Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1800 | 1801 | (Page 1802) | 1803 | 1804 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na ANDREW CHALE, ZANZIBAR

  KUNDI la wanamuziki wanaokuzwa la Mkubwa na Wanawe usiku wa 7 Februari 2019 limeweza kukonga nyoyo za watu waliojitokeza kushuhudia tamasha la 16 la Kimataifa la Sauti za Busara, kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja.

  Kundi hilo limeweza kuonesha umahri wao wa kuimba na kucheza jukwaani huku wakiendana sambamba na mapigo na ala za muziki wa bendi ‘live' iliamsha shangwe za mara kwa mara kwa mashabiki waliofurika Ngome Kongwe.

  Vijana hao wa waliweza kuimba nyimbo zaidi ya tano (5) ikiwemo ya Stata ukiimbwa na mwanadada Catrima Wegesa huku nyimbo zingine zikiimbwa na Abdala Mustapha 'Kisamaki' huku kijana mdogo kabisa wa kundi hilo Abdul Kadry 'Dogo Kadry' akiwa kivutio kila alipopanda kuimba kwenye jukwaa hilo la Busara.

  Dogo Kadry aliweza kuimba nyimbo zaidi ya mbili ikiwemo ule aliyourudua wimbo wa Asu ulioimbwa na Abdul Misambano. pia waliweza kuimba nyimbo za wasanii waliowahi kupitia kundi hilo zikiwemo za ‘Mototo wa udongo’ na ‘Watakubali'. Kundi hilo lililo chini ya muasisi wake, Said Fella ‘Mkubwa Fella’ ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kilungule ya wilayani Temeke, Dar es Salaam hadi sasa lina vijana wanaofanya kazi za Sanaa za Muziki zaidi ya 100.

  Miongoni wa wasanii waliowahi kuwa kwenye kundi hilo na kwa sasa wanajitegemea ni pamoja na Dogo Aslay, Mboso na wengine wengineo.Miaka miaka kadhaa iliyopita wasanii hao Dogo Aslay na Mboso waliwahi kushiriki tamasha hilo huku wakiwa vijana wenye umri mdogo ambapo walikuwa kivutio kama ilivyo kwa sasa kwa msanii mpya wa kundi hilo Dogo Kadry ambaye kwenye shoo hiyo aliweza kuonesha uwezo wake licha ya kuwa na umri wa chini ya miaka 15.

  Mpaka sasa Mkubwa na Wanawake Crew wameshatoa nyimbo mbalimbali zikiwemo : Tofauti, 2012; Nawashusha Down, 2013; Fanya Yako, 2014; Unanitusi, 2015; Sitakitararira, 2016; Naelewa, 2016; Yerere, 2016Lakini pia baadae waliweza kutoa nyimbo kupitia bendi ya Yamoto ambapo napo walitoa nyimbo mbalimbali .
   Kundi la Mkubwa na Wanawe wakishambulia jukwaa katika onesho lao la jana usiku 7 Februari 2019, kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar
  Mmoja wa Wasanii kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe, Abdala Mustapha 'Kisamaki' akionesha uwezo wa kuimba na kucheza jukwaani wakati wa tamasha hilo la Sauti za Busara, 7 Februari 2019
   Msanii mwenye umri mdogo katika kundi hilo la Mkubwa na Wanawe, Abdul Kadry 'Dogo Kadry' akiimba kwa hisia nyimbo ya Asu.
   Dogo Kadri akifanya mahojiano baada ya kumalizika kwa  shoo yao hiyo
  shangwe zilizokuwa zikiendelea wakati wa shoo hiyo

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki, katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Adis Ababa Ethiopia Februari 10, 2019, (katikati) ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Augustine Mahiga, Waziri Mkuu yupo nchini Ethiopia kumwakilisha Rais Magufuli kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika (AU). 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika (AU) kumwakilisha Rais Magufuli, mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Adis Ababa Ethiopia Februari 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa kampuni ya Liyan African iliyowekeza nchini Tanzania Hakim El- Shwehdi, kwenye ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Adis Ababa Ethiopia Februari 10, 2019, Waziri Mkuu yupo nchini Ethiopia kumwakilisha Rais Magufuli kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika (AU), katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Augustine Mahiga.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Augustine Mahiga, ndani ya ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Adis Ababa Ethiopia Februari 10, 2019, Waziri Mkuu yupo nchini Ethiopia kumwakilisha Rais Magufuli kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika (AU)

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (mwenye tisheti nyeupe) akizungumza na mmoja ya wasimamizi wa Kichina ambaye ndiyo wanaokarabati reli ya kati kupitia kampuni ya CCECC wakati anapita kuelekea katika ukaguzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge mwishoni mwa wiki hii. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (wa kwanza kulia) akizungumza na msimamizi wa Kichina ambao ni wakarabati wa reli ya kati. Ambapo hapa Msimamizi huyo alikataa kuongea nao maana hajui kingereza. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (mwenye tisheti nyeupe) akipiga simu kwa bosi wake na huyo msimamizi wa kichina ili kuweza kuwaachia njia baada ya huyo mchina kukataa kwa madai ukarabati unaendelea.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (mwenye tisheti nyeupe) akizungumza na wafanyakazi wa Kitanzania ambao wamepewa ajira na kampuni ya CCECC jinsi wanavyofanyakazi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (wa mbele) akiendelea kukagua ukarabati wa reli ya kati kupitia kampuni ya CCECC wakati anapita kuelekea katika ukaguzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge mwishoni mwa wiki hii. 
  Shughuli ya ukarabati wa reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma. 
  Msimamizi wa Kichina wa kampuni ya CCECC akiendelea kusimamia kazi.
   Baada ya kukaa kwa muda wa takribani saa 1:30 ndiyo ilipoamuliwa kuweka magogo ili treni ipite na waendelee na safari. 
  Treni ikipita huku ikiwa na usimamizi wa hali ya juu. 

  Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amechukizwa na utendaji kazi wa kampuni ya Kichina ya CCECC inayohusika na ukaratati wa reli ya kati. 

  Akizungumza mara baada ya kutembelea reli hiyo wakati akipita kukagua mradi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge, Mkurugenzi Masanja Kadogosa amechukizwa na jinsi wafanyakazi wa Kichina wanavyowabagua Watanzania wanaofanya nao kazi. "Leo nimepita kama bahati mbaya na kukutana na haya, kiukweli sijafurahishwa na utendaji kazi wao haiwezekani watu waliopelekwa site hawajui Kingereza sasa wanawezaje kuwasimamia hawa waswahili ambao nao hawajui kichina???," amesema. 

