Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 16 | 17 | (Page 18) | 19 | 20 | .... | 1904 | newer

  0 0  0 0  0 0


  Baada ya majibizano ya hapa na pale kuendelea kwa muda mrefu baina ya Serikali, Wanaharakati na Wananchi wa Mikoa ya Kusini sasa inaonekana mgogoro huo kukua zaidi siku hadi siku. Ililipotiwa hapo kabla kuhusu Naibu Waziri wa Nishati kwenda usiku huko Msimbati na kufukuzwa, ingawaje Serikali kwa upande wake ilikanusha habari hiyo na kudai ni maneno ya kizushi na udanganyifu wa watu kujitafutia umaarufu.

  Katika kile kinachoonekana kuwa ni hatari, asubuhi ya leo tumepata taarifa kwamba gari lililoenda kwa ajili ya kumbeba Bibi kwenda naye kusikojulikana limechomwa moto. Taarifa zinasema, watu kadhaa akiwemo kijana mmoja mwenye asili ya ukaazi wa kijiji hicho walikamatwa jana usiku na wanakijiji cha Msimbati wakidai wameagizwa kuja kumchukua Bibi huyo ili wakafanye maongezi na Wakubwa ambao pia hawakuweza kuwekwa bayana ni Wakubwa gani hao. Kinachoelezwa ni kwamba, baada ya mtafaruku huo, watu hao walichoropoka na kukimbia kitu kilichowapa hasira Wananchi na kuamua kuchoma gali hilo ambalo walikuja nalo.

  Ni hatari, kwasababu mbali na propaganda za viongozi wetu wa Kitaifa kwamba suala la gesi ni la Wanamtwara Mjini tu, eti kwamba wenyewe wa Msimbati na Mtwara Vijijini kwa ujumla wako tayari gesi hiyo kupelekwa Dar es salaam, kumbe si kweli. Leo hii, wale wanaodaiwa kuwa tayari kuruhusu gesi hiyo wameteketeza gari, je wale wasio tayari kwa hilo kesho watafanya nini? Wananchi hao wamesema wako tayari kumlinda Bibi huyo usiku na mchana kwa kuhofia kurubuniwa na Serikali ili abadili simamo wake.

  Serikali isidharau wananchi na wale wenye matakwa mema na nchi hii, kwani mbali na mamlaka ambayo serikali imepewa katika kusimamia rasilimali za nchi bado uhalali wa wamiliki asilia wa rasilimali hizo ambao ni wananchi hauwezi kuporwa. Wananchi wanaozungukwa rasilimali husika ndio wamiliki halali wa rasilimali hizo kabla ya Serikali na jamii zingine za nchi. Hivyo wanufaika wa kwanza wa rasilimali husika ni lazima wawe ni wale wenye uhalali wa Ki-asili na si vinginevyo.

  Tuache dharau, leo gari limechomwa na kama hii hali itaendelea kuwa hivi tusishangae kuambiwa kunamtu pia kachomwa au kapoteza maisha kwasababu hizihizi zinazofanyiwa masihara na viongozi wetu. Tuweni wazalendo jamani, tutetee maendeleo ya nchi na watu wake kwa vitendo, tuache porojo.

  Hassani Samli, Mtwara.

  0 0

  Rais Shirikisho la Filamu Tanzania (TFF), Simon Mwakifwamba akiongea mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
  Msanii Vitalis Maembe akionyesha mfano atakavyokamua siku hiyo.
  Dude akitoa kionjo cha nyimbo yake atakayoitambulisha kwa mara ya kwanza siku hiyo.
  Baadhi ya wasanii hao wakisikiliza mawaidha kutoka kwa rais wao.
  Waandishi wa habari wakichukua matukio ya ishu hiyo.

  RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TFF), Simon Mwakifamba, leo amezungumzia juu ya maandalizi ya tamasha la wasanii wa filamu Bongo, walivyojiandaa kwa makamuzi ya nguvu Jumamosi hii ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza mbele ya wanahabari, katika viwanja vya Leaders Club leo, Mwakifwamba alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na kila kilichopangwa kitafanyika. Katika upande wa burudani, kutakuwa na wasanii mbalimbali waliojitolea kusapoti tamasha hilo ambao ni Vitalis Maembe, Mrisho Mpoto, Scorpion Girls, Dude, Mtunisi, Radon, Ray, JB, Wema, Jack Wolper, Uwoya, Dk Cheni, na wengine kibao.
  (Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akiwa sambamba na mke wake,ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,ya Prime Time Promotions Ltd,Johayna Kusaga,akizungumza mbele ya wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo waliokutana usiku huu kwenye hafla fupi (hawapo pichani) ya kuukaribisha mwaka na kuzungmza mambo mbalimbali ikiwemo na mafanikio yaliyopatikana mwaka jana,pia kuwashukuru kwa ushirikiano wao mkubwa ambao wamekuwa wakionesha kwenye kampuni hiyo kwa ammoja.
  Boss Joe akiwaomba wafanyakazi wote wazinyanyue glassi zao za vinywaji juu na kuzigonganisha kwa pamoja kuonesha upendo,mshikamano na ushirikiano.Baada ya hapo Wafanyakazi walipewa ruksa ya kula kunywa na kujimwaya mwaya.
   Shampeni ikimiminwa baada ya kufunguliwa.
   Eprahim Kibonde akimminia kinywaji aina ya Shampeni meneja wa vipindi Sebastian Maganga baada ya kufunguliwa,ikiashiria kuwa hafla ya kunywa,kula imefunguliwa rasmi usiku huu huku baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media wakishuhudia tukio hilo.
   Mtangazaji wa kipindi cha power breakfast,Gerald Hando akizungumza jambo mbele ya Wafanyakazi wenzake usiku huu kabla ya kufungua shampeni,wa pili kulia ni Barbra Hassan,B Dozen,Eprahim Kibonde,Millard Ayo pamoja na Dina Marious.
  Dj Zero akiangusha ngoma live ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2 usiku huu.

  Baadae wafanyakazi wa Clouds Media Group walianza kupata chakula cha pamoja kama uonavyo pichani. 
    Kulia ni Paul James a.k.a PJ,Suka,Dj Steve B pamoja na Dj Peter Mo wakipata msosi huku wakibadilisha mawazo usiku huu ndani ya kiota cha Escape 2
   Dj Mayanga akiangusha ngoma za kufa mtu usiku huu ndani ya Escape 2
   Pichani kulia ni Dj Venture,Gerald Hando pamoja na Mdau mwingine.
   Kulia ni Dj Too Shot,Dj Bulla akiw ana Mdau kimapozi ndani ya picha.
   Mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast,Paul James a.k.a PJ akifurahia jambo na Meneja vipindi wa clouds FM,Sebastian Maganga usiku huu ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2. 
   Dj PQ aliyekaa wakipiga stori na sebastian Maganga pamoja na PJ.
  Mzee wa Kipindi Cha Jahazi,Eprahim Kibonde na mdau mwingine wakipata vitu laini laini safi kabisa.
   Ilikuw ni full kujichana,kula kunywa na kufurahi pamoja ikiwa ni sehemu ya hafla usikuu huu ndani ya Escape 2.
   Dada Regina Mwalekwa akiwa amepozi na Bonge Barabarani.
   Cheersssss
   Pichani kulia ni mdau mkubwa wa Clouds Media Group,Dauda wa Kota akifurahia jambo na Dada Regina Mwalekwa.
   Sehemu ya kikosi kazi cha Clouds Tv wakishangilia jambo.

  0 0
 • 01/25/13--11:03: Full moon party


 • Full moon party saturday 26/1/2013 northan of Zanzibar Kendwa rock hotel ..B.B.Q on the beach .Traditional ngoma and acrobatic show.. and This Saturday we wil have special band form DCMA  .Selected coctail all night... Delicious barbeque menu. Sushi and Pizza ..Music all around the World Dj side DJ ALLY  and gest Dj frm Ibizaa  Dj leo 

  Full Moon Party
  is organized around the FULL MOON every month. Usually on Saturday, but not always. A delicious grill menu.  
  Amazing acrobats & fire eaters. Dance music up to late. Chill on the beach or join the dancing crowd! FULL MOON parties attract a big crowd of people, locals as well as guests from as far as Dar-es-Salaam.


  Kendwa Rocks is about one hour drive from Zanzibar Town towards the northern tip of the island. The road descends through Kendwa village towards one of the most fantastic beaches of East Africa. Just opposite you can see the lighthouse of nearby Tumbatu Island. Sunbathing may be enough, but you can also snorkel, dive or fish and do small boat trips on the turquoise waters. Beautiful sunsets are everyday thrill and moonlighted nights on the white coral and seashell beach make an unforgettable experience.

