Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

kumekucha kitchen party gala


Nafasi za Kazi Mtwara

$
0
0
Adexec Oil & Gas Company ni kampuni ya wachina ambayo inajishughulisha na masuala ya uchimbaji Mafuta na Gas,kwa sasa kampuni ipo Mtwara kwa shughuli za uchimbai Mafuta na Gas,Kampuni inapenda kuwatangazi watanzania wenye sifa nafazi za kazi zifatazo,

Administrative Assstants  3

QualificationS
-Diploma in Business administration or above
-Knowledge of MS word,Excel and Internet
-No experince required

IT Officers  2

Qualifications
-Diploma in IT or above
-No experience  required


Cashiers   3

Qualifications
-Diploma in Accounting/Atec II or above
-Knowledge of MS word,Excel and Internet
-No experience required


Tafadhali tuma CV yako ukiambatanisha na namba yako ya simu kwenye anwani hapa chini au kwa email kabla ya tarehe 29/11/2013

Adexec Oil & Gas Company

S.L.P 234
Mtwara


NBC YAIMWAGIA TAYOA MSAADA WA SHS MILIONI 100

$
0
0
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Mizinga Melu kusaidia mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA). Hafla ilifanyika wakati wa tukio la uzinduzi wa mradi huo unaodhaminiwa na NBC jijini Dar es Salaam jana. Katikani ni Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Mizinga Melu (katikati) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bi. Mwinda Kiula Mfugale wakionyesha vipeperushi kuashiria uzinduzi wa tofuti ya vijanatz.com ikiwa na habari kuhusu ajira (kazitz.com), fedha (fedhatz.com) na ujasiriamali (biasharatz.com). Hafla hiyo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana  wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA) unaodhaminiwa na NBC.
3: Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu akishikana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika baada ya kukabidhi  mfano wa hundi ya shs milioni 100 zilitotolewa na benki hiyo kusaidia mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA). Hafla ilifanyika wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo unaodhaminiwa na NBC. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maendeleo aya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula Mfugale.
 Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika (kushoto), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), na Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa NBC, William Kallaghe wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika (kushoto), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), na Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa NBC, William Kallaghe wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu akizungumza na vijana na wageni wengine kuhusu huduma za kibenki na kuhusu mikakati ya benki kusaidia suala la ajira na ujasiriamali kwa vijana katika hafla hiyo.
Wasanii wakitoa burudani kusindikiza uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA) unaodhaminiwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jijini Dar es Salaam

MWANAFUNZI MTANZANIA ALIYEFARIKI NAIROBI AZIKWA

$
0
0
NN0909JerryMruma
Jerry Mruma alikuwa mwanafunzi wa uzamili katika chuo kikuu cha kimataifa cha USIU Nairobi alikutwa alhamisi iliyopita katika chumba cha maiti mjini Nairobi baada ya kuripotiwa kupotea tangu Jumamosi iliyopita . Jerry alikuwa mmiliki wa kampuni ya Kilimo yetu akiuza hisa za Kilimo kijana huyu mtanashati na mwenye akili ya biashara alikuwa akisoma wakati huo huo akifanya biashara hii iliyopata umaarufu sana huko nchini Kenya. 

Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi na kamera za CCTV ni kwamba Jerry alionekana hai mara ya mwisho saa tano na dakika tisa usiku alipokuwa akitoka kwenye hafla ya usiku wa Mtanzania aliyokuwa ameandaa katika hoteli ya Sarova. Aliondoka hotelini hapo kwa miguu akiwa peke yake na kwa mujibu wa Chuo hicho alituma ujumbe wa mwisho kwa rafiki yake wa kike mnamo saa 5 na dakika 38 za usiku akimwambia ametoka kwenye hafla hiyo na anaelekea nyumbani kwake.

Jerry aliwahi kufanya mazungumzo na Sauti ya Amerika juu ya kampuni yake Kilimo yetu nchini humo. Jerry amezikwa Jumanne katika makaburi ya Kinondoni mjini Daressalaam. Chuo cha USIU kimeamua kuanzisha mfuko wa kusomesha wanafunzi kwa jina lake. Uchunguzi wa awali unaeleza kuwa kijana huyu alipata majeraha ya kichwa na mpaka sasa Polisi wa Kenya wanasema bado wanafanya uchunguzi. Wanafunzi na wakazi wengi wa jiji la Daressalaam na Nairobi walijitokeza kumzika mwenzao, msiba ambao umeacha majonzi makubwa na simanzi katika familia na kuangalia mazungumzo yake huko Nairobi na GBSTV bofya hapa.

TAKUKURU KWA KUSHIRIKIANA WADAU WA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA WAANDAA TAMASHA JIJINI ARUSHA

$
0
0
DSC_0043
Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd. Chedi Ngulu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya ushauri wa Umoja wa Afrika ya kupambana na Rushwa yaani African Union Advisory Board on Corruption (AUABC) na Tamasha la wasanii lenye lengo la kufikisha ujumbe juu ya Madhara ya Rushwa kwenye Jamii, Kati kati ni Emmanuel Atenga toka (AUABC) na Stephane Ndilimbaye toka AUABC.

