Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Benki ya FINCA Microfinance yatoa zaidi ya milioni 10 kwa wamiliki wa biashara ndogo ndogo kupitia shindano la ‘Kuza Ofisi na FINCA’

$
0
0
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (katikati) akikabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 jana kwa mshindi wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA, Emmanuel Bugingo mkazi wa Mbagala Kuu. Shindano hilo lililoandaliwa na Benki ya Finca Microfinance linashindaniwa kwa washiriki kubuni mradi wenye kuweza kumletea kipato kwa kupitiwa na majaji waliompata mshindi. Pichani Kushoto ni Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Finca Microfinance, Alfred Vanderlin. 
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Walemevu, Mhe. Anthony Mavunde akitangaza mshindi wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA lililofikia kilele jana usiku kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam, Shindano lililoendeshwa kwa miezi mitatu kwa washiriki kubuni mradi chanya wenye kumuwezesha kupata kipato. Wengine pichani kushoto ni Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Finca Microfinance, Alfred Vanderlin na washiriki walioingia nne bora. 
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (katikati) akikabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 5 jana kwa mshindi wa pili wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA, Sadiki Hassani mkazi wa Manzese, Kushoto ni Alfred Vanderlin, Afisa Mkuu Uendesheji wa Finca. 
Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Finca Microfinance, Alfred Vanderlin akipeana mikono na mshindi wa tatu wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA, Reuben Waya, Katikati ni Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde. 
Washindi wakiwa na zawadi zao za mfano wa Hundi walizojinyakulia mara baada ya kutangazwa kwa matokeo. 
Meza ya Majaji ikiongozwa na Nicholous John mkuu wa kitengo cha Masoko FINCA (kulia) akifuatiwa na Catherine Ngobi, Jeff Special na Gloria Gabriel. 
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya FINCA Microfinance, Monica Joseph. 
Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Finca Microfinance Tanzania, Alfred Vanderlin akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya kumpata mshindi wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA jana kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam. 



Shindano hilo lililodumu kwa kipindi cha miezi mitatu lilikuwa na lengo la kutoa elimu ya stadi za biashara na fedha kwa wafanyabiashara wadogo. 

Benki ya FINCA Microfinance imeendelea kuwa benki ambayo inaunga mkono ushirikishwaji wa kifedha katika kipindi cha miaka 20 na zaidi cha uwepo wake nchini Tanzania. Bugingo Emmanuel ameibuka mshindi wa shindano la biashara la Kuza Ofisi na FINCA na kuondoka na kiasi cha TZS milioni 10 baada ya shindano la muda wa miezi mitatu na lililokuwa na zaidi ya washiriki elfu moja walioshiriki, ni washriki wanne ndio waliowasilisha mipango yao ya biashara kwa jopo la majaji na kupigiwa kura na watazamaji. 

Akiongea katika onyesho la mwisho la shindano la Kuza Ofisi na FINCA jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde aliipongeza FINCA kwa kutekeleza jitihada za kibunifu kwa ajili ya kusaidia kukuza wajasiriamali wadogo kwa wakati. Alisema kwamba serikali inaendelea kuandaa mazingira mazuri kwaajili ya maendeleo ya biashara nchini.

“Ninatoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na mifuko ya uwezeshaji ya serikali ambayo imetengwa kwaajili ya maendeleo ya biashara. Vile vile aliipongeza benki ya FINCA Microfinance kwa jitihada zake zenye lengo la kusaidia kukuza wafanyabiashara wadogo SMEs nchini ‘Ninaipongeza FINCA kwa kubuni mipango hii ya kibunifu ambayo sio tu kwamba inasaidia kukuza biashara ndogo ndogo lakini pia inawapatia vijana ujuzi na stadi za biashara alisema Mavunde. 

Afisa Uendeshaji Mkuu wa Benki ya FINCA bwana Alfred Vanderlin alisema ‘Benki ya FINCA inaboresha na kurahisisha mchakato wake wa kutoa mikopo na utoaji wa huduma kwa wateja kwaajili ya kupunguza gharama na kuwawezesha wateja kufanya biashara kwa urahisi’. Aliongeza kuwa, FINCA inaendeleza utamaduni wa ubunifu na uvumbuzi na inaamini kwamba mafanikio ya maisha yajayo katika kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha utapatikana kupitia uboreshaji wa teknolojia na utoaji wa huduma bora zenye kiwango cha juu kwa wateja’. 

Shindano hili lililodumu kwa muda wa miezi mitatu lilikuwa na lengo la kuwezesha wafanybiashara wadogo kwa kuwapatia stadi za biashara, elimu na kuwapatia mtaji wa kiasi cha thamani ya TZS milioni 10 kwa wazo bora zaidi la biashara litakalowasilishwa. Mshindi wa pili wa shindano hilo bwana Sadiki Hassan aliondika na kiasi cha shilingi milioni 5 wakati mshindi wa tatu wa shindano hilo bwana Reuben Waya aliondoka na shilingi milioni 3. 

Shindano la kuza ofisi na FINCA awali lilitekelezwa katika wilaya nne za mkoa wa Dar es salaam ambazo zinajumuisha Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi ziliambatanishwa katika matawi ya benki ya FINCA ambayo yamewekwa kimkakati katika maeneo ya Tegeta, Ilala, Victoria na katika barabara ya Pugu kuelekea uwanja wa ndege.

TBL YANG'ARA TENA TUZO YA MWAJIRI BORA 2018

$
0
0
Meneja ukuzaji wa Vipaji wa TBL ,Lilian Makau ( Kushoto) akipokea tuzo kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Waziri wa Sera , Bunge ,Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu, Mh. Jenesta Mhagama baada ya kampuni kuibuka kidedea kwa kushika nafasi ya pili katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mwishoni mwa wiki, Kulia ni Naibu waziri wa wizara hiyo , Anthony Mavunde.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group, wakifurahia ushindi wa mshindi wa pili wa tuzo za mwajiri bora 2018.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kutunukiwa tuzo. --- 

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imepata tuzo kutoka Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) ya utekelezaji vigezo vya Raslimali Watu kwa viwango vya juu, katika hafla ya kutunukia Waajiri bora nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Sera , Bunge ,Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Mh.Jenesta Mhagama. Mbali na tuzo hiyo,TBL ambayo hivi karibuni ilishinda tuzo ya kimataifa inayotolewa na taasisi ya Top Employers Institute ya nchini Uholanzi, ilipata tuzo ya ATE katika kipengele cha kutoa mafunzo na kuendeleza wafanyakazi wake. Akizungumzia ushindi huo,

Mkurugenzi Raslimali Watu wa TBL,David Magese alisema “Ushindi wa tuzo hii umechangiwa na timu nzuri ya wafanyakazi wa kampuni ,Wafanyakazi wote wa TBL tunashirikiana kufanya kazi kwa bidii na malengo ya kuifanya kampuni kuwa sehemu ambayo inavutia watu kufanya nayo kazi,na hii ni ndoto yetu kubwa katika maeneo yote barani Afrika ambapo kampuni inafanyia biashara zake”.Alisema.

 Magese aliongeza kusema kuwa kampuni ya TBL imewekeza kwa wafanyakazi wake na inazo programu malimbali za mafunzo ya kuendeleza taaluma na ujuzi wao ,ukuzaji vipaji vya wafanyakazi na mpango wa kuwaandaa viongozi wa kampuni wa siku za mbele unaojulikana kama Global Management Trainee (GMT) unaosimamiwa na kampuni yake mama ya ABInBev. 

Alisema tuzo mbalimbali ambazo kampuni ya TBL imekuwa ikitunukiwa na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi zinadhihirisha dhamira ya kampuni ya kufanikisha kuchangia kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini kupitia uwekezaji wake sambamba na kufanikisha mkakati wa Serikali wa Tanzania ya viwanda.

