Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1794 | 1795 | (Page 1796) | 1797 | 1798 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Wananchi katika Kijiji cha Igando, wilayani Chato, mkoa wa Geita, wameanza kupata huduma ya umeme kupitia mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ndiye aliyewasha rasmi umeme jana katika Kijiji hicho, ambapo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Mtemi Semeon na viongozi wengine kutoka Wilaya hiyo, Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

  Aidha, kabla ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Igando, Dkt Kalemani alifika katika Kijiji cha Imwelu kilichopo Kata ya Buseresere wilayani humo ili kukagua kazi ya upelekaji wa miundombinu ya umeme katika Kijiji hicho.

  Akiwa kijijini hapo, Dkt Kalemani aliwaagiza REA, TANESCO pamoja na mkandarasi aliyepewa kazi ya kusambaza umeme kijijini hapo, kuhakikisha kuwa, ifikapo tarehe 28 mwezi huu, kijiji hicho kiwe kimeshawashiwa umeme.

  Kwa nyakati tofauti akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo, alisisitiza kuwa, bei ya uunganishaji umeme katika vijiji vyote nchini ni shilingi 27,000, tu, hivyo wananchi wa vijijini wasitozwe zaidi ya kiasi hicho.

  Aidha, amewataka wananchi hao kutumia umeme huo pia kwa shughuli za maendeleo ambazo zitawaongezea kipato na kukuza uchumi katika maeneo mbalimbali nchini.

  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tatu kulia) akikata utepe kuashiria kuanza kupatikana kwa huduma ya umeme katika Kijiji cha Igando, Kata ya Bwera wilayani Chato. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Mtemi Semeon.
  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Imwelu, Kata ya Buseresere wilayani Chato ambapo alimwagiza mkandarasi kuwasha umeme katika Kijiji hicho ifikapo tarehe 28 mwezi huu.
  Wananchi katika Kijiji cha Igando, Kata ya Bwera wilayani Chato wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati alipofika kijijini hapo kuzindua huduma ya umeme.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe akizungumza na wajumbe walioshiriki warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini (hawapo pichani) wakati wa kufunga warsha hiyo Februari 1, 2019 iliyofanyika Ukumbi wa Mazengo Dodoma Hotel.
  Meneja wa Programu elimu ya majanga kutoka UNISDR Bi.Katarina Mouakkid akieleza jambo wakati wa kufunga warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini iliyofanyika Jijini Dodoma Februari 1, 2019
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa hotuba kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe (hayupo pichani) wakati wa Warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini.
  Mratibu wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. John Kiriwai akiwasilisha mada wakati wa warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini iliyofanyika Jijini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe (wa kwanza kulia) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo anayeshughulikia Mipango na Utafiti Bw.Bashiru Taratibu (wa kwanza kushoto) na Katarina Mouakkid Meneja wa Programu ya elimu ya majanga kutoka UNISDR (katikati) wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa warsha hiyo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe akimkabidhi cheti cha ushiriki Bw. Bashiru Taratibu ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo anayeshughulikia Mipango na Tafiti wakati wa kufunga Warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini iliyofanyika Jijini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe akimkabidhi cheti cha ushiriki kwa Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt.Wilhelim Kiwango mara baada ya kufungwa kwa wa Warsha ya hiyo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Mashirika ya Kimataifa ikiwemo, UNISDR, CIMA na mwakilishi kutoka VU.NL na kulia kwake ni Bw.Charles Msangi mratibu wa maafa wa ofisi hiyo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)  Serikali imedhamiria kuendelea kuchukua hatua za upunguzaji wa athari za maafa kwa kuwa ni moja ya eneo lililopewa kipaumbele katika Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka wa Mitano, 2016/17- 2020/21.

  Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe alipokuwa akifunga warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara Februari 1, 2019 Jijini Dodoma.

  Ameeleza kuwa, hatua hiyo ni muhimu katika mkakati wa upunguzaji wa madhara yatokanayo na maafa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya msingi ya Mfumo wa Sendai wa Kupunguza Madhara ya Maafa wa mwaka 2015 – 2030 sambamba na malengo endelevu ya mwaka 2030 na makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabianchi.

  “imeelezwa kuwa mmepata fursa ya kuandaa mkakati wa kupunguza madhara mafuriko na ukame kwa kutumia taarifa ya muhtasari wa vihatarishi mlioujadili na hii imetoa fursa ya kujiamini katika kusimamia na kutatua majanga haya ambayo yamekuwa yakiikumba nchi mara kwa mara na kusababisha hasara kubwa za kiuchumi na kuongeza wigo wa umasikini nchini”,alisema Kanali Matamwe

  Katika kuhakikisha mipango hiyo inakuwa endelevu Kanali Matamwe alitoa rai kwa washiriki wa warsha hiyo kuainisha maeneo yanayohusu sekta zao na kuyafanyia kazi katika mipango ya bajeti na kuendelea kuongeza nguvu kwa kutenga bajeti ya kutosha katika masula ya kukabiliana na majanga. “Tukumbuke uwekezaji katika kupunguza madhara ya maafa ni hatua muhimu katika kupunguza matumizi ya fedha nyingi kwa ajili ya kukabiliana na madhara ya yanayoweza kutokea”,alisisitiza Kanali Matamwe

  Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na.7 ya mwaka 2015 na kanuni za usimamizi wa maafa za mwaka 2017 zimeanzisha Kamati za Usimamizi wa maafa ngazi ya Mkoa hadi Kijiji kwa lengo la kupunguza madhara ya maafa ili kuwa na jamii stahimilivu.

  Kwa upande wake mshiriki wa warsha hiyo Bw. John Kiriwai alieleza kuwa, kuna umuhimu wa kuwekeza nguvu na fedha katika masuala ya maafa kulingana na takwimu na taarifa zinazoeleza umuhimu wa kuwa na mikakati madhubuti ili kuwa mipango endelevu katika kukabili maafa. “Ni wakati sasa kuendelea kutumia fursa zilizopo kwa kuwekeza kwa kiwango kikubwa na kutumia taarifa za watafiti mbalimbali na kuziweka katika mipango yetu ya maendeleo ili kupunguza athari za maafa,”alisema Kiriwai.

  Naye Mwakilishi kutoka Wakala wa Barabara Bi.Zaharani Madai alieleza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hawana budi kuendelea kuwa na jitihada za makusudi za kuimarisha miundombinu kwa kuzingatia mazingira yaliyopo kwa kutumia wataalam katika kujenga na kuimarisha maeneo yanayodhaniwa kuwa hatarishi pindi maafa yanapotokea.

  “Ni wakati sasa wa kujijenga upya ili kuwa na mikakati inayotekelezeka katika kutatua na kukabili maafa kwa kuimarisha miundombinu tuliyonayo ili kuendana na mazingira ya kukabili maafa nchini,”alisisitiza Madai.

  0 0

  Na Anthony Ishengoma

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameiagiza Idara ya Ustawi wa Jamii kuhakisha inandaa haraka sana Sera ya Wazee kwa kuwa sera iliyopo ni ya siku nyingi na ilianza tangu mwaka 2003 hivyo inatakiwa sera mpya itakayoendana mabadiliko ya sasa.

  Aidha Dkt Ndugulile amesema hayo wakati wa hotuba yake ya kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya wazee nchini.

  Aidha Dkt. Ndugulile ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii pia kuarakisha mchakato wa kukamilisha mapema mswada wa sheria ya wazee wa nchini ili haki na stahili za wazee zisiwe suala la hiari bali ziweze kutekelezwa kwa mujibu wa Sheria.

  Dkt. Ndugulile pia ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii kuzingatia maelekezo aliyoyatoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tarehe 29 Januari Mwaka huu wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Ustawi wa Jamii kukamilisha mapema sheria ya masuala ya ustawi wa jamii Nchini ili ofisi yake iweze kutoa mrejesho kwa ofisi ya Waziri Mkuu juu ya utekelezaji wa suala hilo.