  The choice of accomodation is ample: you can choose a spacious suite or family room, coral stone or palmwood bungalow or just a simple palmwood banda. The rooms are surrounded by coconut trees and lush tropical gardens.


  Booking & enquiries
  Management email: manager@kendwarocks.com
  Director email: kilupy@kendwarocks.com

  0 0

   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM,Ndg Abdulrahman Kinana akipungia mkono wanachana na wampenzi wa CCM waliokuwa wamewasindikiza Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC walioondoka Jijini Dar es Salaam leo kwenda Mkoani Kigoma kwenye Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama hicho.
   Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipungia mkono wanachana na wampenzi wa CCM waliokuwa wamewasindikiza Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC walioondoka Jijini Dar es Salaam leo kwenda Mkoani Kigoma kwenye Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama hicho.
   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM,Ndg Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachana na wampenzi wa CCM waliokuwa wamewasindikiza Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC walioondoka Jijini Dar es Salaam leo kwenda Mkoani Kigoma kwenye Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama hicho.Kulia ni Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam,Ndg. Madabida.

   Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na baadhi ya Wanachama wa CCM waliokuwa wamewasindikiza Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC walioondoka Jijini Dar es Salaam leo kwenda Mkoani Kigoma kwenye Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama hicho.
  Katibu wa NEC-Oganaizesheni,Dkt. Mohamed Seif Khatibu akipanda treni tayari kwa safari ya kwenda Mkoani Kigoma.
   wanachana na wampenzi wa CCM wakiwashangilia viongozi na Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC walioondoka jijini Dar leo.

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkesha wa sherehe za Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W). 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumin wa dini ya Kiislamu, katika mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013. Kushoto kwake ni ,Sheikh Mohamed Ismail. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana Januari 24, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za mkesha wa maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W.).
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh Mohamed Ismail, wakati akiondoka kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013, baada ya kuhudhuria sherehe za mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).
   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya kiislamu katika mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Sheikh Mohamed Ismail, wakati alipokuwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013, kwenye sherehe za mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa salamu zake za mkesha wa sherehe za Maulid, ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), wakati wa sherehe hizo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na waumin wa dini ya kiislamu wakijumuika kwa pamoja katika sherehe za mkesha wa Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika jana usiku katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  . Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR

  0 0

   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwaaga Wanachama wa CCM mkoani Dodoma waliokuwa wamefika Stesheni ya Dodoma asubuhi hii kuwalaki Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM
  Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika stesheni ya treni Mkoani Dodoma Mapema leo asubuhi.
   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya WanaCCM wa Mkoani Dodoma waliofika kuwalaki na kuwatakia safari njema Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka jana jijini Dar kwenda Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akiongoza mapokezi ya ujumbe wa Sekretarieti ya CCM,unaoelekea mkoani Kigoma mapema asubuhi hii kwa usafiri wa treni,ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM yatakayo adhimishwa mkoani humo.

  0 0  Na Mwandishi wa Thehabari.com

  KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi amesema wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri na mfano wa kuigwa katika maeneo mbalimbali endapo watajengewa mazingira na kuandaliwa mapema tangu wawapo shuleni.

  Bi. Liundi ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya TGNP ametoa changamoto hiyo leo katika Shule ya Sekondari ya Loyola ya jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mwanamke shuleni hapo.

  Akizungumza na umati wa wanafunzi wasichana wa shule hiyo na wageni anuai waalikwa, alisema tafiti nyingi zilizofanywa zinaonesha kuwa wasichana wanapoandaliwa mazingira mazuri ya elimu wanafanya vizuri ukilinganisha na wavulana.

  Aidha aliongeza kuwa kwa sasa zipo shule zinazochukua wasichana pekee ambazo zimekuwa zikifanya vizuri zaidi jambo ambalo linaonesha wazi mazingira mazuri yakijengwa jamii hii inaweza kuinuka na kuwa mfano mzuri.

  Alisema kwa sasa vishawishi na changamoto anuai zilizopo katika shule nyingi ndio kikwazo kwa wanafunzi wa kike kufanya vizuri, hali ambayo ikifanyiwa kazi kiufasaha mabadiliko kimafanikio kwa kundi hilo yanaweza kutokea.