  Ameongeza kuwa Kampuni iliyopewa tenda ya kukarabati reli ya Kati ya CCECC wamekuwa wakipeleka wasimamizi wasiojua lugha ya Kingereza jambo linalozorotesha utendaji kazi katika ukarabati huo. Hatua hiyo ilikuja baada ya Mkurugenzi Mtendaji kupita na wasanii na kukuta wanakarabati wakati walipewa taarifa kuwa watapita na wasanii wakielekea mjini Morogoro kukagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge. 

  Katika hali iliyomchukiza Mkurugenzi Mtendaji Kadogosa ni jinsi wafanyakazi hao wa kichina walivyomdharau kwa kukataa kuongea nae eti hawamfahamu licha ya yeye kujitambulisha kwao hawakujali. "Hivi nyie wafanyakazi kiongozi weni ni nani??? nimekuja hapa nikiwa ni Mtendaji Mkuu wa TRC lakini mnavyonijibu kama hamna kiongozi basi niwafukuze wote hata site,' amesema. 

  Ndipo Mtendaji Mkuu alipochukua hatua ya kupiga simu kwa viongozi wao na kuamuru waende ofisini kwake Jumatatu Februari 11, 2019 wakajieleze kwanini wanakuwa na dharau hasa kwa viongozi. 'Binafsi sijafurahidhwa na majibu ya hawa Wachina au wanatuona sisi ngozi nyeusi hatuna thamani kwao??? Niwaombe nyie viongozi wa TRC mlio pamoja na mimi... nawataka Jumatatu mje na hawa mabwana ofisini kwangu," amesema.

   Hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji huyo amewaamuru wafanyakazi wote wanaokarabati reli chini ya kampuni ya kichina ya CCECC kuwa wawazi kusema kero zao ili zitatuliwe. 'Nimeambiwa kuwa wachina wamekuwa wakiwapiga na kuwatukana ila nyie mmekaa kimya hili siwezi livumilia katika shirika langu, nataka wote muwe na usawa,' Amesema. Wafanyakazi wa Kampuni ya Kichina ya CCECC wamekuwa ni wakaidi na hawajui lugha ya kingereza jambo linalozorotesha utendaji kwa vile hawaelewani na vijana wa Kitanzania.

  0 0

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Segerea Mh Bonnah Kaluwa amekutana na Wananchi wake na kufanya Mkutano uliozungumzia changamoto mbalimbali na kutengeneza mikakati ya kuhakikisha jimbo hilo linapiga hatua za kimaendeleo.

  Kaluwa amefanya mkutano huo jana Jumapili februari 10/2019 na Wananchi wa kata ya Vingunguti ,viwanja vya relini ambapo mambo mbalimbali ya maendeleo yamejadiliwa huku wananchi wakikishirikishwa kueleza mawazo yao.

  Akizungumza kwenye mkutano huo,Kaluwa alisema kuwa moja kati ya mambo ambayo aliyazungumzia ni suala la barabara ya Vingunguti ambayo imekuwa kero kwa wananchi wake,Kalua amewaeleza wananchi ambavyo amekuwa akifuatilia kuhusu ujenzi wa bara bara hiyo,akawafafanulia kuwa ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

  " Kabla ya kuanza ujenzi wa barabara nawaomba Wananchi waliojenga juu ya mitaro kupisha mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa ujenzi huo",aliwathahadharisha Wananchi hao. 

  Alisema pamoja na mambo mengine pia lilijadiliwa suala la Afya,ambapo ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuelekeza kiasi cha fedha takribani bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya jimboni Segerea.

  "Ndugu wanannchi wa jimbo la Segerea naamini tunakwenda vizuri na tuko pamoja,kiukweli namshukuru sana Rais wetu Dkt Magufuli,ambaye amekuwa akihakikisha usiku na mchana nchi yetu inapiga hatua za kimaendeleo,hivyo fedha tulizopewa nna hakika sekta ya afya jimboni kwetu itaimarika maradufu" alisema Kaluwa.

  Katika Mkutano wake,Kaluwa aliambatana na Naibu Meya wa Manispaaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti Mh Omari Kumbilamoto.
  Mbunge wa jimbo la Segerea,Mh Bonnah Kaluwa akimuelekeza jambo mmoja wa wananchi wake  aliefika kumsikiliza kwenye mkutano wake.

   Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao Mh Bonnah Kaluwa (hayupo pichani).
   Mh.Bonnah Kaluwa akiteta jambo na baadhi ya wananchi wake 
   Mmoja wa akina mama akichangia jambo kwenye mkutano huo wa kuhakikisha jimbo la Segerea linapiga hatua kimaendeleo 
   Mbunge wa jimbo la Segerea,Mh Bonnah Kaluwa akizungumza na wananchi wake  .

  0 0

  Na  Ripota Wetu Njombe.

  Mtoto Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema Halmashauri ya Mji wa Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo amefariki dunia Februari 09 akiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya alipokwenda kuangaliwa maendeleo ya hali yake.

  Mtoto huyo aliokotwa barabarani jirani na porini akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa koromeo Desemba23 mwaka Jana majira ya saa 4 asubuhi mtaa wa mji mwema.

  Akizungumza katika mazishi ya mtoto huyo jana katika kijiji cha Ngalanga mjini Njombe, mjomba wa marehemu Gisbeth Mlelwa,alisema marehemu alijeruhiwa na watu wasiojulikana na kupelekwa Hospital ya Mkoa Kibena na kisha kupewa rufaa kwenda Mbeya.

  "Marehemu alilazwa na kupatiwa matibabu na baadae Januari 19 mwaka huu aliruhusiwa,na Februari 8 alirudi tena Mbeya kuonana na daktari ambapo Febuari 9 alifariki dunia"alisema Mlelwa.

  Akizungumzia tukio hilo lililotokea Desemba 23 mwaka Jana Mwenyekiti wa mtaa wa mji mwema Alanus Mwalongo alisema alipata taarifa kuwa kuna mtoto kachinjwa kutoka kwa Balozi wake.

  "Alinipigia simu nikiwa dukani kwangu kwamba mwenyekiti kuna tukio limetokea hapa kanisa la Aglikan kuna mtoto kachinjwa nikawaambia wamlete mje nae huku na walipomleta na mtoto bahati nzuri kuna kijana mmoja alikuwa anapita maeneo akawa amemuona mtoto anatokea porini na kuja barabarani ndiye aliyetoa taarifa"alisema Mwalongo.

