Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

UGONJWA WA MALARIA WAPUNGUA KWA KIASI KIKUBWA KWA AKINAMAMA WAJAWAZITO NA WATOTO

$
0
0
   Mtaalamu wa magonjwa ya Damu, Vinasaba na Saratani Professa Lucio Luzatto wa Chuo cha MUHAS akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.   Wageni waalikwa na wafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.    Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akiwasiliasha mada ya 'Malaria kwa akinamama wajawazito na Watoto' katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.  Mtaalam wa Masuala ya Dawa wa Chuo cha MUHAS, Prof. Omary Minzi akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.    Wageni waalikwa na wafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Andrew Barnabas Pembe akifatilia kwa makini mada.  Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha MUHAS, Dkt Bill Ngasala akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.  Wageni waalikwa na wafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.  Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Julie Makani (kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya ugonjwa wa Siko Seli unavyoendana na ungonjwa wa Malaria.  Mtafiti wa Malaria wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu kilichopo Bombo Hospitali, Tanga, Deus Ishengoma akizungumzia ukata wa fedha unavyonyongonyesha tafiti bunifu.  Mmoja ya mdau wa masuala ya afya akiuliza swali...  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma MUHAS na Mloganzila, Hellen Mtui akitoa shukrani zake za pekee kwa wote walioweza kushiriki katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.  Mwenyekiti wa Muhadhara huo, Prof. Lyamuya akihitimisha kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Utafiti umeonyesha ugonjwa wa Malaria kwa akinamama wajawazito na watoto umepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na awali. Kwa upande wa Zanzibar ugonjwa wa Malaria umepungua kwa kiwango kikubwa hivyo ni vyema Tanzania Bara kuendelea kupambana ili ifikapo 2030 tatizo la ugonjwa wa Malaria kwa jamii limekwisha. 

Hayo ameyabainisha Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma wakati akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni 'Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya malaria Tanzania' lililofanyika jijini leo Dar es Salaam. 

Amesema kuwa kadili mama mjamzito anavyotumia vizuri dawa za kujikinga na ugonjwa wa Malaria wakati akiwa amepata ujauzito ndivyo anavyoweza kuepukana na ugonjwa huo. "Kawaida mama mjamzito anapofika wiki ya 13 huwa anapewa dawa za kuzuia Ugonjwa wa Malaria kwa ajili ya yeye na kumkimkinga mtoto, hivyo akizitumia sawa sawa kwa kufuata maelekezo ya dokta pindi anapojifungua huwa salama," amesema. 


Prof Kamuhabwa amesema kuwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam imeonyesha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria yamepungua chini ya asilimia moja jambo linaloletea faraja kubwa. 


"Tafiti ni jukumu letu kubwa na tunaangalia magonjwa ya kipaumbele katika nchi na Malaria ni ugonjwa wa kipaumbe maana unaathiri akinamama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 5 hivyo hatuna budi kupambana zaidi" amesema. Amesema kwa sasa MUHAS wanaendesha tafiti nyingine ya dawa mbadala ya Malaria kwa akinamama wajawazito na watoto maana dawa ile ya awali SP imeonyesha kuwaletea sugu akina mama. 

"Tunafanya tafiti huko Rufiji ya dawa mbadala ya kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria ambapo Shirika la Afya Duniani limetutaka tufanyie utafiki katika nchi mbali mbali dunia japo wenzetu Kenya na Uganda matokeo yameonyesha dawa hiyo inafanya vizuri lakini kabla hapa kwetu hatujaanza kuitumia lazima nasi tufanye utafiki ila matokeo ya awali yanaonyesha dawa hii inafanya vyema. Dawa wanayoifanyia utafiti inamchanganyiko wa mseto na dawa nyingine ili kupata mbadala na kuachana na SP kwa ajili ya kinga ya akina mama wajawazito na watoto ila tunamalizia utafiti ili tuje tutoe matokeo ifikapo machi mwaka huu. 

Kwa upade wake Mtafiti wa Malaria wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilichopo Bombo Hospitali, Tanga, Deus Ishengoma ameiomba serikali kuwasaidia watafiti ili waweze kuibua tafiti zinazotoa majibu tofauti kwa jamii ambapo ka sasa ambapo tafiti nyingi zimekuwa zikigharimiwa na mashirika ya nje jambo linalowanyima uhuru kwa kufanya tafiti za kigunduzi. 

"Serikali iliahidi kutoa asilimia moja ya pato la Taifa ili kuwawezesha watafiti nchi nzima ili waibue tafiti za kigunduzi, lakini mpaka leo kimya... tambueni fedha tunazopewa na mashirika ya nje zinakuwa zimelenga kile wanachokitaka wao na tufanye tofauti na tungewezeshwa kufanya tafiti za kigunduzi zingeleta tija kwa jamii, mfano kubuni mbinu mpya za kukabili Ugonjwa wa Malaria katika maeneo yenye Malaria kubwa kule Kanda ya Ziwa, Kigoma na Kusini mbinu ziwe tofauti, vile vile maeneo yenye maambukizi kidogo kama Dodoma, Kilimanjaro, Arusha na Manyara na kuelekea ukanda wa nyanda za juu kusini mwa Tanzania napo kukawa na mbinu tofauti," Amesema Ishengoma. 

Pia ameomba jamii kutumia vema vyandarua wanavyopewa ili kuzuia wasiumwe na mbu na kuachana na mila potofu zinazoweza kudhoofisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ikiwemo kusema kuwa vyandarua vinazalisha kunguni, vinapoteza hamu ya unyumba kwa wapenzi na wengine wanafugua kuku. 

Awali akifungua kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambapo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, Prof Andrew Barnabas Pembe amewaomba watafiti kujitokeza kwa wingi kufanya tafiti zitakazoleta matokeo Chanya katika jamii yetu. "Niwaombe watafiti wote kujitokeza kwa wingi kuungana na Chuo chetu Cha MUHAS ili tufanye tafiti zenye tija ili kuweza kutatua matatizo mbali mbali kwa jamii," amesema. 

Kongamano hilo la pili limehudhuriwa na watalaamu kutoka Wizara ya Afya, Shirika la Afya Duniani (WHO), SIDA Tanzania, Kituo cha Utafiti Ifakara, Mradi wa Taifa wa kuzuia Malaria pamoja na Vyuo mbali mbali na wadau wa Afya.

TAASISI YA WAHASIBU WANAWAKE (TAWCA) YAMWAGA VITABU VYA HESABU SHULE YA SEKONDARI TURIANI WILAYA YA KINONDONI

$
0
0
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na mwanachama wa Taasisi ya TAWCA Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant kushoto na Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWCA) wa pili kutoka kushoto na wenzao wakikabidhi vitabu mbalimbali vya mahesabu kwa Angalo Izungo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Triani wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni msaada walioutoa kwa shule hiyo kwa ajili ya watoto wanaosoma masomo ya hesabu.
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na mwanachama wa Taasisi ya TAWCA Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant kushoto na Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWCA) wa pili kutoka kushoto na wenzao wakikabidhi boksi la vitabu mbalimbali vya mahesabu kwa Angalo Izungo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Triani wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam na mmoja wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo ikiwa ni msaada walioutoa kwa shule hiyo kwa ajili ya watoto wanaosoma masomo ya hesabu.

Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na mwanachama wa Taasisi ya TAWCA Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant akikabidhi vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Turiani Wilayani Kinondoni kushoto ni Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWCA) na wanachama wenzao wakishuhudia tukio hilo.

Wanachama wa Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant (TAWCA)wakiwa katika picha na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa vitabu hivyo.

Wanachama wa Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant (TAWCA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo.

......................................................................................................

TAASISI ya Wanawake Wahasibu Tanzania(TAWCA)wametoa msaada wa vitabu mbalimbali vya hesabu na masomo ya biashara vyenye thamani ya Sh.milioni 8.5 kwa Shule ya Sekondari Turiani jijini Dar es Salaam.

Uamuzi wa TWCA kutoa msaada huo kwenye shule hiyo ni kuwahamasisha wanafunzi hasa wa kike kupenda masomo ya hesabu nchini ili baadae waje kuongeza idadi ya watalaamu wahasibu nchini.

Akizungumza leo shuleni hapo wakati wa tukio la kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania Tumaini Lawrence amesema wanawake wahasibu nchini wameona haja ya kushiriki kwa vitendo kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo yanayohosu hesabu na ndio maana wameamua kutoa msaada huo wenye lengo la kuwahamasisha wanafunzi wa kike nchini kupenda hesabu.

“Wanawake wahasibu nchini kwa umoja wetu tumeamua kuchangishana fedha ili kufanikisha msaada huu kwa ajili ya wanafunzi wa Sekondari ya Turiani.Tumekuja kuwahamasisha wasome kwa bidi masomo ya hesabu na biashara ili tuongeze idadi ya wahasibu na hawa wahasibu wa kike katika nchi yetu ambapo kwa sas idadi yao ni chini ya asilimia 25 ya wahasibu wote.

“Kuna dhana ambayo inajengeka kuwa masomo ya hesabu ni kwa ajili ya wanafunzi wa kiume tu lakini sisi wahasibu wanawake ambao ndio mama zenu tunawaambia wanafunzi kuwa somo la hesabu ni la wote.Hivyo wanafunzi wa kike jitahidi kusoma hesabu na masomo ya biashara,”amesema Lawrence.

Kuhusu mikakati ya taasisi ya wahasibu nchini, Lawrence amesema ni kuendelea kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya hesabu na huku akitoa ushauari kwa wazazi na walezi kuwajengea uwezo wa kujiamini watoto hao.

“Naomba nisieleweke vibaya ila wahasibu wanawake wakiwa kwenye maeneo yao ya kazi wanakuwa waaminifu sana.Kwa kutambua hilo ni jukumu letu kuwatia moyo wanafunzi wa kike nchini kupenda hesabu,” Lawrence. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo Neema Msusa amesema ni faraja kwao kufika shuleni hapo kuzungumza na wanafunzi hao.

“Tumefika shuleni hapa kwa lengo la kumsha ari kwa wanafunzi wetu wa kike kusoma masomo ya biashara.Tunawaambia hesabu haikimbiliki, hivyo wasome kwa bidi kwani tunaona faida ya kusoma hesabu maana wanawake wahasibu kila mmoja yupo kwenye taasisi anafanya kazi yake vizuri,”amesema

Ameongeza wao kuwa wahasibu kumetokana na msingi mzuri ambao uliwekwa na walimu wao kuanzia ngazi ya chini , hivyo wanaamini wanafunzi wa kike watasoma kwa bidi masomo ya hesabu.

Wakati huo huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Turiani jijini Dar es Salaam Angalo Izungo amesema anashukuru kupata msaada huo na kwamba wahasibu hao wanawake wameonesha upendo wa dhati kwa shule yao. Amefafanua changamoto kubwa iliyopo shuleni hapo ni vitabu vya masomo ya hesabu na biashara pamoja a uhaba wa walimu , hivyo baada ya kupata vitabu ombi lao ni Serikali kuwapatia walimu kwani waliopo ni wawili tu na wanafunzi walionao ni 506.

“Tunao walimu wawili tu wa masomo ya hesabu hapa shuleni kwetu, hivyo tunashukuru kwa msaada huu.Tunaomba Serikali yetu ituongezee walimu wa masomo ya hesabu shuleni kwetu, wanafunzi wetu wanapenda hesabu sana,”amesema Izungo.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARI 1,2019

BENKI YA NMB, WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ZAJA NA MIKAKATI ZAIDI YA UWEKEZAJI SEKTA YA MAZIWA NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Benki ya NMB na menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi 
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao na maafisa kutoka Benki ya NMB na menejimenti wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (hawapo pichani) kuhusu uwekezaji katika sekta ya maziwa 
Meneja Mwandamizi kutoka Benki ya NMB idara ya kilimo Bw. Carol Nyagaro akimuelezea Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anyeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) juu ya uwekezaji wa sekta ya maziwa na Benki ya NMB 

……………………… 

Na. Edward Kondela 

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel ameitaka Benki ya NMB kushirikiana na wizara hiyo katika kukuza sekta ya maziwa nchini kwa kuwa bado kuna mwitikio mdogo wa wananchi kunywa maziwa kutokana na taarifa iliyotolewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP) 

Prof. Gabriel amebainisha hayo leo (31.01.2019) Jijini Dodoma, akiwa kwenye kikao na maafisa kutoka idara ya kilimo ya Benki ya NMB, waliofika ofisini kwake kumwelezea mikakati ya Benki ya NMB ambayo imekuwa ikifanya tafiti na wadau wa sekta ya maziwa lengo likiwa ni kutaka kuwekeza katika sekta hiyo. 

“Kwa takwimu ambazo zimetolewa na Shirika la Chakula Duniani ni kwamba kwa wastani angalau mtu anatakiwa walau atumie lita mia mbili kwa mwaka za maziwa lakini kwa bahati mbaya kwa watanzania wastani ni lita arobaini na saba tu, bado tuna kazi kubwa sana.” Alisema Prof Gabriel 

Prof. Gabriel amesema Benki ya NMB inapaswa kuwa na ushirikiano na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Dawati la Sekta Binafsi ambalo limekuwa likiwaunganisha wadau wa sekta ya mifugo na uvuvi, ili kuhakikisha mazao yatokanayo na ng’ombe yakiwemo maziwa yanatumika ipasavyo. 

Katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa pia na watendaji wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu mkuu huyo pia amesema ni wakati muafaka kwa Benki ya NMB kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuhakikisha inawaletea maendeleo wafugaji, hususan wafugaji wadogo ambao wamefanikiwa pamoja na wafugaji ambao watakuwa tayari kubadilika na kuingia katika ufugaji wa kisasa na kuachana na ufugaji wa kuhamahama. 

Aidha Prof. Gabriel amesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa tafiti kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Benki ya NMB kupitia idara ya kilimo ili tafiti hizo ziweze kufanyiwa kazi na kuleta matokeo chanya kwa wafugaji. 

“Ningependa sekta hii ya mifugo, iwe pia na tafiti nyingi zinafanyika, sasa tukifanya hizo tafiti tutaweza kuleta mabadiliko chanya na yenye uhakika katika maendeleo ya wafugaji kwa sababu lengo siyo tu kufanya jambo, lakini liwe jambo ambalo linaweza kugusa maisha ya wafugaji.” Alisema Prof. Gabriel 

Katika kikao hicho pia Katibu Mkuu Prof. Gabriel ameshauri uwepo wa mahusiano ya karibu kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Benki ya NMB na taasisi za elimu ya juu, ili kuhakikisha tafiti ambazo zimekuwa zikifanywa na wanafunzi ziweze kutumika katika kuleta mabadiliko na kuleta manufaa kwa wafugaji, badala ya tafiti hizo kuwekwa katika maktaba za vyuo hivyo pekee. 

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB kutoka idara ya kilimo Bw. Carol Nyagaro amesema kutokana na kasi ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli pamoja na utendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewalazimu benki hiyo kubadili mtazamo wa namna ya kutafuta wateja wapya kupitia sekta mbalimbali. 

“Kutokana na kasi ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli na uongozi mzima wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwetu inajenga mazingira mazuri ya kufanya biashara, pia kuchangia maendeleo ya jamii na kuweza kutengeneza wateja wa siku zijazo.” Alisema Bw. Ngayaro 

Aidha Bw. Nyagaro amesema Benki ya NMB kupitia idara ya kilimo inafikiria pia kuwekeza katika sekta ya samaki ambayo imekuwa ikifanya vizuri kiuchumi katika siku za hivi karibuni. 

Bw. Nyagaro amemueleza pia Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel, kuwa Muunganiko wa Vyama vya Ushirika Vikuu vya Maziwa Duniani unatarajia kufanya mkutano wake hapa nchini Tarehe 25 na 26 Mwezi Februari mwaka 2019 kwa kushirikiana na Benki ya NMB lengo kuu likiwa ni kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika sekta ya maziwa hapa nchini. 

Amefafanua kuwa muunganiko huo wenye nchi wanachama 95 ambao unafanya biashara ya takriban Dola za Marekani Bilioni 200 kwa mwaka, umeichagua Tanzania kwa ajili ya kufanya majadiliano kwa kuhusisha wadau wa sekta ya mifugo ili kuwekeza katika sekta ya maziwa. 

Amesema mkutano huo pia utaainisha mambo ambayo tayari yalishafanyiwa tafiti kwa ajili ya utekelezaji wa mipango hiyo.

TBA KAMILISHENI MIRADI KWA WAKATI-RC MWANGELA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (rtd) Nicodemus Elias Mwangela amewataka Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) kukamilisha miradi ya ujenzi wanayo pewa ndani ya muda wa makubaliano ya mikataba.

Brig. Jen. (rtd) Mwangela ameyasema hayo jana wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa na ya Katibu ya Katibu Tawala Mkoa kati ya TBA na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.

“TBA mna sifa nzuri ya kujenga majengo ya serikali kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na kwa gharama nafuu lakini kuna wakati kunakuwa na kusita katika kuwapa kazi kutokana na historia yenu ya kuchelewesha kukamilisha miradi mnayopewa ya ujenzi”, ameeleza Brig. Jen. (rtd) Mwangela.

Ameongeza kuwa TBA wamechelewesha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ujenzi wa Hospitali ya Mji wa Tunduma hivyo ucheleweshaji huo usirudie katika mikataba hiyo miwili waliyopewa kwani hatasita kuvunja mikataba hiyo endapo wataonyesha ucheleweshaji.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila ameishukuru serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuupatia Mkoa wa Songwe kiasi cha shilingi bilioni 26.8 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali mkoani hapa.

Kafulila amesema serikali imekuwa ikitoa fedha za miradi mbalimbali lakini kasi ya utoaji wa fedha na matumizi ya fedha hizo kwenye miradi husika imekuwa haiendani na hivyo kusababisha kuchelewa kukamilika kwa miradi hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwa amini na kuwapa miradi hiyo miwili yenye thamani ya shilingi bilioni moja na kuahidi kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Mhandisi Cosmas amesema hapo awali walikuwa na changamoto kama vile ukosefu wa maji, umeme na baadhi ya vifaa lakini wamesha zifanyia kazi changamoto hizo hivyo watamaliza miradi hiyo Juni 30, 2019 kama walivyokubaliana katika Mikataba.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila akisaini mikataba ya Ujenzi wa nyumba za Mkuu wa Mkoa na ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, ambapo Wakala wa Majengo (TBA) wamekubali kukamilisha ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano na kwa gharama ya shilingi bilioni moja.

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila na Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas wakisaini mkataba wa ujenzi wa nyumba za Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa, wa Kwanza Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Rtd) Nicodemus Mwangela.

TAASISI YA WANAWAKE WAHASIBU TANZANIA (TAWCA) YAMWAGA VITABU VYA HESABU SHULE YA SEKONDARI TURIANI WILAYA YA KINONDONI

$
0
0
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na Mwanyekiti wa bodi ya Tanzania Association of Women Certified Accountants (TWCA) wanawake wahasibu kushoto na Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TWCA) wa pili kutoka kushoto na wenzao wakikabidhi vitabu mbalimbali vya mahesabu kwa Angalo Izungo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni msaada walioutoa kwa shule hiyo kwa ajili ya watoto wanaosoma masomo ya hesabu.
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na Mwanyekiti wa bodi ya Taasisi ya Tanzania Association of Women Certified Accountants (TWCA) wanawake wahasibu kushoto na Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TWCA) wa pili kutoka kushoto na wenzao wakikabidhi boksi la vitabu mbalimbali vya mahesabu kwa Angalo Izungo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam na mmoja wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo ikiwa ni msaada walioutoa kwa shule hiyo kwa ajili ya watoto wanaosoma masomo ya hesabu.
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na Mwanyekiti wa bodi ya Taasisi ya wanawake wahasibu Tanzania Association of Women Certified Accountants(TWCA) akikabidhi vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Turiani Wilayani Kinondoni kushoto ni Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWCA) na wanachama wenzao wakishuhudia tukio hilo.
Wanawake wahasibu kutoka taasisi ya Tanzania Association of Women Certified Accountants (TAWCA)wakiwa katika picha na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa vitabu hivyo.

Wanawake wahasibu kutoka taasisi ya Tanzania Association of Women Certified Accountants (TAWCA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo.

