Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 176 | 177 | (Page 178) | 179 | 180 | .... | 1897 | newer

  0 0  0 0
 • 11/29/13--19:08: VACANCIES SALES EXECUTIVES

 • DIRA NEWSPAPER CO. LTD THE PUBLISHER OF - DIRA YA MTANZANIAPATA HABARI AND HEKA HEKA UWANJANI NEWSPAPERS WISHES TO RECRUIT ADDITIONAL SALES EXECUTIVES TO SELL ADVERTISING SPACE IN ITS PUBLICATIONS.

  WE ARE WILLING TO HOLD DISCUSSION WITH INDIVIDUALS WHO POSSESS THE FOLLOWING QUALIFICATIONS:-
   
  Academic: Form Six level, Diploma in Marketing, Business Administration or Sales and above.
  Ability to achieve set targets and objectives
  Identifies potential advertising the Clients, Studies their Business, Current and Potential Customers and to convince the clients the value and benefits of advertising in newspapers published by the company.

  Assists Clients in the Preparation of the advertising copy.
  Ability to effectively handle both allocated and potential clients.
  Communication skills –Excellent  in both English and Swahili
  Presentable and responsible
  Not engaged in any other Similar Publisher Company.
  1-2 years working experience.

  Attractive Commission and Salary will be offered to Successful Persons.
  If you are the right Person and have what it takes to Perform in highly competitive environment, please send your application Cv and Copies of Certificates. Addressed to Managing Director, Dira Newspaper Co. Ltd, P.O.BOX 105497, Dar Es Salaaam. Closing date: 30/11/2013. Or Call 0759 007878, 0222 2669066, Fax 0222 2667900, Email:diramatangazo@yahoo.com.

  0 0

  Picha kwa hisani ya thehabari.com
  Si jambo geni tena hivi sasa nchini Tanzania kusikia fulani kashambuliwa au kauawa kwa risasi.
  Silaha za moto hapa nchini hasa zile zinazomilikiwa kiholela zimekuwa zikimilikiwa na kila anayetaka... kama vocha za simu. Hata mtu mwenye uwezo kidogo, na asiye na sababu ya kuwa na silaha anaweza kumiliki silaha nyumbani kwake . Bastola kwa sasa zimekuwa kama bidhaa ya utashi na watu wanazimiliki kama wanavyomiliki simu za mkononi.
  Ungana na Sophia Kessy (L) na Mubelwa Bandio (R) katika sehemu hii ya kwanza kuangalia tatizo hili linaloonekana kuzidi kuathiri na kutishia maisha ya waTanzania wengi.


  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama wa Uganda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa Wakuu wan chi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(Photos by Freddy Maro)

  0 0


  Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25 katika ukumbi wa friends corner wengine wa pili kushoto ni Rashid Matumla,Christopher Mzazi na mratibu wa mpambano uho Kaike Siraju .
  Mratibu wa mpambano wa ndondi Kaike Siraju akiojiwa akiwa juu ya pikipiki itakayogombaniwa na mabondia Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani siku ya Desemba 25 .
  Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana  na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25  wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mratibu wa mpambano huo Kaike Siraju.
  Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana  na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25  wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mratibu wa mpambano huo Kaike Siraju Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0

  WAANDAAJI wa Tamasha la Krismas wametangaza kuwa tamasha hilo litafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Desemba 25 mwaka huu, pia litafanyika Mikoa ya Tanga na Arusha.

  Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa baada ya kumalizika maonesho ya Dar es Salaam, Desemba 26 itakuwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Desemba 28 Uwanja wa Mkwakwani Tanga na siku inayofuata Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

  Alisema awali pia walipokea maombi kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki wa Injili nchini wakiomba lifanyike katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na Mbeya, Mwanza, Shinyanga na Zanzibar.

  “Kwa sasa tumepitisha mikoa hiyo minne, tunaomba wadau wetu watuunge mkono, tunaamini litakuwa tamasha la aina yake kutokana na aina ya wasanii tulio nao,” alisema Msama.

  Tamasha la Krismas linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.

  Kwa mujibu wa Msama wanataka Tamasha la Krismas liwe bora zaidi kuliko la Pasaka kwa kualika wasanii maarufu kutoka nje na ndani ya Tanzania.

  Alisema hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na tofauti kubwa iilinganisha na matamasha mengine yaliyowahi kuandaliwa na kampuni yake.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi ambapo aliwaambia CCM hii ni CCM inayofanya kazi na asiyeweza kufanya kazi na CCM hii awapishe,kwani wapo kwa ajili ya kutetea wakulima na wafanyakazi na si vinginevyo alisisitiza Vijana kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwani ndio njia nzuri ya kuleta maendeleo na si kuami kuwa Katiba mpya inaweza badilisha maisha yao.
   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Ndugu Abbas Kandoro,Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Dkt Asharose Migiro wakitoka kwenye nyumba ya balozi wa shina namba 8,Hongera Witson katika ya kijiji cha Mtunduru kata ya Isansa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
    Pichani juu na chini ni   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mtunduru kata ya Isansa inajengwa kwa ajili ya kutunza mazingira na kuzuia upepo.
  Dkt.Asharose Migiro akiwahutumia wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi.


