Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 177 | 178 | (Page 179) | 180 | 181 | .... | 1904 | newer

  0 0

  TAMKO LA UMOJA WA MATAWI YA WANACHADEMA MKOA WA MWANZA DHIDI YA UAMUZI HARAMU WA KAMATI KUU YA CHADEMA.


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  UTANGULIZI

  Ndugu wanahabari, mbele yenu ni muunganiko wa wawakilishi wa matawi 189 ya chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa mwanza. Umoja huu wa matawi unawajumuisha wajumbe kutoka majimbo yote ya mkoa wa mwanza.

  Hivyo katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30.nov 2013 kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa kasorobo, pamoja na mambo mengine tumeazimia kuanzisha umoja huu wa wanachama.

  Hii ni kutokana na ukweli kwamba viongozi wetu wanaotuwakilisha kwenye vikao vya maamuzi kama  vile wilaya, mkoa na taifa wamekuwa waoga na wameshindwa kuwakilisha mawazo yetu tuliyowatuma badala yake wengi wao wamekubali kuwa vibaraka wa kile kinachoitwa CHADEMA KASKAZ.

  Kutokana na ukweli kwamba msingi wa chama chetu na chama kingine chochote kile cha siasa, uimara na uhai wake unatokana na uwepo wa misingi na matawi ya chama, hivyo sisi wanachama wa matawi haya 189 tumeamua kuunganisha nguvu zetu kutetea chama chetu na kuhakikisha haki, heshima, katiba na maadili ya chama vinafuatwa bila ya kuogopana wala kuoneana haya. Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo.

  Kwamba:-
  Chadema ni chama cha siasa kinachopaswa kuendeshwa kwa misingi ya kufuata taratibu, kanuni na katiba yake na si vinginevyo. Lakini badala yake kwasasa kumeibuka ombwe kubwa kwa viongozi wetu wa juu kujitwalia mamlaka ya chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama chetu hususan katika kutoa haki sawa kwa viongozi na wanachama wa chama chetu. Kumekuwepo na upendeleo wa hali ya juu sana kwa wale wanao amini kuwa ndani ya chama hawawaungi mkono hivyo kupelekea kuwaadhibu kama ndio kinga yao ya kuendelea kuongoza bila kuhojiwa au kukosolewa.

    
  Sababu zilizotolewa na kamati kuu hazikubaliki

  Maamuzi ya kamati kuu ya tarehe 20-21 /11/2013 ya kuwavua uongozi Mh: Zitto Zuberi Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Ndg Samson Mwigamba, kumeonyesha dhahiri si woga tu wa Demokrasia bali ni unafki na Uzandiki wa hali ya juu sana kwa viongozi wetu kuikwepa Demokrasia kwa kisingizio cha kusaliti na uhaini ndani ya chama. Katiba yetu imeweka wazi Ibara ya 6 Kifungu cha 3 kipengele cha 6. (a – f) Mamlaka za nidhamu na uwajibishaji ndani ya chama. Kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi bila kufuata taratibu hizi kwa viongozi hawa, tuonavyo sisi baadhi ya wanachama huo ni umangi meza na udhalilishaji wa kibaguzi ndani ya chama kwa viongozi wetu waliotumia nguvu zao na akili nyingi sana kukijenga chama.

  Sababu kubwa ya kuandamwa kwa viongozi hawa ni

  1.    Kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha za chama zinazotokana na Ruzuku ya fedha za serikali.
  2.    Michango ya wanachama na wapenzi kwenye mikutano ya wazi.
  3.    Harambee  za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
  4.    Kutaka kujua taratibu za manunuzi ya rasilimali ya chama namna walivyopatikana wadhabuni wa kusambaza bendera na kadi za chama, magari na pikipiki ambapo ununuzi wake ni wa mashaka makubwa.
  5.    Kutaka kuona usawa wa kimadaraka kwa viongozi wote bila ubaguzi wa aina yoyote kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa kinyume na ilivyo sasa hasa makao makuu ya chama ambapo ukanda na ubaguzi wa hali ya juu umetawala.


  Kushamiri kwa migogoro

  Mwenyekiti na katibu mkuu wameshindwa kutatua migogoro ya viongozi na wanachama kutoka mikoani kwa njia sahihi za vikao na kwa wakati hivyo kutoa mwanya kwa viongozi na wanachama kutumia njia ya mitandao ya kijamii tukiongozwa na katibu mkuu mwenyewe, kujitokeza mara kwa mara kwenye mitandao hiyo hiyo kwa madai ya kutolea ufafanuzi ya mambo mbalimbali ya husuyo maswala ya chama ilihali akijua kufanya hivyo ni usaliti mkubwa kwa chama chake, njia hiyo ya nje ya vikao ilipelekea migogoro mikubwa sana hususan mkoa wetu wa Mwanza na kupelekea kupoteza 

  Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kufukuzwa kwa baadhi ya madiwani, kuvunjwa uongozi wa mkoa na wabunge kuwa juu ya chama na kutumia nafasi zao kuopanga safu za uongozi wanao uwona watawatumikia wao na si chama, hivyo kusababisha mifarakano mikubwa ndani ya chama na kupelekea kuvuliwa uongozi kwa viongozi mbalimbali katika mkoa wetu kwa maamuzi yasiyo zingatia utafiti na uhalisia wa kweli ndani ya chama.

