Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 175 | 176 | (Page 177) | 178 | 179 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakisalimiana na viongozi wa wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya, katika mpaka wa wilaya hiyo na Ileje mapema leo asubuhi.
    Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Momba mkoani Mbeya, katika mpaka wa wilaya hiyo na Ileje mapema leo asubuhi.
  Pichani juu ni  Viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Momba, wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, alipokutana nao katika kikao cha ndani kwenye ukumbi wa Uwanji, wilayani humo, leo.  

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Vijana wa UVCCM, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
    makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Vijana wa CCM, baada ya mazungumzo yao alipokutana nao jana kwa ajili ya kumkabidhi ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Beji ya Mapambano dhidi ya Ukimwi na Katibu wa Hamasa na Chipukizi Taifa, Paul Makonda, wakati alipokutana na Vijana hao wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wenye lengo la kusambaza ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Vijana wa UVCCM, baada yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

  0 0

  DUNIA MZOBORA
  DAR ES SALAAM, Tanzania
  MHARIRI Mwandamizi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Dunia Mzobora, ambaye amefariki dunia jana, anazikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
           Habari zimesema Mzobora (49), ambaye alifariki dunia ghafla jana saa 12 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alikokuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi, akitokea Hospitali ya Aga Khan pia ya Dar es Salaam, anazikwa leo saa 7 mchana katika makaburi hayo>>ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda na wafanyabiashara, viwanda na kilimo Tanzania mkoa wa Iringa TCCI , Lucas Mwakabungu (katikati),akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya utafiti  uliofanywa na Institute of Business Environment Strengtheniing for Tanzania (IMED) kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Commerce,Industries and Agriculture (TCCIA) Mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa mwanzoni mwa wiki.(Picha na Denis Mlowe)
  ========  =======  =========
  Na Denis Mlowe,Iringa.

  UTAFITI uliofanywa na Institute of Business Environment Strengtheniing for Tanzania (IMED) kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Commerce,Industries and Agriculture (TCCIA) Mkoa wa Iringa umebaini Tanzania inapoteza mapato zaidi ya shilingi bilioni 174  kwa mwaka kutokana na wakulima kutotumia mizani katika upimaji wa mazao ya mahindi na mpunga.
   Mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda na wafanyabiashara, viwanda na kilimo Tanzania mkoa wa Iringa TCCI , Lucas Mwakabungu amebainisha hayo wakati akzungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa kuwa utafiti huo kuhusu sheria ya vipimo na mizani wa mwaka  1982 unavyosimamiwa na kutekelezwa na kurudiwa Julai na Septemba mwaka 2013.

   Alisema utafiti huo unaonyesha kwa kiasi gani wakala wa vipimo na mizani unatekeleza sheria hiyo na wafabyabiashara na wakulima wanaifuata na kuitekeleza iadha madhara na matokeo ya kutoifuata sheria hiyo.
  Mwakabungu alibainisha kuwa mikoa ya Iringa na Njombe pekee inapoteza ushuru wa mazao (crop Cess) ya mahindi na mpunga zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kwa mwaka kutokana na mikoa hiyo kuhusika na kilimo cha mazao hayo. Alisema ushuru wa kodi ya mazao unaopotea kwa mazao ya mahindi na mpunga kwa nchi nzima kwa msimu ni shilingi bilioni 14.8.

   Alisema utafiti uliofanywa na IMED ulichukua sampuli za magunia 43 ya mpunga yaliyopimwa uzito na wakala wa vipimo na mizani (WMA) kati ya magunia 482 yaliyokamatwa na kubainika kuwa uzito halisi wa kila gunia ulikuwa wa wastani wa kilo 42 zaidi ya uzito unaostahili sawa na asilimia 56.

   Aidha alibainisha kuwa uzito wa wastani wa gunia la mahindi lililojazwa kwa ndoo za plastiki lina kilo 36 zaidi ya uzito unaostahili sawa na asilimia 40 kutokana na lumbesa ambayo wakulima wanadidimizwa na wafanyabiashara.

