Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI OMARY MGUMBA AFANYA KIKAO NA WATUMISHI WA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI DAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe.Omary Mgumba, Amefanya Kikao na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mapema leo Jijini Dar es Salaam akiwa safarini kikazi kuelekea Mkoani Ruvuma.
 
Naibu Waziri Mgumba amewasitiza watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano na ueledi ili kutimiza dhima ya Serikali ya awamu ya Tano ili kuleta maendeleo katika uzalishaji wa chakula kupitia kilimo cha Uhakika cha Umwagiliaji kuelekea Tanzania ya viwanda.
 Picha ya Pamoja Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba akiwa na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Umwagiaji katika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini dar es Salaam.
Katika Picha Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba akiongea na watumishi wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji (hawapo pichani) katika Ofisi za Wizara hiyo Jijiini Dar es Salaam, kushoto ni Bi Aida Tesha Afisa Utawala Mkuu wa Tume hiyo.
 Katika Picha ni baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba.
 Baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Mhe . Omary Mgumba.

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA YAFANYA UPASUAJI KWA ZAIDI YA WATOTO 1000

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

TAASISI ya moyo ya Jakaya Kikwete imefanikisha kufanya upasuaji kwa zaidi ya watoto 1000 ikiwa ni upasuaji mkubwa kwa watoto 600 na upasuaji mdogo kwa zaidi ya watoto 400. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mbio za Heart Marathon kwa mwaka 2019 Rais wa Tanzania Health Summit (THL) Dkt. Omary Chillo amesema kuwa mbio hizo zitafika kilele Aprili 28, 2019 katika viwanja vya Coco Beach ikiwa ni mara ya nne tangu kuanzishwa kwake na kusema kuwa malengo ya kuendesha mbio hizo ni kusaidia juhudi za serikali za kupunguza magonjwa yasio ya kuambukiza kwa kupitia michezo na kuchangia fedha kwa ajili ya watoto wanaohitaji upasuaji katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Aidha amesema kuwa zawadi zitakazotolewa ni pamoja na fedha taslimu zenye jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa wakimbiaji watakaokimbia mbio za kilomita 21, kilomita 5 na mita 700 kwa watoto na ameziomba taasisi mbalimbali nchini kuchangia na kushiriki katika mbio hizo kupitia tovuti yao ya www.heartmarathon.com ili kuweza kuokoa maisha ya watoto na wananchi kutoka katika janga la magonjwa yasiyoambukizwa.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Dkt. Naiz Majani amesema kuwa wanaungana na taasisi ya Tanzania Health Summit katika mbio hizo ili kuweza kuwachangia watoto wenye matatizo ya moyo kuweza kupata matibabu.

Dkt. Majani amesema kuwa kuanzia mwaka 2015 matibabu ya moyo yalianza kufanyika hapa nchini na hasa katika masuala ya upasuaji na hadi kufikia sasa jumla ya watoto 1040 wamepata matibabu ambapo watoto 600wamefanyiwa upasuaji mkubwa na zaidi ya watoto 400 wamefanyiwa upasuaji mdogo.

Pia amesema kuwa serikali imejipanga katika kuhakikisha matibabu yanatolewa nchini na hadi sasa wameshapatiwa wodi maalumu kwa ajili ya matibabu ya watoto pekee.Pia mmoja wadhamini hao kutoka Nexlaw Advocate, Wakili Upendo Mmbaga amesema kuwa ni mara ya pili wanadhamini mbio hizo ikiwa ni moja ya majukumu yao ya kusaidia huduma za afya hasa kuhusiana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Aidha amewapongeza THS kwa kutoa hamasa kwa jamii na amezishauri taasisi na mashirika mbalimbali kushiriki katika kuelimisha umma kuhusiana na magonjwa hayo na wao kama Nexlaw Advocate wametoa jumla ya shilingi milioni 7 ili kuweza kufanikisha mbio hizo.


Rais wa Taasisi ya Tanzania Health Summit (THS) Dkt. Omary Chillo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na msimu wa mbio za Heart Marathon kwa mwaka 2019 na kueleza kuwa tangu kuanza kwake 2016 zaidi ya watu 3000 wamekimbia na watu 1000 wamefanyiwa vipimo vya magonjwa yasiyoambukizwa, leo jijini Dar es Salaam.



Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dkt. Naiz Majani akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mbio za Heart Marathon na namna taasisi hiyo ilivyofanikiwa na kufanya upasuaji kwa watoto zaidi 1000, leo jijini Dar es salaam


Upendo Mmbaga (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 7 Rais wa taasisi ya Tanzania Health Summit (THS) Dkt. Omary Chillo na kuhaidi kuendelea kushirikiana nao ili kufanikisha azma ya uelewa wa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kwa jamii na kuongeza nguvu katika juhudi za serikali za kukabiliana na magonjwa hayo, leo jijini Dar es salaam.(Picha na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii)

Waziri Mhagama-Bilioni 16 zimetumika Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Kigoma na Dodoma.

