Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

JUMUIYA YA WATANZANIA UGHABUNI YAPATA UONGOZI MPYA DALLAS , TEXAS, MAREKANI.

0
0
Kwa mujibu wa taarifa toka Jumuiya ijulikanayo kama Tanzanians Dallas, ambayo ni jamii ya watanzania wanaoishi katika jiji la Dallas, Texas na vitongoji vyake, limefanya mabadiliko siku ya Jumamosi tarehe 12, 2019 kwa kuwachagua viongozi mpito watatu. Uchaguzi huo ulihudhuliwa na wakazi wengi wa sehemu hizo zilizolizunguuka jiji la Dallas na kufanya maamuzi ya uongozi wa dharura kutokana na kujiudhuru kwa uongozi uliyopita.

Watanzania katika jiji hilo la Dallas na vitongoji vyake wanaamini kwamba, mshikamano wao ambao ndio kilikuwa ni chanzo kikubwa cha wao kuwa kitu kimoja wakati wa misiba na dharura za aina yote kimaishi wanavyoishi huko ughabuni. Kufuatana na katiba ya jumuiya hiyo hakuwa nabudi kuitisha kikao na kuwa na maamuzi ya kuteuwa wagombea mpito mpaka hapo mwezi Julai katika uchaguzi mkuu chini ya utaratibu mpya.

Uongozi uliotumikia jumuiya hiyo kwa muda sasa na hatimae kujiudhuru kwa hiyari, ni mwenyekiti Bw. Benedict Kazora, Bi Maria Musomi, Makamo mwenyetkiti na Bi Viola mbise, Katibu. Maamuzi hayo ya ghafla yaliwakilishwa kwenye kamati ya ushauri na kutangazwa rasmi katika tofuti za mitandao ya kijamii mara moja. Harakati zipo mbioni kuwasiliana na uongozi uliopita kukabidhiana nyaraka na uongozi mpya mpito haraka iwezekanovyo.

Jumuiya hiyo, imewachagua viongozi wake mpito wapya kupitia utaratibu wa kuwapigia kura wale wote walioteuliwa na wanajumuiya baada ya mkutano huo mahususi kuziba hizo nafasi hizo. Yafuatayo ni majina ya wachaguliwa wapya, Mwenyekiti ni Bw. Everest M. Michael, Katibu Bw. Godfrey Mwamsoyo na mweka hazina ni Bi Jocyline Vadesto. Wateuliwa wote hao ni wakazi wa Dallas na vitongoji vyake. Jumuiya mzima ya Watanzania Dallas inatoa pongezi na shukrani nyingi kwa wale wote walio pata wasaa na kujitokeza kufanya zoezi hili muhimu.

Pia vilevile, sambamba na mkutano huo lilichaguliwa baraza la ushuri la watu wa jumuiya hiyo chini ya mapendekezo ya wanajumuiya wake, na sio tena kama jinsi baraza lile la zamani kuteuliwa na mwenyekiti. Hii ni kuhamasisha dhamira na malengo ya jamii kupewa kipaumbele katika maswala ya jamii hiyo. Misiba na matatizo yasiyo tabirika, ndivyo vigezo vikuu vilivyo waleta wanajumuiya hao pamoja na kusaidiana kutatua yanayojiri wakati kama huo mgumu kwao.

Hivyo basi, baraza la ushauri lina takribani watu kumi na moja ambao watakuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na uongozi wa juu na kujaribu kuwa na ufumbuzi wa matitizo au misiba inapotokea katika uzio wa mipaka ya vitongoji vyao. Hivyo, walioteuliwa na jamii hiyo katika baraza au kamati hiyo hadi hapo mwezi Julai uchaguzi mkuu ni:
Bw. AloyceChissanga; 2. Bw. Peter Kapanga; 3. Bi Anna Ngoti; 4.Bw. Felix Maganjila; 5. Bw. Kibwana Rumadha; 6. Bi Arafa Manganji; 7. Bw. Ibrahim Kulindwa; 8. Bi Rosemary Kessy; 9. Bw. Erick Joshua; 10. Bi Sofia Lesso; na 11. Bw. Godlisten Lyimo.

Hao ndio wanaoiwakilisha baraza au kamati ya ushuri mpito iliyopo madarakani tokea uchaguzi wake wa tarehe 12 January mwaka 2019.

Juhudi zinaendelea kuhakikisha kwamba kwa mujibu wa katiba, yote yanayojiri katika makabidhiano ya kifedha na vitega uchumi ya Jumuiya vinatendwa chini ya utaratibu sahihi na wenye nidhamu. Hii utawapo urahisi fasaha wale viongozi wapya kufuatialia harakati zote zinazo husiana na jumuiya na kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kupitia vivutio vyake asilia vya kitalii na maliasili.

Kwa mujibu wa taarifa toka kwa mwenyekiti mpya wa mpito, ndugu Everest,  inaeleza kwamba, kazi kubwa iliyopo ni kuwa hamasisha wanajumuiya wote wa asili ya Tanzania kushiriki katika ufumbuzi wa maswala yanayotukabiri na kuwa bora, imara zaidi ya jumuiya zinginezo toka Afrika. Tanzania, hususani sekta ya utalii, madini na nyanja nyinginezo tofauti, tutazidi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha nchi yetu inazidi kutambulika hapa na kuwavutia jamaa na marafiki wetu wa Marekani waje tembelea mbuga zetu za wanyama, mlima wa Kilimanjaro na mengineyo zaidi toka Tanzania.

Mwisho kabisa, Jumuiya hiyo ya watanzania wanaoishi Dallas na vitongoji vyake vya karibu pia wakazi wake ambao kwa namna moja au nyingine waliowahi kuishi huko wanawatakia uongozi huu mafanikio mema yenye mshikamano wa dhati na uzalando halisia kama Tanzania Diaspora.
Everest Michael, Mwenyekiti mpya.
Godfrey Mwamsoyo Katibu mkuu .
Bi Jocylne devosta mweka Hazina.
Wanajumuiya wa Tanzania Dallas,TX Wakisikiliza hoja kwa makini.


TAEC KUANZISHA MRADI KWA KUHIFADHI CHAKULA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akisoma moja ya kitabu alichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu Tume ya nguvu za Nyuklia Nchini (TAEC) Profesa Lazaro Busagala alipotembelea ofisi hiyo leo kujitambulisha. Picha na Vero Ignatus.
Mkurugenzi Mkuu Tume ya nguvu za Nyuklia Nchini (TAEC) Profesa Lazaro Busagala akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Arusha moja ya nyaraka mbalimbalimbali zinazohusiana na TAEC. Picha na Vero Ignatus. 



Na Vero Ignatus, Arusha.

Tume ya nguvu za Atomiki nchini ipo mbioni kuanzisha mradi wa uhifadhi wa chakula kwa kutumia nyuklia (food Irradiator) ambayo itachangia kupunguza upotevu wa vyakula na biashara

Mkurugenzi mkuu wa TAEC Prof. Lazaro Busagala amesema kuwa hiyo ni mipango iliyopo kwa sasa ikiwa ni pamoja na kuanzisha kinu cha tafiti za nyuklia, kuzalisha dawa za kutibu saratani (Research Reactor) ambapo ikifanikiwa Tanzania itakuwa ya pili kwani kwa sasa kipo Afrika ya kusini 

Profesa Lazaro Busagala amemueleza mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo leo alipotembelea ofisini kwake kujitambulisha kuwa wanatazamia kuanzisha kituo cha mafunzo ya fani ya sayansi za teknolojia ya nyuklia na kuboresha miundombinu ya udhibiti wa matumizi salama ya nyuklia. 

