Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1753 | 1754 | (Page 1755) | 1756 | 1757 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga amesema hawaoni sababu ya kubalisha sarafu na kwamba zilizopo zinatosha na wanataka ziwe nyingi zaidi kwa lengo la kuhakikisha noti zilizopo zinatumika kwa muda mrefu.

  Profesa Florens ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati anajibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari za fedha na uchumi kabla ya kufunga semina ya mafunzo ya uandishi wa habari zinazohusu fedha na uchumi iliyoandaliwa na BoT.

  Ambapo waandishi walitaka kufahamu kama Tanzania nayo itabadili sarafu yake kama ambavyo nchi ya Kenye imefanya kwa kutoa sarafu mpya ambapo amesema hakuna mpango huo kwa sasa."Tanzania tuna sarafu za kutosha na tunataka ziwe nyingi zaidi ili zitumike kwa wingi na lengo ni kuona noti zetu zinaishi muda mrefu zaidi.Kuhusu Kenya na uamuzi wa kubadili sarafu yao ni uamuzi wao na hauna tatizo kwenye uchumi wetu," amesema.

  Hata hivyo amesema wakati Kenya imeamua kufanya uamuzi wa kutoa sarafu mpya tayari Jumuiya ya Afrika Mashariki imeshapitisha sheria ya Benki ya Afrika Mashariki na ifikapo mwaka 2024 nchi wanachama zinatakiwa kuwa na sarafu moja.Pia ametumia nafasi hiyo kuzungumzia ubora wa noti ya Tanzania ambayo asilimia 100 inatengenezwa kwa pamba , hivyo kuifanya kuwa imara zaidi kuliko Dola."Noti yetu ni imara sana na ukiwambia watu uimara wake ni zaidi ya Dola wanaweza wasiamini."
   Gavana wa  Benki Kuu Profesa Florens Luoga akifafanua jambo wakati anazungumza na waandishi wa habari za fedha na uchumi ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia sarafu ya Tanzania
   Mkurugenzi wa BoT tawi la Dodoma Richard Wambali akitoa neno la shukrani kwa Gavana wa BoT Profesa Florens  Luoga kabla ya kufunga mafunzo ya habari za fedha na uchumi kwa waandishi wa habari
  Meneja wa Idara ya Uhusiano kwa umma na Itifaki kutoka BoT Zaria Mbeo akitoa majumuisho ya mafunzo ya habari za fedha na uchumi kwa Gavana BoT Profesa Florens Luoga

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka Jamii kubadili fikra kwa kuchunguza na kufikiria jinsi ya kutumia vipengele mbalimbali vya lugha ya Kiswahili na Utamaduni wake kama bidhaa ya biashara.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama Cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) na kuratibiwa na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA). “Sote ni mashahidi wa namna lugha ya Kiswahili imeendelea kukua kwa kasi na kuwa si lugha tena bali ni bidhaa yenye tija katika soko la utandawazi” alisema Makamu wa Rais.

  Kaulimbiu ya Kongamano hilo la siku mbili inayosema KISWAHILI CHETU UMOJA WETU KWA MAENDELEO YETU limehudhuriwa na wadau na wataalamu kutoka Mataifa ya Uingereza, Poland, Marekani, Misri, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Pakistan Ujerumani na Austria. Makamu wa Rais ameipongeza CHAKIDU kwa kuhakikisha Kiswahili hakimezwi na lugha za kigeni na kukifanya kiendelee kukita mizizi kwa kusambaa maeneo mbalimbali.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   
   Sehemu ya Wadau na Wataalamu wa Kiswahili waliohudhuria  ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga. 
  Watoto wa Skuli ya Kisiwandui wakipendezesha Kongamano kwa kuimba nyimbo ya Mwanandege wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga.
   Baadhi ya Vitabu mbalimbali vilivyoonyeshwa leo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 


  0 0


  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

  NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amefanya ziara mkoani Morogoro katika Wilaya za Kilombero na Malinyi ili kutatua migogoro na malalamiko ya wafugaji.

   Katika Wilaya za Kilombero na Malinyi  Ulega aliwataka wafugaji waliopo katika bonde la mto Kilombero kuondoka na kwenda kwenye maeneo waliyotengewa ili kuepusha madhara kwa mto huo ambao ndiyo chanzo muhimu cha maji ya mto Rufiji. 

  Ulega alisema wafugaji hao wanapeleka mifugo hiyo bonde la mto Kilombero kufuata maji na kuagiza Halmashauri za Kilombero na Malinyi kutengeneza mabirika ya kunyweshea maji mifugo ili wafugaji wasiende kufuata maji katika bonde hilo. Aidha, aliwataka TAWA kushirikiana na Halmashauri za Kilombero na Malinyi kutengeza mabirika hayo ambapo moja ni takribani Sh. milioni 20 (birika milioni 5 na kisima Sh.milioni 15).

  Pia wafugaji wa maeneo hayo walikiri kutokwenda bonde la mto Kilombero wakitengenezewa miundombinu ya mifugo hasa maji katika maeneo yao.
  Ulega amesisitiza umuhimu wa kutunzwa maeneo hayo oevu ili kutunza mto Kilombero kwa lengo la kuendelee kupata maji mengi katika mto Rufiji itakayosaidia kufanikisha agenda ya Rais Dkt. John Magufuli ya mradi wa Stieglers Gorge.

  Aidha,  Ulega aliwaagiza Wakala wa Mafunzo na Elimu ya Mifugo (LITA) kuandaa mafunzo ya mda mfupi kwa ajili ya wafugaji hao ili waweze kufuga kisasa wawe na mifugo wenye tija. Pia, aliwataka Serikali ya kijiji kuheshimu mipango ya matumizi bora ya ardhi iliyopo ili kuepusha migogoro.
   Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega(wambele)akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya Malinyi mkoa wa Morogoro wakati wakiwasili kwenye kijiji cha Ngombo,wakati wa ziara yake ya kuzisikiliza kero migogoro mbalimbali ya wafungaji,wavuvi na kuzitafutia ufumbuzi.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngombo wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro,katika mkutano wa hadhara wa  kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji,wavuvi  na kuzitatua.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wapili (kushoto) akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya Malinyi mkoa wa Morogoro wakiwasili katika kijiji cha Ngombo kwenye ziara yake ya kuzisikiliza kero na migogoro mbalimbali ya wafungaji,wafungaji na kuzitatua.

  0 0

  Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara


  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameagiza kurejeshwa ndani ya miezi mitatu madeni yote yaliyokopwa kwenye vyama vya akiba na mikopo (SACCOS).

  Alisema kuwa mwananchi watakaoshindwa kutii maelekezo hayo katika kukamilisha deni lake ndani ya miezi mitatu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.“ Nataka kila aliyekopa kwenye Saccos arejeshe deni lake kwa kufuata utaratibu wa makubaliano na kama wasipotekeleza ndani ya miezi mitatu niliyotoa serikali itaagiza wahusika wote kukamatwa maana dawa ya deni ni kulipa” Alisisitiza

  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa agizo hilo tarehe 14 Disemba 2018 wakati wa kikao cha kazi katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara.

  Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kaimu Mrajisi wa vyama vya Ushirika nchini, Mkaguzi wa vyama vya ushirika na Saccos, Kaimu Mrajisi msaidizi wa mkoa wa Mtwara, Wenyeviti na watendaji wa SACCOS pamoja na vyama vya msingi vya ushirika vilivyopo mkoani Mtwara. 

