Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1784 | 1785 | (Page 1786) | 1787 | 1788 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony  Mavunde ameiomba jamii kuwasaidia watu wenye mahitaji ili kuwawezesha kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

  Mavunde ameyasema hayo leo katika Shule ya Fountain Gate Academy wakati akimkabidhi mtoto Christopher Masaka kwa Uongozi wa shule hiyo na kusajiliwa rasmi kama Mwanafunzi wa shule hiyo.

  Mtoto Christopher Masaka alipatwa na matatizo ya ugonjwa wa viungo uliopelekea kukatwa miguu yake yote miwili katika Hospital ya Benjamin Mkapa ambapo Hospital ya Benjamin Mkapa ilitoa msaada wa kiti mwendo “wheelchair” kwa mtoto huyo na Mbunge Mavunde kumpatia Miguu ya bandia na kumuahidi kumsomesha katika shule za Jijini Dodoma.

  Akizungumza kwa furaha kubwa,Mtoto Christopher ameshukuru Mbunge Mavunde kwa kumsaidia kufika hapo alipofika na kuahidi kusoma kwa bidii na kujituma.

  Naye Mkurugenzi wa Shule za Fountain Gate Academy Japhet Makau  amesema wamempokea Mtoto Christopher na atasoma bure kwa muda wote kufuatia maombi yaliyowasilishwa na Mbunge Mavunde katika shule yao ambayo mpaka sasa inasomesha zaidi ya watoto yatima 20 kwa ufadhili wa shule.

   Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony akiwa  katika Shule ya Fountain Gate Academy wakati akimkabidhi mtoto Christopher Masaka kwa Uongozi wa shule hiyo na kusajiliwa rasmi kama Mwanafunzi wa shule hiyo.
   
   

  0 0


  0 0

  Mwanamuziki nguli kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi amefariki dunia.

  Amefariki hii leo katika hospitali ya Avenues mjini Harare.

  Mtukudzi amekuwa akiugua kwa muda sasa. 

  Alilazimika kukatiza miadi kadhaa katika fani hiyo ya muziki katika mataifa mbali mbali duniani kutokana na kuugua kwake.Muziki wake wa mtindo wa afro-jazz ulivuka mipaka na kupata mashabiki wengi kote duniani.

  Alipata umaarufu nchini Zimbabwe kabla ya nchi hiyo kupata uhuru mnamo 1980 alipojiunga katika jeshi na muimbaji mwenza wa Zimbabwe anayeishi Marekani, Thomas Mapfumo kutoa sauti ya mapinduzi katika wakati ambapo nchi hiyo ilikuwa inakabiliana na serikali ya Ian Smith. 

  Baada ya uhuru wa nchi hiyo, aliitumia sauti yake kuzungumzia masuala ya kisiasa na ya kijamii.Kwa mara nyingi ujumbe ndani ya muziki wake ulikuwa ni wa ndani kukwepa mkono wa serikali iliyokuwa haipendelei kukosolewa.

  Mtukudzi amekuwa katika taaluma ya muziki kwa zaidi ya miongo minne, na amefanikiwa kutoa albamu 67.Albamu yake ya mwisho imeangazia hali ya kisiasa hivi sasa Zimbabwe na matatizo ya kijamii. 

  Nyota huyo wa muziki kutoka Zimbabwe alikuwa anapewa heshima ya muziki wa Afrika kama ilivyo kwa wasanii kama Hugh Masekela, Steve Dyer, Miriam Makeba, Yousssou N dour, Angelique Kidjo, Yvonne Chaka Chaka na Lady Smith Black Mambazo.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati alipokutana na viongozi wa dini Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 23, 2019.  PICHA NA IKULU

