Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

WAHITIMU WA USTAWI WA JAMII KISANGARA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

$
0
0
 Wahitimu wa taaluma ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kilichoko wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma yao ili kujitofautisha na watumishi wengine kutokana na elimu waliyoipata.

Rai hiyo imetolewa na Kamishina wa Ustawi wa Jamii Kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Dkt. Naftali B. Ng’ondi wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kwa wahitimu kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Dkt. Ng’ondi amesema kuwa wataalam mbalimbali wamekuwa wakivamia kazi za Ustawi wa Jamii kwa kudhani kuwa ni kazi holela kuweza kufanywa na mtu yeyote na  kuwakumbusha wahitimu kuwa kazi za ustawi wa jamii ni muhimu na inapaswa kufanywa na wataalam wenye weledi wanatoa huduma kwa kuzingatia maadili na miiko ya kazi.

 Amekipongeza Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kwa kuonesha mafanikio chanya kwani kmwaka wa masomo 2016/2017 wakati chuo kinaanza kulikuwa na wanafunzi 56 tu. Lakini kwa mwaka wa masomo 2018/2019 chuo kimedahili wanafunzi 158 ambapo  wanafunzi wa kike ni 115 na wa kiume ni 43 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100 katika udahili ukilinganisha na mwaka 2016/17.

Kamishna Ngondi amepongeza jitihada uongozi wa Chuo kwa kufanikisha usajili wa kudumu Chuo na mtaala kutolea mafunzo na huduma bora inayotolewa na Chuo katika kusimamia mafunzo na kuongeza nyenzo mbalimbali za kutolea mafunzo kama kompyuta na projector jambo ambalo limekuwa chachu ya ongezeko la udahili wa wanafunzi.

“Wizara inatambua changamoto zilizopo za uchakavu na miundombinu ya madarasa na mabweni hiyo tutaendelea kuimarisha na kukarabati majengo ya chuo ili kuwa na mazingira bora zaidi ya kusomea na kujifunzia”.alisema Dkt. Ng’ondi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Anna Mwingira amewapongeza wazazi  na walezi kwa kuthamini utoaji wa fursa sawa kwa wasichana na Mtoto wa kike na kuwezesha udahili wa wanafunzi wa kike kufikia asilimia 73 ukilinganisha na asilimi 43 ya wavulana, ongezeko ambalo ni takribani ni mara mbili zaidi ya wavulana.

“Hii ni dalili njema kuwa jamii inaendelea kuelewa azma ya Serikali ya kuwawezesha wanawake ili kuwapa mbinu na stadi za kuweza kutoa mchango katika kufikia uchumi wa kati na wa viwanda’’ aliongeza.

Aidha Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa jamii Kisangara Anna Mwingira alieleza kuwa awali kuanzia mwaka 1986 hadi mwaka 2012 chuo kilikuwa kinatoa mafunzo kwa ngazi ya cheti katika fani ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto (ECD, Non NTA level). Kuanzia Julai 2012 mafunzo katika fani ya ustawi wa jamii pia yalianza kutolewa katika ngazi ya cheti kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, American International Health Alliance (AIHA) na Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama (Institute of Social Work D’SALAAM – ISW).

 Mwingira ameleza kuwa Chuo kina usajili wa kudumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) uliopatikana mnamo tarehe 29/3/2017 na Na.  REG/BTP/009 kwa kozi ya Ustawi wa Jamii ngazi ya Astashahada hadi ngazi ya Diploma na kwa sasa Chuo kinatoa mafunzo katika fani ya ustawi wa Jamii ngazi ya Cheti na Diploma (NTA Level 4, 5 and 6) na fani ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (ECD) ambayo inasimiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Chuo kinaendesha amsomo kwa kutumia mtaala wake wa fani ya ustawi wa jamii, ambao ulikamilika mwaka 2016/2017.

Naye mmoja wa wahitimu Immaculate Kinama na Elizaberth Kawishe kwa wakati tofauti walibainisha kuwa wamejengewa weledi kwani wanayo maarifa, mbinu na stadi za kuwawezesha kufanya majukumu yao kwa umahiri katika kusaidia wahitaji kama vile watu wenye ulemavu, wazee, watoto na makundi yote yenye uhitaji maalum katika jamii.

Taaluma ya ustawi wa jamii msingi wake ni haki na ustawi katika jamii ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma na kubaguliwa ama kutengwa katika huduma mbalimbali za maendeleo ya jamii husika. Pia, taaluma hii ni muhimu katika kuwasaidia watu walio katika makundi tete mfano wanaonyanyaswa, wanaonyanyapaliwa na maskini sana ili waweze kufaidika na rasilimali au huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu, afya, shughuli za kiuchumi, burudani na shughuli mbalimbali katika jamii na kupata habari kwa mfano kwa watu wasiosikia.

Haya ni Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii kisangara baada ya kupita miaka 33 bila kusanyiko la mahafali. Wahitimu 158 wametunukiwa vyeti katika ngazi ya Astashahada wakiwa na wajibu wa  kuwezesha huduma za ustawi wa jamii katika ngazi ya kata, mashule ya awali, msingi sekondari, na maeneo mengine kama vile Ofisi za Polisi, Mahakama, Magereza na katika jamii kwa ujumla.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto (Idara kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. Naftali B. Ng’ondi akimtunuku cheti kwa mmoja wa wanafunzi wahitimu wa Astashahada ya Ustawi wa Jamii Esher Reubeni katika Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Kilimajaro.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali B. Ng’ondi akiwahutubia wahitimu na halaiki ya watu waliohudhuria kusanyiko la mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara mkoani Kilimanjaro.
 Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kilichoko Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Anna Mwingira akieleza mafanikio ya Chuo  hicho katika Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Kilimajaro.
 Baadhi ya  ndugu na jamaa wa wahitimu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi katika Mahafali ya Chuo cha hichoa ambaye ni Kamishina wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali B. Ng’ondi katika Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Kilimanjaro.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. Naftali B. Ngondi akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara wakati wa Mahafali ya kwanza ya Chuo hicho. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

SERIKALI YATOA MAAGIZO KWA WAFUGAJI

$
0
0

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akizungumza na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Singida kabla ya kuanza ziara ya uhamasishaji wa kuogesha ng'ombe katika kijiji cha Mgori.
Bw.Rashid Mandoa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Singida akitoa taarifa kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega.
Bw.Elia Digha,Mwenyekiti wa halmashauri ya Singida akitoa ujumbe kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega (hayupo pichani)kuhusu kuweka mikakati katika sekta ya mifugo nchini.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akikagua ng'ombe katika kijiji cha Mgori kilichopo Singida vijijini alipokuwa ameenda kuzindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
Baadhi ya ng'ombe wakisubiri kuogeshwa dawa katika josho la Mgori katika hamshauri ya wilaya ya Singida vijini ambapo Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alizindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akichanganya dawa za kudhibiti magonjwa ya mifugo katika kijiji cha Mgori kwa ajili ya kuhamasisha kuogesha ng'ombe katika majosho yalipo nchini ambapo Serikali imeamua kutoa dawa bure kwa wafugaji.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akisaidiana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo katika josho lenye dawa ambazo zimetolewa bure na Serikali zoezi hilo la uzinduzi katika mkoa wa Singida lilifanyika katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida vijijini.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog



Na.Alex Sonna,Singida

Serikali imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya mifugo pamoja na kudhibiti magonjwa ya mifugo huku ikiwahimiza wafugaji kuzingatia matumizi ya majosho yenye dawa.

Akizungumza na wafugaji Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega wakati wa zoezi la uhamasishaji wa uogeshaji wa ngo’mbe kanda ya kati mkoani Singida, katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida vijijini.

