Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

UTEUZI WA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

0
0

BONDIA SELEMANI GALILE AJIFUA KUMKABILI MBWANA ALLY FEBRUARY 2

0
0

Bondia Selemani Galile kushoto akijifua na Mohamed Mosco wakati wa mazozi yake ya kujitahalisha kupambana na Mbwana Ally mpambano utakaofanyika Yombo Dovya katika ukumbi wa Lupingu Pub February 2. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Selemani Galile yupo katika mazoezi ya maandalizi ya mpambano wake dhidi ya Mbwana Ally utakaofanyika February 2 katika ukumbi wa Lupinga Pub uliopo Yombo Dovya

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Galile amesema yupo fiti kwa mpambano huo kwani kwa sasa anasubiri siku ya siku tu ili aweze kufanikisha,
Galile aliongeza kuwa siku hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa wakazi wa Yombo Dovya kupata burudani ya masumbwi itakayosindikizwa na mabondia chipukizi 

Antony Mathias atapambana na Abuu Mtambwe huku Ramadhani Mkundi akioneshana kazi na Kassim Gamboo na Mohamedi Zungu kutoka Zanzibar atapambana na Mbena Rajabu wa Dar

Siku hiyo ya Mpambano kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi atasambaza DVD zake mpya ikiwemo ya Marvin Hagler vs John Mugabi na Manny Pacuiao va Emanuel Juan Marquize ambazo atasambaza kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo DVD hizo zinazoelekeza mbinu na shelia za masumbwi zenye uwezo wa kuwajengea uwezo mabondia na mashabiki kujua sheria mbalimbali za masumbwi

MASHABIKI WA SOKA JIJINI MWANZA WAENDELEA KUFURAHIA NA KUSHUHUDIA MICHUANO YA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA 2013 LIVE KUPITIA DStv

0
0
Karibu Villa Park Resort jijini Mwanza. Mambo yote soka hutokea hapa Live kupitia SuperSport ndani ya DStv.

Michuano ya kuwania Kombe la Mataifa Afrika 2013 ambayo pia inajulikana kama Orange Africa Cup Of Nations inazidi kupamba moto kutokea katika miji na viwanja mbalimbali nchini Afrika Kusini. Ingawa Tanzania haikufanikiwa kuingia katika michuano hii(one day Yes),watanzania wengi ni mashabiki wa soka. Iwe ni michuano muhimu kwa bara la Afrika kama hii au iwe ni Ligi ya Uingereza,Italy,Spain au kwingineko, una uhakika wa kumkuta mtanzania ambaye ni shabiki wa ukweli wa michuano. 

Hali haikuwa tofauti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki ambapo mashabiki wa soka walifurika katika viota vya Villa Park Resort na Shooters Pub maeneo ya Kirumba jijini hapo katika shughuli maalum ya kushuhudia na kufurahia soka kwa pamoja iliyoandaliwa na kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia Channels zao za SuperSport zinazopatikana ndani ya DStv.

 Huduma za DStv zinapatikana kote nchini. Bonyeza hapa kujua zaidi na pia ili kwenda na wakati wa kile kinachoendelea ungana na DStv kupitia ukurasa wao maalumu wa Facebook kwa kubonyeza hapa.

Kutoka kushoto Gordon Mumbara, Masalu na John Kasuku(MultiChoice Regional Sales Coordinator-Kanda ya Kaskazini)-Experience The Spirit Of Africa
Macho yote kwenye screen. SuperSport 4 inahusika hapa.
Mashabiki hawa waliniambia kwamba wao kwa pamoja ni Manchester United "damu".Lakini kunako Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2013) kila mtu ana taifa ambalo angependa linyakue kombe mwaka huu.Kuna Ivory Coast, Ghana,Mali,Zambia nk.
They sleep and wake up with Manchester United but haven't forgotten home hence carefully following AFCON 2013 through SuperSport on DStv.
Villa Park Resort- Experience The Spirit Of Africa
I Love and Proud Of SuperSport
Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu (mwenye t-shirt nyekundu) akiwa na wadau na wafanyakazi wa ofisi ya MultiChoice Mwanza ndani ya Villa Park Resort-Kirumba Mwanza.
Yellow, Blue or Red, Soccer Fever In Mwanza. Thanks to DStv matches can be seen Live and in HD
Mashabiki wakishuhudia AFCON2013 ndani ya Villa Park Resort jijini Mwanza.
Intesity
Soka lina raha yake.Soka lina karaha zake. Unaweza kuhisi hapo nini kinaendelea. Ivory Coast walikuwa wanamenyana na Tunisia.
Cheers and Thanks to Mwanza Soccer Fans!!!
Kwa huduma na mauzo ya DStv Mwanza na Kanda ya Kaskazini unaweza kuwasiliana na DStv Mwanza kwa kutumia namba +255-28-2500230. Ofisi zipo Kenyatta Road (Masumini Bldg) opposite na Mwanza Engineering.

Serikali iache kutafuta mchawi, iende Mtwara

0
0

TAARIFA YA NDUGU ZITTO KABWE (MB) KUHUSU YANAYOENDELEA
MTWARA NA MRADI WA BOMBA LA GESI ASILIA
 
Serikali iache kutafuta mchawi, iende Mtwara
 
Katika kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamamo, malumbano na vurugu kuhusu mradi wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Mradi huu wa kutandaza bomba la urefu wa kilometa 542 ni mkubwa sana hapa nchini, na una thamani kubwa zaidi kuliko miradi mingine yote  ya miundombinu iliyopata kutokea hapa nchini. Mradi huu utajengwa kwa mkopo wa dola za Kimarekani 1.2 bilioni kutoka Benki ya Exim ya China.
 
Wananchi wa Mtwara kupitia maandamano ya tarehe 27 Desemba 2012 wametaka kujua hatma ya maendeleo ya mikoa wa kusini kutokana na mradi huu wa bomba la gesi. Serikali imewajibu wananchi hawa kwa kuwaita wahaini, watu hatari na wasio elewa. Imefika mahali inapotosha madai yao kwamba hawataki gesi itoke Mtwara.
 
Kimsingi Serikali haijajibu hoja yeyote ya msingi ya wananchi wa Mtwara kuhusu mradi wa kusafirisha gesi. Badala yake imekuwa ikijaribu kupotosha madai ya watu wa Mtwara kupitia mikutano na vyombo vya habari.
 
