Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

KAGERA YATENGEWA HEKTA 58,000 KWA AJILI YA VIWANDA

$
0
0
Na Josephine Majura, WFM, Dodoma

Serikali imeeleza kuwa mikakati inayoendelea kutekelezwa na kuratibiwa katika Mkoa wa Kagera ni pamoja na kutenga maeneo ya uwekezaji yenye ukubwa wa hekta 58,000 kwa ajili ya kuanzisha viwanda vya kusindika na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo (Agro Processing Industries) hususani viwanda vya kusindika nyama, maziwa, asali, ndizi, miwa, kahawa na samaki.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, alipokua akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalaum Mhe. Halima Bulembo, aliyeuliza mkakati wa Serikali wa kuwa na miradi maalum ya kuondoa umasikini kwa Watu wa Kagera ambao ndio Mkoa pekee unaopakana na nchi nyingi zaidi za EAC na hivyo kuufanya kuwa Mkoa wa kimkakati kibiashara.

Alivitaja baadhi ya viwanda hivyo kuwa ni Kagera Fish Co. Ltd na Supreme Perch Ltd vinavyosindika minofu ya samaki, Kagera Sugar Co. Ltd na Amir Hamza Co. Ltd vinavyosindika miwa na kahawa, na Kiwanda cha Mayawa kinachosindika Mvinyo ya Rosella na juisi.

” Kampuni ya Josam imepatiwa eneo lenye ukubwa wa hekta 500 katika ranchi ya Kikulula na tayari imejenga bwawa kwa ajili ya kuvuna maji pamoja na kuanza ufugaji wa ng’ombe wa maziwa wapatao 100 hadi sasa” aliongeza Dkt. Kijaji

Dkt. Kijaji alieleza kuwa mkakati wa kutekeleza miradi maalum ya kuondoa umasikini katika Mkoa wa Kagera imeainishwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2017 – 2020/2021, Mpango Mkakati wa Mpango wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo na Mipango ya Mkoa wa Kagera kwa ujumla.

“ Miradi yote ya kiuchumi na kijamii inayotekelezwa na Serikali na Sekta Binafsi katika mkoa wa Kagera, na mikoa mingine ni kwa ajili ya kuondoa umaskini na kuboresha maisha ya wananchi”, alisema Dkt. Kijaji. Aidha, aliainisha baadhi ya mikakati inayoendelea kutekelezwa na kuratibiwa na Serikali katika mkoa huo kuwa ni pamoja na kuimarisha usafiri wa majini kwa kukamilisha ujenzi wa meli kubwa itakayotoa huduma ya usafiri na usafirishaji kati ya Bukoba na Mwanza.

Dkt. Kijaji aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha miundombinu ya barabara kama vile barabara kwa kiwango cha lami ya Kyaka – Bugene (km 59.1), Kagoma – Lusahunga (Km. 154), Ushirombo – Lusahunga (Km. 50).

Alizitaja barabara nyngine zinazojengwa katika ukanda huo kuwa ni barabara ya Nyakanazi – Kibondo (km 50), ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 40 pamoja na barabara ya Kyamyorwa – Buzirayombo (km 120).

“Kitaanzishwa kiwanda cha kuchakata madini ya bati katika wilaya ya Kyerwa ifikapo Juni, 2021 ambapo Kampuni ya Tanzaplus Minerals na African Top Minerals ltd zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta hiyo na tayari zimeanza kuleta mitambo ya uchenjuaji” aliongeza Dkt. Kijaji .Aliutaja mradi mwingine wa sekta ya madini kuwa ni uendelezaji na uwekezaji wa madini ya Nikeli Kabanga katika Wilaya ya Ngara ifikapo Juni mwaka 2021.

Mbunge wa Ilolo Mhe. Venance Mwamoto, aliuliza mpango wa Serikali wa kukarabati barabara za mkoa wa Kagera kwakuwa una viwanda vingi ili viweze kufikika kwa urahisi na kurahisisha biashara ndani na nje ya nchi.

Akijibu swali la nyongeza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Atashasta Nditiye alisema kuwa Serikali imeshapeleka fedha katika mkoa huo na tayari imetoa tangazo la kutafuta Wakandarasi kwa ajili ya ukarabati wa barabara hizo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji

JAJI MKUU ATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI

$
0
0
Na Lydia Churi-Mahakama, Dodoma

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka wananchi wa mkoa wa Dodoma na Maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kwenye Maonesho ya Wiki ya utoaji wa Elimu ya Sheria na kutumia nafasi hiyo kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu Mahakama. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea maonesho hayo leo, Jaji Mkuu pia amewataka wananchi wenye malalamiko na maoni kuhusu utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania kujitokeza na kutoa hizo ili ziweze kujibiwa na watumishi mbalimbali wa Mahakama walioko kwenye Maonesho hayo. 

Jaji Mkuu pia ameto wito kwa wananchi wa Dodoma kufika na kuiuliza maswali Mahakama hasa juu ya ucheleweshwaji wa kesi zao na kuahidi kuwa maswali hayo yatajibiwa kwa lengo la hakikisha wanapata haki kwa wakati. 

“Nawakaribisha wananchi wenye nafasi kufika kwenye viwanja vya Nyerere Square ili waweze kuona Mahakama ya Tanzania inavyofanya kazi zake kwa kushirikiana na wadau, ni wakati mzuri wa kutathmini utendaji wa Mahakama katika kipindi cha mwaka moja yaani tangu 2018” alisema Jaji Mkuu. 

Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja, Mahakama ya Tanzania imepiga hatua hasa kutokana na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kesi. Aliongeza kuwa kupitia Maonesho ya Wiki ya Sheria, wananchi watajifunza kuwasilisha kesi katika ngazi mbalimbali za Mahakama. 

Akizungumzia mashauri kukaa kwa muda mrefu Mahakamani, Jaji Mkuu alisema Mahakama imekuwa ikilaumiwa kuchelewesha kesi lakini wakati mwingine kesi zimekuwa zikichelewa kwa kuwa ni lazima kesi ishughulikiwe na baadhi ya Taasisi wadau huku akitoa mfano kuwa kesi hupepelezwa na polisi lakini huendeshwa na Mwendesha Mashtaka. 

Wiki ya Sheria imeanza jana Januari 31 jijini Dodoma na itamalizika Februari 5 ambapo siku ya Sheria nchini itaadhimishwa Februari 6, 2019 katika viwanja vya Chimala jijini Dar es salaam.