  Alisema baada ya kumuona mtoto akiwa amekatwa koromeo walimchukua na kumpeleka Hospital ya Kibena ambapo baadae alipata rufaa kwenda mbeya.Mwalongo alisema kwa kishirikiana na Jeshi la Polisi walienda hadi katikati ya msitu alipotokea mtoto na kuliona eneo alilochinjiwa.

  "Majira kama ya saa 10 jioni Polisi walinipigia kuwa wanakuja kuona eneo aliloonekana mtoto tuliondoka pale tukaanza kutoka na ule msitu ambao ni viwanja vya Mekson tulipokua tunakwenda kule kijana alipoelekeza tulipokua katikati tukakuta kweli yule mtoto alipolazwa na kufanyiwa unyama ule tukakuta hapa wameweka ndala zake,sweta hapa suruali walimvua nguo zote na barabarani alikutwa uchi"alisema Mwalongo.

  Mmoja wa mashuhuda wa tukio la mtoto huyo Jeni Chanda alisema alimuona mtoto akiwa na kijana akiwa amechinjwa na alipomuuliza alimwambia alimuona anatokea porini akiwa uchi na hivyo alimfunika.

  "Mimi nilikua napita ndio nikamuona akiwa na kijana mmoja kutoka na hali aliyokuwa nayo nikachukua nguo zangu nikamfunika ili kumpeleka hospitality"alisema Jeni.Akitoa Salamu za Wizara ya Afya, Maendeelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizarani humo Bi. Mwanaisha Moyo amesema kuwa Wizara inatoa pole kwa familia hiyo na kutoa wito kwa wananchi wa Njombe kuhakikisha wanamlinda mtoto asipatwe na majanga kama hayo.

  “Tumesikitishwa na tukio hilo na matukio yote yaliyotokea mkoani Njombe wazazi tuwalinde watoto wetu” alisema.Mpaka sasa vifo vya watoto wadogo kutekwa na kukutwa wakiwa wamechinjwa vimefika nane.
    Ndugu wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake akitengeneza tuta la kaburi mara baada ya mazishi ya mtoto huyo.
   Wanachi wa Kijiji cha Ngalanga wakiwa katika huzuni kubwa mara baada ya kutoka kuuzika  mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake.
   Wanachi wa Kijiji cha Ngalanga wakizika mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake.    Katibu Tawala wa Wilaya ya Njombe Bw. Emmanuel George akiwaongoza wananchi wa kijiji cha Ngalanga kubeba jeneza liliokuwa na mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake.
   Ndugu wakiuaga mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake. 
   Wanachi wa Kijiji cha Ngalanga wakiwa wamebeba  kwenda kuuzika mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake.

  0 0


   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania Mhe. Mhe.Gullam Hafeez Mukadam akiwa na Katibu Mkuu wa ALAT Abdallah S. Ngodu wakielezea kuhusu Tuzo za Meya.

  Mratibu wa Mradi wa Tuzo za Meya Wilman Ndile(kulia) akizungumza namna Tuzo za Meya zitakavyoshindanishwa kwa Halmashauri zote Tanzania. 
   
  Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu ALAT Taifa Abdallah S. Ngodu, Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe. Gullam Hafeez Mukadam, Makamu Mwenyekiti Stephene Mhapa akifuatiwa na Diwani wa Kata ya Maboga Iringa Dc Mhe Veny Muyinga wakati wa utambulisho wa Tuzo ya Meya kwa mwaka 2019.

  ……………………………………………………………………………….
   
  Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
  Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) imehuisha Tuzo ya Meya na kwa mara nyingine tena zitafanyika kuanzia Mwaka huu 2019, ambapo Halmashauri zote nchini zitashindanishwa kupata halmashauri moja katika kila kipengele na hatimaye kupatikana Halmauri yenye kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

  Akizungumza jijini hapa, Mratibu wa Tuzo ya Meya toka ALAT, Wilman Ndile alisema uzinduzi wa tuzo hiyo unatarajia kufanyika Juni mwaka huu katika jiji la Mwanza.

  Alisema tuzo hiyo inalenga kuibua ari na ushindani katika kuwahudumia wananchi na zaidi kuwafanya viongozi na watendaji wa Halmashauri zote kujituma na kubuni miradi itakayowaongezea mapato huku wakimuwezesha mwananchi kutumia njia bora kujiletea maendeleo..

  Ndile alisema mchakato wa uteuzi katika mashindano utahusisha umma wa watanzania ambao watatuma ujumbe mfupi kuchagua halmashauri bora, na kuongeza kwamba majaji watatembelea halmashauri husika kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho wa kuchagua manispaa bora.

  Ndile aliongeza kuwa maombi ya kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho yatahusisha ujazaji wa fomu ambazo kwa wakati huu fomu hizo ni rafiki na unaweza kuzijaza hata kwa njia ya mtandaoni na si zile za kuandika kwa mkono kama ilivyokua hapo awali hivyo halmashauri zote zitajulishwa na kutumiwa fomu hizo kwa njia ya posta lakini pia kwa barua pepe na wao watachagua njia rahisi kwao katika ujazaji wa fomu hizo.

  “Baadhi vipengele ambavyo vitashindwanishwa ni kama vile Halmashauri iliyofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, Halmashauri iliyoleta uvumbuzi na teknolojia katika utoaji wa huduma pamoja na Halmashauri iliyotekeleza miradi kwa ubora unaotakiwa” alisema Ndile.

  Vipengele vingine ni pamoja na Halmashauri iliyotoa mikopo kwa wanawake na vijana kwa mujibu ya mapato yao, Halmashauri iliyowajengewa wananchi uwezo wa kujikwamua kiuchumi, na Halmashauri inayofanya vizuri katika Utawala bora.

  Tuzo hizi zilzoanzishwa Mwaka 2015 zimejikita katika kutunza utendaji kazi bora na jitihada zisizo za kawaida, ugunduzi, moyo wa kujitolea na utayari unaozidi kiwango cha kawaida kinachotarajiwa kwenye kazi za halmashauri

  0 0


   Si wengine ni hile bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni ,inayoongozwa na mwanamuziki Kamanda Ras Makunja wenye makao yao nchini Ujerumani,bendi hiyo iliyojizolea umarufu kila kona barani ulaya na kufanikiwa kuteka washabiki kwa kutumia muziki wao wa dansi wa bongo.