  Mhe Hasunga amelitaka Shirika la Ukaguzi wa Hesabu za Vyama vya Ushirika (COASCO) kutimiza majukumu yake kwa weledi kwa kukagua na kuhakikisha vyama vyote vinafunga mahesabu huku akitaka vyama ambavyo sio hai kuchukuliwa hatua.Pia ameagiza kila chama Tanzania kiwe na daftari la wanachama walio hai na wafu sambamba na kuhakikisha kuwa viongozi wote wawe na maadili na uwezo wa kuvisimamia vyama vyao ipasavyo.

  Katika hatua nyingine alimtaka Mrajis wa ushirika Tanzania Bw Tito Haule kuwasilisha mpango kazi wa namna ya kukutana na wanachama wa ushirika nchi nzima katika kutatua changamoto zao. “ Na ni lazima taarifa itengenezwe ikionyesha idadi ya vyama mlivyokutana navyo na kueleza ni mambo gani mmezungumza kila mwezi” Alisema

  Aliongeza kuwa Viongozi ni lazima kutoa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya Ushirika itakayosaidia kuondoa usumbufu kwenye ushirika ili uendelee kuwa mkombozi wa wananchi. “Mje na mfumo wa namna ya kuwasaidia wananchi kupata pembejeo bila kuingia madeni yasiyokuwa na tija” Alisisitiza
  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
  Viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018.
  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018.  0 0

  *Awataka waliopewa dhamana wazingatie viwango vya kimataifa
  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezinduaChaneli ya Taifa ya Utalii iitwayo Tanzania Safari Channel na amewataka watu wote waliopewa dhamana ya kuiendesha wahakikishe wanazingatia viwango vya kimataifa katika vipindi watakavyokuwa wanaviandaa. “Vipindi vyenu ni lazima vivutie kama vile tunavyoviangalia katika chaneli za wanyama za kimataifa kama vile National Geographic, Discovery, Travel na zingine ili lengo lililokusudiwa wakati wa kuanzishwa kwake litime.”


  Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Desemba 15) wakati akizindua chaneli hiyo kwenye Ofisi za TBC, Mikocheni, jijini Dar es Salaam, ambapo ametoa wito kwa Wizara zote zinazohusika na uanzishwaji wa Chaneli hiyo kuhakikisha zinailea wakati ikijijenga kujiendesha kibiashara.

  Amesema Tanzania ni moja ya nchi duniani zilizotenga moja ya tatu ya eneo lote la nchi kwa ajili ya uhifadhi, ambapo kuna tamaduni za makabila mbalimbali, ngoma za kuvutia, vyakula vya asili, sinema za maisha yetu na lugha adhimu ya Kiswahili.

  “Hivyo, kwa kuanzishwa kwa chaneli hii inayotengeneza vipindi na kuonesha vivutio hivi ndani na nje ya Tanzania itasaidia watalii huko waliko kujua huu utajiri wetu na kuchagua kuja kutalii nchini. Ni matumaini yangu kuwa hii Tanzania Safari Channel ninayoizindua leo itaongeza thamani katika kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea Tanzania.”

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel kwenye  Viwanja vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam Desemba 15, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel kwenye  Viwanja vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam Desemba 15, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, wapili kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Upendo Mbele wakati alipotembelea Studio mpya za TBC kabla ya kuzindua chaneli ya Tanzania Safari Channel, Desemba 15, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC,  Dkt. Ayoub Ryoba.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Chaneli ya  Tanzania Safari Channel kwenye viwanja vya Ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mikocheni jijini Der es slaaam, Desemba 15, 2018. 
   Baadhi ya viongozi na wageni waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa wakati alipozindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel kwenye viwanja vya Ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam, Desemba 15, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuzindua Chaneli ya Tanzania Safari Chanmnel Kwenye viwanja vya TBC,  Mikocheni jijini Dar es salam, Desemba 15, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Na John Nditi, Morogoro

  NAIBU waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye ameiagiza Baraza la Wafanyakazi la Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) pamoja na Menejimenti ya Kampuni kuimarisha kitengo cha masoko na kufanya ufuatiliaji kwa watumishi na mawakala wanaoihujumu Kampuni hiyo.

  Naibu Waziri alisema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha tatu cha baraza la wafanyakazi wa ATCL lililofanyika mjini Morogoro.

  Alisema , kwa muda mrefu kumekuwa na manenoo mengi yanayosemwa juu ya kuwepo hujuma dhidi ya Ndege za ATCL hasa kwenye njia ya Kilimanjaro na Mbeya .

  Mbali na njia hizo pia huduma hizo zinafanywa kwa maeneo mengine ambapo wateja wanapohitaji huduma za ATCL huambiwa kuwa ndege zimejaa wakati jambo hilo si kweli na matokeo yake ndege zinaondoka bila kujaa abiria.

  “ Baadhi ya makawala wanaouza tiketi za ATCL wanaonwa na makampuni mengine ya Ndege ili wajaze kwanza ndege zao kwa kutoa maelezo kwa wateja wanaohitaji kusafiri na ndege zetu za umma kuwa zimejaa , lakini baadaye zinaondoka bila kujaa abiria” alisema Naibu Waziri Nditiye.

  Naibu Waziri huyo alisema “ Huduma za ndege zetu ni nzuri na nauli yake ni ndogo na pia ndege zetu zote ni mpya lakini hazijai tofauti na za makampuni binafsi ambayo bei zake ni za juu na huduma zao hazifanani na za ATCL “ alisema Naibu Waziri Nditiye .

  “ ...Hii ni hujuma ambayo haiwezi kufumbiwa macho , naitaka Menejimenti ya ATCL kuangalia jambo hili ili lipatiwe ufumbuzi na imarisheni kitendo cha masoko” alisema Naibu Waziri Nditiye.

  Hata hivyo alisisitiza kwa kusema , kutokana na jambo hilo , ni wajibu wa Menejimenti ya ATCL kuimalisha kitengo cha masoko na kuangalia ‘ Faulo” hizo zinazochezwa na makampuni mengine ya Ndege ili kuwepo kwa ushindani wa soko na si ushindani unaotokana na kulihujumu ATCL ambalo kwa sasa linaendeshwa vizuri.

  Naibu Waziri Nditiye alisema, ni matengemeo ya Serikali kuona ATCL inafanya vizuri na kwa viwango vya kimataifa kwani ni fahari kwa nchi yetu .

  Alisema , hiyo inatokana na serikali ya awamu ya tano kuweka kipaumbele katika uendeshaji wa Kampuni hiyo ambayo hadi sasa imeshapewa ndege nne ambazo ni Dash 8 Q400 tatu, Boeing 787 Dreamliner moja.

  Akizungumzia kuongezwa kwa Ndege nyingine alisema , hivi karibuni zinategemewa ndege nyingine mbili aina ya Airbus 220-300 ambazo zitaongezwa ambapo pia Kampuni hiyo ikitegemea kupokea ndege nyingine mpya ya Boeing 787 Dreamliner mwakani (2019).

  Mbali na hayo aliipongeza Manejimeti hiyo kwa kuonesha mchakato wa kuanzishwa kwa safari ndege kubwa moja kuanzia mwezi huu ( Des) itakayotoka Jijini Dodoma siku za Jumatatu kwenda Jiji la Dar es Salaam na Ijumaa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ili kulimalisha usafiri wa abiria wengi zaidi.

