Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

KISARAWE YAANZA RASMI ZOEZI LA KUTOA VITAMBULISHO KWA WAJASIRIAMALI

$
0
0



Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akimkabidhi kitambulisho cha ujasiriamali mjasiriamali Indiana Mohamed Mnyukwa katika kikao cha RCC kinachofanyika mjini Kisarawe leo wilaya ya Kisarawe imeanza kutekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyetoa vitambulisho kwa ajili ya wajasiriamali nchini kote.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali waliokabidhiwa vitambulisho vyao leo.

 
NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE .

WILAYA ya Kisarawe,mkoani Pwani imeanza rasmi zoezi la kutoa vitambulisho vya ujasiriamali kwa wafanyabiashara ndogondogo ikiwa ni baada ya zoezi hilo kuanza mkoani hapo. 

Aidha serikali ya wilaya hiyo, imekemea wale wadanganyifu wataojitokeza kufanya ulaghai ili kupatiwa vitambulisho hivyo kinyume na utaratibu.
Akizungumza katika kikao cha kamati cha ushauri cha wilaya (DCC), Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo alisema, wameanza kwa wafanyabiashara watatu kama ishara ya kuanza kwa zoezi hilo . 

Alieleza, baada ya kufanya uhakiki wamebaini kuwepo kwa wafanyabiashara hao 502 ambao wanapaswa kupatiwa vitambulisho hivyo. Jokate aliwaasa watu kujiepusha na udanganyifu wowote utakaoashiria kupata kitambulisho kinyume na utaratibu. “Kusiwepo na udanganyifu na atakaebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria “alisisitiza Jokate. 

Aliwataka wajasiriamali kujiunga vikundi ili kupata mikopo kirahisi na kuingia kwenye mipango rasmi kwa urahisi. Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba kuacha kuacha kuwa mmoja mmoja na kuwa na umoja ili kujiinua kimaendeleo.
Kwa upande wa baadhi ya wajasiriamali wilayani Kisarawe wamepongeza kuwepo kwa zoezi hilo na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kuwaangalia wajasiriamali, wafanyabiashara ndogondogo kwa jicho la tatu ili kutambulika na kujiongezea kipato.

Mkazi wa Simiyu ashinda Milioni 56.1 za M-bet

$
0
0
Mkazi Bariadi Mkoa wa Simiyu, Golesu Maduhu (23) ameshinda Sh 56,137,550 baada ya kubahatisha kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 unaoendeshwa na Kampuni ya M-Bet Tanzania.

Maduhu ameweza kubahatisha matokeo ya droo ya Desemba mwaka jana na kuwa mshindi wa kwanza kuzawadiwa fedha kutoka kampuni ya M-Bet kwa mwaka huu. Maduhu alipatia kiusahihi michezo yote 17.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Maduhu alisema kuwa amefurahi sana kupata kiasi hicho cha fedha ambacho kitamsaidia katika maisha yake. Maduhu amesema kuwa ametumia sh 1,000 kupata mamilioni hayo ya fedha na kuwaomba Watanzania kujiunga na michezo ya kampuni ya M-BET ambayo inachangia kubadili maisha. Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa katika fedha hizo, Serikali imepata Sh milioni 11.2 ikiwa ni kodi ya ushindi. “Nawaomba Watanzania washiriki katika michezo ya kubahatisha ya M-bet ambayo mwaka 2018 iliwazawadia jumla ya washindi 20 ambao walipata mamilioni ya fedha na kubadili maisha yao,” alisema Mushi.

Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Kubahatisha Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Ilala, Shabani Rashid Mwanga naye aliwaomba Watanzania kushiriki katika michezo hiyo ili kuchangia maendeleo ya nchi. Mwanga alisema kuwa unaoposhinda kiasi chochote, serikali inapata kodi yake moja kwa moja na kuongezea fedha za kufanyia maendeleo nchini. “Naishukuru M-Bet ambayo kila mara imekuwa ikitoa washindi wamekuwa wakipata mamilioni ya fedha na kuchangia pato la Taifa, ni chanzo kizuri sana cha mapato kwa ajili ya maendeleo ya nchini,” alisema Mwanga.

Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Catherine Lamwai aliipongeza kampuni ya M-bet kwa kuweka kuendelea kupata washindi wengi na kujizolea mamilioni ya fedha. “Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imekuwa ikifuatilia na kusimamia michezo ya kubahatisha kutokana na kupata washindi wengi. Wametufurahisha sana kutokana kuchangia pato la Taifa kupitia mchezo wa Perfect 12,” alisema Lamwai.
Mshindi wa Droo ya 20 ya mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-bet, Golesu Maduhu (wa pili kushoto) akipokea mfano wa hundi baada ya kushinda Sh milioni 56.1 kutoka kwa meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi (wa tatu kushoto) baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 17. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Kubahatisha Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Ilala, Shabani Rashid Mwanga na wa kwanza kulia ni Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Catherine Lamwai. 

Jafo Asisitiza Viongozi Kutembelea Miradi

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemank Jafo amesisitiza Viongozi na watendaji kutembelea miradi ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo hayo ili miradi hiyo iweze kutekelezwa vizuri Kama inavyotakiwa.

Waziri Jafo aliyasema hayo Leo hii alipokuwa katika ukaguzi wa miradi ya DMDP wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ya kikazi ya waziri wa TAMISEMI ni muendelezo wa kazi tokea kuanza kwa mwaka 2019 iliyoanzia Wilayani Chemba, Kilosa, Kibiti, Rufiji, na Temeke.

Katika ziara hiyo Jafo alifanikiwa kufanya ukaguzi wa barabara za DMDP katika Kata ya Buza, ujenzi wa kituo cha afya Buza, pamoja na soko la kisasa linalojengwa eneo la Makangarawe.

Katika ukaguzi huo Jafo alifurahishwa Sana na kazi nzuri inayo tekelezwa katika eneo hilo. Ameagiza kituo hicho pamoja na soko hilo la kisasa likamilike kabla mwezi June mwaka 2019.

Waziri Jafo anaendelea na ziara ya kikazi mkoani Kigoma kwa lengo la kufuatilia thamani ya fedha zilizotewa chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote Nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua barabara zinazokengwa na mradi wa Dmdp katika kata ya Buza eneo la Makangarawe
Soko la kisasa linaloendelea kujengwa katika Kata ya Buza eneo la Makangarawe kupitia mradi wa Dmdp
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua ujenzi aa Kituo cha Afya kinachojengwa katika Kata ya Buza

Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini (kulia) na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (Kushoto) wakifungua kitambaa katika jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kiwanda hicho cha kuchenjua dhahabu kilichopo mkoani Geita wilaya ya Chato mnamo tarehe 02 Januari, 2019.