  Mwenyekiti na katibu mkuu wamekuwa vinara wa kuvunja katiba Mfano:

  ·        Kitendo cha kutoa muongozo nje na matakwa ya katiba juu ya kuwapata wawakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama wabunge kwamba wanaohitaji kugombea 2015 waandike barua makao makuu na wao ndio watatoa wagombea kinyume na katiba ya chama Ibara 7.2.13 inayotoa taratibu ya kuwapata wagombea, huwo ni uvunjaji wa katiba na ubakaji wa demekrasia ndani ya chama, sizani kama kuna uhaini zaidi ya huu swali la kujiuliza hapa, Je, kama leo sisi Chadema hatuheshimu katiba yetu tuliyoitunga sisi wenyewe itakuwaje siku tukikabidhiwa nchi yenye watu wenye mawazo na mtizamo tofauti na sisi?. Hatutaki kuamini kama nchi hii inaweza kugeuka uwanja wa maopambano ya kivita.

  Tunataka kujua hatua gani zilizochukualiwa dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh: Godbless Lema kumkashfu kiongozi wa chama Mh: Zitto Zuberi Kabwe kuwa ni mnafki na Mzandiki kwendye mitandao ya kijamii pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa na chama dhidi ya Bw Henry Kilewo kwa kuweka  waraka unaoitwa ripoti ya siri inayomhusu Zitto mbao chama makao makuu kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama kukana mbele ya vyombo vya habari kuwa waraka huo chama hakiusiki nao na hakiujui kabisa lakini chakushangaza Bw Kilewo ambaye pia ni kiongozi wa chama ngazi ya mkoa wa Kinondoni kichama, waraka huo ambao chama kiliukana yeye aliweka kwenye Blog yake ilihali akijua kufanya hivyo ni kinyume na kanuni za viongozi wa chama kuhusu maadili ya viongozi kanuni ya 10.

  Pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa kwa waandaaji wa tamthilia hii ijulikanayo kama Ripoti ya siri kuhusu Zitto kwasababu tayari makada na viongozi wetu wamelidhihiri kuwa wao ndo miongoni mwa waandaaji wa tamthilia hii.

  Lakini cha ajabu viongozi wetu wamelifumbia macho na kupelekea kwetu baadhi ya wanachama kuamini zengwe hili la kumchafua Zitto Lina Baraka zote za viongozi wa chama ngazi ya juu.

  Tunataka kuona nguvu iliyotumika kuwaadhibu Mh: Zitto na wenzake kwa kuandaa waraka ujulikanao kama mkakati wa mabadiliko 2013 nguvu hiyo hiyo itumike kwa hawa waliotumia njia chafu ya kuandaa waraka wa kumchafua zitto ambao chama kinawajua na baadhi yao tumewaweka humu kwenye tamko letu.

  Kingine tunataka kwa mara nyingine kwa viongozi wa chama makao makuu kuwaambia umma wa watanzania ni kwanini waraka huo huo uinaoitwa warajka wa siri kuhusu Zitto leo viongozi na wanachama mikoani na kwenye majimbo waraka huo uangawiwa kwa wanachama na wananchi kwa agizo la makao makuu kama si ubaguzi ni nini?.

  Tunaonya na kulaani kitendo cha viongozi wetu kuendeleza utawala wa kibabe na kupelekea kuhatarisha maisha ya baadhi ya wanachama na viongozi wanaotofautiana nao kimtizamo mfano: kumezuka tabia ya baadhi ya viongozi na makada wa chama chetu wasiokuwa na uwezo wa kujenga hoja jukwaani hivyo kujikuta muda mwingi wa kutumia maneno ya uchochezi dhidi ya wanachama na viongozi wanaokinzana nao kifikra na kimtizamo na kuhamasisha wanachama wasiojua itikadi vizuri ya chama kuwa wawashughulikie na maneno haya yamekuwa yakisemwa hadharani kwenye mikutano mbalimbali hivyo wananchi wapenda Demokrasia ya kweli kubaki na maswali magumu kuliko majibu juu ya ukimya wa serikali kuhusiana na jambo hili.
  Hitimisho
  Mwekiti na katibu mkuu wajiudhuru mara moja ili kupisha uchunguzi wa mapato na matumizi ya fedha za chama ambazo zinatokana na kodi za wavuja jasho wan chi hii,  M/kiti na katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya kuvunja katiba kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kutangaza uchaguzi huku mkiwaondoa washindani wenu ni uwoga na ubakaji wa Demokrasia.

  Mwisho tunataka maamuzi haya HARAMU kamati kuu yabatilishwe na mchakato wa kuwavua viongozi hawa nyazifa zao ufuate taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba tofauti na hapo tarehe 4/12/2013 tutaungana na wapigania Demokrasia kote nchini kufanya maandamano yasiyokuwa na ukomo mpaka uongozi uliopo  utoke madarakani.

