Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1785 | 1786 | (Page 1787) | 1788 | 1789 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii 

  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenda gerezani kumuhoji mshtakiwa Alloyscious

  Mandago katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni mbili inayomkabili yeye na wenzake wanne.

  Katika kesi hiyo, mshtakiwa Mandago anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takriban Sh. Milioni saba kwa dakika, Mohamed Yusufali.

  Wakili wa Serikali kutoka Takukuru Leonard Swai Maombi hayo amewasilisha maombi leo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa. 

  Wakili Swai alidai, wapo hatua za mwisho za kukamilisha taarifa ili kuwasomea washtakiwa maelezo ya mashahidi(Commital). pia aliiomba mahakama kumuhoji mshtakiwa huyo akiwa gerezani.

  Mahakama imeridhia mshtakiwa huyo kuhojiwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 8, mwaka huu itakapikuja kwa ajili ya kutajwa. Mbali na Yusufali na Mandago washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni 

  Isaack Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif ambapo wanakabiliwa na mashtaka 39 likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni mbili.

  0 0

  WAKULIMA wa kijiji cha Kapunga kilichopo wilaya ya Mbarali mkoani mbeya wameiomba Serikali kuingilia kati kuwaondoa kwa nguvu wavamizi wa mashamba yao na maeneo ya kijiji chao kinyume cha sheria.

  Wamesemaa kuwa mashamba hayo ambayo wanayamiliki kiharali yamevamiwa na taasisi inayotambuliwa kama umoja wa wakristo Tanzania UWATA kinyume na taratibu na kusababisha uwepo mgogoro kati yao na wananchi wa kijiji cha kapunga.

  Akizungumza na Mwandishi wa habari hii jana wilayani humo kwaniaba ya wenzake mmoja wa wahanga wa mashamba hayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM tawi la Mapogolo Kapunga Sekelaga Sandube alisema kuna umuhimu wa serikali kuu kuingilia kati kwani serikali ya mkoa na wilaya pamoja na juhudi kadhaa kuchukuwa lakini imeshindikana wavamizi kuondoka.

  Amesema awali baada ya wavamizi hao kuingia walilipoti ofisi ya kijiji cha kapunga na baadae wilayani ambapo kote huko viongozi mbali na kushughulikia tatizo hilo lakini wameshindwa kuwaondoa wavamizi hao hali iliyosababisha wao kushindwa kuendelea na kilimo katika maeneo hao.

  "Ndugu Mwandishi mgogoro umechukua miaka zaidi ya 10 na tumehangaika katika ofisi zote za serikali kwa maana kijiji hadi mkoa na mbaya tumefika hadi kwa Waziri mwenye dhamana na ardhi na kutoa maagizo kwa maandishi ya kuelekeza kuondolewa kwa wavamizi hao mara moja lakini viongozi wa wilaya wameshindwa kutekeleza agizo hilo hadi sasa. "alisema Sandube

  Nakuongeza kuwa kutokana na viongozi kushindwa kutekeleza maagizo ya waziri na ofisi ya serikali ya mkoa ndio maana tunaiomba serikali kuu hususani mh Rais Dkt John Magufuli kumaliza mgogoro huo.

  Akizungumzia chanzo cha uvamizi wa maeneo hayo Sandube amesema kwa makusudi huku wakiwa wanajuwa wanachokifanya ni kinyume cha sheria ardhi ya vijiji sura 114 ya 2002 uongozi wa serikali ya kijiji cha Ukwavila uligawa maeneo ya kijiji cha kapunga na kusababisha migogoro inayoendelea hadi sasa.

  Naye Katibu wa umoja wa kilimo cha umwagiliaji Mpunga mmoja (SKIMU) Emmanuel Mwansanga Alisema mgogoro huo umewsatori kutokana na miundombinu kuharibiwa zikiwemo mbegu ambazo zilikuwa zimepandwa kwa ajili ya maandalizi ya kilimo cha msimu huu.

  " Jumla ya hekari 62 ambazo ni mali ya sisi kama wakulima na zaidi ya heri 600 ambazo ndani yake zilitakiwa zigawiwe kwa vijana wa kijiji. nazo zimevamiwa."Amesema Mwansanga

  Aliongeza kuwa hekari hizo 600 zilitengwa kutona na maagizo ya Rais Dkt Magufuli aliyoyatoa mwaka 2016 kupitia Waziri William Lukuvi nakwamba nazo zimevamiwa huku viongozi wakishndwa kusimamia maagizo yaliyotolewa.

  Kwaupande wake Mtendaji wa kijiji cha Kapunga Jackson Mbilinyi alikiri kuwepo kwa uvamizi huo na migogoro ya ardhi nakwamba wao kama viongozi walijaribu kushughulikia tatizo.

  Kwaupande wake Daimon Simwandiya ambaye anadaiwa ni mmoja wa wavamizi wa mashamba hayo akizungumza kwa njia ya simu alisema wao waliyapata maeneo hayo kihalali mwaka 2002 na wakapewa hati ya kimila 2013.

  Alipoulizwa kwanini Serikali ya kijjji cha Ukwavila ikawape mashamba kwenye kijiji cha Kapunga amesema wao ni watanzania wanahaki ya kulima popote hata Dar es Salaam wanaweza wakalima.

