Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46317 articles
Browse latest View live

DULLA MBABE-MABONDIA WOTE WAKUBWA TANZANIA NIMEWAPIGA,CHEKA ALIZIMA PALE ULINGONI


TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2018 NA MATOKEO YA DARASA LA NNE 2018

DC JOKATE AANZA MCHAKATO WA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASIRIAMALI WADOGO KISARAWE

MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA MBINGA - MBAMBA BAY

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Mbunge wa Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga- Mbamba bay kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 66, Januari 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya CHICCO kutoka China inayojenga barabara ya Mbinga – Mbamba bay  kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa Kilomita 66 wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, Januari  4, 2019. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,  Christina Mndeme.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  viongozi wa Mkoa wa Ruvuma na wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya CHICCO kutoka China inayojenga barabara ya Mbinga – Mbamba bay yenye urefu wa Kilomita 66 wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, Januari 4, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi  wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga – Mbamba bay kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 66 unaofanywa na Kampuni  kutoka China ya CHICCO, Januari 5, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu wa Jimbo la Mbinga,  John Ndimbo wakati alipowasili kwenye kijiji cha Nyoni wilayani Mbinga kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 4, 2019. Kulia ni Sheikh wa wilaya ya Mbinga, Said Majid.

WAZIRI MBARAWA ASHIRIKI UPANDAJI MITI 15,000 CHANZO CHA MTO RUVU

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa ameshiriki zoezi la upandaji wa miti 12,000 katika bonde la Mto Ruvu kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji.

Zoezi hilo limesimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na wafanyakazi wote wa Mamlaka hiyo kutoka Mikoa mbalimbali kushiriki katika mitambo ya Ruvu Chini.

Akizungumza baada ya kumaliza kupanda miti, Prof Makame amesema elimu waliyoitoa kwa wananchi ya kukaa umbali wa mita 60 kutoka vyanzo vya maji haitoshi bali wanatakiwa kushirikishwa katika kuvilinda na kuacha kufanya shughuli za kijamii.

Mbarawa amesema, lengo la Wizara ni kuona vyanzo vya maji na kampeni hii iendelee kwenye vyanzo vyote vya maji ili kufikia malengo ya Serikali kufika 2020 asilimia 95 ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kupata maji safi na salama.

Mbali na hilo,Prof Mbarawa ameitaka mamlaka hiyo kutafuta ufumbuzi wa haraka wa Ukadiriaji wa ankara za maji usio na uwiano na kurekebisha dosari mbalimbali zinazoiyumbisha ikiwamo upotevu mkubwa wa maji, ufinyu wa mapato na urasimu wa utoaji huduma.

Mbarawa alisema haridhishwi na utendaji wa Kitengo cha Masoko cha Dawasa na kumekuwapo na malalamiko kwa wateja wanaokadiriwa ankara kubwa na wapo wengine wanaotumia kiasi kikubwa cha maji hasa taasisi na makampuni huku wakilipa ankara ndogo hali inayoisababishia hasara Dawasa.

"Idara ya masoko na biashara nataka ibadilike nataka waone kwamba wakiona tatizo lolote kwenye mfumo wao wa kompyuta waweze kujua pale kuna shida," alisema Mbarawa.Alisema kutokana na hali hiyo, kitaanzishwa kitengo cha Udhibiti wa mapato (Revenue Investigation Unit) kitakachoshughulikia changamoto hiyo.

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema lengo la mamlaka hiyo ni kupanda miti 100,000 ila kwa leo wameweza kupanda miti 12,000 ingawa awali walishapanda miti 3000 .Amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika chanzo cha Mto Ruvu kwa wananchi kufanya shughuli za kijamii na tumeanzia hapa ila tutaenda hadi Morogoro unapoanzia Mto Ruvu

Akizungumzia upotevu wa mapato, Luhemeja amekiri kuwapo kwa tatizo hilo ambalo hasa linajitokeza kwenye taasisi na kampuni kubwa."Tunachangamoto ya makusanyo lakini kwa maana yakuongeza nguvu tunakwenda kuwa na kitengo maalumu cha uchunguzi ambacho kazi yake kubwa ni kuchunguza mapato yote ya ndani pamoja na matumizi yake," alisema.

Alisema kitengo hicho kitaanza kazi wiki ijayo na kwamba lengo kubwa ni kuhakikisha mamlaka inapata pesa ili kufikia asilimia 95 ya usambazaji maji ifikapo 2020.Kwenye mpango huo, jumla ya miti 15,000 ilipandwa huku lengo likiwa ni kufikia miti 100,000 kwenye vyanzo vyote vya maji vya mto huo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika chanzo cha Mto Ruvu Leo na kusisitiza Wananchi washirikishwe kulinda vyanzo hivyo
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja  akishiriki zoezi la upandaji miti leo Mkoani Pwani
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akijadiliana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa zoezi la upandaji wa miti katika chanzo cha Bonde la Mto Ruvu leo Mkoani Pwani.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akiwa anaelekea eneo la bonde la Mto Ruvu leo Mkoani Pwani

LUGOLA AMPA WIKI MBILI BOSI WA UHAMIAJI NCHINI AENDE MIKOA YA KAGERA NA KIGOMA KUFANYA OPERESHENI KUBWA KUWAONDOA WAHAMIAJI HARAMU KABLA YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA HAUJANZA