  0 0

  Shirika la RAFIKI SDO ‘Rafiki Social Development Organization’ limekabidhi vitendea kazi ikiwemo baiskeli 76 na mabegi 76 vyenye thamani ya shilingi milioni 19.4 kwa wasichana na wanawake ‘Wawezeshaji wa vikundi’ kwenye wilaya ya Shinyanga ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao vizuri katika mitaa na vijiji wanavyohudumia.
  Hafla fupi ya makabidhiano ya vitendea kazi hivyo imefanyika leo Jumatano,Januari 23,2019 katika ofisi ya RAFIKI SDO mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
  Awali akizungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a alisema vitendea kazi hivyo vitatumika kwenye kata ambako shirika lao linatekeleza shughuli za miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa baiskeli hizo zinakamilisha idadi ya baiskeli 148 kwani tayair walishatoa zingine 72.
  “Wawezeshaji hawa 76 tuliwapa elimu,sasa wanakwenda kuunda vikundi vya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kwa ajili ya kuwafundisha masuala ya ujasiriamali,malezi,mabadiliko ya tabia na masuala mtambuka,watatumia vitendea kazi hivi kuwafikia wananchi kwenye maeneo yao kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga”,alisema Ng’ong’a.
  “Shirika letu limeajiri wawezeshaji wa vikundi 131 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2019,kati ya 72 ni wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na 59 halmashauri ya Shinyanga,tunawapatia mishahara kila mwezi,wanalipiwa NSSF na wameunganishwa na mfuko wa huduma za afya”,aliongeza Ng’ong’a.
  Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko alilipongeza shirika la RAFIKI SDO kwa kushirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo huku akibainisha kuwa shirika hilo linatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kuwezesha wananchi kiuchumi.
  Mboneko aliwataka Wawezeshaji hao kutumia vyema vitendea kazi walivyopatiwa ,kuomba mikopo kwenye halmashauri na kuhakikisha wanatumia mikopo hiyo kwa shughuli za maendeleo.
  Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wanawake kutoa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto huku akiwashauri kutumia mikusanyiko ya watu kutangaza na kuuza bidhaa wanazotengeneza.
  Aidha aliwaagiza maendeleo ya jamii kutembelea vikundi vilivyoanzishwa na kuvishauri huku akizitaka halmashauri kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyo mstari wa mbele kwenye masuala ya maendeleo.
  Nao wawezeshaji hao walilishukuru shirika hilo kuwa karibu nao na kueleza kuwa hivi sasa wameweza kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa ajili ya kujiinua kiuchumi lakini pia tabia hatarishi zimepungua na wanaendelea kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi begi na baiskeli Anna Kulwa kutoka kijiji cha Kizungu kata ya Lyamidati halmashauri ya wilaya ya Shinyanga . Wa kwanza kushoto ni Afisa Maendeleo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Mhoja na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Jackson Njau, wa kwanza kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a wakishuhudia zoezi la makabidhiano ya vitendea kazi. 
  Anna Kulwa akishikana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi vitendea kazi kwa  Rahim Ibrahim kutoka kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
  Baiskeli na mabegi yaliyotolewa na RAFIKI SDO kwa wawezeshaji wa vikundi. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi vilivyotolewa na shirika la RAFIKI SDO kwa Wawezeshaji wa vikundi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Charles Maugira.
  Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi kwa wawezeshaji wa vikundi.
  Kulia ni Msaidizi wa Meneja shirika la RAFIKI SDO, Neema Lweeka akielezea kuhusu shirika hilo na shughuli za maendeleo wanazotekeleza hususani miradi ya afya,elimu,uwezeshaji kiuchumi,ulinzi wa mtoto,haki na utawala na utoaji elimu ya stadi za maisha.
  Wawezeshaji wa vikundi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiagana na wawezeshaji wa vikundi.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa mkutano tayari kufunga Mkutano Mkuu wa Kisekta wa Madini ulioandaliwa na Wizara ya Madini ambapo wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wa madini walikutana kwa siku mbili katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia  wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Kisekta wa Madini ulioandaliwa na Wizara ya Madini ambapo wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wa madini walikutana kwa siku mbili katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza wakati  hafla ya kufunga Mkutano Mkuu wa Kisekta wa Madini ulioandaliwa na Wizara ya Madini ambapo wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wa madini walikutana kwa siku mbili katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimaji Wadogo (FEMATA) Ndugu John Binna (kushoto) akimkabidhi maadhimio ambayo yamejumuisha maoni na mapendekezo ya kuboresha biashara na shughuli za uchimbaji madini kwa Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko (katikati), kulia Makamu wa Rais akishuhudia makabidhiano hayo mara baada ya Mkutano Mkuu wa Kisekta ulioandaliwa na Wizara ya Madini kukamilika.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe, Samia Suluhu Hassan akipokea maadhimio ya wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wa madini  kutoka kwa Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko mara baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Kisekta wa Madini uliofanyika
  kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe, Samia Suluhu Hassan akisoma maadhimio ya wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wa madini  mara baada ya kuyapokea wengine pichani Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (katikati) na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimaji Wadogo (FEMATA) Ndugu John Binna (kushoto) mara baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Kisekta wa Madini uliofanyika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imetakiwa kuwachukulia hatua kali za kinidhamu viongozi wanaokula Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu na kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni lakini wanashindwa kutekeleza kiapo hicho.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, alipofanya ziara ya kikazi makao makuu ya ofisi hizo jijini Dodoma yenye lengo la  kuhimiza uwajibikaji, kufahamu kwa kina majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kujiridhisha namna inavyotekeleza wajibu wake.