  Naye mkuu wa Wilaya ya Mbarali akizungumzia sakata hilo alisema hana taarifa mgogoro wa uvamizi na kama hao watu waende ofisni kwake.

  "Mimi sina taarifa hiii kwamba kuna mgogoro na anachofahamu yeye kwamba kulikuwa na mgogoro wa mpaka ambao mkuu wa mkoa wa mbeya alishaumaliza "amesema Mkuu huyo wa wilaya.
   
  Mwenyekiti wa CCM tawi la Mapogolo Kapunga Sekelaga Sandube 

  0 0

  Madaktari bingwa wa upasuaji wa kufungua kifua kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia upasuaji mtoto ambaye mishipa yake ya damu safi na damu chafu imekinzana kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Shirika la Healing Little Heart la nchini Uingereza wakati wa Camp maalum ya upasuaji wa kufungua kifua kwa watoto waliozaliwa na matatizo ya moyo leo katika Taasisi hiyo. Jumla ya watoto nane wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi hiyo na hali zao zinaendelea vizuri.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao alichokiitisha cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha Chai cha Mponde katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga kilichowajumuisha Naibu Mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF na Msajili wa Hazina. Kikao hicho kilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 24, 2019. (Picha ba Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo mafupi toka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mamlaka ya Maji safi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Lydia Ndibalema (wa pili toka kushoto) juu ya mradi wa visima vya Kimbiji na Mpera uliopo Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa Kimbiji na Mpera Mhandisi Shiyenze (wa nne toka nne) Bunyese mara baada ya kutembelea katika kisima cha K-17, K-11 na K-3 ambavyo vipo katika hatua ya mwisho ili wananchi waweze kupatiwa maji safi na salama.
  Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa wasimamizi pamoja na mkandarasi wanaosimamia miradi ya Mradi wa Kimbiji katika kisima cha K-17, K-11 na K-3 ambavyo vipo katika hatua ya mwisho ili wananchi waweze kupatiwa maji safi na salama.
  Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Pro. Makame Mbarawa akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizia ziara yake ya kutembelea mradi wa Kimbiji na Mpera katika kisima cha K-17, K-11 na K-3 ambavyo vipo katika hatua ya mwisho ili wananchi waweze kupatiwa maji safi na salama. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. Waziri wa Maji na Unwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amewataka wataalamu wanaokabidhiwa majukumu kufanya kazi kwa wakati na kukamilisha miradi ili huduma zifike kwa wananchi. Ameyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa Visima 20 vya Kimbiji na Mpera vyenye jumla ya thamani ya Bilioni 23.

   Akizungumza baada ya ziara hiyo, Prof Mbarawa amesema kuwa visima 12 vya Kimbiji tayari vimeshakamilika katika uchimbaji kilichobaki ni kupima wingi wa maji na ubora wake. (Pump test) Mbarawa amesema, kwenye visima hivyo viwili vipo tayari kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi ili wapate maji safi na salama. “ Kulikua na changamoto kidogo ya Mkandarasi ila kwa sasa kila kitu kipo sawa, anayesubiriwa ni Mshauri (Consultant) kwa ajili ya kuja kushauri kuhusu upimaji wa wingi wa maji na ubora ili tuendelee na mchakato wa huduma ya maji kwa wananchi,” amesema Mbarawa. 

  “Visima nane kati ya 20 vilivyopo Mpera vipo katika hatua ya Kati ya uchimbaji na nawashauri DAWASA kumaliza kwanza visima vya Kimbiji ili baadae wahamie hivyo vya Mpera, “amesema Mbarawa ameutaka uongozi wa DAWASA kuharakisha katika manunuzi na kumpata Mkandarasi ili kufikia mwishoni mwa Mei mwaka huu wananchi wa Kimbiji na Kigamboni waweze kupata maji. 

  Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mamlaka ya Maji safi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Lidya Ndibalema amesema mradi huu ulikuwa na thamani ya Bilioni 23 mpaka sasa wameshatumia bilioni 17 n kikubwa kwa visima vya Kimbiji ni Mshauri (Consultant) ni kuja kutoa maelekezo katika Pump Test.

   Ndibalema amesema tayari ujenzi wa tanki la Kibada upo katika hatua ya manunuzi na wamefuata maelekezo kama tuliyoagizwa na serikali na ikishakamilika tutaanza mchakato wa kuanza ujenzi. 

   Mradi wa Kimbiji na Mpera unazalisha maji takribani milioni 250 kwa siku ikiwa ni nusu ya maji yanayozalishwa kwa Mkoa mzima wa Dar es Salaam Lita Milioni 504, na mradi huo utawanufaisha wananchi wote kwa Ukanda wa Kusini mwa Dar es Salaam yakiwemo maeneo ya Kigamboni, Kibada, Mkuranga, Temeke, Mtoni Kijichi na maeneo mengine yasiyokuwa na mtandao wa maji wa DAWASA kwa ukanda huo.

  0 0


  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  amekutana na kufanya mazungumzo wa wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma na ameitaka ifanye kazi kwa weledi.Ameiagiza ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi, akitolea mfano kada za elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na kazi wanazozifanya.