Katika uhamasishaji huo waziri Ulega aliwataka wafugaji kufanya zoezi la uogeshaji wa mifugo uliyoanzishwa uwe wenye tija na endelevu, kwa vile hivi sasa hakuna sababu za kushindwa kuogesha mifugo yao katika majosho yenye dawa ya kudhibiditi kupe.

Aidha amesema kuwa kwa sasa serikali katika zoezi hili, imetoa dawa bure kwa halmashauri zote nchini, na kukarabati majosho yote yaliyokuwa hayafanyi kazi, ili wafungaji waweze kuogesha mifugo yao , kukinga ugonjwa hatari unaoenezwa na kupe, ambao unaoongozwa katika vifo vya ng’ombe hapa nchini.

"Mwanzo shughuli hizo zilikuwa zikifanywa kwa ,kutofuata taratibu nzuri za makusanyo yalikuwa yakitoka kwa wafugaji walipokuwa wakipata huduma za kuongesha mifugo yao, hazikuwa na taarifa ya mapato na matumizi na hivyo kushindwa kuwa na utaratibu endelevu wa shughuli hiyo, majosho mengi yalisimama kufanya kazi"amesema Ulega

Katika kampeni hii ya uhamamishaji wa uongeshaji wa mifugo tozo imepunguwa ambapo hivi sasa kila ng’ombe ana ogeshwa katika majosho ni shilingi 50 tu, huko nyuma uogeshaji ulikuwa unatozwa wastani wa shilingi mia 2 kwa kila ngo’mbe na kwa mbuzi ilikuwa shilingi 10.

“Nyie wafugaji msikalie rasialimali hii ya mifugo mliokuwa mnayo, kwani ni uchumi mkubwa sana mliyokuwa nayo kwenu na pia kwa Taifa ili kuongeza mapato, yanayotokana na mifugo yenu”amesisitiza Ulega.Aidha alifafanua kuwa ufungaji kwa kufuata taratibu za ufugaji wa kisasa na kibiashara kwa kuvuna mifugo inapozidi katika eneo uliyokuwa nayo, itakusaidia kupata kipato katika kuboresha maisha yako na ya familia.

Uhamasishaji huu unafuatia uzinduzi wa kampeni ya uogeshaji wa mifugo,iliyofanywa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina katikati ya mwezi jana katika kijiji cha Buzirayombo halmashauri ya chato.

Bilioni 3.5 kujenga makazi ya Askari Dodoma

$
0
0
Jumla ya nyumba Mia Moja za Makazi ya Askari zimeanza kujengwa  mkoani Dodoma  ikiwa ni Mpango  wa  serikali  kukabiliana na changamoto za makazi ya  Askari Polisi watakaohamia hivi karibuni baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kutekeleza agizo la kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani hapa

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama kutembelea eneo la Medeli Mashariki ambapo Awamu ya Kwanza ya mradi huo ukihusisha nyumba 30, Ujenzi wa Shule ya Awali, Ujenzi wa Kantini, Ujenzi wa Viwanja vya Michezo tayari imeshaanza

“Ujenzi wa nyumba hizi unakwenda sambamba na ujenzi wa nyumba kama hizi katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha askari wanaishi sehemu safi na lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha ujenzi wa nyumba kama hizi  kote nchini unafanyika kwa gharama nyepesi na tukitumia wataalamu wa ujenzi waliopo serikalini na katika Jeshi la Polisi..” alisema Masauni

“…..mradi huu utakua na awamu tatu ambapo mwezi April mwaka jana, awamu ya kwanza ilianza na kutarajiwa kukamilika April mwaka huu huku awamu zilizobakia zikitarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu na  hadi kufikia mwaka kesho katikati awamu zote zitakua zimekamilika” aliongeza Masauni

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu amewapongeza Viongozi wa wizara na Jeshi la Polisi kwa mradi huo huku akishauri miradi mingine wajenge maghorofa ili kuweza kuitumia ardhi waipatayo kwa matumizi mengine sambamba na ujenzi wa makazi ya askari.

“Nawapongeza kwa kutumia mapato yenu wenyewe ya ndani kuanzisha miradi mikubwa kama hii na sisi wajumbe wa kamati tumeridhishwa na hatua hizi za kukabiliana na makazi ya wapiganaji wetu wanaotulinda usiku na mchana na nchi yetu kuendelea kuwa na amani,” alisema Zungu

Jumla ya gharama ya mradi huo wa nyumba Mia  Moja za Makazi ya Askari Polisi ni Bilioni Mia Tatu na Laki Tano ambazo zinatokana na Mfuko wa Tuzo na Tozo ikiwemo malipo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na askari polisi na faini zinazotozwa na askari kwenye makosa mbalimbali.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akitoa maelezo ya Ujenzi wa Nyumba mia moja kwa ajili ya makazi ya  askari polisi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Medeli, jijini Dodoma zinapojengwa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Zungu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu akimuuliza maswali Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea eneo la Medeli, jijini Dodoma zinapojengwa nyumba mia moja kwa ajili ya makazi ya askari polisi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) akiongozana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Medeli,jijini Dodoma zinapojengwa nyumba mia moja(pichani) kwa ajili ya makazi ya askari polisi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akiwaongoza  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Ihumwa ,jijini Dodoma yanapojengwa Makao Makuu ya wizara hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Baadhi ya nyumba  zinazojengwa katika eneo la Medeli ikiwa ni mkakati maalumu wa Serikali ya Awamu ya Tano kujenga makazi ya askari polisi nchi nzima ili kuwaondolea askari changamoto za makazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MKUTA YAWAPATIA WACHIMBAJI ELIMU YA KIFUA KIKUU NA UKIMWI

$
0
0
ILI kutokomeza maambukizi ya kifua kikuu, HIV na Silikosis, kwenye migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wachimbaji 13,328 wamepatiwa elimu ya kujikinga kupitia shirika la mapambano ya kifua kikuu na ukimwi (Mkuta). Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Mapambano ya kifua kikuu na ukimwi Tanzania (Mkuta) Thobias Magati aliyasema hayo wakati akizungumzia kazi za huduma ya jamii kwa mwaka jana. 

Magati alisema katika watu hao 13,328 waliofikiwa, wanaume walikuwa 11,307 wanawake 1,804 na watoto ni 217 na wagonjwa waliogundulika ni 123. Alisema uwezeshaji ni mdogo kwao kwani hawana wafadhili ila mwaka jana waliwezeshwa na Kibong'oto OHSC kufikia wagonjwa wengi. "Uwezeshaji ndiyo mdogo ila wameweza kufungua matawi ya Mkuta kwenye maeneo ya kitalu B (Opec) na kitalu D ambayo yapo kwenye migodi inayowazunguka ili kusaidia shughuli za uibuaji," alisema Magati. 

Alisema wanafanya hayo ili kufikia malengo ya tamko la kisiasa la umoja wa mataifa la kutokomeza kifua kikuu ifikapo mwaka 2022. Alisema endapo kuna asasi au taasisi yeyote itakayokuwa inataka kuonana nao wawasiliane nao kupitia namba za simu 0789564832 au barua pepe ya mkutaclubmirerani@gmail.com watawapata. Katibu wa Mkuta, Benjamin Kaba alisema wanakabiliwa na changamoto ya wagonjwa wengi wa kifua kikuu, gharama ya ufuatiliaji na kutopata vipimo kwa wakati. 

Kaba alisema changamoto nyingine ni wachimbaji wengi wanaugua ugonjwa wa Silikosis na Pneumonia ambayo yanahitaji kufanyiwa utafiti wa kina zaidi na mabadiliko ya ukuta yamesababisha wagonjwa kushindwa kutoka kwenda kupata huduma.  Alisema changamoto nyingine ni kuhamahama kwa wagonjwa kwenda migodi mingine ya Kitwai, Lemshuku, Mwajanga, Landanai na Kimwengani. 