Tangu maandamano haya yatokee, na baadaye mikutano ya hadhara na
hatimaye matukio ya kusikitisha ya kuharibu mali za watu, mauaji ya
watu na majeruhi mbalimbli, Serikali na hasa Wizara yenye dhamana ya
mradi huu, imekuwa ikitoa matamko kwenye vyombo vya habari badala ya
kwenda Mtwara kuzungumza na wananchi, kusikiliza madai yao na kuona
namna ya kutekeleza madai hayo. Kutokana na Serikali kutofanya hivyo,
kusikiliza na kuzungumza na wananchi wa Mtwara, vurugu mbaya sana zimeendelea mkoani humo.

Mwezi uliopita, Desemba 2012, tatizo lilionekana kuwa ndogo na lenye kuhusiana zaidi na ukosefu wa kushirikishwa kwa wananchi. Badala ya kushughulikia
tatizo likiwa bado ndogo, Serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisemakuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro
huu.
 
Leo hali iliyopo mkoani Mtwara inasikitisha sana, maana mali za wananchi zinaharibiwa, nyumba zinachomwa moto na watu wanapoteza maisha. Tunalaani matukio haya kwa nguvu zetu zote, maana kinachotokea Mtwara si Utanzania. Tusipowasikiliza wananchi na kutatua mgogoro huu kwa kuwashirikisha, hali itazidi kuzorota wakati tukitupiana lawama.
 
Hivi sasa serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisema kuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro huu.
 
Kwanza, Serikali imekuwa ikiaminisha umma kwanza suala hili limechukuliwa kisiasa. Pili, Serikali imekuwa ikirudia kusema kuwa baadhi ya makampuni ya uwekezaji nchini na mataifa ya Magharibi yamekuwa yakichochea wananchi wa Mtwara.
 
Katika mwendelezo wa mtindo wa Serikali wa ‘management by press conferences’ jana Jumamosi Naibu Waziri wa Nishati na Madini ndugu George Simbachawene aliwaambia wahariri kwamba mimi Zitto Kabwe ninachochea wananchi wa Mtwara, ninatumiwa, na si mzalendo. Vile vile alitoa vielelezo kadhaa kuonyesha kuwa mradi wa kujenga bomba la gesi ni gharama sawasawa. Akasisitiza kwamba mimi ni mwongo.
 
Katika kipindi chote cha mgogoro wa Gesi Mtwara, sijafika Mtwara. Sijafanya mkutano wowote na waandishi zaidi ya kuandika mawazo yangu, kama Mtanzania kuhusu suala hili.
 
Nimeandika makala nne na zimechapishwa katika magazeti kadhaa hapa nchini na kwenye blogu yangu (www.zittokabwe.com).
 
 
Sitaki kubishana na Naibu Waziri ama Kiongozi yeyote ya Serikali kwa sasa. Hatuwezi kuendelea kulumbana, kuzozana, kuzodoana na kurushiana maneno wakati nchi yetu inaungua. Huu sio wakati wa kutafuta mchawi bali kutafuta majawabu ya changamoto zilizopo mbele yetu.
 
Yanayotokea Mtwara ni fundisho kwetu kwa Taifa namna ya kukabili changamoto za utajiri wa rasilimali, ili kuweka mkakati, mambo haya yanayotokea Mtwara yasitokee tena Tanzania. Tutaweza kuzuia maafa haya iwapo tutaweka uwazi katika mikataba, tutashirikisha wananchi kwenye unyonyaji wa maliasili za nchi, na iwapo tutaweka uwajibikaji.
 
 
Rais Kikwete Kikwete ana majibu; ayatoe sasa kwa wana Mtwara
 
Kwa mujibu wa Mpango Kabambe wa Umeme nchini (Power System Master Plan), kulikuwa na mradi wa kufua umeme MnaziBay, ambao Rais Jakaya Kikwete aliagiza utekelezwe mara moja. Serikali ieleze umma kuhusu mradi huo wa kujenga kituo cha kufua umeme 300MW MnaziBay Mtwara na kujenga msongo wa umeme wa 300KV mpaka Singida. Umeishia wapi? Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 12 Oktoba 2012, Rais Jakaya Kikwete alipokea ripoti ya ujenzi wa mradi huu kutoka makampuni ya China National Machinery & Equipment Import & Export Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya Ujerumani, ambayo kwa pamoja yalitarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100 kutoka Mtwara hadi Singida. Mradi huu ungegarimu dola za kimarekani milioni 684 na Rais aliagiza utekelezwe haraka sana. Huu mradi uliishia wapi? Kwa nini Serikali ipo kimya kuhusu mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya watu wa Mtwara? Taarifa ya Ikulu kuhusu mradi huu imeambatanishwa hapa.
 
Tufanyeje?
 
Hapa tulipofikia ni lazima kwanza kabisa kusikia kilio cha wananchi wa Mtwara ikiwemo kuelewa madai yao. Swali kubwa kubwa la watu wa Mtwara na Kusini kwa ujumla ni ‘tunanufaikaje’? Jibu la swali hili si ahadi za miradi bali ni vitendo. Hapa ndipo serikali inaposhindwa kushughulikia suala hili, kutoelewa madai ya wananchi na kuyapotosha.Viongozi wa kisiasa wenye ushawishi kutoka pande zote, chama tawala na vyama vya upinzani, waende Mtwara kuzungumza na wananchi, lakini wawasikilize kwanza.
 
  1. Lazima viongozi tujenge utamaduni wa kusikiliza wananchi na si kuwahutubia tu. Wananchi wa Mtwara wana madai ambayo lazima viongozi tukae kitako kuwasikiliza kisha kufanya nao majadiliano ambayo yatatoa mwafaka. Rais mstaafu, Ndugu Benjamin Mkapa ameshatoa kauli kuhusu suala hili. Ni wakati mwafaka sasa kwa viogozi wengine kumuunga mkono kwa kwenda Mtwara na kukaa na wananchi wa Wilaya zote za Mtwara, kusikiliza hoja zao na kuona namna ya kupata ufumbuzi wa suala hili. Wakati hatua hii inachukuliwa, wananchi waombwe kutulia na kuacha vurugu za aina yeyote ile, na Serikali isimamishe mradi mpaka hapo suluhu na wananchi itakapopatikana.
 
  1. Wakati juhudi hizo zinaendelea Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wa bomba, kwani ni dhahiri gharama za mradi huu ni kubwa mno kulingana na uhalisia wa miradi ya namna hii duniani kote. Katika taarifa zote kwa umma Serikali imekuwa ikisema kwamba mradi utagharimu jumla ya dola za kimarekani 1.2 bilioni, lakini katika taarifa ambayo Wizara ya Nishati na Madini imesambaza jana kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini imesema mradi utagharimu dola za kimarekani milioni 875. Usiri katika mkataba huu unaashiria kwamba Serikali inaficha kitu. Hivyo njia pekee ni kutaka mkataba uwe wazi kwa wananchi.
 
