Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

Rais Kikwete amteua Engineer Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Engineer Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Desemba 2, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza leo hii.

Kabla ya uteuzi wake, Eng. Mramba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo la TANESCO.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

2 Desemba, 2013

WAATHIRIKA WA VVU WILAYANI MAKETE WASUSA KUNYWA DAWA ZA ARV

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani katika kata ya Mbalatse wilaya ya Makete 
 Wakazi wa Mbalatse wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Makete akitoa hotuba yake
 Diwani wa kata ya Mbalatse Sikumu Msigwa akisoma Risala ya wanaoishi na VVU mbele ya mgeni rasmi
 Akimkabidhi mkuu wa wilaya hotuba yao.
====
Na Edwin Moshi, globu ya jamii Makete

Pamoja na jitihada za kuhakikisha kila pembe ya nchi hii dawa za kupunguza makali ya VVU zinapatikana kwa urahisi, kioja kimejitokeza wilayani Makete mkoani Njombe kwa baadhi ya wanaoishi na virusi vya ukimwi ambao walikuwa wanatumia dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo (ARV) kuacha kutumia dawa hizo kwa makusudi

Pamoja na hayo wengine wanakataa kuzinywa dawa hizo licha ya kushauriwa na wataalamu wa afya kuanza kutumia kutokana na afya zao kuanza kuzorota

Hayo yamebainika katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yakliyoadhimishwa kiwilaya katika kata ya Mbalatse wilayani Makete mkoani Njombe

Akisoma risala ya wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika kata ya Mbalatse, diwani wa kata hiyo Mh. Sikumu Msigwa amesema miongoni mwa mambo yanayosababisha kasi ya maambukizi mapya ya VVU katani hapo ni pamoja na mila potofu za kurithi wajane na wagane, wanaume kuoa wake wengi, ngono zembe, wenye vvu kukataa kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia na kufanya ngono bila kondomu

Akihutubia mamia ya wakazi wa Mbalatse waliofika kwenye maadhimisho hayo mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro amekemea vitendo vinavyochangia ongezeko la VVU ikiwemo kuwasihi waviu kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU kama walivyoshauriwa na wataalamu wa afya ili waimarike afya zao na wazidi kujenga nguvu kazi ya Taifa

Amesema endapo watatumia dawa hizo kwa usahihi upo uwezekano wa kuishi zaidi ya miaka 20 na wakaendelea kufanya shughuli zao kama kawaida, ikiwemo kuitunza familia ambayo inamtegemea kwa kiasi kikubwa

"Ukitumia arv ndugu zangu lazima maisha yako yatakuwa marefu, na uzuri serikali yetu inawajali wananchi wake na dio maana hizo dawa zinafika mpaka huku, kwa kweli naombeni tubadilike, mkoa wetu ndio unaoongoza kitaifa, lakini bado jitihada tunatakiwa sisi ndio tuongeze, tukikubali kubadilika sisi, hata hizi kampeni za kupamban na VVU zitafanikiwa sana" alisema Matiro

Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani huadhimishwa Desemba Mosi ya kila mwaka, ambapo mwaka huu kauli mbiu ilikuwa Tanzania bila maambukizi mapya ya VVU, na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana

Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...Majukumu ya Baba katika Familia

$
0
0
Karibu katika kipindi hiki cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Katika kipindi cha wiki hii, mjadala wa WAJIBU WA BABA KATIKA FAMILIA umefungua mfululizo wetu wa mijadala kuhusu wajibu wa mzazi kwa familia yake
Mbali na washiriki waliokuwemo studio, pia tumeshirikisha maoni toka kwa wasikilizaji wetu wapendwa waliyotoa kwenye ukurasa wa Facebook
Msimamizi wa kipindi Abou Shatry akifuatilia mjadala

Karibu uungane nasi

Mjadala ukiendelea
Mgeni wetu katika mjadala huu Isidory Lyamuya

KAMPUNI MPYA YA SIMU KUZINDULIWA NCHINI

$
0
0
Sekta ya Simu Nchini Tanzania Yapata Neema Baada ya Kuingia kwa Kampuni Mpya.Kampuni inayoleta pamoja ubunifu na malengo kwa kuwa pekee kuzinduliwa bila jina.
Dar es salaam, Novemba 25, 2013 - Sekta ya mawasiliano ya simu Tanzania na Afrika Mashariki leo imepata matumaini mapya kufuatia kuingia kwa kampuni mpya ya simu ya kipekee, ya ubunifu, yenye kwa jamii, na yenye ushindani kuliko zote, kuzinduliwa bila jina.  