  Kwa msingi huo aliwataka wafanyakazi wa ATCL kuwajibika kwa umma, kwa vile mafanikio ya biashara ya usafiri wa anga ni utoaji wa huduma bora na uwajibikaji kwa kuwa hudumua wateja na watu wengine kwa heshima.

  Naibu Waziri alitaka umakini zaidi kwa wananchi wenye mahitaji ya pekee kama vile wazee, wanawake , watoto , wagonjwa , weenyeulemavu na kundi lolote la watu ambao wapo katika hali ngumu.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema , Baraza na Menejimenti imepokea maagizo yote na kuahidi kuyatendea kazi kikamilifu ikiwa na kuyapatia majawabu malalamiko na changamoto mbalimbali.

  Hata hivyo alisema, kikao hicho cha tatu cha baraza la wafanyakazi kilikuwa na kaulimbiu ya “ Sasa tuwajibike” kilikuwa na mada nne ambazo ni Mkakati wa kuboresha Huduma kwa Wateja , Udhibiti wa gharama za uendeshaji , Mabadiliko katika Mifuko ya Jamii ,na Elimu kuhusu Mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi.  Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye ( kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi ( wa pili kushoto ) baada ya Naibu Waziri kufungua kikao cha tatu cha baraza la wafanyakazi wa ATCL lililofanyika mjini Morogoro.  Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye ( kulia ) akijadiliana jambo na Mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi ( kushoto ) kwa ajili ya kufungua kikao cha tatu cha baraza la wafanyakazi wa ATCL kilichofanyika mjini Morogoro.  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa ATCL wakimsilikiza Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye ( hayupo pichani ) alipofungua kikao cha tatu cha baraza hilo mjini Morogoro.  Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye ( kulia ) akielekea ukumbini akiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi ( kushoto ) kwa ajili ya kufungua kikao cha tatu cha baraza la wafanyakazi wa ATCL kilichofanyika mjini Morogoro.  Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ( kati kati walioketi ) akiwa pamoja wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa ATCL pamoja na Mkurugenzi mkuu Ladislaus Matindi ( wapili kulia ) baada ya Naibu Waziri kufungua kikao cha tatu cha baraza la wafanyakazi wa ATCL kilichofanyika mjini Morogoro.( Picha na John Nditi).

  0 0

  VICTOR MASANGU, KIBAHA 

  NAIBU waziri wa nishati Subira Mgalu katika kuumga mkono Juhudi za Rais Dk . John Pombe Magufuli ya kuboresha sekta ya afya hapa nchini ameliagiza Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wanapeleka miundombinu ya nishati ya umeme haraka iwezekanavyo katika maeneo ya vituo vipya vya afya 300 pamoja na hospitali 69 ambazo zinajengwa na serikali kwa lengo la kuboresha huduma ya matibabu kwa wananchi wake.

  Mgalu ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia Mkoa wa Pwani alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo katika halmashauri ya mji Kibaha pamoja na kukagua mwenendo wa ujenzi wa upanuzi katika kituo cha afya mkoani kilichopo Wilayani Kibaha.

  “Kwa kweli nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inafikisha kwa haraka miundombinu ya umeme katika vituo vipya vya afya ambavyo vinajengwa pamoja na hospitali hivyo nachukua nafasi hii kuwaagiza Tanesco pamoja na REA kufikisha umeme haraka iwezekanavyo katika maeneo hayo ili wananchi waweze kupata huduma ya afya katika mazingira ambayo ni rafiki kwao na katika hili tunamshukuru sana Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli,”alisema Mgalu.

  Aidha alibainisha kwamba kwa sasa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha miundombinu ya umeme katika maeneo mbali mbali ili zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali ziweze kupata nishati ya umeme wa uhakika ambao utasaidia kuboresha zaidi katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi wa Tanzania ambao hapo awali walikuwa wanateseka.

  Kwa upande wake Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Kibaha Tulitweni Mwinuka alisema kwamba wamepokea kiasi cha shilingi milioni 500 kutoka serikali kuu kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho cha afya mkoani katika maeneo ya wodi ya wazazi,jengo la mionzi jengo maalumu kwa ajili ya kufulia pamoja na jengo la upasuaji ambapo kukamilika kwake kutaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya mlundikano kwa wagonjwa.

  Nao baadhi ya wanawake Wilayani Kibaha Elina Mngonja na Selina Wilsoni wamemshukuru Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuboresha sekta ya afya hapa nchni ambapo wamesema kukamilika kwa upanuzi wa kituo hicho hasa katika wodi za kinamama wajawazito utakuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la utoaji wa huduma hasa wakati wanapokwenda kujifungua.
    Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Kibaha Tulitweni Mwinuka kushoto akimwonyesha ujenzi unavyoendelea  wa mradi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Mkoani kilichopo Wilayani Kibaha, Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu kulia kwake ambaye alifanya ziara kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.(PICHA NA VICTOR MASANGU). 
    Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu kulia akipokea taarifa ya ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya mkoano kutoka kwa Mganga mkuu wa halmashauri ya mjini Kibaha Tulitweni Mwinuka.
   Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu kulia akiangalia mwenendo wa upanuzi wa ujenzi wa kituo cha afya mkoani kushoto kwake ni Mganga mkuu wa halmasshauri ya mji Kibaha
  Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi huo wa upanuzi wa kituo cha afya mkoani ambacho kitajengwa wodi ya wazai, jengo la miozi, jengo la kufulia pamoja na upasuaji.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya Zanzibar Ikulu Zanzibar, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya ya Zanzibar , mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, leo.15/12/2018.kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)

  0 0


  Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamiii

  NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega amempa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara mwezi mmoja wa kuandaa miundombinu ya wafugaji wa vijiji,Vilima Vitatu,Minjingu waliohamishwa katika hifadhi ya wanyamapori ya Burunge.

  Ulega amesema Mkurugenzi huyo Hamis Malinga anapaswa kuandaa miundombinu hiyo ya wafugaji ili wakiondolewa kwenye hifadhi ya jamii ya Burunge waweze kuhamia Mfulang'ombe kwenye eneo lililojengwa.

  Amesema wafugaji hao wanapaswa kuwekewa miundombinu rafiki ikiwemo malambo na majosho ili waweze kuanza maisha mapya ya ufugaji. Amesema wafugaji hao walikuwa wanalalamikia kuondolewa kwenye eneo hilo na kupelekwa sehemu nyingine ambayo haina miundombinu rafiki.

  Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Babati, Hamis Malinga amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa wapo kwenye mchakato wa kuandaa miundombinu rafiki ya wafugaji hao. "Kila mfugaji atapatiwa ekari tatu kwa ajili ya kuhakikisha anazimiliki na tutaandaa malambo na majosho kwa ajili ya mifugo ya hizo kaya 17 zilizoondolewa kwenye hifadhi," amesema.

  Kwa muda mrefu kaya 17 za wafugaji wa jamii ya kifugaji ya wabarbaig waliamriwa kuondoka kwenye eneo hilo lakini waligoma.

