Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

Biteko Amewataka Wachimbaji Wadogo wa Madini Kuwa Wazalendo kwa Taifa

0
0

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo alipokuwa akifungua mafunzo ya namna bora ya uchimbaji yanayotolewa kwa wachimbaji wadogo yenye lengo la kuboresha uchimbaji wao ili kuwaletea tija.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Umma. Wa pili ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico, Kanali Sylvester Ghulika na wan ne kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Fadhili Mkumba
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Umma. Pamoja na wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria mafunzo yanayotolewa na wizara ili kuboresha utendaji wao.
Wachimbaji wadogo wa madini katika mji wa Katente wakifuatilia kwa makini mafunzo juu ya uchimbaji wa madini yanayoendelea kutolewa na Wizara ya Madini

…………………….

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuwa wazalendo na waaminifu kwa nchi kwa kulipa kodi stahiki zinazotokana na biashara ya madini wanayoifanya.

Biteko amesema anashangazwa kuona kuwa mchango wa wachimbaji wadogo katika pato la taifa ni mdogo ilihali asilimia 96 ya shughuli za uchimbaji zinafanywa na wachimbaji wadogo na asilimia nne tu zimeshikwa na wachimbaji wakubwa na ndio wanachangia Zaidi katika ukuaji wa pato la taifa.

Biteko amebainisha kuwa hayo ni matokeo ya ukwepaji wa baadhi ya wachimbaji wadogo katika kulipa kodi stahiki zitokanazo na uchimbaji wa madini.

Ameyasema hayo leo tarehe 2 Januari, 2019 wakati akifungua rasmi mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika eneo la Katente mkoani Geita.

Akifungua mafunzo hayo, Biteko amesema, mnamo mwaka 2016 Serikali ilitenga kiasi cha dola za kimarekani 3,703,630 kwa ajili ya utafiti wa kina wa jiosayansi chini ya mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ili kuboresha maisha ya mchimbaji mdogo na kutatua changamoto zinazomkabili ikiwa ni pamoja na uzalishaji mdogo na uchimbaji usiozingatia usalama na afya kwa mchimbaji.

Biteko alibainisha kuwa kazi ya utafiti katika mji wa Katente umekamilika kama inavyoshuhudiwa kupitia mafunzo yanayotolewa kwa wachimbaji wadogo wa eneo hilo yatakayosaidia kupunguza upotevu wa muda, uharibifu wa mazingira, upotevu wa mitaji pamoja na upotevu wa madini ya dhahabu yanayotokana na uelewa wa namna ya kufanya kazi hiyo.

Aidha, Biteko alibainisha kuwa, Baada ya matokeo ya utafiti huo uliofanywa kwa ushirika baina ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (Stamico) na kubaini changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo katika kukua kiuchumi.

Kutokana na changamoto zilizobainishwa na utafiti huo, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeanza kujenga madarasa na kufunga mitambo kwa ajili ya mafunzo Zaidi na kubainisha kuwa eneo la Katente ni moja kati ya maeneo ambayo mafunzo hayo yatatolewa.

Pamoja na kupewa mafunzo hayo, Biteko amewataka wachimbaji hao kuunda vikundi na kufanya shughuli zao ndani ya vikundi ili kuirahisishia Serikali kuwatambua na kuwapa huduma stahiki zitakazowawezesha kuboresha kazi zao pamoja na afya zao.

Akizungumzia jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha sekta ya uchimbaji mdogo; Biteko alisema ni pamoja na kuendelea kutenga maeneo maalaum kwa ajili ya wachimbaji wadogo, kutoa ruzuku, kurahisisha utoaji wa leseni, pamoja na kutoa mafunzo ya mara kwa mara ili kuwapa wachimbaji wadogo uelewa katika shughuli ya uchimbaji.

Utafiti huo ulifanyika kufuatia nia na adhma ya Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Rais Dr. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanaondokana na uchimbaji usio na tija na kwenda kwenye uchimbaji utakaoongeza kiasi cha uzalishaji na baadaye kuongeza kipato kwa wachimbaji wadogo na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Huduma za Jioloji kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Maruvuko Msechu alisema mafunzo yanayofunguliwa ni matokeo ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano yenye lengo la kuhakikisha watanzania wanafaidika na uwepo wa madini nchini ili kujiondoa katika lundo la umaskini kwa kuongeza kipato na kuimarisha sekta mtambuka za uchumi.

Msechu alisema, Utafiti huo ulifanyika katika maeneo ya Ngazo, Kereza, na Katente wilayani Bukombe ukihusisha matumizi ya taaluma ya jiolojia, jiofizikia, na jiokemia ukihusisha uchukuaji wa sampuli mbalimbali za udongo na miamba.

Msechu aliongeza kwa kusema kuwa matokeo ya utafiti huo yalipelekea kufanyika kwa utafiti wa kina katika eneo la Katente, utafiti ulioanza rasmi tarehe 28 mwezi Oktoba, 2016 ambao ulipelekea jumla ya chorongo 19 za DD na 24 za RC kuchorongwa na kukusanya jumla ya sampuli 2821.

Aidha aliushukuru uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, Mkuu wa Wilaya pamoja na kamati ya ulinzi ya wilaya ya Bukombe kwa ushirikiano waliouonesha kipindi chote cha kufanya utafiti huo.

