Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

JUMLA YA WAGONJWA 19 WAPANDIKIZWA FIGO NDANI YA MIEZI 5

0
0
Na WAMJW - DODOMA

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa katika kipindi cha Mwezi Julai 2018 hadi Desemba 2018 jumla ya wagonjwa 19 walipata huduma ya upandikizwaji wa figo, hivyo kufikisha jumla ya wagonjwa 28 waliopata huduma hii toka Hospitali ilivyoanza kutoa huduma za kupandikiza figo mwezi Novemba 2017. 

Amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Wizara ya Afya mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imeokoa jumla ya shilingi bilioni 2.24, ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa 28 nje ya nchi kupata matibabu yakupandikizwa figo.

"Gharama ya huduma hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kati ya shilingi milioni 20 mpaka 30 kwa mgonjwa mmoja wakati nje ya nchi gharama hii ni kati ya shilingi milioni 100 mpaka 120. Serikali imeokoa jumla ya shilingi bilioni 2.24 ambazo zingetumika kwaajili ya matibabu hayo nje ya nchi" Alisema Waziri Ummy.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili iliona jumla ya wagonjwa 30,189, Idara ya Utengamano ilihudumia wagonjwa 22,379, huku Idara ya Madawa ilihudumia maombi ya dawa 519,216 na Kitengo cha Figo kilitoa huduma za kusafisha damu kwa mizunguko 13,248, huku Jumla ya wagonjwa mahututi 960 walihudumiwa katika ICU za Hospitali. 

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa Katika kipindi cha Mwezi Julai 2018 hadi Disemba 2018 Hospitali imetoa huduma za kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 11 na kufikisha jumla ya watoto 21 waliopata huduma hii toka ilipoanza mwezi Juni, 2017, jambo lililosaidia kuokoa zaidi ya shilingi milioni 840 ambazo zingetibu watoto 21.

"Kabla ya hapo huduma hii ilikuwa inapatikana nje ya nchi kwa gharama kati ya shilingi milioni 80 mpaka 100 kwa mtoto mmoja, huku Hospitali ya Taifa Muhimbili gharama nishilingi milioni 35 mpaka 40" alisema Waziri Ummy.

Wakati akijibu maswali ya Wabunge wa kamati hiyo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Taasisi ya Moyo (JKCI) imeweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 211, kati ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, watu wazima walikuwa 89 na watoto walikuwa 60, huku watu wazima 62 wenye matatizo kwenye mishipa ya damu walifanyiwa upasuaji wa mishipa ya damu.

Aidha, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa, wagonjwa 521 walipatiwa matibabu ya upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwa upande wa mtambo maalum (catheterization laboratory).
 

MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati), mara baada ya kuwasili katika daraja la Dumila lililoathirika na mvua zilizonyesha usiku wa tarehe 15/1/2019 na kuvunja maingilio ya daraja hilo mkoani Morogoro.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Ntenga, akimueleza Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, hatua zilizochukuliwa na wakala huo katika matengenezo ya maingilio ya daraja la Dumila lililoathirika na mvua zilizonyesha usiku wa tarehe 15/1/2019, mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitazama athari za mvua zilizonyesha na kuharibu sehemu ya maingilio daraja la Dumila, mkoani Morogoro.
Kazi za ujazaji wa mawe na kokoto zilizokuwa zikifanyika katika kurekebisha athari za mvua zilizonyesha na kubomoa maingilio ya daraja la Dumila, mkoani Morogoro. Daraja hilo liko katika hatua za usanifu wa kina wa kuongeza tuta la daraja hilo.
Magari yakionekana kupita katika daraja la Dumila ambalo liliathirika na mvua zilizonyesha usiku wa tarehe 15/1/2019, na kukata mawasiliano katika mkoa wa Morogoro na Dodoma kwa takriban saa 7.


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, amewahakikishia wananchi na watumiaji wa barabara ya Morogoro-Dodoma kuwa mawasiliano ya barabara hiyo sehemu ya maingilio ya daraja la Dumila yamerudi kama ilivyokuwa awali.

Kauli hiyo ameitoa leo mkoani Morogoro, alipofika darajani hapo kujionea athari za mvua zilizosababisha kubomoka kwa daraja hilo na wananchi kushindwa kutumia barabara hiyo kwa takriban masaa saba. 

"Kama mlivyoshuhudia tangu asubuhi tumeanza kazi za kurudisha mawasiliano katika barabara hii, matengenezo yakamilika na wananchi tayari wameshaanza kutumia barabara", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, ameupaongeza Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Morogoro, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kampuni ya ujenzi ya Yapi Merkez na wadau wote waliojitokeza katika kuhakikisha wanashirikiana bega kwa bega ili kurudisha mawasiliano katika eneo hilo.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanakuwa imara, Serikali ipo katika mpango wa kuboresha barabara hiyo ambapo kwa sasa wataalam wanafanya usanifu wa barabara hiyo na pindi usanifu huo utakapokamilika basi ujenzi wake utaanza mara moja na wataanza na sehemu korofi.

Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri huyo, Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe, amesema kuwa uongozi wa mkoa ulifika eneo la tukio na kuanza kushirikiana na TANROADS mkoa kuhakikisha miundombinu hiyo inarejea mapema.Amewataka wananchi kujitolea kupanda matete na magugu maji katika eneo hilo ili kuelekeza maji yanayopita katika mto huo kuelekea sehemu husika.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Ntenga, amesema kuwa kazi zilizokuwa zikifanyika katika maingilio ya daraja hilo ilikuwa ni kuweka mawe makubwa na kokoto sehemu iliyobomoka.Amefafanua kuwa kutokana na sehemu hiyo kuwa na maji mengi na mchanga mwingi, wamefikiria kufanya usanifu wa daraja hilo utakaoleta suluhisho la kudumu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

SERIKALI IMEAGIZA WAVUVI WOTE WALIOKAMATWA KWA KOSA LA KUTOHUISHA LESENI ZAO ZA UVUVI NA VYOMBO VYAO KWA MWAKA 2019, WAACHIWE

0
0

TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TANZANIA (TFNC) INAJIVUNIA MIAKA MITATU YA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Imeelezwa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano, Taifa limefanikiwa kuimarisha huduma za lishe ikiwemo kuongeza bajeti ya lishe kuanzia ngazi ya Mikoa na Halmashauri. 

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dkt. Vincent Assey wakati akiongea na maafisa habari/mawasiliano na uhusiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na taasisi zake kwenye kampeni ya "Tumeboresha Afya" .

"Serikali imeziagiza halmashauri zote nchini kuongeza fedha zinazotengwa kugharamia huduma za lishe kutoka shilingi 500 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka 5 iliyokuwa inatengwa mwaka 2015/16 hadi shilingi 1,000 mwaka 2018/19. 

Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 Serikali imetumia shilingi bilioni 11. Hiki ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutumiwa katika historia ya utoaji wa huduma za lishe hapa nchini katika kipindi cha mwaka mmoja wa fedha" alisema Dkt. Assey.

Pia, amesema kwamba Serikali imeendelea kuimarisha huduma ya utoaji wa vidonge vya vitamini A ya nyongeza na dawa za kutibu minyoo kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5. Huduma hii inatolewa mara mbili kwa mwaka. Hadi kufikia mwezi Juni 2018 asilimia 96 ya watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 nchini walipatiwa vidonge vya vitamini A ya nyongeza ili kuimarisha kingamwili dhidi ya magonjwa na kuboresha uwezo wa macho yao kuona vizuri

Aidha Dkt. Assey amesema kupitia viwanda, Serikali imefanikiwa kuboresha lishe za watanzania kwa kuviwezesha viwanda vinavyosindika vyakula kuongeza virutubishi muhimu ikiwemo Vitamini A na D kwenye mafuta ya kula, madini chuma na vitamini ya asidi ya foliki katika unga wa mahindi na unga wa ngano. 

Vitamini A huimarisha kingamwili inayosaidia kudhibiti magonjwa mwilini, vitamini D inasaidia kuimarisha afya ya mifupa. Madini chuma yanayosaidia kuongeza wingi wa damu mwilini na vitamini ya asidi ya foliki inayosaidia pia kuongeza damu mwilini na kuzuia tatizo la watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vikubwa, mgongo wazi na midomo iliyopasuka (mdomo sungura).

Vilevile Serikali imewawezesha wazalisha chumvi kuongeza madini joto kwenye chumvi ili kutokomeza tatizo la upungufu wa madini joto mwilini. Kwa kudhibiti tatizo la upungufu wa madini joto mwilini Taifa linadhibiti kasi ya mimba kuharibika, watoto kufariki wakiwa tumboni, pamoja na kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa na mtindio wa ubongo/taahira na ulemavu wa viungo. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe, Sikitu Saimon ameeleza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imeboresha vitendea kazi vya kutolea elimu ya lishe kwa umma kwa kutumia mfuko wa siku 1000, unaotumika katika ngazi ya jamii kuhamasisha matunzo bora ya mama mjamzito, mama anayenyonyesha, na mtoto mchanga kuanzia wakati wa kuzaliwa hadi anapotimiza umri wa miaka miwili.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dkt. Vincent Assey akielezea mafanikio ya lishe nchini katika miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe na Magufuli, wakati wa kampeni ya "Tumeboresha Sekta ya Afya" inayoendeshwa na maafisa habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na taasisi zake.

MSHINDI WA PROMOSHENI YA TBL KUMENOGA TUKUTANE BAA APATIKANA

0
0

Meneja wa huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kumtafuta mshindi wa tatu wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. ambapo mkazi wa Arusha George Issaya (29) aliibuka mshindi wa gari aina ya Renauld Kwid. Droo hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kutoka Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Adam Kefa, na msimamizi wa michezo ya Kubahatisha nchini ,Majid Bakari.
Meneja wa huduma za Masoko wa TBL,David Tarimo (wapili kushoto) akipofya kitufe cha Komputa wakati wa kumtafuta mshindi wa tatu na wa mwisho wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. ambapo mkazi wa Arusha George Issaya (29) aliibuka mshindi wa gari aina ya Renauld Kwid. Droo hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kutoka Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Adam Kefa, Meneja wa huduma za Jamii wa Aim group, Aidan Mattaka na msimamizi wa michezo ya Kubahatisha nchini ,Majid Bakari.
Meneja wa huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo (kushoto) akiongea na George Issaya (29) mkazi wa Arusha mara baada ya kuibuka mshindi wa gari aina ya Renauld Kwid. Wakati Droo ya tatu ya promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa huduma za Jamii wa Aim group, Aidan Mattaka na msimamizi wa michezo ya Kubahatisha nchini, Majid Bakari.


Droo kubwa ya mwisho ya promosheni ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha, George Isaya (29) amejishindia gari mpya aina ya Renault KWID. Isaya akiongea baada ya kupigiwa simu na Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, kumfahamisha kuwa ameibuka mshindi, alisema anayo furaha kufanikiwa kuwa miongoni mwa washindi kupitia promosheni hiyo kwa kujishindia gari mpya.

“Sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, Habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru TBL kwa kunifungulia mwaka vizuri na kutimiza ndoto yangu ya kumiliki gari “alisema kwa furaha. 
 
Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, kwa niaba ya kampuni ya TBL, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za magari 3 mapya ambayo yalitolewa na kampuni hiyo.

“Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka kumpata mshindi wa tatu wa zawadi kubwa ya mwezi ambayo ni gari mpya. Tunawashukuru wateja wetu kutoka nchini pote walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi uliopita”. alisema Tarimo.

Aliongeza kuwa, promosheni hii ambayo ilikuwa inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa juma za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, kupitia bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager imepata mafanikio makubwa kutokana na wateja wengi kujitokeza kushiriki na baadhi yao kufanikiwa kujishindia zawadi mbalimbali na hivyo TBL kufanikisha lengo lake ambalo lilikuwa ni kuwashukuru wateja kwa kuiunga mkono kampuni kupitia kununua bidhaa zake.

Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, aliwashukuru wateja wote wa TBL kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni hiyo zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.

JIJI LA DAR ES SALAAM LINAVYOONEKANA LEO UKIWA JUU

0
0
 Picha ya Jiji la  Dar es Salaam upande wa Bandari inayoonekana
 Picha ya Jiji la Dar es Salaam linavyoonekana katikati ya jiji na vikwangua anaga vinavyongara.
 Picha ya Jiji la Dar es Salaam kwa upande wa Magharibi inavyooenekana kuelekea Old Bagamoyo Road
 Upande wa Mashariki ya Jiji la Dar es Salaam inavyoonekana na Fukwe zake
City Centre 

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 17,2019

0
0
































KAULI YA DC MUHEZA YAMNUSURU MKUU WA IDARA YA ARDHI KUTUMBULIWA

0
0
Na Munir Shemweta, MUHEZA

Kauli ya Mkuu wa wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga Hajjat Mhandisi Mwanaasha Tumbo kuwa idara ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Muheza haina mtendaji wa sekta ardhi anayeweza kuvaa viatu vya ukuu wa idara iwapo anayeshikilia sasa nafasi hiyo Salehe Kang'e ataondolewa imemnusuru mkuu huyo wa sekta ya ardhi kutumbuliwa katika nafasi yàke.

