Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

SEKTA YA AFYA YAENDELEA KUPAA - SERIKALI

$
0
0
Na WAMJW - DOM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Sekta ya Afya nchini yaendelea kukua kwa kasi, kutokana na Serikali kuendelea kuboresha Huduma kwa Wananchi zikiwemo upatikanaji wa Dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi, huduma za chanjo, huduma za afya ya uzazi na mtoto na Huduma za Dharura.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akitoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari na baadhi ya viongozi wa Wizara, kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa Katika mwaka 2018, jumla ya wajawazito 2,086, 930 walihudhuria na kuandikishwa Kliniki, ikilinganishwa na wajawazito 2,009,879 Mwaka 2017, huku mwongozo wa utoaji huduma za afya ya uzazi na mtoto unaelekeza wajawazito kuanza huduma mapema kabla ya majuma 12 ya ujauzito na kuhudhuria kliniki angalau mara nne katika kipindi cha ujauzito.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa, Katika kipindi cha mwaka 2018 jumla ya watoto 1,568,832 walizaliwa ikilinganishwa na Watoto 1,498,488 mwaka 2017, huku wakipatiwa huduma mbalimbali za chanjo ili kuzuia magonjwa yanayowaathiri Watoto ikiwemo ugonjwa Kupooza, Kuharisha, Pepopunda, Pneumonia, homa ya ini na Surua.

"Katika kipindi cha mwaka 2018 hali ya chanjo kwa Watoto nchini imeendelea kuwa katika kiwango cha juu zaidi ya asilimia 85 ya kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani kama inavyoonyeshaa katik hapa chini" Alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo nWaziri Ummy amesema mwaka 2018 kumetokea jumla ya vifo 20,087 ikilinganishwa na vifo 19,693 mwaka 2017, huku Katika kipindi cha miaka yote miwili 2017 na 2018, homa ya mapafu imeongoza kwa kusababisha vifo, ambapo kwa mwaka 2017, imechangia asilimia 18.2 ya vifo vyote na mwaka 2018 imechangia kwa asilimia 12.9 ya vifo vyote. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Mwaka 2018, ugonjwa usio wa kuambukiza (shinikizo la damu) umejitokeza katika magonjwa 10 yanayoongoza kwa kusababisha vifo ambapo umechangia vifo kwa asilimia 1.9 ya vifo vyote. 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa Hali ya upatikanaji wa Dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini imeendelea kuimarika, hii ni kutokana na Serikali kuongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi Milioni 31 mwaka 2015/16 hadi kufikia Shilingi milioni 251 mwaka 2016/17 na Shilingi 270 mwaka 2018/19.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa hali ya upatikanaji wa Damu Salama ambapo katika kipindi cha mwaka 2018, huku jumla ya chupa za damu salama 307,835 sawa na asilimia 85.5 ya lengo zilikusanywa ikilinganishwa na chupa 233,933 mwaka 2017, huku akiwahasa Wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuendelea kuokoa maisha ya wahitaji.

"Chupa zote 307,835 zilizokusanywa zilipimwa makundi ya damu pamoja na magonjwa makuu manne ambayo ni Ukimwi (HIV,) Homa ya Ini B na C (HBV, HCV) na Kaswende (Syphilis). Jumla ya chupa 262,283 sawa na asilimia 85.3 zilikuwa salama na kusambazwa katika hospitali kwa ajili ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu." Alisema Waziri Ummy. 

Hata hivyo Waziri Ummy amesema kuwa, katika mwaka 2018 jumla watu 47,967 waligundulika kuwa na vijidudu vya Kifua kikuu ikilinganishwa na wagonjwa 44,714 waliogunduliwa mwaka 2017., huku akisisitiza kuwa tatizo la ugonjwa wa Kifua Kikuu limeendelea kuwepo takribani mikoa yote nchini.

kwa upande mwingine, Waziri Ummya amesema kuwa, hadi kufikia Desemba 2018, jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya vilifikia 7,768 kutoka vituo 7,435 mwaka 2017 sawa na ongezeko la vituo 333 kwa mwaka, amedai kuwa Serikali ilikuwa inamiliki asilimia 71 ya vituo vya kutolea huduma; Mashirika ya dini asilimia 12, Taasisi za Serikali asilimia 3 na vituo binafisi asilimia 15.

Sambamba na hilo, waziri Ummy amesema kuwa, hadi kufikia Desemba mwaka 2018, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulikuwa na jumla ya wanachama 899,654 na ikihudumia jumla ya wanufaika 4,219,192 sawa na asilimia 8 ya Watanzania wote.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakar Kambi.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakifuatilia tamko kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018 kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.

MOROGORO WATAKIWA WASIFICHE WAGONJWA WA UKOMA MAJUMBANI

$
0
0
Na WAMJW,Morogoro

Wananchi wa Mkoa wa Morogoro na halmashauri zake wametakiwa kutowaficha wagonjwa wenye ukoma majumbani ili ugonjwa huo uweze kutokomezwa hadi ifikapo mwaka 2020.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari wakati wa ufunguzi wa semina ya uhamasishaji wa uongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya mvomero kuhusu maadhimisho ya miaka sitini (60) ya Ushirikiano kati ya serikali na Shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania(GLRA) pamoja na siku ya ukoma Duniani itakayofanyika Kitaifa wilayani Mvomero mwishoni mwa mwezi huu.

“Serikali inawajali sana wananchi wake hivyo wananchi hampaswi kuwaficha wagonjwa majumbani kwani dawa na vipimo zinatolewa bila malipo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini” Alisema Tandari
Aidha, alisema kuwa mkoa wake utaendelea kufanya kila liwezekanalo ili kutokomeza ugonjwa wa ukoma mkoani hapa kwani wajibu wao ni kuwasaidia watu hao kupona na kurudi kwenye kazi zao za kila siku watu wagonjwa hao wakishapatiwa dawa wanapona kabisa.

Kwa upande wa ongezeko la wagonjwa wilayani Mvomero Katibu Tawala huyo alisema sababu kubwa ya kuongezeka kwa wagonjwa hao wilayani hapo ni muingiliano hususan kwenye mashamba hivyo inakua rahisi maambukizi kuwa juu”tutafanya jitihada ili kuweza kufikia viwango vya Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kutokomeza ugonjwa huu ambapo malengo ni mgonjwa mmoja kati ya watu elfu kumi.

Naye Mratibu wa Taifa wa ugonjwa wa Ukoma kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Deus Kamara alisema kuwa zipo halmashauri 20 ambazo hazijafikia kiwango cha kutokomeza ukoma nchini hivyo wizara kupitia mpango wa Taifa wa kutokomeza Kifua kikuu na Ukoma, Mikoa inatakiwa kutengeneza mkakati wa kuwasaka,kuwafikia, kuwaibua na kuwaweka katika matibabu stahili pamoja na kuzifikia kaya zote zenye wagonjwa wa ukoma kwa kufanyiwa uchunguzi ili wale ambao hawajaugua kuwapatia tiba kinga ili kutokomeza ukoma katika halmashauri zote ifikapo mwaka 2020.

Wakati huo huo Mwakilishii Mkazi wa Shirika la GLRA Buchard Rwamtoga alisema kuwa shirika hilo mwaka huu linatimiza miaka sitini(60) hapa nchini katika kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutokomeza ugonjwa wa ukoma Tanzania ikiwemo ya kuwajengea makazi bora familia 120 kutoka familia 739 ya watu waliougua ukoma hapa nchini.

“Dhamira yetu ni kuhakikisha kwamba kupitia michango ya wadau mbalimbali,shirika linaweza kusaidia mashirika na taasisi nyingine hasa mpango wa taifa wa kudhitibi ugonjwa wa kifua kikuu na Ukoma kupunguza madhara yatokanayo na magonjwa haya”alisisitiza Rwamtoga.

Alitaja mafanikio waliyoyapata kwa miaka 60 Mwakilishi Mkazi huyo alisema shirika lake wameweza kutoa viatu maalum kwa walioathirika na ukoma pea 94,500 kwa watu 47, 250, miguu bandia magongo na baiskeli kwa watu 2, 655, magari 270 kwa Tanzania bara na Zanzibar,kusaidia masuala ya elimu kwa wanafunzi 3,765 pamoja na kuwezesha vikundi vya kusaidiana vipatavyo 50 vyenye wanachama 677 kwa familia za watu wenye kuishi na ugonjwa wa Ukoma nchini.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya ukoma mwaka huu ni “Tutokomeze ubaguzi ,Unyanyapaa na chuki dhidi ya waathirika wa Ukoma” na kitaifa yatafanyika kwenye kitongoji cha Chazi kijiji cha kigugu Wilayani Mvomero tarhe 27 mwezi huu.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw.Clifford Tandari akifungua semina ya Uhamasishaji kwa viongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya serikali  na shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania (GLRA).Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
 Baadhi ya wakuu wa idara kutoka mkoa na wilaya wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa(hayupo pichani)ambapo wametakiwa kuhamasisha utekelezaji wa kuwaibua wagonjwa wa ukoma kutoka kila kaya ili kufanikisha malengo ya kutokomeza ugonjwa wa Ukoma ifikapo mwaka 2020
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw.Clifford Tandari akifungua semina ya Uhamasishaji kwa viongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya serikali  na shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania (GLRA).Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mohamed Utay na kushoto ni Mganga Wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Frank Jacob
Picha ya pamoja ya viongozi wa mkoa,wilaya,Wizara ya afya na GLRA mara baada ya ufunguzi