Pamoja na ahadi yake ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mawasiliano ya mtandao wa simu, kampuni hiyo mpya kwa wakati mmoja imezindua pia kampeni ya kiubunifu inayotambulika kwa jina la “Tupe Jina” itakayofanyika kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi katika simu kwa lengo la kuipa fursa Afrika Mashariki kuichagulia jina bora kampuni hii kwa kupiga kura.  

Hii ni kampuni ya kwanza ya simu Afrika Mashariki ambayo kweli inajali na haigopi kuamini watu, na hakuna kampuni nyingine inaweza kuthubutu kufanya hivyo. Hakuna kampuni yoyote duniani iliyoweza kuzinduliwa bila jina na kutoa jukwaa kwa kampeni ya kusisimua ya siku 10 kabla ya jina kuwekwa hadharani.

“Tupe Jina” ni kampeni itakayoanza Novemba 25, 2013 hadi 4 Desemba 2013  kwa awamu mbili katika mtandao, ujumbe wa simu na mtandao wa kijamii wa facebook. Katika awamu ya kwanza, Afrika Mashariki inapaswa kuteua majina ambayo wanapenda hii kampuni mpya iitwe.

Mshirki anaweza kuchagua jina kwa kuingia katika mtandao wa Unaweza kuteua jina  kwa njia ya magogo kwenye mtandao wa www.giveusaname.net au kutuma ujumbe wa simu ukiambatanishwa na jina analopendekeza kwenda namba  15678 au aingie katika mtandao wa www.facebook.com/giveusaname. Katika awamu ya pili ya kampeni, jopo litatathmini majina yote na itatoa majina matano ambayo yamependekezwa mara nyingi zaidi, ya kipekee na yenye ubunifu.

 Baada ya hapo Afrika Mashariki watapiga kura kwa ajili ya kupata jina bora moja ambalo hatimaye litakuwa jina la kwanza la kampuni hii ya mawasiliano ya simu ambayo daima itakuwa ya kwanza ya Kiafrika Mashariki. Mshindi katika kampeni hii, mtu ambaye atakuwa amechagua jina ambalo hatimaye litakuwa la kampuni atajishindia muda wa bure wa kupiga simu za ndani na SMS bure kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Zawadi zingine zitakuwa simu za kisasa za ‘smartphone’ na kompyuta za kiganjani (tablets) kwa washiriki wa kampeni hii ya “Tupe Jina”. Kwa muitikio wa Afrika mpya, balozi wa jina hilo ambaye ni mchekeshaji Bw  Hemedi Khalida “Mkwere” atasherehekewa, ambaye amesimama katika mstari wake kwa kipindi cha television cha “Mizengwe” ambacho kinapata kasi kila siku.

Kutokana na wataalam kutabiri kuongezeka kwa pato la taifa la Tanzania kutoka asilimia 4 hivi sasa hadi asilimia 7 mwaka 2015, sekta ya mawasiliano ina nafasi kubwa ya katika ukuaji wa uchumi katika miaka ijayo na kampuni hii mpya ya mawasiliano ya inawakilisha sura ya kasi hii kubwa ya ukuaji.

Tanzania inabaki kuwa ni moja ya nchi zenye kiwango cha kuingiza simu chini ya asilimia 50 kufikia Juni 2013, jumla ya matumizi ya mawasiliano ya simu nchini humo ni chini ya wastani kwa nchi za Afrika.

Hii kampuni mpya ya simu kwa umuhimu mkubwa itawekeza kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wateja wake kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu kwa watu wa Uganda katika sekta ya afya na hasa katika tiba za kimtandao na vituo vya elimu ya masafa.

Hii tafsiri yake ni kwamba kuwekeza idadi kubwa ya faida katika kuwezesha Afrika Mpya kuzingatia ongezeko la watumiaji wa mawasiliano ya simu, na zawadi bora ambayo kampuni hii inatarajia katika miaka ijayo ni kukuza sekta ya afya.