  1. Wakati tunawataka wananchi wa Mtwara kuruhusu utulivu, ni vema Serikali ijiandae kutoa majawabu ya madai ya wananchi hao. Majawabu ya Serikali yajikite kueleza wananchi wa Mtwara wanafaidikaje na rasilimali ya gesi asilia kwa maendeleo yao. Wananchi wa Mtwara wanataka uwajibikaji wa Serikali kwenye utajiri wa nchi, na wamechoka na porojo za orodha ya miradi isiyotekelezwa.
 
Viongozi twendeni Mtwara kusikiliza wananchi wetu. Nchi inaungua na hatuwezi kuendelea kuzozana badala ya kuzima moto huu hatari kama vita vya MajiMaji. Mimi nakwenda Mtwara haraka na mara baada ya viongozi wangu wa chama kutoa ridhaa.
 
 
ZITTO KABWE
Mbunge, Kigoma Kaskazini (Chadema)
Waziri Kivuli wa Fedha

UJUMBE WA SEKRETARIETI YA CCM WAWASILI SALAMA MKOANI KIGOMA LEO,walakiwa kwa shangwe na wananchi

0
0

Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa wamekusanyika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akizungumza nao mara baada ya kuwasili na ujumbe wake wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mapema leo asubuhi mkoani humo ukitokea jijini Dar kwa njia ya treni.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) akipeana mkono na Dereva wa Treni ya TRL,Bw. Kambi Ali (wa pili kulia) aliyewasafirisha kutoka Jijini Dar es Salaam mpaka Mjini Kigoma salama. Wengine pichani ni Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM), Nape Nnauye.

Wananchi wa Mkoa wa Kigoma leo wameupokea kwa shangwe Ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) uliowasili mkoani humo ukitokea jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa Treni ya Reli ya Kati.

Wajumbe hao ambao wanaoongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana ni pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM,Martin Shigela.

Akizungumza baada ya kuwasili Mkoani Kigoma mapema leo asubuhi, Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana alisema kuwa lengo la wao kutumia usafari huo wa Treni ni kuwadhihirishia wananchi wa Tanzania kuwa Usafiri wa Treni ni Usafiri wa uhakika na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kupitia Wizara ya Uchukuzi, itasimamia kikamilifu usafiri huo na kuendelea kuuboresha zaidi ya ilivyo sasa na kuhakikisha safari zinaongezeka na kuwa za kila siku na si kuwa kwa wiki mara mbili kama ilivyo sasa.

Nao baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma wameipongeza sana Sekretarieti hiyo kwa uamuzi wao wa kusafiri kwa kutumia Treni kutoka jijini Dar es Salaam hadi Mkoani Kigoma na kujionea hali halisi ya usafiri huo.

Ujumbe huo upo Mkoani Kigoma kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachama pamoja na wananchi wa mji wa Itigi mkoani Singida wakati Treni iliposimama kwa muda mfupi katika mji huo.
Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakielekea kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM wakati ukiwasili Mjini Kigoma leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Mji wa Kigoma waliofika kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM uliowasili mjini Kigoma leo kutokea jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Treni ya Reli ya kati.
Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na wananchi wa Mji wa Kigoma waliofika kuupokea Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM uliowasili mjini Kigoma leo kutokea jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Treni ya Reli ya kati.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma ya utamaduni ya mkoa wa Kigoma iliyokuwa ikipigwa Stesheni leo,huku Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akipiga moja ya ngoma hizo.
Sekretarieti ya CCM ikiondoka Stesheni ya Kigoma.

TAMASHA LA USIKU WA MASTAA WA FILAMU DAR LIVE LAACHA HISTORIA

0
0
Kundi la Scorpion Girls likiongozwa na Isabela Mpanda (katikati) likiporomosha burudani wakati wa Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu lililofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo.

Afande Sele akiwapa 'hi' mashabiki.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo ambaye pia ni Meya wa Ilala, Mhe. Jerry Slaa akiwasabahi mashabiki.
Nyomi iliyohudhuria tamasha hilo.
Afande Sele akiwa amebebwa na mashabiki.
Mrembo Jacqueline Wolper akiwapa 'hi' mashabiki.
Jacob Steven 'JB' akionyesha umahiri wake wa kusakata rhumba wakati wa tamasha hilo.
Mastaa wa filamu wakiwa jukwaani kuwasalimia mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live.


Steve Nyerere naye akionyesha manjonjo yake stejini.
Snura Mushi akiwapagawisha mashabiki.
Msanii Afande Sele akiwarusha mashabiki ndani ya Dar Live.
Tundaman akiwachizisha mashabiki.
...akizidi kuwapa raha mashabiki.
Kingwendu akifanya vitu vyake.
Richie naye akionyesha ufundi jukwaani.
Dk. Cheni na mwanadada wakienda sambamba.
Shamsa Ford akisema na mshabiki.
Bi. Mwenda akiwa kapagawa na shangwe za Dar Live.
Mrisho Mpoto akiwapa raha mashabiki.
Bi. Mwenda akionyesha machejo yake stejini.
Ilikuwa ni full burudani ndani ya Dar Live.
Scorpion Girls wakizidi kupagawisha.
Snura na wanenguaji wake wakilishambulia jukwaa.
Bendi ya Twanga Pepeta ikitoa burudani katika Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu lililofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Shilole akiwapa raha mashabiki.
Burudani zikiwa zimepamba moto mahali hapo.
Wanenguaji wa Shilole wakimpagawisha shabiki aliyepanda jukwaani.
Raha zikizidi kushamiri mahali hapo.
Baadhi ya mastaa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mhe. Jerry Slaa (katikati).
Sabrina Rupia ‘Cathy’ katika pozi.
Baadhi ya mastaa wa filamu wakiwa katika picha ya pamoja na rais wao Mwakifwamba (wa pili kulia).
Mrisho Mpoto akiwa katika pozi.
Tundaman akipozi katika Red Carpet.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba katika pozi.
Jack Wolper katika pozi.
Mrembo Rose Ndauka katika pozi.
Kingwendu akipozi na watoto katika Red Carpet.
Tamasha la Usiku wa Mastaa wa Filamu lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam limeacha historia baada ya kutawaliwa na burudani za kila aina kutoka kwa wasanii wa filamu na wale wa Bongo Fleva. Pichani juu ni baadhi ya matukio yaliyochukua nafasi wakati wa tamasha hilo.
(PICHA ZOTE: ERICK EVARIST NA MUSA MATEJA/GPL)

MTANZANIA KUSIMAMIA PAMBANO LA UBINGWA WA DUNIA KWA VIJANA

0
0

Ngowi akiwa na mwamuzi Jaap Van Niewenhuizen wa Afrika ya Kusini.

Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Matanzania Onesmo Ngowi atasimamia pambano la ubingwa wa dunia la vijana katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.

Mpambano huo utawakutanisha mabondia Ilunga Makaba kutoka Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) mwenye makazi yake nchini Afrika ya Kusini akipambana na bondia Gogita Gorgiladze anayetoka katika jiji la Tiblis, nchini Georgia. Georgia ilikuwa kati ya nchi zilizokuwa Umoja wa nchi za Kisoshalisti wa Sovieti (USSR).

Mabondia hao wenye wiwango vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12) watapambana kugombea mkanda wa vijana wa wa dunia (Youth Title) wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika uzito wa Cruiserweight tarehe 15 February, 2013.

Mpambano wa wawili hawa utafanyika katika hoteli ya nyota 5 ya Emperors Palace in Kempton Park, Gauteng katika jiji la Johannesburg, nchini South Africa.

Ngowi kama kamishna mkuu wa pambano hilo atasaidiwa na maofisa wafuatao: Refarii: Wally Snowball (Afrika Kusini). Jaji Namba moja:Simon Xamlashe (Afrika Kusini), Jaji namba mbili: Manuel Maritxalar (Spain) na Jaji namba tatu: Jaap Van Niewenhuizen (Afrika ya Kusini).

Mpambano huu ni kati ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF yatakayofanyika katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika kipindi cha mwaka huu wa 2013 chini ya mradi wa IBF wa “Utali wa Michezo”
Imetolewa na:
UTAWALA
IBF/ AFRIKA

RAIS WA ZANZIBAR AHUDHURIA DHIFA YA PAMOJA NA VIJANA WA HALAIKI ZANZIBAR.

0
0
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu mbalimbali pamoja na Viongozi wa Vijana wa Halaiki waliohudhuria katika Dhifa ya Pamoja ilioandaliwa hapo Bwawani Hotel Zanzibar.

Viongozi wa Halaiki waliohudhuria katika dhifa ya pamoja na Rais wa Zanzibar ilioandaliwa hapo Bwawani Hotel Zanzibar. 


Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame akitoa hotuba ya Shukurani kwa niaba ya Rais kwa Vijana wa Halaiki pamoja na Walimu wao kwa kufanikisha Sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar,hafla iliofanyika Bwawani Hotel Zanzibar. 


Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akipata Chakula katika Dhifa maalum alioiandaa kwa ajili ya kuwapongeza na kula chakula pamoja nao Vijana wa Halaiki na walimu wao waliofanikisha katika Sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar,hafla iliofanyika Bwawani Hotel Zanzibar.
 


-Vijana wa Halaiki wakipata Dhifa Maalum ilioandaliwa kwa ajili ya Kuwapongeza kwa kufanikisha Sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar,hafla iliofanyika Bwawani Hotel Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI ALI-MAELEZO ZANZIBAR.

Evans Bukuku's Comedy Club - 29th January 2013

0
0



RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA APRM NA AU JIJINI ADDIS ABABA

0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa nane toka kulia, akiwa na viongozi wenzake katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa leo Januari 27, 2013.PICHA NA IKULU
 Rais  Jakaya Mrisho  Kikwete  na ujumbwe wake akitoka nje ya ukumbi baada ya kuhutubua  mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Wanachama wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) baada ya kuwasilisha ripoti ya Tanzania usiku wa kuamkia leo Januari 27, 2013 katika makao makuu ya nchi za Afrika jijini Addis Ababa.


Rais  Jakaya Mrisho  Kikwete akihutubua  mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Wanachama wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) baada ya kuwasilisha ripoti ya Tanzania usiku wa kuamkia leo Januari 27, 2013 katika makao makuu ya nchi za Afrika jijini Addis Ababa.

WANAFUNZI WA DARASA LA MUZIKI LA THT WAHITIMU MASOMO YAO

0
0
Wanafunzi wa darasa la muziki pamoja na Sauti (vocal) wakiwa na walimu wao mara baada ya kupata vyetu vya vya kuhitimu masomo yao.
Wanafunzi wa darasa la muziki pamoja na Sauti (vocal) wakiwa katika picha ya pamoja.