Na Ripota wetu

TAASISI YA KUPAMBANA NA KUZUIA RUSHWA (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC) na Megamark Ltd wameandaa tamasha kubwa litakalowashirikisha wasanii mbali mbali toka Tanzania, Kenya na Uganda katika kuadhimisha miaka 10 tangu bodi hiyo ya Afrika katika maswala ya Rushwa kuanzishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark ltd, Chedi Ngulu amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kufikisha ujumbe kwa umma juu ya kupambana na Rushwa na kuelezea madhara ya Rushwa kwenye jamii na nchi kwa ujumla.
DSC_0063DSC_0075
Bw. Emmanuel Atenga (wa pili kushoto) kutoka na Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC) akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tamasha hilo litakalofanyika tarehe 7 mwezi ujao katika viwanja vya General Tyre Arusha. Kulia ni mmoja wa wasanii wataoimba kwenye Tamasha hilo Fid Q na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd. Chedi Ngulu na kushoto ni Stephane Ndilimbaye kutoka AUABC.

“Muziki upo katika asili ya waafrika na umekuwa ukitumika kuburudisha lakini zaidi kufikisha ujumbe wenye kujenga na kurekebisha jamii (Hadhira) iwe ni nyimbo, kughani ambayo tunatambua kwa njia ya Rap na ngoma za asili, lakini tumechagua muziki kama njia rahisi ya kufikisha ujumbe hasa kwa vijana kuhusu madhara ya Rushwa,” amesema Ngulu.

Amesema kuwa katika tamasha hilo nyimbo mbalimbali zitaimbwa katika kuelezea matatizo ya Rushwa kwenye jamii na hasa kuelimisha vijana umuhimu wa kukataa Rushwa kwa sababu vijana ndio nguvu kazi ya taifa na asilimia 75 ya watu nchini ni vijana.
“kwa mantiki hii, tumeandaa onyesho lenye anuani isemayo “Rushwa sio” ikimaanisha rushwa haina manufaa na ni yenye kutakiwa kupigwa vita kwa gharama yoyote ile,”
DSC_0095
Msanii Fid Q akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo.
“Onyesho hili litafanyika Arusha tarehe 7 mwezi wa kumi na mbili katika viwanja vya General Tyre kuanzia saa saba na nusu mpaka saa kumi na mbili jioni na litahusisha wasanii wenye kukubalika na jamii,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Emmanuel Atenga toka Kitengo cha Mawasiliano (AUABC) amesema Board hiyo ya Umoja wa Afrika ya kupambana na rushwa imepata mafanikio kwa kuanzisha vitengo vya ufatiliaji kwa wanachama wa Umoja wa Afrika wenye lengo la kusaidiana katika mapambano dhidi ya Rushwa. Amesema mapambano dhidi ya rushwa Afrika yanahitaji nguvu ya pamoja kwa ksuhirikisha jamii wakiwemo wasanii katika kuhamasisha mapambano ya kukataa Rushwa kwenye ngazi zote ndani ya nchi na bara zima la Afrika.
DSC_0036
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
DSC_0039
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
DSC_0059

WAZIRI NCHIMBI AZINDUA MPANGOKAZI WA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO

$
0
0

UZINDUZI WA DAWATI LA JINSIA PAMOJA NA MPANGOKAZI WA MIAKA MITATU UNAOONESHA MAJUKUMU YA JESHI LA POLISI KATIKA KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi, amezindua rasmi mpangokazi wa dawati la jinsia na watoto wa jeshi la polisi kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2013 hadi 2016, kwa ajili ya kushughulikia makosa yanayohusu ukatili wa Kijinsia na Watoto. Waziri Nchimbi pia amezindua dawati la jinsia katika kituo cha polisi chang’ombe - Temeke jijini Dar es salaam. Leo ni siku ya pili  kati ya mfululizo wa siku 16 za kupinga ukatili na unyanyasaji dhidi ya Mwanamke na Msichana, zilizoanza Jumatatu, Novemba 25 mwaka huu.

Uzinduzi wa Mpangokazi huo pamoja na Dawati , unaelezea majukumu ya jeshi la polisi katika mapambano dhidi ya vitendo   vya ukatili wa kijinsia pamoja na unyanysaji wa Watoto.   

Matukio ya ukatili wa kijinsia kwa hapa nchini yamekuwa ni mengi sana,kwa mwaka 2010, taasisi  ya utafiti ya Tanzania Health Survey ilitoa makadirio yaliyobainisha kuwa asilimia 45 ya  wanawake na wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15-49, wameripoti kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika maisha yao. Utafiti kuhusu vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia uliozinduliwa na wizara ya maendeleo ya jamii  jinsia na watoto mwaka 2011, ulionesha kwamba karibu mtoto mmoja  wa kike  kati ya watatu na mtoto wa kiume mmoja kati ya saba anakuwa ameshawahi kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia, na zaidi ya 70% ya watoto wa kike na wa kiume wamekumbana na vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa na umri wa kabla ya miaka 17. Ingawa wengi wao hawasemi na matukio yaliyo mengi hayajawahi kuripotiwa katika vituo vya polisi. 

“Jeshi la polisi Tanzania  limejipanga vema katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia  na unyanyasaji wa watoto , jeshi linawahakikishia wote kuwa kila kituo cha polisi kitakuwa ni sehemu salama kwa waathirika wa vitendo hivi,” alisema Inspekta Jenerali wa Polisi, Bw Said  Mwema.

Kutokana na jukumu la Polisi kushughulikia makosa ya ukatili wa kijinsia na Watoto, kila kituo cha polisi wapo askari waliopewa mafunzo maalumu ya jinsi ya kuwahudumia wahanga wa vitendo hivi kwa usiri na faragha  ili kuwafanya watendewa kujisikia huru na salama wanapo toa taarifa/malalamiko yao. 

“Mume wangu alikiri kuninyanyasa na kuahidi kuacha manyanyaso hayo. Sasa tunaishi maisha ya furaha, amani  na upendo na ameacha vitendo hivyo na anaendelea kuwalipia watoto wetu karo za shule. Kama mnavyoniona sasa nimependeza kwa kweli,” alisema Mwanahawa.