SERIKALI YAELEKEZA KUSIMAMISHWA KAZI MKUU WA IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI WA MANISPAA YA ILALA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WENGINE

$
0
0

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ofisini kwake jijini Dodoma leo kuhusu kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Manispaa ya Ilala Bi. Benadeta Mwaikambo na kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wanaohusika na Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akifafanua kuhusu kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Manispaa ya Ilala Bi. Benadeta Mwaikambo wakati akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ofisini kwake jijini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP Ibrahim Mahumi na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bi. Aneth Andrew.

………………………….

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Manispaa hiyo, Bi. Benadeta Mwaikambo na kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wanaohusika na Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Dkt. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo leo wakati akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ofisini kwake jijini Dodoma, kufuatia utafiti uliofanywa kuhusu malalamiko ya watumishi ambao ulibaini Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuongoza kwa kuwa na malalamiko mengi ya watumishi ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Dkt. Ndumbaro amefafanua baadhi ya malalamiko hayo kuwa, ni pamoja na kutopandishwa vyeo kwa watumishi kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi za watumishi, uhakiki wa vyeti, kuwepo kwa upendeleo katika masuala ya kiutumishi, ushughulikiaji usioridhisha wa masuala ya kiutumishi, uwasilishaji wa madai ya malimbikizo ya mishahara Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yakiwa hayana usahihi na yenye mapungufu kutokana na uzembe.

Dkt. Ndumbaro ametoa mfano wa madai ya malimbikizo ya mishahara yaliyowasilishwa Ofisi ya Rais-Utumishi ya walimu wastaafu 40 ambapo kati ya hayo, madai 24 yalikuwa sahihi na 16 yalikuwa hayana taarifa sahihi ikiwemo kutogongwa mhuri wa mwajiri kuthibitisha madai hayo na kuongeza kuwa licha ya Manispaa ya Ilala kurejeshewa madai hayo kwa ajili ya marekebisho takribani miezi saba iliyopita lakini hadi sasa ni madai ya wastaafu wawili tu yaliyowasilishwa.

Sanjari na hilo, Dkt. Ndumbaro ameelekeza kuhamishwa kwa Maofisa Utumishi walio chini ya Idara ya Utawala na Utumishi ya Manispaa hiyo kwenda katika halmashauri ambazo hazihudumii watumishi wengi ili waweze kumudu majukumu yao kikamilifu.

Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa watumishi wa umma nchini hususan maofisa wanaoshughulikia masuala mbalimbali ya kiutumishi kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kutatua changamoto za watumishi kwa wakati na kuongeza kuwa ofisi yake itaendelea kufanya ufuatiliaji kwa taasisi zote zinazolalamikiwa.

KATIBU MKUU UJENZI ATETA NA WAKUU WA TAASISI ZILIZO CHINI YA SEKTA YAKE

$
0
0



Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi). Arch. Elius Mwakalinga, akifafanua jambo kwa Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake jijini Dodoma, leo katika kikao kazi cha kujadili majukumu ya Taasisi hizo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi). Arch. Elius Mwakalinga (katikati), akisikiliza uwasilishwaji wa taarifa za utekelezaji kutoka katika taasisi zilizo chini ya sekta yake jijini Dodoma, leo kwenye kikao kazi cha kujadili majukumu ya Taasisi hizo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizarani hapo Bi. Elizabeth Tagora.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Ujenzi), Bi. Elizabeth Tagora, akizungumza na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo jijini Dodoma, leo katika kikao kazi cha kujadili majukumu ya Taasisi hizo.
????????????????????????????????????
Meneja miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Eng. Crispianus Ako, akitoa taarifa ya utekezaji wa Wakala huo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi). Arch. Elius Mwakalinga, (hayupo pichani), katika kikao kazi cha kujadili majukumu ya Taasisi hizo jijini Dodoma, leo.
5-min
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Arch. Elius Mwakalinga, wakati akifungua kikao kazi cha kujadili majukumu ya Taasisi hizo jijini Dodoma, leo.

SERIKALI KUSIMAMIA MAKUBALIANO NA TAASISI YA BILL AND MELINDA GATES ILI KUKUZA SEKTA YA MIFUGO

$
0
0

Na. Edward Kondela

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel kufanya ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha mikakati ambayo serikali imekubaliana na Taasisi ya Bill and Melinda Gates katika sekta ya mifugo inatekelezwa kama walivyokubaliana.

Naibu Waziri Ulega amesema hayo leo (01.02.2019) jijini Dodoma alipotembelewa na ujumbe kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gates katika ofisi za wizara hiyo na kubainisha kuwa serikali inahakikikisha Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Mifugo Tanzania unatekelezwa na kuishukuru taasisi hiyo kwa kutoa mchango mkubwa katika mpango huo.

“Sisi tuko pamoja na nyinyi na tunathamini makubaliano yetu na hatuwezi kuvunja makubaliano yetu ninawahakikishia kuwa nitamuagiza katibu mkuu afanye ufuatiliaji wa karibu sana kuhakikisha kwamba sisi tuna mikakati yetu tunayoifanya lakini hii mikakati yote inaenda sambamba na kile tulichokubaliana.” Alisema Mhe. Ulega

Naibu Waziri Ulega pia amesema serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa karibu katika sekta za mifugo na uvuvi kwa kulinda rasilimali za nchi kwa kutumia Operesheni Nzagamba na Operesheni Sangara ili kuondoa mambo yaliyokuwa yakifanywa bila utaratibu na kuisababishia serikali hasara.

“Tunafanya ulinzi wa rasilimali na kuondoa ule uholela na kuhakikisha kuwa zile sheria, taratibu na kanuni zinafuatwa sana kwa sababu hata masoko ya kimataifa yalitaka uholela usiwepo, mambo yawe katika utaratibu wa kisheria na kanuni zinazoongoza sekta.” Alisema Mhe. Ulega

Aidha Mhe. Ulega amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi, inahakikisha katika operesheni hizo sheria, kanuni na taratibu za sekta za mifugo na uvuvi zinafuatwa ili sekta hizo ziweze kusonga mbele kwa kumuwekea mazingira mazuri mwananchi ili aweze kufaidika na nchi iweze kuongeza pato la taifa.

Akizungumza katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa pia na wakuu wa idara kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amebainisha baadhi ya mambo ambayo yanapaswa kusimamiwa ikiwemo elimu ili wafugaji waweze kunufaika kupitia sekta hiyo.

“Ningependa katika ushirikiano wetu huu tuzidi kushirikiana katika kutoa elimu kwa wafugaji wetu tuwe na ufugaji wenye tija, lakini eneo lingine la pili ni usimamizi dhidi ya magonjwa, la tatu ni kuwawezesha wafugaji wetu kiuchumi lakini la nne ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Mifugo Tanzania.” Alisema Prof. Gabriel

Prof. Gabriel pia ameainisha mambo mengine kuwa ni umuhimu wa kufanyika kwa tafiti, usimamizi na uhakikishaji wa uzalishaji bora wa mifugo ili sekta ya mifugo iweze kuwa na maendeleo endelevu.