  Amekutana na wajumbe wa bodi hiyo leo (Alhamisi,Januari 24, 2019) katika kikao kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuhakikisha mishara na maslahi ya watumishi wa umma nchini yanaboreshwa, hivyo ameiagiza bodi hiyo ifanye kazi kwa bidii.

  Amesema Serikali imeunda bodi hiyo ili kupata ushauri utakaotokana na tathmini sahihi ya nini Serikali inatakakiwa kufanya ili kuboresha utendaji wa watumishi wa umma nchini. Serikali inaimani kubwa na wajumbe wote wa bodi hiyo kutokana na uzoefu walionao kwenye  utumishi wa umma.

  “Tunataka muongozo mzuri wa kuwafanya watumishi wa umma wafanye kazi yao kwa waledi bila ya kuwa na vishawishi vya aina yoyote ikiwemo kuomba na kupokea rushwa.” Amesema Serikali inataka kila mtumishi wa umma anawajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi mambo ambayo yatakuwa yameimarishwa kutokana na upatikanaji wa maslahi mazuri.
   
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi  katika Utumishi wa Ummam, kwenye  Makazi ya Waziri Mkuu jiji Dar es salaam, Januari 24, 2019. Kutoka kushoto ni  Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula, Mjumbe wa Bodi, George Mlawa na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya  Mishahara na Maslahi  katika Utumishi  wa Umma, George Mlawa baada ya mazungumzo na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019. Wengine kutoka kushoto ni  Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  NA WAMJW-SHINYANGA

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa kiasi cha shilingi bilioni 2.5 zitakazotumika katika ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, lengo likiwa ni kutoa huduma za kibingwa kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea ujenzi wa Hospitali hiyo na kukuta jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na Utawala likiwa limekamilika.

  Waziri Ummy amesema fedha hizo zitafika katika Hospitali hiyo ndani ya wiki mbili ili ziweze kuchochea kasi ya ujenzi na lengo ifikapo mwezi Septemba 2019 Hospitali hiyo ianze kutoa huduma za afya.

  “Ninaahidi kutoa shilingi bilioni 2.5 ndani ya wiki mbili ziweze kutumika katika ujenzi wa jengo la mama na mtoto, lengo la serikali ni kuhakikisha kila mama mjamzito anapofika Hospitalini kujifungua atoke akiwa salama yeye na kichanga chake”. Amesema Waziri Ummy.

  Waziri Ummy amefikia uamuzi huo baada ya kupokea ripoti ya mkoa kuhusu vifo vitokanavyo na uzazi kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mfaume Rashid, ambapo kwa mwaka 2016/2017 kulikua na vifo 73, na mwaka 2017/2018 vikiwa ni vifo 56, hali ambayo Waziri huyo ameonekana kutoridhishwa nayo.

  Hata hivyo Waziri Ummy ameahidi kuongeza fedha zingine kiasi cha shilingi bilioni 3 ndani ya mwezi mmoja, zitakazotumika katika ujenzi wa jengo kwa ajili ya huduma za uchunguzi ikiwemo huduma za maabara, X-ray na CT-Scan pia jengo hilo litakua na vyumba vitatu vya upasuaji.

  Waziri Ummy amesisitiza ujenzi wa jengo hilo utumike wa mfumo wa Force Account ambao utahakikisha wananchi wanashiriki kwa asilimia 100 katika kufanikisha ujenzi huo na huduma za afya zianze kutolewa mapema.

  Wakati huo huo, Waziri Ummy ametembelea kituo cha afya cha Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga kuona hali ya miundombinu ya kituo hicho na utoaji wa huduma za afya huku kwa kiasi kikubwa akionekana kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa majengo ya huduma mbalimbali.

  Kuhusu uhaba wa watumishi wa kada za afya Waziri huyo ameahidi kutatua changamoto hiyo hali inayopelekea kuwepo kwa msongamano wa wagonjwa.

  Aidha, Waziri Ummy amehitimisha ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na kuridhishwa kwa kiasi kikubwa na hali ya utoaji wa huduma za afya hasa katika jengo la huduma za mama na mtoto na pia katika jengo la kuhifadhia watoto wachanga wenye uhitaji wa uangalizi maalumu (NICU).


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ambalo limekamilika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneka na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Albert Msosela.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akioneshwa ramani ya majengo ya kituo cha afya cha Kambarage na Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Lusajo Mwakajoko wakati alipotembelea kituo hicho leo kilichopo manispaa ya Shinyanga.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto mchanga aliyezaliwa katika kituo cha afya cha Kambarage mjini Shinyanga.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipanda mti wa kumbukumbu katika kituo cha afya cha Kambarage kilichopo katika manispaa ya Shinyanga.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiangalia kichanga kilicholazwa katika chumba maalum cha uangalizi wa watoto mahututi na wale waliozaliwa kabla ya siku (njiti) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni daktari bingwa wa watoto Dkt. Mwita Ngutunyi.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA)Bw. Charles Kiondo akizungumza na daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI Dr. Tatizo Waane kulia mara baada ya kumalizika mafunzo hayobyaliyofanyika leo kwa njia ya Video katikati ni Dr. Delillah Kimambo kutoka JKCI na Dr Kilalo Mjema kutoka Hospitali ya Agha Khan na kushoto ni Katibu Mkuu Mstaafu wa Utumishi Joseph Rugiyamheto.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA)Bw. Charles Kiondo akisikiliza mjadala wakati wa mafunzo kwa njia ya mtandao yaliyoendeshwa kwa pamoja na Hospitali Continental ya India pamoja na wakala hiyo yaliyofanyika jijini Dar es salaam yakishirikisha wataalam na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na taasisi zingine kulia ni Balozi Ulisubisya Mpoki na katikati ni Katibu Mkuu Mstaafu Utumishi Joseph Rugiyamheto.

