Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA UCHUKUZI AENDA KIMYA KIMYA KITUO CHA MABASI UBUNGO,ABAINI UPANDISHWAJI NAULI KIHOLELA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

HALI ya usafiri katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam hasa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka inaonekana kubadilika kutokana na nauli kupandishwa kiholela bila kufuata utaratibu was Serikali.

Uwepo wa madalali katika kituo hicho nao umeelezwa unachangia kuongezeka kwa adha ya usafiri na hivyo abiria kutoa ombi kwa Serikali kuhakikisha kituoni hapo taratibu zinafuatwa.

Hayo  yamebainika baada ya Waziri wa  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe kufaya ziara kituoni hapo kuona hali ya usafiri akiwa kama abiria ambapo hata yeye alipewa nauli mpya ambayo haiko katika bei elekezi.

"Nimefika kitoni hapo saa 11:15 alfajiri nakuzunguka kwenye baadhi ya mabasi na kubaini  baadhi ya abiria kulipishwa nauli tofauti na bei elekezi ya  Serikali,"amesema Mhandisi Kamwelwe.Amesema baada ya ukaguzi amebaini abiria kulipa nauli tofautitofauti inatokana na kuwepo kwa madalali nje ya kituo.

Hivyo amesema kuna haja yakupekeka mapendekezo bungeni  ili kuwepo kwa tiketi za mfumo wa kieletroniki zitakazosaidia kuondokana na  ulanguzi unaoumiza abiria.Baadhi ya abiria wamesema kinachosababisha nauli ipande ni madalali wanaokatisha tiketi nje ya kituo.

Mmoja wa abiria Joseph Malisa amesema unapoenda kwenye ofisi au gari husika unaambiwa gari limejaa lakini nje ya kituo unakuta madalali wanauza tiketi za basi hiyo waliodai kuwa imejaa."Unapofika kwenye gari au ofisi zao unaambiwa nafasi zimejaa lakini nje ya kituo madalali wanauza tiketi kwa bei ya juu na mimi nataka kusafiri inanililazimu kukata bei ya juu" amesema Malisa.

 Abiria nwingine  Emili Msuya amesema kupanda kwa nauli kiholela kumechangiwa na watu wasio rasmi ikiwemo wapiga debe wanaolundikana ndani ya kituo, hivyo Serikali iangalie utaratibu wa kuwaondoa.Meneja wa Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam Imani Kasagala amesema mabasi yote yanapaswa kuingia ndani ya kituo cha mabasi Ubungo badala ya wamiliki kupaki nje na kutafuta madalali ambao ndio chanzo cha   kwa nauli hizo kupanda.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ramadhan Kailima amesema kuwa abiria wakiona kuna kupandishiwa nauli wanatakiwa kutoa taarifa.Amesema mabasi yote yanakaguliwa na kupongeza Ukaguzi unaofanywa katika kituo hicho. 
 Askari wa Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi katika kituo  Kikuu cha  Mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam. 
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ramadhan Kailima akizungumza na abiria katika basi wakati alipofanya ziara katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ramadhan Kailima akipewa maelekezo na Askari wakati alipofanya  ziara kuangalia Usalama wa abiria katika mabasi wanayosafiri nayo leo jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Madereva Wafanyakazi (TADWU) Shaban Mdemu akizungumza na waandishi habari wakati ukaguzi wa mabasi ya mikoani kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya wananchi wakiangalia ukaguzi katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ramadhan Kailima Kailima akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofanya ziara katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Usalama Barabarani katika Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi Ibrahim Samwix akizungumza na waandishi habari kuhusiana na ukaguzi  wa mabasi katika kituo cha mabasi leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akiwa katika basi mara alipofanya ziara katika kituo Kikuu cha Mabasi ikiwa ni kuangalia hali ya usafiri kuelekea siku za mwisho wa mwaka,jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Akabidhi Vyeti kwa Wahitimu 345 wa Fani ya Uandishi wa Habari Chuo cha Uandishi wa habari DJS

$
0
0


 Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO  na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wanafunzi wahitimu wa stashahada na Astashahada katika fani ya Uadishi wa Habari( hawapo pichani)  katika mahafari ya 23 ya Chuo cha Uandishi wa Habari (Dar es Salaam School of Journalism ) DSJ iliyofanyika leo katika ukumbi wa chuo hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam, wa  pili kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Joachim Rupepo na kushoto ni Rais wa Serikali ya wanafunzi katika chuo hicho Ester Zalamula na Mwalimu kutoka chuo hicho.
2
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wanafunzi na wazazi katika mahafali ya 23 ya  kutunuku stashahada na Asatashaha katika fani ya Uadishi wa Habari DSJ iliyofanyika leo katika ukumbi wa chuo hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam.
34
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akikabidhi cheti kwa wahitimu waliofanya vizuri katika  vitengo mbalimbali kutoka Chuo cha Uandishi wa Habari (Dar es Salaam School of Journalism) ,DSJ katika mahafli ya 23 ya chuo hicho iliyofanyika leo 20 Desemba, 2018 katika ukumbi wa chuo hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam.
5
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi( watatu kushoto aliyeshika maiki)  akiwatunuku vyeti vya kumaliza Stashahada na Astashahada ya Uandishi wa Habari wanafunzi kutoka Chuo cha Uandishi wa Habari (Dar es Salaam School of Journalism)  DSJ, mahafali ilifanyika leo chuoni hapo
6
Wahitimu wa Stashahada na Astashahada ya Uandishi wa Habari kutoka Chuo cha Uandishi DSJ wakivaa Kofia zao mara baada ya kutunukiwa vyeti vyao katika mahafali iliyofanyika  leo chuoni hapo.
7
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo cha Uandishi wa Habari (Dar es Salaam School of Journalism)  DSJ pamoja na Walimu wa chuo hicho mara baada ya kwatunuku vyeti wahitimu 345 wa Stashahada na Astashahada ya Uandishi wa Habari katika mahafali iliyofanyika leo chuoni hapo.
8
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan  Abbasi akiwaaga wahitimu na Wazazi mara baada ya kutunuku veyti kwa 345 wa Stashahada na Astashahada ya Uandishi wa Habari katika mahafali iliyofanyika leo Desemba 20, 2018, chuoni hapo  wapili kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Joachim Rupepo.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO  

MWENYEKITI WA UVCCM SONGWE AKUTANA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI WILAYA YA ILEJE,ACHANGI LAKI TANO

$
0
0
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege, mapema leo amekutana na kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje mbali na maagizo na maelekezo mbalimbali aliyowapa, lakini pia aliwachangia fedha taslim shilingi Laki Tano ( 500,000/-)  ili kulipia fidia ya eneo la zaidi ya ekari 20 la UVCCM ambapo inahitajika milion 2 kulipia fidia na baadae taratibu za kupata hati miliki zitafuata.