 Ikiwa kampuni kubwa ya kutengeneza bia nchini,TBL imekuwa mstari wambele kuhakikisha inazalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika kimatifa sambamba na kuhakikisha inatumia malighafi za ndani,mpango ambao pia unawanufaisha wakulima na wafanyabiashara wa kitanzania wanaoiuzia kampuni malighafi.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 17,2018

NAIBU WAZIRI KUFUATILIA TATIZO LA UCHELEWESHAJI WA MIRADI ILIYO CHINI YA TBA

$
0
0
RS TABORA

MKANDARASI wa Ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Mji Nzega wenye thamani ya bilioni 4.8 ametakiwa kuhakikisha mradi huo unakamilika katika kipindi ambacho kimekubalika katika mkataba.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali (OR TAMISEMI) Mwita Waitara wakati wa ziara yake wilayani Nzega.

Alisema Wakandarasi wanaopatiwa fursa ya kujenga miradi ya Serikali ikiwemo ile ya Halmashauri ni vema wakajitahidi kuhakikisha wanaitekeleza kwa kiwango cha hali ya juu ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Akijibu hoja za Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) kuchelewesha miradi mingi mkoani Tabora ikiwemo ukarabati wa Shule Kongwe ya Milambo na huo wa ujenzi wa Ofisi hizo alisema atajitahidi kulifikisha katika Wizara inayoisimamia Wakala hiyo ili watekeleze miradi yao kwa wakati.

Alisema TBA kama sehemu ya Serikali ni lazima wabadilike na kuharakisha utekelezaji wa miradi wanayopewa kusimamia ili kutosababishia kuongezeka kwa gharama kutokana na mradi kuchelewa kuanza. Awali Mahandisi wa Halmashauri ya Mji Nzega Mwita Said alisema ujenzi wa Ofisi hizo ulioanza Mei mwaka huu unatarajia kukamilika Novemba mwakani .

Alisema hadi hivi wameshapokea bilioni 2 na wamemlipa Mkandarasi ambaye ni Mzinga Holding milioni 700 na Msimamizi ambaye ni TBA milioni 200. Said alisema mradi huo uko katika hatua ya Msingi ambao umekumbana na matatizo ya kuwepo kwa mvua, ardhi kuwa na mwamba na upungufu wa vibarua unasababisha kazi kwenda polepole.

WAZIRI WA NISHATI AAGIZA BODI TANESCO ICHUKUE HATUA SUALA LA KUKATIKA UMEME

$
0
0

Na Veronica Simba - Dodoma

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuchukua hatua za makusudi ikiwemo kuwavua nyadhifa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uzalishaji, Mhandisi Abdallah Ikwasa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji, Mhandisi Kahitwa Bashaija; kutokana na suala la kukatika umeme sehemu kubwa ya nchi mara kadhaa sasa.

Alitoa maagizo hayo Jumamosi Desemba 15, mwaka huu alipokutana kwa dharura na wajumbe wa Bodi hiyo Makao Makuu ya Wizara jijiji Dodoma.

Akizungumzia sababu za kutaka wakurugenzi hao wawajibishwe, Waziri Kalemani alisema ni kutokana na tatizo la kukosekana kwa umeme sehemu kubwa ya nchi mara nne na kwa kipindi cha muda mrefu unaofikia nusu saa, kwa sababu ambazo zimekuwa zikielezwa kuwa ni kutoka kwa Gridi ya Taifa, wakati nchi ina ziada ya umeme inayofikia wastani wa megawati 250.

Akifafanua zaidi, alisema kutokea kwa tatizo hilo kunamaanisha kuna uzembe katika usimamizi au kutokufuatilia maelekezo ya Serikali, au kunaweza kuwepo na hujuma kwa baadhi ya watumishi wasiokuwa wazalendo. “Nchi inapokuwa gizani hata kwa sekunde moja, maana yake hakuna usalama. Aidha, hakuna sababu ya wananchi kukosa umeme katika mazingira ambapo kuna umeme wa ziada.”

Katika maagizo yake kwa Bodi, mbali na kutaka Wakurugenzi husika wawajibishwe, aliagiza pia wachunguzwe ikiwa ni pamoja na waliohusika kwa namna moja ama nyingine. Aidha, aliitaka Bodi kuunda Timu mahsusi kuanzia siku hiyo (Desemba 15), ili ichunguze na kufuatilia suala hilo, ikihusisha tasnia na taasisi mbalimbali, zaidi ya TANESCO.

“Ndani ya siku saba nipate matokeo ya nini chanzo chat atizo hilo ili lisijirudie kabisa,” alisisitiza. Waziri pia aliitaka Bodi kuhakikisha maeneo yote ya mijini ambayo hayana umeme kwas asa; yakisubiri kuunganishwa na huduma hiyo kupitia shirika hilo, yaanze kuunganishwa kuanzia siku hiyo ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Alisema yako maeneo ya mijini ambayo yanahitaji kuunganishiwa umeme na yamekaa kwa muda mrefu huku yakiwa ndani ya Mpango wa shirika na tayari pesa ilikwishatolewa kwa kila Mkoa. Vilevile, Waziri Kalemani aliagiza wateja wote nchi nzima ambao wamelipia bili zao, waunganishiwe umeme ifikapo Desemba 31 mwezi huu.

Katika hatua nyingine, Waziri aliitaka Bodi kuchunguza mambo mengine pia kadri itakavyoona inafaa ili kuhakikisha ustahimilivu wa umeme nchini unaendelea kuwepo. “Tuhakikishe maeneo yote nchini hayakatiki umeme pasipo sababu ya msingi.” Pia, alitaka pindi matengenezo yanapofanyika wananchi wapewe taarifa na wajulishwe muda yatapokamilika.

Sambamba na maagizo hayo, alimtaka pia Mwenyekiti wa Bodi kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya watumishi wengine wa Shirika hilo watakaoonesha dalili za kuhujumu miundombinu husika. Matukio hayo ya kukatika umeme sehemu kubwa ya nchi hivi karibuni yametokea Novemba 28, Novemba 30, Desemba 4 na Desemba 14 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hamisi Mwinyimvua na baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya Wizara pia walishiriki mkutano huo wa Waziri na Bodi ya TANESCO.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) (hawapo pichani) kuhusu hatua za kuchukua kutokana na suala la kukatika umeme sehemu kubwa ya nchi mara kadhaa. Waziri alikutana na Bodi hiyo Desemba 15, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhusu hatua za kuchukua kutokana na suala la kukatika umeme sehemu kubwa ya nchi mara kadhaa. Waziri alikutana na Bodi hiyo Desemba 15, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma. Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) alipokutana nao na kuwapa maagizo kuhusu hatua za kuchukua kutokana na suala la kukatika umeme sehemu kubwa ya nchi mara kadhaa. Waziri alikutana na Bodi hiyo Desemba 15, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.
 

Idara ya Uhamiaji Tanzania inaadhimisha Siku ya Wahamaji Kimataifa.

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Siku hii ya Kimataifa ya Wahamaji huadhimishwa Duniani kote tarehe 18/12 kila mwaka ikiwa ni kutambua mchango wa Wahamaji katika kukuza uchumi wa nchi za ugeni (horst country) na wanakotoka (origin) kadhalikaa kuheshimu uhuru na haki zao za kibinadamu.

Katika maadhimisho ya Mwaka huu yanapambwa na kauli mbiu isemayo Uhamaji unaozingatia Utu.

Akizungumza na Michuzi Blog Msemaji wa Idara hiyo Ally Mtanda amesema kuwa katika kuadhimisha siku hii, Idara ya Uhamiaji inafanya Maonesho maalum katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa kutoa pasipoti za kielektroniki kwa Watanzania.