Mfano mmoja wapo wa kesi ya unyanyasaji wa kijinsia iliyoripotiwa katika dawati la jinsia na watoto Chang’ombe na kushughulikiwa na wataalam wa dawati hilo ni  wa bi. Mwanahawa mama wa watoto wawili  kutoka Temeke ambaye alikuwa ameolewa kwa miaka 12. Mama huyu alikuwa akinyanyaswa na mumewe ambaye aliacha kuihudumia familia hiyo ikiwa ni pamoja na kukataa kuwasomesha watoto wake ambao walilazimika kuacha shule. 

Baada ya kuishi katika hali hiyo ya manyanyaso kwa takribani miaka mitano, hatimaye aliamua kuomba ushauri kutoka kwa rafiki zake na mmoja wapo alimshauri kwenda kutoa ripoti katika kituo cha polisi chang’ombe kupitia dawati la jinsia na watoto. Hatimaye mume wake aliitwa na waliweza kusuluhishwa na wanaendelea vizuri na maisha yao ya ndoa. 

Malengo  ya jeshi la polisi ni kuhakikisha kuwa katika kila kituo cha polisi Tanzania kunatolewa  huduma hizi za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto kwa ubora wa hali ya juu kabisa. 

Umoja wa Mataifa Tanzania kupitia UNICEF kama mratibu wa “Kikundi cha uratibu na polisi dhidi ya ukatili wa kijinsia“, UNFPA na UN WOMEN wanaungana na jeshi la polisi kwa kuunga mkono jitahada hizi za mapambano dhidi ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na Watoto.

“Ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Sisi sote tunao wajibu wa kuhakikisha kuwa tunatokomeza vitendo hivi. Umoja wa Mataifa(UN) unalipongeza jeshi la polisi kwa hatua walizozichukua kwa mapambano dhidi ya vitendo hivi na kuhakikisha kuwa kunakuwa na madawati ya jinsia na watoto yaliyo kamili katika vituo vyote vya polisi nchini, Umoja wa Mataifa tunajivunia kulisaidia jeshi la polisi katika kutimiza malengo haya”. Alisema Bw.  Alberic Kacou mratibu mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.

Mpangokazi wa dawati la jinsia na watoto kwa mwaka 2013-2016 umeandaliwa ili kusaidia jitihada za mapambano ya ukatili wa kijinsia na manyanyaso  ya watoto na umeainisha malengo makuu ambayo jeshi la polisi limelenga kuyafikia ndani ya miaka mitatu ijayo.

Jeshi la polisi haliwezi kufikia malengo hayo peke yake hivyo basi Kikundi cha uratibu na ushirika na polisi dhidi ya ukatili wa kijinsia na manyanyaso kwa watoto, chini ya uenyekiti wa jeshi la polisi,  washirika toka mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs, na wizara husika, idara na wakala mbalimbali, wana wajibu wa kushirikiana na jeshi la polisi katika utekelezaji wa mpangokazi huu ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na manyanyaso ya kijinsia na watoto.

Edna Kiplagat: Nakuja Uhuru Marathon

$
0
0
BINGWA wa dunia wa mbio za marathon, Edna Ngeringwony Kiplagat wa Kenya amejitokeza kushiriki zile mbio za Uhuru Marathon zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar ers Salaam Desemba 8, mwaka huu.
 
Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck ndiye aliyethibitisha hilo na kusema, wamefarijika kwa kiasi kikubwa kwa Edna mwenye sifa lukuki katika mbio za marathon kujitokeza kushiriki.
 
“Kwetu tumefarijika mno kutokana na ushiriki wa Edna, kwani ni mwanariadha wa kimataifa mwenye rekodi nyingi za kuvutia na hasa hii ya ubingwa wa dunia kwa upande wa wanawake,” alisema.
 
Edna,34, alitwaa ubingwa wa dunia kwa upande wa marathon mwaka 2011 katika mashindano yaliyofanyika Daegu, Korea Kusini na akafanya hivyo tena mwaka huu katika mashindano ya dunia yaliyofanyika Moscow, Urusi.
 
Pia alishinda katika mbio za Los Angeles Marathon na New York Marathon zilizofanyika mwaka 2010 na muda bora zaidi kupata kuuweka katika mbio hizo ni wa saa 2:19:50 katika mbio za London Marathon mwaka jana.
Pia ametwaa medali mbalimbali katika mashindano ya vijana wakati anaanza kukimbia mwaka 1996, pale alipoonyesha uwezo wake katika mashindano ya dunia kwa vijana.
 
Edna ni nani?
Edna Ngeringwony Kiplagat alizaliwa Septemba 15, 1979 na ni mkimbiaji wa mbio ndefu mwenye jina kubwa duniani, hasa baada ya kufanikiwa kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya dunia yaliyofanyika Daegu mwaka 2011 na Moscow mwaka huu.
 
Alianza kujitengenezea jina pale alipofanya vyema katika mashindano ya Los Angeles na New York City Marathons mwaka 2010.
 
Katika mbio za mita 3000, Kiplagat pia alishawahi kufanya kweli kwa kushinda medali ya shaba katika Mashindano ya Dunia ya Vijana yaliyofanyika mwaka 1996 na kufanya hivyo mwaka 1998 kwa kutwaa medali ya fedha.
 
Rekodi yake bora zaidi ya kukimbia katika mita 3000 ni muda wa dakika 8:53.06 ambayo aliiweka mwaka 1996 katika mashindano hayo ya dunia kwa vijana wakati huo akiwa na miaka 16 tu.
 