  Hata hivyo alisema tafsiri iliyojengeka ya kwamba wanafunzi wa kike wanaogopa masomo ya sayansi si sahihi kiuhalisia, kwani mazingira ambayo wanafunzi hawa wanakumbana nayo ndio kikwanzo katika mafanikio yao kimasomo.
  “Mfano shule nyingi za kata ni za kutwa wanafunzi hasa wasichana wanakaa mbali na shule, wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni…wanakumbana na changamoto nyingi njiani hivyo wanajikuta wanashindwa kufanya vizuri au kukatishwa kabisa masomo yao,” alisema Bi. Liundi.

  Aliongeza kuwa eneo kama hili, vyombo husika vikiangalia sheria na sera zinazojenga mazingira mazuri kwa makundi yote, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumika vizuri wasichana wanaweza kuingia katika ushindani kwa fursa zilizopo.

  Kwa upande wake mwanafunzi Grace Ntambi wa kidato cha tano wa shule hiyo aliiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa mikoa ambayo bado inaendeleza mila potofu za kumbagua mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na kuelemea kwenye mfumo dume, ili kuangamiza vitendo hivyo.

  “Na hii ianzie pia katika ngazi za familia kuna kila sababu ya kuondokana na mila potofu za kwamba mtoto wa kike hana haki ya kupata elimu kama ilivyo kwa mtoto wa kiume…tuwatie moyo wasichana kwani wanaweza,” alisema mwanafunzi huyo.

  Katika hafla hiyo pia TGNP ilipata fursa ya kutoa mada mbalimbali za masuala ya wanafunzi kujitambua kwa hatua anuai ikiwa ni pamoja na kutoa ushuhuda ya kwamba wanawake wanaweza wakiamua kufanya hivyo kwa kila hatua wanayopiga.

  Imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)

  0 0

  Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo asubuhi.
   CHAMA cha Wananchi CUF kesho kitafanya Mkutano wake wa hadhara ikiwemo kuwakumbuka wahanga waliofarikidunia kwenye vurugu zilizotokea Zanzibar na jijini Dar es salaam mnamo mwaka 2001 wakitetea haki.


  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za CUF wilaya ya Nyamagana Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji alisema kwamba vyama vya siasa vilivyopo nchini havina budi kushirikiana ili kuiondoa CCM madarakani.

  "Bila kushirikiana hivi vyama vya upinzani na ikiwa kila kimoja ni kutaka kuingia ikulu kivyake basi itakuwa ni ndoto ya kukiondoa madarakani chama tawala (CCM) ambacho kinashikilia dola" alisema mjumbe huyo.

  Haji 'Babu' alisema kwamba Chama kinachohamasisha na kuchochea vurugu kitambue kuwa siyo  njia ya kukiwezesha chama hicho cha siasa (Upinzani) kuingia ikulu pia hakitaungwa mkono na wananchi kwani kwa kufanya hivyo wananchi hawatapata ujumbe na sera nzuri wanazopaswa kuzisikiliza kwenya mikutano ya hadahra ili kufanya uamuzi sahihi wa nani wachaguliwe kuwaongoza kupitia chaguzi mbalimbali. 

  Hata hivyo ameonya kuwa hatopenda kuona wafuasi wa vyama vingine watakao fika kwenye mkutano huo wa hadhara na kufanya fujo, watambuwe kuwa CUF ni chama makini kilicho na ujasiri wa vurugu lakini kwa sasa hakikusudii kufanya vurugu bali kiko kwaajili ya kuzitangaza sera na mikakati madhubuti ambayo itakiwezesha chama hicho kuungwa mkono kwa kupata wanachama wapya ili kuweza kushinda uchaguzi 2015.

  Aidha Chama  cha CUF kimejipanga kujiimarisha zaidi kwa kupata wabunge wengi kwenye uchaguzi ujao nchini ili kuwezesha kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa kama ilivyo Zanzibar.

  Juma Duni Haji  ametoa wito kwa wananchi kufika kwa wingi kwenye mkutano huo utakaofanyika katika viwanja vya Nghokozi al-maarufu 'Dampo' vilivyopo barabara ya Uhuru jijini Mwanza.