  Aidha Dkt. Ndugulile pia ameagiza sambamba na utekelezaji huo pia ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii pia kuharakisha maandalizi ya muundo wa kada ya ustawi wa jamii ambao utaainisha madaraja, kazi na nini watapaswa kufanya suala ambalo pia ni agizo la Waziri Mkuu.

  Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika maandalizi mapya ya Sera ya Afya nchini suala la wazee limepewa kipaumbele kwa kuzingatia masuala ya tiba kwa wazee na kwa mala ya kwanza Wizara imetambua sayansi ya tiba ya wazee na imetamkwa wazi katika sera ya Afya kwa mantiki hiyo katika Wizara ya Afya kutakuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya tiba na afya za wazee.

  Wakati huohuo Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Nchini Bw. Rabikira Mushi alimwambia Naibu Waziri Ndugulile kuwa moja ya maazimio ya Kikao kazi hicho kuarakisha mchakato wa kuanzisha mabaraza ya wazee kuanzia ngazi ya kata ili kuwezesha kuundwa kwa Baraza la Wazee la Taifa.

  Aidha Bw. Mushi pia aliongeza kuwa azimio jingine la msingi ni kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya suala la msingi la kuhakikisha jamii inajenga uelewa kuwa suala la kutunza wazee ni jukumu la familia na jamii yake.

  Aidha wazee hao pia wameazimia kuwa lazima serikali ihakikishe madirisha ya wazee yanakuwa na dawa muda wote kwani pamoja na uwepo dirisha hilo wakati mwingine madirisha hayo yanakuwa hayana dawa za kutosha kukidhi mahitaji ya matibabu ya wazee.

  Aidha wazee kupitia maazimio yao wazee wameiomba serikali kuwapa kipaumbele cha kupatiwa mikopo kama ilivyo kwa makundi mengine tete katika jamii ambayo yanapewa mikopo na serikali kama vile wanawake vijana na walemavu ili nao waweze kujikwamua kiuchumi.

  Aidha Kamishna Mushi alisema kuwa wazee pia walipendekeza kuwepo kwa kampeni ya nyumba kwa nyumba, mkono kwa mkono ili kukabiliana na mauaji ya wazee akiongeza kuwa kama kampeni hii ikifanikiwa Maafisa Ustawi wa Jamii wataweza kubaini wazee wote walioko katika hatari kuuawa.

  Kikao kazi hiki kimefanyika kufuatia kukamilika na kuzinduliwa kwa Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee na uliwakutanisha wawakilishi wazee, Maafisa Ustawi wa Jamii pamoja na Makanda wa Jeshi la Polisi kutoka kanda ya ziwa.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hotuba kwa wazee wakati wa kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hotuba kwa wazee wakati wa kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao mara baada ya kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akibadilisha na mawazo na Bibi Corotrida Kokupima muda mchache baada kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.

  0 0

  Na Ripota Wetu, Mwanza.

  Kijana mdogo mwenye umri wa miaka 18 tu kutokea kisiwani Ukerewe, mkoani Mwanza, anayejihusisha na ujasiriamali, Cathbert Masanal, amekabidhiwa fedha sake alizoshinda kutoka kwenye Bahati nasibu ya Watanzania ya Biko, akitokea kwenye droo ya 177 ijulikanayo kama Jumatamu Jenga.

  Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Mwanza kwa kumpatia mamilioni yake mshindi huyo aliyeanza rasmi harakati zake za kimaisha kwasababu ya kuingia kwenye umri wa ujana wa miaka 18, hivyo ni wazi ameanza vizuri kwenye mbio hizo za kimaisha.

  Akizungumzia ushindi wake huo, Manasal alisema kushinda fedha za biko kutarahisisha maisha yake kwa kuhakikisha kwamba anafanyia kitu cha maana ili ushindi huo uweze kumnufaisha kwa namna moja ama nyingine.

  Kucheza Biko sasa ni kuanzia sh 500 na sh 1000 na kuendelea, huku ushindi wake ukianzia sh 1000 hadi sh 100000 kwa watakaocheza sh 500 hadi sh 9500 wakati watakaocheza kwa sh 1000 na kuendelea, mchezaji anaweza kujishindia zawadi ya papo kwa hapo kuanzia sh 5000 hadi sh milioni moja bila kusahau wote kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili.

  Bahati nasibu ya Biko inachezwa kwa mitandao ya simu minne ambayo ni Tigo Pesa, M-Pesa, Artel Money na HaloPesa, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, huku Watanzania wakiweza kujishindia zawadi kubwa katika droo ya Jumatano na Jumapili.

   Kijana mwenye miaka 18 tu kutoka Kazilankanda, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, Cathbert Marco Masanal, akionyesha pozi baada ya kukabidhiwa fedha zake sh milioni 10 alizoshinda katika bahati nasibu ya Watanzania ya Biko droo ya 177 maarufu kama Jumatamu Jenga iliyotoa washindi sita wa mamilioni na bodaboda. Picha na Mpigapicha Wetu.

   Kijana mwenye miaka 18 tu kutoka Kazilankanda, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, Cathbert Marco Masanal, akionesha mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 alizoshinda katika bahati nasibu ya Watanzania ya Biko droo ya 177 maarufu kama Jumatamu Jenga iliyotoa washindi sita wa mamilioni na bodaboda.

  0 0

  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Shinyanga umefanya Bonanza la michezo lililohusisha michezo mbalimbali kwa lengo la kusherehekea miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  Bonanza hilo limefanyika Februari 2,2019 katika uwanja wa mpira wa CCM Kambarage uliopo mjini Shinyanga. 

  Akifungua bonanza hilo mgeni rasmi,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amepongeza jitihada zilizofanywa na serikali ya CCM kwa awamu nne zilizopita mpaka sasa awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kupiga hatua za kimaendeleo. 

  “Vitu vingi vikubwa vimefanyika kupitia CCM na serikali yake na jumuiya zake kwa ujumla, nchi yetu imeendelea kuwa salama miundombinu imeboreshwa barabara ndiyo usiseme Shinyanga haikuwa hivi, sekta ya afya , elimu vimeboreshwa na tulikuwa na ndege moja leo tunazo saba vyote hivi vipo ndani ya Ilani ya Chama”,alisema Mlolwa. 

  “Na mimi niombe tuendelee kuyaenzi maendeleo haya yaliyoletwa na CCM kwa vitendo”,aliongeza Mlolwa. 

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge aliwakumbusha vijana kuendelea kudumisha ushirikiano katika mambo yote yanayofanywa na chama pamoja na serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi wanaowatumikia. 

  “Nawashukuru sana ndugu zangu wote na viongozi wote wa serikali na chama mlioshiriki katika Bonanza hili tudumishe umoja na mshikamano kati yetu hivi ndivyo serikali yetu inataka” ,alisema Shemahonge. 