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Programu Mwandamizi wa Taasisi ya Bill and Melinda Gates katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki Bibi Mercy Karanja, Mshauri Mwelekezi kutoka taasisi hiyo nchini Tanzania Prof. Marcellina Chijoriga amesema Taasisi ya Bill and Melinda Gates bado itaendelea kufanya kazi nchini kwa kufuata mpango wa serikali. Aidha Prof. Chijoriga ameshukuru uongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambao umekuwa ukitoa ushirikiano mkubwa kwa taasisi hiyo na kutoa ombi kwa uongozi wa wizara kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Bill and Melinda Gates ili iweze kuleta matokeo chanya kwa wafugaji nchini.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega

WASANII WA FILAMU NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA WALEDI NA UFANISI KWENYE KAZI ZAO

$
0
0
KAIMU Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Monica Kinala akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu wa mkoa wa Tanga 
KATIBU Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo akizungumza katika mafunzo hayo
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Mathew Bicco akizungumza katika mafunzo hayo .
Mwezeshaji wa Mada ya Uandishi wa Miswada ya Filamu Dkt Richard Ndunguru kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu mkoani Tanga.
Msanii nguli wa Filamu mkoani Tanga akizungumza wakati wa mafunzo hayo kulia ni KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala
Sehemu ya wasanii wa filamu mkoani Tanga wakifuatilia mafunzo hayo 
Sehemu ya wasanii wa filamu mkoani Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo 
KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinala katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo kulia ni KATIBU Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo kushoto ni nKATIBU Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Mathew Bicco 



WASANII wa filamu hapa nchini wametakiwa kuhakikisha wanazingatia waledi na ufanisi mkubwa kwenye kazi zao ili ziweze kuwa chachu ya maendeleo kwa jamii zinazowazunguka kutokana na tasnia hiyo hivi sasa kuwa mkombozi kwenye jamii.

Hayo yalisemwa na Mwezeshaji wa Mwezeshaji wa Mada ya Uandishi wa Miswada ya Filamu Dkt Richard Ndunguru kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu mkoani Tanga.Alisema kwamba sanaa inaweza kuwa tija kubwa ya maendeleo kwa wasanii kwa kutengeneza ajira nyingi na kuweza kuwakomboa iwapo wataizingatia na kuithamini kwa kuonyesha walezi kwenye kazi zao.

“Ndugu zangu wasanii labda niwaambie kwamba mkiwa makini kwenye kazi zenu na kuzingatia weledi mkubwa mnaweza kufika mbali kimafanikio kutokana na namna tasnia ya filamu hapa nchini iliyokuwa”Alisema.

Aidha alisema pia wasanii lazima watambue kwamba hawawezi kutengeneza filamu nzuri kama hawatakuwa na muda wa kutazama wenzao wanafanya nini kwani kupitia wenzao wanaweza kujifunza na kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa”Alisema.“Labda pia niwaambie kwamba waledi kwenye kazi ya sanaa ni kitu muhimu sana inaweza kukupa maendelea makubwa kwa kuhakikisha mnaipenda na kuithamini “Alisema .

Naye kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fisso alisema sekta ya filamu ni ya kiuchumi kutoka Tanzania ni ya pili kwa idadi uzalishaji ukilinganisha na nchi ya Nigeria lakini ukija kwenye pato la Taifa kidogo wanahitaji kuongeza nguvu.

Alisema bodi ya filamu imeweka mpango mahususi wa kuwajengea uwezo wadau wa filamu hapa nchini hususani kwenye maeneo ya kuboresha kazi zao ili ziwe kuwa na tija.

Aidha alisema hilo linatokana na baadhi ya wasanii hususani wanaochipukia kutokutambua namna ya kuweza kutengeneza kazi zao na kuweza kuzitangaza ili ziweze kuwa na manufaa makubwa kwao.

SERIKALI YASHAURIWA KUCHUKUA HATUA HARAKA KUDHIBITI TATIZO LA VIFO VYA WAJAWAZITO NCHINI

$
0
0
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati akizinduzi wa kimkoa wa kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi mkoa wa Tanga ijulikanayo “jiongeze tuwavushe salama”
 KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza katika uzinduzi hu
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita akizungumza wakati wa uzinduzi huo
 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akichangia jambo kwenye uzinduzi huo
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza wakati wa uzinduzi huo
 MKUU wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza jambo
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah mara baada ya uzinduzi huo ambao uliwenda sambamba na uwekaji saini ahadi
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa mara baada ya uzinduzi huo ambao uliwenda sambamba na uwekaji saini ahadi
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akifuatilia utiaji wa saini na kuweka ahadi Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
  MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Gissa Gwakisa akisaini

 Wakuu wa wilaya wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa taarifa mbalimbali kwenye uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah,Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa,Mkuu wa wilaya ya Lushoto January Lugangika na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo
 KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim kulia akiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza Desderi Haule wakifuatilia kwa umakini uzinduzi huo
 Katibu wa Afya Mkoani Tanga Abdiely Makange kulia akisisitiza jambo na mmoja wa washiriki wakati wa uzinduzi huo
 Sehemu ya washirki wa uzinduzi huo wakimsikiliza kwa umakini mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella


SERIKALI imeshauri kuchukuwa hatua za haraka ilikuweza kudhibiti tatizo la vifo vya wajawazito nchini kuepuka kupoteza nguvu kazi kubwa ambayo ingeweza kuwa msaada mkubwa kwa uchumi wa nchi.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela wakati Uzinduzi wakampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi mkoa wa Tanga ijulikanayo “jiongeze tuwavushe salama”

Alisema kuwa takwimu za vifo vya wajawazito inaonyesha vinazidi kukuwa kila siku hivyo wakati umefika sasa wa kuhakikisha serikali inashughuli kwa haraka changamoto hizo ili kuweza kupunguza vifo hivyo.

“Kwa mkoa wa Tanga pekee kwa kipindi cha mwezi mmoja tayari wajawazito nane wamepoteza maisha hivyo kwa takwimu hizo inamaana mpaka mwisho wa mwaka kutakuwa na vifo vingi “alisema RC Shigela.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Zena Said alisema kuwa miongoni mwa changamoto kubwa ni ukosefu wa miundombinu bora ya afya kama vile gari la wagonjwa pamoja na uhaba wa wataalamu .

Vile vile alisema kuwa changamoto nyingine mama mjamzito kutokwa na damu nyingi,pamoja na kutopatiwa usaidizi wa haraka pindi pale anapokuwa amefikishwa katika kituo cha afya kwa ajili ya huduma.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa mkoa Dkt Asha Mahita aliweza kutaja takwimu za vifo kwa kipindi cha miaka minne ambapo kwa mwaka 2015 jumla ya vifo vilikuwa 67.