  Vile vile baada ya tarehe hiyo muhakikishe mnawaamisha wabunge vibaraka wote wa chadema mkoa wa mwanza, wamchukue wenje wakamtafutie jimbo moshi na highness kiwia wamtafutie jimbo HAI na MACHAME hii ardhi ya kanda ya ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.

  Tunamuagiza mbowe na slaa wasithubutu kukanyaga ardhi hii ya kanda ya ziwa ikiwa bado hawajajiudhuru ama kubadili maamuzi yao HARAMU haraka iwezekanavyo Hatuna sababu ya kuendelea kuwa wsatumwa wa fikra ndani ya chama chetu, Tumekuwa wanyonge kwenye chama hiki vya kutosha, tumedharirishwa kwenye chama hiki vya kutosha, tumeburuzwa na kupuuza kwenye chama hiki vya kutosha, Sasa sisi wanachadema wa matawi ya mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, tunasema kwamba kanda ya ziwa na magharibi watupo chadema kwa bahati mbaya, tupo humu kama wapokezi na waasisi wakuu wa chama hiki, tunajivunia uasisi wa wazee wetu kina Marehemu Bob Nyanga Makani, Marehemu Balozi ngaiza Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, kamanda Zitto Kabwe na sisi wengine wengi.

  Vyovyote itakavyokuwa kamwe, hatutaweza kukubali aina yoyote ya upuuzi huu unaoeneawa na kusimamiwa na WAHUJUMU DEMOKRASIA NDANI YA CHADEMA. 
  Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
  Mapambano yanaendelea. CHADEMA VEMA

  ROBERT E. GWANCHELE
  Mwenyekiti wa umoja wa Matawi ya CHADEMA mkoa wa MWANZA
  Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA CHAMA ZIWA MAGHARIBI
  Mjumbe kamati Tendaji wilaya ILEMELA


  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama(kulia) akikabidhi msaada wa Magodoro kwa Sheikh Abdushakur Omary, kwaajili ya kituo cha Luhila Pachane,kilichoko Songea  mjini,kinacholea  Watoto  Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu, Sheikh Abdushakur,ni mlezi wa kituo hicho,pia ni Katibu wa Bakwata Mkoa wa Ruvuma.
   =======  =====  ======
  Na Mussa Mkama
  MKURUGENZI Mtendaji wa Msama Promitions Alex Msama amekabidhi msaada wa magodoro yenye dhamani ya zaidi ya Shilingi milioni 4 kwa kituo cha watoto yatima Luhila Pachane kilichopo Songea Mkoani Ruvuma.
   
  Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi za Msama Promotions Kinondoni Jijini Dar es Salaam jana Msama alisema msaada huo umetoka kwenye mfuko wa Tamasha la Krismas ambalo linatarajiwa kuanza Desemba 25 jijini hapa na mikoa mingine.
  Tamasha hilo la Krismas linatarajia kufanyika katika mikoa mitano, ambapo ni Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Arusha na Dodoma.
   
  Msama alisema kuwa kutokana na maombi ya kituo hicho na kuguswa na hali waliyokuwa nayo ya yatima hao kulala katika mkeka, aliamua kunyofoa sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye mfuko wa Tamasha la Krismas na kuamuo kuwasaidi watoto hao ili nao waweze kujisikia wapo katika jamii ya Watanzania.
   
  “Nimeamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na hali halisi waliyonayo yatima hao wa kituo cha Luhila Pachane huko mkoani Ruvuma nikaamua kunyofoa fedha katika mfuko wa Tamasha la Krismas kwa ajili ya kuwasaidi ili nao wajisikie wako pamoja na Watanzania wenzao” alisema Msama na kuongeza kuwa;
   
  “Msaada huo wa magodoro hayo ni zaidi ya shilingi milioni 4, hivyo ninaimani kubwa sasa kwa msaada huu yatima wataniombea kwa Mungu ili Tamasha la Krismas liwe la mafanikio kwani lengo la tamasha hilo ni kuweza kujenga kituo cha kisasa cha watoto yatima na wasiojiweza kwani kiwanja tumeshakiona kipo pale maeneo ya barabara ya Pugu Jijini Dar es Salaam.
   
  Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo Mlezi wa kituo hicho ambaye pia ni Katibu wa Bakwata mkoa wa Ruvuma Shekh Abdushakur Omary alisema anamshukuru Msama kwa wema wake aliouonyesha wa kusaidia jamii ya Watanzania wote bila kubagua dini, kabila wala rangi.
   
  “Msama ni mtu wa aina yake hana ubaguzi anashughulikia maombi ya Watanzania wote bila kuangalia dini, kabila, rangi wala utaifa wake kwani amaamini kuwa wote ni wamoja, hivyo naomba nizidi kumuombea aendelee kuwa na moyo huo wa kujitolea kwa ajili ya watu wa taifa lake wasiyojiweza” alisema Omary.
   