Alisema wana mikakati mingi yakufanikisha mipango yao ila wanakwamishwa kutokana na ukata unaowakabili kwani hawana mfadhili wa kukisaidia kikundi hicho chenye wanachama 58. Mjumbe wa Mkuta, Mwasiti Ntandu alitoa wito kwa serikali kuiangalia Mirerani kwa jicho la pekee kwani magonjwa ya kifua kikuu na Silikosis inayosababishwa na ulanga imewaathiri watu wengi. Ntandu alisema baadhi ya wachimbaji wamewaacha wajane na yatima kutokana na kuugua maradhi hayo ambayo yanaweza kutibika. 
 Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Mkuta la Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Thobias Chacha Magati akielezea mikakati ya asasi yao. 
Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Mkuta la Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Thobias Chacha Magatiakisoma kanuni na sheria za Mkuta. 
Wanachama wa shirika lisilo la kiserikali la Mkuta wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakifurahia pamoja baada ya taarifa ya utekelezaji wa huduma kwa jamii ya mwaka jana.

MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA MIKOA YA PWANI, MANYARA,TABORA, NA KIGOMA.

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa pili kushoto aliyevaa suti) akipewa maelezo na wafanyakazi wa kivuko cha MV. MKONGO mara baada ya kukagua kivuko hicho. Kivuko cha MV. MKONGO kinatoa huduma katika mto Rufiji kati ya Mkongo na Utete wilayani Rufiji mkoani Pwani na kina uwezo wa kubeba abiria 40 kwa wakati mmoja.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua mashine ya kupimia uwiano wa tairi za magari katika karakana ya TEMESA mkoa wa Manyara wakati wa ziara yake mkoani humo. Kushoto ni Meneja wa Temesa mkoani Manyara Mhandisi Margreth Julian.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa pili kushoto) akishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. MALAGARASI mara baada ya kumaliza kukagua utendaji kazi na hali ya usalama wa kivuko hicho kinachotoa huduma katika mto Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma, kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50. Wa kwanza Kushoto ni Nahodha wa kivuko Kassimu Mkitege. 
Abiria wakiingia katika kivuko cha MV. MALAGARASI tayari kuanza safari kutokea upande wa Ilagala kuelekea upande wa Kajeje, kivuko cha MV MALAGARASI kinatoa huduma katika mto Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma na kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50. 
Kivuko cha MV. MALAGARASI kikielea katika mto Malagarasi, kivuko hicho cha tani 50 kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 kwa wakati mmoja na kinatoa huduma kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma.
Nahodha wa Kivuko cha MV. MALAGARASI Kassimu Mkitege kushoto akiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kulia wakati alipokua akikagua hali ya usalama na utendaji kazi wa kivuko hicho. Kivuko cha MV MALAGARASI kinatoa huduma katika mto Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma. 

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO - (TEMESA)

Halmashauri 4 zatuhumiwa kwa ubadhilifu

$
0
0

Angela Msimbira OR-TAMISEMI.

Halmashauri nne (4) zimetuhumiwa kwa ubadhilifu wa zaidi ya shilingi milioni 785 fedha zilizotolewa kupitia mradi wa Equip-T kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali za Elimu katika halmashauri hizo. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya tuhuma za ubadhilifu katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya TAMISEMI, Jijini Dodoma 

Amezitaja Halmashauri ambazo zimetumia fedha hizo kinyume na utaratibu kuwa Manispaa ya Kigoma, Butiama, Liwale na Bahi ambapo hadi kufikia sasa halmashauri hizo hazijaweza kurejesha fedha hizo TAMISEMI tangu agizo lilipotolewa. 

Mhe. Jafo amesema OR-TAMISEMI iliziagiza Halmashauri 8 ambazo zilituhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha hizo kuzirejesha lakini mpaka sasa ni Halmashauri nane tu ndizo zilizorejesha fedha hizo kwa wakati na hizo zilizobakia kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kutotii maagizo ya Serikali. 

“Inasikitisha kuona baadhi ya Halmashauri kushindwa kutii maagizo yanayolewa na Serikali ya kutaka Halmashauri zilizotuhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha za Equipt T kurejesha fedha hizo ili ziweze kutekeleza miradi ya elimu nchini” anasema. 

Ameendelea kufafanua kuwa amesikitishwa zaidi na Manispaa ya Kigoma Ujiji na Butiama kutokana na kuwa na tuhuma nyingi za ubadhilifu wa fedha za miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo. 

Mhe. Jafo ameziagiza Halmashauri ambazo bado hazijakamilisha kurejesha fedha hizo kuhakikisha zinawasilishwa kabla ya tarahe 28/3/2019. 

Amezielekeza mamlaka husika kuwachukulia hatua za kinidhamu na kuwashusha vyeo Afisa Mipango, Mweka Hazina na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kwa kushindwa kutimiza wajibu wao. 

Mhe. Jafo ameitaka mamlaka inayohusika kufanya uchunguzi wa aliyekuwa Mkurugenzi, amemuagiza Katibu MMkuu OR-TAMISEMI kuwachukulia hatua Mweka Hazina wa Halmashauri ya Bahi Said Ishabairu ambaye alihamishiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. 

“Kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watumishi kuhamishwa maeneo ya kazi pale wanapokosea, hili si jambo jema Serikali haitavumilia bali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wanaoihujumu Serikali popote pale watakapokuwa” alisema. 

Aidha ameziagiza Mamlaka husika kumtafuta aliyekuwa Mweka Hazina wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye kwa sasa amestaafu ili aweze kuhojiwa kwa tuhuma hizo. 

Jafo aliongeza kuwa Serikali haitavumilia mambo yeyote ambayo yanaleta hujuma katika suala zima la kuwahudumia watanzania hivyo amewataadharisha Wakurugenzi wote katika Halmashauri za Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa katika matumizi ya fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Jafo alimalizia kwa kumuagiza Naibu Waziri Mhe. Mwita Waitara kusimamia kwa makini miradi ya elimu na kuangalia namna fedha zilizvyotumika katika miradi hiyo agizo ambalo Mhe. Mwita amesema alalitekeleza kwa umakini mkubwa. 

WAHITIMU WA USTAWI WA JAMII KISANGARA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

$
0
0
 Wahitimu wa taaluma ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kilichoko wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma yao ili kujitofautisha na watumishi wengine kutokana na elimu waliyoipata.

Rai hiyo imetolewa na Kamishina wa Ustawi wa Jamii Kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Dkt. Naftali B. Ng’ondi wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kwa wahitimu kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Dkt. Ng’ondi amesema kuwa wataalam mbalimbali wamekuwa wakivamia kazi za Ustawi wa Jamii kwa kudhani kuwa ni kazi holela kuweza kufanywa na mtu yeyote na  kuwakumbusha wahitimu kuwa kazi za ustawi wa jamii ni muhimu na inapaswa kufanywa na wataalam wenye weledi wanatoa huduma kwa kuzingatia maadili na miiko ya kazi.

 Amekipongeza Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kwa kuonesha mafanikio chanya kwani kmwaka wa masomo 2016/2017 wakati chuo kinaanza kulikuwa na wanafunzi 56 tu. Lakini kwa mwaka wa masomo 2018/2019 chuo kimedahili wanafunzi 158 ambapo  wanafunzi wa kike ni 115 na wa kiume ni 43 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100 katika udahili ukilinganisha na mwaka 2016/17.

Kamishna Ngondi amepongeza jitihada uongozi wa Chuo kwa kufanikisha usajili wa kudumu Chuo na mtaala kutolea mafunzo na huduma bora inayotolewa na Chuo katika kusimamia mafunzo na kuongeza nyenzo mbalimbali za kutolea mafunzo kama kompyuta na projector jambo ambalo limekuwa chachu ya ongezeko la udahili wa wanafunzi.