Kauli hiyo inafuatia Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula kueleza kuwa Mkuu wa Idara ya Ardhi katika halmashauri hiyo hafai kuwa mkuu wa idara kutokana na kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji mapato yatokanayo na kodi ya ardhi.

Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Bakari Mhando alimuomba Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutomuondoa katika nafasi hiyo mkuu huyo wa Idara na kubainisha kuwa mapungufu aliyoyaonesha atahakikisha yanarekebishwa ndani ya mwezi mmoja.

Akiwa katika ziara ya kustukiza katika halmashauri ya wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga tarehe 15 Januari 2019 Dk Mabula alionesha kuchukizwa na mkuu huyo wa idara kushindwa kusimamia ukusanyaji kodi ya ardhi ikiwemo kutoa hati za madai kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi katika wilaya ya Muheza.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Ardhi halmashauri ya wilaya ya Muheza Kang'e ambaye amebakiza mwaka mmoja kustaafu kazi, halmashauri ya wilaya yake imeingiza viwanja 3000 katika mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya kielektronik na mashamba 1009 lakini imetoa hati moja ya madai kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi.

Dk Mabula alisema alichotegemea baada ya kuingizwa viwanja na mashamba kwenye mfumo huo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektronik mkuu wa idara ya ardhi angehakikisha wadaiwa wote sugu wanafuatiliwa ili walipe kodi lakini kinyume chake kazi hiyo haijafanyika na ni mdaiwa mmoja tu aliyepelekewa hati ya madai.

Alisema msisitizo wa serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inakusanya mapato yakiwemo ya kodi ya ardhi ili kuweza kusaidia shughuli za maendeleo ambazo haziwezi kupatikana iwapo serikali haitakuwa na makusanyo mazuri ya kodi.

" Haya yote yanayofanyika ununuzi wa ndege ujenzi wa SGR bila ya kukusanya kodi hayawezi kufanyika na siku zote Rais wa Janhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amekuwa akisisitiza ukusanyaji kodi, people are not serious" alisema Dk Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitoa mwezi mmoja kwa Mkuu huyo wa Idara ya Ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Muheza kuhakikisha wadaiwa wote wa kodi ya ardhi wanapelekewa hati za madai na watakaokaidi wafikishwe katika mabaraza ya ardhi na ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Kaskazini ifuatilie utekelezaji wa agizo hilo.

Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajjat Mhandisi Mwanaasha Tumbo alisema, baada ya maelekezo ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alihakikisha utekelezaji unafanyika na matunda yameanza kuonekana katika baadhi ya maeneo ya sekta ardhi ikiwemo uingizaji wamiliki wa viwanja na mashamba katika mfumo na amemuahidi Dk Mabula kuwa suala la hati za madai nalo atalisimamia kikamilifu ilii liweze kutekelezwa.

Alisema, changamoto kubwa inayoikabili halmashauri ya wilaya ya Muheza ni kukosekana watendaji wa sekta ya ardhi wenye uwezo mkubwa wa kusimamia masuala ya ardhi na kubainisha kuwa mbali na mkuu wa idara aliyepo sasa lakini halmashauri hiyo haina watendaji wa kutosha. 
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halamashauri ya Wilaya ya Muheza Salehe Kang'e wakati wa ziara ya kushtukiza kufuatilia maagizo aliyoyatoa katika halmashauri hiyo jana. kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajjat Muhandisi Mwanaasha Tumbo.
 Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajjat Muhandisi Mwanaasha Tumbo akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akimpa maelekezo Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halamashauri ya wilaya ya Muheza Salehe Kang'e alipofanya ziara ya kushtukiza katika halmashauri hiyo jana.

QNET YAIPONGEZA CAF,KLABU ZA MPIRA WA MIGUU AFRIKA KATIKA MASHINDANO YA MPIRA YA CAF 2018

0
0
Kampuni inayoongoza ya mauzo ya moja kwa moja QNET, na mbia katika ligi ya mabingwa ya CAF, Kombe la Shirikisho la CAF na kombe la Super Cup imewapongeza Shirikisho la Soka Afrika, CAF na vilabu vyote vinavyoshiriki katika mashindano yote ya klabu ya CAF mwaka 2019. 

QNEt imekaribisha ushirikiano wake na CAF, katika mwaka 2018 na inaelezea fahari yake katika mpira wa miguu wa Afrika. 

Ushirikiano kati ya kampuni ya QNET na CAF ni sehemu ya juhudi za QNET za kukuza michezo Afrika na dunia kote.Kwa kweli, kama ilivyo katika michezo, QNET inaongozwa na ari ya kufanya kazi kwa pamoja kama timu pamoja na shauku wakati inapofanya biashara zake kila siku. 

Ushirikiano huu ni fursa nyingine kwa QNET kuwa karibu na wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs), walaji na wateja ambako QNET inaendesha shughuli zake tangu zaidi ya muongo mmoja iliopita. 

Meneja Mkuu wa QNET wa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, Biram Fall amesema kwamba, “Mwaka uliopita ulikuwa ni mwaka mzuri kwa mpira wa miguu barani Afrika. Katika QNET tunaona fahari sana kujihusisha na CAF na ukuaji wa mchezo wa mpira wa miguu barani. Falsafa ya biashara yetu inashikilia mwenendo wa mpira wa miguu, ambao kimsingi ni ufanyaji wa kazi katika timu, ushirikiano, shauku na kufanyakazi kwa bidii. 

Tunawawezesha wajasiriamali katika bara zima la Afrika na tumejikita katika kusaidia wengi zaidi waweze kufanikiwa. Vilevile ni heshima kwetu kudhamini mashindano haya maarufu na yanayoheshimiwa sana, na tusingeweza kupata mshirika bora zaidi kuliko Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuweza kufanikisha lengo hili. Mwaka 2019 unaonekana kutia matumaini zaidi na QNET itakuwa katika upande wa CAF kwaajili ya kuhakikisha utendaji bora zaidi”. 

Katika mwaka 2019, QNET itakuwepo zaidi viwanjani ikiwa na uhamasishaji, matukio zaidi kwaajili ya kuhamasisha mashabiki kuongeza nguvu kazi ya mauzo ya QNET na wawakilishi wa kujitegemea (IRs). 