  Dkt. Mwanjelwa amesema, baadhi ya viongozi wamekuwa wakila Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu na kusoma Tamko la Rasilimali na Madeni lakini maisha na tabia zao ni tofauti kabisa na viapo wanavyoapa, hivyo ameisisitiza Sekretarieti ya Maadili kutumia sheria kuwawajibisha viongozi wa namna hiyo kwani ni mzigo kwa taifa. Dkt. Mwanjelwa amesema viapo na matamko ni lazima viendane na uhalisia, hivyo ameitaka Sekretarieti hiyo kufanya ufuatiliaji na kuchukua hatua bila uwoga wowote kwa kiongozi anayeenda kinyume kwani kiongozi wa namna hiyo anakosa sifa ya kuwa kiongozi bora. 

  Dkt. Mwanjelwa amesema ni lazima kuunga mkono kwa vitendo jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kupambana na viongozi ambao hawana maadili mema ili kuleta maendeleo kwa taifa. Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa Sekretarieti hiyo kuishi na kufanya kazi katika maadili mema ili wawe mfano kwa wanaowasimamia katika suala zima la maadili. “Ni lazima maadili mema yaanzie kwetu sisi ili tunapozungumza na kutoa elimu ya maadili kwa viongozi tuwe kioo kwani huwezi ukazungumzia maadili kwa viongozi kama wewe mwenyewe huna maadili, hivyo ni lazima kuonyesha mfano,”  Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

  Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu, Harold Nsekela amesema, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba masharti ya Sheria ya Maadili ya viongozi wa umma yanazingatiwa ipasavyo. 

  Nsekela ameyataja majukumu ya Sekretarieti kuwa ni pamoja na kupokea matamko ya viongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni yanayopaswa kutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kuanzisha na kufanya uchunguzi wowote kuhusu ukiukwaji wa maadili yaliyotajwa na Sheria, kupokea na kushughulikia malalamiko na taarifa za ukiukwaji wa maadili kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutoka kwa wananchi na kufanya uhakiki wa Tamko la Rasilimali na Madeni ya Viongozi wa Umma wanaotajwa na Sheria.

   Nsekela ameyataja baadhi ya matarajio ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwa ni kujenga na kuimarisha maadili ya kitaifa na kuyafanya yawe sehemu ya jamii ili kuzuia mmomonyoko wa maadili katika nchi kwa kujumuisha somo la maadili katika mitaala kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu, kufanya marekebisho ya Sheria zinazohusu ukuzaji wa maadili nchini ikiwemo Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma pamoja na kutungwa kwa Sheria ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Sekretarieti hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Kushoto ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mst. Harold Nsekela.
  Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mst. Harold Nsekela (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuhusu majukumu ya ofisi yake wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, alipoitembelea ofisi hiyo kuhimiza uwajibikaji jijini Dodoma.
  Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika katika ofisi ya Sekretarieti hiyo jijini Dodoma.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma kwa ajili ya kuhimiza uwajibikaji.

