Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1758 | 1759 | (Page 1760) | 1761 | 1762 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Afisa wa Elimu Afya Mashuleni wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Avit Maro akitoa hotuba ya kufungua mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
  Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro. Kulia ni Afisa wa Elimu Afya Mashuleni kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Avit Maro, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo (wa pili kulia) pamoja na Ofisa Utawala wa Elimu wa TAMISEMI, Jeanimina Mtitu (kushoto).
  Ofisa anayeshughulikia Masuala ya Mtambuka wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Gerald George akitoa salamu kwa niaba ya wizara wakati wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
  Ofisa Utawala wa Elimu wa TAMISEMI, Jeanimina Mtitu akitoa salamu kwa niaba ya TAMISEMI wakati wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
  Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Herman Mathias akizungumza jambo na washiriki wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
  Mwelekezi wa Afya ya Uzazi kwa Vijana, Bw. Mshana Elineema akiwasilisha mada inayosema ‘Je changamoto ya mimba za utotoni, UKIMWI ni tatizo linaloangaliwa katika sekta ya elimu?’ wakati wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
  Program Meneja wa kitaifa wa elimu ya afya shuleni wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Bw. Clement Mung’alo akisherehesha mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
  Washiriki wa mkutano wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja.  WADAU mbalimbali katika sekta ya elimu wanaokutana mjini Morogoro, wametakiwa kujadiliana kwa kina kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na Ukatili wa Kijinsia kwa kuangalia taratibu zilizopo sasa za kukabiliana na hali hiyo ili kufanya maeneo ya elimu kuwa salama na chanzo cha mabadiliko ya kitabia.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamayira katika hotuba iliyosomwa na Afisa wa Elimu Afya Mashuleni wa Wizara hiyo, Bw. Avit Maro wakati akifungua mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo.

  Mkutano huo ambao umeelezwa kuwa wa kuongeza kasi kwa sekta za elimu kukabiliana na mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia katika maeneo ya shule na vyuo ni wa kamati ya uratibu ya kitaifa na uthamini wa masuala hayo na unafanyika mkoa wa Morogoro katika hoteli ya Kingsway.

  Msingi wa mkutano huo ni kutafuta mkakati wa pamoja wa kuweza kuhuisha sera hizo kulingana na hali ilivyo kwa sasa ili kuweza kukabili changamoto zilizopo.
  Amesema kwamba kuwepo kwa mazungumzo hayo kutasaidia kubadilisha sera na taratibu mbalimbali za kitaifa na mataifa katika kukabili mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia.Alisema nia ni kuweka maeneo ya shule yenye uwezo wa kutoa nasaha zinazosaidia kupambana na changamoto zinazoambatana na matatizo hayo.

  Mkutano huo ambao unatarajiwa kuja na jibu la kuwezesha wadau kushirikiana katika kuratibu na kuangalia masuala ya afya shuleni umedhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

  Aidha mkutano utaangalia uwezekano wa wadau kushirikiana na mradi wa Unesco unaoshirikisha Shirika la Sida na WHO kuhusu masuala ya elimu mashuleni.Akiwasilisha mada katika mkutano huo Program Meneja wa kitaifa wa elimu ya afya shuleni wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Bw. Clement Mung’alo alisema kwamba nyingi ya kanuni na sera zinazotumika ni zile za mwaka 2004 hivyo ipo haja ya kuangalia hali ya sasa ili kupata mwelekeo mpya.

  Haja ya kuwa na mwelekeo mpya unatokana na kasi ya changamoto zinazoletwa na mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia katika maeneo ya vijana.

  Kwa sasa katika nchi zinazoendelea watu 70,000 hufariki kila mwaka kutokana na mimba za utotoni.Aidha alisema kwamba mdondoko wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari ni mkubwa na kwa jinsi hali ilivyo sasa hivi kwa binti kuwa na mimba ni hatari kwake yeye na maisha yake kutokana na jinsi sheria zilivyo na jamii pia.

  Alisema kwa sasa kuna sababu nyingi za mimba za utotoni ingawa kubwa ni balehe, utamaduni na umbali wa wasichana kutembea kutafuta elimu.Aidha alisema kwamba hadi mwaka 2017, watu milioni 1.5 ambapo asilimia 4.5 wana umri wa miaka 15-19.

  Mkutano huo unaofanyika katika mji wa Morogoro unajadili na kuangalia uwezekano wa kuboresha sera, kanuni na taratibu za kitaifa kukabili mazingira ya sasa.Wakati huo huo Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos amesema Tanzania ina kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba inadhibiti mdondoko wa wanafunzi hasa wa kike kutokana na mimba za utotoni.


  Aidha alisema kwamba takwimu zilizopo sasa ambapo mwaka 2017, 2018 wasichana 4,440 wameshindwa kuendelea na masomo kunaonesha haja ya kuangalia kasoro na kujaribu kuziba ili kutoa mwanya wa maendeleo kwa wasichana.Alisema katika tafiti vijana wengi wamekuwa wakilalamikia kutopata elimu ya uzazi na wakati mwingine hutolewa ikiwa imechelewa na hivyo kujikuta kwenye matatizo.

  Aliwataka washiriki wa mkutano huo kuangalia kwa makini taratibu zote na kuona uwezekano wa kushirikiana na majukwaa yaliyopo kama ya ESA kuona namna bora ya kupeleka elimu kukabailiana na changamoto hizo za makuzi.
  Mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka katika wizara tatu zinazoshughulikia elimu nchini Tanzania za Tamisemi, Elimu na Afya.  0 0


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Fainali za mabingwa Afrika kwa vijana chini ya Miaka 17 (AFCON) yanayotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania April 2019 yamefikia katika upangaji wa makundi.

  Droo hiyo iliyochezeshwa jioni ya leo ikishuhuduwa na viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na viongozi kutoka Shirikisho la Mpira Wa Miguu Afrika (CAF) pamoja na nchi washiriki waliofanikiwa kuingia katika fainali hiyo.

  Fainali hizo zinahusisha timu nane zilizofanikiwa kufuzu na zitachuana kuweza kupata wawakilishi wawili kutoka katika kila kundi kwa ajili ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia la Vijana nchini Peru.Kwenye kupanga makundi hayo mwenyeji Tanzania ameangukia katika kundi la A akiwa na timu za Nigeria, Angola na Uganda.