Amesema maeneo ambayo nchi imenufaika kwa mwaka wa fedha uliopita kwa upande wa ni sekta ya Afya, maji, kilimo na mifugo waliweza kupata jumla ya shilingi Bilioni 6.1,na upande wa mafunzo shilingi bilioni 3.2

Amesema maeneo mengine waliyofaidika kwa kutumia teknolojia ya nyuklia ni sekta ya Afya waliweza kupata mashine ya kutibu ugonjwa wa saratani iliyosimikwa mwaka jana hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam na Bugando jijini Mwanza. 

Kwa upande wa kilimo teknolojia hii ya nyuklia imeweza kuwasaidia kuongeza ubora wa mbegu kwa kutumia mionzi katika upandikizaji wa kitaalamu, na kupata mifugo bora zaidi.'' Zanzibar teknolojia hii imewasaidia kwa kuteketeza mbung'o wote kwa kuwaasi madume ya mbung'o hivyo magonjwa yite yanayoenezwa na mbung'o Zanzibar hayapo'' 

Amezitaja changamoto zinazo wakabili ni kutofahamika zaidi kwa kazi za TAEC, uhaba wa fedha za kuleta maendeleo na manunuzi ya haraka, uhaba wa vifaa kwenye kanda, mipakani na Zanzibar pamoja na upungufu wa wafanyakazi kwa sasa jumla 108 wakati mahitaji halisi ni 215

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema Elimu hiyo ya nyuklia ni vyema ikatolewa kwa wajumbe wote wa kamati ulinzi na usalama ya mkoa kwani inahisika moja kwa moja na usalama na itawasaidia katika kutekeleza majukumu yao. 

Amesema hiyo ni fursa adimu kwao kama mkoa na nchi kwa ujumla kwani itawasaidia kuangalia vitu vinavyoingizwa mipakani, mifugo, chakula na hata katika uwanja wa kimataifa wa KIA ambao Arusha nao washea kuangalia vitu vinavyoingia na kutoka. 

Gambo amesema kuwa serikali ngazi ya mkoa ipo tayari kushirikiana na TAEC katika changamoto ambazo wataweza kuzitatua huku akuwataka wasikae kimya hadi changamoto iwe kubwa ndipo waiwasilishe.

RC Wangabo asisitiza ushirikiano Kutatua changamoto za elimu

0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi, kuhakikisha kila mtumishi kwa nafasi yake na majukumu yake anashirikishwa katika kutatua changamoto za wananchi ikiwemo elimu, afya, maji na kilimo pamojana kushirikiana na wananchi kutatua chnagmoto hizo.

Amesema kuwa ili kutatua hayo halmashauri inapaswa kuongeza vyanzo vya mapato ikiwemo kuzidisha malengo ya makusanyo kwa mwaka ili kuweza kukabiliana na changamoto anazokuwa anasomewa kila anapofanya ziara katika shule mbalimbali za halmashauri na kumuomba achangie kutatua changamoto zao.

“Mpige hesabu zote muwarudishie huko jamii ili jamii iguswe kwamba alaa! Kumbe kuna changamoto kubwa sana zisingoje sisi viongozi ambao pengine hatuna nafasi ya kuzunguka sekondari zote, lakini kama tutafanya hivi tutaondoa changamoto zote hizi na matatizo na haya yote mliyoyasema yako chini ya uwezo wenu, sio mambo ya mkuu wa mkoa haya, ni mambo ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi, kata na vijiji vyenu, kama ni “support” tunatoa ya kuhamasisha,naweza kusema nanunua bati mbili tatu, je, ninatatua matatizo yote hayo?”Alibainisha.

Ameongeza kuwa kazi ya shule ni kuandaa taarifa nzuri na kuikabidhi kwa watendaji wa halmashauri kuanzia Mtendaji wa kata na vijiji pamoja na viongozi wa kisiasa akiwemo diwani wa kata husika ili taarifa hizo ziwafikie wananchi watambue kupitia vikao vya kamati ya maendeleo ya kata ambao ni mfumo mzuri uliowekwa na serikali katika kutambua changamoto na kuzitatua.

Ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya shule ya sekondari Chala, iliyopo kata ya Chala Wilayani Nkasi na mkuu wa shule hiyo Fatma Mchomvu aliyemuomba kufanya harambee ya haraka kutoka kwa msafara alioambatana naoi li kuweza kukarabati nyumba ya “Matron” ambapo hadi wanafikisha ombi hilo waalimu walikwishajichangisha shilingi 50,000/-.

“Walimu wamejitolea kuchangia 50,000/- kusaidia kukarabati nyumba moja ya mwalimu ya “matron” kwasababu kule wanafunzi wako peke yao hakuna ulinzi kwahiyo nao wakaomba kupitia msafara wako, na wewe ndio kiongozi wetu tupate harambee ya haraka ili angalau tuanze kufanya ukarabati wa jengo hilo ili angalau wanafunzi wawe salama kwasababu wanakaa mbali na hakuna mlezi wa kukaa nae kule,” Alifafanua.

BENKI YA NMB KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUSAIDIA SEKTA ZA ELIMU NA AFYA

0
0
BENKI ya NMB imesema inatambua umuhimu wa elimu na afya kwa Watanzania hivyo itaendelea kusaidia katika sekta hiyo ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za Serikali za kuwahudumia wananchi wake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja wa Benki hiyo, Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Chilongola wakati akikabidhi msaada wa madawati 102 kwa shule za Msingi Mwasanga na Hekima za Jijini Mbeya.

Pia Benki ya NMB imekabidhi jumla ya mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli ya Wilaya Mbeya na Mapinduzi ya Jijini Mbeya na vitanda, magodoro na mashuka kwa Hospitali Teule ya Mbalizi vyote vikiwa na thamani ya milioni Sh25. Alisema NMB ni wadau muhimu kwa Serikali na Watanzania hivyo wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za maendeleo kwa sababu jamii wanayoisaidia ndiyo inayowawezesha kupata faida katika biashara yao.

“Tunambatua changamoto ya elimu na afya, sisi NMB tunazipa kipaumbele sana kwa sababu hizi sekta mbili ni muhimu mno katika ustawi wa jamii yetu,” alisema Chilongola.Chilongola alisema katika kipindi cha mwaka huu wa 2019, NMB imetenga Sh1 bilioni kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwamo afya, elimu na yanapotokea majanga kwa nchi nzima.

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule Msingi Mwasanga, Keneth Amon alisema shule yake inakabiliwa na msongamano wa mkubwa wa wanafunzi madarasani kutokana uhabawa wa vyumba vya madarasa, upungufu wa madawati.Alisema ‘Msongamano ni mkubwa sana darasani, shule nzima tuna madawati 237 lakini kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi, tunakabiliwa na upungufu wa madawati 140, lakini vile vile tuna upungufu wa ofisi za walimu. Shule ina walimu 22 na wote tunatumia ofisi moja ambayo nayo ni finyu mno jambo ambalo kwa kweli inatuwia vigumu kumudu majukumu ya kila siku’.

Akizungumza na baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika alisema Benki ya NMB inatambua umuhimu wa kusaidia jamii kama walivyo fanya ikitambua kwamba Serikali pekee haiwezi kufanya kila jambo kwa wananchi wake licha ya kuwa ndio wajibu wake.