  Bonanza hilo limeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete , mchezo wa kuvuta kamba,kukimbia kwenye magunia ambapo viongozi wa serikali na chama cha CCM walishiriki. Kauli mbiu kwa mwaka huu inasema “Kazi ni kipimo cha utu ,chapa kazi tulinde uhuru na utaifa wetu”.
  Mgeni rasmi katika Bonanza la UVCCM Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akifungua bonanza la michezo lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Shinyanga katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga. Picha zote na Steve Kanyefu- Malunde 1 blog
  Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack katika bonanza hilo ambapo aliwataka vijana kushirikiana katika kuijenga Shinyanga wakishirikiana pamoja na serikali yao.
  Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) akimpatia zawadi ya jezi mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa katika ufunguzi wa bonanza hilo.
  Awali Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Husein Egabano akiongoza msafara wa vijana kuingia katika uwanja wa CCM Kambarage lilipofanyika bonanza hilo.
  Mgeni rasmi katika bonanza hilo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akifungua michezo katika bonanza hilo kwa kupiga penati.
  Baadhi ya wadau waliohudhuria katika bonanza hilo wakifuatilia kwa umakini matukio yanayoendelea uwanjani.
  Timu ya wanawake ambao ni wanachama wa CCM (wenye jezi za kijani) wakichuana vikali na timu ya watumishi wa serikali (wenye jezi za rangi nyekundu) katika mchezo wa pete, ambapo timu ya watumishi ilishinda kwa goli 14 dhidi ya wanachama 9.
  Mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa( katikati) akiwa pamoja mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba(kulia) pamoja na mwenyekiti UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) wakifuatilia michezo katika uwanja wa CCM Kambarage.
  Mpira wa miguu ukiendelea katika uwanja wa Kambarage hapa ni mchezo kati ya timu ya walimu kutoka chuo cha Shy com (wenye jezi ya kijani) na Timu ya Stand United chini ya miaka 20(jezi rangi ya chungwa)
   Mchezo wa kukimbiza kuku ukiendelea.  Kijana mshindi wa mbio za kukimbiza kuku akipongezwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba.
  Mchezo wa kukimbia kwenye magunia ukiendelea. 
  Vijana wa kikundi cha dance kijulikanacho kama The Fighter cha mjini Shinyanga wakionesha moja ya mchezo ambapo waliigiza mtu akicheza kama amechomwa kisu shingoni.  Mgeni rasmi akikabidhi zawadi ya kikombe kwa timu ya watumishi wa serikali walioshinda michezo mingi katika bonanza la michezo lililoandaliwa na UVCCM mkoa wa Shinyanga.

  0 0


  0 0

    Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Imwelu kilichopo wilaya ya Chato mkoani Geita.
   Wataalamu wa Tanesco ,REA na Mkandarasi wakipokea maagizo kutoka kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani
  Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano huo leo
  WACHIMBAJI wadogo mkoani Geita wanatarajiwa kufikishiwa Umeme katika mashimo yao ili kuwawezesha kufanya shughuli zao za uchimbaji kwa ufanisi mkubwa.

  Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Imwelu kilichopo wilaya ya Chato mkoani Geita.

  Alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika maendeleo ya nchi na kwa sasa umeme utafikishwa katika mashimo ya wachimbaji ili kurahisisha shughuli zao za uchimbaji.

  “Ndugu zangu wachimbaji tumeshaanza kuwapa transfoma kwa hiyo kama wewe ni mchimbaji na unataka uchimbaji wao uwe wa kisasa,utajaza fomu itakayowezesha kuendesha mashine zenu za kuchakata madini”Alisema.

  Waziri huyo aliwasihi wachimbaji wadogo kutumia fursa ya umeme ili kuleta tija katika uchumbaji wao na hivyo kuweza kuongeza pia ufanisi mkubwa.

  Hata hivyo Waziri Kalemani alimtaka Mkandarasi na Tanesco kufikisha umeme katika kijiji hicho ndani ya siku ishirini (20)  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Arusha
  WANARIADHA watakaoshiriki mashindano ya mbio za Nyika za Taifa Februari 16, mwaka huu katika viwanja vya Magereza Moshi, mkoani Kilimanjaro wameahidi kufanya makubwa zaidi.
  Kufanya vizuri kwenye mashindano hayo kutawapa fursa ya kushiriki mashindano ya mbio za Nyika za Dunia zinazotarajiwa kufanyika nchini Denmark Machi 30, mwaka huu.  Wakizungumza kwenye mazoezi yaliyofanyika viwanja vya Magereza Arusha wanariadha hao walisema chini ya mdhamini wao Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA),wamejaa tumaini la kufanya vizuri zaidi.
  Mwanariadha kutoka timu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Anjelina Daniel aliwashukuru NCAA kwa kuwadhamini ambapo amekuwa na wakati mzuri zaidi wa kufanya mazoezi.   “Ninawaahidi mashindano ya Nyika Moshi nitashika namba ya kwanza hapa nimekuwa wa pili,” alisema Anjelina.
  Kaimu Meneja wa Uhusiano NCAA Joyce Mgaya alisema Mamlaka ya Ngorongoro ilitambua fursa ya uzalendo kwenye mchezo huo na mingine.“Hili ni jukwaa linaloweza kutangaza vivutio vya utalii. Tuliona vizuri kuungana na RT kuwatia moyo wachezaji, tunaamini watakuwa mabalozi wazuri wa utalii,” alisema Mgaya.
  Naye Katibu Mkuu wa RT Wilhelm Gidabuday aliwashukuru NCAA kwa kuwashika na mkono.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kulia) akikagua mapipa 75 ya mafuta ya dizeli yaliyokamatwa katika bandari bubu eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam leo katika operesheni yake ya kupambana na magendo, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, ufukwe kwa ufukwe, mtu na mtu ili kukomesha biashara hiyo.
  Mapipa 75 ya mafuta ya dizeli yaliyokamatwa katika bandari bubu eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam leo katika operesheni yake ya kupambana na magendo, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, ufukwe kwa ufukwe, mtu na mtu ili kukomesha biashara hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kulia) akikagua mapipa 75 ya mafuta ya dizeli yaliyokamatwa katika bandari bubu eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam leo katika operesheni yake ya kupambana na magendo, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, ufukwe kwa ufukwe, mtu na mtu ili kukomesha biashara hiyo.


  Serikali wilayani Kinondoni, jijini Dar es S Salaam, leo imefanikiwa kuvamia bandari bubu ikiwa imehifadhi shehena ya mapipa 75 ya mafuta ya dizeli yaliyoingizwa nchini kinyemela ili kukwepa kodi. 

  Mafuta hayo yamenaswa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo aliyeongozana na maofisa wa TRA, EWURA na vyombo vya usalama. 

  Mfuta hayo yamekutwa yamehifadhiwa katika nyumba moja iliyopo Mtaa wa Kolekole, Kawe Beach, yenye namba KAW/MZN/1542. 

  Chongolo alisema, mafuta hayo yamethibitika kwamba ni mafuta ya dizeli na Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta (EWURA) na kwamba pia wamejiridhisha ni  dizeli na yameingia nchini kinyemela bila kufuata utaratibu. 

  Alisema mapipa yako 75 ni sawa na lita 17,000 ambapo thamani yake kwa tathimini ya wali ni zaidi y ash.milioni 20. Ofisa Mfawidhi wa Kitengo cha Kuzuia Magendo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania b(TRA) Hafidhi Abdallah, alisema wali tarifa ya kuwepo shehena ya mafuta katika eneo hilo tangu Januari 31 mwaka huu katika nyumba hiyo. 

  Alisema wahusika walifanikiwa kutoroka na wanaendelea kuwasaka na kwamba mafuta hayo yatataifishwa .

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi (kutoka kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Alphaxard Lugola, Waziri wa Katiba na Sheria Paramagamba Kabudi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Augustine Mahiga, ofisini kwake Mlimwa jijjini Dodoma Februari 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akioneshwa jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Richard Mayongera, ofisini kwake Mlimwa jijjini Dodoma Februari 3, 2019. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Katanga, ofisini kwake Mlimwa jijjini Dodoma Februari 3, 2019

  0 0

  Na Editha Karlo,Kigoma

  RAIS wa umoja wa  vilabu vya waandishi wa habari Tanzania(UTPC) Deogratius Nsonkolo ,amewahimiza wanahabari watumie fursa ya umoja wa vilabu vyao, kujiunga na huduma ya mfuko wa  Bima ya afya (NHIF) kwaajili ya kupata kadi za matibabu na kuwa na uhakika matibabu wanapougua wao na familia zao.