  Ngoma Africa band ukipenda waite FFU ughaibuni au viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" mara hii wamepakua CD yao "Awamu Ya Tano Uwanjani" yenye nyimbo
  mbili za "Amkeni Kumekucha" na "Awamu ya Tano Sasa Kazi" nyimbo hizo ni utunzi na uimbaji wake Kamanda Ras Makunja akimshirikisha Chris-B Bakotesa ambaye pia ni solo gitaa na kundi zima la FFU wa Ngoma Africa band wakisindikiza kwa mdundo mzima wa Hapa Kazi Kumpigia Saluti na kumuunga mkono Rais Magufuli

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama wakati akiwasili katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar, kuhudhuria hafla ya chakula cha mchana alichowaandalia Vijana walishoriki Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar, kulia Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maul;id na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na kushoto Kiongozi wa Vijana wa HJalaiki Ndg. Ali Mohammed Bakari.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kulia Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe. Zuberi Ali Maulid na kushoto Kiongozi wa Vijana wa Walioshiri Halaiki za Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Ndg. Ali,Mohammed Bakari, wakiwa wamesimama wakipiga makofi baada ya kuwasili mgeni rasmin Rais wa Zanzibar, kujumuika na Vijana katika chakula maalum alichowaandalia katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, alipowasili katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni kuhudhuria hafla ya chakula alichowaandalia Vijana Walioshiriki Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika Kisiwani Pemba.
  VIJANA Walioshiriki Halaiki ya Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba, wakipiga makofi baada ya kuwasili kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar,(Picha na Ikulu)
  VIJANA Waliuoshiriki katika Halaiki ya kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba, wakijumuika katika chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  KIONGOZI wa Halaiki Ndg. Ali Mohammed Bakari, akitowa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa hafla ya chakula maalumu kilichoandaliwa kwa ajili yao katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar,kwa Vijana walioshiriki Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa meza kuu kulia Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe. Zuberi Ali Maulid, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma na kushoto Kiongozi wa Vijana wa Halaiki Ndg Ali Mohammed Bakari, wakijumuika na Vijana wakiimba “Wimbo wa Sisi Sote Tumegomboka” wakati wa hafla hiyo.

  VIJANA Walioshiriki Halaiki ya Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya wakishiriki katika kuimba “Wimbo wa Sisi Sote Tumegombaka” wakati wa hafla hiyo ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, zilizofanyika katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  /WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu, akizungumza na kutowa shukrani za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kwa Vijana walioshirki katika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  VIJANA Walioshiriki Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika kisiwani Pemba mwezi Januari 2019, wakifuatilia hafla hiyo ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  0 0

   
  Kocha Mkuu wa timu ya KMC ya Manispaa ya Kinondoni, Etiene Ndayiragije akiwa pamoja na Mchezaji wa timu ya Alliance FC yenye maskani yake jijini Mwanza Tanzania, Dickson Ambundo.
  Kocha Mkuu wa timu ya KMC ya Manispaa ya Kinondoni, Etiene Ndayiragije, akionyesha furaha baada kupokea tuzo ya Bikosports Tanzania, kufuatia kuwa kocha kocha bora wa mwezi Januari, ambapo Kampuni ya BikoSports waendeshaji wa mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani ndio wadhamini wa tuzo hiyo waliobarikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Picha na Mpigapicha Wetu.
  Mchezaji wa timu ya Alliance FC yenye maskani yake jijini Mwanza Tanzania, Dickson Ambundo, akiwa mwenye shangwe nyingi baada ya kupokea tuzo ya mchezaji bora wa mwezi January kutoka kwa Msemaji wa Bikosports, Geofrey Lea, waendeshaji wa mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani ambao ndio wadhamini wa tuzo hiyo waliobarikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

  WAENDESHAJI wa mchezo wa kubashiri matokeo wa Bikosports, jana wamewakabidhi tuzo zao,  Etiene Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya KMC ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na mchezaji wa Alliance FC ya jijini Mwanza, Dickson Ambundo, baada ya kuibuka kocha bora na mchezaji bora wa mwezi January.

  Makabidhiano ya tuzo hizo yalifanyika Makao Makuu ya Bikosports jijini Dar es Salaam, huku tuzo hizo zikiwa na lengo mahususi la kuongeza ari katika harakati za kukuza na kuendesha mpira wa miguu nchini Tanzania.

  Akizungumzia tuzo hiyo, Kocha wa KMC, Etiene Ndayiragije, aliwashukuru Bikosports kwa kuamua kuingia kwenye tuzo hizo akiamini kuwa kwa pamoja zitafanikisha sekta ya mpira wa miguu kupiga hatua kubwa.

  "Nawashukuru walioniona kwamba nastahili kuwa kocha bora wa mwezi January, huku tuzo hii nikiamini nimeipata kwa sababu ya sapoti kubwa ninayoipata kutoka kwa wachezaji wangu wote pamja na uongozi wangu wa KMC," Alisema Ndayiragije.

  Naye Ambundo aliyeibuka kwenye Mchezaji Bora wa mwezi January, alisema kwa kupata tuzo ya Bikosports anaamini ataongeza bidii kubwa katika safari yake ya mpira wa miguu, jambo ambalo limechangiwa na nguvu kubwa anayoiweka katika timu yao ya Alliance yenye ndoto kubwa ya kufanya vizuri.

  "Nadhani nimestahili kabisa kuitwaa tuzo hii na ninaamini kuwa naweza kuipata tena kwa sababu lengo langu ni kucheza mpira mzuri na kuisaidia timu yangu ya Alliance, hivyo ninachofanya ni kuongeza nguvu katika kumsikiliza mwalimu wangu, kuishi vizuri na wachezaji wenzangu ili wote tufikie malengo yetu," Alisema Ambundo.

  Akizungumzia tuzo hiyo, Msemaji wa Bikosports, Geofrey Lea alisema kuanzisha tuzo hiyo ni sehemu ya kuhakikisha kwamba mpira unakuwa kwa kiasi kikubwa, huku wakiomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau wa mpira wa miguu wakiwamo wanaobashiri matokeo kwa kupitia kampuni yao ya Bikosports.
  "Hii ni safari nzuri ya kukuza mpira wa miguu hivyo wadau wote kwa pamoja tunaomba ushirikiano wao, ambapo katika nyanja ya ubashiri wa matokeo, 

  Bikosports ndio Kampuni inayotoa zawadi kwa haraka huku jamvi lao likiwa ni rahisi kushinda kuliko michezo yoyote Tanzania, ambapo namba ya Kampuni ni 101010, huku mchezaji akiweza kubashiri kwa simu ndogo kwa namba *149*89# au wanaobashiri kwa mtandao https://www.bikosports.co.tz/ ambao ni rahisi kucheza na kushinda pia," Alisema Jeff Lea.