  Katika kundi B, kuna timu za Cameroon , Guinea, Morroco na Senegal.
  Waangalizi kutoka CAF wameshakagua viwanja, mahospitali na hoteli kwa ajili ya timu zinazokuja nchini mwakani pamoja na waalikwa kutoka nchi mbalimbali.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Kikosi cha Yanga kimeendeleza ushindi wake mfululizo na kujikita zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya AFrican Lyon.

  Mchezo huo wa 17 kwa mabingwa hao wa Kihistoria uliochezwa kwenye Uwanja wa Shekhe Amri Abeid Karume Jijini Arusha uliweza kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

  Mechi hiyo ilianza majira ya saa 10 Alasiri, ukiwa ni mchezo wa kasi ya kawaida kila timu ikimsoma mpinzani wake ila kwa Upande wa Yanga waliweza kuwatoa wachezaji wake wawili Jaffar Mohamed na Ramadhan Kabwili baada ya kupata maumivu kwenye Kipindi cha Kwanza.

  Mabadiliko hayo Yanga waliyafanya kwa kumuingiza Deus Kaseke na Klaus Kindoki na mpaka mpira unafika mapumziko, kila upande ulikuwa haujaona lango la mwenzake.Kipindi cha Kilianza na African Lyon wakionesha kuhitaji zaidi alama tatu ili kuweka matumaini ya kutoka katika nafasi ya chini huku Yanga nae akitaka kuweka rekodi yake ya kutokufungwa.

  Kupitia kwa Beki wake wa Kati Abdalla Shaibu 'Ninja' katika dakika ya 64 aliweza kuiandika Yanga goli la Kuongoza baada ya kuupiga kwa kichwa mpira wa adhabu ulipigwa na Ibrahim Ajib.African Lyon walindelea kusaka goli la kusawazisha na kupata alama moja lakini umakini wa safu ya ulinzi wa Yanga uliwanyima nafasi washambuliaji wake na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa kupoteza kwa goli 1-0.

  Baada ya ushindi huo, Yanga imefikisha alama 47 wakiwa wamecheza michezo 17 wakishinda 15 na kutoa sare 2, akifuatiwa na Azam mwenye alama 40 akiwa amecheza mechi 16 huki mabingwa watetezi Simba wakicheza mechi 13 na wakisalia nafasi ya tatu kwa alama 30.

  Katika mchezo huo uliochezwa Jijini Arusha uliweza kuonesha hamasa kubwa ya mpira wa miguu kwa mashabiki kujitokeza kwa viongozi wa kiserikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na aliyewahi kuwa Afisa habari wa Yanga na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro.
  Kikosi cha Yanga.

  0 0

  Mlezi wa Serengeti Boys, Dkt Reginald Mengi amekutana na kikosi cha Srengeti Boys kilichotwaa ubingwa wa kombe la Cosafa, hivi karibuni nchini Botsw ana ili kuwapongeza. 

  Hafla hiyo ya chakula cha mchana ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, Rais wa TFF Wallace Karia na wadau wengine wa Soka.

  Katika hafla hiyo Dkt Mengi aliwapongeza kwa ubingwa huo huku akiitoa zawadi ya fedha kwa wachezaji na benchi zima la ufundi huku akiwaambia kuwa kutwaa kombe hilo ni moja ya safari nzuri ya kuelekea kutwaa ubingwa katika michuano ya Afcon inayotarajiwa kurindima mwakani hapa nchini.Mengi amesema hii ni historia kwa nchi na pia timu hii ya vijana kufanya vizuri kwenye Mashindano makubwa mawili ikiwemo kombe la Cosafa na kurejea na Kombe, hivyo wanastahili pongezi.

  “Pia niipongeze serikali kwa sapoti kubwa wanayoendelea kuitoa katika timu yangu hii ya vijana, hivyo tutampatia kombe hili mheshimiwa Rais Magufuli kama zawadi ya krismasi, kwani tunajua atafurahia kwakuwa ni mmoja ya viongozi wapenda mafanikio", alisema Mengi.

  Amewaeleza kuwa, ana zawadi kubwa zaidi kwa vijana hao, ila amewasihi kuwa kuwaambia vijana hao wa Serengeti Boys kuwa zawadi hii ya leo ameipunguza baada ya kushauriwa kuwa umri wao ni mdogo sana hivyo kwahoyo yeye kama Mlezi na ataendelea kuwa nao atatatumia mali zake zote ili ahakikishe huko badaye maisha yao yanakuwa mazuri.

  Kwa upande wa Waziri Mwakyembe amesema Kombe hilo ni zawadi ya sikukuu ya Krisimas kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli na ameahidi atazifikisha salam zao kwake pamoja kuahidi kwenda kumkabidhi kombe hilo.
  Mlezi wa Timu ya Vijana Serengeti Boys Dkt Reginald Mengi akizungumza na wachezaji wa Serengeti Boys na wadau wengine wakati wa hafla ya kuwapongeza Vijana hao iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akitoa pongezi kwa timu ya vijana ya Serengeti Boys iliyofanikiwa kurudi na Kombe kwenye mashindano ya nchi za ukanda wa kusini COSAFA, hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Mlezi wa Timu ya Vijana Serengeti Boys Dkt Reginald Mengi akipokea kombe kutoka kwa Nahodha wa Serengeti Boys Abraham Morice na wakati wa hafla ya kuwapongeza Vijana hao iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0  MGENI Diwani wa Kata ya Goba, Muslima Mwenda akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori wakati wa uzinduzi wa mradi wa mfano wa usimamizi wa maji mtiririko, kwenye Shule ya Sekondari Kinzudi, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Pamoja naye ni Mratibu wa Mradi huo, kutoka Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Wilbard Kombe (kulia), Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Saimon Mpyana (wa pili kulia), Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Given Mhina (kushoto) na Wataalam kutoka ARU na Halmashauri za jiji hilo. Mradi huo umedhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA) na kutekelezwa na wataalam wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU).  (Imeandaliwa na Robert Okanda)
  MGENI Diwan wa Kata ya Goba, Muslima Mwenda (wa tatu kulia) kwa niaba ya Mkuu wa  Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori akipata maelezo baada ya kuzindua mradi wa mfano wa usimamizi wa maji mtiririko, kutoka kwa Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Kinzudi, Juma Mbwana iliyopo Goba Wilayani humo jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni Mratibu wa Mradi huo, kutoka Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Wilbard kombe (wa pili kulia), Mhadiri Msaidizi wa ARU, Saimon Mpyana (kulia), Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Given Mhina (kushoto) na Wataalam kutoka ARU na Halmashauri za jiji hilo


  Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Given Mhina (kushoto) akimpatia maelezo Mgeni Rasmi, Diwani wa Kata ya Goba, Muslima Mwenda alipotembelea maeneo mradi wa mfano wa usimamizi wa maji mtiririko, kwenye shule ya Sekondari Kinzudi ulivyotekelezwa katika Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Disemba 18 2018.

  Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Given Mhina (kushoto) akimpatia maelezo Mgeni Rasmi, Diwani wa Kata ya Goba, Muslima Mwenda namna mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua na jinsi yanavyoweza kutumiwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kinzuri baada ya kuzindua mradi wa mfano wa usimamizi wa maji mtiririko, kwenye shule ya Sekondari Kinzudi, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Disemba 18 2018.

  INI ni baadhi ya taswira mbalimbali za eneo la mradi kabla ya utekelezaji wa mradi huo uliodhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA) na kutekelezwa na wataalam wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU).  

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  NAIBU Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema Serikali imejenga miundombinu ya usafirishaji yakutosha ambapo Chuo cha Usafirishaji (NIT) ndio watumiaji wa miundombinu hiyo.

  Serikali haitegemei kutafuta watalaam kutoka nje kwa ajili kutumia miundombinu yetu katika ndege Boti pamoja na Reli.
  Nditiye amekitaka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuhakikisha kinatoa mafunzo bora yatakayosaidia kupatikana kwa wataalamu wa kisasa wataofanya kazi hapa nchini katika sekta mbalimbali za usafirishaji.

  Waziri Nditiye ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana katika mahafali ya 34 ya chuo cha NIT yaliyofanyika katika viwanja Chuo hicho jijini Dar es Salaam.Amesema chuo hicho kikianza kutoa kozi ya marubani na wataalamu wa reli itaongeza wigo la watalaamu nchini.

  "Rai yangu kwa NIT kuhakikisha kuwa kozi hizo zinaanza mapema hapo mwakani ili kuokoa fedha zilizokuwa zinatumika kusomesha marubani na wataalamu wa reli za kisasa nje ya nchi ambapo Serikali imekuwa gharamia kwa fedha nyingi"amesema Nditiye. Aidha Nditiye amewataka wahitimu kuhakikisha wanatumia maarifa na ujuzi waliyoupata wakiwa chuoni kuleta maendeleo ya kwao binafsi na taifa kwa ujumla kwa kujiajiri au kuajiriwa.

  "Niwaombe wanafunzi mkiwa shuleni acheni uharakati fanyeni kile kilichowaleta, kuweni wabunifu na kusoma kwa bidii ili utakapomaliza uweze kupata ajira au kujiarili, "alisema. Naye Mkuu wa Chuo cha NIT, Prof. Zacharia Mganilwa alisema kwa sasa nchi inakabiriwa na upungufu wa marubani zaidi ya 800 hivyo mwakani chuo hicho mwakani kinatarajia kuanza kufundisha masomo ya marubani ili kupunguza gharama zinazotumika kuwasomesha wataalamu hao nje ya nchi.

  "Kwa sasa nchini kuna marubani wapatao 400 lakini mahitaji halisi ni 700 hadi 800, mwakani chuo kikikamilisha ununuzi wa ndege tano kwa ajili ya mafunzo tutaanza kutoa kozi hii ya marubani kwani tunaamini jambo hili likifanikiwa litasaidia kupunguza uhaba wa wataalamu, " alisema.

  Aidha alisema NIT imepokea mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB) wenye thamani ya dola za Marekani Milioni 21.5 ambazo zitatumika kujenga kituo cha umahiri pamoja na ununuzi wa ndege tatu za mafunzo na kwanza Julia mwakani zitakuwa zimeshanunuliwa.
   
   Wahitimu wakiwa wametunukiwa shahada na Mgeni Rasmi katika mahafali ya 34 ya Chuo cha NIT yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo jijini Dar es Salaam.
   Wahitimu wa Chuo cha Usafirishaji cha (NIT) wakiwa katika maandamano katika mahafali ya 34 ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza katika mahafali ya 34 ya Chuo cha Usafirishaji yaliyofanyika viwanja ni hapo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha NIT katika mahafali ya 34 yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo jijini Dar es Salaam.
   Wahitimu katika mahafali.
  Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) Profesa Zakaria Mganilwa akizungumza kuhusiana na mafanikio ya Chuo hicho katika Mahafali ya 34 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

  0 0  NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE 

  MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Zainab Vullu ametoa msaada wa mapazia mazito yanayotumika kusaidia kuweka usiri kwa akinamama wanaokwenda kujifungua katika wodi ya uzazi hospital ya wilaya ya Kisarawe.

  Msaada huo unaelezwa kuwaondolea kero waliyokuwa wakiipata akinamama hao kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wakikataa kujifungua hospitalini hapo kwa kuhofia kukosa faragha wakati wa kujifungua. 

  Mbali ya msaada huo pia ametoa mifuko 80 ya saruji kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya ,zahanati na shule vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh.milioni mbili. 

  Akitoa msaada huo ,Zainab alieleza kipindi cha nyuma akinamama wanaojifungua walikuwa wanakaa sehemu ambayo haijazibwa jambo ambalo limemsukuma kujitolea mapazia hayo. “Faragha inaanza tangu pale anapoanza kutafutwa mtoto hadi anapozaliwa lazima usiri uwepo,” alifafanua Zainab.
  Nae mkuu wa wilaya ya Kisarawe ,Jokate Mwegelo alimshukuru mbunge huyo na kudai suala la ukosefu wa mapazia hayo ilikuwa ni changamoto kwa akinamama wanaojifungua. 

  Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Hamis Dikupatile alisema, serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha mazingira ya kutolea huduma lakini bado jitihada zinapaswa kufanywa na kila mmoja. Mganga mkuu wa halmashauri ya Kisarawe, Jonathan Budenu alibainisha kutokana na changamoto hiyo baadhi ya akinamama walikuwa wakikataa kujifungulia hapo kutokana na hali hiyo.

  MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Zainab Vullu akikata utepe,kulia ni MKuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo

  0 0


  Akina Mama wakiwa bega kwa bega na  vibarua wenzao wanaume katika  kubeba zege linalotumia kwa ujenzi wa msingi na nguzo  za jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  katika eneo la Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma
  IMG_4604-MACHINE
  Kazi ya  uchanganyaji zege ikiendelea katika eneo la ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ihumwa.( Picha na Habari kwa Hisani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali)
  IMG_4647
  Mama Regina akijitwika ndoo ya maji na  kuipeleka kunakoojengwa Msingi. Mama Rejina anasema anamshukuru Mungu kwa  kupata fursa ya kushiriki  ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kama ilivyo kwa akina mama wengi, Anasema  kazi hiyo anaifanya kwaajili ya  watoto wake ( ada)
  -PICHA 3
  Maafisa kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiangalia na kukagua maendeleo ya ujenzi wa  msingi na usimikaji   wa nguzo mwenye kofia nyekundu ni Injinia  Shadrack Ng’wiza  kutoka Kampuni ya Ujenzi  ya Corporation Sole ( Works Superntent) kutoka Mwanza.
  ………………………………………………………………………….


  Na Maura Mwingira , Ihumwa Dodoma

  Mama Regina (55) ni kati ya akina mama takribani kumi, ambao ni sehemu ya vibarua wanaoshiriki kwa kufanya kazi mbalimbali zikiwamo za kubeba zege katika eneo la Ihumwa inapojengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  Eneo hili la Ihumwa na ambalo lipo takribani kilometa 17 kutoka Dodoma Mjini, limetengwa maalum kuwa Mji wa Kiserikali ambapo kunajengwa Majengo ya Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali. 

  “Karibu habari za kazi” ananisalimia mama huyu ambaye anajitabulisha kama Mama Regina wakati nilipomsogelea mahali alipokuwa akichota maji kutoka kwenye simutanki kubwa lililopo eneo la Ujenzi.“ Unataka kunipiga picha” ananiuliza Mama Regina, baada ya kuniona nimeshika Kamera. Ni kamjibu kama yuko tayari na ananiruhusu kumpiga picha”.

  Ninapomuuliza kuhusu kazi yake, Mama Regina kwa tabasamu kubwa ananijibu “ Ninamshukuru Mungu, nimefika leo asubuhi na nikabahatika kupata nafasi ya kufanya kazi kwenye ujenzi huu, ninashukuru sana tunafanya hivi kwa ajili ya ada za watoto” anasema Mama Regina kwa furaha kubwa.Furaha ya Mama Regina ya kupata nafasi ya kushiriki kazi ya ujenzi inajithihirisha wazi wazi usoni mwake ni furaha pia inayonekana kwa wamamawegine wanaobeba zege

  Anajitishwa ndoo yake ya maji kichwani na kuniambia . “ Mimi nakaa kijiji kingine mbali kidogo na eneo hili la ujenzi, kwa hiyo ilinipasa kufika mapema asubuhi na nikapata nafasi, Kwa kweli nina mshukuru Mungu”
  Mwandishi wa habari hii alikuwa miongoni mwa Maafisa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliokwenda jana ( Alhamisi) kuangalia na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo hilo la Ihumwa.

  Sambamba na Mama Regina na ambaye alimweleza mwandishi wa Habari hii kwamba Mume wake ni mlemavu wa miguu, kulikuwapo na wanawake wengine ambao walikuwa wakishiriki ujenzi kwa kubeba ndoo zenye zege wakishirikiana bega kwa bega na wanaume waliokuwa wakizipokea ndoo hizo na kumimina zege kwenye msingi na nguzo.Zege hilo lilikuwa kwaajili ya maendeleo ya ujenzi wa msingi pamoja na nguzo. Akina Mama hawa, walionekana wakipokezana ndoo zilizojaa zege wakiwa katika mstari huku wengine wakiwa wabeba ndoo hizo kichwani.

  Nina muuliza Injinia anayesimamia ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Shadrack Ng’wiza, kuhusu idadi ya wanawake anaowaajiri kwa siku. Naye anasema “ siwezi kukumbuka idadi ya wanawake tunaowaajiri kila siku, mpaka nikaangalie kwenye kitabu ofisini. Lakini nisema tu kila siku tunachukua wanawake kulingana na kazi na mahitaji ya siku ile”.

  Kuhusu maendeleo ya ujenzi wa msingi na nguzo, Injinia Ng’wiza anaieleza timu ya Maafisa kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba, kazi inakwenda vizuri na kwa kasi inayoridhisha. Anasema kila hatua wanayoifanya inabidi ikaguliwe na wakala wa majengo (TBA) kabla ya kuingia hatua nyingine.
  “Kazi hii ya ujenzi wa msingi inakwenda vizuri na ikibidi tunafanya na usiku pia, wapo mafunzi wanaolala hapa ‘site’ na kesho ( ijumaa) tutakamilisha na kuwaita 
   
  TBA ili watukague na kisha wakirithia tuanze kazi ya kupandisha matofali”
  Ninamuuliza kama kunachangamoto wanazokumbana nazo, kwa ufupi anasema, chagamoto kubwa anayohofia ni mvua “ Mvua zinaweza kuturudisha nyuma kwa sababu zikinyesha mchanga utaingia kwenye msingi, hali itakayolazimu tutumie ghrama nyingine kuutoa kabla ya kuendelea na hatua nyingine ya ujenzi”
  Kwa yeyote anayefika katika eneo la Mji wa Serikali Ihumwa ataona mabadiliko makubwa yanayoendelea kwa maana ya kasi ya ujenzi wa Ofisi za Wizara mbalimbali na Taasisi kana kwamba, kuna mashindano ya aina fulani. Magari ya serikali yakipishana kila moja likelekea eneo lao la ujenzi. 

  Ma- Injinia wakiwa wamevalia vizibau vya rangi, mafundi ujezi wakiwa na kofia ngumu kichwani, vibarua nao wakiwa bize, malori makubwa kwa madogo yaliyosheheni koto koto, sementi, mchanga na matofali yakipishana kila mmoja na uelekeo wake ndiyo hali halisi ya Ihumwa kwa Sasa.Na Maura Mwingira , Ihumwa Dodoma

  Mama Regina (55) ni kati ya akina mama takribani kumi, ambao ni sehemu ya vibarua wanaoshiriki kwa kufanya kazi mbalimbali zikiwamo za kubeba zege katika eneo la Ihumwa inapojengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  Eneo hili la Ihumwa na ambalo lipo takribani kilometa 17 kutoka Dodoma Mjini, limetengwa maalum kuwa Mji wa Kiserikali ambapo kunajengwa Majengo ya Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali. 

  “Karibu habari za kazi” ananisalimia mama huyu ambaye anajitabulisha kama Mama Regina wakati nilipomsogelea mahali alipokuwa akichota maji kutoka kwenye simutanki kubwa lililopo eneo la Ujenzi.