  Alisema wakulima wanatumia ndoo za plastiki na lumbesa kwa kuwa kuna upungufu wa mizani na ushuru wa mazao kulipwa kwa gunia badala ya uzito na kutokuwepo kwa vifungishio vinavyokubalika.

  Mwakabungu alisema utafiti huo ilibainisha kuwa wakala wa vipimo na mizani(WMA) hawana rasimali fedha za kutosha, vifaa vya kutosha na hawana rasimali watu wa kutosha kuwezesha kuitekeleza sheria hiyo kama inavyotakiwa.

  0 0

  Nyota wa mrembo wa Tanzania anayewania taji la Miss Earth, Clara Noor imeanza kung’ara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika taji la fukwe ya Pagudpud iliyopo nchini Phillipines.

  Mbali ya kutwaa taji hilo, Clara pia ameibuka mshindi wa tatu katika taji la vazi la Taifa na kuzipiku nchi nyingine nyingi na kuzawadiwa medali ya shaba.
  Katika mashindano ya tuzo maalum, jumla ya tuzo 11 zilikuwa zinagombaniwa na warembo 88 walikuwa wanawania mataji hayo ambayo zawadi zake zilitolewa na wadhamini hao.
  Clara alionyesha uwezo mkubwa katika taji hilo na kuwa mwafrika wa kwanza kushinda katika historia. Katika vazi la Taifa, Clara aliwavutia wengi na kupata ushindani mkubwa kutoka kwa mrembo wa warembo kutoka Afrika Kusini, Ashanti Mbanga na kutoka Nigeria, Marie Miller ambao walishika nafasi ya kwanza nay a pili.
  Muandaaji wa Miss Earth Tanzania, Maria sarungi Tsehai alisema kuwa ni faraja kubwa kwa Clara kuitangaza Tanzania kwa kupitia mataji hayo mawili kwani mbali ya jina lake, kinachotangazwa pia ni nchi.
  “Amefanya vyema mpaka sasa, tunatarajia kuona anaendelea kufanya vizuri na kutuletea sifa, mpaka sasa anastahili pongezi,” alisema Maria ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications.
  Alisema kuwa fainali ya mashindano hayo yatafanyika Desemba 7 kwenye ukumbi wa Versailles Palace, Alabang, Muntinlupa City na kurushwa live na vituo vya televisheni vya STAR World, ABS-CBN, Velvet, The Filipino Channel, Ustream na Venevisión.

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akisistiza jambo kwa watangazaji wa vipindi vya redio mbalimbali (hawapo pichani) kuhusu vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel ya "Mimi ni bingwa" itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku.Kulia kwake ni ofisa wa matangazo wa Airtel Bw. Abdallah Gunda.
  Toka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airte Tanzania Bw Jackson Mmbando akibadilishana mawazo na watangazaji wa kipindi cha jahazi bw Musa Huseni (kati) na Ephraem Kibonde mara baada ya mkutano maalum na watayarishaji na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio kwa lengo la kuwaeleza vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel Mimi ni bingwa" inayowawezesha wateja wa Airtel kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku

  0 0
 • 11/28/13--09:54: Njia Uhuru Marathon yatajwa
 • Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini, Suleiman Nyambui (Kulia),
  akimkabidhi fomu ya ushiriki wa mbio za kilomita 3 za Uhuru Marathon,
  mwanamichezo Imani Madega (Kushoto), huku mratibu wa mbio hizo,
  Innocent Melleck akishuhudia wakati wa tukio la kuonyesha njia mbio
  hizo zitakazoshirikisha watu wa rika tofauti na viongozi mbalimbali
  zitakavyokuwa kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es
  Salaam leo. Mbio hizo ambazo lengo lake ni kuhamasisha umuhimu wa
  uwepo wa amani nchini zitafanyika Desemba 9 mwaka huu.
  ===========  ========  ========
  KUMEKUCHA! Mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, sasa zimefikia patamu baada ya waandaaji jana kutangaza njia itakayotumika kwa ajili ya mbio hizo.
   
  Mbio za Uhuru Marathon zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu na zitaanzia viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni na kumalizikia hapo.
   