  Sehemu ya wandishi wa habari waliohudhuria kikao cha mazungumzo na Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa.
  Na ujumbe ulihusishwa.
  Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo asubuhi.
  Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo asubuhi.


  0 0


  Na. Lemmy Hipolite-Mo Blog.

  Kofia ngumu za kusaidia kuokoa kichwa dhidi ya majanga mbalimbali iwe ni katika maeneo ya ujenzi au katika vyombo vya usafiri ni muhimu sana kwetu tunapokuwa katika mazingira hayo.

  Tunaishukuru serikali kwa kutumia idara zake husika kuhimiza matumizi ya kofia hizi hasa kwa madereva wa usafiri wa pikipiki maarufu kama Bodaboda.

  Kama inavyojulikana mtu ni afya na pia tunafahamu kuna baadhi ya magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya kugusana, kutumia kitu kimoja watu wawili au zaidi na mengine kwa njia ya maji, hewa, mbu, kujamiiana na kadhalika.

  Hapa kwenye hili la kofia ngumu bado hainiingii akilini vizuri jinsi gani twaweza kukwepa magonjwa ya ngozi na mba japo sio lazima tuyapate wala hatuyaombei ila tunaangalia uhalisia wa matumizi ya kofia hizi.

  Ndugu zangu wataalamu wa magonjwa ya ngozi na tiba hili likoje katika uhalisia wake? Sichokonoi ila naomba kufahamu tu kwamba tuwe tunazifua? Au hakuna neno? Mzingatie pia je zitakauka?.

  Wadau sijasema msivae helmet la hasha nimeulizia tu ili woote tupate fahamu. Karibu uchangie maoni yako kwa kubofya hapa

  0 0


  Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wamepanga kufanya ziara ya kihistoria mkoani Morogoro mwezi wa tatu. Ziara hiyo ya siku tatu waliyoipa jina la Dom mpaka Moro (bata kwenda bata kurudi) inatarajiwa kufanyika sehemu mbalilmbali za mkoa wa Morogoro. 

  Akizungumza na Mhariri wa Lukaza Blog kwa Njia ya Simu Mratibu wa ziara hiyo Mr AMANI KIZUGUTO ameuambia Mtandao huu  ya kwamba taratibu za awali za maandalizi kwa upande mmoja zimekamilika kwani tayari wameshazungumza na mshauri wa wanafunzi (dean of students) katika maandalizi ya awali. Alisema wanatarajia katika ziara hiyo kutembelea mbuga ya wanyama mikumi,maporomoko ya maji katika milima ya udizungwa huku mazungumzo ya kupitia katika vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo Mkoani Morogoro yakiendelea ili kwenda kufanya nao matukio mbalimbali ya kijamii.

  Pamoja na kujadili mambo ya kielimu. haya sasa kazi kwenu wana udom kwa wale mtakaopenda kwenda wasilianeni na mratibu kwa simu namba 0717 3767350769 081122

  0 0  Jinsi ya Kufika:
  Kama unatokea Ubungo , Unachukua Basi kutoka Kituo cha mabasi madogo unapanda basi la Mbezi Mwisho kupitia Njia ya Kimara kisha unashukia Kituo cha Mwisho kabisa cha Mbezi, Baada ya hapo unapanda Basi linalo elekea Kibamba, Mlandizi au Kibaha, Unashukia Kituo kinaitwa NJIA PANDA SHULE. Ukishuka hapo ndio unakuja moja kwa moja Ikondolelo Lodge.

  Kwa wanaotokea maeneo ya Njia inayo tokea Kibaha unashukia NJIA PANDA SHULE

  0 0

  Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na k
  atibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana wa pili kulia
  ukiwasili Mkoani Tabora usiku huu.

  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana sambamba na  Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye wakiwaaga Wanachama wa CCM pamoja na baadhi ya Wanachi maeneno ya Stesheni ya Seranda,wilaya ya Manyoni mkoani Singida,Wakati ujumbe wa Sekretarieti ya CCM,ulipokuwa ukielekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM  leo.
   Vijana wa Chipukizi Wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wakimvisha skafu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana wakati alipofika kwenye Kituo cha Treni cha Saranda mkoani humo na kuzungumza na WanaCCM wa Manyoni.Mh. Kinana na Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM wako safarini kuelekea Mkoani Kigoma kwenye Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM.
  "Bai Baii.........!! "hivi ndivyo Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana sambamba na Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye walivyokuwa wakiwaaga wanaCCM wa mji wa Saranda,Wilayani Manyoni.
  Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na WanaCCM wa Manyoni.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanaCCM wa Manyoni.
  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoani Manyoni wakijitambulisha kwa Sekretarieti.
  Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi pamoja na Wanachana wa CCM wa Manyoni,Mkoani Singida wakati waliposiama katika kituo cha Saranda.
  Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki,Mh. John Chiligati akizungumza.
  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akizungumza na WanaCCM wa Manyoni leo.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na WanaCCM wa Manyoni leo.