Kampeni ya “Tupe Jina” itaisha Desemba 4 baada hapo wananchi wa Tanzania watapata nafasi ya kupeleka namba zao wanazopendekeza kabla ya kutangazwa na kuwekwa hadharani kwa jina la kampuni.

MPIRA WA MIGUU WANOGESHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KWA WILAYA YA MAKETE

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro (katikati) akiongozana na viongozi wengine wa wilaya ya Makete, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka (kushoto) na Katibu wa CCM wilaya ya Makete(kulia) wakielekea uwanjani kukagua timu za mpira wa miguu katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Desemba 2, 2013
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akizungumza na mchezaji wa timu ya Kisasatu wakati akikagua timu hizo kabla ya mechi kuanza
 Akiwatakia kila la heri wapate ushindi
 Akiitakia timu ya Mbalatse iibuke kidedea
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akizungumza machache kabla ya kutoa kombe kwa mshindi ambaye ni timu ya Kisasatu iliyoifunga timu ya Mbalatse kwa bao 1-0
Mshindi wa kwanza alipewa kombe, mpira mmoja na jezi, na mshindi wa pili alipewa mipira miwili.Zawadi hizo zilitolewa na shirika lisilo la kiserikali la PSI
 
Mkuu wa wilaya ya Makete akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu zote mbili baada ya mchezo kumalizika(Picha zote na Edwin Moshi, Makete)

Kifuatacho Jamii Production...Fatuma Matulanga na Evans Mhando

$
0
0

Katika kipengele hiki cha HUYU NA YULE wiki hii, nimepata nafasi ya kuzungumza na vijawa wawili wa kiTanzania wanaosoma nchini China. Nao ni Fatuma Matulanga aliyeko Beijing na Evans Mhando aliyeko Nanchang ambao kwa pamoja tumejadili mambo kadhaa na zaidi kuhusu vijana
Wameeleza mengi wakioanisha kijana na maisha ya China na Tanzania ikiwemo
1: TOFAUTI KATI YA KIJANA WA CHINA NA TANZANIA
2:TOFAUTI KATI YA ELIMU YA CHINA NA KWINGINE. Ni kweli kuwa China haifunzi ubunifu na ndio maana wanasifika kwa kuendeleza kuliko kubuni?
3: MALALAMIKO KUWA BIDHAA ZA CHINA HAZINA UBORA, YANATAZAMWA VIPI HUKO CHINA?
4: NI KIPI WANACHOJUA SASA KUHUSU CHINA AMBACHO HAWAKUJUA KABLA HAWAKWENDA CHINA?
5: MABADILIKO YA SERA YA MTOTO MMOJA MNAONA IMEPOKELEWA VIPI HAPO?
6: NI KIPI WANACHOTAMANI KINGETOKA CHINA KWENDA TANZANIA (HASA KATIKA TASNIA YA HABARI?)
Na mengine mengi
Usikose kutembelea mtandao huu siku ya Jumatano ili kusikiliza mahojiano kamili
Ni huyu na Yule ya Mubelwa Bandio wa Jamii Production akihojiana na Fatuma Matulanga na Evans Mhando, wanahabari wa shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) wanaojiendeleza kielimu nchini China

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU DONATI MWASI KEZIRAHABI

$
0
0

DONATI MWASI KEZIRAHABI


Miaka nane imepita (5 Dec 2005-2013) tangu utangulie katika makazi yako ya milele.

Tunakumbuka sana upendo, ucheshi na mapenzi yako kwetu sisi sote.


Unakumbukwa sana na mke wako Hidaya Kezirahabi, watoto, wajukuu, ndugu,     jamaa na marafiki.


 "Sisi tulikupenda sana lakini Mungu alikupenda zaidi.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe"




Shimivuta kutimua vumbi Des 6 Tanga

$
0
0

MASHINDANO ya Michezo kwa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (SHIMIVUTA), yanatarajiwa kupihwa mkoani Tanga kuanzia Desemba 6 hadi 21 mwaka huu.



Mashindano hayo hujumuisha michezo ya soka, netiboli, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, huku riadha na pooltable vikitarajiwa kuongezwa kwa mara ya kwanza msimu huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa Shimivuta, Mwalimu Rashid, alisema vyo 25 vimetumiwa mialiko kwa ajili ya kushiriki katika mashindano hayo. Mwalimu alisema tayari vyuo hivyo vimeanza kutbibitisha ushiriki wao, ambapo ratiba ya michezo yote itapangwa siku moja kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.