  Nsokolo ameyasema hayo jana Kigoma mjini wakati akifunga  Kikao kazi cha  wanahabari na viongozi wa mfuko wa bima ya afya ngazi ya Taifa  na mkoani humo lengo la kikao hicho ni kujenga mahusiano ya utendaji kazi baina ya Mfuko wa bima ya Afua Taifa(NHIF)na wanahabari wa Kigoma.

  Alisema ni wajibu wa wanahabari kwa kupitia kalamu zao kuelimisha jamii umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili wawe na uhakika wa matibabu pale wanaugua.

  "Hata sisi waandishi tunapaswa kuwa mfano katika suala hili la kujiunga na mfuko wa bima ya afya,kunabaadi hawana mikataba  ya kazi kwenye vituo vyao vya wanavyo fanyia kazi hivyo ni vyema tukanyima kwa fedha chache tunazopata tukajiunga kwani ugongwa ukija hauna taarifa unaweza ugumua huna hata mia ila ukiwa na kadi ya nhif unapata matibabu,"Alisema

  Alisema inatakiwa sasa klabu za waandishi nchini ziweke mkakati wa kila mwanachama atoe fedha kwa utaratibu utakaokubaliana kila mtu atoe kidogokidogo hadi  kiasi cha fedha sh.76,800  na zipelekwe katika mfuko wa NHIF waweze kupata kadi za matibabu.

   Meneja Uhusiano wa Mfuko wa bima ya afya NHIF Taifa Anjela Mziray asema NHIF ina mahusiano mazuri na klabu za waandishi wa habari katika Mikoa yote hiyo ni kwaajili ya kufanya kazi kwa pamoja kama timu hali kama hiyo inachochea wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya CHF au NHIF.

  "Niwaombe hata nyie Waandishi tumieni fursa ya Kikoa kujiunga na mfuko wa bima ya afya ,Serikali inataka kila mwananchi apate huduma bora za afya kuanzia vipimo na dawa kwa wakati,athari ya kutokuwa na bima ya afya ni janga kwa familia kukimbiana linapokuja suala la mchango wa kumtibia mgonjwa mfano,tatizo la kusafisha  figo Kwa mwezi unahitaji uwe na fedha si chini ya sh.milioni moja kwa mwananchi wa maisha ya kawaida ataweza?lakini ukiwa na kadi ya bima ya afya una kuwa na uhakika wa matibabu"Alisema

  Ofisa Uthibiti na Uhakiki wa ubora NHIF mkoani Kigoma  Dkt . Daniel Kihaya amesema waandishi wa habari  wathubutu kutoa habari zenye kuibua uwajibikaji baina ya watumishi wa afya,mwanachama na huduma za mfuko huo ili,kukomesha tabia ya watumishi wa afya wanaokwamisha dhana ya bima ya afya kwa maslahi yao binafsi.

  "Waandishi ni watafiti nyie muwe mnapita pita huko kwenye zahanati na hospital muibue mambo mbalimbali wanayafanya watoa huduma wasiowaaminifu kwa wanachama wa mfuko tukishirikiana tutakomesha tabia mbaya mbaya zote"alisema

  Takimu inaonyesha hadi sasa wananchi waliojiunga na mfuko wa bima ya afya ya NHIF na CHF ni 32% kwa nchini nzima,lengo  kufikia 50%ifikapo mwaka 2020 huku Mfuko wa NHIF ukiwa ni miongoni mwa mfuko bora unaotambulika kimataifa kwa utoaji  wa huduma bora ya Afya (ISO ,901/2015) .

   Kaimu Meneja wa NHIF kigoma Emanuel Kileo ataja moja ya matarajio ya kuongeza wigo wa wanachama ni pamoja na ujio wa  uzinduzi wa kampeni ya  Ushirika afya na kusisitiza kutokana na mashirikiano  na vyombo vya habari na wandishi wake watafanikiwa  kuibua na kutokomeza kero ya ulaghai wa utoaji huduma kwa watumiaji wa Mfuko huo.

  Meneja mahusiano wa mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)Angela Mziray akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi baina ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma na maofisa wa mfuko wa bima ya afya.

  Sehemu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na maofisa wa mfuko wa bima ya afya (NHIF)  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt Edwin P.Mhede akiongea na wadau wa Zao la Muhogo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Zao la Muhogo ulioratibiwa na TanTrade na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
  Wadau wa Zao la Muhogo wakiwa kwenye Mkutano wa wadau wa Zao la hilo ulioratibiwa na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
  Mama MWANTUMU MAHIZA akizungumza na Wadau wa Muhogo baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji na Wachakataji wa Muhogo Tanzania
  Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Wazalishaji na Wachakataji wa Muhogo Tanzania Bw.Burton Mwankuru Nsape(Kushoto) akiwa na Katibu Msaidizi Bw.Victor Vedasto Kabegu(Kulia)
  Afisa Masoko wa Kampuni ya EADL kwa kushirikia na TAEPZ akitangaza kununua Zao la Muhogo wakati wa mkutano na wadau wa zao hilo ulioratibiwa na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wa Kamati ya Muda ya Uongozi wa Chama cha Wazalishaji na Wachakataji wa Muhogo Tanzania chenye lengo la kuwa na sauti ya pamoja katika kuendeleza zao hilo wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mkutano wa Wadau wa Zao la Muhugo ulioratibiwa na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.
  Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Wizara ya Kilimo Bi Upendo Mndeme akizungumza kwenye mkutano wa mkutano wa wadau wa Zao la Muhogo ulioratibiwa na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.

  …………………………………………………………………….

  Wazalishaji wa Zao la Muhogo nchini wameshauriwa kuzalisha zao hilo kitaalam, kwa ubora, kiwango kinachohitajika kwenye soko na kwa kutumia mbegu bora inayozalisha mavuno mengi.

  Rai hiyo imetolewa na Dkt Edwin P.Mhede Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Zao la Muhogo ulioratibiwa na kufanyika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) jijini Dar es Salaam.

  “Wengi mnafahamu kuwa changamoto katika zao hili ni upatikanaji wa mbegu bora, aina ya mbegu inayoweza kukabiliana na magonjwa mbalimbali mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha uhaba wa upatikanaji wa mavuno ya kutosha na uzalishaji mdogo unaochagizwa na kilimo cha mashamba madogo madogo” alisema Mhede

  Alisisitiza kwa kuiomba Wizara ya Kilimo na Vituo vya Utafiti vya Kilimo kuendelea kutafiti juu ya changamoto hizi na kuimarisha huduma za ugani zenye kulenga uzalishaji wa tija ili kupata mazao mengi zaidi.

  Aliongeza kwa kusema kuwa kwa muda mrefu zao hili lilikuwa linategemewa kama zao la chakula pekee lakini kutokana na maendeleo ya uchumi na teknolojia kukuaa katika nchi zinazoendelea zimekuwa zikitumia Zao la Muhogo kutengenezea wanga ambao unatumika kwa matumizi mbalimbali viwandani vikiwemo viwanda vya karatasi, vinywaji na bidhaa kama nguo na makaratasi na kwa nchi nyingine wanatumia kuzalishia nishati mbadala aina ya Ethanol na kuzalisha sukari ya viwandani yenye ubora wa juu.

  Naibu Katibu Mkuu aliendelea kusema kuwa Zao la Muhogo ni zao rasmi la biashara hivyo linasaidia katika kuongezea pato la taifa. Kwa takwimu zilizopo katika kipindi cha mwaka 2015/16 Zao la Muhogo lilichangia asilimia 13.63 ya pato la taifa huku likiajiri wakulima wadogo zaidi ya milioni 1.3 Kati ya mwaka 2012 na 2016 kiasi cha tani 59,447,754 za Muhogo chenye thamani ya Dola za Marekani 4,804,926 uliuzwa nje ya nchi.