QNET inaendelea kuongeza uwepo wake katika bara zima la Afrika, ikiwa inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na kusaidia watu kubadili historia zao vyema zaidi. Ukiachilia mbali ushirikiano wa kimichezo, QNET pia ni kampuni ambayo inajihusisha na majukumu ya kijamii, kutoa kwaajili ya maendeleo endelevu ya jamii katika kanda zote ambako inaendesha shughuli zake. Katika mwezi Novemba, kampuni ya QNET ilitunikiwa tuzo ya mwaka ya e-commerce CSD Company na Kituo cha Uwajibikaji kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for Corporate Social Responsibility West Africa).
Pichani kulia shoto ni Meneja Mkuu wa QNET wa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, Biram Fall akiwa na mchezaji bora  (Afrika) wa zamani 20o1 kutoka nchini Senegal El Hadj Diouf

SPIKA NDUGAI ASEMA ZITTO ANAMUUMIZA SANA KICHWA

0
0
*Akiri kumuonea huruma kwani bungeni yupo peke yake,amshangaa kupotosha umma

*Apigilia msumari kwa CAG Profesa Assad,asema asipofika atajua nani muajiri wake

Na Said Mwishehe,Blogu ya jamii

SPIKA wa Bunge Job Ndugai ametoa msimamo wake kwa mara nyingine kuhusu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG) Profesa Mussa Assad kuwa lazima atafika kwenye Kamati ya Haki,Kinga na Madaraka ya Bunge Maadili huku akieleza kuwa moyo wake unapata taabu sana kwa Mbunge wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe.

Akizungumza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine Spika amemzungumzia Zitto kwa kueleza kuwa amekuwa akipotosha umma kuhusu kinga ya CAG."Kuna rafiki yengu mmoja yupo Uganda , kule Uganda CAG ni Ofisa wa Bunge,na Ofisa wa Bunge anaweza kumgomea Spika? Mihimili iko mitatu na niwahakikishie CAG hiyo tarehe 21 atakuja tu.

"Wengi ambao wanaongea kuhusu hili anajua wanatoka upande gani,wapinzani wengi wao wanawaza kupinga tu," amesema Spika Ndugai na kufafanua kama nchi kuna fedha nyingi zinatumika Ubalozi wa Tanzania nchi Marekani kwa ajili ya kuitangaza nchi lakini anatoka Ofisa wa Serikali anakwenda nje kuisema nchi.

"Huwezi kutoka hapa halafu unakwenda kuisema nchi vibaya.Kazi yetu sote ni kuhakikisha nchi inakaa vizuri," amesema Spika Ndugai huku akisema anasikitishwa na namna Zitto anavyopotosha umma."Zitto amekuwa akinipa tabu sana ,niseme tu kutoka moyoni.Pale Bungeni inakuwa rahisi kuwafukuza wabunge wengine wanapofanya makosa maana hata ukiwafukuza wengine wapo lakini Zitto kwenye Chama chao mbunge ni mmoja.

" Hivyo naamua kumuacha tu kwa kutumia busara lakini ukweli huko mbele ya safari nitachoka na niyamchukulia hatua.Bungeni pale watu wanashindana kwa hoja na inaungwa mkono na wabunge wengine."Ndio maana wabunge wakiunga mkono wanne ujue hilo jambo linatupwa na Zitto anakwama kwasababu hana wa kumuunga mkono katika mambo yake,"amefafanua Spika Ndugai.

Ameeleza kwa sasa wabunge wengine wako Dodoma wakiendelea na Kamati za Bunge lakini Zitto yupo Dar es Salaam anahangaika kwenye korido kuhusu kuupinga muswada wa vyama vya siasa." Muswada unaendelea kama kawaida, na ukifika Bungeni utapitishwa .Zitto alitakiwa kuwa kule ili atoe maoni yake ili yafanyiwe kazi,"amesema Spika.

Akifafanua zaidi kuhusu kumuita Mdhibiti na Mkagazi wa Hesabu za Serikali kwenye kamati, amesisitiza lazima aende kuhojiwa na kamati husika na nia njema tu kwani kabla ya kuchukua hatua lazima utoe haki kwa mhusika kupata nafasi ya kujieleza na asipofika atajua nani muajiri wake.

WAZIRI BITEKO AKUTANA NA WAWEKEZAJI WENYE NIA YA KUFUNGUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NCHINI KWA KIWANGO CHA ASILIMIA 99.5.

0
0
Na Samwel Mtuwa - Dodoma

Waziri wa madini Mh Doto Biteko leo tarehe 17/01/2019 amekutana na wawekezaji wa kiwanda cha Nyakato Gold Refinery (NGR) ofisini kwake jijini Dodoma , wenye nia ya kufungua kiwanda cha kusafisha madini ya dhahabu kwa kiwango cha asilimia 99.5 kwa lengo la kuongeza thamani pamoja na kuboresha soko la dhahabu nchini inayotoka kwa wachimbaji wadogo na wakati. 

Kabla ya majadiliano kuanza waziri Biteko alipokea taarifa juu ya namna ya kiwanda hicho cha NGR kitakavyofanya kazi ya ununuzi na usafishaji wa dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo na wakati, ambapo baadhi ya mapendekezo yaliyowasilishwa na NGR ni juu ya matarajio ya usafishaji wa dhahabu kwa kiasi cha kg50 kwa siku na tani 1.5 kwa mwezi. 

Baada ya majadiliano hayo waziri amewataka wawekezaji hao kuandaa na kuwasilisha andiko la mpango mkakati wa wazi utakaonesha namna uendeshaji wa kiwanda hicho utakavyofanyika ikiwa pamoja na namna serikali itakavyofaidika na uwekezaji huo ndani ya sekta ya madini. 

Tanzania ni nchi ya nne barani afrika katika uzalishaji wa madini ya dhahabu ikiongozwa na nchi ya Ghana naAfrika kusini . 

Pichani waziri wa madini Mh Doto Biteko mwenye suti ya rangi ya Blue aliyekaa mbele akiwa ofisini kwake jijini Dodoma akiongea na wawekezaji wenye nia ya kufungua kiwanda cha kusafisha dhahabu kitakachojulikana kwa jina la Nyakato Gold Refinery (NGR), wengine waliyekaa upande wa kushoto mwekezaji mwenye asili ya India Vaya Rajendra, anayefuata pembeni upande wa kulia ni Baraka Ezekiel yeye ni muhamasishaji kutoka NGR, wengine waliokaa upande wa kulia katika sofa ni watendaji kutoka wizara ya madini pamoja na Tume ya Madini wakifuatilia majadiliano.

Tanzania kushiriki Maonesho ya Biashara ya Dunia ya EXPO 2020

0
0
Tanzania itashiriki Maonesho ya Dunia ya Biashara (Expo 2020 yatakayofanyika Dubai kuanzia mwezi Oktoba 2020 na kumalizika mwezi April 2021.

Uwekaji saini wa Mkataba wa ushiriki wa Tanzania katika Maonesho hayo ulifanywa tarehe 16 Januari 2019 na Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.

Kwa upande wa UAE, mkataba huo uliwekwa saini na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali.