$
0
0
Na. OWM, Kigoma.

Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Biashara, kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji unaotekelezwa katika mkoa wa Kigoma na Dodoma, umefanikiwa kuboresha Mazingira ya Biashara na uwekezaji katika mikoa hiyo kwa kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 16 hadi kufikia Desemba 2018.

Mradi huo ambao utekelezaji wake unajikita katika Uwekezaji na Biashara katika Halmashauri kupitia mfuko wa (SIFF), Kuimarisha minyororo ya thamani pamoja na kuimarisha majadiliano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, tayari umefanikiwa kuboresha Mazingira ya Biashara kwa Wakulima na wavuvi wa mkoani Kigoma.

Akiongea katika ziara yake mkoani Kigoma wakati wa kukagua shughuli za utekelezaji za Baraza la Taifa la Biashara, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amefafanua kuwa Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana na Mradi huo wameweza Kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia uwekezaji kwenye miradi midogo midogo inayochochea ongezeko la ajira na kipato.

“Nimetembelea Mwalo na Soko la Samaki la Kibirizi, hapa mkoani Kigoma nimeridhishwa jinsi Mradi huu ulivyoboresha miundo mbinu ya mwalo huu katika kuhakikisha wavuvi wanapunguza upotevu wa mazao ya samaki na dagaa. Niyaombe Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya yaendelee na mfumo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi ili kuhakikisha walengwa wa mradi huu wanaendelea kunufaika” Alisisitiza Mhagama.

Mhagama alifafanua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amekuwa akisisitiza kupunguza vikwazo na kero kwa wafanyabiashara lakini pia Kuimarishwa kwa mahusiano kati ya Serikalii na Sekta Binafsi na kuongezeka kwa ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika Mipango ya Serikali.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo, Mratibu wa Mradi (Masuala ya Majadiliano ya Sekta ya Umma na Binafsi), Andrew Mhina alibainisha kuwa Mradi huo unalenga kuhakikisha kuwa unaboresha mazingira ya Biashara na uwekezaji nchini tayari umeandaa mwongozo wa Majadiliano Kati ya Serikali na Sekta Binafsi ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kuyajengea uwezo Mabaraza ya Mikoa yaweze kuwa endelevu na yenye ufanisi ambapo Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana.

Katika ziara hiyo, Waziri Mhagama, pamoja na kutembelea mwalo wa soko la Samaki la Kibirizi waziri alitembelea Kituo cha Biashara (One Stop Business Centre – Kigoma), Soko la Jioni la Mwanga, na Mradi wa Kuwezesha Vijana Kushiriki katika Kilimo Biashara na Mnada wa Mifugo Buhigwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Biashara Manispaa ya Kigoma Ujiji, Festo Nashoni, juu ya Uboreshaji wa chanja za kuanika dagaa katika mwalo wa Soko la samaki la Kibirizi wakati akikagua shughuli za Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akiongea na wafanyabiashara wa Soko la Jioni la Mwanga, mkoani Kigoma, ambalo limeboreshwa na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza mfanyabiashara, Justina Damas, Soko la Jioni la Mwanga mkoani Kigoma, ambalo limeboreshwa na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji, (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA UPANUZI WA BARABARA YA MOROGORO KUANZIA KIMARA – KIBAHA YENYE UREFU WA KM 19.2 ITAKAYOJENGWA NJIA NANE KWA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Roberth Mfugale akitoa maelezo ya mradi wakati wa hafla  ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata Utepe  na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Kisiasa pamoja na Viongozi wa Dini wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Kisiasa pamoja na Viongozi wa Dini kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai mara baada ya kufunua kitambaa kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mbunge wa Kibamba  John Mnyika (CHADEMA) wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mbunge wa Ubungo Said Kubenea (CHADEMA) wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso(Mb) alaipowasili katika hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wanachama wa Ccm Ramadhan Madabida,Erasto Kwirasa,Salum Madenge na Christopher Sanya ambao waliorejeshwa kwenye chama na NEC  Desemba 18,2018 ,wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam.Desemba 19,2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Spika wa Bunge Job Ndugai,Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Agustino Mahiga,Waziri wa TAMISEMI Suleiman JaffoWazri wa Maji Profesa Makame Mbalawa,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Seleman Kakoso,Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda pamoja na Viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam.Desemba 19,2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Spika wa Bunge Job Ndugai,Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Agustino Mahiga,Waziri wa TAMISEMI Suleiman JaffoWazri wa Maji Profesa Makame Mbalawa,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Seleman Kakoso,Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda pamoja na Viongozi wengine wakipiga makofi mara baada ya kuimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam.Desemba 19,2018