$
0
0

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa mjini Karagwe Mkoani Kagera, katika Mkutano uliofanyika katika uwanja wa Changarawe mjini humo, leo. Lugola katika hotuba yake kwa wananchi hao, amempa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, awe amefika Mikoa ya Kagera na Kigoma kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkazi wa Mji wa Karagwe, Mkoani Kagera, Clemence Ishelenguzi alipokuwa anatoa kero zake mbalimbali katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Changarawe mjini humo, leo. Lugola katika hotuba yake, amempa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, awe amefika Mikoa ya Kagera na Kigoma kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Na Felix Mwagara, MOHA-Karagwe.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt Anna Makakara, awe amefika Mikoa ya Kagera na Kigoma kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Karagwe katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Changarawe mjini humo, Lugola alisema kuna idadi kubwa ya wahamiaji haramu katika mikoa hiyo, hivyo CGI na Maafisa wake wahakikishe wanawaondoa wahamiaji wote haramu kupitia operesheni kubwa niliyoitangaza. “Nimepata taarifa na ndani zaidi na pia nyie wananchi hapa mmesema leo kuhusu uwepo wa wahamiaji haramu, ndio mana nimekuja hapa kwa ajili ya kuhakikisha wahamiaji hao wanaondolewa haraka iwezekanavyo hapa Kagera na Mkoa wa Kigoma,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, licha ya kutangaza operesheni hiyo, lakini viongozi wa uhamiaji katika mikoa hiyo wawe makini mara kwa mara kuhakikisha wanawafuatilia wahamiaji hao kwa kuwashirikisha wananchi waaminifu ili waweze kutoa taarfia sahihi za wahamiaji hao. “Tunatarajia kufanya uchaguzi hivi karibuni mwaka huu, hivyo mnapaswa kuhakikisha watakaopiga kura ni Watanzania na sio wenginevyo ili kuepusha usumbufu mkubwa katika jamii,” alisema Lugola.

Lugola aliwataka wananchi wa mikoa hiyo watoe ushirikiano na wasiwafiche wahamiaji hao kwasababu kumuhifadhi ni kosa kisheria, hivyo wanapaswa kuhakikisjha wanatoa taarifa za wahamiaji hao kwa maafisa uhamiaji ili waweze kukamatwa. Waziri Lugola katika mkutano huo alijibu maswali mbalimbali ya wananchi wa Karagwe yakiwemo kuhusu uwepo wa wahamiaji hao haramu ambao pia wanalalamikiwa kuwa wanatumia nguvu ya fedha kuwanyanyasa Watanzania wenye kipato kidogo.

“Pia nina taarifa za kutosha kuwa, baadhi ya maafisa uhamiaji wanapewa fedha na wahamiaji hao ili wasiweze kuwakamata, sasa ole wenu, katika Serikali hii ya Magufuli haichezewi na haijaribiwi, ole wako wewe afisa uhamiaji uingie mikononi mwangu, sitakuonea huruma na hakika nitakuondoa kazini,” alisema Lugola. Lugola alisema wahamiaji haramu sio wakuchekewa hivyo amemtaka CGI ahakikishe anawapanga vizuri nmaafisa wake kwa kutembnea nyumba kwa nyumba kuwasaka na kuhakikisha wote wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Lugola alisema alifanya ziara katika Mkoa wa Kigoma kwa kutembelea Wilaya zote kama anavyofanya Mkoa wa Kagera, anapewa kero hiyo katika ziara hiyo, hivyo anataka Uhamiaji wawaondoa wahamiaji wote ndani ya mikoa hiyo ili Watanzania waweze kuishi kwa amani wakiendelea kujionea maendeleo ya uongozi wa Rais Dkt. Magufuli.

Waziri Lugola amemaliza ziara yake Wilaya Karagwe na Wilaya inafuata ni Kyerwa, Ngara, Biharamulo na Muleba, ambapo akiwa ziara hiyo, pia uzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara pia ukutana na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni ambayo jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na Mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya Gereza.

SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA

$
0
0

Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Simon Sirro akimpa zawadi Naibu Kamishna Mstaafu wa Polisi Hussein Laizer (kulia) ,Wakati wa Sherehe za kuwapongeza na kuwaaga Wastaafu wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukaribisha mwaka mpya 2019,Sherehe hiyo imefanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt.Anna Makakala akiongea na Maafisa ,askari waliopo kazini na wastaafu wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), Kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro wakati wa Sherehe za Kuwapongeza na Kuwaaga Wastaafu wa Vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukalibisha mwaka mpya 2019,Sherehe hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiongea na Maafisa, Askari waliopo kazini na Wastaafu wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani) kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Simon Sirro wakati wa Sherehe za Kuwapongeza na Kuwaaga Wastaafu wa Vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukaribisha Mwaka Mpya 2019, Sherehe hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na Inspekta Jenerali wa Polisi ,IGP Simon Sirro wakiingia ukumbini wakati wa Sherehe za Kuwapongeza na kuwaaga Wastaafu wa Vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukaribisha Mwaka Mpya 2019, Sherehe hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amewapongeza Wastaafu wa Jeshi hilo kwa kumaliza utumishi wa umma wakiwa hawana kashfa yoyote ambayo ingelichafua jeshi hilo na kufanya lipoteze uhalali mbele ya wananchi.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya Kuwaaga Askari na Wastaafu wa Jeshi na Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam

“Nawapongeza kwa kumaliza salama naomba mkawe na nidhamu ya fedha mtakayolipwa kama kiinua mgongo na mtumie kiasi hicho cha pesa kwa manufaa ya familia na jamii inayowazunguka” alisema IGP Sirro

Akizungumza katika Sherehe hizo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo amewataka Wastaafu wa Jeshi la Polisi kuhakikisha wanakuwa raia wema na kudumisha amani katika maisha yao mapya baada ya kulitumikia Taifa kwa manufaa,ameongeza kuwa Upendo waliouonesha kwa wafanyakazi wenzao wakati wakiwa kazini wakauonyehe huko wanakoenda

“Mmekua mfano wa kuigwa kipindi chote mlichokua kazini, tunaomba mkawe raia wema huko kwa kuendelea kusimamia matukio ya uhalifu katika maeneo mtakayokua mnaishi, tunaamini nyie bado askari na mnafahamu mbinu zote za kupambana na uhalifu hivyo fahamuni tunawategemea bado,” alisema Jenerali Mabeyo

Maafisa na Askari Wastaafu wa Jeshi la Polisi walioagwa katika sherehe hizo walilishukuru Jeshi la Polisi kwa upendo walioupata katika kipindi cha utumishi kwa umma na kuwaasa maafisa na askari walipo kazini kulitumikia jeshi kwa uaminifu mkubwa.

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AFUNGUA BARABARA YA KIJITOUPELE-FUONI MAMBOSASA ZANZIBAR

$
0
0

-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein akikunjuwa Kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Kijitoupele-Fuoni mambosasa Wilaya ya Magharibi B Unguja ,ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Ufunguzi wa Barabara ya Kijitoupele-Fuoni mambosasa Wilaya ya Magharibi B Unguja ,ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Taswira ya sehemu ya Barabara ya Kijitoupele-Fuoni mambosasa Wilaya ya Magharibi B Unguja iliofunguliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Baadhi ya Wananchi pamoja na Viongozi wa chama na Serikali waliohudhuria katika Ufunguzi wa Barabara ya Kijitoupele-Fuoni mambosasa Wilaya ya Magharibi B Unguja ,ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheir katika Ufunguzi wa Barabara ya Kijitoupele-Fuoni mambosasa Wilaya ya Magharibi B Unguja ,ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheir akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Barabara ya Kijitoupele-Fuoni mambosasa Wilaya ya Magharibi B Unguja ,ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

DKT.NDUGULILE ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA RUVUMA,AKAGUA HALI YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA BORA KWA WANANCHI

$
0
0
NaWAMJW - SONGEA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya bora kwa Wananchi.

Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vifaa vyote vilivyoharibika vinatengenezwa na kuanza kufanya kazi mara moja.Kwa upande mwingine ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanatumia Fedha vizuri katika kufanya maboresho ya majengo ya Hospitali hiyo, ikiwemo kutumia Forced account katika ujenzi huo.

Pia, Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha kila mtoa huduma za Afya anaandika muda kwa usahihi aliomuhudumia mgonjwa kuanzia anapopokelewa, anapofanyiwa matibabu mpaka anapoandikiwa dawa jambo litalorahisisha kubaini mtenda kosa endapo mgonjwa atapata tatizo.

Aidha, Serikali imeahidi kuwapa gari la kubebea wagonjwa katika Hospitali hiyo ili kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika endapo gari hilo litakuwepo ikiwemo vifo vya mama na mtoto.

Mbali Na hayo Dkt. Ndugulile amewapongeza Watoa Huduma za Afya katika Hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya huku akiwatia moyo kuwa Serikali inafahamu mchango wao na itaendelea kuboresha mahitaji yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile akikagua karatasi ya idadi ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine akikagua hali ya upatikanaji wa Dawa kwenye chumba cha kuhifadhia Dawa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine akimjulia hali mtoto aliyepelekwa kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile akikagua miguu bandia katika chumba cha kuhifadhia vifaa mbali mbali vya Hospitali, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

WAZIRI MKUU ANUSA UFISADI UKARABATI WA JENGO SONGEA

$
0
0
*Ni la wajawazito wanaosubiri kujifungua, limegharimu sh. milioni 129 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amenusa harufu ya ufisadi katika mradi wa ukarabati wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO) na amesema kwamba hajaridhishwa na kiasi ya sh. milioni 129 zilizotumika.

Hivyo, amemuagiza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile afuatilie suala hilo ili kumbaini mtu ambaye amehusika katika kupitisha zabuni ya ukarabati wa jengo hilo na kisha kumpelekea taarifa.

Waziri Mkuu amenusa harufu ya ufisadi katika mradi huo leo (Jumamosi, Januari 5, 2019) wakati alipotembelea hospitali hiyo na kukagua ukarabati wa jengo la akinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua (mama ngojea) ambalo umegharimu sh. milioni 129.

“Sijaridhishwa na gharama za ukarabati wa jengo hilo kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika kwani Serikali inajenga vituo vya afya vyenye jengo la maabara, jengo la kujifungulia, wodi ya mama na mtoto, chumba cha upasuaji, nyumba ya watumishi kwa gharama za sh. milioni 400 hadi 500 sasa inawezekajane jengo moja linalokarabatiwa ligharimu kiasi hicho.”