   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa Mbozi Ndugu Geofrey Zambi akihutubia wakazi wa Vwawa na kusema kuna matumizi mabaya ya pesa katika halmashauri za mkoa wa Mbeya na kusababisha kukwama kwa shughuli nyingi za maendeleo.


  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi.

  Nape ampa ushauri wa bure Chiza
  • Amtaka aandae majibu kwa Kamati Kuu sio kumshambulia magazetini
  •  Ahoji busara anayoidai itumike ni ipi?
  •   Asisitiza kutetea wakulima ni msimamo wa Chama
  •   Amkumbusha CCM ni chama cha wakulima
  •   Ahoji busara ya kuachia ushirika kuwadhulumu wakulima.
  •   Ahoji busara ya kulazimisha wakulima kutumia mbolea ya Minjingu inayoharibu mazao yao.

  Katibu wa NEC itikadi na uenezi amemtaka
   Waziri wa kilimo, Chakula na Ushirika kuacha kumshambulia kwenye magazeti badala yake atumie muda huu kuandaa majibu ya kuwasilisha Kamati Kuu kwa hoja zilizoibuliwa na wakulima nchini. 

  Nape akihutubia mamia ya wananchi wa mji wa Vwawa wilayani Mbozi mkoani Mbeya alionyesha kukerwa na tabia ya hivi karibuni ya Waziri huyo kumshambulia Nape kwenye magazeti kwa maneno ya kejeli badala ya kujibu malalamiko ya wakulima.

   " Katibu Mkuu tumezunguka wilaya nyingi sana nchini hakuna mahali hakuna malalamiko ya wakulima ambao ni 80% ya watanzania wote. Sasa tumemtaka waziri aje kwenye kamati kuu kueleza anatatuaje changamoto hizi, yeye amekazana kila kukicha kunishambulia kwenye magazeti. Nataka kumpa ushauri wa bure mheshimiwa sana waziri, anachofanya hanishambulii mimi anawashambulia wakulima kwasababu siongei yangu naongea malalamiko  ya wakulima" alisisitiza Nape .


   "Nimemvumilia sana lakini sasa nimechoka, kila kukicha anatumia maneno ya kejeli na vijembe, kwanini hajifunzi busara ya Naibu wake Adam Malima? aliposikia wito wetu akasema yuko tayari kuja kujieleza kwenye Kamati Kuu kwakuwa chama ndiyo mwajiri wake hivyo atazingatia maamuzi ya chama, yeye waziri kila kukicha Nape Nape Nape, kumshambulia Nape hakuondoi kero za wakulima"! Alisema Nape.


   "Nimesikia leo anasema sina busara!!busara ipi anayohoji? Mie ninayewatetea wakulima wanaolalamika kulazimishwa kutumia mbolea ya Minjingu inayounguza mazao yao na yeye anayeleta mbolea hiyo na kulazimisha wakulima watumie nani anatumia busara hapa? Yeye anayepuuza malalamiko ya wakulima kuumizwa na baadhi ya maafisa ushirika na mimi ninayetaka hatua zichukuliwe dhidi ya maafisa wake nani anatumia busara??"


   " mimi ninayemkumbusha kutembelea mkoa alioutangaza kuwa ghala la taifa la chakula ambao hajautembelea kwa miaka sasa licha ya kuwa waziri wa chakula na yeye ambaye hajatembelea nani anatumia busara?" 


   " mimi ninayemshauri asikilize kilio cha wakulima wa tumbaku,pamba na korosho badala ya kusikia kilio hicho miaka nenda miaka rudi na
   yeye nani anatumia busara?"


  Katika ziara hiyo ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ameongozana na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye imekuwa na mafanikio makubwa  na imeongeza sana imani kwa wananchi wenye mapenzi mema na nchi hii.

  Ziara hii imekuwa ya aina yake kwani Katibu Mkuu amepata fursa ya kusikia matatizo ya wananchi kuanzia wakulima ambao ndio asilimia 80%,walimu ambao ni zaidi ya asilimia 60% ya watumishi wa serikali,na kundi kubwa la vijana ambalo pamoja na kuwepo kwa taratibu za kufanya shughuli zao kwa kujiajiri bado wamekutana na vikwazo visivyo vya kawaida.

  Uamuzi wa kuwaita Mawaziri kwenye kamati kuu ya chama ili watoe majibu kwa nini matatizo ya wananchi hasa wakulima hayashughulikiwi .