????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato  Dkt. Medard Kalemani (kulia) mara baada ya kuwasili katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwenye kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Pedalu kilichopo wilayani Chato mkoani Geita.
TWO
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Wa tatu kutoka Kushoto), Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) wakielekea eneo maalum kwa ajili ya kupata maelezo pamoja na kuweka rasmi jiwe la msingi la kiwanda cha Pedalu uliofanyika tarehe 02 Januari, 2019 mjini Chato.
THREE
Msimamizi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu cha Pedalu mjini Chato akitoa maelezo ya namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi ya uchenjuaji wa dhahabu kwa Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko na wajumbe alioambatana nao wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho.

  • Ni baada ya kubaini ucheleweshaji wa utoaji vibali vya uwekezaji sekta ya madini
Na Nuru Mwasampeta, Geita

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kutoa kibali kwa wamiliki wa Kiwanda cha Kuchenjua Dhahabu kinacho milikiwa na kampuni ya Pedalu ili waweze kupewa leseni na kuendelea na shughuli ya kuchenjua madini hayo.

Biteko aliyasema hayo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha kuchenjua dhahabu kinachomilikiwa na kampuni ya wazawa ya Pedalu, katika kijiji cha Lumasa mjini Chato, iliyofanyika Desemba 2, 2019.

Alisema kuwa, kibali kingine kinapaswa kutolewa na Mkemia Mkuu wa Serikali na kubainisha kuwa, baada ya hafla hiyo atawasiliana naye ili awezeshe upatikanaji wa kibali hicho kwa lengo la kuiwezesha wizara ya madini kuendelea na mchakato wa kuandaa leseni itakayowaruhusu wawekezaji hao wazawa kuendelea na kazi ya uchenjuaji wa madini.“Jamani, Rais anataka viwanda, isitokee mtu hapa katikati anaweka urasimu na kuchelewesha azma ya Rais wetu, nchi hii tunaondoa urasimu tunataka kuondoa na rushwa,” alisisitiza Biteko.

Aidha, alibainisha kuwa, miongoni mwa masuala yanayowakimbiza wawekezaji nchini ni mawili tu, rushwa na urasimu na wala si sheria, na kusema kuwa, vitu hivyo ni kikwazo kikubwa katika kutimiza azma ya Serikali ya Tanzania ya Viwanda.

Aliwapongeza wawekezaji katika kiwanda cha Pedalu kwa kufanya uwekezaji huo mkubwa kwani anaamini madini yatakayopatikana kutoka katika kiwanda hicho yataiwezesha serikali kupata  kodi stahiki. Pia, Biteko aliwaomba wawekezaji hao wazawa kujenga viwanda vingine kama hivyo katika maeneo tofauti na kuahidi kupeleka wadau wenye nia ya kujifunza ili waweze kupata ujuzi wa namna ya kuwekeza ili kukuza sekta ya madini kwa pamoja.

Aidha, alimtaka Kaimu Afisa Madini Mkoa wa Geita, Pius Bajunana kuwalea vema wawekezaji na kuwataka watendaji wa Serikali kuwaendea wawekezaji hao kwa sura ya kirafiki badala ya kufuatilia masuala ya ulipwaji wa tozo mbalimbali kwa ukali. Alisema ili wawe huru kushirikiana na Serikali katika masuala yote yanayohusu utekelezaji wa majukumu yao, suala la urasimu linatakiwa kuondolewa ili kushirikiana vizuri katika kukuza uchumi wa nchi.

Halikadhalika, Biteko alisisitiza kwa kuwataka watendaji wa serikali waliohudhuria hafla hiyo na wengine kuwasidia wawekezaji wazawa ili waweze kukuza viwanda vyao na kuongeza kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya mabadiliko katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kwa lengo la kuwanufaisha watanzania hivyo, hawana budi kumuunga mkono.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kufanya kazi kwa uaminifu huku wakijua kuwa Serikali ipo pamoja nao na kuwataka kuutumia vizuri wakati huu ambao imeazimia kukuza sekta ya uchimbaji mdogo wa madini ili wakati neema hiyo itakapopotea wasije wakajilaumu.

“Ametokea Rais anayewapenda watu hao, wanyonge, anatamani awasaidie waweze kukuza uchumi wao, wajibu wao ni kumuunga mkono Rais wetu, pamoja na kumwombea kwani kazi anayoifanya ni ngumu. Rais ametutuma tuwafikie wachimbaji wadogo kwani anataka ninyi wachimbaji wadogo mgeuke kuwa wachangiaji wakubwa kwenye uchumi wa taifa,” aliongeza Naibu Waziri Biteko.

Alisema Rais Dkt. John Magufuli ametoa Jumla ya Dola za Marekani Milioni tatu laki saba mia tatu elfu mia sita na sitini sawa na shilingi bilioni nane na nusu za kitanzania kwa ajili ya kufanya utafiti ili kuwasaidia wachimbaji wadogo. “ Rais wenu anawapenda, na sisi ametutuma kuja kuwasaidia wachimbaji wadogo ili mtoke kwenye wimbi la umaskini na uchimbaji wa kubahatisha,” alisema Biteko
Aliongeza kwamba, hivi sasa wizara imeanza kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo, katika maeneo mbalimbali ikiwemo Bukombe Kyerwa Kona Z, Mpanda, Tanga na maeneo mengine nchini, kwa la kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata elimu ya uchimbaji wenye tija.

Aidha, Biteko aliwataka wachimbaji wadogo kuachana na biashara ya ujanjaujanja na kuwataka kutenda haki na kuachana na majungu badala yake wafanye kazi kwa upendo na ushirikiano.

Alibainisha kuwa, wapo wachimbaji wadogo zaidi ya milioni nne nchini lakini cha kushangaza wanachangia asilimia 4 pekee katika uchumi wa taifa. Alisema wachimbaji wadogo walio wengi hawalipi kodi, na ni mabingwa wa kutorosha madini. “Mnakwepa kodi lakini mna waibia watanzania wenzenu,” alisema.  

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Mbunge wa jimbo la Chato, Dkt. Medard Kalemani alisema wizara yake iko katika mchakato wa kuwaunganishia umeme wa uhakika wachimbaji wadogo nchini kote ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano ya kuiwezesha sekta hiyo kuwa na uzalishaji wenye tija.

Wakati huohuo, uongozi wa kiwanda cha Pedalu ulikiri kuwa, uamuzi wa kujenga kiwanda hicho ni matokeo ya matakwa ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwataka wachimbaji wa madini kuyaongezea thamani madini nchini badala ya kuyasafirisha yakiwa ghafi jambo ambalo linainyima serikali mapato zaidi

MGALU NA VULLU WAUNGA MKONO KAMPENI YA TOKOMEZA ZERO KISARAWE

$
0
0

Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgagalu wakimkabidhi vifaa mbalimbali mkuu wa wilaya ya Kisarawe ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya “Tokomeza Zero” wilayani humo.

Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgagalu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbaoimbali baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali mkuu wa wilaya ya Kisarawe ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya “Tokomeza Zero” wilayani humo.
Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgagalu wakimkabidhi vifaa mbalimbali mkuu wa wilaya ya Kisarawe ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya “Tokomeza Zero” wilayani humo.


Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu akizungumza katika kikao cha RCC kinachoendelea wilayani Kiswarawe wakati akitangaza utekelezaji wa msaada ambao wabunge hao waliuahidi katika ziara ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakati alipofanya ziara yake kulia ni Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgagalu na wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo katikati ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe Musa Gama. 
 
NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE


WABUNGE wa viti maalum mkoani Pwani ,Subira Mgalu na Zainab Vullu wamechangia magodoro 20 ili kupunguza changamoto ya upungufu wa magodoro uliopo shule ya sekondari Maneromango. 

Aidha Subira ametoa tanki la maji la lita 2,000 litakalosaidia kuhifadhi maji katika shule hiyo na tanki jingine shule ya sekondari Kolesa iliyopo kata ya Vikumburu.

Wakikabidhi msaada wa magodoro na matanki hayo ya kuhifadhi maji, walisema, msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya Tokomeza Zero iliyoanzishwa hivi karibuni na mkuu wa wilaya Kisarawe Jokate Mwegelo.
“Tumejichanga kila mmoja magodoro kumi, kumi na kwa upande wa maji,mimi nipo karibu na shule ya Maneromango hivyo nimewataka wachote maji kwangu buree “alisema Zainab. 

Alieleza, wanafunzi wa kike wanahitaji zaidi maji hivyo kwa hakika kwa misaada hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa. Zainab ,aliwaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia katika tokomeza zero, ili kufikia malengo ya kiwilaya kuinua taaluma. Nae Subira alisema ,wazazi na walezi waelekeze nguvu zao kushirikiana na viongozi na serikali kusimamia watoto kuongeza ufaulu. 

“Fuatilieni watoto, kufuatilia maendeleo ya kimasomo kwa wanafunzi wetu, tusiachie walimu, tusijisahu wajibu wetu,”:Mkoa na wilaya imejikita kuinua sekta ya viwanda ,kama hatutoelimisha watoto jitihada hizo zitakuwa kazi bure “alifafanua Subira.

Subira alimpongeza Jokate kwa kufanya vizuri kwa kampeni hiyo kubwa.
Awali Jokate alibainisha, tangu kuanza kwa kampeni ya Tokomeza Zero, tayari wamejenga madarasa kumi na bweni moja kata ya Kurui kwa zaidi ya sh. mil. 100.

RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA MAUZIANO YA MAHINDI KATI YA NFRA NA WFP IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia Zikankuba na  Mwakilishi Mkazi wa  Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Duncan kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019. Walioketi kushoto ni Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia kubadilishana nyaraka baada ya utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia Zikankuba na  Mwakilishi Mkazi wa  Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Duncan kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia Zikankuba na  Mwakilishi Mkazi wa  Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Duncan kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini Bw. Michael Dunford  pamoja na  Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwa, Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na maafisa wengine waandamizi wa taasisi hizo baad ya  hafla fupi ya utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019. Kati ni Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba..
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini Bw. Michael Dunford  pamoja na  Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwana maafisa wengine waandamizi wa UNFPA baada ya  hafla fupi ya utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019. Kati ni Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba. PICHA NA IKULU

Bosi Lake FM aibuka na kipindi cha televisheni cha Tena na Tena

$
0
0
Mbunifu wa mavazi vyota nchini, Doreen Peter Noni anayetamba na lebo ya Eskado Bird ameibuka na kipindi maalum cha televisheni kijulikanyo kwa jina la ‘Tena Na Tena’ ambacho kinazungumzia shughuli mbalimbali za kutafuta riziki katika maisha mpaka kufanikiwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Doreen ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi na mmiliki wa kituo cha redio, Lake FM cha Mwanza alisema kuwa, sababu kubwa ya kuanzisha kipindi hicho ambacho kitarushwa katika moja ya vituo vya televisheni hapa nchini mwakani, ni kutoa hamasa kwa vijana kuendelea ‘kupambana’ katika kutafuta riziki bila kukata tamaa.

Doreen alisema kuwa kipindi cha Tena na Tena ambacho pia kitaonyeshwa ‘Online’, kimerekodiwa kwenye gari inayotembea ambapo muhusika atatoa ushuhuda wake wa maisha katika mfumo wa majadiliano. Alisema kuwa mbali ya kuburudisha, lengo lingine la kipindi cha Tena na Tena ambacho kitaanza kurushwa hewani hivi karibuni ni kutoa elimu kwa vijana katika kukabiliana na changamoto za maisha.

Alifafanua kuwa kuna vijana wengi wanakata tamaa katika maisha bila kujua walikosea wapi, jambo ambalo limemfanya kuandaa kipindi hicho ili kutumika kama nyenzo ya mafanikio. “Wahusika katika kipindi hiki watapata fursa ya kuzungumzia jinsi alivyohangaika mpaka kupata mafanikio. Ni kumbukumbu ambazo haziwezi kusaulika na kutumiwa na waangaliaji wa kipindi hicho kama nyenzo kwa mafanikio ya vijana wa sasa, ” alisema Doreen.

Alifafanua kuwa ndani ya kipindi hicho, kutakuwa na nafasi ya kutoa burudani kama kuimba kwa mtindo wa karaoke, hali ambayo kinamfanya mtazamaji kutochoka kuangalia. Kwa mujibu wa Doreen, mbali ya wajasiriamali, kipindi cha Tena na Tena pia kitafanya mahojiano na watu mbalimbali maarufu, wanasiasa, wanamichezo kwa lengo la kuhamasisha vijana kutokukata tamaa katika shughuli za kujitafutia vipato. Unaweza kupata taarifa zaidi katika mitandao ya kijamii ya Tena na Tena kupitia @tenanatenashow facebook, instagram, twitter na youtube.
Mbunifu wa Mavazi na Mkurugenzi wa Kituo Cha Redio cha Lake FM, Doreen Peter Noni akirekodi kipindi cha Tena na Tena na wasanii Nevi Kenzo
 Mbunifu wa Mavazi na Mkurugenzi wa Kituo Cha Redio cha Lake FM, Doreen Peter Noni akirekodi kipindi cha Tena na Tena na msanii Vanessa Mdee
  Mbunifu wa Mavazi na Mkurugenzi wa Kituo Cha Redio cha Lake FM, Doreen Peter Noni katika pozi 

DC JOKATE KUMPA SHAVU BONDIA DULLA MBABE

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE 

SERIKALI ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani inatarajia kutoa eneo kwa ajili ya kujenga ukumbi utakaotumika kuwapatia mazoezi ya ngumi vijana wa wilaya hiyo.