  Kwa upande wa masoko serikali inaendelea kuimarisha mfumo mzuri ambao utasaidia upatikanaji wa masoko hasa nje ya nchi. Zipo hatua zilizofanyika kwa nchi kama ya China yenye uhitaji wa Zao hilo kwa kuwa na mikataba ya pamoja uliohusu punguzo la ushuru wa forodha kwa bidhaa za Tanzania kuingia soko la China, mkataba wa itifaki ya Muhogo wa namna ya uingizaji wa zao hilo nchini China na kupitia mahusiano kati ya nchi na nchi. Na matokeo ya juhudi hizi zimeonekana kwa makampuni mbalimbali kutoka China kama vile Epoch Agriculture, Foshang Guangji Co. Ltd na Dar Canton Co Ltd zinazojishughulisha na ununuzi wa Muhogo na zikijiandaa kwa ujenzi wa viwanda nchini.

  Nae Bw Edwin Rutageruka, Mkurugenzi wa TanTrade alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili changamoto zinazolikabili Zao la Muhogo ili kujua jinsi ya kulikabili ingawa changamoto kubwa katika uzalishaji wa Muhogo ni namna ya kuliongezea thamani ili kuepuka changamoto za kimasoko

  Aidha aliongeza kwa kusema kuwa TanTrade itasimamia uanzishwaji na usajili wa Chama cha Wazalishaji na Wachakataji wa Muhogo Tanzania, lengo ni kuwa na sauti ya pamoja katika kuendeleza zao hilo. Chama hicho kitakuwa chini ya uangalizi wa TanTrade na makao makuu yake yatakuwa katika ofisi za TanTrade.

  Bi Upendo Mndeme Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Wizara ya Kilimo amewashauri wazalishaji wa Zao la Muhogo ili liwe la Kibiashara hasa katika nchi ya China lazima wazingatie vigezo vilivyoainishwa katika itifaki ya soko la Muhogo ambapo baadhi ya vitu ni bidhaa za Muhogo zisiwe na visumbufu vya wadudu na magojwa, wazalishaji na makampuni ya kuuza Muhogo nchini China kutambulika Kisheria, ubora wa bidhaa, bidhaa zifungashwe kulingana na matakwa ya soko la China, ukaguzi wa bidhaa kabla ya kuvuna na Wizara ya Kilimo au Kampuni/ Taasisi iliyopata kibali cha Wizara kwa ajili ya kazi hiyo n.k

  Baadhi ya Viwanda vya ndani vilivyojitokeza kununua Zao la Muhogo wamethibisha utoshelezi wa soko la ndani na uhitaji wao wa Zao hilo na wamehakikisha kuwa watalipandisha thamani Zao hilo kabla soko la nje kuwa na uhitaji mkubwa zaidi

  Hadi sasa mikoa inayozalisha Muhogo kwa wingi ni Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Lindi, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Kigoma

  0 0


  IMG_1712-min
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Kilimo na Masuala ya Ardhi wa Jamuhuri ya Kiarabu wa Watu wa Misri.Dkt.Ezzaldin O.Abusteit, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzi, akiongozana na Ujumbe wake na kulia Balozi wa Misri Nchini Tanzania Mhe. Gaber Mohamed
  IMG_1730-min
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Kilimo na Masuala ya Ardhi wa Jamuhuri ya Watu wa Misri. Dkt. Ezzaldin.O.Abusteit, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais Ikulu Zanzibar
  IMG_1783-min
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na mgeni wake Waziri wa Kilimo na Masuala ya Ardhi Jamuhuri ya Kiarabu ya Watu wa Misri.Dkt. Ezzaldin O.Abusteit, wakitoka katika ukumbi baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar.3-2-2019
  IMG_1797-min
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Waziri wa Kilimo na Masuala ya Ardhi wa Jamuhuri ya Kiaranu ya Watu wa Misri Dkt. Ezzaldin .O. Abusteit, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar.3-2-2019, anayefuata Balozi wa Misri Nchini Tanzania Mhe. Gaber Mohamed.(Picha na Ikulu)

  0 0  NJOMBE 

  Mtoto mwenye umri wa miaka 7 anaefahamika kwa jina la Recho Malekela mkazi wa kitongoji cha Lung’angali kijiji cha Matembwe wilayani Njombe ameuawa kwa kuchinjwa koromoe na kutupwa katika msitu uliojirani na nyumbani kwao. 

  Mtoto huyo wa darasa la pili katika shule ya msingi Matembwe ameuwawa ikiwa siku mbili zimepita tangu kikosi maalumu cha kiinteligensia kiwasiri mkoani Njombe kuongeza nguvu katika kuwasaka watu wanaotekeleza mauaji hayo ya kikatili dhadi ya watoto wadogo ambayo yaliomengi yanahusishwa na visasi pamoja imani za kishirikina. 

  Akizungumza nyumbani kwa marehemu mara baada ya kushiriki mazishi ya mtoto Rachel na kutoa rambrambi kwa wafiwa Mbunge wa viti maalumu kupitia CCM Neema Mgaya amewata wananchi kuachana na tabia ya kushambulia watu watuhumiwa wa matukio hayo ya ukatili dhidi ya watoto pindi wanapo wabaini na badala yake wawafikishe katika vyombo vyenye dhamana ya ulinzi ili wahojiwe na kusaidia kubaini mtandao wa wauaji hao. 

  Mgaya anatoa kauli hiyo ikiwa tayari watu wawili wameuawawa na wananchi wenye hasira kali wilayani Ludewa na Mmoja Wilayani Wanging’ombe baada ya kuhisiwa kujihusisha na matukio ya utekaji hatua ambayo imefanya jeshi la polisi kukosa taarifa kutoka kwa watuhumiwa. 

  Awali akizungumza katika ibada ya kuaga mwili wa marehemu mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amesema serikali imeshitushwa na mauaji yanayoendelea na kwamba tayari kikosi kilichosheheni wataalamu mbalimbali wa upelelezi kilichotumwa na mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Saimon Siro kimeanza kazi ya kuwabaini wahusika huku kikiwa tayari na kimewashikiria watu kaadhaa kwa mahojiano. 

  Msafiri amesema mauaji yanayoendelea yanachafua sura ya amani na kudai kwamba damu ya mtoto Rachel itawatafuta popote walipo wauaji na kuwafikisha katika vyombo vya sheria . Baba mkubwa wa marehemu akizungumza na mwandishi wetu amesema mtoto huyo alitekwa mchana wa february mosi akiwa anatoka shambani jirani na nyumbani kwao baada ya kutumwa na mama mzazi kwenda nyumbani kupika maharage. 

  Nae Bryson Mlote mwenyekiti wa kijiji cha Matembwe anaeleza historia ya matukio kama hayo kijijini hapo ambapo anasema inaelezwa miaka ya zamani kulitekelezwa matukio kama hayo na kwamba taarifa za kutekwa zianza kusambaa jioni ya februari mbili ambapo zoezi la kumtafuta lilianza saa kumi na mbili na kufanikiwa kumpata majira ya saa nne usiku katika msitu uliojirani na nyumba yao akiwa amekatwa shingoni na kitu chenye ncha kali.

  0 0

  5
  6
  Washiriki wa Mkutano wa NHIF na Wanahabari  wa Kigoma wakifuatilia ufafanuzi wa hoja zinazohusu huduma za Mfuko.
  Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anjela Mziray akizungumza katika mkutano wa Mfuko na Wanachama wa Chama cha Wanahabari wa Mkoa wa Kigoma.
  2
  Kaimu Meneja wa NHIF Kigoma, Bw. Emmanuel Kileo akiwasilisha mada kwa wanahabari wa Mkoa wa Kigoma.
  3
  Washiriki wa Mkutano wa NHIF na Wanahabari  wa Kigoma wakifuatilia ufafanuzi wa hoja zinazohusu huduma za Mfuko.
  4
  Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Mkoa wa Kigoma, Bw. Deogratius Nsokolo akifafanua jambo juu ya mchango wa wanahabari katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko.
  7
  Picha ya pamoja kati ya Maofisa wa NHIF na Wanahabari wa Mkoa wa Kigoma

  ……………………………………………………………………………….