  Wakulima wamelalamika sana kuhusu dhuluma  zinazofanywa na vyama vya ushirika na upatikanaji wa pembejeo kuwa wa tabu na cha ajabu Waziri wa Kilimo na watumishi wake wameziba masikio hata kutembelea wakulima kutaka kujua matatizo yao hawataki.

  0 0  ALLY OMARY CHITANDA
  MWENYEKITI WA CHADEMA
  MKOA WA LINDI

  30/11/2013

  KATIBU WA CHADEMA
  MKOA WA LINDI


  YAH; KUJIUZURU UENYEKITI WA MKOA

  Somo la hapo juu lahusika.

  Napenda kuchukua nafasi hii kukuarifu kuwa kwa hiari yangu bila ya kushawishiwa na mtu yeyote, nimeamua kujiuzuru nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa tangu leo tarehe 30/11/2013.

  Nashukuru sana kwa ushirikiano wako pamoja na Vionmgozi wote wa Baraza la Uongozi pamoja na Baraza la Mashauriano la Mkoa, lakini pia niwashukuru Viongozi wote wa Majimbo naWilaya hasa Nachingwea ambao kwa kiasi kikubwa, wameniwezesha kufika hapa hasa wakati mgumu wa Ujenzi wa Chama  na  kugombea Ubunge 2005 na 2010.Matarajio yangu ya kuweza kukomboa wanyonge kupitia CHADEMA kwa sasa  sioni kama yanaweza kufikika.

  Nitabaki kuwa Mwanachama wa kawaida na ninaahidi kuwa Mwanachama  mwaminifu na pale  nitakapohitajika  nikotayari kusaidiana na Viongozi  kujenga Chama.Nawataki kazi njema na Ujenzi wa Chama.


  Ahsante kwa ushirikiano.


  ………………………………..
  A.O. CHITANDA

  ==========  ========  ========== 
  MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI, MJUMBE BARAZA KUU TAIFA NA MKUTANO MKUU. KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU WA CHAMA MAKAO MAKAUU


  NDG: WANA HABARI:
  Kwanza kabisa ninawashukuru kwa kuitika wito wangu.
  Jina langu naitwa ALLY OMARY CHITANDA,nimejiunga CHADEMA mwaka 2003 nikitokea NCCR –MAGEUZI.

  Nyadhifa  nilizowahi kuzishika na kukitumikia Chama ni:-
             
  Kuanzia mwaka 2004- Mjumbe wa Baraza kuu Taifa  nikiwakilisha vijana Bara niliendelea kuaminiwa na Chama na kupewa kazi nyingine za kukitumikia Chama, nimewahi kuwa  Afisa wa Vijana Makao Makuu, Afisa wa sheria na Haki za binadamu Makao Makuu, Katibu wa Kamati ya muda ya Baraza la Vijana Taifa (BAVICHA) kwa sasa ni Mjumbe wa Mkutano Taifa nawakilisha Nachingwea, Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi tangu  tarehe 26/05/2013.Pia ni Afisa Mwandamizi  Ofisi ya Katibu Mkuu Makao makuu Dsm.
  vile vile kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikifanya shuhuli ya uandishi wa kumbukumbu za sekretarieti ya chama kama KATIBU WA SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.
  Hivyo sasa, pamoja na mambo  mengine yapo masuala nyeti na muhimu ninayoyafahamu na ikibidi kuwaarifu watanzania kwa njia mbali mbali pindi itakaponihitaji kufanya hivyo.

  Ndugu zangu wanahabari, nimewaita ili kupitia nyinyi niwaambie Watanzania wenzaqngu juu ya hali ya kisiasa ilivyo hasa ndani ya Chama chetu. Itakumbukwa kuwa tarehe 20-21/11/2013 Kamati kuu ya Chama ilikaa pamoja na mambo mengine ilifanya maazimio ya kuwavua nafasi za Uongozi ndani ya Chama alikuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Mhe. ZITTO KABWE na Mjumbe wa Kamati kuu wa kuchaguliwa Mhe. Dr. FITILA MKUMBO, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa sababu:-

  (a)  Mhe. ZITTO KABWE (Mb) alishiriki kusaidia Wabunge watatu wa CCM kupita bila kupingwa kenye Majimbo yao ya Uchaguzi 2010.

  (b)  Kuandaa mkakati waliouita mabadiliko ya Chama 2013. Mkakati uliolenga kumuwezesha Mhe. Zitto kushinda nafasi ya Uenyekiti wa Chama Taifa endapo angekubali kugombea.

  (c)  Mhe. Zitto alishindwa kutimiza majukumu yake ndani ya Chama kwa kutoshiriki pamoja na Viongozi wenzake kwenye matukio makubwa yaliyokikumba Chama kama:-
  (i)            Maandamano ya Arusha.
  (ii)          Operesheni zilzofanyika Morogoro na Iringa nk.

