Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

hapatoshi leo leo ccm kirumba,ni Yanga dhidi ya black leopards ya afrika kusini

$
0
0

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Ernest Brandts amesema timu yake itafanya vizuri katika mechi ya marudiano ya kirafiki dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini niliyopangwa kufanyika mapema jioni ya leo ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba mjini Mwanza.

Brandts alisema wachezaji wake wote wamefikia kiwango kile anachotaka na mchezo huo utakuwa muhimu sana kwake kwani ni wa mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Alisema kuwa Black Leopards ni timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.

“Ni mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa ni kipimo kikubwa kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wachezaji wangu wana viwango vizuri sana kwa sasa na naamini makosa yaliyofanyika katika mechi ya kwanza hawatayafanya tena,” alisema Brandts.


Msemaji wa Klabu Yanga, Baraka Kizuguto alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani mashabiki wa Mwanza.

Kizuguto alisema kuwa Yanga haitakuwa na mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo ndiyo nafasi yao ya kuwaonesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa Mwanza nini wamekipata kutoka Uturuki.

“Tuna mashabiki wengi sana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki na wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto.

Flaviana Matata ashinda tuzo ya mwanamitindo bora wa Afrika 2012

$
0
0

MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara kimataifa baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).
Tuzo hiyo utolewa kwa wanamitindo ambao bado wanailetea sifa Afrika kimataifa na Flaviana amekuwa katika chati ya juu. Mwaka jana Desemba,  Flaviana alishinda tuzo nyingine  ya uwanamintindo bora kutoka kwa diaspora ya Waafrika.
Flaviana kwa ambaye kwa sasa  anaishi na kufanya kazi ya uanamitindo New York nchini Marekani kupitia shirika la Wilhelmina Models, mpaka sasa ameweza kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na umahiri wake katika maonyesho ya mavazi.
Tangu ashinde taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana amekuwa aking’ara katika kona zote za dunia na hasa baada ya kumaliza katika nafasi ya sita katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, huku Tanzania ikishiriki kwa mara ya kwanza.
Ameweza kushiriki katika maonyesho ya mavaz mengi Ulaya na Amerika huku akitoa misaada mingi kwa Watanzania wenzake ambao wamekuwa na ndoto ya kufika mbali katika fani hiyo.
Kwa sasa Flaviana anaendesha taasisi yake, Flaviana Matata Foundation ambayo inasomesha watoto wa kike 16 na mwaka jana alitoa msaada wa vifaa vya kuokoa maisha kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba huku ikiwa kumbukumbu ya kifo cha mama yake mzazi katika ajali hiyo ya mwaka 1996.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa wamejisikia faraja sana kwa kumvumbua mwanamitindo huyo ambaye kwa sasa anashika chati ya juu Tanzania na nje ya nchi.
Maria alisema kuwa Flaviana amedhihirisha ubora wake na mpaka sasa amepitiliza kiwango cha kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake, ndoto ambayo alikuwa nayo muda mrefu.

mpya kutoka bbc-dira ya dunia

$
0
0
Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakipita chini ya bango la BBC mapema leo mchana maeneo ya barabara ya Mwaloni

tumekuwa watu wa kudharau kila jambo sijui nani alaumiwe.?!

