Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

MAKONDA AWATAKA WAKAZI WA DAR KUCHANGAMKIA MPANGO WA BIMA YA MSINGI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa huo kutumia fursa ya upatikanaji wa bima ya msingi hili kujiwekea nafuu ya Maisha kama alivyoagiza Rais Magufuli.

Makonda amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mpango mpya wa bima ya afya ya msingi kwa wakzi wa mkoa huo.“Bima hii ni nafuu san asana kwani familia ya watu sita itaweza kulipa kiasi cha Shilingi laki moja na amsini tu huku mtu ambaye atakuwa anaishi peke yake atalipa shilingi elfu arobaini kwa mwaka”amesema Makonda

Amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam umeandaa wataalamu Zaidi ya 1000 ambao watakuwa wanapita kila mtaa katika wilaya zote tano hili waweze kuandikisha kila kaya kuweza kupata huduma hii.

Makonda ametaja kuwa uwepo wa Bima hiyo ya Msingi utasaidia watu kuacha kuchangishana kwa ajili ya mtu katika familia kuchangiawa kwa ajili ya matibabu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mpango wa bima ya aAfya unaotolewa na mkoa wa Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Dr. Grace Maghembe akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mpango wa bima ya Afya unaotolewa na mkoa wa Dar es Salaam.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF na CHF),Nicholaus Mwangomo akieleza na namna mfumo wa bima ya msingi utakavyowasaidia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Mshauri kiongozi wa HPSS, Ally Kebby akizungumza namna gani walivyojipanga kukamilisha mpango wa bima ya msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Waandishi wa Habari wakifatilia Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda juu ya mpango wa bima ya aAfya unaotolewa na mkoa wa Dar es Salaam.

NDUGU WADAIWA KUSHIRIKI KUFICHA USHAHIDI VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO-SHINYANGA

$
0
0
Na Anthony Ishengoma.

Matendo ya ukatili yaliyolipotiwakatika Jeshi la Polisi hapa Nchini yamefikia 13 elfu mpaka kufikia mwaka jana tofauti na matukio takribani elfu 10 yaliyolipotiwa katika jeshi hilo kwa takwimu za mwaka 2016-17.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kinachoendelea katika Manispaa ya Shinyanga kujadili jumbe mahususi zitakazotumika katika jitihada za serikali kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Sebastian Kitiku amesema vitendo vya ukatili vinazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka hapa Nchini.

 Kitiku amewaambia wajumbe wa kikao kazi hicho kuwa Wizara ya Afya inatengeneza jumbe mahususi za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na wadau wa Mkoa wa Shinyinga kwa kuwa mkoa wa Shinyanga ni moja ya mikoa inayoongoza katika kiwango kikubwa cha Mimba na Ndoa za utotoni hapa Nchini.

Wakati huohuo Mkurugenzi wa Utawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela amewataka viongozi wa Mkoa na Almashauri, viongozi wa dini, vyombo vya ulinzi na usalama vya Mkoa huo  kuhakikisha wanafanya kazi kubwa kumaliza tatizo hilo kwa kuwa haamini kama tatizo hilo linatokana na mila za wakazi wa mkoa wa Shinyanga.

‘’Siamini kama vitendao hivi vinatoka na mila potofu bali ni mmomonyoko wa maadili kwa kuwa wazazi na walezi wameacha jukumu lao la kuwalea watoto kama inavyostahili bali wanafuata hali ya sasa ya utandawazi’’. Alisema Msovela.

Aidha Msovela alionya kuwa Serikali ya Mkoa wa Shinyanga haitaendelea kuvumilia vitendo hivyo kwa kuwa kwa matukio ya Mkoa huo unaweza ukajiuliza kama unahitaji huruma ya mweneyezi Mungu kwasababu kumekuweko mauaji ya vikongwe, Watu wenye Uaribino, vipigo kwa akina mama na sasa mimba na ndoa za utotoni.

Msovela ametaja takwimu za hali ya ukatili Mkoani humo kuwa ni kubwa kwa kuwa kwasasa mkoa unaonesha una kiasi cha 34% za mimba za utotoni na ndoa za utotoni  ni asilimia ni asilimia 59%na kuzitaka jamii mkoani humo kubadilika ili watoto wa kike wapate fursa ya kutimiza ndoto zao.

Aidha amewaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa tatizo la mimba za mapema ni kubwa sana kwani kwa Wilaya ya Kishapu pekee kwa mwaka jana jumla ya watoto 57 wa shule walipata ujauzito.

Ameongeza kuwa kwasasa wazazi wamekuwa wakishirikiana na waalifu kuficha ushaidi baada yukupewa ng’ombe na hivyo kushindwa kutoa taarifa ili waanga wa ukatili waweze kupata haki baada ya kugwa wamefanyiwa vitendao vya ukatili.

‘’Hata ikitokea suala la ukatili limepelekwa mahakamani wanajamii husika wamekuwa hawajitokezi mahakamani kutoa ushahidi jambo ambalo linasababisha utokomezaji wa vitendo vya ukatili kuwa mugumu kwa kuwa mahakama inawaachia huru wahusika kwa kukosa ushaidi’’. Alilamika Kiongozi huyo wa Utawala Mkoani hapo Msovela.

Amemwagiza Afisa Elimu wa Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha walimu wanatoa taarifa za wanafunzi wanaoacha shule kwa sasbabu za ndoa na ujauzito ili mkoa uweze kuchukua zinazostahili ikiwemo kuwafikisha wahusika katika vyombo vya sheria.

Kazi ya kutengeneza ujumbe kwa ajili ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni inaendelea itaendelea katika mikoa yenye takwimu za juu katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo ni mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida na Rukwa.   
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Sebastian Kitiku akiongea na wadau kujadili hali jumbe zitakazotumika kutokomeza vitendo vya ukatili mkoani Shinyanga leo mjini Shinyanga.
 Afisa Tawala Mkoa wa  Shinyanga Albert Msovela akiongea na wadau kujadili hali jumbe zitakazotumika kutokomeza vitendo vya ukatili mkoani Shinyanga leo mjini Shinyanga.
 Baadhi ya  wadau kujadili hali jumbe zitakazotumika kutokomeza vitendo vya ukatili mkoani Shinyanga leo mjini Shinyanga.
Baadhi ya  Wajumbe  kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii wakiwa Mkoani Shinyanga  kujadili hali jumbe zitakazotumika kutokomeza vitendo vya ukatili.