  “ Unataka kunipiga picha” ananiuliza Mama Regina, baada ya kuniona nimeshika Kamera. Ni kamjibu kama yuko tayari na ananiruhusu kumpiga picha”.
  Ninapomuuliza kuhusu kazi yake, Mama Regina kwa tabasamu kubwa ananijibu “ Ninamshukuru Mungu, nimefika leo asubuhi na nikabahatika kupata nafasi ya kufanya kazi kwenye ujenzi huu, ninashukuru sana tunafanya hivi kwa ajili ya ada za watoto” anasema Mama Regina kwa furaha kubwa.

  Furaha ya Mama Regina ya kupata nafasi ya kushiriki kazi ya ujenzi inajithihirisha wazi wazi usoni mwake ni furaha pia inayonekana kwa wamamawegine wanaobeba zege

  Anajitishwa ndoo yake ya maji kichwani na kuniambia . “ Mimi nakaa kijiji kingine mbali kidogo na eneo hili la ujenzi, kwa hiyo ilinipasa kufika mapema asubuhi na nikapata nafasi, Kwa kweli nina mshukuru Mungu”Mwandishi wa habari hii alikuwa miongoni mwa Maafisa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliokwenda jana ( Alhamisi) kuangalia na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo hilo la Ihumwa.

  Sambamba na Mama Regina na ambaye alimweleza mwandishi wa Habari hii kwamba Mume wake ni mlemavu wa miguu, kulikuwapo na wanawake wengine ambao walikuwa wakishiriki ujenzi kwa kubeba ndoo zenye zege wakishirikiana bega kwa bega na wanaume waliokuwa wakizipokea ndoo hizo na kumimina zege kwenye msingi na nguzo.

  Zege hilo lilikuwa kwaajili ya maendeleo ya ujenzi wa msingi pamoja na nguzo. Akina Mama hawa, walionekana wakipokezana ndoo zilizojaa zege wakiwa katika mstari huku wengine wakiwa wabeba ndoo hizo kichwani.

  Nina muuliza Injinia anayesimamia ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Shadrack Ng’wiza, kuhusu idadi ya wanawake anaowaajiri kwa siku. Naye anasema “ siwezi kukumbuka idadi ya wanawake tunaowaajiri kila siku, mpaka nikaangalie kwenye kitabu ofisini. Lakini nisema tu kila siku tunachukua wanawake kulingana na kazi na mahitaji ya siku ile”.

  Kuhusu maendeleo ya ujenzi wa msingi na nguzo, Injinia Ng’wiza anaieleza timu ya Maafisa kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba, kazi inakwenda vizuri na kwa kasi inayoridhisha. Anasema kila hatua wanayoifanya inabidi ikaguliwe na wakala wa majengo (TBA) kabla ya kuingia hatua nyingine.
  “Kazi hii ya ujenzi wa msingi inakwenda vizuri na ikibidi tunafanya na usiku pia, wapo mafunzi wanaolala hapa ‘site’ na kesho ( ijumaa) tutakamilisha na kuwaita TBA ili watukague na kisha wakirithia tuanze kazi ya kupandisha matofali”

  Ninamuuliza kama kunachangamoto wanazokumbana nazo, kwa ufupi anasema, chagamoto kubwa anayohofia ni mvua “ Mvua zinaweza kuturudisha nyuma kwa sababu zikinyesha mchanga utaingia kwenye msingi, hali itakayolazimu tutumie ghrama nyingine kuutoa kabla ya kuendelea na hatua nyingine ya ujenzi”
  Kwa yeyote anayefika katika eneo la Mji wa Serikali Ihumwa ataona mabadiliko makubwa yanayoendelea kwa maana ya kasi ya ujenzi wa Ofisi za Wizara mbalimbali na Taasisi kana kwamba, kuna mashindano ya aina fulani. Magari ya serikali yakipishana kila moja likelekea eneo lao la ujenzi. 

  Ma- Injinia wakiwa wamevalia vizibau vya rangi, mafundi ujezi wakiwa na kofia ngumu kichwani, vibarua nao wakiwa bize, malori makubwa kwa madogo yaliyosheheni koto koto, sementi, mchanga na matofali yakipishana kila mmoja na uelekeo wake ndiyo hali halisi ya Ihumwa kwa Sasa.

  0 0


  Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiongoza Kikao cha Kamati ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Wizara jijini Dodoma. Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome na kushoto kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Ndg. Amon Mpanju.
  Sehemu ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake.
  Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiongoza Kikao cha Kamati ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Wizara jijini Dodoma. Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome na kushoto kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Ndg. Amon Mpanju.
  Sehemu ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake.

  0 0

  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ametoa shilingi Milioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya soko la Mlango Mmoja iliyoteketea kwa moto miezi mitatu iliyopita.


  Mabula aliyasema hayo jana baada ya kuwatembelea wafanyabiashara wadogo (machinga) katika soko hilo na kubainisha kwamba fedha hizo kutoka mfuko wa jimbo zitasaidia ujenzi wa paa lote.


  Mwenyekiti wa soko hilo, Jackson Kayoza alisema kulingana na tathmini iliyofanyika, shilingi Milioni 98 zinahitaji kwa ajili ya ujenzi wa sehemu iliyoungua moto hivyo alimshukru mbunge Mabula kwa mchango huo.


  Mmoja wa machinga katika Soko la Mlango Mmoja ambaye pia bidhaa zake zilitekeketea kwa moto, Isaack Julius, alisema mchango wa mbunge Mabula uwe chachu kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuhakikisha inakamilisha kiasi cha fedha kinachohitajika ili ujenzi huo uanze mara moja.


  Septemba 28, 2018 majira ya alfajiri, ajali ya moto ilizuka katika Soko la Mlango Mmoja na kusababisha meza 83 za wajasiriamali, maduka 23 na vyoo vitatu kuteketea ambapo hasara yake haikujulikana mara moja.

  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (katikati), akizungumza na wafanyabiashara wadogo (machinga) katika Soko la Mlango Mmoja Jijini Mwanza.
  Tazama BMG Online TV hapa chini

  0 0

  Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesaini makubaliano ya kuanzisha ushirikiano kati yake na Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo lengo la kuboresha utoaji wa mafunzo kwa njia ya kutembeleana na kubadilishana ujuzi na maarifa kwa walimu na wanafunzi na shughuli zingine za kitaaluma.