ukarabati unafanyika bustani ya jiwe la bismaki -jijini mwanza

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATOA MAONI KWA TUME YA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA MPYA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya, Jaji Joseph Sinde Warioba, wakati tume hiyo ilipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuchukua maoni yake binafsi ikiwa ni sehemu ya kuchangia maoni ya katiba mpya. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati akitoa maoni yake kwa Viongozi wa Tume ya katiba mpya, iliyofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo ikiwa ni sehemu ya jukumu la tume hiyo la kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa maoni ya Katiba mpya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati akitoa maoni yake.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya, Jaji Augustino Ramadhan,  wakati Tume hito ikiondoka Ikulu baada ya kupokea maoni ya Mhe. Makamu leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa tume ya Kukusanya maoni ya Katiba Mpya, baada ya mazungumzo yao ya kupokea maoni yaliyofanyika leo Januari 23, 2013, Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
*******************************************
*MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ATOA MAONI YAKE KWA TUME YA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA MPYA JANUARI 23, 2013, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na ujumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Agostino Ramadhan. Mheshimiwa Makamu wa Rais amepata fursa ya kukutana na Tume hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Warioba kabla ya kumruhusu Mheshimiwa Makamu Wa Rais kutoa maoni yake, alimuelezea namna tume hiyo inavyofanya kazi na namna zoezi zima la kukusanya maoni ya mtu mmoja mmoja lilivyofanyika na kisha akaeleza kuwa, tume hiyo inaendelea na zoezi hilo kwa kukutana na makundi maalum sambamba na mtu mmoja mmoja kufuatia umuhimu wa hoja ambazo tume inakutana nazo na hivyo kuhitaji ufafanuzi. 

Katika muktadha huo, Jaji Warioba sambamba na kumpa fursa ya kuchangia maoni yake mengine anayopenda alimtaka Mheshimiwa Makamu wa Rais kujikita zaidi katika suala la Muungano kufuatia yeye kuwa na uzoefu wa kiuongozi katika serikali zote mbili yaani ya Muungano sambamba na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumzia suala la Muungano Makamu wa Rais Dkt. Bilal ameieleza Tume kuwa yeye ni muumini wa Muungano wa serikali mbili na kwamba haoni sababu ya kubadili mfumo uliopo kwa kuwa umeipatia tija nchi yetu na kuipambanua kama nchi yenye muungano wa mfano katika dunia. 

Pia alifafanua kuwa mfumo wa serikali mbili  umesaidia kujenga na kudumisha udugu, amani na utulivu baina ya wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani kwa kipindi cha miaka 49 sasa.

Tanzania imechangia kitu kikubwa katika historia, kudumisha Muungano wa mfumo wa serikali mbili kati ya nchi mbili, kubwa na ndogo, jambo ambalo kwa nchi nyingine za Afrika wameshindwa. Kumekuwepo na nchi nyingi ambazo ziliungana na kushindwa kudumu kama tulivyo sisi. Hatuna haja ya kujifunza mfumo mpya wakati tulionao umeweza kudumu, « alisema.

Katika ujumbe wa tume uliofika kuchukua maoni ya Mheshimiwa Makamu wa Rais ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Profesa wa Sheria Palamagamba Kabudi, Ndugu Simai Said, Ndugu Assa Rashid, Ndugu Sasmir Kyuki, Ndugu Salum Athuman, Ndugu Juma Mzalau na Mratibu wa Tume hiyo Ndugu Ramadhan Kailima.

halmashauri ya jiji la mwanza mbona sato wenu hana maji ya mbwembwe..!?

$
0
0
Pichani ni mfano aina ya samaki Sato (anayepatikana jijini Mwanza),aliyeko kwenye moja ya kipita shoto cha jiji la Mwanza,ambapo hapo awali Sato huyo alikuwa akiwavutia watu wengi kwa staili yake ya kutema maji mdomoni,ilipelekea watu kibao kwenda hata kupiga picha maeneo hayo,ingawaje mpaka sasa wapiga picha wapo wanakula vichwa ado ado,lakini si kama vile awali  watu walikuwa wakifurika na wengine kujongea tu hapo kushangaa shangaa ili mradi tu,na palikuwa pako bize kweli.lakini nimepita mchana wa leo daa pamechoka kweli kweli,Sijui halmashauri ya jiji ilikuwa ni nguvu za soda ama zile mbwembwe za awali tu.

yanga yadhihirisha ubabe wake kwa black leopards,yaifumua 2-1 ccm kirumba jijini mwanza.