  Kuanzishwa kwa tuzo ya Bikosports kwa kocha bora na mchezaji bora ni sehemu muhimu ya kuhakikisha kwamba wachezaji na makocha wao wanaongeza bidii kubwa katika kuhakikisha kwamba wanapata maendeleo makubwa ndani ya uwanja, ambapo mbali na tuzo hizo, pia huambatana na Sh Milioni moja.
  mwisho

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo chake cha Huduma kwa wateja wakubwa wameshiriki kampeni maalum yakusaidi jamii inayojulikana kama Aitel Tunakujali kwa kuandaa hafla maalum ya Chai ya asubuhi (breakfast) iliyowakutanisha na wateja wao wakubwa kwa lengo la kukusanya fedha ili kuwasaidia watoto zaidi ya 100 ambao wazazi wao wameshindwa kumudu gharama za kuwalipia huduma za afya.

  Airtel Tunakujali ni programu maalum ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo uchangia sehemu ya kipato chao kwa ajili ya huduma za kijamii na hasa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

  Akiongea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja wakubwa Boniface Mbwambo alisema kuwa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wakubwa na makampuni wameamua kuja pamoja na kukusanya fedha hizo ambazo zitaelekezwa kwenye ksaidia kufanikisha kuwapa bima afya kwa watoto 100 hapa nchini. 
   
  ‘Kama unavyoona hapa leo hawa wote ni wafanyakazi wa Airtel ambao tumeungana na baadhi ya wateja wetu ambapo tumeamua kuja pamoja na kukusanya fedha kwa lengo ya kuasaidia Jamii yetu inayotuzunguka na yenye uhitaji maalum. Kwa miaka kadhaa sisi wafanyakazi tumekuwa tukifanya hivi na kwa kweli tumeona ni kwa jinsi gani Jamii imekuwa ikiguzwa na michango yetu, alisema Mbwambo.

  Tumeona ni vyema tuelekeza makusanyo yetu ya siku ya leo kwenye kusaidia afya kwa watoto ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa bidii kwa kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata tiba pale atapohitaji, Mbwambo.

  Mbwambo aliongeza kuwa tukio la leo la kukusanya fedha limefanikiwa sana kwani muitikio ni mkubwa mno. ‘ Natoa pongezi zangu za dhati kwa wanafanyakazi wenzangu wa muitikio na hamasa yenu mkubwa. Lazima niwaambie ya kwamba kuwepo kuweni hapai hii ya leo ndio kumeifanya tukio letu kupata mafanikio. Vile vile, napenda kutoa pongezi kwa uongozi wa Airtel, vitengo vingine na wadau wote kwa kutuunga mkono, alisema Mbwambo.
  Kwa upande wake, Teddy Chamsama Meneja wa Airtel kitengo cha wateja wakubwa alisema kuwa Airtel Tunakujali imekuwa ikisaidia Jamii yenye uhitaji maalum kwa lengo la kuonyesha kujali na pia kuwafanya wajisijikie kama wenzao kwenye Jamii.


  Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw Sunil Colaso akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Airtel waliohudhuria hafla ya chai ya asubuhi maalum kwa kuchangisha fedhazitakazotumika kulipa BIMA ya Afya kwa zaidi ya watoto 100 ambao wazazi wao wameshindwa kulipia bima watoto wao. Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Airtel mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wafanyakazia na baadhi ya wateja wa Airtel. katika hafla hiyo zaidi ya shilingi milioni 6 zilikusanywa.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Airtel wanaohudumia wateja maalum na makampuni wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada hafla ya chai ya asubuhi iliyoandaliwa na kitengo hicho kwa lengo la kukusanya fedha zitakazolipia BIMA ya Afya kwa zaidi ya watoto 100 ambao wazazi wao wameshindwa kumudu gharama hizo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na wafanyakazia wa Airtel pamoja na baadhi ya wateja wake, zaidi ya shilingi milioni 6 zilikusanywa


  Mkurugenzi kitengo cha wateja wakubwa na Makampuni wa Airtel Bw, Boniface Mwambo akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa wakala wa barabara nchini (Tanroad) wakati wa hafla ya chai ya asubuhi iliyoandaliwa na Airtel kitengo cha wateja wakubwa kwa lengo la kukusanya fedha zitakazotumika kulipa BIMA ya Afya kwa zaidi ya watoto 100 ambao wazazi wao wameshindwa kulipia bima watoto wao. Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Airtel mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wafanyakazia na baadhi ya wateja wa Airtel.zaidi ya shilingi milioni 6 zilikusanywa

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019 akisaini kitabu cha wageni alipofika katika kiwanja ambacho ujenzi wa ofisi ya wizara unaendelea katika Mji wa Serikali uliyopo maeneo ya Ihumwa jijini Dodoma,kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya ujenzi huo ambao unatakiwa kumalizika hivi karibuni,anayemulikia tochi ni Mhandisi Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo hilo la Wizara Bw. Hagay Mziray kutoka Kampuni ya Mzinga Holding Company Ltd.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza Mhandisi Hagay Mziray (kulia) kutoka Kampuni ya Mzinga Holding Company Ltd alipokuwa akitoa maelezo kuhusu hatua walizofikia katika ujenzi wa ofisi hiyo ya Wizara,usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019 wakati Mheshimiwa Waziri huyo alipotembelea eneo hilo la ujenzi kufuatila utendaji kazi na kasi ya ujenzi ya ofisi hiyo unaotarajiwa kumalizika hivi karibuni, katika Mji wa Serikali uliyopo eneo la Ihumwa Jijini Dodoma,wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Hagay Mziray Mzinga Holding Company Ltd ambaye ndiye msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo la wizara kwa kumtaka aongeze juhudi ili waweze kumalizi kazi hiyo kwa wakati, alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019 kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya wizara unaondelea katika Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Hagay Mziray Mzinga Holding Company Ltd ambaye ndiye msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo la wizara kwa kumtaka aongeze juhudi ili waweze kumalizi kazi hiyo kwa wakati, alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019 kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya wizara unaondelea katika Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.

  ………………………………………………………………………..