  Na Grace Michael, Kigoma
  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeimarisha utekelezaji wa majukumu na kurahisisha huduma kwa uwekezaji kwenye mifumo ya TEHAMA inayomwezesha mwanachama kupata huduma kwa haraka zaidi pamoja na Watoa huduma kuwasilisha madai yao kwa haraka.
  Maboresho haya yamefanyika na yanaendelea kufanyika kwa lengo la kuwarahisishia wanachama upatikanaji wa huduma na kuondokana na changamoto ambazo awali zilikuwepo za ucheleweshaji wa huduma mbalimbali ikiwemo utoaji wa vitambulisho na upatikanaji wa taarifa za wanachama.

  Akizungumza katika mkutano baina ya NHIF na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma, Meneja Uhusiano wa Mfuko, Bi. Anjela Mziray alisema kuwa uimarishaji wa mifumo ya huduma unaofanywa na Mfuko umewezesha kutatua changamoto za upotevu wa muda kwa wanachama wanapokuwa vituoni, kurahisisha utambuzi wa mwanachama kabla ya huduma, lakini pia kurahisisha uwasilishaji na ulipaji wa madai ya Watoa Huduma.

  “Lengo la Mfuko ni mwanachama wetu apate huduma kwa haraka na aweze kuwasiliana nasi kwa haraka anapohitaji, uimarishaji huu wa Mifumo ambao umefanyika na unaoendelea kufanyika, kwanza kabisa unawezesha upatikanaji wa taarifa za wanachama kwa haraka wanapokuwa katika vituo vya kupata huduma na inapotokea changamoto yoyote inatatuliwa kwa haraka zaidi tofauti na awali,” alisema Bi. Mziray.

  Alieleza kuwa Mfuko sasa unaendelea na jitihada za kuwaunganisha watoa huduma wengi zaidi na mifumo hiyo ili waweze kuwasilisha madai yao kila siku mara huduma inapotolewa kwa mwanacha bila kusubiri mwisho wa mwezi. Hii inasaidia kushughulikia dai la mtoa huduma kila linapowasilishwa na hivyo kupunguza muda unaotumika kuchakata madai na hivyo kuongeza ufanisi. 

  “Kwa sasa tayari kuna baadhi ya Watoa huduma ambao wameanza kutumia mfumo wa uwasilishaji wa madai kwa Mfuko kila siku na hatua hii mbali na kurahisha malipo lakini pia inaziba mianya ya udanganyifu na kuwezesha ulipaji wa madai halali yaliyotumiwa na wanachama,” alisema Bi. Mziray.
  Akizungumzia suala la kuongeza wigo wa wanufaika wa huduma za NHIF, alisema kuwa Mfuko kwa sasa uko katika hatua za mwisho za kuanzisha utaratibu ambao utawezesha watu wengi kujiunga na kunufaika kwa namna mbalimbali kulingana na mahitaji yao.

   “Mipango yetu ni kuhudumia asilimia 50 ya wananchi ifikapo mwaka 2020 na badae kuwafikia wananchi wote hivyo maboresho na uimarishaji wa huduma tunaoufanya ni kujipanga na utoaji wa huduma kwa wananchi wote ili kila mtanzania aweze kupata huduma za matibabu kwa utaratibu rahisi wa bima ya afya,” alisema Bi. Mziray.

  Naye Kaimu Meneja wa NHIF Mkoa wa Kigoma, Bw. Emmanuel Kileo alisema kuwa uwepo wa Ofisi ya NHIF mkoani hapo imesaidia kwa kiasi kikubwa kusogeza huduma kwa wananchi ambapo kwa sasa maofisa wa Mfuko wanawafikia wananchi mpaka ngazi ya kijiji na kuwapatia elimu ya umuhimu wa kujiunga na huduma.

  Wakichangia hoja juu ya huduma za Mfuko, wanahabari wa Mkoa wa Kigoma, wameupongeza Mfuko kwa jitihada kubwa ambazo zimefanyika hususan katika kuyafikia makundi mbalimbali na kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama wake.

  Akitoa  shukrani kuhitimisha mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kigoma Bw. Deogratius Nsokolo alisema watauendeleza uhusiano uliopo baina yao na Mfuko huu  hususan katika kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua.

  0 0
  0 0


   Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akikabidhi kompyuta kwa Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (wa pili kulia) kwa ajili ya shule za sekondari mjini humo. Wakishuhudia, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela (wa pili kushoto)
   Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na waalimu wa sekondari (hawapo pichani) kuhusu ukuaji na maendeleo wa sekta ya Mawasiliano nchini. Kulia kwake ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela 
   Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard akitoa maelezo ya kompyuta walizotoa kwa shule za sekondari za Mpanda. Walioketi wakimsikiliza, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na  katikati ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi
   Afisa Elimu wa Shule za Sekondari wa Manispaa ya Mpanda, Enelia Lutungulu akisoma risala ya shukrani kwa Serikali kwa niaba ya waalimu na wanafunzi wa shule kwa kuzipatia shule hizo kompyuta 25. Walioketi wakimsikiliza wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na  katikati ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi
   Waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati akiwahutubia kabla ya kukabidhi kompyuta kwa ajili ya shule za sekondari za Mpanda
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akisisitiza jambo kwa Afisa Usalama Msaidizi wa Uwanja wa Ndege wa Katavi, Fredrick Valentine(wa kwanza kulia) wakati akikagua miundombinu na hali ya uwanja huo akiwa ziarani mkoani humo. Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (wa tatu kulia) akifuatilia kwa makini mazungumzo hayo .
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama mbele amefunga mikono) akiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda. Wan ne kulia ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi na wa tano kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amekabidhi kompyuta 25 kwa shule za sekondari Mpanda mkoani Katavi kwa lengo la kukuza kiwango cha ufaulu na kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) shuleni kwa kuwawezesha waalimu kutumia kufundishia na wanafunzi kujifunzia

  Nditiye amewataka waalimu na wanafunzi wa shule hizo kuhakikisha kuwa kompyuta zilizotolewa zinatumika kwa nia njema kutoa elimu kwa watoto wetu kwa kuwa sasa dunia ni kijiji. Amefafanua kuwa lengo ni tupate wanafunzi mahiri kwa kompyuta hizo kutumika na wanafunzi wengine kwenye shule mbali mbali kwa kuziunganisha kompyuta hizo kwenye mtandao ili mwalimu mmoja aweze kufundisha wanafunzi wengi wengine wa shule nyingine

  “Kumbukeni hapo zamani wanafunzi wa mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma ilikuwa inatoa wanafunzi wenye ufaulu mzuri, hivyo tuwarithishe wanafunzi wetu,” amesisitiza Nditiye

  Kompyuta hizo zimetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambao una dhamana ya kuhakikisha wananchi waishio vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara wana wasiliana kwa kuzipatia kampuni za simu za mkononi ruzuku ya kujenga minara ili kufikisha huduma za mawasiliano maeneo mbali mbali nchini

  Nditiye amekabidhi kompyuta 25 zenye thamani ya shilingi milioni 46 kwa Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi kwa niaba ya waalimu na wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo mjini humo kwa kuwa aliiomba Serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu ili shule hizo ziweze kupatiwa kompyuta hizo

  “Nimeanza kumsumbua Nditiye zaidi ya mwaka mmoja na nusu kuomba kompyuta, unaweza kuona kompyuta ni chombo chepesi ila sio hivyo kwa kuwa ni chombo muhimu na kitatunza siri,” amesema Kapufi