$
0
0
 
Golikipa wa timu ya Black Leopards,Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.Picha na JICHIE BLOG-jijini Mwanza.
 Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
 Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.
 Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya saba.
 Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
 Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


 Baadhi ya mashabiki wa Mpira wakiwa wamepanga mstari kwa ajili ya kununu tiketi na kujionea kandanda safi kabisa kati ya timu ya Yanga na Black Leopards ya Afrika kusini.
 Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.
Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo,ambapo timu ya Yanga imetoka kifua mbele goli 2-1 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,mchezo huo umechezwa leo kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
 Mtanange ukikaribia kuanza.
 Kikosi cha timu ya Black Leopards.
 Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Ilikuwa ni patashika ngua kuchanika,mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete akiwatoka baadhi ya mabeki wa timu ya Black Leopards,Jerry alifanikiwa kufunga goli la pili mnamo dakika ya 54 kipindi cha pili.

  Nginja nginja tuu
 Makocha wakipongezana mara baada ya mpira kuisha.
 Sehemu ya Umati wa mashabiki wa timu ya Yanga.
 Mashabiki wakiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia uwanjani.

Vanessa Mdee: Mtangazaji anayefanya vizuri kwenye tasnia ya muziki

$
0
0

Mwaka huu umeanza na ingizo jipya kwenye tasnia ya muziki hpa nchini baada ya mwanadada Vanessa Mdee kutoa wimbo wake mpya unaofahamika kama Closer.

Mwanadada huyu, ambaye alishirikiana na Ommy Dimpoz kwenye wimbo wake wa Me and You mwishoni mwa mwaka jana, amewashangaza wengi kwa kipaji alichokionyesha katika wimbo wake wa Closer.


Vanessa ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio cha Choice FM lakini pia anafanya kazi na kituo cha luninga cha MTV, amejipatia umaarufu zaidi baada ya kuwa  mtangazaji wa kipindi cha kusaka vipaji cha Epiq Bongo Star Search.


Wimbo huo ambao umetayarishwa na waandaji mahiri wa muziki nchini, Hermy B na Pancho Latino, unamfanya Vanessa kuwa mmoja wa waimbaji wa kike wanaorajiwa kufanya vizuri. Hermy B na Pancho wanasifika kwa kufanya kazi na wanamuziki wakali kama AY, Chidi Benz na Nakaaya.

Wimbo wa Closer ulianza kuandaliwa miaka miwili iliyopita kabla ya Vanessa kuamua kuuachia rasmi wiki mbili zilizopita. Akiuzungumzia wimbo huo, Vanessa anasema ni mchanganyiko wa ‘Afro pop, RnB, Soul na Hip pop’.

Tokea wimbo huo umeachiwa rasmi wiki mbili zilizopita umeshika kwa kasi, kiasi ambacho wengi wanaamini ni mwanzo mzuri kwa mwanadada huyu.

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA NA BIASHARA YATEMBELEA VIWANDA VYA KONYAGI NA TBL DAR

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo (kushoto), ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara walipotembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), juzi katika Makao Makuu kampuni hiyo, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo,  Ahmed Salum na Mahamoud Mgimwa ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo.

 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wanachama na Mawasiliano wa CTI, Neema Mhondo akielezea jinsi Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilivyopandisha kiholela ada kwa kampuni mbalimbali kutoka sh. 400,000 hadi milioni 7 kwa mwaka.

 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda  na Biashara, Deo Sanga (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa,kuhusu utengenezaji wa konyagi kubwa wakati wa ziara ya kamati hiyo, kwenye kiwanda hicho, Dar es Salaam juzi.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji walipotembelea kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.


 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Mahamoud Mgimwa (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea kiwanda hicho Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji walipotembelea kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), ares SDalaam.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara wakitembelea sehemu ya mitambo ya kujaza bia kwenye chupa katika kiwanda cha TBL, Dar es Salaam
 Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania, Martine Calvin (kulia), akiwapatia maelezo kuhusu historia ya kiwanda hicho, wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, walipotembelea kiwanda hicho
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakipita eneo la matanki ya uchachuaji wa bia walipotembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), juzi katika Makao Makuu kampuni hiyo, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG


 Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu (kulia) akiwakaribisha wajumbe wa kamati hiyo kwenye chumba cha mikutano tayari kupata taarifa ya utendaji wa kampuni hiyo.
 Mkurugenzi wa Miradi Maalumu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Phocas Lasway akitoa maelezo jinsi ongezeko la kodi ya asilimia 25 lililovyoathiri uzalishaji wa kampuni hiyo.
 Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mgimwa akielezea jinsi watakavyoshirikiana na TBL kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazikabili kampuni hiyo.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo.
Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara kiwandani hapo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Used Desktop Computers, Printers, Badge Printers, Office Furniture for sale in Dar