Alisema ‘Niwatake wazazi kwamba shule zimeshafunguliwa sasa hivyo asiwepo mwanafunzi ambaye hafiki shuleni, na nyinyi wanafunzi hakikisheni mnatunza madawati haya na msome kwa bidii. Leo NMB imetambua umuhimu wa elimu bora kwa kuwatengenezea mazingira bora ya kusomea na ndiyo maana imeleta madawatin haya’.

Ntinika amefafanua kuwa mahitaji ya huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu yanahitaji kuungwa mkono na taasisi na mashirika mbalimbali ya kijamii kama ilivyofanywa na Benki ya NMB ambayo imechangia vitanda na mashuka kwa Hospitali Teule ya Mbalizi.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika mabati 144 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Msingi Mapinduzi Jijini Mbeya. Kwa ujumla, Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.  

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya - William Pauk Ntinika akipokea Msaada wa madawati 51 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za juu - Straton Chilongola kwa ajili ya shule ya Msingi Mwasanga Jijini Mbeya. Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akipokea mashuka kwa ajili ya Hospitali Teule ya Ifisi ya jijini Mbeya kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu - Straton Chilongola. Kwa ujumla, Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.
 

Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwasanga wakiwa wameketi kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB baada ya makabidhiano yaliyofanyika shuleni hapo. Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.

KANGI LUGOLA ATUMBUA MAKAMANDA WATATU WA POLISI,AMTAKA KAMANDA USALAMA BARABARANI KUJITATHMINI

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametengua uteuzi wa Makamandaa wa polisi watatu wa mikoa ya Temeke,Ilala, na Arusha kwa makosa mbalimbali ikiwemo kujihusisha na vitendo vya Rushwa kulinda Askari wanaohusishwa katika kusindikiza utoroshwaji wa Bidhaa, na madawa ya kulevya.

Lugola ametaja Makamanda hao kuwa ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi

Waziri Lugola ametangaza uamuzi wake huo leo Jumatano Januari 16, 2019, katika mkutano na waandishi wa habari akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kushauriana na vyombo anavyoviongoza.

Lugola pia amemtaka Kamanda Wa kikosi cha Usalama barabarani nchini kujitathmini kama anatosha katika nafasi hiyo. "Mimi ndio waziri wa mambo ya ndani ya nchi nasimamia vyombo vyote hivyo, nikitengua uteuzi inabaki kazi ya IGP kuteua mtu mwingine kujaza nafasi" amesema waziri Kangi Lugola.

MAWAKALA WA T-PESA KUHUDUMIWA NA TPB NCHI NZIMA

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi (kulia) wakisaini mkataba wa ushirikiano kibiashara, ambapo sasa Benki ya TPB itawahudumia mawakala wa T PESA tataweza kununua Floats za T Pesa kutoka katika Matawi yote 76 ya TPB yaliyopo katika Mikoa na Wilaya anuai nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi (kulia) wakibadilishana nakala za mikataba ya ushirikiano kibiashara mara baada ya kusaini leo jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA NIGERIA OLUSEGUN OBASANJO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.



RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WATATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick .Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 16, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Malawi hapa nchini Mhe. Glad Chembe Munthali Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Malawi hapa nchini Mhe. Glad Chembe Munthali  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Malawi hapa nchini Mhe. Glad Chembe Munthali  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Balozi mteule wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil hapa nchini Mhe. Antonio Augusto Martin Cesar kabla  ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil hapa nchini Mhe. Antonio Augusto Martin Cesar. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil hapa nchini Mhe. Antonio Augusto Martin Cesar mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil hapa nchini Mhe. Antonio Augusto Martin Cesar mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019. 
 Balozi Mteule wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick akiandika katika kitabu cha wageni kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 16, 2019.
  Balozi Mteule wa Malawi hapa nchini Mhe. Glad Chembe Munthali  akiandika katika kitabu cha wageni kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Balozi Mteule wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil hapa nchini Mhe. Antonio Augusto Martin Cesar akiandika katika kitabu cha wageni kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.

PICHA NA IKULU

Tunasheherekea utajiri wa muziki wa Kiafrika huku tukipambana na rushwa-sauti za busara.

0
0
Homa ya Maandalizi ya tamasha la 16 la Sauti za Busara imezidi kupanda, kwani wahudhuriaji kutoka ndani na wale wageni wa kimataifa wanajiandaa kwa ajili ya msimu mwingine wa muziki unaopigwa (live) mubashara kutoka katika kila kona ya bara la Afrika. 

Busara Promotions limethibitisha kuwa mpangilio wa tamasha hilo lililojizolea heshima kubwa miongoni mwa watu upo vizuri kwani lilianza rasmi siku ya Jumanne, Februari 7 na linaendelea. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud kauli mbiu ya tamasha la mwaka huu inalenga kupambana na rushwa kwa kuwa wanaamini wasanii wanaweza kutumia sauti zao kukabiliana na tatizo hilo wakati wanasheherekea utajiri na mkusanyiko wa tamaduni mbalimbali za muziki wa Afrika. 

“Katika kuunga mkono wasanii wanaotumia muziki kusimamia amani, umoja, haki za binadamu na uhuru wa kujieleza, ujumbe wenye nguvu ambao unaonekana katika tamasha la mwaka huu ni (“Potezea Rushwa, Sio Dili!),” alisema Mahmoud. 

Aliongeza kuwa, “Rushwa ni janga linalotafuna/ linalomomonyoa maadili ya jamii zetu barani Afrika na nje ya Afrika. Kibaya zaidi imefikia hatua kuwa hata baadhi ya watu wamekuwa wakichukulia ni jambo la kawaida. Hata hivyo, tamasha moja pekee haliwezi kubadili jamii yote kikamilifu, hivyo, tunashirikiana pamoja na washirika wa ndani na wa kimataifa kuendeleza majadiliano/mazungumzo, kubadili mitazamo na kuchochea hatua mbalimbali kwa ajili ya uongozi bora,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara. 

Baadhi ya wasanii watakaounga mkono jitihada za kusambaza ujumbe wa kukabiliana na rushwa ni pamoja na Faith Mussa (Malawi), Fadhilee Itulya (Kenya), Fid Q (Tanzania), BCUC (Afrika Kusini) na wengineo watakaokuwa wakitumbuiza katika tamasha. “Hatua hizi ndogo ndogo zitasaidia kuweka muongozo mwishoni katika kuleta mabadiliko yale tunayoyakusudia kwa pamoja,” anasema Mahmoud. 

Meneja wa Tamasha la Sauti za Busara, Journey Ramadhan anasisitiza kuwa tamasha hili la Sauti za Busara linaendelea kuzitangaza Tanzania na Zanzibar ulimwenguni kote, kwa kuwa tamasha huvuta waandaaji wengi wa matamasha wa kimataifa, hivyo linatoa fursa kwa wasanii wa muziki wa Afrika Mashariki kusambaza muziki wao na kuifikia hadhira ya kimataifa. 

“Orodha yetu ambayo inaonekana kuwa ni ya kawaida sana lakini yenye utajiri mkubwa wa vipaji, inahusisha upekee wa sauti kutoka Zanzibar na Tanzania, pamoja na makundi yale yanayojiandaa kwa ajili ya kuudhihirishia ulimwengu mkusanyiko wa aina mbalimbali ya miziki ya wazawa hasa,” alisema Ramadhan. 