  0 0

   Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akipata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi juu ya mradi wa Tanki la Maji litakalochukua lita milioni tatu na kumaliza tatizo la maji katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kongwa.
   Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akizungumza jambo  na Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai wakati waziri  uyo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji katika eneo hilo.
   Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wakazi wa Mtanana Wilayani Kongwa  mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji.
    Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji mji mdogo wa Kibaigwa Mhandisi Bonifas Bihemo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji katika eneo hilo.Kushoto kwake ni Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai.
   Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa(Kushoto) kukagua miradi ya maji Wilayani Kongwa.Pembeni ya Waziri ni Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai.
   Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akizungumza na wananchi wa Kibaigwa (Hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa kukagua miradi ya maji na kutatua changamoto mbalimbali za maji.
   Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akitoa tamko la kuivunja Bodi ya Maji Mji mdogo wa Kibaigwa kutokana na utendaji mbovu na kushindwa kutekeleza  majukumu yake vyema.
  Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Wilayani Chamwino.
  Picha na Daudi Manongi,MAELEZO

  0 0  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akishuhudia tukio hilo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega (kulia).
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wanaotoa huduma ndani ya duka hilo jipya la TTCL lililo zinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TTCL, Mhandisi Omary Nundu akimsikiliza.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kulia) akiingia kwenye duka hilo mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba (wa pili kushoto) wakionesha baadhi ya bidhaa za TTCL zinazopatikana katika duka jipya la TTCL lililozinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega (kulia) pamoja na Kaimu Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar Es Salaam, Bi. Jane Mwakalebela.
  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega wakionesha baadhi ya bidhaa za TTCL zinazopatikana katika duka jipya la TTCL lililozinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam.
  Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililo zinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam.  SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo limezinduwa duka jipya na kituo cha huduma Kariakoo eneo la Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu alisema kwa Mwaka 2019, TTCL imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Huduma za Shirika hilo zinasambaa zaidi kote nchini huku ikisimamia ubora na unafuu wa gharama ambazo zitakuwa nafuu kwa wananchi.

  "...Tunakusudia kuendelea kufanya mageuzi makubwa ndani ya Shirika ili kuliwezesha kushindana kikamilifu katika Soko la Huduma za Mawasiliano Nchini sambamba na kutimiza wajibu wa kimsingi wa kuwa mchangiaji muhimu katika Pato la Taifa," alisema Mhandisi Omary Nundu.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Waziri Kindamba awali akizungumza alisema uzinduzi huo wa duka na kituo cha Huduma kwa Wateja ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu, 2016-2019 ambao umeweka msisitizo mkubwa katika kuboresha eneo la Huduma kwa Wateja.

  "Uzinduzi wa leo unaonesha kwa vitendo jinsi gani TTCL mpya ilivyojipanga vyema kuhakikisha huduma zake zinawafikia Wateja katika mazingira mazuri, yanayovutia na kuwakilisha hadhi ya Shirika letu. Kukamilika kwa Duka hili/ Kituo hiki cha Huduma kwa Wateja kuonaongeza idadi ya Maduka mapya ya TTCL kufikia maduka 10 ambayo yamejengwa kwa viwango vya hali ya juu na kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya utoaji bora wa Huduma kwa Wateja,"