Waziri Mkuu amesema kila mtumishi wa umma lazima azingatie maadili ya kiutumishi na kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa na Serikali. Amesema Serikali imeagiza miradi ijengwe kwa kutumia force accountna kuhakikisha miradi inalingana na thamani ya fedha.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu utoaji wa huduma ya watoto waliochini ya miaka mitano zinazotolewa katika hospitali kwani baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa wakiwatoza gharama za dawa wakati wanatakiwa watibiwe bure.

Waziri Mkuu amesema hayo baada ya Kanisia Fusi ambaye amelazwa na mtoto wake katika hospitali hiyo kumueleza kwamba ameandikiwa dawa na kuambia akanunue wakati mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anatakiwa atibiwe bure.

Pia baada ya Dkt. Ndungulile kuangalia cheti cha mtoto huyo alisema dawa aliyoandikiwa ipo hospitalini hapo jambo ambalo lilithibitishwa na Mganga Mfawidhi wa hopitali hiyo Dkt. Majura Magafu, hivyo Waziri Mkuu amemuagiza mganga huyo amtafute mtendaji aliyemuambia mama huyo akanunue.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezindua mpango wa usambazaji wa x-ray za kidigitali ambazo zitazambazwa kwenye hospitali mbalimbali za rufaa za mikoa ili kuboresha utoaji wa huduma zinazotolewa kwa njia ya mionzi.

Waziri Mkuu amesema kwa kuanzia x-ray hizo zitasambazwa kwenye hospitali za rufani katika mikoa 11 na kisha baadae zitasambazwa kwenye hospitali zingine 20, lengo ni kuhakikisha hospitali zote za rufaa za mikoa zinakuwa na x-ray hizo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Ndungulile amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za nchini.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma za afya zinawafikia Watanzania wote karibu na maeneo yao ya makazi tena kwa gharama nafuu. ”Katika kufikia azma hii moja wapo ya kipaumbele ni kununua vifaa vya kisasa vinavyoendana na teknolojia iliyopo.”

Amesema kwa sasa wizara hiyo imenunua mashine 11 za x-ray za kidigitali zenye thamani ya zaidi ya shilingi 2,027,029,794.60 ambazo zimekusudiwa kupelekwa kwenye hospitali 11 zenye x-ray za zamani. Hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi, Morogoro, Njombe, Ruvuma, Simiyu, Singida na zingine tatu zitafungwa katika hospitali za wilaya za Chato, Magu na Nzega. 



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JANUARI 5, 2019.

WAZIRI MKUU ACHUKIZWA NA TAARIFA YA KUZUIWA KWA NGUZO ZA UMEME

$
0
0
*Aitisha kikao na viongozi wa maeneo hayo pamoja na Mawaziri husika

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuita Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi pamoja na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote zinazozalisha nguzo za umeme katika mkoa huo kufika ofisini kwake ili waeleze sababu za kuzuia nguzo za hizo zisitoke. 

“Wanieleze kwa nini wanazuia nguzo,Wakati wananchi wanasubiri kuunganishiwa huduma ya nishati ya umeme wao wanazuia nguzo wanasubiri posho, Wanaidai Serikali wakati ni wao ni sehemu ya Serikali Tutakutana ofisini kwangu Januari 7, saa tano kamili asubuhi.”

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji Nyoni, wilayani Mbinga akiwa katika siku ya tatu za ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma. Alisema jambo hilo linakwamisha zoezi la usambazaji umeme.

Aliyasema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walilalamikia kitendo cha kutofikishiwa huduma ya umeme katika maeneo yao kutokana na kukosekana kwa nguzo ambazo zimezuiwa kwa sababu ya wahusika wanaidai Serikali posho.

Waziri Mkuu alisema viongozi wengine watakaokuwepo kwenye kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo, Wenyeviti wa halmashauri hizo zilizozuia nguzo ili wamueleze sababu za kuzuia nguzo hizo.

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli iAlisema Serikali imedhamiria kusambaza huduma ya nishati ya umeme katika vijiji vyote nchini vikiwemo na wananchi hao wataunganishiwa umeme huo kwa gharama ya sh. 27,000 tu.

Pia Serikali imeondoa gharama za kulipia nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali na kwa vijiji ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo linalenga kufungua fursa za ajira na kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa.

Serikali imefanya maamuzi hayo kwa sababu huduma hiyo ya umeme ni muhimu kwani mbali ya kutumika katika matumizi ya majumbani, pia kwa kusogezwa karibu na maeneo ya pembezoni itawezesha zahanati, shule ,viwanda na vituo vya afya kuwa na umeme.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JANUARI 5, 2019.

POLEPOLE ACHARUKA UZINDUZI WA KAMPENI KATA YA MAGOMENI ASEMA WAPINZANI WANABWABWAJA TU

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Humphrey Polepole amefungua Kampeni na kumnadi mgombea Udiwani wa kata ya Magomeni, Shaweji Mkubura, katika Viwanja vya Magomeni Makuti.

Akifungua Kampeni hizo Polepole amewaambia wakazi wa magomeni kuchagua mgombea kutoka CCM kwani Wapinzani wameishiwa sera wanabwabwaja tu mitandaoni na kuisema vibaya Tanzania kwa mataifa Rafiki.