Aidha imempongeza bondia Dulla Mbabe mzawa wa wilaya ya Kisarawe kwa ushindi alioupata dhidi ya mpinzani wake Fransis Cheka lillilofanyika hivi karibuni. 

Hatua hiyo ya kupatiwa eneo hilo imetokana na bondia huyo kutoa kauli ya kutaka kutoa mafunzo kwa vijana wa kisarawe ili waweze kujifunza mchezo huo. Akizungumza  kuhusu mpango huo Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema,Mbabe amewatendea haki kwa kushinda pambano lililofanyika Desemba 26 mwaka uliopita dhidi ya Cheka. 

Jokate alieleza, Kisarawe imejaa vipaji sio tu mpira wa miguu bali katika michezo mbalimbali. Aliahidi serikali ya wilaya kumpa uahirikiano kuhakikisha kipaji chake kinakua na kuibua vijana wengine. 

Nae bondia huyo Mbabe alijigamba kwa kasema amecheza mipambano zaidi ya 20 ikiwemo ya kimataifa. Hata hivyo aliwaahidi watanzania kufanya vizuri katika Mchezo wa kimataifa unaokuja ambao unatarajiwa kufanyika mwezi march mwaka huu. 

Katika hatua nyingine mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Zainab Vullu, alimhakikishia bondia huyo, wabunge wa mkoa huo watamkaribisha Dodoma katika bunge ili kumtambulisha na kuitambulisha Kisarawe kuwa inawanamichezo lukuki sio tu wa mpira wa miguu bali na masumbwi.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akimpongeza Bondia Dulla Mbabe,ambaye ni mzawa wa wilaya ya Kisarawe kwa ushindi alioupata dhidi ya mpinzani wake Fransis Cheka lillilofanyika hivi karibuni.

MKUU WA KIKOSI DHIDI YA UJANGILI KANDA YA ARUSHA KUSIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI WA TUHUMA ZINAZOMKABIRI

RC MAKONDA ATAKA WATENDAJI KUONGEZA KASI YA MAKUSANYO YA KODI PASIPO KUWASUMBUA WANANCHI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo makusanyo ya kodi ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu mpya na rafiki za ukusanyaji pasipo kuwatisha wala kuwabugudhi wananchi. 

RC Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa kikao mkakati baina yake ya mamlaka za ukusanyaji wa kodi ambapo amesema mwaka huu jiji hilo limedhamiria kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ili kuendelea kuwa kinara.

Aidha RC Makonda amewataka watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato, kuongeza idadi ya walipa kodi, kufanya mabadiliko ya sheria kandamizi zilizopitwa na wakati pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo kwa kadi Kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Pamoja na hayo RC Makonda ameshauri kuanzisha kwa kitengo cha ushauri kwa wafanyabiashara jambo litakalowajengea wananchi hamasa ya kulipa kodi na kuondoa dhana ya kuonekana ni watu wa kukusanya mapato pekee.

RC Makonda anaamini kuwa wananchi wapo tayari kulipa kodi serikalini endepo watawekewa mazingira rafiki ya kuwawezesha kulipia ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kuwekwa katika data base moja.

Kikao hicho kimehusisha wakuu wa wilaya, makatibu tawala, TRA, BOT, TIC, NBS, Wizara ya fedha na kamati za ulinzi na usalama.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda  akizungumza na na Watendaji kuhusu  kuhakikisha wanasimamia ipasavyo makusanyo ya kodi ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu mpya na rafiki za ukusanyaji pasipo kuwatisha wala kuwabugudhi wananchi.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUANZA KWA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE, JANUARI 2019

WAZIRI UMMY ATOA MABATI 100 KATA YA KIRARE JIJINI TANGA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANCHI.

$
0
0

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi mabati 100 Diwani wa Kata ya Kirare Jijini Tanga Mwagilo ambazo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa zahanati za Mapojoni na Ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Kirare wanaoshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudu Mayeji kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mganga wa Mfawidhi wa Zahanati ya Mapojoni mara baada ya kukabidhi mabati hayo wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukabidhi mabati hayo kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kulia akimsikilkiza kwa umakini Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mapojoni wakati alipokwenda kukabidhi mabati 100
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto akikagua dawa kwenye zanhanati ya Mapojoni wakati alipokwenda kuwakabidhi mabati 100 .
 
MBUNGE wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekabidhi mabati 100 katika Kata ya Kirare Jijini Tanga kwa ajili ya zahanati za Mapojoni na Ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Kirare

Ujenzi huo wa Bweni la Wasichana kwenye shule hiyo litasaidia kuondosha changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu umbali wa kilomita 15 jambo ambalo linaweza kupelekea kukumbana na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha ndoto zao.

Halfa ya makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye Kata hiyo ikiwa ni juhudi kubwa zinazoonyeshwa na Mbunge huyo kwa ajili ya kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wananachi anashirikiana nao kuweza kuzipatia ufumbuzi. kizungumza mara baada ya kukabidhi mabati hayo Waziri Ummy alisema serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchapa kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kutatua changamoto wa wananchi ili ziwez kupata ufumbuzi .

Sambamba na Waziri huyo kuchangia mabati hayo wakati huo huo Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imeguswa na changamoto hiyo na kuchangia mabati 50 na saruji 70 katika ujenzi wa bweni la wasichana la shule ya Sekondari Kirare na kushiriki kwenye shughuli za ujenzi.

Alisema kwani wao watahakikisha wanashirikiana na wananchi kwenye maeneo mbalimbali kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto za Afya ambazo zinaweza kuwa kikwazo kwenye kujiletea maendeleo. “Labda niwaambie tu kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dkt John Magufuli imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha changamoto mbalimbali zinbapatiwa ufumbuzi hivyo endeleeni kushirikiana nayo kuweza kupata mafanikio “Alisema Waziri Ummy.