Ndg Kadege amesisitiza hadi januari mwishoni lazima tuwe tumemalizana na jambo la fidia kisha tuanze mchakato mapema wa kupata hati na kuanza kutekeleza mipango yetu ya kuhakikisha UVCCM tunakuwa na miradi mbalimbali  na kukuza uchumi na kujitegemea ili kuepukana na hii omba omba toka kwa wadau ambao mara zote wamekuwa na masharti ya kiuchaguzi.
Pia kamati ya Utekelezaji UVCCM wilaya ya Ileje ilimpatia zawadi ya kuku kwa ajili ya Christmass.
HapaKaziTu
TukutaneKazini
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege, akikabidhi kiasi cha shilingi laki tano kwa kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje  ili kulipia fidia ya eneo la zaidi ya ekari 20 la UVCCM, ambapo inahitajika milion mbili kulipia fidia na baadae taratibu za kupata hati miliki zitafuata.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege akipokea jogoo wa sikukuu kutoka kwa kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje mara baada ya kukutana nao mapema leo.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege akisaini kitabu cha wageni mapema leo baada ya kukutana na kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje

WATENDAJI DODOMA WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA ZAIDI WAWEKEZAJI

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith   Mahenge akifungua kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
????????????????????????????????????
Muwakilishi wa Katibu Mtendaji wa  Baraza la Taifa la Biashara Bw. Patrick Mavika akizungumza wakati  wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
????????????????????????????????????
Wajumbe wa Baraza la Biashara la mkoa wa Dodoma wakifuatilia kikao  kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma   Bw. Godwin  Kunambi  akizungumzia  fursa zilizopo katika Jiji Dodoma wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
????????????????????????????????????
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii  (ESRF) Bw. Mussa Martine akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
????????????????????????????????????
Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe akizungumza wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………….

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amewataka watendaji wa Mkoa wa Dodoma kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kujenga mazingira rafiki na kuboresha mazingira ya biashara.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua kikao kazi cha siku moja cha Baraza La Biashara Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo Desemba 21, 2018 katika Chuo cha Mipango.Dkt.Mahenge aliwataka watendaji kuzingatia utendaji wenye weledi, tija na unaovutia wawekezaji kuwekeza mkoani humo  kwa kuzingatia kuwa ndiyo Makao Makuu ya Nchi.
“lazima utendaji wetu uwe wa namna bora na upekee katika kuweza kuvutia wawekezaji kwa kuwa na miundombinu rafiki ya biashara na kutatua changamoto zozote zinazoweza kuwakwamisha wawekezaji”.Alieleza Dkt.Mahenge.

Aliongeza kuwa, Halmashauri zote zione umuhimu wa  kuboresho mazingira ya uwekezaji na kutumia fursa zilizopo katika kufikia malengo ya kujenga uchumi endelevu.“Nivyema sasa kila Halmashauri ikaona fursa na kuzitumia ikiwemo zile za kifedha na kuhusisha taasisi za kifedha ikiwemo Mabenki ili kuona kila lengo linafikiwa na kuwa na uwekezaji wenye tija nchini”.alisisitiza Dkt.Mahenge
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi alieleza umuhimu wa kuzitumia fursa zilizopo Dodoma na kuwa na uwekezaji wenye tija kwa kila eneo kwa kuzingatia mazingira yaliyopo.

“Lazima fursa zilizopo Dodoma zitumike kwa malengo yenye tija kwa kuhakikisha mkoa unabaki kuwa kivutio cha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ,”Alieleza Kunambi.Aliongeza kuwa Jiji hilo limetenga maeneo mbalimbali ya uwekezaji na kuyapima kulingana na mahitaji ya uwekezaji ikiwemo ya viwanda, Biashara na makazi.Kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kimefayika ili kupitia muongozo wa uwekezaji katika mkoa wa huo hali itakayochochea uwekezaji na kukuza uchumi na kuchochea maendeleo

WAGONJWA WA SARATANI WAONGEZEKA KUTOKA 2500 HADI 6500.

$
0
0

Na.WAMJW-LINDI

SERIKALI Kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa kutoka kipindi cha mwaka 2002 mpaka hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la Wagonjwa wa Saratani kutoka wagonjwa 2500 hadi wagonjwa 6500, kutokana na mitindo tofauti ya maisha na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya na uhamasishaji kwa wakulima kujiunga na mfuko wa Bima ya afya (#UshirikaAfya) katika Mkoa wa Lindi.

"Kama Serikali, Tumeshtushwa na ongezeko la Wagonjwa wa Saratani na magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza, mwaka 2002 wagonjwa wa Saratani nchini walikuwa kati 1500 mpaka 2000, lakini kwa takwimu za mwaka Jana, wagonjwa wa Saratani wameongezeka kutoka 2500 hadi 6500" alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Serikali imeona upo ulazima wa kuchukua hatua za makusudi katika kupambana na Saratani ya Mlango wa kizazi na magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza yakiwemo shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na ugonjwa wa Kisukari.

Pia, Waziri Ummy alisema kuwa katika kila Wagonjwa 100 wa Saratani, Wagonjwa 34 ni wa Saratani ya mlango wa Kizazi, Wagonjwa 12 ni wa Saratani ya Matiti, kibaya zaidi katika kila Wagonjwa 100 wa Saratani, Wagonjwa 80 wanafika wakiwa wamechelewa na wengine ugonjwa ukiwa katika hatua ya tatu au ya nne, hivyo kupona kwao kunakuwa ni kugumu.

Awali akisoma taarifa ya Mkoa, Katibu tawala Mkoa wa Lindi Bi. Rehema Madenge alisema kuwa Mkoa umeweza kuanzisha utoaji wa chanjo ya kukinga Saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa Wasichana wa umri wa miaka 9 hadi 14 ambapo leo tutashudia ikizinduliwa na rasmi kimkoa na Waziri wa Afya mhe. Ummy Mwalimu.

Hata hivyo Bi. Madenge alisema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 jumla ya mahudhurio 164,259 yalirekodiwa katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya vya Serikali, binafsi na vile vya dini huku Hospitali ya Mkoa Sokoine ikirekodi mahudhurio 39,324 na kulipwa shilingi 1,654,964,965 katika kipindi hicho.

"Mkoa umeendelea kuhudumia wanufaika wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) kwa ufanisi mkubwa na katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 jumla ya mahudhurio 164,259 yalirekodiwa katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya vya Serikali, binafsi na vile vya dini" alisema Bi. Madenge

Aidha, alisema kuwa ili kuweza kuwafikia wananchi wengi kupitia makundi mbali mbali, mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekuja na mpango uitwao #Ushirika Afya ambapo wakulima wanaungana pamoja katika vyama vyao vya mazao na kuweka mkakati wa kujiunga na Bima ya Afya kwa utaratibu wa ushirika wao.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa maelekezo ndani ya chumba cha kuhifadhi Dawa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya kwa wananchi mkoani Lindi.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyefika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya kwa wananchi.
 Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akikagua miundombinu  katika chumba cha X- ray  wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya kwa wananchi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akiongea na wananchi (Hawapo kwenye picha)  waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya kwa wananchi

KUMBUKUMBU

$
0
0


 “Hata ingawa ninatembea katika bonde lenye kivuli kizito, Siogopi chochote kibaya,Kwa maana wewe uko pamoja nami; Fimbo yako na gongo lako ndivyo vitu vinavyonifariji.” (Zaburi 23:4)

LUTENI KANALI (MSTAAFU) WILLY JOHN MASOI


Miaka 4 imetimia leo tangu Mwenyezi Mungu alipokuita kwake. Hata hivyo kutokana na upendo wako kwetu tunaamini Baba yetu kipenzi unaendelea kutulinda, kutusimamia na kutuongoza katika kila tufanyalo. Baba, endelea kuimba na Malaika.

Unakumbukwa na mke wako kipenzi Mary-Salome, watoto, wakwe, wajukuu, shemeji, ndugu, jamaa, marafiki na majirani zako.