  0 0
 • 01/27/13--01:27: THIS WEEK ON THE SPORAH SHOW

 •   "WOMEN DO HAVE MEN IN BENEFITS AS WELL, AS WELL AS MEN DO HAVE WOMEN IN BENEFITS" VALENTINE ARTIST.

  0 0

   Mratibu wa Kituo cha Mabinti kilichopo chini ya Hospitali ya CCBRT Bi. Katia Geurts  akiwaelezea Maafisa wa Vodacom Foundation  shughuli zinazofanywa na kituo hicho wakati walipotembelea kuona miradi mbalimbalia wanaoyoifadhili ,Mabinti hao wanapata elimu ya kazi za mikono mara baada ya matibabu ya Fistula katika Hospital ya CCBRT na Kupona  ili waweze kujikimu kimaisha wakati wanaporudi makwao.
   Mmoja  wasichana  wa kituo cha "Mabinti" aliyepata kutibiwa Fistula na kupona katika Hospitali ya CCBRT Bi. Roida George  akionesha umahiri wa kushona kofia wakati Maafisa wa Vodacom Foundation  ambao ndio wadhamini wa miradi yao walipotembelea katika kituo hicho  kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.Kituo hicho kinawawezesha mabinti hao  kupata elimu ya kazi za mikono  ili waweze kujikimu kimaisha pindi wanaporudi makwao.
  Mratibu wa Kituo cha Mabinti kilichopo chini ya Hospitali ya CCBRT Bi. Katia Geurts  akifafanua jambo Maafisa wa Vodacom Foundation jinsi  shughuli zinazofanywa na kituo hicho wakati walipotembelea kuona miradi mbalimbalia wanaoyoifadhili ,Mabinti hao wanapata elimu ya kazi za mikono mara baada ya matibabu ya Fistula katika Hospital ya CCBRT na Kupona  ili waweze kujikimu kimaisha wakati wanaporudi makwao,wapili toka kuliani Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon,Afisa wa Vodacom Foundation Ally Mbuyu na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu.
  ==========  =============  =============
  Wanawake waliougua  kutibiwa na hatimaye kupona maradhi ya fistula katika Hospitali ya CCBRT iliyopo Dar es Salaam wameamua kujikita katika sanaa ya kazi za mikono kwa lengo la kujiajiri sambamba na kujikwamua na wimbi la umasikini.

  Takribani wanawake wapatao 62, chini ya mpango madhubuti ulioratibiwa na hospitali ya CCBRT, wamekuwa wakihitimu mafunzo mbalimbali ya kazi za mikono zikiwemo sanaa za ushonaji wa batiki, nguo za aina tofauti, utengenezaji wa mabegi, kofia, ususi na kadhalika, katika Kituo kinachoendeshwa na hospitali hiyo kijulikanacho kama 'Mabinti' tangu mwaka 2007.

  Akizungumza mbele ya ujumbe wa wadhamini waliotembelea kituo hicho kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mratibu wa Kituo hicho, Katia Geurts, alisema kituo hicho kinatoa mafunzo mahsusi kwa wakinamama waliopona baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa fistula. "Wengi wao wanatoka katika familia duni, hivyo mafunzo haya wanayoyapata baada ya kumaliza matibabu ya Fistula yanakwenda kuwasaidia kujiajiri wao wenyewe jambo linalowasaidia kupunguza ukali wa maisha," alisema Geurts.

  Aliongeza kuwa baada ya kuhitimu mafunzo hayo kituo hicho huwapatia vyeti vya uhitimu vinavyotambulika, sanjari na vitendea kazi vinavyoendana na stadi stahiki aliyohitimu mwanafunzi kwa minajiri ya kuwarahisishia upatikanaji wa mahitaji muhimu ya maisha yao.