Aidha, elimu kwa Umma kuhusu Uraia, Viza na Vibali vya Ukaaazi itatolewa. Pia Wananchi watapata fursa ya kujua mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda Moshi (Tanzania Regional Immigration Training Academy-TRITA)

"Ninawasihi Watanzania, Taasisi, Makampuni na Mashirika mbalimbali kutumia fursa ya maonesho haya kupata huduma zetu kwa kufika wenyewe na kuepeukana na vishoka" Aliongeza Mtanda.

Maadhimisho hayo huanza Desemba 16 na kufikia kilele chake Desemba 17.
 Picha ya pamoja wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamaji Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mrakibu Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Grace Rutachokozibwa akitoa huduma katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamaji Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Shule za Jumuia ya Wazazi (CCM) kufundisha ufugaji nyuki

$
0
0
Na Joseph Zablon

Jumuia ya Wazazi (CCM), imeanza kutekeleza mpango wa kutoa elimu ya ufugaji nyuki kibiashara kwa wanafunzi wa shule zote zinazomilikiwa na jumuia hiyo na kwa wananchi wa wilaya zote nchini kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi na pia kutoa ajira kwa vijana mara baada ya kuhitimu masomo yao ya sekondari

Akizungumza na waandishi wa habari kufuatia ziara ya hivi karibuni ya kukagua utekelezaji wa mpango huo, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dk Edmund Mndolwa alisema ufugaji nyuki licha ya kuwezesha upatikanaji wa asali lakini pia kuna mazao mengi yanayotokana na wadudu hao.

“Tutalenga kwanza kwenye asali ingawa kuna mazao mengi na yenye thamani kubwa kuliko asali” alisema na kuongeza kuwa ameziagiza shule zote 55 za sekondari za wazazi nchi nzima kuhakikisha hadi Aprili 2019 mazao ya kwanza au kabla ya hapo” alisema mwenyekiti huyo.

Alisema anawapongeza viongozi na watendaji wa shule hizo kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwani utakuwa na mchango mkubwa katika kuitoa ajira kla vijana,jamii, pato la ndani la Taifa, upatikanaji wa fedha za kigeni, huanzishwaji wa viwanda vidogo na kupunguza umaskini kwa jamii.

Alisema mpango huo ambao ulibuniwa na yeye mwenyewe, ukakubaliwa na kamati ndogo ya baraza, kisha ukapitishwa na Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi Taifa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kuziendesha shule hizo na kuziimarisha kiuchumi tofauti na ilivyokuwa awali.

“Tunatekeleza mpango mkakati tuliojiwekea wa kuhakikisha pamoja na mambo mengine shule zinakuwa na ongezeko la wanafunzi katika muhula mpya wa masomo 2019 na pia kupata fedha za ziada kwa ajili ya kulipa madeni ya shule hizo za Wazazi” alisema Dk Mndolwa.

Alisema katika ziara yake ya ukagua uhai wa jumuia katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha hivi karibuni, alisema ameridhishwa na mipango ya utekelezaji wa mradi huo na alibainisha kuwa tayari kuna walimu wakufunzi ambao wamepata mafunzo ya ufugaji nyuki.

Dk Mndolwa alisema walimu hao ambao waliteuliwa walimu wakuu wa shule za jumuia hiyo, walipata mafunzo yao mkoani Singida na wanatarajiwa kuwa chachu kwa wenzao na wanafunzi kwa ujumla wake na mafunzo hayo ya ufugaji nyuki yatakuwa yakitolewa katika shule hizo kwa wakati usioingiliana na wa masomo ya kawaida.

Pia Dk Mndolwa alibainisha kuwepo kwa changamoto za upatikanaji wa mbao kwa ajili ya utengenezaji wa mizinga hususan wilaya za mjini na kuwataka viongozi na watendaji kuichukulia kama fursa kwa kutafuta ufumbuzi kwa kuwashirikisha viongozi wa serikali. 
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi (CCM) Taifa, Dk Edmund Mndolwa (kulia), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza Kuu la Jumuia hiyo jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kuanza kutekeleza kwa mradi wa mafunzo ya ufugaji nyuki mashuleni kwa shule zinazomilikiwa na jumuia hiyo. Picha na Joseph Zablon.

WAZIRI MPINA ATANGAZA NEEMA KWA WAFUGAJI KWA KUGAWA EKARI 972,500 ZA ARDHI

$
0
0

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina akimwangalia farasi anayetumika kwenye doria katika ranchi ya Kalambo Mkoani Rukwa
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Luhaga Joelson Mpina akiangalia nyama inayochakatwa katika kiwanda cha SAAFI mkoani Rukwa kushoto kwake ni mmiliki wa kiwanda hichi Dkt Chrisant Mzindakaya .
Kundi la Ng'ombe bora katika ranchi ya Kalambo mkoani Rukwa



NA JOHN MAPEPELE, RUKWA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina ametangaza neema kwa wafugaji kwa kugawa ekari 972, 500 za ardhi ajili ya wafugaji wanaotangatanga kutafuta malisho ya mifugo yao ili kupata ufumbuzi wa kudumu ambao utamaliza kabisa migogoro baina ya wafugaji na wakulima iliyodumu kwa miaka mingi na kusababisha uvunjifu wa amani.

Akizindua zoezi la ugawaji wa ardhi hizo kwa wafugaji nchini katika Ranchi ya Kalambo wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Waziri Mpina amesema uamuzi huo wa Serikali umekuja kufuata wafugaji wengi nchini kuhangaika kila mahali kutafuta malisho na kusababisha migogoro mingi baina ya wafugaji, wakulima na watumiaji wengine wa ardhi.

“Pia wafugaji wengi walipata harasa kubwa kwa mifugo yao kutaifishwa kutozwa faini kubwa na hata mingine mingi kufa kutokana na kukamatwa kisha kushikiliwa kwa muda mrefu bila huduma muhimu ikiwemo maji, malisho na matibabu kwenye hifadhi mbalimbali za taifa nchini.” Alisisitiza Mpina

Alisema hadi sasa ekari 25,000 zenye uwezo wa kuhifadhi mifugo 6,000 katika Ranchi ya Kalambo mkoani Rukwa wafugaji zimemegawiwa ambapo na jumla ya ng’ombe 3,000 wameshaingia kwenye ranchi hiyo wakati Serikali na wafugaji wenyewe wakiendelea kutafuta suluhisho la kudumu la kupata malisho.

Amewataka wafugaji wote wanaohangaika kutafuta malisho kutumia fursa hiyo iliyotangazwa na Serikali ya uwepo wa maeneo kwa ajili ya kulishia mifugo ili wawe karibu pia huduma za tiba na chanjo pindi mifugo yao inapopata maradhi.

Akiwa katika mkutano wa pamoja baina ya Rachi ya Kalambo na wawekezaji Waziri Mpina alipongeza Timu maalum aliyoiunda ya kutatua migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi kwa kufanikisha zoezi la upimaji na ugawaji wa ardhi hiyo kwa wafugaji pamoja na kutatua migogoro yote iliyokuwepo baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi katika mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.

Aidha ailiiagiza Timu hiyo kuhakikisha kwamba inazunguka nchi nzima kwenye migogoro na kuitatua ili kuboresha mifugo iweze kuchangia katika viwanda hapa nchini.

Pia alimwagiza Katibu Mkuu Mifugo kuhakikisha ukaratabi wa kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya wanyama cha Kanda ya Kusini Magharibi kinakamilika ifikapo Februari mwakani ili kutokana na mikoa ya Katavi, Rukwa kutokuwa na kituo hicho licha ya kuwepo mifugo mingi.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Halfan Haule alisema kutokuwepo kwa maeneo ya malisho na maji ya kutosha kwa ajili ya mifugo kumekuwepo na migogoro kati ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi na kumshukuru Waziri Mpina kwa uamuzi wa kugawa vitalu kwa wafugaji.

