Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimezindua Kozi ya wahudumu wa ndege ili kuhakikisha uwekezaji wa ndege nchini unaendana na Rasilimali watu wenye ujuzi.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kozi hiyo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe amesema kuwa kuna mahitaji makubwa katika Sekta ya anga hivyo vyuo viendelee kuzalisha Rasilimali watu ambao wanaweza kutumika ndani na nje ya nchi.

Mhandisi Kamwelwe amesema upatikanaji wa rasilimali watu katika Sekta ya anga ndani changamoto kutokana na kutokuwepo kwa rasilimali hiyo ilisoma katika vyuo vyetu na kuhitajika kwa watu wa nje ya nchi ambao wanalipwa fedha nyingi.

Amesema kuwa uchumi wa viwanda unategemea na usafiri wa anga katika usafirishaji wa bidhaa katika masoko ya nje kwa haraka zaidi.

Kamwelwe amesema kuwa NIT waendelee kubuni zaidi katika kuzalisha Rasilimali watu wa kuweza kuhudumia ndege zetu na kuacha kutegemea rasilimali inayotoka nje ya nchi.

Nae Mkuu wa Chuo cha NIT Profesa Zakaria Mganilwa amesema kuwa wamejipanga katika uzalishaji wa rasilimali watu katika Sekta ya anga ili kuendana na Uwekezaji wa ndege unaofanywa nchini.Amesema wahudumu ndani ya Ndege ni muhimu sana ambao ndio waangalizi wa usalama wa abiria na mali zao.
 Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa kozi ya Uhudumu Ndani ya Ndege.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kozi ya Uhudumu Ndani ya Ndege.
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo cha Usafirishaji (NIT)

MKUU WA WILAYA JOKATE MWEGELO AWEKA WAZI MADINI YALIYOPO KISARAWE YATAKAVYOWANUFAISHA WANANCHI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo ameweka wazi kuwa atapambana kwa juhudi na maarifa kuhakikisha uwepo wa madini katika ardhi ya Kisarawe unaleta tija na neema kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza kuhusu hilo leo DC Jokate amesema chini ya uongozi wake kuanzia mwishoni mwa mwaka 2018 alianza mchakato wa kufanya Geological Survey/Mapping kwakushirikiana na Geological Survey of Tanzania na Ofisi ya Kamishna wa Madini Ukanda wa Mashariki.

Lengo likiwa kutambua aina ya madini na ubora wake na kiasi ambacho kitapatikana ili kuanza kuweka mikakati endelevu na yenye tija ya muda mrefu kwa wilaya na Taifa kwa ujumla.

Amefafanua madini ambayo wilaya ya Kisarawe imejaaliwa kuwanayo kuwa ni; Madini ya udongo jasi, madini aina ya chokaa, malighafi za ujenzi kama vifusi/mchanga, mawe, na kokoto.

Mwegelo amesema Kisarawe haiwezi kuendelea kuwa masikini na kuwa na upungufu wa huduma muhimu za afya na elimu wakati kuna madini katika aridhi ya kisarawe ambayo watu wa Kisarwe wamepewa zawadi na Mungu.

Ameeleza kuwa nia yake ya kushirikiana na vyombo vyote vinavyohusika kuhakikisha kunawekwa utaratibu mzuri utakao hakikisha mapato yote yanayotokana na madini wilayani Kisarawe yanawekewa utaratibu mzuri wa matumizi ikiwa ni pamoja na kuongeza na kuboresha miundombinu ya afya, elimu kama vile kujenga madarasa na kufikia lengo la kuwa na matundu ya vyoo ya kutosha ili kukidhi haja na viwango vinavyohitajika.

Pia DC Mwegelo amesema niwakati wa yeye kusimama imara na viongozi wote waliochini yake na Serikali kwa ujumla kuunganisha nguvu pamoja na kushirikisha wananchi ambao ndiyo wadau muhimu katika kuleta maendeleo.

"Naamini kuwa jambo hili litasaidia sana kutimiza muono mpana na ndoto kubwa ya Rais wa awamu ya tano na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.John Magufuli ya kulifanya Taifa la Tanzania kuwa Taifa lenye uchumi wa kati na kuwa taifa lenye kutegemewa na mataifa mengine.

" Uanzishwaji wa vituo maalumu vya biashara ya madini kama ilivyoelekezwa na kuagizwa na Rais Dk. Magufuli ni njia bora ya kuhakikisha madini yanainufaisha jamii kwa kuondoa umasikini na kuwa na jamii yenye kupata huduma bora katika nyanja zote za maisha,"amesema.

Amesisitiza ni kuwa, niwakati muafaka wa wananchi wa Kisarawe kutambua thamani ya madini yaliyopo katika kuongeza fursa za uchumi na maendeleo kwa kushirikiana na viongozi waadilifu, waanaojali uzalendo na wenye kutanguliza maslahi ya Taifa kwanza.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema niwakati sasa wa jamii yote ya Kisarawe kutambua kuwa fursa ya kuwepo madini ya aina tofauti wilayani humo ni mkombozi muhimu katika nyakati hizi ambazo Taifa la Tanzania linakua kiuchumi kwa kasi na kutumia rasilimali zake za ndani katika kukuza uchumi.

Mambo ya kutarajia katika sekta ya biashara za mtandaoni 2019

$
0
0
Kwa mujibu wa mtandao wa Statista, mpaka kufikia mwaka 2021 mauzo yatakayotokana na biashara za mtandaoni yatafikia Dola za Kimarekani trilioni 4.88. Kiasi hiko kitakuwa ni maradufu ya sasa ambapo mauzo yaliyopatikana kwa mwaka 2018 ni Dola za Kimarekani trilioni 2.84. 

Hii inaasharia kukua kwa sekta hii pamoja na kutengeneza faida kubwa kwa wauzaji wa bidhaa mbalimbali kwa njia ya mtandao duniani. 

Kasi ya ukuaji wa biashara za mtandaoni inaenda sanjari na maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayopelekea tabia za wateja kubadilika kwa kasi. Wateja wa sasa wamekuwa na tabia tofauti ukilinganisha na awali ambapo hakukuwepo na matumizi ya mifumo ya kidigitali.

Mifumo ya kidigitali imebadili kwa kiasi kikubwa tabia za wateja ambapo watoa huduma hawana budi kubadilika ili kuendana nao. Kwa mfano, sasa hivi mtu anaweza kufanya shughuli tofauti akiwa eneo moja. Malipo ya huduma mbalimbali kwa kutumia simu ya mkononi kama vile ada, umeme, visimbuzi, maji, faini, benki, leseni na mengineyo yanawezekana bila ya kwenda moja kwa moja kwenye ofisi za watoa huduma. Pia, mtu anaweza kuwa ofisini akiendelea na shughuli zake lakini akafanya huduma za manunuzi, malazi na hata kuagiza chakula pale pale alipo.