"Tumepanga kupanga ratiba hivyo kuepuka usumbufu wa siku ya mwisho, timu nyingi zimethibitisha kushiriki na tumeongeza michezo miwili tuone kama itawezekana.

"Lakini licha ya kuitaja michezo hii tuklioiongeza, Kamati ya Utendaji inakutana Desemba 4 kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kuiweka michezo hii ya pooltable na riadha kwa mafanikio," alisema Mwalimu.

Rais huyo aliongeza kuwa changamoto kubwa wanayokutana nayo kwa sasa ni kutojitokeza kwa wadhamini licha ya kuwaomba mara kwa mara kuwaangalia katika uendeshaji wa michezo hiyo ya vyuo vya elimu ya juu.

Mwalimu alimtaja mgeni rsmi katika uzinduzi wa michezo hiyo katika Uwanja wa CCM Mkwakwani kuwa atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga.

VIDEO MAKING: ZIGGY DEE - LIVINGSTONE CITY

$
0
0
Ziggy Dee akiwa location akiendelea na kazi
Crew nzima
Mrembo aliyefanya video na Ziggy kama mrembo aliyekutana naye Tabora huko Livingstone City
Wakitembelea makumbusho
Team Kapestone Production
Eneo la makumbusho ya Tembe la Dr. David Livingstone lililopo Kwihala Tabora 
Ziggy akutana na wazazi wa binti kijijini

*SHUKRANI ZA DHATI KWA YEYOTE ALIYEFANIKISHA ZOEZI LA UFANYAJI WA VIDEO HII*



Wasanii watamba Uhuru Marathon

$
0
0
 Katibu wa Kamati ya Mbio za Uhuru Marathon,Innocent Melleck (kulia) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza maendeo ya Mbio hizo pamoja na Wasanii watakaotoa Burudani siku ya Mkesha wa Uhuru itakayofanyika Desemba 8,2013 kwenye viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania,Suleiman Nyambui. 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania,Suleiman Nyambui akielezea namna Mbio hizo zitakavyoenda ikiwa ni pamoja na kuelezea njia kulingana na makundi mbali mbali yatakayoshiriki mbio hizo. 

000000000000000 0000000000.

 Wasanii watamba Uhuru Marathon

ZIKIWA zimebaki siku chache kwa ajili ya shindano la mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, kufanyika, wasanii watakaotoa burudani siku ya mkesha wa uhuru wameapa kufanya kweli.
 
Wasanii wanaotarajiwa kutoa burudani ni Roma Mkatoliki, Joh Makini, G Nako, Nick wa Pili, Mrisho Mpoto, Mrisho Mpoto, TMK Wanaume, Mfalme Siboka na kundi la Twanga Pepeta.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema wanashukuru kupewa heshima kubwa kutumbuiza siku hiyo na hasa ukichukulia umuhimu wa amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu.
 
“Nitafanya makamuzi ya kweli siku hiyo na watu wategemee mistari iliyokwenda shule,” alisema Roma Mkatoliki, huku Mrisho Mpoto akidai ana vitu vikali zaidi atakavyoweka hadharani siku hiyo.
 
Naye Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, homa ya mbio hizo imepanda, hasa baada ya kujitokeza kwa wanariadha wengi wa mataifa mbalimbali.
 
Melleck alisema, mbali na wengi kujitokeza bado anaamini wengi wataendelea kujiandikisha ili kufanikisha lengo la mbio hizo.
 
Alisema usajili bado unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki ambapo fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.

Wasanii walipopewa somo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi

$
0
0
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza na wasanii mbalimbali wa Bongo Movie na Bongo Flava wakati alipokuwa akiifungua semina yao hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wasanii mbalimbali wakiwa katika semina hiyo, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati alipokuwa akiifungua semina yao hiyo, jijini Dar es Salaam jana. P 3. Mtaalamu wa masuala ya ukimwi, Mrina Cyanus, akiwasilisha mada ya Ukimwi na Vijana wakati wa semina hiyo.