......................................................................................................

TAASISI ya wanawake wahasibu Tanzania Association of Women Certified Accountants (TAWCA) wametoa msaada wa vitabu mbalimbali vya hesabu na masomo ya biashara vyenye thamani ya Sh.milioni 8.5 kwa Shule ya Sekondari Turiani jijini Dar es Salaam.

Uamuzi wa (TAWCA) kutoa msaada huo kwenye shule hiyo ni kuwahamasisha wanafunzi hasa wa kike kupenda masomo ya hesabu nchini ili baadae waje kuongeza idadi ya watalaamu wahasibu nchini.

Akizungumza leo shuleni hapo wakati wa tukio la kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania Tumaini Lawrence amesema wanawake wahasibu nchini wameona haja ya kushiriki kwa vitendo kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo yanayohosu hesabu na ndio maana wameamua kutoa msaada huo wenye lengo la kuwahamasisha wanafunzi wa kike nchini kupenda hesabu.

“Wanawake wahasibu nchini kwa umoja wetu tumeamua kuchangishana fedha ili kufanikisha msaada huu kwa ajili ya wanafunzi wa Sekondari ya Turiani.Tumekuja kuwahamasisha wasome kwa bidi masomo ya hesabu na biashara ili tuongeze idadi ya wahasibu na hawa wahasibu wa kike katika nchi yetu ambapo kwa sas idadi yao ni chini ya asilimia 25 ya wahasibu wote.

“Kuna dhana ambayo inajengeka kuwa masomo ya hesabu ni kwa ajili ya wanafunzi wa kiume tu lakini sisi wahasibu wanawake ambao ndio mama zenu tunawaambia wanafunzi kuwa somo la hesabu ni la wote.Hivyo wanafunzi wa kike jitahidi kusoma hesabu na masomo ya biashara,”amesema Lawrence.

Kuhusu mikakati ya taasisi ya wahasibu nchini, Lawrence amesema ni kuendelea kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya hesabu na huku akitoa ushauari kwa wazazi na walezi kuwajengea uwezo wa kujiamini watoto hao.

“Naomba nisieleweke vibaya ila wahasibu wanawake wakiwa kwenye maeneo yao ya kazi wanakuwa waaminifu sana.Kwa kutambua hilo ni jukumu letu kuwatia moyo wanafunzi wa kike nchini kupenda hesabu,” Lawrence. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo Neema Kiure Mssusa amesema ni faraja kwao kufika shuleni hapo kuzungumza na wanafunzi hao.

“Tumefika shuleni hapa kwa lengo la kumsha ari kwa wanafunzi wetu wa kike kusoma masomo ya biashara.Tunawaambia hesabu haikimbiliki, hivyo wasome kwa bidi kwani tunaona faida ya kusoma hesabu maana wanawake wahasibu kila mmoja yupo kwenye taasisi anafanya kazi yake vizuri,”amesema

Ameongeza wao kuwa wahasibu kumetokana na msingi mzuri ambao uliwekwa na walimu wao kuanzia ngazi ya chini , hivyo wanaamini wanafunzi wa kike watasoma kwa bidi masomo ya hesabu.

Wakati huo huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Turiani jijini Dar es Salaam Angalo Izungo amesema anashukuru kupata msaada huo na kwamba wahasibu hao wanawake wameonesha upendo wa dhati kwa shule yao. Amefafanua changamoto kubwa iliyopo shuleni hapo ni vitabu vya masomo ya hesabu na biashara pamoja a uhaba wa walimu , hivyo baada ya kupata vitabu ombi lao ni Serikali kuwapatia walimu kwani waliopo ni wawili tu na wanafunzi walionao ni 506.

“Tunao walimu wawili tu wa masomo ya hesabu hapa shuleni kwetu, hivyo tunashukuru kwa msaada huu.Tunaomba Serikali yetu ituongezee walimu wa masomo ya hesabu shuleni kwetu, wanafunzi wetu wanapenda hesabu sana,”amesema Izungo.

MTENDAJI MKUU TEMESA AKAGUA MASHINE YA KISASA YA KUKAGUA MAGARI KARAKANA YA MT. DEPOT

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe (wa pili kushoto) akimpa maelezo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe (wa pili kushoto) wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo ili kurahisisha utendaji kazi. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.

Pichani, gari linaonekana likiwa limenyanyuliwa juu na mashine ya kisasa (3D Wheel Allignment) tayari kwa kuanza kukaguliwa, mashine hiyo ya kisasa imefungwa katika karakana ya TEMESA Mt. Depot Keko Jijini Dar es Salaam. Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA una mpango wa kufunga mashine nyingine kama hizo katika karakana za mkoa wa Mwanza na Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akikagua maboksi maalumu ya kuhifadhia mtambo wa kuongozea taa za magari (traffic light controller) katika karakana ya Mt. Depot kikosi cha Umeme. Kushoto ni Kaimu meneja wa kikosi hicho Mhandisi Pongeza Semakuwa na wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe. PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO – (TEMESA)

WAFANYABIASHARA WANAOINGIZA BIDHAA KUPITIA NJIA ZA PANYA ILI KUKWEPA USHURU KUKIONA-RPC WANKYO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI .

JESHI la polisi mkoani Pwani, limeweka bayana kuendelea kukaza uzi, katika kupambana na wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kwa njia za magendo kwa lengo la kukwepa ushuru na kuisababishia serikali kukosa mapato. 

Kutokana na kuchukua hatua hiyo jeshi hilo, limefanikiwa kukamata madumu 86 ya mafuta ya kula ambayo hayajalipiwa ushuru yakiwa yamehifadhiwa ndani ya stoo ya mfanyabiashara Mmas Athumani (35) mkazi wa Kongowe Kibaha mkoani hapo. 

Akieleza juu ya suala hilo, kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP) Wankyo Nyigesa alisema, madumu hayo yamefikia jumla ya madumu 107 ya mafuta ya kula yaliyokamatwa katika kipindi cha wiki moja. 

“Taarifa tumezipata kutoka kwa raia wema, ambapo walieleza mafuta hayo yameingizwa nchini kupitia Bagamoyo na kukwepa ushuru wa serikali kisha kusafirishwa kwa njia za panya hadi kwenye stoo hiyo eneo la Kongowe “alifafanua Wankyo. 

Alitaja mafuta ni dumu moja lita 20 aina ya jenau, madumu 26 ya lita 20 aina ya MTRA pamoja na madumu 59 ya lita 20 aina ya oki. Aidha Wankyo alisema, pia limekamata mifuko 18 ya sukari ambayo imeingizwa nchini kutoka nchi jirani kwa kukwepa ushuru. 