 Muonekano wa barabara ya Morogoro ambayo ipo katika hatua za ujenzi Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia Wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
PICHA NA IKULU

HOTUBA YA RAIS DKT.MAGUFULI WAKATI WA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI BARABARA YA KIMARA - KIBAHA. KM 19.2

MAGAZETI YA LEO AL-HAMISI DESEMBA 20.2018

Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy

$
0
0
Na Grace Michael, Nachingwea

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa mpango wa Ushirika Afya ndio njia pekee na ya kisasa inayomwezesha mkulima kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote na kuepukana na upotevu wa fedha nyingi kwa kulipia gharama za matibabu.

Amesema kuwa ili mkulima aweze kunufaika na fedha anazozipata kutokana na kuuza mazao yake ya biashara ni lazima awe na uhakika wa kupata huduma za matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Ameyasema hayo wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya upatikanaji wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma pamoja na uhamasishaji wa wananchi na wakulima kujiunga na mpango wa Ushirika Afya ili waweze kunufaika na huduma za matibabu kwa gharama nafuu.

“Ndugu zangu wana Nachingwea, nafahamu kabisa mmeweka mipango mingi kwenye fedha zenu mtakazopata kutoka kwenye mazao mliyouza lakini niwaombe sana katika vipaumbele vyenu suala la Ushirika Afya liwe ni miongoni mwake, kuwa ndani ya mpango huu kunakusaidia wewe na familia yako kutokupoteza fedha zako unapopatwa na magonjwa,” alisema Mhe. Ummy.

Alifafanua kuwa gharama atakayotumia mkulima huyo kujiunga na Ushirika Afya ni ndogo sana ikilinganishwa na kugharamia huduma za matibabu kwa fedha taslimu hali ambayo imesababisha wananchi wengi kuingia kwenye umasikini kwa kuuza mali zao ili wapate fedha za kujitibia.

“Kuwa ndani ya NHIF ni nafuu kubwa sana, familia itakuwa na amani wakati wote hata pale wanapopatwa na magonjwa, gharama kwa mtu mmoja kupitia Ushirika Afya ni shilingi 76,800 tu lakini unatibiwa katika vituo vya ngazi zote hapa nchini na hata kwa yale magonjwa ya gharama kubwa hivyo niwaombe sana mtakapopata fedha mhakikishe mnajiunga mara moja,” alisema Mhe. Ummy.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga aliwahakikishia wananchi wilayani Nachingwea kuwa, Mfuko umejipanga vyema katika kutoa huduma kwa wanachama wake kwa ngazi zote za vituo vya kutolea huduma za matibabu.

Alisema kuwa Mfuko umeweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha unawafikia wananchi katika maeneo yao na kuwasajili lengo ni kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na huduma za matibabu kupitia NHIF.

Katika hatua nyingine, Waziri Ummy aliwahakikishia wananchi hao juu ya upatikanaji wa huduma za matibabu kuwa ni mzuri na bora zaidi hususan upatikanaji wa dawa ambao ni zaidi ya asilimia 93 katika vituo vya kutolea huduma. 

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akielezea umuhimu wa kujiunga na Ushirika Afya kwa viongozi wa Vyama vya Ushirika wilayani Nachingwea.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mhe. Hassan Masala.

 Wananchi wilayani Nachingwea wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akielezea upatikanaji wa huduma za matibabu.
 Wananchi wakisoma vipeperushi vya Ushirika Afya wakati wa uhamasishaji wilayani Nachingwea.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi fomu 1,000 kwa Kiongozi wa Vyama Vya Ushirika wilaya ya Nachingwea.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi kadi kwa Mwanaushirika aliyejiunga na mpango wa Ushirika Afya.
 Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi. Rukia Muwango akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Benard Konga wakifuatilia maelezo ya Mhe. Waziri.Mhe. Waziri akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya Ushirika katika Wilaya ya Nachingwea.

Zaidi ya wanafunzi 4,000 hatarini kukosa masomo wilayani Ilemela

$
0
0

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG.


Zaidi ya wanafunzi 4,000 waliohitimu darasa la saba mwaka huu na kufaulu, wako hatarini kukosa fursa ya kujiunga na kidato cha kwanza hapo mwakani kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa katika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.


Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula aliyasema hayo jana wakati akipokea mifuko 100 ya saruji kutoka benki ya Diamond Trust (DTB).