WANAFUNZI VYUO VIKUU WAALIKWA KUJIFUNZA TEKNOLOJIA MPYA YA COMBINE CYCLE MITAMBO YA KUFUA UMEME WA GESI KINYEREZI II

$
0
0
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MITAMBO ya kufua umeme wa gesi asilia kwenye kituo cha Kinyerezi II jijini Dar es Salaam imetumia teknolojia ya kisasa kabisa ijulikanayom kama combine cycle na kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kutumia teknolojia hiyo.Akifafanua kuhusu teknolojia hiyo, Meneja Miradi (uzalishaji) wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Mhandisi Stephene S. A. Manda, amesema baada ya mitambo ya kufua umeme utokanao na gesi, mvuke unaozalishwa kwa awamu ya kwanza kutokana na joto hupelekwa tena kwenye mtambo mwingine na huko unazalisha umeme wa awamu ya pili.Alisema, tayari TANESCO imepokea maombi kutoka nchi mbalimbali zikiwemo zile za SADC kuja kujifunza teknolojia hiyo, ambapo katika mitambo nane ya kufua umeme iliyoko Kinyerezi II, miwili ni ile itokanayo na mvuke (steam turbines)“Tulivyokuwa na mkutano wa SAPP kule Arusha yaani Southern Africa Power Pool nchi mbalimbali zimeonyesha nia ya kuja kujifunza teknolojia hii.” Alisema. Mhandisi Manda ametoa wito kwa vyuo mbalimbali vinavyotoa taaluma ya uhandisi wa umeme kupeleka wanafunzi ili wajifunze teknolojia hiyo ya kisasa.“Wanafunzi wanao….Practice engineering wako kwenye field ambao hawajaona teknolojia inavyofanya kazi waje wajifunze.” Alisema.

 Moja ya mitambo ya kufua umeme utokanao na mvuke (steam turbine) kwenye kituo cha kufua umeme wa gesi asilia Kinyerezi II jijini Dar es Salaam.
 Meneja Miradi (uzalishaji) wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Mhandisi Stephene S. A. (kulia) na Meneja wa kituo cha kufua umeme wa gesi cha Kinyerezi II,  Mhandisi Ambakisye Mbangula, (katikati), wakimsikiliza mhandisi huyu kutoka nje anayehudumu kwenye mitambo hiyo wakati huu wa kumalizia ujenzi.
 Mhandisi Manda akifafanua kuhusu mitambo ya kisasa iliyofungwa kwenye kituo hicho.
Mhandisi Manda akizungumza na wafanyakazi wa TANESCO kwenye chumba cha udhibiti mwenendo wa mitambo ya umeme (control room) Kinyerezi II.

TCAA YAZINDUA MNARA WA KUONGOZEA NDEGE KATIKA UWANJA WA NDEGE PEMBA, ZANZIBAR

$
0
0
 Mgeni rasmi, Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof.Makame Mbarawa, akikata utepe kuzindua mnara wa kuongozea ndege wa Pemba, baada ya kufanyiwa Ukarabati mkubwa. Hafla hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.  Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Prof. Makame Mbarawa akizungumza mbele ya umati uliofika katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege Pemba. 
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba Dr. Sira Ubwa Mamboya akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege Pemba.  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari akihutubia katika katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege Pemba.  Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Pro. Makame Mbarawa, Katika picha ya pamoja na viongozi wengine was serikali wakaribishaji wa hafla ya Uzinduzi wanara wa kuongozea ndege wa Pemba.  Mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege Pemba. 
Baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi mnara wa kuongozea ndege wa Pemba, baada ya kufanyiwa Ukarabati mkubwa. Hafla hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Mgeni rasmi akiwasili Katika hafla ya Uzinduzi mnara wa Kuongozea ndege Pemba.



Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezindua mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Pemba, Zanzibar.

Mradi huu umegharimiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Prof. Makame Mbarawa amesema mnara huo umezinduwa mara baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ulioanza Novemba 2017 hadi Agosti 2018.

Amesema kuwa mradi huu wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 300 ni miongoni mwa miradi inayozinduliwa katika wiki ya maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Mradi unalenga kuboresha huduma za uongozaji ndege katika uwanja wa ndege wa Pemba pamoja na kuimaimarisha usalama wa abiria na vyombo vinavyotumia uwanja huu. Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba Dr. Sira Ubwa Mamboya ameishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha miundo mbinu inayopelekea kupata matokeo chanya. 

"Binafsi sina la kusema leo nimefurahi sana kuona jinsi serikali zetu zinavyopambana kuleta miundo ya kisasa ili kuweza kwenda na teknolojia ya kisasa," amesema. Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari amesema ukarabati umefanywa na Kampuni ya kitanzania ya M/s Future Century Limited ambapo kazi zilizofanyika ni pamoja na kubadilisha vioo vinavyozunguka mnara wa kuongozea ndege, kurekebisha paa na kuzuia kuvuja, kuweka vizuizi vya usalama (guard rails) na kuweka upya mfumo wa viyoyozi (Air conditioning), kuweka upya mfumo wa umeme, kuweka upya mfumo wa simu na taarifa za kieleckroniki na kupaka rangi upya. 


Ameongeza kuwa TCAA ina jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Majukumu ya kisheria ya Mamlaka ni pamoja na kudhibiti masuala ya ki-usalama, ki-uchumi katika usafiri wa anga na kutoa huduma za uongozaji ndege. TCAA inatoa huduma za uongozaji ndege kwenye vituo kumina nne (14) ambavyo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Mwanza, Tabora, Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Songea, Mtwara, Zanzibar na Pemba

TUME YA MAADILI KUMALIZA KESI ZAIDI YA MIA NDANI YA MIEZI MITANO

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mwenyekiti wa Tume ya Maadili Jaji Steven Bwana amesema tume yake itashughulikia kesi Zaidi ya 100 zilizorundikana kwa muda wa miezi sita kuanzia sasa.

Akizungumza wakati wa kutoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mwenyekiti amesema mara baada ya kupata nafasi ya kuaminiwa na Mh Rais Kuongoza tume hiyo wamegundua kuna mafaili mengi ayajafanyiwa kazi.

“Tumekuta kesi Zaidi ya 100 ambazo zimelimbikizwa kuanzia mwezi wa 2/2018, hivyo tunashukuru sisi kuwa wa kwanza kupata nafasi ya uteuzi katika mwaka huu wa 2019 hivyo tunahahidi kuchapa kazi kwa spidi ileile anayokwenda nayo Rais wetu, hivyo tunajipanga kufika mwezi wa sita tuwe tumemaliza kesi zote”alisema 

Amesema kuwa wao kama viongozi wa tume wanajua kuna changamoto kubwa ya rasilimali fedha katika ofisi yao lakini watajitahidi kufanya kazi kwa bidi bila kusubiri posho hili kuweza kutatua kero za Watanzania ambao wamesubiri kwa muda mrefu.

“tunatambua Changamoto wanayokutana nayo watumishi wa Umma ambao wameleta malalamiko yao katika tume ya maadili na kuna wengine wanategmea ukumu ndio waanze kulipwa stahiki zao hivyo tunawaomba wawe wavumilivu ndani ya miezi hii sita kila kitu kitakuwa sawa”alisema.