Wakati huo huo, wanamsaka mfanyabiashara mmoja ambae kwa sasa jina linahifadhiwa aliyetoroka baada ya kuona maafisa wa polisi wakimfatilia na kutelekeza madumu 21 ya mafuta ya kupikia aina ya Micogold yenye ujazo wa lita 20 kila moja ambayo hayajalipiwa ushuru eneo la Magomeni Bagamoyo. 

Kamanda huyo alitoa wito kwa wafanyabiashara, kuacha kujihusisha na biashara za magendo na ukwepaji wa ushuru katika biashara wanazofanya .
Wankyo aliwapa salamu kwamba, watambue hawapo salama kwani jeshi hilo limejipanga vilivyo kwenye KUTINDUA mitandao yote ya wafanyabiashara wanaoingiza mali za magendo na ukwepaji ushuru kupitia bandari bubu.

CGP – PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA ENEO LA UJENZI OFISI ZA WIZARA MAMBO YA NDANI, WIZARA YA ELIMU NA OFISI YA WAZIRI MKUU AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU, JIJINI DODOMA

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akitembelea maeneo ya mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma yanapojengwa majengo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Walemavu, leo januari 31, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akimsikiliza Msimamizi Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi cha Magereza katika mradi huo, ACP. Aron Lunyungu alipotembelea katika eneo la ujenzi wa Ofisi Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Walemavu, leo januari 31, 2019.
Ujenzi wa majengo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Walemavu, leo januari 31, 2019 ukiendelea katika hatua mbalimbali kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akisaini kitabu cha ukaguzi katika ujenzi wa Ofisi Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Walemavu, leo januari 31, 2019(Picha na Jeshi la Magereza).



……………………..

Na ASP. Lucas Mboje, Dodoma

KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike leo januari 31, 2019 ametembelea maeneo ya mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma yanapojengwa majengo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana na Walemavu ambapo amekiagiza Kikosi cha ujenzi cha Jeshi la Magereza kinachoshiriki katika ujenzi wa ofisi hizo kuzingatia ubora katika ujenzi wa majengo hayo.

Kamishna Jenerali Kasike amewataka pia Maafisa na askari wanaoshiriki katika ujenzi wa ofisi hizo kuongeza kasi ya ujenzi kama ambavyo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alivyoagiza lakini wazingatie viwango vya ubora katika ujenzi huo.

“Hakikisheni ujenzi unafanyika usiku na mchana kama tulivyokwishajipanga lakini zingatieni viwango vya ubora katika ujenzi”. Amesisitiza Jenerali Kasike.

Aidha, Kamishna Jenerali Kasike amemtaka Msimamizi Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi cha Magereza katika mradi huo, ACP. Aron Lunyungu pamoja na Mhandisi Mradi, SSP. Alfred Bundala kuhakikisha kuwa wanakusanya mahitaji yote muhimu katika eneo la ujenzi ili kufanikisha kasi ya ujenzi huo.

Ujenzi wa majengo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi ulitarajiwa kukamilika mapema ifikapo tarehe 31 Januari 2019 lakini kutokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa nje ya uwezo wa Kikosi cha ujenzi cha Jeshi la Magereza, ujenzi huo umechelewa kukamilika kwa wakati na hatua za ukamilishaji zinaendelea kwa kasi ya kuridhisha.

RC MAKONDA AWATAFUTIA WASANII MKOPO WA BILIONI 2 BILA RIBA.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda katika kujali na kunusuru kazi za Wasanii amewatafutia mkopo wa Shilingi Bilioni 2 bila riba zitakazotolewa kwenye Halmashauri za Mkoa huo kupitia fungu la mkopo wa 10% zinazotolewa kwa Vijana, Walemavu na kinamama  kwa lengo la kuwawezesha wasanii kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuziingiza sokoni.

RC Makonda amesema wasanii wengi wamejikuta wakizalisha kazi nzuri lakini wanakosa mitaji ya kuingiza kazi zao sokoni kutokana na kukosa mitaji jambo linalowapelekea wenye pesa kutumia fursa hiyo kunyonya kazi za wasanii na mwisho wa siku wanazidi kudidimia.

Aidha RC Makonda amesema hadi kufikia mwezi March 01 mkopo huo utakuwa tayari na ameshazielekeza halmashauri kutoa fedha hizo huku akiwasihi wasanii kuchangamkia fursa hiyo.

Hayo yote yamejiri wakati wa kikao baina ya RC Makonda na Wasanii kilicholenga kutatua kero za wasanii wa tasnia mbalombali.












RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA MKUTANO WA KAWAIDA WA 20 WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Liberat  Mfumukeko na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Ijumaa Februari 1, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Mhe. Gaston Sindimo alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Ijumaa Februari 1, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudani ya Kusini Mhe. Barnaba Marial Benjamin akiwa na Balozi wa Nchi hiyo nchini Mhe. Mariano Deng Ngor wakati alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Ijumaa Februari 1, 2019.
 Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akilakiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Liberat Mfumukeko na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Ijumaa Februari 1, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) muda mfupi kabla ya kuanza kwa  Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Ijumaa Februari 1, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kabla ya kuanza kwa  Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Ijumaa Februari 1, 2019.
 Rais wa Uganda Mhe. Yowweri Kaguta Museveni akilakiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Liberat Mfumukeko na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Ijumaa Februari 1, 2019.
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) wakihudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Ijumaa Februari 1, 2019. Picha na IKULU

WAZIRI MKUU AREJEA DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amerejea jijini Dodoma leo Februari 1, 2019 baada ya kumuwakilisha Rais, Dkt. John Magufuli katika mazishi ya mke wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary bin Zubeir yaliyofanyika katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Tanga, Januari 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi  (watatu kulia) na  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge (kulia) kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma wakati aliporejea jijini Dodoma baada ya kumuwakilisha Rais, Dkt. John Magufuli katika mazishi ya mke wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary bin Zubeir yaliyofanyika katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Tanga, Januari 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAASISI YA OCEAN ROAD YAWAFUNDA WAANDISHI KUHUSU SARATANI

$
0
0
 Mkurungenzi wa Huduma za kinga Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Crispin Kahesa akizungumza katika semina ya kuwjengea uwezo waandisi wa habari iliyofanjika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road leo jijini Dar es Salaam.
 Daktari Bingwa wa Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Nanzake Mvungi akitoa elimu kuhusu  kinga dhidi ya saratani pamoja na huduma zitolewazo na kitengo cha kinga ya Saratani katika Hospitali hiyo.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Meneja  Elimu na Huduma za Uchunguzi Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Maguhwa Stephano akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tiba ya mionzi pamoja na kuwaomba  wananchi waache dhana potofu juu ya tiba hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam.

TANZANIA HIGH COMMISSIONER HONOURED IN LONDON

$
0
0
 By Ayoub Mzee.

The Tanzania High Commissioner in UK  Dr Rose  Asha Migiro was the guest of Honour  at a  fundraising  event  to  purchase  a building that  will  be used  as a community centre for the Diaspora community  .This  event was  organised by a Tanzania Diaspora  group called East Africa Education Foundation-a Registered charity number: 1096912;  headed  by  Dr Mohammed Salim.