“Wizara inatambua changamoto zilizopo za uchakavu na miundombinu ya madarasa na mabweni hiyo tutaendelea kuimarisha na kukarabati majengo ya chuo ili kuwa na mazingira bora zaidi ya kusomea na kujifunzia”.alisema Dkt. Ng’ondi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Anna Mwingira amewapongeza wazazi  na walezi kwa kuthamini utoaji wa fursa sawa kwa wasichana na Mtoto wa kike na kuwezesha udahili wa wanafunzi wa kike kufikia asilimia 73 ukilinganisha na asilimi 43 ya wavulana, ongezeko ambalo ni takribani ni mara mbili zaidi ya wavulana.

“Hii ni dalili njema kuwa jamii inaendelea kuelewa azma ya Serikali ya kuwawezesha wanawake ili kuwapa mbinu na stadi za kuweza kutoa mchango katika kufikia uchumi wa kati na wa viwanda’’ aliongeza.

Aidha Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa jamii Kisangara Anna Mwingira alieleza kuwa awali kuanzia mwaka 1986 hadi mwaka 2012 chuo kilikuwa kinatoa mafunzo kwa ngazi ya cheti katika fani ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto (ECD, Non NTA level). Kuanzia Julai 2012 mafunzo katika fani ya ustawi wa jamii pia yalianza kutolewa katika ngazi ya cheti kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, American International Health Alliance (AIHA) na Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama (Institute of Social Work D’SALAAM – ISW).

 Mwingira ameleza kuwa Chuo kina usajili wa kudumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) uliopatikana mnamo tarehe 29/3/2017 na Na.  REG/BTP/009 kwa kozi ya Ustawi wa Jamii ngazi ya Astashahada hadi ngazi ya Diploma na kwa sasa Chuo kinatoa mafunzo katika fani ya ustawi wa Jamii ngazi ya Cheti na Diploma (NTA Level 4, 5 and 6) na fani ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (ECD) ambayo inasimiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Chuo kinaendesha amsomo kwa kutumia mtaala wake wa fani ya ustawi wa jamii, ambao ulikamilika mwaka 2016/2017.

Naye mmoja wa wahitimu Immaculate Kinama na Elizaberth Kawishe kwa wakati tofauti walibainisha kuwa wamejengewa weledi kwani wanayo maarifa, mbinu na stadi za kuwawezesha kufanya majukumu yao kwa umahiri katika kusaidia wahitaji kama vile watu wenye ulemavu, wazee, watoto na makundi yote yenye uhitaji maalum katika jamii.

Taaluma ya ustawi wa jamii msingi wake ni haki na ustawi katika jamii ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma na kubaguliwa ama kutengwa katika huduma mbalimbali za maendeleo ya jamii husika. Pia, taaluma hii ni muhimu katika kuwasaidia watu walio katika makundi tete mfano wanaonyanyaswa, wanaonyanyapaliwa na maskini sana ili waweze kufaidika na rasilimali au huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu, afya, shughuli za kiuchumi, burudani na shughuli mbalimbali katika jamii na kupata habari kwa mfano kwa watu wasiosikia.

Haya ni Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii kisangara baada ya kupita miaka 33 bila kusanyiko la mahafali. Wahitimu 158 wametunukiwa vyeti katika ngazi ya Astashahada wakiwa na wajibu wa  kuwezesha huduma za ustawi wa jamii katika ngazi ya kata, mashule ya awali, msingi sekondari, na maeneo mengine kama vile Ofisi za Polisi, Mahakama, Magereza na katika jamii kwa ujumla.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto (Idara kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. Naftali B. Ng’ondi akimtunuku cheti kwa mmoja wa wanafunzi wahitimu wa Astashahada ya Ustawi wa Jamii Esher Reubeni katika Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Kilimajaro.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali B. Ng’ondi akiwahutubia wahitimu na halaiki ya watu waliohudhuria kusanyiko la mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara mkoani Kilimanjaro.
 Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara kilichoko Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Anna Mwingira akieleza mafanikio ya Chuo  hicho katika Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Kilimajaro.
 Baadhi ya  ndugu na jamaa wa wahitimu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi katika Mahafali ya Chuo cha hichoa ambaye ni Kamishina wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali B. Ng’ondi katika Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara Kilimanjaro.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. Naftali B. Ngondi akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara wakati wa Mahafali ya kwanza ya Chuo hicho. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

MILIONI 1500 ZILIZOTOLEWA NA OFISI YA RAIS –TAMISEMI KUJENGA HOSPITALI YA KISASA HALMASHAURI YA MUFINDI

$
0
0
Na Ofisa Habari Mufindi 

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetiliana saini na Mafundi Uashi saba (07), watakaotekeleza kandarasi za awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya Wilaya katika kata ya Igowole, eneo ambalo liliteuliwa rasmi kuwa makao makuu mapya ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Hafla fupi ya kusaini kandarasi hizo imefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ambapo, jumla ya Majengo saba muhimu yatajengwa ambayo ni Jengo la Utawala, Jengo la Wagonjwa wa nje, Jengo la kuhifadhia dawa, Jengo la kufulia, Jengo la Mionzi, Jengo la Wazazi sanjari na Jengo la Maabara ambayo yanatajikiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi nane (08)

Aidha, kiasi cha Fedha kitakachotumika kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi huu mkubwa na muhimu kwa ustawi wa Afya za wakazi wa Mufindi ni shilingi Milioni elfumoja na miatano (1,500) sawa na shilingi Bilioni 01 na Milioni 500 zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini, Mwenyekiti wa Halmashari Mhe. Festo Mgina, amewataka Mafundi hao kutekeleza maradi kwa wakati sanjari na kuzingatia viwango vilivyokubalika na atahakikisha wanapata vifaa na malipo yao kwa wakati ili Hospitali hiyo ikamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Halmashauri ya Mufindi.

Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bw. Isaya Mbenje, ametoa rai kwa wataalamu hao wa ujenzi kufanya kazi kwa weledi mkubwa, kuacha visingizio vya mara kwa mara vitakavyochelewesha kukamilika kwa mradi.

“Pigeni kazi Fedha tunayo, yote ipo kwenye akaunti inawasubiri ninyi, hivyo yeyote atakayekwamisha tutavunja mkataba, atafukuzwa pamoja na kufunguliwa mashitaka” akihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu huyo.

Imetolewa na
Ofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano
HALMSHAURI YA WILAYA MUFINDI
  ikionesha ramani ya majengo mara baada ya kukamilika
Mafundi wateule wakisaini kandarasi za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina kushoto, akikabidhi mkataba kwa mmoja kati ya Mafundi Saba walioshinda zabuni ya kujenga Hospitali.


SEKRETARIETI YA AJIRA YATAKIWA KUTENDA HAKI ILI KUIWEZESHA SERIKALI KUPATA WATUMISHI WENYE SIFA STAHIKI

$
0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Sekretarieti hiyo Magogoni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier M. Daudi akieleza majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika katika ofisi ya Sekretarieti hiyo Magogoni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Magogoni katika ofisi ya Sekretarieti hiyo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier M. Daudi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuhusu namna mfumo wa upokeaji wa maombi ya kazi (Recruitment Portal) na mfumo wa kupanga wasailiwa waliofaulu inavyofanya kazi wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira alipoitembelea ofisi hiyo kuhimiza uwajibikaji.


Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetakiwa kuendelea kutenda haki katika kuratibu mchakato wa ajira ili kuiwezesha Serikali kupata watumishi wenye sifa stahiki na maadili mema ambao watatoa huduma kwa umma kwa kuzingatia weledi na kuwajali wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Taasisi za umma. 