  MAAMUZI MENGINE YA UBORESHAJI WA MAKAO:
       Ni kweli kuwa pamoja na mambo mengine Baraza kuu la Chama iliridhia pendekezo lililetwa kwake na Kamati Kuu kuhusu jambo hili.Na katika utekelezaji wake Kamati Kuu ya juzi iliridhia kuwa, uteuzi wa Wakurugenzi watano ambao ni:-
  1.    Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
  2.    Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).
  3.    Mkurugenzi wa Fedha na uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
  4.    Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
  5.    Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.

  Uteuzi huu hauonyeshi sura ya Kitaifa Wakurugenzi wote watano ni Wakristo kanakwamba CHADEMA hakuna Waislamu wenye uwezo wa kushika nafasi hizo.

  Lakini pia hauzingatii mgawanyo wa kijamii kwa kuwa kati ya kurugenzi hizo sita wakurugenzi wanne kati yao wanatokea mkoa mmoja wa kilimanjaro

  Na uteuzi huu unakwenda sambamba na kuboresha maslahi yao kwa kuongeza posho, -kutoka Tshs. 800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanzia Tshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs. 6,800,000/= kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni Tshs.1,000,000-1,500,000/=.

  Pamoja na kwamba uboreshaji uliridhiwa, lakini katika mpango ulioridhiwa na Baraza kuu ni pamoja na kulipa Posho kwa Makatibu wa Wilaya na Mikoa. Hawa ndio watendaji muhimu katika Ujenzi na Uhai wa Taasisi hii lakini, hawakuangaliwa wala kuguswa  badala yake wanatakiwa kujitolea tu kwa hali na mali.

  Mimi kama nilivyotangulia kusema hapo awali, kuwa niko kwa kwa miaka 10 sasa na nimeshiriki kwa kiasi kikubwa katika Ujenzi wa Chama hiki.Sioni sababu ya kutoharakisha kulipa posho ya Mkatibu wa Wilya na Mikoa pamoja na watendaji wengine na badala yake tunaharakisha kujilipa posho nono sisi watendaji wa Makao Makuu, wakati hawa wa ngazi za chini wanamaeneo makubwa ya Kiutendaji na wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa kujitolea hata Ofisi zao wanajitolea wenyewe.

  MAAMUZI YA KAMATI KUU.
  Ningependa kuwaambia wanachadema na watanzania kwa ujumla, maamuzi haya ya kamati kuu ya kuwavua uongozi zitto kabwe na dkt mkumbo ni maamuzi ya kijuha na yanayowafanya watanzania sasa waangalie mara mbili mbili kama hawa watu wapo makini na huo ukombozi wanaousema.

  Tumekuwa tukiweka mikakati mbali mbali ya ushindi ili chama kishinde, kwa mfano, kabla hata ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa arumeru mashariki, wakati tu ilipobainika anaugua, chama kiliandaa mkakati wa kushinda ubunge wa jimbo hilo na uchaguzi uliporudiwa mkakati ule ulitumika na kushinda.

  Nikiwa mtendaji wa ofisi ya katibu mkuu, nimeshiriki pamoja na zitto kabwe na dkt Slaa kupanga mikakati mbali mbali mizuri na mibaya kwa nchi, lakini hatukuwahi kuitwa wasaliti, wahaini wala sina lolote baya. Ni fedheha leo mimi kuwa sehemu ya watu wanaomuita zitto kabwe ni msaliti. Siwezi kuendelea na ujinga huu na sipo tayari tena.

  Si dhambi kumuhukumu mtu kwa kuwa anapanga mipango ya kukushinda kwenye uchaguzi, dawa ya mpinzani wako ni kumkabili.

  Naomba nikiri kwamba nikiwa katibu wa sekretarieti tumekuwa tukilazimishwa mara kadhaa kuwashawishi wajumbe wengi kutowaunga mkono watu wenye misimamo thabiti ndani ya chama na badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali za chama kuwajenga wajumbe ndio.

  Kwa mfano hivi sasa tunapozungumza, wakati katibu mkuu wa chama anasema mjadala wa zitto kabwe umefungwa rasmi, amewaagiza wakurugenzi wa chama kuzunguza nchi nzima kusambaza waraka waliouandaa ukimchafua zitto. Hii si sawa hata kidogo, si vema kutumia rasilimali za chama kuwanufaisha watu binafsi kutimiza matakwa yao ya kisiasa.

  Nafsi yangu haipo tayari kuendelea kuwa sehemu ya upotoshaji dhidi ya watanzania wenzangu. Nafsi yangu inanikataza kabisa kuendelea kufumbia macho maovu yanayoendelezwa na chama changu.

  Nafsi yangu imechoka kuendelea kushuhudia ubaguzi wa kidini na kikabila unaofanywa wazi wazi na viongozi wa chama changu. Nafsi yangu imekataa sasa, haipo tayari tena kuwa kuwadi wa kuwahadaa Watanzania kuyafikia matarajio tunayowapa ambayo kamwe hayafikiki.

  Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa zitto kabwe na dkt kitila mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.