  Aidha aliongeza kuwa TTCL itaendelea kuboresha Maduka na Vituo vyetu Nchi nzima, sambamba na Ofisi zake za Mikoani na Wilayani ili ziweze kuwa mahali bora kabisa kwa Watumishi wa TTCL wanaotoa huduma na Wateja wote watakaofika kupata huduma za aina mbalimbali.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa TAWJA uliofanyika kwenye Hotel ya Verde, Mtoni Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Jaji Prof. Ibrahim Juma kabla ya akihutubia hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa TAWJA uliofanyika kwenye Hotel ya Verde, Mtoni Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji Imani Aboud (kulia) wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa TAWJA uliofanyika kwenye Hotel ya Verde, Mtoni Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0
  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola wakionesha mkataba wa ushirikiano wa kupinga ukatili wa kijinsia katika masoko ya Mikoa ya Shinyanga na Mbeya baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano jijini Dar es Salaam. 
  Mwenyekiti wa Bodi ya EfG, Penina Leveta (kulia), akiwa na viongozi wa mashirika yaliyofanya mkataba wa ushirikiano. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga na Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga. 
  Mtathimini Miradi wa EfG, Samora Julius, akitoa mada katika semina ya maofisa wa mashirika hayo iliyofanyika hivi karibuni.
  Maofisa wa mashirika hayo wakiwa kwenye semina hiyo.
  Semina ikiendelea.
  Mwezeshaji katika semina hiyo, Pentaleon Shoki akitoa mada.
  Usikivu katika semina hiyo.
  Mwonekano wa chumba wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika moja ya kumbi zilizopo Baraza ka Maaskofu Kurasini jijini Dar es Salaam. 
  Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa semina hiyo na kusaini mkataba wa ushirikiano.  Na Dotto Mwaibale

  MASHIRIKA matatu yasiyo ya kiserikali yametiliana saini mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kupinga ukati wa kijinsia kwenye masoko`katika mikoa ya Mbeya na Shinyanga.

  Mkataba huo ulihusisha shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, Shirika la Miiko la mkoani Mbeya na Shirika la Equality for Growth (EfG) la jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa kufunga semina ya siku tatu iliyowashirikisha maofisa kutoka katika mashirika hayo jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita alisema wameona waungane ili kuongeza nguvu ya kampeni ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika masoko ndani ya mikoa hiyo.

  "Sisi shirika letu kwa hapa Dar es Salaam tulianza na mradi wa mpe riziki si matusi ambao ulilenga kuwalinda wanawake wafanyabiashara sokoni dhidi ya ukatili. Katika kupunguza ukatili dhidi ya wanawake katika masoko mradi huo umeweza kubadilisha mtazamo na tabia dhidi ya ukatili kwa wamawake, kuwahakikishia waathirika wa ukatili wanapata hakizao" alisema Magigita.

  Alisema utafiti uliofanywa na EfG mwaka 2015 katika masoko 6 kuhusu ukatili wa kijinsia na uelewa wa sheria katika Wilaya za Temeke na Ilala jijini Dar es Salaam ulionesha kuwepo na ukatili dhidi ya Wanawake katika masoko ambapo asilimia 95.97 ya waliohojiwa katika masoko yote walisema kulikuwa na ukatili dhidi ya wanawake kwenye masoko yao.

  Alisema zaidi ya wafanyabiashara 6500 waliweza kufikiwa na kampeni za kupinga ukatili, kampeni za kuongeza uelewa juu ya ukatili dhidi ya wanawake, sheria na haki za binadamu.Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola alisema sasa wanakwenda kufanya kampeni kubwa ya kupinga ukaliti wa kijinsia katika Soko Kuu, Nguzonane, Kambarage, Ngokolo, Ndembezi na Majengo Mapya.

  Na Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga alisema kampeni hiyo wataifanya katika masoko yote ya jijini humo.

  0 0

  *~ Wananchi waanika hali ilivyo*


  Na Ripota wetu, Mihambwe

  Afisa Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu amefanya ziara ya kushtukiza kwenye Zahanati ya Mkoreha iliyopo Kata ya Mkoreha ili kubaini ukweli juu ya huduma zitolewazo.

  Gavana Shilatu alitembelea Leo Jumatano Januari 23, 2019 ambapo amebaini uwepo wa huduma nzuri inayoghubikwa na changamoto ya uwingi wa Wagonjwa na kutoa maagizo kwa watoa huduma kuongeza kasi ya utoaji huduma.