“siku zote Mnyororo huwa unafanana sasa ni aibu kama mtachagua wapinzani ambao wao kazi yao kubwabwaja kila kukicha kuanzia mitandaoni kazi kuisema vibaya serikali yetu aitoshi wamesafiri kwenda nje kutusema vibaya kana kwamba awaoni Maendeleo yanayoletwa na Mwenyekiti wa chama chetu”alisema Polepole

“Mzee mwenye Madevu ametembea nchi za ulaya wa marafiki zetu kuwasihii wasitusadie baada ya ziara hiyo tukasikia nchi kadhaa zinatuchimba mkwara kwa mambo yanayotuhusu wenyewe matokeo yake wakatuambia kama unataka msaada lazima tufuate sera za ushoga jambo ambalo serikali ya CCM Imegomea”.

Alisema Sasa chama cha uliberali ambacho hakieleweki kina Makatibu wawili,Wenyeviti wawili na mlengo wao kila kitu hewala, hivyo wao suala la vijana wa kiume kuvaa madela kwao ni sawa tu hivyo sio watu wakuwachagua.

Polepole alisema kuwa CCM inayoongozwa na Rais Magufuli inamleta kwenu Shaweji kwa wakazi wa kata ya Magomeni waweze kumchagua ifikapo January 19 aweze kuwaongoza wakazi wa magomeni.Alimaliza kwa kusema kuwa Magomeni ndipo waktoka watoto wa Mjini hivyo wakazi wa magonei awatakiwi kukosea kwa kupiga kura kwa wapinzani bali wanatakiwa kupeleka kura zote kwa shaweji.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole, akimnadi Mgombea Udiwani wa CCM Kata ya Magomeni Ndugu Shaweji Mkumbura wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo Jijini Dar es Salaam leo.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Magomeni kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ndugu Shaweji Mkumbura akiwa amepiga magoti kuomba kura kwa wakazi wa Magomei waliofika katika uzinduzi wa kampeni zake zilizofanyika katika Viwanja vya Magomeni Makuti Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole, akihutubia wakazi wa Kata ya Magomeni eneo la Magomeni Makuti wakati akimuombea kura Mgombea wa CCM aweze kuchaguliwa kuwa Diwani katika wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba akizungumza na wakazi wa kata ya Magomeni eneo la Makuti B kumnadi Mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia CCM
MNEC wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam , Yusuph Nassoro akihutubia wakazi wa Magomeni wakati wa uzinduzi wa Kampeni za udiwani wa kata hiyo
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Mkoa wa Dar es SalaaSimon Mwakifamba akipokea kadi na kumkaribisha Mwanachama Mapya wa CCM kutoka Chadema
Baadhi ya Wanachama waliofika katika Mkutano huio wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa udiwani kata ya Magomeni

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 6,2019

MAJALIWA AZINDUA X- RAY YA KIDIGITALI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA RUVUMA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua  X-Ray ya kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, Januari 5, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt, Faustine Ndugulile na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5739
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu Mashine ya Kidigitali aliyoizindua katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kutoka Mtalaam wa tiba ya mionzi (Medical Technologist), Lincleth Gingo kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5,2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wtoto, Dkt. Faustine Ndugulile. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5787
PMO_5803
Wananchi wa Songea wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua Mashine ya  X-Ray ya Kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, Januari 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5605
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza taarifa ya Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Majura Magafu kuhusu ukarabati wa Jengo la Wakinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2019. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile,  wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5615
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiongozwa na  Kaimu Mganga Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma, Majura Magafu (kulia) kukagua  ukarabati wa jengo la wakinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2019.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5616
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiongozwa na  Kaimu Mganga Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma, Majura Magafu (kulia) kukagua  ukarabati wa jengo la wakinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2019.   Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulie na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5644
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mtoto, Patric Chenya  wakati alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa  wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2019. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5684
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa  akizungumza na Bibi Kanisia Fusi anayemuuguza mwanae, Mushidi Ngonyani wakati alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PMO_5826
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua mashine ya X- Ray ya Kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5845
Wananchi wa Songea wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua Mashine ya  X-Ray ya Kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, Januari 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Pata punguzo na unufaike kwa kuwa mteja wa akaunti ya muda maaulum

$
0
0

NOTES ON FIXED ACCOUNT.

·        Pata punguzo na unufaike kwa kuwa mteja wa akaunti ya muda maaulum
·        Riba hadi asilimia 12 kwa mwaka kwa mteja mwenye amana ya kuanzia Milioni 5 kwa kipindi cha miaka miwili na kuendelea
·        Ni fursa nzuri kwa Mstaafu  anayepokea pensheni yake badala ya kununua gari alipendalo awekeze TPB Bank
·        Mtu yeyote anaweza akafungua akaunti hii na kuwekeza
·        Riba inalipwa kila baada ya mwezi, miezi mitatu mpaka sita kulingana na matakwa ya mteja.

GROUP ACCOUNT
Katika kutambua uwepo wa makundi mbali mbali ya watu, kujali mahitaji yao ya huduma za kifedha na adha wanazozipata katika kupata huduma za kibenki, TPB Bank ina akaunti maalum kwa vikundi.  Vikundi rasmi na visivyo rasmi.

Vikundi kama vile, vikundi vya wafanyakazi, vikundi vya ndugu, vilabu vya michezo mbali mbali, wasuka nywele, wasuka mikeka, wavuvi, mafundi seremala, vikundi vya kidini, vikundi vya sehemu ya kazi n.k.