$
0
0

1. HP Color LaserJet 2550L printer - $300

2. HP LaserJet 1022 printer (Black and White) - $250

3. HP LaserJet 4250DTN printer (prints only in Black) -$400

4. Minolta CS Pro 4000/5000 (prints only in Black) - $350

5. Canon - NP 1820 Copier/Printer ((prints only in Black) - $400

6. Fargo DTC525 Color Double-Sided ID Badge Card Printer (2 units) -$1250 each

7. Lot of 10 used Dell GX745 desktop computers with peripherals - $250 each

8. Office furniture: 15 used office chairs and 8 used PC desks - $1050 for whole lot

9. Various photo equipment and accessories (passport photo 
cameras, camera stand, photo screen) - $450

Please contact 0715 455 346 or computersDAR@gmail.com

MKUTANO WA MASHEHA KUHUSU UHIFADHI WA MITI YA MIKOKO

$
0
0

 Jeshi la Polisi na Mahakama za Zanzibar zimetupiwa lawama kali kufuatia kutowachukulia hatua watu wanaokamatwa wakiharibu mazingira kwa makusudi na kukata miti ovyo ikiwemo miti ya mikoko katika maeneo mbali mbali ya Kisiwa cha Unguja.

Wakizungumza katika mkutano wa Uhifadhi wa miti ya mikoko katika Ukumbi wa EACROTANAL, Masheha hao wamesema juhudi za kupambana na uharibifu wa mazingira zinakwamishwa na kurudishwa nyuma na Taasisi hizo mbili na imekuwa kikwazo kikubwa kwao.

Wamesema wanapowakamata watu wanaoharibu mazingira  huwapeleka katika vituo vya Polisi kwa lengo la  kuwapeleka mahakamani lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na  wachache wanaofikishwa mahakamani kesi zao hufutwa bila ya kupewa taarifa.

“Sisi Masheha tunasikitishwa na vitendo vya Jeshi la Polisi na Mahakama kwa kuwaachia watu wanaoharibu mazingira kwa makusudi na wamekua wakitishia maisha yetu”, alieleza Sheha wa Muyuni B, Ali Haji Mume na ameongeza kuwa

Kuna kila dalili ya vitendo vya rushwa katika taasisi hizo mbili na iwapo hali hiyo haitadhibitiwa  Visiwa vya Zanzibar vitakabiliwa na athari kubwa ya kimazingira katika miaka michache ijayo.

Sheha wa Shehia ya Shaurimoyo Muhammed Salum amesmea masuala mengi ya maendeleo yamekuwa yanakwama kutokana na tatizo la wananchi kutofuata sheria bila ya kutiwa hatiani.

Amezitaka taasisi zinazosimamia sheria kuacha muhali katika kuzitekeleza na kuwa tayari kushirikiana na wananchi katika kupambana na wanaokata miti ya kudumu ikiwemo Mikoko ambayo ni muhimili mkubwa  katika kuzuia mmongonyoko wa ardhi sehemu za fukwe.

Katika kufanikisha uzuiaji wa ukataji  mikoko ovyo, masheha wameshauri kukamatwa watu wanaojishughulisha na biashara ya kuuza bidhaa zinazotokana na miti hiyo ikiwemo majengo na mkaa na kuwahamasisha wananchi kupanda mikoko katika maeneo iliyopungua.


Aidha wametaka kuzuiwa misumeno ya moto isiingizwe Zanzibar kwani inaonekena kuwa tishio na adui mkubwa wa Misitu.

Akifungua mkutano huo Afisa Tawala wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohd Mahmoud, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, amesema uchafuzi wa mazingira na ukataji miti ovyo ni hatari kwa maisha ya binadamu na viumbe vyengine.