Baada ya uwekaji saini wa Mkataba huo, Mhe. Balozi Mbarouk alieleza kuwa Serikali inayapa umuhimu mkubwa maonesho hayo kwa kuwa ni fursa adhimu ya kuitangaza Tanzania kwenye sekta za uwekezaji, biashara, viwanda, utalii na mila na utamaduni.

Aidha, Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020 alieleza kuwa amefurahishwa na hatua ya Tanzania kusaini Mkataba huo ambapo itatoa fursa kwa nchi kujiandaa mapema na taratibu nyingine za ushiriki.

Baada ya uwekaji saini wa Mkataba huo,` kitakachofuata ni utayarishaji wa simulizi ya maudhui ya maonesho (pitch story) ambayo inatakiwa kuthibitishwa na Kamati ya Kitaifa ya Tanzania ya DUBAI Expo 2020. Simulizi ya maudhui hayo yatahusu vipaumbele vya Tanzania kama vile maendeleo ya viwanda, miundombinu, masuala ya biashara na uwekezaji, utalii, kilimo, elimu, afya, sanaa na utamaduni. Simulizi ya maudhui pia itatumika katika kusanifu muonekana wa banda la maonesho la Tanzania.

Tanzania inakuwa miongozi mwa nchi washiriki zipatazo 100 ambazo tayari zimesaini Mkataba wa Ushiriki tangu Dubai ilipochaguliwa kuwa mwenyeji wa maonensho hayo.Wengine walioshuhudia uwekaji saini wa Mkataba huo ni Bw. Ali Jabir Mwadini, Kansela Mkuu, Ubalozi Mdogo wa Tanzania, Dubai; Bi Samira Ahmed Diria, Afisa Ubalozi; na kwa upande wa DUBAI EXPO 2020 ni Bi Manuela Garcia Pascual, Mkurugenzi wa Washiriki wa Kimataifa na Bi. Esther Omondi, Meneja wa Nchi/Afisa dawati la Tanzania. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma.
17 Januari 2019

 
Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakiweka saini Mkataba wa ushiriki wa Tanzania katika Maonesho ya Biashara ya Dunia (Dubai Expo 2020. Uwekaji saini huo ulifanyika Dubai jana Januari 16, 2019. 
 
Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakionesha Mkataba mara baada ya zoezi la kuweka saini kukamilika.
 
Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wao. 
 
Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakibadilishana mawazo mara baada ya zoezi la kuweka saini kukamilika.

WAZIRI WA KILIMO AIAGIZA BODI YA TUMBAKU KUHAKIKISHA TUMBAKU YOTE ITAKAYOVUNWA MSIMU HUU INAUZWA

0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisiitiza jambo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi - Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Agrey Mwanri akitoa taarifa ya Mkoa huo mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kabla ya kufungua mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. 
Mzee Hassan Wakasuvi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa bodi ya Tumbaku akitoa maelezo ya awali kuhusu Tumbaku wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. 
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Shinyanga (KACU) na baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi - Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. 


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Tabora


Bodi ya Tumbaku nchini imeagizwa kuhakikisha kuwa Wakulima wote wa zao hilo wanasajiliwa katika mfumo unaoeleweka kwani hilo ni lengo la haraka la Wizara kwa taasisi zote la kuwasajili wakulima wote nchini ili kujua kiasi cha maeneo wanayolima.

Hayo yameelezwa leo tarehe 17 Januari 2019 na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Mhe Hasunga ameitaka Bodi ihakikishe kwamba tumbaku yote itakayovunwa msimu huu inauzwa ifikapo Juni 2019 sambamba na kuagiza masoko kuwahi kuanza msimu huu ili kurahisisha kuanza mapema maandalizi ya zao hilo msimu wa 2019/2020.

Vilevile Waziri Hasunga ameagiza upatikanaji wa pembejeo kwa wakati. “Hili linaenda sambamba na utekelezaji wa Agizo la Mhe: Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) - Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuhakikisha unakuwepo utaratibu wa kumwezesha mkulima anajitegemea kwa pembejeo ili aache kuwa tegemezi wa mikopo ya mabenki” Alikaririwa Mhe Hasunga

Mhe Hasunga alisisitiza kuwa lazima Bodi kutilia mkazo malengo ya muda mrefu kwenye Tumbaku ambayo ni pamoja na utafutaji wa masoko (mhakikishe mnapata wanunuzi wengine wapya ifikapo 2022), Kuhakikisha kuwa kwa ubia au ushirikiano uliopo kijengwe kiwanda kipya cha kuchakata tumbaku ili kutoa ushindani wa gharama za uchakataji wa tumbaku nchini, Kuongeza ubora wa zao kutoka asilimia 87 ya sasa hadi asilimia 92 ifikapo June 2022 na Kuongeza mbegu mpya na bora za tumbaku ili kuweza kupenyeza katika masoko ya nchi zingine kama China n.k.

Tumbaku ni miongoni mwa mazao makuu matano ya kimkakati ya biashara katika Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe: Dkt. John Joseph Pombe Magufuli – Rais waJamhuri ya Muunganowa Tanzania. Mazao hayo ni Tumbaku, Kahawa, Pamba, Korosho, na Chai. Takwimu zinaonesha kwamba kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 hadi kufikia mwaka 2016 tumbaku imekuwa na mchango mkubwa kuliko mazao mengine makuu ya biashara kwa kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni. 

“Natambua juhudi mnazofanya katika hifadhi ya mazingira. Lakini mnatakiwa muongeze juhudi kwani taarifa zinaonesha kuwa hadi kufikia msimu wa kilimo uliopita wa 2017/2018 wastani wa miti iliyopona baada ya kupandwa na wakulima ni asilimia 40.46 tu, kiwango hiki hakiridhishi maana kiko chini mno” Alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema Ili uzalishaji wa tumbaku uwe katika mtazamo wa kibiashara wataalam mnapaswa kuwaelimisha wakulima ili waelewe kwa dhati umuhimu wa kuzingatia taratibu za kilimo cha tumbaku (Compliance). 

Alisema kuwa Baadhi ya wakulima katika vyama vya msingi vya ushirika wameshindwa kulipwa malipo yao kutokana na vyama kuwa na madeni yasiyokuwa wazi na yasiyolipika. Hali hii imesababishwa na ubadhirifu wa baadhi viongozi na watendaji wasio waaminifu katika ushirika, utoroshaji na ulanguzi wa tumbaku. 

Moja ya maeneo yanayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na masuala yanayohusu hatua za kutatua changamoto za kulikomboa zao la tumbaku na kulipa sifa zinazohitajika katika soko la dunia. Mfano wa masuala hayo ni pamoja na Wingi na ubora wa zao, Kuongeza tija, Malipo stahili kwa wakulima, Utunzaji wa Mazingira na Kuzuia utumikishwaji wa watoto.