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Selemani Nyambui alisema, njia hizo zimepimwa kwa kuzingatia taratibu zote za mbio za kimataifa.
   
  Nyambui alisema, upimaji ulifanyika kwa umakini mkubwa kwa kuhakikisha wale watakaokimbia mbio za kilomita 42, kilomita 21 na kilomita 5 wanakimbia kwa kiwango sahihi zaidi.
   
  Nyambui alitaja njia zitakazotumika kwa wanariadha wa kilomita 42 kuwa, wataanzia Viwanja vya Leaders na kupitia Barabara ya Alli Hassan Mwinyi kuelekea Morocco, watapitia Old Bagamoyo kuelekea Kawe na kufuata barabara ya Tegeta.
   
  Wanariadha hao watapita pia Mwenge hadi Makumbusho ambapo watafika eneo la Morocco na kuchukua Barabara ya Kawawa hadi katika taa za Chang’ombe, ambapo wataelekea Tazara na wakifika hapo watafuata Barabara ya Mandela hadi Uwanja wa Taifa.
   
  Wakifika hapo watapita Barabara ya Taifa na kutokea Chang’ombe na kwenda hadi Kinondoni kwa Manyanya watakapochukua barabara ya kuelekea makaburini (Kinondoni Road) na kutoka Barabara ya Alli Hassan Mwinyi na hatimaye kuingia Viwanja vya Leaders.
   
  Nyambui alisema, mbio za kilomita 21 zitatumia njia hizo lakini lakini hazitafika eneo la Chang’ombe kama ilivyo kwa zile za kilomita tano.
   
  “Naamini kwa dhati kabisa mbio hizi zitafanikiwa kwa kiasi kikubwa na mpaka sasa wanariadha wengi wamejitokeza kushiriki,” alisema.
   
  Naye Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent Melleck alisema, wanaamini kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa haswa kwa mipango waliyoiweka.
   
  Melleck alisema, mpaka sasa usajili unaendelea ambapo kwa wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.

  0 0


  Fions McGloin Meneja Mkuu Uganda na Tanzania akisisitiza jambo. Kushoto Madaha Francis Mkuu wa Mtandau , Kulia Deo Ndejembe Mkuu wa Mauzo kwenye mkutano na Waandishi wa habari jijini Arusha leo asubuhi
  ====  =====  ======
  SMILE YAZINDUA MTANDAO WENYE KASI ZAIDI ARUSHA

  Leo, Smile Communications Tanzania (Smile) inazindua huduma zake za Fourth Generation Long Term Evolution (4G LTE) mkoani Arusha, ikileta mapinduzi ya intaneti yenye kasi kwa wafanyabiashara, mashirika na wakazi wa ndani na wanaozunguka jiji la Arusha.
  Smile inatoa intaneti yenye kasi zaidi katika soko; mtandao wake 4G LTE hutoa huduma za intaneti kwa kasi ambayo watoa huduma wengine hawawezi kuifikia. Mtandao wa Smile hutumia teknolojia ya mawasiliano iliyoendelea zaidi na viwango vya ubora vinavyoendana na sehemu nyingine duniani, na hutoa kasi isiyo na mpinzani, uhakika, ubora na urahisi wa matumizi ambao huboresha matumizi ya mtandao.

  LTE (Long Term Evolution) ambayo pia inajulikana kama 4G LTE inawezesha upatikanaji wa intaneti yenye kasi zaidi kwa sababu ndiyo kiwango cha teknolojia cha kisasa cha kizazi cha nne (fourth generation – 4G) na inawakilisha mabadiliko ya hatua katika mageuzi kutoka kwenye teknolojia zilizopo za mawasiliano bila waya (wireless) kama vile GSM- 2G/GPRS/EDGE na UMTS-3G/3.75G. 4G LTE ni kizazi kipya cha mtandao pamoja na mawasiliano ya sauti na intaneti, na muundo wake unaoweza kubadilika na kuboreshwa mara kwa mara, una hakikisha kuwa 4G LTE itabaki kuwa kiwango bora zaidi cha huduma za intaneti na sauti kwa miaka ijayo.