Aidha pia Waziri huyo alisisitiza umuhimu wa wananchi kuhakikisha wanakata bima za Afya ili ziweze kuwasaidia kunufaika na huduma za matibabu wanapokuwa wakiugua. “Niwasisitize kwamba kateni bima ya Afya mkiumwa muweza kupata huduma za matibabu kwani wengine fedha zenu ni za msimu hivyo mkiwa na bima mnaweza kupata matibabu bure”Alisema

Waziri huyo alisema kwani gharama za matibabu zimekuwa kubwa hivyo iwapo wakijiunga na bima hususani iliyoboreshwa ukitoa elfu thelathini kwa kaya ya watu sita unaweza kupata huduma za matibabu kwenye maeneo mbalimbali. “Bima kubwa ya kitaifa ya NHIF wanabima ya mtoto wameona badala ya kusema mtoto aishie elfu thelathini tu kwa hiyo ukimliptia mtoto 50400 atapata huduma mzuri”Alisema

Alisema sababu ya kusaidia juhudi hizo za wananchi ni kutokana na kuguswa namna walivyojitahidi kuhakikisha wanajenga jengo hilo mkishirikiana na viongozi wenu namna nikaona bora niwaunge mkono. Aidha alisema anaamini mabati hayo yatakuwa chachu katika kutatua changamoto iliyopo kwenye jengo hilo ili kuweza kuzimaliza na kutoa fursa kwa wananchi kuweza kupata huduma bila kuwepo vikwazo.

“Lakini hapa nimeambiwa mnachangamoto ya vifaa hivyo nitashirikiana nanyi kuweza kuzipatia ufumbuzi vifaa vyote vinavyoihitaji kwenye zanahati hii”Alisema .Awali akiz Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Isango Isubiri alisema wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa fedha za ukarabati za vituo vya afya kwenye Jiji ambavyo ni Makorora,Ngamiani,Mikanjuni na Duga ambao kwa sasa unaendelea.

Alisema kwenye zahanati ya Mapojoni Jijini Tanga kulikuwa na uhaba wa chumba cha maabara na daktari hivyo kilichofanywa na Waziri huyo ni kutambua umuhimu kuunga mkono nguvu za wananchi katika ujenzi wa jengo hilo lenye uhitaji mkubwa ambalo baada ya kulijenga walikosa mabato na saruji ili kuweza kulikamilisha.

Mganga huyo wa Jiji alisema ujenzi wa Jengo hilo ulianza mwaka 2016 ambapo litakapokamilika litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi ambao wanakwenda kupata huduma za matibabu kwenye zahanati hiyo. Aidha alisema pia suala lingine ni ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Tanga ambapo zilitolewa Bilioni 3.6 katika kipindi cha mwaka 2018 jambo ambalo limesaidia kuweza kuondosha changamoto ya afya.

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0


Ndugu Lister Joseph Muro wa Dar es Salaam anatangaza kifo cha Mama yake AMIN-RUTH LAZARO JOSEPH MURO, kilichotokea Machame Nkuu Kilimanjaro,Januari 1,12019, Mazishi
 yatafanyika Machame Nkuu Jumamosi hii Januari 5,2019 saa Saba mchana.

BITEKO AKALIPIA AJALI MAENEO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

$
0
0








Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi (aliyesimama) akieleza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Kushoto) alipofika ofisini kwake kuelezea uwepo wake katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza jambo akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama Annarose Nyamubi (Hayupo pichani) juu ya uwepo wake wenye lengo la kufungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini wa Mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza jambo mbele ya wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo ya namna bora ya kuboresha uchimbaji wao yanayofanyika katika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara.
Baadhi ya Wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao yenye lengo la kuboresha sekta ya uchimbaji mdogo wa Madini yanayoendelea katika wilaya ya Butiama mjini Buhemba mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (aliyekaa kushota) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria mafunzo ya namna bora ya kujikita katika uchimbaji wenye tija.


Na, Nuru Mwasampeta

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuzingatia uchimbaji salama ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara katika maeneo ya migodi. Ametanabaisha kuwa akifa mtanzania mmoja huyo Mtanzania ni muhimu kuliko mgodi wote, ‘kuliko mtanzania mmoja afe ni bora huo mgodi usiwepo’.

Aliyasema hayo leo tarehe 04 mwezi Januari alipokuwa akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo katika eneo la uchimbaji mji wa Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara inayoendelea kwa siku mbili.

Biteko alibainisha kuwa, Buhemba ni eneo linaloongoza kwa ajali kwenye migodi, huu mgodi ulifungwa na toka umefunguliwa kuna vifo vya wachimbaji kumi na mbili na majeruhi 20, Serikali haiwezi ikakubali hali hiyo iendelee “Mimi nakwambia mwenyekiti sitakubali hali hii iendelee mimi mwenyewe nitakuja kuufunga tena mgodi huu kama hali hiyo itaendelea hatuwezi kupoteza maisha ya watanzania” Biteko alisisitiza.

Biteko aliongeza kwa kusema, Serikali haiko tayari kuona kuwa watu wanaendelea kufa ndio maana imeamua kufika na kuandaa mafunzo kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili waweze kufundishwa namna bora za uchimbaji salama na wenye tija. Biteko alisema mafunzo hayo yanalenga kuwafundisha wachimbaji wadogo masuala ya uchimbaji salama, uchenjuaji, afya, na mazingira ya uchimbaji katika mkoa huu wa Mara.

Akiwapongeza wananchi na wachimbaji wadogo wa madini Buhemba, Biteko alisema kumetokea ugonjwa mmoja kwa watanzania wa kukwamisha mradi wa Serikali, wananchi wanaanza vurugu na kudai fidia lengo ikiwa ni kukwamisha tu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa watanzania lakini Buhemba mmeonesha ushirikiano mkubwa kutoka mwanzo mpaka mwisho wa utafiti.

Aidha, Biteko alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa ushirikiano anaoufanya katika kusimamia shughuli za uchimbaji wa madini. Amesema mara nyingi wachimbaji wadogo wanakuwa kama watoto yatima lakini si kwa hapa Buhemba. Hawana mlezi, wanajiendesha wenyewe na wakati mwingine mamlaka za serikali zinajitokeza pindi matatizo yanapotokea lakini Mkuu wa wilaya amekuwa bega kwa bega.

Aidha, Biteko aliwasihi wachimbaji wadogo wa Buhemba kuchangia kwa ukamilifu katika pato la taifa. Alisema wakati wote ukikutana na kesi ya utoroshwaji wa madini mhusika mkuu anakuwa ni mchimbaji mdogo. Aliendelea kwa kuwaeleza wachimbaji hao kuwa wamepata Rais ambaye anawapenda, anawajali anawadhamini, Rais anayependa wachimbaji wadogo wahame kutoka kwenye daraja la chini na kuwa watanzania wanaofurahia maisha kwenye nchi yao kwa kuthaminiwa na kuheshimiwa, “nilidhani zawadi pekee ambayo mngeipa Serikali na Rais wetu DKt ni nyie kusimamiana mkalipa kodi vizuri, mhame kwenye mfumo wa kukwepa kodi na kutorosha madini”. Biteko alisisitiza

Pamoja na hayo Biteko alibainisha kuwa, katika mkoa wa Mara wilaya inayoongoza kwa kulipa kodi ni wilaya ya Butihama, alisema kiasi cha milioni 57 za kitanzania zimelipwa kwa mwezi jana, hata hivyo aliwahimiza wachimbaji hao kufanya zaidi ili kuipa serikali wajibu mkubwa wa kuwahudumia.