Mwalimu wa Tanzania House of Talent (THT) ya jijini Dar es Salaam, Michael Nkya akitoa cheti cha kumaliza masomo ya muziki pamoja na Sauti (vocal) Ishengoma Mwombeki ambaye ni mlemavu wa macho, masomo hayo yaliyokuwa yakitolewa na THT kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana  juu ufahamu wa Muziki. Darasa hilo la muziki pamoja na Sauti (vocal) lilikuwa likiendeshwa kila mwenzi na Tanzania House of Talent (THT) jijini Dar es Salaam. Katikati ni mwalimu Aidan Magawa ambaye alikuwa akifundisha jinsi ya kutumia Vyombo vya Muziki (Music Instruments). Sherehe hiyo ya kuwaaga ilifanyika THT jijini Dar Jana.
Mwalimu wa Tanzania House of Talent (THT) ya jijini Dar es Salaam, Michael Nkya akitoa cheti cha kumaliza masomo ya muziki pamoja na Sauti (vocal) kwa mwanadada Neema Aggrey, masomo hayo yaliyokuwa yakitolewa na THT kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana  juu ufahamu wa Muziki. Darasa hilo la muziki pamoja na Sauti (vocal) lilikuwa likiendeshwa kila mwenzi na Tanzania House of Talent (THT) jijini Dar es Salaam. Katikati ni mwalimu Aidan Magawa ambaye alikuwa akifundisha jinsi ya kutumia Vyombo vya Muziki (Music Instruments).
Mwalimu wa Tanzania House of Talent (THT) ya jijini Dar es Salaam, Michael Nkya akitoa cheti cha kumaliza masomo ya muziki pamoja na Sauti (vocal) kwa mwanadada Gracesandra Isaac, masomo hayo yaliyokuwa yakitolewa na THT kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana  juu ufahamu wa Muziki. Darasa hilo la muziki pamoja na Sauti (vocal) lilikuwa likiendeshwa kila mwenzi na Tanzania House of Talent (THT) jijini Dar es Salaam. Katikati ni mwalimu Aidan Magawa ambaye alikuwa akifundisha jinsi ya kutumia Vyombo vya Muziki (Music Instruments).
Mwalimu wa Tanzania House of Talent (THT) ya jijini Dar es Salaam, Michael Nkya akitoa cheti cha kumaliza masomo ya muziki pamoja na Sauti (vocal) Guan Fabian, masomo hayo yaliyokuwa yakitolewa na THT kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana  juu ufahamu wa Muziki. Darasa hilo la muziki pamoja na Sauti (vocal) lilikuwa likiendeshwa kila mwenzi na Tanzania House of Talent (THT) jijini Dar es Salaam. Katikati ni mwalimu Aidan Magawa ambaye alikuwa akifundisha jinsi ya kutumia Vyombo vya Muziki (Music Instruments). Sherehe hiyo ya kuwaaga ilifanyika THT jijini Dar Jana.
Mwalimu wa Tanzania House of Talent (THT) ya jijini Dar es Salaam, Michael Nkya akitoa cheti cha kumaliza masomo ya muziki pamoja na Sauti (vocal) Hawa Lipapapa, masomo hayo yaliyokuwa yakitolewa na THT kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana  juu ufahamu wa Muziki. Darasa hilo la muziki pamoja na Sauti (vocal) lilikuwa likiendeshwa kila mwenzi na Tanzania House of Talent (THT) jijini Dar es Salaam. Katikati ni mwalimu Aidan Magawa ambaye alikuwa akifundisha jinsi ya kutumia Vyombo vya Muziki (Music Instruments).
Mwalimu wa Tanzania House of Talent (THT) ya jijini Dar es Salaam, Michael Nkya akitoa cheti cha kumaliza masomo ya muziki pamoja na Sauti (vocal) Ramadhani Rashid, masomo hayo yaliyokuwa yakitolewa na THT kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana  juu ufahamu wa Muziki. Darasa hilo la muziki pamoja na Sauti (vocal) lilikuwa likiendeshwa kila mwenzi na Tanzania House of Talent (THT) jijini Dar es Salaam. Katikati ni mwalimu Aidan Magawa ambaye alikuwa akifundisha jinsi ya kutumia Vyombo vya Muziki (Music Instruments). Sherehe hiyo ya kuwaaga ilifanyika THT jijini Dar Jana.

UN YAENDESHA MAFUNZO KUHUSU SHUGHULI ZA UNDAP NA HAKI ZA BINADAMU KWA WAANDISHI WA HABARI VISIWANI ZANZIBAR

0
0

Afisa habari ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama akieleza nia ya Umoja wa Mataifa Tanzania kuendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa Visiwani Zanzibar juu ya Haki za binadamu na jinsi Mpango wa msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP) unavyoshirikiana na Serikali ya Zanzibar katika maeneo matatu muhimu ambayo ni Uchumi, Kupunguza umaskini na Utawala na uwajibikaji. Semina hiyo imefanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View visiwani Zanzibar.

Mratibu wa FAO Ofisi ya Zanzibar Ali Haji Ramadhan akitoa hotuba ya makaribisho katika mkutano na waandishi wa habari wa Visiwani Zanzibar ambapo amesema wanatarajia kupata mawazo mengi zaidi ya kujenga kutoka kwa waandishi ambapo yatasaidia Umoja wa Mataifa pamoja na Serikali kuihudumia nchi kwa upeo wa juu zaidi.

Mwakilishi wa mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Zanzibar Anna Senga akizungumza na waandishi wa habari wa visiwani Zanzibar kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wao kama UN katika kutekeleza hoja za mipango wa maendeleo (UNDAP) kutokana na kuchelewa kupewa majibu na uchelewashaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo ambapo ameelezea Mpango Mkakati wa UNDAP visiwani Zanzibar ikiwemo kutoka ufafanuzi wa mafanikio pamoja na changamoto zinazoukabili mpango huo.

Amesema mpango huu ni wa pamoja kwa ajili ya Tanzania unaendena na mafanikio ya malengo ya maendeleo ya kimataifa ambapo unachukua nafasi ya program za pamoja na miradi mingi inayodhaminiwa na UN chini ya Model ya misaada ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kwa mpango wa kazi moja ulioshikamana kwa ajili ya mifuko ya fedha, program na wakala zote za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ya siku moja wakimsikiliza Afisa Mawasilano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu.

Katibu wa Chama cha wanasheria wanawake Zanzibar Hamisa Mmanga Makame akitoa somo katika mafunzo hayo ambapo amezungumzia masuala ya Haki za Binadamu, umuhimu wa kuzingatia jinsia na wajibu wa vyombo vya habari katika kuleta usawa.

Afisa Mipango mwandamizi wa shirika la kazi duniani (ILO) Anthony Rutabanzibwa ambapo amevipongeza vyombo vya habari vya Afrika Mashariki kwa kutoa kipaumbele katika habari zinazohusu haki za binadamu na kuwataka waandishi kuzingatia zaidi habari za kiuchunguzi ili kuwa na uhakika zaidi na yale wanayoaandika ikwemo kujua chanzo cha habari unayoitoa.



Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin akielezea mada ya umuhimu wa mawasiliano kwa maendeleo na kuwataka wamiliki wa vyombo vya habari na serikali kwa ujumla kubadilisha sera zinazosimamia vyombo hiyo ili ziweze kutoa fursa kwa waandishi kuwa huru katika uandishi na kuripoti habari bila kubanwa.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zanzibar Hassan Khatibu, Mratibu wa FAO Ofisi ya Zanzibar Ali Haji Ramadhan, Mwakilishi wa mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Zanzibar Anna Senga, Mwezeshaji wa mafunzo hayo mwandishi mkongwe Salim Said Salim na Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin.

Rais wa Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Kenneth Simbaya akitoa maoni yake kuhusiana na nini kifanyike katika kuboresha tasnia ya habari ambapo ameshauri mafunzo kuendelea kutolewa si tu kwa waandishi pia kwa wamiliki wa vyombo vya habari.

Pichani Juu na chini ni baadhi ya waandishi ws habari wa visiwani Zanzibar wakichangia mawazo yao wakati wa mafunzo hayo.

Afisa mipango wa Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.

Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya siku yaliyoendeshwa na Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar.

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akijadili jambo na wafanyakazi wenzake wakati wa mafunzo hayo.