“Kwa mwaka 2016 kuliuwa na vifo 46 ,huku mwaka 2017 kukiripotiwa vifo 45,ambapo mwaka 2018 kukiwa na vifo 54”alibainisha Mganga Mkuu huyo.

Aidha alisema kuwa mikakati iliyokuwepo ni kupeleka elimu kwa jamii kuona umuhimu wa kuhudhuria cliniki kwa wakati,kushughulia kwa haraka changamoto za vifo vitokanavyo na uzazi.

“Tumejipanga katika kuhakikisha kila wilaya, huduma ya mama na mtoto inakuwa ni kipaumbele chetu lakini pia kutenga bajeti kubwa ili kuweza kutatua kwa haraka changamoto za wajawazito na watoto wachanga”alisema Dkt Mahita.

MAJALIWA AFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA WADAU WA KAHAWA TANZANIA,OFISINI KWAKE MLIMWA JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwenyekiti wa Wadau wa Kahawa Tanzania Tinson Nzunda, ofisini kwake Mlimwa jijjini Dodoma Februari 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wananchi Wajitokeza kufanyiwa Uchunguzi wa Kuangalia Uvimbe kwenye Matiti

$
0
0
Madaktari kutoka Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) wakitoa elimu kuhusu uchunguzi wa uvimbe kwenye matiti kabla ya kuanza kwa huduma hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na watalaam wa hospitali hiyo. 
Baadhi ya wananchi wakisubiri huduma ya kufanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji. 
Mtaalam wa Radiolojia Dkt. Ndigwake Mallango akimuelekeza Bw. Diatrick Luoga mkazi wa Kimara namna ya kujifanyia uchuguzi wa awali wa uvimbe kwenye matiti. 
Dkt. Irene Godlove akimsajili Bi. Sadia Sinani kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji wa awali wa uvimbe kwenye matiti. Huduma hiyo inatolewa bure leo na kesho hospitalini hapo. 


Dar es salaam 

Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) leo imetoa huduma ya uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji. 

Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu amesema katika zoezi hilo endapo mgonjwa atagundulika kuwa ana uvimbe, sampuli itachukuliwa kwa njia ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi zaidi. 

Hivyo ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi ili kufanyiwa uchunguzi wa awali ambao unafanyika leo na kesho na huduma hiyo inatolewa bure. 

Akielezea kuhusu ugonjwa wa saratani ya matiti Dkt. Sakafu amesema saratani ya matiti ni namba mbili kati ya saratani zinazowapata wanawake hapa nchini, pia katika vifo vyote vitokanavyo na saratani kwa wanawake Saratani ya matiti ni ya pili. 

“Wengi wanafika hospitalini kwa kuchelewa na ugonjwa unakua umefika hatua ya mwisho na hivyo kusababisha matatibabu yake kuwa na changamoto’’. Amesema Dkt. Sakafu. 

Kwa upande wake Daktari kutoka MEWATA, Dkt. Deograsia Mkapa ametaja visababishi vya ugonjwa wa saratani ya matiti kuwa ni kutonyonyesha, kutofanya mazoezi mara kwa mara na uvutaji wa sigara. 

Dkt. Mkapa amewashauri wanawake endapo wakiona mabadiliko yoyote kwenye mwili hasa kwenye matiti kuwahi hospitalini kwa ajili ya uchunguzi. 

Katika zoezi hilo zaidi ya watu 70 wamefanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji.

MAGWIJI WA HABARI WAKUTANA KUJADILI UPIGAJI PICHA ZA HABARI TANZANIA

$
0
0

Mkuu wa kitengo cha Mission Katika Ubalozi wa Uholanzi,Lianne Houben akitoa neno la ufunguzi katika kongamno la upigajipicha na Mjadala wa picha za habari
Muongozaji wa Mjadala wa upigaji picha za Habari Valerie Msoka akichambua mada itakayojadiliwa katika mjadala huo ya Upigaji picha za habari nchini Tanzania
 Mkurugenzi wa Misa Tan Garisigwa Sengiyuvwa akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa Shindano la upigaji picha za Habari lililoandaliwa na Tasisi ya Voice, Imani Nsamila wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa  Alliance Francai's Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Misa Tan Garisigwa Sengiyuvwa akikabidhi zawadi kwa Mshindi wa Pili wa shindano la upigaji picha Aika Kimaro ambaye alipiga picha ikumuonyesha Mwanamke akiwa na Mtoto Mdogo huku kabeba mzigo wa Makopo kwa ajili ya kwenda kuuza hili ajikimu yeye na familia
 Mkufunzi wa Upigaji Picha za Habari Mwanzo Milinga akichangaia mada wakati wa mjadala wa upigaji picha za habari
 Mpigapicha wa picha za Habri ,Raqey Mohamed akizungumza uzoefu wake katika taaluma ya picha hapa nchini
 Mtaalamu wa Mawasiliano ya Umma na upigaji picha za Habari,Innocent Mungi akizungumza juu ya umuhimu wa picha katika kufikisha taharifa kwa jamii
 Mkurugenzi wa Misa Tan,Garisigwa Sengiyumva akizungumzia umuhimu wa Tasisi za Habri kuwekeza katika upigaji picha za habari hapa nchini hili kuleta matokeo mazuri
 Mkurugenzi Mkuu wa Chama Cha  Waandishi wa Habari Wanawake nchini,Rose Rueben akieleza ni namna gani wapiga picha wa habari wanavyotakiwa kuzingatia miko ya uandishi wa habari wakati w aupigaji picha zao
 Wadau mbalimbali wakipiga kura kwa ajili ya kumpata mshindi wa shindano la upigaji picha lililoandaliwa na Voice
Washiriki kutoka Sehemu Mbalimbali wakisikiliza Mdahalo huo--