Idadi ya abiria bado kubwa Ubungo.

$
0
0
*Wengi ni wanafuzi katika mikoa ya Tanga,Morogoro na Dodoma

Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii

Idadi ya abiria katika kituo cha mabasi Ubungo imeendelea kuongezeka kwa kwa sehemu kubwa wakiwa wanafunzi.

Akizungumza na Michuzi Blog Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria Hassan Mchanjama amesema kuwa abiria katika kituo cha Ubungo ni kubwa lakini wanasafiri kutoka na baadhi daladala kupata vibali.

Amesema abiria wengi ni mikoa ya Tanga, Dodoma pamoja na Morogoro ikiwa sehemu kubwa abiria hao ni wanafunzi.

Mchanjama amesema abiria wanavyofika katika kituo cha mabasi Ubungo wakate tiketi ndani ya Kutuo.Mmoja wa abiria Hamis Seif amesema kuwa kuna changamoto ya Usafiri katika msimu wa siku kuu na kuomba yaongezwe mabasi hata daladala katika mikoa ya jirani na Dar es Salaam.

Aidha amesema kuwa suala la ukaguzi katika kituo cha mabasi Ubungo ni mzuri na kutaka na mikoa mingine wafanye hivyo kwa ajili ya usalama wa abiria.
 Askari wa usalama barabarani Grant Pawa akiandika makosa ya basi wakati wa ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Maafisa Polisi wakiwa katika ukaguzi katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam 
 Moja ya tiketi aliyekatiwa msafiri ambaye kampuni ya basi hilo halipo katika kituo cha Ubungo abiria anadai kuwa aliyemkatia na kutia saini ni Rama Tall.
 Abiria wakisubiri Usafiri katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Abiria wakiwa wamefurika katika katika Kituo cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani katika kituo cha mabasi Ubungo wakiwa na fundi wakufanya ukaguzi wa basi katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nuru Hussein akifanya Ukaguzi katika basi kuangalia uimara wa Gurudumu pamoja na Brenk katika kituo mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Askari wa kituo cha mabasi Ubungo Nuru Hussein akimpa maelezo Dereva  wakati akifanya Ukaguzi ,jijini Dar es Salaam.

SERIKALI KUENDESHA OPARESHENI KUBWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU NA MAPORI YA AKIBA

$
0
0
Serikali kuendesha operesheni kubwa kuwaondoa wavamizi wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji pamoja na watu wengine wanaofanya shughuli zisizo halali katika misitu na mapori yaliyohifadhiwa kisheria zikiwemo hifadhi za misitu ya serikali Kuu na halmashauri za vijiji.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo wakati akisoma  maazimio ya kikao cha mawaziri watano kilichofanyika mkoani Kigoma leo kutafuta utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi na Mapori ya Akiba ya Moyowosi.

Jafo alisema, wale wote  waliovamia hifadhi wanatakiwa kuondoka kwa hiari kabla ya zoezi la kuwaondoa kwa lazima, operesheni hiyo itafanyika wakati wowote ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia Januari 2019.

Na kusisitiza kuwa wale wenye mazao katika hifadhi na mapori ya akiba wanaweza kuomba idhini ya kuvuna mazao yao.

Jafo alisema Serikali imetenga jjmla ya hekta 10,012.61 kutoka kwenye hifadhi ya msitu wa Makere kusini kwa ajili ya kilimo na mipango ya halmashauri ya wilaya ya Kasulu ambapo Hekta 2,174 kwa ajili ya kijiji cha Mvinza, hekta 2,496 kwa kijiji cha Kagerankanda na halmashauri ya wilaya ya Kasulu Jumla ya hekta 5,342.61.

Kwa mujibu wa Jafo uamuzi huo unafuatia kuwepo kwa changamoto katika maeneo ya hifadhi za misitu na mapori ya Akiba ambapo maeneo mengi yamevamiwa kwa shughuli za kilimo na ufugaji  na hivyo kupoteza uoto wa asili katika hifadhi na mapori ya Akiba.

Mapema jana Mawaziri watano wakioongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo wamekagua hifadhi ya  Msitu  wa Makere Kusini  uliopo wilaya ya Kasulu mkoa wa Kigoma kwa takriban saa tano ili kubaini changamoto mbalimbali za msitu huo na kuzipatia ufumbuzi.

Mawaziri hao ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamis Kigwangala, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima.

Ziara ya mawaziri hao katika hifadhi ya msitu huo ambao pia unatambulika kama Kagera Nkanda ambayo ni ya kihistoria kutokea hapa nchini ilianza majira ya saa saba mchana jana Mawaziri hao wakitokea wilayani Kigoma ambako walikuwa na kikao cha utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi ya Msitu na Pori la Akiba Moyowosi mkoani Kigoma na kumaliza ukaguzi majira ya saa kumi na mbili jioni.

Baada ya kumaliza ukaguzi katika Msitu wa Makere Kusini, Mawaziri hao watano walielekea kijiji cha Kabulanzwili na kukagua mpaka baina ya kijiji hicho na hifadhi ya msitu huo kwenye mto Migezibiri na baadaye kukutana na wananchi wa kijiji hicho kwa lengo la kuwaeleza nia ya serikali kunuru hifadhi ya msitu ambapo walizungumza nao hadi saa moja na nusu usiku.