MAMBOSASA ASEMA DAR IKO SALAMA,HAKUNA 'PANYA ROAD'

0
0



Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema Jiji hilo liko shwari na hakuna tukio lolote la uvunjifu wa amani ambalo linahusishwa na uwepo wa 'Panya road'.

Akizungumza leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewahakikishia wananchi wa Jiji hilo kuwa hali ni shwari na hakuna tukio ambalo limetokea hasa kwenye siku ya mkesha wa mwakya mpya wa 2019.

"Tumeona moja ya gazeti likisema 'Panya road watikisa Dar'.Ukweli hakuna tukio limehusisha panya road siku ya mkesha wa mwaka mpya.Dar iko salama sana , hivyo taarifa hizo hazina ukweli wowote,"amesema Kamanda Mambosasa na kusisitiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum limejipanga kuhakikisha usalama upo wa kutosha.

Amefafanua katika siku ya mkesha wa mwaka mpya kulikuwa na makundi ya watu mbalimbali wakiwamo wanaosheherekea mwaka mpya,makundi ya watu waliotoka Kanisani na maeneo mengine, hata hivyo hakukuwa na tukio ambalo limefanywa na hao wanaodaiwa kuwa panya road kwani hakuna panya road .

"Tupo kwa ajili ya kuhakikisha hali ya usalama inakuwa salama,hivyo asitokee mtu mmoja kwa utashi wake awatia hofu wananchi kwa kudai kuna panya road wakati hakuna," amesema Kamanda Mambosasa na kuongeza kuwa wananchi wasiwe na hofu na kuwatataka waendelee na shughuli zao kama kawaida za ujenzi wa uchumi wao na Taifa kwa ujumla kwa mwaka huu wa 2019.

VIJANA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU

0
0

NA DENIS MLOWE, IRINGA

MWENYEKITI wa Serikali za vyuo vikuu vya Kikatoriki chini, Anord Mvamba ametoa wito kwa vijana kujenga utamaduni wa kutembelea vituo vinavyowalea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu sanjari na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo hatua itakayowasaidia kufikia malengo yao.

Ametoa rai hiyo juzi mara baada ya kujumuika pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Tosamaganga kilichoko wilaya ya Iringa mkoani Iringa wakati akiadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.

Mvamba alisema kuwa kundi la watu wasiojiweza wanahitaji kupata misaada kutoka kwa jamii inayowazunguka na hasa vijana ambao wamekuwa wakitumia sehemu ya fedha katika mambo ya starehe zaidi kuliko kuwajali yatima ili wapate furaha.

Aliongeza kuwa ni vema kuona umuhimu na haja ya kuwasaidia ili wapate faraja hivyo na katika kusherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwake ameona umuhimu kama kijana kutoa sadaka na kusheherekea na watoto ho kwa wa vitu mbalimbali vikiwemo, chumvi, sukari, sabuni na vifaa vya shule.

Mvamba ambaye pia ni rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruaha Iringa (RUCU)alisema kuwa endapo vijana wengi wakijenga tabia ya kuwatembelea watoto yatima na wanaoshi katika mazingira magumu itakuwa fursa kwao kujifunza zaidi na kuwa na moyo wa huruma katika kuwasaidia kuliko kupoteza fedha nyingi katika starehe ambazo ni za muda mfupi tofauti na kuwekeza katika watu.

Aidha ameitaka jamii kujitolea kwa dhati kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji, ikiwa pamoja na kuwatembelea ili kujenga upendo kwa makundi maalumu yenye uhitaji kwa lengo la kupunguza changamoto zinazoyakabili makundi hayo.

Kwa upande wake,Sister Helena Kihwele ni msimamizi mkuu wa kituo cha watoto Yatima cha Tosamaganga alisema kituo kina jumla ya watoto 60 ambao hawajafikisha mwezi mmoja hadi miaka sita, na kuwa changamoto kubwa ni walezi kuwasahau watoto mara baada ya kukabidhiwa kituoni hapo.

“Changamoto hii inatusumbua sana maana baadhi ya walezi hawaji kuwasalimia wala kuwachukua watoto sasa tunapata shida wakati wanapotakiwa kurudi nyumbani, maana umri wa mwisho wa kukaa kituoni hapa ni miaka 6,” alisema Kihwele

Alisema kituo kinapokea watoto wasio na mama au wenye mama ambaye ni anatatizo la akili, na kuwa baadhi ya ndugu ndiyo wamekuwa wakiwatelekeza watoto mara tu wanapowafikisha kituoni hapo.

Changamoto nyingine zinazowakabili watoto ni baadhi ya wazazi kushindwa kuwaendeleza kielimu watoto, kwani baadhi ya walezi huwa hawana mwamko wa kuwaendeleza watoto hao, na hivyo kusababisha watoto hao kutoendelea na masomo.
Mwenyekiti wa Serikali za vyuo vikuu vya Kikatoliki chini, Anord Mvamba ambaye pia ni Rais wa Serikalia ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruaha Iringa, (RUCU) akimkabidhi moja vitu mbalimbali mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Tosamaganga kilichoko wilaya ya Iringa mkoani Iringa Helena Kihwele wakati akiadhimisha siku ya kuzaliwa mwanzoni mwa ka. (picha na Denis Mlowe)