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo iliyopo Magogoni jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu kwa kina majukumu ya Sekretarieti hiyo na kujiridhisha namna Sekretarieti hiyo inavyotekeleza majukumu yake ya kila siku. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kinatakiwa kutenda haki ili Serikali ya Awamu ya Tano ipate watumishi wenye sifa na vigezo watakaoendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuliletea taifa maendeleo katika sekta za miundombinu, afya, viwanda, biashara, kilimo, usafiri wa anga, elimu na uchumi kwa ujumla wake. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, awali Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilikuwa ikilalamikiwa sana kuwa, mchakato wa kuomba kazi Serikalini ulikuwa ukichukua muda mrefu kiasi cha waombaji kusahau kama waliwasilisha maombi, hivyo ameipongeza Sekretarieti kwa kubuni mfumo wa upokeaji wa maombi ya kazi (Recruitment Portal) na mfumo wa kupanga wasailiwa waliofaulu ambayo kwa kiasi kikubwa imepunguza malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na waombaji wa ajira Serikalini na kuongeza kuwa, hivi sasa mchakato wa ajira mpya unachukua siku 52 tu licha ya kuwepo taratibu nyingi zinazozingatiwa kukamilisha mchakato mzima. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua kuwa, mfumo huo una kanzi data ya waombaji wote waliofanyiwa usaili na kupata ufaulu mzuri lakini kutokana na uwepo wa fursa chache za ajira hawakupangiwa vituo vya kazi, hivyo unaiwezesha serikali kupata watumishi kwa wakati pindi wanapohitajika haraka katika Taasisi za Umma. 

Sanjari na hayo, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameitaka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kutobweteka kwa mafanikio waliyoyapata kupitia mfumo wa Ajira Portal na badala yake waongeze kasi ya ubunifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imedhamiria kwa dhati kuboresha huduma zinazotolewa na Taasisi za Umma nchini. 

Kwa upande wake, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier M. Daudi, amesema ofisi yake ilianzishwa kwa lengo mahususi la kukabiliana na changamoto za ajira zilizokuwa zikijitokeza hapo awali, hivyo iliundwa ili kuongeza uwazi, kutenda haki na kuhakikisha kuwa ajira zinapatikana kwa kuzingatia sifa. 

Bw. Daudi amesisitiza kuwa, ofisi yake kwa kushirikiana na waajiri inazingatia Sera ya Ajira, Sheria, Kanuni na Taratibu katika kusimamia mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kuiwezesha Serikali kupata watumishi wenye sifa na maadili mema watakaoisaidia Serikali kufikia malengo yake makubwa iliyojiwekea, ikizingatiwa kuwa watumishi ndio injini ya utekelezaji wa majukumu ya Serikali. 

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Mbarak Abdulwakil amemshukuru Mhe. Dkt. Mwanjelwa kwa nasaha zake za kuitaka Sekretarieti kuzingatia weledi katika jukumu zito la kuwezesha ajira za watumishi wa umma na kumhakikishia kuwa, maelekezo yote aliyoyatoa yatatekelezwa kikamilifu na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inatekeleza majukumu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutafuta wataalam wenye ujuzi maalum na kuandaa mfumo wa kuifadhi taarifa za wataalam, kutangaza nafasi wazi za kazi zinazojitokeza katika Utumishi wa Umma, kuhusisha wataalam ili kushirikiana nao kwa ajili ya kufanya usaili kulingana na mahitaji, kuwashauri waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na mchakato wa ajira, kuandaa orodha ya wahitimu wa vyuo na wataalam kwa weledi kwa madhumuni ya kurahisisha rejea za ujazaji nafasi na kuendesha mchakato wa ajira wa Watendaji Wakuu wa Wakala na Idara zinazojitegemea za Serikali.

WADAU WA MAENDELEO WAMUUNGA MKONO DC MURO UJENZI WA MADARASA

$
0
0
Wadau mbalimbali wa maendeleo Wilayani Arumeru wameendelea Kujitokeza na kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Jerry Cornel Muro katika ujenzi wa madarasa.

Wadau hao wa maendeleo Waliahidi kuchangia mifuko 100 ya Saruji na kwa Awamu ya kwanza leo Hii wamemkabidhi Dc Muro mifuko 50 ya saruji na kuahaidi ndani ya wiki mbili zijazo watakamilisha ahadi yao. 

Wakizungumza mara baada ya kukabidhi mifuko hiyo ya saruji wameeleza kuwa Lengo la kumuunga mkono Dc Muro katika ujenzi wa madarasa ni kwamba wanaamini Katika kujenga jamii imara lazima kuhakikisha Elimu inapewa kipaumbele cha pekee pia wameeleza hawana budi kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amewashuku wadau hao wa maendeleo kuendelea kujitolea katika kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanapata madarasa ya kutosha

Pia Dc Muro amewaomba Wadau wengine kuja kumuunga mkono katika kuchangia ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Arusha Dc na Halmashauri ya Meru. 

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
20/01/2019

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 21 2019

LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Arusha


Waumini wa dini ya Kikristo Jijini Arusha wametakiwa kulipa kodi ya serikali kama inavyotakiwa siyo kuiba, kwani wao wanatakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii inayowazunguka

Hayo yamesemwa na Makamu wa Askofu Dayosisi ya kaskazini Kati Gidion Kivuyo alipokuwa akihubiri katika katika la KKKT Usharika wa Engarenarok uliopo Jiji Arusha.

Amesisitiza kuwa kumjua Mungu Pamoja na kukataa rushwa, kutokuiba mali ya serikali kwani hata neno la Mungu linasisitiza kulipa kodi.'' Lipeni kodi ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu nanukuu maandiko siyo mimi''Alisema Mchungaji Kivuyo.Amewataka waumini hao kuishi maisha safi ya kuigwa maana ni chachu katikati ya kwa watu wengine wanaowatazama ambapo uadilifu, nidhamu na uchaji ambao kizazi kijacho kitajifunza kutoka kwao.

Amewasisitiza kuwa na utayari na kujifunza,akisema uanafunzi ni pamoja na kujikana wenyewe, kuepuke mambo ambayo siyo sahihi katika imani yao, na waenende sambamba na neno la Mungu linavyowataka.

Amewataka kujifunza na kutafakari siyo kufuata mkumbo bila Kuwa na mipangilio katika maisha bila kusahau uzalendo na kuchunguza mambo kwa kina.
'' Kuna watu wanaojifunza bila kufuzu mafunzo ya kweli, msiwe watu wasiopenda mema na kupenda anasa bali dumuni katika kweli ya Mungu ambayo itawaweka huru,epukeni kutangishwatangishwa kwenye mafundisho ya uongo nakupenda fedha" Alisema.

Amewataka kuwa na uelewa kwamba Imani haijengwi juu juu bali kwa mafundisho, huku akiwataka kuepuka utumwa ambao utawafanya mateka.
Amewaonya waumini hao na kuwataka makini na mafundisho ya uongo ambayo yanayogusa hisia lakini hayafundishi ukweli bali ni misisimko na wala hayana ukweli sawasawa na Mungu anavyoamuru.

Kadhalika amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii iliwaweze kupata mafanikio sambamba na kulipa kodi ya serikali, na siyo kuzurura hovyo. '' Wacheni kuzunguka kwenye maombi kila mahali unachelewa wenzio wamefungua biashara zao na wamefanikiwa, wewe kutokana na kutokutulia kwako unabakia ukilaumu'' alisema

Amewaataka viongozi wa kanisa hilo kuwakumbusha waumini wao neno la Mungu mara kwa mara na kuwafundisha, Kutambua, kujuta, kutubia, kupokea, kuishi maisha na dhamiri safi mbele za Mungu. Amewataka kuweka malengo ya mwaka 2019 na siyo kuishi bila utaratibu ili waweze kurejea katika msingi mzuri wa kanisa hilo.