  "Smile ilizinduliwa jijini Dar es Salaam tarehe 16 Mei 2013, na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata mapinduzi haya ya kiteknolojia. Tuna furaha kubwa kuwaletea huduma hii jijini Arusha. Kama kitovu mashuhuri kimataifa ambacho kina sekta iliyo kubwa, inayokua kwa kasi na yenye nguvu zaidi katika huduma za utalii na taasisi mbalimbali za elimu, Arusha ina biashara nyingi, mashirika na watu ambao watafaidika kutokana na huduma zenye intaneti yenye kasi, "alisema Fiona McGloin , Meneja wa Smile Tanzania na Uganda.

  "Smile tuna uhakika kuwa kutoa intaneti ya kuaminika na yenye kasi zaidi, itachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya biashara zilizopo Arusha na pia kuwapa wakazi wa Arusha huduma yenye kasi, ya kuaminika na gharama nafuu,” alisema Bi McGloin.

  Katika sekta inayokuwa kwa kasi ya mawasiliano hapa Tanzania, intaneti ya 4G LTE kwa sasa ndiyo inaongoza kwa kuwa na kasi mara sita zaidi kuliko 3G na mara nne  zaidi kuliko 3.75G. Smile inatoa wastani wa kasi ya kupakua ya 6Mbps na kiwango cha 3Mbps kasi ya kupakia. Kwa teknolojia hii, watumiaji wana uhakika wa kasi ya upakuaji na muhimu zaidi, kasi ya upakiaji wa mafaili, barua pepe, taarifa, nyimbo na michezo; matumizi ya nyenzo mbalimbali za kwenye mtandao, na kwa kuangalia video/TV bila kugomagoma.

  "Tunajivunia kuwaletea intaneti yenye kasi zaidi jijini Arusha ambayo inalingana na kasi na ubora wa intaneti barani Ulaya. Smile sio tu kwamba tutatoa huduma ya intaneti peke yake, bali tutatoa huduma ya intaneti yenye kasi zaidi, ya kuaminika na kwa bei ya kiushindani na pia tuna nia ya kutoa huduma kwa wateja zenye kuridhisha,” aliongeza Bi. McGloin.

  Kama sehemu ya mpango wa kuwajibika kijamii wa kampuni ya Smile, kampuni inatoa huduma za bure za intaneti yenye kasi katika shule za kiserikali: hadi sasa, Smile imewezesha shule 10 jijini Dar es Salaam na inaleta mpango huo katika jiji la Arusha.

  Wateja wa Arusha sasa wanaweza kujiunga na Smile kwa kutembelea maduka yetu ya rejareja ambayo yanazidi kuongezeka ,duka la Smile mtaa wa  India, jiji la Arusha , au kwenye kioski ndani ya duka la E-Tronic, gorofa ya kwanza, Njiro Complex, Arusha, au wasiliana na Huduma kwa Wateja kwa barua pepe (customercare@smile.co.tz) au simu +255 (0) 222 199 840.


  Kupata taarifa zaidi kuhusu Smile tembelea tovuti: www.smile.co.tz


  0 0

  Mratibu wa matembezi hayo Bw, Matukio Chuma akiwaonyesha waandshi wa habari vazi litakalotumika kwenye matembezi hayo (kushoto), Mratibu wa matembezi hayo Carren Mgonja.

  Mratibu wa matembezi hayo Bw, Matukio Chuma akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam wakati akizindua Matembezi ya Nchi Yangu Wajibu Wangu, yanayo tarajiwa kuanza, Januari 11-2014 kuanzia jijini Dar es Salaam hadi Mkoani Morogoro.

  Matembenzi hayo ya kilomita (200km), ambayo yatachukua siku kumi 10,lengo la matembezi hayo kuhamasisha kila Mtanzania anaamua kuamua kuchukua hatua ya kujikwamua kimaisha.