Tiketi za mwanzo bado zinaendelea kufanya vizuri katika mauzo na waandaaji wanaamini kuwa fedha hizo zitasaidia kugharamia kwa takriban asilimia 30 ya matumizi ya tamasha. Hata hivyo, licha ya kufanikiwa kwake katika miaka iliyopita, tamasha hilo kwa miaka ya hivi karibuni halikuweza kwenda vizuri kutokana na changamoto za ufadhili ambazo zinalifanya tamasha hilo liendelee kufanyika kwa bajeti hafifu/ndogo jambo linalosababisha hatua za uombaji msaada kwa wahisani. 

“Mvuto wa tamasha unaendelea kukua, licha ya vikwazo vya kifedha kuendelea kuliandama. Kumekuwa na msaada mdogo sana kutoka kwa Serikali kuhusiana na Sanaa hii. Sekta binafsi nazo bado hazifanyi masuala ya kuzisaidia jamii zinazowazunguka na ufanyaji harambee umekuwa mgumu kila mwaka. Wakati huo huo, ukilinganisha na matamasha mengine, tumekuwa tukiendelea kujiendesha kwa bajeti finyu huku tukiendelea kuweka kiingilio wanachomudu wazawa, mauzo ya tiketi yanagharamia asilimia 30 ya gharama zote,” anasisitiza 

Mkurugenzi wa Tamasha, Yusuf Mahmoud. Kipaumbele cha Tamasha la Sauti za Busara ni kuendelea kuwa tamasha ambalo Watanzania wanaweza kumudu kuhudhuria kwa gharama nafuu, hivyo kiingilio kwa mzawa ni Sh 10, 000

DOCUMENTARY KUHUSU MAONESHO YA UTALII WA NDANI - 'UWANDAE EXPRO 2019' YAZINDULIWA DAR

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (kushoto) akiongea na wandishi wa habari ( hawapo pichani ) jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza Maonyesho ya biashara ya Utalii wa Ndani ya Kwanza nchini yatakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta Dar es Salaam, Februari 15 hadi 17 ,2019. ” Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni Tambua Ushindi wa Kibishara katika Utalii wa Ndani Tanzania” Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TTB ,Geofrey Tengeneza na Mwenyekiti wa chama cha wanawake Tanzania katika biashara (Tanzania Women Chamber of Commerce) Jacqueline Maleko. 
Mwenyekiti wa Chama cha wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (kushoto) Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) ,Geofrey Tengeneza (katikati) na Mwenyekiti wa chama cha wanawake Tanzania katika biashara (Tanzania Women Chamber of Commerce) Jacqueline Maleko, wakiwa wameshikana mikono kuonyesha ushirikiano wao kwa wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza Maonyesho ya biashara ya Utalii wa Ndani ya Kwanza nchini yatakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta Dar es Salaam, Februari 15 hadi 17 ,2019.” Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni Tambua Ushindi wa Kibishara katika Utalii wa Ndani Tanzania. 

Chama cha Wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na shirika la maendeleo la Ujerumani GIZ, wameandaa documentary ambayo imeziduliwa leo jijini Dar es Salaam. 

Hafla ya uzinduzi wa documentary hiyo ambayo inahusu tukio la maonyesho maonesho ya Utalii wa ndani UWANDAE EXPO 2019 yatakayofanyika mwezi ujao mwezi wa Februari tarehe 15 hadi 17 katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa (National Museum –Posta). ilifanyika katika katika ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii na waandishi wa habari. 

Akizungumza kuhusu maonyesho haya ambayo yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza, Mwenyekiti wa AWOTTA, ambayo inaratibu maonyesho hayo, Mary Kalikawe, alisema AWOTTA na washirika wake waamua kutekeleza mpango mkakati wa Bodi ya Utalii wa kuutangaza utalii wa ndani kwa vitendo kupitia UWANDAE EXPO 2019 na kauli mbiu ya maonyesho haya ni “Tambua ushindani wa Kibiashara katika Utalii wa Ndani Tanzania”. 

“Kuzindua kwa documentary hii ikisisitiza mchango wa akina mama “Nani kama mama” kunaenda sambamba na kuzindua matangazo kwa umma wa Tanzania juu ya uwepo wa sekta kubwa ya utalii humu nchini ambayo ni muhimu ikatambuliwa kusudi ihudumiwe na kupewa umuhimu wake. Sekta hii inachochea uwekezaji kwa wingi kama tunavyoona mahoteli, usafirishaji tangu wa ndege hadi wa bodaboda, biashara ya chakula kila pembe ya nchi, burudani na utalii wa aina nyingine nyingi. 

Sambamba na uwekezaji huu, sekta ina uwezo mkubwa wa kutengeneza ajira kwa wakubwa na wadogo pia inabeba uwezo mkubwa wa kutengeneza kipato kwa mtu mmoja mmoja, makundi na kuchangia kipato cha taifa kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa utalii wa mbuga za wanyama unachangia asilimia 17 ya pato zima la taifa ambayo ni takribani dola Bilioni 2.1 au shillingi zaidi ya trillion 4.7 kila mwaka”. alisema Kalikawe. 

Maonesho haya yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Mhe. Dr. Hamisi Kigwangala, Waziri wa Maliasili na Utalii siku ya Ijumaa tarehe, 15 Februari 2019. Lengo la Maonyesho haya ni kuanzisha utambuaji wa mapana ya sekta ya Utalii wa ndani na fursa kubwa za uwekezaji na ajira zinazoambatana na kukua kwa sekta hii muhimu. 

Maonyesho yatawaunganisha wafanyabiashara wa bidhaa na huduma katika maeneo mbali mbali yanayosababisaha safari za watanzania. Wafanya biashara hawa na vyombo vinavyowezesha uwekezaji, watatumia jukwaa hili kukuza uhusiano baina ya washiriki na Watembeleaji wa maonesho. Watu elfu tatu wanategemewa kuhudhuria maonyesho. Taarifa ya tovuti https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/Br/2014_15_SBR.pdf inaonesha takwimu zifuatazo: Kuwa mwaka 2014 jumla ya vitengo rasmi vya chakula vinywaji na malazi wakati huo Tanzania bara vilikuwa 11,136. Kati ya hivi asilimia 51.7 vilikuwa vya chakula na vinywaji wakati asilimia 48.3 vilikuwa ni sehemu za watu kulala. Kwa upande wa sanaa na burudani, jumla ya vitengo rasmi katika utafiti wa mwaka 2014/15 vilikuwa 239 ambayo ni chini ya asilimia 1 ya vitengo vyote vya biashara vilivyotambuliwa mwaka huo. 

Kati ya hivi ubunifu na burudani vilikuwa asilimia 35.6, michezo na starehe vilikuwa asilimia 24.3, michezo ya kubahatisha na kubeti ilikuwa asilimia 23.8 na vitengo vya library, kujisomea, makumbusho na burudani za utamaduni ilikuwa asilimia 16.3 Waandaaji wa maonesho wanapenda kutangaza kuwa kupitia uelewa wa upana wa sekta zilizomo katika utalii wa ndani, takwimu hizo hapo juu zimekwishaanza kubadilika na kupanda na mwamko wa watanzania na watoa huduma katika kuboresha utalii wa ndani utapandisha sana ukuaji wa vitengo hivi vya biashara.