BENKI YA NMB YATOA MFUNGAJI BORA BBL 2018/19

$
0
0

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Juma Kimori, akimkabidhi nahodha wa timu ya kikapu ya NMB, Danford Kisinda, kombe la ushindi wa pili wa Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya DTB, iliyopigwa leo Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda kwa pointi 90-73.


Mshambuliaji wa NMB, Kaikai Leka, akipaa hewani kuifungia timu ya kikapu ya NMB wakati wa fainali ya Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya DTB, iliyopigwa Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda kwa pointi 90-73.
Mfungaji Bora wa mashindano ya kikapu kwa taasisi za fedha (BBL 2018/19), Kaikai Leka wa NMB, akipokea kombe dogo kama zawadi ya ufungaji bora kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Juma Kimori, baada ya pambano la fainali ya michuano hiyo Januari 19 kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa NMB, Kaikai Leka, akipaa hewani kuifungia timu ya kikapu ya NMB wakati wa fainali ya Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya DTB, iliyopigwa leo Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda kwa pointi 90-73.


NA MWANDISHI WETU


NYOTA wa mpira wa kikapu wa kikosi cha Benki ya NMB, Kaikai Leka, ameibuka Mfungaji Bora (Best Scorer) wa Ligi ya Kikapu kwa Taasisi za Fedha (Bankers Basketball League - BBL 2018/19), baada ya kufunga pointi 160 katika mechi za michuano hiyo iliyofikia tamati juzi, jijini Dar es Salaam.

Katika fainali ya kukata na shoka jana kwenye Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam, Benki ya DTB iliibuka mshindi baada ya kuifunga NMB kwa pointi 90-73, huku mchezaji wa NMB Leka akifunga zaidi ya nusu ya pointi zao hivyo kutangazwa Mfungaji Bora akifuatiwa na Acram Majid wa DTB, aliyefunga pointi 129.

Leka alizawadiwa Tuzo ya Mfungaji Bora, kama ilivyokuwa kwa Mchezaji Bora (MVP) Leonard Benedict wa DTB, Beki Bora Frank Mwemezi wa DTB na kinara wa kufunga pointi tatu kwa mtupo mmoja (Leading Three Pointer), Acram Majid aliyefanya hivyo mara 13 katika michuano yote.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi na kufunga mashindano, Mratibu wa BBL 2018/19, Gozbert Boniface, alizipongeza timu sita zilizoshiriki michuano hiyo kwa upande wa mpira wa kikapu na kuzitaka kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao, utakaoanza baadaye mwaka huu.

“Tunaipongeza DTB kwa kutwaa taji, lakini pia kwa NMB kwa kutwaa medali za fedha za ushindi wa pili na pia kwa kutoa Mfungaji Bora wa michuano hii, iliyoshirikisha mabenki sita ya NMB, DTB, Azania, CRDB, TADB na NBC,” alisema Boniface wakati akitoa neno la shukrani.

Kwa upende wake, Mgeni Rasmi wa fainali hiyo, Juma Kimori, ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, aliwapongeza waratibu kwa wazo zuri la kuanzisha michuano hiyo, iliyoimarisha mahusiano baina ya taasisi za kifedha nchini, huku akiwapongeza mabingwa na washindi wa pili wa michuano hiyo.


Mshambuliaji wa NMB, Kaikai Leka, akiwatoka walinzi wa timu ya kikapu ya DTB wakati wa fainali ya Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya timu hizo mbili uliyopigwa Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda pointi 90-73.

HATIMAYE TAMASHA LA PASAKA KUREJEA KWA KISHINDO,KUANZIA JIJINI DAR

$
0
0
Hatimaye tamasha la Pasaka ambalo limekuwa likisindikizwa na kishindo cha muziki wa injili chini ya uratibu wa  kampuni ya Msama Promotions Ltd ya jijini Dar es Salaam, limerejea tena kwa maandalizi makubwa.

Tamasha hilo kongwe ambalo limekuwa likifanyika tangu mwaka 2000, kwa miaka miwili halikuweza kufanyika katika jiji la Dar es Salaam kutokana na sababu maalumu zilizowahi kuelezwa na waratibu wa tukio hilo la kimataifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa habari jana Januari 21, 2019, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema baada ya tafakuri ya kina pia kwa kuzingatia maoni ya wadau wa muziki wa injili, wameamua kurejesha tukio hilo jijini humo.

“Kama mnavyojua, kwa miaka kama mitatu hivi, tamasha la Pasaka lilikuwa likifanyika mikoani tu, lakini kwa mwaka huu litatafanyika pia katika jiji hilo kwa sababu vilio vya wadau wa muziki wa injili ni vikubwa mno,” alisema Msama."Kutokana na maombi ya Wadau kuw mengi kuhusu tamasha hilo, Wadau kilio chao kimesikika,hivyo tamasha hili litaanzia hapa hapa jijini Dar na kuendelea mikoa mingine ambayo itatajwa hapo baadae"aliongeza Msama

Alisema mbali ya malengo ya msingi ya kueneza ujumbe wa Neno la Mangu na sehemu ya mapato kusaidia makundi maalumu, safari hii tamasha hilo litatumika pia kuhimiza hali ya amani chini ya kaulimbiu isemayo ‘Upendo, haki na Amani ndio msingi wa amani.’

Msama alisema, kwa kuzingatia uhalisia huo tamasha hilo litabeba agenda ya kuombea amani taifa na kumwombea Rais John Magufuli aweze kuongoza kwa ufanisi na mafanikio zaidi kwa maslahi ya watanzania wote.

Kwa upande wa maandalizi, Msama alisema tofauti na miaka mingi, safari hii wamejiandaa kuhakikisha linakuwa la kimataifa zaidi ikiwemo kuwaleta waimbaji mahiri wa kutoka nje watakaoshirikiana na wengine wa Tanzania.

Mbali ya Dar es Salaam, Msama alisema tamasha hilo litafanyika pia katika mikoa mingine 10 ambayo itajulikana baadaye kwa kuzingatia vigezo stahiki vilivyowekwa na kamati ya maandalizi.

Chini ya maudhui ya msingi ya Tamasha hilo, ni kueneza ujumbe wa Neno la Mungu kupitia waimbaji, kukuza muziki wa injili ili kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji vya kuimba na kumiliki jukwaa na wauzaji wa kazi za kimuziki.

Tangu kuanza kwa tamasha hilo, waratibu wamekuwa walitumia sehemu ya mapato ya viingilio kuyafariji makundi maalumu katika jamii; walemavu, yatima pamoja na wajane.

Tukio hilo ndilo limechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili nchini kutokana na waratuibu kuwaleta waimbaji mbalimbali wa kimataifa kama Solly Mahlangu, Sipho Makabane na Rabeca Malope wa Afrika Kusini. 

Wasanii wengi wamekuwa wakishiriki katika tamasha hilo wakiwepo wa Tanzania kama Upendo Nkone, Christopher Mahangila, Rose Mhando, Sifael Mwakabuka , Matha Mwaipaja, Beatrice Mwaipaja, Joshua Mlelwa pamoja na kwaya mbalimbali, huku katika mataifa kama ya Kenya wasanii wa Injili kama Solomon Mukubwa,Kutoka Afrika kusini kama vile  Solly Mahlangu, Sipho Makabane na Rabeca Malope na wengine wengi.
 Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akizungumza jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa habari jana Januari 21, 2019,kuhusu ujio upya na maandalizi ya tamasha la Pasaka 2019,linatarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar.Msama amesema kuwa kwa miaka kama mitatu hivi, tamasha la Pasaka lilikuwa likifanyika mikoani tu, lakini kwa mwaka huu litaanzia jijini Dar  kwa sababu vilio vya wadau wa muziki wa injili ni vikubwa mno

 Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alipokuwa akifafanua zaidi kuhusu ujio mpya na maandalizi makubwa ya tamasha la Pasaka 2019,ambalo linatarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar.