  Eneo la jamii la hifadhi ya wanyamapori Burunge lenye ukubwa wa kilomita za mraba 283 linaundwa na vijiji 10 vya Sangaiwe, Mwada, Ngoley, Vilima Vitatu, Minjingu, Kakoi, Olasiti, Manyara, Magara na Maweni. 
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Minjingu na Vilima Vitatu wilaya ya Babati mkoani Manyara ,katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji,wavuvi na kuzitafutia ufumbuzi .
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Babati mkoa Manyara wakiangalia hifadhi ya jamii ya Burunge.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwasikiliza wafugaji wa wilaya ya Babati mkoa Manyara walipokuwa wakiwasilisha changamoto zao.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa mkoa wa Manyara katika ziara yake ya kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji na wavuvi na kuzitafutia ufumbusi.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)


  0 0   Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza  na watumishi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini wa Ofisi yake kuhusu utekelezaji wa Mfumo wa  Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa watumishi wa umma, alipoitembelea Idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
  002
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akielezwa majukumu ya Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini na mkurugenzi wa Idara hiyo,  Bw. Hassan Kitenge, alipoitembelea Idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
  003
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akihimiza usimamizi mzuri wa Mfumo wa  Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS)  kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Bw. Hassan Kitenge, alipoitembelea Idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
  …………………….
  Watendaji Wakuu katika Taasisi za Umma nchini wametakiwa kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuhakikisha wanasimamia vizuri utekelezaji wa Mfumo wa  Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) wa mtumishi mmoja mmoja ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa maslahi ya maendeleo ya taifa.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa alipoitembelea Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini ya Ofisi yake kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.

  Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, usimamizi na utekelezaji mzuri wa Mfumo wa  Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) utaondoa tatizo la ufanyaji kazi wa mazoea kwa baadhi ya watumishi wa umma nchini na kuongeza kuwa, utawezesha kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga utamaduni wa kila mtumishi wa umma katika nafasi aliyonayo kufanya kazi kwa bidii, ufanisi na weledi ili utumishi wake uwe na tija katika maendeleo ya taifa.

  Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano inataka kuwa na OPRAS ambayo ni chachu ya kuimarisha utendaji kazi na uwajibikaji kwa kila mtumishi wa umma, hivyo ameitaka Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini ambayo ina majukumu la kutoa miongozo na kusimamia OPRAS, kuweka msingi imara wa usimamizi na utekelezaji wa OPRAS katika Taasisi za Umma.

  Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua kuwa, lengo la Serikali kuwa na Mfumo wa  Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) limejikita katika kuimarisha utendaji kazi  na kuongeza kuwa, linaenda sambamba na Kaulimbiu ya HAPA KAZI TU, hivyo Taasisi za umma hazina budi kuzingatia OPRAS ili kuitekeleza kwa vitendo kaulimbiu hiyo.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Bw. Hassan Kitenge amesema idara yake ilianzishwa kwa lengo la kutoa miongozo na kusimamia utendaji kazi katika ngazi ya taasisi na ngazi ya mtumishi mmoja mmoja hivyo ina jukumu la kuhakikisha kuwa, taasisi zote za umma zinakuwa na mikataba ya utendaji kazi pamoja na kusimamia utekelezaji wa Mfumo wa  Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) ambao ni wa uwajibikaji kwa mtumishi mmoja mmoja.

  Bw. Kitenge ameainisha kuwa, kwa maana ya majukumu ya jumla, Idara yake ina jukumu la kusanifu na kufanya mapitio ya Mfumo wa Mikataba ya  Utendaji Kazi katika ngazi ya taasisi na Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa mtumishi mmoja mmoja.

  Bw. Kitenge amefafanua kuwa, pamoja na majukumu mengine, idara yake inanafanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mifumo hiyo katika taasisi za umma zipatazo 480 na kufanya uchambuzi wa taarifa hizo pindi zinapowasilishwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kutoa ushauri wa kisera kwa mamlaka na kuandaa taarifa ya mwaka ya tathmini.

  Bw. Kitenge ameahidi kuwa, atahakikisha anatumia weledi wake kuiongoza idara yake kutekeleza  vema jukumu la usimamizi wa utekelezaji wa Mfumo wa Mikataba ya Utendaji Kazi na Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) katika Utumishi wa Umma,  ili mifumo hiyo iwe na manufaa na tija katika kuimarisha utendaji kazi wa taasisi za umma na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma.

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ameitembelea Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini  ikiwa ni sehemu ya ratiba yake ya kutembelea Idara na Vitengo vyote vilivyopo ndani ofisi yake kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kufahamu vema majukumu ya kila idara na kitengo ili aweze kuiongoza ofisi hiyo kwa mafanikio.

  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu
   
  Jumla ya Wanafunzi 12,399 mkoani Simiyu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 katika shule za Serikali za kutwa na bweni kwa awamu ya kwanza. Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Desemba 14, 2019 wakati akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 Mjini Bariadi.
   
  Sagini amesema jumla ya wanafunzi waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba ni 24,983 sawa na asilimia70.68 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani, ambapo amebainisha kuwa wanafunzi 12, 584 kati ya 24,983 waliofaulu hawajachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu.
   
  Sagini amesema lengo la Serikalini kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaenda sekondari hivyo, amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa wanafanya jitihada katika ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu, ili wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba waweze kuanza kidato cha kwanza kwa wakati.
   
  “Lengo la Serikali ni kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza ; nimetoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri  kukamilisha miundombinu inayohitajika ili wanafunzi watakaochaguliwa awamu ya pili waweze kuripoti shuleni kabla ya Februari 15, 2019”
   
  “Nawasihi wazazi na walezi wa wanafunzi watakaokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa awamu ya kwanza kuwa wavumilivu wakati Halmashauri zinajiandaa kuwapokea wanafunzi hao”  alisema Sagini. Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 67.73 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 70.68, ambapo wavulana wameonekana kufanya vizuri zaidi kwa ufualu wa asilimia 74.61 na wasichana asilimia 67.57.
   
  Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa amesema mahitaji ya miundombinu yameongezeka kutokana na ufaulu  kuongezeka kila mwaka, hivyo jitihada zitafanyika ili kuhakikisha miundombinu inayohitajika inajengwa na wanafunzi wenye sifa za kwenda kidato cha kwanza wanapata nafasi.
   
  Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Chenge, Mwl.Mhinga Bulenzi amesema wamefanya mikutano kadhaa na wazazi na wakakubali kushirikiana na Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ili wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba na hawakuchaguliwa kwa awamu ya kwanza waanze kidato cha kwanza ifikapo Februari 15, 2019.
   
  Jumla ya wanafunzi 35,346 kati yao wasichana wakiwa 19,743 na wavulana 15,603 walifanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu darasa la saba mwaka huu 2018 mkoani Simiyu.
    Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
  PICHA%2BB
    Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya hali ya ufaulu katika Mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2018, katika kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019 kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
  PICHA%2BC
   Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Mhe. Paul Maige  wakifuatilia kwa makini nyaraka zenye taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, katika kikao kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
  PICHA%2BD
   Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kikao hicho na Katbu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua kikao hicho  Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
  PICHA%2BE
  Baadhi ya waandishi wa habari na wajumbe wa Kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kikao hicho na Katbu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua kikao hicho  Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.