MAHAKAMA YA WATOTO KISUTU YAPOKEA MASHAURI 118 YA JINAI KWA MWAKA 2018

0
0
Katibu Mkuu Wizara yaAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) (kushoto) Dkt. John Jingu akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa kazi za Maendeleo na Ustawi wa Jamii na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Mkoa Dar es salaam (katikati) ni Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Bi. Rehema Kombe na kulia ni Afisa Ustawi wa Jamii wa mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sufiani Mdolwa.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Given Sure (kulia) akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa kazi za Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Mkoa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu (hayupo pichani) na kulia ni Afisa Ustawi wa Jamii wa mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sufiani Mdolwa. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


Kwa mwaka 2018 Mahakama ya watoto ya Kisutu ilipokea jumla ya mashauri 118 ya jinai na makosa 295 ya madai yalipokelewa na kufanyiwa kazi na matukio ya kesi za watoto yakiwa wengi wa watoto hao ni wale ambao wamekinzana na Sheria na pili ni wale ambao Sheria inawakuta na makosa.

Hayo yamebainishwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu Bi. Agness Mchome wa jijini Dar es Salaam wakati akitoa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu alipotembelea
katika Mahakama ya Watoto Kisutu jijini Dar es Salaam.

Hakimu Agness Mchome amewataka wazazi kutimiza wajibu wao wa malezi kwa watoto ili kuwaepusha na mashitaka yanayozuilika kwani watoto wanaofikishwa mahakamani ni wale ambao wazazi au walezi wao hawakutimiza wajibu wao wa kutoa malezi stahiki. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu ameridhishwa na utendaji kazi wa Mahakama ya Watoto ya Kisutu jijini Dar Es Salaam kwani imekuwa ikifanya kazi nzuri ya kusaidia kurekebisha maadili ya watoto nchini.

Dkt. Jingu amesisitiza wazazi kuzingatia malezi bora na kutoacha watoto kuangalia televisheni na mitandao ya kijamii wakati wote ambapo kwa kiasi kikubwa mitandao ya kijamii na video zisizo na maadili zinachangia kuharibu maadili ya watoto nchini.  Naye Afisa Ustawi Mwandamizi kutoka Mahakama ya Watoto ya Kisutu Bi.Asha Mbaruku ameiasa jamii kutosambaza picha za watoto waliofanyiwa vitendo vya ukatili ikiwa ni kwa mujibu wa Kifungu 158 cha Sheria ya Mtoto kinazuia utoaji wa taarifa na kusambaza picha za mtoto aliyeumizwa au kufa.

Wakati huo huo Katibu Mkuu Dkt. Jingu alitembelea Kituo cha Kutoa Huduma cha Mkono kwa Mkono ( One Stop Centre) kilichopo katika Hospitali ya Aman jijini Dare es Salaam na kuridhishwa na huduma inayotolewa kituoni hapo. Dkt Jingu aliongeza kuwa vitendo vya ukatili vimekuwa vikishamiri sana nchini kwa kipindi cha hivi karibuni hivyo uwepo wa vituo vya kutoa Huduma ya Mkono kwa mkono (One Stop Centre) nchini utasaidia kuwapatia huduma waathirika wa vitendo vya ukatili.

Ameongeza kuwa ukatili unaofanyika kwenye familia ni unasikitisha hivyo kituo cha huduma ya mkono kwa mkono kitasaidia kutoa mchango katika kunusuru waathirika wa ukatili na amewasisitiza wazazi kutimiza wajibu wao wa malezi kwa watoto na na kuhamasisha jamii kuachana na tabia potofu ya mmomonyoko wa maadili. “Nimeridhishwa na kazi inayofanywa na kituo katika kuwapokea na kuwafanyia uchunguzi watoto na wanawake waliofanyiwa ukatili wa kijinsia, kuwa kubaini kiini cha ukatili na kutoa huduma stahiki kwa wahanga” alisema Dkt. Jingu

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Suphian Mndolwa ameeleza kuwa kituo hicho ni miongoni mwa vituo vinavyotoa huduma bora katika utetezi wa ulinzi na usalama wa watoto
na wanawake nchini.

DC MUHEZA:NITASHIRIKIANA NA WANAMICHEZO KUHAKIKISHA TUNAPATA TIMU YA LIGI KUU

0
0

MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifunga Mashindano ya Kombe la Kabunda Cup

MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Kabunda Cup Nahodha wa timu ya Ushirika Amiri Nko kushoto ni Afisa Michezo wa wilaya ya Muheza Anania Sama
Nahodha wa timu ya Ushirika Amiri Nkoa akiwa ameinua kombe hilo juu mara baada ya kukabidhiwa
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi Kitita cha Milioni moja Nahodha wa timu ya Ushirika Amiri Nko baada ya timu yao kuibuka na ushindi kwenye michuano ya Kombe la Kabunda Cup kushoto ni Afisa Michezo wa wilaya ya Muheza Anania Sama

Katibu Msaidizi wa Kamati ya Mashindano hayo akisoma risala
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji
Sehemu ya Mashabiki wa soka wakiwa wamnefuatilia mchezo huo














MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mwanasha Tumbo amesema atashirikiana na wanamichezo ili kuhakikisha wanaweza mazingira mazuri yatakayowezesha kupatikana timu ambayo itaweza kushiriki ligi madaraja ya juu ikiwemo Ligi kuu.