FAREWELL TO AMBASSADOR MWANAIDI MAAJAR

0
0

FAREWELL TO AMBASSADOR MWANAIDI  MAAJAR

                                     Tribute to her historical appointment and legacy  


                            BY MOHAMED MATOPE, Washington DC, January 28, 2013

  
Two and a half years ago, President Jakaya Kikwete made history by appointing seasoned lawyer, Mwanaidi S. Maajar, Tanzania’s first female ambassador to the United States. Ambassador Maajar’s pick surprised many observers. People did not doubt her capabilities but it had not been done in the more than 50 years that Tanzania and the US have maintained diplomatic relations.


Despite the fact that she had been High Commissioner to Britain before coming to Washington DC, many questioned whether a Tanzanian woman could effectively perform the duties of ambassador in this citadel of global power play. To say the least, expectations were low founded equally on baseless fears.


But as Mrs. Maajar’s tour of duty winds up, it is imperative that we put in perspective what this formidable woman has accomplished in her rather short stay here and, by extension, the fundamental impact of her presence on the Tanzanian community here and in the US generally. First and foremost, Mrs. Maajar is a highly talented and skilled diplomat of our time.


What has been most striking about her tenure of office is how effective on the job she has proven to be, improbable as it once seemed. She transformed the ambassador’s role as radically as President Barack Obama changed the American presidency. Before her arrival, the ambassador’s office was regarded as elitist post and generally detached from mainstream life and society.


That negative perception changed completely as she connected outright with the people and the community at large to the extent that she became, and was seen, as part of the community itself. She is a dynamic and likeable leader, who leaves behind unmatched inspiration as her biggest legacy in this country where ambitions can be easily lost in the fast paced lifestyle of doing anything, from politics to scientific inventions.


She will be remembered more as a bridge builder and unifier of what was once a highly fragmented community here in America. Before she came, the general perception was that the embassy was a separate entity (not a mission for the people) and therefore, had no business linking up with the Diaspora community. That perception was debunked under her tenure of office.



We also witnessed the transformation of the ambassador’s persona from the traditional diplomatic aloofness to that of a more engaging and role model organizer for results. Through her untiring efforts, the society of Tanzanians living in Washington DC, Maryland and Virginia (DMV) and other organizations of Tanzanians in the United States were strengthened and contributed markedly to the reawakening of our cultural and national identity as Tanzanians living abroad.  


Also, Mrs. Maajar has arguably done more to integrate our community than any of her predecessors. We should remember that Mrs Maajar around during the 2010 general election, which was characterized by hyper partisanship and polarization of the national agenda  here in United States as well as in Tanzania.  Mrs. Maajar had all the reasons to also advance partisan actions that would have split our community even further. Instead, she steadfastly remained non-aligned and chose to tread the unifying path. As a result, the Tanzanian community in the United States emerged more integrated today than it was three years ago.


After two and a half years of meritorious service through her unrelenting efforts, she has succeeded immeasurably to unify our community, shaped as much by her experience as a lawyer, as well her skills as an administrator. We measure our leaders’ greatness by their ability to do big things, Mrs. Maajar was able to organize our community and overcome huge obstacles even in the face heartbreaking despair. She simply never gave up even when matters appeared to be hopelessly out of hand. 


Aisha Damji, a Tanzanian business woman in California, said there was a reason the community held seemingly endless farewells parties for Mrs Maajar. “She is people’s person,” said Aisha. “Her performance as ambassador was spectacular. All Tanzanian women should be proud of her, and now, the pressure is on our leaders to appoint another female ambassador,” she concluded and lobbied in typical American style. 

Huawei pledges more support to development of ICT in Tanzania

0
0

The Huawei Technologies Tanzania Company Limited PR Manager Peter Jiang (second right) hands over five computers to the Matimbwa Secondary School Head Teacher Hamza Msagule (second left) being part of the company’s ‘ICT Star Program for Tanzania Education’. Looking on at the right is the Huawei General Director Kennth Luo Channel. 

HUAWEI Technologies Tanzania company Limited through, its ‘Huawei ICT Star Program for Tanzania Education’ has pledged to render more support to development of conducive learning environment for ICT in Tanzanian schools in a bid to enable Tanzanian students move in line with the globalizing world.

The ICT program was launched in November last year and seeks to support primary & secondary schools as well as universities, to develop ICT interests, which will contribute to the development of ICT industry in Tanzania.

Speaking during the official handover of 15 computers in Dar es Salaam, pledged by the company last year, the Huawei PR Manager Peter Jiang said the company is committed to improving more schools’ infrastructure and studying environment gradually through “Huawei ICT Star program”. “We have already rendered support to three different schools as part of this programme. We may consider bringing on board sponsorship of ICT students at university level to enrich this programme,” he added.

Jiang said ICT if well utilized can not only help in stimulating social and economic development but is also a powerful tool for extending educational opportunities, both formal and non-formal. "In order to compete with the rest of the world, one needs to be computer literate. Our donation to schools will be a breakthrough and a new beginning in ensuring that school going children are computer literate, from the very beginning, we hope the students can touch the computers and use it, which will help in disseminating  computer and ICT basic knowledge transfer to Tanzania students" he added.

Hamza Msagule, the Matimbwa Secondary School Head Teacher located in Bagamoyo while receiving the computers on behalf of his school pledged to make good use of the computers so as to benefit future generations.

“I pledge to take good use of the computers. We have teachers to teach the students the basic programs. In today’s world one has to be computer literate. Thanks very much to Huawei’s support. I know they are a great telecommunication company in the world,” he said. Huawei Technologies towards the end of last year donated a total of USD 30,000 to three schools in Tanzania two in Mainland Tanzania and one in Pemba.

Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yatembelea uwanja wa ndege wa kigoma

0
0





Meneja uwanja wa Kigoma Elipid Tesha,wa pili kuli akifafanua jambo kwa ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM),uliofanya ziara fupi ya kuukagua uwanja huo na kujionea ujenzi wake unavyoendelea kwa kasi,kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Mh Issa Machibya akishuhudia tukio hilo adhimu, na shoto ni  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM,Martin Shigela,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye, pamoja na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na 
Ujenzi ukiendelea.
Mafundi ujenzi wakipaka rangi sehemu ya barabara ya kurukia na kutua ndege mapema jioni ya leo.

Sehemu ya eneo ambalo linaendelea kupanuliwa ikiwa ni sehemu ya ongezeko ya marekebisho ya kiwanja hicho cha Kigoma
Pichani kati Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo akifafanua jambo mbele ya ujumbe wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa.
 Sehemu ya kuruka na kutua ndege ikiwa katika hutua ya mwisho mwisho,Kwa mujibu wa Meneja mradi wa kampuni ya Howard Humphrey,Bwa,Cleopa Mpembeni inayosimamia ujenzi wa uwanja huo ameeleza kuwa unatarajiwa kukamilika mnamo juni mwaka huu,ambapo kwa asilimia 80 maeneo mengi yatakuwa yamekwishakamilika.