  Makubaliano hayo ya awali yaliafikiwa na kusainiwa leo (tarehe 20 Desemba 2018) kati ya Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo, Profesa Dou Ruimu kwa upande mmoja na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dr. Pancras Bujulu kwa upande mwingine na kwamba yatafuatiwa na utiaji saini wa Waraka wa Makubaliano (MoU) siku za mbeleni.

  Utiaji saini wa makubaliano ya awali uishuhudiwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Noel Mbonde na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET Board), Peter Maduki, wawakilishi wa Chuo cha Henan na Wajumbe wa Menejimenti ya VETA.

  VETA ina nia ya kuimarisha mafunzo katika sekta ya kilimo na miongoni mwa malengo yake ni kukiimarisha na kukiboresha chuo cha VETA Kihonda ili kiweze kubobea na kuwa kituo bora cha mfano katika mafunzo ya ufundi stadi kwenye sekta ya kilimo.

  Kabla ya kusaini makubaliano, ujumbe wa watu sita kutoka Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo ukiwahusisha watendaji wakuu na wataalam mbalimbali umekuwepo nchini tangu Jumanne tarehe 18 Desemba 2018 ambapo ulifanya majadiliano na Menejimenti ya VETA Makao Makuu, ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt Pancras Bujulu na Jumatano, tarehe 19 Desemba 2018 ulitembelea ofisi ya VETA Kanda ya Mashariki, kisha chuo cha VETA Kihonda na kujionea karakana, mashine na vifaa mbalimbali vinavyotumika kufundishia fani ya Ufundi wa Zana za Kilimo (Agro-mechanics), mafunzo ambayo yanagusa sekta ya kilimo ambayo ndio mkondo wa chuo cha Henan.

  Akizungumza kabla ya kutiwa saini makubaliano hayo ya awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET Board), Peter Maduki alisema Bodi yake inaunga mkono ushirikiano huo kutokana na kutambua umuhimu wake wa uwezekano wa kuchangia kuboresha mafunzo kwenye sekta ya kilimo ambayo ni ya msingi katika uchumi wa nchi.

  “Zaidi ya asilimia 70 ya wa Watanzania wanategemea kilimo, kwa hivyo kuboresha mafunzo kwenye kilimo maana yake ni kuboresha maisha ya Watanzania,” alisema.

  Aliongeza kuwa hata katika mkakati wa sasa wa nchi kuelekea kwenye uchumi wa viwanda, kuboreshsa ujuzi katika kilimo ni sawa na kuhakikisha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda kwa kuwa viwanda vingi vya nchi zinazoendelea kama Tanzania hutegemea zaidi malighafi kutokana na mazao ya kilimo.
  Vilevile, Mkurugenzi wa Mafunzo na Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Noel Mbonde aliahidi kusaidia uharakishwaji wa ushirikiano huo kwa kuwa una fursa kubwa ya kuboresha utoaji wa mafunzo ambao ndio eneo analosimamia.

  Kwa sasa mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vinavyomilikiwa na visivyomilikiwa na VETA hutolewa katika kozi za Ufundi wa Zana za Kilimo, Teknolojia ya Usindikaji wa Nyama, Usindikaji wa Mbegu za Mafuta, Kilimo cha Bustani na Mazao ya Nafaka, Uhudumu wa Misitu, Uokaji, Kilimo cha Uyoga, Utengenezaji wa Mvinyo, Usindikaji wa Mboga na Matunda, Usindikaji wa Samaki na Usindikaji wa Asali.

  Kwa upande mahsusi wa vyuo vinavyomilikiwa na VETA, mafunzo ya muda mrefu ambayo ni ya kipindi cha miaka miwili hadi mitatu hutolewa katika fani za Ufundi wa Zana za Kilimo (VETA Kihonda, VETA Manyara, VETA Arusha-Oljoro, VETA Mpanda na VETA Dakawa); Ufugaji (VETA Singida); Teknolojia ya Usindikaji wa Nyama (VETA Dodoma). Vilevile VETA huendesha kozi za muda mfupi ambazo ni za kati ya miezi miwili hadi sita kupitia programu yake ya Uboreshaji Ujuzi kwa Wajasiriamali kwenye Sekta Isiyo Rasmi (INTEP) ukihusisha mafunzo mbaimbali kama Kilimo cha Uyoga, Ufugaji wa Samaki, Utengenezaji Mvinyo, Usindikaji wa Mboga na Matunda, Usindikaji wa Samaki na Usindikaji wa Asali.

  Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo (Henan Vocational College of Agriculture) kilianzishwa mwaka 1952. Chuo hicho kilichopo katika jimbo la Henan kinachomilikiwa na serikali ya China ni chuo cha mfano katika utoaji wa elimu ya ufundi stadi katika fani ya kilimo ikiwa ni pamoja na kilimo cha bustani na mbogamboga, ufugaji na usindikaji wa chakula.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu (wa pili kutoka kulia, waliokaa) na Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo, Profesa Dou Ruimu (wa pili kutoka kushoto,waliokaa) wakisaini makubaliano ya awali ya ushirikiano kati yao. Wa kwanza kulia, waliokaa ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Noel Mbonde na wa kwanza kushoto waliokaa naye ni Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan, Chen Yueying.
     Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu (wa pili kutoka kulia, mstari wa mbele) na Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo, Profesa Dou Ruimu (wa pili kutoka kushoto, mstari wa mbele) wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya awali ya ushirikiano kati yao. Wa kwanza kulia, mstari wa mbele ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Noel Mbonde na wa kwanza kushoto, mstari wa mbele naye ni Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan, Chen Yueying. Wengine ni wajumbe wa Menejimenti ya VETA na Wawakilishi wa chuo cha Henan.


  0 0

  Mkurugenzi wa taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania, Donald Kasongi (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu Mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) wakati wa zoezi la kukabidhi matenki ya kuvuna maji ya mvua yaliyojengwa kupitia mradi huo katika Shule za Msingi Mabatini A na B zote za Jijini Mwanza, hii leo Disemba 21, 2018.