  *"Wananchi wanakiri huduma ni nzuri, nawapongeza. Japo Kuna changamoto ya uwingi wa Wagonjwa. Nawapa maelekezo Wauguzi jitahidini kuongeza kasi ya Watu kuhudumiwa kwa haraka, muhakikishe mnatoa dawa kwani nimeziona zipo nyingi.",Alisema Gavana Shilatu.

  Gavana Shilatu amewasihi Wauguzi kuzingatia maadili, nidhamu, miiko na uwajibikaji zaidi kazini ili kuleta tija zaidi kwani maendeleo ya Watu yanategemea zaidi uwepo wa afya njema.

  0 0

  Mshindi wa gari la tatu kupitia promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane Baa, George Isaya mkazi wa Arusha, akifurahi baada ya kukabidhiwa gari lake. Kushoto ni Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, Meneja Masoko na Biashara wa TBL Edith Bebwa (kulia) na Afisa Mawasiliano wa TBL Amanda Walter.
  Meneja ukuzaji Masoko wa TBL na ABInBev Afrika Mashariki Edith Bebwa (katikati) akimkabidhi ufunguo wa gari mkazi wa Arusha, George Issaya mshindi wa gari la promosheni iliyomalizika ya TBL Kumenoga Tukutane Baa. 

  Mkazi wa Arusha, George Isaya (29) ambaye wiki iliyopita aliibuka mshindi wa gari mpya aina ya Renault KWID, katika droo ya promosheni ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’leo amekabidhiwa gari katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, alisema gari hilo ndio la mwisho katika promosheni hii iliyodumu kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo pia imewezesha wateja wengine Julitha Kilawe wa Dar es Salaam na Frank Nathan wa Iringa kujishindia magari.

   “Kwa niaba ya kampuni ya TBL, nawapongeza wateja wetu wote ambao wameshiriki katika promosheni hii na wale ambao wamefanikiwa kujishindia zawadi kubwa za magari na zawadi nyinginezo ambazo zilikuwa zinatolewa kupitia kununua bia za chapa za bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.” 

  Akizungumza kwa furaha baada ya kukabidhiwa gari lake, George Isaya alisema siku zote tangu apigiwe simu na kupewa habari za kushinda gari alikuwa haamini kama kama ni za kweli, leo baada ya kukabidhiwa gari lake ndio ameamini. “Ninayo furaha kubwa kuona ndoto yangu ya muda mrefu ya kumiliki gari imetimia kupitia kunywa bia aina ya Kilimanjaro, gari hili litanisaidia kunirahisishia usafiri katika kutekeleza majukumu yangu mbalimbali, nashukuru kampuni ya TBL kwa kubuni promosheni zenye kuleta manufaa kwa wateja wake” alisema George Isaya. 

   Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, aliwashukuru wateja wote wa TBL kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.

  0 0

  Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amendelea na ziara yake ya kukagua ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika kata ya Bwawani.

  Dc Muro akiwa katika ziara hiyo ameeleza kuwa wanafunzi zaidi ya 245 mpaka sasa wote waliopangwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019 katika shule ya Sekondari Bwawani wamepata nafasi ya  kuendelea na masomo yao bila hata mmoja wao kukosa.

  Ziara  ya Mkuu wa wilaya  Ndugu Jerry Muro imelenga kufahamu upatikanaji wa Elimu bora  kwa wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza kwa mwaka huu.

  Pia Dc Muro amewapongeza wananchi wa kata ya bwawani kwa jitihada zao kuweza kujenga madarasa mawili kwa kipindi cha muda mfupi na kuanzia wiki ijayo wanafunzi wataanza kutumia madarasa hayo.

  Sambamba na hapo Mkuu wa Wilaya hiyo ametoa wito kwa wananchi wote na wadau  mbalimbali wa maendeleo Wilayani Arumeru kuendelea kuchangia ujenzi wa madarasa pasipo kuvunjwa moyo na Baadhi ya wanasiasa wanaojaribu kuhujumu zoezi la ujenzi wa madarasa.
   Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akitoa maelekezo kwa watendaji,wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika kata ya Bwawani.
   Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akikagua ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika kata ya Bwawani.