   Ni changamoto inayotolewa mbele ya Watanzania,kukumbuka maana halisi ya uzalendo kujitoa mhanga kuweza kufanikisha maendeleo yao wenyewe kwa kujishughulisha na kujibidiisha katika Nyanja mbalimbali kwa manufaa ya Taifa,kujitolea kuanzia ngazi ya kaya mpaka taifa,kuacha kulalama tu kuwa serikali haijawafanyia moja ama mbili lakini wao wenyewe kutambua mchango wao kama Watanzania na wajibu wao kama wananchi.

  Kubwa zaidi kujivunia nchi iitwayo Tanzania kwa yale mema na adimu yaliyopo na kurekebisha palipo na kasoro kwa moyo mmoja bila kujali itikadi,imani, asili ama mtizamo miongoni mwetu, Tanzania,kwa nini Dar es Salaam mpaka Morogoro.

  Dar es Salaam imendelea kuwa kituo kikuu cha shughuli nyingi za kiuchumi,kiserikali na vilevile ni mkoa ulio na watu wengi zaidi Tanzania, ta kribani milioni mbili na nusu (2.5mil) kawa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2002, wakati Morogoro ina watu wasiofika laki tatu tu, na kwa ukuaji wa asilia 4.39,hii inawakilisha tofauti kubwa sio tu kwa idadi lakini ya ukuaji, upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii, ukuaji wa kiuchumi na vilivile hali ya kipato na fursa za iuchumi” alisema Chuma.
  Mratibu wa matembezi hayo Bw, Matukio Chuma akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam wakati akizindua Matembezi ya Nchi Yangu Wajibu Wangu, yanayo tarajiwa kuanza, Januari 11-2014 kuanzia jijini Dar es Salaam hadi Mkoani Morogoro.
  Waandishi wa habari wakishuhudia uzinduzi huo.

  0 0

   - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hituba yake ya uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Miaka 10 ya Mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania, yaliyozinduliwa rasmi leo katika Ukumbi wa Mliman City,jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
    Wadau wakisikiliza hotuba ya ufunguzi
   Wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi

  0 0

  DSC_0170

  The Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel speaks to invited guests and reporters (not in picture) during the official handing over ceremony of the New Model Volkswagen Touareg held at Umoja House premises in Dar.(All photos by Zainul Mzige).
  .Germany Embassy in Dar has chosen TOUAREG has it’s official car

  By Damas Makangale, MOblog
  THE Embassy of the Federal Republic of Germany has launch the new model of the Volkswagen TOUAREG sport utility vehicles as part of the Embassy’s mobility fleet. It has been established.

  Speaking to invited dignitaries during the official handover ceremony at Umoja House in Dar es Salaam, the Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel said that Volkswagen is one of the largest automobile company in the world, in Tanzania and underlined that German products are known worldwide for high class technology and innovative engineering.

  “The embassy of Germany is promising to provide high quality products into Tanzanian market and while assuring Tanzanians to see the new model of Volkswagen in the street,”
  DSC_0183
  The Managing Director of Alliance Autos Wayne McIntosh pointed out to the newly Volkswagen Touareg during the official launching and handing over ceremony to the Embassy of the Federal Republic of Germany in Dar.
  “The Touareg redefines the Sports Utility Vehicle (SUV) featuring extraordinary luxury, exceptional versatility and technological advances that are simply ahead of their time,” he said.

  Koeppel further said that the innovating of another model of Volkswagen is a clear picture of the spirit of cooperation between Tanzania and Germany and mutual respect between the two countries.