Raha ya Milele umpe, ee Bwana, na Mwanga wa Milele Uingazie Roho ya Marehemu Luteni Kanali (Mstaafu) Willy John Masoi. Apumzike kwa Amani, Amina. Zab: 23:4

UJUMBE MAALUM KUTOKA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)

DKT. MWANJELWA AELEKEZA KUSIMAMISHA MISHAHARA YA WAAJIRI NA MAAFISA UTUMISHI WATAKAOWASILISHA TAARIFA ZISIZO SAHIHI KWENYE MFUMO WA MALIPO YA MISHAHARA (HCMIS)

$
0
0

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimali Watu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Ibrahim Mahumi (kushoto) akifafanua majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Baadhi ya watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji




Mishahara ya Waajiri na Maafisa Utumishi watakaobainika kuwasilisha taarifa za kiutumishi zisizo sahihi kupitia Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS) itasimamishwa mara moja na Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kuwakumbusha waajiri na maafisa hao kuhakikisha wanawasilisha taarifa sahihi na kwa wakati.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kufahamu vema majukumu ya idara hiyo.

Ili kuimarisha nidhamu ya utendaji kazi, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kutosita hata mara moja kusimamisha mshahara wa mwajiri au afisa utumishi yeyote atakaebainika kuwasilisha taarifa zenye udanganyifu na kuwataka kutozifanyia kazi na kuzirejesha mara moja kwa waajiri na maafisa hao.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameainisha kuwa, lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa Ofisi ya Rais-Utumishi hata kosa linapokuwa kwa waajiri, hivyo amewataka waajiri wote nchini kuhakikisha wanatenda haki kwa kuwasilisha taarifa sahihi na kwa wakati ili ziweze kufanyiwa kazi.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amehoji kuwa, inawezekanaje mtumishi wa umma kukatwa mshahara wake kwa madai ya kukopa kwenye taasisi ya kifedha wakati hajakopa? na ni kwanini mtumishi husika asiarifiwe na mwajiri au afisa utumishi juu ya makato hayo?

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameeleza kuwa, kuna uwezekano wa baadhi ya waajiri na maafisa utumishi kushiriki katika mchezo mchafu wa kutumia mishahara ya watumishi kujinufaisha, hivyo amesisitiza watakaobainika wachukuliwe hatua za kinidhamu, kisheria na kusimamishiwa mishahara yao pale inapobidi, lengo likiwa ni kurejesha nidhamu ya kazi na kuimarisha uwajibikaji katika Utumishi wa Umma.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amehuzunishwa na kitendo cha watumishi wa umma kudai malimbikizo ya mishahara ya muda mrefu wakati maafisa utumishi wanaowahudumia wapo, na amehoji uhalali wa uwepo wao wakati malalamiko mengi kuhusu malimbikizo ya mshahara (arreas) yamekuwa yakiendelea kuwasilishwa kwa wingi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuchelewa, hivyo amewataka kuwajibika ipasavyo ili kupunguza malalamiko hayo.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ibrahim B. Mahumi amesema kuwa, majukumu ya msingi ya Idara hiyo ni kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika usimamizi wa rasilimaliwatu, kuratibu malipo ya mishahara ya watumishi wa umma kupitia Mfumo wa Malipo ya Mshahara (HCMIS) na kuhakikisha utumishi wa umma nchini unakuwa na watumishi wenye sifa stahiki.

ACP Mahumi ameainisha kuwa, Idara ina sehemu kuu tatu zinazotekeleza majukumu, ambazo ni eneo la usimamizi wa rasilimaliwatu, eneo la Usimamizi wa Orodha ya Malipo ya Mishahara (Payroll) na eneo la Uhakiki wa Rasilimaliwatu na Malipo ya Mshahara na kuongeza kuwa, kazi kubwa ya eneo la Usimamizi wa Rasilimaliwatu ni kuandaa Ikama na Bajeti ya Mishahara ya Serikali.

ACP Mahumi amefafanua kuwa, pia Idara yake ina jukumu la kutoa vibali vya ajira mpya na mbadala Serikalini, kuhakiki uhalali wa sifa za watumishi wa umma wanaoajiriwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma na kuidhinisha taarifa hizo pamoja na nyingine za kiutumishi na mishahara zinazowasilishwa na waajiri kwa usahihi kupitia Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS).

Kuhusu utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa Mhe. Dkt. Mwanjelwa, (ACP) Mahumi amethibitisha kuwa, Idara yake itatekeleza na tayari imeshaanza kuchukua hatua kwa kuwasimamishia mishahara maafisa utumishi zaidi ya 56 walioshindwa kutekeleza wajibu wao, na watumishi wengine zaidi ya 500 wenye dhamana ya kufanya kazi kwenye Mfumo wamefikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa makosa mbalimbali yanayohusu kuchezea mfumo ikiwa ni pamoja na baadhi ya waajiri waliohusika.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameitembelea Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Utawala Bora ili kuhimiza uwajibikaji.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI , MAKATIBU WAKUU,WATENDAJI WA WIZARA ZA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI NA WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI

$
0
0


PMO_2625PMO_2633
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao cha Kazi alichokiitisha Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es salaam, Desemba 22, 2018.  Kikao hicho kiliwahusisha Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji kutoka Wizara za  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na baadhi ya Taasisi zilizo chini ya Wizara hizo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DKT. ABBASI: SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI HAKI ZA WAANDISHI WA HABARI

$
0
0
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi mara baada ya kuwasili katika semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambako Dkt. Abbasi alikuwa Mgeni Rasmi.
3
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala( wa tatu kulia)  akitoa moja ya maada zilizokuwa zikijadiliwa kwenye Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam,  kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Ofisi ya Shekhe Mkuu wa Tanzania, Haris Othmani na Kushoto ni `Mkurugenzi Mkuu TAMWA Eda Sanga, Mwanyekiti wa Blogu (Bloggers ) Joachim Mushi, Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Hassan Abbasi wakifuatilia semina hiyo.
4
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina ya Jukumu la Mwanahabari wakati wa utoaji maada katika semina hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
5
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina Jukumu la wanahabari wakati wa utoaji maada katika semina hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi wakifuatilia semina hiyo.
7
9
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza jambo  kuhusu maada ya uhuru wa habari kwa mwandishi katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akifuatilia hotuba hiyo na kushoto ni Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa wakifuatilia maada hiyo.
10
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa dini pamoja na watoa maada katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)
……………………

Na Mwandishi Wetu,MAELEZO,DAR ES SALAAM.

SERIKALI imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi  na kuimarisha misingi ya haki na wajibu ya waandishi wa vyombo vya habari nchini ili kuwawezesha kutekeleza vyema majukumu yao yaliyoanishwa katika Mikataba na Sheria mbalimbali za kitaifa na Kimataifa.

Hayo yamesema leo Jumamosi (Desemba 22, 2018) Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi na wahariri wa vyombo vya habari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu ya Shia Ithsheriya.

Dkt. Abbasi alisema kwa kuzingatia Mikataba na Sheria mbalimbali za Kimataifa ikiwemo Kifungu cha 19 cha Mkataba wa Kimataifa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kiutendaji ili kuhakikisha maboresho na tasnia ya habari na utangazaji inapiga kubwa za maendeleo.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema moja ya mafanikio ya Serikali ni pamoja na kutungwa kwa Sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari na Sheria Haki ya Kupata Taarifa ambazo kwa kiasi zimeweka mazingira wezeshi ikiwemo kuwepo kwa vipengele vya kisheria zinazopaswa kutekelezwa na Taasisi za umma na Binafsi katika utoaji na upatikanaji wa taarifa kwa umma.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema pamoja na kuwepo vya vipengele hivyo vya kisheria, Serikali pia iliamua kuweka kipengele cha haki ya ukusanyaji, usambazaji na upatikanaji wa taarifa katika jamii kupitia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo pia imewazesha waandishi wa habari kutekeleza vyema majukumu yao.