Siku za hivi karibuni biashara nyingi zimekuwa zikikumbwa na changamoto ya kupokea idadi ndogo ya wateja wanaotembelea madukani mwao. Sababu kubwa iliyopelekea hili kutokea ni kutokana na kuibuka kwa sekta ya mtandaoni ambayo huwapatia wateja uwezo wa kupata huduma na bidhaa tofauti kwa urahisi na haraka ndani ya muda mfupi. Hivyo basi, imekuwa ni vigumu kwa wafanyabiashara wasiotaka kubadilika kushindana na mahitaji ya sasa ya wateja.

Tunapouanza mwaka mpya wa 2019, Jumia inawashauri wafanyabiashara kuwa hawana budi kutumia fursa zote za kiteknolojia zinazopatikana kwa sasa ili kukuza biashara zao na kupata faida zaidi. Tanzania kwa sasa ina watumiaji wa simu za mkononi zaidi ya milioni 40, kati yao zaidi ya milioni 23 wanatumia huduma ya intaneti. 

Pongezi kubwa kuendelea kuongezeka kwa uwekezaji kwenye sekta za mitandao ya mawasiliano ya simu, makampuni ya uuzaji wa simu pamoja na watoa huduma wa intaneti kwa kuchochea kwa kiasi kikubwa watanzania wengi kuweza kutumia huduma za simu na intaneti.

Kutokana na upatikanaji wa huduma za intaneti hususani kupitia simu za mkononi miongoni mwa watanzania wengi, kumepelekea shughuli nyingi kufanyika mtandaoni. Asilimia kubwa ya wateja hivi sasa wakihitaji bidhaa au huduma yoyote ni rahisi kwa wao kuingia mtandaoni kupitia simu zao za kiganjani kupata taarifa zaidi kabla ya kufanya maamuzi ya kufanya manunuzi.

Hivyo basi, wafanyabiashara hawana budi kuwa na uwepo wa kutosha mtandaoni. Hapa inamaanisha kuwa na tovuti, kufungua akaunti katika kurasa tofauti za mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram, Youtube na hata blogu kama ikiwezekana. 

Uwepo tu mtandaoni hautoshi endapo hakutokuwa na taarifa za kutosha zinazoendana na wakati. Imekuwa ni kasumba kwa wafanyabiashara wengi kuwa na kurasa za mitandao ya kijamii au tovuti lakini taarifa nyingi si sahihi au zimepitwa na wakati. Hivyo, hakikisha kunakuwa na taarifa za kutosha, sahihi na zinazokwenda na wakati ili kujibu maswali yote ya mteja atakayokuwa nayo. 

Kingine ambacho wafanyabiashara wanatakiwa kukizingatia kwa umakini ni kutambua wateja wao wanataka nini. Wateja wengi wa sasa hivi ni werevu na wanakwenda na wakati. Takribani kila mteja anapendelea bidhaa au huduma atakayoiona mtandaoni apalekewe mpaka pale alipo, tena kwa ubora na sifa zilezile kama alivyoziona mtandaoni. Hii itapelekea kujenga imani baina ya mfanyabiashara na mteja kuendelea kununua bidhaa siku zijazo.

Yapo mengi ya kutarajia katika mwaka huu kwa upande wa biashara kwa njia ya mtandaoni, pengine kwa kufanya tathmini ya ndani utakuwa umegundua ni vitu gani zaidi vya kufanya marekebisho. Je, ni kwa upande wa bidhaa? Huduma kwa wateja? Huduma baada ya mauzo? Au pengine namna za malipo wanazopendelea wateja? Ni lazima kuyazingatia yote haya ili kuwa na mwaka wenye mafanikio zaidi.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA SUNIL MITTAL MWENYEKITI WA BHARTI AIRTEL IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel  ( kampuni ya Simu ya Airtel ) mara baada ya kuwasili kwaajili ya mazungumzo , Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel  ( kampuni ya Simu ya Airtel ) Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Mwaluko pamoja na mwakilishi kutoka kampuni ya Bharti Airtel. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel aliyeambatana na ujumbe wake kutoka kampuni ya Simu ya Airtel pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Kabudi, Gavana wa BOT Profesa Luoga, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Mtendaji mkuu wa kituo cha Uwekezaji (TIC ) Geoffrey Mwambe  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL  Mhandisi Omary Nundu. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma taarifa ya majadiliano kutoka kwa mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel ( kampuni ya Simu ya Airtel ) mara baada ya Mazungumzo yao . Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel aliyeambatana na ujumbe wake kutoka kampuni ya Simu ya Airtel pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Kabudi, Gavana wa BOT Profesa Luoga, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Mtendaji mkuu wa kituo cha Uwekezaji (TIC) Geoffrey Mwambe  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL  Mhandisi Omary Nundu, Mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Mwenyekiti wa Bharti Airtel (kampuni ya Simu ya Airtel) Bw. Sunil Mittal akizungumza na Wana habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo  yao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wana habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo  yao na Mwenyekiti wa Bharti Airtel (kampuni ya Simu ya Airtel) Bw. Sunil Mittal, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
PICHA NA IKULU

NEWZ ALERT: BOSI WA ZAMANI TRA NA WENZAKE ,MTUHUMIWA WA KUUIBIA SERIKALI MIL 7 KWA DAKIKA WAACHIWA HURU,WAKAMATWA TENA

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia kesi ya utakatishaji fedha  aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya, na wenzake wawili kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi  hiyo.

Pia Mahakama hiyo imemfutia kesi mfanyabiashara aliyewahi kutajwa na Rais John Magufuli kuiibia serikali Mil.7 kwa dakika, Mohamed Yusufal na wenzake kwa sababu DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kesi hizo zote zimefutwa mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mbando baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Hashim Ngole kueleza kuwa kesi hizo leo zilikuja kwa  kutajwa.

Wakili Ngole ameeleza kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashauri hayo kwa kutumia kifungu cha 91(1) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 marejeo ya mwaka 2002.

Kifuatia taarifa hiyo, Hakimu Mmbando ameziondoa kesi hizo mbili.
Hata hivyo, baada ya kutoa uamuzi huo washtakiwa wote walikamatwa na sasa wako ndani ya ukumbi wa wazi wa mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando wakisomewa mashtaka mapya.

 Kitilya anashtakiwa pamoja na aliyekuwa miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Ofisa wa benk ya Stanbic Sioi Solomon.