  Mradi wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) ulibuniwa na taasisi ya Governance Links Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ukilenga kuwajengea uwezo wananchi pamoja na wadau/ taasisi mbalimbali kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na hatari ya Majanga ikiwemo mafuriko.
  Mkurugenzi wa taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania, Donald Kasongi amesema ujenzi wa matenki ya mfano ya kuvuna maji ya mvua katika Shule za Msingi Mabatini A na B Jijini Mwanza, umegharibu shilingi Milioni tano hivyo wananchi na Shule nyingine zinaweza kutumia mradi huo kujifunza namna bora ya kuvuna maji ya mvua badala ya kupoteza kiasi kikubwa wakati wa mvua.
  Utekelezaji wa Mradi wa majaribio wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) ulianza mwezi Otoba 2017 na unafikia tamati mwezi huu Disemba 2018 huku kukiwa na matarajio makubwa ya mradi huo kuwa endelevu.
  Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
  Taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania imekabidhi manteki mawili ya kuvuna maji ya mvua katika Shule za Msingi Mabatini A na B, yaliyojengwa kupitia mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience).

  Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Donald Kasongi amesema ujenzi wa matenki hayo ya mfano umegharimu shilingi Milioni tano hivyo wananchi na Shule nyingine Jijini Mwanza zinaweza kutumia mradi huo kujifunza namna bora ya kuvuna maji ya mvua badala ya kupoteza kiasi kikubwa cha maji wakati wa mvua.

  Kasongi amesema hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) unaolenga kuwajengea uwezo wananchi pamoja na wadau/ taasisi mbalimbali kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na hatari ya Majanga ikiwemo mafuriko.

  Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, wanafunzi Mariam Thomas (Mabatini B), Rayton Mandalu (Mabatini A) pamoja na Rhoda Madaraka (Mabatini B) wamesema uvunaji wa maji ya mvua umewasaidia kupata maji ya kutosha kwa ajili ya usafi wa madarasa, vyoo, kumwagilia miche ya miti na hivyo kuwaondolea adha iliyokuwepo awali.
  Tazama BMG Online TV hapa chini
  Mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience)

  0 0

   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akitia saini katika kitabu cha Maombelezo cha Marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)  mara baada ya kuwasili Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18,2018 Nchini Afrika Kusini. 
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu  aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)  , Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18, 2018 nchini Afrika Kusini.
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akimpa pole mjane Joyce Chamhuro (Mke wa Marehemu) pamoja na familiya ya Marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu  aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM), Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18, 2018 nchini Afrika Kusini.
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na Wafiwa na Waombolezaji wengine mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu  aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM), Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18, 2018 nchini Afrika Kusini.
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Wafanyakazi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) pamoja  na Waombolezaji wengine mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu  aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)  , Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18, 2018 nchini Afrika Kusini.

   Picha na Ikulu.

  0 0

  Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na SHIVYAWATA wametoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakurugenzi wa Sera na Mipango na Maafisa Utumishi Waandamizi juu ya masuala ya Watu wenye Ulemavu.

  Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Peter Kalonga amesema kuwa masuala ya Watu wenye Ulemavu ni mtambuka, hivyo ili kuifikia jamii jumuishi ni vyema kuhakikisha masuala ya wenye Ulemavu yanajumuishwa vyema katika mipango mkakati wa kila sekta.

  “Sera ya Taifa ya huduma na maendeleo kwa Watu wenye Ulemavu pamoja na Sheria ya Watu wenye Ulemavu zinasisitiza ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika nyanja mbalimbali za kijamii.” Alisema Kalonga. Aliongeza kuwa, Nchi yetu iliridhia Mkataba wa Kimataifa wa haki za Watu wenye Ulemavu wa mwaka 2006 unaotoa tafsiri ya mambo mbalimbali kuhusu haki za Watu wenye Ulemavu na kupelekea kutungwa Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 ili kufanikisha utekelezaji wa mkataba huo na kukuza haki za watu wenye ulemavu nchini.
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Peter Kalonga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo wakati wa mkutano wa kuwajengea uelewa Wakurugenzi na Maafisa Utumishi Waandamizi ngazi ya Wizara juu ya masuala ya Watu wenye Ulemavu yaliyofanyika Disemba 21 na 22, 2018 Jijini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bi. Ummy Nderiananga akiwasilisha mada juu ya ujumuishwaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.
  Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Josephine Lyengi akelezea jambo kuhusu ukondoishwaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.
  Baadhi ya washiriki wakimsikiliza hotuba ya Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Peter Kalonga (hayupo pichani).
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Peter Kalonga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Sera na Mipango, Maafisa Utumishi Waandamizi na Wawakilishi kutoka Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA). PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU


  0 0

  *Ahimiza ushiriki wao kwenye ujenzi wa viwanda
  *Aahidi kutoa milioni 700/- Chuo cha Polisi Dar


  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

  RAIS Dk.John Magufuli ametoa maagizo kwa vyombo vya ulinzi na salama kujipanga kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za uchumi ikiwemo ujenzi wa viwanda nchini.

  Ametoa kauli hiyo leo Desemba 21, 2018 jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mafunzo ya maofisa wa Polisi na wakaguzi wasaidizi wa jeshi hilo zilizofanyika viwanja vya Chuo cha Polisi ambapo amesisiiza umuhimu wa vyombo vya ulinzi kujikita kwenye shughuli za kiuchumi.

  "Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama jipangeni kushiriki kwenye kujenga uchumi wa nchi yetu.Hakuna ubaya kuwa na kiwanda cha kutengeneza viatu, maji na nafaka.Sioni sababu ya kila mara jeshi la polisi kupewa mchele kutoka kwa watu binafsi.Jeshi la Magereza mnao wafungwa ambao wanapaswa kulima na kuzalisha chakula cha kutosha ambacho mnaweza kukigawa kwa taasisi nyingine,"amesema Rais Magufuli.

  Wakati huo huo Rais Dk.Magufuli ameahidi kutoa Sh.milioni 700 kwa lengo la kuboresha Chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam na kutaka fedha hizo zitumike vizuri na kinyume na hapo zitageuka kuwa kaa la moto huku akisistiza ameamua kutoa fedha hizo kwa lengo la kulinda heshima na hadhi ya chuo hicho.

  "Fedha hizo nitazitoa kabla ya Ijumaa ya wiki ijayo , kubwa zaidi fedha hizo zitumike kwa malengo ambayo nimeyakusudia.Nimekusikia Mkuu wa Chuo hichi cha Polisi Naibu Kamishna wa Polisi (DCP)Anthony Rutta ukiomba Sh.milioni 700 nitakuletea ili parekebishwe na kupendeza .Najua sisi Serikali tunahamia Dodoma lakini hapa chuoni lazima pawe pazuri na pakuvutia.