Katika Mbio za Nyika za Dunia zilizofanyika mwaka 2006, Kiplagat alimaliza katika nafasi ya 13 na akaja kuweka muda mzuri wa mita 5000 mwaka huo wa dakika 15:57.3 katika mashindano yaliyofanyika Nairobi na baadaye katika nusu marathon akaweka muda wa saa 1:09:32.
 
Juni 2007 alikimbia mbio za mita 10,000 kwa muda wa dakika 33:27.0 mashindano yaliyofanyika Nairobi, ambapo pia mwaka 2006 alishinda mashindano ya Virginia Beach Rock 'n' Roll Half Marathon, huku 2007 akishinda yale ya Lilac Bloomsday Run na Bay to Breakers yaliyofanyika San Francisco.
 
Kiplagat alishinda mashindano ya Los Angeles Marathon mwaka 2010 na baadaye akaenda kufanya kweli New York City Marathon na mara mbili aliwashinda wapinzani wake wakubwa Shalane Flanagan wa Marekani na Mary Keitany wa Kenya, ambapo wapinzani wake hao walishika nafasi ya pili na tatu.
 
Katika mashindano ya riadha ya dunia ya mwaka 2011, Kiplagat ‘alipiga’ muda wa saa 2:28:43 lakini ilikuwa ngumu kwake kwani ikiwa bado kilomita 5 alionekana kushindwa, lakini mshirika mwenzake Sharon Cherop aliamua kusimama na kumsaidia kuhakikisha anamaliza mbio hizo.
 
Kiplagat, Cherop na Priscah Jeptoo walifanikiwa kutwaa medali zote tatu za juu na kuifanya Kenya kuwa taifa la kwanza kutwaa medali tatu katika mashindano makubwa kama hayo. Baadaye alishiriki Montferland Run huku akiwa na maumivu lakini akamaliza wa pili nyuma ya Abebech Afework.
 
Mwanariadha huyu anafundishwa na mumewe Gilbert Koech, kitu kinachodaiwa kumfanya kuwa bora zaidi kila siku.
 
Uhuru Marathon
Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema wamefurahishwa na ujio wa mwanariadha huyo na kusema wazo kubwa la kuanzisha mbio hizo ilikuwa ni kutaka kuwakumbusha Watanzania kuuenzi umoja, amani, mshikamano ulipo pamoja na uhuru wetu.
 
“Sisi kama vijana tukaona kuna haja ya kufanya kitu cha kuwakumbusha Watanzania wenzetu kwani tunatakiwa kudumisha urithi wa amani, mshikamano na uhuru wetu tulioachiwa na mababu zetu,” alisema.
 
Melleck alisema mbali na mbio hizo kufanyika siku hiyo, pia kutakuwa na tamasha kubwa la burudani litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam ikiwa ni mkesha wa kusubiri siku ya Uhuru.
 
Melleck, anasema lengo la mbio hizo ni kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa kukumbuka, kuzingatia na kuuenzi urithi waliaochiwa na viongozi waliopigania uhuru wa nchi.
 
Anasema, urithi huo ambao utakuwa ukikumbukwa kila mwaka kupitia mbio hizo, ni upendo, mshikamano, umoja na amani iliyopo.
 
Mratibu huyo anasema, ana imani mbio hizo zitajizolea umaarufu mkubwa, kutokana na jinsi zitakavyoteka hisia za watu mbalimbali, wakiwemo wanamichezo.
 
Katika mbio hizo, zitakazowashirikisha watu wa kada mbalimbali, zitakuwepo pia mbio za kilomita 3, kilomita 5, Half Marathon kilomita 21 pamoja na Full Marathon yenyewe kilomita 42.
 
Mratibu huyo anasema mbio za kilomita 3 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi wa kada mbalimbali, wakiwemo pia wale wa dini na zile za kilomita 5 pia zitakuwa za kuchangia kwa ajili ya watu wa mahitaji ya aina mbalimbali.
 
Tusubiri kuona ushindani halisi kutoka kwa bingwa kama Edna Kiplagat katika Uhuru Marathon.
 
WASIFU
Jina: Edna Kiplagat
Kuzaliwa: Novemba 15, 1979
Nchi: Kenya
Urefu: Futi 5 inchi 4
Uzito: Kilo 50
Mchezo: Riadha -MarathonAthletics
Rekodi:    Dhahabu -2011 Daegu Marathon
Dhahabu- 2013 Moscow Marathon
Mashindano ya Vijana
Shaba- 1996 Sydney mita 3000
Fedha- 1998 Annecy mita3000

WASHINDI WA DROO NDOGO YA CHAMPIONI 'SHINDA MAHELA' WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO LEO

$
0
0
Clement Michael (kulia) ambaye ni mkazi wa Mbagala-Zakhem, Dar, akikabidhiwa Sofa Set yake na Mr Championi.
Clement akichekelea baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya Sofa Set leo nje ya ofisi za Global Publishers zilizopo Mwenge, Bamaga jijini Dar.
Bashir Hassan (kushoto) mshindi wa friji akikabidhiwa zawadi yake na Mr Championi nje ya ofisi za Global Publishers.
Radephili Mcharo (kushoto) akikabidhiwa jezi yake na Mr Championi.
WASHINDI wa Droo Ndogo ya Promosheni ya Shinda Mahela na Championi iliyochezwa juzi, leo wamekabidhiwa zawadi zao nje ya ofisi za kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd wachapishaji wa magazeti ya Championi, Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa washindi waliofika kuchukua zawadi zao ni Clement Michael mshindi wa Sofa Set, Bashir Hassan aliyejishindia Friji na Radephili Mcharo aliyejinyakulia Jezi.
(PICHA NA ISSA MNALLY / GPL)