 Ni muhimu mikoa yote itambue umuhimu wa kuvuta wageni wa ndani kwenda kutembea kwa sababu mbali mbali katika mikoa yao. Kuwasili kwa wageni ndio ukuaji wa sekta ya utalii wa ndani. Takwimu hizo hapo juu zitajidhihirisha katika mikoa mbali mbali ikifanya bidii kuvuta wageni wa ndani na kuwapa huduma nzuri kama vile wanataka wageni wasahau kurudi kwao! 

Faida ya kushiriki: -Kuonyesha bidhaa au huduma wanazozalisha au wanazotoa; -Kupata fursa ya kujifunza teknonolija mpya na ujuzi kutoka kwa washirikiwengine; -Kupata fursa ya kushiriki katika kongamano na semina ya bure itakayofanyika sambamba na maonyesho hayo; -Kukutana na Wafanyabiashara, Wawekezaji, washauri wa kibiashara na Wasambazaji wa huduma mbalimbali; -Kupata kutangazwa kwenye utandawazi wa kitaifa na kimataifa kwa njia mbalimbali; -Kupata fursa mbali mbali ambazo ni pamoja na tiketi ya raffle, vocha ya malazi, zawadi za kusafiri n.k. Aidha, ni fursa ya kimkakati ya kuwahamasisha wananchi wa Tanzania kupenda kutumia huduma zinazotolewa na wadau wa sekta ya utalii hapa nchini. Maonyesho haya yanatarajiwa kushirikisha, Wizara, Taasisi, Makampuni pamoja na Wafanyabiashara wa sekta mbalimbali. Kongamano litakuwa juu ya "Biashara, Uwekezaji na Ajira katika Utalii wa Ndani ambalo litatolewa bure (idadi ni watu 250 tu kwa siku moja wataruhusiwa, hivyo jiandikishe mapema kabla nafasi hazijaisha). Kiingilio kwenye maonesho ni bure asubuhi hadi saa 10 jioni. Kisha yanafuata masaa ya burudani ambayo inalipiwa kiasi kidogo.

ACACIA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI WA SHULE KAHAMA

0
0
Kampuni ya Uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu imetoa msaada wa mabati 2347 yenye thamani ya shilingi milioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu katika shule za msingi na sekondari kwenye halmashauri za wilaya ya Msalala na Kahama Mji mkoani Shinyanga. 

Mabati hayo yenye geji 28 yamekabidhiwa leo Januari 16,2019 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha na Meneja Mwendeshaji mgodi wa Buzwagi, Arthur Mgongo akimwakilisha Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mgongo alisema Acacia inaunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. 

"Katika muitikio wa ombi la msaada wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya madarasa na nyumba za walimu,migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu imechangia vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 150,mpaka sasa tumechangia mifuko ya saruji 3200 ambapo halmashauri ya Kahama Mji imepokea mifuko 1600 ya saruji na Msalala mifuko 1600 jumla ina thamani ya shilingi milioni 80",alieleza Mgongo. 

"Kiasi cha ziada ya fedha iliyobaki ambacho ni sh. Milioni 70 kimetumika kununua mabati haya 2347 yaani mabati 1173 kwa Halmashauri ya Kahama Mji na mabati 1174 Msalala",aliongeza Mgongo. Alisema msaada huo utasaidia kuongeza miundo mbinu katika shule ili kukidhi ongezeko la wanafunzi kwani tangu serikali ianze utekelezaji wa mpango wa kutoa elimu bure,uandikishaji wa wanafunzi shuleni umeongezeka na uhitaji wa miundombinu umeongezeka. 

Mgongo alielezea kuwa, kupitia mpango wake wa maendeleo ya jamii, Acacia imeendelea kuboresha upatikanaji wa elimu katika jamii zinazozunguka migodi yake na kuleta mapinduzi ya kijamii na kiuchumi nchini sambamba na ajenda kuu ya viwanda. Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha aliishukuru Acacia kwa kuwa sehemu ya jamii kuchangia sekta ya elimu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Macha alisema wilaya yake ina uhitaji wa madarasa 250 na kubainisha kuwa mabati yaliyotolewa na Acacia yatatumika kwenye ujenzi wa madarasa 50 huku akitaja kipaumbele ni kwenye shule ambazo tayari wazazi wamejenga maboma. Aidha aliwataka wadau kushirikiana na serikali kuchangia kwenye elimu kwani kila mmoja ni sehemu ya jamii hivyo anatakiwa kuchangia badala ya kuiachia serikali pekee. 
Mwendeshaji mgodi wa Buzwagi, Arthur Mgongo akizungumza kwa niaba ya Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakati akikabidhi mabati 2347 yaliyotolewa na Acacia kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kahama Mji na Msalala leo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kahama.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mgongo akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha (kulia) wakati akikabidhi mabati 2347 (pichani nyuma) yaliyotolewa na Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kahama Mji na Msalala. Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji, Abel Shija.
Mgongo akielezea shughuli zinazofanywa na Acacia katika jamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa maktaba mjini Kahama,Nyang'hwale na Tarime lakini pia maboresho na utanuzi wa shule za msingi na sekondari ikiwemo ujenzi wa maabara na mabweni. Acacia pia inadhamini wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kupitia programu ya CanEducate.
Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Kahama Mji, Anderson Msumba akiangalia mabati matatu kati ya 2347 ambapo 1173 ni kwa ajili ya Kahama Mji yaliyotolewa na migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akizungumza wakati akipokea mabati yaliyotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia kupitia migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha akiishukuru Acacia kwa kuendelea kuwa mdau muhimu wilayani Kahama kwa kuchangia shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kahama Mji, Abel Shija akielezea jinsi Acacia wanavyoshirikiana na halmashauri hiyo kuwaletea maendeleo wananchi.
Katibu wa CCM wilaya ya Kahama Alexandrina Katabi (kwanza kushoto) akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabati ambapo alisema mchango wa Acacia ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM. 
Viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji na Msalala na waandishi wa habari wakiwa katika hafla fupi ya makabidhiano ya mabati. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Benki Ya NMB, Kilimo, TPB Wakubaliana Kuwasaidia Wakulima Wadogo Nchini

0
0
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Benki za Biashara za NMB na Benki ya Posta (TPB) lengo likiwakuwasaidia wakulima wadogo wadogo kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo chini ya TADB. Makubaliano hayo yamefikiwa ili kumwezesha na kumwinua mkulima mdogo aweze kumudu kilimo chenye tija, kupunguza umaskini na kufikia malengo ya serkali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo hayo, Meneja anayesimamia Mfuko, Bw. James Mwakilima alisema Serikali imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 45 kwa mfuko kwaajili ya kuwakopesha wakulima wadogo sehemu mbalimbali hapa nchini.

“Katika kutimiza azma yake ya kujenga uchumi wa kati na viwanda, Serikali imeshatoa shilingi bilioni 45 kwa TADB kupitia mfuko wake wa dhamana kwa wakulima wadogo ili wakulima waweze kujikita kwenye kilimo chenye tija.” alisema Bw. Mwakilima. Bw. Mwakilima alitoa wito kwa wakulima nchini kuitumia vyema fursa hiyo kwa kuwa itakuwa fahari kubwa kwa Benki ya Kilimo kuona wakulima wanainuka kiuchumi na kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa kati na viwanda kwa kuwa hakuna viwanda visivyo na malighafi.