Mwanasha aliyasema hayo wakati fainali michuano ya kombe la Kabunda Cup iliyokuwa ikichezwa kwenye viwanja vya Vikonge Mtindiro wilayani Muheza ambapo alisema ili kuweza kuhakikisha wanafanikisha jambo hilo wataendelea kuhamasisha vijana kujikita kwenye michezo.

Alisema licha ya kuhamasisha michezo kutokana na kwamba ni ajira ambayo inaweza kuwainua vijana kuichumi na kupata maendeleo lakini pia aliwahaidi kuwajengea kiwanja cha mpira chenye matofali ili waweze kuonyesha umahiri wao na hatimaye wilaya hiyo iweze kupata mafanikio kwenye soka.

“Leo nimekuja hapa kuhimitisha Ligi hii kwanza nimefurahishwa sana na viwango ambavyo mmekuwa mkivionyesha kwenye mchezo huu nimeongeza na Diwani wenu hapa na niwahaidi kwamba nitawajengea kiwanja chenye matofali ili hari ya kushiriki kwenye michezo muweza kuendelea nayo na tunaamini siku zijazo tutairudisha Muheza kwenye ramani ya soka “Alisema DC Mwanasha.

Alisema kwamba anafanya hivyo ili kuweza kuchochea maendeleo ya mchezo huo ambao vijana wakiweka bidii na nia wanaweza kufika mbali ikiwemo kuitangaza wilaya hiyo lakini pia kupata manufaa kama walivyokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Awali akizungumza katika fainali hiyo Katibu Msaidizi wa Kamati ya Mashindano hayo Salehe Mwinjuma alisema lengo la mashindano hayo yalikuwa ni kuweza kuinua vipaji vya wachezaji wachanga kwenye Kata hiyo yaliyoanzishwa na mdau wa michezo Seif Kabunda kwa kushirikisha timu 20 zilizocheza kwa mtindo wa makundi.

Alisema kwamba msimu ujao ligi hiyo itakuwa na mabadiliko makubwa kutokana na mdhamini wa mashindano hayo kuamua kujipanga upya na kuja kinyengine lengo kubwa likiwa kuhakikisha michezo inapata mafanikio.

Katika fainali hiyo timu ya Ushirika FC waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Kabunda Cup baada ya kuibamiza Kwarabuye FC mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Vikonge Mtindiro na kujiny’akulia kombe na kitita cha sh.milioni moja . Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na wenye ushindani mkubwa uliohudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo ambaye ndie alikabidhi zawadi kwa washindi kwenye michuano hiyo.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAUNGANA NA WATUMISHI DAR KUMPONGEZA RAIS DKTMAGUFULI

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva (aliyesimama) ambae ni mgeni rasmi katika maandamano ya kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kulipatia ufumbuzi suala la kikokotoo kwa ajili ya mafao ya watumishi wastaafu mapema leo asubuhi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.)

Watumishi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiingia kwa maandamano katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kulipatia ufumbuzi suala la kikokotoo kwa ajili ya mafao ya watumishi wastaafu, mapema leo asubuhi tarehe 03/01/2018. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.)
Bango la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaloonesha pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kulipatia ufumbuzi suala la kikokotoo kwa ajili ya mafao ya watumishi wastaafu mapema leo asubuhi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji).

Jafo apongeza Ujenzi Ofisi za Halmashauri-KIBITI

0
0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(katikati) akitoa maelekezo wakati akikagua ujenzi wa Ofisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo aKiwa na viongozi wa Wilaya ya Kibiti wakati wa ziara yake Wilayani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(katikati) akitoa maelekezo wakati akikagua ujenzi wa Ofisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.


Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti linaloendelea kujengwa.

……………………………………………………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Kibiti kwa Ujenzi mzuri wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya Kibiti mradi unao tarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu.

Waziri Jafo alitoa pongezi hizo Leo hii alipokuwa katika ziara ya kikazi Wilayani Kibiti Mkoani Pwani. Ujenzi huo unaojengwa na mkandarasi SUMAJKT chini ya Mshauri Chuo Kikuu cha Ardhi umemridhisha sana Waziri Jafo kutokana na kuzingatiwa kwa viwango vya ubora katika ujenzi huo. Hata hivyo Jafo ameagiza kuongezwa kwa kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kabla ya mwezi Julai, 2019.

Katika ziara hiyo ya kikazi wilayani Kibiti Waziri Jafo alifanikiwa kutembelea mradi huo pamoja na mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Kivinja “A” ambao unagharimu shilingi milioni 400. Katika kuhitimisha ziara yake wilayani humo waziri Jafo ameutaka uongozi wa wilaya hiyo kutumia fursa waliyonayo ya tofali nzuri zenye ubora zinazo zalishwa na SUMAJKT katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo wameshapokea shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe. Seif Ungando ameishukuru sana Serikali ya DKT. John Pombe Joseph Magufuli kwa msaada mkubwa wa miradi ya maendeleo inayo elekezwa wilayani Kibiti