SERIKALI YAKANUSHA TAARIFA ILIYOSAMBAZWA KUPITIA CCTV-AFRIKA


MTUMISHI WA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ALIYEPOTEA

$
0
0
NICKSON .K. KEIYA AMBAYE NI MTUMISHI WA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KAMA MENEJA WA SHAMBA LA KUZALISHA MITAMBA LA SAO HILL L.M.U LILILOPO WILAYANI MAFINGA MKOA WA IRINGA AMEPOTEA TANGU 15/01/2019 AKIWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA YA USAJILI MC 214 BZZ AINA YA KING LION NYEKUNDU KATIKA MAENEO YA ILUNDI/MISITU YA SAO HILL.

TAARIFA ZA KUPOTEA KWAKE ZIMERIPOTIWA KITUO CHA POLISI MAFINGA – IRINGA (MFG/RB/166/2019).

KWA MARA YA MWISHO ALIKUWA AMEVAA SURUALI YA KAKI NA SHATI LENYE RANGI YA UDONGO YENYE MICHIRIZI MYEUPE NA RABA ZA RANGI YA KAKI YENYE SOLI NYEUPE.

KWA ATAKAYEMUONA TUNAOMBA ATOE TAARIFA KWENYE KITUO CHOCHOTE CHA POLISI KILICHOPO KARIBU NAE. 

AU APIGE SIMU NAMBA
• 0713 757157
• 0762 952766


Imetolewa na R. Mbulalina.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
DODOMA.

Waziri Ummy Mwalimu akagua ukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya Moyo

$
0
0
Na Genofeva Matemu – JKCI.

20/01/2019 Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI) imekuwa   taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na wodi pekee ya kuwahudumia watoto wenye magonjwa ya moyo bila kuwachanganya na watu wazima.

Eneo la wodi hiyo lilitolewa mwaka 2017 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli alipokua akizindua Hospitali ya Mloganzila na kuiagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoa sehemu ya jengo linalohudumia watoto kwa JKCI ili watoto wenye magonjwa ya moyo waweze kuwa na wodi yao katika kuleta ufanisi wa matibabu ya moyo kwa watoto hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi hiyo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamaii, Jinsi, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema upatikanaji wa wodi hiyo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha utolewaji wa matibabu ya moyo kwa watoto ya kibingwa yanaendelea kuboreshwa hapa nchini.

“Kwa wodi za watoto wenye magonjwa ya moyo peke yake kwa hapa Afrika Mashariki na kati hii ndio itakua wodi ya kwanza inayowahudumia watoto bila kuwachanganya na watu wazima na hii italeta ufanisi zaidi kwani nafasi ya kufanya makosa haitakuwepo kwasababu kutakuwa na wataalamu wanaohudumia watoto tu” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy, alisema  wodi hiyo ambayo ukarabati wake umekamilika inatarajiwa kuwa  na vitanda 32 na chumba cha uangalizi maalum (ICU) kitakachokuwa na vitanda 15 jambo ambalo litasaidia kuwafanyia upasuaji watoto wengi zaidi waliopo katika foleni ya upasuaji na kuokoa maisha yao. 
“Serikali ilitoa milioni 700 kwa ajili ya ukarabati wa wodi hii na sasa kwa mara nyingine tena serikali imetoa milioni 500 kukamilisha miundombinu ya ukarabati wa wodi hii. Nawashukuru sana taasisi ya Baps Charity ambao nao wamewekeza  milioni 800 katika kuhakikisha kuwa wodi hii inakarabatiwa, serikali tutazidi kuunga mkono ju

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prf. Mohamed, Janabi alisema kwa shifti mbili za kliniki ya watoto zilizopo JKCI inaona wagonjwa wa moyo hadi sitini kwa siku thelathini wakiwa ni watoto, hivyo kulikuwa na umuhimu wa kuongeza wodi hiyo ya watoto. 

Akizungumzia upasuaji wa magonjwa ya moyo prof. Janabi amesema kuwa jumla ya wangonjwa 1356 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa mwaka 2018, hii kwa mwaka jana ukiondoa Afrika kusini JKCI ndio hospitali iliyofanya upasuaji kwa wangonjwa wa moyo wengi zaidi kuliko nchi yoyote ya Afrika.
“Wodi hii mpya ni kwaajili ya watoto chini ya miaka 13 pekee na hii itatufanya kuwa taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na kati kuwa na jengo lenye kuhudumia watoto bila kuwanchanganya na watu wazima “alisema prof. Janabi
 Meneja wa Jengo la Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Kikwete Flora Kassembe akimwelezea Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu namna ambavyo wodi ya watoto itakavyotumika wakati wa ziara fupi ya waziri huyo kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na mtoto Shakira Athumani kutoka Tanga anayesubiria kufanyiwa upasuaji wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) baada ya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza baada ya kufanya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Meneja wa Jengo la taasisi hiyo Flora Kassembe. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wadau wa taasisi ya Baps Charity  baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo na kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto katika taasisi hiyo Jinini Dar es Salaam. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wagonjwa wanaosubiri kupatiwa huduma za matibabu ya moyo baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.  Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa katika Taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto Loveness Richard anayesubiri kuingizwa katika chumba cha upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cathlab baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.  Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa katika taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza aliyemfikisha mjukuu wake katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupata matibabu ya moyo Donata John (kushoto) baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.  Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa katika taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwenye paja alipotembelea wodi za wagonjwa wa moyo baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam. 

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza aliyemfikisha mjukuu wake katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupata matibabu ya moyo Donata John (kushoto) baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.  Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa katika taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwenye paja alipotembelea wodi za wagonjwa wa moyo baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam. 

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo  tarehe 21/01/2019 Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Angela Kairuki kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo  tarehe 21/01/2019 Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na wanahabari mara baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo  tarehe 21/01/2019 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo  tarehe 21/01/2019 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU



Waziri Mkuu Majaliwa kufungua Mkutano wa Maafisa Ustawi wa Jamii

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kufungua mkutano wa siku tatu wa maafisa ustawi wa jamii mikoa 26 na halmashauri zote nchini wenye lengo la kujadili utendaji kazi, utoaji huduma za ustawi wa jamii na mifumo ya utendaji kazi. 

Akizungumza na habarileo jijini hapa, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi, Rashid Maftaha, alisema mkutano huo unatarajia kuanza Januri 29 hadi 31 mwaka huu jijini Dodoma. 

Alisema mkutano huo unatarajia kushirikisha washiri takribani 370 ikiwamo maafisa ustawi wa jamii wa mikao 26, halmashauri 184, wadau wa maendeleo, na wizara za kisekta ambazo zinahusiana na utoaji wa huduma za ustawiwa jamii, kama wizara ya elimu, afya, Katiba na Sheria, Viwanda na Biashara, madini na kilimo. 

“ Unaweza jiuliza, Wizara ya Madini inahusikajie na huduma za ustawi wa jamii, hawa ni wadau muhimu, kwani kwenye migodi kuna utumikishwaji wa watoto, na hata watumishi wake wanakuwa wako mbali hivyo ni lazima wafikiwe na huduma za jamii, halii hii pia iko kwenye viwanda. 

“Pia unaweza kujiuliza kwa nini wizara ya kilimo, lakini ukweli ni kuwa asimia 80 ya watanzania wanafanya shughuli za kilimo na asilimia 70 yao wako vijijini, na takwimu zetu zinaonesha kuwa watoto wengi walio katika mazingia hatarishi wanatoka vijijini ambaochanzo kikubwa na umasikini na jangwa la Ukwimi. 