========== ========== ===========

The Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation’s (BMAF) experience in managing HIV/AIDS projects extends from various initiatives it has implemented in improving health services in underserved areas of Tanzania through strengthening health workforce situation as well as reaching the community through outreach health services. The Foundation has reached 83% of the Tanzania regions and the beneficiaries are mainly district health managers and the community ranging from men, women and youth including People Living with HIV (PLHIV).

In its continuous efforts to contribute to the Government efforts, BMAF commemorated the globally-celebrated World AIDS day with the support from its partners Vodacom Foundation and Montage. 

This year’s World AIDS Day theme is ‘Towards Tanzania without new HIV infection, Stigma and discrimination and AIDS related deaths.’ The theme has been derived from the global move towards the three Zeros: Zero new HIV infection, Zero stigma and discrimination and Zero AIDs related deaths. 

Considering that 47% of Tanzanian population is below the age of 15, reaching youth remains one of the major strategy in achieving the three zeros. The use of popular art form, such as music has been advocated as one of the ways to reach youth. This approach has proven to be effective and sustainable, by working in ways that traditional methods of outreach has its limitations. Access to reading materials or educational lectures and access to temporary health clinics, is severely limited for non-urban communities. Music plays a pivotal role in socialization of adolescents: an average adolescent may listen to approximately three or more hours of music daily.

BMAF hosted a lunch workshop that involved around 60 bongo flava and bongo movie artists to raise awareness on HIV AIDS among the local artists as means of commemorating the 2013 World AIDS day.

The workshop refreshed and updated the musicians and movie artists of the HIV status in our country, the meaning of three zeros and preventive measures to be advocated. The workshop was also a platform to sensitize the artists to become ambassadors and Champions for the national AIDS response and youth reproductive health matters.

It is envisaged that the artists will become an important agent of change advocating for HIV preventive measures such as Circumcision, use of condoms and other youth reproductive health matters. 

The workshop was officially opened and enjoyed the participation of Hon. Ummy Mwalimu, the Deputy Minister for Community Development, Gender and Children. Likewise present in the event was the CEO of the Mkapa Foundation, Dr. Ellen Mkondya Senkoro, who welcomed all participants to the event.

UWT ZANZIBAR YAFANYA MKUTANO NA WANDISHI WA HABARI OFISI KUU YA CCM KISIWANDUI ZANZIBAR

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Bi. Salama Abuud Talib akimkaribisha Makamu Mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame kuzungumza na wandishi wa Habari kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Jumuiya hiyo.
Makamu Mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame akizunguza na wandishi wa Habari kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa Chuchu Fm Radio Rahama Suleiman akitaka ufafanuzi wa kitu kwenye Mkutano wa UWT ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI YALIYOZUNGUMZA

MSIMAMO WA CHADEMA MKOA WA SINGIDA DHIDI YA MAAMUZI YA KAMATI KUU - TAARIFA KWA UMMA

$
0
0
                     
WILFRED NOEL KITUNDU
MWENYEKITI CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013
KATIBU WA CHADEMA MKOA
S.L.P 260
SINGIDA
YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI MKOA SINGIDA
Somo hapo lahusika,
Ninapenda kukuarifu kuwa nimeamua kujiuuzuru nafasi yangu ya uenyekiti wa mkoa ambayo nimekuwa nikiitumikia kwa kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha kuamini na kudai demokrasia ya kweli ndani ya chama.

Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mwanachama wa 300 kitaifa, hiyo ni heshima kubwa sana kwangu na sipo tayari kuipoteza kwa kukubali kuwa sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia uliopitiliza

Maamuzi na vitendo vinavyoendelea ndani ya chama chetu kwa sasa ni ubakaji na udharirishaji wa demokrasia ya kweli tunayoihubiri mbele ya umma.

Kwa barua hii basi, nimeonelea bora upate ufahamu huo kuwa si vema mimi kuendelea kupingana na dhamira yangu inayonituma kuwa mwanademokrasia wa kweli.

Kwa kipindi hiki kifupi mnaweza mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mpaka hapo mtakapopata anuani yenu tayari.

Ninatanguliza shukrani zangu za dhati kwa wanachadema wote wanaopinga upuuzi huu uliofanywa na kamati kuu ya chama.