Alisema Mkoa wa Rukwa umekuwa ukikabiliwa na magonjwa ya mifugo ikiwemo homa ya nguruwe(ASF), Homa ya Mapafu ya Ng’ombe(CBPP), Homa ya mapafu ya mbuzi(CCPP), Ugonjwa wa miguu na midomo(FMD), Ugonjwa wa mapele ngozi(LSD), Ugonjwa wa kichaa cha mbwa na ugonjwa wa mdondo(ND).

Katibu wa Umoja wa Wafugaji Ranchi ya Kalambo, Benuel Benzeth aliishukuru Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kugawa maeneo hayo ya Serikali kwa wafugaji katika kipindi ambacho wanaendelea kutafuta suluhisho la kudumu la changamoto ya malisho.

Alisema mifugo yao mingi imekufa na mingine kudhoofika kutokana na kukamatwa na kushikiliwa kwenye hifadhi bila matunzo na wakati wote Serikali haijawahi kuchukua hatua za kuwasaidia wafugaji na kumshukuru Waziri Mpina kwa uamuzi huo ambao umewezesha mifugo mingi kupona na kuendelea na uzalishaji.

Awali akizungumza mara baada ya kutembelea Kiwanda cha Nyama cha SAAFI kilichopo mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, Waziri Mpina amesema Serikali inafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza kufanya kazi haraka ili kusaidia upatikanaji wa mifugo takribani milioni 6 iliyoko katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Songwe na Mbeya.

Hivyo changamoto zote zinazokikabili kiwanda hicho zitatatuliwa haraka ikiwemo ukosefu wa mtaji pamoja na uongozi wa kuendesha kiwanda hicho jambo linalosababisha kiwanda hicho kusimama kwa muda mrefu licha ya kuwa na mitambo bora na ya kisasa ya uchinjaji na usindikaji wa nyama katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Waziri Mpina amesema ni jambo la fedheha kuona kiwanda hicho chenye miundombinu yote kuendelea kubaki katika hali hiyo huku wafugaji wakiendelea kuhaha kutafuta soko la mifugo hali inayosababisha asilimia 80 ya mifugo hiyo kutoroshwa kwenda nchi za jirani na kwenda kuyanufaisha mataifa hayo.

Hali hiyo inaifanya Tanzania kugeuzwa kuwa malisho ya mifugo hiyo huku rasilimali hizo zikishindwa kunufaisha nchi kimapato jambo ambalo Serikali ya awamu ya tano haiwezi kukubali liendelee.

Waziri Mpina pia alimpongeza Mwekezaji wa kiwanda hicho, Dk. Chrisant Mzindakaya kwa ujasiri na uamuzi mkubwa wa kubuni wazo la kuanzisha kiwanda hicho kwa gharama ya sh bilioni 9 na kuwepo na eneo la malisho zaidi ya hekta 6,000 kwani watu wengi wanaweza kukopa fedha na kisha kushindwa kutekeleza mipango yao kwa mujibu wa mpango kazi alioombea mkopo.

Hivyo aliagiza taasisi zote za Serikali kuhakikisha changamoto zote zinakwisha ili kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza kazi mara moja na kwamba kama uvunaji wa rasilimali za mifugo hauko vizuri ni kipimo cha uwajibikaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyopewa dhamana ya kusimamia ukuaji wa sekta hiyo.

Kwa upande wake Mwekezaji wa kiwanda, Dk Chrisant Mzindakaya alisema licha ya kiwanda chake kufanya kazi lakini uzalishaji wake ni mdogo kutokana na changamoto ya mtaji na uendeshaji wa kiwanda na kumshukuru Waziri Mpina kwa kutembelea kiwanda na kutangaza msimamo wa Serikali katika kukinusuru kiwanda hicho.

Jumia yazindua Ripoti ya Utalii Afrika 2018/2019

$
0
0
Toleo hili la pili la Ripoti ya Utalii Afrika kutoka Jumia inaangazia masuala mbalimbali yaliyotokea barani kwa mwaka 2017/2018 katika sekta za huduma za utalii, usafiri, ukarimu na anga. 
 
Inatoa mwanga wa kutosha kwenye ukuaji wa kuridhisha wa sekta za utalii na usafiri Afrika iliyoonyesha kwa miaka ya 2017 na 2018 ambapo imeonyesha kuongezeka kwa wageni kutoka mataifa ya nje. Ripoti hii kutoka Jumia inaenda mbele zaidi kwa kuainisha mchango wa sekta hizi kwenye uchumi, changamoto zilizopo na mustakabali wake kwa siku zijazo, ukizingatia sekta ya utalii Afrika inazidi kukua.

“Soko la usafiri kwa njia ya mtandaoni barani Afrika bado linakua na bila shaka linaonyesha matarajio makubwa. Tunayo furaha kubwa kwa mara nyingine tena kuwaletea ripoti hii iliyosheheni masuala tofauti kwenye sekta za ukarimu na anga Afrika. Na hili limefanikiwa kwa ushirikiano wa karibu na washirika wetu wa karibu,” amesema Bw. Joe Falter, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Travel na Food.

Kusoma ripoti kamili bonyeza hapa

Kubadilika kwa hali ya Usafiri wa Ndani

Ingawa bara hupokea 5% ya wasafiri wote wa nje, sekta ya usafiri na utalii Afrika inazidi kuendelea kuonyesha ukuaji mwaka hadi mwaka. Mwaka 2017, bara lilipokea idadi ya juu ya watalii milioni 63 kutoka mataifa ya nje ukilinganisha na watalii milioni 58 mwaka 2016 (9% zaidi ukilinganisha na 2016). Kutokana na unafuu na urahisi wa kusafiri, utalii wa ndani unakua Afrika, takwimu zinaonyesha 60% walisafiri ndani ya mipaka yao ukilinganisha na 40% kwenda nje.

Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Utalii Duniani (UNWTO), Bw. Zurab Pololikashvili amefafanua kuhusu kubadilika kwa hali usafiri wa ndani Afrika, amesema, “kitendo cha watu kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine sio anasa tena kwa ajili ya watu wachache wenye kipato cha juu bali ni hitaji la muhimu hususani kwa watu wa kipato cha kati wanaoongezeka kwa kasi ambao ndio wanaotengeneza na kuunda kizazi kijacho cha wajasiriamali. 
 
Kukua kwa tabaka la watu wa tabaka la kati ni ishara nzuri ya kuwa na uchumi thabiti. Uwepo wa watalii wa ndani ambao wana pesa za kutumia na ikiwemo kusafiri zaidi, kumepelekea kuibuka kwa mashirika ya ndege yanayotoa huduma nafuu, kukuza huduma ya malazi katika majiji, na hivyo kustawisha uchumi wa pamoja, nakadhilika.”

Pasi ya kusafiria ya kielekiktroniki ya Umoja wa Afrika pamoja na kuundwa kwa utaratibu wa kutolewa viza pale unapowasili na kusafiri bila ya viza kwa raia wa Afrika ikiwa ni kuendana na dhana ya kuwa shughuli zisizo na mipaka za kusafiri kwa watu, bidhaa na huduma baina ya nchi kumebakia kuwa sababu kubwa inayochochea ukuaji wa usafiri wa ndani. 
 
Waafrika sasa hawahitaji viza kusafiri kwenda 25% ya nchi zingine za Kiafrika, wanaweza kupata viza pale wanapowasili katika 24% ya nchi zingine za Kiafrika, lakini bado 51% ya nchi zingine za Kiafrika zinawahitaji Waafrika kuwa na viza ili kuwaruhusu kutembelea nchi hizo.