The High Commissioner was  given an award  by  the  Foundation for  the  good  work shes  been doing  in  terms  of  bringing  the Diaspora Community together.
What services East African Education Foundation provides:

Amateur sport
Other charitable purposes
Education/training
Arts/culture/heritage/science
Economic/community development/employment
General charitable purposes
The prevention or relief of poverty
The advancement of health or saving of lives
Recreation.
Where East African Education Foundation operates:
Redbridge
Barking and dagenham
Waltham forest
Newham
Tower hamlets




TPDC YAIMARISHA SEKTA YA ELIMU MKOANI MTWARA

$
0
0
Bi. Marie Msellemu, Meneja Mawasiliano wa TPDC akimkabidhi hundi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Bw. Gelasius Byakanwa kiasi cha Tsh,. 13, 258,042 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa Mkoani Mtwara.
Katika jitihada za kutekeleza dhana ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kutekeleza kwa vitendo dhana hii kwa kushiriki katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo Mkoani Mtwara. 

Katika tukio la hivi karibuni, TPDC imeweza kumkabidhi Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Mh. Bw. Gelasius Byakanwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni kumi na tatu laki mbili hamsini elfu na arobaini na mbili ili kusaidia ujenzi wa darasa moja katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara. 
Akiongea katika tukio hilo, Mh. Byakanwa alisema TPDC imefanya jambo kubwa na kuonyesha uzalendo kwa kurudisha kwa jamii, na aliishukuru TPDC kwa kuendelea kushiriki katika kutatua changamoto mbalimbali mkoani Mtwara, husani zile zinazoikumba sekta ya huduma za jamii ikiwemo elimu. Vile vile mkuu wa mkoa alitoa rai kwa wadau na wawekezaji waliopo mkoani Mtwara kuiga mfano wa TPDC katika kuwajali wananchi kwa kuchangia katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Ndg.Omari Kipanga akitoa ufafanuzi wa mahitaji ya elimu mkoani Mtwara.

Akimkabidhi mfano wa hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Bi. Marie Msellemu ambaye ni Meneja Mawasiliano wa Shirika alisema “TPDC ni mdau mkubwa wa Mkoa wa Mtwara, na kwa kupitia mfuko wa uwajibikaji kwa jamii (CSR), TPDC imekuwa ikiwashika mkono wananchi wa Mkoa wa Mtwara na mikoa ya jirani katika kuboresha huduma za jamii kama vile elimu, afya, maji na hivyo kiasi hiki cha fedha kitauwezesha mkoa kuendelea kufikia lengo la kuweka mazingira mazuri ya kusomea kwa watoto wetu”. 
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Ndg. Omari Kipanga alieleza kuwa “Sisi kama halmashauri tumefarijika sana kwa msaada huu uliotolewa na TPDC, kwani fedha hizi zitaelekezwa moja kwa moja katika ujenzi wa madarasa katika halmashauri ya Wilaya yetu kama ilivyokusudiwa. Mchango huu uliotolewa na TPDC unakwenda kukamilisha kazi ya kuezeka madarasa manne katika shule ya msingi Mitambo pamoja na madarasa mawili katika shule ya sekondari ya Madimba’’.
Mkurugenzi Kipanga aliendelea kusisitiza kwamba uhitaji bado ni mkubwa kuweza kukamilisha uhitaji wa madarasa kwa Mkoa wa Mtwara na kuwataka wadau wa elimu na wawekezaji mbalimbali waliopo mkoani Mtwara kuiga mfano wa TPDC katika kurudisha kwa jamii na kuimarisha elimu mkoani hapo.
Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu akikabidhi hundi kwa mratibu wa taasis ya TAKUWA Bi. Hadija Malibecha
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Ndg. Evod Mmanda naye aliungana na viongozi waliotangulia kwa kuishukuru na kuipongeza TPDC kwa kusaidia kuboresha huduma mbali mbali za kijamii mkoani Mtwara. Alieleza kuwa “Si mara ya kwanza kwa TPDC kuchangia kwani mwaka jana tumepokea kiasi cha 21,151,500 za kumalizia ujenzi wa zahanati ya kijjiji cha Mngoji pamoja na kiasi cha 12,000,000 za ujenzi wa choo cha wanafunzi wenye uhitaji maalumu katika shule ya msingi Shangani”.
Katika hatua nyingine TPDC ilikabidhi Taasisi ya Kusaidia Wanawake Mkoani Mtwara (TAKUWA) kiasi cha milioni tatu laki tisa na elfu sabini kwa ajili ya unununuzi wa vitendea kazi vya ofisi ili kurahisisha shuguli za kila siku za taasisi hiyo.
Mratibu wa taasiis hiyo Bi. Hadija Malibecha alishukuru TPDC kwa msaada huo na alieleza kuwa “kabla ya upatikanaji wa vifaa hivyo tulikua tunafanya kazi katika mazingira magumu lakini sasa TPDC imetuboreshea mazingira ya kazi na kazi zinaenda vizuri”.

TAKUWA inasaidia vikundi vya wanawake kwa ajili ya kuinua shughuli mbalimbali za kiuchumi na elimu. Jumla ya vikundi 12 vya wakinamama mkoani mtwara vinasimamiwa na taasisi hii katika kupewa mafunzo ya ujasiriamali kama kutengeneza sabuni, ufugaji wa nyuki na ufugaji wa wa mbuzi lengo ikiwa ni kuboresha maisha ya wanawake. 

MAHAKAMA INAYOTEMBEA MWAROBAINI WA HUDUMA ZA UTOAJI HAKI NCHINI

$
0
0

Na. Mwandishi Wetu- MAELEZO

Mahakama ya Tanzania katika kusogeza huduma zake za utoaji haki kwa urahisi kwa wananchi, imelivalia njuga suala la uanzishwaji wa mahakama inayotembea yaani mobile court ili kusogeza huduma karibu zaidi na watanzania.

Akizungumza na mwandishi wa Idara ya Habari MAELEZO, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri katika Mahakama ya Tanzania Bi.Eva Kiaki Nkya amesema kuwa Serikali imeamua kuja na Mahakama zinazotembea ili kuwafikia wananchi kwa wepesi na kupunguza changamoto ya mlundikano wa mashauri katika Mahakama.

Alisema dhana ya Mahakama kuwafata wananchi siyo mpya kwani hapo awali kulikuwa na utaratibu huo ila kilichobadilika ni utaratibu wa kununua magari mawili ya awali ambayo ndani yatakuwa na mgawanyo wa chumba cha Hakimu pamoja na maafisa wa Mahakama.

Utaratibu huo mpya unatazamiwa kuanza katika Mikoa miwili ambayo ni Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Mkoa wa Mwanza kutokana na wingi wa mashauri , uchache wa Mahakama , pamoja na idadi kubwa ya wananchi.