“Ninapima mapenzi ya Rais Kwenu, halafu ninapima kile mnachochangia ninyi kwenye pato la Taifa haviendani” Mimi nilidhani mtu anayekupenda nawewe unamlipa kwa kumpenda zaidi. Rais wetu anawapenda wachimbaji wadogo hataki mtangetange, mpeni sababu ya kuendelea kuwapenda, mpeni sababu ya kuendelea kuwahudumia, siku mtu akiwagusa Rais awateteee kutokana na kodi zenu”

Naomba sana muwe wazalendo, muwe waaminifu, ili mchango wenu katika sekta hii uweze kuonekana na kutumika katika maeneo mengine nchini. Ili Serikali iweze kuhudumia maeneo mengine kama vile elimu, afya, usafirishaji na mambo mengine ni kutoka katika kodi. Simamianeni ninyi kwa ninyi, onyanenyi ninyi kwa nini bora mtu mbaya bora ake nje ya sekta.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Mara (MAREMA) Dave Bita alitoa shukrani zake za dhati kwa serikali kwa kutupa jicho kwa wachimbaji wadogo kwa lengo la kuwawezesha kuwa na uchimbaji wenye tija. Aliishukuru Serikali kwa kujipanga kuwajengea kituo cha mafunzo kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha masuala ya utafutaji na uchimbaji wa madini.

Ameishkuru Serikali kwa kuwasilisha taarifa ya utafiti ulioanza mwezi Oktoba 2016 kwa wachimbaji wa Butiama matokeo yatakayowapelekea kunufaika na uchimbaji wao. Aidha, Dave amewataka wachimbaji wadogo kutengeneza mazingira ya kukubali kuwalipa posho viongozi wanaowasimamia katika shughuli zao vinginevyo wataendelea kugombana na viongozi hao siku kwa siku na hata kupelekea migogoro. Amesema wachimbaji wadogo hawako tayari kuwalipa viongozi wanaowasimamia katika maeneo ya uchimbaji.

Aidha, amewasihi wachimbaji wadogo kutumia mafunzo yanayotolewa kwa manufaa ameomba watoe ushirikiano kwa voiongozi watakaowachagua pamoja na kuwasihi kukitumia kwa manufaa kituo cha mafunzo kinachojengwa na serikali kwa ajili yao.

MTANZANIA VICTORIA MWANZIVA APATA TUZO MAALUMU YA UTAMBUZI MWANAFUNZI BORA CHUO CHA HARBIN NCHINI CHINA

$
0
0
 Mtanzania Victoria Mwanziva akiwa na tuzo yake pembeni bango linalomuelezea kwa ujumla mafanikio yake kitaaluma na uwakilishi alioufanya Harbin Institute Technology nchini China

Victoria akiwa na Tuzo yake ya Heshima ya mmoja wa wanafunzi bora wa kimataifa ukumbini hapo muda mchache baada ya kuipokea Jukwaani


Mtanzania Victoria Mwanziva kulia akipokea tuzo mara baada ya shughuli maalumu ya kutambua wanafunzi bora katika chuo cha Harbin Institute of Technology nchini China

Harbin Institute of Technology

Wakiwa katika picha ya pamoja chuoni Harbin Institute of Technology palipofanyika shughuli hiyo iliyopambwa na vijana wa Jeshi la Chin

Mtranzania Victoria Mwanziva akiwa ukumbini akisikiliza kwa umakini wakati wa shughuli hiyo maalumu ya kutambua wanafunzi bora katika Chuo cha Harbin Institute of Technology

Picha ya Pamoja na washindi wa tuzo hizo na wawakilishi kutoka Chuoni HIT

Mtanzania Victoria Mwanziva, amepata tuzo maalumu na utambuzi maalumu kama Mwanafunzi bora katika chuo kikuu cha Harbin Institute of Technology, Mjini Harbin, China ambapo anasoma Shahada ya uzamili yaani Masters in Public Administration.

Victoria Mwanziva amepata tuzo hiyo ya heshima Tarehe 3 Januari 2019; akiwa mmoja wa wanafunzi 10 pekee wa Kimataifa waliopewa Heshima Hiyo jimboni hapo na akiwa ni Mwanamke pekee wa kiafrika kuipata tuzo hii.

Mgeni rasmi na aliyekabidhi tuzo hizo ni Mh.Rais wa Chuo cha Harbin , Bw. Zhou (Chancellor Mkuu wa Kampasi zote za HIT China)- aliambatana na viongozi waandamizi wa Chuo hicho na viongozi wa Serikali ya China.

Tukio hili lilioneshwa mubashara kwenye Runinga za jimbo la Heilongjiang; na kukusanya mamia ya watu waliotazama moja kwa moja kupitia kampasi za Weihou na Shenzhen za moja ya vyuo 10 bora China cha Harbin anaposoma Victoria.

Bi Mwanziva amepata tuzo hii kutokana na mchango wake maswala mtambuka chuoni; kujituma kwake Kimasomo; kupata ufaulu wa juu (Daraja la kwanza) pia kutokana na uwakilishi mzuri wa Nchi ya Tanzania nchini China kupitia mikutano ya kimataifa,mashindano ya kimataifa ambayo na kushinda tuzo za Uwasilishaji bora wa mada- Kwenye Mkutano Mkuu wa Belt and Road Beijing, Tuzo za Uwasilishaji bora kwenye Mkutano wa UN na Chuo cha Tongji-Shanghai, Pamoja na uandishi wa Makala bora kutoka Chuo cha Chengdu, Sichuan China.

Pamoja na hayo ameendelea kushiriki kuandaa mikutano na midahalo mbalimbali kupelekea kutambulika kwake na kuwakilisha Nchi yake na chuo chake.Victoria Mwanziva anamalizia masomo yake China na kwa sasa anahudumu kama Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watanzania Nchini China, nafasi hii imempelekea kuimarisha mtandao wa Watanzania wanaosoma China kupitia jumuiya zao za miji wanayosoma na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili kupitia kwa nafasi yake.

MastaBata ya NMB yaendelea kumwaga manoti kwa washindi, wengine 20 wajizolea fedha taslimu

$
0
0

Mtaalamu kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Florence Mchau (kushoto) akimjulisha kwa njia ya simu mmoja wa washindi wa Droo ya tatu ameshinda katika droo hiyo ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata'. Kulia ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo akisimamia droo hiyo. Katikati ni Saumu Rajabu kutoka Selcom.




Mtaalamu kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Florence Mchau (kushoto) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Droo ya Tatu ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata'. Kulia ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo akisimamia droo hiyo. Katikati ni Saumu Rajabu kutoka Selcom.