  Nae Mkufunzi wa Kituo hicho ambaye awali alikuwa mmoja wa waathirika wa ugonjwa wa fistula hospitalini hapo, Jane Rugalabamu, alisema katika kipindi cha mwaka mmoja tangu aanze kufundisha wenzake kituoni hapo amebaini kuna idadi kubwa ya wanawake wenye matatizo ya fistula ndani ya jamii lakini waume zao wamekuwa wakiwaficha kwa dhana ya kufisha aibu.

  "Kuna haja kubwa ya kuelimisha akinababa wawaruhusu wake zao wenye matatizo waje kutibiwa. Ugonjwa huu unatibika na wala sio wa kurogwa kama wengi wanavyodhani, sisi sote hapa kwenye kituo cha mabinti tulikuwa na maradhi hayo na sasa tumepona kabisa wanawake jitokezeni," alisema Rugalabamu.

  Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Vodacom  Foundation, Grace Lyon,  baada ya kukagua shughuli mbalimbali za mafunzo zinazoendelea kituoni hapo, alisema kwa niaba ya wafanyakazi wa Vodacom na Vodafone duniani kote, wataendelea kuwasaidia akinamama wote wanaopatwa na maradhi ya fistula hatua kwa hatua, sanjari na kuhakikisha wanazidisha kasi katika kampeni inayoendelea dhidi ya maradhi hayo.


  "Tutaendelea kuwa karibu zaidi na waathirika wa fistula kuanzia hatua ya kuwasafirisha kutoka vijijini na mikoani kwa kuwatumia fedha kupitia huduma yetu ya M-Pesa, pia tutakuwa pamoja wakati wote wa matibabu na baada ya kupona tutawaunga mkono kwenye mafunzo kama haya ili kuwaletea ustawi ulio bora kwa maisha bora kwa ajili yao na familia zao," alisema Lyon.

  0 0


  Bondia Antony Mathias (kushoto) akitunishiana misuri na Fadhili Majia baada ya kupima uzito, Dar es salaam  kwa ajili ya mpambo wao kesho utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Tandare.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)


  Mabondia Hassan Mandulla na Jems Martin wanatarajia kupanda ulingoni  leoo jumapili Janual 27 katika ukumbi wa wa CCM Tandare Dar es salaam akizungumza mpambano huo mwandaaji Waziri Rosta.

  amesema  wamepima uzito leo pamoja na kujua Afya zao mabondia wote watakaocheza kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yakiwemo ya mabondia maarufu na chipkizi alisema mapambano ya utangulizi ni Fadhiri Majia na Anton Matiasi mpambano mwingine

  Utamkutanisha Kalama Nyilawila atakaezidunda na Athumani Pendeza mpambano wa raundi nane kalama anapanda ulingoni baada ya mpambano wake wa mwisho kupondeza kwa K,O raundi ya sita na Francis Cheka 

  michezo mingine ni  Shabani Kilumbelumbe na Mwaite Juma na Chaeles Mashali atavaana na Adam Ngange, Julias Noro atapambana na Abdallah Luwajempambano mwingine utawakutanisha Rajabu Tumaini na Daudi Anton na Rashid Mohamed Atavaana na Eliman Richard wakati Rashid Hamisi atamvaa Omary Shabani 


  Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina. 
   michezo.

  ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. 

  Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.   

  Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa 
  timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

  0 0

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akitoa Maelezo ya Matumizi ya Bajeti ya Nusu  Mwaka wa Fedha 2012/2013 Mbele ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira Kwenye Ofisi za  Bunge Jijini Dar es Salaam. 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Mazingira James Lembeli akitoa Maelekezo kwa Wajumbe wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa kupokea  taarifa ya Matumizi ya Fedha za Bajeti ya  Nusu Mwaka wa 2012/2013 kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Tereyza Huvisa  kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam.

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Charls Kitwanga akizungumza Jambo  na Mbunge wa Jimbo la Pangani Saleh Mbamba Mara Baada ya Kikao cha Bajeti ya Nusu Mwaka kwa  Ofisi ya Makamu wa Rais Kulia Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Julias Ningu  {Picha na Ali Meja]

older | 1 | .... | 16 | 17 | (Page 18) | 19 | 20 | .... | 1904 | newer