  Na Anitha Jonas – WHUSM- Dodoma.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe amemtaka Mhandisi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara katika Mji wa Serikali kuongeza juhudi ili kuweza kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

  Mheshimiwa Mwakyembe ametoa maagizo hayo usiku wa kuamkia Februari 11,2019 alipofanya ziara yake katika eneo hilo panapojengwa katika Ofisi za Wizara eneo la Ihumwa Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo na kasi ya utendaji kazi kwa masaa ishirini na nne ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliyopangwa.

  ‘’Kwanza nawapongeza kwa jitihada mnazozionyesha kwa kuifanya kazi hii kwa masaa ishirini na nne na kwa kazi mliyokwisha kuifanya mpaka sasa, ila nataka niwasisitize kuwa mnahitaji kuongeza juhudi zaidi ili muweze kumaliza ndani ya muda uliyopangwa na mjue kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu anatarajia kuja kukagua ujenzi huu hivi karibuni,hivyo basi mkumbuke mlimwaahidi nini kwani atahitaji mkamilishe ahadi mliyompa,’’alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.

  Naye Mkandarasi Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo hilo la Ofisi za Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kutoka Kampuni ya Mzinga Holdings Company Ltd Mhandisi Hagay Mziray alimweleza Mheshimiwa Waziri Mwakyembe kuwa kwa sasa kazi zinazoendelea ni pamoja na upakaji wa rangi nyeupi kabla ya kupaka rangi,usimikaji wa mabomba ya vyoo na umeme na wanatarajia kufunikia chemba za maji taka pamoja na shughuli nyingine mbalimbali.

  ‘’Hatua ya ujenzi wa jengo ilipofikia kwa sasa ni sawa na majengo mengine ya ofisi za wizara mbalimbali yaliyopo katika Mji huu wa Serikali kwa sasa na wote tunajitahidi kukamilisha kazi hii kwa wakati, ila kufuatia changamoto mbalimbali tuliandika barua ya kuomba kuongezewa siku za kukabidhi jengo hili kuweza kuwa Februari 28,2019 badala ya Februari 15,2019,’’alisema Mhandisi Mziray.

  Akiendelea kuzungumza Mhandisi Mziray alisema pamoja na hapo awali jengo hilo kuonekana kuwepo nyuma katika ujenzi wake kwa sasa hatua walizofikia ni nzuri na hatua wanayoelekea kwa sasa ni ukamilishaji wa ujenzi huo ikiwemo kupaka rangi na kuanza kuweka tiles na kuweka celing board.

  Halikadhalika nae Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu Bibi. Prisca Shewali alimsitisiza mhandisi huyo kuhakikisha wanafunika mashimo hayo ya maji taka kwa zege haraka ili kuepusha athari zinazoweza kutokea kutona na shughuli nza ujenzi zinazoendelea mahali hapo.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Petro Lyatuu (katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe wa mkutano wa ushirikiano kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Tanzania Bara) na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar) mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkuurugenzi wa Mipango toka Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar)Bw. Mahmoud OmarHamad na kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango toka Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Zanzibar) Bi. Saum Ali Said.
  Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ushirikiano kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Tanzania Bara) na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Bw. Petro Lyatuu (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujengeana uwezo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wa mkutano wa ushirikiano kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Tanzania Bara) na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar) wakiendelea na kikao cha kujengeana uwezo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

  Wajumbe wa mkutano wa ushirikiano kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Tanzania Bara) na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar) wakiendelea na kikao cha kujengeana uwezo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na WHUSM –Dar es Salaam

  0 0


  Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi Patterson alipotembelea mkoani Mara leo (Februari 11). Katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mh. Vincent Anny Naanu (kulia), Bi. Karolina Mpapula, Katibu Tawala mkoa wa Mara (wa pili Kulia), na Bw. Emmanuel Kisongo (kushoto) Afisa Elimu Mkoa wa Mara.

  Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi Patterson akifurahi pamoja na walimu na wazazi wa wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Mwisenge iliyopo mkoani Mara leo (Februari 11). Katika Ziara yake mkoani humo, Kaimu Balozi Dkt. Patterson pia anatembelea miradi mbalimbali iliyopo eneo la Ziwa Victoria inayofadhiliwa na serikali ya Marekani. (Picha: Ubalozi wa Marekani)

  0 0

  Na Estom Sanga-DSM

  Ujumbe wa Maafisa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo-DRC- umewasili nchini kwa ziara ya siku 10 kujifunza namna Serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya jamii –TASAF ilivyofanikiwa kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini-PSSN.

  Akiwakaribisha Maafisa hao kwenye Ofisi ndogo za TASAF jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Bwana Ladislaus Mwamanga amebainisha hatua mbalimbali zilizochangia kufanikiwa kwa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini unaohudumia Zaidi ya Kaya Milioni MOJA NA LAKI MOJA nchini kote.

  Bwana Mwamanga amesema mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo yametokana na ushirikishwaji wa jamii huku akisema mchango wa Serikali ya Tanzania na Wadau mbalimbali za Maendeleo umechangia kwa kiwango kikubwa kufanikisha Mpango huo wa aina yake kupata kutekelezwa nchini.

  Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amewaambia Maafisa hao kutoka DRC kuwa Mfuko huo tangu kuanzishwa kwake umejikita zaidi katika kuboresha huduma za kijamii hususani katika sekta za elimu, afya,maji,mazingira,na kuhamasisha walengwa kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ili waweze kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

  Kwa upande wake kiongozi wa ujumbe huo bwana Ruphin Kimuemue Bo- Elongo amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza namna serikali ya Tanzania kupitia TASAF ilivyofanikiwa kuwahudumia wananchi hususani wanaoishi katika hali ya umaskini .

  Amesema wamevutiwa na mafanikio ambayo TASAF imeyapata katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao wamesema utaisaidia pia DRC kutokana na kuwa na wananchi wake wengi wanaishi katika adha ya umaskini.

  Ukiwa katika ofisi za TASAF ujumbe huo umepata fursa ya kufahamishwa utekelezwaji wa shughuli za taasisi hiyo zikiwemo za Ajira za Muda ,Uhawilishaji Fedha, na Uwekaji wa Akiba kwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

  Maafisa hao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo pia watatembelea wilaya ya Kibaha mkoani Pwani ,Temeke na Zanzibar ambako watakutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kujionea namna wanavyonufaika na huduma za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF. 

  Mkurgenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga (wa tatu kulia ) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka DRC ambao uko nchini kujifunza shughuli za huduma ya hifadhi ya jamii 
  Ujumbe kutoka DRC ukimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,(anayeitazama kamera) kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya TASAF jijini DSM.