Wakazi wa kijiji cha Kabulanzwili waliwapokea mawaziri hao kwa mabango wakionesha kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na askari wa wanyama pori kuwaondoa kwa nguvu wananchi wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji kwenye hifadhi hiyo huku baadhi yao wakidai kutofahamu mipaka halisi baina ya kijiji na hifadhi.

Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi Valentine Msusa alisema eneo lote la hifadhi ya Msitu wa Makere Kusini linalopakana na Halmashauri za wilaya za Kasulu na Uvinza lina ukubwa wa hekta 72,000 lakini baada ya hekta 10,000 kutolewa kwa wananchi sasa imebakia na hekta 62,000.

Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Kabulanzwili Nolvet Mtana alieleza kuwa awali waliambiwa waendelee na shughuli za kilimo katika maeneo waliyoanza kufanya shughuli hiyo bila kuanzisha maeneo mapaya lakini wameshangazwa na uamuzi wa kuwaondoa katika maeneo hayo kinyume na kauli ya awali jambo walilolieleza linawafanya waishi maisha ya wasiwasi.

Mkazi mwingine Kidaga Tito alisema hata kama wao walivamia eneo la hifadhi basi  ni vyema wakapewa muda kuvuna mazao yaliyopo shambani ili kuepuka hasara na kutaka mipaka kati ya hifadhi na kijiji iwekwe wazi ili ifahamike kuepuka wananchi kuingia ndani ya hifadhi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula aliwaeleza wananchi wa kijiji cha Kabulanzwili kuwa, tatizo lilipo katika kijiji hicho ni kukosekana mpango wa matumizi bora ya ardhi na kubainisha kuwa suala hilo halihitaji wizara bali kijiji chenyewe kupitia watendaji wake kuanza mchakato wa kupanga maeneo kama vile kilimo, ufugaji, makazi na maeneo ya huduma za jamii.

Aliwataka wananchi wa kijiji hicho kukaa pamoja na kupanga maeneo kulingana na mahitaji na kuacha ile dhana ya kutaka baadhi ya wananchi waliohamia kuondoka na kubainisha kuwa cha msingi ni kujua idadi na mahitaji ya wakulima na wafugaji pamoja na maeneo ya huduma za jamii na halmashauri ya wilaya ya Kasulu na serikali ya kijiji zinapaswa kupanga maeneo na kazi ya wizara yake itakuja kuanisha mipaka na hapo hakutakuwa na migogoro tena.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo alieleza kuwa ujio wa mawaziri hao watano ni wa kihistoria na unaangalia changamoto zinazokabili hifadhi ya msitu wa Makere sambamba na kuona namna bora ya kutatua tatizo linalowakabili wananchi wa eneo linalozunguka hifadhi ya Msitu huo ambapo aliwataka kukubaliana na maamuzi yoyote ya serikali yatakayofikiwa kwa kuwa maamuzi hayo yatakuwa kwa maslahi ya taifa.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Luteni Simon Anange aliwaeleza wananchi wa Kabulanzwili kuwa ujio wa mawaziri watano katika eneo la hifadhi ni kuangalia namna bora ya kuitunza misitu ya Makere na Mvuti iliyopo Kasulu Kigoma ambayo imeanza kuharibika kutokana na uwepo wa shughuli za kilimo na ufugaji na kueleza kuwa kazi ya kushughulikia suala hilo bado haijafika mwisho na kinachofanyika sasa ni kuangalia namna bora ya kunusuru msitu huo.

Hifadhi za Misitu na Mapori ya Akiba ya Moyowosi yamekuwa na mgogoro kwa muda mrefu kutokana na wananchi kuendesha shughuli za ufugaji katika hifadhi za misitu na mapori ya akiba, uchomaji mkaa, uchimbaji haramu wa madini ya chokaa, uwepo silaha za kijeshi, uvunaji haramu mazao ya misitu na uendeshaji kilimo cha mazao ya chakula jambo lililopelekea Katibu Mkuu kiongozi kuandika barua kwa Makatibu Wakuu wa Wizara husika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo Novemba 2018
 Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Kabulanzwili kilichopo Kasulu Kigoma wakiwasikiliza Mawaziri walipofanya ziara katika eneo la hifadhi la Msitu wa Makere lililopo Kasulu Kigoma.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabulanzwili kilichopo Kasulu Kigoma wakati wa ziara ya Mawaziri watano kukagua eneo la hifadhi la Msitu wa Makere.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akikatiza katika moja ya vichaka vilivyopo kwenye hifadhi ya Msitu wa Makere Kasulu Kigoma wakazi wa ziara ya Mawaziri watano kukagua msitu.
 Mawaziri Dk Hamis Kigwangala Waziri wa Maliasili na Utalii, Suleiman Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina na Dk Angeline Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwasikiliza wananchi wa kijiji cha Kabulanzwili alipofanya ziara katika eneo la hifadhi la Msitu wa Makere Kasulu Kigoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo (wa kwanza kushoto) , Dk Hamis Kigwangala Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Angeline Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima wakiangalia ndege inayochukua picha angani (Drones) wakati wakikagua hifadhi ya Msitu wa Makere uliopo Kasulu Kigoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo akiwaongoza Mawaziri wenzake kukagua maeneo mbalimbali katika hifadhi ya Msitu wa Makere Kasulu Kigoma.
 Moja ya eneo ndani ya hifadhi ya Msitu wa Makere uliopo Kasulu Kigoma ambapo Mawaziri watano walibaini uendeshaji shughuli za kilimo ukifanyika ndani ya hifadhi.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima (kushoto), Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina na Dk Angeline Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwa katika gari wakati wa kukagua hifadhi ya Msitu wa Makere Kasulu Kigoma.
Moja ya eneo ndani ya hifadhi ya Msitu wa Makere uliopo Kasulu Kigoma ambapo Mawaziri watano walibaini uendeshaji shughuli za kilimo ukifanyika ndani ya hifadhi.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Luteni Simon Anange akiwaonesha Mawaziri Dk Hamis Kigwangala Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Angeline Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Suleiman Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina eneo la hifadhi la Msitu wa Makere lililopo Kasulu Kigoma walipofanya ziara katika hifadhi hiyo kujionea changamoto mbalimbali ndani ya Msitu huo.