  Pia, ameongeza kuwa tunalotekeleza hapa ni upendo na na litaenda kufuta ujinga wa watoto wetu kwenye shule za sekondari kwa kutumia kompyuta hizi. Vile vile ameishukuru Serikali kwa ahadi ya mafunzo ya kompyuta ambayo yatatolewa kwa waalimu wa shule ili kuwawezesha namna ya kutumia na kufanyia matengenezo madogo madogo kompyuta hizo ambapo ameahidi kuwa atakwenda yeye mwenyewe binafsi kukabidhi kompyuta hizo kwa kila shule

  Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka UCSAF Mhandisi Albert Richard amesema kuwa UCSAF imekuwa ikitoa kompyuta hizo kwenye shule mbali mbali nchini kupitia mradi wa kuunganisha shule ujulikanao kama “School Connectivity”. Richard amesema kuwa ni imani yao kuwa kompyuta hizo zitatumika kwa malengo yaliyopangwa kwa nia ya kuwasaidia wanafunzi kusoma na waalimu kufundishia. Ameongeza kuwa UCSAF itatoa mafunzo kwa waalimu wa shule za sekondari za Mpanda ya namna ya kutumia kompyuta hizo kufundushia pamoja na waalimu wao wenyewe kuweza kuzifanyia matengenezo madogo madogo kompyuta hizo pale zinapoharibika

  Akizungumza kwa niaba ya waalimu wa shule za sekondari za Mpanda, Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Mpanda, Enelia Lutungulu amesema kuwa shule za msingi na sekondari zina uhitaji mkubwa sana wa kompyuta kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia na TEHAMA ambapo kazi nyingi zinahitaji mawasiliano kwa kutumia kompyuta

  “Shule hizi zina uhitaji mkubwa wa kompyuta kwa kuwa baadhi ya shule kompyuta zinazotumika ni za waalimu binafsi na hivyo kuleta ugumu wa utendaji wa kazi wa kila siku ukizingatia upokeaji na utoaji wa taarifa ni wa kila mara,” amefafanua Lutungulu

  Ameongeza kuwa kompyuta hizo zitakuwa kichocheo cha kuongeza na kurahisisha ufanisi wa kazi katika shughuli mbali mbali zikiwemo za uchapishaji wa mitihani ndani ya shule, ukusanyaji na uhifadhi wa data za kielimu katika shule, utoaji rahisi na wa haraka wa taarifa kwa kutumia TEHAMA, kupokea miongozo na maagizo mbali mbali ya kikazi kwa kutumia mawasiliano ya barua pepe, kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ikiwemo TEHAMA na mawasiliano katika kazi za kila siku. Makabidhiano ya kompyuta hizo yamehudhuriwa na wakuu wa shule za sekondari, viongozi na wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mpanda na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya hiyo

  Akiwasilisha taarifa ya mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Abdallah Malela amemuomba Nditiye kuipatia mkoa huo ofisi ya TTCL ya ngazi ya mkoa tofauti na hali ilivyo sasa ambapo ipo ofisi ya TTCL ya ngazi ya wilaya. Pia, ameongeza kuwa mkoa upatiwe usafiri wa ndege kwa kuwa ina kiwanja kizuri na kuna wateja wa kutosha

  Nditiye amepokea changamoto hizo na kuielekeza Bodi ya TTCL na menejimenti yake kufungua ofisi ya Shirika hilo lenye hadhi ya mkoa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja. Pia, ameuhakikishia uongozi wa mkoa na wananchi wa Katavi kuwa Serikali inaleta gari la zimamoto kwenye uwanja huo na huduma za usafirishaji utaanza kutolewa kwa wananchi na wadau wa mkoa huo. Pia, Nditiye alitembelea na kukagua kiwanja hicho cha ndege na kuona hali ya kiwanja na miundombinu yake


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Na Imma Msumba na Elinipa LUPEMBE, Arumeru

  Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro, amewataka Maafisa watendaji wa kata na vijiji wilayani humo, kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, kwa kuweka mbele maslahi ya taifa ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.

  Mkuu huyo wa wilaya ametoa rai hiyo, wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha maafisa tarafa na Maafisa watendaji wa kata na vijiji wa halmashauri zote mbili za wilaya ya Arumeru, chenye lengo la kuwakumbusha na kuwajengea uwezo watalamu hao katika kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.

  Amesema, kama wilaya wamemekubaliana kuanzisha programu maalumu ya mafunzo kwa watendaji hao, kwa kushirikiana na chuo kilichopo ndani ya wilaya hiyo, chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, baada ya kugundua uhitaji wa mafunzo kwa watalamu hao, mafunzo yatakayowawezesha kuwa na uelewa wa pamoja katika kuteleleza majukumu yao.

  Amesema kuwa Maafisa hao huajiriwa kutoka kwenye kada tofauti, jambo ambalo wakati mwingine, linalopelekea changamoto ya kukwamisha baadhi ya kazi, kupitia mafunzo hayo yatawawezesha kuwa na uelewa wa pamoja na kufahamu majukumu yao na mipaka ya kazi yao, kufanya kazi kwa uadilifu, kujiamini, kuongeza ari na morari ya kazi, pamoja na kuweka mbele uzalendo kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

  "Tumegundua kuna umuhimu kupata mafunzo kwa watendaji wote, yatakayowakumbusha na kuwawezesha kutambua namna sahihi ya utekelezaji wa kazi zenu za kila siku, hii imetokana na baadhi ya watendaji kushindwa kutekeleza majukumu yenu kwa usahihi na kusababisha malalamiko mengi kwa wananchi" amesema Mkuu huyo wa wilaya.8

  Hata hivyo Mhe. Muro amewasisitiza watendaji hao kusimamia hali ya usalama katika maeneo yao, kwa kutambua wageni wanaoingia na kutoka katika maeneo yao, kuhamasisha wananchi kushiriki kuchangia maendeleo katika maeneo yao, huku kipaombele kikiwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa hususani kwenye shule za sekondari, lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za serekali la kutoa elimu bila maliopo linalotoa fursa ya kila mtoto kupata nafasi ya kusoma mpaka kidato cha nne.

  "Kazi kubwa ya mwaka huu ni kujenga vyumba vya madarasa, ninawaomba Maafisa Watendaji, tuelekeze nguvu zetu kuhamasisha jamii kujikita katika kujenga madarasa, nataka nione kila Tarafa ina shule ya kidato cha 5-6 na kila kata ya kidato cha 1-4" amesema Mhe. Muro

  Kwa upande wao wakurugenzi wa halmashauri zote mbili, wamewataka Maafisa Watendaji hao kusimamia shughuli za maendeleo kwa kuendana na kasi ya serikali iliyopo madarakani,serikali ya awamu ya tano, kuwa waadilifu katika kutekeleza kazi zao, kutoa huduma sawa kwa wananchi na kusimamia haki, na kuongeza kuwa hawatosita kuwachukulia hatua wale wote watakaofanya kazi kinyume na maadili.

  Kikao kazi hicho, kiliambatana na mafunzo yaliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii kutoka chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, Mkufunzi Douglas Mwadolago, mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo watendaji hao ya mbinu bora za kuhamasisha jamii, kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

  Hata hivyo watendaji hao, wamesifu juhudi zinazofanywa na halmashauri zao kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya, na kusema kuwa mafunzo hayo yanawaongezea ujuzi na maarifa zaidi ya kutekeleza kazi zao na kuahidi kwenda kutumia maarifa waliyoyapata katika kazi zao za kila siku.

  Afisa Mtendaji wa kijiji cha Kikuletwa kata ya Mbuguni, halmashauri ya Meru, Flora Maghimbi amesema kuwa, amefurahishwa na mafunzo hayo na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi, huku akiahidi pia kutekeleza maagizo yaliyotolewa kwa kuwa yote yanalenga maslahi ya jamii wanayoihudumia.