MADINI KUFANYA MAZUNGUMZO BARABARA MGODI WA MAKAA, NGAKA

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akiongozwa na Meneja wa mgodi wa Makaa ya Mawe TANCOAL, David Kamenya (aliyenyoosha mikono) kutembelea maeneo ambapo uchimbaji wa makaa hayo unafanywa katika machibo yaliyopo Wilayni Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akiongozwa na Meneja wa mgodi wa Makaa ya Mawe TANCOAL, David Kamenya (aliyenyoosha mikono) kutembelea maeneo ambapo uchimbaji wa makaa hayo unafanywa katika machibo yaliyopo Wilayni Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akieleza jambo baada ya kutembelea eneo ambalo shughuli za upakiaji makaa ya mawe zinafanywa na mgodi wa TANCOAL kwa ajili ya makaa hayo kusafirishwa maenezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Makaa ya Mawe wa TANCOAL 
Baadhi ya magari yakisubiri kupakia makaa ya mawe tayari kwa usafirishwa maeneo mbalimbali ndani nan je ya nchi,
Sughuli za upakiaji Mkaa ya Mawe zikiendelea katika Mgodi wa TANCOALtayari kwa ajili ya kusafirishwa maeneo mbalimbali.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Makaa ya Mawe wa TANCOAL. Wengine ni baadhi ya Wataala kutoka ofisi ya Madini Songea na baadhi viongozi wa wachimbaji wadogo Mkoa wa Ruvuma. 



Na Asteria Muhozya, Mbinga 

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema Wizara yake itafanya mazungumzo na Mamlaka zinazohusika na masuala ya barabara ili kuweka mazingira bora ya miundombinu hiyo kwa lengo la kuwezesha biashara ya makaa ya mawe na shughuli za uzalishaji makaa hayo kufanyika kwa ufanisi zaidi katika mgodi wa makaa ya mawe Ngaka, uliopo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma. 

Alisema mgodi huo wa Ngaka chini ya kampuni ya TANCOAL ndiyo taswira ya uzalishaji makaa ya mawe nchini hivyo, serikali haina budi kuweka mazingira bora yatakayowezesha kupunguza gharama za uendeshaji jambo ambalo litapunguza gharama kwa walaji wa nje na ndani ikizingatiwa kuwa, ni kampuni ya Kimataifa kutokana na kuhudumia wateja kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Rwanda, Burundi, Uganda nchi na nyingine. 

Kauli ya Naibu Waziri Nyongo inafuatia changamoto ya barabara iliyowasilishwa kwake na Meneja Mgodi wa TANCOAL Mhandisi David Kamenya, ambaye alimweleza Naibu Waziri kuwa, ukosefu wa miundombinu imara ikiwemo madaraja imechangia shughuli za upakiaji makaa hayo kutokuzidi tani 20 kwa kila gari jambo ambalo linapelekea kuwepo na foleni kubwa kutokana na uhitaji wa makaa hayo. 

Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara mgodini hapo Januari 17 ikilenga kukagua shughuli za madini mkoani Ruvuma pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali ambazo mgodi huo unakabiliana nazo katika utekelezaji wa shughuli zake. 

Pamoja na kuridhia ombi hilo, Naibu Waziri aliitaka kampuni hiyo kuongeza kasi ya uzalishaji kutokana na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo katika soko la nje na ndani na kuitaka kutobweteka huku ikitakiwa kuboresha huduma inazotoa ikiwemo kuongeza vifaa vya kazi. 

“Nimeona changamoto ya barabara. Kama serikali ni lazima tuifanyie kazi changamoto hii ili kuwezesha uzalishaji zaidi wa makaa. Sisi tutaendelea kutoa leseni kwa wazalishaji wengine ili kuweka ushindani, hivyo msibeweteke, tunahitaji sana makaa haya kwa uchumi wa taifa letu kwa kuwa tunayo hazina ya kutosha ya rasilimali hii,” alisema Nyongo. 

Aliongeza kuwa, kufuatia serikali kuweka zuio la uingizaji makaa kutoka nje, ni lazima kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa madini hayo ikiwemo kuwezesha biashara hiyo na kuutaja mgodi wa makaa ya mawe wa Kabulo unaomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwa ni eneo jingine ambalo miundombinu ya barabara ni lazima iboreshwe kuwezesha ufanisi zaidi wa shughuli za uzalishaji madini hayo. 

Alisema kuwa, ili serikali iendelee kupata mrabaha zaidi kutokana na rasilimali hiyo suala hilo lazima lichukuliwe kwa uzito ili kuongeza mapato zaidi. 

Aidha, akijibu ombi la kampuni hiyo kutaka kurudishiwa eneo ambalo lilitolewa kwa ajili ya Kiwanda cha Dangote na Rais John Magufuli, kwa kuwa bado haijanza kuchimba mpaka sasa, Naibu Waziri Nyongo alizitaka pande zote ikiwemo wizara na kampuni hizo kukutana Januari 22 mara baada ya kikao cha wadau wa sekta ya madini ili kujadili suala hilo ili hatimaye shughuli za uzalishaji zianze katika eneo hilo. 

Mbali na hilo, kampuni hiyo ilimwomba Naibu Waziri kuwezesha upatikanaji  wa leseni mbili zilizoombwa na kampuni hiyo ikilenga kutumia makaa hayo kuzalisha umeme kwa ajili ya matumizi ya mgodi. Naibu Waziri aliahidi kuwa, kupitia Tume ya Madini, suala hilo litakuwa limekamilika ndani ya kipindi cha wiki mbili. 

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo aliitaka Halmashauri ya Mbinga kubuni miradi kwa ajili ya vijana na wanawake yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya makaa ya mawe kwa ajili ya matumizi ya majumbani na kuachana na matumizi ya mkaa kwa kuwa umekuwa ukisababisha uharibifu wa mazingira. 

Wakati huo huo, akizungumzia suala la Mrabaha wa serikali wa asilimia 3, alisema usilipwe kwa bei ya maeneo ya uchimbaji bali ulipwe kwa bei ya sokoni. Hivyo, aliwataka wazalishaji wote na Maafisa wa Tume ya Madini kuhakikisha wanatoza bei ya sokoni na siyo ya uzalishaji. 

Kwa upande wake, Meneja wa mgodi Mhandisi David Kamenya akizungumzia ubora wa makaa hayo, alisema kuwa, Makaa ya Ngaka yana ubora wa kimataifa na ndiyo sababu imepelekea kupata wateja wengi kutoka nchi mbalimbali na kuongeza kwamba makaa hayo yana uwezo wa kufanya matumizi mbalimbali na kuongeza kuwa, kwa siku kampuni hiyo inapakia idadi ya magari yapatayo 100. 

AKizungumzia malengo ya baaaye, alisema kuwa, idadi ya mashine ndani ya siku chache zinatarajiwa kuongezwa na kwamba kampuni imelenga kuzalisha hadi tani 5,000 kwa siku kutoka 3,000 za sasa. 

Akizungumzia uwezeshaji kwa vijana na akina mama, alisema kuwa, tayari kipo kikundi cha wakina Mama cha Mbarawala ambacho kimewezeshwa na mgodi huo kwa kupatiwa mafunzo ya namna ya kuandaa makaa hayo maalum kwa matumizi ya majumbani na kuongeza kuwa, hivi karibuni kikundi hicho kimepata Cheti cha ubora kutoka shirika la Viwango nchini (TBS) jambo ambalo litawezesha kikundi hicho kuuza makaa yake kwa ajili ya matumizi ya majumbani na hivyo kupunguza matumizi ya mkaa unaotokana na kukatwa miti. 

Pia, Mhandisi Kamenya alimweleza Naibu Waziri Nyongo kuwa, mbali na kupatiwa mafunzo kikundi hicho pia kimepatiwa mashine ambayo inauwezo wa kuzalisha tani mbili za makaa hayo kwa saa. 

Akishukuru kwa niaba ya kikundi, Meneja Usimamizi wa Mbarawala, Joyce Haule alisema kuwa, wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuwawezesha na kwamba kikundi kinalenga kuzalisha tani 10 kwa siku na kuongeza kuwa, hadi sasa tayari kimepata wateja kutoka maeneo mbalimbali zikiwemo nchi za Rwanda ambao awali walitaka kwanza kikundi hicho kuwa na cheti cha ubora wa makaa hayo. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Cosmas Ishenyi alimweleza Naibu Waziri kuwa, kama Wilaya itahakikisha kuwa, inashirikiana na mamlaka zinazohusika kuweka mazingira bora ya kuwezesha mundombinu bora ya barabaraba ili TANCOAL iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi zaidi. 

Katika hatua nyingine, akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Prof. Riziki Shemdoe, ofisini kwake Januari 18, Naibu Waziri alimweleza Prof. Shemdoe umuhimu wa kuwezesha miundombinu ya barabra kuelekea katika mgodi huo wa Ngaka. 

