupekuwa magari yote yakiwemo ya abiria huku akiwataka abiria kutoa ushirikiano kwa jeshi l a Polisi pindi wanapoona mizigo yenye mashaka ili kuwaondolea adha ya kuchelewa kufika safari zao kutokana na usumbufu watakao pata barabarani.
   
  “Tunawasihi abiria maana kuna abiria wengine wakiona askari   wanapekua gari wanakasirika,msikasirike hii ndio kazi ya kupekuwa ,vinginevyo  muwe mnatuambia ndani ya gari amepanda mtu wa ajabu na amebeba madawa ya kulevya  aina ya mirungi  hapo ndio itakuwa ni nanafuu na tutafanya kazi kwa muda mfupi li muendelee  na safari “alisema Issah.
   
  Kamanda Issah aliwataka wamiliki wa mabasi ya abiria kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi  ili kuhakikisha biashara hiy inakoma kwa kukataa kubeba abiria wenye mizigo ambayo wanatilia shaka na kwamba kwa kuendelea kuwabeba itapelekea kuwaingiza katika matatizo na vyombo vyao.
   
  “Sasa hivi sio imekuwa ni wanafunzi ambao madaftari yao ni mirungi iliyobebwa nyuma ,kwa hali kama hiyo tunawasihi  wale wote wasafirishaji wa abiria kutokea Moshi kwenda Arusha wawe makini  utawachelewesha abiria wako,upekuzi utaendelea  na ninaelekeza askari waendelee usiku iwe mchana”alisema Issah.
   
  “Kuna watu wakiona gari inapekuliwa wanatubeza ,sasa hivi tukikuona wewe unatubeza askari watakukamat,a  wanawabeza askari wanaofanya kazi yao  halafu tutakuhoji unatubeza kwa sababu gani,kwa hali kama hiyo tunaagiza askari waendelee kukamata mirungi na wasiiache”aliongeza Kamanda Issah.
   
   Kukamatwa kwa Dawa hizo  zinafanya idadi kamili ya Dawa za kulevya aina ya Mirungi zilizokamatwa katika kipindi cha wiki mbili kufikia kilogramu 564 pamoja na vyombo vya usafiri yakiwemo magari matatu na pikipiki moja.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (katikati) wakati wa Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano, kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
  Kikao hicho kimefanyika jana Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea hati ya umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa hekari 30 kwenye mji wa Serikali Dodoma kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika jana Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma.
   
  akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ali Iddi (kushoto) hati ya umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa hekari 30 kwenye mji wa Serikali Dodoma kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika jana 
   Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wa kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika jana Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Hamida Mussa Khamis akimkabidhi cheti mwanafunzi Rahma Juma Juma mmoja kati ya wanafunzi wawili waliopata daraja la kwanza Skuli ya Stone Town International.
  Mwanafunzi Asia Juma Ali (kushoto) na Nathania Sleiman wakighani utenzi kwenye sherehe ya mahafali yakuwapongeza wanafunzi wa kitado cha nne waliomaliza Stone Town International School iliopo Kilimani Mjini Zanzibar mwaka jana.
  Mkurugenzi wa Stone Town International School Bi. Jamila Gulam Hussen akisoma hutuba katika mahafali ya kidato cha nne yaliyofanyika skulini kwao Kilimani Mjini Zanzibar.
  Mjumbe wa Bodi ya Ushauri Tasisi ya Elimu Zanzibar Charles Lubega akielezea umuhimu wa elimu katika mahafali ya Stone Town International School pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kuwahutubia wahitimu wa kidato cha nne na wanafuzi wanaoendelea na masomo.
  Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Hamida Mussa Khamis akizungumza na wazazi na wanafunzi wa Stone Town International School ya Kilimani katika mahafali ya kidato cha nne ya skuli hiyo.
  Wahitimu wa Kidato cha Nne wa Stone Town International School wakiwa katika mahafali yao yaliowashirikisha pia wanafunzi wa darasa la sita yaliyofanyika skulini kwao Kilimani.Picha na Makame Mshenga.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki na waumini wengine katika Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 5 ya Makasia katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo February 10, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Mkate wa Sakramenti Takatifu toka kwa Paroko wa Parokia ya Oysterbay Padri Dkt. Alister Makubi wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 5 ya Makasia katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo February 10, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa amani na masista na waumini wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 5 ya Makasia katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo February 10, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko wa Parokia ya Oysterbay Padri Dkt. Alister Makubi baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 5 ya Makasia katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo February 10, 2019. Katikati ni mmoja wa viongozi wa kanisa hilo Dkt. Adelhelm James Meru
  0 0   Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen akizungumza na wageni waalikwa juzi jijini Dar Es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma mpya za Teknolojia ya ulinzi wa kisasa zenye kulinda watu na mali zao kutoka kampuni ya G4S Tanzania.
   Henrik Krag kutoka Zonith akiwa na askari wa kampuni ya Q4S akielezea jambo kwa wageni waalikwa
   Inj.Omar Bakar kutoka Tanzania Data Lab akiwasilisha mada kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma mpya za Teknolojia ya ulinzi wa kisasa zenye kulinda watu na mali zao kutoka kampuni ya G4S Tanzania.
   Sugandran wa Geo Tab akiwasilisha mada kwa wageni waalikwa
  Wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.