  Hata hivyo aliomba Wizara husika kuharakisha upatikanaji wa hati ya kiwanja kile kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kutolea misaada (Center)  pamoja na kiwanda cha kisasa cha kuzalishia kazi za wasanii  kwa manufaa ya Taifa na watu wake, kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imesaidia Watanzania wengi wenye ndoto ya kuwa wasanii wakubwa nchini.
   
  “Uwepo wa Msama katika ulimwengu huu kunamuwakilisha Mwenye Mungu, kwani Mungu si mbaguzi kwa watu wake anawapenda wote na anatoa sawa kwa kila mtu, hivyo ndivyo alivyo Msama, kwa moyo mmoja namuombea yeye na taasisi yake isiyokuwa na ubaguzi wa dini kuendelea 
   
  kuwa hivyo wakati wote” alisema Omari na kuongeza kuwa;
  “Naomba Wizara au Waziri husika kuona umuhimu wa ujenzi wa kituo hicho cha kisasa cha kutolea misaada pamoja na kiwanda cha kuzalishia kazi za wasanii, kwani wapo Watanzania wengi wenye vipaji lakini hushindwa kufanya kazi za kisanii kutokana na viwanda kuwa na gharama kubwa wasizoweza kuzimudu”
   

  0 0


   Hawa ni wazee wa zamani ambao sasa ni walimu wa mchezo wa Ngumi, Wakati wao ndio walikuwa Mabondia Wakubwa.


   Mpambano wa kwanza kati ya Gervas Rogiansion aliyevaa gloves nyekundu akipambana vikali na mpinzani wake John Christian aliyevaa Gloves za rangi ya bluu , ambapo John Christian aliibuka mshindi kwa Makonde mawili kwa moja.
   Umati wa watu waliojitokeza kutazama Bonanza la wazi la Ngumi katika kituo cha mabasi cha Mwenge
  Wapigangoma wa Kikundi cha Ngoma ya Mchiriku cha Jagwa wakitumbuiza katika Bonanza la Masumbwi.
   Mwimbaji wa Kundi la Jagwa akitumbuiza vilivyo katika Bonanza hilo la Masumbwi.
   Afisa habari wa Shirikisho la Ngumi Tanzania Salim Mwiduka akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Bonanza la wazi la ngumi.
   Mwenyeji wa Maandalizi ya Bonanza la Ngumi Kessy Juma akiwa anafungua Bonanza hilo.
   Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za ngumi Said Masanga akielezea juu ya Tuzo hizo za ngumi.
   Mjumbe wa Shirikisho la Ngumi wanawake Bi. Aisha George Vaniatis akiwa anafuatilia mpambano

  Kulia ni Mwalimu mkongwe wa Mchezo wa ngumi bwana Rashid au anafahamika kwa jina la  Super D
   Mashabiki wa Ndondi wakishangilia
   Mpambano wa pili  kati ya Haruna Swanga  aliyevaa gloves nyekundu aliyepambana vikali na na mpinzani wake Kulwa Makenzi  aliyevaa Gloves za rangi ya bluu , ambapo Haruna Swanga aliibuka mshindi kwa kumtandika mpinzani wake makonde matatu kwa sifuli.