Kwa upande wake Naibu WazirNaibu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary M. Mwanjelwa, amesema watumishi wa tume wanapaswa kujituma na kufuata sharia bila kuangalia nafasi ya mtu.Dk. Mwanjelwa amewataka Watanzania kuwa na Imani na tume hiyo kwa sasa na itafnya maamuzi kwa kutenda haki
Naibu WazirNaibu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary M. Mwanjelwa,akizungumza na Watumishi wa Tume ya Taifa ya Maadili 
Naibu WazirNaibu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary M. Mwanjelwa,akizungumza na Makamishna wa Tume ya Maadili walieteuliwa hivi karibuni
Wajumbe na Wafanyakazi wa tume ya Maadili wakimsikiliza Naibu WazirNaibu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary M. Mwanjelwa.
Naibu WazirNaibu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary M. Mwanjelwa,akiwa katika Picha ya Pamoja na Makamishna wa Tume ya Maadili. Picha na Zote na Humphrey Shao wa MMG

Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) yatoa mashine ya Ultrasound ambayo itatumika kwa ajili ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiograph) kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea mashine ya Ultrasound kutoka kwa Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiograph). Thamani ya mashine hiyo ambayo itatumika kwa watoto ni shilingi milioni 34.
Mhandisi wa vifaa tiba Evance Swai kutoka Pacific diagnostic akiwaonyesha madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sulende Kubhoja na Naiz Majani jinsi mashine ya Ultrasound ambayo imetolewa na Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) inavyofanya kazi. Mashine hiyo itatumika kwa ajili ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiograph) kwa watoto wenye matatizo ya moyo ni thamani yake ni shilingi milioni 34.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sulende Kubhoja na Naiz Majani wakiangalia mashine ya Ultrasound ambayo imetolewa na Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiograph) kwa watoto wenye matatizo ya moyo.Picha na JKCI

Benki ya CRDB yakabidhi Milioni 20 katika Hospitali ya Sekou Toure Jijini Mwanza

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Benki ya CRDB imekabidhi hundi ya shilingi Milioni 20 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza, Sekou Toure ili kusaidia ukarabati na ununuzi wa vifaa tiba katika wodi ya upasuaji (Theatre) ya akina mama katika Hospitali hiyo.


Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi hundi hiyo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alisema benki hiyo ni mdau mkubwa katika kuboresha huduma za afya hapa nchini ambapo imekuwa ikitoa asilimia moja ya faida yake kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza, Dkt. Bahati Msaki aliishukru Benki ya CRDB kwa mchango huo na kwamba utasaidia kuondoa changamoto ya utoaji huduma za afya kwa akina mama.


Mbali na hundi hiyo, pia Benki ya CRDB ilikabidhi luninga (TV) tatu za kisasa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa, Bugando  ili kutoa huduma kwa wananchi na wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akizungumza kwenye hafla hilo.
Baadhi ya watumishi wa Benki ya CRDB.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akipokea hundi ya shilingi Milioni 20 kutoka Benki ya CRDB. Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Katibu Tawala mkoani Mwanza, Dkt. Christopher Kadio, Mwenyekiti wa Bodi Hospitali ya Sekour Toure, Christopher Gachuma, Mganga Mkuu Hospitali hiyo, Dkt. Thomas Rotachunzibwa pamoja na watumishi wa Hospitali hiyo.
Makabidhiano hayo yakiendelea
Tazama BMG Online TV hapa chini

WAHUKUMIWA KULIPA FAINI ZAIDI YA SH MILIONI 200 BAADA YA KUKIRI KUENDESHA BIASHARA HARAMU YA UPATU NA UTAKATISHAJI FEDHA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii.

VIGOGO wawili na Wakurugenzi wa Kampuni ya Rifaro Africa Limited, Jones Moshi (42) na James Gathonjia (35), wamehukumiwa kulipa faini ya zaidi ya Sh. Milioni 200 baada ya kukiri mashtaka ya kuendesha biashara haramu ya upatu na kutakatisha zaidi ya Sh. Bilioni Moja.

Hukumu hiyo imesomwa leo mchana January 10.2019 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya washtakiwa hao kukiri kutenda makosa wao wenyewe .Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amesema, mahakama imewatia washtakiwa hao hatiani baada us wao wenyewe kukiri Majira yap.

"Mahakama imewatia hatiani sababu nyie wenyewe mmekili kutenda makosa", amesema hakimu Mashauri.Akiwasomea adhabu washtakiwa amesema, Katika kosa la kuendesha biashara haramu ya upatu washtakiwa kila mmoja anahukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni mbili name kama wakishindwa wataenda jela miaka miwili kila mmoja. Aidha katika shtaka La kutakatisha Fedha zaidi ya Sh. Bilioni moja kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni mmoja na Kama akishindwa ataenda jela miaka mitano.

Washtakiwa hao ambao wamekaa rumande Kwa takribani mwaka mmoja, Kwa Kuwa shtaka La kutakatisha fedha lililokuwa linawakabili halina dhamana, wameachiwa huru baada ya kufanikiwa kulipa faini hiyo na kunusurika kwenda jela.

Kabla ya kusomewa hukumu hiyo, hakimu Mashauri aliuuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ambapo wakili wa serikali Mkuu, Shadrack Kimaro aliiomba mahakama kutoa adhabu inayostahili kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa wengine wanaoweza kufikiri kutenda makosa kama haha.

Mapema baada ya washtakiwa kukiri kosa walisomewa maelezo ya awali ambapo wanadaiwa kuisajili kampuni hiyo ya Rifaro name kupewa leseni ya kampuni ya kuuza simu vocha na vifaa vya simu na kwamba waliingia mkataba na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.

Imedaiwa, hata hivyo washtakiwa hao walienda kinyume na leseni yao ya biashara na kuanza kuhamaisha watu kujiunga na kampuni hiyo kupitia warsha mbalimbali za vipeperushi kwa kiingilio cha Sh. 76500 ambayo baadae kilipanda na kufikia Sh. 128,000 Huku wanaofanikisha wakipewa muda wa maongezi wa Shule. 5000 name ili mtu apate Faida kubwa alitakiwa kushawishi watu wengi zaidi kujiunga na kampuni hiyo.

Akisoma Maelezo Hayo, Kimaro amedai, fedha zilizopatikana Sh. 1,022, 560, 854 ziliingizwa katika akaunti namba 3301106013 iliyopo Kenya Commercial Bank (T)Ltd (KCB) tawi la Mlimani City yenye jina la Rifaro Africa Limited ambayo washtakiwa ndio walikuwa Watia saini.

Katika kesi ilidaiwa, kati ya Julai 14, 2014 na Julai 31, 2016 ndani ya Jiji la Dar es Salaam na maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliendesha biashara ya upatu kwa kukusanya fedha kutoka kwa mwananchi kwa ahadi kuwa fedha hizo zitazaa.

Pia wanadaiwa kujihusisha na miamala ya fedha moja kwa moja ya Sh. 1,022, 560, 854 kupitia akaunti namba 3301106013 iliyopo Kenya Commercial Bank (T)Ltd (KCB) yenye jina la Rifaro Africa Limited, wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuendesha biashara ya upatu.