Dkt. Mabula alisema wanafunzi 8,350 wamefaulu mtihani wao wa darasa la saba lakini kuna upungufu wa vyumba 84 vya madarasa hivyo wenye uhakika wa kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza ni wanafunzi takribani 4080. Wilaya ya Ilemela ilishika nafasi ya kwanza kwa ufaulu mkoani Mwanza na kitaifa nafasi ya sita.


Hivyo Dkt. Mabula alisema mifuko hiyo ya saruji kupitia taasisi yake ya The Angeline Foundation inayoshirikiana vyema na Halmashauri ya Ilemela, itasaidia kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha wanafunzi waliofaulu wanapata nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza ambapo aliwahimiza wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo.


Naye Meneja wa DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor alisema benki hiyo itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijamii katika Mkoa Mwanza hususani katika sekta ya elimu na afya.

Kutoka kushoto ni Meneja Msaidizi DTB Tawi Kuu la Mwanza, Ezra Shandu, Meneja DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor, Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula pamoja na Afisa Masoko DTB Tawi Kuu la Mwanza, Boniphace Mwita.
Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula akishiriki zoezi la kupanda miti iliyotolewa na Benki ya "DTB" katika Shule ya Msingi Kitangiri C
Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Msaidizi DTB Tawi Kuu la Mwanza, Ezra Shandu (kushoto), Meneja DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor ( wa pili kulia) na Afisa Masoko DTB Tawi Kuu la Mwanza, Boniphace Mwita (kulia).
Tazama BMG Online TV hapa chini
Benki ya Diamond Trust (DTB) yamuunga mkono Mbunge wa Nyamagana

MAJALIWA AKUTANA NA BODI YA TCCIA PIA AKUTANA NA MAWAZIRI PAMOJA KAMISHINA WA UHAMIAJI NA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC

$
0
0


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya TCCIA, Ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Desemba 19, 2018.
PMO_2567PMO_2566
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao cha Kazi alichokiitisha cha kujadili namna ya kuondoa kero zinazowapata wawekezaji  kuhusu upatikanaji wa vibali vya Kazi na Uhamiaji. Kikao  hicho kilichofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Desemba 19, 2018, kiliwahusisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni (watatu kushoto) ,  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,  Anthony Mavunde (watatu kulia), Kamishina wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala (wapili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geofrey Mwambe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAA YAAHIDI KUBORESHA HUDUMA KUANZIA JANUARI 2019

$
0
0

 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia), changamoto zinazoikabili Mamlaka hiyo, wakati alipotembelea kukagua miundombinu mbalimbali kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
2-min
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na Menejimenti na Waandishi wa Habari baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela.
3-min
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) jana akizungumza na Wafanyakazi wa Kampuni ya inayotoa huduma kwa abiria na mizigo ya Swissport Tanzania, Bi. Sarah Mlawa (kushoto) na Fliora Temba, alipokuwa akikagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
4-min
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) akimsikiliza Msimamizi Kitengo cha Mitambo, Bw. Gregory Kosamu (wa pili kushoto) aliyekuwa akielezea mifumo ya Kiyoyozi ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Roichard Mayongela na kushoto ni Kaimu Meneja Matengenezo na Huduma za Kiufundi, Bi. Diana Munubi.
5-min
Madereva wanaotoa huduma ya usafiri wa taxi katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakizungumza na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alipokuwa akikagua miundombinu ya Kiwanja hicho jana.
6-minRaia wenye asili ya Asia kuanzia kulia Bi. Amina Alblai, Bi. Amata Zavery na Bw. Aunali Zavery wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alipofanya ukaguzi kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela. (PICHA NA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA).

………………………
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, ameahidi kufanya Maboresho makubwa katika Miundombinu ya Viwanja vya Ndege Tanzania na katika kuhamasisha kasi ya utendaji ya wafanyakazi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.

Hayo ameyazungumza mbele ya Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kufanya ukaguzi wa miundombinu katika jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Awali Waziri Kamwelwe alianzia ziara yake Katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe na kubaini kwamba njia ya kuruka na kutua ndege imejegwa chini ya kiwango na mkandarasi lakini pia alipotua JNIA alibaini pia baadhi ya changamoto.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Kamwelwe ametoa maagizo kwa TAA kwamba kuanzia Januari mwakani kuwe na mabadiliko katika namna ya utendaji.
“Nawaomba ndugu zangu kuanzia Januari mwakani mbadilike na kama mtu hata badilika basi tutamtoa. Malalamiko ya watu mimi nayapokea na ninayafanyia kazi, kwa maana hiyo ni vyema pia muyafanyie kazi”, alisema Mhandisi Kamwelwe.