  Hivyo basi, nikiwa na akili timamu kabisa, leo tarehe 30.11.2013 nimeamua kujivua nyadhifa zangu zote nilizokuwa nazo ndani ya  chama.

  Sioni tena sababu ya kuendelea kuwa MwanaCHADEMA, sioni tena sababu ya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA MKOA WA LINDI, sioni tena sababu ya kuwa KATIBU WA SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.
  Kwa kuwa vipaumbele vya chadema ni kukijenga chama mikoa ya kaskazini. Basi sisi wananchi wa mkoa wa lindi tunawatakia kila la heri, na kwamba waendelee kukijenga chama chao huko huko waliko.


  Nashukuru wote ambao nilifanya nao kazi pamoja katika kutekeleza majukumu yangu.

  Ahsante Sana

  A.O. CHITANDA

  0753418510

  MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI
  MJUMBE BARAZA KUU TAIFA
  KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU- SEKRETARIETI

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi chaeti, Mkurugeniz wa Kagera Sugar, Bw. Hamadi Yahaya, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake wa kuchangia maendeleo ya Elimu ya Jimbo la Nkenge mkoa wa Kagera,wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali (mst) Fabian Masawe. Jumla ya Shilingi milioni 114, pesa taslimu milioni 65.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal Fabian Masawe. 
   - Sehemu ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo
   Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo
   Meza Kuu wakijumuika kuimba wimbo maalumu wa mkoa wa Kagera wa kuhamasisha maendeleo ya mkoa huo, hususan katika suala la elimu na kuchangia madawati.
  Msanii Saida Karoli na kundi lake wakiburudisha wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Picha na OMR.

  0 0


  KAMPUNI ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha la Krismas wametangaza viingilio vya tamasha hilo ambavyo kima cha chini ni shilingi 5000.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama viingilio vingine viti vya kawaida, 10000 VIP B na VIP A 20000.

  Msama  alisema watoto katika tamasha hilo watachangia shilingi 2000 ambako alitoa wito kwa jamii kujipanga kwa ajili ya tamasha hilo. Aidha Msama alisema viingilio katika mikoa yote litakakofanyika ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000na kuendelea kueleza kwamba wadau wajipange vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo. 

  “Tunafanya taratibu za tiketi za tamasha hilo ambazo tumepanga zitoke Uingereza, ili kukwepa wizi utakaofanywa na baadhi ya wasiolitakia mema,” alisema Msama. Msama alisema wanajipanga vilivyo kuhakikisha wanakomesha ujanja unaotarajia kufanywa na wasiolitakia mema tamasha hilo ambalo dhamira yake ni kusaidia wanaoishi katika mazingirahatarishi wakiwemo yatima, wajane na walemavu.


   Waimbaji katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, John Lisu na New Life Band (Tanzania) na waimbaji kutoka nje ya Tanzania ni pamoja na Solly Mahlangu, Liliane Kabaganza, Solomon Mukubwa na Eiphraim Sekeleti.    

  0 0

   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete together with his East African Heads Of States  Counterparts shortly after they signed the Protocol on the Establishment of the East African Monetary Union at Speke’s Bay Resort Munyonyo in Kampala this afternoon.Others from Left Presidents Pierre Nkurunzinza of Burundi, Yoweri Kaguta Museveni of Uganda, The new EAC chairman Uhuru Kenyatta of Kenya, and Paul Kagame of Rwanda.(photos by Freddy Maro.   

  0 0


  Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu Ali Omari. Chitanda, huku pia waandishi wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;

  Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama, Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, chama kimeshafunga mjadala kwenye vyombo vya habari kwa kuheshimu na kuzingatia taratibu za kikatiba za ndani ya chama kuendelea.


  Pili kuhusu suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni wapya;


  1.Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
  2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika 
  3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
  4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
  5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.


  Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.

  Kama ni suala la kuangalia mtu anatokea wapi (ambalo halijawahi wala haliwezi kuwa moja ya vigezo), ili kuonesha ukweli na kubainisha uongo wa watu wanaojaribu kufanya kazi ya CCM wakisema wao ni wanaCHADEMA, kwa kutumia propaganda zile zile na kuzifanya kuwa ni kete zao za kisiasa ndani ya chama, tunaweza kutaja maeneo ya wanakotoka au asili yao kama ifuatavyo;


  Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji, Antony Komu- Kilimanjaro.

  Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare- Kagera.
  Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila- Dodoma.
  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John John Mnyika- Mwanza
  Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema- Kilimanjar.o
  Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala- Morogoro.

  Hadi sasa uteuzi wa kurugenzi za Makao Makuu ya CHADEMA haujakamilika. Bado kuna nafasi zinazotakiwa kujazwa kwa kufuata taratibu za chama. 


  Hii ni kwa sababu maboresho yanayofanyika ndani ya chama, hadi sasa yanaendelea katika ngazi ya Makao Makuu na kanda, kisha itaendelea kwa ngazi za mikoa, wilaya, majimbo, kata, kijiji na hatimaye kitongoji.