Mashine mpya ya Utrasound kuwanufaisha watoto wachanga Muhimbili

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wa pili kutoka kushoto, Bi. Veronica Hellar, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Prof. Lawrence Museru akimshukuru muwakilishi kutoka The German Society for Tropical Paediatrics (GTP), Dkt. Antke Zuechner (wa pili kutoka kulia) kwa kutoa msaada wa mashine ya Utrasound ambayo itatumika katika wodi ya watoto wachanga kwa ajili ya kuwafanyia vipimo vya moyo, kichwa na tumbo.
Dkt. Zuechner akiwapatia maelezo watalaam wa Muhimbili namna ya kutumia mashine hiyo ambayo imetolewa kwa ajili ya wodi ya watoto wachanga.
Dtk. Zuechner akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Muhimbili mara baada ya kukabidhi mashine hiyo.



Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepatiwa msaada wa mashine ya kisasa ya Utrasound ambayo itatumika katika wodi ya watoto wachanga kwa ajili ya kuwafanyia vipimo vya moyo, kichwa na tumbo. 

Mashine hiyo yenye teknolojia ya juu na uwezo mkubwa wa kuchunguza magonjwa hayo ina thamani ya dola za kimarekani 17,000 imetolewa na Taasisi ya Kijerumaini inayoitwa The German Society for Tropical Paediatrics (GTP). 

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru, Mkuu wa Kitendo cha Sheria katika hospitali hiyo Bi. Veronica Hellar amesema mashine hiyo imetolewa maalum kwa ajili ya kuwahudumia watoto wachanga hivyo itatumika kama ilivyokusudiwa. 

“Tunashukuru kwa msaada huu mliotupatia ambao umekuja wakati muafaka hasa ukizingatia lengo la hospitali ni kuendelea kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto,” amesema Bi. Hellar. 

Kwa upande wake muwakilishi kutoka taasisi hiyo Dkt. Antke Zuechner amesema msaada huo una lenga kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Muhimbili katika kuhudumia watoto wachanga. 

Watalaam wa MNH watapatiwa mafunzo maalum ili kuweza kutumia mashine hiyo ambayo ni ya kisasa zaidi.

LUNDO LA NGUO ZINAZOFANANA NA SARE ZA KIJESHI ZAKAMATWA MAKAMBI YA WAKIMBIZI KIGOMA

$
0
0

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma.

KAMATI ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kibondo wamekamata nguo zinazofanana na za sare za kijeshi katika makambi ya wakimbizi.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake pamoja na kamati ya ulinzi ya usalama ya Mkoa, Kaimu Mkuu wa  Mkoa wa Kigoma Samson Hanga alisema kuwa nguo hizo zilikamatwa tarehe 31 mwezi wa 12 mwaka jana majira ya kati  saa tano asubuhi hadi sita mchana kwenye kwenye makambi ya wakimbizi.

Hanga alisema kuwa jumla ya nguo zinazofanana na sare za kijeshi 1947 zilikamatwa katika kambi ya wakimbizi ya Mtendeli na Nduta zilizopo Mkoani Kigoma.

"Kambi ya wakimbizi ya nduta zilikamatwa nguo 1325 na kambi ya wakimbizi ya mtendeli pia zilikamatwa nguo 1325"alisema

Alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili  kuwabaini waliongiza sare hizo na lengo lao.



 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Samson Hanga akiongea na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa lundo la nguo zinazofanana na sare za kijeshi katika makambi ya wakimbizi Wilayani Kibondo

52% YA WATANZANIA WAMEPIMA VVU-SERIKALI

$
0
0

Na WAMJW-DOM

SERIKALI imesema kuwa Watanzania wapatao 2,405,296 hadi kufikia tarehe Oktoba 2018 walipima VVU kupitia Kampeni ya ‘Furaha Yangu’ ambao ni sawa na asilimia 52 ya lengo la kuwapima watanzania wapatao 4,638,639 hadi Desemba 2018.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika kikao cha kamati ya bunge ya huduma za jamii kilichofanyika leo jijini Dodoma.

“Hadi kufikia tarehe 31 Oktoba 2018, jumla ya watanzania 2,405,296 walikuwa wamepima VVU kupitia Kampeni ya ‘Furaha Yangu’ ambao ni sawa na asilimia 52 ya lengo la kuwapima watanzania wapatao 4,638,639 hadi Desemba 2018” Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa Miongoni mwa wote waliopima, wanaume walikuwa ni asilimia 44 huku wanawake wakiwa ni asilimia 56. Kati yao, watu 70,436 (2.9%) walikutwa na maambukizi ya VVU, ambapo wanaume 27,984 (2.6%) na wanawake ni 42,452 (3.2%).

Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Wizara kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya UKIMWI namba 28 ya mwaka 2008 ili kupendekeza marekebisho yatayoruhusu upimaji Binafsi wa VVU (HIV Self-testing).

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kupunguza umri ya kupima VVU kwa ridhaa ya mzazi au mlezi kutoka miaka 18 hadi 15, hii ni kutokana na kasi ya maambukizi kuongezeka katika umri huo.

Pia, aliendelea kusema kuwa Wizara imeendelea kutoa huduma za Tohara ya Kitabibu kwa Wanaume kwa lengo la kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume katika mikoa ya kipaumbele ambayo haina utamaduni wa kutahiri na ina kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU. 

“Hadi kufikia Septemba, 2018 Mikoa kumi na saba (17) inatoa huduma za Tohara ambayo ni Iringa, Njombe, Tabora, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Kigoma, Mara na Morogoro” Alisema Dkt. Ndugulile

Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inaendelea kutoa Huduma ya tohara kwa wanaume bila malipo katika vituo vya huduma za afya na kupitia huduma mkoba ngazi ya jamii ambapo hadi kufikia Septemba 2018, jumla ya watu 3,702,387 wamefanyiwa tohara nchini ambao ni wanaume, vijana na watoto wa kiume.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile alisema kuwa Hadi kufikia mwisho wa Desemba 2018, Wizara iliweza kuwaandikisha katika huduma za tiba na matunzo watu wanaoishi na VVU wapatao 1, 087,382. Watu 68,927 waliandikishwa katika kipindi cha robo ya mwaka cha Juai hadi Septemba 2018 ambapo kati yao, 1,068,282 wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU, ambapo watoto walikuwa ni 58,908.

Idadi ya vituo vinavyotoa huduma na matunzo vimeongezeka hadi kufikia 6,206 Desemba 2018. Sawa na asilimia 72.7 ya vituo vyote vya huduma za afya nchini. Miongoni mwa vituo hivyo, vituo kamili vinavyotoa huduma za tiba na matunzo ni 2,103 wakati vituo vinavyotoa huduma ya afya mama na mtoto (RCH) ni 4,103. 
Naibu Waziri wa Afya, Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Wabunge na viongozi wa Wizara wakati wa kikao cha Bunge cha huduma za jamii, jijini Dodoma.
Wabunge na Viongozi wa wizara na baadhi ya taasisi zake wakiwa katika Kikao cha kamati ya Bunge ya huduma za jamii kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (Wapili kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya Mpango wa taifa wa kudhibiti Ukimwi ulofanywa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile katika kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jijini Dodoma.
Wabunge na Viongozi wa wizara na baadhi ya taasisi zake wakiwa katika Kikao cha kamati ya Bunge ya huduma za jamii kilichofanyika leo jijini Dodoma.