Katika kesi ya awali, washtakiwa walikabiliwa na makosa ya utakatishaji fedha, kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani Milion 6 katika akaunti tofauti tofauti  za benki ambapo inadaiwa walitenda makosa hayo kati ya March 2013 na September 2015.

Wagonjwa 11 wafanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua

$
0
0
 Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha valvu katika kambi maalum ya matibabu ya siku 12 inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
 Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha valvu kwenye  kambi maalum ya matibabu ya siku 12 inayoendelea  katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
  Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani wakijadili maendeleo ya  wagonjwa waliolazwa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo. Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika Taasisi hiyo na hali zao zinaendelea vizuri ambapo wengine wamesharuhusiwa kutoka  ICU  na kurudi wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu ikiwa ni pamoja na mazoezi.
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha valvu kwenye  kambi maalum ya matibabu ya siku 12 inayoendelea  katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
Picha na JKCI

KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI YAFANYA KIKAO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda  na Kimataifa, Dkt. Damas Ndumbaro akiwasilisha Taarifa ya Wizara yake kuhusu Utekelezaji wa afua za UKIMWI mahali pa kazi kwa wizara na namna inavyoshirikiana na Mataifa mengine katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI, Mhe. Oscer Mukasa akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masula ya UKIMWI, wakiwa katika kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kamati hiyo ilipokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa kuhusu Utekelezaji wa afua za UKIMWI mahali pa kazi kwa wizara na namna inavyoshirikiana na Mataifa mengine katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masula ya UKIMWI, wakiwa katika kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kamati hiyo ilipokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa kuhusu Utekelezaji wa afua za UKIMWI mahali pa kazi kwa wizara na namna inavyoshirikiana na Mataifa mengine katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya

AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
JUMLA ya watoto wachanga 475 wamefariki dunia baada ya akinamama 41,064 kujifungua mkoani Pwani, mwaka 2018 ,hali ambayo inaonyesha idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi kimkoa bado ipo juu. Aidha kati ya akinamama hao 41,064 waliojifungua akinamama 67 walifariki dunia kutokana na uzazi. 

Hayo yalisemwa na mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, dokta Gunini Kamba wakati mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo aliposaini hati ya makubaliano na wakuu wa wilaya ya kampeni ya kuzuia vifo vya uzazi, kampeni ambayo itafanyika kwa miezi 12 nchini. Alisema, vifo vya watoto wachanga na akinamama wanaojifungua hali hairidhishi hivyo kampeni hiyo itasaidia kupunguza idadi hiyo. 

Kamba alisema, lengo hilo linaweza kufikiwa endapo akinamama watafuata maelekezo ya kiafya wanayopatiwa wakati wa uzazi ili waweze kuvuka salama katika kipindi cha uzazi. "Vifo 67 kwa waliojifungua na watoto wachanga 475 ukilinganisha na malengo ya Kitaifa bado hali sio nzuri sana "alisisitiza Kamba. Pamoja na hayo Kamba aliwataka ,akinamama wajawazito kuhakikisha wanaanza klinik ndani ya miezi 12 ya kwanza ili kujua afya zao. 

Pia waendelee na kufuatilia afya zao kulingana na utaratibu watakaopatiwa hadi wakati wa kujifungua bila kupuuzia. "Na wakijifungua inapaswa kuhakikishwa ndani ya lisaa limoja baada ya kujifungua mtoto anyonye "alifafanua Kamba. Awali mkuu wa mkoa wa Pwani, Ndikilo aliwaasa wakuu wa wilaya kwenda kusimamia malengo hayo ili kufanikisha kampeni hiyo kiwilaya, mkoa na Taifa kijumla. 


FAO Yaahidi Ushirikiano Zaidi na Serikali

$
0
0
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kuiinua sekta ya kilimo nchini. Hayo yamesemwa na Ndugu muwakilishi wa Shirika hilo nchini Ndugu Fred Kafeero alipokutana na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa katika ofisi za FAO jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho Ndugu Kafeero alieleza namna ambavyo shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali katika kutunga sera na kuandaa mikakati yenye lengo la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele katika kilimo. Amesema FAO kwa miaka ya karibuni imefanya kazi kwa ukaribu na Shirika la Takwimu Tanzania (NBS) kwa kulijengea uwezo wa ndani unaoisaidia pia serikali katika ufuatiliaji wa bei ya mazao nchini.

Nae Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa alimueleza muwakilishi huyo mpango wa Serikali ya awamu ya tano wa kuorodhesha wakulima wote nchini ili kuweza kupanga vizuri kuhakikisha kila mkulima anapata huduma muhimu zitakazomsaidia toka hatua za uandaaji shamba mpaka masoko, na kuiomba FAO kama mdau muhimu wa kilimo kuipa Serikali ushirikiano ambapo Ndugu Kafeero aliahidi kulifanyia kazi ombi hilo.

Aidha, Naibu Waziri Bashungwa ameomba IFAD (shirika tanzu la FAO) isaidie Serikali kwa kushirikiana na  Benki ya Kilimo nchini kuwapatia wakulima nchini kupata mikopo ya riba nafuu, kusaidia taasisi za utafiti wa kilimo nchini, kujenga uwezo wa kuzalisha mbegu za mazao ya kimkakati na mchanganyiko, kujenga maghala ya kuhifadhi mazao ili kupunguza hasara wakati wa mavuno shambani (post harvest losses) na kuwajengea uwezo maafisa ugani nchini kufundisha kilimo cha tija kwa wakulima nchini. 

Mwakilishi wa FAO nchini amekubaliana na Naibu Waziri Bashungwa kufanyika kikao mwezi Februari 2019 cha Wizara ya Kilimo, FAO na mashirika mengine ya kimataifa yanayohusika na kilimo nchini kujadili vipaumbele tajwa ili kuijengea uwezo Wizara wa kuweza kuihudumia sekta ya kilimo nchini ili iendelee kukua na kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa kati
 Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akizunguza na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Ndugu Fred Kafeero na msaidizi wa mwakilishi huyo Ndugu Charles Tulahi katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam
 Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimueleza muwakilishi wa FAO nchini mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kuinua kilimo
 Fred Kafeero akimkabidhi Naibu Waziri wa Kilimo baadhi ya machapisho yanayoonyesha mikakati ya FAO 
 Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akiagana na msaidizi wa muwakilishi FAO nchini Ndugu Charles Tulahi mara baada ya kumalizika kwa kikao
 Innocent Bashungwa akimsikiliza kwa makini muwakilishi wa Shirika la FAO wakati akimuelezea shughuli za shirika hilo
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akiagana na msaidizi wa muwakilishi FAO nchini Ndugu Charles Tulahi mara baada ya kumalizika kwa kikao

WAWILI WONGEZWA KESI YA KITILYA, WAACHIWA HURU NA KUKAMATWA TENA. WASOMEWA MASHTAKA MAPYA 58

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea mashtaka mapya 58 yakiwemo ya utakatishaji  fedha na kuisababishia serikali hasara ya dola milioni sita aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake wawili ambao ni, aliyekuwa Miss Tanzania 1999 Shose Sinare na Sioi Solomon baada ya mapema leo asubuhi kuwafutiwa mashtaka nane yaliyokuwa yanawakabili.