SHINDANO la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata', limefanyika tena ikiwa ni droo ya tatu ambapo wateja wa benki hiyo wameendelea kujishindia fedha taslimu kwenye akaunti zao. Droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam imewapata washindi wengine 20 waliojishindia kiasi cha shilingi 100,000/- kila mmoja.

Akizungumza katika droo hiyo , Mtaalamu kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Florence Mchau alisema wateja wengine 20 wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja katika droo hiyo ya tatu kuchezeshwa, baada ya kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass'.

Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia kitita hicho.Aidha droo ya tatu iliyofanyika leo inakamilisha jumla ya idadi ya wateja 60 ambao hadi sasa wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja, huku ikiendeshwa kwa wazi ambapo wateja wakipigiwa simu na kujulishwa kabla ya kuingiziwa fedha walizojishindia.

Hata hivyo, aliwataka wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika. Licha ya fedha zawadi nyingine ambazo washindi watajipatia ni pamoja na simu janja za kisasa 'Samsung S9+' na mwisho washindi wengine 3 kati yao wawili kujishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai iliyolipiwa kila kitu na NMB.

Droo hiyo ikiendelea kuchezeshwa kushoto huku wakishuhudia

JAFO AINYOOSHEA KIDOLE OFISI YA TRA KIGOMA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amefadhaishwa kwa kukosekana kwa afisa wa TRA katika Kituo cha Kibiashara cha Pamoja ambacho lengo lake ni kurahisisha shughuli za kibiashara kwa wananchi wa Wilaya ya Kigoma kwa kupata huduma zote za uwezeshaji wa biashara katika eneo moja.

Licha ya kuwepo kwa kituo hicho kilichojengwa na kukamilika tangu miezi sita iliyopita lakini afisa kutoka TRA anakosekana licha ya ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Ujiji kufanya mawasiliano na TRA kwa miezi sita hadi sasa.

Kituo hicho ni miongoni mwa miradi kadhaa iliyo chini ya mradi wa Local Investment Climate(LIC) unao ratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Kutokana na hali hiyo waziri Jafo ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Kigoma kufanya ufuatiliaji wa haraka ndani ya siku nne ili kituo hicho kiweze kuwa na Wadau wote wa kutoa huduma na wananchi waweze kupata huduma ya kuanzisha na kuratibu biashara zao kwa haraka. 

Imesemekana kwamba TRA walishafika kituoni hapo na kuahidi kuleta Afisa mmoja lakini hadi leo bado jambo hilo halijafanyika hivyo kuleta usumbufu kwa wafanya biashara wanaohitaji huduma kutoka katika kituo hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alizungumza na viongozi wa Wilaya ya Kigoma ndani ya kituo cha Biashara kilichopo Wilayani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akikagua kituo cha uwezeshaji wa biashara kilichopo Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akipokea taarifa ya uendeshaji wa kituo cha biashara toka kwa watendaji wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma .

Idara ya Uhamiaji kutumia jengo jipya la Kisasa jijini Dodoma

$
0
0
Jengo la Ofisi ya Makao Makuu mpya ya Uhamiaji lililoahidiwa na Mhe. John Joseph Pombe Magufuli mapema mwaka jana alipoitembelea Idara hiyo kuzindua Pasipoti za Kielektroniki laanza kujengwa, jengo hilo jipya la ghorofa nane litakuwa Ofisi ya Makao Makuu mpya jijini Dodoma. Jengo hilo la kisasa linajengwa katika viwanja na. 18 na 19 vilivyopo Kitalu A, eneo la NCC, jijini Dodoma.

Jengo hilo lenye thamani ya Shilingi Bilioni kumi litatoa nafasi kwa huduma, na shughuli zote muhimu za kiuhamiaji kufanyika Jijini Dodoma badala ya Kurasini, jijini Dar es Salaam ambako ndiko ilikokuwa Ofisi ya Makao Makuu ya zamani ya Idara hiyo. 

“Kazi itafanywa kwa kasi na waledi, na tunaamini hakuna kikwazo chochote cha kutufanya tushindwe kufikia lengo letu kwa muda wa miezi 18 ya makubaliano na kwa viwango sahihi”, Mhandisi Ujenzi wa SUMA –JKT Ndugu Mahenge alimhakikishia Mkuu wa Kitengo cha Majenzi na Majengo, Mrakibu Mwandamizi Basil Likasi. 

Aidha, Ndugu Simon Mpyanga , Msanifu Majengo toka Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam ambao ndio wamepewa jukumu la Mshauri Mwelekezi wa Mradi huu amesema kuwa Taasisi yake ina uwezo wa kutosha kutekeleza jukumu hilo muhimu walilopewa na taifa,. 

Jengo la Makao Makuu mpya ya Uhamiaji ni miongoni mwa ahadi nyingi za Mhe. Magufuli ambazo utekelezaji wake unaendelea kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini.  
 Mtambo wa Kampuni ya SUMA-JKT ukiendelea  na kazi ya kusafisha  eneo la Mradi wa Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Makao Makuu ya Uhamiaji eneo la NCC, jijini Dodoma, ambapo kazi hii ya awali inakwenda sambamba na uwekaji wa Vifaa eneo la Mradi tayari kwa ujenzi . 
 Mkuu wa Kitengo cha Majenzi na Majengo wa Idara ya Uhamiaji (aliyeko katikati), Mrakibu Mwandamizi Basil Likasi akifurahia jambo pamoja na Wahandisi wanasimamia kazi ya kuandaa eneo la Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu mpya ya Idara ya Uhamiaji, eneo la NCC, jijini Dodoma, ambapo kazi hii ya awali inakwenda sambamba na uwekaji wa Vifaa eneo la Mradi tayari kwa ujenzi  
Wahandisi wakijadili jambo wakati wa zoezi la kusafisha  eneo la Mradi wa Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Makao Makuu ya Uhamiaji eneo la NCC, jijini Dodoma, ambapo kazi hii ya awali inakwenda sambamba na uwekaji wa Vifaa eneo la Mradi tayari kwa ujenzi .  Kutoka kushoto ni Mhandisi Umememitambo, Mkaguzi Msaidizi, Kulthum Tamba toka Uhamiaji, katikati ni Mhandisiujenzi , Mahenge kutoka SUMA-JKT, na kulia ni Msanifu Majengo, Simon Mpyanga kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.

MARUFUKU KUSAFIRISHA KAHAWA YA MAGANDA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema hakuna kahawa itakayoruhusiwa kuuzwa nje ya nchi kabla ya kukobolewa, kwa lengo la kuiongezea thamani kabla ya kuingizwa sokoni.