  0 0


  ZAIDI wa Wachama Wastaafu 5000 mkoani Tanga waliondikishwa kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuanzia Julai 2009 hadi Septemba 2018 wameanza kuhakikiwa.

  Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Mfuko mkoani Tanga Ally Mwakababu (Pichani Juu) wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema zoezi hilo lilianza Januari 2 mwaka huu na litamalizika Machi 30 mwaka huu.

  Alisema kwamba uhakiki huo unafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu huku akiwataka wastaafu mkoani hapa ambao walioandikishwa kufika kwenye ofisi za mfuko huo kwa ajili ya kuhakikiwa. Mwanachama Mstaafu afike ofisini akiambatana na mwenza wake (endapo yupo hai)endapo mwanachama mstaafu amefariki ,mwenza aliyebaki afike kwa ajili ya uhakiki huo “Alisema Meneja huyo.

  “Lakini pia mwanachama anapaswa kufika na vitu muhimu ikiwemo kitambulisho cha NHIF, Cheti cha Ndoa (kwa mstaafu mwenye mwenza),Kitambulisho cha Uraia au mpiga kura ,leseni ya Gari au hati ya kusafiria ikiwemo barua ya kustaafu “Alisema Meneja huyo.

  Hata hivyo alisema kwamba ofisi inawataka wanachama wastaafu kufika kwa uhakiki ndani ya muda uliowekwa ili kuepuka usumbufu wa kukosa huduma kwa kutokufanya hivyo.

  0 0  Kutazama matokeo BOFYA HAPA 
    
                                au    BOFYA HAPA

  0 0

  NA WAMJW-GEITA.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameuagiza uongozi wa Hospitali ya mkoa wa Geita kuhakikisha wanafungua duka la dawa ili kutoa huduma karibu na wananchi pia kuongeza mapato ya Hospitali.

  Waziri Ummy ametoa agizo hilo mapema leo wakati alipoitembelea hospitali hiyo ili kuona hali ya miundombinu pamoja na utoaji wa huduma za afya.
  “Tumeshaagiza Hospitali zote nchi nzima kuwa na maduka ya dawa ya Hospitali, kwanini hapa hamjafungua duka lenu? Alihoji Waziri Ummy na kuongeza “sasa nawapa miezi miwili uongozi wa Hospitali kuhakikisha mnafungua duka la dawa la Hospitali ili liweze kuwasaidia kupandisha mapato lakini pia kusogeza huduma karibu na wananchi. Alisema Waziri huyo.

  Pamoja na hayo Waziri Ummy ameonekana kuridhishwa na hali ya upatikanaji wa dawa wa zaidi ya asilimia 90 na uboreshwaji wa huduma za afya zinazotolewa katika Hospitali hiyo.Kabla ya hapo Waziri Ummy alitembelea ujenzi wa Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita ambapo alishuhudia ujenzi huo ukiwa umekamilika kwa asilimia 54 lakini amemtaka mkandarasi anayesimamia ujenzi huo ambaye ni wakala wa ujenzi (TBA) kufanya kazi usiku na mchana ili Hospitali hiyo ianze kufanya kazi ifikapo Mwezi Julai 2019.

  Waziri Ummy amekamilisha ziara yake ya mkoa wa Geita kwa kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Chato ili kujiridhisha na hali ya utoaji wa huduma za afya na miundombinu pamoja na kuhakikisha kama vifaa na vifaa tiba vinapatikana Hospitalini hapo.

  Waziri Ummy ameridhishwa na utolewaji wa huduma za afya lakini ameitaka Hospitali hiyo kuwa na chumba maalum chenye vifaa maalum vya uangalizi wa watoto wachanga mahututi na wale waliozaliwa kabla ya siku (watoto njiti) lengo likiwa ni kupunguza vifo vya watoto wachanga nchini.