Pichani kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa   Machibya,akimtambulisha  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana kwa baadhi ya wanachama wa CCM waliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot) kuwapokea,ambapo Mh Kinana na ujumbe wake waliwasili mapema leo jioni kuangalia maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje. 
Katibu wa NEC, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa (CCM),Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na wananchi wakiwemo wanachama wa CCM,waliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma mapema leo jioni walipokwenda kutazama maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho.
Pichani kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya,akipokea  Ujumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,ulioongozwa na  Katibu Mkuu wa Chama hicho,Ndg. Abdulrahman Kinana uliofika kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma (Kigoma Airpot),kuangalia maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho ambacho kinategemewa kwa asilimia kubwa na wakazi wa Kigoma,ndani na nje.UJumbe huo umewasili mapema leo kutoka jijini Dar kwa njia ya Treni ( reli ya kati),ambako wamekuja kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi.

MEYA JERRY SILAA AHIMIZA KUKAMILISHWA KWA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA PUGU KAJIUNGENI

0
0


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akitoa taarifa wakati akizindua Mradi wa Maji Pugu Kajiungeni ambapo amesema mradi huo unatokana na kisima cha maji chenye urefu wa mita 122 toka usawa wa ardhi. Mstahiki meya amesema kisima hicho kina uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita 60,000 kwa saa. Ameongeza kuwa mradi huo utakuwa na mtandao wa mabomba wa kilometa 9, vituo 25 vya kuchota maji, nyumba ya pampu, fensi pamoja na uzio.

Aidha amewataka wananchi wa maeneo husika ya Pugu Kajiungeni ni kuitunza miradi hii na kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili kuweza kufanikisha malengo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Pugu Emelda Samjela na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kassim Mjesa na Kulia ni Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd inayoshughulikia mradi huo Method Mlay.

Diwani wa kata ya Pugu Kajiungeni Emelda Samjela akizungumza na wakazi wa Kata yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akisani kitabu cha wageni wakati wa Halfa fupi ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni. Kushoto ni Diwani wa kata ya Pugu Kajiungeni Emelda Samjela.

Pichani Juu na Chini ni baadhi ya wakazi wa Kata Pugu Kajiungeni watakaofaidika na mradi huo wakimsikiliza mstahiki Meya Jerry Silaa (hayupo pichani).

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akimkabidhi Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd Method Mlay (kulia) barua rasmi ya mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni unaotekelezwa kwa ushirikiano na wahisani /wafadhili wa Serikali ya Ubelgiji, Umoja wa Ulaya (EU), Serikali ya Tanzania, Halmashauri ya manispaa ya Ilala na wafadhili wengine mbalimbali. Anyeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Kassim Mjesa.

Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd Method Mlay (kulia) akitoa neno la shukrani baada Mstahiki Meya kumkabidhi barua rasmi ya ujenzi wa mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni na kuahidi kutoa ajira kwa Vijana wa maeneo ya Pugu kuanza sasa mpaka mradi utakapokamilika.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akipongezwa na wakazi wa Pugu baada ya kuzindua rasmi mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni ulioanza kubuniwa rasmi mwaka 2011.

Sehemu ya wakazi wa Pugu Kajiungeni waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo utakaochukua miezi Sita kukamilika na kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa maeneo hayo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa sita kushoto) akikagua sehemu ya mradi huo kilipojengwa kisima chenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita elf 60,000 kwa saa.

Muonekano wa Kisima hicho.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa nne kushoto) na Diwani wa Kata ya Pugu Kajiungeni Emelda Samjela katika picha ya pamoja na viongozi wa kata hiyo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza na vyombo vya habari ambapo amesema mradi huo wa maji wa Pugu Kajiungeni uhahudumiwa na tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita 140,000 lilipo katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto na matenki mnegine ya maji yenye ujazo wa lita 45,000 na 100,000 ambayo yanapatikana Pugu Kajiungeni karibu na Zahanati ya Pugu.

Amefafanua kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imechangia kiasi cha Shilingi 378,000,000 na kiasi kingine kinachobaki kinatolewa na Serikali Kuu pamoja na wahisani. Mradi wote utagharimu kiasi cha shilingi 1,024,000,000/=.

Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa kata ya Pugu Kajiungeni Nuru Daniel akitoa shukrani zake za pekee kwa Serikali ya awamu na uongozi kwa kutekeleza ilani za Chama ikiwemo kuwapatia maji wakazi wa Pugu Kajiungeni.

UMOJA WA WANATAALUM WA KIISLAM TANZANIA (TAMPRO) NA WANAZUONI WA KIISLAMU (HAYAT-ULAMAA) WAHAMASISHA UTEKELEZAJI WA NGUZO YA ZAKAT UL-MAAL

0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu (Hayat-ulamaa) Shk. Suleiman Amran Kilemile Akitoa Nasaha Juu ya Umuhimu wa Waislam Kiimarisha utekelezaji wa Ibada ya Kutoa Zakat kwa Makundi yaliyotaja Katika Qur'an kwani ndio Njia rahisi ya Kuimarisha Uchumi wa Jamii na Nchi kwa Ujumla.  
 
 Kijana Mfanyabiashara Ndogo Ndogo Ambae amekuwa akitoa Zakat mara kwa Mara akitoa ushuhuda jinsi gani utoaji wa Zakat Umemsaidia kulinda na Kukuza Biashara yake katika Mkutano wa Ugawaji Zakat.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Baytul -ulmaal (Charity Fund) Tanzania akisisitiza Umuhimu wa Matajiri na Wasomi wa Kiislam Kushiriki Kikamilifu kuimarisha Mfuko huo kwa Maslahi ya Ustawa wa Jamii hasa Masikini na wenye mahitaji maalum ili kuleta uiano wa kimaendeleo.
 Baadhi akina Mama wakifuatilia kwa Makini Mada Juu ya Utekelezaji wa Ibada ya Zakat ambayo ni Nguzo Muhimu katika dini ya Kiislam yenye lengo la kupambana na Umasikini ndani ya Jamii ya eneo husika.
   Kijana Mwanafunzi Yatima anayejiunga na Shule ya Serikali Akipokea Tshs 100,000 Kutoka kwa Sheikh Suleiman Kilemile kama Fungu la Zakat lililotolewa Katika Ukumbi wa Lamada Ilala. Mfuko wa Baytul –ul maal Unaendeshwa pamoja kati ya Wanataalum wa fani mbali mbali za kimazingira pamoja na Wanazuoni wa Kiislam kukuzanya Zakat pamoja na Waqfu kwa manufaa ya Jamii ya Kiislam.
.        Waumini wa Kiislam wakimsikiliza Shk Twaha Bane wakati akieleza Umuhimu wa Waislam kuitekeleza Nguzo ya Zakat kwani inaleta Upendo, Amani na Uimara wa Biashara kwa Mtoaji na Anayepokea.