“Serikali imeamua kuja na Mahakama zinazotembea ikiwa na lengo la kuwasogelea watu katika maeneo yao ili kuwapunguzia muda, kuwapunguzia gharama za wao kuifuata Mahakama badala ya wao kuifata Mahakama , Mahakama inawafuata wao”alisema.

Zamani tulikuwa tunatumia majengo ya Mahakama lakini sasahivi tumenunua magari maalum ambayo yataenda kusikiliza mashauri mtaani ili kurahisha huduma zetu.

Mahakama hizi zitakuwa na kazi ya kusikiliza mashauri ,kutoa elimu kwa umma na kufanya usuluhishi wa malalamiko ya wananchi, pia kutakuwa na utaratibu maalumu wa namna ya kusikiliza kesi na mpangilio wa kesi utategemea na tarehe tajwa. 
 

Wajasiliamali wasiotambulika wapewa wiki tatu kujisalimisha

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo 

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa wiki tatu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo waliopo ndani ya manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho vitakavyowafanya kutambuliwa rasmi na serikali na hivyo kujulikana shughuli zao wanazozifanya katika maeneo mbalimbali ndani ya Manispaa hiyo.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuyatambua makundi yote ya wafanyabiashara nchini na katika kufikia lengo hilo imeweka utaratibu maalum wa kuwapatia vitambulisho wajasiliamali ili wasibughudhiwe, na kuongeza kuwa ili waweze kutafutiwa maeneo yao maalum ya kufanyia kazi ni lazima watambuliwe.

“Kama hana kitambulisho hiki ambacho amekitoa Mh. Rais na wakati huo huo hana TIN ya biashara ya TRA sasa yeye ni nani? Narudia kusema kwamba yeyote baada ya wiki tatu ambaye hana kitambulisho, hatauza hata nyanya nje ya mlango wake, kwasababu ni mfanyabiashara mdogo, na kama haupo kwenye ufanyaji biashara mkubwa wa kuwa na TIN na hauna kitambulisho cha ujasiliamali inamaana haufanyi shughuli za biashara,” Alisisita.

Aidha alibainisha makundi ambayo ni walengwa wa vitambulisho hivyo wakiwemo, mafundi baiskeli, wauza mkaa, wauza nyanya, wauza “viosk” mitaani, mafundi seremala wa mitaani, mama ntilie, wauza matunda wa mitaani, waendesha bodaboda, pamoja na wale wote wanaojishughulisha na biashara ambao hawajafikia vigezo vya kusajiliwa na TRA.

Ameyasema hayo katika kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa kata na mitaa wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ili kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano katika manispaa hiyo.

Halikadhalika aliwaonya wale wote wanaosita kuchukua vitambulisho hivyo wakidhani kuwa havina umuhimu na kwamba hakuna tofauti ya kuwa nacho na kutokuwa nacho wasubiri baada ya wiki hizo tatu kupita ndipo itajulikana umuhimu wa kitambulisho hicho.

UVCCM WAISHAURI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUKUZA VIPAJI VYA WATOTO WANAOTAMANI KUWA MADAKTARI WA MOYO

$
0
0
Daktari bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Vivian Mlawi akielezea namna chumba cha ICU kinavyowahudumia wagonjwa waliotoka katika chumba cha upasuaji kwa viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni walioongozana na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 Maria Manyama walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiongea jambo na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 Maria Manyama mwenye ndoto ya kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alipotembelea taasisi hiyo pamoja na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi Robert Mallya wakizungumza na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni walioongozana na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 Maria Manyama walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wa taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo ziara.
Picha na JKCI .

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wameishauri Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kufuatilia na kulea vipaji vya watoto wenye ndoto ya kuwa madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa siku zijazo.

Rai hiyo imetolewa hospitalini hapo leo na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni, Rashid Semindu, wakati walipofanya ziara wakiwa wameambatana na Maria Manyama ambaye ni msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 yaliyotangazwa hivi karibuni na Baraza la Mitihani la Taifa.

“Tunaipongeza serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika taasisi hii”.

“Tunawapongeza nanyi wafanyakazi wa Taasisi hii kwa kuendelea kufanya kazi kwa moyo mkubwa kusaidia watanzania na wagonjwa wengine ambao mmetueleza huwa wagonjwa wengine mnawapokea kutoka nje ya nchi, kwa kweli mnafanya kazi kubwa na nzuri,” alisema.

Ameongeza, “Tunao vijana wengi ambao wana ndoto ya kuwa madaktari bingwa kama ambavyo Maria ametueleza ndoto yake, vijana wa chipukizi, tunaomba JKCI muwalee ili waweze kufikia ndoto zao hizo, kwani hii ni hazina ya Taifa letu.

Akizungumza, Maria amesema alidhamiria kusoma udaktari na kubobea katika masuala ya moyo tangu alipokuwa akisoma mkoani Mbeya.

“Tulipofanya ziara za kimasomo katika hospitali mbalimbali, nilikuwa nashuhudia jinsi ambavyo watanzania wenzangu wakubwa kwa wadogo wanavyoteseka kwa kuugua magonjwa haya.

“Nikaweka bidii katika masomo yangu, namshukuru Mwenyezi Mungu amenisaidia nimefanya vizuri, nawashukuru wazazi wangu kwa kuniwezesha kila hatua, walimu wangu kwa kunifundisha kwa moyo na wanafunzi wenzangu kwa ushirikiano wao,” amesema.

Baba mlezi wa Maria, Leonard Manyama amesema matokeo ya binti huyo yaliwashangaza. “Alianza kutueleza juu ya ndoto yake ya kuwa daktari kabla hata hajafanya mtihani, alianza kutafuta shule ya kwenda kusoma kwenye mtandao, akasema Feza Sekondari itamfaa, tukaendelea kumfuatilia kwa ukaribu, matokeo yake yalipotoka tulistaajabu, amefaulu kwa kiwango cha juu na Feza wamekubali kumsomesha bure,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI, Delila Kimambo amempongeza msichana huyo kwa kuamua kutembelea taasisi hiyo kujifunza.

“Nimekubali kuwa mlezi wake, nitamsaidia popote pale atakapokuwa akihitaji msaada ili aweze kufikia ndoto yake,” alisema Dk. Kimambo.