UCSAF YALETA CHANGAMOTO CHANYA KWA KAMPUNI ZA SIMU ZA MKONONI

0
0
Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Albert Richard amemweleza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kuwa UCSAF imeleta changamoto chanya kwa kampuni za simu za mkononi zinazotoa huduma za mawasiliano nchini
Richard ameyasema hayo wakati wa ziara ya Nditiye ya kukagua changamoto za mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali wilayani Sengerema mkoani Mwanza.  Richard amefafanua kuwa awali kampuni za simu za mkononi nchini zilisita kuwekeza kwenye vijiji mbali mbali ambavyo havina mawasiliano nchini kwa kuwa havina mvuto wa kibiashara ambapo kampuni hizo zilikuwa zinakwenda maeneo ya mijini yenye mvuto wa kibiashara
“Ila sasa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano tunashirikiana na kampuni za simu za mkononi kufikisha huduma za mawasiliano vijijini na kampuni zimepata mwako,” amesema Richard. Ameongeza kuwa Serikali imekuwa inatoa ruzuku kwa kampuni hizo ili waweze kujenga minara kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za mawasiliano
Nditiye amesema kuwa amefanya ziara ya siku tatu ya kukagua mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali wilayani Sengerema ili kuona changamoto za mawasiliano ambapo amekiri uwepo wa changamoto za mawasiliano kwenye Wilaya hiyo kwenye baadhi ya kata ambapo ina jumla ya kata 21 na kubaini uwepo wa ukosefu wa mawasiliano kabisa kwenye baadhi ya maeneo, mawasiliano ya kusuasua na mahitaji ya kuongeza nguvu ya usikivu wa mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) akisikiliza kwa makini taarifa kutoka kwa Afisa Mtendaji Kata ya Katwe, Wilaya ya Sengerema, Mwanza, Deus Ngodagula Masasi (aliyenyoosha kidole) kuhusu ukosefu wa mawasiliano kwenye kisiwa cha Maisome wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya mawasiliano wilayani humo. Naibu Katibu Mkuu – Sekta ya Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (aliyeshika ramani) akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji, UCSAF, Mhandisi Albert Richard (wa kwanza kushoto).
Naibu Katibu Mkuu – Wizara Ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (aliyeinua mkono) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua changamoto ya mawasiliano kisiwani Maisome, Mwanza. Anayesikiliza wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt. Jones Kilimbe.
Diwani wa Kata ya Bangwe, wilayani Sengerema, Mwanza, Yonas Magikulu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya mawasiliano Wilayani humo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara Ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi.



DAWASA YAKABIDHIWA JENGO, WATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa DAWASA kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa machache.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akisaini mkataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni kulia ni mmoja ya wajenzi wa kampuni ya CCECC ambao ndiyo wakandarasi. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akisaini mkataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni kulia ni mmoja ya mkandarasi msahauri wa jengo hilo. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akimkabidhi makataba wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto).Wafanyakazi wa DAWASA na wageni waalikwa wakifuatiliwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage (anayefuata kushoto) wakifurahi pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) mara baada ya kuzindua picha ya jengo la Maji linalotarajiwa kumalizika Februari 2020.
Muonekano wa jengo la Maji litakalohamishiwa ofisi za DAWASA mara baada ya kumalizika.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kusimamia miradi ya maji kwa umakini mkubwa. Amewataka DAWASA kuhakikisha kufikia 2020 asilimia 85 ya vijijini na asilimia 95 ya mijini inapata maji safi na salama. 

Mkumbo amesema hayo wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya jengo la Maji lililopo Ubungo jijini Dar es Salaama na linalotarajiwa kumalizaika Februari 2020. Utiaji wa saini hiyo ulihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja. Akizungumza baada ya utiaji wa saini, Mkumbo amesema DAWASA lazima wahakikishe wanasimamia mapato ili kuweza kuendeleza miradi ya maji ili wananchi waweze kufaidika. 

 Amesema, hafla ya leo sio ya kukabidhiwa jengo tu ila wanatakiwa kusimamia mradi wa Kidunda, visima vya Kimbiji Mpera pamoja na kuwaunganishia wateja wapya. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi Mwamunyage amesema changamoto kubwa iliyokuwepo katika mamlaka hiyo ni maeneo ya kufanyia kazi ila baada ya kukabidhiwa jengo hilo wanaamini kwa sasa kazi zitafanyika kwa wakati. 

Amesema, kwa sasa DAWASA wanajiendesha wenyewe kwa mapato ya ndani na watasimamia mpaka kumalizika Februari 2020. Naye Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Luhemeja amewashukuru Wizara kwa kuwakabidhi jengo hilo lenye ghorofa 15 kwa ajili ya kuweka ofisi na itawasadia kufanya kazi kwa uharaka zaidi na ameahidi kuwa jengo hilo litakamilika kwa wakati kwani tayari ameshamuagiza Mkurugenzi wa Fedha kuanza kufanya malipo. 

 Pia ameeleza kuwa kwa sasa DAWASA ndani ya miezi mitatu wameweza kufikia malengo ya kufikia Bilioni 10 kwa mwezi katika ukusanyaji wa maji ila wamejizatiti kwa mwaka huu kufikia malengo ya serikali ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini kabla ya 2020 ikiwemo na kupunguza mivujo kwa asilimia 25.