  ...................................................................................................

  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) imeendesha mafunzo ya uzibuaji valvu ya Moyo kwa njia Video na Hospitali ya Continental ya nchini India ili kubadilishana uzoefu na wataalam wa nchini.

  Akizungumza katika mafunzo ya uzibuaji wa Valvu ya Moyo Mkurugenzi Mkuu wa wakala hiyo Charles Senkondo amesema kuwa katika mkutano huo watalaam wamepata uzoefu kutoka kwa Mkuu wa Cath Lab ya Hospitali ya Continental ya nchini India Profesa Bharath Purohit. Senkondo amesema kuwa tangu kuanza kwa mkutano kwa njia ya Mtandao kada mbalimbali zimepata mafunzo katika Mada zinazoandaliwa na taasisi hiyzo kwa kushirikiana na wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao TaGLA. Amesema wakala hiyo ndio inaongoza kwa nji za Afrika katika uendeshaji wa mafunzo.

  Aidha amesema kuwa eneo hilo la uzibuaji valvu ya Moyo umekuwa na mwitikio mkubwa kwa upande wa madaktari wetu katika kupata uzoefu wa Hospitali ya Continental ya nchini India. Daktari Bingwa wa Moyo Dkt.Tatizo Waene amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu katika Sekta ya Afya kwa watalaam kupata ujuzi zaidi kutoka kwa wabobezi wa masuala ya magonjwa ya moyo na pia mafunzo hayo yanapunguza hata gharama za matibabu kwakuwa wataalamu wengi wanapopata mafunzo wanapata uzoefu na kufanya kazi nzuri ya kutibu wagonjwa HAYO hapahapa nyumbani.

  Dr. Tatizo Waane ameongeza kuwa kuna kila sababu ya kuwa na mipango mahsusi kati ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Walala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) ili kufanya uchambuzi ulio makini na wenye tija wakati wa kuwapata washiriki wa mafunzo hayo ili kupata uwiano wa kada zote jambo ambalo litawezesha wataalam hao kupata weledi wa namna ya kukabili magonjwa ya moyo kwa uwiano mzuri
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) na Katibu Mkuu Mstaafu Utumishi Joseph Rugiyamheto wakimsikiliza Dr. Bharath Purohit kutoka Hospitali ya Continental ya india wakati akitoa mafunzo ya uzibuaji wa valvu ya moyo kwa njia ya video leo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu Mstaafu Utumishi Joseph Rugiyamheto akichangia jambo wakati wa mafunzo kwa njia ya video huku Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) akifuatilia mjadala huo.
  Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya washiriki wakifuatilia mjadala huo ulifanyika kwa njia ya video.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeiondoa timu ya Ismailia nchini Misri kutokana na mashabiki wake kuwafanyia vurugu timu ya Club African Ya Tunisia.

  Maamuzi hayo yamekuwa baada ya CAF kupokea ripoti ya mchezo namba 96 kati ya Ismailia na Club African uliochezwa Januari 18 mwaka huu nchini Misri ikielezea vurugu zilizotokea kwenye mchezo huo.

  Ripoti hiyo imeeleza kuwa mashabiki wa timu ya Ismilia walianza kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi wa mchezo huo pamoja na timu ya Club African hususani katika dakika ya 86 ya mechi hiyo.

  Baada ya kushindwa kuendelea na mchezo huo kutokana na vurugu za mashabiki wa Ismailia, mwamuzi aliamua kusimamisha mchezo huo na kuzitaka timu zote kuingia vyumbani na walipelekwa wakisindikizwa na walinzi.

  Katika kanuni ya 12, kifungu cha 3 kinaeleza kuwa kama mwamuzi atalazimika kusimamisha mchezo au kuumaliza basi timu iliyohusika na vurugu itahesabiwa imepoteza mechi au ikiwemo na kuondolewa kwenye michuano.

  Baada ya kamati kukutana na kuipitia ripoti ya kamisaa wa mchezo huo, wamefikia maamuzi ya kuiondoa timu hiyo katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na kufuta matokeo yote kwa zile timu ambazo walishacheza nazo.