   Mpambano wa tatu  kati ya George Costantino   aliyevaa gloves nyekundu aliyepambana vikali na na mpinzani wake Hamadi Furahisha   aliyevaa Gloves za rangi ya bluu , ambapo Hamadi Furahisha  aliibuka mshindi kwa kumtandika mpinzani wake makonde mawili kwa moja.
   Leonard Machichi aliyevaa gloves nyekundu akiwa anajikimu kukwepa ngumi kutoka kwa mpinzani wake Abuu Bakari wakati wa mpambano huo
   Abuu Bakari akipokea kipigo cha nguvu kutoka kwa mpinzani wake Leonard .. ambapo hali ilikuwa mbaya sana kwa Abuu
   Mwamuzi wa Mpambano huo Michael Mwamkenja akisimamisha mpambano huo katika Mzunguko wa pili baada ya Bondia Abuu kunyosha mikono juu ishara ya kushindwa .
   Leonard Machichi akitangazwa mshindi wa pambano hilo kali ambalo wanaliita RDT
   Makamu wa Raisi mpya wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania Lukelo Anderson au Man Power akiwa anatoa Neno la Shukurani Mara baada ya mpambano huo kuisha.
   Kutoka Kushoto ni Bi. Zuena Kipingu ambaye ni Mjumbe wa Maendeleo ya Vijana na wachezaji katika Shirikisho la ngumi za Ridhaa Tanzania,Mutayoba Rwakatale Katibu wa maandalizi hayo, na Bondia Haruna Swanga. 
  Picha zote na Dar es salaam yetu.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi na Wanachama wa Kijiji cha Udinde  Mkwajuni mapema leo jioni,Wilayani Chunya mkoani Mbeya,Kinana aliwahimiza wananchi hao kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika suala zima la kujiendelea maendeleo yao,alieleza kuwa Serikali haiwezi kumpa ajira kila mtu,isipokuwa inasaidia kwa namna moja ama nyingine kuongeza nguvu katika suala zima la kimaendeleo,hivyo amewataka vijana kutobweteka na kusubiri ajira kutoka serikalini na badala yake wajitume kujikwamua na lindi la umaskini.Ndugu Kinana akiwa sambamba na  ujumbe wake,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt Asharose Migiro,wamemaliza ziara yao leo Wilayani Chunya na kesho wanaelekea wilaya Mbarali mkoani Mbeya.
   Ndugu Kinana akizungumza na Wafugaji hao wa kabila la Wasukuma karibu na mradi huo wa maji ambao wameupokea vyema,katika kijiji cha Mteka kata ya Kapalala wilayani Chunya mkoani Mbeya.½
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake wakielezwa jambo namna mradi huo wa maji unavyowasaidia wafugaji wa kabila la Wasukuma.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mteka,Bi.Gegwa Luhende mara baada ya mradi huo kuzinduliwa rasmi. 
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akioneshwa sehemu ya kunyweshea mifugo ya wafugaji hao wa Kisukuma ndani ya kijiji cha Mteka,Kata ya Kapalala.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na  Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro kwa pamoja wakishiriki ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Kapalala kata ya Kapalala,ambalo limejengwa na Wakulima wa Tumbaku kupitia taasisi ya Chunya Development Trust.
  Pichani kulia ni Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akishiriki kufurahia jambo na wanakijiji cha Iudinde,Mkwajuni mapema leo wakati katibbu mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akizungumza nao.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na baadhi ya Wanachama na Wananchi wa Mwambani kata ya Mwambani mara baada ya kushiriki ujenzi wa Soko la Mulugo Market Mwambani,Soko hilo linajengwa na Mbunge wa jimbo la Songwe na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh Phillip Mulugo katika suala zima la kuwakomboa wananchi wake kuondokana na umaskini na kulifanya jimbo hilo lizidi kufanya vyema katika masuala mazima ya ukuaji wa Uchumi.Ndugu Kinana akiwa sambamba na  ujumbe wake,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NECSiasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt Asharose Migiro,wamemaliza ziara yao leo Wilayani Chunya na kesho wanaelekea wilaya Mbarali mkoani Mbeya.

  0 0


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake wakisalimiana wananchi na wanachama wa CCM wakati wa mapokezi Igawa, alipoanza ziara ya kuimarisha uhai wa chama katika Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya asubuhi leo.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na wafuasi wa CCM wakati wa mapokezi Igawa, alipoanza ziara ya kuimarisha uhai wa chama katika Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya asubuhi leo.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi, eneo la Igawa, wilyani Mbarali, Mbeya.
   Kinana akikata utepe kuzindua jengo la ofisi za CCM Tawi la Ihanga, wilayani Mbarali leo.
  Jengo jipya la CCM Tawi la Ihanga, wilayani Mbarali
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Ujumbe  wake wakizungumza na Wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya asubuhi leo.

  0 0

   Neema  Herbalist    Foundation  Ni  Kituo  Cha   Utafiti  wa  Tiba Asilia  na   Msaada  Wa  Matibabu  kwa  Njia  Ya  Dawa  Za  Mimea  na Vyakula  -Lishe.   Tunapenda  kuwatangazia  watu wote  kuwa , sasa tunatoa  msaada  wa  Dawa  za  mimea   na  vyakula  lishe  kwa  watu wanao  kabiliwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya  kama vilei.                  
  i.                    Presha  na  Kisukariii.                    
  ii.                  Vidonda  Vya  Tumbo
  iii.                Uvimbe  wa Tumboni  Kwa  Wanawake(Fibroid)
  iv.                Tatizo  la  Uzazi  Kwa  Wanawake  na  Wanaume
  v.                  Tatizo  la  Ukosefu  wa  Nguvu  Za  Kiume,
  vi.                Tatizo  la  Ukosefu  wa  Hamu   Ya  Tendo  La  Ndoa  Kwa Wanawake
  vii.              Kuongeza  CD 4  Kwa  watu  wanaoishi  na  Virusi  Vya Ukimwiviii.
  viii.           Mzio ama  allergy
  ix.               Pumu  ama  Asthma.
  x.                  Kupunguza  Uzito, Unene  na   KUONDOA  Vitambi  kwa wanawake  na  wanaume.            
  xi.               Kuondoa  harufu  mbaya  kinywa
  xii.             Matatizo    Yote  Ya  Ngozi
  xiii.            Kukosa  Hamu  Ya  Chakula
  xiv.           Makovu   Ya  Aina  Zote
  xv.              Matatizo  Yatokanayo  na  Upigaji  Punyeto  kwa  Wanaume
  xvi.           Dawa  Ya  Upara
  xvii.         Matatizo  Ya  Watoto pamoja  na   matatizo  mengineyo mengi.
  GHARAMA   ZA      HUDUMA  HII  NI  RAHISI  SANA ! Tunapatikana  jijini  Dar  Es  Salaam   katika  eneo  la CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU . Kufika Ofisini  kwetu , panda  magari  ya  UBUNGO-CHANGANYIKENI kasha  shuka  kituo  Cha  TAKWIMU  halafu   fuata  barabara ya  lami  hatua  ishirini  mbele  kasha  tazama  uapnde  wako  wa kulia  utaona  ofisi  imeandikwa  NEEMA  PRODUCTS Co. LTD. Hapo  ndipo  zilipo  ofisi  zetu
  Kwa   maelezo zaidi  wasiliana  nasi  kwa  Simu  namba 0766538384  Au  Tembelea  :www.neemaherbalist.blogspot.com