  0 0

  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akisaidiana na wahandisi na mafundi wa kikosi kazi cha kufufua kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) kushusha kaangio la korosho ghafi kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati. Kiwanda cha BUCO kinafanyiwa ukarabati tayari kwa kuanza kubangua korosho zilizonunuliwa na serikali. 
  Fundi wa kurekebisha mashine za kubangua korosho Dastan Milanzi akifanya marekebisho ya mwisho kwenye moja ya mashine za kubangua korosho za kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) kama alivyokutwa na mpiga picha wetu. 
  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, akipata maelezo ya ukarabati wa mashine ya kubangua korosho kutoka kwa mratibu wa kikosi kazi cha kufufua kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) Dkt. Isack Legonda (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa kiwanda hicho kilichokabidhiwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Sylvster Mpanduji. 
  Baadhi ya wahandisi na mafundi wa kikosi kazi cha kufufua kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) wakibeba kaangio la korosho ghafi. Kikosi kazi hicho kinatekeleza agizo alilolitoa wiki iliyopita Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda Vidogo (SIDO), Profesa Sylvester Mpanduji, akikagua shughuli za ubanguaji wa korosho unaofanywa na wabanguaji wadogo kwenye eneo la SIDO Mtwara. SIDO kwa kushirikiana na wajasriamali wadogo inatekeleza azma ya serikali kuhakikisha korosho zinabanguliwa nchini. 
  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akishuhudia zoezi la kubangua korosho linalofanywa na wabanguaji wadogo kwenye eneo la SIDO mjini Mtwara. Mhandisi Manyanya yuko kwenye ziara ya kukagua uwezo wa viwanda vya kubangua korosho mikoa ya Mtwara na Lindi kujiridhisha kabla ya kuingia makubaliano ya kubangua korosho ya serikali. (Picha zote na Idara ya Habari-MAELEZO)

  0 0
  Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, wakisakata muziki wakati wa sherehe ya kuuaga mwaka 2018 iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano, Rosalynn Mworia, (Kushoto) akimsikiliza Goodluck Mushi, wakati akishukuru kwa kutunukiwa tuzo ya mfanyakazi bora wakati wa sherehe ya kuuaga mwaka 2018 iliyofanyika Mlimani City Jijijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (kushoto) akimpongeza Christina Murimi, mara baada ya kukabidhiwa TUZO ya mfanyakazi bora, wakati wa sherehe ya kuuaga mwaka 2018 iliyofanyika Mlimani City Jijijini Dar es Salaam.

  0 0


   Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Jayne Nyimbo-Taylor akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya kutoa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na chama hicho katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akiwa mgeni rasmi ilitoa tuzo kwa kutambua vipengele 17 kutambua waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu.
  Image002
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo Mh. Anthony Mavunde (MB), Mhe. Stella Ikupa (MP), wawakilishi wa balozi za Norway, Denmark, China  pamoja na taasisi mbali mbali ikiwemo TUKTA na ILO na waajiri mbali mbali nchini.
  Image003
  Mwakilishi wa Tanzania Cigarette Company (TCC), akipokea Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 baada ya kampuni hiyo kuibuka washindi afasi ya tatu katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba mgeni rasmi akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB).
  Image004
  Mwakilishi wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Bi. Lilian Makau akipokea Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 baada ya Kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi ya pili katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba mgeni rasmi akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB).
  Image005
  Wafanyakazi wa Geita Gold Mine (GGM) wakifurahiya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) baada ya kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi ya kwanza kwenye hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba 2018.
  …………………………………………………………….
  Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Disemba 14 2018 kimeandaa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, tuzo hizo zimejikita katika kutambua waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa guvu kazi na rasilimali watu kwa lengo la kuwawezesha kutimiza wajibu wao kikamilifu na kupelekea kukuza uzalishaji wa kibiashara. 

  Tuzo hizo zilihudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo Mh. Jenista Mhagama, Mh. Anthony Mavunde, Mhe. Stella Ikupa, Mkuu wa Mkoa DSM, Mhe. Paul Makonda, Balozi wa Norway nchini, Bi. Elisabeth Jacobsen, Balozi wa Denmark nchini, Bw. Einer H. Jensen na Balozi wa China nchini Nd. Wang Fe, pamoja na taasisi mbali mbali ikiwemo TUKTA na ILO.

  Tuzo hizo zinazofanyika kila mwaka zimasaidia kuhamasisha wanachama kuchukulia masuala ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama misingi muhimu katika kumwezesha mwajiri kuwana wafanyakazi wenye uwezo na ueledi ili kukidhi mahitaji ya ushindani katika biashara.

  Sherehe ya utoaji tuzo iliyohudhuriwa na Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa Mgeni Rasmi, zimekuwa maarufu hapa nchini katika muktadha wa biashara hasa kwa kuhamamasisha makampuni makubwa na madogo na ya ukubwa wa kati kuhusu umuhimu wa kuzingatia misingi bora ya kufanya biashara nchini.

  Tuzo hizo ambazo kwa mwaka 2017 ziliboreshwa kwa kuongezewa vipengele 12 vipya vya Hali nzuri kwa Wafanyakazi (Employee Wellness), Kuvutia na kutunza wafanyakazi wenye ujuzi (Attraction and Retention), Mahusiano Mazuri Mahali pa Kazi (Industrial Relations), Kujali kazi na maisha nje ya Kazi (Work Life Balance), Mwajiri anayekubalika na Kufahamika (Employer Branding), Usimamizi wa Wafanyakazi kwa kuzingatia Umri (Managing an Aging Workforce), Uwekezaji katika Teknolojia (Technology Investment), Tuzo kwa ajili ya Sekta Binafsi (Private Sector Award), Tuzo kwa Sekta ya Umma (Public Sector Award), Tuzo kwa Ajili ya Mashirika ya Kijamii ( Civil Society Award) na Tuzo ya Mwajiri Mzawa (Indigenous Employer Award) , zitaendelea na vipengele hivyo vipya kwani vinatoa fursa kwa wanachama kufanyia kazi vipengele hivyo kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi na ajira kulingana na mahitaji ya waajiri nchini.

  Akizumgumza na wageni waalikwa Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu alisema kwamba serikali inatambua mchango wa waajiri kutoka sekta zote na itaendelea kushirikiana nao pamoja na Vyama vya Wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika kutimiza azma ya nchi yetu kujitegemea. 

  Mhe. Jenista Mhagama aliongeza kuwa serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania, Dr. John Joseph Magufuli imebeba jukumu la kuboresha miundombinu katika nyanja za usafirishaji wa anga, reli na maji, afya, nishati, elimu na mawasiliano ambayo kwa kiasi kikubwa zinaongeza uzalishaji wa nchi kupitia waajiri wa sekta binafsi na umma.

  Aidha Mh. Mhagama alipongea Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa shughuli zake mbaliikiwemo Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka, Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Uongozi kwa Mwaka2018, Mwanamke wa Wakati Ujao inayofanyika kwa ushirikiano na Shirikisho la Vyama vya
  Waajiri nchini Norway (NHO) kutoa mafunzo kwa wanawake ili waweze kushika za juu zauongozi katika makampuni na taasisi mbali mbali ambapo tangu kuasisiwa kwake mwaka 2016, wanawake 66 wamehitimu mafunzo hayo.
   Akiongea na wageni waalikwa, Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. JayneNyimbo Taylor alishukuru serikali ya awamu ya tano kwa juhudi zake katika kuboreshamazingira ya kufanya biashara nchini kama punguzo la tozo inayolipwa na waajiri kwa ajili ya kukuza ujuzi mahali pa kazi maarufu kama “Skills Development Levy (SDL)” kutoka 6% mpaka kufikia 4.5% huku akiiomba serikali kuipunguza tozo hiyo hadi kufikia 2%. 

  Pamoja na mapendekezo hayo, Bi. Jayne Nyimbo pia aligusia changamoto mbali mbali zinazowakabili waajiri kama ufuatiliaji wa vibali vya kufanya kazi nchini, utaratibu wa malipo ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo sekta binafsi wanalipa 1% huku waajiri wa umma wanalipa 0.5% ya mshahara anaolipwa mfanyakazi, aina mikataba ya ajira pamoja na tozo na faini zinazotozwa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).