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WANYUMBA YA MAKAZI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR

$
0
0








Picha za michoro ya nyumba ya Makamu wa Pili wa Rais ambayo inajengwa Pagali Shehia ya Mkoroshini, Chake Chake Pemba ambapo jiwe la msingi wa ujenzi wa makazi hayo limewekwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa shamra shamra za kuelekea kwenye kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi Tukufu Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi kuashiria zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar limekamilika, mwingine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud, makazi hayo yanajengwa katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Msanifu wa Majengo kutoka Ofisi ya Wakala wa Majengo Bi. Hawa Natepe mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba.
Wachezaji ngoma za asili wakionyesha umaridadi kwa kucheza ngoma ya Kilumbizi yenye asili ya Pujini wilaya ya Chake Chake Pemba wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya Makamu wa Pili wa Rais katika eneo la Pagali, Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutumia Vikosi vyake katika ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Makamu wa Rais ametoa pongezi zake leo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar katika eneo la Pagali Shehia ya Mkoroshoni Chake Chake Pemba.

Hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ni sehemu ya shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi Takatifu ambayo kilele chake itakuwa Jumamosi tarehe 12 Januari, 2019.

“Sote tutakumbuka kuwa wakati wa kupigania uhuru wetu Chama cha Afro Shirazi Party (ASP) kiliwaahidi wananchi wake kuwajengea makaazi bora yenye heshima ya utu. Ahadi za ASP zimerithiwa na Chama cha Mapinduzi na ndio maana leo hii tupo hapa kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la makazi bora ya mwananchi mwenzenu, kiongozi wetu, Makamu wa Pili wa Rais”. Alisema Makamu wa Rais.

Ujenzi huo wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.6 za kitanzania. 

Kwa Upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed amesema Serikali imeweka umuhimu katika kujenga makazi ya watumishi wake pamoja na Ofisi.

WAZIRI HASUNGA ASHUHUDIA HAFLA YA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UBANGUAJI KOROSHO

$
0
0

Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania Dkt Hussein Mansoor (Kushoto) akisalimiana na Muwakilishi wa kiwanda cha ubanguaji korosho cha Hawte Investiment Ltd Ndg Jamal G. Kamtwanje mara baada ya kusaini mktaba wa ubanguaji korosho, Leo Tarehe 10 Januari 2019 kwenye ukumbi wa Bodi ya Korosho Mkoani Mtwara. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akishuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya ubanguaji Korosho kati ya Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko Tanzania na wenye viwanda vya ndani, Leo Tarehe 10 Januari 2019, kwenye ukumbi wa Bodi ya Korosho Mkoani Mtwara.

Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania Dkt Hussein Mansoor (Wa pili kulia) pamoja na Muwakilishi wa kiwanda cha ubanguaji korosho cha Hawte Investiment Ltd Ndg Jamal G. Kamtwanje wakisaini mikataba ya ubanguaji wa Korosho, Leo Tarehe 10 Januari 2019 kwenye ukumbi wa Bodi ya Korosho Mkoani Mtwara. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Ndg Aristides Mbwasi (Wa kwanza kushoto), Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo (Wa kwanza kulia).






Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo Tarehe 10 Januari 2019 ameshuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya ubanguaji korosho kati ya Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania na wenye viwanda vya ndani.

Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania Dkt Hussein Mansoor ndiye ametia saini kwa niaba ya serikali na Kampuni nne zimesaini mikataba ya awali kuanza kazi hiyo ambazo ni kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd, Micronix Mtwara, Korosho Afrika, na Micronix-Newala.

Kampuni hizo zimeingia mikataba ya Jumla ya Tani 7500 ambapo kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd yenye uwezo wa kubangua Tani 2000 kwa mwaka imesaini mkataba wa Tani 1500.

Kampuni ya Micronix ya mjini Mtwara yenye uwezo wa kubangua Tani 2400 kwa mwaka imeingia mkataba wa Tani 1200. Kampuni ya Korosho Afrika ya Mjini Tunduru Mkaoni Ruvuma yenye uwezo wa kubangua Tani 5000 kwa mwaka imeingia mkataba wa kubangua Tani 2400 ilihali Kampuni ya Micronix ya Wilayani Newala yenye uwezo wa kubangu Tani 5000 kwa mwaka imeingia mkataba wa kubangua Tani 2400.

Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa serikali imepitia vifungu vyote vya kisheria kabla ya kuanza kuingia makubaliano na kampuni hizo kwa ajili ya ubanguaji wa Korosho.


Alisema kuwa zoezi la ubanguaji tayari lilikuwa limeanza kupitia Shirika la Kushughulikia viwanda vidogo vidogo (SIDO) ambalo tayari limeajiri wafanyakazi 160.Alisema kuwa Shirika la Kushughulikia viwanda vidogo vidogo (SIDO) pamoja na majukumu mengine lakini lilikuwa na kazi mbili ambazo ni kuhakikisha wanatengeneza vipuli na mashine mbalimbali ambazo zimeharibika. Vileviele kuhamasisha wabanguaji wadogo wadogo na kuwasajili.


“Baada ya kuwasajili mtatakiwa kuingia nao mikataba kwa kiasi cha korosho wanachokihitaji kwa ajili ya ubanguaji” Alikaririwa Mhe Hasunga

Mhe Hasunga alisema kuwa serikali ina matumaini makubwa kuwa mikataba ya ubanguaji iliyosainiwa itazingatiwa kwa kufuata taratibu na masharti yote kwa mujibu wa sheria.Alisisitiza kuwa serikali inaingia mikataba na viwanda ambavyo vimekuwa vikibangua kwa muda mrefu hivyo haina mashaka na ubora wa ubanguaji.

Aidha, Alisema kuwa viwanda hivyo vitakuwa na uhakika wa kufanya kazi usiku na mchana kutokana na malighafi nyingi iliyopo tofauti na miaka iliyopita ambapo malighafi ilikuwa haipatikani kutokana na korosho kubanguliwa nje ya nchi.

Mhe Hasunga amesisitiza kuwa serikali imeamua kubangua korosho zote nchini ili kuongeza wigo wa ajira kwa wananchi sambamba na kuongeza thamani ya korosho inayozalishwa nchini ili iweze kuuzwa kwa jina la Tanzania. Ambapo Wizara ya Kilimo itaweza kuchangia kwa ufasaha katika uchumi wa nchi.