“Ni nafasi pekee kwa wakulima wadogo hapa nchini kuitumia vyema fursa hii kwani Benki ya kilimo ni moja ya madaraja ya kumvusha mkulima kutimiza malengo yake. alisisitiza Bw. Mwakilima.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Posta (TPB), Bw. Ramadhan Mganga alisema kuwa kupitia Mfuko huo Benki yake imefanikiwa kuwakopesha wakulima wadogo hapa nchini. Bwana Mganga alitumia nafasi hiyo kutaja mikoa ambayo imenufaika na mikopo kuwa ni pamoja na Simiyu, Iringa na Singida.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha wakulima wananufaika na mikopo hiyo, Benki ya Posta imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa wakulima wadogo juu ya mazao gani walime na kwa wakati gani ili waweze kuwa na kilimo chenye tija

TADB imejipanga kuhakikisha kuwa inashirikiana na mabenki ya biashara ili kunifanikisha azma ya serikali ya Awamu ya Tano ya kuleta mageuzimakubwa katika sekta ya kilimo ikiwemo kuwainua wakulima wadogo na kuchagiza maendeleo ya sekta ya viwanda.

Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo toka Benki ya Posta Bw, Ramadhan Mganga (wapili kulia) akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari kuhusu Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo nchni (SCGS). Mkutao ulifanyika Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Meneja Miradi wa TADB, Bw. James Mwakilima (wapili kushoto), Meneja Masoko na Uhusiano wa TADB, Bw. Said Mkabakuli (kushoto) na kulia ni Meneja Mikopo wa Benki ya Posta Bw. Mtewele Lucius.

Meneja Miradi wa TADB, Bw. James Mwakilima (wapili kushoto) akifafanua jambo kuhusu Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo nchini (SCGS) wakati wa mkutano na wanahabari kuhsu Mfuko huo. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo toka Benki ya Posta Bw, Ramadhan Mganga. Wengine pichani ni Meneja Masoko na Uhusiano wa TADB, Bw. Said Mkabakuli (kushoto) na Meneja Mikopo wa Benki ya Posta Bw. Mtewele Lucius (kulia).

Maafisa kutoka TADB na TPB wakionesha nyaraka kuhusu Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo nchini (SCGS) . SCGS inalenga kuwawezesha wakulima kukopa katika taasisi za fedha za ikiwemo benki za biashara pamoja na kuziwezesha taasisi hizo kuwa na uwezo wa kuwakopesha wakulima nchini.

Hospitali ya Kibong'oto yajizidhatiti katika utoaji tiba ya kifua Kikuu

0
0
 
Mtaalam wa Mionzi Bw. Faustine Kavishe akiwa kwenye mashine hiyo katika kituo cha kuhudumia wagonjwa yanayotokana na kazi (occupational health service centre). Na wa pili upande wa kulia ni Bw. Emmanuel Darabe akiwa kwenye chumba cha kupima uwezo wa kusikia kwa wagonjwa kutoka katika migodi ya madini .
 Pichani ni  Mashine za kisasa za Gene expert module 4 na 16 za uchunguzi wa vimelea vya kifua kikuu na usugu wa vimelea kwa dawa za kifua kikuu ambapo pia zinapima viral load kwa wateja wa VVU
 Meneja wa Maabara ya hospitali ya Kibong'oto Bi.Mary Mtui  akielezea jinsi wanavyotoa huduma kutumia mashine moya ambazo zinatumia masaa mawili kutoa majibu
 Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ya magonjwa ambukizi Kibong'oto Dkt.Riziki Kisonga akizungumza na maofisa habari wa wizara na taasisi waliofika kwenye hospitali hiyo iliyopo Wilayani siha
 
 
Na.WAMJW,Siha

Hospitali ya Magonjwa ambukizi Kibong'oto inayotoa huduma ya Kifua Kikuu 'TB' na magonjwa mengine ya kuambukiza hasa UKIMWI imeendelea kutoa huduma bora kutokana na serikali ya awamu ya tano kuwekeza katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi na tiba.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dkt.Riziki Kisonga wakati akizungumza na maofisa habari na uhusiano wa wizara na taasisi walofika hospitalini hapo katika kampeni ya "Tumeboresha Sekta ya Afya" ambayo inaelezea mafanikiao ya miaka mitatu inayofanyika katika sekta hiyo.

Dkt.Kisonga alisema kuwa ununuzi wa vifaa hivyo umeweza kurahisisha utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.

Aidha, alisema katika kufanya kazi na jamii ya wachimbaji wadogo wadogo kutoka machimbo ya Tanzanite Mererani,kumekuwepo na idadi kubwa ya wanaougua ugonjwa wa kifua kikuu.

"Ufuatiliaji uliofanywa unaonyesha maambukizi ya TB katika jamii hiyo ni mara kumi na tano(15) zaidi ikilinganishwa na jamii isiyofanya kazi katika machimbo".Alisema Dkt.Kisonga.Alisemaa hospitali yake imeendelea kutoa elimu ya kujikinga na vumbi ambayo ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa mapafu hivyo kufanya iwe rahisi kwa jamii ya wachimbaji wadogo wadogo na familia zao kupata maambukizi ya mimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu.

Hata hivyo Serikali imenunua mashine ya zinazorahisisha ugunduzi wa haraka wa vimelea hivyo katika muda wa masaa mawili na mara wanapogundua wanaanza tiba mara moja.Dkt.Kisonga amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo pia wameanzisha kituo cha afya Mirereni ambacho kinatoa huduma za matibabu ya TB.

“Tumenunua mashine za kisasa zenye thamani ya Sh.milioni 201 ambazo zina uwezo wa kubaini kifua kikuu ambacho hakijaanza kuwa na dalili zilizozoelekea na kubaini usugu wa dawa kwa mgonjwa ambaye haponi licha ya kutumia dawa," alisema Dk. Kisonga.Amesema hospitali hiyo kwa sasa ina wagonjwa waliolazwa wagonjwa 123 na kati yao wagonjwa 86 ni wagonjwa wa kifua kikuu sugu

Aidha, kutokana na kuboresha huduma ya matibabu ya TB, serikali imeanzisha huduma za kifua kikuu sugu katika hospitali za serikali kwenye mikoa nchini na hivyo hospitali hiyo kupokea wagonjwa sugu na wanaohitaji uchunguzi zaidi.

Pia alisema wana mpango wa kuanzisha maabara inayotembea ili kufika kwenye jamii kwa ajili ya kutoa elimu na kufanya vipimo.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Dunuani (WHO) watu 246 kati ya watu 100,000 wanaugua TB duniani.

Dkt. Mahiga akagua ujenzi wa ofisi ya Wizara Ihumwa, Dodoma

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye eneo linalojengwa jengo la ofisi ya Wizara Ihumwa, Dodoma. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Wizara Ihumwa Dodoma. Mhe. Waziri alielezwa kuwa ujenzi huo unaenda katika kasi inayoridhisha ambapo wakandarasi wapo mbele ya mpangoa kazi. 
Waziri Mahiga na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Hamid Mbegu wakioneshana alama za mipaka ya kiwanja cha Wizara. 
Waziri Mahiga akiendelea na ukaguzi wa jengo la ofisi ya Wizara. 
Waziri Mahiga akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Hamid Mbegu

TASWA YAITISHA MKUTANO KWA WANACHAMA WAKE KUJADILI RASIMU YA KATIBA YAKE.

0
0
Mkutano wa waandishi wote wa habari za michezo unatarajiwa kufanyika Jumapili Februari 10 mwaka huu kujadili Rasimu ya Kwanza ya Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA).