Ripoti pia inaelezea kwa undani zaidi vyanzo mbalimbali vinavyotumiwa katika kuzifikia huduma za Jumia. Takwimu zinaonyesha chanzo kikuu ni simu, hii ni pengine ni kutokana na matokeo ya kuongezeka kwa matumizi ya simu za mkononi Afrika, ambapo ni 34% mwaka 2018. 61% ya wasafiri wanatumia simu za mkononi kufanya huduma za malazi au kukata tiketi ya ndege kwenye mtandao wa Jumia Travel. Bado idadi kubwa ya waafrika wanapendelea kufanya malipo moja kwa moja wafikapo hotelini ambapo ni 65% katika mwaka huu wa 2018, hata uaminifu kwa upande wa malipo kwa kutumia kadi za Credit & Debit yameongezeka mpaka 21% kutoka 15% mwaka 2017.

Sekta ya Usafiri wa Anga Afrika

Afrika inachangia idadi ya kiasi cha 2.2% ya wasafiri wa anga duniani ambapo kulikuwa na jumla ya wasafiri milioni 88.5 katika mwaka 2017, ongezeko la 6.6% kutoka mwaka 2016. Inatarajiwa kukua kwa 4.9% kila mwaka kwa miaka 20 ijayo, na kutengeneza fursa kubwa kwa mashirika ya ndege kukua barani.

Akielezea namna ya kuyafanya mashirika ya ndege ya Kiafrika kuwa ya kishindani katika soko la dunia, Mjumbe Maalum wa Afrika juu ya mambo ya Aeropolitiki kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (IATA), Bw. Rapahel Kuuchi amesema kuwa, “mustakabali wa ukuaji wa mashirika ya ndege ya Kiafrika unategemea kuondolewa kwa vikwazo ili kuwa na muunganiko wenye ufanisi, kushusha gharama za uendeshaji na kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya mashirika. Kukiwa na uhakika wa usalama, ulinzi, mazingira yenye ushindani, urahisi wa upatikanaji wa soko na utolewaji wa viza, idadi ya abiria barani Afrika itazidi milioni 320 kufikia mwaka 2037,” alihitimisha.

BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAFANYA MKUTANO WAO MKOANI MBEYA

$
0
0
ZAIDI ya wakulima 1,032 wameanza kutumia Teknolojia ya Kilimo Hifadhi inayomuwezesha mkulima kukabilaina na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kupata mavuno mengi zaidi tofauti na Kilimo cha mazoea cha kutegemea Mvua Pekee.Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ubia wa kilimo Tanzania mwaka 2018 ulio chini ya baraza la kilimo Tanzania imesema wakulima hao ni kutoka Wilaya za Same, Moshi Vijini, Babati, Monduli na Kiteto ambapo wakulima zaidi ya 2500 walipata mafunzo kuhusu kilimo hifadhi.

Hayo yalielezwa na Mratibu Taifa wa Ubia wa Kilimo Tanzania Mark Magila wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe waliohudhulia Warsha ya wadau TAP II iliyofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya ambapo aliwaeleza kuwa teknlojia hiyo inamsaidia mkulima kupata mavuno mengi huku akitumia sehemu ndogo ya ardhi. 

“Mpaka sasa TAP II tumekwisha fanikiwa kutoa mafunzo ya stadi za kilimo biashara kwa wakulima 700 kutoka kwa wilaya 7 za Meru, Kiteto, Babati, Kilombero, Morogoro Vijijini, Namtumbo na Songea Vijijini lengo ikiwa ni kuendelea kuwajengea uwezo wakulima nchini, “Lakini pia AMCO 20  zilijengewa uwezo juu ya masuala ya mikopo na kuwaunganisha na watoa huduma za kifedha kwenye wilaya 10 ambazo ni Sumbawanga, Mpanda, Kyela, Mvomero, Morogoro Vijijini,Kilombero, Ulanga, Mufindi, Iringa na Mbeya” ilisema taarifa hiyo iliyosomwa na Mark Magila mratibu wa taifa wa TAP II.
 Mratibu wa Taifa wa Ubia wa Kilimo Tanzania Mark Magila akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TAP II kwa Mwaka 2018 kwa wajumbe waliohudhulia  warsha  ya wadau wa TAP iliyofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya.
 Afisa Masoko wa Ubia wa KIlimo Tanzania Alinanuswe Ambalile aakiwasilisha mada kwa wajumbe waliohudhulia warsha ya wadau wa TAP kuhusu mnyororo wa thamani kwenye mazao.
 Mwakilishi wa Ubia wa kilimo Tanzania kwa  ZONE 1 yenye mikoa ya katavi, songwe na rukwa, Wilson Ernest Loth (wa pili kulia) akiwa na wadau wengine wa TAP wakifuatilia warsha ya wadau wa TAP iliyofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya.
Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku moja ya wadau wa TAP iliyifanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya.

TCAA YASITISHA SAFARI ZA NDEGE ZA FASTJET, YATOA NOTISI SIKU 28 KUJIPANGA UPYA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya safari za anga Tanzania (TCAA) , Hamza Johari akitangaza notisi ya siku 28 ya kusudio la kusitisha leseni ya kampuni ya FastJet kutoa huduma za usafiri wa anga Tanzania. 
Wanahabari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya safari za anga Tanzania (TCAA) , Hamza Johari wakati akitoa ufafanuzi juu ya notisi ya siku 28,
Wanahabari wakiuliza maswali. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Mamlaka ya safari za anga Tanzania (TCAA), imetangaza kuwa kampuni ya ndege ya Fastjet imepoteza sifa za kufanya biashara nchini. TCAA imetoa notisi ya siku 28 ya kusudio la kusitisha leseni ya kampuni ya kutoa huduma za usafiri wa anga Tanzania. 


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema kuwa kwa sasa wameamua kuwapa notisi ya siku 28 ili waweze kujipanga upya kama wanaweza kuendelea na biashara au imeshawashinda kutokana na mwenendo mzima wa biashara wanavyoiendesha. 

Amesema kuwa Fastjet limepoteza sifa ya kufanya biashara nchini, na wameizuia ndege moja waliyonayo kuruka kutokana na matatizo ya mara kwa mara na kukosekana kwa meneja mwajibikaji wa shirika.

"Tumekuwa tukiwaandikia barua ya kuwataka watueleze kuhusu mwenendo wao wa biashara tangu Fastjet Plc wajiondoe lakini pia shirika limekuwa na madeni mbalimbali ambayo hayajalipwa. Tukiomba watupe mpango wao wa fedha na biashara kwa mujibu wa sheria hawafanyi hivyo," amesema Johari. 
Amesema shirika hilo linadaiwa na watoa huduma wake wengi ikiwemo TCAA inayolidai Sh1.4 bilioni lakini pia halina meneja mwajibikaji ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ndege anayepaswa kutoa majibu ya hali ya ndege. 

"Kwa sasa fastjet hawana ndege. Ndege yao tangu jana tumeizuia kuruka kwa kuwa imekuwa ikipata hitilafu mara kwa mara na hawana mtu ambaye anaweza kutoa taarifa kuhusu mwenendo wake jambo ambalo linahatarisha usalama endapo itaruka," amesema Johari.

 Amewaomba wananchi kuepuka kutapeliwa na wale watoa huduma watakaowakatia tiketi za Fastjet wakati hazifanyikazi kwa sasa, hawana ndege wameyumba. Mapema leo FastJet imesimamisha safari zake zote na tayari imetangaza kuanzia Desema 20, kuwarudishia nauli kwa abiria waliokuwa wasafiri Disemba na Januari mwaka huu.

Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro

$
0
0
 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba  kutoka Morogoro (wa kwanza kushoto) akiwa na uso wa furaha na binti yake Irene Hatibu (wa pili kushoto) muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake.  Wa kwanza kulia ni mtangazaji wa Clouds FM Mina Ally akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa. Wengine ni Viongozi wa Tigo Kanda ya Pwani.
 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba  kutoka Morogoro akijifuta machozi  ya furaha muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Kulia ni mtangazaji wa Radio Clouds FM Mina Ally na wengine ni viongozi wa Tigo kanda ya Pwani.
 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba  kutoka Morogoro (wa tatu kulia), akiwa na washindi wa shilingi milioni moja moja kutoka mkoani Morogoro muda mfupi baada ya wote kukabidhiwa zawadi zao. Kulia ni mtangazaji wa Clouds FM Mina Ally na wengine ni viongozi wa Tigo Kanda ya Pwani
Mmoja wa washindi wa zawadi ya shilingi milioni moja wa Promotion ya Tigo Jigiftishe Suleimani Ndago (wa kwanza kushoto) kutoka Morogoro  akicheza muziki muda mfupi kabla kukabidhiwa zawadi yake mjini Morogoro. Wa kwanza kulia ni mtangazaji wa Clouds FM Mina Ally na anayefuatia ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa

WAZIRI LUKUVI ALINIKABA NA KUNIPORA MKOBA WANGU ULIOKUWA NA FEDHA-KILUWA.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii.

MSHITAKIWA Mohamed Kiluwa (50) anayekabiliwa na shtaka la kutoa rushwa ya Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, ameieleza mahakama ya Wilaya ya Ilala kuwa Waziri Lukuvi alimkaba na kumpora mkoba uliokuwa na fedha zake. 

Kiluwa ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone amedai hayo leo Desemba 17.2018 wakati akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Samweli Obas.

Akiongozwa na Wakili wake Imani Madega kutoa utetezi wake, Kiluwa amedai Julai 14 mwaka huu  alipata taarifa kutoka kwa  Shabani Selemani aliyemtaarifu kuwa anatakiwa kupeleka hati zake za viwanja ofisini kwa Waziri Lukuvi, ndipo Julai 16, 2018 alifanikiwa kufika ofisini hapo kwa Waziri na kumkuta akiwa peke yake.

Amedai baada ya kumuelekeza Mahali pa kukaa alimuuliza hati zake ziko wapi na yeye akamjibu kuwa anazo mbia mwenzake ambaye kwa wakati ule alikuwa amesafiri.

Aliendelea kudai kuwa, Waziri Lukuvi  alimuuliza tena kuwa hati ziko wapi na kumjibu kuwa mwenzake akirudi ataziwasilisha kwake baada ya majibu hayo Waziri Lukuvi alikaa kimya kama dakika tatu kisha akanyanyuka na kumuuliza kwenye mkoba wake amebeba nini.

Nilimwambia kuna fedha za shoping za ofisini kwangu, baada ya jibu hilo Waziri aliinuka na kuniambia nimpatie mkoba huo, mimi nikawa namwangalia, ikafika wakati alinishika, akaniinua na kuninyanganya begi kisha akalifungua  akatoa fedha na kuziweka juu ya meza.

"Baada ya kitendo kile cha kuninyanganya begi nikawa napiga kelele nikisema nisaidieni.... Muda mfupi kidogo mlango ulifunguliwa na akaingia mtu mmoja na kuniambia nipo chini ya ulinzi lakini Kabla hajamaliza akaingia mwingine naye akasema nipo chini ya ulizi nirudi nyuma hatua mbili, "alidai Kiluwa.

Baada ya watu hao kuingia Waziri Lukuvi alitoka nje ya ofisi na kumuacha yeye pamoja na watu hao wawili waliongia na kumuweka chini ya ulinzi,  ambapo walianza kujiuliza maswali juu ya nani wamfanye shahidi katika tukio hilo.

"Tumfanye nani shahidi,  waliulizana mmoja akajibu muulize mheshimiwa ndipo akatoka nje,  aliporudi akasema Waziri amesema wamwite Sekretari wake ili awe shahidi, Sekretari alikuja na wakamwambia kuwa asome namba za kila fedha iliyopo mezani na ndivyo alivyofanya, "alidai Kiluwa.

Akizidi kujitetea,  Kiluwa ameiomba mahakama imuachie huru kwa kuwa si Waziri Lukuvi wala mashahidi wa upande wa mashitaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi waliothibitisha kuwa alitoa rushwa.

"Mimi sina hatia naiomba Mahakama iniachie huru mimi na pia inirejeshee mali zangu walizozishikilia, naiomba pia inipatie hati zangu na kuzirudisha katika daftari la msajili, "alidai.

Aidha Kiluwa alidai kuwa Waziri Lukuvi anatumika na baadhi ya wafanyabiashara nchini kumuharibia jina lake na biashara zake, jambo ambalo litakwamisha azma ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ya kufikia uchumi wa viwanda.

Kilua Aliendelea kudai Kuwa,  anaviwanja 73 lakini mpka sasa ameshapata hati za viwanja 57 na kwamba  katika hatua zote za kupata hati hizo hajawahi kuombwa wala kutoa rushwa.

Naye shahidi wa pili upande wa Utetezi, ambaye ni miongoni mwa wamiliki na mwanahisa katika Kampuni ya Kiluwa, Jurijs Martinovs alidai mahakamani hapo kuwa Julai 3 mwaka huu alisafiri kupeleka watoto likizo kwa bibi yao nchini Latvia na kurejea Tanzania Agosti 16 mwaka huu.

Martinovs aliwasilisha nakala ya pasipoti ya kusafiria kuonyesha kwamba alisafiri na mahakama iliipokea kama kielelezo cha utetezi katika kesi hiyo.

Baada ya kusikilizwa utetezi huo Hakimu Obas aliharisha kesi hiyo hadi Desemba 24 kwa ajili ya kutoa hukumu.

Kiluwa  anadaiwa kutoa rushwa ya USD 40,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 90 kwa Waziri Lukuvi.
Fedha ambazo inadaiwa lengo lake ilikuwa asiwasilishe hati ya umiliki wa kiwanja namba 57 Block B Kikongo na D Disunyura kilichopo eneo la viwanda lililopo Kibaha mkoani Pwani. Kiluwa yupo nje kwa dhamana.

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA FAMASI LEO JJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amezindua Baraza la Famasi na kuwataka kusimamia sheria ili kudhibiti uuzwaji wa dawa katika maduka ya dawa yasiyo na vibali.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa,  jukumu la Baraza la Famasi ni kuleta msukumo wa utoaji huduma bora ya afya kwa mtanzania.  Hili linawezekana kwa kuhakikisha kuwa wanataaluma wanazingatia maadili na nidhamu ya taaluma katika ununuaji, utunzaji na matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba vilivyo salama na ubora wa hali ya juu. 

Amesema, anapenda nisisitize kuwa Baraza lione umuhimu wa kuweka msukumo wa pekee kwenye masuala ya kuboresha mafunzo na elimu ili  tuwe na wanataaluma  wenye uwezo wa utendaji wa kiwango cha hali ya juu katika nchi yetu katika maeneo yote ikiwamo uzalishaji wa dawa Viwandani ili kwenda sambamba na adhima ya Serikali kuelekea uchumi wa Viwanda.

Ummy anesema anapenda kuwahakikishia kuwa, jamii ya watanzania wanahitaji huduma hii, hali inaonesha kuwa, kupitia takwimu mbalimbali zaidi ya 40% ya wananchi wanapopata tatizo la afya huanza kwenda kupata huduma ya awali kwenye maduka ya dawa (famasi na maduka ya dawa muhimu), hivyo basi kushindwa kuwa na huduma bora katika maeneo hayo  na inahatarisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wananchi. 