  Katika maboresho hayo, kwa nafasi za uteuzi, yanayoendelea sasa ambayo yanakwenda hatua kwa hatua, hadi kuwa na makatibu wa kuajiriwa ngazi ya chini ya chama, chama kinazingatia uwezo, uadilifu na utayari wa mtu katika kutoa utumishi bora kwa wanaCHADEMA na Watanzania wote katika nafasi husika. 

  Suala la maslahi ya watumishi wa CHADEMA ni utaratibu wa chama ambao unajadiliwa, kufikiwa uamuzi na kisha kuridhiwa  kwenye vikao vya chama, kama ilivyofanyika kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichoketi karibuni. 


  Katika suala hili la maslahi ya watumishi wanaojitolea Makao Makuu ya CHADEMA ambayo si siri, Ndugu Chitanda amesema uongo mkubwa. Kusema kwamba Ofisa Mwandamizi anaweza kulipwa posho kubwa kuliko Mkurugenzi wa kurugenzi husika, ni uongo unaovuka mipaka. 


  Ndugu huyo anadhihirisha uongo huo yeye mwenyewe kwa kuandika hivi; 800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanzia Tshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs.6,800,000/= kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni Tshs.1,000,000-1,500,000/=”.


  Pia si kweli kuwa kila mtumishi anayejitolea Makao Makuu analipwa. Mathalani, wakurugenzi wenye nafasi za ubunge, hawalipwi hata shilingi moja kwa kazi zote wanazokitumikia chama na Watanzania kwa ujumla.


  Kwa maelezo hayo ya kutengeneza, ni kwamba hadi sasa Ofisa Mwandamizi anapokea posho kubwa kuliko Mkurugenzi na hata baada ya maboresho atapata posho kulingana na Mkurugenzi. Anapaswa kuwa mkweli. Mtu anayetaka kuonekana muungwana, anapaswa kujiweka mbali na uongo pamoja, maneno ya kutunga pamoja na upotoshaji wa makusudi.


  Kama ilivyoelezwa hapo juu, restructuring inaendelea. Ni hatua kwa hatua. Itafika ngazi za chini kama Baraza Kuu lilivyoagiza. Kwa sababu hiyo hadi sasa uteuzi wa Makatibu wa Mikoa na Wilaya haujafanyika. 


  Hata hivyo ruzuku imekuwa ikipelekwa kila kanda, mkoa, wilaya na jimbo kama ilivyoridhiwa na Kamati Kuu. Na hii ni zaidi ya pikipiki, kompyuta na magari yaliyopelekwa kila kanda. Angelikuwa mkweli, nagelisema na hili pia.

   
  Ndugu Chitanda anajichanganya sana katika taarifa yake yote. Hii ni moja ya sifa ya kukosa hoja hivyo mtu anaamua kuibua viroja au kutunga maneno kwa sababu ya kujaribu kuukana ukweli anaoujua moyoni. Tutatoa mfano mmoja; 


  Kupitia taarifa yake, anasema alikuwa mtu aliyeaminiwa hadi kuwa katika vikao muhimu, lakini wakati huo huo anasema kuna ubaguzi! Tunapaswa kumhurumia kwa kushindwa kuunganisha hata mawazo yake na kupata mtiririko wa hoja zenye mantiki! Angelikuwa mkweli angesema katika vikao vya sekretarieti na CC, aliingiaje kama kuna ubaguzi wa dini!


  Kwa sababu anazozijua yeye, Ndugu Chitanda ameamua kujipachika cheo ambacho hajawahi kuwa nacho. Amejiita kuwa ni Katibu wa Sekretarieti ya Makao Makuu. 


  Ndani ya CHADEMA pamoja na kwamba nafasi hiyo imetajwa ndani ya Katiba ya Chama, hakuna mtu ambaye ameteuliwa kutumikia nafasi hiyo. Kama anaweza  athibitishe kwa kutoa barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu Mkuu.


  Mahali pengine amejitambulisha kuwa ni Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu. Ofisi hiyo ina Katibu Mtendaji mmoja ambaye ni Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa CHADEMA.


  Operesheni ya Chama inayoendelea nchi nzima kwenye majimbo 103, si suala la siri wala lengo bovu kama anavyotaka umma uamini. 


  Ni mwendelezo wa mpango mkakati wa chama kupitia progamu za Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), unaotekelezwa kwa hatua mbalimbali na kwa mbinu tofauti tofauti pamoja na dhana ya CHADEMA ni msingi. 

  Operesheni hiyo ambayo ni mwendelezo wa nyingi za namna hiyo zinazokwenda ngazi za chini kabisa za chama, zikilenga kuimarisha taasisi na mifumo, imeanza wiki hii na ilitangazwa mbele ya waandishi wa habari.