Hata hivyo katika mashtaka mapya TAKUKURU imewaongeza watuhumiwa wawili kwenye kesi hiyo ambao ni  Bedason Shallanda  ambaye ni Kamishina wa  uchambuzi wa  madeni kutoka Wizara ya Fedha  na msaidizi wake Alfredy  Misana.

Katika kesi hiyo mpya washtakiwa wanakabiliwa na  na mashtaka matatu ya kughushi, mashtaka mawili ya kutoa nyaraka za uongo, shatka moja la kujipatia pesa takribani dola milioni mia sita kwa njia za udanganyifu shtaka moja la kutoa nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya Katibu Mkuu Wizara ya fedha, shtaka moja la kuongoza uhalifu, mashtaka 49 ya  utakatishaji fedha na shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya dola milioni  sita.

Akisoma mashtaka hayo wakili wa wa Serikali Mkuu Hasan Ngole amedai mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Agustina Mmbando ,kuwa kati ya Machi 15,2013 na Januari 10 2014 ndani ya jiji la Dar es salaam kwa nia ya kudanganya washtakiwa wote walijipatia USD milioni sita kutoka Serikali ya Tanzania wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji wa upatikanaji wa mkopo na zililipwa  kupitia kampuni ya  EGMA Ltd na benki ya Stanbic

Aidha, miongoni mwa kosa la utakatishaji fedha inadaiwa washtakiwa wote walilitenda March 18, 2013 na January 10, 2014 wakiwa jijini Dar es Salaam ambapo walitakatisha USD 6,000,000 kwa kuzitoa fedha hizo kupitia njia ya benki kwa jina la Enterprises Growth Market Advisors (EGMA) katika benki ya Stanbic Tanzania.

Pia katika kosa la kusababisha hasara kwa serikali, wanadaiwa kwa pamoja walilitenda kosa hilo Mei 1, 2012 na Juni 1, 2015 wakiwa jijini Dar es Salaam walijipatia USD Milioni 600, 000,000 kama ada ya mkopo uliochukuliwa na Serikali ya Tanzania kutoka katika asilimia 1.4 hadi 2.4 na kusababisha serikali ipate hasara ya USD Milioni 6,000,000.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote,wamerudishwa rumande, kwa sababu mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, wakili Ngole amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 24, 2019.

 

WATUMISHI WA TASAF WAELEKEZWA KUZIHUDUMIA VIZURI KAYA MASKINI ILI KUZIWEZESHA KAYA HIZO KUJIKIMU KIMAISHA NA KUONDOKANA NA UMASKINI

$
0
0


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga akieleza majukumu ya taasisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa TASAF kilichofanyika Makao Makuu ya TASAF jijini Dar es Salaam chenye lengo la kuhumiza uwajibikaji.
Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mara baada ya kuzungumza na watumishi wa mfuko huo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

…………………………

Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wametakiwa kuhakikisha wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanahudumiwa vizuri kwa kupata ruzuku zao kwa wakati ili kuziwezesha kaya hizo kujikimu kimaisha na kuondokana na umaskini.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa TASAF makao makuu katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu kwa kina majukumu ya TASAF na kujiridhisha namna inavyotekeleza wajibu wake.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, kwa kuwahudumia vizuri wanufaika hao, TASAF pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itapata baraka za Mwenyezi Mungu ambaye kupitia vitabu vyake vitakatifu ameelekeza kuwasaidia maskini na pia watakuwa mfano bora wa kuigwa na nchini nyingine barani Afrika kwa kutekeleza vema Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa TASAF kuwa tayari muda wote katika kuhakikisha kaya zote maskini zinapata stahili zao kwa wakati na kufurahia matunda na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kuziwezesha kaya maskini kuondokana na umaskini.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameitaka TASAF kuhakikisha inaweka taratibu madhubuti za kisheria zitakazowaadhibu na kuwadhibiti wote watakaobainika kufanya udanganyifu kujipatia fedha za mpango wakati hawana sifa za kuwa wanufaika, lengo likiwa ni kujenga nidhamu katika jamii ili fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ziwafikie walengwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anavyotaka.

Katika kutekeleza azma hiyo, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa TASAF kufanya kazi kwa ari na uzalendo mkubwa na kuipongeza TASAF kwa jitihada na mafanikio waliyoyapata katika kuzinusuru kaya maskini mpaka hivi sasa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga amemhakikishia Mhe. Dkt. Mwanjelwa kuwa, atahakikisha anasimamia vizuri utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini kama alivyoelekeza, ili uwe ni mpango bora zaidi katika bara la Afrika, na kuongeza kuwa, hadi sasa, tayari mpango umeonekana kuwa ni miongoni mwa mipango bora barani Afrika kwani umeweza kuboresha maisha ya kaya maskini ambapo utekelezaji wake umewezesha kuzitambua kaya maskini, umesimamiwa vizuri, malipo yanafanyika kwa wakati na hakuna ubadhilifu mkubwa wa fedha zilizotengwa kwa ajili ya wanufaika.

Akithibitisha ubora wa mpango, Bw. Mwamanga amesema, hivi sasa Rais wa Benki ya Dunia katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku, anapozungumzia programu za kupambana na umaskini, haachi kuutaja Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa nchini Tanzania kuwa ni bora na unasimamiwa vizuri.

Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. John P. Magufuli aliyejipambanua kwa vitendo kuwajali wanyonge, imedhamiria kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini kuwafikia walengwa katika kaya zote maskini nchini ili walengwa hao waweze kunufaika na kuboresha maisha yao.

Balozi Seif aongoza matembezii ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema Vijana walioshiriki matembezi ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar wanapaswa kujenga ufahamu wa kujuwa Mapinduzi ndio yaliyoleta Ukombozi na kupatiana Mamlaka kamili ya Mwafrika yanayoharakisha Maendeleo ya Jamii hivi sasa.

Alisema jukumu la Vijana hao kwa wakati huu waelewe kwamba Uhuru wa Taifa hili wakati wowote utalindwa na wao wenyewe kwa vile hakuna Mtu au Kikundi kitakachokuja Zanzibar na Tanzania Nzima  kuwalindia Uhuru walioachiliwa kama urithi wao.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiyapokea na kuyafunga Matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi {UVCCM} ya kuunga mkono Mapindui ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyohitimishwa hapo katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chake Chake Kisiwani Pemba.