WAZIRI UMMY ACHANGIA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA SEKONDARI TANO JIJINI TANGA

$
0
0
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji sehemu ya matofali aliyotoa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili wanafunzi wapata fursa ya kusoma
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akilakiwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Pongwe Jijini Tanga wakati alipokwenda kuwakabidhi matofali na mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akikagua madarasa kwenye ambayo hayajakwisha kwenye shule ya Sekondari Pongwe kabla ya kuwakabidhi mifuko ya saruji na matofali  kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na kushoto ni Diwani wa Kata ya Pongwe(CCM) Mbaraka Sadi
Diwani wa Kata ya Pongwe(CCM) Mbaraka Sadi akizungumza kulia ni MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi mifuko ya saruji Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasaa kwenye kata yake
sehemu ya mifuko ya saruji ilioyotolewa na Waziri Ummy
 Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Pongwe wakifuatilia hotuba ya MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya Sekondari Pongwe
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katikati ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mikanjuni mara baada ya kukabidhi msaada wa matofali na mifuko ya saruji
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio kwenye hafla hiyo

 


Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Tanga na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo amekabidhi matofali 3,500 zenye thamani ya shilingi milioni 5.6 na mifuko ya Saruji 250 yenye thamani ya shilingi milioni 3 ili kuweza kusaidia kutatua tatizo la uhaba wa madarasa.

Msaada huo aliuta  kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa ya Sekondari zilizopo katika Jiji la Tanga ambazo ni Shule za Sekondari   Pongwe, Maweni, Mikanjuni, Horten na Kiomoni ambapo kila shule imepatiwa Matofali 700 na saruji mifuko 50.

Akizungumza ktk makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Mikanjuni, Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM)alieleza kufurahishwa na jitihada za Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli za kuboresha Elimu nchini na katika Jiji la Tanga

Alisema juhudi hizo zimesaidia  kuwezesha uwepo wa idadi kubwa ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na Elimu  ya Sekondari katika Jiji la Tanga. Hivyo yeye kama mbunge ameona anao wajibu wa kuchangia ujenzi wa madarasa ili kuwezesha watoto wote 6,024 wa Jijini Tanga waliofaulu Elimu ya Msingi kuendelea na Elimu ya Sekondari.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga  Tobias Mwilapwa alisema katika mwaka huu 2019 jumla ya wanafunzi 6,024 wamefaulu kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza katika Jiji la Tanga kutoka wanafunzi 5,332 mwaka 2018.
Hali hii imesababisha mahitaji zaidi ya Vyumba vya madarasa 71 ili kumudu kuchukua ongezeko la wanafunzi 1,324 waliofaulu kwenda Sekondari katika Jiji la Tanga.

Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Tanga Ndugu Kidima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Bwana Daudi Mayeji, Waheshimiwa Madiwani wa Kata husika, Watendaji wa Idara ya Elimu na Bodi za Shule husika.

KIPINIDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 11,2019

NIMEIKUMBUKA ZAMANI ILE YA MICHEZO YA KOMBOLELA...SIO SASA YA SULTANA

$
0
0
 
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMA binadamu wa kawaida ninayeishi kwenye dunia hii ambayo muumba wa mbingu na ardhi ameitengeneza kwa umaridadi mkubwa huwa inafika mahali nakumbuka zamani.

Zamani yangu mimi Said Mwishehe.Zamani ambayo ni tofauti na zama hii ya sasa.Huwa namshukuru Molla kwa kunipa nafasi ya kuishi ile zamani yangu na sasa.Hakika huwa naangalia watoto na vijana wa sasa na aina ya maisha yao na kisha narudisha kumbukumbu zamani yangu.Zamani ambayo mawasiliano yetu yalitawaliwa na barua ambazo ili ifike kwa mhusika unampa dereva au kondakta wa basi ili ifike unakota iende.

Naizungumzia zamani ambayo barua unaweza kuituma kwa njia ya posta na kisha inamfikia muhisika bila tatizo.Zamani ambayo nilikuwa nasubiri niitwe mbele ya wanafunzi wengine shuleni kwa ajili ya kupewa barua.Siku ambayo nitapewa barua mbele ya wanafunzi najiona bonge la mtu.Yaani mtu ni mimi tu na wengine ni viumbe tu wa duniani.

Naikumbuka zamani ambayo hakukuwa na filamu za akina Sulatani chini ya uhusika wa Mtukufu Suleiman.Zamani ambayo naiuzungumzia ni ile iliyotaliwa na michezo ya kombolela.Zamani ambayo watoto walifurahia maisha yao halisi ya Mtanzania.Naizungumzia zamani ambayo watoto walijifunza maisha ya familia kupitia michezo ya baba na mama .Ukweli naikumbuka zamani ambayo watoto walifundishwa namna ya kuishi maisha mema.Zamani ambayo mtoto alikuwa wa jamii na akikosea anapewa adhabu na mzazi yoyote.

Naizungumzia zamani ambayo watoto tulishindana kutengeneza watoto wa udongo.Zamani ambayo tulishindana kutengeneza magari kwa kutumia maboksi, mabati au waya za umeme.Zamani ambayo hatukuwa na ujeri kwani tulikuwa tunatumwa na mtu yoyote ambaye amekuzidi umri.

Sizungumziii maisha ya watoto wa sasa ambao wengi wao wamekosa malezi halisi ya baba na mama.Watoto ambao wanalelewa na 'House Girl' na 'House Boy' .Siizungumzii sasa ambayo watoto wanapelekwa kuoga kwenye bwawa la kuogelea a.k.a Swimming Pool.Jamani naikumbuka zamani ambayo watoto tulienda kuoga mtoni.Zamani ambayo tunashinda kucheza kidali poo ndani ya maji.

Naizungumzia zamani ambayo shuleni tulikwenda kwa miguu .Zamani ambayo hakuna aliyefikiria kupanda School Bus.Zamani ambayo watoto walivalisha viatu vya DH. Naikumbuka zamani ya viatu vya Laizoni.Zamani ambayo watoto walivaa nguo za ndani za kiume za VIP.Usiombee ikatike kwani ilikuwa inapanda hadi kifuani.

Naizungumzia zamani ambayo siku nyumbani kukipwa wali ...unaoga saa 12 jioni kusubiri ubwabwa.Naikumbuka zamani ambayo haikuwa na papara ya maisha.Kimepatikana sawa kikikosena Ishallah.Naizungumzia zamani ambayo mtoto alikuwa wa mwisho kunawa wakati wa chakula.Zamani
ambayo mtoto alilazimika kupewa nyama ndio ale.Kinyume na hapo ataishia kuziona kwenye bakuli.

Naikumbuka zamani ambayo chakula kiliwekwa kwenye sahani moja na watoto wakala kwa pamoja.Zamani ambayo baba aliweza kujua tabia ya mtoto.Zamani ambayo mama alijua tabia ya mtoto wa kike.Zamani ambayo mtoto wa miaka mitano au sita aliweza kufua nguo zake.Siizungumzii sasa ambayo mtoto wa miaka 13 nguo zake anafuliwa na house girl.