“Katika Sheria hizi kwa mara ya kwanza katika historia ya Nchi yetu na hata Bara la Afrika kwa ujumla wake, waandishi wa habari wamepewa haki tatu za msingi ambazo ni pamoja na Haki ya kukusanya Habari, Uhuru wa Kuhariri Habari pamoja na Uhuru wa kusambaza Habari, na hili limendelea kuwafanya kutekeleza vyema wajibu wao” alisema Dkt. Abbasi.

Aidha Dkt. Abbasi alisema Serikali kwa kutambua misingi ya haki na wajibu wa vyombo vya habari nchini kupitia mikataba mbalimbali ya kimataifa na Sheria za Kitaifa, waandishi wa habari wameendelea kupewa fursa kwao ya kueleza hisia zao katika masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa masuala mbalimbali ya kitaifa nchini.

Akifafanua zaidi Dkt. Abbasi alisema iwapo waandishi wa vyombo vya habari nchini wataweza kutambua wajibu na haki walionao katika jamii, itawawezesha utekelezaji wa haki zote za msingi zilizoanishwa kwa mujibu wa misingi ya kimataifa na Sheria mbalimbali za Kitaifa.

Awali Kiongozi Mkuu wa  Jumuiya ya Waislamu ya Shia Ithsheriya, Sheikh Hemed Jalala alisema nafasi ya waandishi wa habari katika jamii ni sawa na mitume ya mungu kwa kuwa wanawajibika kutambua maadili mema katika jamii ikiwemo kuhamasisha umoja, upendo na mshikamano ndani ya jamii.
Sheikh Jalala alisema waandishi wa vyombo vya habari watatakiwa kutafuta, kusambaza habari zilizo sahihi mbele ya jamii, kwa kuwa jukumu hilo la msingi litawezesha jamii kuishi katika mazingira yenye utulivu na kuimarisha misingi ya amani na utulivu.

KAKUNDA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUZINGATIA VIWANGO VYA KIMATAIFA

$
0
0

Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda akizungumza wakati akifungua semina ya ajira na maonesho ya ujasiriamali yaliyoandaliwa kwa pamoja na taasisi za AN NAHL, TAMPRO, TAMSIA, UKUEM na Pamoja Foundation kwa udhamini wa Taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation ya nchini Malaysia yanayofanyika katika viwanja vya city Garden jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa semina ya ajira wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda wakati wa ufunguzi wa semina hiyo na maonesho ya ujasiriamali yaliyoandaliwa kwa pamoja na taasisi za AN NAHL, TAMPRO, TAMSIA, UKUEM na Pamoja Foundation kwa udhamini wa Taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation ya nchini Malaysia yanayofanyika katika viwanja vya city Garden jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda akipata maelezo kutoka Afisa Mradi taasisi ya Milele Zanzibar Eshe Haji Ramadhan katika maonesho ya ujasiriamali yanayoendelea Dar es Salaam katika viwanja vya city Garden Gerezani Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda akimsikiliza Mjasiriamali wa taasisi ya SMV Health Centre Dk Hanifa Murithi Wakati wa semina ya ajira na maonesho ya ujasiriamali yaliyoandaliwa kwa pamoja na taasisi za AN NAHL, TAMPRO, TAMSIA, UKUEM na Pamoja Foundation kwa udhamini wa Taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation ya nchini Malaysia yanayofanyika viwanja vya city Garden jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni mwenyekiti wa Taasisi ya AN NAHL Trust Injinia Ally Shaban Kilima.
Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda akinunua bidhaa ya unga wa muhogo kutoka mjasiriamali kijana Zaheer Mfaume wa kampuni ya RUM-Zahrain wakati wa maonesho ya ujasiriamali na semina ya ajira katika viwanja vya City Garden Gerezani Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Tanzania (FAT) Alhaji Muhidin Ndolanga akifuatilia hotuba na waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda wakati wa ufunguzi wa semina ya ajira na maonesho ya ujasiriamali yaliyoandaliwa kwa pamoja na taasisi za AN NAHL, TAMPRO, TAMSIA, UKUEM na Pamoja Foundation kupitia programu ya GET HIRED kwa udhamini wa Taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation ya nchini Malaysia yanayofanyika katika viwanja vya city Garden jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi zilizoshiriki kuandaa semina ya ajira na maonesho ya ujasiriamali kupitia program ya GET HIRED kwa udhamini wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation ya nchini Malaysia yanayofanyika viwanja vya City Garden Gerezani Dar es Salaam.

………………………..
Na Mwandishi Wetu

Waziri wa viwanda na Biashara Joseph Kakunda amewataka wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini kuzingatia ubora wa bidhaa kwa kuangalia viwango vya kimataifa na kitaifa wakati wa kusambaza bidhaa zao.

Waziri Kakunda alisema hayo leo tarehe 22 Disemba 2018 wakati akifungua semina ya ajira pamoja na maonesho ya ujasiriamali yaliyoandaliwa kwa pamoja na taasisi za AN NAHL, TAMPRO, TAMSIA, UKUEM na Pamoja Foundation kupitia program ya GET HIRED kwa udhamini wa Taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation ya nchini Malaysia yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema, wafanyabiashara wa Tanzania ni lazima waelewe viwango vya kimatiaifa wakati wa kuzalisha bidhaa zao kwani mbali na kunufaika na ubora wa bidhaa lakini pia watakuwa wanaitangaza nchi na uzalishaji bidhaa wowote usio na ubora wanaopaswa kuwajibika ni wao.

Waziri wa Viwanda na Biashara alibainisha kuwa,kwa Tanzania kuna vyombo vinavyoangalia ubora wa bidhaa na kuvitaja kuwa ni shirika la viwango Tanzania ( TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na kusisitiza kuwa ili wafanyaiashara wafanye kazi kwa ufanisi wanapaswa kuzingatia masharti ya vyombo hivyo.

Hata hivyo, Kakunda alisema jukumu la kutangaza bidhaa inayozalishwa ni la wafanyabiashara na hivyo kuwataka kuhakikisha bidhaa zinakuwa na Msimbohuria (Barcode) kwa lengo la kutambulisha sehemu bidhaa ilipotoka ama kuzalishwa.

Kwa mujibu wa Kakunda, kukosekana kwa Barcode katika bidhaa za Tanzania kumesababisha baadhi ya wafanyabiashara wa nchi jirani kutumia mwanya huo kuonesha kama bidhaa hizo zimetengenezwa katika nchi hizo jambo linalofanya Tanzania kushuka katika soko la kimataifa.

Alisema, Tanzania imekuwa ikishuka katika soko la AGOA kadri miaka inavyokwenda na kufikia chini ya asilimia nne kutokana na kushindwa kujitangaza kimataifa wakati inazalisha bidhaa zenye ubora.

Kakunda alibainisha kuwa, kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano kwa sasa ni kuwa na viwanda vinavyosindika mazao ya kilimo kwa kuwa asilimia 70 ya watanzania wanajishughulisha na kilimo.

Kwa mujibu wa Kakunda, vipaumbele vingine ni viwanda vinavyoajiri wanachi wengi kama elfu moja pamoja na viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotumika majumbani kama vile mafuta ya kula, dawa za binadamu, chumvi sukari, unga maendeleo nguo.