  Aidha kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania(ATE), Dkt.Aggrey K. Mlimuka, alitoa shukrani zake za dhati kwa Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, wageni waalikwa na wadau mbali mbali waliofanikisha Tuzo ya Mwajiri wa Mwaka 2018. “Naomba nikushukuru tena Mhe. Mgeni Rasmi, na Washiriki wote kwa kuja kujumuika na sisi katika utoaji wa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018, na naamini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa kushikiana na TUCTA pamoja na Serikali hasa tunapoendelea kujenga nchi yetu kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Naomba kutumia fursa hii pia kuwashukuru na kuwapongeza wanachama wote walioshiriki katika zoezi hili hasa kwa kujaza dodoso ili kupata fursa ya kulinganisha utendaji wa makampuni yao na ya wengine.” Alisema Dkt. Mlimuka.

  “Naomba kuhitimisha salamu zangu kwa kuwatambua uwepo wa baadhi ya wanachama nawadau wetu kwa michango yao ambayo imetuwezesha kufanikisha utoaji wa tuzo hii ambao ni wafuatao.” Alimalizia Dkt. Mlimuka. Kuhusu Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ni chombo pekee cha waajiri

  0 0


   Wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii muda mchache kabla ya kuanza uchaguzi wa viongozi wa Baraza hilo Kitaifa.
  2
  Mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Taifa la Watoto akikusanya kura kutoka kwa wajumbe wa Baraza wakati wa zoezi la kuwapigia kura wagombea wa uongozi wa Baraza la Taifa la Watoto.
  3
  Baadhi ya Wagombea wa uongozi katika Baraza la Watoto Taifa wakisubiri matokeo kujua kama bahati iko upande wao wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Taifa la Watoto jana katika Manispaa ya Singida.
  4
  Viongozi wa nafasai nne za juu za Baraza la Taifa la Watoto wakiwa tayari kwa majukumu mapya wakawanza kushoto ni mweka hazina mpya wa Baraza hilo Ince Frank kutoka mkoa wa Mbeya, wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Aidathi Ismail kutoka Mkoa wa Mwanza na katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Joel Festo kutoka Mkoa wa Mwanza na kulia kwake ni Katibu wa Baraza Thuwaiba Abdallah kutoka Unguja Magharibi.


  Na Mwandishi Wetu -Singida

  Baraza la watoto la Taifa leo limepata uongozi mpya baada kukamilisha uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Baraza hilo na pia uchaguzi wa Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti, Katibu na Mweka hazina wa Baraza hilo uchaguzi uliofanyika jana katika Manispaa ya Singida.

  Akiongea mara baada ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi huo Mwenyeliti wa Uchaguzi wa Baraza hilo Bi. Joyce Mugambi amewataka viongozi wa Baraza hilo kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo kwa kushirikiana na viongozi wa Wizara Mama ili kuleta ufanisi kiutendaji.

  Uchaguzi wa Viongozi wa Baraza hilo ufanyika kila baada ya kipindi cha miaka miwili kwa kuwa na Wajumbe kutoka Tanzania Zanzibar ambao kwa pamoja wanaunda wajumbe wa Baraza Kuu la Baraza hilo ambapo Mwenyekiti na Makamu wake wanaweza kutoka upande wowote wa Muungano, ikitokea mwenyekiti katokea  Zanzibar inabidi Makamu wake pia atokee huko ili Katibu atoke Tanzania Bara.

  Viongozi walioshinda kwa nafasi ya Mwenyekiti ni Johel Festo kutoka Mkoa wa  Mwanza, Makamu Mwenyekiti ni Aidath Ismail pia kutoka Mkoa wa Mwanza, Katibu ni Thuwaiba Abdallah anayetokea  Unguja Magharibi na viongozi hao utadumu kwa kipindi cha miaka miwili.

  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku amemtaka Mwenyekiti mpya wa Baraza la Watoto Taifa kuhakisha anaongeza  idadi ya mabaraza katika ngazi ya Mkoa na Wilaya na kumtaka kufanya hivyo kwa kushirikiana na Wizara ili kila mkoa upate uwakilishi wake.

  0 0


  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akielekeza jambo kwenye sehemu ya kukusanya madini ya jasi iliyopo katika eneo la Hoteli Tatu Wilayani Kilwa mkoani Lindi. Kushoto mbele ni Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Sophia Omari.
  PICHA NA 5
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akiangalia madini ya chumvi katika eneo la Jangwani kwa Chinja lililopo Wilayani Kilwa mkoani Lindi.
  PICHA NA 6
  Sehemu ya wazalishaji wa madini ya chumvi katika eneo la Kilwa Masoko lililopo Wilayani Kilwa mkoani Lindi wakisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika katika eneo hilo wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero zao.
  ……………………

  Na Greyson Mwase, Kilwa.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameitaka Tume ya Madini kufanya uchunguzi kuhusu mgogoro kati ya kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa madini ya jasi ya Kizimbani inayomilikiwa na Seleman Mohamed na wananchi wa kijiji cha Hotel Tatu kilichopo Wilayani Kilwa mkoani Lindi.

  Naibu Waziri Nyongo ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Desemba, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho wakati wa utatuzi wa mgogoro huo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua shughuli za madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

  Alisema kuwa, baada ya kusikiliza pande zote mbili imeonekana kuna haja ya  Tume ya Madini kufanya uchunguzi ili kubaini namna utoaji wa leseni ya uchimbaji wa madini ya jasi kwa kampuni ya Kizimbani ulivyofanyika kabla ya kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria na kanuni za madini.
  Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo alisisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini haitasita kuwaondoa maafisa madini wakazi wa mikoa watakaobainika kuwa ndio chanzo cha migogoro kwenye maeneo ya uchimbaji wa madini.

  “ Kama Serikali tunataka kuhakikisha leseni za utafiti na uchimbaji wa madini zinatolewa kwa kufuata sheria na kanuni za madini bila kuwepo kwa migogoro ya aina yoyote, aidha hatutasita kumwondoa afisa madini mkazi yeyote atakayebainika kuwa chanzo cha migogoro kwenye shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini,” alisema Naibu Waziri Nyongo huku akishangiliwa na wananchi.

  Awali wakielezea mgogoro huo kwa nyakati tofauti, wananchi hao walisema kuwa walikuwa na mgogoro wa muda mrefu kati yao na Seleman Mohamed aliyedai kuwa mmiliki halali wa eneo husika hali iliyopelekea mgogoro kuwasilishwa kwenye Ofisi ya Madini Mtwara, ambapo  mtaalam kutoka ofisi hiyo alifika kwa ajili ya kuchukua alama za eneo husika kwa ajili ya kwenda kuhakiki umiliki wa eneo husika.

  Waliendelea kusema kuwa, walifika katika Ofisi hiyo baada ya siku mbili na kuelezwa kuwa eneo hilo lilishaombewa leseni na kutolewa kwa mmiliki wa kampuni ya Kizimbani, Seleman Mohamed.
  Walisema kuwa tangu kuzuka kwa mgogoro huo mwaka 2013, wamekwenda katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Mkoa pasipo mafanikio yoyote na kusisitiza kuwa wanahitaji eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya jasi kwa kutumia mwekezaji na  kujipatia kipato pamoja na kulipa kodi Serikalini.