  Tungependa kumalizia ufafanuzi huu mfupi kwa kutoa tahadhari kwa umma kuwa makini na matamko ya watu wa namna hii. Maana tunajua kwa uhakika yako mengi ya namna hii yataandaliwa na kutolewa kadri ambavyo Watanzania wanakaribia kuona na kuishi matumaini ya mabadiliko ya kiutawala na mfumo ndani ya nchi yao.


  Mathalani katika taarifa yake, Ndugu Ali Chitanda amedhihirisha na kuonesha kuwa ni aina ya watu ambao wanaCHADEMA na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuwaangalia kwa macho ya kuhoji na tahadhari ya hali ya juu, anasema hivi; 


  “Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.”  


  Aya hiyo pekee inayotumia lugha wanayotumia mahasimu wa CHADEMA, wakiongozwa na viongozi waaandamizi wa CCM, wanaohangaika kutokana na Watanzania kuwakataa, wakijiandaa kuwaondoa madarakani kwa sababu sera zao zimeshindwa, inatosha kuonesha uhalisia wa yeye mwenyewe (mtoa taarifa) alivyo. 


  Ni kauli za namna hii (kuwatisha na kutaka kuwatenganisha  Watanzania) ambazo zimekuwa zikitumiwa na watawala kama njia pekee ya kutaka kuzuia upepo wa mabadiliko unaovuma nchi nzima, zimekuwa zikiwaunganisha zaidi Watanzania kuiunga mkono CHADEMA bega kwa bega, ili kupata haki na matumaini ya wanyonge, katika mapambano ya awamu ya pili, kuelekea uhuru wa kweli.  

   
  Imetolewa leo Novemba 30, 2013, Dar es Salaam na;

  Tumaini Makene

  Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA

  0 0

   Katibu wa chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya,Bwa.Bryson Mwasimba akionesha kadi yake ya chama hicho akiirejesha kwa chama cha CCM,mara baada ya kuachia ngazi,kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga,Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko mkoani Mbeya kwenye ziara kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama,kukagua miradi mbalimbali ya chama na wananchi sambamba na kusikiliza matatizo ya wananchi na namna ya kuyatafutia ufumbuzi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya chama cha CCM,Katibu wa chama cha CHADEMA Wilayani Chunya,Bwa.Bryson Mwasimba aliyeamua kujiuzuru wadhifa wake mapema leo na kurejea CCM,huku umati mkubwa wa watu uliofika kwenye mkutano wa hadhara ukishangilia kwa mayowe na miluzi,uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga,Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
   Bwa.Bryson Mwasimba akionesha kadi ya CCM mara baada ya kutangaza kuachia ngazi CHADEMA.
   Bwa.Bryson Mwasimba akizungumza mbele ya wananchi na wanachama wa CCM kuhusiana na kuachia ngazi kwake na kurejea chama cha CCM mapema leo.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandoro akwaelekeza jambo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro,walipokuwa wakielekea wilayani Chunya mapema leo.Kwa mujibu wa Barabara hiyo inajengwa na kampuni ya China (China Communications Construction Company),yenye urefu wa Km 36 kwa gharama ya shilingi Bilioni 53.
   Ujenzi ukiendelea kwa nguvu.
   Sehemu ya ujenzi wa barabara ya Mbeya mpaka Chunya ukiendelea
   Sehemu ya ujenzi wa daraja barabara ya Mbeya kuelekea Chunya kama ionekanavyo pichani
   Mmoja wa wakazi wa Chunya akikatiza kwenye kipande cha sehemu ya barabara iliotiwa lami
  Barabara ya Mbeya kuelekea Chunya ikiendelea kujengwa.

  0 0

  TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema  amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kagera pamoja na baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wakuu wa Polisi wa Wilaya katika baadhi ya mikoa hapa Nchini.
  Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia usalama wa Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Mayunga ambaye alikuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia mazingira Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
  Aidha,   baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa (RCO) na wakuu wa Polisi wa Wilaya(OCD) waliobadilishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Tabora ACP Edward Bukombe amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Geita (RCO) ACP Francis Kibona amehamishiwa mkoa wa Njombe kuwa mkuu wa Upelelezi mkoa na nafasi yake inachukuliwa na SSP Simon Pasua  kutoka Makao makuu ya Upelelezi Dar es salaam.
  Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Wanging’ombe SSP. Francis Maro amehamishiwa Mkoa wa Katavi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Katavi ACP. Emmanuel Nley   amehamishiwa kikosi cha Polisi  wanamaji Dar es Salaam.  Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Rukwa SSP. Peter Ngussa amehamishiwa Makao makuu ya Upelelezi Dar es salaam, nafasi yake inachukuliwa na SSP Alan Bukumbi aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya kati( OCD) Mrakibu wa Polisi (SP) Salum Ndalama anaenda kuwa kaimu mkuu  wa upelelezi mkoa wa Tabora na aliyekuwa mkuu wa Polisi wa wilaya ya Tunduru (OCD) SP. Amadeus Tesha anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Polisi reli.
  Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi. 
  Imetolewa na:
  Advera Senso-SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi.