  "Kwa Jeshi la Magereza niliamua kutoa fedha ili kujengwe nyumba z askari lakini hazikujengwa , wakati mwingine unapata shida kwasababu unatoa fedha zijengwe nyumba lakini hazijengwi.Nimeshatoa maagizo hizo fedha zifuatiliwe ili nijue zilikopotelea,"amesema Rais Magufuli.
   Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia Viongozi wa Majeshi na Serikali pamoja na Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia Viongozi wa Majeshi na Serikali pamoja na Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Saimon Sirro akizungumza mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
  Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhe.Ahmad Masauni akizungumza mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Omary Mahita akitoa salamu zake mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
  Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Paredi ya Maafisa na Wakaguzi wahitimu wa Jeshi la Polisi katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
  Paredi ya Maafisa na Wakaguzi wahitimu wa Jeshi la Polisi ikipita mbele ya Mgeni rasmi Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
  Wahitimu Maafisa na Wakaguzi wa Jeshi la Polisi wakiapa kiapo cha Utii na Uadilifu mbele ya Mgeni rasmi Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
   Maafisa na Wakaguzi wapya wa Jeshi la Polisi wakitoa salamu ya heshima walipopita mbele ya Mgeni rasmi Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba

  PICHA NA IKULU  0 0

  Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

  MDOGO wake mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, Akram Azizi amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya Sh.milioni 259.5 au kwenda jela miaka 20 jela baada ya kukiri mashtaka 73 ya kukutwa na nyara za Serikali.

  Hukumu hiyo imetolewa leo mahakamani hapo ambapo Akram amefanikiwa kulipa faini kwa kulipa fedha hizo, hivyo amekwepa kifungo cha kwenda jela miaka 20 jela.Hata hivyo Mahakama imeamua kuitaifisha nyara hizo na kuwa mali ya Serikali na kuamuru silaha zote ziwe chini ya Polisi hadi mshitakiwa atakapokamilisha taratibu za kisheria za kumiliki silaha.

  Akram alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Oktoba 31,2018 akikabiliwa na mashitaka 75 katika kesi namba 82/2018 ikiwemo kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018 lakini kwa mujibu wa sheria alifutiwa mashitaka hayo na kusomewa upya mashitaka 73 ukitoa ya utakatishaji fedha na meno ya tembo.

  Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri aliyetoa hukumu hiyo amesema katika mashitaka ya kukutwa na nyama ya nyati, mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh. 43,529,000 na katika makosa 72, yaliyobaki kila moja atatakiwa kulipa Sh milioni tatu.Katika mashitaka hayo 72, jumla ya faini aliyotakiwa kulipa Akram ni Sh.milioni 216. Alisema mshitakiwa akishindwa kulipa faini hiyo atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela.

  Awali kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Paul Kadushi akisaidiana na Wakili wa Serikali Wankyo Simon aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa adhabu kali kutokana na uzito wa makosa hayo ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya vitendo hivyo na kuomba Mahakama itaifishwe nyara zote iwe mali ya Serikali.Hata hivyo mshitakiwa alidai anasumbuliwa na shinikizo la juu la damu na kwamba ni mkosaji wa kosa la kwanza, ana watoto 10 wanaomtegemea
  pamoja na mama yake mzazi ambaye ni mzee.

  0 0


  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akizungumza na washiriki wa Wizara hiyo (hawapo Pichani) waliohudhuria mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu ambayo yamekamilika leo mkoani Morogoro.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya siku tano ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu ambayo yamefungwa leo mkoani Morogoro.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu.

  .............................

  Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha amesema ni kosa kusambaza nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini ya Mamlaka husika, hivyo ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria kwa watumishi watakaobainika kusambaza nyaraka hizo.

  Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Morogoro wakati akifunga semina ya mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu kwa baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo na kusisitiza kuwa hakuna mtumishi yeyote wa serikali asiyefahamu kuwa kutoa nyaraka za serikali bila idhini ni kosa la jinai.

  “Kumekuwa na usambazaji wa nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini na kwa bahati mbaya wakati mwingine unakuta nyaraka imewekwa mhuri wa siri lakini bado unaikuta huko, watumishi wa serikali lazima watambue kuwa kuna utaratibu wa kutoa nyaraka za serikali na kuna sheria ambazo zinawabana wale wote wanaotoa taarifa hizo bila kuidhinishwa”alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.

  Mhe. Ole Nasha amewataka watumishi hao kutambua kuwa hakuna taasisi yeyote inayoweza kufanya kazi bila kuwa na kumbukumbu au nyaraka hivyo amewataka kuhakiksha utunzaji mzuri na salama wa nyaraka hizo kwani ni nguzo muhimu katika kufanikisha utendaji wa majukumu.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu, Moshi Kabengwe amesema mafunzo hayo yametolewa ili kusaidia watumishi kufanya kazi ambazo zitaleta tija kwa jamii inayohudumiwa na kuondoa changamoto ambazo zimebainika katika utoaji wa huduma.

  Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku tano na yameshirikisha watumishi zaidi ya 50 kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Makao Makuu, Vyuo vya Ualimu vilivyopo Morogoro na baadhi ya watumishi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).

  0 0

  *Ni baada ya kusambaza taarifa ya kuruhusiwa kufanya maonesho nje ya nchi.


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaonya wasanii kutoka kundi la WCB   Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz 'na Msanii mwenzake Raymond Mwakyusa 'Rayvan' kuacha kusambaza taarifa za uongo.

  Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA Onesmo Kayanda baada ya wasanii hao kutoa kauli jana ya kuruhusiwa kufanya maonesho nje ya nchi baada ya kuwaandikia barua baraza na kuwaomba na wakawaruhusu.

  Baraza limekanusha habari zinazosambaa kwenye vyombo vya habari hususani mitandao ya kijamii kuwa limewaruhusu Diamond na Rayvan.

  Mnamo Desemba 18 2018, Baraza liliwafungia wasanii hao kutokujiahughulisha na sanaa ndani na nje ya nchi kwa kipindi kisichojulikana kutokana na kutumia kwa makusudi wimbo wa Mwanza ambao umefungiwa kwa sababu za kimaadili.

  Baraza limeendelea kusisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao Diamond na Rayvan kufanya onesho lolote la sanaa ndani na nje ya nchi.

  Aidha, baraza kwa mara nyingine linawataka wasaii hao kutii maagizo waliyopewa na kuacha mara moja kupotosha umma kwa kusambaza taarifa za uongo kabla ya hatua kali zaidi kuchukuliwa dhidi yao.


older | 1 | .... | 1758 | 1759 | (Page 1760) | 1761 | 1762 | .... | 1898 | newer