Alisema Vijana hao ndio warithi halali wa Mapinduzi hayo kwa sababu Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yalifanywa na Vijana chini ya Viongozi wa ASP Youth Leagae kwa wakati huo wakitekeleza Muongozo wa Afro Shirazy Party uliolenga kuondoa matendo mabaya, madhila na manyanyaso kwa Waafrika wa Zanzibar.

Balozi Seif aliwataka Vijana hao kuziepuka fitina za kudharauliana wenyewe kwa wenyewe na badala yake waimarishe Umoja na Mshikamano waliokuwa nao miongoni mwao na kamwe wasikubali kutenganishwa kwa vile makundi ni sumu ya Umoja wao.

Alieleza kwamba Waafrika wa Zanzibar baada ya kuchoshwa na Utawala wa Kikoloni waliendelea kushikamana , kuungana kuwa wamoja  kulikowasaidia kuikomboa Nchi yao toka mikononi mwa wageni kwa nia ya kujitawala na kujiamulia mambo yao wenyewe katika Ardhi yao.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alifahamisha kwamba wakati wananchi na Viongozi wanaposema Mapinduzi Daima inamaanishwa kwamba Serikalki itaendelea kuondoa matendo mabaya, udhalilishaji wa Wanawake na Watoto pamoja na mambo yote yanayorejesha nyuma  au kukwamisha juhudi za kujiletea Maendeleo.

Balozi Seif alielezea faraja yake kutokana na ushiriki wa Vijana kwenye Matembezi  hayo ukiwa  mkubwa jambo ambalo linadhihirisha wazi jinsi gani walivyokomaa Kisiasa pamoja na utayari wao wa kutetea, kulinda na kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar  kwa vitendo.

Alisema Nchi imetoka mbali kutokana na majaribu mengi iliyopata zilizotokana na changamoto nyingi zinazoonekana kusababishwa na wale wasioitakia mema ambao ni vibaraka wa hao waliopinduliwa Mwaka 1964.

Aliwapongeza Vijana wa kuendelea kulinda Amani ya Taifa huku wakitambua kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zimepiga hatua kubwa ya Maendeleo kutokana na  Amani hiyo.

Balozi Seif Ali Iddi akiwa pia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliendelea kuwakumbusha Wananchi kushiriki sherehe za Mapinduzi katika misingi ya Amani na utulivu kama ilivyozoeleka.

Alisema ni vyema kwa Mtu au Kikundi chochote kilichotia niya ya kushiriki sherehe hizo katika mazingira ya kutaka kufanya ushawishi wa vurugu Vyombo vya Dola havitakuwa na mzaha wa kuwadhibiti watu hao hao.

Akitoa Taarifa ya Matembezi  hayo ya Umoja wa Vijana wa CCM Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Mussa Haji Mussa alisema matembezi hayo yaliyozinduliwa Tarehe 5 Januri na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdullah Juma Saadala katika Kijiji cha Chokocho Mkoa Kusini Pemba.

Nd. Mussa alisema zaidi ya Vijana 400 walishiriki matembezi hayo kwa kuamua kubadilika katika kushiriki zaidi kwenye kazi za Jamii ikiwemo ujenzi wa Taifa wa  Majengo ya Skuli na Matawi ya Chama cha Mapinduzi kwa kuweka alama mote walimopita.

Alisema Umoja wa Vijana utaendelea kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa gharama yoyote ile na kamwe hakutakuwa na Mapinduzi mengine tena kwa vile kila Mwana jamii ameshuhudia kuwa huru kufanya analotaka kwa mujibu wa sheria.

Nd. Mussa alieleza kwamba Mapinduzi hayo ya Zanzibar yameleta utu na usawa wa Wananchi wote wa Zanzibar licha ya baadhi ya Wanasasa uchwara wakijaribu kudhihaki Mapinduzi hayo.

Akimkaribisha Mgeni rasmi kuyafunga matembezi hayo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Nd. Kheri Denis James alisema Vijana wa CCM wana jukumu la kutangaza kazi kubwa inayoendelea kutekelezwa na Marais wote wawili wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Nd. Kheri alisema tafsiri sahihi ya Mapinduzi Daima inayoendelea kutekelezwa hivi sasa imelenga katika kuimareisha Uchumi na Maendeleo ya Taifa ambayo Vijana wanalazimika kupigana kiume katika kuyalinda Maendeleo pamoja na Uchumi huo.

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa aliwaeleza Washiriki wa Matembezi hayo kwamba Wazee Waasisi wa Bara na Zanzibar waliacha Vyama vyenye nguvu kubwa  Vya TANU na ASP na baadae CCM zinazopaswa kudumishwa kwa ustawi wa Kizazi kijacho.

Ujumbe wa Mwaka huu wa Matembezi hayo ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi {UVCCM} ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar YA Mwaka 1964 unaeleza kwamba “ CCM na Vijana Mapinduzi yanaendelea kufana”.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif  akiwa pamoja na Viongozi wa UVCCM Wakijiandaa kuyapokea Maandamano ya Umoja wa Vijana wa CCM kuadhimisha kumbukumbu za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hapo Uwanja wa Gombani ya Kale Chake Chake Pemba.
Kanyaga kanyaga ni nyimbo wanaoimba Vijana hao wa UVCCM wakati wakiingia kwenye Uwanja wa Gombani ya Kale baada ya kumaliza Matembezi yao katika sehemu mbali mbali za Kisiwa cha Pemba.
Vijana wa UVCCM  wakionekana kuhamasika na umalizaji salama wa Matembezi yao ulioambatana na kazi za kujitolea  katika Miradi ya Kijamii na Kisiasa.
 Balozi Seif  akimpongeza Kiongozi wa Matembezi ya UVCCM Abdullah Ali Chum { Koti } baada ya kukabidhiwa  salama Picha ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Dr. John Pombe Magufuli iliyotumika kwenye Matembezi hayo.
Vijana wa matembezi ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 wa UVCCM wakifurahia na kushukuru huduma nzuri za Afya na lishe walizozipata wakati wa Matembezi yao ya Siku Tano Pemba.
Baadhi ya Vijana wa UVCCM wakifuatilia matukio mbali mbali yaliyokuwa yakifanyika katika Uwanja wa Michezo wa Gombani ya Kale wakati wa kuhitimisha Matembezi yao yaliyoanzia katika Kijiji cha Chokocho Mkoa wa Kusini Pemba.
Balozi eif akikabidhi Vyeti Maalum kwa Vijana wa UVCCM walioshiriki matembezi ya kumbukuimbu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyomng’oa Mkoloni katika Ardhi ya Visiwa vya Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa (UVCCM ) Mkoa wa Kibaha  Azilongwa Bohari akipokea Cheti Maalum kwa niaba ya Washiriki wenzake  cha Kuchiriki Matembezi hayo. Picha na – OMPR – ZNZ.