  On his part the Managing Director of Alliance Auto, Wayne McLntosh felt honored that the TOUAREG was chosen as the official Embassy car while introducing the product to Tanzanian market.
  “It provides a unique combination of four-wheel drive, off road capabilities, sustainable energy efficiency and high driving performance,”
  “Not only winning prizes as “Best Luxury SUV” and “Sport/Utility of the year, the TOUAREG also introduces success and experience of Rally Dakar-winners onto the road,” He underscored.
  He said that in the coming months, the stylish, sophisticated and refined second generation of the TOUAREG will conquer the streets of Dar es Salaam.
  McLntosh explained further that Volkswagen has opened its showroom in Tanzania in collaboration with Alliance Auto in March 2013 and is aiming to provide Tanzanians with high quality engineering “Made in Germany’ offering the TOUAREG Amarok pick-up and Tiguan.
  DSC_0189
  The Managing Director of Alliance Autos, Wayne McIntosh together with the Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel showing invited guests and reporters the newly Germany Auto mobile product Volkswagen TOUAREG during the official launching held in Dar at Umoja House.
  DSC_0196
  Congratulating each other.
  DSC_0202
  The Managing Director of Alliance Autos, Wayne McIntosh hands over a key to the Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel.
  DSC_0216
  Volkswagen TOUAREG at the back.
  DSC_0139
  CFAO Motors Commercial Director, Charles-Edouard CAMBOURNAC explains to the invited guests how the newly Volkswagen TOUAREG operates and other specifications.
  DSC_0137
  Bongo5 CEO, Luca Neghesti with other invited guests enjoying refreshments.
  DSC_0125
  Sudan Ambassador to Tanzania Dr. Yassir Mohammed Ali shares a light moment with one of the invitees.
  DSC_0152
  Alliance Autos Marketing Manager, Tharaia Ahmed exchange views with one of the invitees during the event.
  DSC_0218
  Alliance Autos Marketing Manager, Tharaia Ahmed in tete-a-tete with the Sudan Ambassador to Tanzania Dr. Yassir Mohammed Ali.
  DSC_0235
  The Charge d’ Affaires from the Embassy of the Federal Republic of Germany, Hans Koeppel shares a light moment with the Embassy of Turkey Third Secretary, Berat Colak (left).
  DSC_0210
  Invited Guests following up the launching ceremony of new Volkswagen TOUAREG at Umoja House.

  0 0

    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, mjini Tunduma, wilayani Momba, jioni hii, Nov 28, 2013,Kinana ameitaka Serikali kupunguza ama kuwaondolea vikwazo  wananchi katika suala zima la kujiletea maendeo yao,pia ameongoza kuwa Viongozi wawasikilize Wananchi badala ya kuka maofisni na semina kila wakati ambazo hazina tija yoyote kwa wananchi,Ndugu Kinana na ujumbe wake yupo katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuzungumza nao njia ya kuzitatua, katika mkoa wa Mbeya.
   Sehemu ya umati wa watu waliofurika kwenye mkutano huo wa hadhara wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye aliwakonga nyoyo wakazi wa eneo hilo wakiwemo wapinzani kwa kusema kuwa hatakuwa tayari kuwavumilia viongozi wanaoshindwa kutatua kero za wananchi,waliojawa na umangimeza na urasimu.
   Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati mwenye  miwani) akiserebuka na wananchi kwenye mkutano, Uwanja wa shule ya  Mwaka, Tunduma leo.
    Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
   Wananchi wakiwa wamembeba Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo.
   Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro , akihutubia katika mkutano huo,ambapo alisisitiza kuweka kipaumbele cha elimu kwa watoto wa kike pamoja kupiga vita unyanyasaji wa wanawake na watoto.
  Chifu wa kabila la Wanyamwanga,Jubec Chipansia akikambidhi silaha za jadi katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ikiwa ni ishara ya kuilinda amani na utulivu tulionao nchini kwa namna moja ama nyingine.

  0 0


  Ujumbe wa benki ya dunia (WB) kutoka ofisi ya kanda ya Afrika Mashariki ukiongozwa na Mkuu wa miradi ya sekta ya usafirishaji Eng. Solomon Waithaka wa pili kulia leo umetembelea TPA kukagua miradi inayofadhiliwa na benki hiyo. 

  Wengine kwenye picha ni Eng. A. Matei Naibu Mkurugenzi Mkuu - TPA katikati na kulia kwake ni Ndg. Phares Magesa Mkurugenzi wa ICT - TPA na Kiongozi Msimamizi wa miradi ya WB, na wa kwanza kulia ni Ndg. Suluo Mratibu wa miradi hiyo kwa sekta ya usafirishaji na wengine ni wakuu mbali mbali wa vitengo TPA.