Bw. Mayongela akizungumza kwa niaba ya Menejimenti katika kikao hicho amebainisha kwamba ujio wa Waziri ni changamoto kwa watendaji wote wa TAA kila mtu ajithimini katika kipindi hiki na kukaa tayari kwa ajili ya maboresho makubwa na utendaji wa kasi wa Mamlaka.

“Kwa niamba ya Wenzangu tunakuahidi kwamba kuanzia januari mwaka unapoanza tutajitahidi kufanya kazi kwa weledi na kwa uadilifu Mkubwa. Kwa upande wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kuendelea kulalamikiwa kwa kwa mambo madogo madogo ya kiutendaji haioendezi na ni aibu kwetu, mimi mwenyewe kama mtendaji mkuu nitachukua hatua na kuhakikisha kwamba tunakipa hiki kiwanja kipaumbele”.

Hatahivyo, Waziri Kamwelwe amewatakia watanzania wote heri ya sikukuu za mwisho wa Mwaka na kuwaasa kwamba watumie hii nafasi kujiandaa ili kuja kufanya kazi vizuri mwakani.

UCSAF KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA KWA WANACHI WA PEMBA

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akiwasili kisiwani Pemba kukagua changamoto za mawasiliano. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maida Hamad Abdallah na wa kwanza kushoto ni Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Baucha
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyenyoosha mkono) akijadiliana na Shehia wa Sheha ya Kiungoni, Omari Khamisi Othman kuhusu eneo la kujenga mnara wa mawasiliano katika ziara yake ya kukagua changamoto za mawasiliano Pemba. Aliyevaa miwani akisikiliza kwa makini ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Peter Ulanga
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akiwa kwenye boti eneo la Makangale – Mnarani akikagua upatikanaji wa mawasiliano wakati wa ziara yake Pemba. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maida Hamad Abdallah na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Peter Ulanga



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano ya simu za mkononi kwa wananchi waishio kwenye Mkoa wa Kaskazini kisiwani Pemba na kubaini kuwa yapo baadhi ya maeneo yana usikivu mdogo wa mawasiliano na mengine hakuna kabisa mawasiliano ya simu za mkononi

Nditiye aliambatana na Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maida Hamad Abdallah ambaye ndiye chimbuko la ziara hiyo kwa kuuliza maswali Bungeni wakati wa vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu changamoto ya mawasiliano kisiwani Pemba.

“Zipo changamoto mbali mbali ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, wananchi wanapata tabu za kuwasiliana hasa nyakati za usiku hasa wakipata msiba au mgonjwa, tuliwasilisha changamoto hizi Bungeni ili ziweze kutekelezwa,” amesema Maida

Nditiye amebaini uwepo wa usikivu mdogo wa mawasiliano na ukosefu wa mawasiliano wakati wa ziara yake kwenye Shehia ya Kiungoni – Wingwi, Dodeani, Kiuyu Mbuyuni, Sizini – Chwaka, Tumbe, Kipande Konge na Makangale – Mnarani zilizopo kwenye Wilaya ya Micheweni pamoja na kwenye Shehia nyingine za Weni – Tungamaa – Machwengwe, Mtambwe, Mkanjuni na Kivumoni zilizopo kwenye Wilaya ya Wete

“Kuna maeneo ambayo minara ipo ila mawasiliano hayana nguvu na sehemu nyingine hakuna mawasiliano kabisa kutokana na jiografia ya Pemba, nimekuja na wataalamu wa kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), nimewaelekeza hili walifanyie kazi, raha yangu ni kuona wananchi wote wana wasiliana,” amesema Nditiye

Amefafanua kuwa masuala ya mawasiliano ni masuala ya muungano ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanzisha UCSAF ili kupeleka mawasiliano nchi nzima, Tanzania Bara na Visiwani kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara

“Nimeshuhudia hapa nilipo hamna mawasiliano na simu yangu ni kopo tu, sipati mtandao wowote”, amesema Nditiye. Ameongeza kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa popote ambapo hamna mawasiliano wanafikisha mawasiliano kwa wananchi, kwa kuwa akiwa njiani ziarani humo ameshuhudia ukosefu wa mawasiliano

Katika ziara hiyo, Nditiye aliambatana na Mtendaji Mkuu wa UCSAF Mhandisi Peter Ulanga ambapo amemwelekeza kuchukua maeneo yote ambayo hayana usikivu wa kutosha na yale ambayo hayana mawasiliano kabisa ili waanze kuyafanyia kazi mapema mwezi Januari mwakani

“Tunachukua changamoto hizi ili tuweze kuongeza usikivu wa mawasiliano” amesema Mhandisi Ulanga. Ulanga ameongeza kuwa UCSAF itahakikisha mwananchi akiwa ndani au nje ya nyumba yake kwenye eneo lote la kisiwa cha Pemba mwananchi anapata mawasiliano mazuri