  Ismailia ilikua katika kundi C wakiwa sambamba na Timu ya Tp Mazembe, Club African na Cs Constatinios na kwa sasa zinasalia timu tatu.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia vazi la kiraia) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Songwe leo Januari 24, 2019 tayarri kwa ziara ya kikazi katika baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwemo Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi na Ruvuma.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(vazi la kiraia) akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya mapema alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Songwe leo Januari 24, 2019 kwa ziara ya kikazi katika baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kusini.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati vazi la kiraia) akiteta jambo na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo mara baada ya kuwasili jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mbeya, SACP. Luhende Makwaia(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya awali ya Uaskari Magereza – Kiwira, ACP. Mathias Mkama(wa pili toka kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mbeya, ACP. Lyzek Mwaseba 
  . Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Chocha Peter(kushoto) alipokutananaye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Songwe leo Januari 24, 2019.

  0 0


  Mkurugenzi kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Bw. Sailesh Pandit
  Meneja Uendeshaji wa kiwanda cha Sunflag Bw. Magessa Charles(kulia), akifafanua jambo kuhusu utengenezaji wa nguo
  Wafanyakazi wa kiwanda cha A -Z wakiwa kazini
  Meneja Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, anayeshughulikia miradi, Mhandisi Emmanuel G. Munirabona(kulia), akizungumza na Mkurugenzi kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Bw. Sailesh Pandit.Picha zote nz Vero Ignatus
  Na.Vero Ignatus, Arusha

  Shirika la umeme nchini Tanzania TANESCO limepongezwa kwa kuimarisha huduma zake kwa wateja wa wakubwa na wale wa kati jijini Arusha
  Akizungumza Mkurugenzi kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Bw. Sailesh Pandit amesema huduma za TANESCO zimeimarika kiasi kwamba ameshawishika kufungua viwanda vingine vitatu Jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga

  “Zamani tulikuwa na shida sana miaka miwili mitatu iliyopita, power cut (kukatika kwa umeme), sasa hivi hamna ni mara chache sasa labda ikitokea kwenye gridi ya taifa hapo hatuna ha kufanya, lakini sasa hivi hatuna tatizo la umeme kabisa.” Alisema Bw. Sailesh ambaye kwa mwezi anailipa TANESCO kiasi cha kati ya shilingi milioni 500 hadi 600 kama bili ya umeme.

  Akizungumzia ushirikiano wa kikazi kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO na kiwanda chake, Bw. Sailesh amesema, hakuwahi kuuona ushirikiano huo miaka ya nyuma ila ndio ameanza kuona hivi sasa ambapo inawatia moyo wao kama wawekezaji na kuona wanaifikia Tanzania ya viwanda

  “Kwakweli sina cha kusema au kibaya chochote, namna ninavyofanya kazi nao ni very friend manner, mimi ninaweza kumpigia simu Injinia hata saa nane usiku, sina umeme ata respond simu yako hapo hapo na kuchukua hatua wakati kipindi cha nyuma haikuwa hiovyo.” Hali kadhalika uongozi wa kiwanda cha nguo Sunflag, nao umetoa pongezi kwa TANESCO kwa kusema kuwa huduma zimeboreka na kwamba kuna matatizo madogomadogo tu.

  “Nina kila sababu ya kuwashukuru TANESCO kipindi cha nyuma kila mtu ni shahidi tulikuwa na matatizo kwenye eneo hili la upatikanaji wa umeme lakini pia ushirikiano haukuwa mzuri sana, lakini kwa sasa, panapotokea tatizo response ya TANESCO panapotokea tatizo ni ni very fast na very incouraging mtu atakayewanyooshea kidole itakuwa ni sababu zake mwenyewe.”

  Alipongeza pia mfumo wa utoaji taarifa, ambapo hata kama kuna katizo la umeme wamekuwa wakipata taarifa mapema na wao kama kiwanda hujipanga na hivyo kuondoa usumbufu.Aidha uongozi wa kiwanda cha A to Z pamoja na kuponegza kuimarika kwa upatikanaji wa umeme, wao bado kuna wakati umeme unapungua nguvu (fluctuation) na hivyo kusababisha mitambo yao kusimama kufanya kazi

  “Lakini kwa ujumla kumekuwa na maendeleo mazuri ya hali ya umeme ukilinganisha na kipindi cha nyuma, wito wetu ni kufanyia kazi mapungufu hayo,” Alisema Afisa Mterndaji Mkuu wa A to Z, Bw.Viral Shah.

  Akizungumzia mapungufu hayo, Meneja Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, anayeshughulikia miradi, Mhandisi Emmanuel G. Munirabona, alisema wao kama shirika watafuatilia kwa kina kujua hasa nini chanzo cha tatizo hilo.

  “Tumefanya maboresho makubwa ya mitambo yetu ikiwa ni pamoja na kupanua vituo sita vya kupoza umeme jijini Arusha, ambavyo vimewezesha wateja wakubwa kufunguwa laini zinazojitegemea ili kuondoa uwezekano wa kukatika kwa umeme na hivyo kuathiri shughuli za uendeshaji

  Jiji la Arusha ni miongoni mwa miji mitatu ambayo ilikuwa kwenye mpango wa kukarabati na kuimarisha miundombinuya umeme (TEDAP), ambapo Shirika hilo lilifanya ukarabati mkubwa wa njia za kusafirisha umeme lakini pia kufanya upanuzi wa vituo vya kupoza umeme.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro  ameendelea kuungwa mkono na wadau wa Maendeleo Kwa kukabidhiwa awamu ya kwanza ya Mifuko 100 ya Saruji kutoka katika Kampuni ya Farm Acces Ltd kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi 100 Arumeru.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa saruji hiyo Ndugu Muro mbali na kushukuru Kwa msaada huo , amepongeza jitihada zinazofanywa na  kampuni hiyo ambayo bado haijaanza uzalisha wa Dawa za mifugo lakini wameweza kuchangia mifuko 100 Kwa awamu ya kwanza na kuwataka wadau wengine kuunga mkono juhudi Za ujenzi wa vyumba vya madarasa .