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WATOA ELIMU YA KUPAMBANA NA UKATILI NA UNYANYASAJI KWA WATOTO WILAYANI MAKETE

$
0
0
 Miongoni mwa vitendo vinavyoshamiri Makete vya watoto kujihusisha na biashara ya kuuza mkaa
 Hapa watoto hao wakiandaa mkaa kwa ajili ya kuuza kwa wateja wao
 Mkaa ukisubiri wateja.
------- 

Mafunzo ya ulinzi na usalama wa mtoto dhidi ya ukatili na unyanyasaji yaliyoanza jana wilayani Makete mkoani Njombe yanaendelea katika ukumbi wa Sumasesu Tandala

Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Makete Bw. Leonce Panga yameshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, dawati la jinsia kutoka kituo cha polisi Makete, maafisa elimu, mwanasheria, magereza, wauguzi, madaktari pamoja na hakimu mfawidhi wa wilaya ya Makete

Katika mafunzo hayo yanayowezeshwa na Bi Asha Mbaruku pamoja na Ramadhani Yahaya kutoka  ustawi wa jamii makao makuu jijini Dar es Salaam wamesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau hao namna ya kuwahudumia watoto wanaokuwa wamefika kwenye ofisi zao kupata msaada endapo anakuwa amepata tatizo akitolea mfano kufukuzwa shule kwa kukosa ada

Wamesema washiriki hao wanapaswa kuwa timu ya ulinzi na usalama wa mtoto ili waweze kumsaidia mtoto, huku Bi Asha akisisitiza kuwa kuna huduma ya msaada kwa watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili iliyoanzishwa wizarani inayoitwa huduma mtandao (Child helpline) inayohusu mtoto kupiga simu moja kwa moja na kueleza shida yake na kupatiwa suluhu

Washiriki pia wamefundishwa njia mbalimbali za ufundishaji wa masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto kwa ngazi ya chini ya serikali

Kwa upande wao washiriki wametoa visa mbalimbali vinavyoendelea katika jamii ya Makete ikiwemo kata ya Mbalatse ambayo watoto wa kike wanafanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa siri kubwa

Mafunzo hayo yameweka wazi hatua zinazochukuliwa na serikali kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo kutunga na kusimamia sheria mbalimbali zinazomlinda mtoto

Mafunzo hayo ya siku 5 yaliyoanza jana yameandaliwa na ustawi wa jamii makao makuu jijini Dar es Salaam na yanatarajiwa kuhitimishwa Jumamosi wiki hii

Na Edwin Moshi

Solly Mahlangu kutumbuiza Tamasha la Krismas

$
0
0
Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama, akimtangaza mwimbaji kinara wa Tamasha la Krismasi 2013 kutoka Afrika Kusini, Pastor Solly Mahlangu “Obrigado” ambaye ataimba na kundi lake uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Desemba 25.

=====  =====  ====
WAKATI Tamasha la Krismas likikaribia, muimbaji nguli wa muziki wa Injili wa Afrika Kusini, Solly Mahlangu ‘Obrigado’ni mmoja wa waimbaji ambaye anatarajia kuimba kwenye tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.



Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama mwimbaji huyo ataimba live siku hiyo pamoja na waimbaji wake wengine 14.Msama alisema mwimbaji huyo anatarajia kushiriki katika tamasha hilo jijini Dar es Salaam, tamasha ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Morogoro (26), Tanga (28), Arush(29) na Dodoma (1). 



Aidha Msama alisema bado wanaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine yameshakamilika kwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja, Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia), Liliane Kabaganza (Rwanda). Waimbaji wa Tanzania ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, New Life Band na John Lissu.

kumekucha Fainali za EBSS 2013

$
0
0
Katika kuelekea Fainali ya EBSS 2013 kesho kutakuwa na Press Conference pale katika ufukwe wa ESCAPE ONE  Saa Tano Asubuhi, ambapo utawaona washiriki wote walioingia Fainali kwa pamoja kabla ya siku yenyewe ya Jumamosi tarehe 30 ambapo wote kwa pamoja tutashuhudia Yule Mshindi wa Milioni 50.

Waliofanikiwa kuingia fainali ni Amina Chibaba (MBEYA), Melisa John (DSM), Elizabeth Mwakijambile (DSM), Emannuel Msuya (MWANZA) na Maina Thadei (DSM)

Pia siku ya Fainali kutakuwa na Burudani kutoka kwa Snura, Barnaba, Young Killer, Shaa, Walter Chilambo, Peter Msechu  na Makomandoo

Kiingilio katika Fainali hizo kitakuwa : VIP TSH 50,000/= KAWAIDA  : TSH 20,000/=

Tiketi  za siku ya Fainali zinapatikana sehemu zifuatazo :
-          Shear illusion
-          Biggy Respect (Kariakoo)
-          Steers Mjini
-          Zizzoue Fashion (Victoria na Sinza)
-          Photo Point (Mayfair)
-          Robby One Fashion (Kinondoni)
-          Best Bite
-          Engen Mbezi
-          Escape One (Mikocheni)
-          Benchmark Office Mikocheni
-          American Nails (Kinondoni)

Gazeti la Mwananchi wajitokeza kudhamini Tamasha la Handeni

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Handeni

KAMPUNI ya Mwananchi Communication Ltd (MCL), imejitokeza kudhamini Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni mkoani Tanga, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 katika Uwanja wa Azimio Handeni Mjini na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Tamasha hilo linalojulikana pia kwa jina la Handeni Kwetu linafanyika kwa mara ya kwanza likiwa na shauku ya kutangaza utamaduni na fursa nyingine za kimaendeleo wilayani humo, kama sera ya kuwapatia maendeleo.