  Aidha, waziri huyo ameagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuanzisha kitengo cha huduma za wagonjwa wa dharura na wale waliopata ajali ikiwa ni agizo la serikali kwa hospitali zote za wilaya na mikoa nchi nzima.Huo ni muendelezo wa ziara za Waziri Ummy katika mikoa ya kanda ya ziwa kutembelea Hospitali mbalimbali kuangalia hali ya miundombinu na utoaji wa huduma za afya.  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongozana na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita Bw. Josephat Maganga (kulia) wakitoka kukagua jengo la hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia mashine mpya ya X-ray ya kidigitali iliyifungwa katika Hospitali ya wilaya ya Chato wakati alipoitembelea hospitali hiyo kuona hali ya utoaji huduma za afya.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia ramani ya majengo za majengo ya Hospitali ya rufaa ya Geita wakati alipotembelea ujenzi huo. Pembeni ni msimamizi wa ujenzi huo Injinia Grace Elias.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyekuja kupata matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Geita. Katikati ni mama wa mtoto huyo Bi. Jenista Benedicto.


  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 8 mwaka huu imepanga kumsomea maelezo ya mashahidi (commital) aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya na mwenzake wawili wanaokabiliwa na mashtaka 58 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

  Hatua hiyo imefikiwa leo Januari 24,2019 baada ya upande wa utetezi kupinga maombi ya upande wa mashtaka ya kutaka kesi hiyo iahirishwe kwa siku 14 wakieleza kuwa wapo katika hatua za mwisho za kufaili taarifa (fail information), hivyo wanaomba siku hizo kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo. 

  Hata hivyo upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Masumbuko Lamwai ulidai "Washtakiwa hao wamekaa ndani miaka mitatu sasa, walifutiwa kesi kiujanja na kuleta tena kesi hii ili wakae tena ndani, hivi ni kitu gani kinazuia commital, wiki iliyopita walisema leo watawasomea na sasa wanasema wapo kwenye hatua za mwisho watueleze hiyo hatua, " alidai Wakili Lamwai. 

  Mapema Wakili wa Takukuru Leonard Swai alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa wanaomba tarehe nyingine ili wakamilishe zoezi la kuwasilisha taarifa kwani wapo katika hatua za mwisho. Hata hivyo, hakimu Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hiyo, alikubaliana name upande wa utetezi name kesi hiyo itakuja Kwa ajili ya commital Februari 8, mwaka huu. 

  Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni maofisa wa Benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, Kamishna wa Sera ya uchambuzi wa Madeni kutoka Wizara Fedha na Mipango, Bedason Shallanda na msaidizi wake Alfred Misana.

  Katika mashtaka hayo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kughushi, moja la kuongoza uhalifu, 49 utakatishaji fedha, mawili ya kutoa nyaraka za uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanyanyifu moja na shtaka moja la kutoa nyaraka kwa nia ya kumdanganya kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango. 

  Wanadaiwa kati ya Machi 15, 2013 na Januari 10, 2014 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kudanyanya washtakiwa wote walijipatia Dola za Kimarekani Milioni sita wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji wa upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.


  0 0

   Mtayarishaji wa Mashindano ya upigaji picha kutoka World Press, Sophie Boshouwers akizumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kabla ya kufunguliwa Maonesho ya Picha Duniani katika Ukumbi wa Aliance Francai's
  Mkuu wa Idara ya Mission katika Ubalozi wa Falme za Uholanzi nchini,Lianne Houben akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Maonesho kwa siku ya wapiga picha za Habari Duniani yanayofanyika leo Aliance Francai's
  Kaimu Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Hbari Wanawake(TAMWA),Davis Lumala akiongelea ushiriki wa TAMWA katika Maonesho hayo kabambe
  Mkurugenzi wa kituo cha Utamduni cha watu wa Ufaransa nchini Tanzania,Aliance Francais ,Frederic Tiberti akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kituo chake kujihusisha na Maonesho mbalimbali.
   Mtayarishaji wa Mashindano ya upigaji picha kutoka World Press, Sophie Boshouwers akitoa maelezo kwa moja ya waandishi wa Habariolder | 1 | .... | 1784 | 1785 | (Page 1786) | 1787 | 1788 | .... | 1897 | newer