Kabla ya mkutano huo wa wadau wa habari za michezo, pia kutafanyika mkutano wa wahariri wa habari za michezo Februari 6 mwaka huu, lengo ikiwa ni kupitia rasimu hiyo kwa pamoja kabla ya kuifikisha kwa wadau wengine. Mikutano yote itafanyika Dar es Salaam, lakini ukumbi utatangazwa hivi karibuni.

Ni imani ya Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya TASWA kwamba mikutano hiyo yote miwili itakuwa na tija na itakuwa muongozo mzuri katika kuandaa Katiba bora kwa maslahi mapana ya waandishi wa habari za michezo nchini. Hivyo kamati inawaomba waandishi wote wa habari za michezo wajitokeze kwa wingi , ili kwa pamoja wajadili namna ya kuboresha rasimu ambayo ilitolewa Desemba 9 mwaka jana.

Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya TASWA imeandaa mapendekezo ya rasimu iliyoandaliwa kwa kuangalia Katiba za vyama mbalimbali duniani vinavyohusiana na waandishi wa habari za michezo na pia kupitia muongozo kutoka Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS), ambacho TASWA ni mwanachama.

Pia Kamati imechambua Katiba ya sasa ya TASWA na kupokea maoni kutoka kwa waandishi wa habari za michezo kuhusu maeneo yenye upungufu kwa nia ya kuiboresha.

Maeneo mbalimbali yamefanyiwa kazi katika rasimu hiyo baadhi yakiwa ni sifa za mwanachama, wajibu wa mwanachama, muundo wa uongozi, sifa za viongozi na pia ukomo wa uongozi. Pia kuna mapendekezo katika rasimu hiyo ya kuanzishwa kamati mbalimbali kwa nia ya kuisaidia Kamati ya Utendaji.

Kamati ya Katiba ya TASWA imeundwa kutokana na agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe aliyeitaka BMT isitishe uchaguzi wa TASWA uliokuwa umepangwa kufanyika Novemba 25 mwaka jana na badala yake BMT ikutane na viongozi wa TASWA pamoja na baadhi ya wanahabari wa michezo kuona namna ya kuifanyia marekebisho Katiba ya TASWA iendane na wakati.

Nawasilisha,Amir Mhando
Katibu wa Kamati ya Katiba/ Katibu Mkuu TASWA

BALOZI WA ITALIA ATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NJE

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Roberto Mengoni. Wawili hao walijadiliana umuhimu wa kuibua maeneo mapya ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Italia hussusan katika sekta ya biashara na uwekezaji. Dkt. Mahiga alitumia fursa hiyo pia kueleza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano za kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini. 
Balozi Mengoni akimwelezea jambo Dkt. Mahiga 
Katibu wa Mhe. Waziri, Bw. Magabilo Murobi pamoja na Bi Happyness Lwangisa wakifuatilia na kunukuu mambo muhimu ya mazungumzo hayo.

WATAKAOSHINDWA

0
0
Waajiri na Mamlaka za Ajira nchini watakaoshindwa kuwasilisha vielelezo vya rufaa zilizokatwa na watumishi wa umma  kwenye Tume ya Utumishi wa Umma ndani ya siku 14 kama sheria inavyoelekeza watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuikwamisha Tume ya Utumishi wa umma kutekeleza jukumu lake la kushughulikia kwa wakati rufaa za watumishi. 

Tahadhari hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma  Makao Makuu ya Tume hiyo, akiwa katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu kwa kina majukumu ya Tume na kujiridhisha namna Tume  hiyo inavyotekeleza majukumu yake.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, kitendo cha waajiri kutowasilisha vielelezo vinavyohitajika na Tume ya Utumishi wa Umma kwa wakati ili kuiwezesha Tume kufanya maamuzi sahihi ya rufaa  imekuwa ni kikwazo cha utekelezaji wa majukumu ya Tume, ambayo moja ya jukumu lake ni kusimamia, kufuatilia na kutathmini uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Utumishi wa Umma nchini.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameisisitiza Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma  kuhakikisha inatoa elimu kwa umma kuhusu utaratibu wa kufanyia kazi rufaa zinazowasilishwa ili waweze kujua ni muda gani unaotumika kushughulikia rufaa zao, na kuongeza kuwa elimu hiyo itapunguza malalamiko dhidi ya Tume kuwa haifanyii kazi rufaa zao kwa wakati.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameelekeza kuwa, kuanzia sasa ni marufuku kwa mwajiri yeyote kumhamisha mtumishi aliyebainika kuwa na kosa  mahala pa kazi, kwasababu Tume ya Utumishi wa Umma itashidwa kushughulikia suala la mtumishi huyo na kuna uwezekano mkubwa akafanya tena makosa yale yale anakohamia. 

Kwa upande wake, Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo amesema kuwa, majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma yameainishwa katika Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298  Kifungu 10 (1) ambapo imepewa mamlaka ya kutoa miongozo na kuhakikisha Utumishi wa Umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu. 

Bw. Odongo ameendelea kufafanua kuwa,Tume ya Utumishi wa Umma ni mamlaka ya rufaa kwani inapokea na kushughulikia rufaa za watumishi wa umma, hivyo inafanya kazi kama mahakama ndani ya Utumishi wa Umma na ni chombo cha kutoa haki kwa watumishi wanaoonewa, na kuongeza kuwa, Tume inasimama kama mdhamini kuhakikisha haki inatendeka pande zote yaani kwa mwajiri na mtumishi.

Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu, Dkt. Steven Bwana, amemshukuru Dkt. Mwanjelwa kwa maelekezo ya kuboresha utendaji kazi aliyoyatoa na kuahidi kusimamia utekelezaji wake.
Tume ya Utumishi wa Umma iliundwa kwa Mujibu wa Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 2008 ili kuhakikisha kuwa, Utumishi wa Umma unakuwa mmoja na watumishi wote wanakuwa na taratibu za usimamizi, hadhi, haki na masilahi yanayofanana.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Tume hiyo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo akieleza  majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Tume chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Makao Makuu ya Tume hiyo yaliyopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani)  wakati wa kikao kazi cha  Naibu Waziri huyo na watumishi hao cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya Tume hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo akifafanua jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Tume chenye lengo la  kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya Tume hiyo yaliyopo Ubungo Plaza  jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu, Dkt. Steven Bwana, akifafanua majukumu ya bodi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya Tume hiyo yaliyopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo akielezea mchakato wa kushughulikia rufaa kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) aipotembelea moja ya ofisi zinazofanyia kazi rufaa zinazowasiliswa Tume ya Utumishi wa Umma. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma, mara baada ya kumalizika kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi  wa Tume hiyo cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya Tume hiyo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA KAMATI MAALUM YA KUBORESHA CHANNEL YA UTALII YA TBC,APOKEA LESENI YA USAJILI - TANZANIA SAFARI CHANNEL

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea leseni ya usajili wa chaneli ya utalii ya Tanzania Safari ambayo itaiwezesha kuoneshwa kwa umma bila ya malipo yoyote (a must-carry channel) na wamiliki wa visimbusi.

Waziri Mkuu amekabidhiwa leseni hiyo leo mchana (Jumatano, 16 Januari, 2019) kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma ambako alitaka apewe mrejesho kutoka kwa wajumbe wa Kamati Maalum ya kusimamia uboreshaji wa Chaneli ya Utalii (Tanzania Safari Channel).

Akikabidhi leseni hiyo kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba amesema kukamilika kwa usajili huo kumeiwezesha chaneli hiyo ianze kuonekana kwenye kisimbusi cha AZAM namba 109.

Akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Dkt. Rioba amesema Kamati hiyo iliundwa Desemba 21, mwaka jana na inajumuisha wajumbe kutoka taasisi ambata za maliasili na utalii kutoka Tanzania bara na Zanzibar.

“Baada ya kupata leseni, sasa hivi tunaonekana kwenye kisimbusi cha AZAM chaneli namba 109 na pia kwenye intelsat ambako tutaweza kuonekana kwenye nchi zote barani Afrika, sehemu kubwa ya bara la Ulaya na Uarabuni,” amesema.

Mapema, akichangia hoja kwenye kikao hicho, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali (Mst.) Hamisi Semfuko alisema chaneli hiyo inaweza kunufaika kwa kupata matangazo kutoka kwa wamiliki wa mahoteli, makampuni ya kutoa huduma za utalii na wenye magari ya utalii.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Allan Kijazi alisema chaneli ya Tanzania Safari imekuja katika wakati muafaka kwa kuwa itaongeza juhudi za taasisi zao kutangaza vivutio vilivyopo nchini na hivyo kuongeza idadi ya watalii wa ndani na wa nje.

“Uwepo wa chaneli hii utasaidia kuondoa upotoshaji wa makusudi uliokuwa ukifanywa na baadhi ya nchi kuwa vivutio fulani viko kwenye maeneo yao wakati siyo kweli,” alisema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza  na wajumbe wa Kamati Maalum iliyoundwa na serikali ya kusimamia uboreshaji wa Channel ya Utalii ya  TBC ya Tanzania Safari Channel, Ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma Januari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Katibu, Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bibi Doroth Mwaluko  (kushoto) wakati alipokabidhiwa Hati ya Usajili wa Channel ya Utalii ya TBC ya  Tanzania Safari Channel  katika kakao cha kuboresha Channel hiyo alichokiitisha, Ofisini kwake jijini Dodoma, Januri 16, 2019. Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),  William Kallaghe na Watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha  Cheti cha Usajili wa Channel ya Utalii ya Shirika la Utangazaji Tanzania  (TBC) ya Tanzania Safari  Channel baada ya kuzungumza na Kamati  Maalum iliyoundwa na Serikali ya Uboreshaji wa  Channel hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa  jijini Dodoma, Januari 16, 2019.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha  Cheti cha Usajili wa Channel ya Utalii ya Shirika la Utangazaji Tanzania  (TBC) ya Tanzania Safari Channel  baada ya kuzungumza na Kamati  Maalum iliyoundwa na Serikali ya Uboreshaji wa  Channel hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa  jijini Dodoma, Januari 16, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bibi Doroth Mwaluko,  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazji Tanzania (TBC)  William Kallaghe na  Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Mamlaka ya Usimazi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali Mstaafu, Hamisi Semfuko baada ya kuzungumza na  Kamati ya Maalum ya Uboreshaji wa   Channel ya  Utalii ya TBC ya Tanzania Safari Channel, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma,  Januari 16, 2019

KAMATI YA BAJETI YA CPA KANDA YA AFRIKA YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Mwekahazina wa Kamati ya Bajeti ya Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA-AFRICA REGION) ambaye pia ni Mbunge wa Uganda Mhe. Elijah Okupa (katikati)akiongoza kikao cha Kamati hicho kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni Spika wa Bunge la Kenya ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CPA AFRIKA Mhe. Justin Mturi na wa kwanza kulia ni Katibu wa CPA AFRIKA ambaye pia Katibu wa Bunge la Tanzania Ndugu Stephen Kagaigai. Wengine katika picha ni Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Sekretarieti ya CPA AFRIKA.
Mwekahazina wa Kamati ya Bajeti ya Chama cha Mabunge ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA-AFRICA REGION) ambaye pia ni Mbunge wa Uganda Mhe. Elijah Okupa (katikati)akiongoza kikao cha Kamati hicho kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni Spika wa Bunge la Kenya ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CPA AFRIKA Mhe. Justin Mturi na wa kwanza kulia ni Katibu wa CPA AFRIKA ambaye pia Katibu wa Bunge la Tanzania Ndugu Stephen Kagaigai. Wengine katika picha ni Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Sekretarieti ya CPA AFRIKA.
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Chama cha Mabunge ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA-AFRICA REGION) (waliokaa) katika picha ya pamoja wakati walipokutana Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Katikati kwa waliokaa ni Spika wa Bunge la Kenya ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CPA AFRIKA Mhe. Justin Mturi na waliosimama ni Sekretarieti ya CPA AFRIKA.
Spika wa Bunge la Kenya ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CPA AFRIKA Mhe. Justin Mturi akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Chama cha Mabunge ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA-AFRICA REGION) walipotembelea kiwanja kilichopo eneo la Mwongozo Kigamboni, kinachomilikiwa na Chama hicho.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA-AFRICA REGION) Ndg. Said Yakubu akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wa chama hicho walipotembelea kiwanja kilichopo eneo la Mwongozo Kigamboni, kinachomilikiwa na Chama hicho.PICHA NA BUNGE.

SERIKALI YABAINISHA VIPAUMBELE MUHIMU KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

0
0
Na. WAMJW-DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imebainisha maeneo muhimu yaliyowekewa kipaumbele katika bajeti ili kuboresha miundombinu na hali ya upatikanaji wa Huduma za afya nchini.

Akieleza taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba, 2018 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma, Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee Mh. Ummy Mwalimu amesema wizara hiyo iliidhinishiwa na Bunge kupokea na kutumia bajeti ya jumla ya shilingi bilioni 866.24 ambapo Kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 304.44 ilikua ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo shilingi 88.47 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 216.7 kwa ajili ya Mishahara ya watumishi walio makao makuu ya Wizara pamoja na Watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Waziri Ummy amesema fedha zilizopokelewa katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2018 zimeainishwa katika utekelezaji wa majukumu ya wizara katika kipindi hicho ambapo maeneo muhimu kama Chanjo, afya ya mzazi na mtoto, mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, upatikanaji wa damu salama, uimarishaji wa huduma za kibingwa, Utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali za Kanda, Maalum, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali za Rufaa za Mikoa pamoja na uhakiki ubora wa huduma za afya yalipewa kipaumbele.

Aidha, Waziri Ummy amesema Wizara imeendelea kusimamia na kuratibu shughuli zilizokuwa zimepangwa kutekelezwa na Taasisi zilizopo chini yake. Taasisi hizo ni pamoja na Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Mabaraza ya Kitaaluma.

Hata hivyo, pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika utekelezaji wa Majukumu ya Wizara (Idara Kuu ya Afya), Waziri Ummy amebainisha changamoto mbalimbali zikiwemo Vituo vya kutolea huduma za Afya kutowasilisha mahitaji ya dawa, Vifaa, Vifaa tiba na Vitendanishi kwa wakati, Upatikanaji wa Huduma Bora na za Uhakika za Uzazi Mama na Mtoto, Upungufu wa watumishi wenye taaluma ya kutoa huduma za afya ikilinganishwa na mahitaji, Wigo mdogo wa wananchi walio katika mifumo ya Bima za Afya pamoja na Kuongezeka kwa watu wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza jambo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma.


Naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) na katibu mkuu wa wizara ya afya Dkt. Zainab Chaula (kushoto) wakisikiliza kwa makini na kutafakari jambo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma.

wajumbe na kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara katika kamati hiyo.

Wajumbe na kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara katika kamati hiyo.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images