  0 0

   Matukio Chuma, muandaaji wa matembezi ya hisani akizungumzia matembezi hayo yatakayofanyika Januari 11, 2014 yenye kauli mbiu Nchi yangu, wajibu wangu, taifa kwanza.
  Katika mahojiano haya Chuma anazungumzia mambo mbalimbali kuhusu matembezi hayo, ikiwemo sababu ya kuyaandaa, sababu za kuyafanya katika njia waliyoamua kuyafanya (Dar-Moro), mambo ya kufanya kabla hujashiriki matembezi haya na mengine mengi.
  Unaweza kuwasiliana nao kwa simu namba 0784 311-056, 0772 545-562 ama barua pepe ambayo ni kwetutanzania@yahoo.com

  0 0

  Timu inayoundwa na wachezaji wa zamani wa timu Taifa ya Tanzania “Tanzania All Stars” na wale wa Kenya “Wazee wa Kazi” wataonyeshana kazi mjini Nairobi, Kenya siku ya fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji Desemba 12, 2013.
  Nyota wa zamani wa timu ya Yanga na ya Taifa, Kitwana “ Popat” Manara alisema jana kuwa mechi hiyo ya kihistoria imebalikiwa na Baraza la Vyama la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na wameanza mazoezi makali chini ya usimamizi wake. Timu hiyo inatarajiwa kuondoka jijini Desemba 10.
  Mbali ya Manara, mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa, Talib Hilal naye anasimamia mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kila siku jioni kwenye viwanja vya Leaders Club jijini. Manara alisema kuwa wapo katika mazoezi ya kina kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itachezwa kabla ya fainali ya mashindano hayo.
  Alisema kuwa wachezaji wote wapo vizuri na malengo yao ni kuonyesha ubora na vipaji vilivyotukuka walivyokuwa enzi ya ujana wao na kuleta sifa kubwa katika soka laTanzania. Mbali ya Manara, wachezaji wengine wanaounda timu hiyo ni Isihaka Hassan, Mohamed Mkweche, Lawrence Mwalusako, David Mwakalebela, John Mwansasu, Ali Yusuph Tigana, Sekilojo Chambua na Rashid Idd Chama.
  Wengine ni  Edibily Lunyamila, Mohamed Hussein Mmachinga, Khaleed Abeid, James Kisaka, Omari Gumbo. Kutoka Zanzibar ni golikipa Gopi na Mwinyi Bwanga. Alisema kuwa wanatarajia kumjumuisha kipa nyota wa zamani, Juma “Mensah” Pondamali ambaye kwa sasa yupo na timu ya Taifa ya Tanzania, Kilimajaro Stars inayoshiriki mashindano hayo. Kwa upande wa viongozi ni Hassan Mnyenye na mjumbe wa Baraza la Michezo nchini (BMT), Jamal Lwambo.
  “Lengo letu ni kuwa na wachezaji wengi zaidi, lakini wengi wao wameshindwa kujiunga na sisi kutokana na matatizo mbali mbali, hao ndiyo walioitikia wito huo na wameanza mazoezi, tunaomba wadhamini mbali mbali kutusaidia ili kuweza kufanikisha safari hiyo, ni gharama kubwa sana na lengo letu ni kuhamasisha mchezo wa soka, ” alisema Manara.
  Huku timu ya Tanzania ikisaka wadhamini, wenzao wa Kenya wanaendelea na mazoezi na wamekwisha taja kikosi kitakacho ikabili timu hiyo. Kikosi hicho kipo chini ya kocha George Sunguti kina wachezaji 30 ambao waliwika Harambee Stars enzi zao.
  Wachezaji hao ni makipa James Siang’a,  Mohammed Abbas, John Busolo huku mabeki ni , Josphat Murila, Elly Adero, Sammy Pamzo Omollo, Thobias Jua Kali Ochola, Ben Oloo, George Onyango, Wycliffe Anyangu, Paul Ochieng na John Bobby Ogola.
  Viungo ni  Allan Thigo, Paul Onyiera,  ambapo washambuliaji ni Joe Kadenge , Peter Dawo , Ben Musuku, Aggrey Lukoye, J.J Masiga , Mike Amwayi, Douglas Matual, Joe Birgen, Abdul Baraza, Ricky Solomon,  James Nandwa, Ambrose Golden Boy Ayoyi, John Nyawaya, David Ochieng’, George Sunguti na  Austin Oduor.