Akielezea mafunzo ya ajira na maonesho ya ujasiriamali, Kakunda alisema kuwa vijana ni hazina ya kesho hivyo kuna kila jitihada za kuhakikisha nguvu kazi ya vijana haikumbani na kizuizi chochote kitakachowachelewesha kufikia malengo.

“Ni lazima tulinde kazi za vijana na wasiwekewe vigingi visivyo na maana na kama kuna figisu yoyote basi sisi kama serikali tuhakikishe inaondolewa” alisema Kakunda.

Awali Mwenyekiti wa Taasisi ya AN NAHL Injinia Ally Shaban Kilima alieleza kuwa semina ya ajira na maonesho ya ujasiriamali inayofanyika yana lengo la kuwapatia ujuzi vijana waliomaliza vyuo kuwa na ari ya kujiajiri na suala hilo limechagizwa na juhudi za serikali ya awamu ya tano kuelekea uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda.

Alisema juhudi za taasisi zilizoandaa semina na maonesho ya ujasiriamali ni kutekeleza ibara ya nane hadi kumi ya ilani ya CCM kuhusiana na masuala ya ajira kwa vijana.

Mmoja wa vijana anayeshiriki maonesho hayo Zaheer Mfaume kutoka RUM-Zahrain Investment inayozalisha unga wa Muhogo alisema maonesho yanayofanyika yanasaidia kutangaza bidhaa wanayozalisha. Hata hivyo alielezea changamoto kubwa inayowakabili kuwa ni uhaba wa masoko na kuiomba serikali kusaidia kuwatafutia masoko.

Yapi Merkezi yafanya usafi Ufukwe wa Coco

$
0
0
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii .

Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga Reli ya Kisasa imefanya usafi katika ufukwe wa Coco, ikiwa ni utunzaji wa Mazingira katika jamii inayowazunguka katika mradi wa Reli hiyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jioni ya leo, Mratibu wa Mazingira wa Kampuni hiyo Evodiaglory Mrengo amesema kuwa katika Ujenzi wa Reli wanatambua umuhimu wa utunzaji wa Mazingira katika kujenga afya salama kwa jamii wanayoizunguka katika miradi.

Amesema kuwa kufanya usafi  Ufukwe wa Coco ni mojawapo ya kazi za kijamii na Mazingira,na kwama kila Kampuni ikipata muda wa kufanya kazi ya kijamii ni vyema ikafavya hivyo.Mrengo amesema kuwa kufanya usafi ni kuhamasisha Wafanyakazi na jamii ya Mkoa wa Dar es Salaam kuwa mstari wa mbele katika utunzaji na uhifadhi wa fukwe za bahari ikiwa ni sehemu muhimu za mapumuziko.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira Oysterbay Peter Mushi amesema wanatambua mchango wa Kampuni ya Yapi Merkezi kufanya usafi katika ufukwe wa Coco.
 Wafanyakazi wa Yapi Markezi wakiweka Takataka katika mifuko walivyofanya usafi katika ufukwe wa Coco, leo jijini Dar es Salaam.
 Kiongozi Mkuu wa Afya na Mazingira wa Kampuni ya Yapi Markezi Erdem Yuksel akizungumza  kuhusiana na Kampuni hiyo kutoa mchango katika maeneo mbalimbali ikiwemo kufanya usafi katika ufukwe wa Coco leo  jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira wa Mtaa huo Peter Mushi akizungumza kuhusiana na Ujio wa Kampuni ya Yapi Markezi kufanya usafi katika ufukwe wa Coco,jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Mazingira wa Kampuni ya Yapi Markezi Evodiaglory Mrengo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na usafi wa Kampuni hiyo waliofanya katika Ufukwe wa Coco ,jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa Yapi Markezi wakifanya usafi katika ufukwe wa Coco ikiwa ni kutoa msaada kwa jamii

AIRBUS YATUA GHANA, KUTUA DAR KESHO SAA NANE UNUSU MCHANA

$
0
0
Accra, Ghana.
Ndege ya kwanza kati ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania imewasili Mjini Accra nchini Ghana ikiwa safarini kuja hapa nchini.

Ndege hiyo itawasili kesho majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Mhe. Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo imetua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege.

Balozi Mboweto wafanyakazi na baadhi ya abiria waliokuwapo katika uwanja huo wameonesha shauku kubwa ya kutaka kuiona ndege hiyo ambayo ni ya kwanza kutua Barani Afrika tangu kampuni ya Air-Bus ianze kutengeneza ndege za kizazi cha A220. “Wafanyakazi wa hapa uwanja wa ndege na baadhi ya abiria baada ya kutangaziwa kuwasili kwa ndege hii aina ya A220 wamekuwa na shauku kubwa ya kuiona na kwa kweli ni ndege nzuri inapendeza na inawavutia zaidi kumuona Twiga na jina la nchi yetu Tanzania ambalo lina sifa kubwa duniani” amesema Balozi Mboweto.

Balozi amesema Watanzania waishio Nigeria na Ghana wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano na Mhe. Rais Magufuli kwa mafanikio haya makubwa ambayo yatasaidia kukuza uchumi kupitia usafiri wa anga, utalii na uwekezaji.Ndege hiyo A220 iliondoka Montreal Canada jana saa 1:00 Jioni kwa saa za Canada na ikatua visiwa vya Santa Maria saa 5:00 usiku kwa saa za huko.

Hii leo imetua Accra Ghana majira ya saa 4:00 kwa saa za Ghana na kupokelewa na Balozi Muhidin Mboweto wa Nigeria anayehudumia na Ghana. Pamoja na marubani wa kampuni ya Air-Bus na Marubani wa Tanzania walioongoza katika safari ya ndege hiyo kuja nchini Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi ndiye anaongoza safari ya ndege hiyo kutoka Canada hadi itakapowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kesho Itatua  saa 8:30 mchana.
 

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA UJENZI

$
0
0

Karibu Tuelimishane Mambo Muhimu Kadhaa Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuanza Ujenzi

Unaweza Ku-Share Na Watu Zaidi Ujumbe Huu, Unaweza Ukawasaidia Sasa Au Hata Wakati Mwingine Kwa Namna Moja Au Nyingine


NOTE: Kufuata taratibu za kitaalamu katika UJENZI kunaweza kukusaidia kupunguza gharama za ujenzi mpaka 15% pamoja na kukuepushia hasara inayoweza kutokea mbeleni, sambamba na kukupatia kitu bora, kizuri na chenye thamani

1. Baada Ya Kuwa Umetayarisha Kiwanja Chako Kizuri Katika Eneo Ulilochagua, Anza Kujiridhisha Na Unachotaka Kujenga, kwa mfano

(i) Matumizi, jengo lako ni kwa ajili ya matumizi gani, makazi, biashara, ofisi, taasisi, starehe, godown/kiwanda n.k.

(ii) Jengo la aina gani, ghorofa au nyumba ya chini ya kawaida?