Amesema maji ya bahari yamekuwa yakipanda kwa kasi katika makaazi ya wananchi na kupunguza eneo la ardhi kutokana na kukatwa miti ya mikoko ambayo ni kinga kubwa ya kupunguza kasi ya maji.

Mkuu wa Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)  Gharib Hamza Muhammed amewaeleza washiriki wa mkutano huo kwamba Chuo hicho kimeanzisha Taasisi ya Kikanda yenye lengo la kuratibu na kutafiti masuala ya uhifadhi wa mazingira, bahari na Mali Asili zinazopatikana katika ukanda wa Mashariki ya Afrika.

Mkutano  huo wa siku moja uliowashirikisha Masheha na Wakuu wa Wilaya imeandaliwa na SUZA kwa kushirikiana na Ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara yake ya  Mazingira. 
                             
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR. 

Anusurika kichapo baada ya kudaiwa kula fedha za msiba.!

$
0
0
Mtuu mmoja ambaye jina lake halikujulikana mara moja,mkazi wa eneo la CCM Kirumba amenusurika kupewa kichapo cha nguvu mara baada ya kudaiwa kula michango ya marehemu rafiki yao,kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa mchango ulikusanywa kwa ajili ya marehemu aliyekuwa rafiki yao kiasi cha shilingi laki moja na nusu,lakini mtuhumiwa ambaye jina lake halikufahamika mara moja,alikabidhiwa fedha hizo kwa ajili ya kuziwakilisha kwa ndugu wa marehemu,lakini kwa bahati mbaya alikutana na rafiki yake ambaye alimshawishi wazitumie  fedha hizo,na kweli wakazitumia bila kuziwasilisha kwa ndugu wa Marehemu,ndipo aliponaswa na kupata kichapo kiduchu na kufikishwa mbele ya mikono ya sheria.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATEMBELEA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika Picha ya Pamoja na viongozi na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kukamilisha ziara yake.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (kulia)akimfafanulia jambo  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati)  kuhusu takwimu za Kilimo na uchumi. Kushoto kwa waziri Mkuu ni Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimweleza jambo Meneja wa Takwimu za Kilimo Bi. Joyce Urassa alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dar es salaam. 


 Mkuu wa Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu Vincent Mgaya (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu matumizi ya ramani  kupata Takwimu za Kilimo, Uchumi na Utalii.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu matumizi ya ramani katika upataji  na ukusanyaji wa takwimu mbalimbali zinazotumiwa katika masuala mbalimbali nchini kutoka kwa Kaimu Meneja wa Idara ya Mbinu  za Kitakwimu, Viwango na Uratibu Bw. Emilian Karugendo.
 Waziri mkuu Mizengo pinda (kulia katikati) akitazama takwimu mbalimbali alipotembelea kitengo cha ramani  akiwa na Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa (kushoto), Dkt. Albina Chuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (kulia).

Waziri mkuu Mizengo Pinda akipokewa na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Ofisi hiyo  jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
 

RAIS KIKWETE AMALIZA ZIARA YAKE YA KISERIKALI NCHINI UFARANSA LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemaliza ziara yake ya Kiserikali ya Siku tano nchini Ufaransa leo, Januari 23, 2013. Zifuatazo ni picha mbalimbali wakati akiagwa na mwenyeji wake, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Orly, Ufaransa.

Airtel yapunguza gharama za kupiga simu hadi senti 10 kwa sekunde

$
0
0
 Wataalamu wa Airtel kitengo cha masoko na Mawasiliano wakionyesha vipeperushi vitakavyotumiwa kuelimisha jamii juu ya punguzo hilo wakiwa kwenye bonge la pozi.
 Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania akifafanua jambo jinsi wateja wa Airtel watakavyofaidika na huduma ya punguzo la gharama za maongezi hadi senti 10 kwa sekunde
 Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Rwebugisa Mutahaba akifafanua  jambo jinsi wateja wa airtel watakavyoweza kufurahia punguzo nafuu ya la senti10 kwa sekunde baada ya dakika ya pili kuanzia leo
 Mfanyakazi wa Airtel kitengo cha ugavi akielezea kufuruahishwa na punguzo la kupiga simu kwa senti 10 baada ya dakika ya pili wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo leo ktk ofisi za Airtel dar. 
Baadhi ya wafanyakazi wa airtel wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa punguzo gharama za huduma ya kuongea yaa Airtel-airte hadi senti 10 kwa sekunde baada ya dakika ya pili