Akizungumza jana mjini hapa, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema wamekubaliana na wenzao Mwananchi kwa ajili ya kuwezesha tamasha hilo. Alisema kitendo cha Mwananchi kuingia katika tamasha hilo ni kuonyesha ushirikiano mkubwa waliokuwa nao katika jamii ya Kitanzania.

“Wakati naandaa tamasha hili sehemu mbalimbali niliweza kuingia kwa ajili ya kusaidiana na wadau juu ya Tamasha la Handeni linalofanyika kwa mara ya kwanza, huku likijiweka katika nafasi nzuri mno.

Tunashukuru kwa wale walioguswa na kujitokeza kwa namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa Kampuni kama Mwananchi kuingia ni cha kuungwa mkono na Watanzania wote kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mambo yanakuwa mazuri,” alisema Mbwana.

Kuelekea kwa tamasha hilo, vikundi mbambali vimeonyesha kuliunga mkono tamasha hilo litakalowaunganisha Watanzania wote, hususan wakazi wa wilaya ya Handeni, mkoani Tanga na Tanzania kwa ujumla.

Wadhamini wengine ni Phed Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com, huku likipangwa kuanza saa 2 za asubuhi hadi saa 12 za jioni.

GEPF yaendelea kuboresha huduma kwa watanzania.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa GEPF  Bw.Daudi Msangi akifafanua kuhusu fursa inayotolewa na Mfuko huo kwa raia wa Kigeni wanaoishi na kufanya kazi Nchini ambapo wanaweza kujiwekea akiba katika mfuko huo,kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi. Fatma Salum.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa GEPF  bw.Daudi Msangi akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijijini Dar es Salaam kuhusu mfumo mpya unaowawezesha wananchi wasio katika sekta rasmi kujiunga na mfuko huo na kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo,kushoto ni Meneja Masoko na Huduma wa Mfuko huo bw.Aloyce Ntukamazina.(Picha na Frank Mvungi)


Na Fatma Salum-Maelezo.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii GEPF umetoa fursa kwa wananchi walio katika Sekta  isiyo rasmi kujiunga na mfuko huo ili kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Bw.Daudi Msangi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maboresho yanayofanywa na mfuko huo ili kuwanufaisha wanachama wake.

Bw. Msangi alibainisha kuwa  wanachama wanaojiunga na mfuko huo toka sekta  isiyo rasmi wanao uhuru wa kuamua ni kiasi gani watachangia katika mfuko kulingana na vipato vyao ili kujiwekea  akiba .

Aidha alisema  mfuko huo utaanza kutoa pensheni kwa wanachama wa hiari watakaochangia kwa muda usiopungua miaka kumi na tano. Akifafanua zaidi Bw Msangi alisema mfuko huo umepanua wigo kwa kuwapa nafasi raia wa kigeni kujiunga na mfuko ili wajiwekee akiba katika kipindi watakachokuwa wakifanya kazi hapa nchini.

Aliongeza kuwa Mfuko huo pia umetoa fursa kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi kujiunga na mfuko na kujiwekea akiba kwa faida ya maisha yao ya baadae hasa wanapostaafu na pia kuwapa uwezo wa kuendesha maisha yao watakaporudi nchini.


Bw.Msangi alitaja baadhi ya mafao yanayotolewa na mfuko huo kuwa ni mafao ya warithi,mafao ya kuumia kazini, fao la elimu na msaada wa mazishi na kuongeza kuwa kwa sasa thamani ya mfuko huo ni shilingi bilioni 210 na inatarajiwa ifikapo mwakani thamani itaongezeka hadi shilingi bilioni 250.

Rais Kikwete akagua na kuzindua miradi Mkoa Mpya wa Simiyu

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(watatu kushoto),Mbunge wa Bariadi  Mhe. Andrew Chenge(kushoto)pamoja na viongozi wengine w akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi wa Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 huko enelo la Old Maswa mkoa mpya wa Simiyu leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Old Maswa muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya kilometa ya Bariadi-Lamadi 71.8 huko eneo la old Maswa, Mkoani Simiyu.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(pembeni ya Rais kulia) pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Barbara ya Bariadi Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 huko eneo la Old Maswa leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bwana Saguda Kasili mlemavu ambaye pia ni mtendaji wa kijiji cha Ng’wang’wali leo wakati aliposimama kijijini hapo kuwasalimia wananchi wa eneo hilo
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Umeme katika kijiji cha Nkololo wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu leo.Weninge katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh. Steven Masele, Mbunge wa Bariadi Mhe.Andrew Chenge(wapili kushoto),Paroko wa Nkololo Padri Paulo Fegan(wanne kushoto) na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti.





 Msanii wa kundi la sanaa kutoka Bariadi akicheza na nyoka aina ya Chatu wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi –Lamadi leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Barabara ya Bariadi Lamadi leo.