Kupitia mkutano huo Waziri wa Kilimo amebainisha kuwa Serikali iko thabiti kusimamia uendelevu na uzalishaji wenye tija wa zao la tumbaku kama zao mojawapo la biashara la kimkakati. Ni kwa msingi huo, Serikali inaendelea na jitihada za kupata ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili tasnia ya tumbaku.

“Tarehe 28-30/12/2018 niliwaita viongozi wa Bodi za mazao ikiwa ni pamoja na Bodi ya Tumbaku na kuwapa malengo ya muda mfupi (Januari - Juni, 2019) na mrefu (Julai - Juni, 2022) ni pamoja na nyie wadau katika nafasi zenu mshirikiane ili kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa” Alisisitiza

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Agrey Mwanri alisema kuwa mkutano huo maalumu wa mwaka wa wadau wa Tumbaku ni mkutano ambao upo kwa mujibu wa sharia ya sekta ya Tumbaku Na 24/2001 kifungu cha 49 cha marekebisho ya sheria yam waka 2009 ambao imeweka ulazima wa wadau kukutana walau mara moja kwa mwaka kujadili masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta hii na kutatua changamoto zilizopo na kukubaliana utaratibu wa ugharamiaji wa majukumu ya pamoja ambayo yameainishwa na sharia ya sekta ya Tumbaku.

Alisema uwepo wa mkutano huo umekuwa miongoni mwa mikutano yenye tija kwa kukutanisha madau wote na kuwa na mikakati ya pamoja, kuongeza ufanisi wa masoko ya Tumbaku, na uhai wa kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa pamoja.


Kwa upande wake Mzee Hassan Wakasuvi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa bodi ya Tumbaku akitoa taarifa ya utangulizi wakati wa mkutano huo alizitaja changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Tumbaku kuwa ni pamoja na kutokuwepo kwa mkakati utakaotekeleza na shirikishi wa uhifadhi wa mazingira, kuchelewa kwa upatikanaji wa mikopo ya pembejeo kwa ajili ya kununua pemebejeo za kilimo.


Zingine ni utaratibu wa upatikanaji wa bei ya zao la Trumbaku katika kuhakikisha kuwa bei inapatikana mapema na kwa wakati, kushuka kwa mahitaji ya Tumbaku katika soko la Dunia, Kushuka kwa ubora wa Tumbaku ambao unachangiwa na masuala mbalimbali, Vita dhidi ya matumizi ya Tumbaku Duniani na kuboreka kwa bei ya pembejeo.


Sambamba na hayo pia ameishukuru serikali kwa mchango wake kwenye sekta ya Tumbaku kwa ushirikiano inaouonyesha katika suala la kuhakikisha kuwa wanapatikana wasambazaji wa pembejeo za kilimo na kufanikiwa kupunguza bei ya pembejeo za kilimo kwa msimu wa mwaka 2018/2019.

Rais Dkt.Magufuli Mgeni Rasmi makabidhiano ya mfumo wa mawasiliano ya simu (TTMS

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

RAIS John Pombe Magufuli kesho anatarajia kuwa mgeni rasmi katika makabidhiano ya Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) unaosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), ambao pamoja na mambo mengine mfumo huo utahakiki mapato yote ya watoa huduma za mawasiliano na kugundua mawasiliano ya simu ya ulaghai.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alisema shughuli za kiuchumi zinazohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) zimeongezeka na zinaendelea kuongezeka kwa kasi nchini hivyo kunahitajika kuwepo kwa mifumo mahiri ya usimamizi kama huo. 

Amesema mfumo huo ambao ulianza kufanya kazi rasmi Oktoba mosi 2013, pamoja na mambo mengine umewezesha upatikanaji wa takwimu za mawasiliano ya simu yanayofanyika ndani na nje ya nchi pamoja na kutambua mapato na takwimu za miamala ya fedha mtandaoni. 

"Mfumo huu utawezesha kusimamia kwa ufanisi ubora wa huduma za mawasiliano na hivyo kuboresha viwango vya huduma hizo, utatambua taarifa za laini ya simu na namba tambulishi za kifaa cha mawasiliano," amesema. 

Aliongeza kuwa kazi nyingine za mfumo huo, utaweza kubaini na kufungia simu zenye namba tambulishi zilizonakiliwa pamoja na kutoa takwimu zinazohusiana na matumizi ya data na jumbe fupi. 

"Mfumo huu unaweza pia kusimamia shughuli nyingi zaidi kutokana na mazingira na mabadiliko ya teknolojia mpya zinapojitokeza aidha mfumo huo wa TTMS ni chombo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na kijamii nchini," amesema. 

Hata hivyo amesema katika makabidhiano hayo zaidi ya viongozi na wananchi mbalimbali ambao ni wadau wa sekta ya mawasiliano wapatao 1500 wamealikwa kuhudhuria shughuli hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na makabidhiano ya mfumo wa mawasiliano

WAKAZI WAZO NA VITONGOJI VYAKE WAPATA MAJI, WAZIRI MBARAWA AWAPA DAWASA KONGOLE

0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imeanza kuwasambazia maji wananchi wa Kata ya Wazo na vitongoji vyake ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotoa jumapili Jan 13, 2019. DAWASA imewekeza na imejenga tanki kubwa lenye uwezo wa kihifadhi lita milioni sita itakayofanya wakazi wa kupata maji kwa kipindi chote bila mgao. 

Akizungumza na wananchi mara baada ya kumaliza kazi na kuwapatia wananchi maji, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa amewaomba wasimamizi wa vizimba (Maduka ya kuuzia maji) kuuza maji kwa tsh. 50 kwa ndoo na si tsh. 100 kama ilivyokuwa awali. "Leo mnafurahi kufunguliwa maji ila naomba muuze maji tsh. 50 kwa ndoo, sitaki kuona wananchi wanalalamika eti bei kubwa, mimi ndiyo msimamizi naomba mtekeleze mkumbuke na kulipa ankara zenu za maji ili DAWASA waweze kuwahudumia vyema," amesema. 

Mwishoni kwa wiki iliyopita DAWASA kupitia Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja mbele ya wananchi akiwemo Mkuu wa Wilaya Kinondoni Daniel Chongolo, aliwaahidi wakazi wa kata ya Wazo na vitongoji vyake kuanzia wiki hii maji watapata bila mgawo wowote.