  0 0


  Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakimfanyia mgonjwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.
  Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumaliza kufanya uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa mgonjwa wa kwanza kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwafundisha wataalamu wa afya wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma kuhusu madhara ya moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure) kabla ya kuanza kwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa wagonjwa kupitia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma pamoja na timu ya wataalamu wa Taasisi hiyo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization) kupitia tundu dogo linalitobolewa kwenye paja. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Dkt. Alphonce Chandika.Picha na JKCI

  0 0

  Umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa pwani umeendelea kutoa mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana na wananchi wa kisarawe yaliyoyofunguliwa jana na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Jokate Mwegelo.

  Akifungua Mafunzo hayo DC Jokate amesisitiza vijana kuchangamkia FURSA na Amewapongeza Uvccm Mkoa wa pwani kwa kuandaa Mafunzo hayo katika wilaya hiyo.

  DC Jokate ameahidi kuwapa ushirikiano washiriki wa mafunzo hayo na amesema wajasiliamali wajitume kufanya kazi kwa maendeleo ya kisarawe.

  "Niwasihi Vijana Wenzangu Mjikite kwenye Ujasiliamali wa Kilimo ambapo kwa ardhi ya wilaya yetu inakubali nasi viongozi wenu tutahakikisha tunawatafutia soko la uhakika na wadau wa kilimo hicho;

  "Kwa Sasa wilaya yetu tunafanya vizuri Sana katika sekta mbalimbali mfano nilipokuja hapa wilaya nzima matokeo ya kidato cha nne daraja la kwanza wanafunzi walikuwa wanatoka 4 tu Ila kwa kampeni yetu ya Tokomeza Zero Kisarawe Imesaidia kwa Sasa wanafunzi 41" Alisema DC Jokate.

  Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Pwani Cde Charangwa Selemani, amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa kuwapa vijana ujuzi katika wilaya zote za Mkoa wa pwani na mpaka sasa wameshafanya wilaya mbili ikiwemo RUFIJI na KISARAWE. 

  Aidha Mwenyekiti Charangwa amesisitiza umoja na mshikamano katika kazi na wao kama viongozi watahakikisha wanawapa vijana ujuzi Ili waweze kujiajiri.

  Comrade Charangwa amewapongeza Viongozi wa Chama na serikali kwa Uchapakazi na amempongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Joseph Pombe Magufuli, kwa kazi kubwa anayoifanya kwa Watanzania.

  "Mwaka Huu Kuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vijana Ndo Injini ya Chama Shirikianeni na Chama Kuhakikisha Wilaya ya Kisarawe Tunapata Ushindi wa Kishindo pia Mafunzo Haya Myafanyie Kazi Tengenezeni Bidhaa za Ushindani katika Soko" Alisema Cde Chalangwa.

  Katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa Uvccm Wilaya ya Kisarawe,Asha Lusonzo, Amemshukuru mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa pwani kwa namna anavyoshirikiana nao katika kuwapelekea fursa na wameahidi kuzifanyia kazi.

  mafunzo hayo ya ujasiliamali yalihudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Mkoa wa Pwani,Abdallah Makelo, Katibu Msaidizi wa Mwenyekiti Taifa, Abdulrahaman Killo, Katibu wa Uvccm Mkoa wa Pwani,Ramadhan Kapeto, Viongozi wa UWT wilaya ya Kisarawe, viongozi wa jumuiya ya wazazi wilaya kisarawe,Katibu Uvccm wilaya kisarawe, waheshimiwa madiwani , DAS wa wilaya ya kisarawe,afisa maendeleo wa wilaya na afisa vijana wa wilaya.

  Vijana wa Wilaya ya kisarawe walijifunza mambo mbalimbali ikiwemo Kilimo ,Ufugaji wa Kuku,Uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani Mafunzo yaliyo tolewa na Taasisi ya TAEDO chini ya Mkurugenzi wake Kenani Kihongosi.

  Mafunzo hayo yalifungwa na mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Kigoma,Cde Silvia Sigula ambaye aliwaasa vijana kutumia fursa zilizopo na kufanyia kazi mafunzo waliyopewa katika kujiongezea kipatao chao.
    Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Jokate Mwegelo (katikati) Akifungua Mafunzo ya Ujasiliamali kwa Vijana wa wilaya Hiyo  yakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.Mafunzo Hayo yameandaliwa na Taasisi ya Taedo na Uvccm Mkoa wa Pwani. Kulia Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Pwani,Chalangwa Seleman na Mwenyekiti Uvccm Wilaya ya Kisarawe,Asha Lusonzo. 
   Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Pwani,Chalangwa Seleman (katikati) akichanganya dawa kwenye maji wakati wa mafunzo ya Ujasiliamali wa vitu mbalimbali wilayani Kisarawe jana. Wa Kwanza Kushoto ni Mwenyekuti wa Uvccm wa Wilaya ya Kisarawe,Asha Lusonzo. 
    Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (Uvccm), Chalangwa Selemani Akizungumza Jana katika Mafunzo ya Ujasiliamali kwa Vijana wilayani Kisarawe.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Hiyo,Jokate Mwegelo.
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefungua warsha ya siku mbili kuanzia leo Februari 11, 2019 kwa wadau wa madini inayolenga kujadili maudhui ya kanuni mpya za uanzishwaji masoko ya madini kama alivyoagiza Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni.

  Warsha hiyo inayofanyika Jijini Mwanza imeandaliwa na Wizara ya Madini kupitia uratibu wa taasisi ya Uongozi Institute na kuwashirikisha wadau na viongozi mbalimbali kutoka mikoa 12 nchini. 
  Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa watu kushoto waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimali akiwemo Katibu Mkuu Tume ya Madini, Profesa Simon Msanjila, (wa pili kushoto waliokaa), Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa (wa kwanza kushoto waliokaa) na Wakuu wa Wilaya zilizoshiriki warsha hiyo. 

  Wengine waliokaa ni Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda (wa pili kulia) aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza pamoja na Mkuu wa Idara ya Mafunzo kwa Viongozi kutoka taasisi ya UONGOZI Institute, Kadari Singo (wa kwanza kulia) aliyemwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo.
  Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashari za Wilaya zilizoshiriki warsha hiyo.
  Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Tawala kutoka wilaya zilizoshiriki warsha hiyo.
  Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa wizara hiyo.
  Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa wachimbaji wadogo wa madini.
  Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi ya UONGOZI Institute.