  Awali, Wilaya ya Arumeru inaundwa na halmashauri mbili, halmashauri ya Arusha na Meru, ikiwa na jumla ya Tarafa 6, kata 53 na vijiji193.
  .
   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro akizungumza na Maafisa Watendaji wa kata na vijiji,  wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
   Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Meru Emanuel Mkongo, akizungumza na Maafisa Watendaji wa kata na vijiji,  wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha

  Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Dc Dr. Wilson Charles Mahera, akizungumza na Maafisa Watendaji wa kata na vijiji,  wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.

  0 0

  Je, unafahamu kwamba unaweza kujiajiri kupitia Jumia?
  • Pata kamisheni kwa kuuza bidhaa zinazopatikana Jumia.
  • Zaidi ya mawakala 600 wamekwishajiunga.

  Timiza ndoto zako za kibiashara kwa kujipatia kipato zaidi na zaidi! Kuwa bosi wako mwenyewe kwa kufanya shughuli zako na kujiingizia kipato bila ya mtu kukusimamia. Ndiyo kauli mbiu ambayo Jumia inaitumia kwa sasa katika kuwahamasisha vijana wa kitanzania kutumia fursa zilizoletwa na teknolojia kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa pekee.

  Kampuni hii ambayo inajishughulisha na kuuza bidhaa kwa njia ya mtandaoni Tanzania imeanzisha programu inayokwenda kwa jina la ‘Jumia JForce.’ Huu ni mtandao wa wataalamu wa ushauri wa mauzo ambao hujiingizia kipato kwa kuwasaidia wateja kufanya manunuzi ya bidhaa zinazopatikana kwenye tovuti ya Jumia. Kwa sasa kuna mawakala takribani 600 waliotapakaa Tanzania nzima.
  Changamoto ya ajira ni kubwa duniani kote na sio nchini Tanzania pekee au barani Afrika kwa ujumla. Kwa mujibu wa Ripoti ya Mtazamo wa Uchumi wa Afrika ya mwaka 2019 iliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, imeainisha kuwa nguvu kazi ya Afrika inatarajiwa kuongezeka kwa 40% zaidi kufikia 2030. Inaendelea zaidi kwa kufafanua kuwa, endapo mienendo iliyopo sasa ikiendelea, ni nusu pekee ya nguvu kazi mpya inayoingia ndiyo itakayopata ajira, na ajira nyingi zitakuwa kwenye sekta zisizo rasmi. Hii ina maanisha kwamba vijana takribani milioni 100 watakuwa bila ya ajira.

  Akifafanua namna Programu ya Jumia JForce inavyoweza kuwa mwarobaini wa changamoto ya ajira kwa vijana, Nahodha wa Wakala wa Mauzo wa Jumia - Tanzania, Bi. Elizabeth Samson amesema kuwa, “Kuwa bosi wako mwenyewe, ‘kamwe usiseme haiwezekani.’

  Mwaka mmoja nyuma kama angekuja mtu na kuniambia kuwa unaweza kujiingizia kipato cha zaidi ya laki moja na kuendelea kwa kujifanyia shughuli zako mwenyewe, ningemwambia apeleke hizo hadithi kwa ndege wa mwituni. Mtu pekee ambaye anaweza kukuzuia kufanya hivyo ni wewe mwenyewe. Kwa mafunzo na nyenzo zinazopatikana Jumia JForce, ni rahisi kuanza kuingiza kipato mara moja na kukuza mapato yako kwa urahisi, hakuna kuwekeza mtaji kabisa. Kama wakala wa JForce, unaweza kuwa vile unavyotaka kuwa, ishi ndoto zako na ujenge mustakabali wa baadaye!”

  Programu ya mawakala wa mauzo kutoka Jumia ina malengo ya kuwapatia uwezo na kuwaimarisha watu wanaotarajia kuwa wajasiriamali kwa kuwapatia msaada wa kukuza biashara zao. Jiunge kwa kulipia gharama ndogo na kisha uanze kuingiza kipato kwa kuuza bidhaa za Jumia zinazokuzunguka.

  Faida 5 za kujiajiri kupitia Jumia JForce

  Unajiingizia kipato chako mwenyewe. Unapata kamisheni kwa kuuza bidhaa zinapatikana katika tovuti ya Jumia kutoka kwa wauzaji tofauti. Unalipwa kutokana na juhudi zako za kuweza kuwashawishi wateja wengi zaidi kununua bidhaa: kadri unavyofanya kazi, ndivyo unavyolipwa zaidi!

  Bosi ni wewe mwenyewe. Ukiwa kama wakala wa programu ya mauzo, una uhuru kamili na udhibiti wa shughuli uzifanyazo. Jenga biashara yako yenye kukunufaisha wewe mwenyewe. Hakuna cha kukuzuia! Pia, unaunda timu yako mwenyewe ya mawakala wa mauzo ambayo itakuwa inaripoti kwako na kuisimamia.

  Unapatiwa mafunzo bure. Kadri unavyokua ndivyo unavyozidi kujiongezea malipo ya kamisheni. Utapatiwa ujuzi na mafunzo ya hali ya juu. Utanahakikishiwa kwamba unakuaa mfanyabiashara uliyewezeshwa kikamilifu.

  Unafurahia kile unachokifanya. Uza bidhaa na uzawadiwe. Pata maarifa mapya na ujijengee uwezo wa kujiamini. Kutana na watu wapya na utengeneze marafiki wapya. Pata fursa ya kuhudhuria matukio ya Jumia kama vile hafla, semina na warsha mbalimbali.

  Faida. Pata fursa ya kujua promosheni za kila siku. Furahia kujipatia kipato kupitia kulipwa kamisheni. Shiriki bure mafunzo yote ya Jumia na ujipatie ujuzi wa kazi yako! Hauhitajiki kuwa na uzoefu, bali msukumo na shauku kubwa ya biashara!

  Unasubiri nini kuichangamkia fursa hii? Ikiwa ndio mwanzo wa mwaka wa 2019 ambao umejaa fursa lukuki siku za usoni ni vema kufanya maamuzi ya kujiunga sasa. Kwasababu hivi punde kampeni mbalimbali za mauzo zinatarajiwa kuzinduliwa ikiwemo ya msimu wa wapendao au ‘Valentine’s’ ambayo inatarajiwa kuanza Februari 4 mpaka 16.  

  0 0

   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mstaafu (Mdau wa Maendeleo), Injinia, Rajabu Rukombe (katikati) wakati alipomtembela ofisini kwake kwa ajili ya kumgawia vitabu ambavyo Mhe. Spika pia atawapatia viongozi mbali mbali wa kitaifa, vitabu vyenye maudhui makuu matatau (3), ikiwemo kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuonyesha jitihada na umuhimu wa uchumi wa viwanda pia tufanye nini kufikia lengo la viwanda kikao kilichofanyika leo tarehe 4 Februari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni mwanae Injinia, Ndg. Rukombe Rukombe.
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipokea vitabu kutoka kwa Mstaafu (Mdau wa Maendeleo), Injinia, Rajabu Rukombe (katikati) alipomtembela leo tarehe 4 Februari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Vyenye maudhui makuu matatau (3), ikiwemo kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuonyesha jitihada na umuhimu wa uchumi wa viwanda pia tufanye nini kufikia lengo la viwanda, Kulia ni mwanae Injinia, Ndg. Rukombe Rukombe
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mstaafu (Mdau wa Maendeleo), Injinia, Rajabu Rukombe (kushoto) alipomtembelea leo tarehe 4 Februari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kumgawia vitabu ambavyo Mhe. Spika pia atawapatia viongozi mbali mbali wa kitaifa, vyenye maudhui makuu matatau (3), ikiwemo kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuonyesha jitihada na umuhimu wa uchumi wa viwanda  pia tufanye nini kufikia lengo la Tanzania ya viwanda. Kulia ni mwanae Injinia, Ndg. Rukombe Rukombe
  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

older | 1 | .... | 1794 | 1795 | (Page 1796) | 1797 | 1798 | .... | 1897 | newer