Malaika Orphanage Foundation yakaribisha wadau kusaidia kituo

0
0
 Wikiendi hii Mkurugenzi na muasisi wa kituo cha kulelea watoto yatima,kinachoitwa Malaika Orphanage Foundation,  Rahma Manji(Pichani kushoto) alipokea msaada kutoka kwa mwambata wa jeshi kutoka nchini Ujerumani, Bw Abel Gunta(Pichani kulia) ambaye aliguswa na moyo wa mwenyekiti huyo aliyemua kuanzisha kituo cha kusaidia watoto baada ya yeye mwenyewe kujikuta akilea watoto wengi wa ndugu zake kwa sababu mbali mbali takriban miaka 1o iliyopita
 Abel ambaye aliambatana na mkewe walitoa vifaa vya zahanati vikiwemo vitanda na madawa ambavyo kwa ujumla wake, vimegharimu fedha za kitanzania shilingu milioni 10. Hapa Gunta akimkabidhi Bi Manji msaada wa madawa huku mkewe Nana, ambaye aliambatana naye akishuhudia
 Vaeni watoto...
 Gunta pia alikabidhi fulana ambazo zitatumika kama sare baada ya masomo kwa watoto hao, hapa akishiriki katika kuwakabidhi watoto wenyewe. Kituo hicho kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani kina watoto 61 wanaoishi hapo huku 48 wakiwa wanasoma za msingi zilizopo wilayani Mkuranga, saba shule ya Sekondari na waliobaki wakiwa hawajafikia umri wa kwenda shule
Hii ni picha ya pamoja ya wanakituo
Chuo kinakabiliana na changamoto mbali mbali katika kipindi hiki ambacho bado hawajakuwa na miradi ya kujiendesha, vitu kama mavazi, chakula, ada za watoto ambao wanasoma nje ya Kituo, na waalimu wa kujitolea kuwafundisha watoto masomo ya ziada baada ya saa za masomo.

Kufuatia hilo unakaribishwa kutembelea Kituo na kujionea mwenyewe hali halisi na kutoa chochote utakachojisikia iwapo utahamasika. namba ambayo unaweza kupiga pia ili kupata maelekezo zaidi ni  +255 655 786 011 
Unaweza kusaidia wanakituo hawa kupitia akaunti ya KBC namba 3300828357

gazeti lako la dira liko sokoni sasa kwa sh 500/= tu

0
0



TIGO KUFANYA DROO KUBWA YA PROMOSHENI YA SMARTCARD

0
0

Dar Es Salaam Tanzania, Januari 28, 2013: Tigo Tanzania leo imetangaza kuwa itafanya droo kubwa ya promosheni yake ya Smartcard ambapo washindi 43 watabahatika kujishindia zawadi  mbali mbali  za kusisimua ikiwemo zawadi kuu ambayo ni tiketi ya bure ya kwenda na kurudi Madrid Uhispania pamoja na kulipiwa gharama zote za safari kwenda kutizama  mechi  ya soka kati ya Real Madrid na FC Barcelona.

Droo hii ambayo imepangwa kufanyika Januari 30, 2013 ni mwendelezo wa  droo za promosheni ya Smartcard ambazo zinaendelea kufanyika  kila mwezi, robo mwaka,  na kila mwaka. Smartcard promosheni ilizinduliwa Septemba 2012 hususan kwa ajili ya wateja wa Tigo ambao wanatumia smartphones.

Meneja  wa Tigo Internet Broadband, Bw.Tito Kafuma alisema "Mbali na zawadi kuu ya droo hii, washindi 42  watabahatika  kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo tiketi 12 za sinema, tiketi 12 za klabu, tiketi 12 za kuangalia mechi za mpira kwenye klabu ya hapa nchini, vocha 3 za kununua bidhaa mbalimbali na vocha 3 za chakula cha jioni.” Aliongeza kuwa “mshindi wa kwanza  wa droo hii atajishindia tiketi ya bure ya kwenda na kurudi Madrid Uhispania na kulipiwa gharama zote za safari kwenda kuangalia  mechi  ya soka kati ya Real Madrid na FC Barcelona"


"Promosheni  hii ilizinduliwa baada ya Tigo  kutambulisha kwenye soko la Tanzania vifurushi vya "Smartcard "  vilivyobuniwa hususan kwa ajili ya watumiaji wa simu za Blackberry,  Android na Iphone mwaka jana baada ya kuona upendeleo wa kutumia simu za smartphone ukiongezeka miongoni mwa wateja wetu." alisema William.


Mpinga, meneja  wa brand ya Tigo. "Bidhaa hii inapatikana kwa wateja wetu wa zamani na wapya, na inasukumwa vizuri sana na vifurushi vyetu vipya vya intaneti. Kama kiongozi wa ubunifu wa bidhaa za simu Tanzania, Tigo inahakikisha kuwa wateja wake wote wanapata ofa za huduma na bidhaa zenye thamani zaidi ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya kipekee ya wateja wake wote". Alihitimisha Bw. Mpinga.


Kifurushi cha "Tigo Smart" kiilizinduliwa ili kuwawezesha watumiaji wa smartphone kufurahia huduma za Internet kupitia simu zao kwa bei nafuu ya Tsh. 30,000 tu kwa mwezi. Kupitia huduma hii ya smartcard,  wateja wanapata intaneti ya bila kikomo pamoja na muda wa maongezi wenye thamani ya Tsh 30,000 ambayo inaweza kutumika  kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi  kwa wateja wa Tigo kwa Tigo, na mitandao mingine yeyote Tanzania. Kushiriki katika shindano hili, mteja alitakiwa awe amejiunga na kifurushi cha Smartcard na ametumia huduma hii kwa miezi mitatu mfululizo na vilevile awe amejiunga na jamii ya smartcard kupitia www.tigo.co.tz/smartcardcommunity.

Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images