  0 0  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar Kanali.S.S.Mugoba, alipowasili katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba mwaka huu 2019.(Picha na Ikulu)
  IMG_3471
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Kambi ya JWTZ Chukwani Zanzibar, kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kushoto Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar Kanali S.S.Mugoba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mhe. Haji Omar Kheri.(Picha na
  IMG_3479
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama, ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika Viwanja vya Kambi ya Chukwani kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kujumuika katika chakula maalum aliowaandalia kushoto Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar, Kanali S.S.Mugoba na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ. Mhe. Haji Omar Kheri,(Picha na Ikulu)
  IMG_3485
  ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar, wakijumuika katika hafla ya chakula maalum walioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika Kambi ya Chukwani Zanzibar..(Picha na Ikulu)
  IMG_3501
  KAIMU Kamanda Brigedi ya 101 KV Zanzibar Kanali S.S.Mugoba, akizungumza wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Aki Mohamed Shein, kwa ajili ya Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi zilizofanyika mwaka huu kisiwani Pemba January,12, 2019.(Picha na Ikulu)
  IMG_3505
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akijumuika katika chakula maalum aliowaandalia, Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, katika kambi ya chukwani  walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar mwaka huu zilizofanyika Kisiwani Pemba katika uwanja wa gombani.(Picha na Ikulu)
  IMG_3519
  ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakijumuika katika hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_3522
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_3528
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  IMG_3533
  ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili yao katika kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu).

  0 0

  Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Bandari hiyo kwa wafanyabiashara wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini waliotembelea na kuvutiwa kupitisha shehena za mizigo yao
  Wafanyabiashara hao wakiendelea kupata ufafanuizi wa masuala mbalimbali
   Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiwa na Katibu tawala Msaidizi wa mkoa wa Kilimanjaro wakitembelea eneo la Bandari ya Tanga.
   Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na wafanyabiashara hao
   Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bandari nchini Lydia Mallya akizungumza ambapo aliwataka wafanyabiashara hao kutumia bandari hiyo kwani tayari ni bandari ya viwango vya kimataifa.
   Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Kilimanjaro akizungumza kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
  Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro Patrick Shirima akizungumza katika hafla hiyo
   Sehemu ya ujumbe wa wafanyabiashara kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini wakifuatilia nyumba anayefuatilia ni Moni Jarufu PRO wa Bandari ya Tanga akifuatilia mkutano huo
   Wadau mbalimbali nao wakifuatilia ziara hiyo
  Sehemu ya wafanyabishara wakifuatilia mkutano huo katikati ni Meneja wa Bohari ya Mafuta ya GBP mkoani Tanga Amour

  WAFANYABIASHARA wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini wameonesha nia ya kuanza kutumia Bandari ya Tanga kupitisha shehena ya mizigo yao baada ya kuridhishwa na mabadiliko makubwa ya mfumo wa utendaji wa Bandari hiyo.

  Wameonesha nia hiyo kwenye mkutano wa siku moja baina ya Uongozi wa mamlaka hiyo na wafanyabiashara hao na wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha.

  Katika mkutano huo wafanyabiashara hao waliongozwa na viongozi wa vyama vya Chemba za Biashara,Kilimo na Viwanda(TCCIA),Katibu tawala Msaidizi wa oa wa Kilimanjaro na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini na uongozi wa mamlaka ya Bandari Tanga.

  Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama amefafanua kuwa katika kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma bora kwa wateja wake imeboresha miundombinu na mifumo ya utendaji na ulinzi katika bandari hiyo.

  Amesema kuwa kutokana na maboresho hayo taratibu za uchukuaji wa mizigo zinatumia muda mchache tofauti na awali kutokana mamlaka zote za serikali zinazohusika na Bandari zipo kwenye jengo moja.

  " Tunataka kuwaondoa hofu wafanyabiashara kuwa sasa hivi Bandari ya Tanga ni nzuri,salama kwa mizigo na ni ya uhakika kutokana tumeboresha kuanzia mifumo ya ulinzi,miundombinu,utendaji kazi na Tehama" alisema.

  Alieongeza " Kutokana na maboresho hayo ikiwa mteja atakamilisha taratibu zote za uchukuaji wa mizigo basi kuanzia mizigo kufika bandarini atatumia siku tatu tu" alisema.

  Katika kusogeza huduma zake kwa wateja wa mikoa ya Kaskazini ya Kilimanjaro na Arusha tayari uongozi wa mkoa wa Arusha kupitia mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo ametoa eneo lenye ukubwa wa ekari 500 eneo la Malula katika wilaya ya Arumeru kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu.

  " Wafanyabiashara wa Arusha na Kilimanjaro mtakuwa hamna haja ya kuja hadi Tanga kuchukua mizigo mtakuwa mnasubiri mizigo yenu huko huko Arusha sisi tunamiambia gharama zetu tu mnalipia moja kwa moja na sisi tutajuana na Shirika la Reli( TRC) ambao tunategemea ukarabati wa reli ukikamilika uwatumie wao" alisema.

  Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bandari nchini Lydia Mallya aliwasihi wafanyabiashara hao kutumia bandari hiyo kwani tayari ni bandari ya viwango vya kimataifa.

  Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro Patrick Shirima amesema kuwa waliikimbia Bandari ya Tanga na kuhamia Bandari ya Mombasa nchini Kenya kutokana na urasimu uliokuwa unafanywa na taasisi za serikali zilizokuwa zinahusika na utoaji wa mizigo jambo ambalo lilikuwa linachelewesha mizigo.

  " Leo mmetufumbua masikio kusikia haya mabadiliko sasa tunaahidi kutumia Bandari yetu kwa ajili ya kuingizia mapato serikali yetu, kwani neno Bandari ya Tanga tuliisahau kabisa" alisema.

  Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Arusha Walter Maeda aliongeza kuwa kwa wafanyabiashara wa Arusha wanafahamu kuwa kikwazo kikubwa katika bandari ya Tanga ni taasisi za serikali katika kuchelewesha mizigo ndiyo maana waliachana nayo.

  " Sisi tuliikimbia Bandari ya Tanga na kuamua kutumia Bandari ya Mombasa kutokana na nenda rudi zilizokuwa zinafanywa na TRA,TFDA,TBS kwa kweli walikuwa hawana ushirikiano mzuri hali iliyotuletea tabu sisi wafanyabiashara " alisema.

older | 1 | .... | 1800 | 1801 | (Page 1802) | 1803 | 1804 | .... | 1897 | newer