  · G4S inatoa huduma za ulinzi zinazotumia teknolojia kusaidia taasisi na watu binafsi kulinda watu na mali zao.

  Tarehe 8 Februari 2019, Dar es salaam. Wakati ambapo ni muhimu kupunguza gharama za uendeshaji, sio tu kwamba teknolojia itasaidia kufikia malengo haya lakini pia itaweza kutoa manufaa zaidi ya kuaminika na ufanisi. Kwa kuongezea zaidi matuko mengi ya matumizi ya teknolojia inayostahili imeweza kuondoa maofisa wa ulinzi katika maeneo ambayo kuna hatari ya watu kuumia.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa teknolojia mpya ya ulinzi inayotolewa na G4S, Balozi wa Denmark Mhe. Einar H. Jensen alisema kwamba uimarishaji wa usalama wa watu na mali zao katika kanda hili umekuja katika wakati muafaka kwaajili ya kukabiliana na vitisho vilivyoshuhudiwa hivi karibuni. 'Dunia inabadilika kwa kasi sana na mahitaji ya kulinda watu na rasilimali hayajawahi kuwa makubwa kama hivi sasa. Mahitaji ya usalama kwa watu wa Afrika Mashariki vile vile yanazidi kuongezeka. Si muda mrefu tulikabiliana na uvamizi wa kikatili wa magaidi katika hoteli nchini Kenya, tunapaswa kuwa tayari kwa mashambulizi ya aina hiyo katika siku zijazo.

  Akitangaza uzinduzi wa bidhaa za kisasa mwaka 2019, Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa G4S Secure Solutions Tanzania, Andrew Lauwo amesema 'Mfumo wa Ulinzi wa ishara ya kengele ya video (A video alarm security system) (Videofied) iliyotengenezwa Ufaransa yenye uwezo wa kuhisi mtu anapoingia na kisha kutuma video ya haraka kwenye control room ya G4S na kwenye simu yako pale mtu anapoingia katika sehemu husika ni bidhaa nyingine iliyoko katika ofa: Mfumo huu unatumia betri na hauna waya na unaweza kufungwa nje au ndani. Mfumo wa VIDEOFIED unatumika zaidi kulinda mali na pia unatumika katika mazingira ya nje kama vile sehemu za kuhifadhia boti, maeneo ya burudani ya nje, katika njia na sehemu nyingine ambako nishati ya umeme hakuna.'

  'At the Gate' (Katika Mageti) ni mfumo wa kudhibiti waingiaji ambao unaruhusu ufuatiliaji wa nani anaingia na kutoka katika eneo lako kwa kuskani magari na taarifa za leseni za madereva wanapoingia na kutoka kupitia kifaa cha Android. Kifaa hiki kinafanyakazi kwa kutumia mtandao wa simu au kuunganishwa na Wi-Fi na kutoa vipengele mbalimbali vinavyokutaarifu mgeni anapofika getini, picha nyingi za magari na walioko ndani, taarifa za laptop, silaha,simu za smart, tablets nk. zinazoingia na kutoka katika eneo nk.'. aliongeza.