Pia, Naibu Waziri alimweleza Prof. Riziki kuhusu mipango ya Serikali ya kuwa na vituo kwa ajili ya biashara ya madini na umuhimu wa mikoa kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli hizo. “ Tunataka kuwa na utaratibu wa kuwa na maeneo ya kuuza na kununua madini ili kuwa na utaratibu maalumu,” aliongeza 

Kwa upande wake, Prof. Shemdoe alimwomba Naibu Waziri kusaidia upatikanaji wa wawekezaji kwa ajili ya viwanda vya kuchenjua dhahabu mkoani humo na kukumbushia suala la uchimbaji madini katika Mto Muhuwesi. 

TANCOAL ni kampuni yenye ubia na Serikali kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) ambapo serikali inamiliki hisa kwa asilimia 30.

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI

$
0
0
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) jinsi maji yanavyovunwa katika Mtambo wa Ruvu Juu - Ruvu Kibaha - Pwani. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakiwa wamefika katika mtambo wa Ruvu Juu ikiwa ni ziara kwa ajili ya kujifunza baadhi ya mambo mbali mbali. 
Ziara ikiendelea.
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) mitambo ya mashine za maji eneo la Ruvu Juu walipofanya ziara ya kwa ajili ya kujifunza. 
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaongoza Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) mitambo ya kusafisha maji enwalipofanya ziara ya kwa ajili ya kujifunza. 
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akitoa maelezo. machache. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakionyeshwa mitambo ya mashine za maji.
Meneja wa DAWASA Kibaha - Pwani, Crossman Makere akitoa ripoti mbele ya Wakurugenzi Bosi ya DAWASA mara baada ya kutembelea ofisini hapo. 
Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakiwasili katika mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba, Ubungo kujionea walipofikia. 
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba injinia Ishmaeli Kakwezi akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange. 
Msimamizi wa Mradi wa Kisarawe na Kibaha injinia Ishmaeli Kakwezi akitoa maelezo mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kufika eneo la Minarani Kisarawe, Pwani kujionea ujenzi wa tanki la maji. 
Mafundi wakiendelea na kazi. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Mwamunyange akiwa na Wajumbe wa Bodi wakitoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali yahusuyo miradi hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kujifunza wanavyofanyakazi. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Mwamunyange amewataka wananchi wa maeneo yanayozunguka miradi ya maji ikiwemo miundo mbinu kuweza kuitunza ili iweze kudumu. Jenerali Mstaafu Mwamunyage akiwa na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA wameanza ziara ya siku tatu ya kutembelea miradi mbalimbali ya mamlaka hiyo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

 Akizungumza baada ya kumaliza siku ya kwanza Jenerali Mstaafu Mwamunyange amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kuwapatia maji safi na salama. "Niwaombe wananchi watunze miundo mbinu ya maji maana ujenzi wake ni gharama sana tofauti na wao wanavyofikiria wanapoona maji yamewafia majumba," amesema Jenerali Mstaafu Mwamunyange. Ziara hiyo ilianzia katika chanzo cha maji cha Mto Ruvu Juu, Ofisi ya DAWASA ya Kibaha, Tenki la Kibamba lenye ujazo wa lita Milioni 10 na ujenzi wa tanki la Kisarawe lenye ujazo wa Lita Milioni sita. 

Katika ziara yake Mwamunyage ametembelea pia Ujenzi wa mradi wa bomba la maji kutoka Kibamba (Bomba kuu la kusafirisha maji kutoka Ruvu juu) hadi Kisarawe utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha maji Lita Milioni 4 kwa siku na wananchi mbalimbali wa maeneo ya Kisarawe watafaidika na maji. Amesema kuwa, ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa tenki hilo na kama wakandarasi wataendelea hivyo kufikia mwezi Septemba mwaka huu ujenzi utakua umekamilika. 

Katika mradi huo Jenerali Mstaafu Mwamunyange ametembelea tenki la maji lenye ukubwa wa lita milioni 10 kwenye eneo la Kibamba na kuoneshwa pampu nne za kusukumia maji hadi Kisarawe. Kazi zingine zinazoendelea kutekelezwa na Mamlaka hiyo kwenye mradi wa Kisarawe ni ujenzi wa bomba la kusafirishia maji lenye kipenyo cha inchi 16 urefu wa Km 15.65, mabomba ya kusafirisha na kusambaza maji kwenda kwenye maeneo ya Viwanda lenye urefu wa Km 5.15 na kipenyo cha inchi 12 na lingine likiwa ni urefu wa Km 8 na kipenyo cha inchi 8.9 Ujenzi wa tenki la kuhifadhia na kusambaza maji lenye ukubwa wa Lita milioni 6 katika eneo la Mnarani Kisarawe na ujenzi wa Kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba. 
 
Maeneo yatakayofaidika na mradi huo ni kata ya Kisarawe, Kata ya Kazimzumbwi pamoja na maeneo ya Kiluvya, Kisopwa, Mloganzila na maeneo maalumu ya viwanda.

AFISA ELIMU ASIMAMISHWA KAZI ARUSHA

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Arusha. 

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemsimamisha kazi Ofisa elimu wa mkoa huo Gift Kyando kwa madai ya kuzuia wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza huku akilazimisha kila darasa kuwa na wanafunzi 40 tu.

Pia anadaiwa kusababisaha wanafunzi hao kukosa nafasi za masomo kwa kukataa kusajiliwa kwa shule mbili mpya za Oldonyowasi na Losikito kwa madai ya kukoda mahabara.

Gambo amesema kitendo hicho ni cha kukwamisha juhudi za serikali kupitia ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuwa uamuzi aliouchukua Ofisa huyo haukumuhusisha kiongozi yeyote yule wa serikali ngazi ya wilaya au mkoa

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha Dk. Wilson Mahera amesema kitendo hicho alichokifanya ofisa huyo kiliwachanganya na kusababisha ugomvi kati yao na wazazi wa wanafunzi hao

Amesema ofisa huyo angesababisha wanafunzi 6,819 kukosa elimu wakati yapo madarasa ambayo yaliachwa na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne ambayo yangeweza kutumiwa na wanafunzi hao

'' Madarasa yaliyopo yangeweza kuchukua wanafunzi kwa kipindi kifupi wapatao 55 kwa darasa moja '' alisema Mahera.Dkt. Mahera amesema kuhusu mapokezi wanafunzi kati ya shule 4239 wameshapokelewa katika shule 28 za halmashauri ya Arusha wakiwemo wavulana 1,853 na wasichana 2,386 ambao ni sawa na asilimia 62 huku waliobakia wakiendelea kuripoti na wengine wakichukua fomu za kujiunga.

Kwa upande wake Mwenyakiti wa CCM mkoa Loata Sanare amesema alichokiona ni hujuma za waziwazi kwa ofisa huyo dhidi ya serikali na kutaka kuzuia wanafunzi wasianze masomo.Sanare anasema alianza kupokea simu za malalamiko kutoka kwa wazazi wawanafunzi hao na alipompigia ofisa elimu huyo alimjibu majibu ambayo hayakumridhisha ndipo alipoamua kuwasikiana na mkuu wa mkoa.

TAIFA BADO LINAHITAJI WATUMISHI WENYE UJUZI UNAOKWENDA SAMBAMBA NA MABADILIKO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA - BALOZI SEIF ALI IDDI

$
0
0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea Gwaride la Wahitimu wa Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar katika mahafalio yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dr. Ali Mohaed Shein uliopo ndani ya Viunga vya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA}kiliopo Tunguu Mkoa Kusini Unaguja.Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria na Utawala Bora Mh. Haroun Ali Suleiman Waziri wa Elimu Mh. Riziki Pembe Juma, Kushoto ya Balozi ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Bibi Fatma Said Ali,Waziri wa Vijana Balozi Ali Karume na Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mh. Hassan Khatib.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha Utawala wa Umma Tunguu wakiingia ndani ya ukumbi wa Dr. Ali Mohamed Shein SUZA kukamilisha mahafali yao ya 11.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubia kwenye Mahafali ya 11 ya Chuo cha Utawala wa Umma Tunguu Mkoa Kusini Unguja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar Bibi Fatma Said Ali akitoa salamu wakati wa kuanza kwa Mahafali ya 11 ya Chuo hicho hapo Tunguu.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar wakifuatilia matukio mbali mbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye Mahafali yao ya 11 kwenye Ukumbi wa SUZA.
Muhitimu Abass Bakari Yakoub akipokea zawadi ya Mwanafunzi Bora wa {DRM} kutoka kwa Mgeni Rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Muhitimu Maryam Said Omar akipokea zawadi ya Mwanafunzi Bora wa {DSS} kutoka kwa Mgeni Rasmi WA Mahafali yao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.Picha na – OMPR – ZNZ.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Taifa bado linahitaji kuwa na Watumishi wenye ujuzi ili kwenda sambamba na mabadiliko mbali mbali ya sayansi na Teknolojia itakayoweza kuzikabili changamoto tofauti zilizopo Ulimwenguni hivi sasa.