  Kwa upande wake mmiliki wa leseni hiyo, Seleman Mohamed alidai kuwa aliomba leseni kwa kufuata sheria na kanuni za madini na kupatiwa leseni yake.Wakati huo huo akizungumza katika nyakati tofauti kupitia mikutano na wazalishaji wa chumvi iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na katika eneo la Kilwa Masoko Wilayani Kilwa mkoani Lindi, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini inatambua mchango wa wazalishaji wa chumvi hususan katika mkoa wa Lindi kwenye Sekta ya Madini hivyo imeweka mikakati mbalimbali ya kuwasaidia.

  Alieleza mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuondoa tozo mbalimbali tisa kisheria zilizokuwa zinatozwa na halmashauri ili uzalishaji wao uwe na tija na kuinua uchumi wa mkoa wa Lindi.
  Alieleza kuwa mikakati mingine kuwa, ni pamoja na kuendelea kushughulikia changamoto zilizopo kwenye uzalishaji chumvi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha chumvi katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi mara baada ya kupata eneo na fedha kutoka Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini. (SMMRP) uliopo chini ya Wizara ya Madini.

  Aliendelea kusema kuwa mahitaji ya chumvi nchini ni takribani tani laki tatu na nusu kwa mwaka ambapo asilimia 70 ya chumvi inaagizwa kutoka nje ya nchi  na kusisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imejipanga katika uboreshaji wa uzalishaji wa chumvi nchini.“ Kama Wizara ya Madini tunataka ifike mahali tuzalishe chumvi bora ya kutosha na kuuza ya ziada nje ya nchi na kujiingizia fedha za kigeni,” alisema Naibu Waziri Nyongo.Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo aliwataka wazalishaji wa chumvi hao kufuata sheria na kanuni za madini.

  Wakizungumza katika nyakati tofauti wazalishaji wa chumvi mkoani Lindi waliwasilisha changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na tozo zilizoondolewa kisheria kwenye madini ya chumvi kuendelea kutozwa na halmashauri, ukosefu wa mitaji pamoja na masoko.Changamoto nyingine ni pamoja na miundombinu duni kwenye maeneo yenye uzalishaji wa chumvi, madini joto yanayotumika kwenye uzalishaji wa chumvi kuuzwa kwa gharama kubwa na kutotambuliwa katika halmashauri na taasisi  nyingine za kifedha.

  0 0


  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika kikao cha ndani kilichojumuisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Manyoni wakati wa ziara ya kikazi, lengo ikiwa ni kuweka mikakati ya kudhibiti hujuma na uhalifu katika maeneo inapopita miradi mbalimbali ya serikali. Naibu Waziri yuko mkoani Singida kwa ziara ya kikazi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto), akiangalia ramani ya eneo linarotarajiwa kuejngwa kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Manyoni Naibu Waziri yuko mkoani Singida kwa ziara ya kikazi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati mstari wa mbele), akiongozana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Manyoni kuingia katika Kituo cha Polisi cha Manyoni kinachojengwa baada ya kituo cha awali kupitiwa na Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa . Naibu Waziri yuko mkoani Singida kwa ziara ya kikazi.


  Muonekano wa nje Kituo Kipya cha Polisi Wilaya ya Manyoni ambacho kipo mbioni kukamilika ambacho kinategemewa kudhibiti hujuma na uhalifu katika maeneo mbalimbali inakopita miradi mikubwa ya serikali .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  ……………………..

  Na Mwandishi Wetu

  Serikali iko katika mpango wa kujenga Kituo cha Polisi katika Halmashauri ya Itigi ikiwa ni juhudi za kulinda hujuma na uhalifu katika Ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge) na Mradi wa Umeme katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (Stiegler’s Gorge) baada ya wavamizi kuingia eneo la hifadhi ya Rungwa ambayo kuna mito 18 ambayo ni chanzo cha Mto Rufiji ambako mradi wa umeme unajengwa.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitembelea na kukagua Mradi wa Kituo kipya cha Polisi cha Wilaya ya Manyoni na kukagua eneo linarotarajiwa kujengwa Kituo cha Polisi Itigi lengo ikiwa kudhibiti matukio ya uhalifu.

  Akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Manyoni, Naibu Waziri Masauni amesema Serikali iko tayari kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha miradi mikubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeianza inakamilika bila kufanyiwa hujuma zozote na wahalifu.

  “Miradi mikubwa ambayo Rais wetu Dkt. John Magufuli na serikali anayoiongoza ameianzisha ni muhimu ikalindwa ili ilete manufaa kwa nchi pindi itakapokamilika na sisi kama wizara tutahakikisha tunasogeza huduma za Ulinzi na Usalama katika maeneo yote ambayo miradi hiyo inapitia, ndio maana leo nimetembelea ujenzi wa Kituo cha Polisi Manyoni ambacho kiko mbioni kukamilika lengo ikiwa ni kulinda miradi hiyo mikubwa,” alisema Masauni

  Akizungumza katika ziara hiyo, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka amekiri kuwepo na haja ya kituo katika Wilaya za Manyoni na Itigi ili kuweza kuboresha usalama katika maeneo hayo ambayo yanapitiwa na miradi hiyo mikubwa miwili huku akiiomba wizara kuleta askari katika vituo hivy pindi ujenzi utakapokamilika.

  0 0   
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuwawashia vifaa vya kusaidia kusikia kwa watoto 10 waliopandikizwa vifaa hivyo Novemba 12 hadi 16, 2018. Kutoka kushoto ni mtaalam wa usikivu, Fayaz Jaffer na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa Muhimbili, Dkt. Aveline Aloyce .
  ????????????????????????????????????
  Wazazi wa watoto wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Dkt. Liyombo kabla ya vifaa hivyo kuwashwa  tangu walipopandikizwa Novemba 12 hadi 16, 2018.
  003
  Mtoto Rehoboth Kivuyo akisikia kwa mara ya kwanza tangu wazazi wake walipobaini kwamba ana tatizo la kusikia.
  004
  Baadhi ya wazazi wakisikiliza mambo ambayo wanapaswa kuzingatia baada ya watoto kuwashiwa vifaa hivyo leo.
  ????????????????????????????????????
  Katika mkono wa kushoto, Dkt. Edwin Liyombo akionyesha moja ya kifaa cha kusaidia kusikia ambacho watoto hao walipandikizwa Novemba 12 hadi 16, 2018. Katika mkono wa kulia ni kifaa kingine ambacho kinawekwa juu ya sikio la mtoto aliyepandikizwa kifaa cha kusaidia kusikia.
  006
  Mtoto Eliada Mukama akionyesha kushangaa baada ya kusikia kwa mara ya kwanza.
  ????????????????????????????????????
  Watoto waliopandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia Novemba 12 hadi 16, 2018 wakisubiri kuwashiwa vifaa hivyo leo.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
  ………………………

  kumi ambao wamewekewa vifaa maalum vya kusaidia kusikia (Cochlear Implant) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wameanza kusikia kwa mara ya kwanza baada ya kuwashiwa vifaa hivyo (switch on).

  Watoto hao ambao wametoka katika mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Dar es Salaam, Kilimanjaro, Tanga, Pwani na Ruvuma walifanyiwa upasuaji Novemba 12 hadi Disemba 16 mwaka huu ambapo zaidi ya asilimia 90 ya upasuaji huo ulifanywa na watalaam wa Muhimbili.Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa magonjwa ya Pua, Koo na Masikio, Dkt. Edwin Liyombo amesema mbali na zoezi hilo la kuwawashia vifaa vya kusaidia kusikia, lakini pia watoto wengine ambao waliwekewa vifaa hivyo nao wamekuja kwa ajili kuangaliwa maendeleo yao na kupatiwa elimu ya kutunza mashine hizo.