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Azania Bw.William Erio(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bwana Charles Singili(kulia) wakifuana kitambaa katika jiwe la msingi kushiria kuzindua Benki ya Azania tawi la Lamadi, Mkoa mpya wa Simiyu  jana.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Azania Bwana William Erio(wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bwana Charles Singili(kushoto) wakikata utepe kuzindua rasmi Benki ya Azania Tawi la Lamadi jana.Kulia nia mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti. Picha na Freddy Maro


  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa droo ya kwanza ya ‘Mimi Ni Bingwa’ iliyowapata washindi 23 ambao wawili kati yao walijishindia shilingi milioni tano, washindi 20 walijishindia shilingi milioni moja kila mmoja na mshindi mmoja akashinda tiketi mbili na safari ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) katika ligi kuu ya mpira wa miguu nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford. Kushoto ni Msmamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania Bw Abdallah Hemedy. Droo hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
  Wananchi wakiwa wanafuatilia vyema burudani iliyokuwa ikitolewa na vikundi mbalimbali vya burudani wakati wa kuchezeshwa kwa droo hiyo ya Mimi ni Bingwa jana kwenye viwanja vya Coco Beach jijini Dar es salaam.

  KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imetangaza washindi wa droo ya kwanza ya ‘Mimi Ni Bingwa’ inayolenga kuwazawadia wateja wake waaminifu.

  Katika droo hiyo pia washindi wawili walizawadiwa safari ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) katika ligi kuu ya mpira wa miguu nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford.

  Akizungumza wakati wa droo hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema droo hiyo imefuatia baada ya kampuni yake kuingia katika ushirikiano na klabu ya Manchester United wiki chache zilizopita.

  “Leo hii tunatangaza washindi wa droo yetu ya kwanza ya promosheni ya ‘Mimi Ni Bingwa’. Tunaamini kuwa ushirikiano wetu na klabu ya Manchester United utawapa wateja wetu uzoefu mpya katika uangaliaji wa soka. “Bado kuna zawadi nyingi zitashindaniwa ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa ya Shilingi milioni 50. Kadri unavyoshiriki kwa kujibu maswali ndivyo utakapopata nafasi kubwa ya ushindi,” alisema Mmbando.

  Alimtaja mshindi wa tiketi mbili kuwa ni Leonard Dickson Lyatuu, mkazi wa Njiro mkoani Arusha na kuongeza kuwa nafasi nyingine 13 na tiketi bado zitashindaniwa mwishoni mwa droo ya mwezi wa kwanza itakayomalizika katikati ya mwezi Desemba mwaka huu.

  Pia aliwataja Harrison Wilson Mwambogola, mkazi wa Kigogo jijini Dar es Salaam na Stephen Asheri Chapile, mkazi wa Tengeru mkoani Arusha waliojishindia shilingi milioni 5 kila mmoja na wateja wengine 20 ambao wamejishindia shilingi milioni moja (1) kila mmoja.

  Washindi wengine walioibuka na zawadi ya shilingi milioni moja kila mmoja ni Tabu Nasiru, David Geoffrey Mtitu, Fikiri Samuel Ndaki, Godfrey David Msiu, Dickson Victor Mjata, Joseph Dominic Mboya, Benezek Bahati Macha , Stephen Asheri Chapile, Bida Edwin Mwaisoloka, Rashid Jacob Kagombola, Joseph Steven Mambo, Harrison Wilson Mwambogolo,Andronice Constantine Lashayo, Abdi Ibrahim Mohammed.

  Mmbando alisema kuwa bado zawadi nyingi zaidi kushindaniwa na kuongeza kuwa ili kushiriki katika promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) ukiwa na neon “BINGWA’ kwenda namba 15656.

  Aliongeza kuwa Airtel pia imeweka vituo maalum kwa ajili ya wapenzi wa Man U kuangalia mechi za Manchester United bure kupitia luninga kubwa, hususani katika maeneo ya Coco Beach huku wakipata burudani kabla na baada ya mechi. Droo hiyo ilishuhudiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.

  0 0

   Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya LG Electronics wa Afrika Mashariki, Moses Marji (kushoto), Mtafiti katika Idara ya Vijidudu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Dk Billy Ngasala na Meneja Masoko wa LG, Soyoung Lee, wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa viyoyozi vya kufukuza mbu viitwavyo ‘LG Mosquito Away’ jijini Dar es Salaam leo.  
  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya LG Electronics wa Afrika Mashariki, Moses Marji (katikati), Mtafiti katika Idara ya Vijidudu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Dk Billy Ngasala (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alshaaf, Aliraza Rajani wakifanya mahojiano na waandishi wa habari katika uzinduzi wa LG Mosquito Away jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa DADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo leo, Dec 2, 2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa DADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo leo, Dec 2, 2013. Kushoto ni Ofisa Mawasiliano, Charles Mubita. Picha na OMR

  0 0

  Picture 019
  Aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akipozi mara baada ya kulamba Nondozzz ya shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine jijini Mwanza.
  Picture 018
  Hoyce Temu akipata Ukodak na Mdau wa tasnia ya habari nchini.
  Picture 013
  Hoyce Temu katika pozi na marafiki zake mara baada ya kulamba Nondozz.