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamisi Othmani amemwambia Nditiye kuwa, “tuna imani ujio wako utatuondolea changamoto ya mawasiliano katika mkoa wa Kaskazini na kisiwa cha pemba kwa ujumla kwa kuwa umeona hali halisi,”

Sheha wa Shehia ya Kipange, Ramadhan Omari Ahmed akizungumza kwa niaba ya masheha wenzake amesema kuwa anamshukuru Nditiye na msafara wake pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maida Hamad Abdallah kwa kupata ujio huu ili kufika maeneo hayo ambapo amesema kuwa, “hamna mawasiliano popote ya TIGO, Vodacom au Zante, pale tunapohitaji mawasiliano tunakwenda sehemu kama vile kupanda juu ya mlima au uende kwenye uwanja wa mpira au kwa kutembea umbali wa kilomita 1.5 hadi 3.1 kutafuta mawasiliano,”.

“Ni faraja kubwa sana kwa kutembelewa na kuja kusikiliza maoni ya wananchi kwa kuwa mawasiliano hayako vizuri, tukitaka kupiga simu tukiwa ndani inatukwaza, hatupati mawasiliano, lengo tupate mawasiliano na wametuahidi tatizo la mawasiliano sio tu kwa Kiungoni ila litaisha Pemba yote”, amesema Shehia wa Kiungoni, Omary Khamisi Othmani

“Kilio hiki kimetukwaza muda mrefu, naamini alichokuarifu Maida kitafanyiwa kazi, tumefarijika sana kuona viongozi mnashuka hadi chini kusikiliza wananchi, naamini wataalamu wako wataifanyia kazi changamoto ya mawasiliano ili wananchi waweze kuwasiliana,” amesisitiza Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Salama Mbarouk Khatib

Katika hatua nyingine, Nditiye amekagua vituo viwili vya TEHAMA kati ya kumi vilivyojengwa na UCSAF kwenye kisiwa cha Unguja na Pemba ili wanafunzi waweze kujifunza TEHAMA na wananchi watumie TEHAMA ambapo ametoa wito kwamba wananchi waruhusiwe kutumia bure kituo cha TEHAMA kwa muda kabla ya kuanza kuwatoza gharama za uendeshaji wa vituo hivyo ili wafaidi matunda ya Serikali yao

Nditiye ameongeza kuwa mawasiliano ni ulinzi na usalama na mawasiliano ni uchumi ambapo mwananchi akiwa na simu, inamuwezesha kuuza na kununua kiurahisi bidhaa zake, hivyo kwa kutumia TEHAMA tunajiunga na dunia kupitia mawasiliano

VIWAVIJESHI VYAWATESA WAKULIMA WA MAHINDI MBEYA

RAIS MAGUFULI: TUNATAKA TANZANIA IWE KAMA ULAYA

HOSPITAL YA WILAYA YA MBINGA INAKABILIWA NA CHANGAMOTO NNE

$
0
0

Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mbinga Mkoni Ruvuma inakabiliwa na changamoto kubwa nne zinazopelekea kushindwa kutoa matibabu bora kwa wananchi. Akizungumza na Ruvuma TV on line Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo Dkt Nicholas Kapunga , amesema kwa sasa tiba wanazotoa haziwafikii walengwa ipasavyo hivyo anaiomba serikali isaidie kutatua changamoto hizo ili waweze kutoa huduma za matibabu bora kwa walengwa. Kwa undani wa habari hii tizama video yake. 

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA UJENZI WA DARAJA JIPYA NA BARABARA UNGANISHI TOKA AGA KHAN HADI COCO BEACH

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Cho Tae-ick kufunua pazia kuashiria   kuwekwa kwa jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine wanashuhudia.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana  na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Cho Tae-ick   baada ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine wanashuhudia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana  na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe baada ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine wanashuhudia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakipata maelezo toka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Robert Mfugale kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selanderna Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018    
 Hili ndilo eneo la  Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selanderna Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach kama linavyoonekana jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018. Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Robert Mfugale, toka hapo eneo la ufukweni hadi sehemu ya baharini  itajengwa barabara unganishi juu ya tuta la mita 600 kabla ya daraja kuanza na kuishia kwenye ncha ya ardhi kule ambako ndiko CoCo Beach.  

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea kwenye sherehe za kuweka jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018.
PICHA NA IKULU

Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ( wa pili toka kulia) akipewa maelezo ya kitaalamu juu ya matumizi ya vifaa tiba vilivyotolewa na mradi wa Uzazi Salama na mmoja wa wawakilishi wa mradi huo (wa kwanza Kulia).
Baadhi ya Vifaa tiba vilivyotolewa na mradi wa Uzazi salama Mkoa wa Rukwa kwa Ofsi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo. Wakuu wa Wilaya za Sumbawanga, Kalambo na NKasi (kushoto) wakiweka saini mkataba wa usimamizi wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) katika hafla fupi ya uzinduzi wa Kampeni ya “JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA” katika Mkoa wa Rukwa.