  Akitolea maoni kuhusu mfumo wa kufuatilia magari (Vehicle Tracking Management System) alisema, ‘Geotab kutoka Canada: ni mfumo wa kufuatilia magari na kufuatilia tabia za dereva ambao pia unatoa kifaa cha ufahamu wa dereva (Driver Awareness tool) kinachobadilisha jinsi mafunzo ya mereva yanavyofanyika wakati wa kuendesha kwa kutoa maelekezo ya sauti ya hapo kwa hapo kwa dereva. Zaidi ya eneo halisi gari liliko, taarifa za kasi ya gari idadi ya tripu na umbali ambao tayari ameshasafiri, utendaji wa dereva kama vile kufunga breki kwa haraka, kukata kona na takwimu za utulivu wa kupita kiasi pia zinapatikana. Mfumo huu umetengenezwa kusimamia na kufuatilia utendaji wa gari, tabia za dereva na kuboresha mifumo ya usalama.'

  Vilevile alisema kwamba, ‘The Sentinel Perimeter Protection kutoka Afrika ya Kusini ni mfumo wa masafa marefu wa kutambua uvunjaji na kuzuia ambao unatoa ishara ya kengele unapokuwa umekiukwa na kutuma video za tukio kwa kutumia Wi-Fi wakati pia ikiwa inatuma ishara ya tahadhari kwenye Control room yetu na katika simu yako ya mkononi masaa 24/7 Ina uwezo wa kusimamia eneo la mita 150 na vipengele vya ziada vinaweza kuongezwa kwenye mfumo huu kutoa ulinzi wa asilimia 100% katika eneo husika.

  Akiongea kuhusu mfumo wa ulinzi kwa kutimia video ulioko katika ofa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa ZONITH, Kristian H Stiesmark amesema kwamba 'Ishara ya Kengele ya Hofu Binafsi (Personal Panic Alarms) iliyoundwa na ZONITH, kampuni ya teknolijia ya kiwango cha juu ya watu wa Denmark inatoa kifaa cha kutolea ishara ya kengele ya hofu binafsi cha kufunga mahali na cha kutembea nacho ambacho kinamruhusu mtumiaji kuita msaada kutoka katika kikosi cha kuitikia matukio cha G4S panapotokea vitisho vya kiusalama au huduma ya kimatibabu au dharura ya moto.
   
   Zonith inatoa teknolojia ya kuchagua inayotumia Bluetooth ambayo inaruhusu ishara ya kengele na sehemu ulipo kutumwa kutokea sehemu yoyote ambako mtandao wa GSM unapatikana.'

  0 0  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akipokea muhtasari wa mafunzo ya Mfumo wa Ukusanyaji Maduhuri ya Serikali (GePG) kutoka kwa mhasibu Bi. Sophia Lukas mara baada ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam na kuendeshwa na wakufunzi kutoka Wizara ya Fedha na mipango (Hazina).
  ????????????????????????????????????
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akizungumza na wahasibu wa wakala huo kutoka mikoa mbalimbali mara baada ya kufunga mafunzo ya Mfumo wa Ukusanyaji Maduhuri ya Serikali (GePG) yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Wizara ya Fedha na mipango (Hazina). Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam.
  ????????????????????????????????????
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akizungumza na wahasibu (hawapo pichani) wakati akifunga mafunzo ya Mfumo wa Ukusanyaji Maduhuri ya Serikali (GePG) yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Wizara ya Fedha na mipango (Hazina). Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha GePG Bazil Baligumya, Mhandisi Sylvester Simfukwe, Mhandisi Lukombe King’ombe na CPA Hans Lyimo.


  ……………………………………………………………………………………

  NA ALFRED MGWENO- TEMESA

  Wahasibu na mameneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) mwishoni mwa wiki hii wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Ukusanyaji Maduhuri ya Serikali, mafunzo hayo yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Hazina kitengo cha (GePG) yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam na yamelenga kuwapatia uelewa mpana wa matumizi ya mfumo huo na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza kwenye utekelezaji wa mfumo huo.

  Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle alisema mfumo huo utausaidia sana Wakala kwenye utendaji kazi wake kwani utapunguza gharama za uendeshaji kwakuwa hauna tozo lolote na wakati huo huo mtumiaji atakuwa na uwezo wa kupata taarifa wakati wowote akizihitaji.

  ‘’Ninaamini mfumo huu utatusaidia kutoa taarifa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya taasisi yetu hivyo basi tuutumie kama kitendea kazi chetu muhimu katika kuboresha na kuongeza tija kwa maslahi mapana ya Wakala wetu, wizara na taifa kwa ujumla’’, alisema Mhandisi Maselle.