SERIKALI KUPELEKA ZAIDI YA MILIONI 500 KUBORESHA ELIMU NA MIRADI MINGINE RUKOMA

$
0
0
Jengo la Vyumba vya Madarasa (4) ya Shule ya Msingi Karama, Vimejengwa na World Vision Rukoma AP, vikisubiriwa kukabidhiwa, World Vision tayari wamejenga na Kukabidhi vyumba (2) Shule ya Msingi Luzila Katani Rukoma.
Vifaa vilivyokusanywa kwa Nguvu za Wananchi Kata Rukoma, vikiwa tayari eneo La Ujenzi wa Sekondari ya Kata (Abutaraka), kinachosubiriwa ni Serikali kutenga kiasi kilichopendekezwa ili shughuli ya Ujenzi iendelee 
Wanafunzi wa Darasa la pili Shule ya Msingi Luzila wakiendeea na masomo kama walivokutwa na kamera yetu, Hali kama hiyo inawakumba pia Darasa la sita, changamoto kubwa ni wakati wa mvua, na kuandika, tayari Rasimu ya Bajeti imependekeza Kiasi cha Shilingi Milioni 40 kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa yote mawili ingawa uhitaji ni madarasa saba.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukoba Vijijini Ndg. Evalista Babyegeya akisaidiwa na Mwenyekiti wa Vijana Ndg. Philipina, katika zoezi la Upandaji miti, ambapo CCM Kata Rukoma kinatarajia kupanda miti Elfu Tano. 
Mh. Murshidi Ngeze Diwani wa Kata Rukoma, na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba, akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM Kata Rukoma katika sherehe za Miaka 42 ya Chama hicho katika Kata yao. 
Bibi Husina Sadara mmoja kati ya wazee 200 Ndani ya Kata Rukoma, waliopatiwa Vitambulisho vya Wazee awamu ya kwanza tayari kwa Utekelezwaji wa Sera ya Afya ya kuwapatia Wazee wanaostahili Matibabu bure. 
Ndg. Evalista Babyegeya M/kiti wa CCM Bukoba Vijijini akihutubia Wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa Chama hicho katika Kata ya Rukoma, zilizofanyika Kijiji Nsheshe Januari Mosi, 2019. (Picha zote na Abdullatif Yunus) 

………………….. 

Na. Abdullatif Yunus – Kagera 

Kufuatia Hali ya Elimu katika Kata ya Rukoma , Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba imepanga kuboresha sekta ya Elimu katika Kata hiyo kwa kutenga zaidi ya Milioni 500, za kutatua changamoto mbalimbali katika sekta hiyo, zikiwemo upungufu wa Walimu, Madarasa, Vitabu katika Baadhi ya Shule za msingi na Kubwa ikiwa ni Ukosefu wa shule ya Sekondari katika kata Hiyo. 

Kutengwa kwa Kiasi hicho kwa Kata hiyo kimezzua mjadala mkubwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, cha kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti ya mwaka fedha ujao 2019 – 2020 kilichomalizika hivi karibuni, Msuguano mkubwa ukiwa ni kwanini kiasi cha Shilingi Milioni 260 zimeelekezwa kujenga Sekondari katika Kata hiyo, wakati. Hata hivyo baada ya mvutano huo, hatimae kwa pamoja Baraza hilo limekubaliana kwa pamoja kuhusu Kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 500 kuelekezwa Kata ya Rukoma ili kundeleza na kuibua miradi mbalimbali ya Jamii na maendeleo kwa ujumla ikiwemo Ujenzi wa vyumba vya madarasa, Zahanati, Nyumba ya Mwalimu , na Ujenzi wa Shule ya Sekondari. 

Hali halisi kwa sasa inaonesha upungufu wa madarasa kadhaa katika baadhi ya shule Katani humo, walimu, Madawati, Vitabu, n.k hivyo kuna uhitaji mkubwa, na nguvu ya ziada inatakiwa ili kuendelea kuboresha Mazingira ya Elimu katika Kata hiyo, kwani ukiachilia mbali Nguvu za Mashirika wahisani kama World Vision Rukoma AP, ambao wametekeleza miradi mbalimbali kama Ujenzi wa Vyumba (2) vya Madarasa ya shule za msingi Luzila na Kamkole, Choo cha Shule ya Msingi Nsheshe, Kuweka Sakafu Darasa Moja S/M Bituntu, na Uanzishwaji wa madarasa ya kila jumapili kwa watoto wenye mahitaji maalumu, kuna haja kubwa ya Serikali kuweka jitihada kuinua Elimu Kata Rukoma. 

Akitoa salaamu zake katika Maadhimisho ya Kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi ngazi ya Kata, zilizofanyika katika kitongoji cha Karama Kijiji Nsheshe, Diwani wa Kata hiyo Mh. Murshidi Ngeze amebainisha Kero kubwa mbili katika kata hiyo, moja ikiwa ni Ukosefu wa Sekondari ya Kata, kwani wanafunzi wamekuwa wakitembea umbali wa takribani Kilometa 13, kwenda Kata ya Jirani ya Rubale kufuata Elimu hivyo kwa mazingira ya Kijijini na watoto wa kike ni hatarishi sana, na akiongeza kuwa Kata hiyo kwa matokeo ya Darasa la saba Mwaka jana Idadi ya Ufaulu imeongezeka. 

Aidha Mh. Ngeze amebainisha changamoto ya pili kubwa kuwa ni ukosefu wa Umeme katika kata hiyo toka Uhuru, hivyo suala hilo limekuwa likizorotesha maendeleo hata ya Elimu kwani, wamekuwa wakiletwa walimu na kuondoka kutokana na mazingira yalivyo. Tayari katika hali ya Uhitaji wa Shule ya Sekondari katika kata yao, Wananchi wamekwisha tenga Eneo na kusanya vifaa vya kuanzia Ujenzi huo, ikiwemo Mchanga , kokoto ,mawe, na tofali kadhaa, kinachosubiriwa ni Kuanza Ujenzi huo. 

Sherehe hizo za Mazazi ya Chama cha Mapinduzi Kata Rukoma, zimeambatana na Zoezi la Upandaji Miti 5,000 likiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bukoba Vijijini, Ndg. Evalista Babyegeya, kuwapokea wenyeviti wa Vitongoji (3), na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji Bituntu Ndg. Swahibu Sambamba na ugawaji wa Vitambulisho 200 vya Wazee ikiwa ni kutekeleza Sera ya Afya ya kuwapatia Wazee matibabu bure, zimehudhuliwa na Wananchi na wakereketwa wa Chama katika Kata hiyo na Kata za jirani, pamoja na Viongozi mbalimbali wa Chama Ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji.

WAZIRI MKUU AFUNGUA WIKI YA SHERIA

$
0
0
*Asema Serikali ni mdau muhimu wa Mahakama
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeendelea kushirikiana na Mhimili wa Mahakama katika kuhakikisha huduma bora za utoaji haki zinawafikia wananchi kwenye maeneo wanayoishi kwa wakati.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ni mdau muhimu wa Mahakama na inafuatilia kwa karibu changamoto zote zinazoikabili pamoja na wadau wengine katika mfumo wa utoaji haki.” 

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Februari 2, 2019) wakati akifungua wiki ya Sheria Tanzaniakatika viwanja wa Nyerere Square jijini Dodoma. Ametoa wito kwa wananchi watembelee mabanda ya maoneshohayo.

Amesema kupitia wiki ya sheria wanachi watapata elimu kuhusu masuala ya sheria pamoja na kushuhudia na kunufaika na maboresho yanayofanywa na Mahakama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika utoaji haki.