Mradi wa uzazi salama Mkoani Rukwa umekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi 211,145,850/= kwa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa ili kuvisambaza katika vituo 198 vya kutolea huduma za afya, ikiwa ni muendelezo wa jitihada na dhamira yao ya kuhakikisha wanashirikiana na Mkoa katika kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto katika Mkoa.

Mradi huo unaoundwa kwa ushirikiano wa mashirika matatu ya Plan International Tanzania, AFRICARE na JHPIEGO kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Canada umekabidhi vifaa hivyo vikiwemo vitanda vya kujifungulia, vifaa vya upasuaji kwa kinamama wajawazito, vifaa vya kumsaidia mtoto mchanga na mama kupumua, vifaa vya kuwasaidia watoto njiti, majokofu ya kuhifadhia damu na vifaa vya kufanyia tathmini ya hali ya lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanaratibu kufanyika kwa siku ya afya kwa mwaka mara moja kwa kila kijiji na kuwataka wakuu wa wilaya wasimamie zoezi hilo. Na kuwaomba wanaume, wazee na viongozi wote wa dini pamoja na vijiji kutambua jukumu la afya ya uzazi na mtoto pamoja na familia ni la wote na sio la kinamama na wanawake peke yao.

“Viongozi wa serikali katika ngazi za vijiji na kata wanao wajibu wa kuhakikisha akina mama wanahudhuria katika vituo vya afya pindi wanapojigundua ni wajawazito kwa huduma na ushauri wa kiafya. Tuwe mstari wa mbele kuelimisha wengine hasa vijana wetu kuhusu afya ya uzazi na kuwasisitiza kushiriki katika matukio mbalimbali yahusuyo afya kama huduma rafiki kwa vijana na siku ya afya ya kijiji “village health day” yanayoratibiwa na mradi wa Uzazi Salama.”

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Plan International Tanzania Paul Lusato aliziomba halmashauri pamoja na vituo vinavyotoa huduma za afya vitakavyopatiwa vifaa hivyo kuhakikisha wanavitunza vizuri ili kuendelea kutoa huduma tarajiwa kwa wananchi.

“Tunashauri pia viongozi katika ngazi ya mkoa kuendelea kutembelea maeneo ambayo wadau mbalimbali wa maendeleo wametoa msaada ili kujiridhisha kuwa uwekezaji uliofanywa unathaminiwa na kutunzwa na kuwa na manufaa yaliyotarajiwa,” Alibainisha.

Awali akitoa taarifa ya huduma za afya ya uzazi na mtoto Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu alieleza kuwa katika kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka 2018 tayari kina mama 39 wameshapoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi ambayo ni sawa na uwiano wa vifo 97 kati ya vizazi hai 100,000 huku watoto wachanga 537 wakipoteza maisha kwa kipindi hicho hicho ambao ni sawa na uwiano wa vifo 14 katika kila vizazi hai 1000.

Makabidhiano hayo yamefanyika pamoja na uzinduzi wa kampeni inayojulikana kwa jina la “JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA” katika Mkoa wa Rukwa, Kampeni ambayo ilizinduliwa kitaifa tarehe 6 Novemba, 2018 na Mh.Samia Suluhu Hassani, Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayolenga kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga nchini Tanzania.

MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM TAIFA AKUTANA NA KAMATI YA SIASA MKOA WA PWANI

$
0
0

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Francis Koka pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya utambulisho kama Mlezi wa Chama hicho mkoa wa Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Kibaha mjini Bi. Azilongwa Bohari pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya utambulisho kama Mlezi wa Chama hicho mkoa wa Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndugu Ramadhani Maneno (kulia) akimtambulisha Mlezi wa CCM mkoa huo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani mara baada ya kujitambulisha rasmi kama Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani, hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya mji Kibaha.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani mara baada ya kujitambulisha rasmi kama Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani, hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya mji Kibaha.



Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kutumia fedha za ndani zaidi kwenye shughuli za kimaendeleo kuliko kutegemea misaada.

Mhe. Samia ameyasema hayo leo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Pwani kwenye ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Kibaha.Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alijitambulisha rasmi kama mlezi wa CCM mkoa wa Pwani na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha .

Akizungumza na Wajumbe hao Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Chama mkoani hapo kuhakikisha mali zote za Chama zinaleta tija kwa Chama.“Sasa ni wakati umefika kuangalia mali zetu ndani ya Chama labda Wilaya ilikuwa inamiliki vitu gani? Viwanja vya kujenga nyumba au vya michezo mali zozote ni kuziweka vizuri na kuhakikisha zinazalisha kwa manufaa ya Chama.”

Mhe. Samia amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kimejipanga kutoa mafunzo ya Uongozi katika ngazi mbali mbali ambapo yeye binafsi amepangiwa mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Morogoro ambapo atashirikiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndugu Rodrick Mpogolo.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Samia amewataka Viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani kufanya kazi kwa Umoja na Ushirikiano ndani ya Chama pamoja na Serikali.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Ramadhani Maneno amemshukuru Mjumbe huyo wa Kamati Kuu kwa kuja kujitambulisha na kutoa muongozo mzuri uliokubalika na kila mjumbe na kuahidi kutoa ushirikiano mzuri kwa manufaa ya Chama Cha Mapinduzi.

MAVUNDE AFANYA ZIARA YA GHAFLA TIC KUFUATILIA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde amefanya ziara ya ghafla kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kwa lengo la kufuatilia maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambayo aliyatoa Desemba 4 mwaka huu.

Baadhi ya maagizo hayo ni pamoja na uboreshaji wa utoaji wa huduma kwa wawekezaji kupitia Mfumo wa Mahala Pamoja 'One Stop Facilitaion Centre', ambapo Waziri Mkuu baada ya kupata maelezo kuna mambo hakukubaliana nayo na hivyo akatoa maagizo.

Hivyo Mavunde amefanya ziara ya ghafla TIC ili kujionea namna shughuli hizo zinavyoendeshwa hasa katika Idara ya Kazi. Akiwa TIC amezungumza na maofisa kutoka Wizara/Taasisi/Idara/Mamlaka mbalimbali wanaotoa huduma kwa wawekezaji ,kupitia mfumo wa Mahala Pamoja na kuwakumbusha kuwa wao ni sehemu ya uchakataji wa vibali na leseni mbalimbali za wawekezaji, hivyo waongeze kasi katika kutekeleza majukumu yao ili huduma husika zipatikane kwa wakati sahihi.

Aidha ,baada ya mazungumzo hayo Mavunde amefanya kikao kazi kati yake na Kamishna wa Kazi Tanzania Gabriel Malata, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe na Ofisa Kazi Mfawidhi ndani ya Mfumo wa Huduma za Mahala Pamoja TIC, Emiliana Rweyendela.

Ziara ya Naibu Waziri inakuja takribani wiki mbili tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea TIC na kukutana na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TIC na kutoa maagizo ya kufanya maboresho mbalimbali ya utoaji wa huduma bora kwa wawekezaji ndani ya Mfumo wa Mahala Pamoja.

Imeelezwa kuwa tangu Waziri Mkuu atembelee TIC kituo hicho chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji kimefanya kikao na Kamishna wa Kazi Tanzania, Kamishna Mkuu wa TRA, Kamishna wa Uhamiaji Tanzania na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kwa pamoja walikubaliana kuboresha mifumo ya utoaji wa vibali, kutoa elimu kwa umma juu ya taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kupata vibali husika na kufanya kazi kama timu ili kushauriana zaidi katika utoaji wa vibali mbalimbali kwa wawekezaji.

Pia kama sehemu ya kazi za kila siku, kituo kinaendelea kushughulikia changamoto za uwekezaji kwa kushirikiana na wadau husika ili kufikia lengo la kuwa na mazingira bora ya uwekezaji nchini yatakayowezesha kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya Wananchi na Taifa kiujumla.

MSD NA AGA KHANI WAKUBALIANA KUFANYA KAZI PAMOJA

$
0
0


MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki, wa Taasisi Aga Khan, Sulaiman Shahabuddin wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya Kiutendaji jijini Dar es Salaam Desemba 20 2018. Wanaoshuhudia (kulia) ni Meneja Msaidizi wa Kisheria wa Hospitali ya Aga Khan, Kieran Kitojo na Mwanasheria Mkuu wa MSD, Christopher Kamugisha. (Imeandaliwa na Robert Okanda)

MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Laurean Bwanakunu akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya utiliaji saini makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji na Taasisi ya Taasisi Aga Khan. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Hospital ya Aga Khan, Lucy Kwayu.
MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki, wa Taasisi Aga Khan, Sulaiman Shahabuddin wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wandamizi wa Taasisi waliohudhuria hafla hiyo.

Rais Dkt Magufuli alivyochomekea Tanzanite Bridge liwe jina la daraja jipya la kisasa la selander

Viewing all 46329 articles
Browse latest View live




Latest Images