(iii) Unahitaji kuwe na vyumba vya matumizi gani(functional requirements) kama vile vyumba vingapi vya kulala pamoja na nini cha ziada kama vile movie theatre, maktaba n.k, kwa jengo la nyumba ya kuishi, au kama ni matumizi mengine ujue mahitaji yake

2. Tafuta mtaalamu wa majengo, msanifu au mbunifu majengo(architect), huyu ana utaalamu juu ya jengo, kazi zake na mipangilio yake yote ya kitaalamu. Atakushauri na kukuongezea uelewa wa sayansi ya majengo kwa ujumla

-Baada ya kumpeleka kuona eneo lako(site visit) mkajadiliana mkaelewana mwambie akafanye michoro ya mwanzo arudi mjadiliane na kujiridhisha kama kilichofanyika kimeendana na mahitaji yako, kisha mkishapitisha akafanye michoro ya 3D's(picha) za muonekano wa jengo husika uzione na ujiridhishe kama umeridhika na muonekano huo kisha ndio umruhusu amalizie michoro ya mwisho kwa ajili ya kufuatilia kibali cha ujenzi halmashauri husika
 
NB; Ni muhimu sana kujiridhisha na jengo lako usije kujuta baadaye au kujikuta unabomoa na kubadilisha baada ya kuona makosa, kwa sababu unakwenda kuweka pesa zako nyingi sana usije ukaingia gharama zaidi baadaye ambazo ungeweza kuziepuka mapema kwa kujiridhisha wakati wa michoro
Likifanyika vile unavyotaka utalifurahia na hutaona umepoteza

3. Kama jengo lako ni la ghorofa hutaishia hapo, unalazimika kumtafuta mtaalamu mwingine wa kutengeneza muundo wa mihimili ya jengo(structural engineer au mhandisi mihimili). Huyu hataongeza au kupunguza chochote ila atatumia michoro iliyofanywa na architect kutengeneza michoro ya muundo wa mihimili inayoshikilia jengo, kisha atakukabidhi michoro hiyo iliyopigwa mhuri kabisa kwa ajili ya kufuatilia kibali cha ujenzi halmashauri

4. Umeshakabidhiwa michoro yote ya msanifu/mbunifu majengo(architect) ambayo ni (architectural drawings) na ya mhandisi mihimili(structural engineer) ambayo ni (structural engineering drawings) yote ikiwa imepigwa mhuri utaenda nayo katika halmashauri yako kuomba kibali cha ujenzi ukiwa pamoja na hati yako ya kiwanja

5. Baada ya kupata kibali cha ujenzi halmashauri unaweza kuanza ujenzi lakini kama jengo lako ni la ghorofa utatakiwa kufuatilia vibali vingine kutoka kwenye bodi mbalimbali za ujenzi kutegemeana na ukubwa na matumizi ya jengo lako.

Bodi za ujenzi utakazopaswa kuchukua vibali kabla ya kuanza ujenzi wa jengo la ghorofa ni hizi zifuatazo;-

(i) AQRB(Architects Quantity Surveyors Registration Board)
(Hii ni bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi)

(ii) ERB(Engineers Registration Board)
Hii ni bodi ya Wahandisi

(iii) CRB(Contractors Registration Board)
Hii ni bodi ya Wakandarasi

Utapatiwa vibali vya bodi hizi(kwa mfumo wa stikers) ambazo utaweka kwenye kibao chako cha ujenzi kwa ridhaa za kampuni zilizokupatia huduma za ushauri wa kitaalamu na michoro husika

6. Baada ya hapo unaweza kuanza ujenzi sasa. Kitu cha kuzingatia ni kwamba siku hizi kuna usumbufu mwingi na ni vigumu kujenga bila kuwa na kibali hasa kibali cha halmashauri na hasa katika eneo lililopimwa, ni rahisi kukutana na usumbufu mkubwa.

 Faida nyingine za kupata kibali cha ujenzi ni kwamba utaingiza katika kumbukumbu zako na utaingia pia katika kumbukumbu za halmashauri husika hivyo inaweza kukusaidia muda wowote utakaohitajika kuwasilisha taarifa hizo sehemu yoyote kuhusiana na jengo lako katika kuonyesha uhalali wa umiliki na uhalali wa jengo lenyewe ili kukusaidia katika mambo mbalimbali

7. Mwisho napenda nigusie kidogo swala la matumizi ya eneo maana ni swala ambalo limekuwa changamoto kwa wengi katika kupata kibali
Kiuhalisia maeneo mengi yamepimwa kwa matumizi ya makazi japo kuna watu pia wengi wanaonunua maeneo kwa ajili ya kujenga majengo ya biashara au makazi biashara(residential apartments) Utakapotengeneza michoro kwa ajili ya jengo la biashara au makazi biashara wakati eneo lako hati inaonyesha matumizi yake ni makazi pekee hutapewa kibali na wakati huo pengine umeshafanya michoro yote na kuwalipa watu pesa halafu halmashauri wanakukwamisha na kukutaka uanze mchakato wa kuomba kubadili matumizi.

 Huu ni mchakato mrefu na utakaoweza kukuchukua tena muda mwingi na gharama wakati huo pengine ulishachukua mkopo ambao unatakiwa uwe umeanza kuulipa japo bado hujapata hata hicho kibali. Endapo umejikuta kwenye jambo kama hili unaweza kumtafuta mtaalamu mkashauriana nini cha kufanya kwa haraka wakati mchakato wa kubadili matumizi unaendelea

Karibu kwa swali au ufafanuzi wowote maana mengi nimeeleza kwa kifupi ili nisikuchoshe msomaji

Ahsanteni
Arch. Sebastian Moshi
+255717452790

HASUNGA ASIMIKWA KUWA CHIFU NZUNDA, ASEMA HAKUNA MBADALA WA CCM

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Katikati) amesimikwa Kiongozi wa Machief katika Wilaya ya Mbozi Chief Muleshwelwa Nzunda kuwa Chief Nzunda kutokana na majukumu makubwa anayoyafanya katika wizara yake sambamba na uwajibikaji uliotukuka katika Jimbo la Vwawa, Tarehe 22 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akicheza ngoma ya jadi, mara baada ya kuwasili Mkoani Songwe kwa ajili ya ziara ya kijimbo, Tarehe 22 Disemba 2018. 
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akicheza ngoma ya jadi, mara baada ya kuwasili Mkoani Songwe kwa ajili ya ziara ya kijimbo, Tarehe 22 Disemba 2018. 
Baadhi ya Machief Wilayani Mbozi wakifatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano uliofanyika leo tarehe 22 Disemba 2018 katika viwanja vya Stendi ya Maroli akiwa katika ziara ya siku tano ya kijimbo.
Baadhi ya wananchi Wilayani Mbozi wakifatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga wakati akihutubia kwenye mkutano uliofanyika leo tarehe 22 Disemba 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe.


Na Mathias Canal, Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) amesimikwa kuwa Chief Nzunda kutokana na majukumu makubwa anayoyafanya katika wizara yake sambamba na uwajibikaji uliotukuka katika Jimbo la Vwawa.

Mhe Hasunga amesimikwa kuwa Chief na Kiongozi wa Machief katika Wilaya ya Mbozi Chief Muleshwelwa Nzunda wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano uliofanyika leo tarehe 22 Disemba 2018 katika viwanja vya Stendi ya Maroli akiwa katika ziara ya siku tano ya kijimbo.

Sambamba na kusimikwa kuwa Chief Nzunda vilevile amekabidhiwa silaha za jadi ikiwemo mkuki wa kujilinda na maadui kutoka kwa Chifu huyo wa Mbozi.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo, Mhe Hasunga amewashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa mbunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi wa Octoba 25, 2015 jambo lililompelekea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kumteua kuhudumu katika Wizara muhimu nchini ya Kilimo.

Alisema ushindi wake katika kiti cha ubunge ulisababishwa na imani kubwa ya wananchi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani pamoja na changamoto mbalimbali ambazo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi na serikali ya Awamu ya tano lakini CCM Pekee ndicho kitakachowaletea maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa hivyo wananchi wanapaswa kuendelea Kukiunga mkono.