 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akishuhudia utokaji wa maji eneo la Kata ya Wazo mara baada ya kukamilika kwa tanki kubwa litakalowapatia maji kwa kipindi cha mwaka mzima bila kukatika. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongea na wananchi waliojitokeza kuchota maji.  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongea na wananchi waliojitokeza kuchota maji huku akitoa maelekezo ya kuuza maji kwa tsh. 50 kwa ndoo tu.  Maji yakitoka. 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akipata maelezo toka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja. 

MOROGORO WATAKIWA WASIFICHE WAGONJWA WA UKOMA MAJUMBANI

0
0
Na.WAMJW,Morogoro

Wananchi wa Mkoa wa Morogoro na halmashauri zake wametakiwa kutowaficha wagonjwa wenye ukoma majumbani ili ugonjwa huo uweze kutokomezwa hadi ifikapo mwaka 2020.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari wakati wa ufunguzi wa semina ya uhamasishaji wa uongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya mvomero kuhusu maadhimisho ya miaka sitini (60) ya Ushirikiano kati ya serikali na Shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania(GLRA) pamoja na siku ya ukoma Duniani itakayofanyika Kitaifa wilayani Mvomero mwishoni mwa mwezi huu.

“Serikali inawajali sana wananchi wake hivyo wananchi hampaswi kuwaficha wagonjwa majumbani kwani dawa na vipimo zinatolewa bila malipo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini” Alisema Tandari
Aidha, alisema kuwa mkoa wake utaendelea kufanya kila liwezekanalo ili kutokomeza ugonjwa wa ukoma mkoani hapa kwani wajibu wao ni kuwasaidia watu hao kupona na kurudi kwenye kazi zao za kila siku watu wagonjwa hao wakishapatiwa dawa wanapona kabisa.

Kwa upande wa ongezeko la wagonjwa wilayani Mvomero Katibu Tawala huyo alisema sababu kubwa ya kuongezeka kwa wagonjwa hao wilayani hapo ni muingiliano hususan kwenye mashamba hivyo inakua rahisi maambukizi kuwa juu”tutafanya jitihada ili kuweza kufikia viwango vya Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kutokomeza ugonjwa huu ambapo malengo ni mgonjwa mmoja kati ya watu elfu kumi.

Naye Mratibu wa Taifa wa ugonjwa wa Ukoma kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Deus Kamara alisema kuwa zipo halmashauri 20 ambazo hazijafikia kiwango cha kutokomeza ukoma nchini hivyo wizara kupitia mpango wa Taifa wa kutokomeza Kifua kikuu na Ukoma, Mikoa inatakiwa kutengeneza mkakati wa kuwasaka,kuwafikia, kuwaibua na kuwaweka katika matibabu stahili pamoja na kuzifikia kaya zote zenye wagonjwa wa ukoma kwa kufanyiwa uchunguzi ili wale ambao hawajaugua kuwapatia tiba kinga ili kutokomeza ukoma katika halmashauri zote ifikapo mwaka 2020.

Wakati huo huo Mwakilishii Mkazi wa Shirika la GLRA Buchard Rwamtoga alisema kuwa shirika hilo mwaka huu linatimiza miaka sitini(60) hapa nchini katika kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutokomeza ugonjwa wa ukoma Tanzania ikiwemo ya kuwajengea makazi bora familia 120 kutoka familia 739 ya watu waliougua ukoma hapa nchini.

“Dhamira yetu ni kuhakikisha kwamba kupitia michango ya wadau mbalimbali,shirika linaweza kusaidia mashirika na taasisi nyingine hasa mpango wa taifa wa kudhitibi ugonjwa wa kifua kikuu na Ukoma kupunguza madhara yatokanayo na magonjwa haya”alisisitiza Rwamtoga.

Alitaja mafanikio waliyoyapata kwa miaka 60 Mwakilishi Mkazi huyo alisema shirika lake wameweza kutoa viatu maalum kwa walioathirika na ukoma pea 94,500 kwa watu 47, 250, miguu bandia magongo na baiskeli kwa watu 2, 655, magari 270 kwa Tanzania bara na Zanzibar,kusaidia masuala ya elimu kwa wanafunzi 3,765 pamoja na kuwezesha vikundi vya kusaidiana vipatavyo 50 vyenye wanachama 677 kwa familia za watu wenye kuishi na ugonjwa wa Ukoma nchini.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya ukoma mwaka huu ni “Tutokomeze ubaguzi ,Unyanyapaa na chuki dhidi ya waathirika wa Ukoma” na kitaifa yatafanyika kwenye kitongoji cha Chazi kijiji cha kigugu Wilayani Mvomero tarhe 27 mwezi huu.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw.Clifford Tandari akifungua semina ya Uhamasishaji kwa viongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya serikali  na shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania (GLRA).Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
 Baadhi ya wakuu wa idara kutoka mkoa na wilaya wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa(hayupo pichani)ambapo wametakiwa kuhamasisha utekelezaji wa kuwaibua wagonjwa wa ukoma kutoka kila kaya ili kufanikisha malengo ya kutokomeza ugonjwa wa Ukoma ifikapo mwaka 2020
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw.Clifford Tandari akifungua semina ya Uhamasishaji kwa viongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya serikali  na shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania (GLRA).Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mohamed Utay na kushoto ni Mganga Wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Frank Jacob
Picha ya pamoja ya viongozi wa mkoa,wilaya,Wizara ya afya na GLRA mara baada ya ufunguzi

RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA MAKABIDHIANO YA MFUMO WA KUTHIBITI MAWASILIANO YA NDANI NA NJE YA NCHI (TTMS)

0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. James Kilaba akiwa kapigwa na butwaa na baadaye kushukuru wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipomhakikishia kumwongeza mkataba wa miaka mitano kuongoza taasisi hiyo katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA  Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine meza kuu wakimsikiliza Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiongea machache wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na viongozi wengine wakipata picha ya kumbukumbu na viongozi wa dini katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA  Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aakipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. James Kilaba   katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA  Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zacharia Kakobe  katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA  Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na  viongozi wengine meza kuu  wakishuhudia makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) baina ya wakandarasi Bw. James Gabriel Claude CEO wa kampuni ya GVG na Samuel Kiki Gyan Mkurugenzi wa kampuni ya SGS na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA  Dkt. James Kilaba katika hafla iliyofanyika makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
 : Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine akiwasili katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.