Waziri Mkuu amesema jambo hilo ni jema kwani masuala ya kisheria si mepesi kujulikana kwa kila mwananchi na kwa sababu hiyo, wananchi wengi wamekuwa na uelewa mdogo wa masuala hayo ya kisheria. 

Amesema wananchi wengi hawajui taratibu na mienendo ya kimahakama na wakati mwingine wanakosa au kupoteza haki zao kwa kigezo cha kutofuata taratibu ili kupata haki zao hizo.

“Nitoe rai kwa wananchi watumiae ipasavyo fursa hii ya Wiki ya Sheria inayoambatana na maonesho kwa lengo la kupata elimu na huduma mbalimbali hususan za kisheria.”

Akizungumzia kuhusu dhamira ya Mahakama kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuleta mabadiliko kwenye utoaji haki, amesema ni hatua nzuri na itasaidia kuboresha utoaji wa haki kwa wakati.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewasihi katika matumizi hayo ya mifumo ya TEHAMA wasikatishwe tamaa na changamoto zitakazojitokeza kwani mara nyingi kitu kipya chochote hakikosi changamoto za hapa na pale. 

“Binafsi naunga mkono uamuzi wa dhati wa Mhimili wa Mahakama kutumia TEHAMA katika usajili wa mashauri. Uamuzi huo unakwenda sanjari na azma ya Serikali ya kuhakikisha TEHAMA inatumika vema kwenye taasisi za umma kwa lengo la kutoa huduma bora na kwa wakati.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema matumizi bora ya TEHAMA yataipunguzia Serikali na mihimili mingine ya dola gharama za uendeshaji hususan katika utoaji huduma kwa wnanchi.

Amesema lengo la Serikali ni kuona kuwa huduma bora zinawafikia wananchi kwa urahisi na vilevile, zinapatikana wakati wote. “Nitoe wito kwa wadau muhimu wakiwemo Mawakili wa Serikali na Mawakili wa Kujitegemea, nao kutumia mifumo ya TEHAMA katika kusajili mashauri na wala wasiwe wao wa kwanza katika kulaumu na kubeza.” 

Amesema Mawakili wote wa Serikali na Kujitegemea, wanapaswa kuwa sehemu ya kutatua changamoto zitakazoibuka katika matumizi ya mifumo hiyo ya TEHAMA kwa kuwasilisha mapendekezo kuhusu namna bora ya kuiboresha. 

Ameongeza matumizi ya TEHAMA siyo tu yatawawezesha kutoa huduma kwa wakati, lakini yataweka uwazi ambao utawapunguzia malalamiko mengi kuhusu watumishi wenu na utoaji haki. 

Waziri Mkuu amewataka watumie vema Wiki ya Sheria kwa ajili ya kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu mapinduzi ya matumizi ya TEHAMA yanayoendelea Mahakamani.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma amesema kwa kipindi cha wiki nzima, maonesho ya Wiki ya Sheria yatafanyika jijini Dodoma pamoja na kwenye Mahaka zote nchini, kuanzia ngazi ya wilaya.

Pia, Jaji Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa vijiji, kata, wilaya, mkoa, idara na wizara, wabunge, majaji, mahakimu na watumishi wa umma wahudhurie maonesho hayo ya Wiki ya Sheria.

Ametolea mfano banda la maonyesho la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu litawakumbusha kuwa mamlaka yao mihimili mitatu ya dola yanatokana na nguvu ya sheria, nguvu ambayo haimuonei mwananchi yeyote.

Jaji Mkuu amesema watu watakaoshiriki katika maonesho hayo kwa kutembelea mabanda watumie nafasi hiyo kujifunza na kutathmini umuhimu na hadhi ya mfumo wa kimahakama katika kustawisha maisha yao pamoja na kuwasaidia kupata haki kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya kufungua maadhimisho hayo ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika nje ya jiji la Dar es Salaam, Waziri Mkuu alishiriki matembezi ya kilomita tano pamoja na Jaji Mkuu na viongozi wengine yaliyoanzia Mahakama Kuu Dodoma hadi viwanja vya Nyerere Square na kisha alitembelea mabanda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi waliyohudhuria katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma, akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya kuadhimisha Wiki ya Sheria, jijjini Dodoma  Februari 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifanya mazoezi ya viungo nje ya viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019, baada matembezi ya kuadhimisha Wiki ya Sheria, kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia mifumo ya kisasa ya Mahakama Mtandao wakati alipokagua mabanda katika kuadhimisha Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019 kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tehama Kalege Anock, Athumani Kanyegezi na Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa picha na Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba hadija Mwema, wakati alipotembelea banda la Mkemia Mkuu wa Serikali katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa Chama cha Wanasheria  Tanganyika Fatma Karume, wakati alipotembelea mabanda katika Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu na Mtendaji Mkuu RITA, wakati alipotembelea banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini RITA, katika Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019, kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma na Afisa Usajili Msaidizi RITA Joseph Mwakatobe. 
 Wananchi waliyohudhuria katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019. 

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI MHE. CHARLES KITWANGA ALIYELAZWA HOSPITALI MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Charles Kitwanga 8-min
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mbunge wa Misungwi,Charles Kitwanga ambaye amelazwa katika Hospitali  ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa matibabu.Picha na IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Februari, 2019 amemjulia hali Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Charles Kitwanga ambaye amelazwa katika wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam kwa matibabu.

Mhe. Kitwanga alilazwa hospitalini hapo tangu tarehe 31 Januari, 2019.

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dkt. Juma Mfinanga amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa hali ya Mhe. Kitwanga inaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofika hospitalini hapo.

Akiwa wodini hapo Mhe. Rais Magufuli ameshiriki sala ya kumuombea Mhe. Kitwanga ilia pone haraka na amewashukuru Madaktari na Wauguzi kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuwahudumia wagonjwa.


MAGEREZA KUU ARUSHA YAPATIWA NISHATI YA UMEME JUA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizindua Mtambo wa sola uliofungwa na kampuni ya Mobisol Gereza kuu ya Arusha.


Na Vero Ignatus, Arusha.

Gereza kuu la Arusha limepatiwa msaada wa nishati ya umeme jua iliyotolewa na kampuni ya sola ya Mobisol ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika katika Gereza hilo na kuondokana na changamoto ya kukatika kwa umeme Mara kwa Mara.

Mtambo huo wa umeme wa jua umezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo amesema kuwa itasaidia kuimarisha usalama kwa wafungwa na askari magereza kwani eneo hilo linahitaji nishati ya uhakika.