Alisema Watumishi hao wakiandaliwa vyema katika maadili bora ya Utumishi wa Umma uliojaa Ubunifu, weledi na uchungu wa Rasilmali za Taifa ndio watakaokuwa tayari kuibadilisha Zanzibar kufikia Maendeleo yanayokusudiwa na Jamii.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wahitimu wa Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar wa ngazi na Fani mbali mbali za Elimu pamoja na Walimu na Wananchi kwenye Mahafali ya Kumi na Moja ya chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Dr. Ali Mohamed Shein SUZA Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema kwa vile Mtumishi wa Umma ndio Rasilmali ya msingi na nguvu kazi ya Maendeleo ya Taifa lolole, Chuo cha Utawala wa Umma kina dhima ya kumuandaa na kumuendeleza Mtumishi wa Umma ili amudu kutekeleza majukumu aliyopangiwa kwa ueledi, uaminifu, upendo na Uzalendo.

Balozi Seif alisema Chuo hakina budi kujikita katika kufanya tafiti mbali mbali zitakazosaidia kuandaa Programu za mafunzo ya muda mrefu na mfupi zitakazokwenda sambamba na mahitaji ya Wanajamii ili kuisaidia Serikali kuwa na Watumishi Bora wanaotoa huduma kwa vigezo na viwango kulingana na matarajio makubwa ya Wananchi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa wito kwa Uongozi wa Chuo hicho kuendelea kuongeza Uwezo wa kubadili Wanafunzi wengi zaidi lakini kwa kuzingatia vigezo na masharti yanayowekwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini pamoja na mahitaji ya sasa na baadae ili kufikia malengo ya Nchi iliyojiwekeza.

“ Tukumbuke kuwa Taifa linahitaji wasomi walioandaliwa vyema na kushiba Maadili bora ya Utumishi wa Umma, Weledi wenye Uchungu wa Rasilmali za Nchi”. Alieleza Balozi Seif.

Alielezea faraja yake kuona jinsi Chuo kinavyoendelea kutanua wigo wake wa kutoa Mafunzo mafupi ya kujenga uwezo kwa Watumishi wa Umma ikiwemo kuijengea uwezo Idara husika kwa kuandaa Programu Maalum ya Mafunzo iliyotokana na ziara ya kujifunza uendeshaji katika vyuo mbali mbali vya Zanzibar na Tanzania Bara.

Balozi Seif alisema kitendo cha kutoa mafunzo kwa Watumishi Wastaafu watarajiwa pamoja na watumishi wapya ni ishara tosha ya namna Chuo kinavyopiga hatua ya kutekeleza majukumu yake ya msingi ya maandalizi ya Watumishi Wastaafu.

Alisema wakati umefika sasa wa kukithamini na kukiheshimu Chuo cha Utawala wa Umma na kukitumia ipasavyo kama alivyosema Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ywa Mwaka 1964 Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ya kutukuza chake Mtu mpaka asahau cha mwenzake.

Alieleza kwamba Taasisi za Umma na hata zile binafsi wajenge Utamaduni wa kukitumia Chuo cha Utawala wa Umma katika kuwaendeleza Watendaji wao chenye Walimu waliobobea wenye uwezo wa kuwabadilisha wanafunzi wao Kimaadili, Kitaaluma, Kifrikra, Kimawazo na Utendaji .

Kwa upande wa Wahitimu hao, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwakumbusha kuitumia Taaluma wanapokwenda eneo lolote ili kubadilisha utendaji kazi wa mazoea kwenda kwenye Utumishi wenye kuzingatia uweledi, tija na utoaji huduma wa wakati kwa Wananchi.

Alisema Taifa linafurahia siku muhimu na adhimu ya ongezeko la Wataalamu wa fani mbali mbali wanaoingia kwenye tanuri la uwajibikaji utakaotegemewa katika kuleta mabadiloko ya Maendeleo endelevu Nchini.

Mapema Mkurugenzi wa Chuo cha Utawala wa Umma Dr. Mwinyi Talib Haji Alisema Chuo hicho ni Taasisi inayojitegemea na kupewa dhamana ya kutoa Mafunzo yanayohusiana na masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Nchini.

Dr. Mwinyi alisema Watumishi wa Umma ni Rasilmali muhimu inayopaswa kuenziwa kwa kupatia nyenzo ya kuwajibika Kitaaluma ambayo ni Elimu inayohusiana na Fani yao.

Alisema Chuo kimepata maendeleo makubwa tokea kuasisiwa kwake kwa kuzalisha Wahitimu wenye hadhi ya kukubalika katika ajira za Taasisi tofauti ambapo kwa sasa tayari kinawanafunzi 1,510 wanaoendelea kupata mafunzo katika fani tofauti.

Dr. Mwinyi alifahamisha kwamba Mwaka huu Chuo hicho kimezalisha Wahitimu wapatao 746 wa Ngazi ya Stashahada na Cheti katika fani mbali mbali sambamba na Wafanyakazi 2,675 wa Taasisi za Umma waliopatiwa Mafunzo.

Mkurugenzi huyo wa Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar alieleza kwamba Uongozi huo tayari umeshafungua Tawi lake Kisiwani Pemba linaloendelea kuwafinyanga Wanafunzi 235 hivi sasa.

Licha ya Mafanikio hayo Dr. Mwinyi alieleza kwamba zipo changamoto zinazokikabili chuo hicho akizitaja baadhi kuwa ni pamoja na uhaba wa Ofisi za Watendaji na Uzio unaotia hofu ya kuvamiwa na wahalifu hasa nyakati za Usiku.

Akimkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza na Wahitimu hao Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mh. Haroun Ali Suleiman alitoa wito kwa Viongozi na Wafanyakazi wa Taasisi za Umma kujipangia utaratibu wa kupata mafunzo ya Kazi chuoni hapo.

Waziri Haroun alisema Chuo kimebarikiwa kuwa na Walimu wenye uwezo mkubwa wa kutoa mafunzo yenye muelekeo wa kumuwezesha Manafunzi kufikia ngazi ya Stashahada kwa hivi sasa.

Kabla ya Mwaka 2007 Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar kilikuwa kikitoa Mafunzo kwa Watumishi wa Kada ya Chini, lakini kwa sasa kinadahili Wanafunzi wa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Kada tofauti zikiwemo Utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka, Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia na Usimamizi wa Rasilmali Watu.

Wengine ni Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari, Uongozi wa Biashara, ununuzi na Ugavi, Mipango ya Maendeleo, Utawala wa Serikali za Mitaa, Uhazili, Uongozi wa Elimu na Utawala pamoja na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

MAARIFA YA TEHAMA YAENDELEA KUONGEZEKA KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA –DKT. YONAZI

$
0
0
 Maprofesa na Madaktari wakifatilia mjadala wa Profesa Henk Sol wa Chuo Kikuu  cha Groningen nchini Uholazi warsha hiyo iliandaliwa na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) .
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akizungumza kuhusiana na Ujio wa Profesa Henk Sol wakati uwasilishaji wa maandiko mbalimbali.


WAKATI jamii mbalimbali duniani wakiendelea kutumia mfumo wa teknolojia habari na Mawasiliano (TEHAMA) imeelezwa kuwa maarifa zaidi yataendelea kuongezeka katika kuelekea uchumi wa viwanda. .

Moja ya mafanikio ya  Tehama ni kubuniwa kwa mfumo wakufuatilia madereva wanaoendesha mwendo wa haraka ambapo mfumo huo umesaidia kupunguza ajali ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.

Hayo aliyasema Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasialiano) Dk.Jim Yonazi amesema Tehama imesaidia kutatua matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi.

Dk. Yonazi aliyasema hayo juzi wakati wa semina ya siku mbili juu ya umuhimu wa Tehama katika kujiletea maendeleo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.“Tehama ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla hivyo hatunabudi kuhimiza wananchi kutumia Tehama ili kujiletea maendeleo na kutatua changamoto mbalimbali,”alisema

Dk. Yonazi alisema Tehama ikitumiwa vizuri inaweza okoa maisha ya mama mja mzito kwakufuatilia programu mbalimbali za lishe na malezi bora kupitia simu ya kiganjani.Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta alisema  tehama ikitumiwa vzuri huongeza ubunifu na maarifa hivyo aliwataka wananchi kutumia Tehama kujiletea maendeleo.

“Tehama hadi sasa inaendelea kusaidia kuongeza ubunifu na maarifa ambapo wengi wamenufaika ili kufanikisha hilo IFM tumeandaa washa ya siku mbili kwa watumishi na wanafunzi wa IFM kama sehemu yakujuzana umuhimu wa Tehama,”alisema.Profesa Satta alisema semina hiyo itawajengea uwezo watumishi wa IFM ikizingatiwa kuwa muongoza mada katika washa hiyo ni mbobevu katika masuala ya Tehama ambaye ni Profesa Henk Sol wa Chuo Kikuu cha Groningen cha nchini Uholanzi.

“Tumekuwa tukibadirishana uzoefu na vyuo vya kimataifa ili kuweza kuleta maendeleo katika Taifa letu kwakuwa ukiwajengea uwezo wanataaluma umeelimisha Taifa zima hususani katika mmatumizi bora ya teknolojia katika kuboresha huduma na ufanisi,”Naye Muongozaji wa mada mbalimbali zihusuzo Tehama katika washa hiyo Profesa  Henk Sol alisema nchi za magaharibi ikiwemo Uholanzi zimepiga hatua kubwa sana kutokana na matumizi ya Tehama.

"Ugunduzi wa Tehama ulianzia katika nchi za mabara ya Ulaya na Marekani lakini lakini umekuwepo ukweli kwa watu wake ambao wamechangamkia fursa na wameweza kujiletea maendeleo kikubwa nikuwa wabunifu nakuitumia Tehama kama injini yakujiletea maendeleo."