Kusimamia haki, katiba na misingi ya chama ni wajibu wangu, hivyo kwa namna yoyote ile sitaweza kuwa tayari kufumba macho pindi ujinga wa namna hii unapoendelea kutekelezwa kwa uwoga wa uchaguzi.


Nakutakia kila la heri kwenye majukumu yako.

………………………………………………….
Wilfred N. Kitundu

MWENYEKITI CHADEMA
MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013

FARAJA KWA WANAWAKE WASIO SHIKA UJAUZITO.

$
0
0
Katika  makala  yetu  ya  nyuma  tulielezea chanzo cha  tatizo  la wanawake  kutopata  ujauzito  ( Ugumba ) tukatoa  na  mapendekezo  ya  vitu  gani vya  kufanya  kumsaidia  mwanamke  asiye  shika ujauzito  aweze  kushika  ujauzito.

Kabla  sijaendelea  na  makala  haya  naomba niwaombe  radhi  wasomaji  wangu  kwa  kutumia neno ( ugumba ) hapo  juu, kwa  sababu  “ ugumba” ni  kitu  tusicho  kiamini  kabisa!  
Badala  ya  kumuita  mwanamke  mgumba, sisi hutumia  neno  “  Mwanamke  ambaye  bado hajapata  ujauzito  “.
Kupata  ujauzito  na  kuzaa  watoto  ni  haki  ya kila  mwanamke  anaye  ishi   katika  dunia  hii tunayo  ishi  mimi  na  wewe.
Kila  mwanamke  anapaswa  kuwa  na  “legitimate expectation “  ya  kupata  ujauzito  kwa  sababu kupata ujauzito  ni  jambo  ambalo  Mungu ameliahidi  na  kuliamuru  kwa  kila  mwanamke.
Kama  wewe  ni mwanamke  ambaye  bado haujapata  ujauzito, haupaswi  kukata  tamaa hata kidogo na  kudhani  labda  Mungu  amekusahau au amepanga  wewe  uwe  hivyo, la!
Kama  Mungu  alikumbuka  kukupa  vitu  kama kucha, kope, vinyweleo  vya  miguuni  nakadhalika, sidhani  kama  atakuwa  ame  sahau  kukupa  mayai ya  uzazi.
 Zipo  dawa  za  asili  za  aina  mbalimbali  ambazo zimewasaidia  mamia  kwa  maelfu  ya  wanawake  kushika  ujauzito  na  kuzaa  watoto.

Nitakuwa  nazieleza  hapa  kila  nitakapo  kuwa ninapata  nafasi  ya  kufanya  hivyo.
Leo  nitaanza  na  hii  ya  mizizi  ya  muembe  na mgomba .

MAHITAJI  ;
i.                     Bakuli  moja  kubwa  la  Mizizi  ya  mwembe.
ii.                  Bakuli  moja  kubwa  la  Mizizi  ya  mgomba.
iii.               Maji  safi  na  salama  kiasi  cha  lita tatu.


MATAYARISHO
Chukua  mizizi  ya mwembe, changanya  na mizizi  ya  mgomba, weka kwenye  sufuria  kisha ongeza  maji  safi  na salama  kiasi  cha  lita mbili  halafu  chemsha mpaka  mchanganyiko wako  utakapo  anza  kutoa supu. Chukua  supu  yako na  uihifadhi  kwenye   chupa  ya  chai.

MATUMIZI :
Tumia  kikombe  kimoja cha  chai  cha  dawa  yako, mara  mbili  kwa  siku, asubuhi  na  jioni  kwa muda  wa  siku  kumi  na nne  na  bila  wasiwasi wowote, utabeba  ujauzito.
Kama  huwa  unabeba ujauzito  halafu  unatoka,dawa  hii  itakusaidia  sana.

Kufahamu kuhusu  dawa  zingine za  asili  zinazo  saidia  kubeba  ujauzito, tafadhali tembelea ;

MSIKILIZE MSANII AFANDE SELE NDANI YA KIPINDI CHA MKASI WA SALAMA.


SHIRIKA LA AFYA DUNIANI LAKABIDHI MAGARI KWA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII NA TAMISEMI.

$
0
0

HOTUBA YA MWAKILISHI WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI, TANZANIA, DR. RUFARO CHATORA, KATIKA HAFLA YA KUKABIDHI MAGARI KWA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII NA TAMISEMI.