MCHANGE AWAVAA WAPINZANI WANAOPOTOSHA MSWAADA WA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
Humphrey Shao, Globu ya Jamii

ASASI ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) imesema kuwa muswada mpya wa sheria wa vyama vya siasa uliyotolewa hivi karibuni una lengo la kudhibiti kikamilifu fedha za ruzuku za vyama vya siasa.

Asasi hiyo pia imesema muswada huo kama utapitishwa na kuwa sheria rasmi, utadhibiti ukomo wa uongozi wa juu katika vyama vya siasa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo, Habibu Mchange alisema kwa sasa baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikilaumiwa juu ya matumizi mabaya ya fedha hivyo anaamini uwepo wa muswada huo ambao kama ukipitishwa utakuwa sheria itadhibiti jambo hilo.Alisema licha ya baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kuulalamikia muswada huo, yeye kama mwanademokrasia nchini anaamini kuwa sheria hiyo itasaidia kukuza na kuvijenga vyama vya siasa.

“Mimi na asasi yangu pamoja na vijana wenzangu tunamshukuru aliyependekeza muswada huu, kwani huko nyuma niliwahi kukandamizwa nikiwa katika vyama kutokana na kutokuwepo kwa sheria hii.“Kupitia muswada huu ambao kama ukipitishwa utakuwa sheria utakwenda kusimamia vema ruzuku za kila chama cha siasa, kwani Sheria inaeleza kuwa Msajili wa vyama vya siasa atatoa ruzuku kwa vyama na kuelekeza namna ya kuzisimamia , nashangaa kwanini baadhi ya vyama vya upinzania vinapinga jambo hili,” alisema.

Alisema demokrasia ni kugombea nafasi na si watu kushikiria madaraka muda mrefu kwa kuwakandamiza wanasiasa waliopo hivyo kwa kupitia sheria hiyo itawafanya wanasiasa wote kuwa sawa.“Kutugwa kwa muswada huu kutawasaidia wanasiasa wanaoumia ndani ya vyama vyao kuwa kitu kimoja na kuondoa ukilitimba na Umungu watu,” alisema na kuongeza kuwa

“Viongozi wa chama wengi wamekuwa wakijimikisha vyama kwa kudai wanamichango mikubwa ndani ya vyama, sheria hii itaondoa migogoro na kuwa sehemu ya kusimamia maendeleo ya nchi,” alisema.Aidha alisema Muswada huo utampa nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi za wananchi ipasavyo pasipo kuingiliwa na chama chochote cha siasa.

“Ndani ya vyama vya siasa kuna watu ambao awandi vyeo kila siku wana cheo kilekile, hii yote ni kutokana na uwepo wa mfumo usiokuwa bora wa chaguzi ndani ya chama,” alisema.Hata hivyo, Mchange amewataka watanzania kutambua kuwa mabadiriko ya Katiba ni pamoja na mabadiriko ya sheria ndogo ndogo ikiwemo ya vyama vya siasa.“Sheria itakayotungwa itawapa wanasiasa sehemu moja ya kulalamika na kuwaweka kati wanasiasa wote kwa kuongea lugha mojab,”alisema .Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu muswaada huu unafaida kubwa kwa nchi kwani itasaidia kudhibiti fedha za ruzuku na kukuza vipawa kwa wanachama
.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi  ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange akizungumza na Waandishi wa habari juu ya upotoshwaji unaofanywa na vyama vya upinzani juu ya Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi  ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange 
  Sehemu ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi  ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi  ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMJULIA HALI DKT SALIM

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisindikizwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim wakati  alipomjulia hali  Waziri Mkuu Mstaafu huyo, jijini Dar es salaam, Januari 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO 6198  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary   wakisindikizwa na Waziri Mkuu, Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakati alipomjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu huyo, jijini Dar es salaam Januari 6, 2018. Watatu kushoto ni Mama Amen Salim. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT.SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO JIOYA LA OFISI YA ZURA ZANZIBAR

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la msingi Jengo Jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi mbalimbali wakilitembelea Jengo Jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)baada ya kuliwekea jiwe la Msingi Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
-Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba Maji na Nishati Ali Khalil Mirza akisoma risala katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo Jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ardhi Nyumba Maji na Nishati Salama Aboud Talib akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo Jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jengo jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)lililowekwa jiwe la msingi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)waliohudhuria katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo Jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la mamlaka hio Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Viewing all 46317 articles
Browse latest View live




Latest Images