  Naye mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Hazina kitengo cha (GePG) Ndugu Bazil Baligumya alisema mfumo huo utaisaidia TEMESA kuhakiki kwa urahisi malipo yote yatakayokuwa yanafanywa na wateja wake na utarahisisha upatikanaji wa taarifa za fedha zinazohitajika kutoka katika vituo, ‘’tumewafundisha jinsi ya kuandaa ankara za madai, kuangalia na kuhakiki malipo yaliyokwisha fanywa na wateja, namna ya kutambua na kufanya usuluhisho kwa kutumia taarifa itokayo katika mfumo wa (GePG) pamoja na taarifa ya makusanyo kutoka benki na jinsi mfumo unavyoweza kuzalisha taarifa za wateja’’, aliongeza mkufunzi huyo.

  Mfumo huo wa ukusanyaji wa maduhuri ya serikali unatambua na kukusanya fedha zote za Umma na kuziweka kwenye akaunti maalumu ya serikali iliyopo Benki kuu (BOT) na umetokana na marekebisho ya sheria ya mwaka (2017 sura ya 348 kifungu cha 6 cha sheria ya fedha kifungu kidogo cha 6a i na ii) inayoelekeza fedha zote za umma kukusanywa kwa mfumo huo. Mfumo wa (GePG) ulianza kwa kutumiwa na jeshi la polisi nchini hususani askari wa barabarani pamoja na Wakala wa Misitu ambapo ulionyesha mafanikio makubwa na hivyo kupata baraka za kuenezwa zaidi katika taasisi na asasi zaidi za serikali ambapo hadi kufikia sasa wadau zaidi ya 500 wameshaunganishwa kwenye mfumo huo.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango(Mb) akifafanua hoja wakati wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali, uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus L. Kilangi, Bungeni Jijini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani(Mb) wakijadili jambo kabla ya kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali, Bungeni Jijini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akijadiliana jambo na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb), bungeni Jijini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango(Mb) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus L. Kilangi wakijadili jambo baada ya kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali, bungeni Jijini Dodoma.


  Na. Josephine Majura, WFM, Dodoma 

  Bunge limepitisha Muswada wa Sheria wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba mbili ya Mwaka 2019 ambao umelenga kutatua changamoto za za kodi ikiwemokodi ya Majengo, madini na Kodi uya Ongezeko la Thamani (VAT). 

  Muswada huo uliopelekwa Bungeni kwa Hati ya Dharura ulijadiliwa na kupitishwa ambapo Wabunge mbalimbali walipata fursa ya kutoa maoni yao. 

  Akizungumza wakati wa kuwasilisha Muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Prof. Adelardus Kilangi, alisema kuwa marekebisho hayo yameondoa kodi ya zuio (withholding tax) kutoka 5% hadi asilimia sifuri kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote kwa wachimbaji wadogo ili kuwahamasisha wachimbaji hao kuuza madini katika masoko ya madini. 

  Alisema marekebisho hayo yanalenga kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali na kuhakikisha mapato yanayotokana na biashara ya madini yanakusanywa ipasavyo. 

  Aliongeza kuwa Muswada huo umependekeza kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa wachimbaji wadogo wa madini watakaouza madini yao katika masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini. 

  Aidha, Prof. Kilangi alibainisha kuwa Muswada huo pia umependekeza kila kiwanja kitozwe Kodi ya Majengo badala ya kila jengo lililopo ndani ya kiwanja husika kwa maeneo ya Halmashauri za Wilaya. 

  Sheria zilizopitishwa ni pamoja nma Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya 147, Sheria ya Kodi ya Mapato Sura ya 332, Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ya Utozaji wa Kodi ya Majengo Sura ya 289, Sheria ya Madini Sura ya 123 na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura ya 148. 

  “Madhumuni ya marekebisho ya Sheria hizo pamoja na mambo mengine ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuondoa changamoto kwa wachimbaji wadogo wa madini, wakulima wa zabibu ndani ya nchi na viwanda vinavyotumia zabibu hiyo katika uzalishaji pamoja na kuweka viwango mfuto (fixed rate) vya kodi ya majengo.” Alisema Prof. Kilangi. 

  Alisema kuwa Serikali imeona upo umuhimu wa kuwasilisha Muswada huu kwa haraka kupitia Hati ya Dharura ili kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kupunguza utoroshwaji wa madini nje ya nchi unaofanywa na wachimbaji wadogo ambao wanakwepa kodi. 

older | 1 | .... | 1799 | 1800 | (Page 1801) | 1802 | 1803 | .... | 1897 | newer