PICHA NA IKULU

TAMKO LA HALI YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA - WAZIRI UMMY MWALIMU

0
0

Shirika la posta lahamasisha ufundishwaji uandishi wa barua kwa wanafunzi ngazi zote

0
0
 Meneja Masoko Msaidizi wa Shirika la Posta mkoa wa Dar es Salaam, Evord Mwauzi amesema tatizo la uandishi wa barua kwa wanafunzi ikiwamo wa elimu ya juu bado ni tatizo kubwa. Meneja huyo,ameyasema hayo leo Januari 18.2019 wakati wa maadhimisho ya siku ya Umoja wa Posta Afrika yaliyofanyika katika ofisi za Posta zilizopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilala.
Amesema, katika utekelezaji wao wa majukumu, wamebaini kuwa uandishi wa barua hasa kwa wanafunzi wakiwamo wa vyuo vikuu bado ni tatizo kubwa hapa nchini. Akiwaelezea wanafunzi hao jinsi shirika hilo la posta linavyotoa huduma,Mwauzi ametoa wito kuwa  siku  zijazo baadhi ya huduma za Shirika la Posta ziingizwe katika mitaala ya elimu.

Amebainisha kuwa, Shirika la Posta limetenga siku ya Jumatano kwa ajili ya kutoa elimu hasa ya uandishi wa barua kwa wanafunzi na  huduma wanazozitoa na kuzitaka shule kuwatumia maombi  iwapo wanahitaji elimu hiyo. Ameongeza,  hali hiyo inatokana na kuwa namabadiliko ya teknolojia, kitu ambacho kimepelekea pia hata hali ya watu kumiliki masanduku ya posta kupungua, lakini utaratibu uliopo  mtu yoyote anayekuja nchini kuwekeza  lazima awe na sanduku la Posta.

Hata hivyo alibainisha kwa kwa sasa Shirika la Posta linatoa kila huduma kwa kutumia njia ya mtandao  ikiwamo huduma ya Post Code ambayo humfanya mtu, kufahamu nyumba ya mtu  anayoitafuta iko mahali gani ikiwa tu atakuwa akifahamu jina la mtaa na barabara husika.

Kwa upande wake, Afisa Masoko Mwandamizi wa shirika hilo, James Musyangi amesema maadhimisho hayo ya Siku ya Umoja wa Posta Afrika yalianzishwa Januari 17, mwaka 1980 yakiwa na lengo la kuhakikisha uelewa wa wafanyakazi wa Posta Afrika kuwa mmoja katika mambo mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao na kutetea maslahi na hata katika nyanja ya elimu pia.

Aidha,Afisa Masoko huyo Mwandamizi aliwatembeza wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilala katika vitengo mbalimbali vya shirika hilo ikiwamo maeneo ya kutuma barua za ndani na nje ya nchi na  ukaguzi wa mizigo inayotumwa kutoka ndani kwenda nje ya nchi na inayotoka nje ya nchi kuingia nchini kama ni halali na inastahili kulipiwa kodi ama la.

WAZIRI MKUU AKAGUA ENEO LA UJENZI WA HOSPITALI YA UHURU CHAMWINO

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua eneo la ujenzi wa hospitali ya Uhuru lenye ukubwa wa ekari 109 lililoko katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Maduma wilayani humo leo mchana (Ijumaa, Januari 18, 2019), Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Serikali ya kijiji hicho wa kutenga maeneo ya maendeleo ni wa kupigiwa mfano na vijiji vya maeneo mengine.

“Uamuzi wenu wa kutenga maeneo ya miradi ya maendeleo umekuwa na tija, ndiyo maana Mheshimiwa Rais Magufuli aliposema ijengwe hospitali, hamkupata shida sababu eneo tayari lilikuwepo. Ninawapongeza wazee waliojitolea maeneo yao ili kuongeza kwenye eneo la hospitali,” amesema.

Wazee waliotoa maeneo yao ni Mzee Meshack Njamasi (ekari 5.50), Mzee Jobu Malogo (ekari 3.50) na Bw. Nehemia Mwikwi (ekari 4.50). Ekari 95.5 zilizobakia, zimetolewa na Seriakli ya kijiji hicho.

Waziri Mkuu aliwataka wakazi wa wilaya ya Chamwino wasibweteke bali wajipange na kila mmoja ajipange kufanya kazi kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa akihimiza. “Ujenzi wa mji wa Serikali unaoendelea hivi sasa ni fursa kwenu. Na ujio wa hospitali hii ni fursa nyingine kwa wana-Chamwino hasa kwa vile ujenzi wake utatumia mfumo wa force account ambao unatoa fursa kwa wanajamii kushiriki kazi za miradi ya eneo husika,” amesema.

Waziri Mkuu amesema ujenzi wa hospitali hiyo yenye hadhi ya wilaya ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoelekeza wananchi wapatiwe huduma za matibabu huko huko waliko. “Hadi sasa tumeshajenga vituo vya afya 350 ili kusogeza huduma kwa wananchi na jumla ya hospitali za wilaya 67, zinajengwa nchi nzima kwa mwaka huu,” amesema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wakazi wa vijiji jirani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. Selemani Jafo alisema eneo la ujenzi wa hospitali hiyo liko umbali wa kilometa mbili kutoka barabara kuu ya Dar es Salaaam-Dodoma na kilometa tatu kutoka Ikulu ya Chamwino.

Naye, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine aliwataka wakazi hao wachangamkie fursa hiyo kwa kusomba mawe, mchango, maji na kwamba Kamati za usimamizi wa ujenzi zitapaswa kusimamiwa na wanakijiji.

Aliwataka wakazi hao wasiishie kwenye lengo la kuwa na hospitali ya wilaya, bali walenge kujenga hospitali yenye hadhi ya mkoa kwa kadri bajeti itakavyoruhusu.

Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Bilinith Mahenge alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni wa hadhi ya wilaya ikiwa na nyongeza ya huduma za wagonjwa wa dharura na wagonjwa mahututi (Emergency Department and Critical Care Unit).

Alimshukru Rais Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa hospitali hiyo sh. milioni 995.18 ambazo zilipaswa kutumika kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru, Desemba 9, mwaka jana. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutuongezea kiasi kingine cha fedha cha sh. bilioni 2.35 na kutufanya sasa tuwe na sh. bilioni 3.22 za ujenzi huo,” alisema.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge  (kulia) wakati alipokagua eneo itakapojengwa Hospitali ya Uhuru katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino, Januari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha michoro ya majengo ya Hospitali ya Uhuru inayotarajiwa kujengwa katika  kijiji cha Maduma wilayani Chamwino wakati alipokagua eneo hilo, Januari 18, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (katikati) na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Faustine Ndugulile wakati alipokagua eneo itakapojengwa  Hospitali ya Uhuru katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino, Januari 18, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mzee, Meshack Njamasi, mmoja wa wananchi waliotoa maeneo yao bure kwa serikali ili yatumike kwa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino, Januari 18, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru  Mzee,  Job Mahogo, mmoja wa wananchi waliotoa maeneo yao bure kwa serikali ili yatumike kwa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino, Januari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images