DAR ES SALAAM, 3RD DECEMBER 2013.

 Mheshimiwa Dr. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Mwakilishi kutoka TAMISEMI,

Maafisa wa Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii na TAMISEMI,

Mwakilishi wa UNFPA Tanzania,

Wawakilishi kutoka Wilayani,

 Waandishi wa Habari,

Mabibi na Mabwana,


Mheshimiwa Waziri, nakushukuru kwa kutenga muda kuhudhuria hafla hii ya kukabidhi magari ya wagonjwa na magari kwa ajili ya kuimarisha Huduma za Afya Wilayani na kuboresha mifumo ya rufaa, kwa kuanzia katika wilaya za mfano. Tunayo nia hasa ya kuchangia katika kupunguza vifo vya wajawazito na kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.


Mheshimiwa Waziri,
Kama ilivyoripotiwa kwako katika Mkutano mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya (RMOs/DMOs),  mapema mwaka huu, Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na TAMISEMI , tulitembelea wilaya kumi na saba (17) ili kupata taarifa za msingi na kutambua maeneo yanayohitaji kupewa kipaumbele.


Katika ziara hizo, timu ziligundua kwamba utekelezaji mzuri  wa usimamizi na mfumo wa rufaa kwa ajili ya huduma za afya kwa wajawazito na watoto, zinaathiriwa na uhaba wa wafanyakazi wa afya wenye ujuzi, upatikanaji mdogo wa magari ya wagonjwa, vifaa tiba pamoja na madawa.


Tunatambua kwamba mifumo bora ya rufaa na usimamizi elekezi ni nguzo muhimu katika kuhakikisha huduma bora za afya. Tunatambua pia haja ya wasimamizi kutoka ngazi ya Wizara ya Afya na TAMISEMI kufanya usimamizi elekezi katika mikoa na serikali za mitaa, ili kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa mujibu wa miongozo ya kitaifa. 

Wataalam kutoka Hospitali za rufaa pia wana haja ya kutoa mafunzo elekezi na msaada wa ziada kwa hospitali na vituo vya afya. Tunatambua pia umuhimu wa kuboresha huduma ya rufaa kwa kuwa na magari ya wagonjwa ya kutosha. Maeneo mengine yanayohitaji kuboreshwa ni kama vile wafanyakazi wa afya wa kutosha na wenye ujuzi, madawa na vifaa tiba.


Mbinu hizi zikitekelezwa, zina uwezo wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Tunazo taarifa kutoka Kanda ya Ziwa, kuwa wameweza kupunguza vifo vya uzazi kwa kiasi kikubwa kupitia njia hizi.


Mheshimiwa Waziri,
Shirika la Afya Duniani leo linakabidhi:


• Toyota Land Cruiser Ambulensi zenye vifaa vya dharura 18
 Toyota Land Cruiser 1
 Toyota Prados 2


Thamani ya vitu hivi ni dola za kimarekani laki nane na hamsini elfu (846,385.45) sawa na shilingi bilioni moja na milioni mia nne (1,359,295,033)  


Ambulensi kumi na nane (18) zitachangia kuboresha mifumo ya rufaa hasa kwa dharura ya uzazi na watoto katika vituo vya afya 18. Magari matatu (3) yatawezesha vitengo husika kuratibu usimamizi wa huduma za afya . Vitengo hivi ni: Kitengo cha afya ya Uzazi na Huduma za Afya kwa Mtoto (RCHS), Kitengo cha Huduma za Afya za Mikoa katika Wizara ya Afya; na kitengo cha Huduma za Afya za Wilaya katika TAMISEMI.

Mheshimiwa Waziri, 

Ni matumaini yetu kuwa magari haya yatatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Napenda kutoa shukrani zetu kwa ushirikiano mzuri ulioonyeshwa na Wizara hizi mbili ( Wizara ya Afya na TAMISEMI ) na kuthibitisha dhamira yetu ya kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Tanzania .



Mabibi na Mabwana, Asante kwa kunisikiliza.