  0 0

  PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MAJIMBO NA HII NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

   
  1. Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma 5/12/2013
   
  -      Ambapo atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano ufanyike makao Makuu ya Jimbo. Lengo likiwa kuangalia uhai wa chama.
   
  -      Mambo makuu na muhimu yalizingatiwa
   
  -      Usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe.Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.
   
  -      Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao.
   
  -      Baada ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo
   
  i.             Mkoa uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uwezekwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu yetu. 

  Hata kama yanamaumivu ….katiba yetu ifuatwe katika kutatua tatizo – Maoni ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya k/kuu ambayo dhahiri yalilenga kumilika Zitto – Kisiasa.
   
  ii.            Mkoa ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ya mkoa kwa hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa kiongozi wetu Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.
   
  iii.           Kwa hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6 kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake Kitaifa.
   
  iv.          Hivyo Mkoa kupitia kikao hicho kuwa ni bora kuzuia kuliko kutibu, tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana mitazamo ni HATARI katika hali hiyo. Mkoa ulijiridhisha usalama hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo salama tu.
   
  v.            HOFU/TAHADHARI -   Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.

  Mkoa hautokwepa lawama na Uzembe wa makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu. Hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa Taifa.
     
  LENGO KUU:  NI KUHAKIKISHA CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA
   
  Asanteni
    
                                                 
  ALHAJ. JAFARI KASISIKO                                           MSAFIRI WAMALWA
  M/KITI MKOA                        01/DEC.2013                KATIBU MKOA
  0756439200                                                                0786448443
  0714439200                                                               0756448442
   
    
  CHADEMA MKOA KIGOMA
   
   

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Kuhudumia Waathirika wa Dawa za kulevya na UKIMWI iitwayo Medicins Du Monde - Harm Reduction Programe alipofika na ujumbe wake Ikulu jijini dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Rujewa,Mbarali na Vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Barafu mapema leo,mkoani Mbeya.Kinana amesema kuwa Serikali inapaswa kutengeneza njia nzuri na ya haraka ya kuwajibisha Ofisi za Umma ili kuweza kuwachukulia hatua Wafanyakazi wanaofuja fedha za umma ambao ndio walipa Kodi,Kinana ameyasema hayo katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika Lujewa Wilaya ya Mbarali ambayo imetuhumiwa kufanya ufujaji wa fedha za  maendeleo shilingi bilioni 2.4  na baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kati ya 2010 mpaka 2012.
   Sehemu ya eneo la mto Mbarali,kama lionekanavyo pichani ikiwa ni mradi wa ujenzi  wa skimu ya umwagiliaji Mwandamtitu,unaohusisha kata tatu za Rujewa,Ubaruku na Imalilo,Wilayani Mbarali mkoani Mbeya,ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake walitembelea mradi huo unaofaa kwa kilimo cha umwagiliaji mapema leo jioniMradi huo ambao umechangiwa kiasi cha shilingi milioni 50 na Wananchi ikiwa ni sehemu ya asilimia 20 ya mchango wa jamii kwa ajili ya uchimbaji wa mfereji mkuu.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbarali,Bwa.Adam Mgoyi alieleza kuwa Ujenzi huo haukukamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa kutokana na kukosekana kwa fedha kutoka serikalini kupitia Wizara ya Kilimo,chakula na Ushirika kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi. Mkurugenzi huyo alieleza pia changamoto za Mradi huo wa Mwendamtitu kuwa unakabiliwa na changamoto ya kutopatikana kwa kibali cha matumizi ya maji kinachotolewa na Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji,kutopatikana kwa kibali hicho kunahatarisha umuhimu mkubwa wa uwepo wa mradi huu.
   Mkuu wa Mkoa,Mh.Abbas Kandoro akifafanua jambo kuhusiana na mradi huo wa umwagiliaji kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda kutembelea eneo hilo mapema leo jioni akiwa sambamba na ujumbe wake,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt Asharose Migiro.
   Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt Asharose Migiro akiwahutubia wakazi wa mji Rujewa,Mbarali na Vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Barafu mapema leo,mkoani Mbeya.
  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni Rujewa,Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.Katika mkutano huo Nape aliwatahadharisha wakazi wa eneo hilo hasa vijana kuwa makini na maneno ya Wanasiasa,ambayo baadhi yao wamekuwa wakiwapotosha na kiasi hata kupelekea vurugu ambazo hazina msingi wowote na zinaweza kuepukika iwapo busara ikitumika.

  0 0
 • 12/02/13--10:47: Article 2

 • 0 0
 • 12/02/13--10:47: Article 1

 • 0 0
 • 12/02/13--10:47: Article 0

older | 1 | .... | 177 | 178 | (Page 179) | 180 | 181 | .... | 1904 | newer