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Dkt. Saimoni amepongeza juhudi zinazofanywa  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru chini ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli na kusisitiza kutoa msaada zaidi pindi watakapoanza uzalishaji kiwandani hapo.

  Wadau hao wa maendeleo Waliahidi kuchangia mifuko 200 ya Saruji na kwa Awamu ya kwanza wamemkabidhi Dc Muro mifuko 100 ya saruji na kuahaidi ndani ya muda mfupi watamkabidhi tena Mkuu wa Wilaya mifuko 100 mingine iliyobakia.

  Dc Muro anaendelea na ziara yake ya kuhamasisha, na kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule mbalimbali Za sekondari katika Wilaya ya Arumeru Kwa lengo la kumaliza changamoto ya madarasa kuanzia shule Za msingi, sekondari na kidato Cha tano na sita .
   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro  ameendelea kuungwa mkono na wadau wa Maendeleo Kwa kukabidhiwa awamu ya kwanza ya Mifuko 100 ya Saruji kutoka katika Kampuni ya Farm Acces Ltd kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi 100 Arumeru.

  0 0
  0 0
 • 01/24/19--20:50: OHOOOO...! AJALI KAZINI
 • Mmoja wa waendesha pikipiki wa kata Bupu Wilaya ya Mkuranga mkoa wa  Pwani akiwa amepakia mzigo wa mkaa katika pikipiki  huku akiwa hajavaa  kofia ngumu pamoja na viatu  jambo ambalo ni hatalisha  kwa usalama wake kama anavyo onekana pichani (Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
   Ajali kazini.
  wasamalia wema wakafika na kumsaidia kunyanyua pikipiki yake  pamoja na Mizigo aliyokuwa amebeba.

  0 0

  Timu ya kitaifa ya kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji imefanya ziara wilayani Mkuranga ,lengo ikiwa ni kutatua migogoro ya aina zote  za ardhi na kuiainisha.

  Akizungumza wakati wa ziara wilayani Mkuranga mkoa wa pwani,kiongozi wa timu ya serikali ya ufuatiliaji wa migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi Dkt.Martin Ruheta amesema timu hiyo sio ya kisiasa bali ni ya kitendaji na matarajio yao mpaka ifikapo 2020 itakuwa imepatiwa suluhu kama sio kwisha kabisa.

  Aidha Dkt.Ruheta amewaahidi wanachi hao kuwa watahakikisha migogoro yao inapatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa sababu tume yao ipo makini.

  Kwa upande wake katibu wa mbunge wa jimbo la Mkuranga Omary kisatu amewaomba wanachi hao kuwa na imani na tume hiyo."wakulima na wafugaji naomba muendelee kudumisha amani na utulivu iliyopo,tume hii ni ya kitaifa ya kuhakikisha haki ya mkulima na mfugaji inapatikana ."alisema Kisatu

  Hata hivyo tume hiyo inaundwa na watu mbalimbali akiwemo Ofisa kutoka ofisi ya Rais,Wizara ya Ardhi,Wizara ya mambo ya ndani ya nchi,Ofisa wa ardhi na wa maliasili,lengo kuu ni kuhakikisha migogoro  ya ardhi inakwisha nchini
   Kiongozi wa Timu ya Serikali ya ufuatiliaji na Utatuzi wa Migogoro na watumiaji wengine wa Ardhi Dkt.Martin Ruheta akizungumza na wakulima pamoja na wafugjia wa kata ya Bupu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
  Kiongozi wa timu ya Serikali  ya ufuatiliaji,Utatuzi  wa Migogoro ya watumiaji wa Ardhi, Dkt.Martin Ruhete(kushoto) akiteta jambo na  Katibu wa Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Omary Kisatu.
  Katibu Mkuu wa  Chama cha wafugaji Tanzania, Magembe  Makoye akiwasihi wafugaji wa kijiji cha Matanzi kata ya Beta wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, kutulia na kusubiri taratibu za serikali.

  0 0

  Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Kitila Mkumbo kuitisha haraka Mkutano kwa Wadau wote wanaohusika na Mradi wa Maji Chalinze Jumanne ya Januari 29, mkutano utakaojadili changamoto za upatikanaji Maji katika Halmashauri hiyo.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutembelea Mradi huo katika eneo la Chalinze, Mhe. Aweso amesema mpaka sasa mradi huo umefika asilimia 78 na Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 95 kuhakikisha Wananchi wa Chalinze wanapata Maji ya kutosha. 

  Katika ziara yake hiyo, Mhe. Aweso amesema ameona changamoto katika uendeshaji wa mradi huo ikiwemo vituo vya Maji zaidi ya 200 lakini 86 ndio vinafanya kazi ya utoaji huduma ya Maji pamoja na changamoto ya uendeshaji ikiwa sambamba nakuwapa Watoto wadogo kusimamia vituo hiyo. 