"Huu ni muda wa kuungana na Rais katika kuhakikisha nchi inasonga Mbele kijamii na kiuchumi, Itikadi za kidini, Kisiasa na kikabila zinapaswa kuwekwa kando kwa maslahi mapana ya Taifa" Amesema Mhe Hasunga na kuongeza kuwa "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Mhe Dkt John Pombe Magufuli anatuhimiza kufanya kazi kwa bidii na hivyo ili kupambana vizuri katika hali zetu kiuchumi ni wazi kuwa lazima tukubali kuweka siasa kando" 

Mhe Hasunga ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwani ndiyo silaha pekee ya maendeleo huku akisisitiza kuwa serikali inaendelea kuimarisha upatikanaji wa masoko ya mazao hivyo wakulima wanapaswa kuzalisha kwa bidii mazao mbalimbali ya kibiashara.

Aidha, ameahidi kuyafanyia kazi malalamiko ya wakulima kuhusu bei za pembejeo za kilimo ili kuwa na unafuu wa gharama zitakazoendana na uwezo wa wananchi.

WAFANYAKAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU WASHEREHEKEA SIKU YA FAMILIA KUAGA MWAKA 2018

Next: Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikitua kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikimwagiwa maji ikiwa ni ishara ya karibu na heshima (Water salute) kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Leonard Chamuriho wakisaini mkataba wa makabidhiano ya Ndege mpya ya Airbus 220-300 itakayokabidhiwa katika shirika la ndege la Tanzania mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakishuhudia kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Rubani mstaafu Kapteni Mapunda kutokana na uzalendo wake kwa Taifa kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rubani mstaafu Kapteni Mapunda na mkewe kutokana na uzalendo wake kwa Taifa na kumpa zawadia ya kiasi cha Tsh Milioni kumi kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Balozi wa Canada Pamela O’donnel pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya ndege na Mkewe Janeth Magufuli ,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na simu alipokuwa anakagua ndege mpya ya Airbus 220-300 ndani ya ndege hiyo na mmoja wa Marubani Kapteni Pandya aliyekuja na ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege mpya aina ya Airbus 220-300 na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi na Wafanyakazi wa Shirika La ndege la Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. PICHA NA IKULU KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
$
0
0
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben akifungua sherehe za Siku ya Familia ya Buzwagi na Bulyanhulu niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta Disemba 22,2018 katika viwanja vya Mgodi wa Buzwagi uliopo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu , Bw. Benedict Busunzu akielezea kuhusu Siku ya Familia ya Acacia mwaka 2018. Alisema kwa mara ya kwanza wameamua kuadhimisha siku ya Familia kwa kuwaleta pamoja wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na familia zao ili kuimarisha ushirikiano zaidi.

Wanafamilia kutoka kwa wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiangalia eneo la wazi la uchimbaji madini katika mgodi wa Buzwagi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Familia Buzwagi na Bulyanhulu, Kambula Lumbu akitambulisha wajumbe waliofanikisha maadhimisho ya sherehe hiyo.
Wanafamilia wa Buzwagi na Bulyanhulu wakicheza muziki.
Hermangild Seki kutoka mgodi wa Bulyanhulu na mkewe wakipokea zawadi ya majiko ikiwa ni zawadi ya ushindi iliyotokana na kuwa mstari wa mbele kuimarisha usalama mgodini.
Elizabeth Sambuka kutoka mgodi wa Buzwagi ambaye ni mfanyakazi bora mwaka 2018 kutokana na kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha usalama mgodini akipokea zawadi ya majiko ya kupikia.
Banana Zoro akiendelea kutoa burudani kupitia B Band.
Msanii Barnaba akigawa zawadi ya pipi kwa watoto.
Watoto wanaendelea kucheza.
Mchezo wa kukimbiza kuku ukiendelea
Mchezo wa kubeba wenza ukiendelea...kila mmoja kabeba mke wake.
Wanafamilia wanaangalia michezo iliyokuwa inaendelea.
Mpira wa kikapu ukiendelea.


Wanafamilia wa Acacia wakiangalia mpira wa kikapu.
Wafanyakazi wa Acacia wakiwa eneo la tukio.
Wanafamilia wakipata huduma ya chakula.
Meneja wa NHIF mkoa wa Shinyanga Imani Emmanuel akitoa maelezo kuhusu bima za afya.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Janeth Reuben akiangalia mafuta ya kupaka yaliyotengenezwa kwa asali na kikundi cha wajasiriamali wa Mwendakulima waliowezeshwa na Acacia.



Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 

Wafanyakazi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Acacia kupitia migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na familia zao wamesherehekea siku ya Familia ‘Buzwagi &Bulyanhulu Family Day 2018’ kuaga mwaka 2018 na kukaribisha mwaka 2019.

Sherehe hiyo iliyofanyika Jumamosi Disemba 22,2018 katika Viwanja vya Mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama,pia imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ambapo mgeni rasmi alikuwa Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta.

Akifungua sherehe hizo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Bi. Janeth Reuben aliwashukuru wafanyakazi wote wa migodi hiyo kwa juhudi walizofanya katika mwaka 2018 kuhakikisha kampuni ya Acacia inaendesha biashara kwa ufanisi.

“Sote tunatambua jinsi Acacia tulivyopitia katika mazingira magumu sana mwaka huu na uliopita,lakini tumepata faraja kubwa sana kutoka kwenu kwa sababu mmeweza kufikia na kuvuka malengo tuliyojiwekea ikiwemo malengo ya uzalishaji na ya kiusalama,naomba tuendelee na kasi hiyo hiyo mwaka 2019”,alieleza.

“Nawashukuru sana pia wanafamilia waliofika hapa na wale ambao hawakuweza kufika,sisi wafanyakazi hasa wa migodi tunahitaji na tunapata ushirikiano na upendo mkubwa sana kutoka kwa wenzi wetu na watoto kwa sababu mazingira ya kazi yanatulazimu wengi wetu kuwa mbali na familia”,aliongeza Bi. Reuben.

Alisema ushirikiano na upendo wa wanafamilia wakiwemo wenzi na watoto unawatia moyo hivyo kuwawezesha wafanyakazi kufanya kazi kwa amani katika kulijenga taifa la Tanzania.

Kwa upande wake,Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu , Bw. Benedict Busunzu aliwashukuru viongozi mbalimbali wa serikali kwa ushauri na ushirikiano wanaotoa katika kuhakikisha Acacia inaendelea kufanya kazi kwenye mazingira stahiki na kusababisha maendeleo endelevu kwa jamii.

“Licha ya kampuni yetu kupitia katika changamoto za kibiashara,lakini tunajitahidi kadri inavyowezekana kuhakikisha tunaendelea na shughuli za uzalishaji na kwa wakati huo huo kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi wetu”,alisema Busunzu.

Akielezea kuhusu Siku ya Familia yenye kauli mbiu ya ‘Tufanikiwe pamoja’, Busunzu alisema kwa mara ya kwanza mwaka huu Acacia inaadhimisha siku ya familia kwa kukutanisha pamoja migodi miwili ya Buzwagi na Bulyanhulu ili kuimarisha zaidi mahusiano ya kijamii na kiutendaji kazi.

“Hii ni siku maalumu kwa ajili ya kufurahi pamoja na familia zetu na wadau wetu,kupitia siku hii,ninayo matumaini kwamba ushirikiano na mahusiano yetu na familia na wadau wetu yataimarika ili kutengeneza kesho iliyo bora zaidi kwa sisi sote”,aliongeza Busunzu.