WANANCHI WA WILAYA YA ILEJE WAIKATAA MBOLEA YA MINJINGU,WAITAKA SERIKALI IINGILIE KATI KUTATUA TATIZO HILO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmna Kinana akishiriki ujenzi wa msingi ya wodi y a wazazi ya kituo cha afya kata ya Lubanda wilayani Ileje.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akishirikiana na wananchi wa kata ya Lubanda kujenga msingi wa wodi ya akina mama katika kituo cha afya cha kata hiyo wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwa nyumbani kwa Balozi wa Shina namba 1 Balozi Nosadi Edward (mwenye fulana kulia),Katibu Mkuu amekuwa na utamaduni wa kutembelea mabalozi katika ziara zake .
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akisalimiana na wakazi wa shina namba 1 kata ya Sange ,wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
Mmoja wa wasanii wa kundi la ngoma ya Ibandi ,ngoma maarufu ya kabila la Wandari akipiga filimbi wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake ambao walitembelea kata ya Kalembo ,wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
Wasanii wa ngoma wakicheza ngoma ya Ibandi ngoma maarufu ya kabila la Wandari wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu  Abdulrahman Kinana Ujumbe wake ambao walitembelea kata ya Kalembo ,wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
 Diwani wa Kata ya Isongole Ndugu Gwalusako Kapesa akielezea namna gani wananchi wa wilaya ya Ileje walivyochoshwa na taratibu za serikali za kuwalazimisha kununua mbolea za ruzuku za Minjingu, kwani zimekuwa hazina faida kwao kama wakulima na zimewaletea hasara kubwa sana, wananchi hao wameiomba serikali na viongozi wake kuwasikiliza zaidi wao katika kutatua kero zao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Kalembo na kuwaambia kilio cha wakulima kinafanana karibia nchi nzima hasa kuhusu matatizo ya mbolea na kusema CCM itachukua hatua kwa kukutana na waziri husika kwenye kamati kuu itakayofanyika mapema mwezi ujao.
 Wananchi wa Kata ya Kalembo wakiwa wamejifunika miamvuli kujikinga na mvua wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake ambao upo ziarani mkoani Mbeya.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za kumbukumbu za kifo cha marehemu Steven Kibona kwa wananchi wa kata ya Kalembo, kushoto ni mjane wa marehemu Mama Kibona.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje Ndugu Rosemary Sinyamule kwenye daraja la mto Songwe mpakani mwa Tanzania na Malawi,Mkuu wa Wilaya alimueleza Katibu Mkuu kuwa eneo hilo lina fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi kama barabara ya lami  itajengwa na ikiwa pamoja na ofisi za kudumu za uhamiaji zitajengwa katika kata ya Isongole.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro wakizungumza na wananchi wa kata ya Isongole wilaya ya Ileje mpakani mwa Tanzania na Malawi.
 Katibu Mkuu wa CCM akiwa nje ya ofisi ya uhamiaji ya kata ya Isongole wilaya ya Ileje mkoani Mbeya,kushoto ni mkuu wa kituo hicho cha uhamiaji Ndugu  Fredrick Luhanga.


WAKONGWE KIBAO WAPANIA KUSHIRIKI TAMASHA LA GURUMO DESEMBA 14

$
0
0
MKONGWE wa muziki wa dansi Kassim Mapili amethibisha kushiriki Tamasha la Gurumo 53 litakalofanyika Jumamosi ya tarehe 14 mwezi Disemba mwaka huu.

Mapili amesema si yeye tu, bali pia ataratibu mpango mzima wa kuhakikisha wakongwe wote wa muziki wa dansi wanashiriki tamasha hilo bure bila malipo yoyote.


Tamasha hilo ambalo ni mahsusi kwa ajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidi Maalim Gurumo litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.


Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo amesema Mapili ameamua kubeba jukumu la kuandaa wakongwe ambao ambao watatengeneza wimbo maalum wa kumuaga Gurumo utakaosikika kwa mara ya kwanza TCC Club Disemba 14.


Baadhi ya wakongwe  wengine waliothibitsha kushiriki Tamasha la Gurumo 53 ni pamoja Komandoo Hamza Kalala, Tshimanga Kalala Assossa na Waziri Ali.


Gurumo anaagwa kufuatia  kutangaza kwake kuachana rasmi na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 53.

Bendi za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao waliowahi kung’ara na Sikinde ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu.


Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha,Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma.


Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachale, Benno Villa Anton, na Ibrahim Mwinchande.


Hata hivyo, licha ya wasanii hao waliowahi kuitumikia Sikinde kuwemo kwenye tamasha hilo, bendi ya Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae” haitashirki katika Gurumo 53 kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Mbizo amesema Mlimani Park ina mkataba unaowabana kufanya onyesho lolote litakalowakutanisha na Msondo hadi baada ya sikukuu ya Krismasi (Disemba 25, 2013).


Juma Mbizo amesema licha ya Sikinde kutoshiriki tamasha hilo lakini nyimbo zote zilizotamba ndani ya bendi hiyo ambazo zilitungwa na Gurumo, zitarindima TCC Club kwa ubora ule ule.


“Wanamuziki wengi waliofanya kazi na Gurumo katika Sikinde enzi hizo, hawako tena katika bendi hiyo, hivyo watakuwa huru kuungana na mwimbaji huyo mkongwe na kushusha burudani nzito.

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA MAOMBOLEZO KUFAUTIA MSIBA WA MZOBORA

$
0
0
Marehemu  Dunia Mzobora enzi za uhai wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kufuatia kifo cha Mwandishi wa Habari na Msanifu wa Habari Msaidizi Mkuu wa Gazeti la Uhuru, Bwana Dunia Mzobora, kilichotokea tarehe 27 Novemba, 2013 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya shinikizo la damu.
Marehemu aliajiriwa katika Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mwaka 1989 kama Mwandishi wa Habari Mwanafunzi, kisha akaendelea kupanda ngazi hadi kufikia cheo cha Msanifu wa Habari na hatimaye kuwa Msanifu Mkuu Msaidizi, cheo alichokuwa akikishikilia hadi mauti yalipomkuta.
“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha mmoja wa Waandishi wa Habari Shupavu na Mchapakazi, Dunia Mzobora aliyekuwa akilitumikia Gazeti la Chama Cha Mapinduzi (CCM) la UHURU, kilichosababishwa na ugonjwa wa shinikizo la damu baada ya kuwa amepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu”, amesema kwa masikitiko Rais Kikwete.
Rais Kikwete amesema binafsi alimfahamu vyema Marehemu Dunia Mzobora, enzi za uhai wake, kama Mwandishi wa Habari aliyejituma vilivyo katika kazi zake za kuuhabarisha, kuuelimisha na kuuburudisha Umma kwa kutumia vyema kalamu yake, na kwa kuzingatia kikamilifu Maadili ya Taaluma yake ya Uandishi wa Habari.