  Mhe. Aweso amewata Watendaji wa Wizara hiyo kuhakikisha wanatafuta Wakandarasi wenye weledi na kazi zao ili kuhakikisha miradi hiyo inasimamiwa ipasavyo bila kusuasua licha ya mradi huo kufika asilimia 78. 

  "Mkandarasi anayesimamia mradi huu ni changomoto, hatuwezi kumuachia mpaka amalize mradi huu, tayari amechukua fedha zaidi ya asilimia 62 kwenye Bilioni 95", amesema Aweso

  Kwa upande wake, Msimamizi wa Mradi wa Maji, Chalinze - DAWASA, Mhandisi Modesta Mushi amesema kuwa mradi huo umefika jumla ya asilimia 78 pamoja na ujenzi wa Miundombinu eneo la mtambo, ujenzi wa matenki kufikisha Maji maeneo tofauti na ujenzi wa vitekeo Maji (Viosk) jumla ya 351 maeneo mbalimbali katika eneo la mradi.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainabu Kawawa ameshukuru kuona ziara ya Naibu Waziri wilayani humo, amesema wataendelea kusimamia kuhakikisha Mkandarasi wa Mradi wa Maji, Chalinze anamaliza mradi huo kwa wakati licha kuahidi kumaliza Desemba 31, 2018, amesema wanahitaji kuona usimamizi mzuri katika Vitekeo Maji vilivyopo ili kutoa fursa kwa Wananchi wa Chalinze kupata huduma hiyo ya Maji Safi na Salama. 

  Utekelezaji wa Mradi huo wa Chalinze, awamu ya tatu unatekelezwa na Mkandarasi Overseas Infrastructure Alliance (India) Private Limited pamoja na Kampuni ya Platiba kwa gharama ya Dollars za Kimarekani Milioni 41.1 ambao ni Mkopo wa gharama nafuu kutoka Serikali ya India.
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akisaidia uchimbaji moja ya Mfereji utakaotumika kutandika mabomba katika eneo la mradi wa Maji, Chalinze.
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja na Msimamizi wa Mradi wa Maji, Chalinze, Mhandisi Modesta Mushi katika eneo la mradi huo. 
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) (aliyevaa Kofia) akishuka chini pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainabu Kawawa (aliyevaa Koti) baada yakukagua moja ya Tenki lililopo kwenye Mradi wa Maji, Chalinze mkoani Pwani. 
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja.
  Moja ya Tenki lililopo kwenye utekelezaji wa mradi wa Maji, Chalinze.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Congo imeandika historia mpya kwa kukabidhiana madaraka kwa upendo na ana imani Viongozi wataendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo na maslahi mapana ya nchi yao.

  Makamu wa Rais ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameyasema hayo mara baada ya sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Tshisekedi.

  “Linalofurahisha ni kwamba ni mara ya kwanza kwa nchi hii ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanya uchaguzi wa kidemokrasia na kukabidhiana madaraka kwa usalama kabisa” alisema Makamu wa Rais.

  Uchaguzi huo uliofanyika Desemba 30, 2018, Mhe. Felix Tshisekedi alipata takribani kura milioni 7 sawa na asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa ambapo wagombea wenzake kama Martin Fayulu alipata ailimia 34 sawa na kura milioni 6.4, Bw. Emmanuel Ramazani Shadary alipata asilimia 23 sawa na takribani kura milioni 4.4. 

  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeandika historia kwa mara ya kwanza tangu ilipopata uhuru kwa kukabidhiana madaraka kwa njia ya Amani.
  Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Tshisekedi.
  Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Tshisekedi akiteta jambo na Rais wa zamani wa nchi hiyo Mh.Joseph Kabila.

  0 0

  *Ni kauli ya wateja wakubwa mkoani Arusha wanaomiliki viwanda vikubwa
  *Wakiri kuimarika kwa umeme imekuwa chachu kwao kuongeza uzalishaji
  Na Said Mwishehe,Arusha

  HATUNA tena za umeme katika Mkoa wa Arusha!Hivyo nidvyo ambavyo wamiliki wa viwanda ambavyo vinazalisha bidhaa mbalimbali mkoani Arusha wanavyoeleza baada ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), kuboresha upatikanaji wa umeme.

  Wakizungumza mbele ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambao wamepata nafasi ya kutembelea viwanda vilivyopo mkoani Arusha jana na kupata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wamiliki wa viwanda hivyo wamekiri kwa sasa hali ya umeme inaridhisha kwai huko nyuma hali ilikuwa mbaya na ilisababisha hata uzalishaji wa bidhaa kutofanyika kwa kiwango ambacho walikuwa wanakitarajia.

  Wamiliki hao wamesisitiza kuwa kuimarika kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika wameongeza uzalishaji huku wengine wakifafanua wameamua kuanzisha na viwanda vingine kwani hivi sasa Serikali kupitia TANESCO imefanya kuwe na uhakika wa kufanya uwekezaji kwani kama hakuna umeme basi hakuna uwekezaji hasa wa viwanda.


  Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Lodhia Steel Industries, Sailesh Pandit amesema kiwanda chao kinatumia umeme wa megawati saba ambapo kwa mwezi wanailipa TANESCO kati ya Sh.milioni 500 hadi 600 kwa mwezi kutokana na uzalishaji wake.

  Amefafanua zamani kulikuwa na shida sana yaumeme lakini sana miaka miwili mitatu iliyopita maana umeme ulikuwa unatakatika mara kwa mara lakini sasa hali ni tofauti na hivyo lazima tuwapongeze Serikali na TANESCO kwa juhudi zao za kuboresha umeme.

  ”Ni kweli huko nyuma kulikuwa na shida ya umeme na sote ni mashahidi lakini leo hii hatuna tatizo la umeme tena.Kama tulipaza sauti kulalamika na hivyo hivyo tupaze sauti zetu kupongeza,”amesema Pandit.

  Kuhusu ushirikiano wa kikazi kutoka kwa wafanyakazi wa Tanesco na kiwanda chake, amesema wanashirikiana vema na muda wote linapotokea Tanesco hata ikiwa usiku wa manane hupatiwa ufumbuzi wa haraka na kwa muda mfupi.
  “Kwakweli sina cha kusema au kibaya chochote, namna ninavyofanya kazi nao ni very friend manner, mimi ninaweza kumpigia simu Injinia hata saa nane usiku, sina umeme ata respond simu yako hapo hapo na kuchukua hatua wakati kipindi cha nyuma haikuwa hiovyo.

  Kwa upande wake Meneja Utawala na Rasilimali Watu wa Kiwanda cha nguo cha Sunflag, Magesa Charles, amesema kwa sasa huduma za umeme zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa licha ya kuwepo matatizo madogo ambayo hayathiri shughuli za uzalishaji kama ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.

  Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha A to Z, Viral Shah, amefafanua hakuna tatizo la kukatika kwa kama huko nyuma ila kuna wakati umeme unapungua nguvu.

  “Kwa ujumla kumekuwa na maendeleo mazuri ya hali ya umeme ukilinganisha na kipindi cha nyuma, mwito wetu ni kufanyia kazi mapungufu hayo.Hapa kwetu tunatumia megawati 9 hadi 10 kwa mwezi na tunalipa bili zetu Tanesco Sh.bilioni 1.1 kwa kila mwezi na hapa tuna viwanda tisa,” amesema Shah.

  Akizungumzia hali hiyo, Meneja Mwandamizi wa Miradi wa Tanesco, Mhandisi Emmanuel Munirabona, ameeleza kama shirika watafuatilia kwa kina kujua hasa nini chanzo cha tatizo hilo la kupungua kwa umeme katika kiwanda hicho.
  “Tumefanya maboresho makubwa ya mitambo yetu ikiwa ni pamoja na kupanua vituo sita vya kupoza umeme jijini Arusha, ambavyo vimewezesha wateja wakubwa kufunguwa laini zinazojitegemea ili kuondoa uwezekano wa kukatika kwa umeme na hivyo kuathiri shughuli za uendeshaji.

  “ TANESCO tumeamua kuhakikisha tunatafuta ufumbuzi wa changamoto zote kama zipo , lengo letu ni kuhakikisha Tanzania ya viwanda inatekelezwa kwa vitendo na hii itatokana na uwepo wa umeme wa uhakika.

  “Ndio maana tumeendelea kuboresha huduma zetu na lengo lake ni kuona hatuna matatizo ya umeme na tayari tumefanikiwa , hivyo tuendelee kutoa rai wawekezaji waje tu nchini kwetu kuwekeza kwani tunao umeme wa kutosha,”amesema.
   Meneja Rasilimali Watu wa Kiwanda cha Sun Flag kilichopo mkoani Arusha akitoa ufafanuzi  kuhusu bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo
   Mfanyakazi wa kiwanda cha TANELEC ambacho kinatengeneza trasfoma akiendelea na majukumu yake katika kiwanda hicho kilichopo Themi mkoani Arusha
   Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TANELEC wakiendelea na kazi ya kusuka transfoma
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha A to Z  Viral Shah akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea kiwandani hapo kuona shughuli za uzalishaji
   Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha A to Z mkoani Arusha akiendelea na kazi kiwandani hapo
   Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha A to Z wakiendelea na majukumu yao wakati wa hariri wa vyombo vya habari nchini pamoja na maofisa wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) walipofanya ziara kiwandani hapo kuona shughuli za uzalishaji pamoja na hali ya upatikaji umeme kwa sasa
   Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha TANELEC mkoani Arusha Zahir Saleh akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari(hawapo pichani) baada ya kutembelea kiwanda hicho ambacho kinatengeneza matransfoma ya umeme nchini
  Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha TANELEC Zahir Saleh akiwaongoza wahariri na maofisa wa TANESCO kuelekea ndani ya kiwanda hicho ambacho kinatengeneza matransfoma ya umeme.Kiwanda hicho ni moja ya wateja wakubwa wa utumiaji umeme mkoani Arusha

older | 1 | .... | 1785 | 1786 | (Page 1787) | 1788 | 1789 | .... | 1898 | newer