RAIS MAGUFULI ATOA NDEGE MBILI ZA RAIS KWA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA,ZITOE HUDUMA

$
0
0

*Aagiza zipigwe rangi zisafirishe Watanzania...asema kwanza yeye hasafiri sana

*Azungumza mambo makubwa kuhusu Watanzania, Balozi wa Canada aacha somo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ameagiza ndege za Rais mbili zipigwe rangi ya Shirika la Ndege Tanzania(ATCL) ili zitoe huduma ya kusafirisha Watanzania kati ya eneo moja na jingine.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza baada ya kupokea ndege mpya ya Airbus 220-300 iliyowasili leo Januari 11 ,2018 ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia uamuzi wake wa ndege mbili za Rais zitumiwe na Shirika la Ndege.

Amefafanua kuwa ndege ambazo zimetengwa kwa ajili ya Rais zipo tatu na hivyo ndege mbili amezitoa ili zitumike kutoa huduma."Kwanza Rais mwenyewe sisafiri ,hivyo ndege hizo zipigwe rangi ya ATCL zitoe huduma ya kwenda mikoa mbalimbali nchini,"amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Dk.Magufuli amesema Shirika la Ndege la Air Tanzania kwa asilimia 100 linamilikiwa na Watanzania wenye na hilo ni jambo la kujivunia sana na hayo ndio matokeo ya kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo.

Amesema kuna mashirika makubwa ya ndege ambayo yameandikwa majina ya nchi zao lakini si za nchi hizo lakini kwa ndege za ATCL ni mali ya Watanzania huku akifafanua ndege hizo ni za Serikali kwa asilimia 100.

Amesema Tanzania tunaweza na moyo wa kizalendo wa Watanzania upo ukiondoa wachache ambao hawana uzalendo na hao hawakosekani."Niwaahidi kwa nguvu zangu zote na ajili zangu zote niwatumikie Watanzania.

"Namuomba Mungu nisiwe na kiburi na majivuno.Namuomba Mungu aniongeze mimi na Serikali tuwatumikie Watanzania na hasa wanyonge bila kujivuna," amesema Rais Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Bunge ambalo limekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za Serikali na kwamba hata walipoamua kupitisha bajeti ya ununuzi wa ndege hizo ilitokana na uzalendo wao.

"Nawapongeza wabunge wote na haswaaa wabunge wa CCM ambao linapokuja suala la maendeleo wanaitikia ndiooo," amesema Rais Magufuli huku akisisitiza upendo na mshikamano kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Akizungumzia ndege hizo amesema miaka ya nyuma ndege kubwa zilikuwa zipo kwa nchi nyingine lakini leo hii zipo Tanzania na ndege ambazo zimebunuliwa za Airbus zipo nchi kwetu tu na hazipo mahali popote Afrika.

Amesema kuwa Tanzania itakuwa kama Ulaya na amewataka Watanzania kuamini kwenye hilo na kwamba ukiwa na imani unafanikiwa na hivyo Watanzania watafanikiwa sana.Amesema Tanzania ambayo anaitaka yeye ni ile ambayo huduma mbalimbali za kijamii ziwe zimeboreshwa na kwamba anaamini ndege zitaendelea kuongezeka.

Amesema Tanzania mpya inakuja na wanaochonganisha washindwe kwa la Yesu na Mtume Muhhamad huku akifafanua dua ambazo zimeombwa na viongozi wa dini Mungu amesisikia.

Ametumia nafasi hiyo kuwaombea Watanzania wote wafanikiwe kwenye mambo yao mbalimbali.Wakati huo huo Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kumpongeza Balozi wa Canada nchini Tanzania kwa uamuzi wake wa kuzungumza Kiswahili na amewafundisha Watanzania umuhimu wa kuzungumza Kiswahili.

Amesema kuna Watanzania ambao wamekuwa wakizungumza Kingereza na kujiona ni ufahari ambapo wanashindwa kuwafundisha lugha ya makabila ya Tanzania."Balozi na kupongeza na wale Watanzania wanaona 
aibu kuzungumza Kiswahili uwe mwalimu wao."

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI MFIKIWA ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya Askari Polisi Mfikiwa Chake Chake Pemba. Makamu wa Rais ambaye yupo Pemba kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ambapo jana tarehe 10 Januari 2019 aliweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar eneo la Pagali Chake Chake Pemba.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo Makamu wa Rais aliwataka Viongozi wa Vikosi kuongeza nguvu na kuhakikisha usimamizi wa shughuli za ujenzi wa makaazi ya askari unakamilika kama ulivyopangwa. “Mwaka jana tarehe 20 Machi 2018 niliweka jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba za makaazi wa askari wetu hivyo basi lazima lengo litimie kama tulivyozungumza siku ya uwekaji jiwe la msingi” alisema Makamu wa Rais.

Kwa upande mwingine Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji amesema kuwa mipango ya kumalizia ujenzi wa makaazi bora ya askari polisi bado inaendelea na kuahidi kuikamilisha kwani ni dhamira ya jeshi la polisi kuhakikisha askari wake wanaishi sehemu salama.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais aliwasalimia Askari wa Kike waliokuwa kwenye maandalizi ya gwaride maalum la siku ya maadhimisho ya kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi Takatifu ya Zanzibar yatakayofanyika kesho kwenye uwanja wa Gombani, Chake Chake Pemba.

“Mtapanda vyeo kwa jitihada ya kazi si vinginevyo hivyo Askari unatakiwa ufanye kazi kwa bidii sana” aliwahusia Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya askari Polisi  Mfikiwa Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na askari polisi wa kike waliokuwa wakijiandaa kwa ajili ya gwaride la maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi Takatifu ya Zanzibar mara baada ya kuwaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya askari Polisi  Mfikiwa Pemba. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassan Haji wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya askari Polisi  Mfikiwa Pemba.


TUNA KAZI KUBWA YA KUPANDA MITI NCHI ISIGEUKE KUWA JANGWA-PROFESA MKENDA

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania Profesa Adolf Mkenda akizungumza na akizungumza katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha leo. Picha na Vero Ignatus

Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Wakala wa Misitu Nchini Profesa D.Santos Silayo akizungumza katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha.