WAZIRI WA UTALII AFUNGUA NYUMBA YA WALIMU ZANZIBAR

0
0


Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akiwa pamoja na Mshirika wa Maendeleo Mkurugenzi Mkuu wa DSTV Jacqueline Woiso wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
????????????????????????????????????
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo kushoto akimkabidhi Mshirika wa Maendeleo Mkurugenzi Mkuu wa DSTV Jacqueline Woiso zawadi ya Cheti maalum katika ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
????????????????????????????????????
Nyumba ya Walimu wa Skuli ya Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja iliofunguliwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya mapinduzi ya Zanzibar.
????????????????????????????????????
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na Mshirika wa Maendeleo Mkurugenzi Mkuu wa DSTV Jacqueline Woiso mara baada ya kuwasili katika Ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar
????????????????????????????????????
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo kushoto akimkabidhi Mshirika wa Maendeleo Mkurugenzi Mkuu wa DSTV Jacqueline Woiso zawadi ya Cheti maalum katika ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
????????????????????????????????????
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akitoa hotuba ya ufunguzi wa Nyumba ya Walimu katika ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akitoa hotuba ya ufunguzi wa Nyumba ya Walimu katika ufunguzi wa Nyumba ya Walimu Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amefungua mradi wa maghala ya kuhifadhi nafaka na soko la mazao la OTC-Lilambo katika Halmashauri ya Songea uliogharimu sh. bilioni 1.5.

Amesema Rais Dkt. John Magufuli ameazimia kuwawezesha wakulima kuwa na mahala pa uhakika pa kuhifadhia mazao yao na sehemu ya kufanyia biashara ili kuwaongezea tija.Amefungua soko hilo leo (Alhamisi, Januari 3, 2019) akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Ruvuma.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ujenzi wa soko hilo pamoja na maghala kwani umezingatia viwango. Maghala hayo mawili yana uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 za nafaka.“Licha ya soko hili kuwapa wakulima wetu fursa ya kupata masoko ya kuuzia mazao yao, pia watapata mafunzo ya namna ya kuhifadhi bidhaa zao pamoja na taarifa za masoko.”Kadhalika, Waziri Mkuu ameiagiza bodi ya soko hilo kuhakikisha inatoa matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari ili wakulima waweze kupeleka mazao yao sokoni hapo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka wananchi kutumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha nchini kuandaa mashamba, kupanda mazao mbalimbali ya chakula na biashara.“Nawaagiza viongozi wa kata na vijiji hakikisheni wananchi katika maeneo yenu wanaandaa mashamba na kupanda kwa wakati, tunataka tuwe na chakula cha kutosha na ziada tuuze.”Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songea, Martin Mtani ameiomba Serikali iwapatie mashine itakayowawezesha kupanga madaraja ya mazao ya nafaka mbalimbali.

Mkurugenzi huyo ameomba soko hilo liwekwe kwenye mpango wa kujengewa vihenge vyenye uwezo wa kukausha mazao kwa viwango vya kimataifa ili kutatua tatizo la unyaufu.Pia Mkurugenzi huyo ameiomba Serikali iwasaidie katika kuliunganisha soko hilo na TMX ili waweze kuuza mazao ya nafaka ndani na nje ya nchi .Ufunguzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga.

Wengine ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na maafisa wengine wa Serikali.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,AHAMISI, JANUARI 3, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua  Soko la Mazao   la OTC Lilambo  wilayani Songea Januari 3, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, Watatu kushoto ni Waziri wa kilimo, Japhet Hasunga, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Jacqueline Ngonyani Msongozi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua  Soko la Mazao   la OTC Lilambo  wilayani Songea Januari 3, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, Kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro,  wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali vilitokana na unga wa mhogo vilivyoandaliwa na kikundi cha wanamawake wajasiriamali cha  Muungano - Mpandagindo,   wakati lipofungua  Soko la Mazao la OTC Lilambo wilayani Songea, Januari 3, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 5000 za nafaka  la OTC Lilambo wilayani Songea ambalo lilifunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Januari 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali  vilivyoandaliwa na kufungashwa kitaalam  na Mtandao wa Wajsiriamali Wadogowadogo Ruvuma (MWARU) wakati alipofungua  Soko la Mazao la OTC Lilambo wilayani  Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Mtandao wa MWARU, Lucida Chowo (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KATIBU MKUU WA CCM DKT. BASHIRU ALLY ATEMBELEA KABURI LA BABA WA TAIFA MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE

0
0
Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally amepokelewa Mkoa wa Mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera .Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally atafanya ziara ya siku mbili kuimarisha Chama Mkoa wa Mara ikiwa ni pamoja na kutembelea Wilaya ya Butiama alikozikwa mwasisi wetu Mwl. Julius kambarage Nyerere .Aidha, Ndg. Bashiru Ally amesema katika ziara yake hii ni kukijenga chama nakukiimarisha katika Misingi iliyowekwa na Mwasisi wetu Mwl.Nyerere
Ndg. Bashiru Ally ameyasema hayo Mbele ya wananchi na viongozi wa Chama na serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Ndg. Samweli Kiboye (namba 3) wakikagua kituo cha Afya jimbo la Bunda

Katika ziara hiyo ameshiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Butiama. Katika kikao hicho Dkt.Bashiru Ally ametoa salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh. John Pombe Magufuli kwa wana Mara na kuwambia anawahakikishia kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Mkoa na Uwanja wa ndege wa kisasa Musoma itatekelezwa.
Katibu Mkuu wa CCM amehitimisha kikao hicho kwa kusisitiza Umoja kwa watumishi wa Chama na Serikali, kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendeleza misingi iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Huu ni Mwendelezo Wa Uimarishaji wa Chama Cha Mapinduzi kanda ya ziwa

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 4,2019

0
0











WANANCHI OLDONYOWASI WACHANGIA SEKTA YA ELIMU

0
0
Na Imma Msumba Arumeru

Wananchi wa Kata ya Oldonyowasi Wilayani Arumeru wameitikia wito wa serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuchangia miradi ya maendeleo kwa kuchanga zaidi ya sh. milioni 22.8 ili kuondoa adha ya watoto wao kutembea umbali mrefu kusaka elimu. 