MADAKTARI WA KICHINA WAZINDUA HUDUMA MPYA (ENDOSCOPE) HOSPITALI YA MNAZIMMOJA ZANZIBARI

$
0
0
Daktari Wang Lei akiangali sehemu ya ndani ya tumbo la mfanyakazi wa Hospitali ya Mnazimmoja kwa kutumia mashine ya (Endoscope) ambayo imeanza kufanyiwa marajabio rasmi katika Hospitali hiyo. Kushoto ni muuguzi Halima Habib Abdalla anaefuatilia kwa karibu majario ya mashine hiyo.
Daktari bingwa kutoka China Sun Kewen akimfanyia uchunguzi wa maradhi ya tumbo na koo mgonjwa mmoja kwa kutumia mashine ya kisasa (Endoscope) iliyofayiwa majaribio katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja leo.
Dkt. Sun Kewen na Dkt Wang Lei wakionyeshana Lei matokeo ya uchunguzi wa mgonjwa Halima Habib aliefanyiwa uchunguzi wa tumbo kwa kutumia mashine ya (Endoscope).
Dk. Wang Lei akitoa maelezo ya namna mashine ya (Endoscope) inavyofanyakazi na kutoa matokeo ya uhakika matatizo ya mgonjwa kwa muda mfupi. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA UTURUKI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa vionmgozi wa Umoja wa wafanyabishara wa Uturuki (RSKON) alipokutana nao Ikulu jijini Dars ea salaam leo Novemba 3, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe wa vionmgozi wa Umoja wa wafanyabishara wa Uturuki (RSKON) alikoutana nao Ikulu jijini Dars ea salaam leo Novemba 3, 2013. PICHA NA IKULU. 

Kinana na ujumbe wake awasili wilaya ya mbeya vijijini mkoa mbeya,ashiriki kazi za kijamii.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na baadhi ya wanachama wa CCM,wakishiriki ujenzi wa  Zahanati katika kijiji cha Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya mapema leo.
 Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiroakishiriki ujenzi wa  Zahanati katika kijiji cha Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya mapema leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh Abbas Kandoro sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini,Mh.Norman Sigala pichani shoto wakishiriki ujenzi wa  Zahanati katika kijiji cha Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh Abbas Kandoro na Wajumbe wengine wakitoka kushiriki na kukagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua Mradi wa ujenzi maji safi wa Izumbwe ,Iwindi  unaojumuisha vijiji nane ambavyo ni Shongo,Igale,Horongo,Itimu,Mwampalala,Izunbwe,Iwindi na Mwashiwala,Mradi huo umejengwa katika kijiji hicho kufuati vijiji hivyo kukosa maji safi kwa muda mrefu.Mradi huo unatekelezwa chini ya programu ya Taifa ya usambazaji wa maji safi vijijini na usafi wa binafsi na mazingira na ulianza rasmi septemba 2013 na ulitarajiwa kukamilika mnamo Mei,2014.
Pichani ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakifanya mkutano na Wajumbe Halmashauri kuu ya CCM wilaya katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Mbalizi,wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya.
 Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akisalimiana na baadhi ya Wanakijiji cha Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya. mapema leo walipokuwa wakipokelewa kwa ajiri ya kuendelea na ziara yao ya Kuimarisha chama cha CCM.
 Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Mbeya Vijijini,Bwa.Ipyana Harrison akimtambulisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kwa wanakijiji na wanachama wa CCM,katika kijiji cha Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya. mapema leo walipokuwa wakipokelewa kwa ajiri ya kuendelea na ziara yao ya Kuimarisha chama cha CCM.
 Ndugu Kinana na Ujumbe wakizungumza na Wanakijiji wa Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya. mapema leo walipokuwa wakipokelewa kwa ajiri ya kuendelea na ziara yao ya Kuimarisha chama cha CCM.
  Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa sambamba na wakazi wa kijiji cha Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya. mapema leo wakielekea kukagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho ambayo inajengwa na Wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini,Mh.Norman Sigala walipokuwa wakielekea kukagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho ambayo inajengwa na Wananchi,kushoto ni Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro pamoja na  Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Mbeya Vijijini,Bwa.Ipyana Harrison 

Rais Kikwete amteua Dr. Asha-Rose Migiro kuwa mbunge wa heshima

$
0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dr. Asha-Rose Migirokuwa Mbunge.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumanne, Desemba 3, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Desemba 2, 2013.

Dr. Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

3 Desemba, 2013





Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images