=====  ======= ====== =====


Airtel yapunguza gharama za kupiga simu hadi senti 10 kwa sekunde

*       Wateja kufurahia punguzo la asilimia 70 kupiga simu Airtel kwenda Airtel
*       Wateja wa Airtel kupiga simu kwa senti 10 tu kwa sekunde baada ya dakika mbili
*       Hakuna kujiunga, kila mteja wa malipo kabla ameunganishwa kufurahia viwango hivyo.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea na dhamira yake ya kutoa mawasiliano nafuu nchini kwa kutangaza punguzo la gharama za kupiga simu kwa lengo la kutoa fulsa zaidi kwa wateja wa Airtel wa malipo ya kabla kuendelea kufurahia huduma za Airtel

Sasa wateja wa Airtel watatozwa senti 10 kwa sekunde baada ya dakika ya pili ya maongezi kwa kupiga simu Airtel kwa Airtel.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Bw Sam Ellangallor alisema" tumepunguza gharama zetu za kupiga simu kwa asilimia 70 ili kuendelela kutoa huduma za kisasa, rahis na  za bei nafuu kuweza kukidhi mahitaji ya wateja wetu  sasa kupiga simu Airtel kwenda Airtel  ni kwa bei nafuu zaidi ambapo wateja wa Airtel watatozwa senti 10 kwa sekundi baada ya dakika mbili za awali pale watakapopiga simu Airtel kwenda Airtel. Hakuna sababu ya kushindwa kuwasiliana kwani Airtel inakuwezesha kuongea na familia na marafiki zako siku nzima bila kikomo kwa gharama nafuu ya senti 10 kwa sekunde"

"Tunafahamu huduma ya mawasiliano ni nyenzo kubwa kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wateja wetu, Hivyo ndio maana Airtel tunajitahidi sana kuwaletea wateja huduma zenye ubunifu wa hali ya juu ili kutoa unafuu wa mawasiliano zaidi.

Airtel bado tunaendlelea na mkakati wetu wa kupunguza gharama za mawasiliano ili kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma bora".aliongeza Elangallor.

Airtel hivi karibuni imepunguza gharama za kutuma sms kwa kupitia huduma yake ya SMS Kichizi ambapo ujumbe mfupi wa maneno kwenda mtandao wowote unatozwa shilingi moja mara baada ya kutuma ujumbe mfupi wa kwanza kwa shilingi 125 tu.

Akitoa maelezo zaidi ya huduma hiyo ya ya punguzo la gharama za mawasiliano Mkurugenzi  wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya "leo tumewawezesha wateja wake kuongea kwa senti 10 tu kwa sekundu na kutoa uhuru zaidi wa kuongea.Hakuna haja kwa mteja wa Airtel kujiunga na gharama hizi mpya nafuu, ukiwa unatumia Airtel tu moja kwa moja utakuwa umeunganishwa na huduma hii nafuu.

Akizungumza juu ya muda Mallya aliongeza hizi ni gharma za kudumu  zitakazopatikana nchi nzima

Airtel Tanzania ni kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora na nafuu kama Airtel money na huduma ya internet ya kasi ya 3.75G. Mwanzoni mwa mwaka huu Airtel  imetoa punguzo la gharama za ujumbe mfupi (SMS) ijulikanayo kama  SMS kichizi inayowawezesha wateja wakel kutuma kila SMS kwa shilingi 1 kwa siku