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Cornel Muro pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC, Dkt. Wilson Mahera katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana wilayani Arumeru.

Pongezi za Wananchi hao zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye yupo katika ziara Wilayani Arumeru baada ya kujionea changamoto za upungufu wa madarasa sambamba na kuzitatua ili Januari saba mwaka 2019 wanafunzi hao waweze kuingia madarasani kuanza masomo yao ya kidato cha kwanza. 

Rc Gambo alisema juhudi walizozifanya wananchi hao wa Kata ya Oldonyowasi zinapaswa kuigwa na wananchi wengine kwani wamejitolea nguvu kazi watu pamoja ni fedha za wadau wa maendeleo ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) waliotoa sh. milioni 237 pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) waliotoa sh. milioni 30, akiwemo mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Aminah Mollel kutoa mifuko kadhaa ya saruji huku Halmashauri ya Arusha Dc ikitoa sh. milioni 20.

Alisema tayari ameshaandika barua Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kwaajili ya kuomba usajili kwa shule kadhaa za Mkoa wa Arusha ikiwemo shule hiyo ya Oldonyowasi ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma badala ya kukaa nyumbani wakisubiri usajili wa shule huku wakikosa vipindi madarasani. 

"Nawapongeza kwa ushirikiano kati ya DC Muro na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dc Dkt. Wilson Mahera pamoja na wananchi ambao mnajitajidi kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa kujenga madarasa naomba ushirikiano huu udumu zaidi ili wananchi mfaidi matunda ya elimu bure "

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Ndugu Jerry Cornel Muro amempongeza Rc Gambo kwa kuhakikisha shule hiyo inapata usaili na kusisitiza kuwa shule hiyo itakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita ili watoto wa Kata hiyo na kata nyingine za Jirani waweze kupata elimu. 

Awali Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari, Nelson Saro alisema halmashauri ya Arusha Dc wanafunzi 6,846 walifaulu wakiwemo wasichana 3,884 na wavulana 2,962.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro wakiwa wameambatana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wakikagua madarasa Wilayani Arumeru.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Mashaka Gambo Akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Cornel Muro wakiwa katika moja ya shule walizozitembelea kukagua ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Arusha Dc Wilayani Arumeru

HALOTEL KULIAMSHA DUDE MBAGALA KWA SHUKRANI CONCERT

0
0


Pata punguzo na unufaike kwa kuwa mteja wa akaunti ya muda maaulum

0
0
NOTES ON FIXED ACCOUNT.

·        Pata punguzo na unufaike kwa kuwa mteja wa akaunti ya muda maaulum
·        Riba hadi asilimia 12 kwa mwaka kwa mteja mwenye amana ya kuanzia Milioni 5 kwa kipindi cha miaka miwili na kuendelea
·        Ni fursa nzuri kwa Mstaafu  anayepokea pensheni yake badala ya kununua gari alipendalo awekeze TPB Bank
·        Mtu yeyote anaweza akafungua akaunti hii na kuwekeza
·        Riba inalipwa kila baada ya mwezi, miezi mitatu mpaka sita kulingana na matakwa ya mteja.

GROUP ACCOUNT
Katika kutambua uwepo wa makundi mbali mbali ya watu, kujali mahitaji yao ya huduma za kifedha na adha wanazozipata katika kupata huduma za kibenki, TPB Bank ina akaunti maalum kwa vikundi.  Vikundi rasmi na visivyo rasmi.

Vikundi kama vile, vikundi vya wafanyakazi, vikundi vya ndugu, vilabu vya michezo mbali mbali, wasuka nywele, wasuka mikeka, wavuvi, mafundi seremala, vikundi vya kidini, vikundi vya sehemu ya kazi n.k.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI LUYEHELA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua tangi la maji wakati alipoweka jiwe la msingi la  Mradi wa Maji wa Luyehe katika kijiji cha Muungano Zomba kwenye jimbo la Peramiho wilayani Songea, Januari 3, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda juu tangi la Maji ili kujiridhisha kuhusu  ubora  wake wakati alipoweka jiwe la msingi la  Mradi wa Maji wa Luyehela katika kijiji cha Muungano Zomba kwenye jimbo la Peramiho wilayani Songea, Januari 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba  ndoo ya maji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, ikiwa ni ishara ya kuzindua   kituo cha kuchotea maji  katika kijiji cha  Lugagala wilayani Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kumsaidia  kubeba ndoo ya maji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, ikiwa ni ishara ya kuzindua   kituo cha kuchotea maji  katika kijiji cha  Lugagala wilayani Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba ndoo ya maji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, ikiwa ni ishara ya kuzindua  kituo cha kuchotea maji  katika kijiji cha  Lugagala wilayani Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO.

0
0
Na Yeremias Ngerangera,Namtumbo.

Mradi wa maji katika kijiji cha Likuyusekamaganga wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma umeingia dosari baada ya vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 500 vya kutekeleza mradi huo kuteketea kwa moto na watu wasiojulikana.