Sasa ambayo mtoto anawekewa chakula kwenye sahani yake.Sasa ambayo mtoto ndio mwenye kutoa maagizo kwa mzazi anataka kula nini, anataka kuvaaa nini.Sitaki kabisa kuizungumzia sasa.Naikumbuka zamani, zamani ambayo kwenye harusi hakukua na kadi za kuingilia getini.Zamani ambayo watu walikaribishana chakula .Zamani ambayo kila mtu alikuwa ndugu wa mwingine.

Mimi Said Mwishehe yaani mimi Said naikumbuka zamani ambayo maisha ya nyumbani yalikuwa yanafuraha na watoto wote ni sawa.Zamani ambayo watoto wote tuliishi maisha ya kufafana.Maisha ambayo nguo mpya zitapatikana wakati wa sikukuu.Zamani ambayo haikuwa na utitiri wa wasanii
wa muziki wa kizazi kipya.

Zamani ambayo haikuwa na Bongo Muvi.Naizungumzia zamani ya akina Yondo Sister.Zamani ya akina Rambo na Bluce Lee.Zamani ambayo Pepe Kale alisikika bila tatizo.Zamani ambayo nyimbo za akina Mbaraka Mwinshehe zilipewa nafasi ya kusikika na redio Tanzania.Naikumbuka zamani ambayo ili uende kuanza darasa la kwanza lazima mkono uzunguke kichwa kwa juu na kushika sikio.

Hivyo wazazi walikuwa na kazi ya kutufanyisha mazoezi ya kushika sikio.Zamai ambayo mtoto alianza darasa la kwanza hata akiwa na umri wa miaka 10,11 au miaka 12 poa tu.Kwani kitu gani bwana wakati kikubwa ni elimu.

Sitaki kuizungumzia sasa kwani ni sasa ambayo ina kera.Sasa ambayo mwanaume anapiga goti anapomvisha pete ya uchumba binti wa kike.Sasa ambayo mwanaume anamwaga chozi hadharani kisa amependa.Naikumbuka zamani ambayo mtoto wa kike alipiga goti kwa mumewe.Alilia kuonesha hisia
za upendo kwa mwenza wake.

Yaani naomba nieleweke tu sitaki kuizungumzia sasa ambayo wazazi walio wengi hawana habari na watoto wao.Sasa ambayo mtoto wa kike anamiliki simu ya shilingi milioni moja na mzazi wala hana nafasi ya kuuliza imetoka wapi.Sasa ambayo mtoto wa kiume anashinda kwenye vijiwe vya kuvuta bangi na dwa za kulevya.

Sasa ambayo baba na mtoto wanashindana kwenye kubeti na mkeka ukichanika wote wanabaki wakiwaza.Eti kamkosa muhindi.Ujue sitaki kuizngumzia sasa ambayo utu umetoweka duniani.Sasa ambayo ndugu wanakutana siku ya msiba tu.Sasa ambayo hakuna mwenye habari na mwingine.Wenyewe wanasema kila mtu na maisha yake.Naikumbuka zamani ambayo ili uende kucheza baba au mama anakwambia imba tebo ya kwanza hadi ya 12.Zamani ambayo bibi na babu walitufundisha hadithi za kale.Hadithi ambazo zilitufundisha mambo mengi ya kwenye maisha.Naikumbuka zamani ambayo ukiwa darasa la tatu unafundishwa kupiga pasi nguo, unafundishwa namna ya kufagia.Unafundishwa kuheshimu
jamii inayokuzunguka.

Zamani ambayo haikuwa na wimbi la matapeli.Zamani ambayo watu walikuwa wakweli .Zamani ambayo tulishindana kuonesha vipaji vyetu shuleni.Zamani ambayo walipatikana mabingwa wa hesabu baada ya shule kushindana kwa ngazi ya mbalimbali hadi ya kitaifa.Zamani ambayo watoto walionesha umahiri wao katika fani mbalimbali.Sitaki kuizungumzia sasa ambayo watu wanashindana kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuonesha mambo ya hovyo.Unabisha nini?Kumbuka ya Amber Ruty na mpenzi wake.Acha niikumbuke zamani.Sitaki kuingia kwenye malumbano,kisa nazungumzia ya sasa.
Inatosha bwana...yaani imetokea tu nimeikumbuka zamani.Sijui nini

kimetokea ila ndio hivyo tena zamani itabaki kuwa zamani.Zamani ambayo barua ilianza kwa kusema "Wewe uliye mbali na upeo wa macho yangu.Mimi ni mzima wa afya , hofu ni kwako.Upatapo barua hii utambue ndugu yako nimekukumbuka na nakupenda sana.Baba na mama wanakusalimia."Naikumbuka zamani ambayo hata hii namba ya simu 0713833822 sikuwa nayo.

NAIBU WAZIRI WA MAJI AWESO AMPA KONGOLE DKT. ANGELINE MABULA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akipanda katika Tanki la maji kujionea ujenzi wa tanko hilo wakati Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso alipokagua miradi ya maji katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso Akielekea kukagua tanki la Maji katika mradi wa Igogwe katika Manispaa ya Ilemela wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. Wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Wazari wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso (wa tatu kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mijini mkoani Mwanza Injinia Anthony Sanga wakati wa wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso (wa pili kulia ) akimsikiliza Mhandisi wa Maji katika Manispaa ya Ilemela Anna Mawala wa wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula.

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso (wa pili kushoto) akiangalia ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya Bugogwa Manispaa ya Ilemela wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. Wa tatu kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza baada ya Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kukagua miradi ya maji katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wanaojenga tanki la maji katika mradi wa maji vijijini eneo la Igogwe Manispaa ya Ilemela Mwanza wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA)




Na Munir Shemweta, ILEMELA

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametembelea miradi ya Maji katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa jitihada za kuwapatia wananchi wa jimbo hilo huduma ya maji safi na salama.

Katika ziara hiyo Aweso alijionea changamoto mbalimbali zinazoikabili miradi ya maji katika manispaa hiyo pamoja na kero ya maji wanayoipata wananchi wa Kata ya Bugogwa yenye mitaa kumi na tano na wakazi wapatao 32,000 ambao kwa muda mrefu hawana huduma ya maji licha ya juhudi za mbunge wa jimbo la Ilemela Dk Mabula kuwachimbia visima.

Mbunge wa Jimbo hilo Dk Mabula ameiomba Wizara ya Maji kuwapatia wananchi wa kata ya Bugogwa huduma ya maji katika mradi wa maji vijijini kutokana na chanzo cha maji cha mradi huo kupitia eneo lao.

Kwa Mujibu wa Dk Mabula, pamoja na chanzo cha mradi wa maji vijijini kuwa katika kata ya Bugogwa jimboni humo lakini wananchi wake hawajajumuishwa kwenye mradi jambo linaloleta sintofahamu kwa wakazi hao ambao sasa wanaona kutengwa na serikali jambo alilolieleza kuwa linaweza hata kutishia usalama wa mradi.