  Kwa mujibu wa Dkt. Liyombo, tangu kuanza kwa huduma hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Juni 2017 mpaka Disemba 2018, watoto 21 tayari wamewekewa vifaa hivyo ambapo jumla ya shilingi milioni 777 zimetumika kwa ajili ya upasuaji huo na endapo wangepelekwa kutibiwa nje ya nchi Serikali ingetumia shilingi Bilioni 2.1 kwa ajili ya kufanikisha matibabu hayo.Hivyo kutokana na upasuaji huo wa ubingwa wa juu kufanyika hapa nchini Serikali imeokoa shilingi Bilioni 1.3.

  “Lengo la hospitali ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, kwani matibabu haya yanagharama kubwa kwani kupeleka mtoto mmoja nje ya nchi kwa ajili ya kupandikizwa kifaa cha usikivu ni shilingi milioni 100 wakati akipatiwa matibabu hayo Muhimbili hugharimu shilingi milioni 37 kwa mtoto mmoja,” amesema Dkt. Liyombo.

  “Tunaishukuru Serikali kuwezesha upasuaji huu kufanyika hapa nchini, mbali na kupunguza gharama lakini faida kubwa ni watalaam wa ndani kujengewa uwezo wa kutoa matibabu haya,” amesisitiza Dkt. Liyombo.Akielezea ukubwa wa tatizo Dkt. Liyombo amesema takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinaonesha kuwa hivi sasa watu milioni 466 wana matatizo ya usikivu na hadi kufikia 2050 karibu watu Bilioni moja watakua na matatizo hayo.

  Pia, amesema katika kila watoto 1,000 wanaozaliwa, watoto 3 hadi 6 wana matatizo ya usikivu.
  Ametaja baadhi ya sababu zinazochangia mtoto kuzaliwa na tatizo la usikivu kuwa ni pamoja na matumizi mabaya ya dawa, kupata maambukizi kama homa ya uti wa mgongo.Zoezi la kuwawashia vifaa vya usikivu limefanywa na watalaam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalam wa Medel.
  Huduma ya upandikizaji wa kifaa cha usikivu (Cochlear Implant) ilizinduliwa Juni 2017 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu, hivyo Tanzania kuwa nchi ya pili kutoa huduma hiyo katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Kenya. Pia, Tanzania ni nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo kupitia hospitali ya Umma ambayo ni Muhimbili.

  0 0


  Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) mkoa wa Arusha,Isaya Shekifu akizungumza wakati wa mkutano na viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika wa mazaoa na mfuko huo,kushoto ni Afisa Matekelezo wa NHIF,Miraji Kisile na Mrajisi wa Ushirika mkoa wa Arusha,Emmanuel Sanka.
  Baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika wa mazao mkoa wa Arusha wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) kwaajili ya kuwapa uelewa wa namna ya kujiunga jana,Emmanuel Sanka.Picha na Filbert Rweyemamu  Na mwadishi wetu,Arusha .

  Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF)umewataka wanachama wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa Mazao kujiunga na Bima ya Afya kwaajili ya kupata matibabu bora ambao ni mpango wa serikali ya awamu ya tano ifikapo mwaka 2020 idadi kubwa iwe imejiunga na mfuko huo.

  Meneja wa NHIF mkoa wa Arusha,Isaya Shekifu amesema Ushirika Afya ni mpango mahususi ulioanzishwa na serikali kwa lengo la kutoa huduma ya bima ya afya kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika vya msingi kwa kuanzia na mazao matano.

  Ameyataja mazao hayo matano ya kimkakati kuwa ni Korosho,Pamba,chai,Kahawa na Tumbaku ambayo baada ya kuzinduliwa kwa mpango huo na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa mwaka huu mfuko ulianza kutoa huduma za matibabu kwa wakulima.

  Shekifu amesema mkulima anatakiwa kulipa kiasi cha Sh 76,800 ukiwa ni mchango wake kwaajili ya kupata Ushirika Afya na itamwezesha kupata huduma ya matibabu kwa mwaka mzima pia ataruhusiwa kuwakatia bima hiyo kwa mwenza,mzazi,mkwe na watoto.

  Mrajisi wa Ushirika mkoa wa Arusha,Emmanuel Sanka amesema mpango huo utasaidia wanachama wake kunufaika na matibabu yanayotolewa na mfuko huo hatua itakayoongeza tija katika shughuli zao za kilimo cha Kahawa.

  Amesema gharama za matibabu bila kutumia bima ya afya zipo juu na kuwataka viongozi hao wa ushirika kuwahamasisha wanachama wao kujiunga kwa wingi ili kuanza kunufaika na mpango wa serikali wa mazao matano ya kimkakati unaleta matokeo yaliyokusudiwa.

  0 0

  Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo na ufafanuzi mbalimbali kutoka msimamizi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mhandisi Uday Dadrawalla (kulia) walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzo wa Miundombinu ya Mahakama hiyo unaosimamiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.
  Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo na ufafanuzi mbalimbali kutoka msimamizi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mhandisi Uday Dadrawalla (kulia) walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Mahakama hiyo unaosimamiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa gharama ya shilingi bilioni 6.2.
  Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Maafisa wa Mahakama Kuu-Musoma na Wakandarasi wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, wakinyanyua kofia za usalama baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa Mahakama hiyo uliofikia asilimia 80 na umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 6.2
  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-


  Na Benny Mwaipaja, WFM, Musoma

  WAKAZI wa mkoa wa Mara wanatarajia kuondokana na adha ya kufuata huduma za Mahakama Kuu mkoani Mwanza, umbali wa zaidi ya kilometa 200 kutoka mjini Musoma, baada ya ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma kukaribia kukamilika mapema mwakani.

  Wakizungumza na timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, baadhi ya wakazi wa mji wa Musoma Mary Mohamed na Happy Mjito, wamesema kuwa hivi sasa wanatumia fedha nyingi kufuatilia haki zao Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza hali inayowafanya wengi wao kukata tamaa kufuatilia kesi zao hivyo kupoteze haki zao

  “Ukikata rufaa ya kesi unaambiwa uende Mwanza wakati hata Mahakama Kuu yenyewe ya Kanda ya Mwanza hatuijui mahali ilipo, sasa tunafurahi kwamba tutakuwa tumiendesha kesi zetu hapa hapa Musoma” alisema Bi. Happy Mjito

  Akielezea hatua ya ujenzi wa Mahakama hiyo Kuu Kanda ya Musoma ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 6 nukta 2, Wakala wa Mkandarasi anaye jenga Mahakama hiyo, Kampuni ya DF Mistry, Mhandisi Uday Dadrawalla, ameiambia timu hiyo ya Wizara ya Fedha na Mipango inayofuatilia utekelezaji wa miradi ya Maendeleo mkoani Mara kwamba ujenzi huo umefikia asilimia 80.

  “Mkataba wetu unaonesha kuwa tunatakiwa kukabidhi jengo ifikapo tarehe 21 mwezi Mei, 2019 lakini kwa kasi tunayokwenda nayo tutakabidhi jengo hili mapema zaidi Mwezi April, 2019” alisema Mhandisi Dadrawalla.

  Mradi huu unaotekelezwa na Mahakama Kuu Nchini ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele iliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18 hivyo utekelezaji wake ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2021, hususani katika eneo la Utawala Bora.

older | 1 | .... | 1753 | 1754 | (Page 1755) | 1756 | 1757 | .... | 1897 | newer