MAAFISA MADINI WATAKIWA KUTOBAGUA MIGODI

$
0
0
Sehemu ya Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Saphire wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe Maalum kwa Naibu Waziri Stanslaus Nyongo baada ya kuwasili katika kijiji cha Masuguru Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo mwenye sweta (nyekundu) katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini ya Sapphire katika kijiji cha Masuguru Wiaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisamiliana na baadhi ya wachimbaji wa madini ya Sapphire katika kijiji cha Masuguru mara baada ya kuwasili kijijini hap wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uchimbaji madini wilayani humo
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Cosmas Ishenyi akizungumza jambo wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Masuguru. Katikati ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.
Mmoja wa wachimbaji wananwake katika kijiji cha Masuguru akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Cosmas Ishenyi ( hawapo pichani) wakati wa ziara ya viongozi hao kijijini hapo.
Sehemu ya wachimbaji na wananchi katika kijiji cha Masuguru wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo hayupo pichani wakati wa ziara yake kijijini hapo kukagua shughuli za uchimbaji madini.



Na Asteria Muhozya, Mbinga 

Maafisa Madini nchini wametakiwa kutobagua migodi midogo kwa kuelekeza nguvu kwenye migodi mikubwa tu huku wakisisitizwa kutatua migogoro kwenye maeneo yao ya kazi na kuelezwa kuwa, watakaobainika wakibagua migodi hiyo na kutotatua migogoro wataondolewa kwenye nafasi zao. 

Hayo yalibainishwa Januari 17 na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini aina ya Sapphire wakati wa ziara yake katika kijiji cha Masuguru, Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma. 

Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara hiyo ikilenga kukagua shughuli za uchimbaji madini wilayani humo pamoja na kusikiliza kero za wachimbaji katika migodi hiyo, ambapo wachimbaji waliwasilisha kero za kutaka kutengewa maeneo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji, bei elekezi za madini ikiwemo kuunganishwa na huduma ya umeme kwenye migodi yao. 

Akizungumza kijijini hapo, alimtaka Afisa Madini mkoa wa Ruvuma hukakikisha anaishughulikia kero hiyo na kuitatua mara moja na kuongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano anataka wachimbaji nchini wachimbe madini, hivyo, maafisa madini kote nchini wahakikishe wanashughulikia kero katika maeneo yao ya kazi ikiwemo kusuluhisha migogoro. 

“Sisi ni matajiri, tumebarikiwa madini ya vito. Wachimbaji chimbeni lakini mchimbe katika maeneo yaliyoruhusiwa kuchimbwa”.alisisitiza. 

Alisema kuwa, kama mgogoro ni mkubwa wapo viongozi wa vyama vya wachimbaji wahakikishe kuwa wanafikisha migororo hiyo na kusema “tuleteeni na sisi lakini usipoishughulikia migogoro hiyo tutakuondoa. 

Aliongeza kwamba, serikali inalenga katika kuwatoa wachimbaji wadogo kutoka katika uchimbaji mdogo kwenda uchimbaji wa kati na hatimaye mkubwa na ndiyo sababu inaendelea na ujenzi wa vituo vya umahiri katika maeneo mbalimbali nchini ikilenga katika kutoa elimu ya uchimbaji bora, uchenjuaji bora, biashara ya madini na ujasiliamali ili kuhakikisha kwamba wachimbaji wadogo wanakua. 

Aliongeza kuwa, elimu ya ujasiliamali ni muhimu kwa wachimbaji wadogo kwa kuwa itawaandaa kuwa na uchimbaji endelevu na wenye tija. 

Akijibu ombi la ruzuku, aliwataka wachimbaji wadogo kujiunga katika vikundi vidogo vidogo ili iwe rahisi kwa wachimbaji hao kufikiwa ikiwemo kupatiwa huduma za leseni, elimu, vifaa, kuwamilikisha, kuwapatia mikopo na kuwafuatilia jambo ambalo litapelekea wafanye kazi kwa urahisi na kwa kulipa kodi za serikali na wao kubaki na kipato kitakachowezesha maisha bora. 

Alisema uwepo wa mazingira mazuri migodini utasaidia vijana kufanya kazi na hivyo kuwa na taifa lenye watu wanaofanya kazi. Aliwataka maafisa madini wote kuhakikisha wanashughulikia migogoro ya wachimbaji wadogo na kueleza kwamba, endapo serikali itakuta migogogoro ya wachimbaji wadogo katika maeneo yao wataondolewa. 

Aliongeza kwamba, wizara imejipanga na tayari kuna baadhi ya maeneo yametengwa kwa ajili ya wachimbaji na kuwasisisitiza kuhakikisha wanauza madini wanayoyachimba katika maeneo rasmi. 

Akizungumzia suala la broker, aliwataka kuhakikisha wanakuwa na leseni ya kufanya shughuli hizo ikiwemo vifaa vya kupimia madini na kuwataka kulipa kodi. Pia, aliwatahadharisha wachimbaji wanaoshirikiana na broker wasiokuwa na leseni kuacha kwani kwa kufanya hivyo ni kwamba kwamba wote wanaliibia taifa.” Maafisa madini hakikisheni mnawajua ma broker wote na wawe na leseni na walipe kodi, “ alisisitiza Nyongo. 

Akijibu ombi la ruzuku lililowasilishwa kwake, alisema fedha za ruzuku zilizokuwa zikitolewa awali hazikuwafikia walengwa wote na kueleza kuwa, wapo waliopata ruzuku hizo lakini hawakuwa wachimbaji na kuongeza kwamba, hivi sasa wizara inaangalia namna bora ya kuwasaidia wachimbaji. 

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkoa wa Ruvuma Abraham Nkya alisema kuwa, mkoa huo tayari umetenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kwamba watashirikiana na wachimbaji hao ili suala hilo liweze kuwasilishwa Tume ya Madini kwa ajili ya hatua zaidi. 

Awali , kiongozi wa wachimbaji aliwasilisha ombi kwa Naibu Waziri la wachimbaji kupatiwa ruzuku. Alisema mkoa huo umebarikiwa madini ya ujenzi, nishati, viwanda huku eneo la Masuguru likibariwa madini ya Sapphire. Alisema eneo hilo liliombwa kwa ajjili ya uchimbaji mdogo lakini mpaka sasa bado halijatengwa. 

Pia, alisema ipo changamoto ya kukosekana elimu kwa watendaji vijijini ambao wamesababisha mgizo mkubwa wa kodi kwa wachimbaji.

WABUNGE CCM WAMPONGEZA CAG KUITIKIA WITO WA KAMATI YA BUNGE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda. 

WAZIRI KIGWANGALLA AKUTANA NA WAKALA ATAKAYELETA WATALII 10,000

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla amekutana na kufanya mazungumzo  na Wakala wa watalii kutoka  Beijing nchini China, Bw.He Liehui ambaye kwa mwaka huu amepanga kuwaleta watalii 10,000 nchini Tanzania na kwa sasa yupo nchini kwa ajili ya kufanya maandalizi ya watalii hao.

Mazungumzo hayo kati yao  yamefanyika katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo Mpingo House jijini Dar es Salaam

Aidha,  Wakala huyo Bw.He  anatarajia pia leo  kuonana na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa.

MWANAMITINDO WA MAREKANI AFURAHISHWA NA VIVUTIO HIFADHI YA TAIFA TARANGIRE.

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga, Tarangire.

 
MWANAMITINDO na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo aliwasili nchini hivi karibuni ametembelea Hifadhi ya  Taifa ya Tarangire na kupokelewa na Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi hiyo.

 Muda mfupi baada ya kuwasili Mwanamitindo huyo aliyekuwa ameongozana na Mama yake mazazi pamoja na anayetajwa kuwa  mchumba wake ,alikabidhiwa zawadi mbalimbali yakiwemo mavazi maalumu yanayotumiwa na Jamii ya Maasai.

Marisela baada ya kutembelea mane mbalimbali ya Hifadhi hiyo wakiwemo wanyama alieleza furaha yake huku akiahidi kuwa balozi wa vivutio vya utalii atakavyotembelea hapa nchini .

Mrembo huyo ambaye kwa sasa anaishi Los Angels amesema lengo la kuja nchini kutembelea vivutio vya utalii ni pamoja na kuangalia fursa mpya ipatikanayo katika sekta ya Utalii Duniani pamoja na kuvitangaza.

Mwanamitindi huyo anaendelea na ziara yake hiyo ya kitalii katika Hifadhi ya Ngorongoro ambako atashuhudia maajabu ya wanyama katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Bonde la ufa la Ngorongoro (Ngongoro Creator).”



 

Hospitali ya Bugando kuajiri Madaktari na wauguzi kutoka nchini Cuba

$
0
0
Hospitali ya Kanda ya Bugando inatarajia kuajili Madaktari na wauguzi 13 kutoka nchini Cuba katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za afya kwa wananchi kutokana na kuongeza idadi hiyo ya madaktari.

Akizungumza Balozi wa Cuba nchini Tanzania Profesa Lucas Polledo amesema ziara yake katika hospitali Bugando ni kutokana ushirikiano uliopo kati ya Bugando na nchi ya Cuba.