Maftaha aliongeza:” Tunashuku wenzetu wa kilimo katika Mpango wa Maendeleo ya Kilimo kwa kwanza na huu wa pili ni jumuishi kwani kuna dirisha maalumu kwa ajili ya watu walio katika mazingira hatarishi wakiwemo, wenye ulemavu, wajane, wazee ambao wanapata pembejeo na wana uwakilishi katika kamati za ugawaji pembejeo 

Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Weledi, uadilifu, uwajibikaji ni nguzo ya msingi katika kuleta usatawi wa makundi maalumu kuelekea katika uchumi wa kati wa viwanda.” 

Maftah alisema: “ Tunaamini watendaji wetu kwenye halmashauri na mikoa wakifanya kazi zao kwa kuzingatia uadilifu, weledi, wakifuata sheria, kanuni na taratibu tunaamini makundi yenye uhitaji maalumu wanaweza kufikiwa inavyotakiwa hivyo mchango wao ukaongezeka katika uchumi wa viwanda, 

Mkutano huu ni wa kwanza ikiwa ni takribani miaka 15 baada ya kutokea mabadiliko ya kimuundo kwa kuiondoa Idara ya Ustawi wa Jamii kutoka Serikali kuu kwenda Serikali za Mitaa. 

Akifafanua zaidi, Maftaha alisema serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikifanya kwa vitendo katika kuwahudumia wananchi hususani wale wanyonge ikiwamo wazee, wenye ulemavu, watoto wa mitaani na wale wanaoishi katika mazingira magumu, wanawake wenye mahitaji maalumu kama wajane, wenye magonjwa sugu na walio katika kaya masikini. 

Alisema lengo la mkutano ni kuwakutanisha watendaji hao na kutoa mrejesho wa utekelezaji wa huduma za jamii katika maeneo ya serikali za mitaa, utendaji kazi na namna mfumo inavyofanya kazi. 

“ Pia tutaangalia mafanikio na changamoto na kwa upamoja na kuja na mapendekezo ya kutatua changamoto stahiki za za kiutendaji na mfumo ili kusogeza na kuimarisha zaidi hudumua za ustawi wa jamii kwenye mamlaka ya serikali za mitaa. Kama kuna yale ambayo yatataka kuwepo mabadilko ya kisera basi tutafikisha katika mamlaka husika. 

Aidha, Maftah ametumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kuendelea kuwalinda watoto kwa kutoa taarifa haraka kwa mamlaka pale panapokuwa na viiashiria ay dalili au kitendo cha ukatili kwa mtoto. 

Alisema pamoja na pamekuwa na changamoto ya ushahidi pale kesi zinapofika mahakamani au wahanga na mashahidi kubadili taarifa walizotoa awali, lakini ni vyama jamii ikaungana kutakabiliana na ukatili kwa watoto. 

“Hatuwezi kukubali vitendo vya ukatili anavyofanyiwa mtoto alafu tuambiwe kuwa wamekubaliana pembeni hilo hatulikubali mpaka sheria ichukue mkondo wake.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI, Rashid Maftaha.

JIJI LA ARUSHA LINA ZIADA YA UMEME MEGAWATI 50, TANESCO YAALIKA WAWEKEZAJI ZAIDI KWENYE VIWANDA

$
0
0
Na Ripota Wetu, MIRERANI .

 UWEKEZAJI kwenye miundombinu ya umeme uliofanywa na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania TANESCO umeanza kuzaa matunda eneo la machimbo ya madini Mirerani mkoani Manyara. 

 Serikali kupitia TANESCO iliwekeza kwa kujenga kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha KIA na hivyo kuwezesha hali ya upatikanaji umeme ulio bora na wa uhakika kwenye eneo la Mirerani kuongezeka. 
 Kwa sasa matumizi ya umeme kwenye eneo lote la Mirarani ni kiasi cha Megawati 3.5 lakini kubwa zaidi miongoni mwa watumiaji wakubwa walioanza kufaidika na uwekezaji huo ni pamoja na kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (Graphite) na kile cha Mirerani Tanzanite vyote viko Mirerani. 

 Meneja wa Shirika la Umeme wilaya ya Ki-TANESCO Mirerani Mhandisi Zacharia Masatu amewaambia waandishi wa habari wanaotembelea eneo hilo kuwa kiwanda hicho pekee kinatumia kiasi cha Megawati 1.1 ya umeme. 
 Aidha Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina amesema jiji lina ziada ya umeme Megawati 50, na hivyo amewahimiza wawekezaji katika sekta ya viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kuwekeza ili kufaidi uwekezaji wa serikali katika miundombinu ya umeme nchini. 

 “Wito wetu kwa wafanyabiashara na wawekezaji, waje wawekeze kwenye mkoa wetu wa Arusha sababu kama tulivyoeleza awali tuna umeme wa kutosha, kwa mkoa mahitaji ni Megawati 75 na uwezo wa kituo chetu ni Megawati 120 kwahiyo unaweza kuona tuna ziada inayofikia Megawati 50.” alisema Mhandisi Mhina. 

 Mhandisi Mhina alibainisha kuwa, viwanda vinaweza kuleta matokeo makubwa ya uwekezaji katika miundombinu ya umeme uliofanywa na serikali kwani matumizi ya kiwanda kimoja inaweza kuwa ni mahitaji ya wilaya nzima. 

 “Viwanda ni njia mojawapo inayoweza kutupeleka kwenye uchumi wa kati tunaotaka kwa haraka zaidi.” Alisisitiza. TANESCO ilifunga mitambo ya kuingiza umeme wa kutosha kwenye kiwanda cha Godmwanga Gems Limited na kwamba kinajitegemea ambapo kuna jumla ya transfoma pozo kubwa tatu na gharama za ufungaji wa mitambo hiyo zinakadiriwa kufikia shilingi Milioni 60.

Aidha afisa wa kiwanda hicho cha kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (graphite), Nai Mainga alisema kiwanda kilianza uzalishaji wa madini hayo ya graphite (kinywe) Juni 2018 na kwamba tangu uzalishaji uanze hadi hivi sasa, tayari wamezalisha kiasi cha tani 5,600 na wateja wakubwa wa madini hayo ni China. 

 “Matumizi makubwa ya madini hayo ya kinywe hutumika kutengeneza vitu maka betri na tunapozungumzia betri ni pamoja na betri zile kubwa za magario na mitambo, lakini pia kuna taarifa kuwa madini hayo hutumika kutengeneza bati maalum la kuzuia injini ya ndege ili isipate moto sana kwani madini haya huchomwa sana ili kupata zao la mwisho.” Alifafanua. 
 Alisema kuna baadhi ya nchi ambazo tayari zimeanza mchakato wa kusitisha matumizi ya petrol kuendeshea magari na hivyo kuna uwezekano wa kutumia madini haya ili kutengeneza betri za kuendesha magari.

Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina(kushoto), akimsikiliza Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Ki-TANESCO Mirerani, Mhandisi Zacharia Masatu, akifafanua kuhusu namna TANESCO ilivyoweza kufikisha umeme wa kutosha kwenye eneo la Mirarani leo Januari 21, 2019.
Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina
Kituo cha kupokea umeme kilichoko ndani ya kiwanda cha kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe, (graphite) huko Mirerani mkoani Manyara ambapo TANESCO imefu nga mitambo na transfoma kubwa tatu ili kutoa umeme toshelezi kwa kiwanda hicho.transfoma pozo kubwa tatu zilizofungwa na TANESCO kwenye kiwanda hicho.
Kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (Graphite)
Kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (Graphite)
Mhandisi Zacharia Masatu, akifafanua jambpo ndani ya kituo cha kupokelea umeme kwenye kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (Graphite).

Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images