Maadhimisho ya Siku ya Familia Buzwagi na Bulyanhulu yameongozwa na shughuli mbalimbali ikiwemo wanafamilia kutembelea mgodi wa Buzwagi,maonesho ya kazi za wadau wa Acacia,michezo na burudani kadha wa kadha zikiongozwa na Wasanii Banana Zoro na Barnaba.

Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikitua kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikimwagiwa maji ikiwa ni ishara ya karibu na heshima (Water salute) kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Leonard Chamuriho wakisaini mkataba wa makabidhiano ya Ndege mpya ya Airbus 220-300 itakayokabidhiwa katika shirika la ndege la Tanzania mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakishuhudia kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Rubani mstaafu Kapteni Mapunda kutokana na uzalendo wake kwa Taifa kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rubani mstaafu Kapteni Mapunda na mkewe kutokana na uzalendo wake kwa Taifa na kumpa zawadia ya kiasi cha Tsh Milioni kumi kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Balozi wa Canada Pamela O’donnel pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya ndege na Mkewe Janeth Magufuli ,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na simu alipokuwa anakagua ndege mpya ya Airbus 220-300 ndani ya ndege hiyo na mmoja wa Marubani Kapteni Pandya aliyekuja na ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege mpya aina ya Airbus 220-300 na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi na Wafanyakazi wa Shirika La ndege la Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. PICHA NA IKULU KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

$
0
0
  Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikitua kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikimwagiwa maji ikiwa ni ishara ya karibu na heshima (Water salute) kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
  Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Leonard Chamuriho wakisaini mkataba wa makabidhiano ya Ndege mpya ya Airbus 220-300 itakayokabidhiwa katika shirika la ndege la Tanzania mbele ya   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakishuhudia kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla  iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Rubani mstaafu Kapteni Mapunda kutokana na uzalendo wake kwa Taifa kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na  Rubani mstaafu Kapteni Mapunda na mkewe kutokana na uzalendo wake kwa Taifa  na kumpa zawadia ya kiasi cha Tsh Milioni kumi kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Balozi wa Canada Pamela O’donnel pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya ndege na Mkewe Janeth Magufuli ,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na simu alipokuwa anakagua ndege mpya ya Airbus 220-300 ndani ya ndege hiyo na mmoja wa Marubani Kapteni Pandya aliyekuja na ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege mpya aina ya Airbus 220-300 na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi na Wafanyakazi wa Shirika La ndege la Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. PICHA NA IKULU

SIMBA SC YAFUZU HATUA YA MAKUNDI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, TAZAMA MABAO YOTE 3-1 DHIDI YA NKANA

Previous: Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikitua kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikimwagiwa maji ikiwa ni ishara ya karibu na heshima (Water salute) kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Leonard Chamuriho wakisaini mkataba wa makabidhiano ya Ndege mpya ya Airbus 220-300 itakayokabidhiwa katika shirika la ndege la Tanzania mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakishuhudia kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Rubani mstaafu Kapteni Mapunda kutokana na uzalendo wake kwa Taifa kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rubani mstaafu Kapteni Mapunda na mkewe kutokana na uzalendo wake kwa Taifa na kumpa zawadia ya kiasi cha Tsh Milioni kumi kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Balozi wa Canada Pamela O’donnel pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya ndege na Mkewe Janeth Magufuli ,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na simu alipokuwa anakagua ndege mpya ya Airbus 220-300 ndani ya ndege hiyo na mmoja wa Marubani Kapteni Pandya aliyekuja na ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege mpya aina ya Airbus 220-300 na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi na Wafanyakazi wa Shirika La ndege la Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. PICHA NA IKULU KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: FURAHA YA RAIS MAGUFULI WAKATI WA KUPOKEA NDEGE MPYA AINA YA AIRBUS A220-300

WAZIRI JAFO AKABIDHI KOMPYUTA 25 KWA SHULE ZA SEKONDARI 14 KATIKA WILAYA YA KISARAWE

$
0
0

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) kati kati akimkabidhi kompyuta mmoja wa walimu wa shule za sekondari,kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo katika halfa iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kati kati akiwa ameshika moja ya kompyuta ambazo zmezitoa kwa niaba ya serikali, kushoto kwake ni Naibu waziri wa uchukuzi na Mawasialiano Injinia Atashasta Nditiye, na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kisarawe Mussa Gama wa kwanza kulia akishuhudia ugawaji wa kompyuta hizo ambazo zimetolewa na serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote ambapo shule 14 za sekondari zimeweza kunufaika na msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza jambo na baadhi ya walimu wa shule za sekondari hawapo pichani katika halfa hiyoya ugawaji wa kompyuta hizo
Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na baadhi ya walimu wa shule za sekondari katika halfa hiyo ya kukabidhi kompyuta 25 kwa shule 14 zilizopo katika halmashauri ya Kisarawe..(PICHA NA VICTOR MASANGU



VICTOR MASANGU, KISARAWE


WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri nchini pamoja na maafisa elimu kuachana kabisa na vitendo vya kuwanyima fursa walimu ambao wanahitaji kujifunza somo la tehema na badala yake wahakikishe wanatoa vibali bila ya kuwa na ukilitimba wowote kwa lengo la kukuza teknolojia na mawasiliano.

Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa halfa ya kukabidhi kompyuta 25 ambazo zimetolewa na serikali kupitia mfuko wa mawasilino kwa wote ambapo zitazinufaisha shule za sekondari 14 zilizopo katika halmashauri ya Kisarawe.

Jafo alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawajengea uwezo walimu ambapo hadi sasa tayari walimu wapatao 570 wameshapatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya somo la tehema ili kuendana na kasi na mabadiliko ya kiteknolojia.

“Kitu kikubwa sisi kama serikali kwa sasa tumejipanga kuhakikisha kwamba somo hili la Tehama kwa walimu linapewa kipaumbele zaidi, lakini sipendi kuona walimu wananyimwa vibali kwa ajili ya kwenda kuongeza ujuzi katika somo hilo hivyo kuanzia sasa ofisi yangu italisimamia hili na kwamba wakurugenzi wote na maafisa elimu msiwanyime vibali kabisa wapeni acheni roho mbaya,”alisema Jafo.

Naye Naibu waziri wa uchukuzi na mawasiliano Injinia Atashasta Nditiye amesema kwamba kwa sasa serikali imeshaanza mchakato kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vituo 20 vya Tehama kwa upande wa Tanzania bara ambapo kwa upande wa Tanzania visiwani tayari wameshajenga vituo vya Tehama vipatavyo 10 ambavyo ni mahususi kwa wanafunzi, wanafanyakazi, pamoja na walimu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema kwamba katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu wanatarajia kuanzisha kituo maalumu kwa ajili ya kufundishia somo la tehema kwa walimu pamoja na wanafunzi ili kuweza kupanua zaidi katika Nyanja ya teknolijia.

“Kwa kweli tunaishukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa kutupatia vifaa hivi vya kompyuta 25 kwa ajili ya shule zetu za sekondari 14, bah ii itaweza kusaidia kwa kisi kikubwa kuongeza uwezo kwa walimu katika suala zima la teknolojia pamoja na mawasiliano,”alisema Jokate.

Komputa hizo 25 ambazo zimetolewa kwa shule 14 za Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani zimenunulia kwa kiasi ya shilingi milioni 43 zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa walimu pamoja na wanafunzi katika kusaidia suala zima la teknolojia pamoja na mawasiliano
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images