Balozi amesema kuwa lengo ni kuangalia utoaji wa huduma za afya kwa wananchi. Aidha amesema kuwa wanaendelea kushirikiana na hospitali hiyo katika maeneo mengine ambayo yana changamoto katika utoaji wa huduma za afya.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kanda Bugando Profesa Abel Makubi amesema kuwa Madaktari saba wanakuja mwezi ujao na wengine watakuja.
Amesema kuna ushirikiano wa karibu kati ya hospitali ya Bugando na Cuba hivyo wanatarajia kupata mengi katika nchi hiyo.

Profesa Makubi mesema Madaktari wataokuja Madaktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo,Koo-pua na masikio (ENT),Wataalamuwa usingizi ,mionzi,na madaktari bingwa wa huduma za dharula pamoja na madaktari bingwa wa magonjwa ya ubongo na uti wa mgongo.


Balozi wa Cuba nchini Tanzania Profesa Lucas Polledo akitia saini kitabu cha wageni katika hospitali ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza wakati alipotembelea hospitali hapo akiwa na familia yake.
Balozi wa Cuba nchini Tanzania Profesa Lucas Polledo akizungumza na menejimenti ya Hospitali ya Bugando wakati alipofanya ziara akiwa familia yake ikiwa na mahusiano yaliyopo katika ya hospitali nan chi ya Cuba.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA TOUCHROAD GROUP YA CHINA, BW.He LIEHUI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameahidi kupokea kundi la watalii wasiopungua 300 ambao wanatarajiwa kuwasili nchini Machi, mwaka huu.

Watalii hao ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 wanaotarajiwa kuwasili nchini katika mwaka 2019 chini ya mpango unaosimamiwa baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania na kampuni ya TouchRoad International Holding Group ya China.

Ametoa ahadi hiyo leo (Jumamosi, Januari 19, 2019) alipokutana na Mwenyekiti wa Touchroad Group, Bw. Liehui He na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Thomas Mihayo ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kuelezwa na Bw. He huyo kwamba kundi hilo la watalii likiwa Djibouti litapokelewa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo na likienda Zimbabwe, litapokelewa na Rais wa nchi hiyo.

“Tanzania imeamua kuweka mkakati wa kuongeza idadi ya watalii nchini kwa kuboresha miundombinu ya usafiri na kukuza utalii kupitia vivutio vya vyakula vya asili, mavazi ya asili, wanyama, fukwe za bahari na milima. Kwa hiyo, ujio wa kundi hili kubwa, unatoa fursa mpya ya kutangaza vivutio vya nchi yetu,” amesema.

“Nitoe wito kwa Watanzania wanaoishi maeneo ya jirani na vivutio vyetu, wachangamkie fursa ya ujio wa watalii hawa katika maeneo mbalimbali. Wakifika Dar es Salaam, wanaweza kwenda Kigoma kuona Ziwa Tanganyika, mbuga zilizoko Nyanda za Juu Kusini, Arusha au vivutio vya Zanzibar. Tujiandae, tuwe tayari kuwauzia bidhaa mbalimbali,” amesema.

Pia amesema amefurahishwa na wazo lao la kuifanya Dar es Salaam iwe kitovu cha utalii (tourist hub) kwa makundi ya watalii ambayo yatakuja Tanzania na baadaye kutoka Tanzania kwenda Lusaka, Harare, Johannesburg na Djibouti.

Mwenyekiti huyo ambaye aliwasili nchini juzi, ameambatana na ujumbe wa watu 31 ambao unajumuisha waandishi wa habari, wasanii, wanamuziki na watu mashuhuri.

Akiwa Beijing, China, wakati akishiriki mkutano wa Jukwaa la Biashara baina ya Tanzania na China lililofanyika Septemba mwaka jana, Waziri Mkuu alikutana na uongozi wa kampuni ya TouchRoad ambayo ilionesha nia ya kutangaza fursa za utalii zilizopo hapa nchini.Ziara ya Bw. He ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyoingiwa kati ya kampuni ya TouchRoad na Bodi ya Utalii ya Tanzania, Novemba 2018.

Mapema, Bw. He alimweleza Waziri Mkuu nia ya kampuni hiyo kutekeleza makubaliano yao ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika soko la China ili kuvutia watalii wapatao 10,000 waitembelee Tanzania katika mwaka 2019.

“Tumepanga kuleta watalii 10,000 kwa mwaka huu wa 2019 na tumeweka lengo la kuongeza idadi hiyo kwa asilimia 20 kila mwaka kwa muda wa miaka mitano. Pia tuna lengo la kuitumia ndege ya ATCL ili ilete watalii moja kwa moja kutoka Shanghai, China,” alisema.Akielezea ujio wa kundi la kwanza la watalii, Bw. He alisema kundi hilo litakaa Djibouti kwa siku moja, Tanzania siku nne (tatu za kulala) na Zimbabwe siku tatu (mbili za kulala) na kisha kurejea China.

Alisema wanapanga kila mwezi wawe na kundi kubwa la watalii ambao watakuwa wanafikia Tanzania na kupelekwa nchi nyingine kwa sababu Wachina wengi hupenda kufanya utalii kwa siku walau 10, lakini wapelekwe maeneo matatu au manne tofauti kuona vivutio vya aina nyingine badala ya kukaa sehemu moja kwa kipindi chote hicho.

“Watalii hawa wakija kwa siku tatu au nne, wana uhakika wa kutumia dola za Marekani zaidi 2,000, wakienda eneo jingine watatumia fedha pia, namna hiyo tuna uhakika wa kuongeza pato la Taifa, lakini pia tuna uhakika wa kutengeneza ajira kwa Watanzania,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – DODOMA, 

JUMAMOSI, JANUARI 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Kampuni ya Touchroad Group ya China, Bw. He Liehui, ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dodoma, Januari 19, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Touchroad Group ya China, Bw. He Liehui, ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dodoma, Januari 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

TaESA yajengea uwezo wa kutafuta ajira wanafunzi 500 ATC

$
0
0
WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA), imewajengea uwezo na kuwapa mbinu za kutafuta ajira pindi wanapomaliza masomo zaidi ya wanafunzi 500 wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).

Huduma zinazotolewa na TaESA ni kuunganisha watafuta kazi na waajiri, kutoa mafunzo kuhusu mbinu za usaili ambayo huwajengea uwezo wa kujiamini, kutoa ushauri kuhusu masuala ya ajira na kutoa taarifa za soko la ajira.

Akizungumza mjini Arusha Afisa Kazi Mwandamizi wa TaESA na Mratibu wa Mafunzo hayo kwa wanafunzi Peter Ugata alisema, Tanzania na dunia kwa sasa kuna changamoto zinazohusiana na Soko la Ajira. Alisema hatua hiyo imechangiwa na mahitaji ya Waajiri kuhamia kwa watu wenye ujuzi wa ziada mbali ya na weledi wa kusomea, kwani mara nyingi ujuzi wa ziada hausomewi.

“Changamoto zilizopo zimeletwa na mabadiliko ya dunia ya utanfawazi ambapo watu, huduma na bidhaa ziko huru kutoka sehemu moja hadi nyingine. “Ili kukabiliana na hali hiyo nchi mbalimbali duniani zilianzisha huduma za Ajira kupitia Sera, Sheria, Kanuni na maazimio ya Shirika la Kazi Duniani (ILO),” alisema.

Akifafanua namna huduma za ajira zinavyotolewa Ugata alisema Wakala husajili na kutunza taarifa za watafuta kazi kwa kutumia Kanzidata iliyopo. “Wakala huoanisha sifa za mtafuta kazi kulingana na mahitaji ya kazi husika kama yalivyoanishiwa na mwajiri, lakini pia wakala unaoanisha ujuzi, uzoefu, elimu na sifa nyingine za watafuta kazi na mahitaji ya sifa za kazi za mwajiri,” alisema Ugata.

Anazitaja baadhi ya faida za kutumia TaESA ni Waajiri kupewa ushauri mzuri kuhusu mwenendo wa soko la Ajira na mahitaji na aina ya watu na ujuzi utaokamsaidia kuleta tija. “TaESA itamuwezesha mwajiri kupata wafanyakazi kazi waadilifu na waaminifu katika kazi, wabunifu na wakujituma kazini , lakini pia kuiwezesha serikali kupata takwimu za uamuzi na mipango kwa haraka,” alisema Ugata.

TaESA inafanya kazi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu. 
Afisa Kazi kutoka TaESA Emma Mangesho akiwajengea uwezo na kuwapa mbinu Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kuhusu namna bora ya kutafuta kazi 
Meneja wa Karakana ya uchomeleaji Chuo cha Ufundi Arusha Expedito Miliaso akiwaonyesha maofisa wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA), vifaa vipya vya uchomeleaji wanavyotumia wanafunzi wa Chuo hicho kwa ajili ya mafunzo. 
Maofisa wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) kutoka Dar es Salaam na Arusha wakiangalia kifaa maalumu cha uchomeleaji ndani ya Karakana ya Chuo cha Ufundi Arusha anayewaonyesha ni Meneja wa Karakana ya uchomeleaji Expedito Miliaso. 
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), wakimsikiliza Afisa Kazi wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESO) kutoka Dar es Salaam Emma Mangesho akifundisha namba bora ya uandishi wa barua za kuomba ajira.
Afisa Kazi wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESO) kutoka Dar es Salaam Emma Mangesho akifundisha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), mbinu za kuomba ajira ikiwamo namna bora ya uandishi wa barua za kuomba kazi. 
Afisa Kazi Mwandamizi kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) na Mratibu wa mafunzi Peter Ugata akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) wakati wa kuwajengea uwezo wa namna bora ya kutafuta kazi.
 