“Kufuatia taarifa za kifo cha Dunia Mzobora, ninakutumia wewe Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara na Wafanyakazi wote wa Kampuni ya Magazeti ya Chama ya Uhuru na Mzalendo na kwa kweli Waandishi wote wa Habari nchini, Salamu zangu za Rambirambi kwa kumpoteza mmoja wa Waandishi wa Habari Mahiri ambaye amelitumikia vyema Taifa lake kupitia Tasnia ya Habari”.

“Aidha kupitia kwako, naomba unifikishie Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi kwa Familia ya Marehemu Dunia Mzobora kwa kumpoteza Baba, Kiongozi na Mhimili wa Familia”.
​Rais Kikwete amewahakikishia Wanafamilia kuwa yeye binafsi yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba wa mpendwa wao, na anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu Dunia Mzobora, Amina.
Rais Kikwete amewaomba wawe na moyo wa uvumilivu, utulivu na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia baada ya kumpoteza mtu muhimu aliyekuwa kiungo cha Familia yao, kwani yote ni Mapenzi yake Mola.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA MTOTO WA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM, PHILP MANGULA, PETER MANGULA, OYSTERBAY DAR JANA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, wakati alipofika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam,jana jioni kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Peter Mangula, aliyefariki juzi asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili. Peter anatarajia kuzikwa kesho Ijumaa jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, marehemu Peter Mangula, wakati alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana jioni kwa jili ya kumpa pole.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phili Mangula, wakati alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana jioni kwa jili ya kumpa pole. 
 Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, marehemu Peter Mangula, wakati alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana jioni kwa jili ya kumpa pole.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, akimfariji Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, wakati alipofika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam,jana jioni kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Peter Mangula, aliyefariki juzi asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili. Peter anatarajia kuzikwa kesho Ijumaa jijini Dar es Salaam.

MTEMVU AFUNGUA NJIA KWA WATANZANIA NAFASI ZA AJIRA UGHAIBUNI

$
0
0

 Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo Job Centre Agency (LTD)Abbas Mtemvu, Akifafanua jambo  Mbele ya waandishi na Wanao Safirishwa na Kampuni hiyo Mwishoni Mwa Wiki Dar es Salaam.  
 Baadhi ya wahudhuriaji wa tukio hilo
 Mmoja wa Wasafiri hao Shamimu Mwarufai  Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD) 
  Mmoja wa Wasafiri hao Fatuma Chambo  Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD) 
 Dominica Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD) kwa niaba ya Tabu Khalfani
 Lita  Dominik Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD) kwa niaba ya Tabu Khalfani mwishoni mwa wiki Dar es Salaam.
 Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD) katika Picha ya Pamoja na wasafiri hao na ndugu na jamaa Pamoja na viongozi wa nao husika na Ofisi hiyo(PICHA NA KHAMISI MUSSA)

USAFI WA MITARO ENEO LA MAKUMBUSHO IMEKUWA TATIZO KUBWA,MAGONJWA YA MLIPUKO YANAWEZA KUTOKEA

$
0
0
Huu ni mtaro ambao umeziba na maji hayaendi,na watu kutupa uchafu ndani yake kama unavyoonekana.
Juu ya huo mtaro kuna mgahawa wa chakula,ambao watu wanautumia kwa mahitaji ya chakula.
Kama picha inavyoonesha maji machafu yakiwa yametuama,na uchafu ukiwa umetupwa ndani yake.
Ikifika mchan watu hukaaa hapo juu na kupata chakula hii ni hatari kwa afya ya binadamu.


Ukifika maeneo ya makumbusho nyuma ya Jengo la Tigo maarufu mtaa wa kwa bwela kwa wauza viatu maarufu kwa wakina dada,hali ya usafi katika mitaro ya eneo hili ni ya kutisha ingawa imezungukwa na maofisi makubwa kama kampuni za simu na mabenki mengi.Dj sek blog ilifanya utafiti makini na kujione hali ya mitaro hiyo ikiwa katika hali mbaya kiusafi,Kwanza mitaro hiyo imeziba hivyo kusababisha maji kutuama na kupelekea maji hayo kuvunda na kuwa rangi ya njano.



Kingine cha kushangaza zaidi ndani ya mitaro hiyo watu hutumia kama sehemu ya kutupia uchafu kama mifuko ya rambo,makopo n,k.Jambo lingine ambalo ni la hatari zaidi ni eneo la juu ya mitaro hiyo kuna mgahawa ambao unauza chakula kwa ajili ya matumizi ya binadamu.Jambo la kujiuliza je watoa huduma katika mgahawa huo hawaoni hali hiyo ya uchafu ambao upo kwenye eneo lao?na je hawaoni kwamba ni hatari kwa afya za binadamu wanaokula eneo hilo?Tulipojaribu kuwauliza walikuwa hawana majibu ya kutoa.Tunaomba serikali ya mtaa wa makumbusho walione hili na kulishughulikia na sio kukaa ofisini mpaka magonjwa yatokee ndipo tuanze kuhangaika.

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images