Mwenyekiti wa TFS Francis Kiondo Mwenyekiti Tughe,Meneja Misitu Wakala wa Huduma za Misitu wilaya ya Temeke

Hamisi Jori Afisa misitu wa wakala wa huduma za misitu kanda ya kati Dodoma na mjumbe Baraza

Wakwanza kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania Profesa Adolf Mkenda akifuatiwa na Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Wakala wa Misitu Nchini Profesa D.Santos Silayo. Picha na Vero Ignatus

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) walipokutana Jijini Arusha leo.

Mgeni rasmi pamoja na walio Meza kuu wakiwa wameshikana mikono wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa Solidarity Forever.

Mgeni rasmi Profesa Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.
Na. Vero Ignatus, Arusha


KATIBU Mkuu wa Wizra ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania Tafori na Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo kufanya tafiti maeneo ilioisha miti ili ipandwe mingine kwa ajili ya uvunaji wa haraka utakaoingizia serikali kipato.

Ametoa agizo hilo leo wakati akifungua mkutano wa saba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha kukumbushana utawala,haki na wajibu wa Mfanyakazi.

Amesema wajibu mkubwa wa wafanyakazi hao ni kulinda rasilimali za Umma kwa kupambana na uvunaji haramu usiokuwa na utaratibu,uchomaji moto misitu na uvamizi wa mapori kwa ajili ya malisho ya mifugo."Kutokana na hali hii lazima mtafute njia mbadala ya ufugaji wenye tija ili kulinda misitu na mapori yetu na pia kuhakikisha haturuhusu kilimo cha uharibifu wa mazingira,"Alisema Profesa Mkenda

Prof.Mkenda alisema serikali inatambua kazi inayofanywa na wafanyakazi hao na mazingira magumu yanayohatarisha maisha yao,ikiwemo kuzushiwa vitu vya uongo,kupigwa hata kuuwawa, hivyo hawatafungia macho suala hilo.

Ameagiza wafanyakazi hao kuhakikisha wanaacha tabia ya kutoa mizinga bure kwa wafugaji wa nyuki,badala yake wawakodishie ili kuipatia kipato serikali.
"Mizinga hii mnatoa bure lakini wengi hawaitumii,kodisheni ili watu waone uchungu wawese kuitumia ipasavyo kuzalisha asali,"alisema Prof. Mkenda

Alisema Tanzania ina uwezo wa kuongoza dunia kwa uzalishaji asali endapo misiti na mapori iliyopo itatumika vizuri kufunga nyuki ili kujipatia asali ambayo masoko yake yapo.Akitoa mfano alisema mapori ya Kakonko na Kibondo yana misitu na mapori makubwa ambayo tayari serikali imeshapeleka timu ya wataalamu wa kufundisha uzalishaji wa asali kwa wingi ili kukidhi soko la Uholanzi lililopatikana.

Naye Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) D.Santos Silayo, alisema changamoto kubwa walizonazo kwa sasa ni ongezeko la uhalifu maeneo ya misitu,uvamizi,kupambana na ugumu katika kudhibiti wahalifu kwani wengi wao wana silaha za moto.Pia alitaja changamoto nyingine kuwa ni misiti mingi ipo nje ta maeno yaliohifadhiwa rasmi,watumishi kutishiwa na kuzuiwa kutekeleza majukumu yao na baadhi ya watumishi wasiozingatia kanuni na sheria za uwajibikaji kazini.

"Kutokana na hali hiyo TFS inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kinidhamu za kudhibiti hali hiyo kwa watakaobainika,"alisema Pofesa Silayo.Pia amesema TFS wanatarajia kuanzisha mfuko wa kuweka akiba na kukopa SACCOS, kwa wafanyakazi wao na kujali afya za wafanyakazi wao wawapo kazini.

MFANYABIASHARA MAARUFU NA MFANYAKAZI WAKE WASOMEWA MASHTAKA 601,LIKIWEMO LA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA ZAIDI YA BILIONI 14

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu Mohamed yusufali na mfanyakazi wake Arital Maliwala wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 601 likiwemo la kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 14.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na jopo la mawakili wa kutoka Takukuru wakiongozwa na Hashimu Ngole, Pendo Makondo, Leornad Swai ambao walikuwa wakisaidiana na wakili wa serikali Patrick Mwita mbele ya hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Katika mashtaka hayo, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi, kuwasilisha taarifa za mwezi za mahesabu ya uongo kwa TRA, kukwepa kodi na kuisababishia serikali hasara ya sh. 14,987,707,044.58

Katika shtaka la kuisababishia serikali hasara, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa la kusabisha hasara ambayo imetokana na kukwepa kodi ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008 hadi 2015 kupitia kampuni ya Pamplant ltd iliyokuwa inamilikiwa na mshtakiwa Yusufali ambapo mshtakiwa Paliwala alikuwa mfanyakazi wake.

Imeendelea kudaiwa kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo wakiwa wanatumia stakabadhi za kughushi pamoja na kutumia makampuni ya kughushi wakidai kuwa wamenunua vitu kutoka katika makampuni mbali mbali wakati wakijua baadhi ya kampuni hizo ni za kughushi huku zikiwa hazijasajiliwa brella.

Pia imedaiwa kampuni hizo zina majina ya makampuni ambayo hayapo brella na yana namba  za usajili ambazo brella haijazifikia huku pia wakiwa wanaghushi stakabadhi za malipo.Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika na kesi hiyo itakuja tena mahakamani hapo January 24  mwaka huu kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo yao (commital).

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA WAZIRI MHAGAMA OFISI ZA PSSSF NA NSSF MOSHI

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghwira wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli kwa mifuko ya hifadhi ya jamii NSSF na PSSSF aliyoyatoa Desemba 28, 2018 alipokutana na viongozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (kulia) akimsikiliza Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF Bi. Neema Kuwite wakati wa ziara yake katika ofisi hizo Januari 10, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akimsalimia Bi.Mary Kiramvu mmoja wa wastaafu waliojitokeza kuhakiki taarifa zake katika Ofisi za PSSSF Moshi ikiwa ni utekelezaji wa majukumu ya Mhe.Rais alipokutana na viongozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Ikulu Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akifurahi na baadhi ya wastaafu walioripoti katika ofisi za PSSSF Moshi wakati wa zoezi uhakiki wa taarifa za uanachama ili kubaini wastaafu hewa.
Baadhi ya wastaafu wakijaza fomu za taarifa zao wakati wa zoezi la uhakiki katika ofisi za PSSSF Moshi mkoani Kilimanjaro Januari 10, 2019
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na baadhi ya wastaafu wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Mhe.Rais Dkt. John Magufuli kwa mifuko ya NSSF na PSSSF.
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi wa NSSF Tawi la Moshi Bi.Mary Onesmo akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama namna huduma zinavyotolewa katika madirisha ya kusikiliza wastaafu katika Ofisi hizo alipotembelea Januari 10, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya jamii NSSF Bw.William Erio (katikati) akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama wakati wa ziara yake katika Ofisi za NSSF Moshi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiangalia namna watumishi wa NSSF wanavyotoa huduma kwa wateja wao wakati wa ziara yake katika Ofisi hizo Moshi Mjini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya jamii NSSF Bw.William Erio maelezo ya ufafanuzi kuhusu mifuko ya Hifadhi nchini kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama alipotembelea Mfuko wa NSSF Moshi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (wan ne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali pamoja na wale wa mifuko ya Hifadhi wakati wa ziara yake katika ofisi za Moshi mkoani Kilimanjaro.Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya jamii NSSF Bw.William Erio



PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WANANCHI KUPOKEA NDEGE YA PILI YA AIRBUS A220-300

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kupokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 iliyowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Isaack Kamwelwe wakipewa maelezo na  Rubani Patrick kuhusu ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 walipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi baada ya kupokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019

 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakiwa na viongozi wengine mbalimbali wakishuka kutoka katika ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 ilipowasili na kupokelewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019.
 Maafisa waliokwenda Canada kuipokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 wakilakiwa kwa shangwe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019
Picha na IKULU

MAMLAKA YA NGORONGORO YAKABIDHI SH.BILIONI MOJA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI,VITUO VYA AFYA KARATU

$
0
0
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Professa Abiud Kaswamila akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mfano wa hundi ya Sh milioni 500,000 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya Samunge na Arash wilayani humo zilizotolewa na NCAA kama sehemu ya mchango wa shughuli za maendeleo.
 Viongozi wa wilaya ya Ngorongoro na Karatu mkoani Arusha wakiwa wameshika hundi za mfano wa fedha zilizotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Sh Bilioni 1 walizokabidhiwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Karatu na vituo viwili vya afya wilayani Ngorongoro.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka mfano wa hundi ya Sh milioni 500 zilizotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya ujenzi wa vituo viwili vya afya katika Kijiji cha Samunge na Arash wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo mfano wa hundi ya Sh milioni 500 zilizotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya ujenzi wa vituo viwili vya afya katika Kijiji cha Samunge na Arash wilayani humo. 


NA MWANDISHI WETU, ARUSHA


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Profesa Abiud Kaswamila amekabidhi Sh bilioni 1 za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Karatu na vituo viwili vya afya wilayani Ngorongoro.

  Mchango huo wa maendeleo kutoka NCAA ulipokelewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, ambapo wilaya ya Karatu imepokea Sh milioni 500 na Ngorongoro Sh milioni 500.Akizungumza wakati wa kukabidhi mchango huo Prof. Kaswamila alisema, msaada huo utakuwa chachu ya uhifadhi endelevu ikizingantiwa wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo ni wadau wakubwa.

 “Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inayo majukumu makubwa matatu, kuhifadhi maliasili na malikale, kuendeleaza wenyeji na kuendeleza utalii,” alisema Prof Kaswamila na kuongeza:“Katika kuendeleza majukumu hayo chanzo kikuu cha mapato ni utalii, aidha maendeleo ya utalii yatafikiwa iwapo maliasili zilizopo ndani ya hifadhi wakiwamo wanyamapori wanahifadhiwa kwa kushirikiana na wenyeji wa Ngorongoro na jamii inayozunguka hifadhi,” alisema.

Alisema NCAA imekuwa ikichangia miradi ya maendeleo kupitia ujirani mwema ambapo mwaka 2016-2017 ilitumia Sh 359,117,500 na mwaka 2017-2018 Sh 295,000,000 na mwaka 2018-2019 imetenga Sh 1,415,000,000 kufadhili miradi ya ujirani mwema.Kwa upande wake Gambo akipokea hundi hizo kisha kuzikabidhi kwa wakuu wa wilaya husika alisema, tangu nchi ilipopata Uhuru ni wilaya ya Monduli na Arumeru ndio zilizokuwa na hospitali za wilaya.

 Kutokana na juhudi hizo Gambo aliishukuru Bodi ya NCAA kwa kutoa fedha hizo akisema zimekua chachu kwa wananchi wa Kata ya Samunge wilayani Ngorongoro ambao baada ya kusikia habari hizo walianza kuchimba misingi nane ya ujenzi wa kituo chao cha afya kwa kujitolea.“Kwa wilaya ya Ngorongoro Sh milioni 400 zitakwenda kujenga kituo cha Afya Samunge na Sh milioni 100 zitakwenda Kata ya Arash kujenga Kituo cha Afya, wilaya ya Karatu wao watazielekeza zote kwenye ujenzi wa Hospitali ya wilaya,” alisema Gambo.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo alishukuru kupokea fedha hizo na kuahidi kuwahamasisha wananchi kuanza kufanya kazi za kujitolea kuanzia wiki ijayo.Naye Mkuu wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka alisema, mchango huo umekuwa ni neema kwao kwani umewafungulia ukurasa mpya wa maendeleo ya sekta ya afya.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WANANCHI KUPOKEA NDEGE YA PILI YA AIRBUS A220-300

$
0
0

 Ndege mpya ya kisasa aina ya Airbus 220-300 iliyopewa jina la moja ya hifadhi ya  mbuga za wanyama  (Ngorongoro), ikikaribishwa kwa water salute mara baada ya kutua leo 11 Januari 2019 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere  ikitokea Canada ilikotengenezwa.  
 Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ikiwasili kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo, ndege hiyo imepewa jina la moja ya hifadhi  ya mbuga za wanyama  Ngorongoro kama inavyoonekana kwenye picha. 
 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) wakiwa wamesimama mbeleya  ndege mpya aina ya Airbus 220-300 mara baada ya kuipokea leo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ndege hiyo ni ya kwanza kununuliwa na serikali ya Afrika (Tanzania). 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ndege mpya aina ya Airbus 220-300 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius  Nyerere, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Ally Bashiru, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania Pamela O’Donnel ,na Kulia ni Mkrugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)  Mhandisi Ladislaus Matindi, Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge ya Miundombinu Suleiman Kakoso na Waziri  wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa mara baadya ya kuzindua ndege mpya aina ya Airbus 220-300 iliyowasiri leo 11 Januari, 2019 kulia ni , Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge ya Miundombinu Suleiman Kakoso na Waziri  wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson na Balozi wa Canada nchini Tanzania Pamela O’Donnel
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi mara baada ya mapokezi ya Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 iliyopokelewa uwanja wa Kimataifa Julius Nyerere leo 11 Januari 2019.
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images