Wateja 100 wa Benki ya NMB wajishindia shs 100,000/- kila mmoja za shindano la 'MastaBata'

$
0
0

Remida Mosi (kulia) kutoka Benki ya NMB kitengo cha Kadi akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tano ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata'. Kushoto ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdallah Hemedy na Florence Mchau kutoka kitengo cha kadi cha NMB (katikati).
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Oyster Plaza, Hildegard Mng'ong'o akizungumza leo kwenye droo ya tano ya Masta Bata iliyochezeshwa katika tawi hilo.
Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi Benki ya NMB, Manfredy Kayala (kulia) akizungumza leo kwenye droo ya tano ya shindano la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata'. Kushoto droo hiyo ikiendelea kuchezeshwa.
Remida Mosi (kulia) kutoka Benki ya NMB kitengo cha Kadi akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tano ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata'. Kushoto ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdallah Hemedy na Florence Mchau kutoka kitengo cha kadi cha NMB (katikati).




JUMLA ya wateja 100 wa Benki ya NMB wamejishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila mmoja na wengine sita wakijishindia simu janja 'Samsung S9+' zenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kila moja. Idadi ya wateja hao imefikiwa leo baada ya kuchezeshwa droo ya tano ya shindano la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata' na wateja wengine 20 kujipatia kitita hicho.

Droo ya tano imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam katika Tawi la NMB Oyster Plaza na kupatikana kwa washindi hao 20 chini ya uangalizi wa Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdallah Hemedy.

Akizungumza katika droo hiyo Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi Benki ya NMB, Manfredy Kayala Alisema wateja 20 wamepigiwa simu na kujulishwa ushindi wao na fedha walizojishindia zitaingizwa kwenye akaunti zao ndani ya saa 24 tangu kuchezeshwa kwa droo hiyo.Alisema kupatikana kwa washindi wa leo kunatimiza idadi ya wateja 100 hadi sasa ambao wamejishindia shilingi 100,000 kila mmoja, huku kukiwa na wengine 6 walionyakuwa simu aina ya Samsung S9+' droo iliyopita.

Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi hizo.

Hata hivyo, aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika na shindano zima.

TGNP MTANDAO YAENDESHA WARSHA KWA WAHARIRI KUHUSU BAJETI YA MRENGO WA KIJINSIA

$
0
0

TGNP Mtandao imeendesha warsha kwa Wahariri na baadhi ya waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa ajili ya kuwaongezea uelewa na uwezo kuhariri na kuripoti masuala ya kijinsia.

Warsha hiyo ya siku moja imefanyika leo Jumamosi Januari 19,2019 katika ofisi za TGNP Mtandao zilizopo jijini Dar es salaam.

Akifungua warsha,Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema mafunzo hayo yawawezesha wahariri na waandishi wa habari kuhamasisha uingizwaji wa masuala ya kijinsia katika mipango,miongozo na sera za serikali.

"Tumekutana hapa kwa ajili ya kukumbushana dhana kuu za jinsia na umuhimu wa kuzingatia masuala ya jinsia kwa maendeleo lakini pia kuweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti masuala ya kijinsia katika vyombo vya habari kwani tunaamini vyombo vya habari ni muhimu kwa maendeleo ya jamii",alisema Liundi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akizungumza wakati akifungua warsha ya wahariri kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia katika ukumbi wa ofisi za TGNP Mtandao jijini Dar es salaam. Picha zote na Kadama Malunde - na Frankius Cleophace Malunde1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akielezea kuhusu dhana nzima ua bajeti yenye mrengo wa kijinsia.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.

Regina Mziwanda wa BBC Swahili akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Warsha inaendelea..
Mhariri wa gazeti la Majira,Imma Mbuguni akichangia hoja ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - na Frankius Cleophace Malunde1 blog

KLABU ZA FEMA ZACHANGIA UFAULU WA WANAFUNZI MASHULENI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

KATIKA kusherekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirika lisilo la kiserikali la FEMINA, mchango wa shirika hilo umeonekana kwa vijana hasa kwa kuonesha juhudi zao za kuwafikia vijana nchini kote na kuwapa elimu kuhusiana na afya ya uzazi, uwezeshaji kiuchumi pamoja na ushiriki katika masuala ya uraia.

Akizungumza na waandishi wa habari katika warsha uliowakutanisha, Mkurugenzi wa Habari wa FEMINA Amabilis Batamula amesema kuwa miaka 20 ya shirika hilo imekuwa ya mafanikio makubwa kwani tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999 vijana wengi wamenufaika na wanaendelea kulea vijana wapya na kusema kuwa programu zote zitakuwa endelevu.

Akieleza maeneo ambayo wao kama FEMINA wanayafanyia kazi Amabilisi amesema kuwa wanajiegemeza katika maeneo makuu matatu ambayo ni kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia ambayo ilianza kutolewa mwaka 1999 kwa kutoa elimu kuhusia na ugonjwa wa UKIMWI na baadae stadi za maisha na taarifa kuhusu afya ya uzazi na kwa sasa katika shule wanatumia mbinu ya kusubiri pamoja na kufikia huduma za afya.

Pia eneo jingine ambalo wanaliegemea ni uwezeshaji wa kiuchumi kwa vijana ambapo huwapa taarifa za fursa zinazowazunguka vijana hao na sio pesa wala mitaji na hiyo ni katika kuwasaidia kwa kuwajengea wigo wa kujitegemea na katika hilo hushirikiana na wadau mbalimbali wa kimaendeleo katika kupata taarifa ambazo wao huzichakata.

Ameeleza kuwa FEMINA pia hutoa elimu kwa vijana kuhusu kushiriki mambo mbalimbali ya kijamii kama mikutano ya kata, vijiji na Wilaya pamoja na kujitolea katika nafasi mbalimbali kama vile kufanya usafi katika hospitali, masoko na kujitolea damu na hiyo ni pamoja na kupiga vita tamaduni potovu ikiwa ni pamoja na ukeketaji na ndoa za utotoni.

Amabilisi amesema kuwa lazima wazazi pamoja na walezi wawe wawazi kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha kuhusiana na afya ya uzazi pamoja na kukabiliana na changamoto katika ukuaji wao.

Kuhusiana na mchango wa FEMINA katika klabu za FEMA kote nchini Afisa ufuatiliaji na tathimini kutoka FEMINA Martha Samwel amesema kuwa ufaulu kwa shule zenye klabu za FEMA uameongezeka na hiyo ni kutokana na mirejesho wanayoipata kutoka kwa walimu na walezi wa klabu hizo kwani kupitia klabu hizo wanafunzi wamekuwa wakielimishana na kuhimizana kuhusu masomo na katika baadhi ya maeneo wanafunzi watoro darasani wamerudi shule kutokana na nguvu ya klabu za FEMA.

"Kuna baadhi ya shule zimekuwa na misimamo yao ambapo wanakauli mbiu zao za kutoruhusu mwanaklabu ya FEMA afeli darasani, hii inawapa nguvu na ari ya wao kusoma zaidi na hatimaye kufanya vizuri katika masomo yao" ameeleza Martha.

Aidha amesema kuwa mafanikio waliyoyapata kwa miaka 20 ni makubwa sana hasa kwa kuwafikia vijana wengi Tanzania kote na kutoe elimu ambayo imewasaidia kwa kiasi kikubwa hivyo wanajivunia kuwa sehemu ya maisha kwa vijana hao.

Pia amewashauri vijana wengine kujiunga na klabu za FEMA ili waweze kupata elimu ya afya na ujinsia pamoja na elimu ya ujasiriamali ambayo itawasaidia katika kujenga taifa na kujenga nchi ya viwanda kwa kuwa wao ndio nguvu kazi ya taifa.
Mkurugenzi wa Masuala ya Habari katika shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya vijana la Femina Hip, Amabilis Batamula (kulia) akizungumza kuhusiana na miaka 20 ya shirika hilo wakati wa semina na wanahabari, jijini Dar es Salaam juzi. Picha na Joseph Zablon

BODI YA WAKUREGENZI DAWASA KUENDELEA KUKAGUA UTOAJI HUDUMA YA MAJI KWA WANANCHI WA DAR NA PWANI

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA),Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ametembelea mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini na kushiriki upandaji wa miti pembezoni mwa chanzo cha Mto Ruvu.

Mwamunyange amepanda mti sambamba na wajumbe wa bodi kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji vya mto Ruvu ikiwa ndio chanzo kikubwa kinachozalisha maji kwa asilimia 88 katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.Akiwa katika ziara yake ya siku ya pili, Mwamunyange ametembelea mtambo huo ikiwa ni mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo.

Mwamunyange ametembelea mtambo huo akiwa ameongozana na wajumbe wa bodi ya DAWASA kuona namna uzalishaji maji unavyoanzia na kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wahandisi wa Mamlaka hiyo.Akizungumza baada ya kumaliza kutembelea mtambo huo, Mwamunyange amesema kiwango kikubwa cha uwekezaji kimefanyika na wataalamu wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata maji.