"Wataalam wa fani ya famasia ndio wahusika wakuu katika masuala yote yanayohusu dawa katika kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana katika hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini. Serikali kwa upande wake imeongeza bajeti ya Dawa kutoka Shilingi bilioni 30 mwaka 2015/2016 hadi Tsh 270 Bilioni mwaka 2018/2019, hivyo ni Wataalamu hawa wa Famasi wanaotakiwa kuhakikisha kuwa ongezeko la bajeti linaenda sambamba na upatikanaji wa dawa na matumizi sahihi kwa kuzingatia miongozo ya tiba," Ummy

Ummy amesema, kuhusu migogoro ambayo amekuwa akiisikia kati ya Baraza na Wafanya biashara wa Maduka ya Dawa ni vyema wachukue hatua za haraka ili kuondoa changmoto hizo na katika hili anaelekeza Baraza kuhakikisha maduka ya Dawa yasiyo na vibali yaliyopo katika maeneo yasiyoruhusiwa kuendesha maduka ya ADDO, kwa sasa yapewe muda wa mpito wa miaka miwili (2) kuanzia tarehe ambayo utatoa taarifa hiyo kwa umma.

Ameeleza kuwa, katika kipindi hicho maduka hayo yauze dawa zisizohitaji cheti cha Daktari (general sales medicines) kwa utaratibu ambao utaandaliwa na Baraza la Famasi kwa masharti kwamba endapo watakiuka utaratibu huo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao;
Baada ya muda huo kupita, maduka haya yatatakiwa aidha kufungwa, kupandishwa hadhi kuwa Famasi au kuhamia maeneo yanyoruhusiwa ADDO na kuendelea kutoa huduma hiyo; na
Wamiliki wa Maduka ya Dawa ambayo yapo katika maeneo yanayoruhusiwa kuendesha ADDO wayapandishe hadhi maduka yao mara moja.

Aidha, amechukua nafasi hii kwa niaba yangu binafsi na ya Wizara kuupongeza uongozi wa Baraza chini Mwenyekiti Ndugu Legu Mhangwa kwa moyo wa kujitolea na kufanya kazi nzuri pamoja na changamoto zilizokuwepo.  Ni ukweli usiofichika kwamba mmefanya kazi nzuri katika kulijenga Baraza la Famasi.

Ni dhahiri kuwa utaalamu wa kutengeneza, uagizaji, usafirishaji, usambazaji, utoaji dawa sahihi  kwa wagonjwa, utunzaji na utoaji mafunzo yahusuyo dawa ndiyo msingi mkubwa wa taaluma hii. Hivyo basi Baraza ambalo ndilo lililopewa dhamana ya kusimamia kazi za utendaji wa taaluma hii kuongeza nguvu za usimamizi na udhibiti wa sheria na miongozo  na kuhakikisha kazi za wataalamu hawa zinafuata miiko na taratibu za kitaaluma zilizowekwa na zinafanyika kwa uangalifu; na kuchukua hatua zinazostahili pindi inapogundulika kuna ukiukwaji wa Sheria na taratibu

Kwa upande wa Msajili wa Famasi Elizabeth Shekalaghe amesema kuwa changamoto iliyokuwepo ni wafamasi ila wanaendelea kufanya mchakato wa kutoa mafunzo kwa wataalamu na kufikia 1700 kutoka 1263.

Baraza la famasi limezinduliwa leo likingozwa na Mwenyekiti wake Legu Mhangwa akisaidiwa na Emanuel Bujiku, Prof Kennedy Mwambete na mfamasia mkuu wa serikali.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Baraza la Famasi na kuwataka kusimamia sheria ili kudhibiti uuzwaji wa dawa katika maduka ya dawa yasiyo na vibali leo Jijini Dar es Salaam.
  Msajili wa Famasi Elizabeth Shekalaghe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Famasi leo Jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa tuzo kwa kwa wajumbe wa baraza la famasi lililomaliza mda wake, Kushoto ni Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi.

Puma Energy yaendelea kung’ara tuzo za Mwajiri Bora

$
0
0
Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania imeendelea kung’aa kwenye Tuzo za Mwajiri Bora (EYA) za mwaka 2018 baada ya kuibuka mshindi wa tuzo ya ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi (the Employee Engagement Company of the Year 2018) kwa mwaka 2018.

Pamoja na tuzo hiyo kampuni hiyo ambayo imekuwa miongoni mwa wadhamini wakubwa na tuzo hizo, pia ilifanikiwa kutwaa tuzo nyingine ya mahusiano mazuri ya kikazi (Industrial relations).

Kila mwaka Chama cha Waajili Tanzania (ATE) kimekuwa kikiandaa tuzo maalum kutambua wanachama wake wake ambao wanafanya vizuri katika masuala mazima ya rasilimali watu ikiwemo kuwa sera nzuri katika nyanja hiyo.

"Mafanikio ya Puma katika kutoa huduma nzuri kwa wateja wetu kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na jitihada madhubuti zinazofanywa na wafanyakazi wetu ikiwemo kujitoa kwa dhati katika kutimiza majukumu yao," alisema Dominic Dhanah, Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo.

Aliongeza: "Kiwango cha juu cha ushirikishwaji wa wafanyakazi kimekuwa kikisaidia ukuaji wa biashara sambamba na kurahisisha kukabiliana na changamoto zilizo mbele yetu na zaidi inatusaidia kuongeza uzalishaji.Ushirikishaji wa wafanyakazi namna bora katika kufanikisha biashara na inaweza kuongeza ukuaji wa mapato zaidi hadi mara mbili na nusu.’’

"Kwetu ni heshima kubwa kwa kampuni yetu kupewa tuzo hii na ATE. Tunawashukuru sana wafanyakazi wetu wote ambao walishiriki katika kutambua na kutupendekeza ili tuweze kupata tuzo hizi, hakika Puma Energy tunajivunia kuwa na aina hii ya wafanyakazi,’’ alisema.

Katika utoaji wa tuzo hizo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, kampuni ya Puma Energy pia ilifanikiwa kutangazwa kuwa miongoni mwa waajiri kumi bora kwa mwaka 2018.


Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah akitoa neno la shukrani wakati wa Tuzo za Mwajiri Bora (EYA) za mwaka 2018 zilizoandaliwa na Chama cha Waajili Tanzania (ATE) na kufanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Puma Energy ilifanukiwa kuibuka mshindi wa tuzo ya ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi (Employee Engagement Company of the Year 2018) kwa mwaka 2018 pamoja na Tuzo ya Mahusiano mazuri ya kikazi (Industrial relations).
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah (kulia) pamoja na Meneja Rasilimali Watu Kampuni ya Puma Energy Loveness Hoyange wakionyesha tuzo ya ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi (Employee Engagement Company of the Year 2018) kwa mwaka 2018 pamoja na Tuzo ya Mahusiano mazuri ya kikazi (Industrial relations) mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo kwa niaba ya kampuni hiyo.
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah (wa tatu kulia waliokaa), Meneja Rasilimali Watu Kampuni ya Puma Energy Loveness Hoyange (kulia kwake) wakifurahia pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi (Employee Engagement Company of the Year 2018) kwa mwaka 2018 pamoja na Tuzo ya Mahusiano mazuri ya kikazi (Industrial relations) kwenye wa hafla hiyo.

MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kipi Warioba akiotesha Kahawa katika shamba darasa katika kijiji cha Mwasi Kusini



Na Vero Ignatus,Kilimanjaro.

Mafunzo yametolewa kwa Maafisa Ugani 30 kutoka katika kata mbali mbali za wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kujua kanuni bora za kilimo cha kahawa yatakayosaidia kufufua zao hilo na kuhamasisha kilimo cha zao hilo ili kukuza pato la mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Dafrosa Sanga ni Meneja Uendeshaji wa Shirika la Cafe Africa lililoendesha Mafunzo hayo amesema kuwa wameamua kujikita katika zao la kahawa kwani ni moja kati ya mazao yaliyopewa kipaumbele na serikali ikiwemo Korosho,pamba na chai.Dafrosa amesema kuwa mafunzo hayo huendeshwa kwa vitendo kuanzia kwenye kutesha miche,kuvuna na mnyororo wa thamani ili Maafisa Ugani hao waweze kuwasaidia wakulima kuboresha kilimo cha kahawa.