Gambo alisema kuwa kampuni hiyo imefanya ubunifu mkubwa wa kuikumbuka magereza taasisi ambayo ilikua ikisahaulika na wadau wa maendeleo.Mmoja wa Waasisi wa Kampuni ya Mobisol Livinus Manyanga alisema kuwa msaada huo ni kutambua changamoto ya nishati iliyopo ila kwa sasa mitambo waliyoiweka itasaidia kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa shughuli za magereza.

"Mitambo hii imegharimu kiasi cha shilingi milioni 16 na tutaihudumia kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu ili kusaidia Wafungwa na Mahabusu wapate mwanga wa uhakika" Alisema Manyanga

Mkuu wa Gereza la Arusha Anderson Kamtyaro wameishukuru kampuni ya Mobisol kwa msaada huo ambao itasaidia kuwezesha magereza na wafungwa kufanya kazi katika mazingira bora ya kazi.Anderson aliwataka Wadau wengine kuiga mfano wa kampuni ya Mobisol kwa kujitoa kutatua changamoto zilizoko kwenye taasisi za serikali.

MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akilikagua jengo jipya la Wizara yake linalojengwa katika Mji wa Serikali, Ihumwa, jijini Dodoma, wakati alipofanya ziara katika eneo hilo leo, kwa lengo la kukagua ujenzi unavyoendelea. Meja Jenerali Kingu amemtaka Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari awe amemkabidhi jengo hilo. 

Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na Wakandarasi wa Ujenzi wa Jengo jipya la Wizara yake, Mshauri Mwelekezi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), pamoja na wawakilishi wa Wizara yake wanaosimamia ujenzi unaoendelea wa jengo hilo katika Mji wa Serikali, Ihumwa, jijini Dodoma. Kingu amemtaka Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari awe amemkabidhi jengo hilo. 

Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kamishna Msaidizi wa Magereza, Aron Lunyungu, akionyesha madirisha ambayo yapo tayari kwa ajili ya kufungwa katika jengo hilo la Wizara. Lunyungu ambaye pia ndiyo Mkandarasi wa Ujezni huo ameagizwa awe amemaliza ujenzi wa jengo hilo na kumkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,  Mwezi huu wa Februari. 

…………………… 

Na Felix Mwagara, MOHA. 

KATIBU Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amemtaka Mkandarasi anaejenga Jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma, afanye kazi usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari awe amemkabidhi jengo hilo. 

Meja Jenerali Kingu amesema kasi ya ujenzi huo umenza kusuasua kwasababu Wizara yake ilifikia hatua kubwa lakini sasa imepitwa na baadhi ya Wizara kutokana na Mkandarasi anayejenga jengo hilo kupunguza kasi ikiwa ni tofauti na ile walioanza nayo awali. 

Katibu Mkuu aliyazungumza hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo la ujenzi, jijini humo, leo, na alifanya ukaguzi na baadaye alizungumza na wadau kutoka pande tatu zinazoshirikiana katika kufanikisha ujenzi huo ambao ulianza mwezi Desemba mwaka jana. 

Wadau wa pande tatu wanaofanikisha ujenzi huo ni Mmiliki wa Jengo hilo ambaye ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mshauri Mwelekezi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) pamoja na Mkandarasi ambaye ni Jeshi la Magereza. 

“Nimepokea taarifa ya ujenzi unaoendelea, lakini sijaridhishwa nayo kutokana na asilimia ya ujenzi huu ulipofikia mpaka sasa, mmenipa ratiba mpya ya kukamilika kwa jengo hili, kasi yenu imekua ndogo mpaka tumeanza kupitwa na baadhi ya Wizara ambazo sisi tulikua tunaongoza, sasa nataka mfanye kazi hii usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari ujenzi huu uwe umekamilika na mnikabidhi jengo hili,” alisema Meja Jenerali Kingu. 

Kwa upande wake Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka TBA, Arch. Hassan Mnandala alimwambia Katibu Mkuu huyo kuwa, ataendelea kusimamia na kushauri ili Mkandarasi awe amemaliza kazi hiyo kwa wakati kama ratiba ilivyopangwa. 

Naye Mkandarasi wa ujenzi huo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Aron Lunyungu, kwa upande wake amesema ujenzi huo unaendelea na tayari ujenzi wa kuta umefanyika, na imefikia usawa wa kupaua na tayari upigaji wa ripu ndani ya jengo hilo umefanyika. 

“Tunamshukuru Katibu Mkuu Meja Jenerali Kingu, leo katutembelea na ametuagiza tujipange ili tuweze kukamilisha kwa wakati ujenzi wa jengo hili, nasi tumejipanga kazi tutaifanya usiku na mchana kuhakikisha jengo hili tunalikamilisha na tunalikabidhi kwa wakati,” alisema ACP Lunyungu.

UFAFANUZI WA KODI YA MABANGO

DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, mhandisi Tumaini Magessa akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Lairumbe Mollel akifungua kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Diwani wa kata ya Makame Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, Jacob Nini (CCM) akiapishwa baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, awali alijiuzulu kwa kuondoka Chadema kwa kumuunga mkono Rais John Magufuli na Mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti.
 
…………………….
MKUU wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, mhandisi Tumaini Magessa amewataka wakulima na wafugaji kutovamia maeneo ya hifadhi kwa kupotosha kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa hivi karibuni juu ya vijiji 366 vinavyopakana na hifadhi. 

Mhandisi Magessa aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo. Mhandisi Magessa alisema baadhi ya wafugaji na wakulima hawakuelewa ipasavyo taarifa ya hiyo hivyo kusababisha upotoshwaji. 

Alisema baada ya taarifa hiyo kutolewa baadhi ya wafugaji na wakulima walijiandaa kulima na kufugia mifugo ambayo itasababisha migogoro upya.
“Kwenye hivyo vijiji 366 vilivyotajwa na Rais Magufuli na kunufaika na tamko hilo sisi Kiteto tuna vitongoji viwili pekee sasa hao wengine wasiokuwepo wasijiingize huko,” alisema mhandisi Magessa. 

Alisema utaratibu ulishawekwa vizuri juu ya maeneo hayo na wao kama serikali ya wilaya hawatakubali kuona watu wachache wanawaingiza kwenye migogoro.
Diwani wa Kata ya Partimbo, Paul Tunyoni alisema baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto linapaswa kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwajali wafugaji na wakulima. 

Tunyoni alisema kauli ya Rais Magufuli ya kuwajali wanyonge na kuhakikisha jamii ya wafugaji na wakulima wanafaidi rasilimali zilizopo ni jambo la kupongezwa. 

Hata hivyo, mbunge wa jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian alisema pori la akiba la Mkungunero linatambulika kisheria hivyo baadhi ya viongozi wasipotoshe hilo.
Papian alisema kumekuwepo na wapotoshaji juu ya kauli ya Rais Magufuli juu ya sehemu zenye migogoro ya hifadhi na jamii inayowazunguka. 