Mwamunyange amesema jitihada kubwa za serikali zinafanyika kuhakikisha wananchi wote wanapata maji hususani kwenye maeneo yaliyokuwa hayana maji kwa kipindi chote kikubwa wananchi wawe wavumilivu kwakuwa DAWASA wanafanya kazi kuwapelekea maji.Baada ya kuwasili katika mtambo huo Mwamunyange alipata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa mtambo huo na kuwataka wafanye kazi kwa juhudi kubwa ili kutimiza adhma ya serikali ya kufikia asilimia 95 ya wananchi wote ifikapo 2020.

Mwamunyange amesema, anafahamu kuna changamoto mbalimbali za wafanyakazi ila amewaahidi atazifanyia kazi atakapokutana na Sekretarieti ya DAWASA.Mbali na kutembelea mtambo wa Ruvu Chini, Mwamunyange ametembelea Tenki la maji la Changanyikeni, Busta pampu zilizofungwa Makongo kwa ajili kusukuma maji na maunganisho mapya Salasala.

Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi itaendelea kwenye maeneo mengine tofauti kwa ajili ya kujifunza na kuona namna DAWASA wanavyotoa huduma ya maji kwa wananchi wa Dar esSalaam na Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Mhandisi Arone Joseph walipotembelea mtambo wa Ruvu Chini ikiwa ni ziara ya siku tatu.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka (DAWASA) Jenerali Davis Mwamunyange akipanda miti pembezoni mwa chanzo cha Mto Ruvu wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo.

UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

UMOJA wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Tanzania kwa upande wa Zanzibar, leo umezindua rasmi kamati ndogo ndogo nne zitakazokuwa na majukumu mbali mbali ya kufanisha kwa ufanisi kazi za umoja huo kwa mwaka 2019/2020.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi alizitaja kamati zilizozinduliwa kuwa ni pamoja na Kamati ya Uchumi, Mipango na Fedha, Kamati ya Mawasiliano kwa Umma, Kamati ya Elimu,Malezi na Mafunzo pamoja na Kamati ya Mahusiano na Taasisi za Wanawake ndani na nje ya Nchi.

Alisema kuwanzishwa kwa kamati hizo ni matarajio makubwa zaidi ni kuwafikia Wanawake na Vijana pamoja na makundi mbali mbali yaliyopo katika jamii na watoto ili kushinda Uchaguzi ujao mwaka 2020.

Katika maelezo yake Makamu Mwenyekiti huyo aliwasisitiza Wajumbe wote wa Kamati hizo kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ya UWT pamoja na CCM kwa ujumla.

“Wanawake ni Jeshi kubwa tena la ukombozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, nasaha zangu kwenu ni kwamba tutumie nafasi hii kuhakikisha tunawafikia wanawake wote hasa waliopo Vijijini na Pembezoni kwa nia ya kuwaweka karibu na kufanya nao shughuli zetu za kisiasa.

Pia Wanawake wa UWT lazima tupate Sauti zetu kila mmoja kwa nafasi yake ndani ya Umoja Wetu kuyasema mambo mema yanayotekelezwa na CCM chini ya Viongozi wetu Wakuu ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wanaoendelea kusimamia kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.”, alisema Makamu Mwenyekiti Thuwayba Kisasi.

Aliwataka Wanawake nchini kushirikiana katika malezi ya Watoto ili waweze kukuwa wakiwa katika malezi na maadili bora yatakayowasaidia kupambana na changamoto za mmomonyoko wa maadili.Awali akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo , alieleza kuwa UWT imejipanga kufanya kazi zake Kisayansi zaidi kwa lengo la kufanikisha kwa wakati malengo waliyojiwekea ndani ya Umoja huo.

Aidha alifafanua kuwa Kamati hizo zilizozinduliwa zitakuwa ni chachu ya kubuni miradi mipya ya kiuchumi itakayoongeza kipato ndani ya UWT pamoja na kupatikana fursa ya mahusiano mazuri na Taasisi mbali mbali za Wanawake Duniani.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati tekelezaji WUT Taifa Ndugu Lucy Mwakembe alisema Umoja huo utaendelea kupanga mikakati mbali mbali ya kimaendeleo ili kujiinua kiuchumi.
MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi akizungumza na Wajumbe wa Kamati ndogo ndogo za Umoja huo mara baada ya kuzinduliwa.
NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo akitoa ufafanuzi wa majukumu mbali mbali ya Kamati hizo ambazo ni nne zilizozinduliwa kutokana na Matakwa ya Kanuni ya Umoja huo.
BAADHI ya Wajumbe wa Kamati ndogo ndogo za UWT Zanzibar zilizozinduliwa leo wakiwa katika Kikao cha Awali cha utambulisho wa Kamati hizo, huko Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui.
Picha ya Pamoja ya Wajumbe wote wa Kamati Nne za UWT zilizozinduliwa.


WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUUGEUKIA UTALII WA FUKWE

$
0
0
NA LUSUNGU HELELA- KIBAHA
Wizara  ya Maliasili na Utalii, imeanza kuyatambua na kuainisha maeneo kwa ajili ya utalii wa Fukwe katika Kisiwa cha Mafia mkoani Kibaha kwa ajili ya kuhamasisha Wawekezaji kuchangamkia fursa ya ujenzi wa Hoteli za kitalii ili kuwavutia watalii kutembelea katika kisiwa hicho.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwaka jana kwa Wizara hiyo  kuwa ianzishe Kurugenzi ya Fukwe itakayokuwa na jukumu la kusimamia na kuendeleza  Fukwe zote nchini.

Lengo likiwa ni kuhakikisha mapato yatokanayo na sekta ya Utalii kupitia Utalii wa Fukwe yanaongezeka kwa mfano Kisiwa cha Mafia ni cha tano duniani kwa uzuri wa vivutio vya utalii na rasilimali bahari na  cha pili barani Afrika, Hivyo kina sifa kemkem za kuongeza pato la Taifa zaidi.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya siku mbili kisiwani humo ya kutembelea Fukwe pamoja na magofu ya kale,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu  amesema Wizara imejipanga kikamilifu kwa ajili kuwasaidia  Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye Fukwe kwa ajili ya utalii.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Kanyasu alitembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii vilivyopo kisiwani humo ukiwemo Msitu wa Mlola, Magofu na fukwe katika kijiji cha Kanga  pamoja na maeneo ya uwekezaji ya Ras Mlundo Jojo, Banja, Rasini Kanga na Tembo Unyama.

Hata hivyo, Baada ya ziara hiyo Naibu Waziri huyo alisema kuwa baadhi ya wamiliki wa maeneo hayo ya fukwe yamefanya kuwa mashamba ilhali ni kivutio kikubwa cha utalii ambapo baadhi ya nchi zimekuwa ziikingiza fedha nyingi za kigeni kupitia utalii wa fukwe.

Aidha, Kanyasu amewataka wananchi wanaomiliki maeneo karibu na Fukwe kuyatumia kwa ajili ya utalii wa fukwe  badala ya kuyageuza kuwa  mashamba.

Amesema kuwa watalii walio wengi kutoka nje za nchi mara baada ya kutembelea Hifadhi za Taifa kama vile Serengeti Mikumi, husafiri kwenda Msumbiji au Zanziba' kwa ajili ya kutembelea Fukwe ilhali kuna fukwe nzuri mbali na Kisiwa cha Mafia ambazo hazijaweza kuendelezwa

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaib Nnunduma alieleza kuwa wilaya yake inawakaribisha Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika wilaya hiyo na kuahidi kuwa atatoa ushirikiano wa kutosha.

Aliongeza kuwa Wilaya hiyo tayari imeshatenga maeneo kwa ajili ya Wawekezaji kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli za kiutalii katika maeneo ya ufukweni.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ( watatu kulia)  akiwa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama akipewa maelezo na Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi, Maliasili na Utalii, Juma Hassan kuhusu eneo la fukwe lililotengwa kwa ajili ya  uwekezaji  wa  ujenzi wa Hoteli za kitaliii wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwa ajili ya kuhamasisha utalii wa Fukwe katika wilaya ya Mafia mkoani Kibaha. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mohammed Kongo wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea maeneo ya fukwe ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwaka jana kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa 
ianzishe Kurugenzi ya Fukwe 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Constantine Kanyasu akishuka kwenye ndege  ndogo wakati alipowasili  wilayani Mafia mkoani Kibaha  kwa ajili ya kutembelea maeneo ya fukwe kwa ajili ya uwekezaji wa Utalii
 Baadhi ya rasilimali bahari maarufu kwa jina la  Matumbawe ambayo ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika kisiwa cha Mafia mkoani Kibaha
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu (  kulia)  akiwa ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Mafia pamoja na kamati ya ulinzi na usalama  wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya fukwe yanayofaa kwa ajili ya uwekezaji lengo likiwa ni kuhasisha utalii wa fukwe 
 Moja ya magogfu ya kale lililojengwa karne ya 18 ambalo linapatikana pembezoni mwa fukwe katika kisiwa cha Mafia mkoani Kibaha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mafia. Erick Mapunda akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu kabla hya kufanya ziara ya kutembelea maeneo ya fukwe kwa ajili ya uwekezaji wa utalii.  

  (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images