  Kwa ujumla benki imeridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo.
  Miradi inayofadhiliwa na WB na wadau wake katika Mamlaka ya Bandari ni:
  I. Integrated security system( ISS)
  II.electronic Single Window System(eSWS)
  Iii.Port security Training (ISPS )
  Iv. Mradi wa Patrol boats

  0 0

  MO SFW Banner

  Or by TextingSWFA SMP O3TO15678

  0 0

  Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisaini mkataba wa wa kupiga show jijini Mwanza itakayofanyika mnamo tarehe 24/12/2013 mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo, tukio linalotazamiwa kufanyika katika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza.
  Picha zaidi za Mwanamuziki mkali Afrika akisaini mkataba baina yake na viongozi waandaaji wa Show hiyo. Makubaliano haya ya kuweka mkataba yamefanyika jumatatu ya wiki hii tarehe 25/11/2013 jijini Kampalanchini Uganda.
  Mwanamuziki Dr. Jose Chameleone (katikati) akiwa na Mapromota wa show itakayofanyika jijini Mwanza Dennis Mshema (Kushoto) na Mr. Ben Mwangi (kulia) mara baada ya utiaji wa saini wa kupiga show moja kali tena takatifu itakayofanyika mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas katika ufukwe wa Charcoal Ribs jijini Mwanza.
   Kwa mujibu wa moja wa Mapromota hao Mr. Ben amesema kuwa ile kiu ya mashabiki wa muziki wa ukweli toka kwa Mwanamuziki Jose Chameleone sasa inakwenda kupata dawa yake, kwani maandalizi mazuri yameanza kufanyika kuhakikisha kila kilichobora kina tukia kwenye jukwaa la burudani siku hiyo ya mkesha wa Christmas.


  "Tutafunga sound mpya ya mtikisiko, tutajenga jukwaa kubwa bora tena la kisasa, tutafunga taa za kisasa pamoja na huduma nzuri kwa wateja watakaofika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza, nia na madhumuni kuufanya usiku huo kuwa mkubwa, mzuri wenye mengi maajabu katika burudani" Alisema Ben.   Ameongeza kuwa bado milango iko wazi kwa makampuni mbalimbali na sekta binafsi kushiriki katika suala zima la udhamini. Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0752813212.  Mbali na kuwa na masongi makali kama Bei kali, Kamila na kadhalika ambayo hadi sasa utamu wake uko pale pale Jose Chameleone kwa sasa anatikisa ulimwengu wa burudani ya muziki na ngoma zake kali kama Badilisha, Sumula, Valu valu, Tubonge na nyingine kibao... 

  0 0


   Pichani kulia ni Mkuu wa MKoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandoro akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,mara baada ya kuwasili mapema leo asubuhi kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya..Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko ziarani mkoani humo kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM,kusikiliza kero za Wananchi na namna ya kuzipatia ufumbuzi,
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Machifu wa Wilaya ya Mbozi walipowasili mapema leo asubuhi kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Mbozi.Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko ziarani mkoani Mbeya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM,kusikiliza kero za Wananchi na namna ya kuzipatia ufumbuzi,
  Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Mbozi mapema leo asubuhi,ndani ya ofisi za CCM Wilaya ya Mbozi,mkoani Mbeya.
  Pichani kulia ni Mkuu wa MKoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandoro akisalimiana na Katibu wa NEC,Siasa  na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.Rose Migiro akiwa sambamba na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,mara baada ya kuwasili mapema leo asubuhi kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya..Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko ziarani mkoani humo kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM,kusikiliza kero za Wananchi na namna ya kuzipatia ufumbuzi,
  Pichani ni baadhi ya Wanachama wa CCM na Wananchi wakiupokea ujumbe wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana walipowasili mapema leo asubuhi kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Mbozi.Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko ziarani mkoani Mbeya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM,kusikiliza kero za Wananchi na namna ya kuzipatia ufumbuzi,

  0 0

  MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili nchini Kenya, Anastazia Mukabwa, aliyethibitisha kuwa miongoni mwa watakaotumbuiza katika Tamasha la Krismasi litakalorindima Dar es Salaam Desemba 25 mwaka huu, pia katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki.