Pia, Waziri Mkuu ameziagiza halmashauri zinazolima kahawa nchini kuwa na kitalu chenye miche zaidi ya laki mbili ifikapo mwisho wa mwezi wa pili mwaka huu.“Wakati utakapofika uongozi wa Wizara ya Kilimo utakwenda kukagua iwapo agizo hili limetekelezwa’’.

Aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akizungumza na wadau wa kahawa wa mkoa wa Ruvuma kwenye ukumbi wa Jimboni wilayani Mbinga.Waziri Mkuu alisema kuanzia sasa kahawa yote itakayozalishwa nchini ni lazima iongezewe thamani na hakuna kahawa yenye maganda itakayoruhusiwa kuuzwa nje ya nchi.

“Hairuhusiwi kutoa kahawa nchini na kuiuza nje ya nchi ikiwa bado na maganda, ni lazima iongezewe thamani ndipo ipelekwe katika masoko ya nje ya nchi ili iuzwe kwa bei nzuri. Hatua hii itasaidia kuongeza mnyororo wa thamani na kusaidia kulinda uwekezaji wa viwanda uliofanyika nchini’’

Akizungumzia kuhusu madeni ya wakulima, aliagiza watendaji wote wa AMCOS waliohusika watafutwe na walipe deni. “Kwa sasa Serikali haina taratibu za kununua madeni ya chama chochote cha ushirika. Kuendelea na utaratibu huo kunachochea viongozi wa ushirika kufuja mali za ushirika. Lazima watambue ukifuja fedha za wanaushirika , Serikali iko na wewe.”

Alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haitorudi nyuma katika msimamo wake wa kuwasimamia wakulima nchini ili nao waweze kunufaika na kazi kubwa wanazofanya.
Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaagiza viongozi wa AMCOS wahakikishe wakulima wote wanasajiliwa na taarifa zao ikiwemo ukubwa wa mashamba,kiasi cha uzalishaji na mahali walipo zinatunzwa vizuri katika kompyuta.

Pia, Waziri Mkuu alimuagiza Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Ruvuma akague AMCOS zote na kujiridhisha kama ziko hai na kwenye tatizo la uongozi aitishe uchaguzi.Wakati huo huo, Waziri Mkuu alisema minada yote ya kahawa itafanyika kwenye maeneo yanayolima ambayo yamegawanywa kwa kanda 1.Moshi (Kilimanjaro,Arusha,Tanga,Manyara) 2. Kagera ( Kigoma, Geita, Kagera, Mara) 3. Songwe ( Rukwa,Mbeya,Iringa,Katavi), na Mkoa wa Ruvuma utafanyika Mbinga 

Alisema lengo ya kufanya minada hiyo katika maeneo yanayolima kahawa ni kuongeza uwazi katika biashara hiyo na kuwawezesha wakulima kujua bei ya mnada na kulipwa kwa wakati. Mkulima anaruhusiwa kupeleka kahawa katika mnada wowote nchini ilimradi azingatie sheria na taratibu husika .“Kila kanda inayolima kahawa nchini itakuwa na maeneo yake ya kuuzia kahawa na kahawa ya Mbinga itauzwa katika minada itakayofanyika Mbinga na bei kila mtu ataijua siku hiyo.”

Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuimarisha kilimo cha zao la kahawa ili kila mmoja anayehusika na zao hilo akiwemo mkulima aweze kunufaika na kuongeza tija.Kwa upande wao, wadau walifurahishwa na uamuzi wa Serikali wa kulisimamia zao kwa ukaribu na hasa baada ya kutangaza minada yote ya kahawa kufanyika katika maeneo yao na kwa uwazi.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JANUARI 5, 2019.
 Baadhi ya wadau wa zao la kahawa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, Janujari 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wadau wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, Januari 4, 2019.   Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wadau wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, Januari 4, 2019. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MOFUGA AZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO MBULU

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Mofuga amezindua ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo kwa kwa kuwataka watumishi wanaosimamia zoezi hilo kutowapa usajili wafanyabiashara wakubwa.

Wafanyabiashara wadogo 5,000 wanatarajia kupata vitambulisho hivyo wilayani Mbulu ambapo kwa kuanzia wamegawa vitambulisho 1,008 kati ya 2,500 vinavyotolewa kwa awamu ya kwanza.

Mkuu wa wilaya ya hiyo, Chelestino Mofuga aliyasema hayo wakati akizindua zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo wa Mbulu mjini, Haydom na Dongobesh. Mofuga aliwaagiza mkurugenzi wa mji wa Mbulu, Anna Mbogo na mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Hudson Kamoga kuhakikisha zoezi hilo linawanufaisha wahusika pekee.

Alisema zoezi hilo linapaswa kufanyika kwa umakini mno ili kuepuka kuwasajili wafanyabiashara wakubwa jambo linaloweza kushusha mapato ya serikali. "Msikiuke maagizo ya Rais John Magufuli aliyotoa wakati anakabidhi vitambulisho hivi aliagiza viwanufaishe wafanyabiashara ambao mauzo yao hayazidi sh4 milioni kwa mwaka," alisema Mofuga.

Aliwaagiza wafanyabiashara wote wenye mauzo zaidi ya sh4 kwa mwaka wasajiliwe katika mfumo wa kawaida wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) wilayani Mbulu. Alisema wafanyabiashara wadogo wanatakiwa kunufaika na zoezi hilo ni wale wanaopata sh11,000 kwa siku sawa na sh330,000 kwa mwezi na siyo vinginevyo.

Mmoja kati ya wafanyabiashara wadogo wa Haydom waliopata vitambulisho hivyo, Evarest Mao aliishukuru serikali kwa kuwapatia vitambulisho hivyo kwani imewatambua. "Serikali imetambua jitihada zetu sisi wamachinga, washona viatu, baba na mama lishe na tunaahidi kuongeza juhudi katika kutimiza wajibu wetu," amesema Mao.

Mfanyabiashara mwingine James Boay alisema alidhani vitambulisho hivyo watapatiwa wafanyabiashara wakubwa lakini imekuwa tofauti. "Serikali imeangalia walengwa japokuwa wafanyabiashara wengine wadogo hawajapata kutokana na wingi wao ila kwa hakika hakuna upendeleo," alisema Boay.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Simbalimile Mofuga akipeana mkono baada ya kumkabidhi kitambulisho mfanyabiashara wa mji mdogo wa Haydom, James Boay. 
 Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Simbalimile Mofuga akiongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na wasimamizi wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Simbalimile Mofuga akizungumza na wafanyabiashara wadogo watakaopatiwa vitambulisho vinavyotolewa na Rais John Magufuli.
 Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wa wilaya ya Mbulu mkoani Manyara wanatarajia kupatiwa vitambulisho vilivyotolewa na Rais John Magufuli.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images