MTANDAO WA LIGI KUU WAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
7
Ofisa Masoko wa Benki ya ABC Evelyne Auguste akizindua mtandao wa http://www.ligikuu.co.tz/ utakaoandika habari za Ligi Kuu ya Vodacom, uliozinduliwa jana kwenye Hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam, kutoka kulia katika picha wanaoshuhudia tukio hilo ni Rodney Rugambo Meneja Masoko wa Push Mobille, Wawila Nzowa Meneja Maendeleo ya Biashara kampuni ya Lajann E Systems na kushoto ni Dennis Rauya Meneja wa Benki ya ABC tawi la Quality Centre jijini Dar es salaam na Salum Mwalimu Meneja Mawasiliano wa Vodacom
6
Kutoka kulia ni Rodney Rugambo, Wawila Nzowa, Evelyne Auguste na Dennis Rauya wakifuatilia maelezo ya mmoja wa wataalam wa mtandao huo wakati wa uzinduzi huo.
1
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika uzinduzi wa mtandao huo.
2
Ofisa Masoko wa Benki ya ABC Evelyne Auguste akitoa maelezo juu ya udhamini wa benki hiyo kwa mtandao wa Ligikuu.
3
Rodney Rugambo Meneja Masoko wa Push Mobile akizungumzia udhamini wa kampuni hiyo kwa mtandao huo ili kuboresha mchezo wa miguu hapa nchini 4
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salim Mwalim akiishukuru kampuni hiyo kwa kuanzisha mtandao huo ambao amesema utasaidia sana kutangaza mpira wa miguu nje ya nchi na kuwatangaza wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom.

udhamini wa masomo ya afya

TAMASHA LA MISS UTALII TANZANIA VIPAJI KUFANYIKA TAREHE 27.01.2012, IKONDOLELO LODGE KIBAMBA.

$
0
0

Washiriki wa Miss Utalii wakiwa katika Picha ya Pamoja

TAMASHA  LA  MISS UTALII VIPAJI KUFANYIKA TAREHE 27.01.2012, IKONDOLELO LODGE KIBAMBA.

Tamasha kubwa la vipaji litafanyika katika Ukumbi wa Ikondolelo Lodge  Hoteli ya Kitalii  Kibamba Jumapili hii, ambapo warembo zaidi ya Thelasini   wataingia katika kuonesha vipaji mbalimbali vikiwemo na, Kucheza ngoma, Kuimba, pamoja kuonesha mavazi mbalimbali ya Asilia.

Katika Tamasha hilo Maalum Mgeni Rasmi atakuwa Muheshimiwa Iddy Azan Zungu  Mbunge wa  Jimbo la kinondoni. Sambamba na Hayo Muheshimiwa Zungu atazindua tuzo Mbalimbali za Utalii Tanzania, kama Tuzo ya Mazingira, Tuzo ya Utamaduni, Tuzo ya Jinsia, wanawake na watoto, Tuzo ya Polisi Jamii, Tuzo ya Elimu ya Jamii, Tuzo ya Hifadhi ya Serengeti, Tuzo ya Mlima Kilimanjaro, Tuzo ya Michezo pamoja na Tuzo  zengine mbalimbali.

Viingilio katika Tamasha hilo vitakuwa kama ifuatavyo, V.I.P 20,000 , Watu wa kawaida 10,000 na watoto 5,000.
Tamasha litaanza kuanzia sa nane mchana na kuendelea.

Asante.
Fredy Tony Njeje
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano

breaking newwwzzz:WANANCHI WAVAMIA KITUO CHA POLISI kibiti ,wachoma nyumba za askari.

$
0
0

Kundi la wananchi waliojawa na gazabu wamevamia kituo cha Polisi Kibiti Wilayani Rufiji na kuleta vurugu kubwa kufuatia raia mmoja kufa kwa kile kilichodaiwa kipigo cha Polisi.

Chanzo chetu cha Habari kutoka Kibiti kinaipasha Father Kidevu Blog kuwa kijana aliyefariki kutokana na kipigo hicho ni Hamis Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili.

Habari zaidi zinapasha kuwa hivi sasa wananchi hao wanateketeza nyumba za Askari Polisi hao zilizopo jirani na kituo hicho, licha ya juhudi za Polisi kuwatawanya kwa mabomu kuendelea kufanyika.

Aidha wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.

Hali inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu kutawanya umati huo wa watu.

Father Kidevu Blog, ipo eneo la tukio na itakuletea taarifa zaidi 
Habari hii kwa hisani ya Father Kidevu Blog.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images