Alisema, njia pekee ya kuwafanya wananchi wa kata ya Bugogwa kufurahia matunda ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ni kuwapatia huduma ya maji safi na salama kitendo kinachotafsiriwa kama kumtua ndoo mama kichwani.

Kufuatia ombi hilo, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso alimuagiza Mhandisi wa Maji katika Manispaa ya Ilemela Anna Mawala pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Mwanza (MWAUWASA) Injinia Anthony Sanga kushirikiana kuandaa mpango mdogo utakaowezesha wakazi wa kata nao kufaidika na mradi na mapendekezo hayo yawasilishwe wizarani mapema ili kufanyiwa kazi.

Aweso alisema kuwa, Wizara ya Maji haiwezi kuwa kikwazo kwa wananchi kupata huduma ya maji kwa kuwa huduma hiyo haina mbadala hivyo Serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha wananchi hao wanapata huduma ya maji safi na salama ili kuondokana na kero ya muda mrefu.

Mtendaji wa Kata ya Bugogwa Manispaa ya Ilemelea mkoa wa Mwanza Rashid Sukwa alisema kata yake imekuwa na tatizo la maji kwa muda mrefu pamoja na juhudi za mbunge wa jimbo hilo Dk Mabula kusaidia kuchimba visima lakini baadhi ya wananchi wanatumia visima vya asili.

Ameitaja baadhi ya mitaa yenye changamoto kubwa ya maji katika kata hiyo kuwa ni pamoja na Lugezi, Igombe A na B, Bugogwa, Kigote, Bugigwa, Kabaganja, Kasamwa, Kayenza Ndogo, Kisonde, Kilabela, Isanzo, Igogwe pamoja na Nkoronto.

Mmoja wa wakazi wa Bugogwa Janet Lusia alimshukuru Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa kuona umuhimu wa wananchi wa kata hiyo nao kufikiriwa kupata maji katika mradi huo kwa kuwa wametaabika kwa muda mrefu pamoja na jitihada za mbunge wao kuwachimbia visima.

RC GAMBO:PELEKENI WANAFUNZI SHULE HATA KAMA HAWANA SARE

$
0
0

Baadhi ya Wajumbe wa halmashauri ya Kijiji cha Lositete wakiingia kwenye gari la polisi kuelekea kituo cha polisi Karatu kuandika maelezo ya kwanini wanashawishi wananchi kugomea shughuli za maendeleo. Agizo hili limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo


Na.Vero Ignatus, Karatu


Wito umetolewa kwa wazazi pamoja na walezi wilayani Karatu kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule hata kama hawana sare za shule.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katika kijiji cha Lositete Kata ya Mbulumbulu Wilayani Karatu wakati alipokwenda kukagua hali halisi ya madarasa pamoja na wanafunzi wangapi wameshaanza masomo ya kuanza kidato cha kwanza.

Gambo ameuagiza uongozi wa serikali ya kijiji cha Lositete kuchukuliwa maelezo polisi ni kwanini hawachangii maendeleo ya elimu badala yake kuingiza siasa na kusababisha saruji kuganda pamoja na mifuko 71 ya saruji, mbao kuoza kwa kipindi cha miaka miwili.

Yote hayo yamekuja mara baada yakushtushwa na taarifa aliyoitoa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Upper Kitete, Josephat Mau iliyodai kuwa wanafunzi tisa kati ya 171 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shuleni hapo hawajaripoti shuleni kutokana na kukosekana kwa sare za shule.

Mwalimu Mau alisema wanafunzi hao 9 hawajaripoti shuleni hapo kutokana na kukosekana na sare za shule huku walioripoti wakiwa ni tisa tu kwasababu ya wazazi au walezi wao kutouza maharage kutokana na kukosekana kwa soko.

Baada ya Mwalimu huyo kutoa taarifa hiyo ndipo Rc Gambo aliagiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza kuripoti shuleni na nguo za nyumbani hata kama hawana sare ili waendelee na masomo wakati wazazi wao wakisubiri kuwanunnulia mahitaji ya shule.

"Rais ameagiza elimu bure hivyo wazazi au walezi watoeni watoto wenu majumbani ili waende shule bila ya kuwa na sare za shule huku mkiendelea kutafuta sare lakini pia nasisitiza nyie wananchi acheni kuingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo na wewe nyie viongozi wa vijiji pamoja na kata muwe na tabia ya kusoma mapato na matumizi ya vijiji "Alisema Gambo

Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lositete na Upper Kitete Rc Gambo aliagiza mwenyekiti wa kijiji cha Upper Kitete, William Safari pamoja na William Marmo kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi ya kijiji ambayo wananchi wanadai hawajasomewa tangu mwaka 2017 hadi mwaka 2018.

Awali baadhi ya wananchi hao, Pascal Paulo na Kastuli Dizderi walidai kuwa wameshindwa kujenga madarasa pamoja na maabara kwasababu walichanga fedha ambazo zililiwa na aliyekuwa Mkuu wa shule hiyo wa zamani Andrew Sulle ambaye alichukua sh, milioni 8 walizochanga kwaajili ya ujenzi wa madarasa na maabara kuliwa na aliyekuwa mwalimu mkuu wa zamani.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo alisema wananchi zaidi wa vijiji vya Lositete na Upper Kitete wanapenda kuingiza masuala ya siasa katika maendeleo na amejitahidi kutatua changamoto zao ikiwemo kuhakikisha Mwalimu Mkuu huyo wa zamani Sulle anachukuliwa hatua za kinidhamu na ameshahukumiwa kifungo.

Alisema wanafunzi 5,313 walifanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana huku wanafunzi 4,000 sawa na asilimia 75.3 walifaulu ambapo wanafunzi 3,446 wakiwa wamepangwa kwenye shule za kata zilizokuwa na madarasa 83 na wanafunzi 539 walikosa nafasi.

Alisisitiza kuwa wanafunzi hao 539 waliokosa nafasi hivi sasa wameshaanza masomo katika shule mbalimbali za wilaya hiyo kutokana na kubainika kunashule wanafunzi hawkaupangwa kabisa huku wakiandika barua kw wadau nakuhamasisha wanananchi kujenga madarasa pamoja na kikarabati viti na meza ili wanafunzi waweze kusoma.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWASILI KISIWANI PEMBA KUHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman Abdallah, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume Kisiwani Pemba,kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika kesho Januari 12/2019, katika Uwanja wa Ngombani Pemba.(Pichja na Ikulu)
IMG_8767
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman Abdallah, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa  Karume Chakechake  Kisiwani Pemba, akielekea katika chumba cha VIP.(Picha na Ikulu)
IMG_8769
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Chama waliopfika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Karume Chakechake Kisiwani Pemba, baada ya kuwasili kisiwani humo kuhudhuria Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar,(Picha na Ikulu)
IMG_8770
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Kisiwani Pemba, baafda ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Karume Chakechake Kisiwani Pemba.(Picha na Ikulu) 
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live


Latest Images