HAKUNA ATAKAYESALIMIKA MAUJI YA WAZEE NCHINI-KANGI LUGOLA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola akibadilishana mawazo na baadhi ya Wawakilishi wa Wazee nchini wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kujadili mbinu mpya za kutokomeza mauaji ya wazee kilichofanyika leo mjini Dodoma.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Naftali Ngodi akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kujadili mbinu mpya za kutokomeza mauaji ya wazee wa Nchini kwa kutumia Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee na Vikongwe nchini uliozinduliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa hivi karibuni mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kujadili mbinu mpya za kutokomeza mauaji ya wazee na vikongwe Nchini kwa kutumia Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee na Vikongwe Nchini uliozinduliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa hivi karibuni mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kujadili mbinu mpya za kutokomeza mauaji ya wazee wa Nchini kwa kutumia Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee na Vikongwe Nchini uliozinduliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa hivi karibuni mjini Dodoma.
Baadhi ya wawakilishi wa wazee wakifuatilia jambo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kujadili mbinu mpya za kutokomeza mauaji ya wazee wa Nchini kwa kutumia Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee na Vikongwe Nchini uliozinduliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa hivi karibuni mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW



Na Mwandishi wetu Dodoma

Waziri Mambo ya Ndani Kangi Lugola ametoa wito kwa vijana wote nchini kuachana na tabia ya mauaji ya vikongwe na Wazee Nchini na kutoa onyo kwamba hakuna muuaji hata mmoja atakaye salimika na kukwepa mkono wa sheria.

Amesema hayo leo jijini Dodoma katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao kazi kilichowakutanisha wazee makamanda wa jeshi la polisi na maofisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa kujadiliana kwa pamoja kuhusu mbinu mpya za kutokomeza mauaji hayo kwa kutumia Mkakati mpya wa miaka 5 wa Kutokomeza Mauji ya Wazee na Vikongwe Nchini.

Mkakati huo uliozinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Tanzania tarehe 29, January 2019 wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Nchini uliofanyika Jijini Dodoma. Aidha Waziri Lugola amewataka vijana kutambua kuwa kijana wa leo ni Mzee wa Kesho hivyo atambue kuwa machungu ya mauaji ya wazee wanayoyapata leo naye ayatarajie baadae kwa kuwa kila mtu atazeeka.

Kufuatia hali hiyo Waziri Lugola aliwataka Vijana kutunza wazee wao kwasasababu machozi ya wazee wanayolia kila siku kwa kwa kukosa matunzo ya watoto wao yanapelekea wazee wengi kuwa na macho mekundu yanayoplekea watu wenye imani potofu kuwapoteza maisha yao kwa imani za kishirikina.

Aliongea kuhusu Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee Waziri Nchini Lugola alisema lengo la mkakati huu ni kuhakikisha tunashirikiana ili ifikapo mwaka 2023 mauaji ya wazee yawe yamekomeshwa kabisa. ”Hatutakua na sababu yoyote ya kueleza tukishindwa kutekeleza wajibu huu muhimu wa kulinda uhai wa kundi hili tete. Naomba muongeze kasi ili tufikie lengo hili, tena ikiwezekana mapema zaidi kwani tutapimwa kwalo 2023’’. Aliongeza Mhe. Lugola.

Alitoa wito kwa vyombo vya dola hasa Jeshi la polisi kuendelea kufuatilia kwa ukaribu sababu na vichocheo vya mauaji haya ikiwa ni pamoja na kuwabaini wahusika wanaopanga na kutekeleza mauaji haya ili wafikishwe kwenye vyombo vya Sheria, na pale inapothibika wahusika wachukuliwe hatua kali ili tukomesha kabisa vitendo hivi vya kikatili.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu aliwaambia wajumbe wa Mkutano kuwa mahuaji ya vikongwe yalianza tangu miaka ya 1960 na serikali imekuwa ikipambana nayo lakini yamekuwa yakiendelea. Dkt. Jingu aliongeza kuwa jughudi za serikali kupitia Jeshi la Polisi zimefanikiwa kupunguza mauaji haya lakini hayajakwisha kwasababu bado kuna watu wengi wenye Imani potofu katika Jamii hivyo ni lazima mapambano dhidi yao yaendelee.

Alisema kuwa Mkakati wa Kutokomeza Mauaji dhidi ya Wazee unalenga kuwa na Taifa linaloazingatia haki na ustawi wa wazee kwa kupiga vita imani za kushirikina, ubaguzi, ukatili na mauaji.

Aidha Dkt. Jingu aliongeza kuwa tafiti zilizopo zinaonesha mauaji na ukatili dhidi ya Wazee yanachochewa na Imani za kishirikina pamoja na migogoro ya ardhi hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau imeandaa Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee Nchini kwa lengo la kutokomeza kabisa mauaji haya.

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO

$
0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifungua rasmi kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichowajumuisha Watendaji Wakuu Serikalini katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge akiwakaribisha katika mkoa wake wajumbe wa kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kabla ya kuanza kwa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akimkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichowajumuisha Watendaji Wakuu Serikalini katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge wakati wa kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.


Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao, Dkt. Jabiri Bakari akizungumza kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.


Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Taasisi serikalini wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.


………………………..


Taasisi za Umma nchini zimetakiwa kuzingatia viwango vya usalama wakati wa uundaji wa mifumo ya TEHAMA ya utoaji huduma kwa umma ili kukabiliana na changamoto ya usalama wa taarifa za serikali mitandaoni.

Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akifungua kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichowajumuisha Watendaji Wakuu Serikalini chenye lengo la kubadilishana uzoefu, kujenga uelewa wa pamoja na kuendeleza uhusiano katika utendaji kazi na wadau mbalimbali wa Serikali Mtandao.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, suala la usalama mitandaoni lisipokabiliwa kikamilifu, linaathiri kwa kiasi kikubwa jitihada za serikali zilizofanyika katika eneo la Serikali Mtandao na kuongeza kuwa tatizo la usalama mitandaoni linazidi kukua kadri maendeleo ya teknolojia yanavyozidi kukua.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, usalama wa taarifa za serikali liwe jambo la kwanza na la lazima wakati wa kubuni, kusanifu, kujenga, kusimika na kuendesha mifumo ya TEHAMA badala ya kujenga mifumo hiyo kwanza na ndio suala la usalama lifuate.

“Njia mojawapo ya kuhakikisha usalama, ni kuhakikisha utengenezaji wa mifumo yetu unazingatia programu ambazo wataalamu wetu wanaweza wakatambua kinachofanyika badala ya kuwa na mifumo ambayo hatujui kinachoendelea nyuma ya pazia,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amezihimiza taasisi zote za umma kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao iliyowekwa na inayoendelea kuwekwa ili kuhakikisha matumizi sahihi ya TEHAMA ndani ya Utumishi wa Umma.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, iwapo utekelezaji wa mifumo na miundombinu ya TEHAMA utawianishwa na kuwezesha ubadilishanaji wa taarifa ndani ya taasisi za umma na baina ya taasisi za umma, ni dhahiri kuwa utoaji wa huduma kwa njia ya mtandao utakuwa ni kichocheo muhimu katika kufikia maendeleo ya viwanda ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kuyapata.

Serikali imedhamiria kuimarisha miundo mbinu ya TEHAMA, uratibu wa shughuli za TEHAMA na usalama wa taarifa za Serikali ili kuongeza ufanisi katika sekta ya umma, kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za serikali na kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images