  0 0

  WAFANYAKAZI wa Bodi ya Chakula, dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDB) wakiwa katika harakati za kuangamiza vyakula vilivyomaliza muda wake wa matumizi pamoja na dawa zilizokua hazina kiwango kwa matumizi ya Binaadamu vilivyokamatwa katika maduka mbali mbali pamoja na vingene katika bandari ya Zanzibar vikiingizwa Nchini. Vyenye zaidi ya tani 40 viliangamizwa katika eneo la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Haroub Hussein).


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid, (wa pili kulia) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi moja kati ya Vitabu vya Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Alhad Mussa, baada ya ya kuzindua mpango mkakati huo wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.

  0 0

  Na Kambi Mbwana, Handeni.

  WANAUME wametakiwa kujenga tabia ya kucheki afya zao badala ya kuwaachia akina mama peke yao, ikiwa ni njia ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi uliozimishwa leo Dunia nzima, huku kiwilaya ya Handeni, yakifanyika katika Kata ya Kwasunga, wilayani Handeni.
  Kamanda wa Polisi wa Wilaya Handeni, OCD Zuberi Chembera, wa pili kulia mwenye koti jeusi akionyesha ujuzi wa kusakata rhumba katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, ambapo kiwilaya, yalifanyika Kata ya Kwasunga, ambapoi alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alihudhuria majukumu mengine ya Kitaifa. Picha zote kwa hisani ya Handeni Kwetu Blog. 
   Kaimu Mkurugenzi wa Handeni, Mr Mdoe, aliyesimama, akizungumza jambo katika madhimisho ya Ukimwi katika Kata ta Kwasunga, wilayani Handeni mkoani Tanga.
   Kamanda wa Polisi wa Handeni, OCD Zuberi Chembera, akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, ambapo kiwilaya yalifanyika katika Kata ya Kwasunga wilayani Handeni mkoani Tanga. Chembera alimuwakilisha DC Muhingo Rweyemamu.


  Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya Handeni, OCD Zuberi Chembera, akimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, ambapo maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wilayani hapa.

  Akizungumza mbele ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo, OCD Chembera, alisema wanaume wengi hawapendi kupima afya zao, hususan kujua kama wameambukizwa ugonjwa wa Ukimwi, badala yake wanasubiri matokeo ya wake zao.   Wanafunzi katika shule ya Sekondari Kwasunga, wakiigiza mbele ya wahudhuriaji katika Maadhimisho ya Ukimwi duniani, katika Kata yao.
   Hapa wanafunzi wakiingia kwa ajili ya kuimba kwaya katika maadhimisho hayo. Hakika yalipendeza kupita kiasi.


  OCD Chembera, hapa aliacha kiti na kuwasogelea kwa karibu wananchi kwa ajili ya kuzungumza nao juu ya ugonjwa Ukiwi.

  Alisema inapotoke wake zao au wapenzi wao wamepata ujauzito, hugoma kabisa kwenda kupima afya zao, jambo linaloweza kukwamisha harakati za mapambano ya ugonjwa wa Ukimwi ndani nan je ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.

  "Wanaume tuacheni tabia za kuachia akina mama waende wakapimwe afya zao pale wanapopata ujauzito, maana hiyo si njia nzuri badala yake wote tuwe kitu kimoja na kuyapokea matokeo hayo kwa ajili ya kulinda afya zetu.

  "Aidha ni wakati wa kila mmoja wetu kushirikiana kwa dhati katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi ambao unaendelea kuangamiza ndugu zetu, japo kiwilaya maambukizi ya Ukimwi yanaonekana kupungua hadi asilimia 2,” alisema.

  Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kwasunga, wananchi wengi walihuudhuria sambamba na kujionea burudani kutoka katika bendi ya Azimio pamoja na magizo kutoka kwa wanafunzi kwenye kata hiyo ya Kwasunga.

  Habari hii na picha zote ni kwa hisani ya Handeni Kwetu Blog.

  0 0

  Khadija Yusuf akiimba.
  Mzee Yusuf akinengua na mpiga gitaa wake.
  …Akiwaimbisha mashabiki.
  Mashabiki wakiserebuka kivyao.


  Shabiki akijimwaya.
  Shabiki aliyevaa kihasara akinengua jukwaani.
  Kijana aliyetuhumiwa kukwapua pochi akiwa chini ya ulinzi na pochi alilokwapua.
  UKUMBI wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam, jana usiku ulifurika mashabiki katika onyesho la bendi ya taarabu ya Jahazi inayoongozwa na staa Mzee Yusuf. (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)

older | 1 | .... | 176 | 177 | (Page 178) | 179 | 180 | .... | 1897 | newer