Mwakilishi wa kampuni ya Elegance Developers Company Ltd ya Dar es salaam inayojenga mradi huo,  fundi Ramadhan Abrahaman alisema vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 500 vimeteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana .

Kaimu Mtendaji wa kata ya Likuyuseka bwana Petro Nyoni alidai jeshi la polisi linawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo akiwemo mlinzi wa kambi bwana Ramadhani Salumu Liyoka pamoja na Athumani Awami Kimbengite .

Aidha bwana nyoni alisema Serikali ya kijiji inatarajia kufanya kikao cha kulijadili swala hilo pamoja na baraza la wazee wa kijiji hicho nao wanatarajia kufanya kikao cha kujadili mienendo mibaya ya kijiji hicho ,kubaini chanzo cha kuibuka kwa matukio mabaya kijijini hapo na kutafuta njia sahihi za kutatua au kudhibiti matukio mabaya yasiendelee kutokea kijijin hapo.

Mhandisi mshauri bwana Nashoni Charles kutoka kampuni ya Norplan Tanzania Ltd ya Dar es salaam alisema kitendo cha kuchoma vifaa hivyo kimeiingizia hasara kampuni lakini pia kitafanya kampuni hiyo kutumia muda mwingine kwenda kununua vifaa , huku muda wa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo upo palepale.

Kwa mujibu wa mhandisi mshauri wa kampuni hiyo bwana Nashon alidai mradi huo wa maji wa Likuyumandela umefikia asilimia 45 katika utekelezaji wake na unategemea kuhudumia watu 13,319 kwa kipindi cha miaka kumi baada ya kukamilika kwake.

Kaimu Mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Salumu Nachundu alidai mradi unatekelezwa chini ya progamu ya maendeleo ya sekta ya maji (WSDP)kupitia program ndogo ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RWSSP)

Gharama za ujenzi wa mradi huo ni shilingi 4,915,864,910 ikiwa mkataba wa mradi huo unategemea kukamilika tarehe 16 marchi 2019 na kiasi cha shilingi 983,172,982 zimelipwa kwa mkandarasi kama malipo ya awali.
 Baadhi ya vifaa vilivyoteketezwa kwa moto na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana 
Baadhi ya Mabomba ya kupitishia maji yakiwa yamechomwa moto na watu wasiojulikana.

TANZIA

0
0

 Ndugu isaac zumba wa ngarenaro, arusha. Anatangaza kifo cha mke wake amabilis zumba kilichotokea jana katika hospitali ya taifa ya muhimbili. Mwili unategemewa kuagwa kesho ijumaa saa sita mchana, muhimbili hospital-katoliki, na baada ya hapo  kuelekea Arusha kwa ajili ya mazishi siku ya Jumanne tar 8 january. Salaam ziwafikie ndugu wote wa  koo za Zumba na Mumba waishio ndani na nje ya nchi.

WAZIRI MAKAMBA AONGOZA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KATIKA MJI WA SERIKALI

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo ameongoza watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kupanda miti zaidi ya elfu moja (1000) katika eneo la Mji wa Serikali, inapojengwa Ofisi ya Makamu wa Rais.

Waziri Makamba amesisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu na takribani miti 1000 ya aina ya mdodoma inayostahimili ukame imepandwa hii leo. “Sisi ni watu wa Mazingira, ni lazima tuonyeshe mfano, hapa kila mtumishi atakuwa na wajibu wa kutunza miti atakayokabidhiwa na kuhakikisha inakua” Makamba alisisitiza.

Waziri Makamba amesema kuwa Jiji la Dodoma linakabiliwa na changamoto ya mandhari kutokana na ardhi yake kuwa kame na kupelekea uoto wa asili kupungua kwa kiasi kikubwa. Hivyo, ametoa wito kwa kila taasisi na Idara kuunga mkono kwa vitendo kampeni iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Novemba 2017 ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani, kwa kupanda miti kwa wingi katika Mji wa Serikali na Dodoma kwa ujumla ili uwe mji wa mfano kwa kuwa na mandhari yakuvutia.

“Kwa kuwa sisi ndio wasimamizi wa Mazingira, upandaji na usimamizi wa miti ni sehemu ya Hifadhi ya Mazingira, hivyo lengo la Ofisi yetu ni kuonyesha mfano, watumishi wote kuanzia Waziri mpaka Mhudumu kila mmoja atakuwa na miti yake ya kutunza na kuhakikisha inakua” Makamba alisisitiza.

Awali Waziri Makamba alipata fursa ya kutembelea eneo inapojengwa Ofisi ya Makamu wa Rais na kuridhishwa na kasi ya ujenzi katika eneo hilo na kumtaka Mkandarasi wa Mradi kutoka (Vikosi vya Ujenzi) Mhandisi Simeo Machibya kukamilisha kazi yote kwa wakati. “Ujenzi huu ufanyike usiku na mchana” Makamba alisisitiza.

Katika zoezi la leo Waziri Makamba ameambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo, Naibu Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali kutoka kwa Mhandisi Simeo Machibya ambae ni Meneja Msimamizi wa Mradi kutoka Vikosi vya Ujenzi. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizindua zoezi la upandaji miti katika mji wa Serikali Dodoma. Miti 800 aina ya “midodoma” imepandwa katika eneo hilo na miti 200 ya aina nyingine pia imepandwa ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani. Kulia ni Bw. Timothy Mande Afisa Misitu kutoka Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images