  Tamasha hilo la Krismasi limepangwa kusheheni waimbaji kochokocho wa nyimbo za Injili, miongoni mwao akiwamo mwimbaji huyo galacha wa nyimbo za Injili, Mukabwa.

  Mukabwa anatoa mwito kwa watu kujitokeza kwa wingi ili 'wavue viatu' siku hiyo aliyopania kukonga nyoyo za mashabiki atakapopanda jukwaani katika tamasha hilo. Kulingana na taarifa yake iliyotolewa na waandaaji wa tamasha hilo, msanii huyo amepanga kuwapa mashabiki raha na kuwataka wake mkao wa kula wakisubiri vitu vyake.

  “Nimejipanga, najua mashabiki wa Tanzania wanataka kitu gani, nitawapa raha, mambo ya Kuvua Viatu watayasikia na mengine, watafurahi sana. “Kwa vile Rose (Muhando) atakuwepo, nitashirikiana kwenye wimbo huo na nyimbo zangu mpya nitazitoa huko kwa mara ya kwanza, ni mambo mazuri yatakuwepo,” alitamba.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama alisema Mukabwa aliyeimba kwa kumshirikisha mwimbaji nguli wa Tanzania, Rose Muhando katika wimbo wa Vua Kiatu, ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki.

  0 0

  WAZIRI wa Viwanda na Biashara,ambaye pia ndio mbunge wa Handeni, Dkt Abdallah Kigoda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Utamaduni, lililopangwa kufanyika Katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni mkoani Tanga, Desemba 14 mwaka huu.

  Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani hapa, huku likitarajiwa kuwa la aina yake kutokana na maandalizi yanayoendelea kushika kasi, ambapo kwenye uwanja huo, Tamasha hilo litaanza saa 2 asubuhi hadi saa 12 za jioni.

  Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema maandalizi yamezidi kushika kasi kwa kuangalia mazoezi ya vikundi kadhaa vitakavyotoa burudani katika tukio hilo.

  “Tunashukuru Mungu kuona mambo yanazidi kuwa mazuri kwa kuhakikisha kuwa Desemba 14 mwaka huu tunafanya tamasha lenye mguso na kila mmoja wetu kufaidishwa.

  “Huu ni wakati wa kila mtu kujipanga ili aje kushiriki kwa namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa juhudi hizi zote zipo kwa ajili ya kujenga ushirikiano kwa watu wote,” alisema Mbwana.

  Wadhamini katika tamasha hilo ni pamoja na gazeti la Mwananchi, Clouds Media Group, niPhed Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog, Pamoja Pure Blog na Taifa Letu.com.

  0 0

  TAHADHARI:- KUNA TAPELI MWENYE ASILI YA KIZUNGU ANADAI YEYE NI RAIA WA AFRICA KUSINI MREFU ANAONEKANA SANA MITAA YA KINONDONI MANYANYA MIDA YA USIKU AMETAPELI WATU WENGI SANA AKIDAI KUA AMEIBIWA HOTELINI NA MWANAMKE NA ANADAI ANAISHI MBEZI KIMARA KWA WENYEJI WENGI WA KINONDONI WANAMFAHAMU NA WENGI WAMESHAMSIKIA NA WANADAI NI MSWAHILI CHUKUENI TAHADHARI NA TUKO KWENYE HARAKATI ZA KUMKAMATA KWASABABU AMESHA TAPELI WENGI AKIJIFANYA KUCHUKUA NAMBA ZA SIMU KWA AJILI YA KUREJESHA FEDHA HIZO TUNAOMBA WENYE TARIFAA ZAIDI WATUSAIDIE KWA USHIRIKIANO NA POLISI KUMTIA MBARONI IMETOLEWA NA MMOJA YA WALIOLIZWA

  0 0

  5-1Waziri Mkuu Mstaafu, Salim Ahmed Salim,akiwaongoza mawaziri wenzake wastaafu, kuweka mashada ya maua.

older | 1 | .... | 175 | 176 | (Page 177) | 178 | 179 | .... | 1897 | newer