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Lairumbe Mollel alisema wananchi wanapaswa kuwa watulivu wakati huu ambapo serikali inaweka utaratibu vizuri.
Mollel alisema wananchi wote wanapaswa kusubiri ili uhakiki ufanyike kwa ushirikishwaji wa uwazi kuliko kuingia sehemu zisizoruhusiwa na kuzua migogoro upya.

DKT. MWANJELWA AWAONGOZA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUPANDA MITI ILI KUTEKELEZA KWA VITENDO KAMPENI YA MAKAMU WA RAIS YA KULIFANYA JIJI LA DODOMA KUWA KIJANI

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipanda mti katika eneo la ofisi yake inayojengwa kwenye mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akitoa maelekezo kwa Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la ofisi yake inayojengwa kwenye mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akiandaa eneo kwa ajili ya kupanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inayojengwa kwenye mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.

…………………………..

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) mapema leo amewaongoza watumishi wa ofisi yake kupanda miti katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inayojengwa kwenye Mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma ili kutekeleza kwa vitendo kampeni ya Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani.

Mhe Dkt. Mwanjelwa (Mb) amesema, watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kama kioo cha Utumishi wa Umma nchini, wamejitokeza kuunga mkono kwa vitendo kampeni hiyo ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani kwa kupanda miti ili kuwa mfano bora kwa taasisi nyingine za umma ambazo hazijatekeleza kampeni hiyo.

Akiongoza zoezi hilo, Mhe Dkt. Mwanjelwa (Mb) amesema, pamoja na kuunga mkono kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora inatambua kuwa mazingira ni uhai ndio maana Jumamosi hii, yeye pamoja na watumishi wa ofisi yake wamejitokeza kwa wingi kupanda miti.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi wa ofisi yake kuendelea na moyo wa kujituma katika utekelezaji wa kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya Nchi kuwa la kijani.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi hao kuhakikisha wanahudumia miti hiyo ili iweze kustawi na kulifikia lengo la kuwa na Dodoma ya kijani.

CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE 

KATIKA kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 42 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kata ya Pera Chalinze, Bagamoyo, Shawali Ndembo amekihama chama hicho na kukimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Pia wanachama wengine wanne kutoka chama hicho wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM. 

Akimpokea Ndembo wakati wa sherehe za maadhimisho hayo wilaya ya Bagamoyo, yaliyofanyika Pingo kata ya Pera, mwenyekiti wa CCM Bagamoyo, Abdulsharif Zahoro alisema ilani ya chama inatekelezwa na kuleta heshima kwa wananchi. 

Alisema, serikali ya awamu ya tano inaitendea haki ilani hiyo hivyo kazi kubwa kwa wanaCCM ni kuisemea serikali kwa yale inayotekeleza na kutatua changamoto mbalimbali kwa watanzania. "Nampongeza mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, Dk.John Magufuli kwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo "alisema Sharif. 

Sharif ,alisema uongozi ni dhamana mwenyekiti wa kitongoji na vijiji wafanye ziara za kuelezea utekelezaji wa ilani na kutimiza wajibu wao ili kukiweka chama sehemu nzuri uchaguzi serikali za mitaa 2019.

Hakusita kukemea makundi ambayo kwa upande mwingine yanasababisha migongano baina ya wanachama na kusababisha kukiyumbisha chama. 
Aliwaasa viongozi na wanaCCM kujenga umoja,upendo,mshikamano ili kukiimarisha chama hicho. 

Awali akirudisha kadi ya CHADEMA, Ndembo alimpongeza na kumwagia sifa Rais dk. John Magufuli kwa kuitendea haki ilani ya chama kivitendo. 
"Vyama vya upinzani vilikuwa vikihitaji utatuzi wa kero na changamoto, sasa Tanzania inaneemeka, uchumi unapanda siku hadi siku, kutokana na hayo ni vema nije CCM ,kwakuwa kule nilipotoka hakuna jipya "alifafanua Ndembo. 

Nae mwenezi wa CCM Bagamoyo ,John Francis Bolizozo alisema tukielekea katika chaguzi mbalimbali zijazo, wamejipanga kushinda kwa kishindo uchaguzi wa serikali ya mitaa na hatimae madiwani na urais 2020.

Katika maadhimisho hayo kiwilaya waliweza kujitolea nguvu kazi kwenye ujenzi unaoendelea shule ya sekondari Pera na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM Pingo .
Mwenyekiti wa CCM Bagamoyo, Abdulsharif Zahoro (kulia) akimpatia kadi ya CCM, katibu wa CHADEMA kata ya Pera, Shawali Ndembo ambae amekihama chama hicho na kujiunga na CCM, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 42 ya CCM wilaya ya Bagamoyo, yaliyofanyika Pingo kata ya Pera.(picha na Mwamvua Mwinyi) 
Mwenyekiti wa CCM Bagamoyo, Abdulsharif Zahoro akimvisha fulana ambayo ni sare ya chama cha mapinduzi, katibu wa CHADEMA kata ya Pera, Shawali Ndembo ambae amekihama chama hicho na kujiunga na CCM, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 42 ya CCM wilaya ya Bagamoyo, yaliyofanyika Pingo kata ya Pera.(picha na Mwamvua Mwinyi)

Ofisi za RC na Dc zisiwe mahakama

$
0
0
Wiki ya kutoa  elimu na ushauri wa kisheria imezinduliwa katika Mkoa wa Shinyanga mapema leo tarehe 02/02/2019 huku watendaji wa Idara mbalimbali wakitakiwa kutenda haki kwa wananchi ili kupunguza malalamiko kwenye ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa. 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema wananchi wengi wanakwenda kwenye Ofisi yake na Mkuu wa Wilaya kulalamika kuhusu kutokamilika kwa mashauri yao Mahakamani.

" Nimechoka kusikia Shinyanga ikizungumziwa kwa rushwa rushwa, watu wanakimbia mahakamani kwa sababubhawatendewi haki, wanakuja Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya ndiyo kwenye haki"

Mhe. Telack amesisitiza kuwa, hawezi kukaa akaangalia wananchi wakilalamika watumishi kuwataka rushwa ili kutekeleza majukumu yao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe,. Zainab Telack akisaini kitabu cha wageni huku akipata maelekezo ya Afisa Huduma kwa jamii kutoka Idara ya huduma za uangalizi,Wizara ya mambo ya ndani, Bi Monica Dawa.
Mkuu w Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, akielekea kwenye mabanda ya wadau wa sheria katika kuzindua wiki ya sheria Duniani, Mkoani Shinyanga mapema leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Venant Mboneko.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>