Kipi Warioba ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi amewataka Maafisa Ugani hao wasikae Maofisini bali waende kupeleka ujuzi na marifa waliyoyapata kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wa kahawa kwani uchumi wa mkoa huo umekua ukitegemea zao hilo kwa miaka mingi.Warioba alisema kuwa soko la kahawa la dunia bado linafanya vizuri hususan kwa kahawa bora imekua ikipata bei nzuri ukilinganisha na kahawa isiyokua na ubora imekua ikipata bei ya chini.

Mwakilishi wa Mafisa Ugani hao Magnus Mwang`ata alisema kuwa wanatarajia kuandaa mpango kazi pamoja na kuwa na mashamba darasa kila kata ili kuweza kuwaelimisha wakulima juu ya kilimo bora cha kahawa kitakachowasaidia kuinua pato la mkulima.

Magnus alisema kuwa Mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza mbinu mpya za kilimo cha kahawa kwani teknolojia hubadlika kadiri miaka inavyokwenda hivyo ushirikiano wa Cafe Africa na Jukwaa la Wadau wa Kahawa (ANSAF) utawajengea uwezo Maafisa hao kukuza zao la kahawa.

MAGEREZA YAZINDUA MAKAKATI WA KUMALIZA UHABA WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA JESHI HILO, DODOMA LEO

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa miradi ya ufyatuaji matofali za kuchoma na hydrofom kitaifa kutegemeana na hali ya udongo katika kituo husika. Zoezi la uzinduzi kitaifa limefanyika leo Desemba 6, 2018 katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga, Dodoma. Kulia ni Kamishna wa Fedha na Mipango,Gedeon Nkana, Kamishna wa Miundombinu ya Magerezana Uzalishaji, Tusekile Mwaisabila na Mkuu wa Gereza Isanga ACP Keneth Mwambije. Kushoto ni Kamishna wa Huduma za Urekiebishaji Augostine Mboje na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Omary Salum.
Mtaalam na msimamizi wa mradi wa ufyatuaji tofali katika Gereza Kuu Isanga Dodoma Sajin Modern Mwakialinga wa Gereza Isanga akitoa maelezo kwa viongozi mbalimbali wa Jeshi la Magereza  juu ya namna mradi huo unavyotekelezwa.
Baadhi ya wafungwa waliopo katika programu za urekebishaji ambao wanafundishwa kufyatua, kuchoma tofali na wengine kujenga nyumba wanaotumika katika mradi wa ujenzi wa nyumba za kujitolea katika Gereza Kuu Isanga mkoani Dodoma wakionesha umahiri wao wa kufyatua tofali  leo Desemba 17, 2018.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kujitolea za maafisa na askari wa Jeshi la magereza nchini.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akiangalia ubora wa tofali  za kuchoma alipofanya uzinduzi wa programu ya ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za maafisa na askari wa Jeshi hilo ili kukabiliana na tatizo la makazi kwa watumishi.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna, Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Mikoa ya kiutawala ya Magereza waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa programu ya ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kujitolea za maafisa na askari wa Jeshi hilo. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga Dodoma leo Desemba 17, 2018.Katika hafla hiyo Kamishna Kasike amewataka Wakuu wa Magereza wa Mikoa yote nchini kwa wale ambao hawajaanza utekelezaji wa agizo la ufyatuaji tofali kuanza mara moja kwa kuzingatia hali ya udongo katika maeneo yao. Jeshi la Magereza linaupungufu wa nyumba za watumishi zaidi ya 9000 kote nchini.
Muonekano wa sehemu ya tofali 100,000 moja zilizofyatuliwa na kuchomwa tayari kwa ujenzi wa nyumba 30 za maafisa na askari wa Gereza Kuu Isanga na Ofisi ya Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Dodoma.Nyumba hizo zitakuwa na vyumba vitatu kila moja na mambo mengine muhimu kama sebule, choo, bafu, jiko na store na zinatarajiwa kukamilika kwa mwaka 2019. 
Picha zote na Jeshi la Magereza)

NAIBU WAZIRI MHANDISI HAMAD MASAUNI AFANYA ZIARA WILAYANI MKALAMA MKOANI SINGIDA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na watumishi wa Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida leo   baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli zinazofanywa na Idara zilizopo chini ya wizara.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mbunge  wa Jimbo la Mkalama, Allan Kiula, akiwa ndani ya gari la polisi  muda mfupi  baada  ya  kukabidhiwa na  Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), alipokuwa ziara katika Wilaya hiyo, lengo ikiwa ni kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Idara za wizara, mkoani Singida. 
 Mbunge  wa Jimbo la Mkalama, Allan Kiula(kushoto), akimshukuru Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni baada ya kushuhudia gari la polisi (pichani), lililoletwa  kwa  ajili  ya  shughuli  za kudhibiti uhalifu, Naibu  Waziri yupo mkoani Singida  lengo ikiwa ni kukagua  shughuli  mbalimbali  zinazofanywa  na  Idara  za wizara.
 Naibu Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,  akizungumza   na Askari Polisi wa Kituo cha Nduguti kilichopo  Wilayani ya Mkalama, mkoani Singida leo   baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi  ya  kukagua shughuli zinazofanywa na Idara  zilizopo  chini  ya  wizara. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Polisi wilayani Mkalama, John Ntalima, mkoani Singida Leo, ikiwa  ziara ya kikazi ya kukagua shughuli zinazofanywa na Idara zilizopo chini ya wizara.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAPOKEA MSAADA WA DAWA KUTOKA CHINA WENYE THAMANI ZAIDI YA SHILING BILIONI MOJA

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar                  
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed amewataka wafanyakazi wa Bohari Kuu kutumia mifumo ya kisasa ya kuagiza dawa kujuwa takwimu sahihi ya dawa zilizopo kuepuka kununa dawa ambazo zipo kwa wingi katika Bohari na hazitumiki kwa wingi ili kuzinusuru kuharibika .

Waziri Hamad ameeleza hayo Bohari Kuu ya Dawa Maruhubi alipokuwa akipokea msaada wa dawa tafauti na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kutoka kundi la Madaktari wa China wanaofanyakazi Hospitali ya Mnazimmoja na Abdalla Mzee Mkoani.

Alisema kuwa na takwimu sahihi ya dawa, matumizi ya kila siku na sehemu ambazo aina ya maradhi yanawasumbua zaidi wananchi ni hatua muhimu ya kufanikisha kutoa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.

Waziri wa Afya aliishukuru Serikali ya Watu wa China kwa misaada mikubwa wanayotowa katika kusaidia sekta ya Afya ikiwemo dawa na vifaa tiba na kufanya tafiti za magonjwa mbali mbali yanayosumbua Zanzibar na hatimae kuyatafutia suluhisho bila ya kuweka masharti.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed na Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar  Xie Xiaowu wakisaini hati ya makabidhiano ya dawa zilizotolewa na Serikali ya watu wa China.
 Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu akimkabidhi Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed msaada wa dawa uliotolewa na Serikali ya China, makabidhiano haya yamefanyika Bohari Kuu ya dawa Maruhubi Mjini Zanzibar.
  Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed akizungumza na wafanyakazi wa bohari kuu ya dawa mara baada ya makabidhiano ya dawa yaliyofanyika katika Ofisi hiyo Maruhubi Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed katikati na Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu katika picha ya pamoja na timu ya madaktari wa china wanaofanyakazi Hospitali kuu ya Mnazimmoja. Picha na Makame Mshenga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU JIJINI DAR ES SALAA LEO

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry shilingi milioni 30 taslimu wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Hati ya Heshima Mzee Mohamed Songambele, mmoja wa wazee mashuhuri wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018. Wengine katika meza kuu ni pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jajji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry na viongozi mbalimbali.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na waumini wa Kiisalamu kinamama akishiriki katika dua wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018. Kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa na Jajji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry na viongozi mbalimbali wakishiriki katika dua wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images